Header Ads

MAGUFULI TUOKEE SINZA VUMBI LINATUTESA


Na Happiness Katabazi

AWALI ya yote napenda kutangaza maslahi yangu Katika makala hii kuwa Mimi ni miongoni mwa wakazi wa Mtaa wa Sinza C ,Kata ya Sinza Dar Es Salaam, ambapo Nyumba zetu zimetazamana uso kwa uso na Kituo kipya cha Daladala  Simu 2000 na ni muathirika mkubwa wa vumbi.

Kituo hicho cha mabasi ambacho pia kumepakana na Shule ya Sheria nchini, ni kipya na kimejengwa hapo baada ya kilichokuwa Kituo cha mabasi Ubungo kuondolewa ndiyo kikaamishiwa hapo.

Kilipoanza Kazi rasmi Kituo hicho cha mabasi simu 2000 ,Makala yangu ya Oktoba 28 Mwaka 2014 iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho ; ( MANISPAA YA KINONDONI MTATUUA KWA TB).

Makala hiyo na ile Habari ya kupongeza serikali kuamishia Kituo hicho hapo zote niliziifadhi Katika ukurasa wangu wa Facebook book .

Na ndani ya makala hiyo niliomba serikali ijenge barabara hiyo kwa Kiwango cha lami kipande cha barabara kutoka Kituo cha Basi Mawasiliano kilichopo katika  Barabara  ya Samnujoma karibu na Kituo cha watoto yatima (SOS VILLAGE ) hadi Barabara ya Shekilango Katika Kituo cha basi Shule ya Mugabe Kwani kipande hicho cha barabara ndicho kinachotumiwa na madaladala kuingia na kutoka Katika Kituo hicho cha mabasi cha Simu 2000.

Nirejee Katika mada yangu ya Msingi. .5/12/2015   alfajiri Gari kubwa lilopita Katika kipande hicho cha barabara kama kawaida yake na kuchonga hiyo barabara ambayo ni ya vumbi na Kisha kuondoka bila hata kumwagia Maji.

Na hiyo siyo Mara ya kwanza ni zaidi ya Mara Sita sasa tangu Kituo hicho Kujengwa hapo, Gari kubwa linakuja kufanya danganya toto kinachoangaliwa barabara likishamaliza Kuchonga hiyo Barabara wakazi wa eneo tunaanza kuteseka kwa vumbi nje na ndani ya nyumba hata udeki Mara nne kwa siku ni Kazi bure.

Wananchi wa eneo hili Tumeishalalamika weee bila mafanikio ,hatusikilizwi tunazidi kuteseka na vumbi ambalo hadi hivi sasa makabati ya nguo ,makapeti, nguo ukifua ukianika nje ni Kazi bure vumbi la hatari watu wanaugua mafua, vikoozi,Hakuna Amani na Furaha tena kukaa eneo hili kwaajili ya vumbi hilo ambayo yanahatarisha   Afya za wakazi wa eneo Hilo.

Wananchi tunajiuliza hivi hawa viongozi wa Manispaa ya Kinondoni wanaakili timamu au ni wendawazimu? 

Hivi ni kwanini hata kwa wiki Mara mbili wasitoe Fedha wakaja Maji Kwenye Gari    likaja kumwagia Maji hiyo barabara hili vumbi litulie  wakati wakisubiri kama ni Fedha za Bajeti za Kuja Kujenga hiyo barabara ?

Ni mikusanyiko mangapi ya kodi Manispaa inakusanya  kila siku hadi washindwe kuleta Gari la Maji Lije limwagie Maji hiyo barabara vumbi litulie?

Mbona Fedha za kuweka mafuta Magari ya Kuja Kuzuia mama tilie wasipike Chakula wanazo?

Disemba 7 mwaka huu,  Askari polisi wa Kinondoni na watu wa Afya walifika eneo Hilo  lilopakana na Kituo hicho cha mabasi huku wakiwa na Mabunduki wakiwa wamebeba chupa zinazozaniwa zilikuwa na mafuta ya taa na kuanza kupita Kwenye vyakula vyote vilivyokuwa vimepikwa na Mama Ntilie Katika Migahawa hiyo na makarai yaliyokuwa yamefadhi mafuta ya kupitia Chips na chips zenyewe na kuanza kumiminia humo Kwenye vyakula vimiminika hivyo kwa Madai Kuwa walishawapa mapema taarifa mama Ntilie wasipike kuna kipindupindu lakini wakakaidi.

Hata hivyo dakika Chache baada ya askari Polisi kumaliza kuwatia Hasara mama Ntilie Hao ambao waliingia Hasara kweli na wa kamwaga Chakula na kuanza kupika tena .

Mama Ntilie hao Walisema wataendelea na Biashara hiyo kama kawaida Kwani ni Rais John Magufuli Katika kampeni zake alisema akiwa rais ataakikisha mamtilie hawatabughudhiwa  sasa wa nashangaa Polisi wanawabughudhi.

