SHAHIDI KESI YA EPA MATATANI

Na Happiness Katabazi

UPANDE wa mashitaka katika kesi ya wizi wa sh bilioni 1.8 katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inayomkabili Shabani Maranda na mwenzake, umewasilisha ombi la kutaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, itoe amri ya kukamatwa shahidi wa saba kutokana na kushindwa kufika mahakamani hapo kutoa ushahidi.

Ombi hilo liliwasilishwa jana na wakili wa serikali, Timon Vitalis, mbele ya jopo la Mahakimu wa Kazi watatu - Cypriana William, Saul Kinemela na ahidi huyo kuwa ni wakili wa kujitegemea, Abdallah Kihule.

Vitalis alidai wamefikia uamuzi wa kuwasilisha ombi hilo baada ya shahidi huyo jana kushindwa kutokea mahakamani kutoa ushahidi bila kutoa taarifa za udhuru.

Vitalis alidai Februali 23 walimpelekea hati ya kuja kutoa ushahidi jana na shahidi huyo aliipokea hati hiyo na kuisaini, lakini cha kushangaza ameshindwa kutokea mahakamani.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi William alipokea ombi hilo, lakini alisema jopo lake haliwezi kutoa hati ya kukamatwa kwa shahidi huyo kwa sababu hati hiyo ya wito wa kuitwa mahakamani kwa shahidi huyo haikuwa imewasilishwa.

Wakati huo huo, jopo hilo lilitupilia mbali pingamizi la wakili wa utetezi, Majura Magafu, lililokuwa likitaka maelezo ya onyo ya mshitakiwa Rajabu Maranda yasipokelewe na mahakama hiyo kama kielelezo.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu William alisema baada ya kupitia kwa makini hoja za pande mbili, wamebaini hoja za Magafu hazina msingi na badala yake wamekubaliana na hoja za Wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus Boniface, kwamba waliokuwa wajumbe wa timu ya Rais ya kuchunguza wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), kwamba nyadhifa zao hazikuwa zimekoma wakati walipokuwa wajumbe wa timu hiyo.

“Magafu ameshindwa kuonesha ni kifungu gani cha sheria kinatamka kuwa kazi za wajumbe wale zilikoma wakati walivyokuwa wajumbe wa timu ile…hivyo mahakama imeona shahidi wa sita, Mrakibu wa Polisi (SSP) Salum Kisai, alikuwa na uhalali wa kuchukua maelezo ya Maranda kwa sababu ni ofisa wa polisi,” alisema William.

Alisema kuhusu hoja maelezo ya onyo ya Maranda na Farijala kufanana, anatupilia mbali hoja hiyo ya Magafu na kukubaliana na wakili Boniface kwamba kuna maelezo yanafanana, kama miaka ya washitakiwa, kiwango cha elimu na makazi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Februari 28 mwaka 2009

LIYUMBA APONZA WADHAMINI WAKE

*Hati zao zenye utata zapelekwa kwa DCI Kuchunguzwa

Na Happiness Katabazi

HATI za watu 10 waliojitokeza awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, kutaka kumdhamini aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, anayekabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221, zimeanza kuchunguzwa na Jeshi la Polisi, imefahamika.

Hati za wadhamini hao kumi, zenye thamani ya sh bilioni 55, ndizo zilizotumika kujaribu kumdhamini Liyumba, mara ya kwanza, lakini zilikataliwa baada ya kubainika kuwa zilikuwa na kasoro kubwa za kisheria, huku nyingine zikidaiwa kuwa ni za kughushi.

Miongoni mwa watu wanaomiliki hati hizo zilizobainika kuwa na upungufu kisheria ni pamoja na aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Jamila Nzota, ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya rushwa katika Mahakama hiyo ya Kisutu.

Hati nyingine ni ya Cecil Chiwango, Abubakar Ogunda, Avogiti Chiwando, Mikidadi Mtumbati, Selemani Kaboke, Justas Samson, Gideon Chipange, Hashimu Mwinyimvua na John Ngutilo, ambaye amewasilisha hati mbili na kufanya thamani ya hati hizo 10, kufikia sh bilioni 55 ambazo zingetosha kumtoa Liyumba katika mahabusu ya Keko, alikorejeshwa wiki iliyopita baada ya kufutiwa dhamana iliyozua utata ya hati ya sh milioni 882.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, vinaeleza kuwa hati hizo zilitoka mahakamani hapo juzi na kupelekwa siku hiyo hiyo katika ofisi ya Makao Makuu ya Upelelezi ambapo zilipokewa na kuanza kufanyiwa kazi.

Kwa mujibu wa habari hizo, tayari uchunguzi wa kujua uhalali wa hati hizo unaofanywa na Idara ya Utambuzi wa Maandishi kwa umakini mkubwa, umeanza mara moja na utakapokamilika, utarejeshwa katika Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kutolewa taarifa.

“Hati hizo ziliondoka Kisutu juzi, na ofisa mmoja kutoka mahakamani hapo ndiye alizipeleka ofisini kwa DCI, ili zifanyiwe uchunguzi kama zimeghushiwa au la, na ninakuhakikishia DCI ameishawaagiza vijana wake waanze kuzifanyia kazi mara moja na pindi watakapokamilisha uchunguzi huo utakabidhiwa katika Mahakama ya Kisutu,” kilidai chanzo chetu.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, alikiri kupokea hati hizo na kwamba ameishaagiza Idara ya Utambuzi wa Maandishi izifanyie uchunguzi wa kitaalamu.

“Ni kweli hati hizo tumezipokea jana (juzi) na tayari nimeishaagiza idara husika zianze kuzifanyia uchunguzi kama ilivyoamriwa na mahakama na kwamba tayari idara yetu husika imeishaanza kazi mara moja ya kuchunguza hati hizo na uchunguzi ukikamilika, tutaupeleka Mahakama ya Kisutu,” alisema Manumba.

Hata hivyo, Manumba alisema ni mapema kuahidi muda ambao uchunguzi huo utakuwa umekamilika, lakini alisisitiza kuwa utakapokamilika majibu yatapelekwa mahakamani, kwani mahakama ndiyo iliyotoa amri ya hati hizo kupelekwa polisi.

Jumanne wiki hii, Februari 24, wakati akitangaza kufuta dhamana ya Liyumba, Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Hadija Msongo, alizungumzia hati 10 zilizotumika kumdhamini mshitakiwa huyo awali kuwa zina kasoro za kisheria.

Alisema mahakama imegundua hati ya Avogiti Chiwando, ambayo inaonyesha ilitolewa na Ofisa wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wakati hakuna mtu kama huyo wizarani hapo na hati ya Abubakar Ogunda, ilionyesha kuwa ana mali kama kuku na ng’ombe haikubaliki, kwani sharti la dhamana lilitaka kuwasilisha hati ya mali zisizohamishika.

“Kwa ujumla hati zote 10 zinazoonyesha nyumba na viwanja katika maeneo mbalimbali zina kasoro, kwani majengo katika hati hizo yanaonekana kufanana.

“Na hati hizo ambazo zinaonyesha ziligongwa muhuri na Mtathimini wa Gharama za Majengo, Thomas Antabe, hazikubaliwi na mahakama, kwani muhuri wa mtu huyo hauonyeshi mahali ilipo ofisi yake, hivyo mahakama inaona mshitakiwa hajatimiza masharti ya dhamana.

“Kwakuwa masharti ya dhamana hayajatimizwa, mahakama hii inatoa amri ya kumfutia dhamana mshitakiwa na hati hizo kumi zipelekwe Jeshi la Polisi, ili ziweze kufanyiwa uchunguzi wa kimaandishi na kuahirisha kesi hiyo hadi Machi 10, mwaka huu,” alisema Msongo.

Hakimu huyo akisisitiza kuhusu uamuzi wake wa kumfutia dhamana Liyumba, alisema amelazimika kumfutia dhamana baada ya kubaini mshitakiwa huyo aliidanganya mahakama.

Mahakama ya Kisutu ndiyo iliyoanza kusikiliza ombi la dhamana la Liyumba kwa kuweka masharti ya dhamana hiyo Januari 27, mwaka huu.

Masharti hayo yalieleza kuwa watuhumiwa wanapaswa kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali, kusalimisha hati ya kusafiria mahakamani, kila Ijumaa kuripoti ofisi za Takukuru na kutoa fedha taslimu au hati zenye thamani ya sh bilioni 55 kila mmoja.

Lakini Februari 17, mwaka huu, Liyumba aliwasilisha hati yenye thamani ya sh milioni 882, hati ya kusafiria ambayo muda wake wa matumizi umekwisha, huku wadhamini wawili wakiwa hawana barua zilizosainiwa na mwajiri wao kama masharti ya dhamana yalivyotaka, na alifanikiwa kutoka kwa dhamana.

Mbali na Liyumba, mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Meneja Mradi wa BoT, Deogratius Kweka, ambao kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Februari 27 mwaka 2009

USHAHIDI KESI YA MAHALU KUTOLEWA KWA VIDEO

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imekubali ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na mwenzake kwa njia ya video.

Mahakama hiyo imekubali ombi hilo baada ya Wakili wa Serikali, Ponsiani Lukosi, kuwasilisha ombi hilo na kuiomba mahakama iwape muda wa kuwasilianana na shahidi wake aliyepo nchini Italia, ili aweze kutoa ushahidi wake kwa njia hiyo.

Nakubaliana na ombi la upande wa mashtaka la kutaka shahidi wao atoe ushahidi wake kwa njia ya mawasiliano ya video; naahirisha kesi hii hadi Machi 26 mwaka huu na mahakama itahamia Tanzania Global Develepment Learning Center,” alisema Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Sivangilwa Mwangesi, anayesikiliza kesi hiyo.

Katika ombi jingine wakili huyo wa utetezi, aliomba mahakama hiyo ihamie nchini Italia mbayo kosa limetendeka na kuongeza kuwa ombi la kutaka shahidi wao atoe ushahidi kwa njia ya mawasiliano ya video ni muhimu.

Hata hivyo, Wakili Cuthbert Tenga, ambaye anayemtetea mshtakiwa wa pili, Grace Martin, alidai sheria za nchi zinataka shahidi afike mahakamani kutoa ushahidi wake na siyo kutumia njia ya mawasiliano ya video na kuiomba mahakama hiyo iuone upande wa mashtaka umeshindwa kuendelea kuleta mashahidi.

Januari 21 mwaka huu, Mwangesi wakati akiahirisha kesi hiyo ambayo siku hiyo ilishindwa kuendelea kusikilizwa baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuleta mashahidi; alisema anaahirisha kesi hiyo kwa mara ya mwisho.

Januari mwaka 2007 ilidai mahakamani hapo kuwa Mahalu na Grace ambao walikuwa ni maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, waliisababishia serikali hasara ya sh bilioni tatu.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Februali 27 mwaka 2009

MAPYA YAIBUKA KESI YA EPA

Na Happiness Katabazi

WAKILI wa upande wa utetezi katika kesi ya wizi wa sh bilioni 1.8, katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Majura Magafu, amepinga kupokewa kwa maelezo ya onyo ya mteja wake, Rajabu Maranda, kwa madai kuwa yalichukuliwa na wajumbe wa timu ya rais ya kuchunguza wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ambayo kisheria haina mamlaka ya kuendesha kesi mahakamani.

Magafu alitoa pingamizi hilo muda mfupi baada ya shahidi wa sita, Mrakibu wa Polisi (SSP) Salum Kisai (45), kutoa maelezo ya onyo aliyochukua kwa Maranda, Oktoba 3 mwaka jana, kwenye ofisi ya timu hiyo, Mikocheni, Dar es Salaam.

Magafu alidai kuwa kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, inalitaka Jeshi la Polisi kuendesha kesi hiyo badala ya timu ya rais.

Alidai licha ya shahidi huyo kuwa ni ofisa wa polisi, alikuwa mjumbe wa timu hiyo iliyoongozwa na Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika, alikiuka sheria kuchukua maelezo ya mshitakiwa huyo ambayo jana aliyaleta mahakamani hapo na kutaka kuyatoa kama kielelezo.

“Kisheria timu ya rais haina mamlaka ya kuendesha kesi mahakamani, sasa timu ile ya rais ambayo huyu shahidi alikuwa mmoja wa wajumbe wa fani mbalimbali, wakiwemo watu wa Idara ya Usalama wa Taifa, alichukua maelezo ya Maranda wakati kufanya vile ni kinyume cha sheria na kwa sababu hiyo, napinga maelezo ya Maranda ambayo yanataka yatolewe kama kielelezo mahakamani hapa,” alidai Magafu.

Akijibu hoja za wakili huyo, wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus Boniface, aliomba mahakama ipokee maelezo hayo kwa madai kuwa timu ile ilikuwa na polisi na Takukuru, ambao ni wachunguzi na wanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Hata hivyo Naibu Mwenyekiti wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Cypiriana William, ambaye anasaidiana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Phocus Bampikya na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Saul Kinemela, alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili na kuahirisha shauri hilo hadi leo ambapo atatoa uamuzi kuhusu pingamizi hilo.

Awali kabla ya kuwasilisha pingamizi hilo, Bampikya alitupilia mbali pingamizi la wakili Magafu aliloliwasilisha wiki Jumanne iliyopita la kutaka jopo hilo lisipokee maelezo ya onyo la mteja wake, Farijara Hussein, ambaye ni mshitakiwa katika kesi hiyo kwa madai kuwa si la msingi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Februali 27 mwaka 2009

MAPYA YAIBUKA KESI YA EPA

Na Happiness Katabazi

WAKILI wa upande wa utetezi katika kesi ya wizi wa sh bilioni 1.8, katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Majura Magafu, amepinga kupokewa kwa maelezo ya onyo ya mteja wake, Rajabu Maranda, kwa madai kuwa yalichukuliwa na wajumbe wa timu ya rais ya kuchunguza wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ambayo kisheria haina mamlaka ya kuendesha kesi mahakamani.

Magafu alitoa pingamizi hilo muda mfupi baada ya shahidi wa sita, Mrakibu wa Polisi (SSP) Salum Kisai (45), kutoa maelezo ya onyo aliyochukua kwa Maranda, Oktoba 3 mwaka jana, kwenye ofisi ya timu hiyo, Mikocheni, Dar es Salaam.

Magafu alidai kuwa kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, inalitaka Jeshi la Polisi kuendesha kesi hiyo badala ya timu ya rais.

Alidai licha ya shahidi huyo kuwa ni ofisa wa polisi, alikuwa mjumbe wa timu hiyo iliyoongozwa na Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika, alikiuka sheria kuchukua maelezo ya mshitakiwa huyo ambayo jana aliyaleta mahakamani hapo na kutaka kuyatoa kama kielelezo.

“Kisheria timu ya rais haina mamlaka ya kuendesha kesi mahakamani, sasa timu ile ya rais ambayo huyu shahidi alikuwa mmoja wa wajumbe wa fani mbalimbali, wakiwemo watu wa Idara ya Usalama wa Taifa, alichukua maelezo ya Maranda wakati kufanya vile ni kinyume cha sheria na kwa sababu hiyo, napinga maelezo ya Maranda ambayo yanataka yatolewe kama kielelezo mahakamani hapa,” alidai Magafu.

Akijibu hoja za wakili huyo, wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus Boniface, aliomba mahakama ipokee maelezo hayo kwa madai kuwa timu ile ilikuwa na polisi na Takukuru, ambao ni wachunguzi na wanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Hata hivyo Naibu Mwenyekiti wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Cypiriana William, ambaye anasaidiana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Phocus Bampikya na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Saul Kinemela, alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili na kuahirisha shauri hilo hadi leo ambapo atatoa uamuzi kuhusu pingamizi hilo.

Awali kabla ya kuwasilisha pingamizi hilo, Bampikya alitupilia mbali pingamizi la wakili Magafu aliloliwasilisha wiki iliyopita la kutaka jopo hilo lisipokee maelezo ya onyo la mteja wake, Farijara Hussein, ambaye ni mshitakiwa katika kesi hiyo kwa madai kuwa si la msingi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Februali 27 mwaka 2009

MAWAKILI WAHAHA KUMUOKOA LIYUMBA

Na Happiness Katabazi

MAWAKILI wanaomtetea Amatus Liyumba, Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), anayekabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kusababisha hasara ya sh bilioni 221, wamewasilisha ombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wakitaka mteja wao aachiliwe huru.

