Header Ads

LAWRENCE MASHA KORTINI KWA LUGHA CHAFU



LAWRENCE MASHA KORTI KWA LUGHA CHAFU

Na Happiness Katabazi

ALIYEKUWA  Waziri wa Mambo ya Ndani na sasa ni Kada Mpya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wakili Lawrence Masha amefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Leo akikabiliwa na kosa Moja tu la kutoa chafu maofisa wa Jeshi la Polisi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, Wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi alidai Kuwa Kesi hiyo ya jinai Na.190 ya Mwaka huu, mshitakiwa ametenda kosa Hilo la kutoa lugha chafu kinyume cha Kifungu cha 89(1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.

Wakili Kishenyi alidai Kuwa Agosti 24 Mwaka huu, ndani ya Kituo Cha Polisi Oysterbay  Jijini Dar Es Salaam, Masha ambaye ni Wakili kitaaluma alitumia lugha chafu dhidi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Juma Mashaka na maofisa wenzake wa Polisi kwa Kuonyesha Kuwa Juma na maofisa wenzake wa Polisi Kuwa ni ' washenzi na waonevu hawana shukrani,huruma wala dini maneno ambayo yalikuwa yanataka kuatarisha Amani. 

Hata hivyo Masha alikanusha kosa Hilo na Hakimu Lema alisema ili mshitakiwa Huyo apate dhamana ni lazima awe na wadhamini Wawili watakao saini bondi ya sh.milioni Moja.

Baada ya Hakimu Huyo kutoa Masharti hayo upande wa jamhuri uliomba muda utahaki barua za wadhamini na muda ulikuwa umeishakwenda hivyo Hakimu Lema akaairisha Kesi hiyo hadi Septemba 8 Mwaka huu,kwaajili ya kutajwa na akaamuru mshitakiwa apelekwe gerezani kwasababu Masharti ya dhamana bado hayajatimizwa.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg:www.katabazihappy.blogspot.com

071











No comments:

Powered by Blogger.