NECTA PAMECHAFUKA,PASAFISHWE

Na Happiness Katabazi

IMEANZA kuwa mila na desturi kwamba kila mwaka kipindi cha mitihani ya taifa ya kidato cha nne, zinakuwepo taarifa za kuvuja kwa mitihani hiyo.

Inapovuja, wanaotiwa nguvuni ni watahiniwa wanaodaiwa kukutwa na majibu.

Hata siku moja, Jeshi la Polisi lenye makachero wengi halielezi limewakamata wanaodaiwa kuvujisha mitihani. Nikirifikiria, napata mashaka juu ya utendaji wa makachero wa jeshi hilo.

Mapema Oktoba mwaka huu, wanafunzi wa kidato cha nne kote nchini walianza kufanya mtihani wa taifa. Siku tatu kabla, vyombo vya habari viliwakariri baadhi ya watahiniwa hao wakisema mitihani imevuja.

Kama ilivyo ada ya watawala kupinga hata mambo ya wazi, walikubali kwa shingo upande kwamba mtihani wa hisabati umevuja na kujinasibu, mitihani mingine haijavuja.

Hivyo, Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), walilazimika kuahirisha mtihani wa hisabati hadi Oktoba 27. Wanaoitakia mema nchi yao waliendelea kusema wazi kwamba mitihani yote imevuja.

Lakini, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mtendaji wa NECTA, Joyce Ndelichako, walishupaza shingo zao na kubuni mbinu mpya ya kuwakimbia wanahabari.

Tukio la mwaka huu, ni tofauti na miaka mingine ambapo ilivuja kwa kuipora, ilipokuwa ikisafirishwa kwenda mashuleni. Kwa mtazamo wangu, safari hii, imevuja ndani ya ofisi za NECTA iliyokabidhiwa jukumu la kitaifa.

Nafahamu, mtihani unapima kiwango cha uelewa wa mwanafunzi kwa aliyofundishwa katika kipindi cha miaka minne. Kuvuja kwa mitihani kunaharibu dhumuni lake.

Mwanafunzi anayepata mitihani iliyovuja, anajijengea msingi wa kushindwa kuelimika, anakuja kufanya kazi ya kitaalamu bila uelewa, mwisho wa siku analeta madhara kwa taifa. Nalazimika kuamini yaliyotokea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ulipofanyika upasuaji tata, ni mtiririko wa wataalamu feki.

Ni dhahiri kwamba mchezo wa kuvujisha mitihani unaimarika, ndiyo maana Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Idara ya Usalama wa Taifa, haliwagusi tatizo hili linalohatarisha usalama wa taifa letu.

Niliamini, baada ya taarifa za awali, wahusika wangeingia mtaani kuchunguza mtihani umevuja kwa kiwango gani, badala yake NECTA inajichunguza yenyewe.

Kwa kuwa Mungu amfichi mnafiki, amewafunulia Watanzania ‘uozo’ wa kufunga mwaka, unaofanyika ndani ya ofisi za NECTA. Mwanzoni mwa wiki hii, imeripotiwa kwamba baraza hilo limesambaza vyeti bandia vya matokeo ya kidato cha nne mwaka jana (result slip) kwenye shule mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa habari hiyo, wanafunzi walioathirika ni waliohitimu kidato cha nne mwaka jana. Baadhi yao wamepata misukosuko ikiwemo kufikishwa mahakamani kwa maidai ya kughushi.

Mmoja wa waathirika hao ni Alexander Gundula (22) aliyekuwa mahabusu mjini Mbeya, kwa kosa la kupatikana na cheti feki, lililofanywa na NECTA.

Huyu alikuwa miongoni mwa askari wanafunzi wa Chuo cha Magereza Kiwira. NECTA imekiri udhaifu na kumwomba radhi kijana huyo kwa maandishi.

Katika hili, nampa pole Alexander kwa msukosuko na kulipongeza Jeshi la Magereza na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Azania, kwa sababu wametimiza wajibu wao kikamilifu.

Wakati nikitoa pole na pongezi kwa makundi hayo, walaaniwe baadhi ya watumishi wa NECTA walioshiriki kutengeneza ‘result slip’ feki ya kijana huyu na wengine. Nawalaani kwa sababu watu hao wanacheza na maisha ya watoto ambao wazazi wao walijinyima ili kuwapeleka shule.

Nalazimika kuamini kwamba, mchezo huo haujaanza leo, kwa sababu Azania ni shule iliyopo jijini Dar es Salaam, kama wameweza kufanya hivyo hapo, kwenye sekondari za vijijini hali itakuwa mbaya zaidi.

Kwa tukio hili, kila aliyemaliza kidato cha nne hapa nchini asijiamini kwamba cheti alichonacho si halisi, ni cha kughushi, hivyo kila mtu kwa wakati wake analazimika kufika NECTA ili kukihakiki.

Tukio hili lisipodhibitiwa, ni dhahiri kwamba wananchi watajenga chuki kwa serikali yao kwa sababu ya dhuluma kama hii kutoka kwa watumishi wake ambao mishahara yao inatokana na kodi za wananchi.

Vijana wataona hakuna umuhimu wa kusoma, badala yake watatafuta fedha za kuwahonga baadhi ya watendaji wa NECTA ili wauziwe vyeti. Tusifikishwe huko.

Nalazimika kuamini kwamba NECTA imeoza, hivyo inahitaji kupanguliwa. Haiingii akilini kuwa ofisi hii ya umma inakumbwa na kashfa halafu kiongozi wake hataki kujiuzulu, wala hatusikii watumishi wake wakifikishwa mahakamani.

NECTA inapokumbwa na uozo wa namna hii, naamini serikali na vyombo vyake vimeshindwa kazi, vimepania kuliteketeza taifa letu.

Wananchi tumeipa dhamana serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ituongoze, ikitokea baadhi ya vyombo vyake vya utendaji vikashindwa kutimiza wajibu na hatuoni viongozi kushtuka, maamini umefika wakati wa kuiwajibisha serikali.

Migomo ya kudai haki, ubadhirifu wa fedha za umma ni matukio yaliyotamalaki na hakuna jitihada zozote za serikali kuwashughulikia watuhumiwa.

Nalazimika kukubali kwamba nchi inaelekea pabaya, moyo wa kizalendo kwa wananchi na taifa umetoweka na baadhi ya watawala ni wachumia tumbo. Wakati umefika kila Mtanzania kwa nafasi yake kubadili tabia.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

0755 312 859
katabazihappy@yahoo.com
Chanzo:Gazeti la Tanzania la Alhamisi, Oktoba 30 mwaka 2008

MSAFARA WA JK KUPIGWA MAWE:TUMEVUNA TULICHOPANDA

Na Happiness Katabazi
WIKI iliyopita vyombo vya habari vya hapa nchini viliripoti habari kwamba msafara wa Rais Jakaya Kikwete umepigwa mawe katika kijiji cha Kange wilayani Chunya mkoani Mbeya, ambapo rais alikuwa na ziara ya kikazi mkoani humo.

Hakuna sababu ya kulionea haya tukio hili la msafara wa rais Kikwete kupigwa mawe kwasababu mficha uchi azai.

Hivi sasa Tanzania inavuna ilichopanda.Kuna namna tatu ya kuliangalia tukio hili.Ulipopigwa mawe mkutano wa chama cha CHAUSTA kule Tarime Agosti 29 mwaka huu, hakuna mtu aliyepoga kelele kwasababu mkutano wa chama hicho ni sawa na kifaranga na wala haikuonekana ni ishara mbaya kwa nchi.

Hakuna mtu aliyepiga kelele mkutano wa NCCR-Mageuzi uliofanyika Agosti 31 mwaka huu, huko Tarime kwasababu waliona NCCR-Mageuzi ni kitu gani.

Siku chache baada ya mkutano wa NCCR kupigwa mawe aliyekuwa wakwanza kujibu ni Dk.Willbroad Slaa aliyesema mwanasiasa anayefanya siasa zinzokera unampiga mawe.Hakuna aliyepiga kelele alipopigwa jiwe Mwenyekiti wa (DP) Mchungaji Christopher Mtikila.

Haya mambo wamefanyiwa watu ambao ni wanasiasa wakitekeleza wajibu wao wa kisiasa.Ukishaalalisha hayo huna sababu ya kulaani kupigwa mawe kwa msafara wa Kikwete.
Kwa sababu tumeishajijengea utamaduni wa kupigana mawe kwa kipindi kifupi.

Hiyo ni namna moja ya kuliona hilo jambo.Basi tuvune matunda haya japo ni machungu.Hivyo kukurupuka kwa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kwenda kukamata vijana zaidi ya 60 eti ndiyo waliorushia mawe msafara huo,inashangaza sana.