Mbali na Liyumba, mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ambayo siku za hivi karibuni imevuta hisia za watu wengi, ni Meneja Mradi wa BoT, Deogratius Kweka. Washitakiwa wote wapo rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya sh bilioni 55 kila mmoja au hati za mali zisizohamishika zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Mawakili hao waliwalisha maombi hayo mahakamani hapo juzi chini ya hati ya kiapo iliyosainiwa na wakili Profesa Gamaliel Mgongo Fimbo.

Kwa mujibu wa hati hiyo, mawakili hao wanapinga uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, wa kuwafungulia mashitaka watuhumiwa hao kwa madai kuwa una dosari za kisheria.

Hati hiyo, inataka shitaka la tatu katika kesi ya jinai namba 27 ya mwaka huu linalosomeka kuwa washitakiwa wote waliisababishia serikali harasa ya sh bilioni 221 lifutwe, kwa madai kuwa haliweki wazi kisheria kosa lililofanywa na washitakiwa hao.

“Kwa sababu hiyo, shitaka hilo la tatu halijaandaliwa kisheria kama kifungu cha 135 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, inavyotaka…na kwa sababu hiyo tunataka uamuzi uliotolewa na DPP wa kuwashitaki wateja wetu ufutwe,” alidai Profesa Mgongo Fimbo.

Hata hivyo, Hakimu Hadija Msongo aliutaka upande wa serikali kujibu ombi hilo Machi 2 na upande wa utetezi ujibu kwa maandishi Machi 4 mwaka huu. Januari 27 washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza wakikabiliwa na mashitaka matatu.

Mashitaka hayo ni matumizi mabaya ya ofisi ya umma, kuidhinisha ujenzi wa minara pacha (Twin Towers) bila idhini ya Bodi ya Wakurugenzi ya BoT na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.Washitakiwa wote walikana shitaka.

Msongo alisema ili mshitakiwa apate dhamana, ni lazima atoe hati au fedha taslimu sh bilioni 55, kusalimisha hati ya kusafiria na kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi serikalini.

Februali 17 hakimu Msongo - kwa mshangao wa wengi - alimpatia dhamana mshitakiwa huyo baada ya kuwasilisha hati zenye thamani ya sh milioni 882, badala ya sh bilioni 55 na hati ya kusafiria iliyokuwa imekwisha muda wake.

Hata hivyo, juzi Msongo alilazimika kufuta dhamana ya Liyumba, baada ya kubaini mshitakiwa huyo aliidanganya mahakama kwa kudai kuwa hakuwa na hati mbili za kusafiria wakati anazo.

Pia mahakama ilibaini hati 10 zilizoletwa na wadhamani wake zilikuwa na upungufu wa kisheria. Alitoa amri ya kutaka hati hizo zipelekwe katika Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 10, mwaka huu, kwa ajili ya kusikiliza ombi hilo la mawakili wa Liyumba.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Februali 26 mwaka 2009

MASIKINI LIYUMBA

*Yabainika hati zake za dhamana zina upungufu
*Hakimu Msongo asema aliidanganya mahakama

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ilimfutia dhamana aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba, ambaye ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na kusababisha hasara ya sh. bilioni 221, baada ya kubaini aliidanganya mahakama.

Aidha mahakama imebaini hati 10 zilizotumika kumdhamini mshitakiwa huyo zilizowasilishwa wiki iliyopita zina mapungufu makubwa na hivyo kuamuru hati hizo zikabidhiwe kwa Jeshi la Polisi ili zifanyiwe uchunguzi.

Uamuzi huo ulitolewa jana majira ya saa 8:02 na Hakimu Mkazi Hadija Msongo, katika chumba namba moja ambapo umati wa watu ulifurika kufuatilia kesi hiyo, alisema baada ya kusikiliza hoja za pande mbili amekubalina na hoja za upande wa serikali za kumfutia dhamana mshitakiwa ameidanganya mahakama kwa kutoa taarifa za uongo.

Februali 17 mwaka huu, Hakimu Msongo alimpatia dhamana mshitakiwa huyo baada ya kuwasilisha hati zenye thamani milioni 882 badala ya sh bilioni 55 na hati ya kusafiria ambayo ilikuwa imekwisha muda wake.

Msongo, alisema kwa mujibu wa kumbukumbu za mahakama katika maombi ya dhamana aliwasilisha hati ya kusafiria ambayo ilikwisha muda wake wa matumizi Februali 12 mwaka 2007.

Katika kumbukumbu za mahakama zinaonyesha alimuuliza kama ana pasi nyingine za kusafiria mshitakiwa huyo alikana na ili kuthibitisha taarifa hizo mahakama iliiomba Idara ya Uhamiaji ambayo ilibainisha kuwa Liyumba ana hati nyingine ya kusafiria yenye namba AB 019418 iliyotolewa Juni 10 mwaka 2005 ambayo muda wake wa matumuzi unamalizika mwaka 2015, ambayo aliwasilisha mahakamani hapo siku moja baada ya kupata dhamana.

Alisema kutokana na sababu hiyo mahakama imeona mshitakiwa huyo ametoa taarifa za uongo kwa vile hati ya kusafiria inamruhusu mtu kusafiri ndiyo maana Jumatano iliyopita mahakama hiyo ikatoa amri ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo.

“Baada ya kupokea taarifa hizo mahakama imebaini Liyumba alitoa taarifa za uongo, mimi nilimuuliza kama ana hati mbili za kusafiria alikana lakini uhamiaji imethibitisha ana hati mbili, leo mahakama inatoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

Baada ya taarifa hizo Februali 18 mwaka huu mahakama ililazimika kutoa amri ya kukamatwa kwa mshitakiwa kwa sababu aliidanganya mahakama kuwa hakuwa na pasi nyingine ya kusafiria.

“Mshitakiwa baada ya kutoa Pasipoti iliyoisha muda wake aliwasilisha nyingine kwa kupitia njia zisizo na utambulisho na alimtuma mtoto wake kuileta.

Msongo alisema baada ya kupitia kwa kina hoja za pande mbili amebaini mshitakiwa aliidanganya mahakama na kutupilia mbali hoja za wakili wa mshitakiwa Majura Magafu kwasababu hoja zake alizozitoa hakuzielekeza kwenye suala la msingi lililopo mahakamani kwani mshitakiwa ndiye alikana kwa kinywa chake kwamba hana hati nyingine ya kusafiria.

“Jibu kwamba hana Pasipoti nyingine lilitolewa na Liyumba mwenyewe na alijibu hivyo kwasababu alikuwa akijua hana hati nyingine ya kusafiria hivyo hoja ya Magafu ya kudai mteja wake hakuwa na lengo la kuiadaha mahakama haikubaliki kwasababu Magafu hawezi kudhibitisha kauli ya Liyumba aliyokana kuwa na pasipoti mbili” alisema Msongo.

Hakimu Msongo, alisema anakubalina hoja za wakili wa serikali Prosper Mwangamila kwamba Liyumba aliidanganya mahakama na kupinga hoja ya Magafu kwamba mshitakiwa ndiye aliyegundua kuwa alitoa hati zilizoisha muda wake bali ni mahakama, hivyo kutokana na kumbukumbu mahakama inamuona siyo mkweli.

Akizungumzia hati 10 zilizotumika kumdhamini mshitakiwa huyo, alisema mahakama imegundua hati ya Avogiti Chiwando ambayo inaonyesha ilitolewa na Afisa wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, si kweli mtu huyo hayupo kwenye wizara hiyo na hati ya Abubakar Ogunda ambayo ilionyesha kuwa na mali kama Kuku, ng’ombe haikubaliki kwani sharti la dhamana lilitaka kuwasilisha hati ya mali zisizohamishika.

‘Kwa ujumla hati zote 10 zinazoonyesha nyumba na viwanja katika maeneo mbalimbali zimeonekana kuwa na kasoro kwani majengo katika hati hizo zinaonekana kufanana.

“Na hati hizo ambazo zinaonyesha ziligongwa mhuri na Mtathimini wa Gharama za Majengo, Thomas Antabe, hazikubali na mahakama kwani mhuri wa mtu huyo hauonyeshi mahali ilipo ofisi yake hivyo mahakama inaona mshitakiwa hajatimiza masharti ya dhamana.

“Kwakuwa masharti ya dhamana hayajatimizwa mahakama hii inatoa amri ya kumfutia dhamana mshitakiwa na hati hizo kumi zipelekwe Jeshi la Polisi ili ziweze kufanyiwa uchunguzi wa kimaandishi na kuahirisha kesi hiyo hadi Machi 10 mwaka huu, ambapo mahakama itakuja kusikiliza ombi la upande wa utetezi.

Kabla ya kutolewa uamuzi huo, wakili Mwandamizi wa Serikali Justas Mulokozi, aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na mahakama hiyo iliyotoa hati ya kukamatwa mshitakiwa wa kwanza ambaye amekuja leo (jana) mahakamani hapo.

Baada ya kusema hayo, wakili Majura Magafu alisimama na kusema awali kuwa anapinga maelezo Mulokozi kwamba mteja wake amekamatwa bali alifika mahakamani hapo kama alivyotakiwa na mahakama hiyo wiki mbili zilizopita.

“Mteja wangu amekuja mwenyewe mahakamani, hakuwa na habari kuwa anatafutwa licha ya magazeti kuandika habri nyingi kuwa anatafutwa, alivyofika asubuhi aliripoti kwa Mkuu wa waendesha mashtaka, Kamishna Msaidi wa Polisi, Charles Kenyela kujua kama ni kweli alikuwa akitafutwa au ni maneno ya magazeti.

“Kwa hiyo tunaomba ieleweke Liyumba hajakimbia na wala hajakamatwa na taarifa za yeye kutafutwa zilikuwa zikitolewa kwenye magazeti …, leo amekuja mwenyewe kwasababu alikuwa akifahamu ndiyo kesi yake inakuja kutajwa” alidai Magafu.

Aidha alikiri hati ya kusafiria ya mshitakiwa ilikuwa imeisha muda wake lakini alidai hali hiyo ilitokea kwa bahati mbaya kwani mteja wake alikaa mahabusu kwa muda mrefu hivyo alichanganyikiwa na aliagiza watoto wake ndiyo walete hati na wakaleta hati iliyokwisha muda wake, mteja wake aligundua kosa hilo na alihakikisha analeta hati mpya ambayo imechukuliwa na mahakama hiyo.

“Hivyo mheshimiwa hakimu, mteja wangu hakuwa na nia mbaya ya kuihadaa mahakama, kwakuwa hati hiyo ipo mahakamani na hatukufanya makusudi tunaomba ile amri ya kumkamata mteja wangu iondolewe na dhamana yake iendelee” alidai Magafu.

Akijibu hoja hiyo wakili Mulokozi alidai pamoja na maelezo marefu na matamu ya wakili Magafu , bado amri iliyotolewa na mahakama ya kumkamata mshitakiwa inatekelezwa na ndiyo maana mshitakiwa alivyofika mahakamani alikuwa chini ya ulinzi na kuongeza kuwa hoja ya wakili wa utetezi kwamba hajakamatwa haina msingi.

Hata hivyo wakili wa serikali Prosper Mwangamila ambaye aliinuka kuomba ridhaa ya mahakama ili aweze kujibu hoja ya Magafu na alikubaliwa na hakimu huyo.

“Wakili Magafu kwa mujibu wa hoja zake hizo zimeonyesha uzalendo na amekomaa kitaaluma kwani amekiri mbele ya mahakama hiyo kwamba hati ya kusafiria iliyowasilisha awali na mteja wake ilikuwa imeisha muda wake na kwamba hivyo ndivyo Afisa wa mahakama anatakiwa atende hivyo.

“Lakini Jumanne iliyopita mteja wake alivyopewa dhamana, upande wa mashtaka ulipinga kwa nguvu zote hati hiyo ya kusafiria isipokelewe hivyo haingii akilini kwamba hati hiyo iliyokwisha muda wake ilitolewa mahakamani hapo bila kukusudia.

“Hakimu ni wewe mwenyewe ulimwuliza mara mbili na sisi ni mashahidi mshitakiwa na alikana kwamba hana hati nyingine ya kusafiria, Kwakuwa sisi tulipinga utolewaji wa hati hiyo hivyo hoja ya Magafu kuwa hawakuwa wamedhamiria kuihadaa mahakama siyo ya msingi” alidai Mwangamila huku akionyesha kujiamini.

Alindelea kudai kuwa kutokana hali hiyo ni dhahiri shahiri kuwa Liyumba si muaminifu na haaminiki, hawana pingamizi la kufutwa kwa amri ya kukamatwa ila wanapinga ombi la kutaka asifutiwe dhamana kwasababu mshitakiwa huyo ameonekana siyo mwaminifu.

“ili siku nyingine mshitakiwa awe mwaminifu, sisi upande wa mashtaka tunaomba afutiwe dhamana, arudishwe mahabusu hadi tutakaporidhika kwamba ametimiza masharti ya dhamana ili sisi tuwe tumepata majibu ya hati zilizotumika kumdhamini kutoka kwenye taasisi za serikali kama ni halali au la” alidai Mwangamila.

Aidha Magafu aliinuka kwenye kiti na kudai kuwa dhamana ni mkataba kati ya mahakama na mshitakiwa na kusisitiza mteja wake hakufanya makusudi kuwasilisha hati hiyo iliyomaliza muda na kuongeza kuwa mtu akitoka jela huwa amechanganyikiwa.

Baada ya kumalizika kwa kesi hiyo saa 9:04 Liyumba alipakizwa kwenye basi la Jeshi la Magereza chini ya Ulinzi mkali lakini hata hivyo alikosa kiti cha kukaa kwenye basi hilo na kulazimika ‘kushika bomba’ huku mahabusu waliokuwa kwenye basi hilo wakishangilia na kumwambia karibu na umerudi tena gerezani’,

Nje ya mahakama hiyo umati mkubwa wa watu ulikuwa umetanda kushuhudia basi lililombeba mshitakiwa huyo likiondoka kuelekea gerezani.

Wakati Liyumba akisimamba kwenye basi hilo, mshitakiwa mwenzake ambaye ni Meneja Mradi wa Benki Kuu, Deogratius Kweka anayetetewa na mawakili wa kujitegemea Profesa Mgongo Fimbo na Hurbet Nyange, alipandishwa peke yake kwenye Toyota Land Cruser lenye namba za usajili STK 4479 na kurudishwa gerezani.

Liyumba aliwasili mahakamani hapo saa 2:47 akiwa kwenye gari lenye namba za usajiri T526AVB aina ya NOAH, ambapo alitangulia kushuka wakili wake Magafu na akafuata Liyumba.

wakili wake akawaambia waandishi wa habari ambao walifika mahakamani hapo tangu saa 12:45 asubuhi mahakamani hapo, wampige picha mteja wake na alivyoshuka moja kwa moja alienda kwenye ofisi ya Mkuu wa Waendesha Mashtaka ACP-Charles Kenyela, ambapo alikaa hadi saa 3:30 ambapo aliingizwa kwenye mahabusu ya mahakama hiyo hadi saa 5:10 alivyoingizwa mahakamani.

Liyumba na Kweka, wanakabiliwa na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuidhinisha ujenzi wa minara pacha ya BoT, maarufu kama ‘Twin Towers’ na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Chanzo:Gazeti la Jumatano ,Februali 25 mwaka 2009

JE MAHAKAMA ILIYUMBA KWENYE DHAMANA YA LIYUMBA?

Na Happiness Katabazi

TUME ya Jaji Joseph Warioba iliyochunguza mianya ya rushwa nchini Tanzania, ilisema kwamba moja ya taasisi za dola ambazo zimegubikwa na rushwa ni Mahakama.

Ibara ya 107-B ya Katiba ya nchi, inayolinda uhuru wa Mahakama ina lengo la kuhakikisha kwamba mahakama haziingiliwi wala kutishwa na mtu au taasisi yoyote wakati zinapotekeleza wajibu wake wa kutoa haki na kutafsri sheria.

