MALECELA,MALECELA UMENISIKITISHA SANA

Na Happiness Katabazi

WIKI iliyopita, jabali katika ulingo wa siasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), John Malecela, alizungumzia mambo mbalimbali yanayohusu chama hicho ikiwemo kukemea wanachama wanaolumbana hadharani bila kupitia vikao halali vya chama.

Pamoja na hilo, alizungumzia mambo mengi ikiwemo mgogoro ndani ya chama na kuwataka wanachama wanaotaka kukihama chama hicho wafanye hivyo haraka .

Pia aliwataka wanachama wanaotaka kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani, wasahau kwa sababu hawawezi kumshinda Rais Jakaya Kikwete.

Malecela hakuishia hapo, alikwenda mbali zaidi, tena bila haya, kwa kueleza kuwa kamwe chama hicho hakiwezi kuyumbishwa na matajiri kwani chama hicho ni cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi. Kauli hii ya Malecela imenisikitisha sana.

Ili mtu uheshimike, ni lazima kwanza wewe binafsi ujiheshimu. Ujiheshimu katika nyendo zako, kauli zako unazotoa mbele ya jamii ziwe na ukweli ndani yake, busara na hata kufundisha jamii inayomzunguka.

Na kama mtu atayafanya hayo, basi atakuwa amempendeza Mungu na wanawadamu ambao aliwaumba kwa mfano wake. Usipotenda hayo hata ukiwa ni kiongozi mwenye madaraka makubwa katika taifa lolote au mzee unayeheshimika katika jamii, ukweli ni kwamba utadharaulika hata na watoto wadogo.

Nimelazimika kutumia maneno haya ninayoamini ni yenye hekima kwa sababu, moja ya kauli iliyotolewa na Malecela ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wachache wanaoheshimika nchini kutokana na mchango wao katika taifa hili, kuwa CCM ni chama cha wakulima, wafanyakazi na wanyonge.

Nimuulize mzee Malecela, anazungumzia CCM ya awamu ipi? ni ile ya Awamu ya Kwanza iliyokuwa ikiongozwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, au ni CCM hii iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa na sasa Rais Jakaya Kikwete au hipi?

Mzee Malecela, ni CCM hii ambayo uchaguzi wa mwaka 2005 ambapo na wewe ulikuwa ni miongoni mwa wanachama 10 waliokuwa wakiparurana na kutengeneza mitandao yenu hadi kumwaga fedha kwa waandishi wa habari ili wawarembe kwenye vyombo vya habari muweze kuchaguliwa na Mkutano Mkuu! Mmoja kati yenu aweze kupeperusha bendera ya kuwa mgombe urais?

Mzee Macelela, CCM ya wakulima, wafanyakazi na wanyonge, ndiyo hii ambapo baadhi ya wanachama wake hawasemezani, wanazuliana fitna, hawapikiki chungu kimoja na hawapendani?

Malecela, ni CCM hii ambayo gazeti la Habari Leo hivi karibuni, liliandika habari kwamba kuna baadhi ya wabunge wamepanga njama ya kumuondoa kwenye nafasi ya uenyekiti, mwenyeketi wa sasa Rais Kikwete.

Ni CCM hii ambayo sote tunashuhudi kwamba ili upate madaraka ni lazima ushikwe mkono na vigogo au uwe na fedha za kuwamwagia wapiga kura?

Ebu mzee Malecela weka pembeni unafiki, ghiliba za kisiasa kama ulivyozoea na ueleze umma kwamba ni CCM gani hivi sasa ni ya wakulima, wanyonge na wafanyakazi, ama sivyo hutaamika tena kwani katika hili umezungumza uongo wakati ukweli unaujua.

Wazee wetu tunawaheshimu sana kwani mmetutangulia kuona na kujua mengi hivyo sisi vijana tunapenda kujifunza kutoka kwenu iwe mavazi, aina ya maisha mnayoishi na hata mtindo mnaoutumia kufanya kazi. Sasa ikifikia mahala mkashindwa kutambua hilo mjue nanyi mnachangia kulipeleka taifa kuzimu.

Amekufa Nyerere, lakini kwa kauli zake dhabiti na matendo yake bado tunamheshimu utafikiri bado yupo hai. Lakini yupo Simba wa Vita, Rashid Kawawa, ambaye naye amelitumikia taaifa hili kwa uadilifu mkubwa.

Alijiheshimu, ndiyo maana leo hii tunamheshimu. Hakuwa mchumia tumbo kama walivyo viongozi wengine. Hakutaka kuendelea kung’ang’ania ubunge ili aendelee kuhudhuria vikao vya bunge, akapate posho kama walivyo wabunge wengine ambao hawataki kabisa kupisha wanachama vijana nao wagombee katika majimbo wanayoyashikilia hadi sasa.

Leo hii baadhi ya Watanzania wameanza kumuita Kawawa kuwa ni ‘Baba Mdogo’ wa Taifa letu kwani Baba wa Taifa, Nyerere amefariki dunia.

Nawaunga mkono kwani ndiyo mzee asiye na makuu aliyebaki ambapo hivi sasa baadhi ya viongozi, wananchi, taasisi mbalimbali akiwemo, Rais Kikwete, wamekuwa wakienda kijijini kwake, Madale kumuomba ushauri wa masuala mbalimbali.

Hivyo, kauli ya Malecela kusema chama hakiyumbishwi na matajiri ni uongo mtupu, na kwamba chama hicho ni cha wafanyakazi, wanyonge na wakulima ni uongo mkubwa.Tumuulize Malecela hivi Rostam Aziz, Christopher Gachuma, Yusuf Manji na matajiri wengine ni wanyonge?

Mbaya zaidi , matajiri wengi ndani ya chama hicho, wana haki ya kuwa wanachama, utajiri wao wanautumia kwa ajili ya kukigawa chama kwa kutapanya fedha kwa wanachama wanaowaunga mkono ili wapate madaraka na mwisho wa siku waweze kuwanyoshea biashara zao na kupata tenda kilaini.

