Header Ads

MWAKA MMOJA LEO BILA DK.SENGONDO MVUNGI






MWAKA MMOJA LEO BILA DK.SENGONDO MVUNGI 

Na Happiness Katabazi
LEO Novemba 12 Mwaka 2014, Mhasisi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), Dk.Sengondo Mvungi Ametimiza  Mwaka mmoja tangu alipofariki Dunia .

Dk.Mvungi alifariki dunia tarehe kama ya Leo Hospitali  Milpark  nchini  Afrika Kusini ambako alikuwa amelazwa  kwaajili ya kupatiwa matibabu baada ya  usiku wa kuamkia Novemba  3 Mwaka 2013 kuvamiwa na wahalifu na kujeruhiwa vibaya maeneo Mbalimbali ya mwili wake ikiwemo kichwai na hivyo kumsababishia majeraha makubwa na kupoteza fahamu tangu siku hiyo hadi anafariki Dunia.

Kwangu Mimi binafsi nitaendelea kumkumbuka Dk.Mvungi Kwani nilimheshimu sana na alikuwa ni mtu wangu wa karibu na ndiyo uwa nikimkubuka Mzee wangu Huyo ambaye alikuwa akipenda kunitia Mimi ni Mkewe 'First Lady'  na Mimi Namuita yeye ni ' Rais Mdhulumiwa'  uwa nakosa raha ila sina la kufanya zaidi kuzingatia Yale aliyokuwa akinihusia ni yafanye kwa uzalendo wa taifa langu na Maisha yangu binafsi.

Mbali  ya Dk.Mvungi Kuuwawa akiwa na wadhifa wa Mjumbe wa Tume ya Madiliko ya Katiba , pia Mvungi alikuwa ni miongoni wa wahasisi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB) na ndiye aliyekuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo anayeshughulikia Taaluma.

Dk.Mvungi Leo ukiwa unatimiza Mwaka mmoja tangu ufariki, napenda kukwambia kuwa UB, imekuwa sasa wanafunzi ni wengi  wanazidi kujiunga  Katika chuo hicho kadri siku zinavyozidi kwenda Taasisi ya Vyuo Kikuu(TCU)
 Inakipatia chuo idadi ya wanafunzi.

UB ilianzishwa rasmi Mwaka 2011. Ushahidi wa UB inakuwa ni kwa hatua ya  TCU kuzidi  kuleta  idadi kubwa ya wanafunzi  waje kusoma UB kozi mbalimbali ni huu.

Katika mwaka wa  kwanza wa masomo wa chuo hicho kilipoanzishwa ulitambulika kuwa ni mwaka wa 2011/2012 chuo kilianza kikiwa na jumlanya wanafunzi 64 tu.

Mwaka wa masomo wa 2012/2013  TCU ilipeleka jumla ya wanafunzi  154. Mwaka 2013/2014 wanafunzi 234. Na mwaka mpya wa masomo ulioanza Novemba tatu mwaka 2014  yaani Mwaka wa masomo wa 2014/2015 jumla ya wanafunzi 254  la Katiba.

Licha ya Mahalu kuwa mjumbe wa bunge hilo pia ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kutunga Kanuni zilizoliongoza Bunge kufanyakazi zake na pia Mahalu alikuwa ni mjumbe wa Kamati ya kuandika Katiba iliyopendekezwa na Bunge Hilo kuanzia Februali 18 hadi Oktoba 4 Mwaka 2014. usajili na wameanza masomo na kuna wanafunzi wengine bado wanaendelea kufanya usajili.

Ninaposema UB inazidi kutanuka kwasababu wakati unafariki Dunia ukiacha UB ikiwa na madarasa yake Eneo la Kawe Beach na Makao Makuu yake Mikocheni kwa Warioba Dar es Salaam.

Lakini wanafunzi wapya waliojiunga Mwaka huu  kwa idadi ya wanafunzi imeongezeka ,uongozi wa Chuo umekodi  jengo lililopo ndani ya eneo la Kanisa la Kiinjili la Kilutheli (KKKT), linalomilikiwa na Kanisa  hilo Kinondoni Dar es Salaam ambalo jengo Hilo lilikuwa  likitumiwa na Chuo Kikuu cha Tumaini.

Ishara ya chuo hicho ulichokiasisi kimekua,UB imezidi kutoa ajira za kudumu kwa walimu na watumishi wa Kada mbalimbali na ajira za muda kwa walimu.

Desemba 7 Mwaka Jana ,Chuo Kilifanya mahafali yake ya kwanza Katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na mwizi wa   First Lady wako, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Mohammed Ghalib Bilal ndiye alikuwa mgeni rasmi na Kabla ya sherehe kuanza tulikukumbuka kwa kusimama juu na kukuombea ikiwa ni Ishara ya kuthamini mchango wako kwa UB.

Na Mungu akipenda Desemba 6 Mwaka huu, UB itafanya mahafali ya pili.Tuna kukumbuka  sana Kwani ulikuwa ni miongoni mwa wahasisi wa UB lakini umefariki na hivyo kushindwa kuona ni jinsi gani  chuo ulichokibuni na kukianzisha  wewe na Balozi Mahalu na wengine jinsi kinavyozidi kukua  kwa kasi.

Tukiachana na eneo la elimu ambapo Marehemu Dk.Mvungi alikuwa ni Mwanataaluma kwa maana  ni Mhadhiri wa fani ya Sheria na Mtetezi wa Haki za binadamu.

Dk.Mvungi ,Septemba 26 Mwaka huu, Kituo Cha Utetezi wa Haki za Binadamu (LHRC), kilifanya sherehe ya kutimizwa Miaka 19 tangu Kituo hicho kilivyoanzishwa na miongoni mwa waasisi wa Kituo hicho ni wewe.

 Aidha siku hiyo LHRC  ilizindua   Kitabu kilichobeba makala za waandishi Mbalimbali ikiwemo makala yangu yenye kichwa cha habari ' Dk.Sengondo Mvungi ameniuma'.

Kila mwandishi wa makala zilizowekwa kwenye kitabu hicho ,alikuelezea jinsi alivyokufahamu maisha uliyoishi hapa duniani na k kitabu hicho kimepewa jina  la ' Dk.Sengondo Mvungi  , Breathing the Constitution'.

Katika Medani siasa Dk.Mvungi alikuwa ni Mwanachama wa muda mrefu wa Chama Cha NCCR- Mageuzi ,Chama alichokipenda kutoka Moyoni na alijitolea kwa Moyo wake wote kukijenga Chama hicho na kujitolea Fedha, mahalifa   ya fani yake ya Sheria na Katiba.

Licha ya Kuwa Mwana NCCR - Mageuzi hakuwa akiwachukia wanachama wa vyama vingine. Dk.Mvungi aliamini Katika kumcha   Mungu, siasa za kuvumilia na kushimiana nakupenda siasa za vurugu.

