Header Ads

MADEREVA WAMEBANA WAMEACHIA



Na Happiness Katabazi

LEO chama cha Umoja wa Madereva nchini umetangaza kusitisha mgomo baada ya kumaliza majadiliano na serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuzungumza nao kuaidi kupeleka matatizo ya madereva serikali ilizifanywie Kazi.

Hatua hiyo ya kuungwana na ambayo umeonyesha sasa Yule shetani Aliyekuwa akiwakabili madereva wao na kuwatumia Kutenda tendo lile la kishetani la kugoma kuendesha mabasi na kusababisha watu wa Mungu wateseke ni aibu na fedhea kwa wale wanasiasa waliokuwa wakiratibu mgomo huu na ni aibu pia kwa madereva hao  ambao ni wanaume na ndevu zao lakini walikubali kushikiwa akili na wanasiaa walikuwa kugeuzwa Kama chapati na wanasiasa hao mashetani kugoma kufanyakazi

Kwa hapa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda na maofisa wengine walifika katika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo na kufanya mazungumzo na madereva na wamiliki wa mabasi kwa saa kadhaa ambapo kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vimesema serikali imeyapokea madai yao na itayafikisha sehemu husika.

Wakati Makonda Leo akifanya Mkutano na madereva Hao ,Jana madereva Hao waliogoma Kwenda kuzungumza na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakidai hawana Mualiko wa kimaandishi na wakataka yeye ndiyo awafuate Katika Kituo cha Mabasi Ubungo .

Pinda  Leo hakwenda amekwenda Makonda na akafanikiwa kuzungumza kwa kuwapa ahadi a kufikisha kilio chao Katika mamlaka husika na hatimaye uongozi wa madereva ukawataka madereva wenzake waanze Kazi na kweli wameanza Kazi.

Lakini kule Mkoani Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Liberatus Sabasi yeye alichukue hatua za kisheria na madereva walisalimu amri na kuanza kutoa huduma ya usafiri tangu Jana hadi Leo huko Arusha kulikuwa Hakuna mgomo.Nampongeza Kamanda Sabasi na Timu yake.

Jana niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho ( KWANINI SERIKALI INA PEMBELEZA PENZI KWA MADEREVA?).

Ndani ya makala hiyo niliandika mambo mengi ambayo niliishutuhumu serikali na madereva pia na Kuonyesha wasiwasi wangu Kuwa isijekuwa mgomo huu pia unasiasa chafu ndani yake.

Wako walioiunga  mkono makala hiyo na wapo walioipinga ,lakini waliyopinga walishindwa kunipa Sababu za Msingi za kuipinga zaidi kutoa porojo tu ambazo  zilishindwa kuvunja uhalali wa makala yangu ya Jana ambayo ndani ya makala hiyo nilihoji iweje Madai ya madereva Hao yashike Kazi Kipindi hiki wakati taifa linaelekea Katika uchaguzi Mkuu na wananchi wanajiandikisha Kwenye daftari la Wapiga kura?

Baadhi ya madereva ambao hawaungi mkono mgomo huo walinipigia simu na Kusema mgomo huo  ni mgomo ambao unachochewa na wanasiasa wa Chama Kimoja cha siasa na kwamba wao walichoamua wanakaa majumbani Kwao hawapendi kuungana na madereva wenzao ambao wamekubali kutumiwa na wanasiasa kuendesha mgomo huo haramu.

Na nikweli kuna taarifa za chini chini zinadai Chama cha Chadema  kinadaiwa Kuwa nyuma ya mgomo huo licha hadi sasa bado Chama hicho hakijakanusha.

Na Leo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA), Freeman Mbowe alifika Katika Kituo na mabasi Ubungo lakini hakupewa nafasi ya kuwahutubia madereva wale licha wakati akiondoka, umati ule wa madereva ulimshangilia sana.

Hakuna Sheria yoyote inayokataza Mbowe asiende pale Kituo cha Mabasi Ubungo, lakini watu wenye akili timamu wanajiuliza hivi kwanini aende Leo Katika eneo Hilo la mgomo? Kwanini asiende eneo Hilo Kipindi ambacho madereva walikuwa hawajagoma?

Mbowe Hana mamlaka yoyote ya kidola ya kuweza kutatua matatizo ya madereva wale Kwanini madereva wale wakamshangilia  sana Mbowe na siyo viongozi wa dola ambao ndiyo hasa wenye mamlaka ya Kiserikali ya kutatua matatizo Yao na kuwafikisha matatizo Yao Katika meza ya serikali na kuyatatua?