Napenda kumsihi mzee wangu Malecela atambue kwamba zile zama na mababu kupiga hadithi za uongo ili wajukuu zao wapate usingizi zimepitwa na wakati, kwani hivi sasa wajukuu tumeelevuka karibu kila nyanja na tumegundua baadhi ya wazee wetu, kwa ujinga, uoga au ubinafsi wao wamelifikisha taifa letu hapa lilipo.

Hivyo, bado tunahitaji mawaidha yenu, ila tunaomba mtuongoze katika mstari ulionyooka na si kutuweka kwenye makundi makundi ambayo yanafadhiliwa na manyang’au kwa maslahi yenu.

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, April mosi , 2009

DK.SALIM AWAFUNDA ASKARI WANAOENDA DARFUR

Na Happiness Katabazi, Bagamoyo

MSULUISHI wa mgogoro wa jimbo la Darfur nchini Sudan, Dk. Salim Ahmed Salim, amewataka maofisa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), wanaokwenda kulinda amani katika jimbo hilo, watimize majukumu yao bila ubaguzi.

Dk. Salim alisema hayo jana wakati akizungumza na wanajeshi 875 wanaokwenda Darfur, katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika kwenye kambi ya Mafunzo ya Ulinzi wa Amani –Msata, wilayani Bagamayo.

“Wanajeshi mkiwa Darfur, nawaombeni sana mkafanikishe jukumu la ulinzi wa amani na kufikisha misaada ya kibadamu kwa wananchi walioathirika na vita, naamini mkizingatia haya ninayowaeleza pamoja na mafunzo mliyoyapata, mtafanikio,”.

“Darfur siyo sehemu zote zina machafuko, hivyo jukumu lenu si kwenda kupigana tu bali pia kulinda amani. Na ninataka mtambue kule mnakokwenda kuna magenge mbalimbali ya kiharifu, hivyo nasisitiza mzingatie mafunzo mliyoyapata,” alisema Dk. Salim.

Alipoulizwa na waandishi wa habari kwamba haoni kutolewa kwa hati ya kukamatwa na kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifaya The Hegue iliyopo Ufaransa kwa rais wa Sudan, Ally Bashir, kunaweza kuathiri kazi inayofanywa na vikosi vya walinzi wa amani, Dk Salim alisema, unaweza kuathiri kwa kiasi fulani ila hakutavuruga kazi ya walinzi wa amani.

Aidha akijibu swali kwanini Umoja wa Mataifa (UN), ulichelewa kupeleka walinzi wa amani katika jimbo hilo, Dk. Salim aliwataka wananchi watambue kuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe historia inaonyesha huwa inadumu kwa muda mrefu lakini, alisema uchelewaji huo umetokana na uzembe wa jumuiya hiyo ya kimataifa.

Kwa upande wake, Mnadhimi Mkuu wa Jeshi hilo, Luteni Jenerali, Abdurhman Shimbo alisema, wanajeshi wanaokwenda Darfur ni 875 kati yao wanawake 20 na 75 ni Waandisi wa Medani.

Shimbo alisema askari hao wakiwa Darfur, wataishi kwenye maeneo mawili ya Muhajaria na Khor Abeche.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 1 mwaka 2009

CHENGE KIZIMBANI

*Asomewa mashitaka ya kusababisha vifo
*Yuko nje kwa dhamana ya milioni moja
*Ndugu zake wawakejeli wanahabari Dar

Na Happiness Katabazi

MBUNGE wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, akiwakabiliwa na mashitaka matatu yakiwemo ya kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake
wawili.

Chenge (61), alifikishwa mahakamani hapo jana, chini ya ulinzi mkali wa wanausalama na kupelekwa moja kwa moja katika chumba cha mahakama ambako alisomewa mashitaka hayo.

Chenge aliingia mahakamani hapo majira ya saa 5:57 asubuhi kwa msafara wa magari mawili, akiwa ameketi kiti cha nyuma kwenye gari PT0217 aina ya Yundai, mali ya Jeshi la Polisi.

Nyuma lilifuatiwa na gari lingine, lenye namba za usajili, T 200ACC, aina ya Toyota Land Cruser ambapo ndani alikuwa amepanda mke wake Chenge na ndugu zake ambao walifika mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo iliyoshuhudiwa pia na umati wa watu ulifurika kushuhudia Waziri huyo wa zamani, akipandishwa kizimbani.

Gari hizo ziliingia mahakamani hapo kwa mwendo kasi na mtuhumiwa aliposhuka, alizongwa na wananchi lakini makachero walijitahidi kudhibiti hali hiyo na kumuongoza hadi kwenye chumba cha kimoja mahakamani hapo na kusomewa mashitaka.

Akimsomea mashitaka hayo, Mwendesha Mashtaka Mkuu, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), David Mafwimbo, alidai mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi, Emiliusi Mchaulo, kuwa katika shitaka la kwanza, Chenge anadaiwa kusababisha kifo cha Victoria George kwa uendeshaji wa gari kizembe.

Alidai kuwa Machi 27 mwaka huu, saa 10:30 alfajiri katika barabara ya Haile Selaissie, Wilaya ya Kinondoni, akiwa anaendesha gari namba T13 ACE, Toyota Hilux Double Cabin, kwa uzembe na kushindwa kuchukua tahadhari kama inavyotakiwa kwa watumiaji wa barabara, aligonga Bajaji T739 AXC na kusababisha kifo cha Victoria ambaye alikuwa abiria katika bajaj hiyo.

ASP Mafwimbo alidai katika shitaka la pili, Chenge anadaiwa siku na muda huo huo, alisababisha kifo cha Beatrice Constantine kwa kuendesha gari kizembe.

Aidha, alidai shitaka la tatu ni kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha uharibifu wa bajaji ambayo ilikuwa imebeba marehemu hao.

Mshitakiwa huyo alikana mashtaka yote na ASP Mafwimbo aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Akitoa masharti ya dhamana, Hakimu Mchaulo, alisema ili mshitakiwa adhaminiwe, lazima awe na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya sh milioni moja.