Namna ya pili ya kuliona hilo jambo,ni utendaji kazi wa rais Kikwete na serikali anayoingoza ambayo utendaji wake unakatisha tamaa na kuwakosesha matumaini wananchi kwakuwa inaonekana wazi rais ana huruma na mafisadi lakini hana huruma na wannachi wake wema wanaogelelea kwenye lindi la umaskini.

Rais na serikali yake imekaa kitako na kujadiliana na mafisadi walioiba fedha za EPA, hata fisadi mmoja hadi leo hii ajatajwa kwa hiyo hawa mafisadi ni waheshimiwa.Kwa kuwa rais amewakumbatia mafisadi na kuwatupa mkono raia wake, hivyo raia wake wamebakia na njia ya kufanya vitendo vya kupiga mawe viongozi na kuwazomea.

Ipo siku tutaona watu wakijitoa muhanga wa kujilipua mabomu na hapo ndipo tutakapotambua Watanzania ni binadamu kama binadamu wengine duniani kwamba nao wanapata na kusikia njaa, mateso,wanakata tamaa na wanaweza pia kujilipua na mabomu.

Kwa hiyo cha msingi sio kukataa msafara wa rais Kikwete haujapigwa mawe, tukubali yaliyotokea na tuyatafutie ufumbuzi na yaliyotokea ni ishara ya taifa lililokata tamaa.

Maisha bora kwa kila Mtanzania yako wapi?Wale waliowavalisha wananchi T-shirt,kapero,skafu,kuwalisha pilau wananchi hivi leo wako wapi?Hao ndiyo wanaotakiwa kujibu hoja ya msafara wa rais kupigwa mawe kwa kuwa matumaini yaliyoamshwa na hizo Tshirt,kapero,skafu na pilau yamekufa.

Kama rais anataka aendelee kuwa mpendwa wa watanzania aache kutangatanga nchi za nje, apambane na umaskini unaowakabili wananchi wake ,awape Watanzania matumaini kuwa umaskini unaopindukia sasa utakomeshwa.

Aoneshe hatua za wazi wazi za kukomesha umaskini miongoni mwa watu wakawaida kwa kusimamia miradi ya uzalishaji viwandani,mashambani kwa namna ambayo kukuwa kwa uchumi na kuongezeka kwa ajira na kuongezeka kwa kipato kwa mtu wa kawaida.

Rais Kikwete asisimame na kuona walimu wanateseka akakaa kimya kwani kwenye kampeni za mwaka 2005 alipowaaidi walimu kuwa atawatatulia matatizo yao , alikuwa anaomba kura tu?

Rais Kikwete asisimame na kuona migomo ikisambaa nchi nzima ya walimu,wanafunzi, wafanyakazi wa NMB, na sasa atakuja kupata migomo ya wakulima akazani kila kitu bado kipo shwari.

Rais Kikwete asisimame na kuduwaa anapoona bomoabomoa inayofanywa na vyombo vyake vya serikali na uchukuaji wa ardhi ya wakilima na wafugaji nchini ili kuwapisha wawekezaji akazani kuwa Watanzania watakubali kuishi kama wakimbizi kwenye nchi yao.

Rais Kikwete asifikiri Watanzania wa leo ni sawa na Watanzania wa jana ambao unaweza kuwaundia tume za kuchunguza mikataba ya Richmond,EPA,madini nk.na kisha ukafukia kashfa hizo kwenye mafaili ya Ikulu usichukue hatua zozote.

Rais Kikwete anapojizungushia marafiki ambao wanatuhumiwa kuwa ni mafisadi anatazamia wananchi wamweke kwenye fungu gani?Je si kweli ndege wenye manyoya yanayofanana wanaruka pamoja?

Namna ya tatu ya kuliona jambo hili ni yale mawe yaliyorushwa kwenye msafara aliyataka mwenye rais Kikwete, kwa kuwakorofisha watu wa Mbeya.Kwa sababu mwaka 2005 watu wa Jimbo la Kyela walimkataa John Mwakipesile asiwe mbunge wao wakamchagua Dk.Harrison Mwakyembe awe mbunge wao.

Sasa kama rais aliwapenda kikwelikweli watu wa Mbeya asingemteua Mwakipesile kuwa Mkuu wa Mkoa huo kwasababu kufanya vile ni kugombanisha watu wa Mbeya .Kama anampenda Mwakipesile angemteua kwa nafasi hiyo hata zaidi ya nafasi hiyo katika mkoa mwingine.

Lazima tuwe wa kweli kwa rais wetu, kwa namna mmoja ama nyingine rais anasababisha mgogoro ndani ya mkoa huo.Hao washauri wake hawakwambii ukweli au wanamshauri vizuri anapuuza ushauri wao?.

Hivyo hili la Mbeya hatutaki maelezo ya kipumbavu kwamba waliopiga mawe msafara wa rais walikuwa walevi wa pombe, watu wa Mbeya ninavyowafahamu mimi siyo walevi kihivyo ni watu wenye hoja ambazo rais na serikali yake wanakataa kuzisikiliza.

Ieleweke wazi hatutetei matumuzi ya fujo ,silaha,umwagaji damu katika kutafuta ufumbuzi katika medani ya siasa, tunasema kwamba tulizarau mwiba sasa umetuchoma ,tusiamaki,tuanze upya kwa kuutoa mwiba,kutibu kidonda ,tuendelee.

Na kuondoa mwiba hapa ni kumuondoa Mwakipesile kwa kumuamishia mkoa mwingine na kutibu vidonda ni kuwaachilia huru vijana waliokamatwa na jeshi la polisi mkoani humo ili taifa letu liende mbele.

Mungu Tanzania,Mungu ibariki Afrika

0755 312859
katabazihappy@yahoo.com;www.katabazihappy.blogspot.com
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi,Oktoba 23 mwaka 2008

MWALIMU NYERERE NATAMANI UONE TUNAVYOKUENZI



Na Happiness Katabazi

MWALIMU Julias Nyerere Baba wa Taifa letu,jana tumeadhimisha miaka tisa tangu ulipotutoka Oktoba 14,1999, na tukakupumzisha kwa amani katika Kijiji ulichozaliwa cha Mwitongo-Butiama mkoani Mara.Tunaendelea kukuenzi baba japo kwa mitindo mbalimbali.Tukikuita baba kwa sababu wewe ni mwasisi wa taifa letu la Tanzania.

Baba,ulikuwa Mwalimu wetu na hata leo hii unaendelea kutufundisha katika yale yote uliyotuusia.Kuondoka kwako kulituachia majonzi mazito ambayo uzito wake haujapungua hadi leo.

Tunazidi kukukumbuka baba na tunaendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi yetu ya kukuenzi milele na milele.

Baba katika wingi wetu wapo wanaokuenzi au tupo tunaokuenzi kikweli kweli na wapo wanaokuenzi kinakfi.
Kwa sababu hiyo na kwa mara nyingine tunakusii uchungulie duniani na ujisomee na kujionea mwenyewe yale yanayojiri katika harakati za kukuenzi siku hadi siku.

Baba, si unakumbuka kile chama ulichokiasisi mwenyewe,mapema mwaka huu kilikuenzi wazi wazi pale kilipoamua kufanya kikao chake cha Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) katika kijiji ulichozaliwa Butiama ambako mwili wako ilipopumzishwa ukingojea parapanda ya mwisho.

Katika kikao hicho vigogo wa chama chako cha CCM, walikuenzi kwa kuibuka na Azimio la Butiama ambalo lilitutoa machozi tukikukumbuka kwa kuwa lilielekea kupingana na kile ulichokiamini pale waliposhindwa kuamua kukataa kuridhia makubaliano yao na CUF kuhusu Mwafaka wa kisiasa Zanzibar, badala yake wakapiga kalenda mwafaka huo kwa kusingizia suala hilo likapigiwe kura na wananchi.

Mbaya zaidi baba, wakaibuka miongoni mwetu wakaamua kuuenzi Muungano uliouasisi wewe na Mzee Abeid Aman Karume, kwa mabishano makali juu ya ‘Zanzibar ni nchi au laa’.

Usishangae baba hivi ndivyo tunavyolienzi onyo lako kwamba tusithubutu kubaguana maana dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu.

Vilevile baba wakiwa kule Butiama waliamua kukuenzi kwakukumbatia wahujumu uchumi lakini usishangae siku hizi wahujumu uchumi tunawaita ‘mafisadi’, badala ya kuwatimua uanachama kama ambavyo ungependa iwe lakini walitetewa, kuchekewa na kupakatwa.

