Header Ads

MAYAGE S MAYAGE UMENIACHIA KOVU LISILOFUTIKA


Na Happiness Katabazi

LEO  25 /12/2017  ikiwa Wakristo  Duniani  kote tunasherehekea Sikukuu ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo pia mimi Happiness Katabazi nasherehe siku ya kuzaliwa  ambapo leo natimiza umri wa miaka 38 toka nilipozaliwa  katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Dar es Salaam, 25/12/1979.

Lakini sherehe hizi Leo kwa upande wangu zimeingiwa na simanzi kufuatia Saa tano asubuhi  Mimi kuingia Katika group la Whatsup la waandishi wa Habari Tuliowai kuandikiaga Gazeti la Tanzania Daima,nikakutana na taarifa ya kifo cha Mhariri wangu wa zamani wa makala wa Gazeti la Mtanzania kati ya Mwaka 2003- 2006  na Mtani wangu Mayage S Mayage Kuwa amefariki Dunia.Taarifa ya kifo hicho iliwekwa Katika group Hilo na Mwandishi mwenzangu ambaye Niliwahi fanyanae Kazi Katika Gazeti la Tanzania Daima, na kwasasa yeye ni Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mtanzania, Charles Mulinda.

Nilimhoji Mulinda kupitia group Hilo la Whatsup Mara mbili Kuwa ni kweli Kaka Mayage kafariki ,akathibitisha Kuwa ni kweli amefariki Leo saa Tatu asubuhi katika Hospitali ya Misheni Mbweni alikokuwa amelazwa kwaajili ya matibabu.

Na dakika Chache baadae Mke wa marehemu Mayage, Dina Mayage naye aliandika ujumbe mfupi wa kuthibitisha kifo cha mumewe Mayage ambapo ujumbe huo uliingizwa Katika group Hilo na Mwandishi wa Habari mwenzangu ambaye Niliwahi fanyanae Kazi kama waandishi wa Habari Katika Gazeti la Tanzania Daima, Edmund Mihale.

Nilijikuta naanza kulia hapa kitandani kwa uchungu na Kusema Kwani Mayage amefariki tarehe ya Leo ya siku ya Christimas ambayo Mimi binafsi nisiku yangu ya kufurahi Kwani ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwangu ? Lakini mwisho Nikahitimisha kwa Kusema Nisiingilie mipango ya Mungu.

Kwa zaidi ya Mara nne Kabla Mayage anakumbwa na umauti Niliwahi kukutana na Mayage  ambaye salamu zetu tukutanapo kwanza yeye alipenda kuniita NYAMBIZI Ujambo?

Nami namjibu sijambo fisadi naendelea vizuri .Nilikuwa nikimwambia wazi wazi tena Mbele za watu Kuwa hapa nchini Mwariri wa makala za siasa ambaye Nina makubali na kuheshimu mno kwa uwezo wake ni yeye Mayage. Alikiwa akicheka huku akiendelea Kuvuta sigara yake na kugonga Bia yake .

Kwa wale wasiyomfahamu Mwandishi huyu Mkongwe nchini ,Mayage aliwahi andikia sana magazeti ya RAI , MTANZANIA  Enzi zile yakiwa chini ya Uongozi wa waandishi maarufu nchini Jenerali Twaha Ulimwengu, Salva Rweyemamu,Johnson Mwambo Enzi Utawala wa Rais Benjamin Mkapa na Kikwete.Aliandika sana makala Mtani wangu Mayage.

Hata hivyo aliwahi kuandikia magazeti mbalimbali likiwemo Gazeti la Raia Mwema .

Napenda kuweka wazi Kuwa hadi Leo hii nimekuwa Hodari wa kuandika na kufanya chambuzi za makala za siasa ni Mayage S Mayage Enzi zile akiwa ni Mhariri wa makala za Gazeti la Mtanzania  nikiwa ndiyo naanza kuchipukia Katika uandishi wa chambuzi za makala za siasa  alinipa fursa ya Kuwa naandika makala za siasa na nikizipeleka Katika Dawati lake anazisoma halafu ' anazichonga ' upya ,yaani anaziboresha kwa kuweka maelezo mengine ambayo Mimi kwasababu nilikuwa Mchanga na yeye Alikuwa mzoefu Katika uandishi /chambuzi za kisiasa  Kesho yake makala ilichapishwa gazetini unakuta makala yako imeboreshwa zaidi na anakuita kukuuliza umebaini nini Katika makala yako iliyochapishwa Gazeti namjibu kuna aya zimeongezwa na nzuri .