Hawa madereva walikuwa wakimtaka Pinda wala waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta hawakwenda kuzungumza nao leo serikali ikamtuma Makonda na Makonda alifika pale kwenda kuzungumza nao na kuna makubaliano yalifikiwa kwa ahadi ya kufanyiwa kazi na hatimaye madereva wakarejea kazini?

Hivi Mbowe alikwenda katika eneo lile eneo la mgomo kama nani?Hivi Mbowe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yoyote inayohusiana na masuala ya Uchukuzi  hadi aende Katika mgomo ule?

Kwani wenyeviti wa vyama Vya upinzani Kama Augustine Mrema, John Cheyo, James Mbatia ,Ibrahim Lipumba na wengine Wengi Mbona hatukuwaona Leo wakifika Katika eneo Hilo?

Kwani mkusanyiko huo wale madereva Leo asubuhi  ulikuwa ukiropoka maneno haya ' CCM Tumeichoka' na Mbowe alipoingia na kutoka eneo Hilo Maderva Hao walikuwa wakimshangilia na madereva Hao  kumuonyeshea harama ya vidole viwili ambayo ni salamu inayotumiwa na Chadema? 

Kwanini waliokuwa wanafanya uhuni wa kurushia Polisi mawe,na kukatisha MADERW waliokuwa wapo Tayari kuendesha Magari ,kwanini vijana Hao Hao waliopokea Mbowe nakumsukuma Mbowe.je huu Sio ushahidi wa mazingira wa Kuonyesha Chadema sana usika Katika huu mgomo.

Jana nilisema mgomo huu ni wa kihuni kwa Sababu mhuni yoyote anatumia njia za kihuni Kudai anachodai na walichokifanya  baadhi ya madereva hao ni uhuni Kwani upande wa serikali ulikuwa radhi kuzungumza nao na Jana Waziri Mkuu Pinda alichukua  Hatua kwa Kuunda Kamati ya Kuchunguza mgogoro .

Lakini  madereva hao walipuuza uamuzi huo wa Pinda Matokeo yake eti Leo wamekubali mazungumzo waliyoyafanya na Mkuu wa Wilaya Makonda ambaye hayo waliyoyayajidili  na Makonda mwisho wa siku yatafikishwa mezani kwa Pinda ambaye Jana waligoma kwenda kuzungumza nae.

Ni  Ujinga wa aina yake unamdharau Na kukataa kumsikiliza Baba mwenye nyumba (Waziri Mkuu) halafu unaenda kumpelekea shida zako kwa mtoto wa baba mwenye nyumba yaani ni (Mkuu wa Wilaya).

Na Ujinga huu utadumu vichwani Mwao endapo wataendekeza tabia ya kukataa kwenda shule.

Hii ni Mara ya pili kwa viongozi wa serikali kwenda kuzungumza na madereva wanaogoma ,Mara ya kwanza kwa Mwaka huu ilikuwa ni ule mgomo uliofanyika Aprili Mwaka huu ambapo serikali ilimtuma Waziri wa Kazi na Ajira ,Gaudensia Kabaka na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ambao walifika na kuzungumza nao lakini Jana na Leo madereva Hao wakaibuka na mgomo Mkali kuzidi mgomo wa awali.

Hakuna ubishi Kuwa mgomo wa mabasi wa Jana na Leo umeleta Usumbufu mkubwa kwa wananchi na hata kuwathiri Biashara za watu  wakati Kumbe madereva hawa walikuwa wanaweza kutumia njia ya busara Kama hii ya kukaa mezani na serikali na kuzungumza nao.

Ndiyo maana Katika makala yangu ya Jana nilisema haina maana yoyote ya mtuhumiwa wa Kesi ya kuua kwa kukusudia halafu akiri kosa Hilo ,haitasaidia kurejesha Uhai wa marehemu.

Sasa ndiyo Kama uhuni uliofanywa na madereva hawa wa kuwaletea Usumbufu wananchi kukosa usafiri ,na dhiki za kila aina hata madereva wakituomba msamahaa Leo haitatusaidia.