Chenge, alidhaminiwa na Mkurugenzi wa Fedha toka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHCR), Ezekiel Masanja na kesi hiyo kuahirishwa hadi Aprili 30, itakapotajwa.

Kutokana na uamuzi wa mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo katika chemba ndogo, kulisababisha waandishi wa habari wengi kushindwa kuingia kuisikiliza, huku waandishi wa habari wawili ndio waliofanikiwa kuingia katika chumba hicho.

Wakati hali hiyo ikijitokeza, baadhi ya ndugu za Chenge walikuwa wakitoa kauli za kuwakejeli wanahabari waliokuwapo mahamani hapo kwamba kamwe kesi hiyo haitawaondoa kwenye umaskini.

“Mnajifanya mnaandika na kupiga picha sasa kwa taarifa yenu andikeni weee… lakini kamwe mkijua kesi hii haitawaondoa kwenye umaskini unaowakabili,” alisema mwanamke mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni ndugu wa mshitakiwa.

Hata hivyo, wakati wapiga picha wakizingira gari lililomleta Chenge mahakamani hapo, ili waweze kumpiga picha wakati akitoka mahakamani, katika hali isiyotarajiwa ndugu na jamaa wa mshitakiwa huyo waliwapiga chenga ya mwili na kumpitishia mlango wa nyuma na kisha kupanda gari ambalo liliondolewa kwa mwendo wa kasi.

Chenge ambaye amepata kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika serikali ya awamu ya tatu na Waziri wa Miundombinu katika serikali ya awamu ya nne, wakati ajali hiyo ikitokea alikuwa akiendesha gari lake binafsi.

Tangu kutokea kwa ajali hiyo, dereva wa bajaj alitoroka na hadi sasa hajulikani alipo.

Kwa Chenge, tukio hilo ni mkasa wa tano mkubwa tangu ilipoanza kumwandama ambapo alishinikizwa ajiuzulu Uwaziri katika Wizara ya Miundombinu mwaka jana kutokana na kashfa ya kuhifadhi zaidi ya bilioni moja katika akaunti aliyokuwa akiimiliki katika visiwa vya New Jersey

Kujizulu kwake kulitokana na kauli yake aliyoitoa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam kwamba fedha zilizokutwa kwenye akaunti hiyo ni Vijisenti tu, akiwa na maana kuwa ni fedha chache kwa mtu wa hadhi yake kuzimiliki.

Kauli hiyo iliamsha hasira kwa wananchi waliokuwa wakimwandamana kupitia vyombo vya habari na hatimaye kuliomba radhi taifa kwa kauli hiyo na baadaye kutangaza kujizulu Uwaziri.

Kabla ya kugundulika kuhifadhi fedha hizo, Chenge alikuwa akikabiliwa na kashfa ya ununuzi wa rada ya serikali inayodaiwa kununuliwa kwa bei kubwa zaidi (sh bilioni 40) na serikali ya awamu ya tatu.

Tukio jingine lilomkumba mbunge huyo ni kuzushiwa kifo ambapo baadhi ya watu walidai amekunywa sumu, ili kukwepa uchunguzi unaofanywa na taasisi ya kuchunguza makubwa ya jina ya Uingereza (SFO)

Baada ya Chenge kujiuzulu, siku chache baadaye alikwenda Bungeni ambako alipatwa na mkasa mwingine pale alipodaiwa kukutwa akitangatanga ndani ya ukumbi wa Bunge, akiambatana na Ofisa mmoja wa Bunge na kudaiwa kuwa alikuwa akimwaga kitu kilichosadikiwa kuwa ni sumu ya kisasa kwenye viti vya baadhi ya wabunge.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 31,2009

SERIKALI YAFUNGA USHAHIDI KESI YA BALOZI MAHALU

Na Happiness Katabazi

BAADA ya kesi ya wizi wa Euro milioni 1.3 inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Ricky Mahalu na Meneja Utawala na Fedha, Grace Martin kuairishwa kwa muda mrefu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana upande wa mashtaka ulitangaza rasmi kufungusha ushahidi wake.

Sambamba na hatua hiyo, jana Mhimili mahususi wa mahakama nchini uliandika historia mpya kwa kesi hiyo ya jinai namba 1/2007 kupokea ushahidi wa shahidi kwa njia ya video katika Kituo cha Mafunzo ya Maendeleo ya Dunia Tanzania (TGDLC) kilichopo katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).Ambapo shahidi alikuwa akitoa ushahidi wake kwa lugha ya Kiitaliano na kutafriliwa kwa lugha ya Kiswahili na mkalimani ambaye ni Paroko Kanisa Katoliki Boko, Evarist Lefiyo.

Wakili wa (Takukuru) Ponsian Lukosi na Joseph Ole walifikia umauzi wa kufunga ushahidi katika kesi yao baada ya Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa Sivangilwa Mwangesi ambaye ndiye anasikiliza kesi hiyo kukataa ombi la mawakili hao wa mashtaka kuiomba mahakama hiyo iairishe kwa kipindi kifupi kesi hiyo ili waweze kuleta shahidi mmoja ambaye naye yupo nchini Italia.

“Baada ya maairisho ya muda mrefu katika kesi hii na ndipo maana Februali 26 mwaka huu, pale Kisutu nilitamka wazi kabisa kwamba lile lilikuwa ni aiirisho la mwisho kwahiyo upande wa mashtaka leo(jana)mnaomba nitoe tena aiirisho la mwisho nasema hivi ombi lenu silikubali kwani endapo nitalikubali mimi ndiyo nitakuwa nachelewesha kesi hii hivyo basi Lukosi unafunga ushahidi au nifunge mwenyewe ushahidi?” alisema Mwangesi kwa sauti ya ukali.

Ghafla Lukosi akajibu kwa unyeyekevu na kueleza kuwa atafunga mwenyewe. “Mheshimiwa nitafunga mwenyewe ushahidi hivyo leo sisi upande wa mashtaka katika kesi hii napenda kuiambia mahakama hii kuwa tumefunga ushahidi wetu” alidai Lukosi.