Tamko la Tume ya Jaji Warioba limekuwa likiangaliwa katika upeo huo, kwamba pamoja na tuhuma za rushwa, isije ikatokea vita dhidi ya rushwa na ufisadi vikatoa mwanya kwa Mahakama kuingiliwa na kutishwa.

Matukio yaliyotokea kwenye kesi ya jinai namba 27 ya mwaka 2009, Jamhuri dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba na Meneja Mradi wa Benki hiyo, Deogratius Kweka, iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Hadija Msongo, yamenishtua sana.

Mahakama ya Kisutu ndiyo iliyoanza kusikiliza ombi la dhamana la Liyumba kwa kuweka masharti ya dhamana hiyo Januari 27, mwaka huu.

Masharti hayo yalieleza kuwa watuhumiwa wanapaswa kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali, kusalimisha hati ya kusafiria mahakamani, kila Ijumaa kuripoti ofisi za Takukuru, kutoa fedha taslimu au hati zenye thamani ya sh bilioni 55 kila mmoja.

Lakini Jumanne iliyopita, nilishangaa kusoma katika vyombo vya habari kuwa Liyumba aliwasilisha hati yenye thamani ya sh milioni 882, hati ya kusafiria ambayo muda wake wa matumizi umekwisha, huku wadhamini wawili wakiwa hawana barua zilizosainiwa na mwajiri wao kama masharti ya dhamana yalivyotolewa na mahakama hiyo ili Liyumba apewe dhamana.

Licha ya Wakili wa Serikali, Justas Mlokozi, kupinga kwa nguvu zote uamuzi huo, Hakimu Msongo, aliweka pamba masikioni na kutupilia mbali madai ya upande wa wakili Mlokozi na kumwachia Liyumba kwa dhamana huku akiagiza upande wa utetezi kujipanga kukamilisha masharti ya dhamana wakati mtuhumiwa akiwa nje.

Ikumbukwe kuwa masharti hayo ya dhamana katika kesi hiyo yalibishaniwa Mahakama Kuu mbele ya Jaji Projestus Rugazia, na jaji huyo Februari 13, mwaka huu, akitoa uamuzi wake alithibitisha masharti hayo yaliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, isipokuwa sharti moja linalomtaka mshitakiwa kuripoti Takukuru kila Ijumaa.

Kwa kuwa masharti yote yalithibitishwa na Mahakama Kuu na hapakuwa na rufaa iliyokatwa dhidi ya masharti hayo, ulikuwa ni wajibu sasa wa Mahakama ya Kisutu kuhakikisha kwamba dhamana inatolewa mara tu mtuhumiwa anapotimiza masharti yaliyowekwa.

Hata hivyo, hilo halikutokea na badala yake Mahakama ya Kisutu ilipitia upya masharti hayo na kubadilisha kwa namna ambavyo inaweza kulinganishwa na kula matapishi yake. Hivyo sivyo sheria inavyotaka.

Si tu kwamba Kisutu haikuwa na mamlaka ya kuyabadili masharti yale kwa vile yalikuwa yameshabishaniwa Mahakama Kuu na kufanyiwa maamuzi na mahakama hiyo ya juu, bali pia hapakuwa na ombi la kuomba marejeo (review) ya uamuzi huo wa Mahakama Kuu, hata kama ombi hilo lingekuwepo lisingepelekwa Mahakama ya Kisutu, lingepelekwa Mahakama Kuu.

Kumbe basi, kioja kilichotokea kinaleta utata na wasiwasi mwingi kuhusu uwezo wa Hakimu Mkazi, Hadija Msongo na Mahakama ya Kisutu kwa ujumla katika kufanya maamuzi katika shauri hili, kwa kuwa mahakama hii haionekani kuwa na weledi wa kutosha katika tasnia ya sheria.

Katika hali hii, yawezekana kabisa raia wasio na taaluma ya sheria kuchanganyikiwa wanapoisoma Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayosema watu wote ni sawa mbele ya sheria.

Kama wale watuhumiwa wa kesi za EPA walikabwa koo na Mahakama ya Kisutu na hawakupewa dhamana hadi walipotimiza kila kipengele cha masharti ya dhamana na wakafanya hivyo, iweje sasa Liyumba alegezewe masharti na kisha akaachiwa na kuambiwa masharti mengine akatimize akiwa nyumbani kwake?

Kwani Liyumba na hao washtakiwa wa EPA, Basil Mramba, Daniel Yona, wezi wa mabeseni na hata kuku, wanatofauti gani mbele ya sheria?

Lakini pia ni vyema tujiulize kama Mahakama ya Kisutu ilifanya hivyo kwa nia njema bila shinikizo.

Tukumbuke maneno ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP) Said Mwema, kwamba ‘mafisadi ni watu wenye nguvu kubwa.’

Watanzania tunauliza kama nguvu hiyo ya kifisadi imeikumba Mahakama ya Kisutu.

Sisi raia wa kawaida hatushabikii sheria mbaya zinazoweka masharti makali ya dhamana kwa watuhumiwa, lakini ili mradi hatujazibadili sheria hizo ili tuwe na masharti nafuu, kwa kila mtuhumiwa, ni vyema kila raia atendewe sawa mbele ya sheria.

Kitendo kilichofanywa na Hakimu Msongo cha kumpatia dhamana Liyumba wakati hajatimiza masharti ambayo Januari 27 mwaka huu, ni yeye aliyeyaweka na yakasisitizwa na Mahakama Kuu, kimetia doa mhimili mahususi wa Mahakama nchini, kuhusu uwezo wa kusimamia haki na usawa mbele ya sheria.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Februali 25 mwaka 2009

LIYUMBA KUIBUKIA MAHAKAMANI LEO

Na Happiness Katabazi

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba, ambaye ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na kusababisha hasara ya sh bilioni 221, leo anatarajiwa kuibukia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Tanzania Daima imeelezwa.

Kwa mujibu wa watu wa karibu na Liyumba, wamesema ataibukia mahakamani leo.
Vyanzo hivyo vilikanusha madai kwamba Liyumba alikuwa ametoroka na kubainisha kwamba aliamua kuzima simu yake ya kiganjani ili aweze kupumzika, baada ya kusota rumande kwa siku 22.

“Tunashangaa sana huu uvumi kwamba Liyumba katoroka, kimsingi ajatoroka, yupo hapa hapa jijini, kajichimbia na alizima simu zake ili aweze kupumzika na kuhakikisha anakamilisha masharti ya dhamana, kwani tayari kuna taarifa kuwa mahakama itabatilisha taratibu zilizotumika kumpatia dhamana, hivyo atatakiwa aanze upya kuomba dhamana.

“Nakuhakikishia kesho (leo), Liyumba ataibukia Mahakama ya Kisutu, kwani ndiyo tarehe ya kesi yake inayokuja kwa ajili ya kutajwa na haya ninayokueleza, vyombo vya ulinzi na usalama vinajua kwamba yupo na ana fanya nini.

“Navishangaa sana vyombo vya habari vinavyoandika Liyumba ametoroka, nyie andikeni wee lakini ukweli ni kwamba Liyumba ajatoroka, yupo hai na hivyo vyombo vya dola vilivyopewa amri na mahakama ya kumkamata Liyumba, vinafahamu kwamba yupo wapi, anafanya nini na anaishi wapi,” kilisema chanzo chetu.

Mbali na Liyumba, mshitakiwa mwingine ni Meneja Mradi wa BoT, Deogratius Kweka, ambaye hadi sasa anaendelea kusota rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Alhamisi ya wiki iliyopita, uvumi ulizagaa jijini Dar es Salaam kwamba mshitakiwa huyo ametoroka.

Kutokana na uvumi huo, mahakama ililazimika kutoa hati ya dharura ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo na wadhamini wake wawili.

Hata hivyo vyanzo vyetu vya habari vilidai kuwa mshitakiwa huyo aliitwa kwa hati ya dharura mahakamani, huenda kutokana na mazingira ya utata wa dhamana yake, kwani alidhaminiwa kwa hati ya mali ya sh milioni 882, badala ya mali zenye thamani ya sh bilioni 55.

Siku hiyo, saa sita mchana, wadhamini wake wawili ambao ni wafanyakazi wa BoT, Otto Agatoni, Ofisa Usalama wa Ndani ya benki hiyo, na Benjamin Ngulugunu, ambaye ni mhasibu, walikamatwa na kuswekwa katika mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuanzia majira ya saa sita mchana hadi saa 10:32 jioni, walipopandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi, Hadija Msongo.

Msongo alisema kesi hiyo itatajwa leo kama ilivyopangwa awali na kwamba wadhamini hao nao wanatakiwa kufika pamoja na mshitakiwa.

Liyumba na Kweka, wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuidhinisha ujenzi wa minara pacha ya BoT, maarufu kama ‘Twin Towers’ na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne,Februali 24 mwaka 2009

MALUMBANO YASITISHA KESI YA EPA

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ililazimika kisitisha kuendelea kusikiliza ushahidi uliokuwa ukitolewa na shahidi wa sita Mrakibu wa Polisi(SSP) Salum Kisai(45), katika kesi ya wizi wa sh bilioni 1.8 katika Benki Kuu(BoT), kufuatia kuibuka malumbano makali ya kisheria kati ya upande wa serikali na utetezi.

Naibu Mwenyekiti wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Cypiriana William ambaye anasaidiana Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Phocus Bambika na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Saul Kinemela, alisema amekubalina na hoja ya Wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus Boniface na kwamba anasitisha usikilizaji wa ushahidi wa shahidi huyo hadi leo.

Baada ya malumbano hayo ya kisheria, Boniface aliiomba mahakama kuwa iwepo kesi ndani ya kesi ili wakili wa utetezi, Majura Magafu aweze kuleta mashahidi na vielezo ambavyo vitaunga mkono pingamizi lake la kuiomba mahakama hiyo isipokee maelezo ya onyo aliyochukuliwa mshitakiwa wa pili Farijara Hussein kwenye Kikosi Kazi(Task Force), kwasababu mshitakiwa huyo ameyakana maelezo hayo, saini siyo yake,na kwamba anachokifahamu mteja wake ni kwamba aliandika maelezo ya onyo akiwa na watu wa nne na siyo watu wawili kama ilivyodaiwa na shahidi huyo.

“Jopo hili linakubalina na hoja msomi Boniface na kwasababu hiyo kwamba kuwepo na kesi ndani ya kesi na kwasababu hiyo jopo hili haliwezi kuendelea kusikiliza ushahidi wa shahidi huyu hadi kesho(leo) ambapo wakili Magafu atakapokuja kuleta ushahidi utakaoonga mkono pingamizi lake la kutaka jopo hili lisipokee maelezo ya onyo kama kielelezo” alisema William.

Kabla ya malumbano hayo kuibuka , Wakili Boniface alimwongoza Kisai kutoa ushahidi wake.Na ifuatayo ni mahojiano kati ya wakili huyo wa serikali na shahidi;
Wakili:Shahidi iambie mahakama unafanyakazi wapi?
Shahidi:Jeshi la Polisi.
Wakili:Kama nani?
Shahidi:Kama mpelelezi toka Makao Makuu ya Upelelezi.Na nina cheo cha Mrakibu wa Pilisi.
Wakili:Ulijiunga na jeshi hilo lini?
Shahidi:1982.
Wakili:Si vibaya ukiambia mahakama kiwango chako cha elimu?
Shahidi:Shahada ya Sheria toka Chuo Kikuu Huria.
Wakili:Huko kwenye Idara ya Upelelezo kutoka kitengo maalum unashughilikia nini?
Shahidi:Wizi uhausiana na masuala ya kughushi.
Wakili:Kuna kitu kinaitwa Kiloloma &Brothers unakifahamu?
Shahidi:Ndiyo.
Wakili:Lini?
Shahidi:Wakati naendelea na Upelelezi wa kesi za EPA.
Wakili:Upelelezi wa Kesi za EPA ulinaza lini?
Shahidi:Ulianza Januari 2008.
Wakili:Huu upelelezi uliusisha watu gani?
Shahidi:Uliusisha kikosi kazi(Task Force).
Wakili:Iliundwa na Taasisi gani?
Shahidi:Polisi, Takukuru na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wakili:Ofisi za Task Force zilikuwa wapi?
Shahidi:Mikocheni.
Wakili:Na hii Kiloloma &Brothers Enterprises uliifahamu vipi?
Shahidi:Niliifahamu wakati wa upelelezi wa kesi za EPA.
Wakili:Upelelezi wenu ulionyesha Kiloloma&Brothers, wamiliki wake ni wakina nani?
Shahidi: Ulionyesha wamilikiwa wake ni washtakiwa waliopo kizimbani,Farijara Hussein na Rajabu Maranda.
Wakili:Upelelezi huo huo ulionyesha nini kuhusu Kiloloma&Bros, nani ni wamilikiwa wake?
Shahidi:Ulionyesha jina la biashara lililosajiliwa rasmi na BRELA.
Wakili:Vipi kuhusu Kiloloma &Bros nani alikuwa mmiliki wake?
Shahidi:Charles Issac ndiyo mmiliki wake.
Wakili:Sasa ulipogundua Kiloloma&Bros imesajiliwa kihalali na Kiloloma&Brothers haijasajiliwa kihalali ulifanya nini?
Shahidi:Nilitafuta wamiliki wake.
Wakili:Utafutaji wa wamiliki hao uliishia wapi?
Shahidi:Niliwatafuta washtakiwa ambao wapo leo(jana) kizimbani.
Wakili:Mahakama inangependa kujua ni namna gani uliwapata?
Shahidi:Tulitumia Anwani zao na kuwapata,kama mshitakiwa wengine tunavyowapata.
Wakili:Washtakiwa hawa tafadhari ulipataje?
Shahidi:Nilitumia namba zao za simu na mshitakiwa wa kwanza Maranda, ilikuwa ikipatikana.Nilimpigia simu hakapatikana na nikamjulisha anaitajika polisi.
Wakili:Yeye alifanya nini baada ya kumweleza hivyo?
Shahidi:Aliitikia wito akataka kujua nipo wapi,nikamwambia anatakiwa Task force na nikamjulisha afike karibu na Karibu Hoteli , ataona mimi na wenzangu tumeegesha gari pembeni.
Wakili:Mshitakiwa alifanya hivyo?
Shahidi:Ndiyo.
Wakili:Mlikuwa wangapi kati hilo gari?
Shahidi:Wanne.Maofisa wa polisi wawili na yaani mimi na SSP-Sifael Mkonyi na maofisa wa Takukuru wawili, Wandwe na Mushi.Tulijitambulisha kwa mshitakiwa tukamtaka aongozane na sisi kwenye ofisi za Kikosi Kazi(Task Force) zilizopo Mikocheni.
Wakili:Mlipofika Mikocheni mlifanya nini?
Shahidi:Nilianza kumhoji kwmaba yeye anaishi wapi.
Wakili:Ebu tuje kwenye mmiliki mwingine wa Kiloloma &Brothers, Farija, mlipataje?
Shahidi:Wakati tunamtafuta alikuwa hapatikani kwenye simu na hata nyumbani kwake.
Wakili:Sasa mlifanyaje?
Shahidi:Tuliendelea kumtafuta kupitia serikali za mtaa anaoishi bila mafanikio.Na kumbuka siku moja tarehe nimeisahau Farijara alijitokeza na kujisalimisha pale Makao Makuu ya Polisi.
Wakili:Ilikuwaje alivyojisalikisha?
Shahidi:Alipofika Polisi alikutana maofisa wa polisi, na walitujulisha yule mtuhumiwa tuliyekuwa tukimtafuta kajisalimisha.Nikamfuata pale Makao Makuu ya Polisi na akajitambulisha kwamba anaitwa Farijala Shaban Hussein.Alisema ameamu kujisalimisha kwasababu amekuwa akitafutwatafutwa sana.
Wakili:Aliendelea kubaki polisi?
Shahidi:Hapana, nilimchukua nikampeleka kwenye ofisi ya Kikosi Kazi Mikocheni.
Wakili:Ebu ieleze mahakama Oktoba 3 mwaka 2008 asubuhi ulikuwa wapi?
Shahidi:Nilikuwa ofisini Mikocheni nikiendelea na kazi ya Uchunguzi.
Wakili:Siku hiyo kati ya washtakiwa hao alifika ofisini hapo?
Shahidi:Alifika Farijara Hussein na alifika mbele yangu.
Wakili:Ulifanya nini?
Shahidi:Nilianza rasmi kujitambulisha kwake kuwa mimi ni ofisa wa Polisi na nilimtaadhalisha nataka kuchukua maelezo yake ya onyo kuhusiana na tuhuma zonazomkabili za kughushi maandishi, kutoa taarifa za uongo.Nilimtaadharisha pia maelezo atakayotoa ayatoe kwa hiari yake na kwamba yataweza kutumika mahakamani.
Wakili:Yeye alikujibu nini?
Shahidi:Alinijibu yupo tayari kwa hiari yake kabisa kutoa maelezo hayo ya onyo.
Wakili:Wakati huo wewe ulikuwa na nani?
Shahidi:Nilikuwa mimi nay eye tu kwenye chumba maalum kwaajili ya kuchukulia maelezo ya watuhumiwa wa EPA.
Wakili:Ulivyomaliza kuandika maelezo yake ulifanyaje?
Shahidi:Niliandika muda wa kumaliza kuandika maelezo hayo na nilidhibitisha maelezo hayo niliandika kwa usahihi kama alivyonieleza.
Wakili:Tazama hilo kabla ni la nini?
Shahidi:Hili ni kablasha la hati ya onyo la Farijala niloandika maelezo yake mimi.
Wakili:Unapenda ulitoe mahakamani kama kielelezo?
Shahidi:Ndiyo.
Baada ya kusema hayo, Magafu alinong’onezana na mteja wake Farijala na kisha alisimama na kupinga maelezo hayo yasipokelewe na jopo hilo kwasababu mteja wake siku alipohojiwa kuliwa na watu wa nne akiwemo wakili wa serikali Biswalo Mganga ambaye jana alikuwa ni miongoni mwa mawakili wa serikali waliokuwa wakimsaidia Stanslau Boniface.

