SERIKALI ISIKUMBATIE WAWEKEZAJI WABABAISHAJI

Na Happiness Katabazi

SERIKALI imeamua kuikopesha kampuni ya (TRL) Sh.bilioni 3.6 kwa miezi mitano sawa na Sh milioni 700 kila mwezi ili iweze kuwalipa wafanyakazi wake.

, baada ya kudai kuwa haina uwezo wa kuwalipa kima cha chini Sh.160,000 hali iliyosababisha wafanyakazi kugoma.

Imefikia hatua hiyo ,baada ya kampuni hiyo kudai kuwa haina uwezo kuwalipa wafanyakazi wake kima chini sh 160,000.Hali iliyosababisha wagome kufanya kazi.

Aliyetangaza kuikopesha TRL ni Waziri MKuu, Mizengo Pinda , wakati akijaribu kumaliza mgogoro wa mgomo wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo.Hapa nadhani Pinda alilazimika kukubali serikali kubeba mzigo huo ili kuwalainisha wafanyakazi warejee kazini.

Pinda alilazimika kuingilia mgogoro wa wafanyakazi na menejimenti ya TRL baada ya wafanyakazi hao kugoma mwanzoni mwa mwezi huu wakidai makato ya mshahara wao.

Menejimenti ya TRL ilishwa kuwalipa kima cha chini cha Sh 160,000 kama ilivyokuwa imeahidi Machi mwaka huu.

Katika mkataba uliofikiwa baina ya wafanyakazi na menejimenti ya TRL, mshahara mpya ungeanza kutolewa Machi mwaka huu.Mshahara huo ulikuwa ukipanda kutoka sh 87,000 hadi sh 160,000.

Inawezekana Watanzania tumeungalia mgomo ule kama ni wawafanyakazi kudai maslahi yao tu, tukaacha hoja kubwa kuhusu mwenendo wa ubinafsishaji wa mashirika ya Umma .Shirika la reli likiwa ni moja wapo.

Tayari tulishaandika kueleza kwamba sera ya ubinafsishaji wa mali za umma ni mbovu .Ubovu wa sera ile upo, umejikita kwenye msingi wa kuabudi na kutukuza wawekezaji toka nje badala ya kutegemea kwanza nguvu za wananchi.

Nakuona jinsi nguvu hizo zikiwekwa pamoja zinaweza kuzaa mtaji mkubwa kuliko mitaji wanayoweza kuleta mwekezaji yeyote.

Hivyo basi tulikosea tulipo binafsisha mali zetu kwa wageni bila kuangalia kwanza uwezekano wa sisi wenyewe kujibinafsishia sekta hizo.

Somo kuu ni Benki ya Taifa ya Biashara(NBC),TTCL na mashirika mengine ambayo tuliwapa wawekezaji kwa bei ya kutupa mithili ya bei ya nazi sokoni wakati mtaji wa kuyaendesha tunayo.

Shirika la Reli limebinafsishwa kwa kampuni ya TRL kampuni ambayo haina sifa katika Sayansi ya Teknolojia ya reli na uendeshaji wake duniani.

Tunajua kwamba nchi zinazoongoza katika Teknolojia hiyo ni Ujerumani,Japan,China na Ufaransa.Inashangaza kwamba Watanzania tumejifunga kwa wawekezaji njaa wa Kihindi kwa miaka 25 ijayo. Wawekezaji ambao hata fedha ya kuwalipa wafanyakazi kwa wakati hawana.

Sasa wawekezaji kama hawa tunatizamia vipi walete vichwa vipya ,injini mpya na mabehewa mapya ya treni?

Aiyumkini hawa watapaka rangi mabehewa yaliyopo na kukarabati vichwa vya treni vilivyopo na labda kama wataagiza,wataagiza vichwa vilivyochoka kufanya kazi huko India.

Hivi Watanzania tumekosa nini hadi tunajidharirisha kiasi hicho?

Lakini hoja nyingine kubwa kuhusu ufumbuzi mwingine uliofanywa na Waziri Mkuu Pinda, walipa kodi watamlipia mwekezaji mishahara ya wafanyakazi kwa miezi mitano .

Je huo ndiyo wajibu wetu katika mkataba wa mwekezaji huyu wa Kihindi?Kama sivyo, si anayeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa, si anafutiwa mkataba?

Ikiwa kwamba kila mwekezaji atashindwa kutekeleza wajibu wake, kisha serikali itambebea mzigo wake, kuna sababu gani ya kuwaita wawekezaji wa aina hii kuja kuwekeza hapa nchini kwetu?

Kwa lugha nyepesi, sisi walipa kodi hatukufurahishwa na hatua iliyochukuliwa na serikali ya kuwalipa mishahara wafanyakazi wa reli, kwasababu hatua hiyo ni sawa na serikali inamfunga nepi mwekezaji.

Nianavyo mimi, alichotakiwa kufanya Pinda katika mgogoro huo ni kumwamuru mwekezaji kufungasha vilivyo vyake na kuondoka kwa sababu haiingi akilini kwa mtu tulimpa kutuendesha mradi wetu wa mabilioni kushindwa kulipa mshahara wa wafanyakazi wake.

Pinda asidhani kwamba kwa kufanikiwa kumaliza mgogoro huo kwa njia ya kuchukua fedha zetu na kumpa mwekezaji kutainusuru serikali na maswali kutoka kwa hawa wanaochukuliwa fedha na kupewa mgeni ambaye anachuma faida kubwa kutoka kwenye mradi tuliompa.

Namshauri, athubutu kuchukua hatua ngumu katika mambo magumu kama haya, kwa sababu Watanzania hawataki kuiona serikali ikikumbatia wawekezaji uchwara na wababaishaji.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika

0755 312859

Chanzo:Gazeti la Tanzania Jumapili la April 27,2008

NAMLILIA DITOPILE

Na Happiness Katabazi

ILIKUWA juzi saa 4:39, asubuhi, nikiwa nimeketi sebuleni na kunywa chai nyumbani kwetu Sinza ‘C’, nilipokea simu kutoka kwa mfanyakazi mwenzangu ambaye ni mchora katuni aitwaye, Said Michael ‘Wakudata’ akiniambia rafiki yako, Brother Ditopile, amefariki dunia.

Nilishtuka na ghafla mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio huku mikono ikitetemeka na kusababisha simu yangu ya kiganjani kuanguka kwenye zulia.

Kwakuwa hapo sebuleni nilikuwa nimekaa na mama yangu mzazi na kaka zangu, mama yangu alishtuka, akanikaribia na kuniuliza kulikoni? Ndipo nilipomweleza kwamba nimepokea simu inayosema rafiki yangu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (60) amefariki dunia.

Kwakuwa mama yangu naye alikuwa akimfahamu Ditopile, alishikwa butwaa. Kwakuwa siku hizi taarifa za kuzushiana vifo zimekuwa za kawaida ndani ya taifa hili, sikutaka kuziamini moja kwa moja taarifa hizo, niliamua kuokota chini ile simu yangu na kuanza kupiga kupitia namba zake (Ditopile) zote nne, ambazo nilizitumia kuwasiliana naye mara kwa mara.
Nilipokuwa napiga simu kwenye line zote hizo, line zote zilikuwa hazipatikani.

Ndipo nilipochukua uamuzi wa kumpigia simu aliyekuwa Katibu Mkuu wa timu ya Ashanti, Arafat Said, kwa kuwa marehemu alikuwa ni mlezi wa timu hiyo, kumuuliza kuhusu tukio hilo, naye alinithibitishia ni kweli. Nikabaki nimejiinamia kwa simanzi kutwa nzima na kuishia kumwombea kwa Mungu.

Mara ya mwisho kuwasiliana na Ditopile ilikuwa ni Ijumaa saa mbili usiku ya wiki iliyopita.
Alinipigia akaanza kwa kunitania kwamba muda si mrefu nitakuwa mkwe wake kwa mtoto wake wa kiume aitwaye Ramadhani, ambaye yupo masomoni Uingereza.

Nikamjibu kwa kumtania kwamba sitakuwa tayari kuwa na baba mkwe ambaye ni chakaramu kama yeye, akajibu kwamba hiyo ndiyo tabia yake tangu mdogo, hivyo hawezi kuibadili ukubwani na kwamba yeye ataongoza msafara wa wazee wa Pwani kwenda kwa mzee Katabazi kumchumbia paparazzi (yaani mimi), ili familia yake iwe na mwandishi wa habari, kwani waandishi wa habari ambao enzi za uhai wake alipenda kuwaita paparazzi, walimuandika sana kwa mabaya yake na mazuri yake.

Baada ya kunieleza hayo, nilimweleza kwamba kuna mtoto wako aitwaye Ramadhani Mzuzuri, mapema wiki iliyopita alitembelea blog yangu na kuniachia ujumbe wa kupongeza kazi zangu, nami nilimuliza Ramadhani kwakutumia e- mail kwamba Ditopile ni baba yake na kama ni baba yake basi mimi rafiki yake.

Nilivyomweleza hivyo Ditopile, akaniambia hiyo ni sababu moja wapo iliyosababisha anipigie simu siku hiyo na akanieleza kweli yule ni mtoto wake.

Baada ya kumaliza hadithi hiyo akaniomba nimsaidie kufahamu kesi yake imepangwa lini na kwa jaji yupi.

Nilimwambia kuwa nipe sekunde chache nitoe kitabu changu cha kumbukumbu ili niweze kukutajia tarehe, nikamweleza kwamba kesi yake itatajwa kwa mara ya kwanza Aprili 24 mwaka huu, mbele ya Jaji Njegafibili Mwaikugile.

Alishukuru na kuniambia: “Eh siku hiyo mapaparazzi wenzio wamejiandaaje kuja kunipiga picha?”

Nilimjibu huku tupo timamu na kwamba siku hiyo tutahakikisha tunazingira pembe zote za Mahakama Kuu bila yeye kujua ili kuhakikisha tunaipata sura yake.

Akacheka sana, akasema mapaparazzi mna taabu kweli.Namlilia rafiki yangu Ditopile kwani tangu atoke jela nimekuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara kwa simu.

Ila mara ya mwisho kuonana naye ana kwa ana na kuzungumza naye kwa takriban saa mbili ilikuwa ni Desemba 9, 2006 ndani ya Gereza la Keko alipokuwa amewekwa rumande.

Kama inavyofahamika, waandishi wa habari huwa hawaruhusiwi kuingia magerezani, lakini mzee Ditopile alimtuma mtu anipigie simu niende kumuona gerezani, ila nikifika pale gerezani nijitambulishe kwa jina bandia la Koku Katabazi, nimetokea mkoani Kagera na kwamba nivalie mavazi ya gauni kubwa na kitambaa kichwani ili maofisa magereza wa gereza hilo wasinitambue.

Kweli nilifanya hivyo na kabla ya kufikia sehemu ya kujiandikisha kwenye daftari la wageni, nilinunua maji chupa makubwa na mkate na tayari kusubiri niitwe jina la kuingia kumuona Ditopile.

Nilivyoitwa jina hilo, nilishtukia nadakwa kiaina na ndugu na jamaa wa mzee Ditopile na wakanieleza nisiwe na wasiwasi watanipeleka gerezani anapolazwa.

Kweli ilipofika zamu yangu, niliingizwa ndani ya gereza huku nikiambatana na ndugu yake mmoja ambaye ni mtu mzima kiumri, nikapandishwa sehemu ya kuzungumzia wageni ambapo ni hatua tano kutoka chumba alichokuwa akilala yeye na wenzake maarufu kwa jina la ‘Sick Bay’.