Aidha Mwangesi alisema April 16 mwaka huu, siku hiyo ni siku ambayo atatoa uamuzi wa aidha washtakiwa hao wawili wanakesi ya kujibu au la.

Shahidi wa pili katika kesi hiyo ambaye ni raia wa Italia ambaye pia Kamishna wa Viapo, Marco Pape ambaye jana alikuwa akimalizika kutoa ushahidi wake kwa njia ya video akiwa Italia, alidai kuwa licha ya yeye anatoa ushahidi wake ushahidi mahakama wala Wizaira ya Mambo ya Nje ya Italia haijampa kibali cha kutoa ushahidi.

Pape ambaye jana alikuwa akimalizia kutoa ushahidi wake,alihojiwa na mawakili wa utetezi waliokuwa wakiongozwa na mawakili wa kujitegemea Mabere Marando, Alex Mgongolwa na Bob Makani,alidai kuwa taarifa za yeye kutakiwa kutoa ushahidi wake amezipata kwa Revocato Jojo na hata alipotakiwa na mawakili wa utetezi atoe ushahidi unaoonyeshwa kuwa aliitwa kutoa ushahidi alidai hana ushahidi huo kwa wakati ule bali ulikuwepo ofisini kwake.

“Sina ushahidi wa kuitwa kutoa ushahidi hapa ila ninao ofisini kwangu kwa Jojo alitumia kwa njia barua pepe ambapo alieleza leo(jana)natakiwa kutoa ushahidi kwa njia ya video katika kesi hii na hata hivyo ujumbe huo alionitumia hakuwa wa kikazi ulikuwa ni wa kibinafsi na hata leo ninavyotoa ushahidi huu najitolea silipiwi posha na mtu yoyote” alidai Pape.

Ifuatayo ni mahojiano katika wakili Mgongolwa na shahidi huyo;
Wakili:Mko wangapi katika chumba hicho unachotolea ushahidi?
Shahidi:Nipo peke yangu.
Wakili:Unaweza kutuambia chumba hicho kina ukubwa gani?
Shahidi:Mita tano kwa tatu.
Wakili:Shhahidi tukumbushe ulipokuja Dar es Salaam, kutoa ushahidi wako wa awali ulisema uliandaa orginal cell agreement, je wewe unayo?
Shahidi:Ninayo hapa.
Wakili:Ni orginal au photocopy?
Shahidi:Kwa mujibi wa Sheria za hapa Italia orginal inabaki kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mkataba kivuli unabaki kwa wakili husika.
Wakili:Shahidi ujaelewa swali unayo hapo au huna?
Shahidi:Sina.
Wakili:Uliwahi kushuhudia malipo ya mkataba wa nyumba hiyo ya ubalozi wetu hapo Italia?
Shahidi:Sikuona malipo wakati wanalipana.
Wakili:Kwa hiyo kwa maneno mengine wewe ujui walilipana kiasi gani?
Shahidi:Mimi ni mwanasheria kitaaluma kazi yangu ni kuandaa mkatana na kutia saini mambo ya malipo hayanihusu.
Wakili:Katika mahakama hii tuliambiwa malipo ya nyumba hiyo yalifanywa kwa njia Elektroniki, uliwahi kujua hiyo?
Shahidi:Nilisikia ila kimaandishi na kielektroniki sikuona hilo.
Wakili:Licha yaw ewe kuandika huo mkataba wewe uliwahi kuiona hilo jingo kwa macho yako?
Shahidi:Sijapata kuliona.
Wakili:Walipokuwa wanasaini huo mkataba wa ununuzi wa jingo hilo kuwaliwa na watu wangapi?
Shahidi:Nakumbuka Katibu wa Ubalozi alikuwepo na Balozi Mahalu.
Wakili:Unaweza kumkumbuka jina?
Shahidi:Simkumbuki jina.
Wakili:Mlikuwa wa ngapi?
Shahidi:Wanne au wa tano.
Wakili:Lwa maneno mingine ukumbuki idadi kamili?
Shahidi:Yes, sikumbuki idadi kamili.
Wakili:Baada ya kusaini huo mkataba nani alikuwa wa kwanza kutoka?
Shahidi:Mimi, nikawaacha wengine.
Wakili:Kwa hiyo tuchukulie wewe ni shahidi usiyeaminika kwasababu huna kumbukumbu?
Shahidi:Mwenye uamuzi wa mwisho ni hakimu.
Wakili:Tunachotaka uileze mahakama hii huna kumbukumbu sahihi za mkataba huo?
Shahidi:Mimi nina kumbukumbu kwa kila nilichoandika.

Ifuatayo ni mahojiano kati ya Bob Makani na shahidi Pape;
Wakili:Umetuambia baada ya kutia sani sikuile ulitoka?
Shahidi:Ndiyo nilitoka.
Wakili:Na ukarudi tena kwenye chumba kile mlichokuwa mkitiliana saini?
Wakili:Kwa hakika ndiyo nilirudi kwaajili ya kuwaaga.
Wakili:Kwanini ulirudi ukuwaaga wakati ulivyotoka?
Shahidi:Kwasababu wale walikuwa wanafanya taratibu za malipo na mimi nilivyotia saini nilitoka.
Wakili:Nasikia Waitaliano wanakwepa kodi?
Shahihi:Ndiyo lakini naamini hilo ni tatizo la duniano kote.
Wakili:Katika mtindo huo wa ukwepaji kodi,utashangaa ukiambiwa kulikuwa na mikataba miwili ambapo mkataba mmoja wewe ukuona?
Wakili:Sijaona mkataba mwingine.
Shahidi:Inawezekana kuwepo mikataba miwili mmoja ukaenda serikalini na mwingine ukabaki kwa mhusika?
Wakili:Inawezekana.
Makani:Ulijuaje unatakiwa kutoa ushahidi ?
Wakili:Wakili Jojo.
Wakili: Mahakama ya Italia imekupa kibali cha kutoa ushahidi hapo ulipo?
Shahidi:Hapana.
Wakili:Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi yako imekuita kuja kutoa ushahidi katika kesi hii?
Shahidi:Hapana.
Wakili:Nani kakuita kutoa ushahidi?
Shahidi:Revocato Jojo.
Wakili:Mwambie Jojo akuonyeshe ushahidi wa wewe kuitwa kutoa ushahidi ?
Shahidi:Sina hapa, ninayo email yake ofisini.
Wakili:Alikutumia lini hiyo email?
Shahidi:Siku nne zilizopita.
Wakili:Je hiyo email ilikuwa ya kikazi au binafsi?
Shahidi:Email binafsi.
Wakili: Nani anakulipa kwa wewe kutoa ushahidi?
Shahidi:Najitolea, hakuna anayenilipa.