Nguzo Moja wapo ya binadamu ni Imani, ukishakuwa na Imani na upendo kwa mwenzio huwezi kumfanyia ubaya binadamu mwenzio wala kuruhusu binadamu mwenzio ateseke kwaajili yako ,Juzi na Jana madereva wale waliogoma Jana Imani iliwatoka ndiyo mAana wakatundea uhuni ule lakini Leo roho wa Mungu Na Hekima imewaingia wameamua kuachana ushetani wao wa mgomo wameamua kuachana na ushetani wa kugoma na hatimaye wameamua kutufi Kazini.

Kiroho safi napenda kupongeza Umoja wa Madereva kwa uamuzi wao wa Leo wa kukataa kuendelea kutumiwa na wanasiasa uchwara ambao wanataka kuingia madarakani kwakutumia njia dharimu Kama hizi za kuwatumia baadhi ya wananchi wenzetu kufanya matendo ambayo yanaumiza wananchi na mwisho wa siku wananchi Hao kutoka na mateso hayo ya migomo wanaamua kuichukia serikali iliyopo madarakani na Mwisho wa siku chaguzi zinapokaribia wananchi Hao wanaamua kupiga kura za Chuki kwa serikali zilipo madarakani.

Napenda kupongeza umoja wa Madereva kwa kuacha mgomo na kitendo hicho ni wazi sasa wameacha kuitumikia shetani wameamua kumtumikia Mungu maana siku zote Kazi ya shetani ni kuleta uharibifu na kweli mgomo mliojifanya Jana na Leo umelea uharibu kwa binadamu wenzenu.

Nawaasa madereva ,acheni kujazana Ujinga, nendeni shule kila mmoja kwa wakati wake ,msifuate Mkumbo Katika masuala Kama haya KWA taarifa yenu wakati Mlivyogoma kuna watu waliokuwa wakichochea mgomo huo walikuwa wamekaa Mbali wa nakunywa wine Nyie minapigwa mabomu na Polisi na kunyeshewa na Mvua Ubungo Terminal na kuishi kwa wasiwasi wa kusakwa na dola.

Narudia tena madereva acheni jeuri nendeni vyuoni mkasomd , mtakuja kunikumbuka muda simrefu mabasi ya Mwendo kasi yatakapoanza kufanya Kazi na hivi mmeishakiri adharani Hamtaki kwenda kusoma, waliisoma vizuri udereva Msije mkashangaa mwisho wa siku wao ndiyo wakaja kupata ajira Katika basi hayo , mtalia na nani?

Inawezekana Madai yenu madereva ni ya Msingi lakini Kwanini miongoni mnasalitiana na kuvujisha Siri Kuwa mgomo huo Una siasa chafu nyuma yake?

Njia mliyoitumia awali Kudai Madai yenu ni haramu, na Kama ni Waungwana na mnampenda Mungu kila mmoja atubu dhambi hiyo kwa Mungu wake.

Baadhi ya wanasiasa Ifike mahali sasa mjifunze kuanza kufanya siasa safi ambazo zinaleta tija kwa taifa na sio kuleta madhara kwa wananchi ,Kwani Hao wananchi mnao watumia kuendesha  migomo kila kukicha siku watawachoka na watawageuka na mfano mzuri ni wa Mbunge Godbles Lema wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema).

Ambaye  hivi  sasa wale waliokuwa wafuasi wake Katika Yale maandamano haramu aliyokuwa akiyaongoza kila kukicha, hivi sasa wamemgeuka na wanamuanika adharani na Ana hati hati ya kushinda tena Katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu, kwasababu Watanzania hawataki vurugu.

Nimesema Madereva Wamebana wameachia kwasababu walijiapiza Kuwa watagoma wiki mzima mfululizo lakini hatimaye Leo wametangaza kusitisha mgomo huo ambao ili ingia siku ya pili kwasababu hiyo lilekusudio Lao la kugoma muda mrefu hawajalitimiza na huo Ndio ungwana Kwani Muungwana Asifiwi  ushenzi.

MITHALI 4:13-14 ( mkamate sana elimu usimuache aende zake Mshike mAana yeye ni uzima wako. us iingie Katika njia ya waouvu ,wala usitoe bee Katika njia ya wabaya.

 Quranii inasema (usome ili uweze kuitawala Dunia yako).

Mtu yoyote  asiyetaka  kusoma Atakuwa Kama Funza hajui Zuri  limfahalo binadamu mwenzio.

Mungu Ibariki Tanzania.

Facebook: Happy Katabazi
Mei 5 Mwaka 2015.














No comments:

Powered by Blogger.