Baada ya Dk.Mvungi kumaliza kampeni zake za kugombea Kiti Cha Urais  Mwaka 2005 ,mimi nilikuwa ni mwandishi wa kike peke yangu ambaye niliungana na waandishi wa Kiume katika msafara wake wa kampeni ,alitueleza watu wake wa karibu Kuwa alipokuwa Akizunguka nchi nzima Katika mikutano yake ya kampeni amegundua kuing'oa CCM madarakani siyo kazi Rais Kama yeye na wanachama wa vyama Vya upinzani wanavyofikiri.

Dk.Mvungi alisema CCM imejiimarisha toka ngazi ya matawi Katika maeneo yote kitendo ambacho ni tofauti kwa vyama Vya upinzani ambavyo hata kwenye baadhi ya Kata hapa Dar es Salaam, havina Ofisi wala matawi na Matokeo yake kila kukicha vyama Vya upinzani  vimekuwa vikifanya siasa zake kwa kutumia mikutano ya waandishi wa Habari wakati kwa CCM  Hali siyo hivyo.

Na kabla  Kabla hajafariki alikuwa akiniambia mara kwa mara analiona anguko la Chama Kimoja Cha Siasa Cha upinzani (sitakija kwa jina) Kwani chama hicho kinafanya siasa zinazoambatana na vurugu na maandamano kila kukicha na kwamba Watanzania ni watu wanaopenda Amani  ipo siku watakikataa kwa hoja kuwa Chama hicho ni Chama kinachofanya siasa kwa vurugu na kushinikiza kufanya maandamano yasiyo na Kibali.

Na kweli utabiri huo wa Dk.Mvungi wa Miaka minne iliyopita Kwangu Mimi nauona umetimia Kwani HIvi sasa Chama hicho Cha upinzani kinaonekana kina wanachama ambao wanaamini kufanya siasa zinazoambatana na vitendo Vya Uvunjifu wa Sheria na baadhi ya wanachama wake wamefikishwa Katika Mahakama Mbalimbali wakikabiliwa na makosa ya kuingia kwa jinai, kufanya mikusanyiko haramu na kukaidi amri halali ya Jeshi la Polisi.

Leo ninapokuandikia makala hii Dk.Mvungi huko uliko, lile jaribio ulilokuwa ukitamani lifanyike Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 ambalo wazo  ilikuwa imeishaandaliwa Kuwa vyama vyote Vya upinzani viunganishe Nguvu Katika uchaguzi ule kwa kusimamisha mgombea mmoja wa urais ,wabunge na madiwani .

Lakini mwisho wa siku ulinieleza wazo Hilo lilipofikishwa Katika masikio ya Mwanachama mmoja wa Chadema ambaye Chama hicho kinamuamini mno na kupokea ushauri wake wa kisheria ( jina naliifadhi) ,alilipinga wazo hilo kwa nguvu zote na Kusema Kuwa kila Chama kiingie  kivyake Katika uchaguzi ule ambapo Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyeibuka Mshindi Katika uchaguzi ule kwa kupata kura nyingi za ndiyo.

Hata hivyo Oktoba Mwaka huu, Vyama vinne Vya upinzani yaani Chadema, NCCR, CUF  vimeingia makubaliano ya kufanyakazi kwa kushirikiana na kwamba Katika uchaguzi Mkuu Mwakani ngazi ya Kata, Jimbo na rais watasimamisha mgombea ambaye ataonekana Kuwa anakubalika na watu Wengi Katika eneo husika. Tusubiri Tuone Ushirika huo utadumu au laa.

Licha Tayari kuna taarifa za chini kwa chini  zimeanza kuvuja Kuwa kuna baadhi ya viongozi wa Chama Kimoja Katika ushirika huo kimekuwa kikiwatuma makada wake kwenda kuwarubuni wanachama wa vyama vingine Vya upinzani ambao wanakubarika Katika eneo husika Kuwa vyama vyao siyo maarufu na havina Nguvu, hivyo waviame vyama vyao hivyo Vya upinzani wajiunge na Chama hicho Cha upinzani Chenye wabunge Wengi ili Majina  Yao yaweze kupitishwa nawawe  wagombea Katika nafasi za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika Desemba Mwaka huu na uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwakani.

Baadhi ya vyama vinavyofanyiwa usanii huu bado havijagundua Kuwa kuna Chama Kimoja 'kinawageuza wanasesere', vikija kupata Habari lazima vumbi litibuke.

Ningali nikikumbuka ulifariki wakati Tume ya Mchakato wa Katiba Mpya iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba ikiwa Katika hatua ya kuandika rasimu iliyotakana na maoni ya wananchi mliyoyakusanya nchi nzima.

Tume hiyo ambayo ilifanyakazi zake kwa muda wa Miezi 18 na ilitoka na rasimu ambayo pamoja na mambo mengi rasimu hiyo ilisema wananchi Wengi walio hojiwa Walipendekeza kuwepo na serikali Tatu .

Rasimu hiyo ya Tume baada ya kukabidhiwa  kwa Rais Jakaya Kikwete, Kikwete aliipongeza Tume hiyo kwa kazi nzuri .

Baada ya Ripoti hiyo kumkabidhi kwa Rais  na Jaji Warioba Kusema kilichopo ndani ya Tume hiyo, wananchi wa Kada tofauti ambao waliisoma na wengine hawakuisoma ila ni ushabiki tu waliibuka kila kukicha wengine wakisema rasimu hiyo ni Mbaya na Haijazingatia maoni ya wananchi wote na wengine Kusema rasimu hiyo ni nzuri.

Rais Kikwete aliteua wajumbe wa Bunge maalum la Katiba ambapo aliteuwa watu wengi wakiwemo  Balozi Mahalu na Dk.Natujwa kuwa wajumbe wa bunge hilo na hivyo kufanya UB kuwa na wajumbe wawili katika Bunge hilo.

Bunge Hilo kilipoanza kazi yake lilikutana na Vituko Vingi ,malumbano kutoka kwa Baadhi ya wanasiasa wa vyama Vya siasa,wanaharakati uchwara ,viongozi wa dini, vyombo vya habari ambao walikuwa wakirushiana  vijembe na uzushi wa kila aina na kutoleana lugha za kebehi na kudhalilishana.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  Oktoba 4 Mwaka huu, aliwatangazia wanachama wa Chama Chake kote nchini waandae maandamano yasiyo na kikomo bila ya kuomba kibali  cha Polisi ,maandamano ambayo yalikuwa na lengo la kushinikiza  Bunge Maalum lisitishwe kwasababu lilichakachua mchakato wa Katiba limedharau maoni ya wananchi  yaliyomo kwenye rasimu ya Tume ya Warioba.

Hata hivyo Jeshi la Polisi iliyapiga  marufuku  maandamano hayo kila pande zote za nchi hii na waliokaidi amri hiyo   walikamatwa na kufikishwa mahakamani na hatimaye Bunge hilo likamaliza kazi yake na Katiba Pendekezwa ikapatikana.