Baba, kile chama ulichokiasisi si kimoja tena ila ni chama ambacho kimeamua kukuenzi kwa kuunda makundi na mitandao yenye kuasimiana na kuhujumia .Ipo mitandao mingi baba, kuna kundi la mtandao halisi, mtandao maslahi na mtandao majeruhi ambayo utendaji wake unatia shaka na wasiwasi juu ua jinsi gani watakavyokuenzi ifikapo uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Kukuenzi kwetu baba kupo pia kwenye Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM), samahani baba hata huko kuna mkataba feki umeingia.

Tunakuenzi kwa kumkemea na kumshughulikia kwa hira mjukuu wako jasiri, Nape Moses Nnauye ambaye alilalamikia wazi wazi uchafu wa mkataba wa mradi wa jengo la UVCCM kwa kumfukuza uanachama wa jumuiya hiyo.

Kwa ujumla baba nchi inakuenzi kwa kukosa viongozi bora.Hivi sasa tunaviongozi ambao ni mahiri wa kuendesha ‘Fund Rising’,Viongozi wetu walio wengi ni mahiri kuheshimu hotuba na nukuu zako ila matendo yao yako mbali na kile wanachokisema.

Wapo waliodiriki kukuenzi kwa kutumia majukwaa ya kidini ili wajitakase ufisadi wao.Wengine wanakuenzi kwakusema uongo mchana kweupe.Wapo wanaoamini fedha ni msingi wa maendeleo hata wanajilimbikizia ‘vijisenti’ ughaibuni.

Kukuenzi kwao ni kukudharau wewe baba yetu uliyekufa maskini bila kuliibia taifa.

Tunakuenzi baba kwa kuendeleza mapokezi ya kishindo kwa viongozi wetu.Utakumbuka baba ,watanzania walivyokupokea wakati unatoka Umoja wa Mataifa kwa kukuimbia ‘baba kabwela,baba kabwela’.

Tunaendeleza wimbo huu hususani majimboni kwa kuwaimbia ‘baba kabwela’ viongozi wanaokumbwa na kashfa nzito za ufisadi ambazo zimewaladhimu kujiudhuru nyadhifa zao za serikalini.Wana CCM wenzio wanakuenzi kwa kuwafanyia sherehe kubwa kana kwamba makosa yao ni mambo ya kujivunia.

Yule mwanafunzi wako katika medani ya siasa Kingunge Ngombale-Mwiru ambaye sasa amezeeka kiumri na amechoka kimawazo ameamua kukuenzi kwa kuwatishia vijana wako wa ccm wanaokemea maovu ndani ya chama na serikali kwamba hakuna mtu maarufu kushinda chama.

Baba ,viongozi wetu inabidi wakumbuke maneno ya Yesu Kristo aliyowaambia watu wa taifa la Uyahudi,kwamba “Hamjui kwamba mnaye baba mwingine,ninyi si watoto wa Ibrahim,ninyi ni watoto wa ibilisi,kwa kuwa ibilisi amekuwa mwongo na mnafiki tangu mwanzo,nanyi mnayatenda hayo hayo kama baba yenu”.Sasa baba ,wanao tunapojivunia ubaba wako,baadhi ya yetu wanaye baba mwingine ambaye si wewe!Baba yao ni beberu(bepari aliyekomaa),kwani bepari amekuwa mnyonyaji,tangu mwanzo hata leo hii,angali akinyonya kwa kutumia utandawazi,ubinafsishaji na kuendekeza masilahi binafsi.Viongozi wetu wa leo mnamuenzi baba yupi?

Baba tunaendelea kushangaa na kujiuliza hasa tunaposoma andiko lako la “Uongozi wetu na hatima ya Tanzania”.Baba utakumbuka mwanafunzi wako uliyetuachia na ukatudhibitishia ni msafi, aliamua kukuenzi kwa kuigeuza Ikulu kuwa pahala pa ujasiliamali.

Akuishia hapo baba alijimegea pande la nchi hii na kulifanya mali yake binafsi katika harakati za kudhibitisha usafi alionao.

Amekuenzi kwa kuwa mwanafunzi wako mzuri maana kama ulivyosema unang’atuka naye mwezi uliopita ametangaza kung’atuka katika shughuli zote za kisiasa, sasa anaelekeza ujasiriamali wake katika dini.

Samahani baba, imekuwa ndiyo tabia yetu sasa kwamba mhujumu uchumi asikamatwe wala kushitakiwa bali abembelezwe kulipa kidogo kidogo kile alicholiibia taifa.

Si unakumbuka baba ulituambia kwamba ulimchukulia hatua yule raia wa kigeni aliyesema serikali yetu ipo mfukoni mwake,hukungoja ushaidi wala kupoteza muda wala kuunda tume .Sisi baba tumeamua kukuenzi kwakufanya kinyume.

Baba tunakuenzi hata kwakuizalilisha nafasi yako ya kwanza kabisa ya Uongozi wa kiserikali uliyoishika muda mfupi baada ya nchi kupata uhuru .Baba siunamkumbuka yule kijana wako uliyemshangaa mwaka 1995 kwamba utajiri wa chapchap ameupata wapi; amekuenzi kwa kutumia nafasi hiyo ya Uwaziri Mkuu vibaya kiasi cha kuliingiza taifa hasara kubwa pale aliposhinikiza nchi iingie mkataba na kampuni ya kihuni ya Richmond .

Baba kwa mara ya kwanza katika historia, kijana huyu na vijana wenzake Nazir Karamagi ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Ibrahim Msabaha, iliwalazimu kukuenzi kwa kujiuzulu.

Tunaendelea kukuenzi baba kwa kupuuza mafunzo yako ya kwamba kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuheshimiwa utu wake badala yake baba tunakuenzi kwa kuzuliana kashfa, vifo na uongo kila kukicha.

Kwa mfano baba tumefikia hatua ya kusemana adharani kwamba kiongozi huyu ndiye kamuua kiongozi yule ama anataka kumuua.Kashfa hizi baba zinakaribia kutuingiza kwenye uvunjifu wa amani uliyotuachia.Sasa tumeanza kuenzi amani hiyo kwa kutwangana mawe, kuzomeana kwenye mikutano ya ardhara ya vyama vya siasa.

Baba tumezidi kukuenzi kupitia ile sera uliyoacha tumeianzisha ya ubinafsishaji.Utakumbuka baba hukupenda tuuze au tubinafsishe benki zetu wala rasilimali zetu.

Samahani baba hatukukusikiliza tukaziuza benki hizo ikiwemo Benki ya Makabwela(NMB).

Tulidhani baba tukiuza benki hii tunafanya jambo la maana kumbe tunasababisha matatizo makubwa ambayo hivi juzi ilisababisha wafanyakazi wa benki hiyo nchi nzima wakagoma kwa siku mbili mfululizo.

Na hivi leo tunavyokuenzi bado tunaugulia maumivu yaliyotokana na mgomo huo.Mbali na hilo baba tumekuenzi kwa kuuza lilokuwa Shirika la Reli(TRC).Samahani mwekezaji tuliomuuzia hana fedha kiasi kwamba kila siku anakwenda serikalini kulialia ili serikali imsaidie kulipa mishahara wafanyakazi.

Hatuna uhakika kama kilio chake hiki ni cha kweli au ana lake jambo na hao walimpigia chapuo la kuendesha Shirika hilo na wale wanaoidhinisha asaidiwe fedha za kuwalipa mishahara wafanyakazi.

Baba, tumekuenzi kwa kuvunja rekodi ya ziara ulizozifanya kwa kutembele nchi mbalimbali ulimwenguni.

Utakumbuka baba yule kijana wako ambaye wakati anaondoka duniani alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa , sasa hivi ndiye mkuu wa Kaya yako ameamua kukuenzi kikwelikweli kwa kujizolea sifa mbalimbali, moja wapo ya sifa alizonazo ni uwezo mkubwa wa kulimudu vyema somo la Giografia hususani matumizi ya Atlas.

Ni umahiri huo ambao unamuwesha kuvunja rekodi kwa rais wa taifa uliloliasisi aliyetembelea nchi nyingi kwa muda mfupi.

Baba, nitakuwa natenda dhambi kama sitakueleza hili kwamba uendelee kumuombea mkuu wetu wa Kaya Rais Jakaya Kikwete, aendelee na moyo wake wa kuruhusu uhuru wa watu kutoa maoni kwani katika hili binafsi nampongeza.

Huko ulipo baba, uendelee kumuombea kwa mungu ili asibadilishe msimamo wake wa kuturuhusu sisi wananchi wake kutoa maoni.

Katika hili baba nampongeza Kikwete kwani hivi sasa baba ruksa kuikosoa serikali na viongozi wake licha kuna baadhi ya watendaji wake wanakosa uvumilivu.

Tunakuenzi baba kwa kudumisha demokrasia ya vyama vingi.Na utakumbuka ulishauri vyama vingi viwepo na vikawepo ila ukaonya visiwe utitiri.