Hakika Mayage baadhi ya tabia zake nyingi tulifanana .Mayage hakuwa mnafki, muoga, Msema kweli ,muongeaji ,asiye mchoyo na kipaji chake cha uandishi wa habari na muwazi .Ndivyo Mimi nilivyo pia.

Mayage ni miongoni mwa waandishi wa Habari waliokuwa na kalamu Kali ambayo pia ilikuwa ikiwakera baadhi ya watawala wasiyopenda kukosolewa.

Pamoja na mapungufu yake mengine aliyokuwa nayo Mayage kama ni binadamu, nadiriki Kusema Leo hii ni Nadra mno Katika vyombo Vya Habari kumpata Mhariri au Mwandishi wa makala za siasa aina ya Mayage ambaye kichwani alikuwa anakumbukumbu za matukio mengi ya kiasia kichwani.

Mwaka 2005 ,Mayage ambaye ni Mwana CCM tukiwa naye pale Gazeti la Mtanzania, aliamua kwenda mkoani wako Kigoma Kugombea Ubunge jimbo lilokuwa likiongozwa na aliyekuwa Mbunge wa CCM, Kilosti Mporogomi .

Nilimshauri asiende Kugombea kwasababu nilikuwa najua hatoshinda kwasababu nilikuwa namfahamu Vyema Mbunge Mpologomi ambaye bado alikuwa anataka kuendelea mbunge wa jimbo Hilo hivyo alikuwa amejipanga, Mayage alikuwa ajajipanga na alikuwa Hana uwezo wa kifedha ,Mayage ha kunisikia akaenda Kugombea akashindwa Katika kura za maoni Mpologomi akashinda lakini hata hivyo Mpologomi naye hivi sasa siyo Mbunge tena.

Nakumbuka Mayage akiwa huko Kigoma Kugombea Ubunge jina lake lipitishwe na vikao Vya CCM, alikuwa akitigia simu Kulalamika anafanyiwa rafu za kisiasa na akawa anaomba msaada tumchangie Fedha za nauli za kurudi Dar Es Salaam, arejee Katika Kazi yake uandishi wa Habari na kwamba siasa haziwezi ataishia kuziandika tu.Kweli nilimtumia Sh. 30,000 kama mchango wangu kwake.

Alivyorudi Katika chuo chetu cha Habari Gazeti la Mtanzania Mwaka 2005 , nilipomuona  Niliangua kicheko kwasauti akaniita jina alilipenda kuniita " NYAMBIZI " , Kilonsti Mgologomi ni mtu hatari sana.Na akasema angesikiliza ushauri wangu niliyompa wa kumkataza asiende Kugombea Ubunge dhiki zile zisingemkuta.Ila akasema licha Ameukosa Ubunge kuna mengi amenifunza Kuwa ni Ngumu sana kupata madaraka ya Ubunge bila kutumia Fedha na mbinu.

Mayage Utakumbukwa na wanahabari wenzako,mchango wako Katika taifa hili kupitia kalamu yako / Habari na makala zako zisizo na idadi ni uthibitisho ambapo upo Katika maktaba Kadhaa.,familia yako na mashabiki wa makala zako.

Aidha Utakumbukwa na wagonga  glasi ' Wazee wa Kilauli' na wavuta Sigara wenzako. Mayage umeniachia Kovu lisilofutika Mtani wangu Kwani umekufa tarehe ambaye mimi ambaye umeniacha hai ni tarehe ambayo nakumbuka siku yangu ya kuzaliwa.

Mayage wewe Kwangu Mimi utabaki Kuwa ni Mhariri wa makala za siasa ambaye ulininoa Vyema kuandika makala na chambuzi za kisiasa Kwani ulinipa fursa wala hukunipana kama walivyo baadhi ya wahariri wengine ambao wamekuwa na tabia chafu za Kugandamiza waandishi wa Habari wa kike ambao wanawao wanafanya Vyema Katika fani ya uandishi wa Habari Kwani muda wote Mayage ulikuwa ukinitia moyo Kuwa ipo siku nitakuja Kuwa Mwandishi mzuri wa makala za kisasa na kweli Hilo limetimia.

Mungu aiweke roho ya Mwandishi wa Habari Mayage S.Mayage Mahali panapostahili.

CHANZO:
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
25/12/2017

No comments:

Powered by Blogger.