Lakini wakati Mbowe akisema  hayo sijui alikuwa hafahamu Kifungu Cha 25 (2) Cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2013 ambacho Kifungu hicho kinatoa mamlaka kwa Bunge Maalum la Katiba  kuongeza na kuboresha rasimu (work document) yaani rasimu  ya Tume ya Jaji Warioba wakati walipokuwa wakiandika Katiba Pendekezwa.

Agizo Hilo la Mbowe lilikuwa ni dalili za wazi za kushindwa kuzuia bunge lile  lisiendelee.

Kwani baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani wakiwemo wa chama Chako Cha  NCCR- Mageuzi,CUF, Chadema walisusia kikao cha bunge hilo kwa kile walichodai kuwa wamechoshwa kudhalilishwa na wabunge wa CCM Katika Bunge Maalum la Katiba na walijiapiza Kuwa akidi ya kura za kupitisha Katiba Pendekezwa haitapatikana lakini ilipatikana wakaumbuka.

Na Mbaya zaidi baadhi ya wajumbe wenzio wa iliyokuwa  Tume ya Warioba na Warioba Mwenyewe nao wakati Bunge likiendelea nao walikuwa wakihutubia kwenye midahalo na kuhojiwa na vyombo Vya Habari Kuwa akidi haitapatikana lakini akidi ikapatikana .

Hata hivyo watu wako wa karibu ambao walikuwa ni wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Kama mwanetu Balozi Mahalu ambaye alichaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Baadae Mahalu na Dk.Natujwa , Dk.Harrison Mwakyembe hawakususia Bunge Maalum la Katiba ,walikuenzi wewe uliyekuwa miongoni wa Watanzania ambao walikuwa wanataka Tanzania iandike Katiba Mpya lakini mtu wako mwingine wa karibu James Mbatia yeye na wabunge wengine wa NCCR- Mageuzi walikuenzi kwa kususia kuhudhuria vikao Vya Bunge Maalum la Katiba kuandika Katiba Pendekezwa ambayo kwa zaidi ya asilimia 70 imetengenezwa kutoka na maoni ya Tume ya Warioba ambayo wewe ulikuwa ni miongoni mwa wajumbe ambao mlizunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi.

Kwa hiyo NCCR- Mageuzi  ilikuenzi  katika  mchakato wa kuandika Katiba mpya ambao mchakato huo ambao hivi  sasa umefikia hatua ya wananchi kuipigia kura za ndiyo au hapana Katiba Pendekezwa ambapo Tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Kura ya maoni kuhusu Katiba Pendekezwa itapigwa Aprili mwakani 2015.

Licha  ya akidi kupatikana bado baadhi ya waliokuwa wajumbe wenzio wa Tume ya Warioba  walikuwa wakienda kwenye midahalo Kusema Katiba Pendekezwa haina Afya na wakati wakiikandia Katiba Pendekezwa, aliyesababisha wewe usiwe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Kikwete ambaye tulikuwa tunamtani aliiba kura zako kwa maana hiyo wewe ni 'rais Mdhurumiwa'   na Rais wa Zanzibar, Dk.Mohammed Shein wamekuwa wakiisifu wazi wazi.

Kuwa  Katiba Pendekezwa  ambayo imependekeza muundo wa serikali mbili uendelee ni Katiba Bora na wanawashawishi wananchi waipigie kura na kwamba  hawana mashaka kuwa Katiba Pendekezwa itapitishwa na wananchi wengi.

Dk.Mvungi Kama unavyonifahamu mini mwanamke jasiri ambaye usema kile ninachokiamini hadharani, ukweli ni kwamba Katika uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Desemba Mwaka huu na uchaguzi Mkuu mwakani  Dalili za wazi zinaonyesha kuwa vyama Vya upinzani vinaweza kujikuta vikipoteza viti Vingi mno na majimbo mengi yakirudi CCM.

Kwa sababu hakuna wakati wowote ule ambao CCM imejipanga kimkakati NA kushinda kuliko vyama Vya upinzani.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulahman Kinana na Katibu wa Itikadi Unezi , Nape Nnauye wanachanja Mbuga kwenda kuzungumza  na wananchi kuimarisha Chama 'kusteamleti Chama ' .

Baadhi ya  Viongozi wa vyama Vya upinzani   wao Kutwa wapo Kwenye midahalo wakitoa hotuba ya kupinga Bunge la Katiba, Katiba Pendekezwa na Madai mengine ambayo hayana tija kwa vyama vyao zaidi ya kunufaisha kundi Fulani.

Ila mume wangu wa zamani ambaye wewe umpora 'Mke' ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo walikuenzi kwa kukataa kususia Bunge Maalum la Katiba badala yake walihudhulia vikao vyote Vya Bunge lile licha nao kila kukicha walikuwa wakisakamwa na baadhi ya wabunge wa Chama CUF,NCCR- Mageuzi na Chadema Kuwa ni wasaliti wa wananchi na wanafuata  posho bungeni .

Ujinga mtupu Kwani tangu wapinge mchakato wa Katiba wametumia Rasilimali nyingi na muda mwingi kupinga mchakato wa Katiba na hawa mafanikiwa  na wakati wakifanya hay,  viongozi wa CCM walikuwa wakipita  mikoani kuimarisha Chama na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukijenga Chama chao yake Makundi yaliyokuwepo Katika uchaguzi wa Mwaka 2010 ambayo yalisababisha baadhi ya wana CCM Kuwaasaidia wagombea upinzani washinde kwasababu Katika kura za maoni wagombea waliokuwa wakiwaunga mkono walikatwa.

Walianzisha Operesheni 'Delete CCM, Operesheni Sangara Matokeo yake  Samaki Sangara hao wamechina kwasababu Kama wasingekuwa wamechina ,tungeona   Matunda ya operesheni sangara na Kama kweli tungeshuhudia  CCM  inatoka madaraka lakini wapi ndiyo kwanza CCM inazidi kustawi   Kama Shina  la Mgomba.

Kinachonikera kwa vyama vyetu hivi Vya upinzani kweli kuna kazi nzuri zinazofanywa na vyama hivyo,ila tu vyama hivi sijuii kwa kutokujua au la wakati mwingine vikaamua kujiingiza kujadili masuala Fulani ambayo hayapo Kabisa kwenye Kwani za vyama vyao au kutoa matamko ambavyo ni Mwendawazimu peke yake anaweza kuyatoa.

Sasa Misielewi kampeni hizo zinazobeba ujumbe wa kuing'oa CCM  ni kampeni ambazo zinaandaliwa  na wakubwa wa vyama hivyo pindi wanapojisikia  wanahamu ya kufanya utalii wa ndani ili wajiongezee  kipato kwa kisingizio Kuwa wanafanya ziara ya kuimarisha vyama vyao mikoani au laa!