Baada ya kufika na kuketi kwenye kiti, Ditopile alitoka chumbani akaja kuzungumza nami, nilishindwa kujizuia nilibubujikwa machozi. Akaniita jina langu akisema na ujanja wako wote unalia?

Nilimjibu kuwa jela si kuzuri, hasa anapopelekwa mtu unayemfahamu.Akanijibu kwamba yote ni mipango ya Mungu na tumuachie Mungu.

Nilianza kumuuliza maswali ya hapa na pale kwamba ni kweli alikuwa amemuua yule dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), alisema ni kweli Novemba 4 mwaka 2006, alimuua kwa kumpiga risasi, ila hakuwa amekusudia kufanya tukio hilo, kwani dereva wa daladala aliligonga gari lake na alipowaambia kwanini waliligonga, dereva huyo alimtukana kwa kumuonyesha ishara ya kidole cha katikati.

“Happiness, kwakweli kwa utu uzima niliokuwa nao, wadhifa niliokuwa nao kweli mtu dereva alinigonga na nilipomhoji alinitusi kwa kutumia kidole cha katikati ya mkono wa kulia…kwakweli niligadhabika sana nikajikuta nachomoa silaha na kumfyatulia, licha ya kwamba halikuwa lengo langu.

“Siwezi kukana kwamba sikumuua yule dereva, ila nilimfyatulia risasi kutokana na hayo aliyonifanyia, ila naomba Mungu na ninaendelea kumuomba Mungu anisameheme, kwani hata vitabu vya Mungu vinakataza binadamu kutoana roho…hivyo tuiachie mahakama ndiyo itaamua,” alisema Ditopile.

Baada ya kumaliza mazungumzo yetu siku hiyo ambayo taifa likikuwa likisherehekea uhuru wake, nilimuaga kwamba nakwenda, akanisii nisimtupe kwa sababu yupo jela, niwe napita kumjulia hali na kumpatia taarifa mbalimbali, nikamkubalia.

Baada ya kuondoka gerezani hapo, kilichofuata, alikuwa akiletwa kwa nyakati tofauti katika Mahakama ya Kisutu na hatimaye Mahakama Kuu ambapo ndipo kituo changu cha kufanyia kazi.

Machi 9, mwaka jana, viwanja vya Mahakama Kuu viligeuka kuwa uwanja wa mapambano kabla na baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, kufikishwa mahakamani hapo na kutolewa kwa dhamana.

Mapambano hayo yalifanywa na watu wanaosadikiwa kuwa ni ndugu wa mshitakiwa Ditopile dhidi ya waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia mwenendo wake. Nami nilikuwa mmoja wao.

Machi 10, 2007 ambayo ilikuwa siku ya Jumamosi asububi, nikiwa na Mwadhiri Mwandamizi wa Sheria na Katiba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, nilipokea simu ikisema: “Sura yangu mnaitakia nini au mmetumwa na waganga wenu muichukue mkaniroge?”
Nikamuuliza aliyenipigia alikuwa nani, akanijibu kuwa: “ Ni mimi mzee wako Ditopile.” Nilicheka.

Nikacheka sana, ila nikamweleza wazi kabisa kwamba sikufurahishwa na vurugu zilizofanywa na ndugu zake, kwani zilikuwa zikizuia waandishi wasifanye kazi yao, pia lionyesha kuwa familia yake ina watu wa namna gani. Akasema tumsamehe, na nilipomhoji ni kwanini anavaa kofia kubwa ‘pama’, alisema anaivaa kwa makusudi ili wapiga picha wasiipate sura yake kwa urahisi.

Akaniambia kuwa: “Wewe ni mwandishi gani umeingia gerezani kuniona ukashindwa kupiga picha mazingira ya Gereza la Keko?”

Nikamjibu kuwa nisingeruhusiwa. Akaniambia pamoja na sheria kukataza yeye alitumia mbinu zake za kijeshi na alifanikiwa kupiga picha mazingira ya gereza hilo na jinsi mahabusu wanavyolala na wala hajawahi kukamatwa na askari magereza na picha hizo amezihifadhi nyumbani kwake.

Kwa wale wanaomfahamu marehemu, lazima watakubaliana nami kwamba Ditopile alikuwa ni mtoto wa mjini, mwenye kupenda masihara na mzaa, muwazi na mwongeaji kupita kiasi, na mara nyingi nilipokuwa nikionana naye au kuzungumza naye alikuwa akiniasa nipende kusali, kuishi vizuri na watu na alinisisitiza nijiendeleze kielimu, kwani elimu ndiyo mkombozi katika ulimwengu wa sasa.

Pia aliniasa kufanya kazi kwa bidii na kwamba ujumbe huo niusambaze hata kwa vijana wenzagu.
Aliniambia kuwa wakati akisoma chuo kikuu wakati wa likizo alikuwa na ubao wa kuuza mboga na matunda katika Soko la Ilala, hivyo alikuwa akifanya biashara hiyo.

Pia aliwahi kuuza magazeti ya Daily News katika mitaa ya Masaki na Oysterbay. Na alisema kazi hizo zilikuwa zinamsaidia kuongeza kipato.

Baada ya kuniambia kwamba aliwai kufanya kazi hizo, nilimwangalia usoni nikajikuta naangua kicheo kwa sauti ndani ya ofisi yake ya mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Akauliza: “Unacheka hizo kazi?” Akaniambia mwanangu hadi leo hii mnatuaona tunateuliwa kushika nyadhifa mbalimbali, mkae mkijua tumetoka mbali.”

Hatukuishia hapo, tuliendelea kuwasiliana kwa simu na hata Januari 6 mwaka huu, baada ya yeye kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba waandishi wa habari, Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage, wamemwagiwa tindikali, alinipigia simu akasema yupo mkoani Lindi, akasema amesikitishwa na tukio hilo na kwakuwa haishi utani aliniambia wakati umefika sasa mapaparazzi tuanze kuvaa ‘pama’ kama yeye ili watakapotumwagia tindikali isituingie machoni.

“Mapaparazzi anzeni kuvaa pama kama mimi ili mkimwagiwa tindikali isiwaingie machoni au wasilianeni na mimi niwaonyeshe duka niliponunua pama langu,” alisema.
Niliishia kucheka.

Ndugu msomaji mapema mwaka huu, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kwamba Ditopile alikuwa akiuza asali, na kweli hadi anafariki dunia alikuwa akifanya biashara hiyo, ambayo aliwahi kunieleza kwamba inamuingizia kipato kizuri.

Baada ya taarifa hizo kutangazwa, alinipigia simu akiniambia kwamba: “Waandishi hamna dogo, mimi kuuza asali imekuwa nongwa?” Akaniambia mbona Mwenyekiti wenu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Reginald Mengi, anauza soda za Coca Cola amuandiki? Mbona bosi wako Freeman Mbowe anauza pombe kwenye ukumbi wake wa Billicanas auandiki? Nilishindwa kumjibu kwani nilicheka sana, akaniambia usicheke.

Katika viongozi wa CCM hakika naweza kusema kiongozi ambaye nilikuwa naye karibu kikazi na aliyekuwa akinipa ushauri mbalimbali alikuwa ni Ditopile, alinichukulia kama mwanawe, hakika Ditopile nakulilia.

Hakuwa na majivuno kama walivyo viongozi wengine, hata wakati alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani nilipokuwa nikipata nafasi, nilikuwa nikipita kumsalimia ofisini kwake.

Ni Ditopile huyu huyu, siku moja kabla ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika utawala wa Awamu ya Tatu, Jakaya Kikwete, kwenda kujitangaza rasmi kugombea urais katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Pwani, Kibaha, alinipigia simu saa tatu usiku akiniambia: “Wewe si unataka ‘scoop’” (habari moto), akaniambia kesho saa mbili asubuhi panda gari kisha shuka stendi ya mabasi Kibaha.

Nilipomuuliza kuna habari gani mbona hataki kuniambia, akaniambia Nimwaini yeye na kwamba kesho yake nifike bila kukosa.

Kwakuwa nilikuwa nikimuamini na kumheshimu, kesho yake ambayo ilikuwa ni siku ya Jumapili, nilifanya hivyo nikapanda gari la kwenda Kibaha pale Ubungo, na kabla ya gari kuondoka Ubungo, alinipigia simu akiniuliza nilikuwa nimefika wapi, nikamweleza ndiyo tunaondoka Ubungo, akasema sawa.

Lile gari lilipofika stendi ya Kibaha, ghafla nilipokea simu nyingine kutoka kwake akiniuliza nilikuwa nimefika wapi, nikamwambia nimefika stendi ya Kibaha, ilikuwa saa 3 asubuhi.
Akaniambia nikodishe teksi nimwambie dereva anipeleke CCM Mkoa wa Pwani, nilifanya hivyo.

Nilipoanza kuingia ile njia ya vumbi kuelekea kwenye ofisi hizo, nikaona kumepambwa bendera za CCM. Nikamuuliza yule dereva kulikoni? Akaniambia kuwa hata yeye alikuwa anashangaa.
Nilipofika kwenye ofisi hizo za CCM saa nne asubuhi nikakuta wafuasi na viongozi wa CCM wametanda huku viti vikiwa vimepangwa na nikabahatika kumkuta mpiga picha wa TvT, sasa TBC, Chris, nikamuuliza kulikoni? Akaniambia Kikwete siku hiyo anakuja kujitangaza rasmi kwamba atagombea urais.

Aidha, baada ya dakika chache, Ditopile akaniambia: “Umekwishafika?” Nikamjibu, ndiyo.
Akasema: “Eh umekuta nini au umesikia nini?” nikamwambia nimeambiwa kwamba muda mfupi ujao Kikwete atatangaza rasmi azima yake ya kugombea urais, akasema ni kweli na akaniambia hiyo ndiyo ‘surprise’ yake kwangu na kamwe sitakuja kumsahau kwani tukio lile lilikuwa ni la kihistoria. Ni kweli sitamsahau.

Wana CCM walitutangazia kwamba Kikwete angefika pale saa tano kujitangaza lakini alifika saa saba na nusu mchana. Na ilipofika saa sita Ditopile na alinitafuta na kunitambulisha kwa mkewe aitwaye Tabia, kasha tulisalimiana.

Nakumbuka enzi za uwahi wake aliwahi kuniambia kwamba alikuwa
akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari akawa anasema anafuata masharti yote ya daktari.

Na alikuwa aishi utani, nakumbuka kuna siku nikiwa ofisini kwake Pwani nilimkuta anakunywa chai na mkate wa kumimina nikamuuliza kulikoni na mikate ya kumimina asubuhi, akasema ni miongoni mwa kitafunio anachokipenda.

Nasema tukio hili sitalisahau kwakuwa lilihudhuriwa na wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam na walianza kufika eneo hilo saa tano hadi saa saba.

Baadhi ya wahariri walionikuta hapo walishikwa butwaa na kuniambia wewe umepataje taarifa hizo, nikawaambia kwa njia zangu hasa ukizingatia kipindi hicho nilikuwa bado mwandishi mchanga sana na hata nilivyoandika habari ya tukio lile nakumbuka habari ile nilinyimwa ‘by line’ na mhariri wangu bila sababu za msingi.

Nakulilia Ditopile ambaye haupo tena nasi duniani, ila mazuri uliyoachia tutayafuata na kuyatekeleza kwa vitendo.

Hata hivyo Ditopile kama walivyo binadamu wengine alikuwa na upungufu na udhaifu na mabaya yake, hatutayafuata.

Mwanasiasa wa siku nyingi Ditopile amefikwa na mauti Jumapili iliyopita.Alifikwa na mauti katika Hoteli ya Hilux ya mjini Morogoro.