Ifuatayo ni mahojiano kati ya mawakili wa Takukuru, Ole na Lukosi kwa shahidi huyo;
Wakili:Shahidi ulipokea mikataba mingapi?
Shahidi: Mkataba mmoja
Wakili:Ulihusika na mkataba binafsi?
Shahidi:Hapana.
Wakili:Ulisani mkataba wa mauzo ya jengo la kiasi gani?
Shahidi: Euro milioni 1.3.
Wakili:Kwa mujibu wa sheria za Italia zinaruhusu kuwa na mkataba zaidi ya mmoja katika jengo moja?
Shahidi:Zinaruhusu mkataba mmoja tu.
Wakili:Mkataba halali ni upi?
Shahidi:Ni ule uliosainiwa adharani.
Wakili: Hawa washtakiwa wawili walikuwepo siku hiyo ya ya kutiwa saini mkataba?
Shahidi:Nakumbuka alikuwepo Profesa Mahalu wengine sina uhakika.

Awali kabla ya shahidi huyo kutoa ushahudi wake Mabere Marando kwaniaba ya jopo la upande wa utetezi, aliwalisha ombi la kupinga shahidi huyo kutoa ushahidi kwa njia ya video kwasababu Mahaka ya Hakimu Mkazi Kisutu haijapata kibali toka kwa Jaji Mkuu kusikiliza kesi nje ya mkoa wa Dar es Salaam, na kuongeza kuwa endapo Mwangesi atapokea ushahidi huo kwa njia ya video sheria za mipaka ya Italia.

Hata hivyo Mwangesi alilitupilia mbali pingamizi hilo na kuruhusu shahidi aanze kutoa ushahidi wake na Marando akaomba apatiwe mwenendo wa pingamizi hilo ili waweze kulipeleka Mahakama Kuu kwaajili ya mapitio ,ombi ambalo lilikubaliwa na Mwangesi ambapo alisema pindi mwenendo utakapochapwa watakabidhiliwa.

Januari mwaka 2007 ilidai mahakamani hapo kuwa Mahalu na Grace ambao walikuwa ni maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, waliisababishia serikali hasara ya sh bilioni tatu.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Machi 27 ,2009

MFANYABIASHARA MWINGINE KORTINI KWA WIZI WA MABILIONI BENKI

*Ahusishwa na wizi wa Barclays

Na Happiness Katabazi

MFANYABIASHARA maarufu wa madini nchini, Justice Deodatus Rugaibula (36), mkazi wa Msasani Beach, Alhamisi iliyopita alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na kesi ya wizi wa dola za Kimarekani milioni 1.08, (sawa na sh bilioni 1.4) kwa njia ya mtandao wa kompyuta, mali ya Benki ya Barclays.

Rugaibula ambaye hivi sasa jina lake limekuwa likitajwatajwa kwenye baadhi ya nyimbo za bendi maarufu za muziki wa dansi nchini ikiwemo bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, alifikishwa mbele ya Hakimu Eva Nkya na ilidaiwa na wakili wa serikali kuwa anakabiliwa na mashtaka sita ya wizi kwa kutumia mtandao.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ambapo kesi hiyo ya jinai imepewa namba 75 ya mwaka huu, mashtaka hayo baadhi yake yanafanana na mashtaka yanayowakabili wafanyakazi saba wa Barclays na Mkurugenzi Mtendaji wa Dar es Salaam, Cement Muslim na mfanyabiashara maarufu wa mafuta nchini, Merey Ally Saleh (41) maarufu kwa jina la Merey Balhabou na Meneja Mwendeshaji wa Kigamboni Oil Co. Ltd, Abdallah Said Abdallah (48).

Kufikishwa kwa kumshitakiwa huyo mahakamani wiki iliyopita kumesababisha watuhumiwa wa wizi katika benki hiyo ya Barclays kufikia 10 hadi sasa.

Mwendesha mashtaka Inspekta Emma Mkonyi mbele ya Hakimu Mkazi Eva Nkya, alidai kuwa mshitakiwa huyo anakabiliwa na mashitaka ya kula njama kwa nia ya kudanganya kwamba, Oktoba 29-30 mwaka jana, katika eneo lisilofahamika jijini Dar es Salaam, kwa kutumia ujanja, alifanya udanganyifu na kuibia benki hiyo dola za Kimarekani milioni 1,081,263.00.

Inspekta Mkonyi alidai kuwa, katika shitaka la pili, Oktoba 27 mwaka jana, katika eneo lisilofahamika jijini alighushi ujumbe wa kasi (swift message) wenye namba SEQ 000303, kuonyesha kwamba ujumbe huo ulielekea Kigamboni Oil Co. Ltd, kwenye akaunti namba 8001993 kwa ajili ya kuhamisha dola za Kimarekani 700,769.00 kinyume na sheria.