Bunge lile Maalum la Katiba licha lilikuwa likiundwa na wajumbe walioteuliwa na Rais, pia wale wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nao pia walikuwa ni wajumbe wa Bunge lile ambalo bunge lile lianza kazi zake  Februali 18 hadi Oktoba 4 Mwaka 2014.

Dk.Mvungi kwakuwa baadhi ya wanachi walikuwa wamechoshwa na mwenendo wa waliokuwa wajumbe wenzio wa Tume ya licha ya kukabidhi rasimu yao kwa Rais Kikwete walianzisha Kama utaratibu wa Utendaji kazi wa lilokuwa Bunge la Katiba na Katiba Pendekezwa.

Ndipo  wNovemba 2 Mwaka huu, katika  Ukumbi wa Ubungo Plaza, Taasisi ya Mwalimu Nyerere ambapo kulikuwa na mdahalo wa Katiba ambapo mdahalo ulivurugika na kuairishwa hadi siku isiyojulikana kutokana na kuibuka kwa kikundi Cha watu kunyanyua mabango juu ambayo yalikuwa yameandikwa ujumbe uliokuwa ukiunga   mkono Katiba Pendekezwa.

Hali iliyosababisha wale ambao walikuwa hawataki kuyaona mabango hayo  kuanza Kupambana na hivyo kusababisha mdahalo kuvurugika na Mtani wangu Warioba na kundi lake ambao ni waliokuwa wajumbe wa Tume yenu Profesa Paramagamba Kabudi ambaye Katika Harusi yake wewe ulikuwa MC,  Joseph Butiku, Humphery Polepole kunusurika Katika vurugu hizo.

Ilikuwa  ni hatari Tupu  na Mtani wangu  Warioba,hadi sasa hajasikika tena hadharani akizungumzia jambo la Katiba Pendekezwa.

Hata hivyo mwishoni mwa wiki Rais Kikwete alilazwa nchini Marekani na kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume na anaendelea vizuri.Tunamuombea Mungu apone licha  kuna wengine wanakebei ugonjwa anaoumwa na Kuzusha magonjwa Yao wanayoyajua wao.

Lakini Hao ndio  'Watanzania Proper' Tumeishawazoe Kwani wengine ni Kama wana roho za kichawi.

Mkeo Anna na watoto wako wote wapo salama wanaendelea vizuri na shule na kazi. Na dereva wako Emmanuel amepata kazi ya udereva LHRC . Kwa ujumla UB na LHRC inaendelea kuwatazama watoto wako.

Mimi nakuenzi 'Rais Mdhurumiwa ' Dk.Mvungi kwa kuendelea kuikamata elimu na nimeamua kukuenzi kwa kuja kufanyakazi UB kama Afisa Habari na mzee wangu Mahalu ili niweze kuja kuongeza nguvu.

Ila wakati mwingine nikiingia kwenye ofisi yako uliyokuwa ukikaa hapa UB, uwa nakukumbuka lakini sina jinsi.

Hadi sasa Mimi First Lady  wako bado sijampata  mume wa kuniona ( mgombea urais) hivyo uenda Katika kampeni za uchaguzi Mkuu Ujao ninaweza kupata mume mpya baada ya wewe kuniacha Mimi Nikiwa mjane sina mtu wa kunifariji na kunitunza licha walinzi wako uliowacha wananifuatilia nyendo zangu.Teteteee

Septemba 29 mwaka huu wa 2014  saa saba usiku , Mtoto wetu wa kwanza Dk.Natujwa Mvungi 29 alijifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Aghakani Mkoani Dodoma .

Mjukuu wetu Huyo mimi Bibi yake nimempa Majina mawili tofauti jina la kwanza Katiba na jina la pili ni Sengondo. 

Nimempa Majina hayo kwasababu mama yake (Dk.Natujwa) akiwa na ukiwa na ujauzito wa mjukuu wetu Rais Jakaya Kikwete alimteua Kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Hivyo akiwa na ujauzito huo Mtoto wetu mwingi alikuwa akitoka Dar es Salaam kwenye  kushiriki vikao Bunge Hilo ambalo lilikuwa likiongozwa na Mwenyekiti wake Samwel Sitta.

 Ndipo siku ya tarehe hiyo usiku ikiwa ni muda mchache baada ya kutoka kwenye vikao Vya Kamati ya kuandika Katiba Pendekezwa ,mwanetu Dk.Natujwa alijisikia uchungu anakimbiwa kwenye Hospitali hiyo na kulifungua salama mjukuu wetu huyo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo( UB), Profesa Costa Mahalu ndiyo aliyekuwa mtu wa kwanza kunipa Habari  kuwa mwanetu Dk.Natujwa ametuletea mjukuu na hivyo yeye (Mahalu) kuanzia Leo anaitwa Babu, Mimi(Happiness)  naïtwa Bibi na Natujwa anaitwa Mama.

Nilipokea kwa Furaha taarifa hizo lakini dakika Chache  baadae nilipatwa na huzuni  nilianza kukumbuka na kutamani Mungu Angekupa Maisha Marefu na wewe umone mjukuu wako wa kwanza Kwani nilipo mzaa Mwanangu Queen 'Malkia'  na Kusema umefurahi kumpata Mkuu.

Nilijikuta natokwa Machozi ila sikuwa na jinsi nilimshukuru Mungu  kwa kila jambo. 

Binafsi nitaendelea ku kukumbuka Daima, Mema uliyotuasa tufanye sisi vijana ambao tulikuwa karibu yako na kupata ushauri wa mambo mbalimbali nitaendelea kuyapingatia licha siyo Siri kwamba tangu ufariki ule umoja wetu wa vijana ambao tulikuwa tutafika ofisini kwako kupata ushauri na kujadili masuala ya siasa umetoweka naweza Kusema nimebaki Mimi na kaka yangu ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk.George Kahangwa ndiyo tunawasiliana.

Hata hivyo muda mfupi baada ya wewe kuzikwa  ,watu wanaodaiwa Kuwa ndiyo waliovamia nyumbani kwako na ku kushambulia kwa silaha za jadi Kama kibaka ,walikamatwa na polisi na kufikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa kosa la kukuua  wewe kwa kukusudia lakini hadi Leo upelelezi bado haujakamilika.

Aidha Dk.Mvungi bado Tanzania tuna Amani yetu bado tunayo haijavuriguka  na wale waliokuwa wakijaribu kutaka kuiburuga vyombo Vya ulinzi na Usalama imekuwa ikiwadhibiti.

Niitimishe kwa Kusema leo ukiwa unatimiza mwaka mmoja tangu ulipofariki duniani, nitakukumbuka Daima Kwani licha ya kuwa ' Mume wangu' , pia ulikuwa ni mwalimu wangu Mzazi wangu. Pumzika kwa Amani.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Jumatano, Novemba 12 Mwaka 2014.