Na kwamba Farijala aliwahi kuitwa na kusaini maelezo ambapo hadi leo hii hajawahi kuitwa kusomewa.Kesi hii itaendelea leo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Februali 24 mwaka 2009

Na Happiness Katabazi

UPANDE wa serikali katika kesi ya wizi wa sh bilioni 1.1 wa Fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu(BoT)umesema unatarajia kuleta mashahidi 23 katika kesi hiyo pindi itakapoanza kusikilizwa.

Wakili Kiongozi wa Serikali Boniface Stanslaus, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Waliyawande Lema,wakati akiwasomewa maelezo ya awali washtakiwa watano katika kesi hiyo ambapo alidai mashahidi wote watatumia anwani ya Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai(DCI).

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Bahati Mahenge,Manase Makale,Davis Kamungu,Godfrey Mosha na Eda Makale.

Wakili Stanslaus alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka tisa likiwemo kosa wizi,kula njama, kujipatia ingizo kwenye akaunti yao,kughushi ,kuwasilisha nyaraka za uongo.

Akisoma maelezo hayo, wakili huyo alidai washtakiwa wote ni wakazi wa jijini na kwamba mshitakiwa 2 na 5 ni wanandoa na kwamba Desemba 23 na Oktoba 26 mwaka 2005 wote walifanya makubaliano ya kuibia Benki Kuu ya Tanzania.

Alidai ilikukamilisha lengo hilo mshitakiwa wa kwanza Mahenge,alisaini Memorandum Form namba moja enye namba 14 na 15 kwajina la Samson Mapunda ,jina ambalo ni la kufikirika.

Na aliweka katika fomu hizo taarifa za uongo kuhusu anwani ya makazi,eneo la kampuni na taarifa hizo kampuni ya Changanyikeni Residential Complex ilisajiliwa na BRELA na kwa namba 47792.

“Vile vile mshitakiwa wa kwanza alisaini kadi ya benki ya CRDB pamoja General Terms of Condition poamoja na fomu ya kufungulia akaunti kwa jina la kufikirika la Samson Mapunda” alidai Boniface.

Aliendelea kudai washtakiwa hao walifungua akaunti CRDB Tawi la Kijitonyama na Agosti 31 mwaka 2005, Mahenge alisaini fomu nyingine kwa jina hilo la kufikirika na fomu hiyo ilionyesha kufanyika makubalino kati ya kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan na Changanyikeni Residential Complex na katika makubaliano alidai kwamba Changanyikeni imepewa kibali cha kukusanya deni la kampuni ya Marubeni.

Aidha alidai Oktoba 26 mwaka 2005 akaunti ya Changanyikeni iliingiziwa sh 1,186,534,303.27 na baadaye fedha hizo zilianza kuchukuliwa ama kwa keshi au hundi.

Wakili Stanslaus kwa njia ya onyo, Mahenge alikubali kuhusika katika uhalifu na aliwataja wenzake ambao ni washtakiwa katika kesi hiyo.

Na wakili huyo aliomba mahakama imruhusu awasilishe hati hiyo ya onyo mahakamani hapo kama upande wa utetezi utamruhusu.

Wakili wa utetezi, Gabriel Mnyere alipinga ombi hilo la upande wa mashtaka kuwasilisha hati hiyo ya onyo,kuwasilishwa mahakamani hapo kwasababu upande wa mashtaka ulipaswa kuwapatia mapame hati hiyo mawakili wa utetezi waipitie ndiyo ikabidhiwe mahakama.

Hata hivyo wakili Stanslaus aliinuka na kudai kwamba nachotakiwa wakili wa utetezi ni kupinga au kutopinga ombi lake na siyo kutoa maelezo mengine.

Hakimu Lema aliairisha kesi hiyo hadi Machi 12 mwaka huu, ambapo itakuja kwaajili ya kupangiwa tarehe.




Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Februali 21 mwaka 20009.

23 KUTOA USHAHIDI KESI YA EPA

Na Happiness Katabazi

UPANDE wa serikali katika kesi ya wizi wa sh bilioni 1.1 wa Fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu(BoT)umesema unatarajia kuleta mashahidi 23 katika kesi hiyo pindi itakapoanza kusikilizwa.

Wakili Kiongozi wa Serikali Boniface Stanslaus, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Waliyawande Lema,wakati akiwasomewa maelezo ya awali washtakiwa watano katika kesi hiyo ambapo alidai mashahidi wote watatumia anwani ya Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai(DCI).

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Bahati Mahenge,Manase Makale,Davis Kamungu,Godfrey Mosha na Eda Makale.

Wakili Stanslaus alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka tisa likiwemo kosa wizi,kula njama, kujipatia ingizo kwenye akaunti yao,kughushi ,kuwasilisha nyaraka za uongo.

Akisoma maelezo hayo, wakili huyo alidai washtakiwa wote ni wakazi wa jijini na kwamba mshitakiwa 2 na 5 ni wanandoa na kwamba Desemba 23 na Oktoba 26 mwaka 2005 wote walifanya makubaliano ya kuibia Benki Kuu ya Tanzania.

Alidai ilikukamilisha lengo hilo mshitakiwa wa kwanza Mahenge,alisaini Memorandum Form namba moja enye namba 14 na 15 kwajina la Samson Mapunda ,jina ambalo ni la kufikirika.

Na aliweka katika fomu hizo taarifa za uongo kuhusu anwani ya makazi,eneo la kampuni na taarifa hizo kampuni ya Changanyikeni Residential Complex ilisajiliwa na BRELA na kwa namba 47792.

“Vile vile mshitakiwa wa kwanza alisaini kadi ya benki ya CRDB pamoja General Terms of Condition poamoja na fomu ya kufungulia akaunti kwa jina la kufikirika la Samson Mapunda” alidai Boniface.

Aliendelea kudai washtakiwa hao walifungua akaunti CRDB Tawi la Kijitonyama na Agosti 31 mwaka 2005, Mahenge alisaini fomu nyingine kwa jina hilo la kufikirika na fomu hiyo ilionyesha kufanyika makubalino kati ya kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan na Changanyikeni Residential Complex na katika makubaliano alidai kwamba Changanyikeni imepewa kibali cha kukusanya deni la kampuni ya Marubeni.

Aidha alidai Oktoba 26 mwaka 2005 akaunti ya Changanyikeni iliingiziwa sh 1,186,534,303.27 na baadaye fedha hizo zilianza kuchukuliwa ama kwa keshi au hundi.

Wakili Stanslaus kwa njia ya onyo, Mahenge alikubali kuhusika katika uhalifu na aliwataja wenzake ambao ni washtakiwa katika kesi hiyo.

Na wakili huyo aliomba mahakama imruhusu awasilishe hati hiyo ya onyo mahakamani hapo kama upande wa utetezi utamruhusu.

Wakili wa utetezi, Gabriel Mnyere alipinga ombi hilo la upande wa mashtaka kuwasilisha hati hiyo ya onyo,kuwasilishwa mahakamani hapo kwasababu upande wa mashtaka ulipaswa kuwapatia mapame hati hiyo mawakili wa utetezi waipitie ndiyo ikabidhiwe mahakama.

Hata hivyo wakili Stanslaus aliinuka na kudai kwamba nachotakiwa wakili wa utetezi ni kupinga au kutopinga ombi lake na siyo kutoa maelezo mengine.

Hakimu Lema aliairisha kesi hiyo hadi Machi 12 mwaka huu, ambapo itakuja kwaajili ya kupangiwa tarehe.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Februali 21 mwaka 2009

LIYUMBA BADO ASAKWA

*Yadaiwa amejificha Dar kukamilisha dhamana
*Wadhamini wake wafutiwa amri ya kukamatwa

Na Happiness Katabazi

VYOMBO vya ulinzi na usalama nchini bado vinaendelea kumsaka mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na kusabisha hasara ya sh bilioni 221, inayomkabili Amatus Liyumba, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT).


Mbali na Liyumba, mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Meneja Mradi wa benki hiyo, Deogratius Kweka, ambaye hadi sasa bado anasota rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hatua hiyo ya vyombo vya ulinzi kuendelea kumsaka Liyumba, inatokana na juhudi za vyombo hivyo juzi na jana kushindwa kumkamata na kumfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Jumatano wiki hii ilitoa hati ya dharura ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo na wadhamini wake wawili.

Wakili wa serikali, Mwangamilia, aliyekuwa akisaidiana na Tabu Mzee kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), alidai mahakamani hapo jana kuwa bado hawajafanikiwa kumkamata Liyumba kama walivyoamriwa na mahakama hiyo.

Kwa upande wake, wakili wa mshitakiwa wa kwanza, Majura Magafu, aliyejiunga rasmi jana kumtetea mshitakiwa huyo akisaidiana na wakili Hudson Ndusyepo, aliiambia mahakama kuwa mteja wake hajafika mahakamani, lakini wadhamini wake - Otto Agatoni na Benjamin Ngulugunu - wamefika mahakamani hapo.

Akitoa uamuzi wake jana saa 8:52 alasiri, hakimu Hadija Msongo alisema ameshapokea jalada halisi la kesi hiyo kutoka Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, na kwamba amefuta hati ya kukamatwa kwa wadhamini hao isipokuwa hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo bado inaendelea.

Msongo alisema kesi hiyo itatajwa Februari 24 kama ilivyopangwa awali na kwamba wadhamini hao wanatakiwa kufika siku hiyo.

Baada ya kutoa uamuzi huo, Magafu alisimama na kuanza kuulalamikia upande wa mashitaka kwamba umeanza kuinyanyasa familia ya Liyumba na kuiomba mahakama ikemee suala hilo.

Alikuwa anaomba gari la mdhamini wa mshitakiwa huyo lenye namba za usajili T329 AWY Toyota Chaser linaloshikiliwa, liachiliwe.

Hata hivyo, Msongo alimtaka Magafu aache kuwasilisha maombi yake kwani jana haikuwa tarehe ya kesi hiyo.

“Magafu, nimeshasema leo si tarehe ya kesi hii…kama una malalamiko yoyote yawasilishe siku ya tarehe ya kesi,” alisema Msongo na kuahirisha kesi hiyo.

Lakini habari Tanzania Daima iliyozipata jana kutoka vyanzo vya habari vya kuaminika, zinadai kuwa Liyumba hajatoroka, bali yupo nchini amejificha na anachokifanya ni kuhakikisha anakamilisha masharti ya dhamana ili Jumanne atakapofika mahakamani aweze kutimiza masharti hayo.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, taratibu zilizotumika kumpatia dhamana zitafutwa na atatakiwa aanze upya, hali itakayosababisha kurudishwa tena rumande.

Juzi uvumi ulizagaa Dar es Salaam kuwa Liyumba ametoroka. Kutokana na uvumi huo mahakama ilitoa hati ya kukamatwa kutokana na mazingira ya utata wa dhamana yake, kwani alidhaminiwa kwa hati ya mali ya sh milioni 882 badala ya mali zenye thamani ya sh bilioni 55.

Kabla ya kupewa dhamana, Liyumba alikwenda Mahakama Kuu kuomba alegezewe masharti ya dhamana hiyo iliyomtaka atimize masharti ya hati za mali au fedha taslimu sh bilioni 55, wadhamini wawili, kuwasilisha hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na kila Ijumaa kuripoti katika Ofisi ya Takukuru.

Hata hivyo, Mahakama Kuu Ijumaa iliyopita, chini ya Jaji Projestus Lugazia, ilitupilia mbali ombi hilo, kwa madai kuwa haoni sababu za kutengua masharti ya dhamana ya Kisutu.

Baada ya maombi hayo kutupwa, Liyumba Jumatatu wiki hii aliwasilisha hati za dhamana zenye thamani ya sh bilioni 55, ambazo, hata hivyo, zilipangwa na mawakili wa serikali kwa madai kuwa zilikuwa na kasoro.

Liyumba na Kweka wanakabiliwa na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuidhinisha ujenzi wa minara pacha ya BoT, maarufu kama ‘Twin Tower’ na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi,Februali 21 mwaka 2009

LIYUMBA ATOWEKA

*Korti yatoa hati ya dharura kumkamata
*Polisi, Takukuru wamsaka bila mafanikio
*Wadhamini watiwa mbaroni, hatima yao leo

Na Happiness Katabazi

UVUMI umezagaa jijini Dar es Salaam kuwa mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na kusababisha hasara ya sh bilioni 221, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba, ametoroka.


Mbali na Liyumba, mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Meneja Mradi wa benki hiyo, Deogratius Kweka, ambaye hadi sasa bado yuko rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Kutokana na uvumi huo, juzi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ililazimika kutoa hati ya dharura ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo na wadhamini wake wawili.

Hata hivyo vyanzo vyetu vya habari vilidai kuwa mshitakiwa huyo aliitwa kwa hati ya dharura mahakamani, huenda kutokana na mazingira ya utata wa dhamana yake, kwani alidhaminiwa kwa hati ya mali ya sh milioni 882, badala ya mali zenye thamani ya sh bilioni 55.

Vyanzo vya habari kutoka serikalini, viliiambia Tanzania Daima jana asubuhi kuwa vilipata taarifa kwamba, Liyumba alikuwa amepanga njama za kutoroka, huku vyanzo vingine vikidai kwamba alikuwa amepanga njama za kusingizia kuumwa, kwani alipata taarifa kuwa upande wa serikali umechukizwa na jinsi taratibu zilivyokiukwa za kumpatia dhamana na upande wa mashitaka ulikuwa umepanga kuwasilisha hoja ya kutengua dhamana yake.

“Hizo taarifa tumezisikia na tunazifanyia kazi kwa karibu, ila nakuhakikishia hati yake ya kusafiria iliwasilishwa mahakamani jana (juzi), kwani serikali imekerwa na jinsi taratibu zilivyokiukwa kumpatia dhamana na hadi sasa jalada la kesi yake limeitishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kupitiwa.