Nimemfahamu Ditopile kwa miaka sita sasa na hadi sasa kuna baadhi ya watu ukiwaeleza kwamba Ditopile ana elimu ya chuo kikuu wanakukatalia kutokana mzaha wake.

Ni Ditolipe ndiye mwasisi wa msemo wa ‘halo halo’. Ambaye amekuwa akisema yeye si mtu wa kuja, bali yeye ni mzaliwa wa jiji hili na amezaliwa wodi ya ‘Makuti’ enzi hizo ilikuwa ndani ya Hospitali ya sasa Taifa ya Muhimbili.

Ditopile aliitimu shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1973, aliajiriwa na Chama cha TANU kama Katibu Msaidizi, Makao Makuu.
Na kutokana na utendaji wake mwaka 1980 alikwishafikia cheo cha Katibu Msaidizi Mkuu Daraja la Kwanza.

Machi 1983, aliteuliwa kuwa Katibu wa Wilaya wa CCM katika wilaya za Serengerema na Tabora mjini. Nyota yake ilianza kung’ara, na mwaka 1982 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM .

Mwaka 1996 hadi 1997, aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara.
Ditopile alikuwa ni miongoni mwa vijana sita waliokuwa wameamua kujiunga na utumishi wa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) mara baada ya kuhitimu masomo ya chuo kikuu mwaka 1973.

Baada ya kujiunga na utumishi wa TANU , Ditopile alijiunga na Chuo cha Itikadi na Propaganda Kivukoni, wakati ule kikiitwa Chuo cha Chama.

Baada ya kumaliza mafunzo ya Itikadi na Propaganda, alirudi makao makuu ya chama, na hapo alipewa jukumu la kuanzisha maktaba ya CCM ambayo hadi leo ni ya chama tawala.

Pia alikuwa ni mtumishi mwaminifu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Wakati wa utumishi wake alikwenda katika Chuo cha Maofisa Monduli, alikochukua mafunzo ya uafisa wa jeshi.

Pamoja na nyadhifa hizo , Ditopile aliwai kuwa mbunge wa Jimbo la Ilala katika miaka ya 1980. Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Naibu Waziri wa Mawasiliano.

Pia alipata kuwa mkuu wa Mkoa wa Pwani, Kigoma, Lindi, Dar es Salaam na Tabora.
Ditopile alizaliwa Machi 7, mwaka 1948 katika Wilaya ya Ilala, mkoani Dar es Salaam. Alisoma Shule ya Msingi Mchikichini, Dar es Salaam kati ya mwaka 1956 na 1959.

Mwaka 1960 hadi 1963, alisoma Shule ya Kati Magomeni, Dar es Salaam.
Kati ya mwaka 1964 hadi 1967, alisoma Shule ya Sekondari ya Aga Khan, ambayo kwa sasa inajulikana kama Tambaza.

Mwaka 1968 hadi 1969, alihitimu Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Tanga.
Julai 1970, alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1973.
Lakini makala hii haita kamilika kama sitaandika kwamba marehemu Ditopile alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia ya Rais Kikwete.

Na hakuna ubishi kwamba katika uhai wake marehemu alikuwa ni miongoni mwa watu waliopigana kufa na kupona ili Kikwete ateuliwe na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Na kweli hilo walifanikiwa.

Lakini naweza kusema bahati haikuwa upande wake, kwani ndani ya miaka miwili na miezi minne, tangu kijana wake Kikwete ashike kiti cha urais, Ditopile alikumbwa na kesi ya kuua bila kukusudia, na kusababisha kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wa mkuu wa moka.
Pia katika kipindi hicho kifupi cha utawala wa kijana wake, Ditopile amekumbwa na mauti. Hivyo hakuweza kufaidi matunda ya utawala wa kijana wake.
Ditopile anatarajiwa kuzikwa leo katika shamba lake lilipo Kinyerezi, Dar es Salaam.
Ditopile sisi tulikupenda, lakini Bwana amekupenda zaidi.
Mungu ailaze roho yako mahala pema peponi. Amina.
Nakulilia Ditopile.

0755 312859
katabazihappy@yahoo.com:www.katabazihappy.blogspot.com

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne.April 22,2008
Mwisho

NAMLILIA DITOPILE

Na Happiness Katabazi

ILIKUWA juzi saa 4:39, asubuhi, nikiwa nimeketi sebuleni na kunywa chai nyumbani kwetu Sinza ‘C’, nilipokea simu kutoka kwa mfanyakazi mwenzangu ambaye ni mchora katuni aitwaye, Said Michael ‘Wakudata’ akiniambia rafiki yako, Brother Ditopile, amefariki dunia.

Nilishtuka na ghafla mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio huku mikono ikitetemeka na kusababisha simu yangu ya kiganjani kuanguka kwenye zulia.

Kwakuwa hapo sebuleni nilikuwa nimekaa na mama yangu mzazi na kaka zangu, mama yangu alishtuka, akanikaribia na kuniuliza kulikoni? Ndipo nilipomweleza kwamba nimepokea simu inayosema rafiki yangu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (60) amefariki dunia.

Kwakuwa mama yangu naye alikuwa akimfahamu Ditopile, alishikwa butwaa. Kwakuwa siku hizi taarifa za kuzushiana vifo zimekuwa za kawaida ndani ya taifa hili, sikutaka kuziamini moja kwa moja taarifa hizo, niliamua kuokota chini ile simu yangu na kuanza kupiga kupitia namba zake (Ditopile) zote nne, ambazo nilizitumia kuwasiliana naye mara kwa mara.Nilipokuwa napiga simu kwenye line zote hizo, line zote zilikuwa hazipatikani.

Ndipo nilipochukua uamuzi wa kumpigia simu aliyekuwa Katibu Mkuu wa timu ya Ashanti, Arafat Said, kwa kuwa marehemu alikuwa ni mlezi wa timu hiyo, kumuuliza kuhusu tukio hilo, naye alinithibitishia ni kweli. Nikabaki nimejiinamia kwa simanzi kutwa nzima na kuishia kumwombea kwa Mungu.

Mara ya mwisho kuwasiliana na Ditopile ilikuwa ni Ijumaa saa mbili usiku ya wiki iliyopita.
Alinipigia akaanza kwa kunitania kwamba muda si mrefu nitakuwa mkwe wake kwa mtoto wake wa kiume aitwaye Ramadhani, ambaye yupo masomoni Uingereza.

Nikamjibu kwa kumtania kwamba sitakuwa tayari kuwa na baba mkwe ambaye ni chakaramu kama yeye, akajibu kwamba hiyo ndiyo tabia yake tangu mdogo, hivyo hawezi kuibadili ukubwani na kwamba yeye ataongoza msafara wa wazee wa Pwani kwenda kwa mzee Katabazi kumchumbia paparazzi (yaani mimi), ili familia yake iwe na mwandishi wa habari, kwani waandishi wa habari ambao enzi za uhai wake alipenda kuwaita paparazzi, walimuandika sana kwa mabaya yake na mazuri yake.

Baada ya kunieleza hayo, nilimweleza kwamba kuna mtoto wako aitwaye Ramadhani Mzuzuri, mapema wiki iliyopita alitembelea blog yangu na kuniachia ujumbe wa kupongeza kazi zangu, nami nilimuliza Ramadhani kwakutumia e- mail kwamba Ditopile ni baba yake na kama ni baba yake basi mimi rafiki yake.

Nilivyomweleza hivyo Ditopile, akaniambia hiyo ni sababu moja wapo iliyosababisha anipigie simu siku hiyo na akanieleza kweli yule ni mtoto wake.Baada ya kumaliza hadithi hiyo akaniomba nimsaidie kufahamu kesi yake imepangwa lini na kwa jaji yupi.

Nilimwambia kuwa nipe sekunde chache nitoe kitabu changu cha kumbukumbu ili niweze kukutajia tarehe, nikamweleza kwamba kesi yake itatajwa kwa mara ya kwanza Aprili 24 mwaka huu, mbele ya Jaji Njegafibili Mwaikugile.

Alishukuru na kuniambia: “Eh siku hiyo mapaparazzi wenzio wamejiandaaje kuja kunipiga picha?”

Nilimjibu huku tupo timamu na kwamba siku hiyo tutahakikisha tunazingira pembe zote za Mahakama Kuu bila yeye kujua ili kuhakikisha tunaipata sura yake.Akacheka sana, akasema mapaparazzi mna taabu kweli.

Namlilia rafiki yangu Ditopile kwani tangu atoke jela nimekuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara kwa simu.

Ila mara ya mwisho kuonana naye ana kwa ana na kuzungumza naye kwa takriban saa mbili ilikuwa ni Desemba 9, 2006 ndani ya Gereza la Keko alipokuwa amewekwa rumande.

Kama inavyofahamika, waandishi wa habari huwa hawaruhusiwi kuingia magerezani, lakini mzee Ditopile alimtuma mtu anipigie simu niende kumuona gerezani, ila nikifika pale gerezani nijitambulishe kwa jina bandia la Koku Katabazi, nimetokea mkoani Kagera na kwamba nivalie mavazi ya gauni kubwa na kitambaa kichwani ili maofisa magereza wa gereza hilo wasinitambue.

Kweli nilifanya hivyo na kabla ya kufikia sehemu ya kujiandikisha kwenye daftari la wageni, nilinunua maji chupa makubwa na mkate na tayari kusubiri niitwe jina la kuingia kumuona Ditopile.

Nilivyoitwa jina hilo, nilishtukia nadakwa kiaina na ndugu na jamaa wa mzee Ditopile na wakanieleza nisiwe na wasiwasi watanipeleka gerezani anapolazwa.

Kweli ilipofika zamu yangu, niliingizwa ndani ya gereza huku nikiambatana na ndugu yake mmoja ambaye ni mtu mzima kiumri, nikapandishwa sehemu ya kuzungumzia wageni ambapo ni hatua tano kutoka chumba alichokuwa akilala yeye na wenzake maarufu kwa jina la ‘Sick Bay’.

Baada ya kufika na kuketi kwenye kiti, Ditopile alitoka chumbani akaja kuzungumza nami, nilishindwa kujizuia nilibubujikwa machozi. Akaniita jina langu akisema na ujanja wako wote unalia?

Nilimjibu kuwa jela si kuzuri, hasa anapopelekwa mtu unayemfahamu.Akanijibu kwamba yote ni mipango ya Mungu na tumuachie Mungu.

Nilianza kumuuliza maswali ya hapa na pale kwamba ni kweli alikuwa amemuua yule dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), alisema ni kweli Novemba 4 mwaka 2006, alimuua kwa kumpiga risasi, ila hakuwa amekusudia kufanya tukio hilo, kwani dereva wa daladala aliligonga gari lake na alipowaambia kwanini waliligonga, dereva huyo alimtukana kwa kumuonyesha ishara ya kidole cha katikati.

“Happiness, kwakweli kwa utu uzima niliokuwa nao, wadhifa niliokuwa nao kweli mtu dereva alinigonga na nilipomhoji alinitusi kwa kutumia kidole cha katikati ya mkono wa kulia…kwakweli niligadhabika sana nikajikuta nachomoa silaha na kumfyatulia, licha ya kwamba halikuwa lengo langu.

“Siwezi kukana kwamba sikumuua yule dereva, ila nilimfyatulia risasi kutokana na hayo aliyonifanyia, ila naomba Mungu na ninaendelea kumuomba Mungu anisameheme, kwani hata vitabu vya Mungu vinakataza binadamu kutoana roho…hivyo tuiachie mahakama ndiyo itaamua,” alisema Ditopile.

Baada ya kumaliza mazungumzo yetu siku hiyo ambayo taifa likikuwa likisherehekea uhuru wake, nilimuaga kwamba nakwenda, akanisii nisimtupe kwa sababu yupo jela, niwe napita kumjulia hali na kumpatia taarifa mbalimbali, nikamkubalia.