 JIKUMBUSHE MAKALA YANGU YA MWAKA 2013
 
KIFO CHA DK.SENGONDO MVUNGI KIMENIUMA (2013)

Na Happiness Katabazi 

NOVEMBA 12 mwaka 2013, saa 10 jioni nikiwa darasani katika Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) nasubiri mwalimu wa somo la Criminal Law aingie kufundisha , mwanafunzi mwenzangu wa sheria ambaye ni Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Marco Mochiwa alinifuata na kuniuliza mbona watoto wa mwalimu wetu Dk.Sengondo Adrian Mvungi yaani Dk.Natujwa na Nakundwa wamekuja kuchukuliwa ghafla na kurudishwa nyumbani. 

Nilishtuka na kumwambia misijaona na nikamweleza Mochiwa kuwa taarifa hizo alizonipa ni mbaya sana kwangu na licha sina ushahidi nazo natoka darasani naenda ofisi ya walimu ilinikajue ni kwanini wamechukuliwa hivyo kwani saa saba mchana nilionana na Dk.Natujwa chuoni hapo na kuzungumza nae akasema kuwa baba yake hivi sasa anaitaji maombi kila wakati na tuliongea mambo mengi sana ambayo siwezi kuyaandika katika makala hii.Dk.Mvungi umeniuma sana. 

Wakati nikishuka ngazi ghafla nikapokea simu toka kwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mtanzania, Ester Mbusi akinipa pole ya msiba wa ‘mume wangu’ Dk.Mvungi.Niisii kuchanganyikiwa na kushuka ngazi pole pole huku nikienda kwenye ofisi za walimu nikakuta zimefungwa na kwenda kweny ofisi ya Meneja wa chuo,Innocent Mahedi na kumuuliza ni kweli Dk.Mvungi kafariki na nikweli Dk.Natujwa kaondoshwa haraka chuoni hapo? 

Mahedi alikatalia kata kata na kusema kuwa hana uhakika wa taarifa za kifo hicho , nilimuuliza zaidi ya mara saba huku nikilia na kumuliza iweje kama Dk.Mvungi ni mzima watoto wake wachukuliwe kwa dharula chuoni hapo?Iweje kama taarifa hizo ni za uongo, waandishi wa habari wengi wanipigie simu za kunipa pole zakuondokewa na ‘Rais Mdhurumiwa’? Mahedi alijikausha ila niliwambia ukweli kuwa anafahamu ila ananificha.Kutokana na mazingira hayo nilimpigia simu Dk.Natujwa alipokea na kusema hana ushahidi na hilo ila wanaelekea Mwenge lakini nikasikia pembeni yake kwenye simu analia sana anasema baba yake amefariki.

 Siyo siri nilijikuta nikilia kwa sauti ya juu kwenye viunga vya chuo na kukaa chini , namshukuru sana mwanafunzi mwenzangu wa sheria ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la The Citzen,Bernad James ndiye aliyenisubiri nimalize kulia,na kuniinua kwenye mchanga nilipokuwa nimekaa na kunibebea mkoba na kunishika mkono kuelekea kituoni ambapo ni mwendo wa kama dakika 15 tukapanda wote Bajaji nanikamwambia kwakuwa nimeambiwa wakina Dk.Natujwa wamepelekwa Mwenge nyumbani kwa marehemu kaka yake Dk.Mvungi.

Nilianza  safari ya kwenda hadi hapo Mwenge Kijijini  saa 12 jioni na nilipokelewa na wako wapi Dk.Natujwa wakanithibitishia ni kweli Dk.Mvungi amefariki na watoto wake wamepelekwa Kibamba nyumbani kwa Dk.Mvungi alikokuwa akiishi na mke wake Anna na msiba utakuwa Kibamba.Nikapanda kwenye bajaji nalia sana hadi niliporudi nyumbani Sinza saa moja usiku ndipo kidogo nilianza kukubali hali halisi kuwa ni kweli ‘Rais Mdhulumiwa’ amefariki dunia, na kuanza kuandika makala hii. 

Dk.Mvungi alijeruhiwa usiku wa kuamkia Novemba 3 mwaka huu kwa mapanga kichwani na usoni na kusababisha kupoteza fahamu tangu siku hiyo na Novemba 7 mwaka huu, alitolewa MOI na kusafirishwa kwenda Hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini kwaajili ya matibabu zaidi lakini Novemba 12 mwaka huu, alifariki dunia.Dk.Mvungi umeniuma sana. Dk.Mvungi ‘Rais Mdhurumiwa’ ambaye aliwahi kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na hatimaye kufikia nafasi ya kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo UDSM,ni miongoni mwa waasisi Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB) ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katika na Rais Jakaya Kikwete, alikuwa ndiye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo. 

Kabla sijafika mbali napenda kutamka wazi kuwa kifo na ukatili aliofanyiwa na wahuni ‘majini watu’, Dk.Mvungi yaliniumiza sana na yanaendelea kuniumiza sana hasa ukizingatia Dk.Mvungi licha kilikuwa ni chanzo changu cha habari ambaye alikuwa akinipa habari ambazo nyingine nilikuwa naziandika kwenye gazeti na nyingine nilikuwa siziandiki kwenye Gazeti  alikuwa ni kama baba yangu wa kunizaa kwani aliniweka karibu mno na familia yake,alikuwa akinishauri mambo mengi likiwemo la kujiendeleza kielimu kwenda kusoma sheria, kifamilia, kazi yangu ya uandishi wa habari hasa ukizingatia Dk.Mvungi aliwahi kuwa mwandishi wa habari wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo licha hakuwai kusomea chuo chochote kozi ya Uandishi wa habari. 

Sitamsahau Dk.Mvungi katika hili ambapo mwaka 2009 niliomba kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kusoma kozi ya Cheti cha Sheria nikakosa nafasi, nilivyokosa nafasi nilimfuata ofisini katika Shule ya Sheria UDSM, na kumueleza hilo ambapo Dk.Mvungi alinitaka nimfuate anakokwenda ili aende akawauleze ni kwanini mimi nimekosa nafasi ya masomo na fomu zangu zilikuwa na dosari gani, tuliingia katika ofisi ya mhadhiri mmoja anaitwa Semu Thomas ambaye alimsikiliza Dk.Mvungi na akamtaka Dk.Mvungi arudi ofisini akakae na kwamba yeye Semu atabeba jukumu hilo na alinipeleka hadi kwa Mkurugenzi wa Kozi ya Cheti cha Sheria Tairo, ambaye alisikiliza na kulitatua tatizo langu na akanitaka nijaze fomu upya, na kweli nilijaza fomu upya na zikagongwa mhuhuri wa uwakili na Dk.Mvungi na hatimaye nikakubaliwa kujiunga na kozi hiyo.Dk.Mvungi umeniuma sana. 