Utuwie radhi baba kwani kadri muda unavyozidi kwenda vyama vingi vilivyoanzishwa nchini vinazidi kuwa dhaifu.

Sababu ni nyingi za udhaifu huo miongoni mwa udhaifu huo ni kuama ama kwa vijana wako walioamua kukuenzi kwa kuendekeza uchu wa madaraka na binafsi.

Leo hii wakikosa madaraka hapa kesho wakikosa ruzuku pale wanaamua kukimbilia kwingine.

Baba vipo pia vyama vilivyoamua kuenzi mtizamo wako wa umoja na mshikamano kwakuanzisha ushirikiano miongoni mwao japo mara kadhaa vyenyewe kwa vyenyewe vinafanya mambo yanayoashiria kutokuwa na nia ya dhati ya kushirikiana.

Samahani baba demokrasia uliyotuachia tumeshindwa kuifanya ikomae.Baba ulipenda uhuru wa vyombo bila unafki licha katika utawala wako vyombo vya habari vilikuwa ni vichache na uliwapenda pia waandishi wa habari , ni bahati mbaya tumeamua kukuenzi kwa kuuminya uhuru huo na kuwafanyia matendo ya hiana baadhi ya wanahabari.

Mathalani wapo waliokuenzi kwa kuwamwagia tindikali na kuwatishi kuwaua au kwapeleka mahakamani waandishi wa habari, na kuvinyima baadhi ya vyombo matangazo ya kiserikali ili kuvidhoofisha.

Kwa upande mwingine baba, wapo wanaandishi wa habari wenzetu ambao kwa makusudi wameamua kujigeuza ‘disposable tissue’ za wanasiasa manyang’au ambao wanabaka uchumi wa taifa kwa kuwaandikia habari na makala za kuwasafisha ili jamii iwaone ni wanasiasa wema.

Aidha, baba tunakuenzi kwa mifumuko ya migomo na maandamano ya kila kukicha.Hata leo walimu nchi nzima wanatarajia kuanza mgomo usiyonakikomo ili kushinikiza serikali iwalipe haki zao.

Wanafunzi wa Shule za msingi na sekondari nao pia hivi karibuni waliandamana wakipinga ongezeko la nauli.Haijawahi kutokea tangu taifa lipate uhuru.

Huko kwenye Vyuo Vikuu ndiyo usiseme migome imekuwa ni jadi.Pia baba hata mahabusu nao mwaka huu waligoma kushuka kwenye makarandika na wengine waligoma kula wakishinikiza kesi zao zisikilizwe haraka kama zilivyo za mahabusu wengine ambao wanaujaama na vigogo au walikuwa watumushi wa ngazi za juu serikalini.

Baba katika utawala wako elimu ilikuwa ikitolewa bila ubagudhi na kusema watoto wa wakulima na wafanyakazi lazima wapate elimu, lakini hivi sasa tunakuenzi baba kwa kutoa elimu kwa madaraja katika vyuo vikuu.

Baba nao wana Tarime juzi waliamua kukuenzi kwa kukiadhibu vikali chama chako na badala yake wakakipigia kula za ndiyo chama CHADEMA ambacho ulivyokuwa hai uliwai kusema chama hicho cha upinzani kina sera nzuri.

Siyo tu walikitosa chama chako bali wana Tarime waliakikisha wanakula sahani moja na chama chako ambacho hivi sasa kinaonekana kuishiwa sera katika chaguzi zake na badala yake kimekuwa kikitumia hira za kila aina kupata ushindi lakini Mungu amfichi mnafiki,mbinu hizo za hira zimeweza kutokomezwa na wana Tarime.

Nikuume sikio baba, katika uchaguzi huo ulifanyika Jumapili iliyopita, vyama viwili vya CHADEMA na CCM ,baadhi ya wafuasi wake walikuwa wakiudhuria mikutano ya kampeni na silaha za jadi na ikafikia mahala wafuasi hao kujeruhiana kwa silaha za jadi ikiwemo mapanga.

Licha ya Katibu Mkuu wa chama Yusuf Makamba, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja, Waziri Kilimo,Chakula na Ushirika Steven Wassira,Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi John Chiligati, Kaimu Katibu wa Kitendo cha Propaganda Tambwe Hiza, ambaye huyu utakumbuka alikuwa ni yule kijana alikuwa CUF na akawa anakisakama sana chama chako lakini hivi sasa amesalimu amri amejiunga na chama chako na kupewa cheo chapchap,chama ulichokiadidi hazikufua dafu mbele ya Chadema.

Jitihada zao za kuwepo kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Tarime hazikuza matunda.Ama kwa hakika jopo hili la viongozi wa chama na serikali uwepo wao katika kampeni za uchaguzi mdogo halafu uwepo wao ukashindwa kukiletea chama chako ushindi,nadiriki kutamka kumemeendeleza wimbi la kukipaka matope chama chako na kuonyesha ishara mbaya chama chako kwenye chaguzi zijazo.

Sikufichi baba, katika uchaguzi huo mdogo chama chako nacho kiliamua kukuenzi kwa kutumia ‘mijihela’ mingi kiasi cha Sh bilioni moja kwaajili ya kampeni, kukodisha Helkopta ili kuwaamasishe wananchi wa Tarime wakipe kura.

Lakini wananchi hao waliwepa pamba masikioni na kuichagua CHADEMA ambacho pia nacho tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 hadi uchaguzi mdogo wa Tarime,kimeamua kimeamua kukuenzi kikamilifu kwa kutumia Helkopta katika kampeni zake.

Kwa kifupi, baba ile CCM safi ulizikwa nayo pale Mwintongo na CCM chafu ndiyo imebaki na inendelea kututawala.

Hata hivyo baba kampeni za uchaguzi mdogo wa Tarime kutokana na kampeni zake zilitawaliwa na uwamgaji damu wa hapa na pale ikiwemo kukatana mapanga hali iliyosababisha masikio na macho ya watanzania wote kuelekeza kwenye uchaguzi huo;kumewafundisha Watanzania kitu kimoja kwamba siku zote vyama vya upinzani vikitaka kuishinda CCM, lazima vipambane kufa na kupona.

Tunakuenzi baba kwa kuliingiza taifa kwenye aibu iliyopitiliza kule bungeni Dodoma katika bunge la bajeti mwaka huu, tumeamua kukuenzi kwa stahili ya aina yake ya kukumbatia ushirikina.

Mara hii kwa kufanya vitendo vinavyoashiria ushirikina mchana kweupe.Tumekuenzi baba kwa kutuhumiana kwamba tunalogana kwa kunyunyiza unga mweupe ili tusisemane na kukosoana pale kunapokosea.

Baba ushirikina wetu auishii hapo tumeamua kukuenzi kwa kuwachinja Malbino na kunyofoa baadhi ya viuongo vyao0, kwa kuwafanya kafara za kutafutia mali,utajiri na vyeo.Samahani baba kwakukuenzi kwa stahili hii ya kutenda maovu, tunaomba utuombee msamaha kwa mungu kama ulivyoaidi ukisema unajua tutalia lakini utatuombea kwa mungu.

Baba Mungu alikuumba na ukaisha kuifanya kazi yake hapa kwetu duniani,akakutwaa.Jina la Bwana lihimidiwe na aipumzishe roho yako mahali pema peponi.Amina.

0755 312859
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano ,Oktoba 15 mwaka 2008

UMUHIMU WA ELIMU KWA MTANZANIA



George Kahangwa(39) ni miongoni mwa wahadhiri vijana toka Kitivo cha Elimu ,Idara ya Mipango na Utawala wa Elimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anaeleza kwa mapana ni jinsi gani elimu inaweza kulisaidia taifa letu kiuchumi na kijamii katika ulimwengu wa sasa.Kwa simulizi zaidi ungana na Mwandishi Wetu Happiness Katabazi ambaye mapema wiki alifanya mahojiano na mhadhiri huyo ofisini kwake.

Swali:Ni jinsi gani elimu inaweza kulisaidia taifa letu kiuchumi na kijamii katika ulimwengu wa sasa?

Jibu:Takribani nyakati zote katika historia ya mwanadamu, elimu imekuwa ya manufaa sana kwa mtu mmoja mmoja anayeipata na kwa jamii ambayo mpata elimu anaishi. Leo hii zinapoendelea jitihada za kihumizana katika ngazi ya familia na taifa kwamba hapana budi kuwekeza sana katika suala la elimu bila suluhu, kimsingi sababu kuu ni hiyo kwamba elimu ina manufaa kwa mtu binafsi (private returns) na kwa jamii (social returns). Ni dhahiri basi kwamba anapoelimika mtanzania mmoja ananufaika yeye na linanufaika taifa zima la Tanzania.