“Kwa hiyo jalada likirudishwa Kisutu, mambo yatabadilika juu yake, kwani dhamana yake imeshtua wengi, wakiwemo maofisa wa juu wa mahakama,” kilieleza chanzo chetu cha habari.
Hata hivyo, jana saa sita mchana wadhamini wake wawili ambao ni wafanyakazi wa BoT, Otto Agatoni, Ofisa Usalama wa Ndani ya Benki hiyo na Benjamin Ngulugunu, ambaye ni mhasibu, walikamatwa na kuswekwa katika mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuanzia majira ya saa sita mchana hadi saa 10:32 jioni, walipopandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi, Hadija Msongo.

Wakili wa Liyumba, Hudson Ndusyepo, alimweleza Hakimu Msongo kuwa licha ya mahakama kutoa hati ya dharura kukamatwa kwa mteja wake, hakufika mahakamani, lakini hakutoa sababu za Liyumba kutofika mahakamani hapo.

Kwa upande wake, wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Tabu Mzee, alidai kuwa walipokea hati ya dharura ya kukamatwa kwa Liyumba na wadhamini wake wawili jana na taasisi hiyo ilifanikiwa kuwakamata wadhamini hao, lakini jitihada za kumtafuta Liyumba kwa siku nzima ya jana, zilishindikana.

“Tulipokea hati ya mahakama ya kumkamata mshitakiwa Liyumba na wadhamini wake. Tumefanikiwa kuwakamata wadhamini hao, lakini jitihada zetu za kumkamata Liyumba zilishindikana baada ya kumtafuta kwa njia zote, ikiwamo ya simu ya mkononi bila mafanikio,” alidai Tabu.

Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Msongo aliwaeleza wadhamini wa Liyumba kuwa yeye ndiye aliyetoa amri ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa huyo, lakini alisema hawezi kuzungumzia chochote kwa sababu jalada la kesi yao limeitishwa Mahakama Kuu.

“Mahakama hii ndiyo imetoa amri ya kukamatwa kwenu na kwa sababu jalada la kesi ya msingi limeitishwa Mahakama Kuu, siwezi kuzungumza chochote leo, naahirisha hadi kesho (leo), saa nane mchana na nyie wadhamini mfike bila kukosa,” alisema Hakimu Msongo.

Kutokana na uamuzi huo, wadhamini hao waliachiwa huru kurudi majumbani kwao, huku wakionekana kutoamini kilichowatokea.

Kabla ya kupewa dhamana, Liyumba, alikwenda Mahakama Kuu kuomba alegezewe masharti ya dhamana hiyo iliyomtaka atimize masharti ya hati za mali au fedha taslimu sh bilioni 55, wadhamini wawili, kuwasilisha hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na kila Ijumaa kuripoti katika Ofisi ya Takukuru.

Hata hivyo, Mahakama Kuu, Ijumaa iliyopita, chini ya Jaji Projestus Lugazia, ilitupilia mbali ombi hilo, kwa madai kuwa haoni sababu za kutengua masharti ya dhamana yaliyowekwa na Mahakama ya Kisutu.

Baada ya maombi hayo kutupwa, Liyumba Jumatatu wiki hii, aliwasilisha hati za dhamana zenye thamani ya sh bilioni 55, ambazo hata hivyo zilipingwa na mawakili wa serikali, kwa madai kuwa zilikuwa na kasoro.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Fredrick Manyanda, alipinga hati hizo kwa madai kuwa zina makosa mbalimbali, hivyo zinapaswa kurekebishwa kabla ya mshitakiwa huyo kupatiwa dhamana.

Alizitaja kasoro nyingine kuwa hati za mali hizo, zimechanganywa kati ya mali zinazohamishika na zisizohamishika, hivyo kuwafanya washindwe kujua ukweli wa thamani zake.
Pia alidai baadhi ya hati zina jina moja la mmiliki na kusababisha kutoziamini.

Hata hivyo, Jumanne wiki hii, Hakimu Msongo kwa mshangao wa wengi, alimpatia dhamana mshitakiwa huyo baada ya kuwasilisha hati zenye thamani ya sh milioni 882, badala ya sh bilioni 55.

Liyumba na Kweka, wanakabiliwa na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuidhinisha ujenzi wa minara pacha ya BoT, maarufu kama ‘Twin Towers’ na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Februali 20 mwaka 2009

MSHTAKIWA KESI YA ZOMBE YU HOI

* Ashindwa kufika mahakamani kujitetea
* Kesi yasitishwa kumpa nafasi apone
* Ni yule mwenye ushahidi muhimu
* Watu wafurika kusikiliza ushahidi wake

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana ililazimika kusitisha usikilizaji wa kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja kutokana na mshtakiwa wa 11, Rashid Lema, kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi wake, kwa sababu ya afya yake kuwa mbaya.


Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Massati, alisitisha usikilizaji wa kesi hiyo ambayo kwa mujibu wa ratiba ya vikao kesi za mauaji iliyotolewa na kesi hiyo ilikuwa umalizike leo.

Jaji Massati wakati akiahirisha kesi hiyo, alisema anakubaliana na hoja za wakili wa mshtakiwa wa 11 na 12 (Rashid Lema na Rajabu Bakari), Denis Msafiri na kusema kwamba hoja zake ni nzito.

Alisema kwa sababu kikao hicho kinakwisha (kesho) leo na kwa mujibu wa ratiba hakiwezi kuendelea hadi kibali cha Jaji Mkuu, alisema utetezi wa washtakiwa waliosalia utasikilizwa katika kikao kingine.

“Tutaendelea na utetezi hadi kikao cha kesi hii kitakapopangwa na Msajili wa Mahakama na pia naagiza upande wa utetezi upewe mwendo wa kesi hii,” alisema Jaji Massati.

Awali, wakili wa mshtakiwa 11 na 12, ambapo jana Lema alikuwa atarajiwa kuanza kutoa ushahidi wake ambao ulikuwa unasubiriwa kwa shauku na umati wa watu, aliomba mahakama iahirishe kesi hiyo, kwani juzi alienda gerezani kumuona Lema na kuona afya yake haimruhuu kufika mahakamani kutoa ushahidi.

“Mtukufu Jaji kama nilivyoomba juzi kwenda kumuona Lema gerezani, nilikwenda nikaongea naye, hawezi kutoa ushahidi leo (jana) wala kesho, kwani hali yake kiafya hamruhusu. Naomba kesi hii iarishwe,”alidai wakili Msafiri.

Jaji Massati alipomuuliza ni kwa nini mshtakia wa 12, asiendelee jana kutoa ushahidi wake, wakili huyo alidai ni muhimu Lema atoe ushahidi wake kwanza ambao utatoka kwenye kinywa chake ndipo mshtakiwa wa 12 afuate kutoa ushahidi.

Aidha, Jaji Massati alipomuuliza wakili wa mshitakiwa 13, (Festus Gwabusabi), Myovela ni kwanini mshitakiwa wake asijitete, alidai hawakuwa wamejiandaa kutoa ushahidi kwa kuwa kuna baadhi ya nyaraka ambazo wangezitumia wakati mshitakiwa huyo akijitetea bado hawajazipata.

Kwa upande wake, wakili wa Mshitakiwa wa kwanza, Jerome Msemwa, alieleza kuunga mkono hoja zilizotolewa na mawakili wenzake kuwa shauri hilo liahirishwe.

Tanzania Daima ambalo lilifika mahakamani hapo saa 1:02 asubuhi, ilishuhudia umati mkubwa wa watu uliokuwa umekaa kwenye viwanja vya mahakama ukisubiri kusikiliza kesi hiyo.

“Tumefika hapa tangu saa 12 asubuhi tunasubiri mahakama ifunguliwe, ili tuwahi viti kumsikiliza Lema ambaye inadaiwa ndiye mshtakiwa aliyepania kutoa siri ya mauaji hayo,” alisema Jakson John ambaye ni mkazi wa Kimara.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Februari 3 mwaka huu ambapo mawakili wa utetezi waliwasilisha hoja za kwamba wateja wao hawana kesi ya kujibu na upande wa serikali kujibu hoja hizo.

Februali 9 mwaka huu, Jaji Massati alitoa uamuzi kuhusu hoja hizo na kuwaachiwa huru washtakiwa watatu ambao ni Noel Leonard, Koplo Moris Nyangerela na Koplo Felix Sandys Cedrick kwa maelezo kuwa ushahidi uliotolewa umeshindwa kuthibitisha kwamba wana kesi ya kujibu.

Mbali na Lema na Bakari, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe, SP Christopher Bageni, SP Ahmed Makelle, Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Koplo Abeneth Saro, na Festus Gwasabi, ambao wanadaiwa Januari 14 mwaka 2006, huko Mbezi Luisi Msitu Pande, waliwauwa Ephraim Chigumbi, Sabinus Chigumbi na Mathias Lukombe ambao ni wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge na Juma Ndugu ambaye ni dereva teksi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Februali 20 mwaka 2009

'NILIPONZWA NA ZOMBE

*Aliyesema marehemu waliuawa Pande kutoa ushahidi leo

Na Happiness Katabazi

MSHITAKIWA wa 10 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja, Koplo Abeneth Saro (45), ameiambia mahakama kuwa watuhumiwa aliowashuhudia kuwa walikamatwa Sinza wakiwa hai ndio waliouawa.

Sambamba na hilo, mshitakiwa wa 11, Rashid Lema, ambaye tangu washitakiwa wenzake waanze kujitetea Febuari 3 mwaka huu, hajawahi kuhudhuria mahakamani kutokana na afya yake kuwa si ya kuridhisha, leo anatarajiwa kuanza kutoa ushahidi wake.

Mshitakiwa Lema ndiye aliyeeleza katika maelezo yake kwamba mauaji hayo yalifanyika katika msitu wa Pande.
Akitoa utetezi wake jana, Koplo Abeneth ambaye ni askari kutoka Idara ya Upelelezi, Kituo cha Urafiki, alidai yeye alikuwa ni miongoni mwa askari walioongozana na mshitakiwa wa tatu, SP-Ahmed Makele, pamoja na mshitakiwa wa tano, Jane Andrew, Januari 14 mwaka 2006 kwenda Sinza Palestina, ambapo alishuhudia watu wanne wakikamatwa na askari.
Alipoulizwa na Wakili wa Serikali Mugaya Mutaki kwamba watuhumiwa aliowashuhudia ambao walikamatwa siku hiyo ndio waliokamatwa na kuuawa, alikiri kuwa ndio waliouawa, ingawa hakuweka wazi kuwa waliuawa na nani.
“Tarehe hiyo na hao washitakiwa wenzangu tulikwenda katika eneo hilo kufuatilia tukio la ujambazi na wenzangu walishuka mimi nilikuwa na pistol, nilibaki ndani ya gari na baadaye nilishuhudia watuhumiwa wanne waliokamatwa na askari, lakini baadaye nikaja kusikia kuwa wale watu ndio wameuawa,” alidai Koplo Abeneth.
Kwa upande wake, mshitakiwa wa tisa, Michael Shonza, ambaye alitoa utetezi wake juzi na jana, alianza kuhojiwa na Wakili wa Serikali Angaza Mwipopo, alidai mkono wa pongezi aliopewa na Kaimu RPC, Zombe, ndio uliomponza hadi akashitakiwa kwenye kesi hiyo.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya wakili Majura Magafu na mshitakiwa Abeneth:
Wakili: Unafanya kazi wapi?
Abeneth: Kituo cha Polisi Urafiki.
Wakili: Ulijiunga na Polisi lini?
Abeneth: mwaka 1983.
Wakili: Kituo chako cha kwanza kufanyia kazi ni kipi?
Abeneth: Oysterbay hadi mwaka 1996 nikahamishiwa Magomeni na mwaka 2004 nikaamishiwa Urafiki, ambapo nilifanya kazi hadi nahusishwa na kesi hii.
Wakili: Januari 14 mwaka 2006 jioni ulikuwa wapi?
Abeneth: Nilikuwa Polisi Magomeni.
Wakili: Hapo Magomeni ulikwenda kwa shughuli gani?
Abeneth: Tulikwenda pale kupewa maelekezo ya kazi na OCD wa Magomeni, Isunto Mantege.
Wakili: Zoezi la kupangiwa kazi liliisha saa ngapi?
Abeneth: Saa 12 jioni.
Wakili: Wewe ulipangiwa eneo gani la doria?
Abeneth: Nilipangiwa na Jane Andrew, PC Edson, PC Seleman, PC Emmanuel na PC Frolian, tulipangiwa Ubungo Terminal, Mabibo na wote tulikuwa kutoka Idara ya Upelelezi.
Wakili: Hebu tuambie mlitumia usafiri gani kutoka Magomeni kwenda kwenye doria?
Abeneth: Kwanza niliongezewa askari waliovaa sare na natulitumia daladala tofauti, ila mimi na mshitakiwa wa tano tulipanda daladala moja tukashuka kituo cha basi Urafiki, tukaanza kwenda kituoni, kabla hatujafika, Makele alikuwa kwenye gari na askari waliokuwa wamevalia sare za jeshi, wakashuka, akatuambia sisi tupande kwenye lile gari na tuwe makini, kwani kuna tukio la ujambazi limetokea Barabara ya Sam Nujoma, hivyo tulikuwa tunaenda kwenye hilo tukio.
Aliwasha gari na kuingia Barabara ya Morogoro, kisha tukaingia Barabara ya Shekilango, halafu tukafika Mugabe, tukaingia ndani, halafu tukakata kushoto, mbele tukakuta umati wa watu na askari mmoja ambaye alikuwa amevalia sare, alilisimamisha gari letu. Makele na Jane walishuka na kwenda kuzungumza naye, mimi nilibaki ndani ya gari na radio call.
Wakili: Katika kundi lenu la doria nani alikuwa na silaha?
Abeneth: Mimi nilikuwa na pistol na wawili walikuwa wameambiwa waende Urafiki kuchukua silaha.
Wakili: Kwa mara ya kwanza ulijua lini wewe unahusishwa kwenye kesi hii ya mauaji?
Abeneth: Mwanzoni mwa Februari mwaka huo wa 2006, nilipoitwa kwenye Tume ya Jaji Kipenka Mussa kwa ajili ya kuhojiwa.
Wakili: Ujumbe wa wewe kuitwa kwenye tume hiyo uliupata wapi?
Abeneth: Ililetwa summons kituoni Urafiki ikinitaka mimi na Jane twende kwenye Tume ya Kipenka kuhojiwa.
Wakili: Mlikwenda?
Abeneth: Tulikwenda mimi na Jane, ila tulikwenda kwa siku tofauti. (Hata hivyo Jane juzi wakati akitoa ushahidi wake alikana kuitwa na Tume ya Kipenka na kuhojiwa).
Wakili: Uliwahi kuhojiwa kwenye tume iliyoundwa na IGP-Said Mwema iliyokuwa ikiongozwa na ACP-Mgawe?
Abeneth: Sijawahi kuitwa.
Wakili: Mbali na Tume ya Kipenka uliwahi kuandika maelezo sehemu nyingine?
Abeneth: Februari 19 mwaka 2006 niliandika maelezo Kituo cha Polisi Kati nilipokuwa nimekamatwa.
Wakili: Ulihojiwa nini?
Abeneth: Nilitoa maelezo kama ninayoyatoa (leo) jana hapa mahakamani.
Wakili: Wewe unatuhumiwa na kesi ya mauaji, unaomba mahakama ikufanyie nini?
Abeneth: Sikushiriki kukamata wala kuua watu hao na ninaamini mtukufu jaji mahahakama yako itatenda haki.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya wakili wa Serikali Mugaya Mutaki na Abeneth:
Wakili: Baada ya kuandika maelezo yako ulisomewa?
Abeneth: Ndiyo nilisomewa na niliweka saini yangu.
Wakili: Hebu yatambue kama maelezo haya ni yako?
Abeneth: Mmh jina, kabila, shule niliyosoma zipo sahihi, lakini hayo maelezo na hiyo saini si yangu.
Wakili: Kwa hiyo Tume ya Mgawe, Sidney Mkumbi zilikusingizia?
Abeneth: Sijui.
Wakili: Kwanini tukio litokee Barabara ya Sam Nujoma nyie mkakimbilia Barabara ya Shekilango?
Abeneth: (kigugumizi), muulize Afande Makelle (mshitakiwa wa tatu). Afande Makelle alitueleza huenda majambazi wamekimbilia kwenye gereji kubadilisha pleti namba za gari, kwani ni desturi ya wahalifu kubadilisha pleti namba pindi wanapofanya matukio, ili wasikamatwe haraka.
Wakili: Gereji gani hizo?
Abeneth: Tulikagua gereji mbili, moja inaitwa MK na nyingine ni gereji bubu, lakini hata hivyo hatukufanikiwa.
Wakili: Ulisema hukushuka kwenye gari ulipofika eneo la tukio, wakati ni wewe ulikuwa umebeba pistol, sasa kwanini hukushuka? Je, hiyo ndiyo busara ya askari mpelelezi?
Abeneth: (kimya). (Watu wakaangua kicheko). Eeh mtukufu jaji nilibaki kwenye gari na radio call.
Wakili: Unaufahamu msitu wa Pande?
Abeneth: Siufahamu.
Wakili: Kuna ushahidi ulitolewa hapa mahakamani kwamba wewe ni miongoni mwa askari walioenda Pande kwenye tukio la mauaji?
Abeneth: Si kweli.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Wakili wa Serikali Angaza Mwipopo na mshitakiwa wa tisa, Michael Shonza.
Wakili: Juzi katika ushahidi wako ulisemwa ulipewa mkono wa pongezi na mshitakiwa wa kwanza (Zombe), je, hukuona umuhimu wa kuhoji ni kwanini unapongezwa wakati wewe umedai hukushiriki kukamata majambazi siku hiyo?
Shonza: (kimya).
Wakili: Hujawahi kumweleza kiongozi yeyote kuwa wewe hukuhusika na kukamata majambazi siku hiyo na kwamba unashangaa ni kwanini unapongezwa?
Shonza: Nilimweleza Sajenti Nico wakati ananihoji Makao Makuu ya Upelelezi.
Wakili: Pongezi ulizopewa na Zombe zilikuwa ni za nini?
Shonza: Kukamata majambazi.
Wakili: Wewe uliona ni kawaida kupongezwa?
Shonza: Eeh… kwani askari waliopongezwa ni wa Kituo cha Chuo Kikuu ambacho mimi nafanya kazi, hivyo na mimi niliona ni kawaida.
Wakili: Tangu uanze kazi polisi ulishawahi kupongezwa?
Shonza: Awali nilishawahi kupongezwa kwa kukamata silaha.
Wakili: Wewe siku hiyo ya Januari 14 mwaka 2006, ulisema ulikuwa Makongo Juu kwenye doria na wenzio walikuwa Sinza, sasa kwa nini ulikubali kupongezwa wakati hukushiriki kukamata watuhumiwa wa ujambazi?
Shonza: (kimya).
Wakili: Haya maelezo yako yanaonyesha uliyaandika kwenye Tume ya Mgawe, ni yako kweli?
Shonza: Mtukufu jaji, si yangu, licha ya kwamba nilihojiwa na tume hiyo.
Wakili: Iambie mahakama hii jina la ukoo wako ni lipi?
Shonza: (kimya).
Wakili: Tume ya Mgawe na ACP-Isaac Mugasa walikuwa wana sababu gani ya kukusingizia?
Shonza: Kwa sababu mimi ni mtumishi katika Jeshi la Polisi, hivyo ilikuwa rahisi kwao kupata particulars zangu.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Mzee wa Baraza Magreth Mossi na Shonza:
Mzee wa Baraza: Huoni ule mkono wa pongezi ndio umesababisha uingizwe kwenye hii kesi ya mauaji?
Shonza: Huo mkono wa pogezi mtukufu jaji ndio umeniponza hadi leo hii nimesimama kizimbani nikikabiliwa na kesi hii ya mauaji.
Jaji Massati aliahirisha kesi hiyo hadi leo baada ya kukubali ombi la wakili wa mshitakiwa wa 11 na 12 (Rashid Lema na Rajabu Bakari) kuomba kesi hiyo iahirishwe, ili aweze kupata fursa ya kwenda gerezani kumuona Lema.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Februali 19 mwaka 2009