Baada ya kuondoka gerezani hapo, kilichofuata, alikuwa akiletwa kwa nyakati tofauti katika Mahakama ya Kisutu na hatimaye Mahakama Kuu ambapo ndipo kituo changu cha kufanyia kazi.

Machi 9, mwaka jana, viwanja vya Mahakama Kuu viligeuka kuwa uwanja wa mapambano kabla na baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, kufikishwa mahakamani hapo na kutolewa kwa dhamana.

Mapambano hayo yalifanywa na watu wanaosadikiwa kuwa ni ndugu wa mshitakiwa Ditopile dhidi ya waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia mwenendo wake. Nami nilikuwa mmoja wao.

Machi 10, 2007 ambayo ilikuwa siku ya Jumamosi asububi, nikiwa na Mwadhiri Mwandamizi wa Sheria na Katiba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, nilipokea simu ikisema:

“Sura yangu mnaitakia nini au mmetumwa na waganga wenu muichukue mkaniroge?”
Nikamuuliza aliyenipigia alikuwa nani, akanijibu kuwa: “ Ni mimi mzee wako Ditopile.” Nilicheka.

Nikacheka sana, ila nikamweleza wazi kabisa kwamba sikufurahishwa na vurugu zilizofanywa na ndugu zake, kwani zilikuwa zikizuia waandishi wasifanye kazi yao, pia lionyesha kuwa familia yake ina watu wa namna gani. Akasema tumsamehe, na nilipomhoji ni kwanini anavaa kofia kubwa ‘pama’, alisema anaivaa kwa makusudi ili wapiga picha wasiipate sura yake kwa urahisi.

Akaniambia kuwa: “Wewe ni mwandishi gani umeingia gerezani kuniona ukashindwa kupiga picha mazingira ya Gereza la Keko?”

Nikamjibu kuwa nisingeruhusiwa. Akaniambia pamoja na sheria kukataza yeye alitumia mbinu zake za kijeshi na alifanikiwa kupiga picha mazingira ya gereza hilo na jinsi mahabusu wanavyolala na wala hajawahi kukamatwa na askari magereza na picha hizo amezihifadhi nyumbani kwake.

Kwa wale wanaomfahamu marehemu, lazima watakubaliana nami kwamba Ditopile alikuwa ni mtoto wa mjini, mwenye kupenda masihara na mzaa, muwazi na mwongeaji kupita kiasi, na mara nyingi nilipokuwa nikionana naye au kuzungumza naye alikuwa akiniasa nipende kusali, kuishi vizuri na watu na alinisisitiza nijiendeleze kielimu, kwani elimu ndiyo mkombozi katika ulimwengu wa sasa.

Pia aliniasa kufanya kazi kwa bidii na kwamba ujumbe huo niusambaze hata kwa vijana wenzagu.
Aliniambia kuwa wakati akisoma chuo kikuu wakati wa likizo alikuwa na ubao wa kuuza mboga na matunda katika Soko la Ilala, hivyo alikuwa akifanya biashara hiyo.

Pia aliwahi kuuza magazeti ya Daily News katika mitaa ya Masaki na Oysterbay. Na alisema kazi hizo zilikuwa zinamsaidia kuongeza kipato.

Baada ya kuniambia kwamba aliwai kufanya kazi hizo, nilimwangalia usoni nikajikuta naangua kicheo kwa sauti ndani ya ofisi yake ya mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Akauliza: “Unacheka hizo kazi?” Akaniambia mwanangu hadi leo hii mnatuaona tunateuliwa kushika nyadhifa mbalimbali, mkae mkijua tumetoka mbali.”

Hatukuishia hapo, tuliendelea kuwasiliana kwa simu na hata Januari 6 mwaka huu, baada ya yeye kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba waandishi wa habari, Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage, wamemwagiwa tindikali, alinipigia simu akasema yupo mkoani Lindi, akasema amesikitishwa na tukio hilo na kwakuwa haishi utani aliniambia wakati umefika sasa mapaparazzi tuanze kuvaa ‘pama’ kama yeye ili watakapotumwagia tindikali isituingie machoni.

“Mapaparazzi anzeni kuvaa pama kama mimi ili mkimwagiwa tindikali isiwaingie machoni au wasilianeni na mimi niwaonyeshe duka niliponunua pama langu,” alisema.
Niliishia kucheka.

Ndugu msomaji mapema mwaka huu, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kwamba Ditopile alikuwa akiuza asali, na kweli hadi anafariki dunia alikuwa akifanya biashara hiyo, ambayo aliwahi kunieleza kwamba inamuingizia kipato kizuri.

Baada ya taarifa hizo kutangazwa, alinipigia simu akiniambia kwamba: “Waandishi hamna dogo, mimi kuuza asali imekuwa nongwa?” Akaniambia mbona Mwenyekiti wenu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Reginald Mengi, anauza soda za Coca Cola amuandiki? Mbona bosi wako Freeman Mbowe anauza pombe kwenye ukumbi wake wa Billicanas auandiki? Nilishindwa kumjibu kwani nilicheka sana, akaniambia usicheke.

Katika viongozi wa CCM hakika naweza kusema kiongozi ambaye nilikuwa naye karibu kikazi na aliyekuwa akinipa ushauri mbalimbali alikuwa ni Ditopile, alinichukulia kama mwanawe, hakika Ditopile nakulilia.

Hakuwa na majivuno kama walivyo viongozi wengine, hata wakati alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani nilipokuwa nikipata nafasi, nilikuwa nikipita kumsalimia ofisini kwake.

Ni Ditopile huyu huyu, siku moja kabla ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika utawala wa Awamu ya Tatu, Jakaya Kikwete, kwenda kujitangaza rasmi kugombea urais katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Pwani, Kibaha, alinipigia simu saa tatu usiku akiniambia: “Wewe si unataka ‘scoop’” (habari moto), akaniambia kesho saa mbili asubuhi panda gari kisha shuka stendi ya mabasi Kibaha.

Nilipomuuliza kuna habari gani mbona hataki kuniambia, akaniambia Nimwaini yeye na kwamba kesho yake nifike bila kukosa.

Kwakuwa nilikuwa nikimuamini na kumheshimu, kesho yake ambayo ilikuwa ni siku ya Jumapili, nilifanya hivyo nikapanda gari la kwenda Kibaha pale Ubungo, na kabla ya gari kuondoka Ubungo, alinipigia simu akiniuliza nilikuwa nimefika wapi, nikamweleza ndiyo tunaondoka Ubungo, akasema sawa.

Lile gari lilipofika stendi ya Kibaha, ghafla nilipokea simu nyingine kutoka kwake akiniuliza nilikuwa nimefika wapi, nikamwambia nimefika stendi ya Kibaha, ilikuwa saa 3 asubuhi.

Akaniambia nikodishe teksi nimwambie dereva anipeleke CCM Mkoa wa Pwani, nilifanya hivyo. Nilipoanza kuingia ile njia ya vumbi kuelekea kwenye ofisi hizo, nikaona kumepambwa bendera za CCM. Nikamuuliza yule dereva kulikoni? Akaniambia kuwa hata yeye alikuwa anashangaa.

Nilipofika kwenye ofisi hizo za CCM saa nne asubuhi nikakuta wafuasi na viongozi wa CCM wametanda huku viti vikiwa vimepangwa na nikabahatika kumkuta mpiga picha wa TvT, sasa TBC, Chris, nikamuuliza kulikoni? Akaniambia Kikwete siku hiyo anakuja kujitangaza rasmi kwamba atagombea urais.

Aidha, baada ya dakika chache, Ditopile akaniambia: “Umekwishafika?” Nikamjibu, ndiyo.
Akasema: “Eh umekuta nini au umesikia nini?” nikamwambia nimeambiwa kwamba muda mfupi ujao Kikwete atatangaza rasmi azima yake ya kugombea urais, akasema ni kweli na akaniambia hiyo ndiyo ‘surprise’ yake kwangu na kamwe sitakuja kumsahau kwani tukio lile lilikuwa ni la kihistoria. Ni kweli sitamsahau.

Wana CCM walitutangazia kwamba Kikwete angefika pale saa tano kujitangaza lakini alifika saa saba na nusu mchana. Na ilipofika saa sita Ditopile na alinitafuta na kunitambulisha kwa mkewe aitwaye Tabia, kasha tulisalimiana.

Nakumbuka enzi za uwahi wake aliwahi kuniambia kwamba alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari akawa anasema anafuata masharti yote ya daktari.

Na alikuwa aishi utani, nakumbuka kuna siku nikiwa ofisini kwake Pwani nilimkuta anakunywa chai na mkate wa kumimina nikamuuliza kulikoni na mikate ya kumimina asubuhi, akasema ni miongoni mwa kitafunio anachokipenda.

Nasema tukio hili sitalisahau kwakuwa lilihudhuriwa na wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam na walianza kufika eneo hilo saa tano hadi saa saba.

Baadhi ya wahariri walionikuta hapo walishikwa butwaa na kuniambia wewe umepataje taarifa hizo, nikawaambia kwa njia zangu hasa ukizingatia kipindi hicho nilikuwa bado mwandishi mchanga sana na hata nilivyoandika habari ya tukio lile nakumbuka habari ile nilinyimwa ‘by line’ na mhariri wangu bila sababu za msingi.

Nakulilia Ditopile ambaye haupo tena nasi duniani, ila mazuri uliyoachia tutayafuata na kuyatekeleza kwa vitendo.

Hata hivyo Ditopile kama walivyo binadamu wengine alikuwa na upungufu na udhaifu na mabaya yake, hatutayafuata.

Mwanasiasa wa siku nyingi Ditopile amefikwa na mauti Jumapili iliyopita.
Alifikwa na mauti katika Hoteli ya Hilux ya mjini Morogoro.

Nimemfahamu Ditopile kwa miaka sita sasa na hadi sasa kuna baadhi ya watu ukiwaeleza kwamba Ditopile ana elimu ya chuo kikuu wanakukatalia kutokana mzaha wake.

Ni Ditolipe ndiye mwasisi wa msemo wa ‘halo halo’. Ambaye amekuwa akisema yeye si mtu wa kuja, bali yeye ni mzaliwa wa jiji hili na amezaliwa wodi ya ‘Makuti’ enzi hizo ilikuwa ndani ya Hospitali ya sasa Taifa ya Muhimbili.

Ditopile aliitimu shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1973, aliajiriwa na Chama cha TANU kama Katibu Msaidizi, Makao Makuu.

Na kutokana na utendaji wake mwaka 1980 alikwishafikia cheo cha Katibu Msaidizi Mkuu Daraja la Kwanza.Machi 1983, aliteuliwa kuwa Katibu wa Wilaya wa CCM katika wilaya za Serengerema na Tabora mjini.

Nyota yake ilianza kung’ara, na mwaka 1982 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM .

Mwaka 1996 hadi 1997, aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara.Ditopile alikuwa ni miongoni mwa vijana sita waliokuwa wameamua kujiunga na utumishi wa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) mara baada ya kuhitimu masomo ya chuo kikuu mwaka 1973.

Baada ya kujiunga na utumishi wa TANU , Ditopile alijiunga na Chuo cha Itikadi na Propaganda Kivukoni, wakati ule kikiitwa Chuo cha Chama.

Baada ya kumaliza mafunzo ya Itikadi na Propaganda, alirudi makao makuu ya chama, na hapo alipewa jukumu la kuanzisha maktaba ya CCM ambayo hadi leo ni ya chama tawala.