Ndimara Tigambwage ndiye aliyemuingiza Dk.Mvungi katika fani ya uandishi wa habari kwani Dk.Mvungi alikuwa akinielezaga kuwa hapa duniani kuna watu anaweza kuwapinga adharani kupitia vyombo vya habari na siyo Ndimara Tigambwage au Balozi Costa Ricky Mahalu. Kwani alipokuwa amemaliza elimu ya kidato nne alikuwa akiishi kwa Marehemu  kaka yake Mwenge jijini Dar es Salaam, na wakati huo alikuwa akiandika mashahiri na kuyatuma kwenye gazeti la Mzalendo na kuuza duka.Ndimara ndiye aliyefika nyumbani kwa kaka yake Mvungi , Mwenge na kumshika mkono Dk.Mvungi na kumpeleka katika gazeti la Mzalendo na kuwaomba wahariri wampatie kazi ya uandishi wa habari ambapo alipatiwa kazi na alifanyakazi katika gazeti hilo akiwa na rafiki yake ambaye naye ni mjumbe wa Tume ya Mabadilko ya Katiba, Profesa Paramagamba Kabudi ambaye naye pia hakuwai kusomea uandishi wa habari lakini alikuwa ni mwandishi wa habari na mwisho wa siku Profesa Kabudi na Dk.Mvungi waliamua kwenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kusoma sheria na mwisho wa siku walifaulu vizuri uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ukawapatia ajira ya kuwa waadhiri wa sheria wa chuo hicho hadi miaka ya karibu Dk.Mvungi alipostaafu utumishi wa serikali. 

Dk.Mvungi pia alikuwa akinieleza kuwa hawezi kumpinga adharani Balozi Mahalu kwani balozi Mahalu akiwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ndiyo aliidhinisha Dk.Mvungi na wenzake waende kuongeza shahada nyingine ya sheria nchini Ujerumani.Nakusema anawaheshimu sana. Kweli maneno yanaumba.Mara zote Dk.Mvungi alikuwa akimweleza mwanae mkubwa ambae ni Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB), Dk.Natujwa Mvungi siku akifariki ,mkewe mdogo yaani mimi Happiness Katabazi ambaye mara zote alikuwa akipenda kuniita ‘First Lady’ nitaandika makala ambayo itamuelezea yeye alikuwa ni mtu wa aina gani katika dunia hii na tulikuwa tukicheka Dk.Mvungi akisema hivyo na mimi nikawa ninamwambia ata akifariki ghafla tayari nina picha zake nyingi tulizopiga pamoja kwahiyo sitapata shida ya kutafuta picha zake hizo na kweli limetimia. 

Tangu nianze kuwa karibu na Dk.Mvungi kama mzee wangu mwaka 2000- 2013 ,pamoja na mambo mengi alikuwa akinieleza kuwa enzi zaDk. Eliuther Kapinga, mwaka 2002. Kapinga aliuawa kikatili kwa kunyongwa shingo na kupigwa nondo kichwani nyumbani kwake, Mbezi Beach. 


Katika ujana wake Dk.Mvungi alikuwa akinieleza kuwa alikuwa akipenda sana kucheza mchezo wa ngumi na hadi hivi sasa Dk.Mvungi alikuwa akifanya sana mazoezi ya viungo na muongozaji mzuri tu shughuli katika sherehe na misiba. Na hata harusi ya Profesa Kabudi na mkewe ,ni Dk.Mvungi ndiye alikuwa MC wa harusi hiyo. Si hivyo tu hata Chuo Kikuu cha Bagamoyo ambacho kinatarajia kufanya mahafali yake ya kwanza tangu kilipoanzishwa rasmi mwaka 2011, kilikuwa kimepanga Dk.Mvungi ndio awe MC wa mahafali hayo lakini kwa bahati mbaya akakutwa na mkasa huo uliosababisha afariki dunia.Dk.Mvungi ameniuma sana jamani. Itakumbukwa kuwa katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005.

Dk.Mvungi alikuwa ni miongoni mwa wagombea urais.Itakumbukwa kuwa uchaguzi wa mwaka 2005 ulisogezwa mbele kwasababu aliyekuwa mgombea mwenza wa Chadema, alifariki dunia.Katika raundi ya kwanza ya kampeni, aliyekuwa mhariri wangu wa Gazeti la Mtanzania , Gabriel Athuman alinipanga niongozane na Augustine Mrema (TLP)katika kampeni zake ambapo nilizunguka na Mrema katika mikoa 15 kama mwandishi wa habari wa mgombea urais kwa tiketi ya TLP. Tume ya ya Uchaguzi ikasimamisha kampeni kwaajili ya kifo hicho, ilipokuja awamu ya pili ya kampeni, Mhariri wangu Gabriel Athuman ambaye kwasasa anafanyakazi katika Ofisi ndogo za CCM, Lumumba Dar es Salaam,aliniondoa kwenye timu ya Mrema ambaye naye Mrema na mkewe Rose walikuwa wakiniita mimi ni First Lady wa Mrema, na kunipeleka kujiunga kwenye timu ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi ambaye ni Dk.Mvungi. 

Kweli nilikuwa ni mwandishi wa habari wa kike peke yangu katika timu ya waandishi wa habari zaidi watano wanaume na tulifanyakazi yetu vizuri na Dk.Mvungi akawa anajigamba mbele ya Mrema kuwa amemwibia mke yaani mimi enzi hizo nikiitwa ‘First Lady wa Mrema’, na kwamba hivi sasa Happiness ndiye mke wa Dk.Mvungi kwasababu tu mhariri wangu amenipanga mwandishi wa kik kwenye msafara wake na jina hilo la First Lady liliasisiwa na Dk.Mvungi na mkewe Anna katika msafara wake ambao tulizunguka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar akiomba kura kwa wananchi ili awe rais wa Tanzania. 

Lakini kura hazikutosha kwa upande wake , kura zilitosha kwa mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ambaye alitangazwa kuwa rais. Dk.Mvungi hakuwa na kinyongo na Rais Kikwete kushinda naninakumbuka baada ya Dk.Mvungi kumaliza kampeni aliathirika sana kiuchumi , sikumtupa nilikuwa naye katika shida na raha kwani nilipokuwa nafika ofisini kwake mimi ndiyo niligeuka kuwa mhudumu , karani mpokeaji wageni wake kwa kipindi hicho chote ninachokuwa ofisini wake. Ilipofika katika kampeni za uchaguzi mkuu wa wa Urais mwaka 2010, Dk.Mvungi hakugombea na mimi nikiwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima, aliyekuwa Mgombea Mwenza wa CCM, Dk.Mohammed Gharib Bilal aliiomba ofisi yangu iniruhusu niingie kwenye timu yake ya kuripoti mikutano yake ya kampeni ambapo tulizunguka nae mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar , na nilikuwa mwandishi wa kike peke yangu na wanaume watatu. Kampeni hiyo ya Dk.Bilal ambaye kwa sasa ndiye Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilisababisha kwa miezi mitatu niwe mbali na Dk.Mvungi hali iliyosababisha Dk.Mvungi kuwa ananipigia simu ya kunitania huku akilalamika kuwa Dk.Bilal ametumia madaraka yake vibaya amempora ‘First Lady wake‘ ‘Happiness), yaani mimi na kwamba anakusudia kumfungulia kesi madai Dk.Bilal kwa kumpora mkewe. Baada ya kampeni za 2010 kumalizika nikarejea mtaani na nikawa naona mara kwa mara na Dk.Mvungi na kumpatia ‘umbea'unaondelea mitaani nay eye ananipatia taarifa za hali ya kisiasa nchini na huko mikoani walikokuwa wanazunguka wamepata maoni gani ya wananchi. 