Katika ulimwengu wa sasa unaouzungumzia, manufaa hayo ya elimu yanazidi kutambulika na kuongezeka kiasi kwamba kiasi kwamba katika mataifa mbali mbali hususan ya ulimwengu wa kwanza elimu inatazamwa kuwa ndilo tumaini la kipekee kiuchumi na kimaendeleo kwa sasa na kwa siku nyingi za usoni.
Utakumbuka kwamba uchumi wa nchi moja moja una msingi wake, matharani hapa Tanzania kwa miongo kadhaa tunazungumza kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa taifa,kwa maneno mengine msingi mkuu wa uchumi wetu ni kilimo. Utakuwa unafahamu pia kwamba mataifa kadhaaa yaliyoendelea kiviwanda yanazungumzia zalishaji wa viwandani kuwa ndio msingi mkuu wao kiuchumi (industrial economy).
Mtazamo wa kidunia sasa hivi ni kwamba uchumi wa ulimwengu hususan wa mataifa yanayoitwa yaliyoendelea unahama katika kutegemea zaidi viwanda na sekta nyinginezo za uzalishaji, tegemeo kubwa sasa ni maarifa ambayo chimbuko lake ni elimu. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa dunia ya leo na kesho inaelekea zaidi katika uchumi wa maarifa (knowledge economy)

Nchi za ulimwengu wa tatu, ikiwemo Tanzania yetu zimedumu katika kutegemea kilimo, zikashindwa kuingia katika uchumi wa viwanda. Kwa sasa nchi hizi zinayo fursa ya kujikwamua na kutoka katika maendeleo duni endapo zitajielekeza katika kuutafuta uchumi wa maarifa. Kwa mantiki hiyo nchi yetu inayo fursa ya kuingia katika ulimwengu wa kwanza, bila kulazimika kutafuta ufalme wa viwanda mama, yatosha tukiuendea sasa kwa udi na uvumba uchumi wa maarifa. Elimu ndio chombo pekee cha kutupeleka huko.

Swali:Ni nini hasa unachokimaanisha kwa kusema uchumi wa maarifa na una uhakika gani kwamba kwa kuutafuta uchumi huo taifa letu litaondoka katika ulimwengu wa tatu?

Jibu:Ndugu mwandishi, upo ushahidi usiotiliwa shaka kutoka katika mataifa mbali mbali ambayo awali hayakufanikiwa sana katika uchumi wa viwanda yakaja kupata maendeleo makubwa sana kutokana na maarifa. Tuchukulie kwa mfano nchi ya Finland, kwa miongo kadhaa taifa hilo lilikuwa halina mafanikio makubwa kiuchumi, wafinland walitegemea sana zao la mbao na mara kwa mara uchumi wao uliyumba. Lakini tokea serikali ya nchi hiyo ilipofunguka macho ikawekeza kwa nguvu katika maarifa, Finland kwa sasa limekuwa taifa lenye mafanikio makubwa sana kiuchumi kwa kiasi kilichoushangaza ulimwengu. Kwa sasa Finland ni moja ya nchi chache sana duniani zinazoweza kutoa kwa raia wake elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vikuu. Mataifa yaliyoko katika umoja wa nchi za Ulaya yanaendelea kujifunza kwa bidii kile ambacho Finland imekifanya, wakijua fika kuwa katika ulimwengu wa utandawazi ni maarifa pekee yatakaloliwezesha taifa kuwa na nguvu kubwa kiuchumi.

Kwa ufupi uchumi wa maarifa ni uchumi unaotegemea maarifa kama raslimali kuu. Unajua maliasili kama madini na ardhi ni rasilimali, fedha ni rasilimali hali kadhalika watu ni raslimali. Hizo ni raslimali zinazoshikika na kuonekana wazi (tangible resources) lakini maarifa ni tofauti kidogo maana ni intangible. Vile vile wakati rasilimali ‘tangible’ hutumika na kuisha, rasilimali ya maarifa haiwezi kuisha bali huwa bora zaidi na kuongezeka kadiri inavyotumika.
Uchumi huu wa maarifa unaeleweka zaidi unapochanganuliwa katika zile zinazoitwa nguzo zake kuu nne. Hizo nguzo ni Elimu na uendelezi wa rasilimali watu; pili, Utafiti, uvumbuzi na ubunifu; tatu, Tekinolojia na mawasiliano; na nne ,ni Mfumo wa utawala na nyenzo sahihi.
Katika nguzo ya elimu na uendelezi wa rasilimali watu, ili taifa liufikie uchumi wa maarifa linatakiwa kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa ina ubora wa hali ya juu na watu wa nchi husika wanaendelezwa kwa wingi, kama sio wote ili wafikie viwango vikubwa vya elimu na kuyapata maarifa watakayoyatumia kuujenga uchumi wao. Taifa halina budi kuhakikisha si tu kwamba halina raia yoyote mjinga bali pia asilimia kubwa ya raia ni wahitimu wa vyuo vikuu katika fani mbali mbali na ni wasiokoma kutafuta maarifa hata wawapo kazini na katika maisha yao yote ili wazidi kupata ujuzi wa kazi, wawe wazalishaji zaidi na washindani.

Katika nguzo ya utafiti, uvumbuzi na ubunifu taifa linatakiwa kuwa na mchakato endelevu wa kufanya tafiti zinazolenga kugundua maarifa mapya, suluhu za matatizo mbalimbali, ugunduzi wa nyenzo na uboreshaji wa zana za kazi. Tafiti za namna hiyo zitalifanya taifa kuboresha kila sekta ya uzalishaji na zaidi sana zitalinufaisha taifa kwa njia ya kuuza maarifa yaliyogunduliwa kwa mataifa mengine. Nadhani unafahamu ni kiasi gani wagunduzi wa vitu mbali mbali wanazinufaisha nchi zao kwa kile wanachokigundua. Chukulia mfano wa ugunduzi wa simu za mkononi unavyozinufaisha nchi zinazozalisha simu hizo. Ni wazi kuwa elimu yetu inapaswa kuwa na mkono katika hili, tunatakiwa kuwa na elimu inayomfanya mwanafunzi awe na uwezo wa kutafiti na kugundua maarifa mapya au kuwa mbunifu hata akaboresha yale yaliyopo.

Kuhusu nguzo ya teknolojia na mawasiliano, taifa linapasa kuwa la watu wenye kupata kwa wingi habari sahihi na zenye manufaa, wawe na mawasiliano ya kutosha tena ya haraka na wawe watumiaji wazuri wa teknolojia ya habari na mawasiliano kiasi kwamba njia hizo zinawasaidia kuzalisha mali zaidi, na kwa wakati muafaka. Fikiria kwa mfano, unapokuwa na mkulima au mfanya biashara anayeweza kupata mtandao unaomwezesha kupata habari za soko la mazao yake au bidhaa zake kutoka ulimwengu mzima, ni dhahiri mtu huyu akitumia habari hizo vizuri kamwe hatakuwa sawa na yule anayejua tu habari za soko la kijijini kwake. Hata katika hili elimu ina jukumu muhimu kwani ni kupitia katika elimu watu hujifunza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Nguzo ya nne ya mfumo wa utawala na nyenzo sahihi. Katika hili taifa linahitaji kuwa na mfumo unaowezesha maarifa yanayopatikana yanatumika vilivyo katika sekta za uzalishaji. Ili kufanikisha hilo hapana budi kuwe na uhusiano wa maana kati ya taasisi za elimu na sekta mbali mbali za uzalishaji. Matharani, kuwepo kwa uhusiano wa vyuo vikuu na sehemu za ajira ili kinachofunzwa vyuoni kiwe ni chenye manufaa mahali pa uzalishaji. Vile vile kuwe na mfumo unaowezesha maarifa kuzalishwa na kutumika katika nchi. Mfumo huo uwezeshe mambo kadhaa kama vile upatikanaji wa nyenzo za kufanyia tafiti, uhuru wa kujiendeleza kimaarifa mahali pa kazi na uhuru wa watu kufanya ugunduzi majaribio na ubunifu.

Swali:Unafikiri nguzo hizo za uchumi wa maarifa ziko katika hali gani hapa nchini, taifa letu linawezesha hayo unayoyasema?

Jibu:Nchi yetu Tanzania, kwa kweli ina hali mbaya sana katika nguzo zote nne. Laiti kama tungekuwa vizuri katika japo nguzo mbili, uchumi wetu ungekuwa na hali nzuri kiasi chake. Elimu yetu imeendelea kuyumbisha na kuwa na hali duni kuanzia kile tunachokiamini na kukitekeleza kama falsafa ya elimu nchini, sera za elimu, mitaala, mchakato wa kufundisha na kujifunza, uwezeshaji wa watendaji katika elimu na suala zima la utadhimini wa elimu.