Pia alikuwa ni mtumishi mwaminifu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Wakati wa utumishi wake alikwenda katika Chuo cha Maofisa Monduli, alikochukua mafunzo ya uafisa wa jeshi.

Pamoja na nyadhifa hizo , Ditopile aliwai kuwa mbunge wa Jimbo la Ilala katika miaka ya 1980. Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Naibu Waziri wa Mawasiliano.

Pia alipata kuwa mkuu wa Mkoa wa Pwani, Kigoma, Lindi, Dar es Salaam na Tabora.
Ditopile alizaliwa Machi 7, mwaka 1948 katika Wilaya ya Ilala, mkoani Dar es Salaam. Alisoma Shule ya Msingi Mchikichini, Dar es Salaam kati ya mwaka 1956 na 1959.

Mwaka 1960 hadi 1963, alisoma Shule ya Kati Magomeni, Dar es Salaam.
Kati ya mwaka 1964 hadi 1967, alisoma Shule ya Sekondari ya Aga Khan, ambayo kwa sasa inajulikana kama Tambaza.

Mwaka 1968 hadi 1969, alihitimu Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Tanga.
Julai 1970, alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1973.

Lakini makala hii haita kamilika kama sitaandika kwamba marehemu Ditopile alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia ya Rais Kikwete.

Na hakuna ubishi kwamba katika uhai wake marehemu alikuwa ni miongoni mwa watu waliopigana kufa na kupona ili Kikwete ateuliwe na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Na kweli hilo walifanikiwa.

Lakini naweza kusema bahati haikuwa upande wake, kwani ndani ya miaka miwili na miezi minne, tangu kijana wake Kikwete ashike kiti cha urais, Ditopile alikumbwa na kesi ya kuua bila kukusudia, na kusababisha kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wa mkuu wa mkoa.

Pia katika kipindi hicho kifupi cha utawala wa kijana wake, Ditopile amekumbwa na mauti. Hivyo hakuweza kufaidi matunda ya utawala wa kijana wake.

Ditopile anatarajiwa kuzikwa leo katika shamba lake lilipo Kinyerezi, Dar es Salaam.
Ditopile sisi tulikupenda, lakini Bwana amekupenda zaidi.

Mungu ailaze roho yako mahala pema peponi. Amina.

Nakulilia Ditopile.

0755 312859
katabazihappy@yahoo.com:www.katabazihappy.blogspot.com

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne.April 22,2008

NAMLILIA DITOPILE

Na Happiness Katabazi

ILIKUWA juzi saa 4:39, asubuhi, nikiwa nimeketi sebuleni na kunywa chai nyumbani kwetu Sinza ‘C’, nilipokea simu kutoka kwa mfanyakazi mwenzangu ambaye ni mchora katuni aitwaye, Said Michael ‘Wakudata’ akiniambia rafiki yako, Brother Ditopile, amefariki dunia.

Nilishtuka na ghafla mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio huku mikono ikitetemeka na kusababisha simu yangu ya kiganjani kuanguka kwenye zulia.

Kwakuwa hapo sebuleni nilikuwa nimekaa na mama yangu mzazi na kaka zangu, mama yangu alishtuka, akanikaribia na kuniuliza kulikoni? Ndipo nilipomweleza kwamba nimepokea simu inayosema rafiki yangu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (60) amefariki dunia.

Kwakuwa mama yangu naye alikuwa akimfahamu Ditopile, alishikwa butwaa. Kwakuwa siku hizi taarifa za kuzushiana vifo zimekuwa za kawaida ndani ya taifa hili, sikutaka kuziamini moja kwa moja taarifa hizo, niliamua kuokota chini ile simu yangu na kuanza kupiga kupitia namba zake (Ditopile) zote nne, ambazo nilizitumia kuwasiliana naye mara kwa mara.

Nilipokuwa napiga simu kwenye line zote hizo, line zote zilikuwa hazipatikani. Ndipo nilipochukua uamuzi wa kumpigia simu aliyekuwa Katibu Mkuu wa timu ya Ashanti, Arafat Said, kwa kuwa marehemu alikuwa ni mlezi wa timu hiyo, kumuuliza kuhusu tukio hilo, naye alinithibitishia ni kweli. Nikabaki nimejiinamia kwa simanzi kutwa nzima na kuishia kumwombea kwa Mungu.

Mara ya mwisho kuwasiliana na Ditopile ilikuwa ni Ijumaa saa mbili usiku ya wiki iliyopita.
Alinipigia akaanza kwa kunitania kwamba muda si mrefu nitakuwa mkwe wake kwa mtoto wake wa kiume aitwaye Ramadhani, ambaye yupo masomoni Uingereza.

Nikamjibu kwa kumtania kwamba sitakuwa tayari kuwa na baba mkwe ambaye ni chakaramu kama yeye, akajibu kwamba hiyo ndiyo tabia yake tangu mdogo, hivyo hawezi kuibadili ukubwani na kwamba yeye ataongoza msafara wa wazee wa Pwani kwenda kwa mzee Katabazi kumchumbia paparazzi (yaani mimi), ili familia yake iwe na mwandishi wa habari, kwani waandishi wa habari ambao enzi za uhai wake alipenda kuwaita paparazzi, walimuandika sana kwa mabaya yake na mazuri yake.

Baada ya kunieleza hayo, nilimweleza kwamba kuna mtoto wako aitwaye Ramadhani Mzuzuri, mapema wiki iliyopita alitembelea blog yangu na kuniachia ujumbe wa kupongeza kazi zangu, nami nilimuliza Ramadhani kwakutumia e- mail kwamba Ditopile ni baba yake na kama ni baba yake basi mimi rafiki yake.

Nilivyomweleza hivyo Ditopile, akaniambia hiyo ni sababu moja wapo iliyosababisha anipigie simu siku hiyo na akanieleza kweli yule ni mtoto wake.Baada ya kumaliza hadithi hiyo akaniomba nimsaidie kufahamu kesi yake imepangwa lini na kwa jaji yupi.

Nilimwambia kuwa nipe sekunde chache nitoe kitabu changu cha kumbukumbu ili niweze kukutajia tarehe, nikamweleza kwamba kesi yake itatajwa kwa mara ya kwanza Aprili 24 mwaka huu, mbele ya Jaji Njegafibili Mwaikugile.

Alishukuru na kuniambia: “Eh siku hiyo mapaparazzi wenzio wamejiandaaje kuja kunipiga picha?” Nilimjibu huku tupo timamu na kwamba siku hiyo tutahakikisha tunazingira pembe zote za Mahakama Kuu bila yeye kujua ili kuhakikisha tunaipata sura yake.Akacheka sana, akasema mapaparazzi mna taabu kweli.

Namlilia rafiki yangu Ditopile kwani tangu atoke jela nimekuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara kwa simu. Ila mara ya mwisho kuonana naye ana kwa ana na kuzungumza naye kwa takriban saa mbili ilikuwa ni Desemba 9, 2006 ndani ya Gereza la Keko alipokuwa amewekwa rumande.

Kama inavyofahamika, waandishi wa habari huwa hawaruhusiwi kuingia magerezani, lakini mzee Ditopile alimtuma mtu anipigie simu niende kumuona gerezani, ila nikifika pale gerezani nijitambulishe kwa jina bandia la Koku Katabazi, nimetokea mkoani Kagera na kwamba nivalie mavazi ya gauni kubwa na kitambaa kichwani ili maofisa magereza wa gereza hilo wasinitambue.

Kweli nilifanya hivyo na kabla ya kufikia sehemu ya kujiandikisha kwenye daftari la wageni, nilinunua maji chupa makubwa na mkate na tayari kusubiri niitwe jina la kuingia kumuona Ditopile.

Nilivyoitwa jina hilo, nilishtukia nadakwa kiaina na ndugu na jamaa wa mzee Ditopile na wakanieleza nisiwe na wasiwasi watanipeleka gerezani anapolazwa.

Kweli ilipofika zamu yangu, niliingizwa ndani ya gereza huku nikiambatana na ndugu yake mmoja ambaye ni mtu mzima kiumri, nikapandishwa sehemu ya kuzungumzia wageni ambapo ni hatua tano kutoka chumba alichokuwa akilala yeye na wenzake maarufu kwa jina la ‘Sick Bay’.

Baada ya kufika na kuketi kwenye kiti, Ditopile alitoka chumbani akaja kuzungumza nami, nilishindwa kujizuia nilibubujikwa machozi. Akaniita jina langu akisema na ujanja wako wote unalia? Nilimjibu kuwa jela si kuzuri, hasa anapopelekwa mtu unayemfahamu.
Akanijibu kwamba yote ni mipango ya Mungu na tumuachie Mungu.

Nilianza kumuuliza maswali ya hapa na pale kwamba ni kweli alikuwa amemuua yule dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), alisema ni kweli Novemba 4 mwaka 2006, alimuua kwa kumpiga risasi, ila hakuwa amekusudia kufanya tukio hilo, kwani dereva wa daladala aliligonga gari lake na alipowaambia kwanini waliligonga, dereva huyo alimtukana kwa kumuonyesha ishara ya kidole cha katikati.

“Happiness, kwakweli kwa utu uzima niliokuwa nao, wadhifa niliokuwa nao kweli mtu dereva alinigonga na nilipomhoji alinitusi kwa kutumia kidole cha katikati ya mkono wa kulia…kwakweli niligadhabika sana nikajikuta nachomoa silaha na kumfyatulia, licha ya kwamba halikuwa lengo langu.

“Siwezi kukana kwamba sikumuua yule dereva, ila nilimfyatulia risasi kutokana na hayo aliyonifanyia, ila naomba Mungu na ninaendelea kumuomba Mungu anisameheme, kwani hata vitabu vya Mungu vinakataza binadamu kutoana roho…hivyo tuiachie mahakama ndiyo itaamua,” alisema Ditopile.

Baada ya kumaliza mazungumzo yetu siku hiyo ambayo taifa likikuwa likisherehekea uhuru wake, nilimuaga kwamba nakwenda, akanisii nisimtupe kwa sababu yupo jela, niwe napita kumjulia hali na kumpatia taarifa mbalimbali, nikamkubalia.

Baada ya kuondoka gerezani hapo, kilichofuata, alikuwa akiletwa kwa nyakati tofauti katika Mahakama ya Kisutu na hatimaye Mahakama Kuu ambapo ndipo kituo changu cha kufanyia kazi.

Machi 9, mwaka jana, viwanja vya Mahakama Kuu viligeuka kuwa uwanja wa mapambano kabla na baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, kufikishwa mahakamani hapo na kutolewa kwa dhamana.

Mapambano hayo yalifanywa na watu wanaosadikiwa kuwa ni ndugu wa mshitakiwa Ditopile dhidi ya waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia mwenendo wake. Nami nilikuwa mmoja wao.

Machi 10, 2007 ambayo ilikuwa siku ya Jumamosi asububi, nikiwa na Mwadhiri Mwandamizi wa Sheria na Katiba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, nilipokea simu ikisema: “Sura yangu mnaitakia nini au mmetumwa na waganga wenu muichukue mkaniroge?”
Nikamuuliza aliyenipigia alikuwa nani, akanijibu kuwa: “ Ni mimi mzee wako Ditopile.” Nilicheka.

Nikacheka sana, ila nikamweleza wazi kabisa kwamba sikufurahishwa na vurugu zilizofanywa na ndugu zake, kwani zilikuwa zikizuia waandishi wasifanye kazi yao, pia lionyesha kuwa familia yake ina watu wa namna gani. Akasema tumsamehe, na nilipomhoji ni kwanini anavaa kofia kubwa ‘pama’, alisema anaivaa kwa makusudi ili wapiga picha wasiipate sura yake kwa urahisi.