'NILIPONZWA NA ZOMBE

*Aliyesema marehemu waliuawa Pande kutoa ushahidi leo

Na Happiness Katabazi

MSHITAKIWA wa 10 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja, Koplo Abeneth Saro (45), ameiambia mahakama kuwa watuhumiwa aliowashuhudia kuwa walikamatwa Sinza wakiwa hai ndio waliouawa.

Sambamba na hilo, mshitakiwa wa 11, Rashid Lema, ambaye tangu washitakiwa wenzake waanze kujitetea Febuari 3 mwaka huu, hajawahi kuhudhuria mahakamani kutokana na afya yake kuwa si ya kuridhisha, leo anatarajiwa kuanza kutoa ushahidi wake.

Mshitakiwa Lema ndiye aliyeeleza katika maelezo yake kwamba mauaji hayo yalifanyika katika msitu wa Pande.
Akitoa utetezi wake jana, Koplo Abeneth ambaye ni askari kutoka Idara ya Upelelezi, Kituo cha Urafiki, alidai yeye alikuwa ni miongoni mwa askari walioongozana na mshitakiwa wa tatu, SP-Ahmed Makele, pamoja na mshitakiwa wa tano, Jane Andrew, Januari 14 mwaka 2006 kwenda Sinza Palestina, ambapo alishuhudia watu wanne wakikamatwa na askari.
Alipoulizwa na Wakili wa Serikali Mugaya Mutaki kwamba watuhumiwa aliowashuhudia ambao walikamatwa siku hiyo ndio waliokamatwa na kuuawa, alikiri kuwa ndio waliouawa, ingawa hakuweka wazi kuwa waliuawa na nani.
“Tarehe hiyo na hao washitakiwa wenzangu tulikwenda katika eneo hilo kufuatilia tukio la ujambazi na wenzangu walishuka mimi nilikuwa na pistol, nilibaki ndani ya gari na baadaye nilishuhudia watuhumiwa wanne waliokamatwa na askari, lakini baadaye nikaja kusikia kuwa wale watu ndio wameuawa,” alidai Koplo Abeneth.
Kwa upande wake, mshitakiwa wa tisa, Michael Shonza, ambaye alitoa utetezi wake juzi na jana, alianza kuhojiwa na Wakili wa Serikali Angaza Mwipopo, alidai mkono wa pongezi aliopewa na Kaimu RPC, Zombe, ndio uliomponza hadi akashitakiwa kwenye kesi hiyo.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya wakili Majura Magafu na mshitakiwa Abeneth:
Wakili: Unafanya kazi wapi?
Abeneth: Kituo cha Polisi Urafiki.
Wakili: Ulijiunga na Polisi lini?
Abeneth: mwaka 1983.
Wakili: Kituo chako cha kwanza kufanyia kazi ni kipi?
Abeneth: Oysterbay hadi mwaka 1996 nikahamishiwa Magomeni na mwaka 2004 nikaamishiwa Urafiki, ambapo nilifanya kazi hadi nahusishwa na kesi hii.
Wakili: Januari 14 mwaka 2006 jioni ulikuwa wapi?
Abeneth: Nilikuwa Polisi Magomeni.
Wakili: Hapo Magomeni ulikwenda kwa shughuli gani?
Abeneth: Tulikwenda pale kupewa maelekezo ya kazi na OCD wa Magomeni, Isunto Mantege.
Wakili: Zoezi la kupangiwa kazi liliisha saa ngapi?
Abeneth: Saa 12 jioni.
Wakili: Wewe ulipangiwa eneo gani la doria?
Abeneth: Nilipangiwa na Jane Andrew, PC Edson, PC Seleman, PC Emmanuel na PC Frolian, tulipangiwa Ubungo Terminal, Mabibo na wote tulikuwa kutoka Idara ya Upelelezi.
Wakili: Hebu tuambie mlitumia usafiri gani kutoka Magomeni kwenda kwenye doria?
Abeneth: Kwanza niliongezewa askari waliovaa sare na natulitumia daladala tofauti, ila mimi na mshitakiwa wa tano tulipanda daladala moja tukashuka kituo cha basi Urafiki, tukaanza kwenda kituoni, kabla hatujafika, Makele alikuwa kwenye gari na askari waliokuwa wamevalia sare za jeshi, wakashuka, akatuambia sisi tupande kwenye lile gari na tuwe makini, kwani kuna tukio la ujambazi limetokea Barabara ya Sam Nujoma, hivyo tulikuwa tunaenda kwenye hilo tukio.
Aliwasha gari na kuingia Barabara ya Morogoro, kisha tukaingia Barabara ya Shekilango, halafu tukafika Mugabe, tukaingia ndani, halafu tukakata kushoto, mbele tukakuta umati wa watu na askari mmoja ambaye alikuwa amevalia sare, alilisimamisha gari letu. Makele na Jane walishuka na kwenda kuzungumza naye, mimi nilibaki ndani ya gari na radio call.
Wakili: Katika kundi lenu la doria nani alikuwa na silaha?
Abeneth: Mimi nilikuwa na pistol na wawili walikuwa wameambiwa waende Urafiki kuchukua silaha.
Wakili: Kwa mara ya kwanza ulijua lini wewe unahusishwa kwenye kesi hii ya mauaji?
Abeneth: Mwanzoni mwa Februari mwaka huo wa 2006, nilipoitwa kwenye Tume ya Jaji Kipenka Mussa kwa ajili ya kuhojiwa.
Wakili: Ujumbe wa wewe kuitwa kwenye tume hiyo uliupata wapi?
Abeneth: Ililetwa summons kituoni Urafiki ikinitaka mimi na Jane twende kwenye Tume ya Kipenka kuhojiwa.
Wakili: Mlikwenda?
Abeneth: Tulikwenda mimi na Jane, ila tulikwenda kwa siku tofauti. (Hata hivyo Jane juzi wakati akitoa ushahidi wake alikana kuitwa na Tume ya Kipenka na kuhojiwa).
Wakili: Uliwahi kuhojiwa kwenye tume iliyoundwa na IGP-Said Mwema iliyokuwa ikiongozwa na ACP-Mgawe?
Abeneth: Sijawahi kuitwa.
Wakili: Mbali na Tume ya Kipenka uliwahi kuandika maelezo sehemu nyingine?
Abeneth: Februari 19 mwaka 2006 niliandika maelezo Kituo cha Polisi Kati nilipokuwa nimekamatwa.
Wakili: Ulihojiwa nini?
Abeneth: Nilitoa maelezo kama ninayoyatoa (leo) jana hapa mahakamani.
Wakili: Wewe unatuhumiwa na kesi ya mauaji, unaomba mahakama ikufanyie nini?
Abeneth: Sikushiriki kukamata wala kuua watu hao na ninaamini mtukufu jaji mahahakama yako itatenda haki.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya wakili wa Serikali Mugaya Mutaki na Abeneth:
Wakili: Baada ya kuandika maelezo yako ulisomewa?
Abeneth: Ndiyo nilisomewa na niliweka saini yangu.
Wakili: Hebu yatambue kama maelezo haya ni yako?
Abeneth: Mmh jina, kabila, shule niliyosoma zipo sahihi, lakini hayo maelezo na hiyo saini si yangu.
Wakili: Kwa hiyo Tume ya Mgawe, Sidney Mkumbi zilikusingizia?
Abeneth: Sijui.
Wakili: Kwanini tukio litokee Barabara ya Sam Nujoma nyie mkakimbilia Barabara ya Shekilango?
Abeneth: (kigugumizi), muulize Afande Makelle (mshitakiwa wa tatu). Afande Makelle alitueleza huenda majambazi wamekimbilia kwenye gereji kubadilisha pleti namba za gari, kwani ni desturi ya wahalifu kubadilisha pleti namba pindi wanapofanya matukio, ili wasikamatwe haraka.
Wakili: Gereji gani hizo?
Abeneth: Tulikagua gereji mbili, moja inaitwa MK na nyingine ni gereji bubu, lakini hata hivyo hatukufanikiwa.
Wakili: Ulisema hukushuka kwenye gari ulipofika eneo la tukio, wakati ni wewe ulikuwa umebeba pistol, sasa kwanini hukushuka? Je, hiyo ndiyo busara ya askari mpelelezi?
Abeneth: (kimya). (Watu wakaangua kicheko). Eeh mtukufu jaji nilibaki kwenye gari na radio call.
Wakili: Unaufahamu msitu wa Pande?
Abeneth: Siufahamu.
Wakili: Kuna ushahidi ulitolewa hapa mahakamani kwamba wewe ni miongoni mwa askari walioenda Pande kwenye tukio la mauaji?
Abeneth: Si kweli.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Wakili wa Serikali Angaza Mwipopo na mshitakiwa wa tisa, Michael Shonza.
Wakili: Juzi katika ushahidi wako ulisemwa ulipewa mkono wa pongezi na mshitakiwa wa kwanza (Zombe), je, hukuona umuhimu wa kuhoji ni kwanini unapongezwa wakati wewe umedai hukushiriki kukamata majambazi siku hiyo?
Shonza: (kimya).
Wakili: Hujawahi kumweleza kiongozi yeyote kuwa wewe hukuhusika na kukamata majambazi siku hiyo na kwamba unashangaa ni kwanini unapongezwa?
Shonza: Nilimweleza Sajenti Nico wakati ananihoji Makao Makuu ya Upelelezi.
Wakili: Pongezi ulizopewa na Zombe zilikuwa ni za nini?
Shonza: Kukamata majambazi.
Wakili: Wewe uliona ni kawaida kupongezwa?
Shonza: Eeh… kwani askari waliopongezwa ni wa Kituo cha Chuo Kikuu ambacho mimi nafanya kazi, hivyo na mimi niliona ni kawaida.
Wakili: Tangu uanze kazi polisi ulishawahi kupongezwa?
Shonza: Awali nilishawahi kupongezwa kwa kukamata silaha.
Wakili: Wewe siku hiyo ya Januari 14 mwaka 2006, ulisema ulikuwa Makongo Juu kwenye doria na wenzio walikuwa Sinza, sasa kwa nini ulikubali kupongezwa wakati hukushiriki kukamata watuhumiwa wa ujambazi?
Shonza: (kimya).
Wakili: Haya maelezo yako yanaonyesha uliyaandika kwenye Tume ya Mgawe, ni yako kweli?
Shonza: Mtukufu jaji, si yangu, licha ya kwamba nilihojiwa na tume hiyo.
Wakili: Iambie mahakama hii jina la ukoo wako ni lipi?
Shonza: (kimya).
Wakili: Tume ya Mgawe na ACP-Isaac Mugasa walikuwa wana sababu gani ya kukusingizia?
Shonza: Kwa sababu mimi ni mtumishi katika Jeshi la Polisi, hivyo ilikuwa rahisi kwao kupata particulars zangu.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Mzee wa Baraza Magreth Mossi na Shonza:
Mzee wa Baraza: Huoni ule mkono wa pongezi ndio umesababisha uingizwe kwenye hii kesi ya mauaji?
Shonza: Huo mkono wa pogezi mtukufu jaji ndio umeniponza hadi leo hii nimesimama kizimbani nikikabiliwa na kesi hii ya mauaji.
Jaji Massati aliahirisha kesi hiyo hadi leo baada ya kukubali ombi la wakili wa mshitakiwa wa 11 na 12 (Rashid Lema na Rajabu Bakari) kuomba kesi hiyo iahirishwe, ili aweze kupata fursa ya kwenda gerezani kumuona Lema.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Februali 19 mwaka 2009

'ZOMBE ALITUPONGEZA KWA KAZI'

*Watuhumiwa wadai hawakujua kwa nini wanapongezwa

Na Happiness Katabazi

WASHTAKIWA wawili katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja wamedai mahakamani kuwa walishangazwa na kitendo cha kupewa mkono wa pongezi kwa kazi nzuri waliyofanya na aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Abdallah Zombe.


Washtakiwa hao, Emmanuel Mabula (49) na Michael Shonza (45), walidai zaidi hawakujua pongezi hizo zilikuwa za kazi gani.