Ukiangalia katika takwimu zilizotolewa hivi karibuni na benki ya dunia, Tanzania ina alama 7 kwa mia katika elimu na uendelezaji wa rasilimali watu, asilimia 17 katika utafiti na ugunduzi, asilimia 8 katika teknolojia ya habari na mawasiliano, na asilimia 34 katika mfumo na nyenzo. Kwa hiyo uchumi wetu unaitegemea rasilimali ya maarifa kwa asilimia takribani 17 tu, wakati yapo mataifa yamekwisha kufikia asilimia 90 na zaidi.

Swali:Ni jinsi gani elimu inaweza kulisaidia taifa letu kiuchumi na kijamii katika ulimwengu wa sasa?

Jibu:Takribani nyakati zote katika historia ya mwanadamu, elimu imekuwa ya manufaa sana kwa mtu mmoja mmoja anayeipata na kwa jamii ambayo mpata elimu anaishi. Leo hii zinapoendelea jitihada za kihumizana katika ngazi ya familia na taifa kwamba hapana budi kuwekeza sana katika suala la elimu bila suluhu, kimsingi sababu kuu ni hiyo kwamba elimu ina manufaa kwa mtu binafsi (private returns) na kwa jamii (social returns). Ni dhahiri basi kwamba anapoelimika mtanzania mmoja ananufaika yeye na linanufaika taifa zima la Tanzania.

Katika ulimwengu wa sasa unaouzungumzia, manufaa hayo ya elimu yanazidi kutambulika na kuongezeka kiasi kwamba kiasi kwamba katika mataifa mbali mbali hususan ya ulimwengu wa kwanza elimu inatazamwa kuwa ndilo tumaini la kipekee kiuchumi na kimaendeleo kwa sasa na kwa siku nyingi za usoni.
Utakumbuka kwamba uchumi wa nchi moja moja una msingi wake, matharani hapa Tanzania kwa miongo kadhaa tunazungumza kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa taifa,kwa maneno mengine msingi mkuu wa uchumi wetu ni kilimo. Utakuwa unafahamu pia kwamba mataifa kadhaaa yalitoendelea kiviwanda yanazungumzia uzalishaji wa viwandani kuwa ndio msingi mkuu wao kiuchumi (industrial economy).

Mtazamo wa kidunia sasa hivi ni kwamba uchumi wa ulimwengu hususan wa mataifa yanayoitwa yaliyoendelea unahama katika kutegemea zaidi viwanda na sekta nyinginezo za uzalishaji, tegemeo kubwa sasa ni maarifa ambayo chimbuko lake ni elimu. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa dunia ya leo na kesho inaelekea zaidi katika uchumi wa maarifa (knowledge economy)

Nchi za ulimwengu wa tatu, ikiwemo Tanzania yetu zimedumu katika kutegemea kilimo, zikashindwa kuingia katika uchumi wa viwanda. Kwa sasa nchi hizi zinayo fursa ya kujikwamua na kutoka katika maendeleo duni endapo zitajielekeza katika kuutafuta uchumi wa maarifa. Kwa mantiki hiyo nchi yetu inayo fura ya kuingia katika ulimwengu wa kwanza, bila kulazimika kutafuta ufalme wa viwanda mama, yatosha tukiuendea sasa kwa udi na uvumba uchumi wa maarifa. Elimu ndio chombo pekee cha kutupeleka huko.

Swali:Ni nini hasa unachokimaanisha kwa kusema uchumi wa maarifa na una uhakika gani kwamba kwa kuutafuta uchumi huo taifa letu litaondoka katika ulimwengu wa tatu?

Jibu:Ndugu mwandishi, upo ushahidi usiotiliwa shaka kutoka katika mataifa mbali mbali ambayo awali hayakufanikiwa sana katika uchumi wa viwanda yakaja kupata maendeleo makubwa sana kutokana na maarifa. Tuchukulie kwa mfano nchi ya Finland, kwa miongo kadhaa taifa hilo lilikuwa halina mafanikio makubwa kiuchumi, wafinn walitegemea sana zao la mbao na mara kwa mara uchumi wao uliyumba. Lakini tokea serikali ya nchi hiyo ilipofunguka macho ikawekeza kwa nguvu katika maarifa, filand kwa sasa limekuwa taifa lenye mafanikio makubwa sana kiuchumi kwa kiasi kilichoushangaza ulimwengu. Kwa sasa finland ni moja ya nchi chache sana duniani zinzoweza kutoa kwa raia wake elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vikuu. Mataifa yaliyoko katika umoja wa nchi za ulaya yanaendelea kujifunza kwa bidii kile ambacho finland imekifanya, wakijua fika kuwa katika ulimwengu wa utandawazi ni maarifa pekee yatakaloliwezesha taifa kuwa na nguvu kubwa kiuchumi.

Kwa ufupi uchumi wa maarifa ni uchumi unaotegemea maarifa kama raslimali kuu. Unajua maliasili kama madini na ardhi ni rasilimali, fedha ni rasilimali hali kadhalika watu ni raslimali. Hizo ni raslimali zinazoshikika na kuonekana wazi (tangible resources) lakini maarifa ni tofauti kidogo maana ni intangible. Viel vile wakati rasilimali tangible hutumika na kuisha, rasilimali ya maarifa haiwezi kuisha bali huwa bora zaidi na kuongezeka kadiri inavyotumika.
Uchumi huu wa maarifa unaeleweka zaidi unapochanganuliwa katika zile zinazoitwa nguzo zake kuu nne. Hizo nguzo ni Elimu na uendelezi wa rasilimali watu; pili, Utafiti, uvumbuzi na ubunifu; tatu, Tekinolojia na mawasiliano; na nne ,ni Mfumo wa utawala na nyenzo sahihi.
Katika nguzo ya elimu na uendelezi wa rasilimali watu, ili taifa liufikie uchumi wa maarifa linatakiwa kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa ina ubora wa hali ya juu na watu wa nchi husika wanaendelezwa kwa wingi, kama sio wote ili wafikie viwango vikubwa vya elimu na kuyapata maarifa watakayoyatumia kuujenga uchumi wao. Taifa halina budi kuhakikisha si tu kwamba halina raia yoyote mjinga bali pia asilimia kubwa ya raia ni wahitimu wa vyuo vikuu katika fani mbali mbali na ni wasiokoma kutafuta maarifa hata wawapo kazini na katika maisha yao yote ili wazidi kupata ujuzi wa kazi, wawe wazalishaji zaidi na washindani.

Katika nguzo ya utafiti, uvumbuzi na ubunifu taifa linatakiwa kuwa na mchakato endelevu wa kufanya tafiti zinazolenga kugundua maarifa mapya, suluhu za matatizo mbalimbali, ugunduzi wa nyenzo na uboreshaji wa zana za kazi. Tafiti za namna hiyo zitalifanya taifa kuboresha kila sekta ya uzalishaji na zaidi sana zitalinufaisha taifa kwa njia ya kuuza maarifa yaliyogunduliwa kwa mataifa mengine. Nadhani unafahamu ni kiasi gani wagunduzi wa vitu mbali mbali wanazinufaisha nchi zao kwa kile wanachokigundua. Chukulia mfano wa ugunduzi wa simu za mkononi unavyozinufaisha nchi zinazozalisha simu hizo. Ni wazi kuwa elimu yetu inapaswa kuwa na mkono katika hili, tunatakiwa kuwa na elimu inayomfanya mwanafunzi awe na uwezo wa kutafiti na kugundua maarifa mapya au kuwa mbunifu hata akaboresha yale yaliyopo.

Kuhusu nguzo yya teknolojia na mawasiliano, taifa linapaswa kuwa la watu wenye kupata kwa wingi habari sahihi na zenye manufaa, wawe na mawasiliano ya kutosha tena ya haraka na wawe watumiaji wazuri wa teknolojia ya habari na mawasiliano kiasi kwamba njia hizo zinawasaidia kuzalisha mali zaidi, na kwa wakati muafaka. Fikiria kwa mfano, unapokuwa na mkulima au mfanya biashara anayeweza kupata mtandao unaomwezesha kupata habari za soko la mazao yake au bidhaa zake kutoka ulimwengu mzima, ni dhahiri mtu huyu akitumia habari hizo vizuri kamwe hatakuwa sawa na yule anayejua tu habari za soko la kijijini kwake. Hata katika hili elimu ina jukumu muhimu kwani ni kupitia katika elimu watu hujifunza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Nguzo ya nne ya mfumo wa utawala na nyenzo sahihi. Katika hili taifa linahitaji kuwa na mfumo unaowezesha maarifa yanayopatikana yanatumika vilivyo katika sekta za uzalishaji. Ili kufanikisha hilo hapana budi kuwe na uhusiano wa maana kati ya taasisi za elimu na sekta mbali mbali za uzalishaji. Matharani, kuwepo kwa uhusiano wa vyuo vikuu na sehemu za ajira ili kinachofunzwa vyuoni kiwe ni chenye manufaa mahali pa uzalishaji. Vile vile kuwe na mfumo unaowezesha maarifa kuzalishwa na kutumika katika nchi. Mfumo huo uwezeshe mambo kadhaa kama vile upatikanaji wa nyenzo za kufanyia tafiti, uhuru wa kujiendeleza kimaarifa mahali pa kazi na uhuru wa watu kufanya ugunduzi majaribio na ubunifu.