Akaniambia kuwa: “Wewe ni mwandishi gani umeingia gerezani kuniona ukashindwa kupiga picha mazingira ya Gereza la Keko?”

Nikamjibu kuwa nisingeruhusiwa. Akaniambia pamoja na sheria kukataza yeye alitumia mbinu zake za kijeshi na alifanikiwa kupiga picha mazingira ya gereza hilo na jinsi mahabusu wanavyolala na wala hajawahi kukamatwa na askari magereza na picha hizo amezihifadhi nyumbani kwake.

Kwa wale wanaomfahamu marehemu, lazima watakubaliana nami kwamba Ditopile alikuwa ni mtoto wa mjini, mwenye kupenda masihara na mzaa, muwazi na mwongeaji kupita kiasi, na mara nyingi nilipokuwa nikionana naye au kuzungumza naye alikuwa akiniasa nipende kusali, kuishi vizuri na watu na alinisisitiza nijiendeleze kielimu, kwani elimu ndiyo mkombozi katika ulimwengu wa sasa.

Pia aliniasa kufanya kazi kwa bidii na kwamba ujumbe huo niusambaze hata kwa vijana wenzagu.Aliniambia kuwa wakati akisoma Chuo Kikuu wakati wa likizo alikuwa na ubao wa kuuza mboga na matunda katika Soko la Ilala, hivyo alikuwa akifanya biashara hiyo.

Pia aliwahi kuuza magazeti ya Daily News katika mitaa ya Masaki na Oysterbay. Na alisema kazi hizo zilikuwa zinamsaidia kuongeza kipato. Baada ya kuniambia kwamba aliwai kufanya kazi hizo, nilimwangalia usoni nikajikuta naangua kicheo kwa sauti ndani ya ofisi yake ya mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Akauliza: “Unacheka hizo kazi?” Akaniambia mwanangu hadi leo hii mnatuaona tunateuliwa kushika nyadhifa mbalimbali, mkae mkijua tumetoka mbali.”

Hatukuishia hapo, tuliendelea kuwasiliana kwa simu na hata Januari 6 mwaka huu, baada ya yeye kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba waandishi wa habari, Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage, wamemwagiwa tindikali, alinipigia simu akasema yupo mkoani Lindi, akasema amesikitishwa na tukio hilo na kwakuwa haishi utani aliniambia wakati umefika sasa mapaparazzi tuanze kuvaa ‘pama’ kama yeye ili watakapotumwagia tindikali isituingie machoni.

“Mapaparazzi anzeni kuvaa pama kama mimi ili mkimwagiwa tindikali isiwaingie machoni au wasilianeni na mimi niwaonyeshe duka niliponunua pama langu,” alisema.
Niliishia kucheka.

Ndugu msomaji mapema mwaka huu, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kwamba Ditopile alikuwa akiuza asali, na kweli hadi anafariki dunia alikuwa akifanya biashara hiyo, ambayo aliwahi kunieleza kwamba inamuingizia kipato kizuri.

Baada ya taarifa hizo kutangazwa, alinipigia simu akiniambia kwamba: “Waandishi hamna dogo, mimi kuuza asali imekuwa nongwa?” Akaniambia mbona Mwenyekiti wenu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Reginald Mengi, anauza soda za Coca Cola amuandiki? Mbona bosi wako Freeman Mbowe anauza pombe kwenye ukumbi wake wa Billicanas auandiki? Nilishindwa kumjibu kwani nilicheka sana, akaniambia usicheke.

Katika viongozi wa CCM hakika naweza kusema kiongozi ambaye nilikuwa naye karibu kikazi na aliyekuwa akinipa ushauri mbalimbali alikuwa ni Ditopile, alinichukulia kama mwanawe, hakika Ditopile nakulilia.

Hakuwa na majivuno kama walivyo viongozi wengine, hata wakati alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani nilipokuwa nikipata nafasi, nilikuwa nikipita kumsalimia ofisini kwake.

Ni Ditopile huyu huyu, siku moja kabla ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika utawala wa Awamu ya Tatu, Jakaya Kikwete, kwenda kujitangaza rasmi kugombea urais katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Pwani, Kibaha, alinipigia simu saa tatu usiku akiniambia: “Wewe si unataka ‘scoop’” (habari moto), akaniambia kesho saa mbili asubuhi panda gari kisha shuka stendi ya mabasi Kibaha.

Nilipomuuliza kuna habari gani mbona hataki kuniambia, akaniambia Nimwamini yeye na kwamba kesho yake nifike bila kukosa.

Kwakuwa nilikuwa nikimuamini na kumheshimu, kesho yake ambayo ilikuwa ni siku ya Jumapili, nilifanya hivyo nikapanda gari la kwenda Kibaha pale Ubungo, na kabla ya gari kuondoka Ubungo, alinipigia simu akiniuliza nilikuwa nimefika wapi, nikamweleza ndiyo tunaondoka Ubungo, akasema sawa.

Lile gari lilipofika stendi ya Kibaha, ghafla nilipokea simu nyingine kutoka kwake akiniuliza nilikuwa nimefika wapi, nikamwambia nimefika stendi ya Kibaha, ilikuwa saa 3 asubuhi.

Akaniambia nikodishe teksi nimwambie dereva anipeleke CCM Mkoa wa Pwani, nilifanya hivyo. Nilipoanza kuingia ile njia ya vumbi kuelekea kwenye ofisi hizo, nikaona kumepambwa bendera za CCM. Nikamuuliza yule dereva kulikoni? Akaniambia kuwa hata yeye alikuwa anashangaa.

Nilipofika kwenye ofisi hizo za CCM saa nne asubuhi nikakuta wafuasi na viongozi wa CCM wametanda huku viti vikiwa vimepangwa na nikabahatika kumkuta mpiga picha wa TvT, sasa TBC, Chris, nikamuuliza kulikoni? Akaniambia Kikwete siku hiyo anakuja kujitangaza rasmi kwamba atagombea urais.

Aidha, baada ya dakika chache, Ditopile akaniambia: “Umekwishafika?” Nikamjibu, ndiyo.
Akasema: “Eh umekuta nini au umesikia nini?” nikamwambia nimeambiwa kwamba muda mfupi ujao Kikwete atatangaza rasmi azima yake ya kugombea urais, akasema ni kweli na akaniambia hiyo ndiyo ‘surprise’ yake kwangu na kamwe sitakuja kumsahau kwani tukio lile lilikuwa ni la kihistoria. Ni kweli sitamsahau.

Wana CCM walitutangazia kwamba Kikwete angefika pale saa tano kujitangaza lakini alifika saa saba na nusu mchana. Na ilipofika saa sita Ditopile na alinitafuta na kunitambulisha kwa mkewe aitwaye Tabia, kasha tulisalimiana.

Nakumbuka enzi za uwahi wake aliwahi kuniambia kwamba alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari akawa anasema anafuata masharti yote ya daktari. Na alikuwa aishi utani, nakumbuka kuna siku nikiwa ofisini kwake Pwani nilimkuta anakunywa chai na mkate wa kumimina nikamuuliza kulikoni na mikate ya kumimina asubuhi, akasema ni miongoni mwa kitafunio anachokipenda.

Nasema tukio hili sitalisahau kwakuwa lilihudhuriwa na wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam na walianza kufika eneo hilo saa tano hadi saa saba.

Baadhi ya wahariri walionikuta hapo walishikwa butwaa na kuniambia wewe umepataje taarifa hizo, nikawaambia kwa njia zangu hasa ukizingatia kipindi hicho nilikuwa bado mwandishi mchanga sana na hata nilivyoandika habari ya tukio lile nakumbuka habari ile nilinyimwa ‘by line’ na mhariri wangu bila sababu za msingi.

Nakulilia Ditopile ambaye haupo tena nasi duniani, ila mazuri uliyoachia tutayafuata na kuyatekeleza kwa vitendo.Hata hivyo Ditopile kama walivyo binadamu wengine alikuwa na upungufu na udhaifu na mabaya yake, hatutayafuata.

Mwanasiasa wa siku nyingi Ditopile amefikwa na mauti Jumapili iliyopita. Alifikwa na mauti katika Hoteli ya Hilux ya mjini Morogoro.

Nimemfahamu Ditopile kwa miaka sita sasa na hadi sasa kuna baadhi ya watu ukiwaeleza kwamba Ditopile ana elimu ya chuo kikuu wanakukatalia kutokana mzaha wake.

Ditolipe ndiye mwasisi wa msemo wa ‘halo halo’. Ambaye amekuwa akisema yeye si mtu wa kuja, bali yeye ni mzaliwa wa jiji hili na amezaliwa wodi ya ‘Makuti’ enzi hizo ilikuwa ndani ya Hospitali ya sasa Taifa ya Muhimbili.

Ditopile aliitimu shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1973, aliajiriwa na Chama cha TANU kama Katibu Msaidizi, Makao Makuu. Na kutokana na utendaji wake mwaka 1980 alikwishafikia cheo cha Katibu Msaidizi Mkuu Daraja la Kwanza.

Machi 1983, aliteuliwa kuwa Katibu wa Wilaya wa CCM katika wilaya za Serengerema na Tabora mjini. Nyota yake ilianza kung’ara, na mwaka 1982 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM .Mwaka 1996 hadi 1997, aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara.

Ditopile alikuwa ni miongoni mwa vijana sita waliokuwa wameamua kujiunga na utumishi wa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) mara baada ya kuhitimu masomo ya chuo kikuu mwaka 1973.

Baada ya kujiunga na utumishi wa TANU , Ditopile alijiunga na Chuo cha Itikadi na Propaganda Kivukoni, wakati ule kikiitwa Chuo cha Chama. Baada ya kumaliza mafunzo ya Itikadi na Propaganda, alirudi makao makuu ya chama, na hapo alipewa jukumu la kuanzisha maktaba ya CCM ambayo hadi leo ni ya chama tawala.

Pia alikuwa ni mtumishi mwaminifu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Wakati wa utumishi wake alikwenda katika Chuo cha Maofisa Monduli, alikochukua mafunzo ya uafisa wa jeshi.

Pamoja na nyadhifa hizo , Ditopile aliwai kuwa mbunge wa Jimbo la Ilala katika miaka ya 1980. Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Naibu Waziri wa Mawasiliano.

Pia alipata kuwa mkuu wa Mkoa wa Pwani, Kigoma, Lindi, Dar es Salaam na Tabora.
Ditopile alizaliwa Machi 7, mwaka 1948 katika Wilaya ya Ilala, mkoani Dar es Salaam. Alisoma Shule ya Msingi Mchikichini, Dar es Salaam kati ya mwaka 1956 na 1959.

Mwaka 1960 hadi 1963, alisoma Shule ya Kati Magomeni, Dar es Salaam.
Kati ya mwaka 1964 hadi 1967, alisoma Shule ya Sekondari ya Aga Khan, ambayo kwa sasa inajulikana kama Tambaza.

Mwaka 1968 hadi 1969, alihitimu Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Tanga. Julai 1970, alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1973. Lakini makala hii haita kamilika kama sitaandika kwamba marehemu Ditopile alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia ya Rais Kikwete.

Na hakuna ubishi kwamba katika uhai wake marehemu alikuwa ni miongoni mwa watu waliopigana kufa na kupona ili Kikwete ateuliwe na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Na kweli hilo walifanikiwa.

Lakini naweza kusema bahati haikuwa upande wake, kwani ndani ya miaka miwili na miezi minne, tangu kijana wake Kikwete ashike kiti cha urais, Ditopile alikumbwa na kesi ya kuua bila kukusudia, na kusababisha kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wa mkuu wa moka.

Pia katika kipindi hicho kifupi cha utawala wa kijana wake, Ditopile amekumbwa na mauti. Hivyo hakuweza kufaidi matunda ya utawala wa kijana wake.