Wote wawili walikuwa wakifanyakazi Kituo cha Polisi, Chuo Kikuu, cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani.
Mbali na washtakiwa hao, mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo, Jane Andrew (31), wa kituo cha Urafiki, naye alitoa ushahidi wake mahakamani hapo jana mbele ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Massati.
Kwa upande wa Mabula na Shonza, wamedai mahakamani hapo kwamba Januari 15, 2006 walipelekwa na mkuu wa kituo chao cha kazi, Sebastian Masinde, ofisini kwa Zombe; walipofika Zombe aliwapa mkono wa pongezi kwa kazi nzuri waliyokuwa wameifanya.
Katika maelezo yao ya ushahidi, walidai kuwa siku hiyo walishangazwa na kitendo cha wao kupewa mkono wa pongezi kwa sababu hawakuwa wamejua wamefanya kazi gani hata kustahili kupelekwa kwa RPC ili kupongezwa.
“Mtukufu Jaji ni kweli siku hiyo tulipewa mkono wa pongezi na Zombe kwa maelezo kwamba tulifanya kazi nzuri lakini hata hivyo nilishangaa ni kazi ipi nzuri niliyofanya hadi nipewe pongezi,” alidai Mabula.
Kwa upande wake Jane Andrew yeye amedai kwamba hakwenda kupongezwa. Lakini hata hivyo baadhi ya mashahidi wa upande wa mashtaka walidai kuwa siku ya tukio (Januari 14 , 2006), walimshuhudia Jane akigombea mfuko wa fedha za marehemu; hata hivyo alikana tuhuma zote zilizoelekezwa kwake.
Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili Majura Magafu, Jane alikana kuandika maelezo katika Tume ya ACP Mgawe na Tume ya Jaji Kipenka Mussa, licha ya Wakili wa Serikali, Jasson Kaishozi, kumuonyesha maelezo yake aliyoyaandika katika nyaraka za tume hizo kwa nyakati tofauti kabla hajafikishwa mahakamani.
“Mtukufu Jaji hizo ‘statement’ toka Tume ya Mgawe na Jaji Kipenka sizijui, nashangaa wakili huyu ananing’angania kwamba niliziandika mimi. Nimesema siyo zangu…mimi nilihojiwa kwenye tume moja tu ya shahidi wa 36, Sidyen Mkumbi.
“Hivyo hizo statement sijui kabisa na wala usinipe nizisome kwani siyo zangu. Na hili tukio la mauji ambalo limesababisha nishtakiwe kwenye kesi hii mimi silijui na ninaomba mahakama hii itende haki,” alidai mshtakiwa huyo.
Hata hivyo, wakili Kaishozi alimhoji kwamba awali alipoanza kutoa ushahidi wake alidai aliandika maelezo kwenye tume moja ya Mkumbi lakini baadaye akasema alipata taarifa za tukio la mauji ya watu hao alipoitwa kwenye Tume ya Kipenka. Baada ya kuulizwa swali hilo mshtakiwa alijibu kwa sauti ya juu, “Mtukufu Jaji nimeishamweleza huyu wakili wa serikali kuwa mimi nilihojiwa kwenye tume moja tu hivyo hizo statement anazodai zina melezo yangu siyo zangu,” alidai Jane kwa ukali.
Jane aliendelea kudai mahakamani kuwa alisoma na kuishia kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Sangu-Mbeya na aliijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 2000 kwa sababu alikuwa na sifa ya kuwa mwanamichezo.
Ifuatayo ni mahojiano kati ya wakili Majura Magafu na mshtakiwa wa saba, Emmanuel Mabula.

Wakili: Uliajiriwa na Jeshi la Polisi lini?

Mabula: Mwaka 1982 na mwaka 1987 nikahamishiwa Kituo cha Polisi Urafiki hadi matatizo haya yananikumba.

Wakili: Januria 14 mwaka 2006 ulikuwa wapi?

Mabula: Kuanzia asubuhi nilikuwa nyumbani hadi saa 12 kasorobo jioni.

Wakili: Ulipofika muda huo ulielekea wapi?

Mabula:Nilivaa sare za kazi nikaelekea ofisini.

Wakili: Ulipofika kituoni nini kilitokea?

Mabula: Nilimkuta na Mkuu wa Upelelezi wa kituo hicho, Station Sajenti James Masota, ambaye aliitisha foleni na alitoa maelekezo kwamba tupande Pick Up rangi ya bluu.

Wakili: Unakumbuka idadi ya askari uliokuwa nao kwenye hilo gari?

Mabula: Nane.
Wakili: Majina yao unayakumbuka?

Mabula: Naweza kuyakumbuka. DC. James Masota; mshtakiwa wa nne, sita na nane (PC Noel Felix na Koplo Moris Nyangerela) ambao wameachiwa huru; na Koplo Festus, PC Michael Shonza na mimi.

Wakili: James aliwaelekeza muelekee wapi?

Mabula: Gari liliwashwa tukaelekea Changanyikeni halafu likaelekea Makongo juu na James alikuwa amekaa mbele akatoa shingo na kusema yeye na Michael watelemke ambapo Michael Shona alikuwa na bunduki.

Wakili: Kuna maelekezo mengine aliyatoa?

Mabula: Alituambia sisi eneo letu la doria ni Makongo na hayo maelekezo alitupea pale pale Makongo.

Wakili: Mlifanya doria hadi saa ngapi?

Mabula: Saa 11 alfajiri tukaanza safari ya kurudi ofisini na tulifika saa 12 asubuhi.

Wakili: Katika eneo lenu la doria hakukutokea tukio lolote?

Mabula: Hakukutokea tukio lolote.

Wakili: Mlipofika kituoni mliona nini?

Mabula: Michael Shonza alirudisha bunduki lakini hata hivyo haikuwa imetumika.

Wakili: Baada ya kurudisha bunduki nini kilifuata?

Mabula: Mimi na Michael tulirudi majumbani kwetu kupumzika.

Wakili: Hili tukio la Sinza ambalo limetufikisha mahakamani hapa ulilifahamu lini?

Mabula: Nililisikia kwa aliyekuwa mshtakiwa wa nane ambaye ameachiliwa huru Felix, Januari 15 mwaka huo.
Aliniambia naitwa kwa Mkuu wa Kituo chetu, SSP Masinde na niliitikia wito na kwenda.

Wakili: Ulipofika Masinde alikuambia kitu gani?

Mabula: Akatuambia askari wote tuliokuwa kwenye doria jana yake tupande kwenye Pick Up; na kwenye hilo gari kulikuwa na askari wengine ambao niliwataja kwa majina awali pamoja na mimi isipokuwa James.

Wakili: Baada ya kupanda gari mlielekea wapi?

Mabula: Mi sikujua tunaelekea wapi ila tulipofika Ubungo niliwauliza askari wenzangu tunaenda wapi? Ndipo mshtakiwa wa sita Koplo Morris Nyangerela ambaye ameachiwa huru alisema Mkuu wa Kituo chetu ameagiza tupelekwe ofisini kwa kaimu RPC-Zombe.

Wakili: Uliwahi kuhoji kwa RPC mlikuwa mnaenda kufanya nini?

Mabula: Nilimuuliza Nyangerela akasema mkuu wa kituo anasema jana yake tulikuwa tumekamata majambazi.

Wakili: Mlipofika kwa RPC mkaambiwa nini?

Mabula: Nilikuta maofisa wa mkoa lakini niliyemtambua ni OCD wa Kinondoni, Maro.

Wakili: Wakati huo Kaimu RPC alikuwa Zombe alikuwepo ofisini mlivyoenda?

Mabula: Alikuwepo.

Wakili: Kilizungumzwa nini?

Mabula: Nilimsikia Zombe akituambia vijana mmefika njooni niwape mkono wa pongezi.

Wakili: Mbali ya kusema njooni niwape mkono wa pongezi alisema nini?

Mabula: Mbali na hilo sikumbuki alisema nini tena kwani nilikuwa na usingizi kwa vile jana yake nilikuwa nimekesha kwenye doria.

Wakili: Nini kilifuata?

Mabula: Tulitolewa nje na kurudishwa Kituo cha Chuo Kikuu.

Wakili: Hapo awali wakati umenza kutoa ushahidi ulidai kwamba Nyangerela alikwambia jana yake walikamata majambazi wanne , waliwakamatia eneo gani?

Mabula: Sinza.

Wakili: Nyangerela hakuwahi kuwaambia kama kulikuwa na mapambano ya silaha na watu hao?

Mabula: Hakuwahi kuniambia.

Wakili:Suala la mauji ya watu hawa ulianza kulijua lini?

Mabula:Nililijua kupitia Redio Free kwa sababu magazeti yalikuwa yakisomwa kwamba polisi wapambana na majambazi.

Wakili: Ni lini ulikuja kufahamu wewe unahusishwa na mauji haya?

Mabula: Mwishoni mwa Januari mwaka 2006, nikiwa katika mahakama ya Kawe nilipata ujumbe toka kwa Inspekta Omary kwamba natakiwa Makao Makuu ya Upelelezi.

Wakili: Je, ulitekeleza wito huo?

Mabula: Nilikwenda Makao Makuu ya upelelezi saa tano asubuhi na nilikutana na afande Omar mwenyewe akachukua maelezo yangu ya jinsi tulivyowakamata wale watu.

Wakili: Alikwambia nini?

Mabula: Aliniambia askari wote wa UDSM waliokuwa doria siku ya Jumamosi ya Januari 14 mwaka huo wameandika maelezo isipokuwa mimi.

Wakili: Nani aliandika maelezo yako?

Mabula: Inspekta Omar na nilimweleza mimi sitambui mauji ya watu hao.

Wakili: Baada ya kumwambia wewe hutambua mauji hayo, nini kiliendelea?

Mabula: Aliniambia kama sitambui , siku hiyo nilipangiwa wapi, nikamweleza Makongo Juu.

Wakili: Mahakama ilielezwa kwamba IGP-Said Mwema aliunda Tume chini ya ACP Mgawe, pia kulikuwa na tume ya Mkumbi na ya Jaji Kipenka, ulishawahi kuhojiwa katika tume hizo?

Mabula: Mi nafikiri maelezo niliyotoa kwa Inspekta Omar ndiyo tume ya Mgawe na tume hizo nyingine zote nilihojiwa na kutoa maelezo yangu.

Wakili: Katika tume hizo, waliokuhoji waliwahi kukuambia kwa nini wanataka kuandika maelezo yako?

Mabula: Waliniambia wanataka maelezo yangu wapeleke mahakamani.

Wakili: Unapafahamu msitu wa Pande, Bunju na Sinza Ukuta wa Posta?

Mabula: Kwa mara ya kwanza nimepafahamu wakati mahakama hii ilipotembelea huko. Na ninaomba mahakama hii inihukumu kutokana na ushahidi uliotolewa.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya wakili wa Serikali Alexender Mzikila na Mabula;

Wakili: Ni kwa nini hukuhoji ulipopewa mkono wa pongezi?

Mabula: Sikuuliza kwani kijeshi askari mdogo ni mwiko kumhoji askari aliyekuzidi cheo kwa sababu unaweza kufukuzwa kazi na unapoambiwa jambo na mkubwa wako hakuna kusema hapana.

Wakili: Kwa nini ulishindwa kumuuliza ni kazi gani mlifanya hadi mpongezwe?

Mabula: Ni kosa la jinai kumhoji afande.

Wakili: Hebu angalia maelezo yako uliyoyaandikwa kwenye tume ya Mama Mkumbi, ni yako kweli?

Mabula:Mmh kuna baadhi ya maelezo ni yangu mengine siyo yangu.

Wakili: Vipi maelezo haya uliyoyaandika kwenye tume ya ACP Mgawe?

Wakili: Jaji mimi nilihojiwa na Inspekta Omar lakini leo naona maelezo haya yamesainiwa na SSP Mayala na hata saini hii siyo yangu.

Wakili: Ushahidi wako uliotoa leo unatofautiana na ushahidi ulioutoa kwenye tume hizo tatu?

Mabula: Ndiyo.

Wakili: Lakini kwa mujibu wa maelezo uliyoandika kwa inspekta Omar yanaonyesha wewe ulikuwa miongoni mwa askari walikuwepo kwenye eneo la mapambano na kwamba ulisikia milio ya risasi?

Mabula: Nimekwambia Omar alinihoji na Mkumbi alinihoji lakini hiyo statement nyingine ya Mkumbi imesainiwa na mtu mwingine ambaye hakunihoji kabisa na wala simfahamu.

Wakili: Kuna ushahidi ulitolewa wewe ulikamata washtakiwa na ulifika pande ambapo mauji yalifanyika, unasemaje?

Mabula: Sipajui Pande.

Ifuatayo ni mahojiano kati ya Mzee wa Baraza, Magreth Mossi na Mabula:

Wakili: Ni mara ya ngapi kupewa mkono wa pongezi na viongozi wako?

Mabula: Siku hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kupewa mkono wa pongezi.

Wakili: Wewe ukishangaa ni kwa nini?

Mabula: Hata mimi nilishangaa.

Hata hivyo mshtakiwa wa tisa, Shonza ushahidi wake umefanana na Mabula ambapo alimaliza kutoa ushahidi wake na Jaji Massati akaahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo upande wa serikali utaanza kumuuliza maswali.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano ,Februali 18 mwaka 2009

DC MNALI NI ZAO LA KIKWETE

Na Happiness Katabazi

MWISHONI mwa wiki iliyopita, Rais Jakaya Kikwete, alimfukuza kazi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Vijijini (DC), Albert Mnali, kwa kitendo chake cha kuwacharaza bakora walimu, kwa madai kuwa wameshusha kiwango cha elimu katika wilaya yake.


Taarifa ya Ikulu ilieleza kuwa serikali imepokea kwa masikitiko makubwa kitendo hicho cha udhalilishaji wa walimu na kwamba DC huyo amekiuka kanunu za utumishi wa umma.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo Rais Kikwete imetokana na uchunguzi wa kina uliofanywa na kuthibitishwa na Mnali mwenyewe kwamba alifanya hivyo kutokana na uchungu alionao katika suala la elimu.

Taarifa hiyo ilisema kuwa mtumishi yeyote ana haki zake za msingi na kamwe hawezi kufikia hatua ya kudhalilishwa kwa kupigwa kama njia ya kusisitiza uwajibikaji wake kazini.

Wakati taarifa ya Ikulu ikieleza hivyo, mimi napenda kutumia fursa hii kumpongeza Kanali mstaafu, Albert Mnali, kwani ameonyesha uungwana na ushujaa wa hali ya juu kwa kitendo chake cha kukubali hadharani kwamba ni kweli aliamuru walimu wale wacharazwe bakora kutokana na uchungu alionao katika suala la elimu.

Nimelazimika kumpongeza katika eneo hilo la kukiri ukweli ambao umeokoa mamilioni ya fedha za walipa kodi ambayo endapo DC huyo angekana tuhuma hizo, yangetumika kuunda tume kama tulivyozoeshwa na Serikali ya Awamu ya Nne ambayo bila shaka ingechunguza tuhuma hizo. Nampongeza sana kwa ujasiri wake wa kukubali ukweli ambao umesababisha kuvuliwa madaraka.

Nampongeza pia Rais Kikwete kwa uamuzi wa kumtimua kazi Mnali. Kwani ni dhahiri kitendo kilichofanywa naye kimeivunjia heshima Tanzania ambayo inajinasibu kila kukicha kwamba ina viongozi wanaojua wanachokifanya.

Ifahamike kwamba mkuu huyu wa wilaya hakuwa bosi wa wale walimu alioamuru wacharazwe bakora. DC huyu mamlaka yake ni ya kisiasa tu ya Wilaya ya Bukoba Vijijini aliyokuwa akiiongoza. Mamlaka yake hayana uhusiano na wala hayashabihiani na kazi za watendaji na kitaalamu.

Pia mkuu huyu wa wilaya ameonyesha hajui kanuni za adhabu kwa watumishi wa umma, kwa sababu hiyo alikuwa hajui nani anawajibika kwa nani kwani kanuni ya adhabu inatoa adhabu kwa mtu aliyekosea.

Kwa kitendo hicho cha kuamuru walimu wacharazwe bakora, nitakuwa sijakosea nikisema Mnali ni ‘kadikteta ka kijijini ambako kanafikiri’ mtu akikosea bakora ndiyo funzo!