Swali:Unafikiri nguzo hizo za uchumi wa maarifa ziko katika hali gani hapa nchini, taifa letu linawezesha hayo unayoyasema?

Jibu:Nchi yetu Tanzania, kwa kweli ina hali mbaya sana katika nguzo zote nne. Laiti kama tungekuwa vizuri katika japo nguzo mbili, uchumi wetu ungekuwa na hali nzuri kiasi chake. Elimu yetu imeendelea kuyumbisha na kuwa na hali duni kuanzia kile tunachokiamini na kukitekeleza kama falsafa ya elimu nchini, sera za elimu, mitaala, mchakato wa kufundisha na kujifunza, uwezeshaji wa watendaji katika elimu na suala zima la utadhimini wa elimu.

Ukiangalia katika takwimu zilizotolewa hivi karibuni na benki ya dunia, Tanzania ina alama 7 kwa mia katika elimu na uendelezaji wa rasilimali watu, asilimia 17 katika utafiti na ugunduzi, asilimia 8 katika teknolojia ya habari na mawasiliano, na asilimia 34 katika mfumo na nyenzo. Kwa hiyo uchumi wetu unaitegemea rasilimali ya maarifa kwa asilimia takribani 17 tu, wakati yapo mataifa yamekwisha kufikia asilimia 90 na zaidi.

Unaweza kung’amua kwa takwimu hizo jinsi taifa letu lilivyo na elimu isiyokidhi. Vile vile licha ya kwamba watanzania sasa tunakadiriwa kuwa milioni 39 watu wetu wengi hawajaendelezwa kiasi cha kulinufaisha taifa kiuchumi, tunayo rasilimali watu ya kutosha lakina bahati mbaya iliyokosa maarifa. Mwalimu Nyerere aliwahi kutuambia kwamba, ili nchi iendelee inahitaji pamoja na vitu vingine, watu wake. Lakini watu bila maarifa ni hasara tupu.
Kwa upande wa tafiti nako hatuko vizuri kwa sababu nyingi, kwanza matharani katika vyuo vikuu, utakuta tafiti zinafanyika ndio, lakini si kwa maslahi ya taifa bali kwa wafadhili wan je wanaotoa fedha kwa ajili ya tafiti hizo. Ninachosema hapa ni kwamba watafiti wachache tulionao badala ya kutumiwa na taifa wanatumiwa na mashirika ya nje kufanya tafiti ambazo hao wageni wana maslahi nazo, na watafiti wetu wanakubali maana wanataka pesa. Laiti kama Taifa letu, hususan serikali kuu, ingeona haja ya kuwekeza katika utafiti na kuwawezesha watafiti wetu kutumia umahili wao katika kutafuta maarifa mapya, na kutafiti suluhu za matatizo yetu yote sisi wenyewe.
Kibaya zaidi hata tafiti chache zilizokwisha fanyika nchini, matokeo ya tafiti hizo ni nadra kusikia yakitumiwa vilivyo katika sekta za uzalishaji. Ripoti nyingi za tafiti zimeishia kujaa vumbi katika shelf za maktaba za vyuo vikuu bila kutumiwa.
Ama kwa suala la teknolojia ya habari na mawasiliano, licha ya kwamba hatujamudu kuingiza jambo hili katika shule zetu za sekondari, wengi miongoni mwa vijana wanaojua kutumia intertnet na vitu kama simu za mkononi bahati mbaya hawazitumii katika kiwango kizuri cha kuwanufaisha. Kwa walio wengi internet ni kwa ajili ya kutumiana ujumbe wa kirafiki, kuangalia picha za pono, hali kadhalika simu ni kusalimiana tu. Wachache sana wanaotumia mawasiliano kujiendeleza kielimu, kutafuta maarifa na au kupata habari za masoko na biashara.

Swali:Unafikiri ni nini kifanyike?
Jibu:Yapo mengi ya kufanya, labda mimi nizungumze kupitia jicho la taaluma yangu. Hatuna budi kuwa na sera za elimu zitakazotuhakikishia kwamba kila mwenye uwezo wa kupata elimu ya juu anaipata bila vikwazo vya karo, nafasi kidogo na kadhalika. Tunatakiwa kuongeza fursa kwa gharama yoyote ile, huo ni uwekezaji utakaotuletea manufaa makubwa sana kiuchumi kama nilivyoeleza.
Hatuna budi pia kuwa na mitaala inayomwezesha mwanafunzi kuwa wa manufaa kabisa katika ulimwengu wa kisasa. Tunahitaji wahitimu wanaoajirika, tuahitaji elimu ituzalishie wagunduzi na wabunifu mahiri, watafiti wachapa kazi na watu wanaodumu katika kuyatafuta maarifa kwa bidii katika maisha yao yote.
Kadri tutakavyoendelea na sera za kukopesha watu wachache waingie vyuo vikuu ndivyo tutakavyolididmiza taifa. Kadri tutakavyoipuuza taaluma ya ualimu ndivyo tutakavyo dunisha elimu yenyewe na kubaki kuwa wasindikizaji katika ulimwengu wa utandawazi.

Swali:Hujazungumzia manufaa ya elimu kijamii, unasemaje hapo?

Jibu:Nimetaja jambo la social returns, lakini kwa upande mwingine elimu inapaswa kuinufaisha jamii kwa kuzalisha wahitimu waadilifu.kwa sasa mitaala yetu haijakaza sana suala la maadili na shule nyingi hazionekani zikiwaadilidha watanzania. Yamkini ndio sababu tuanpata wingi wa watumishi na viongozi wala rushwa, wabadhilifu na mafidsadi.
Laiti kama mitaala yetu yote kuanzia elimu ya awali hadi vyuo ingesisitiza vya kutosha elimu ya maadili. Tunatakiwa kuwa waadilifu katika mahusiano, katika kazi, katika utunzaji wa mazingira, katika utumiaji wa rasilimali na katika mwenendo kwa ujumla. Elimu inalojukumu la kutuhakikishia hilo.

Swali:Tueleze historia ya maisha yako.
Jibu:Mimi ni mzaliwa wa mkoa wa Kagera. Umri wangu ni miaka 39 sasa. Nimesoma elimu ya msingi katika shule ya Omurushenye na baadaye Bilele ya mjini Bukoba. Nilipata elimu ya sekondari katika shule ya Sekondari Bukoba. Nilisomea ualimu katika chuo cha ualimu Korogwe. Kwa miaka kadhaa nilikuwa mwalimu wa elimu ya Msingi. Baada ya kujiendeleza na kupata shahada ya kwanza ya ualimu katika chuo kikuu cha Dar es salaam, nilifundisha kwa miaka miwili mara hii elimu ya sekondari. Nilifanikiwa pia kusoma shahada ya uzamili katika elimu, hapa hapa chuo kikuu cha Dar es salaam, na hatimaye kuajiriwa na chuo hiki katika kitivo cha elimu, ambapo kazi yangu ni uadhiri katika masuala ya Utawala wa Elimu, Mipango na Sera. Nimepata pia mafunzo ya elimu na Utandawazi katika Chuo Kikuu cha Oulu nchini Finland. Nimeoa na tuna mtoto mmoja.

Swali:Ni nini matarajio yako ya baadaye?
Jibu:Kwa taaluma yangu, inanipasa kujiendeleza zaidi na zaidi katika kuyatafuta maarifa. Natarajia kuanza masomo ya shahada ya juu ya falsafa huko ughaibuni mwishoni mwa mwezi huu. Bila shaka ninalo jukumu la kuitumia elimu yangu katika utumishi kwa taifa langu. Ndoto yangu ni kupata fursa pana za kuwahudumia na kuwatumikia watanzania wengi zaidi kama sio wote kwa kadri Mungu atakavyonipa kibali.

0755312859
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima Jumamosi Septemba 27 mwaka 2008

TUHUMA ZA KOMBA NZITO,ASHITAKIWE

Na Happiness Katabazi
“KAPTENI John Komba akipita njiani watu wote wanalia yooo,tupatie pesa….”hiki kibwagizo kinapatikana kwenye wimbo wa Dakika tisa uliopigwa na Bendi ya TOT Respect, ambao hivi sasa wimbo huo unatamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na Televisheni.