Katika shtaka la tatu, alilodai kuwa ni la kughushi, kwamba mnamo Oktoba 27, mwaka jana, Justice Rugaibula, katika eneo lisilofahamika kwa nia ya kudanganya, walighushi ujumbe wa kasi, wenye namba SEQ 00041, kuonyesha kwamba ujumbe huo unakwenda Kigamboni Oil Co. Ltd, kwenye akaunti namba 8001993 kwa ajili ya kuhamisha dola za Kimarekani 299,974.00 mali ya benki hiyo, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Inspekta Mkonyi aliendelea kudai kuwa shitaka la nne ni wizi, kwamba mshitakiwa mnamo Oktoba 31, mwaka 2002 katika Benki ya Stanbic, tawi la May Fair jijini Dar es Salaam, bila uhalali wowote katika akaunti namba 0222824801, alihamisha isivyo halali dola 200,000.00 kwenye akaunti hiyo fedha ambazo ni mali ya Benki ya Barclays (T) Ltd.

Aidha katika shitaka la tano, mshitakiwa huyo anaidaiwa kuwa Oktoba 31 mwaka 2002 katika benki ya Stansbic Tawi la May Fair jijini Dar es Salaam, bila uhalali wowote kupitia akaunti namba 012282480 aliiba fedha taslimu sh 200,000.00 kwa kutumia hundi namba 000001, mali ya Benki ya Barclays (T) Ltd.

Aidha alidai shitaka la sita ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, ambapo alidai kuwa Oktoba 31 mwaka 2008 katika Makao Makuu ya Benki ya Barclays mtaa wa Ohio jijini, baada ya kuwasilisha hati za uongo, alijipatia sh. 583,620,000 kutoka kwa Daudi wa Kigamboni Oil Co. Ltd na baada ya kupata hizo fedha alidai kuwa hayo ni malipo halali toka kwa mteja wake ambaye wamewekeza naye katika mradi wa machimbo ya madini katika mkoa wa Mara huku akijua si kweli.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshitakiwa alikana shitaka na Hakimu Nkya alisema masharti ya dhamana ni sawa na yaliyotolewa kwa washitakiwa wengine katika kesi hiyo ambao wapo nje kwa dhamana.

Hata hivyo mshitakiwa huyo alipata dhamana.Mbali Rugaibula, wengine ni Merey na Abdallah ambao walifikishwa Machi 5, mwaka huu. Washtakiwa wengine ni ambao walifikishwa mahamani hapo mwishoni mwaka jana ni wafanyakazi wa benki hiyo ni Winford Mwang’onda, Shubira Mutungi, Naima Saria, Upendo Mushi, Magreth Longway, Emmanuel Mukoni na Ramadhani Khamis.

Mapema Machi mwaka huu, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, alitahadharisha mabenki kuwapo kwa mbinu mpya ya wizi unaotumia teknolojia ya kisasa ya kompyuta ambapo benki za CRDB na Barclyas zilishakumbwa na wizi huo.

Alisema aina hiyo ya wizi ni ngeni nchini na wahusika wanaweza kuchota fedha nyingi kuliko wizi uliozoeleka wa kughushi hundi, saini au ule unaofanywa kwa kuvamia na kupora kwa nguvu kutumia silaha za moto.

Alisema wizi huo umeanza kujitokeza zaidi kuanzia mwaka jana, ambapo wezi hao wa mtandao wa kompyuta walifanikiwa kuwashawishi baadhi ya wafanyakazi wa benki na watu wa kupitisha fedha hizo kwenye akaunti zao.

Wiki chache zilizopita, iliripotiwa kuwa kikundi cha watu wachache walichukua sh. bilioni 5, mali ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kwa njia hiyo mpya ya wizi, zilizokuwa ni malipo ya kawaida kwenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kwa mujibu wa taarifa hizo, fedha hizo ziliingizwa kwenye akaunti mbalimbali ikiwamo akaunti ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ambapo ziliingizwa zaidi ya sh. milioni 671 kwenye akaunti yao iliyopo katika Benki ya CRDB, tawi la Lumumba bila wahusika kujua.