Hatua ya Rais Kikwete kumtimua Mnali ni ya kupongeza, lakini tujiulize, rais wetu alimpata wapi mtu wa aina hii? Kwa sababu watu wa aina hii wanatoa picha ya rais tuliye naye.
Mkuu wa wilaya anamwakilisha rais wa nchi katika wilaya anayoingoza.

Hii inatutisha kidogo na kutufanya tuanze kuamini yale maneno yasomekayo hivi: “Rais Kikwete anaongoza serikali kishikaji.” Maneno haya yalibandikwa kwenye mabango na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka jana wakati walipogoma kuingia madarasani
Kumfukuza tu mkuu huyu wa wilaya haitoshi, pia anatakiwa achukuliwe hatua zaidi kwani amewajeruhi walimu hao na kuwasababishia maumivu makali katika sehemu zao za mwili.

Pia nilitegemea wazazi wajitokeze wawatetee walimu, lakini hawajajitokeza hadi leo. Hili linaonyesha kuwa nchi yetu bado inahitaji elimu ya uraia na si tu itolewe kwa wananchi bali kwa viongozi wetu pia.

Namshauri rais wetu kwamba awe anaangalia watu wanaofaa kuteuliwa kuwa viongozi. Hatutaki kuanza kumtilia wasiwasi rais wetu kwa sababu huchaguliwa na wananchi lakini hatujawaona wananchi wakijitokeza kumuunga mkono kwa hatua aliyochukua dhidi ya udhalilishwaji wa walimu hawa.

Hata hivyo tusiishie kunyosheana vidole, tunapaswa kutambua kuwa jamii nzima ina matatizo kwani katika masuala ya msingi hatuna mshikamano wa kweli; kwa mfano wanafunzi wa vyuo vikuu wamefukuzwa vyuoni kwa sababu ya kupinga sheria ya uchangiaji, lakini wazazi ambao wengine huumia kutoa hizo karo hawajajitokeza kuwaunga mkono wanafunzi hao!

Nihitimishe kwa kusisitiza kuwa jamii nzima ina matatizo; yatupasa kubadilike na pale kwenye madai ya msingi ambayo yana masilahi kwa taifa wanachi walio wengi tuwe na mshikamano.

Hata hivyo, tunapaswa kujiuliza wepesi huu wa Rais Kikwete kumtimua kazi DC ulitoka wapi?
Ni kwa nini wepesi huu ulishindwa kumjia siku chache zilizopita wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipovunja Katiba aliyoapa kuilinda kwa kusema atakayekutwa ameua albino naye auwawe?

Je, amemfukuza haraka mkuu huyu wa wilaya kwa sababu walimu wa Bukoba walisema watagoma na wangeliandamana au alitoa uamuzi huo kwa sababu tunakaribia kuingia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo walimu ndiyo wasimamizi wa uchaguzi huo?
Natoa hoja.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano ,Februali 18 mwaka 2009

MAKELE:ZOMBE AMENIPONZA

*Amshangaa kumsingiza, adai hana ugomvi naye
*Akana kupambana na majambazi waliouawa

Na Happiness Katabazi

MSHITAKIWA wa tatu katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja, aliyekuwa Mkuu wa Polisi Kituo cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP), Ahmed Makele (45), amedai mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Abdallah Zombe, ndiye aliyembambikia kesi hiyo ya mauaji.
Sambamba na hilo, hali ilikuwa tofauti kwa Zombe ambaye jana tangu aingie mahakamani muda mwingi alionekana kuwa kimya, tofauti na siku za nyuma ambapo alikuwa akionekana mtu mwenye furaha na kuzungumza na watu.
Makele ambaye jana alikuwa akihojiwa na mawakili wa serikali na mawakili wa utetezi, alieleza hayo alipokuwa akijibu swali la wakili wa mshitakiwa wa kwanza, Jerome Msemwa, ambalo alimuuliza kama anakubaliana na maelezo ya Zombe aliyoyatoa kwenye Tume ya Jaji Kipenka Mussa.
Kwa mujibu wa maelezo ya Zombe katika tume hiyo, Makele alikuwa ni miongoni mwa askari waliopambana na watu wanne walioshukiwa na polisi kuwa ni majambazi.
“Maelezo ya Zombe kwenye tume hiyo ni ya uongo na Zombe ndiye amenibambikia kesi hii. Na mtukufu jaji, huyu Zombe ameniletea mzigo mbaya mimi,” alidai Makele.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Wakili Msemwa na Makele:
Wakili: Zombe katika ushahidi wake alidai wewe ni miongoni mwa washitakiwa waliomwandikia barua DPP. Unasemaje kuhusu hilo?
Makele: Si kweli.
Wakili: Unafahamu kwamba ikibainika mahabusu akiandika barua bila kupitia kwa mkuu wa gereza adhabu yake ni kifungo cha miezi sita, faini au vyote kwa pamoja?
Makele: Nimekwambia sijawahi kuandika barua.
Wakili: Ukiwa gerezani hujawahi kukutwa na simu ya mkononi?
Makele: Sijawahi.
Wakili: Wakati upo gereza la Ukonga ulikuwa unaishi eneo gani na je, sehemu hiyo ilikuwa na mahali pa kuchaji simu?
Makele: Nilikuwa nakaa selo hakuna pakuchaji simu.
Wakili: Ukiwa gerezani hujawahi kukamatwa na simu yenye vocha yenye thamani ya sh 135,000?
Makele: Iwe na vocha, haina vocha sijawahi kukamatwa nayo.
Wakili: Kwenye simu hiyo hujawahi kuingiziwa vocha yenye thamani ya sh 200,000?
Makele: Sijawahi.
Wakili: Unamfahamu Andrew Nyiti?
Makele: Namfahamu.
Wakili: Unamfahamu vipi?
Makele: Nilikuwa shahidi katika kesi ya kughushi aliyoishitaki Kampuni ya Tanzania Afgem, katika mahakama hii na ilikuwa mbele ya Jaji Agustino Shangwa.
Wakili: Kwenye kesi hiyo wakili Hurbet Nyange ambaye ndiye wakili wa gazeti la Tanzania Daima alikuwepo?
Makele: Ndiyo.
Wakili: Maelezo ya Zombe aliyoyatoa kwenye Tume ya Kipenka unasemaje?
Makele: Maelezo yake ni ya uongo na yamesababisha Tume ya Kipenka kuniona mimi ni muuaji. Huyu Zombe ndiye kanibambikia kesi na amenibebesha mzigo mbaya. Amenishangaza sana anavyodai kwamba mimi nilikuwa miongoni mwa askari waliopambana na majambazi siku hiyo. (Watu wakaangua kicheko).
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Wakili wa Serikali Mugaya Mutaki na Makele:
Wakili: Januari 16 mwaka 2006 ulipata taarifa saa ngapi za tukio la uporaji katika duka la BIDCO?
Makele: Saa 12 jioni ya siku hiyo.
Wakili: Co sign yako ilikuwa ni ngapi?
Makele: 158.
Wakili: Ijumaa wakati ukitoa ushahidi wako ulisema siku hiyo uliondoka Kituo cha Polisi Urafiki na askari wawili, ni kina nani hao?
Makele: Ni mshitakiwa wa 10, Koplo Abeneth na mshitakiwa wa tano, Jane Andrew.
Wakili: Gari ulilotumia kwenda nalo kwenye tukio lilikuwa ni mali ya Jeshi la Polisi?
Makele: Ilikuwa ni mali yangu.
Wakili: Ilikuwa na namba gani ya usajili?
Makele: Sikumbuki.
Wakili: Je, siku hiyo ulikuwa unakwenda kwenye tukio, ulikwenda na silaha yoyote?
Makele: Siku zote nilikuwa nabeba bastola.
Wakili: Hao askari uliowabeba walikuwa na silaha?
Makele: Ndiyo.
Wakili: Mlivyotoka Kituo cha Urafiki mlielekea wapi?
Makele: Tuliingia Barabara ya Morogoro kisha tukaingia Barabara ya Shekilango tukafika Shule ya Mugabe tukaingia kwenye barabara ya vumbi kuingia kushoto.
Wakili: Mlivyofika hapo kushoto mlienda wapi?
Makele: Tuliiipita mitaa miwili mbele kidogo tukakuta umati wa watu nikausogelea. Nikasimamishwa na askari aliyekuwa amevalia sare za polisi, Koplo Nyangerela, ambaye ameachiwa huru, akanieleza watu wanne wamekamatwa na akanieleza yeye anaendelea kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.
Wakili: Hao watuhumiwa walivyokamatwa walipakizwa kwenye gari gani?
Makele: Pick Up na wote walikuwa hai na niliwaelekeza askari hao wa Chuo Kikuu ambao ndio waliwakamatwa watuhumiwa hao wawapeleke kwenye kituo chao, kwani ndiyo kituo husika ambapo tukio limetokea.
Wakili: Katika tukio hilo kulikuwa na skari mwenye cheo cha juu kuliko wewe?
Makele: Sijui, kwani nilimuona Koplo Nyangerela, siku hiyo alikuwa na askari wengine walikuwa wamevalia nguo za kiraia.
Wakili: Na hii gari ya Pick Up iliyobeba watuhumiwa uliitambua ni ya wapi?
Makele: Ni ya Kituo cha Polisi Chuo Kikuu na niliitambua kwa sababu ina namba SU na mara kwa mara ilikuwa ikitumiwa na Mkuu wa Kituo cha Chuo Kikuu, Masinde.
Wakili: Mbali na watuhumiwa kupakiwa kwenye hilo gari, ulibahatika kuona vielelezo vingine?
Makele: Niliona begi ambalo askari mmoja wa Chuo Kikuu alikuwa akitaka kumkabidhi Jane Andrew, nikamkatalia.
Wakili: Wewe ulibaini begi hilo lilikuwa na nini ndani yake?
Makele: Sikuweza kubaini.
Wakili: Hukupewa fedha wewe wala bastola na askari wa Chuo Kikuu?
Makele: Sikukabidhiwa chochote.
Wakili: Hao watuhumiwa uliwashuhudia walikamatwa wakiwa hai, walikuwa wangapi?
Makele: Wanne.
Mawakili: Hao watuhumiwa kabla ya kukamatwa na polisi walikuwa na gari gani?
Makele: Gari aina ya Saloon lenye rangi ya light blue na niliikuta eneo la tukio pale Sinza Palestina.
Wakili: Askari walivyowabeba hao watuhumiwa kwenye gari la polisi, gari la watuhumiwa liliendeshwa na nani?
Makele: Koplo Nyangerela.
Wakili: Nani alikuwa akiendesha Pick Up ya Chuo Kikuu ambayo ilibeba watuhumiwa?
Makele: PC Noel ambaye naye ulimuachia huru wiki iliyopita.
Wakili: Wewe ulikwenda eneo la tukio na kushuhudia mapambano ya risasi?
Makele: Hapana sikwenda na sikuona mapambano ya risasi.
Wakili: Kwa hiyo unataka kuiambia mahakama hii kwamba uliwaona watuhumiwa walivyokamatwa waliondoka eneo la tukio wakiwa salama?
Makele: Ndiyo, waliondoka wakiwa salama.
Wakili: Naomba usome kwa sauti kielelezo D10 ambacho kimeishapokelewa na mahakama hii?
Makele: Haya ni maelezo ya Abdallah Zombe aliyoyatoa kwenye Tume ya Jaji Mussa ambayo anadai kwamba yeye alisikia tukio la mauaji kwenye redial call, Makele alisema alikuwa ni miongoni mwa askari waliopambana na majambazi na wakafanikiwa kukamata sh milioni tano na bastola.
Wakili: Je, hayo maelezo ya Zombe uliyoyasoma ni sahihi?
Makele: Mtukufu jaji hayo maelezo anayajua aliyeyaandika (Zombe).
Wakili: Kama unayakana maelezo hayo ya Zombe inamaana alikusingizia?
Makele: Sana tena, ndiyo maana nipo jela na sijui ni kwanini aliamua kuandika hivyo wakati mimi sina ugomvi naye.
Wakili: Wewe unakataa hayo maelezo ukuyasema kwenye redial call?
Makele: Ijumaa iliyopita wakati nikitoa ushahidi wangu nilisema habari za tukio la BIDCO nilizipata kupitia Control Room.
Wakili: Kituo cha Urafiki kipo kwenye wilaya gani ya kipolisi?
Makele: Magomeni?
Wakili: Kituo cha Chuo Kikuu kipo chini ya wilaya gani ya kipolisi?
Makele: Kinondoni.
Wakili: Eneo walilokamatiwa watuhumiwa lilikuwa wilaya gani?
Makele: Kinondoni.
Wakili: Katika ushahidi wako wa juzi ulisema vielelezo kama fedha na bastola vilipelekwa Urafiki, watuhumiwa kadiri ya maelezo yako ulisema walipelekwa Chuo Kikuu, sasa kwa nini hivyo vielelezo visingepelekwa Chuo Kikuu badala yake vikapelekwa Urafiki, hebu iweke wazi mahakama.
Makele: Sijui ni kwanini.
Wakili: Tukio la uporaji katika duka la BIDCO ulilishuhudia?
Makele: Hapana.
Wakili: Lile gari la watuhumiwa lililetwa siku hiyo ya Januari 14 mwaka 2006 Kituo cha Urafiki?
Makele: Hapana, lililetwa kesho yake.
Wakili: Nisaidie ni kwa nini tukio hili lilitokea wilaya ya kipolisi Kinondoni na kwa nini likaletwa wilaya ya kipolisi Magomeni?
Makele: Sijui na hata hivyo jalada la tukio hilo halikufunguliwa Kituo cha Urafiki.
Wakili: Je, mshitakiwa wa kwanza (Zombe) alifika Urafiki siku hiyo?
Makele: Ndiyo alifika saa mbili usiku.
Wakili: Mshitakiwa wa pili (Christopher Bageni) naye siku hiyo alifika kituoni na alifika kwa sababu gani?
Makele: Ndiyo alifika, kwani alifuata vielelezo na awali alikuwa akikataa kupokea vielelezo hivyo.
Wakili: Unafikiri ni kwanini Bageni alikuwa anakataa kupokea?
Makele: Kwa sababu OCD wake Maro, alimwambia fedha ni sh milioni 5, lakini OCD wa Magomeni, Isunto Mantage, alimwambia zipo sh milioni 2.7 na bastola.
Wakili: Uliweza kufahamu zile ndiyo zilikuwa fedha za tukio la Sinza?
Makele: Sikujua.
Wakili: Mwaka 2006 hujawahi kumiliki simu yenye namba 0744 302226?
Makele: Sijawahi kabisa.
Wakili: Unaifahamu hiyo namba?
Makele: Siifahamu.
Wakili: Soma hiki kielelezo kwa sauti ambacho ni statement yako uliyoitoa kwenye Tume ya ACP-Mgawe.
Makele: Inasomeka hivi, haya ni maelezo ya Ahmed Makele (mimi) kwamba Januari 14 mwaka huo, nilikuwa eneo la tukio na kusikia milio ya risasi eneo la Sinza ukuta wa Posta na kushuhudia miili ya watu wanne ikiwa imekufa.
Wakili: Nakuuliza hayo ni maelezo yako?
Makele: Si maelezo yangu kabisa. Kwanza maelezo hayo yaliandikwa Makao Makuu ya Upelelezi na mimi sijawahi kuandika maelezo hadi nafikishwa mahakamani.
(Watu wakaangua kicheko).
Wakili: Hebu angalia hii statement uliyoitoa kwenye Tume ya Sidyen Mkumbi, ni yako?
Makele: Eeh mtukufu jaji, haya si maelezo yangu kabisa, kwani maswali niliyoulizwa na Mkumbi humu hayamo.
Wakili: Na hiyo saini iliyowekwa mwisho wa hiyo Statement pia si yako?
Makele: Saini hii si yangu (watu wakaangua kicheko).
Wakili: Shahidi wa 36, Sidyen Mkumbi na ACP-Mgawe ambao ni maofisa wako wakubwa, una ugomvi nao?
Makele: Hapana.
Kesi inaendelea kusikilizwa leo ambapo mshitakiwa wa tano, Jane Andrew ataanza kutoa utetezi wake.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne,Februari 17 mwaka 2009