Lakini ghafla nikamsikia mtu ambaye mimi na Dk.Mvungi tumekuwa tukimuita kwa utani kuwa ni mwizi wa kura za Dk.Mvungi mwaka 2005 na kwamba Dk.Mvungi ndiye alishinda kiti hicho cha urais ila kura zake ziliibwa, yaani Rais Jakaya Kikwete kamteua Dk.Mvungi kuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Sote vijana wake tulifurahia uteuzi huo na kumtakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya na mara kwa mara nimekuwa nikienda kumtembelea katika ofisi hizo za Tume. Mara baada ya kuteuliwa tukawa hatuonani mara kwa mara kama zamani kwani alikuwa akizunguka mikoni kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba mpya. 

Nilikuwa nikimtania kuwa namimi nakusudia kumshitakiwa Rais Kikwete kwasababu amesababisha ndoa yangu na yeye isambaratike kwasababu tangu apewe ofisi eneo la Posta Mpya karibu na Ikulu, sisi watu wa karibu naye tumekuwa hatumuoni mara kwa mara kwani amekuwa amaliza muda mwingi kwenye vikao vya tume na kusafiri mikoani kukusanya maoni.Tunacheka baada ya kutaniana hivyo kishatunaendelea na majadiliano yetu.

Dk.Mvungi ameniuma. Kwa wanaomfahamu Dk.Mvungi watakubaliana na mimi kuwa kama Taifa tumepoteza mtu aliyekuwa na mchango mkubwa sana hakika wasomi wa kozi ya sheria na kozi ya Uongozi na Utawala ambao walikuwa wakifundishwa na Dk.Mvungi,wale waliokuwa wakitetewa bure kesi zao mahakamani na Dk.Mvungi watakubaliana namimi kuwa wahuni wale wamemuua kikatiri na kinyama mpenzi wetu ambaye bado tulikuwa tukimuitaji. Baada ya uchaguzi mkuu wa 2006, Dk.Mvungi alikuwa ananiambia ametikisika kiuchumi hivyo ‘First Lady wake nisirubuniwe na mafisadi nikamtelekeza.Na alikuwa akiniambia kuwa nimepata mume mwenye kichwa kikubwa ambacho kina akili na kinafikiri sawa sawa. 

Alivyorudi kufundisha UDSM kufundisha na nilipokuwa naenda ofisini nakaa nae hadi wakati mwingine saa tano usiku na kisha dereva wake Emma anamrejesha Dk.Mvungi nyumbani kwake Chuo tunamuamsha mke wake Anna anamfungulia mlango na kisha anamwamuru dereva wake anirejeshe nyumbani, nilikuwa nikimshuhudia Dk.Mvungi pamoja na kazi nyingine alikuwa akiniambia anakiunda Chuo Kikuu cha Bagamoyo , kwani anautaalamu huo na kweli alikuwa akiandaa chuo hicho akishirikiana na Balozi Mahalu mimi nikiwa shahidi wa mchakato huo kwani wazo la kuanzishwa chuo hicho ni la Mahalu na Dk.Mvungi na kweli walifanikiwa hadi chuo kikaanza kufanyakazi. Kwa ufupi Dk.Mvungi muda wake mwingi alikuwa akiumalizia kazini, kujisomea, kutoa ushauri wa kisheria kwa vyama vya siasa,wananchi waliokuwa wakiito huduma hiyo na wengine walikuwa hawana fedha za kumlipa alikuwa akiwatetea bure mahakamani,alikuwa ni mtu mwenye fikra za kimageuzi,hakupenda madaraka yeye alikuwa akinieleza kuwa anapenda kuwasaidia watu kupanga mikakati safi ili watu hao waweze kupata madaraka,aliweka mbele maslahi ya wanyonge na hakuwa mtu mwenye kuwa na tamaa ya fedha na siku zote alikuwa akisema yeye hatembei wala kushika fedha,fedha zake kidogo alizokuwa nazo zinashikwa na mkewe Anna. 

Oktoba 29 mwaka huu,ndiyo ilikuwa ni siku yangu ya mwisho kukutana na kuzungumza kwa zaidi ya saa tatu na Dk.Mvungi ofisini kwake Tume ya Mabadiliko ya Katiba na tulipiga picha za kumbukumbu ya yeye kuwa katika ofisi hiyo mpya, nilipomtembelea ambapo nilifuatana na mdogo wangu Michael Machali alisema yeye yupo kwenye Tume hiyo kwaajili ya kukakikisha watanzania wanapata Katiba bora, na kwamba atatumia taaluma yake ya Sheria ya Katiba kuiwezesha Tume ya Jaji Joseph Warioba kufanikiwa na licha anaishi Kibamba ila anafika ofisini hapo saa 12 asubuhi na kuondoka jioni .

 Kumbe ndiyo ilikuwa ni siku yangu ya mwanzo na mwisho ya kumuona na kumsikia hapa duniani Dk.Mvungi.Dk.Mvungi umeniuma sana. Dk.Mvungi siku hiyo alitueleza na mdogo wangu kuwa siyo kwamba hapendi kuchukua muda mrefu kukaa na familia yake, bali dhamira yake imekuwa ikimtuma kutumia muda mwingi kwenda ofisini kuwatumikia watanzania na mara zote alikuwa akimsifu na kumheshimu Mwalimu Julias Nyerere kuwa Mungu alikuwa amewaletea watanzania kiongozi mwenye maono. 

Dk.Mvungi umeniuma. Dk.Mvungi hakuwa mtu anayependa makuu licha alikuwa ni mtu aliyependa haki,kuwafundisha watu , ukweli na kusimamia kile anachokiamini bila woga na unafki. 

Katika miaka ya karibu Dk.Mvungi alikuwa akilalamika taaluma ya habari imekumbwa na mmomonyoko wa maadili hapa nchini, kwani baadhi ya waandishi wa habari na wahariri wao wamekuwa wakiandika habari ambazo azisaidii sana maendeleo ya nchi isipokuwa kuandika habari zinazojadili tuhuma ambazo wakati mwingine ni za uzushi tu kuhusu ufisadi wa kiongozi fulani na kwamba hivi sasa baadhi ya waandishi wa habari za ufisadi wamezigeuza kama ndiyo dini yao na mara zote akawa ananiasa na kunifundisha jinsi ya kujiingiza kwenye uandishi wa aina hiyo.