Ilielezwa kuwa fedha hizo hazikuwa za TUCTA wala chama chochote chenye uhusiano nayo, na hawajawahi kufanya biashara yoyote na TTCL kuweza kulipwa kiasi hicho cha fedha.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 25 ,2009
Mfanyabiashara mwingine kortini kwa wizi mamilioni benki
*Ahusishwa na wizi wa Barclays
Na Happiness KatabaziMFANYABIASHARA maarufu wa madini nchini, Justice Deodatus Rugaibula (36), mkazi wa Msasani Beach, Alhamisi iliyopita alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na kesi ya wizi wa dola za Kimarekani milioni 1.08, (sawa na sh bilioni 1.4) kwa njia ya mtandao wa kompyuta, mali ya Benki ya Barclays.
Rugaibula ambaye hivi sasa jina lake limekuwa likitajwatajwa kwenye baadhi ya nyimbo za bendi maarufu za muziki wa dansi nchini ikiwemo bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, alifikishwa mbele ya Hakimu Eva Nkya na ilidaiwa na wakili wa serikali kuwa anakabiliwa na mashtaka sita ya wizi kwa kutumia mtandao.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ambapo kesi hiyo ya jinai imepewa namba 75 ya mwaka huu, mashtaka hayo baadhi yake yanafanana na mashtaka yanayowakabili wafanyakazi saba wa Barclays na Mkurugenzi Mtendaji wa Dar es Salaam, Cement Muslim na mfanyabiashara maarufu wa mafuta nchini, Merey Ally Saleh (41) maarufu kwa jina la Merey Balhabou na Meneja Mwendeshaji wa Kigamboni Oil Co. Ltd, Abdallah Said Abdallah (48).
Kufikishwa kwa kumshitakiwa huyo mahakamani wiki iliyopita kumesababisha watuhumiwa wa wizi katika benki hiyo ya Barclays kufikia 10 hadi sasa.
Mwendesha mashtaka Inspekta Emma Mkonyi mbele ya Hakimu Mkazi Eva Nkya, alidai kuwa mshitakiwa huyo anakabiliwa na mashitaka ya kula njama kwa nia ya kudanganya kwamba, Oktoba 29-30 mwaka jana, katika eneo lisilofahamika jijini Dar es Salaam, kwa kutumia ujanja, alifanya udanganyifu na kuibia benki hiyo dola za Kimarekani milioni 1,081,263.00.Inspekta Mkonyi alidai kuwa, katika shitaka la pili, Oktoba 27 mwaka jana, katika eneo lisilofahamika jijini alighushi ujumbe wa kasi (swift message) wenye namba SEQ 000303, kuonyesha kwamba ujumbe huo ulielekea Kigamboni Oil Co. Ltd, kwenye akaunti namba 8001993 kwa ajili ya kuhamisha dola za Kimarekani 700,769.00 kinyume na sheria.
Katika shtaka la tatu, alilodai kuwa ni la kughushi, kwamba mnamo Oktoba 27, mwaka jana, Justice Rugaibula, katika eneo lisilofahamika kwa nia ya kudanganya, walighushi ujumbe wa kasi, wenye namba SEQ 00041, kuonyesha kwamba ujumbe huo unakwenda Kigamboni Oil Co. Ltd, kwenye akaunti namba 8001993 kwa ajili ya kuhamisha dola za Kimarekani 299,974.00 mali ya benki hiyo, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Inspekta Mkonyi aliendelea kudai kuwa shitaka la nne ni wizi, kwamba mshitakiwa mnamo Oktoba 31, mwaka 2002 katika Benki ya Stanbic, tawi la May Fair jijini Dar es Salaam, bila uhalali wowote katika akaunti namba 0222824801, alihamisha isivyo halali dola 200,000.00 kwenye akaunti hiyo fedha ambazo ni mali ya Benki ya Barclays (T) Ltd.
Aidha katika shitaka la tano, mshitakiwa huyo anaidaiwa kuwa Oktoba 31 mwaka 2002 katika benki ya Stansbic Tawi la May Fair jijini Dar es Salaam, bila uhalali wowote kupitia akaunti namba 012282480 aliiba fedha taslimu sh 200,000.00 kwa kutumia hundi namba 000001, mali ya Benki ya Barclays (T) Ltd.
Aidha alidai shitaka la sita ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, ambapo alidai kuwa Oktoba 31 mwaka 2008 katika Makao Makuu ya Benki ya Barclays mtaa wa Ohio jijini, baada ya kuwasilisha hati za uongo, alijipatia sh. 583,620,000 kutoka kwa Daudi wa Kigamboni Oil Co. Ltd na baada ya kupata hizo fedha alidai kuwa hayo ni malipo halali toka kwa mteja wake ambaye wamewekeza naye katika mradi wa machimbo ya madini katika mkoa wa Mara huku akijua si kweli.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshitakiwa alikana shitaka na Hakimu Nkya alisema masharti ya dhamana ni sawa na yaliyotolewa kwa washitakiwa wengine katika kesi hiyo ambao wapo nje kwa dhamana.

Hata hivyo mshitakiwa huyo alipata dhamana.Mbali Rugaibula, wengine ni Merey na Abdallah ambao walifikishwa Machi 5, mwaka huu. Washtakiwa wengine ni ambao walifikishwa mahamani hapo mwishoni mwaka jana ni wafanyakazi wa benki hiyo ni Winford Mwang’onda, Shubira Mutungi, Naima Saria, Upendo Mushi, Magreth Longway, Emmanuel Mukoni na Ramadhani Khamis.Mapema Machi mwaka huu, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, alitahadharisha mabenki kuwapo kwa mbinu mpya ya wizi unaotumia teknolojia ya kisasa ya kompyuta ambapo benki za CRDB na Barclyas zilishakumbwa na wizi huo.Alisema aina hiyo ya wizi ni ngeni nchini na wahusika wanaweza kuchota fedha nyingi kuliko wizi uliozoeleka wa kughushi hundi, saini au ule unaofanywa kwa kuvamia na kupora kwa nguvu kutumia silaha za moto.Alisema wizi huo umeanza kujitokeza zaidi kuanzia mwaka jana, ambapo wezi hao wa mtandao wa kompyuta walifanikiwa kuwashawishi baadhi ya wafanyakazi wa benki na watu wa kupitisha fedha hizo kwenye akaunti zao.

Wiki chache zilizopita, iliripotiwa kuwa kikundi cha watu wachache walichukua sh. bilioni 5, mali ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kwa njia hiyo mpya ya wizi, zilizokuwa ni malipo ya kawaida kwenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kwa mujibu wa taarifa hizo, fedha hizo ziliingizwa kwenye akaunti mbalimbali ikiwamo akaunti ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ambapo ziliingizwa zaidi ya sh. milioni 671 kwenye akaunti yao iliyopo katika Benki ya CRDB, tawi la Lumumba bila wahusika kujua.

Ilielezwa kuwa fedha hizo hazikuwa za TUCTA wala chama chochote chenye uhusiano nayo, na hawajawahi kufanya biashara yoyote na TTCL kuweza kulipwa kiasi hicho cha fedha.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 25 ,2009

WAKILI WA MAINJINIA WA KICHINA ATAKA WAKAISHI MELINI

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ilishindwa kutoa uamuzi wa kupatiwa dhamana au la kwa mainjia watano ambao hivi karibuni walikamatwa wakiwa katika meli ya Tawariq iliyokuwa ikifanya uvuvi haramu katika eneo la Bahari ya Hindi, baada ya kuzuka malumbano ya kisheria toka kwa mawakili wa pande mbili katika kesi hiyo.

Washtakiwa wanaokabiliwa na tuhuma hizo ni Cai Dong Li (44), Chen Rui Hai (34),Vu Dong Liu (39), Zhao Jong (23), Zhao Hoi Gong, wote ni raia wa China.

Hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba, ambaye juzi alisema angelitoa uamuzi wa kutoa dhamana wa mainjinia hao leo, baada kuhoji iwapo wana vibali vya kukaa nchini, jambo lililoibua malumbano toka pande mbili za kesi

Wakili wa utetezi, Kapteni Bendera, aliinuka na kudai kuwa hati za kusafiria za washtakiwa zimechukuliwa na Jeshi la Polisi.