Ditopile anatarajiwa kuzikwa leo katika shamba lake lilipo Kinyerezi, Dar es Salaam.

Ditopile sisi tulikupenda, lakini Bwana amekupenda zaidi.

Mungu ailaze roho yako mahala pema peponi. Amina.

Namlilia Ditopile.

0755 312859
katabazihappy@yahoo.com:www.katabazihappy.blogspot.com

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne.April 22,2008

RAIS KIKWETE NA KILIO CHA MAKANJANJA

Na Happiness Katabazi

“DALILI mbaya za kuwatumia waandishi wa habari wasiozingatia misingi ya kitaaluma, maarufu kama ‘makanjanja’, inaweka fani hiyo katika hatari ya kupoteza heshima yake katika jamii”

“Kutokana na hali hiyo , nawaagiza wamikili wa vyombo vya habari nchini, wahariri na wanahabari , kuzingatia maadili ya taaluma ya habari ili kuinusuru taaluma hiyo isiangamie kutokana na kuvamiwa na ‘makanjanja’.

Maneno haya ameyasema rais Jakaya Kikwete hivi karibuni kwenye sherehe za uzinduzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Alisema iwapo hatua za mara moja hazitachukuliwa mapema,basi wanahabari na wamiliki ndiyo watakaokuwa watu wa kwanza kujuta , hali itakayosabisha kuanza kusemana na kuchimbana wenyewe, ambapo tayari kuna mwelekeo wa mashaka na kwamba dalili zake zimeishaanza.

Binafsi nilipata fursa ya kumsikiliza Rais Kikwete wakati akihutubia kwenye dhifa hiyo, ila nimebaini kwamba hao waliomuandalia hotuba aliyoitoa wamempotosha rais wetu, kwani wameshindwa kutofautisha ‘makanjanja’ ni waandishi wa namna gani na ‘waandishi mtandao'ni wapi.

Kwa sisi wanahabari, ‘makanjanja’ tunaowajua ni wale matapeli wasio na taaluma yoyote ya kuandika habari na ambao hawana vyombo vya kuandikia, lakini hupita hapa na pale kudandia shughuili na dhifa kwa kisingizio cha kuandika habari huku wakidanganya kuwa wanafanyiakazi chombo hiki au kile.Hivyo ‘Makanjanja’ wamekuwa wakijulikana kwa sifa ya kugombea vyakula na kudai fedha (mishiko au mikukuta) kutoka kwa vyanzo mbalimbali. Wakishajaza matumbo yao na kupewa mshiko, hutoweka wasijulikane walipoishia.

Ndugu wasomaji hivi sasa ndani ya vyombo vya habari kuna kundi moja linalojumuisha baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi ambao ni watu wazima na taaluma zao lakini kwa makusudi kabisa wameamua kujigeuza kuwa ‘waandishi mabazazi’ ambao moja ya kazi yao kubwa ni kuwakumbatia wanasiasa wachafu ambao huwajaza mapesa mfukoni ili waweze kuwachafua wanasiasa wengine, hata kama wanaoshambuliwa ni watu waaminifu na waadilifu ambao wamekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya umma.

Ndugu Wananchi kundi hilo dogo ,limeamua wazi wazi kuzika maadili ya taaluma yao, heshima zao mbele ya waandishi wadogo na jamii inayowazunguka na badala yake wameamua kuacha kuandika habari zenye ukweli kwa maslahi ya taifa letu na badala yake wamekuwa wakishinda kwenye vikao vya kupanga fitna za kuwachafua baadhi ya viongozi na watu wengine wenye heshima kwenye jamii ili waonekane siyo mali kitu mbele ya jamii.

Kundi hili linatumiwa na baadhi ya viongozi wa CCM na serikali kwa malipo ya fedha, safari za nje ya nchi, na kuwalipia gharama za kwenye vyuo, ili liweze kuwachafua mahasimu wao kupitia kalamu. Kupitia kazi ya kundi hilo, baadhi ya viongozi wa CCM, serikali na watu wenye heshima kwenye jamii wameishaingia kwenye ugomvi wa chini chini na baadhi ya viongozi wenzao kwa sababu ya kundi hilo ambalo limekuwa likitumiwa kuandika habari za kuwachonganisha na kuwachafua viongozi wengine.

Ni kundi hili hili ndilo limekuwa likipendwa na kulelewa na baadhi ya vigogo hao na waandishi wa habari ambao ni makini na wenye kutanguliza maslahi ya taifa mbele katika utendaji wao wa kila siku, viongozi hao wamekuwa wakiwabagua.

Mfano mkubwa wa kundi hili ni wale waandishi wanamtandao waliotumiwa kwa takriban miaka kumi na mbili iliyopita kujenga hoja ya kuwa Watanzania wanawapenda wanasiasa wa mtandao. Waandishi hawa walitumika kikamilifu kuiweka serikali ya awamu ya nne madarakani.

Ukiangalia kwa makini makundi haya mawili kama nilivyoyaeleza , utabaini kundi la ‘waandishi mabazazi’ ndiyo lenye madhara makubwa kwa taifa kuliko lile kundi la ‘makanjanja’. Nasema kundi hili lina madhara makubwa kwa sababu lina vitambulisho vya kufanyia kazi ya uandishi wa habari (press card), kutwa linaambatana na viongozi kwenye safari za ndani na nje ya nchi, lina sauti ndani ya vyombo vya habari, wameajiriwa na wamekuwa wakivujishiwa siri za ndani ya serikali kupitia hao wanaowatumikia ambao nadiriki kuwaita wanasiasa mafisadi.

Kwa ujumla, Rais mwenyewe umekuwa ukiwatumia waandishi hawa mabazazi katika misafara yako na uliwatumia katika kampeni zako. Hivyo changamoto yako Rais lianzie kwako, hapo Ikulu na timu ya waandishi wako, na pia kwenye mtandao wako ambao bado upo na unakutumikia. Tuwe wakweli kwa taifa letu, na mungu atatubakiri kwa hilo.

Rais umetoa changamoto kubwa sana, unataka nchi yenye vyombo vya habari vyenye viwango na madili. Hata hivyo hatuoni juhudi za kuwawezesha waandishi kielimu zikipewa kipaumbele isipokuwa tunaona sasa wakubwa mnasomesha waandishi wenu, wakuwasifu na kuwalamba miguu.

Pia tunaona mfumuko wa vyombo vya habari vya wakubwa, vyenye lengo la kuwasifu wenye vyombo na kuwabomoa wahasimu wao. Rais, hayo ndiyo mambo yanayobomoa badala ya kujenga tasnia ya habari na hapo tulitegemea tusikie sauti yako ikiunguruma.

Kama yote yaliyosemwa ni kweli, tulitazamia tukusikie rais ukizungumzia uhuru wa wanahabari kuandika habari, haki ya wanahabari kupewa habari na wajibu wa viongozi wakuu kutoa majibu haraka na yanayotosheleza wakihojiwa na wanahabari.

Hivyo Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) halina maana kubwa kwa Watanzania kama siyo shirika huru, lisiloendeshwa kiserikali kwa madhumuni ya kuitetea serikali. Kwa nini hao waliokuandalia hotuba hawakukuambia kuwa habari tunazochapisha ni asilimia tano tu ya habari zote hivyo asilimia 95 zimefichwa kwenye mafaili ya serikali chini ya kinga ya usiri. Kwa nini hawakukuambia pia kuwa habari tunazopewa na viongozi wako ni za uhusiano mwema tu na nyingi zimesukwa kuficha ukweli?.

Hata hivyo waandishi wa habari wenye misimamo yao wamekuwa wakivutana vikali na kundi hilo na hatimaye kundi la waandishi wenye msimamo wanaoneka kushinda vita dhidi ya wahuni hao kwani hivi sasa kundi hilo linakabiliwa na wakati mgumu kwani kila habari ya wanayoiandika kwa lengo la kumchafua mtu asiye na hatia, zimekuwa zikikosolewa wazi.

Hivyo basi nilitegemea aliyemwandalia Rais wetu hotuba aliyoitoa kwenye uzinduzi wa (TBC), angemwandalia haya ili rais aweze kusimama hadharani na kulikemea kundi hili la waandishi mabazazi, kuliko kumwandalia hotuba inayokemea ‘makanjanja’. Tunajua kuwa mkuki ni mtamu kwa nguruwe lakini kwa binadamu ni mchungu.

Waliomwandalia rais hotuba hiyo bila shaka ni wale waandishi wa habari wa kundi la mtandao ambao ni sehemu ya kundi la waandishi mabazazi. Wasingeweza kumwambia Rais kuwa aliwatumia vibaya wakati wa uchaguzi, ila yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo, Rais akubali sasa kukemea kundi hili kwa kuwa ni hatari kwa taaluma ya habari hata kama lilimsaidia kuingia madarakani.

Hivyo rais wetu sisi tumepokea changamoto yako kwamba tuzingatie maadili, tutazingatia, lakini namimi nakupa changamoto hii, uwashikishe adabu baadhi ya wanasiasa wa chama chako ili wawe waadilifu. Sisi waandishi wa habari kazi yetu ni kutafuta ukweli na kuutangaza kwa wananchi.

Ikiwa viongozi wengi tulio nao ni wachafu, sisi tuwape sifa gani? Ikiwa kazi kubwa ya viongozi tulio nao ni kuendeana kwa waganga wa kienyeji na kisha kupora fedha za umma sisi tu tufiche habari hizo?

Kwa nini maadili yanaonekana kutoweka kwa waandishi wa habari tu lakini wanaowapotosha hatuwakemei?

Naamini kuwa ukiwaonya viongozi wako na kuwashikisha adabu, ni dhahiri ufisadi unaojitokeza katika tasnia ya habari utakoma. Lakini kama rais utashindwa kuwadhibiti watu hao ipo siku watakugeukia wewe mwenyewe na kuanza kukupaka matope mbele ya jamii. Hatutaki tufike huko.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika

0755 312859
katabazihappy@yahoo.com:www.katabazihappy.blogspot.com

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi,April 17,2008

CUF KUBALINI YAISHE

Na Happiness Katabazi

BABA wa Taifa Julias Kambarage Nyerere aliwahi kusema kwamba ‘ukweli una tabia moja nzuri sana.Haujali mkubwa wala mdogo , haujali adui wala rafiki’.

Hivi karibuni Chama cha Wananchi (CUF) kimeingia kwenye malumbano na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusu namna ya utekelezaji wa makubaliano ya rasimu ya mwafaka wa tatu.

Sasa CCM imesema majadiliano ya mwafaka yaliyochukua miezi 14 ya pelekewe kwa wananchi ili wapige kura za maoni .CUF kwa upande wake inapinga na kusema kuwa hivyo sivyo walivyokubaliana na kwamba walichokubaliana ni mwafaka kutiwa saini.

Awali ya yote, wananchi hawajui kwa kina kanuni za majadiliano hayo wala ajenda kwani miezi 14 vyama hivyo viwili vilifanya majadilino hayo kuwa siri kubwa baina yao.

Na vyama hivyo vilichangamkia mazungumzo hayo kwasababu walipewa donge nono na wafadhili.Kuna mambo kadhaa ya msingi yanayojitokeza kutokana na malumbano hayo.

Moja,mwafaka huu uliotegemewa kutiwa saini kati ya CCM na CUF baada ya mwafaka wa mwaka 1995 na 2000 kushindwa.Mara zote vyama vya upinzani vilikishauri Chama cha CUF kutoshiriki kwenye mazungumzo ya mwafaka peke yake.