Kwa tafsiri nyepesi kigwazo hicho kinadhiirisha Komba ni Mtanzania mwenye fedha nyingi.Lakini kwa upande mwingine kibwagizo hicho kinachosema ‘Kapten Komba akipita njiani watu wote wanalia yoooo’ kinadhiirisha wanamuziki wa kundi hilo ndiyo haswa wanalia baada ya kulizwa mishahara yao ya miezi 14 na nguli huyo wa sanaa ya muziku nchini .

Nasema wanalia kwasababu wanamuzi wa kundi hilo wamekuwa wakitumia taaluma yao ya sanaa kwa kuimba, kunengua katika bendi hiyo .Na wengine wanaolia ni washabiki,wanachama,wakereketwa wa CCM na wananchi ambao wanachangia fedha chama hicho na wanachi kukatwa kodi na serikali ambazo ugawanya na CCM kupewa ruzuku kutoka na idadi kubwa ya wabunge waliyokuwa nao.

Jumatatu ya wiki iliyopita Tanzania Daima ndilo lilikuwa gazeti pekee liloandika habari kwamba Mkurugenzi wa Kikundi cha Sanaa cha Tanzania One Theatre(TOT), Kapteni John Komba , anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa mamilioni ya fedha katika kikundi hicho kinachomilikiwa na chama tawala CCM.

Tuhuma hizo zimeibuliwa katika taarifa ya ukaguzi maalum, uliofanywa na kitengo cha ukaguzi cha CCM, kwa maagizo ya Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, kutokana na tuhuma zilizowasilishwa kwake dhidi ya Kapteni Komba.

Ukaguzi huo, ulifanyika kuanzia Machi 3 hadi 16, mwaka huu na baadaye April mosi hadi 6, na taarifa yake kuwasilishwa rasmi kwa Makamba April 22. Taarifa hiyo ya Uchunguzi ambayo hadi leo Tanzania Daima ina nakala yake Komba anadaiwa kutafuna sh milioni 30 za mishahara ya wafanyakazi miezi 14.

Uchunguzi huo ambao umepata baraka za chama, unadai kuwa CCM ilitoa sh 37,442,923 kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya mishahara ya miezi 14 kuanzia Juai 2006 hadi Agosti 2007 kwa awamu, lakini ni sh milioni sita tu, ndizo zilizolipwa kwa wafanyakazi kwa mishahara ya miezi miwili.Pia anatuhumiwa kuwapunja wafanyakazi wa TOT kwa kuwalipa posho ya sh 20,000 kwa siku wanapokuwa nje ya Dar es Salaam badala y ash 40,000 zinazotolewa na chama.

Pia Komba na kiongozi mwenzake ndani ya kundi hilo, wanahusishwa na udanganyifu wa kulipa warithi wa marehemu wasio waasisi wa chama jumla y ash 27.3 milioni, lakini baadhi ya waliotajwa kwenye orodha ya malipo, wamekana kupewa fedha zozote.Mbali na tuhuma hizo hizo pia anatuhumiwa kusajili gari la CCM kwa jina la asasi yake isiyo ya kiserikali inayojulikana kwa jina la Educare Girls.

Kwanza kabisa nitoe shukrani zangu za dhati kwa vyanzo vya habari viadilifu toka ndani ya CCM ambavyo kwa siri kubwa walifanikiwa kulipatia gazeti hili nakala hiyo ya ukaguzi ambayo imebaini ufisadi unaodaiwa kufanywa na Komba ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi.

Ni ukweli ulio wazi kwamba vyanzo hivyo visingejitoa muhanga na kulipatia gazeti hili na magazeti mengine nakala hiyo, jamii yote isingejua kwamba Komba ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho kuwa anakabiliwa na tuhuma za ufisadi.

Tungeendelea kumuona Komba ni mwema, Kada mwaminifu wa CCM asiye na mawaa.Lakini kwa kupitia nakala hiyo ya ukaguzi sasa tumeanza kukubaliana na minong’ong’ono iliyokuwa ikilindima chini kwa chini kuwa kiongozi huyo alikuwa akitafuna fedha la kundi hilo, licha ushaidi wa hayo ulikuwa ni mgumu kupatikana.

Sishangai Komba kutuhumiwa na ufisadi kwani kuna viongozi wakubwa wa chama hicho wanaandamwa na tuhuma za ufisadi.Ila kwa wenye tuhuma za ufisadi wa wazi ambao pia wananguvu na uswahiba na kundi la wanamtandao wamekuwa wakilindwa ila wale wanachama ambao wanatuhuma za ufisadi kama aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Abiud Malegesi alishughulikiwa kikamilifu kwasababu hakuwa mwanamtandao.

Hakuna ubishi kwamba CCM safi alizikwa nayo Baba wa Taifa Julias Nyerere na CCM chafu ndiyo imebaki na kwasasa inaongozwa na Mwenyekiti rais Jakaya Kikwete.Kila kukicha makada wake wanakumbwa na tuhuma za nzito za ufisadi unahoujumu uchumi wa taifa hili.

Hii siyo picha nzuri na ishara njema kwa mustakabali wa taifa kwa baadhi ya makada wa chama tawala kuhusishwa na ufisadi.Na kibaya zaidi wanapotuhumiwa na tuhuma hizo wanalindwa bila kufikishwa mahakamani kwa kisingizio kuwa huyu ni ‘mwenzetu’.

Kasumba hiyo ya ‘mwenzetu’ndiyo inayoiangamiza CCM .Komba anajadilika kwani yeye ni mbunge na MNEC ambaye ambako huko jimboni anaongoza Watanzania wenzetu ambao kwakumuamini waliamua kumchagua , sasa anapokumbwa na kashfa kama hii ama kwa hakika hana budi kujiudhuru ili apishe makada wasafi washike nafasi yake.

Kama ameweza kutafuna mishahara ya wafanyakazi wa TOT, hatashindwaje kutotimiza ahadi alizowaaidi wananchi wake wa mchague kwenye uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2005?
Kama ameweza kutapeli magari ya chama kwanini Watanzania tusiamini kwamba nyimbo anazoimba za kuisifu CCM kuwa chama hicho ni kiziru ni kisima cha viongozi, kuwa ni uongo mtupu?

Kwanini Watanzania tusiamini kuwa Komba yupo CCM kwaajili ya kuchumia tumbo?Nasema ni mchumia tumbo kwasababu kama angekuwa ana mapenzi ya dhati ya chama chake asingefanya ubadhilifu huu ambao umeainishwa kwenye ripoti ya wakaguzi wa CCM.

Komba kama kweli anaipenda CCM asingekubali kuvunja maadili ya CCM ambayo yanamtaka mwanachama wake kuwa mwaminifu na asiyesema uongo na asiyebagua.

Sasa ninalazimika kuamini kwamba tuhuma hizi za ubadhirifu wa fedha zinazomkabili, alizitarajia zimkabili tangu miaka ya 1990, nguli huyu alipoamua kuipa kisogo kazi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuingia uraini kuanzisha kundi la TOT kwaajili ya kujiongezea kipato zaidi.

Kitendo kilichofanywa na Komba kinakwenda kinyume na haki za binadamu kwani kila mtu anastahili kulipwa ujira wake kutokana na kazi anayofanya.Na kamwe kitendo hiki hakivumiliki.

Misho nimalizie kwa kumtaka Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) Robert Manumba, aueleze umma kuwa ameishachukua hatua gani dhidi ya Komba kwani kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi imebainisha kwamba komba alitenda jinai kwa kughushi.

Sitaki kumsikia DCI Manumba akijitetea kwamba tuhuma hizo hazijafika mezani kwake, kuna wananchi wanatuhumiwa kufanyamakosa kama hayo na wala yanakuwa hajafikishwa mezani kwake lakini anatuma ‘nusanusa au makachero wake ’wake wanaenda kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani.

Sasa tunataka kuona DCI akionyesha makucha yake kwa kutuma ‘nusanusa’ wake wakamhoji na kumchukulia hatua Komba kwakuwa Komba ni Mtanzania kama walivyo watanzania wengine,
Ambao wanapotuhumiwa kutenda jinai ushitakiwa na Jamhuri ya Muungano na sivinginevyo.

Huu ni mtihani wako wa mwisho DCI, bado tunakumbuka mwaka jana Jeshi la Polisi ambalo hivi sasa limeanza kurejesha imani kwa wananchi, lilisema limebaini Mbunge wa Buchosa(CCM) ,Samwel Chitalilo amegushi cheti cha elimu , lakini katika hali ya kustaajabisha serikali ikashindwa kumshitaki.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima Jumamosi, Septemba 27 mwaka 2008