 Nafahamu kuna wanasiasa na mawakili leo hii watakuwa wanalia na kusaga meno kwasababu ya kifo hiki , kwasababu tulipokuwa wakiitaji kuandikiwa hotuba zao za kisiasa na kufundishwa jinsi ya kujenga hoja katika mijadala mbalimbali , kuwasilisha hoja mahakamani walikuwa wakimfuata Dk.Mvungi hata usiku wa manane na Dk.mvungi alikuwa akiwasaidia na hadi leo wanasiasa hao wamekuwa na majina makubwa sana hapa nchini ila sitawataja majina.Dk.Mvungi umeniuma.

 Kwa wale waasisi wa mageuzi wa nchi hii ambao hivi sasa ni wazee, hawawezi kumtaja Dk.Mvungi enzi hizo akiwa ni kijana mdogo ambaye alikuwa akishiriki kikamilifu kupitia taaluma yake ya sheria katika kuakisha Tanzania inaiingia katika mfumo wa vyama vingi. Mzee James Maparara, Mabere Marando, Dk.Ringo Tengo na wengine wanajua hilo kipindi kile wanaanzisha Taasisi ya TANLET, pia nimiongoni mwa waasisi waliokisuka Kituo cha Kutetetea Haki za Binadamu(LHCR) na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kupitia taaluma yake ya sheria.Dk.Mvungi umeniuma. Nalipongeza jeshi la polisi kwa hatua yake ya kuwakamata watu waliodai kuwa ndiyo waliomsababishia kwa makusudi kifo ‘Rais Mdhurumiwa’.


Naomba jeshi la polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi kufanya kazi yao ya upelelezi ,kukusanya ushahidi thabidi na kuandaa mashitaka kwa uweledi na kisha kuwafikisha mahakamani kwani endapo watakurupuka katika kuiandaa kesi hiyo ni wazi mwisho wa siku washitakiwa hao watakuja kuachiriwa huru na mahakama. Dk.Mvungi ni mwanasheria wa kwanza kuuwawa kinyama Hapa nchini ni Dk. Eliuther Kapinga, mwaka 2002. Kapinga aliuawa kikatili kwa kupigwa nondo kichwani nyumbani kwake, Mbezi Beach. Lakini mwisho wa siku polisi na ofisi ya DPP walifanyakazi yao vizuri ambayo ilimshawishi Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ,Juxson Mlai kuwahukumu adhabu ya kifo.Nilipata fursa ya kuudhuria kesi hii mwanzo hadi mwisho wake.Ilikuwa ni majozi wakati washitakiwa hao wakijitetea kwani walikuwa wakieleza jinsi walivyoitoa roho ya Kapinga. 

Mwanasheria  mwengine ambaye pia alikuwa Mhadhiri wa sheria Mwandamizi wa UDSM ni Profesa Juani Mwaikusya ,Julai 14 mwaka 2010 naye alifariki kikatiri kwa kupigwa risasi akiingia nyumbani kwake eneo laSalasala, na hatimaye polisi ilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa na kesi hiyo ilifunguliwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 

Nimalizie kwa kusema kuwa Watanzania kama taifa hivi sasa miongoni mwetu wenye roho katiri na ambao mnafikiri mungu haoni ukatiri na madhira mnaowafanyia waja wake,mbadilike. Acheni hiyo tabia kwani mnatuweka roho juu wenzenu na kuanza kuishi kwa wasiwasi .Kubalini kuwa mungu yupo, tena hajazeeka wala kupofuka macho na mungu wa siku hizi ni kijana anatembea na IPAD ameiunganisha na Wireles na anafanya mambo yake kisasa na analipa malipo hapa hapa dunia tena haraka sana, na nyie ipo siku atawaadhibu pamoja na vizazi vyenu.

Laiti mngetambua umuhimu wa Dk.Mvungi hapa duniani aliokuwa nao msingethubutu kumtendea unyama ule.Mmemuuzia na kumuua Dk.Mvungi lakini nataka mtambue kuwa mtasababisha watu wengi waliokuwa wakimtegemea kutokana na mchango wa kazi yake waathirike zaidi na wengine waondoe kesi zao mahakamani kwasababu wamekosa wakili wakuwawakilisha mahakamani bure. 

Nchi hii hivi sasa badala ya watu kuumiza vichwa kubuni mambo ya maendeleo kama kuanzisha viwanda vya kutengeneza magari, ndege,Laptop sisi ndiyo tumekuwa vinara wa kubuni mipango mkakati na endelevu ya kufanyiana vitendo vya kikatili vya kutupia majini kwa bei nafuu, kumwagiana tindikali, kutekana na kujeruhiana kwa mapanga, kuzulia uongo, fitna. Tabia hizi ni mbaya sana na zinatisha kwani wahalifu hawa siku hizi wala hawakusubiri njiani wanakufuata nyumbani wanakufanyia unyama. Mmekatisha kikatiri maisha ya Dk.Mvungi ambaye alikuwa anategemewa na familia yake ikiwa ni pamoja na kuwalipia ada za shule watoto wake, kumtunza mkewe Anna na kuwapa mwongozo wanae.Dk.Mvungi ameniuma. 

Dk. Mvungi ameacha mke na watoto watano. Alizaliwa Novemba mosi 1952. Mwaka 1994 alitunukiwa Shahada yake ya Udaktari katika fani ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Hamburg, Ujerumani. Mwaka 1987 alipata Shahada ya Uzamili ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM); mwaka 1981 alipata Shahada ya Kwanza ya Sheria UDSM. 

Dk. Mvungi hadi mauti yanamkuta alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu (LHRC). Mmwaka 1995 hadi 2008 alikuwa Mtetezi na Mtafiti Mkuu wa Sheria na Haki za Binadamu katika Mradi wa Kituo cha Kutetea Haki za Wafugaji. Aliwahi kuwa wakili kutoka LHRC katika kesi ya Kikatiba ya kutetea wananchi wa Kijiji cha Nyamuma. Mwaka 2000 hadi 2003 alikuwa Mkaguzi wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda na mwaka 2003 alishika wadhifa wa kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria UDSM. 

Daima Dk.Mvungi nitakukumbuka kwa mambo mengi likiwemo pia vazi lako la suti kwani nitofauti sana na aina ya suti zinazovaliwa na wanaume wengi, ni wanaume wachache sana wanaovaa aina ya mtindo wa suti alizokuwa anavaa Dk.Mvung na aina ya maisha uliyokuwa ukiishi.Vijana wako umetufundisha mengi mazuri tutayafuata na mabaya tuyaacha. 

0716 774494 
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Novemba 14 mwaka huu 2013.
0716 774494: www.katabazihappy.blogspot.vom






No comments:

Powered by Blogger.