Vilipendekeza kwamba vyama vyote vya upinzani viunde timu moja ya kuikabili CCM kwenye mazungumzo ya mwafaka.CUF ilikataa hoja hiyo ikisema kwamba mazungumzo hayo hayavihusu hivyo vyama vingine kwakuwa CUF ina ajenda binafsi isiyo vihusu vyama hivyo vingine kwenye mazungumzo ya mwafaka.

Matokeo yamekuwa kwamba CCM iliihadaa CUF katika mwafaka wa kwanza, ikarudia tena kuihadaa katika mwafaka wa pili na sasa ama kwa hakika hata huu mwafaka wa tatu yawezekana usipatikane.

Sasa imefika wakati tunaweza kuamini kwamba CUF ni CCM B. Kama CUF siyo CCM B, kwanini inaruhusu kuibiwa kwa kura zake ili ishirikishwe kwenye serikali shirikishi?.Na kwa nini mara zote imekuwa ikikataa vyama vingine vya upinzani visishirikishwe kwenye mazungumzo ya mwafaka isipokuwa chama hicho pekee cha upinzani?

Kwa yoyote anayejua siasa za Zanzibar ni wazi sasa kwamba CUF imekata tamaa ya kupata madaraka na njaa yake ya madaraka imekuwa kali mno.Baadhi ya viongozi wako tayari kupewa Umakamu wa rais bandia ili mradi wajulikane nao wapo serikalini.

Ukiliangalia hili kwa undani utaona kwamba miafaka yote mitatu imelenga maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa CUF wanaotamani uongozi kwa gharama yoyote ile kuliko kutanguliza maslahi ya wananchi wenzetu wa Zanzibar ambao ndiyo wanateswa moja kwa moja na mpasuko huo .Kumbe wenzetu hawapiganii mageuzi bali vyeo?

Tunajua kwamba baada ya kumalizika kwa mchakato wa mwafaka wa pili , Maalim Seif Sharif Hamad alirejeshewa kiinua mgongo chake na marupurupu ya Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sasa katika mwafaka huu Seif anataka kuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar?Kama ni hivyo Wanzanzibar waamue kusuka au kunyoa .

Nilazima Wazanzibar waamke na kuibua chama kitakacho jipambanua kama nguvu ya tatu Zanzibar.Wakati CUF inajigeuza CCM B lazima harakati za mageuzi ziendelee kupitia vyama vingine .

Chaguzi zote CUF imekuwa ikilalamika kuibiwa kura na CCM sasa CUF ina ng’ang’ania kuingia kwenye serikali kwa stahili hii itailetea tija gani?.Sote tunakumbuka ni CUF hii hii muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 ilitangaza haitambui urais wa Rais Aman Abeid Karume kwakuwa umetokana na wizi wa kura na hadi sasa haijafuta kauli hiyo.

Kitendo cha CUF kung’ang’ania mwafaka unaokidharirisha chama hicho na kuchora taswira kwamba CCM ndiyo itakayoingiza chama hicho madarakani na siyo kura za wananchi ni kitendo cha usaliti kwa wananchi waliokuwa wanakiunga na wanaoendelea kukiunga mkono.

Ikumbukwe kwamba mamlaka ya kisiasa Zanzibar yanatoka kwa umma wa wananchi wa Zanzibar na wala siyo kwenye mikoba ya CCM.Kwa hiyo CUF kama inafikiri CCM ndiyo itawaingiza madarakani, nasema hivi imepotea njia tena sana tu.

CUF haina mbadala, ila lazima kurudi kwenye majadiliano, kwasababu miezi 14 ilikubali kulala kwenye kitanda kimoja cha mwafaka na CCM , sasa mtoto amezaliwa CCM inamwambia CUF wamtoe mtoto nje ili ndugu ,jamaa na marafiki wamfahamu mtoto huyo ,CUF ina kataa inang’ang’ania mtoto abaki ndani .Je CUF ni kwasababu ina uhakika kwamba mtoto aliyezaliwa ni mwanaharamu?

Kwa nyakati tofauti wiki iliyopita Mwenyekiti wa (CCM) Rais Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba walitueleza mazungumzo hayo yaliyochukua miezi 14 na kwa mujibu wa maelezo yao.

Kumbe walichokuwa wanazungumzia kwa kipindi chote hicho ni jinsi ya vyama vyao kugawana madaraka katika serikali iliyopo hivi sasa, badala ya kuzungumzia wizi wa kura usije tokea Zanzibar.

Kwa hiyo, suala la kwenda kwa wananchi binafsi naona ni la msingi, kwasababu linatupeleka mbele kidemokrasia, kwa kuwa ni haki ya wananchi kuulizwa kauli yao kabla ya kufanyika maamuzi mazito yanayohusu taifa lao.

Naamini kabisa kwamba kule ZanzĂ­bar kuna Wazanzibar ambao si wanachama wa chama chote kile cha siasa lakini pia kuna wananchi wengine siyo wanachama wa CCM wala CUF ni wanachama wa vyama vingine vya siasa.

Hivyo na sisitiza zoezi la upigaji wa kura za maoni likifanyika kama lilivyokusudiwa,litaleta maslahi kwa wananchi, kuliko masilahi ya vyama hivi viwili.

Ieleweke wazi kwamba Tanzania Bara na Visiwani si mali ya wanasiasa, bali ni mali ya wananchi wote hivyo tunataka kuona endapo maoni ya wananchi yatatolewa,yaheshimiwe kwa maslahi ya wananchi wa pande hizi mbili za muungano.

Umoja ni nguvu ,wabinafsi ni adui zetu.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano ,April 9 mwaka 2008

SERIKALI IWE MAKINI NA UTITIRI WA MAKANISA

Na Happiness Katabazi

IBARA ya 19(1) ya Katiba ya nchi, inasema kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.

Ibara ya 19(2) inasema kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.

Kwa mujibu wa vifungu hivyo vya ibara hizo, tunaona taarifa zilizolisibu Kanisa la Assemblsy of God la Mikocheni B’ linaloongozwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM)Mchungaji Dk.Getrude Rwakatare hivi karibuni kwamba watoto wachawi wawili, waliokuwa wanasafiri kwa ungo walivutwa na kudondoka katika eneo la ibada la kanisa hilo, ni za kusikitisha sana.

Kwanza, habari hizo zina lengo la kupambanisha imani ya kichawi na imani ya Mungu. Lakini zote ni imani, na tayari ibara 19(1) ya Katiba inampa kila mtu haki ya kuwa na imani anayoitaka.

Hao wanaoamini katika kusafiri kwa ungo nao wana imani inayolindwa na katiba sawa na wanaoamini imani ya Yesu.Kwa hiyo tunashangaa ni kwanini watu waanze kuadhiriana kwa mambo yasiyo ya msingi, au labda ni ya kitapeli, ya kutafuta biashara ya waumini.

Lakini tujue kwamba, hili linatia dosari kwa wale wanaotangaza na kueneza dini, japo ibara 19(2) imewalinda na kuwahakikishia kwamba serikali haitaingilia shughuli za uendeshaji wa jumuiya za dini, watakapofanya mambo yanayoweza kuvunja amani ya jamii au hata kuhatarisha maisha ya waumini wao, dola haitakuwa na budi kuingilia kati.

Uhuru wa kuabudu hauwezi kutumika pale baadhi ya wachungaji watakapogeuza taasisi za dini kuwa vyombo vya ufisadi, ambapo matendo machafu yanayovunja maadili, biashara chafu zinazoenda kinyume cha sheria na utapeli wa kawaida unafanyika.

Tukumbuke mfano mmoja wa Uganda pale mchungaji mmoja aliyeitwa Kibwetere alipoangamiza wafuasi wake kwa kutumia wafuasi wa dini.

Jambo kama hilo hilo liliwahi kutokea Novemba 18 mwaka 1978 nchini Guyana, ambapo James Warren aliyejulikana kwa jina la Jim Jones alipounda kanisa lake kule Guyana katika visiwa vya Caribbean na kuua waumini wake 900 kwa sumu ya cyanide, wanaenda kumuona Yesu.

Basi, kwa kuwa dunia imejaa matapeli wa aina hii na dini sasa hivi zimekuwa biashara kubwa hapa nchini ambapo baadhi ya wajanja anakimbilia huko, ingefaa jamii itahadharishwe kuwa si kila anayehubiri dini ni kweli ni mtumishi wa Mungu.

Wapo manabii na watumishi wa Mungu feki wengi sana huko mitaani na yafaa wananchi wachukue tahadhari, kwani hawa wanasingizia kufanya miujiza lukuki na kutoa upako kwa jinsi ambavyo ni ya kushangaza.

Hivi sasa kuna kanisa limetangaza kutoa misukule. Yaani mtu aliyefariki miaka mitano au zaidi iliyopita, eti mchungaji anaweza kumrudisha? Hii inatisha!

Wanajua wananchi wengi wako katika hali ngumu ya maisha, wanakabiliwa na umaskini wa kupindukia, maradhi yasiyoponyeka kama ukimwi, kansa, na msambaratiko wa maisha ya ndoa, basi kwa kuhisi kuwa wana ufumbuzi wa haya yote, wanafanya ibada feki za kuwahadaa wananchi.

Kwa upande mwingine, tunaitahadharisha serikali kwamba utitiri wa taasisi za kidini ni ishara mbaya kwa utawala uliopo madarakani.

Ina maana kwamba hayo matatizo tuliyoyataja hayajapatiwa ufumbuzi na wananchi wamekata tamaa, hivyo ni rahisi kughiribiwa na wajanja wanaotumia dini kujinufaisha.

Tusije tukashangaa yale ya Jim Jones na Kibwetere yakitokea hapa Tanzania na hilo linaweza kuhatarisha amani ya nchi.

Tujiulize maswali, je, hawa watoto matapeli ambao Jeshi la Polisi Kinondoni lina rekodi zao, waliwezaje kumhadaa mchungaji mwenye aiba ya upako wa Roho Mtakatifu kama Dk.Rwakatare?

Tujiulize pia kazi iliyofanywa na taasisi za dini kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, na baada ya hapo, mbona viongozi wa dini na madhehebu ya Kikristo walishiriki kuwarubuni waumini wao kupigia kura mgombea waliyemtaka kwa madai kuwa mgombea huyo alikuwa amechaguliwa na Mungu wao?

Je, huo haukuwa utapeli wa wazi? Walikutana wapi na Mungu wao akawanong’oneza kwamba mwanasiasa huyo alikuwa chaguo lake?

Tangu lini mtu asiyemwamini Yesu kuwa ni mwana wa Mungu na Mungu kamili kwa sura ya binadamu na kwamba alikufa na kufufuka, akawa chaguo la Mungu wa Wakristo?

Mbona hata baadhi ya viongozi wa dini wametumia nafasi zao za dini kujitafutia vyeo kwenye vyama vya siasa?
Je, hizo sadaka na michango wanayopokea kutoka kwa mafisadi na hizo shughuli za uchangishaji wa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa kidini unaofanywa na wanasiasa na baadhi ya mafisadi wanaojulikana, ndiyo njia muafaka ya kueneza shughuli za dini?

Sasa mwananchi wa Tanzania akimbilie wapi, akienda kwenye dini anakuta ufisadi, akienda kwenye jamii anakuta ufisadi, akienda kwenye siasa anakuta ufisadi, sasa kimbilio la Mtanzania litakuwa wapi?

Matukio ya kiimani yanayotokea katika baadhi ya makanisa siku hizi, yatufumbue macho na masikio ya kila mmoja wetu, kwani nyakati zimebadilika, viongozi wametugeuka na hakuna wa kumuamini.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

0755 312859
katabazihappy@yahoo.com:www.katabazihappy.blogspot.com

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi Machi 3,2008