Na Mamantilie Hao ambao nilipata fursa ya kuwahoji Walisema wa nashangazwa na Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kuwazuia wasipike kwakisingizio eti cha ugonjwa wa Kipindupindu wakati wao wanafanya shughuli ya Mama Ntilie Katika mazingira safi kwa kiasi Fulani  isipokuwa tu ni vumbi linalotokana na hiyo barabara ya vumbi ambayo inatumiwa na Magari mengi muda mwingi hivyo linatibuka.

Hivi Manispaa ya Kinondoni Kipindupindu ndiyo mnajifanya mnakiogopa sana kuliko Maradhi kama vifua vikuu, vikoozi na uhalibifu wa Mali za watu kutoka na vumbi ambalo Nyie Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kama mnawatumishi wanaofikiri sawa sawa vichwani mnawaweza kulidhibiti vumbi Hilo lisiendelee kuwanatesa wananchi wenu wa eneo Hilo?

Sisi tunaitaji lami hatuitaji danganya toto ya kutuletea Hilo Ligali Lenu Lije alfajiri kama Wachawi litifue barabara na Kisha kutuachia vumbi Hilo ambalo linasababisha watu Kuishi kwa mateso na bila raha ndani nje ya maeneo hayo ya nyumba zao.

Mbona mmiliki wa Hoteli ya City Style,Picknick Villa wameweza Kuwa Kila asubuhi kumwagilia Maji eneo Lao linalopakana na Hoteli zao tu ili kudhibiti vumbi na wamefanikiwa kwa kiasi Fulani.

Nyie serikali ambao Kutwa mnakusanya kodi kitu gani linawashinda kutumia akili na sehemu ya kodi kujaza Maji Katika Gari na Kuja kumwagia kipande kile  cha barabara hili Nasisi tu nisikie kweli serikali inatujali?

Hivi kwanini mlikuwa na kihelehele cha Kujenga hicho Kituo cha mabasi wakati mkijua mlikuwa hamna Fedha za Kutengeneza hii barabara inayotumiwa na madaladala Kuwa Kiwango cha lami?

Mnatutesa na mmetutesa Vya kutosha.Wananchi wanalalamika watu tunakula na kuvuta na kugusa vumbi .Watu wanaugua  mafua, vikoozi Kutwa tunashindia na kulalia maziwa kwaajili ya kuhofia kupata TB kwasababu tunavuta sana vumbi.

Na kama Mimi ni muongo wa haya ninayoyasema kwamba wananchi wa eneo hili kwanza wamechoshwa na hiyo tabia ya kuona Hilo Gari linakuja kuchimba barabara kwa Madai eti kinachonga barabara ambapo hata hivyo likishachonga baada ya wiki Chache barabara Inaaribika tena .

Rais Magufuli tuma watu wako kimya kimya wafike eneo lote Hilo nililolitaja hadi Katika nyumba zilizopo kama na Mto Ng'ombe ,mjionee vumbi linanavyowatesa wananchi na wananchi wanalalamika sana ila malalamiko yako ni kama kilio cha Samaki Machozi yanaishia Baharini.

Na Mimi ni Mkazi wa muda mrefu wa maeneo hayo,eneo hili wakazi wake hawana historia ya uchafu wa kutililisha Maji machafu au kutupa taka ovyo ovyo au mama Ntilie kupika Katika mazingira machafu na hatuna rekodi ya watu kufariki kwa ugonjwa wa Kipindupindu.

Uchafu mkubwa unaowakabili wakazi wa eneo hili ni Hilo vumbi utafikiri kiwanda cha kuzalisha ciment ambalo vumbi  Hilo limeshika kasi baada ya Kituo hicho cha mabasi kufunguliwa, barabara hiyo ambayo siyo ya lami ilipoanza kutumiwa na Magari mengi na vumbi ndiyo likaanza kuongezeka na vumbi Hilo linaongezeka Mara Dufu na kutishia Usalama wa Afya zetu pindi Gari linalokaa Kuchonga barabara a.

 Rais Magufuli, sitanii ,Nasema ukweli, tunaomba utuukoee tunaangamia wenzio na Hali hii Leo hii watoto hawawezi kukaa hata barazani wanakaa ndani napo hata wakikaa ndani mambo ni Yale Yale vumbi kama tupo nje au ndani ya kiwanda cha kuzalisha cimenti.

Naandika makala hii kwa masikitiko makubwa, kweli tunaangamia wenzenu Tuokoeni.Naimani ombi langu Rais Magufuli na Timu yako mtalo fanyia Kazi maana Manispaa ya Kinondoni siyo kama anawachongea kwako ni wazi Hilo tatizo hawalii maanani wangekuwa wanalitia maanani basi wangejitutumua kwa kufanya kama wanavyofanya Wamiliki wa Hoteli ya City Style au Picknick Villa ambazo hoteli hizo zipo kando kando ya barabara hiyo ya vumbi kumwagia Maji hiyo barabara.

Nawatakia Watanzania wote sikukuu njema ya sherehe ya Uhuru wa Tanzania ninayofanyika Leo.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Facebook: Happiness Katabazi
9/12/2015.






No comments:

Powered by Blogger.