“Sasa nikiwaruhusu wapate dhamana washtakiwa wataenda kuishi wapi?” alihoji Hakimu huyo.

Wakili bendera alieleza kuwa iwapo wateja wake watapewa dhamana watakwenda kuishi kwenye meli kwa sababu maisha yao yote waliishi humo na meli hiyo hivi sasa inashikiliwa na polisi hivyo hawawezi kutoroka.

Kwa upande wa mawakili wa serikali, Biswalo Mganga, yeye alidai kuwa, meli ni kielelezo katika kesi hiyo na wakati wowote upande wa mashtaka utaweza kuitembelea hivyo haiwezekani washtakiwa hao kuishi kwenye meli hiyo.

Baada ya mabishano, Mwaseba aliamuru Machi 27, ndiyo siku ya kutoa uamuzi wa maombi hayo na kuamuru kwamba upande wa mashtaka katika kesi hiyo ulete hati za kusafiria za washtakiwa hao mahakamani na washtakiwa hao kurudishwa rumande.

Juzi washtakiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo kwa mara ya kwanza, wakikabiliwa na shtaka moja la uvuvi wa haramu katika ardhi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya kuwasomea mashtaka hayo, wakili wa utetezi, Kapteni Bendera, aliomba mahakama ilegeze masharti ya dhamana, ili wateja wake waweze kudhaminiwa.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 25 ,2009

MTANGAZAJI MATATANI KWA DAWA ZA KULEVYA

Na Happiness Katabazi

MTANGAZAJI wa Redio Times FM, inayomilikiwa na Kampuni ya Bussiness Times Ltd, Hadija Shaibu, maarufu kwa jina la ‘Dida wa Mchops’ anashikiliwa na askari wa Kitengo cha Kuzuia
Dawa za Kulevya cha Jeshi la Polisi baada ya kumshuku kuwa anasafirisha dawa za kulevya.

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilizolifikia Tanzania Daima Jumatano, zilieleza kuwa Dida alianza kushikiliwa juzi baada ya askari wa kitengo hicho waliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kumkamata wakati akijiandaa kupanda ndege kwenda China.

Habari zilieleza kuwa Dida alikuwa akijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopian Air Line, lakini polisi walilazimika kumtia nguvuni baada ya kumpeleleza kwa muda mrefu na kuhisi kuwa huenda siku hiyo alikuwa amemeza dawa hizo ili azisafirishe nje ya nchi.

Zieleza zaidi kuwa baada ya Dida kukamatwa, alipelekwa kwenye choo maalumu kilichopo uwanjani hapo ambacho hutumiwa na askari wa kitengo hicho kuwahifadhi watuhumiwa wanaowakamata wakiwa wamemeza dawa za kulevya kwa muda ambapo endapo mtuhumiwa alikuwa amemeza dawa hizo atazitoa wakati akijisaidia.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa tangu alipoingizwa kwenye choo hicho juzi jioni hadi jana saa nne asubuhi, hakuweza kugundulika kuwa na dawa hizo tumboni ambapo alichukuliwa hadi makao Makuu ya Kitengo hicho, huko Barabara ya Kilwa kwa ajili ya kuhojiwa.

“Nakuhakikishia kuwa jana (juzi) tulimkamata Dida pale uwanja wa ndege, alikuwa akielekea China kwani tulikuwa tukimshuku kuwa amemeza dawa hizo lakini hadi hivi ninavyoongea na wewe yupo mikononi mwetu ila hatujamkuta na pipi hata mmoja.

“Tumemleta hapa ofisini kwetu Kilwa Road kwa ajili ya mahojiano zaidi na tayari mama yake ameishafika na tunaendelea kuchukua maelezo yake ila kwa sababu bado ni mchana ni mapema kukuhakikishia kuwa tutamalizana naye leo au la,” alisema mmoja wa maofisa wa kitengo hicho.

Taarifa nyingine zilizopatikana jana jioni zilieleza kuwa Dida alidhaminiwa jana majira ya saa kumi jioni.

Hata hivyo alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Godfrey Nzowa, ili aweze kuthibitisha taarifa hizo alishindwa kukubali au kukataa na badala yake akaishia kusema atafuatilia.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano,Machi 25,2009

WAKILI KORTINI KWA UTAPELI

Na Happiness Katabazi

WAKILI wa Kujitegemea, Ademba Gombal, wa Kampuni ya Uwakili ya Agumba ya jijini Dar es Salaam na mwenzake, jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka ya kujipatia dola za Kimarekani 280,000 mali ya kampuni ya DI Abana Co.Ltd
Mbali na Gombal, mwingine ni mfanyabiashara Yusuph Nazir Khan, maarufu kwa jina la Manji Kharim Amir.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Hadija Msongo, ilidaiwa na wakili wa serikali, Dereck Mukabatunzi, kuwa shtaka la kwanza ni kula njama na kutenda kosa.

Mukabatunzi alidai kuwa shtaka la pili ni kughushi katika muda usiofahamika jijini, waliwasilisha hati ya namba 186037/69 ya kitalu namba 104 iliyopo Mtaa wa Uganda, Oysterbay, jijini Dar es Salaam iliyoonyesha kutolewa Oktoba 19, mwaka 1995 kuonyesha kuwa ilikuwa ni halali na imetolewa na Wizara ya Ardhi, kitu ambacho si kweli.

Alidai shtaka la tatu linalomkabili mshtakiwa wa tatu, ni kuwasilisha hati isiyo halali ambayo inaonyesha Desemba 31 mwaka jana, katika Kampuni ya Uwakili ya Gombal iliyopo Mtaa wa Nkurum.

Alidai kuwa shtaka la nne ni kuwasilisha hati za uongo kwa mshtakiwa namba moja kwamba Desemba 31, mwaka jana, katika ofisi za wakili huyo, huku mtuhumiwa akijua kuwa si halali, aliwasilisha hati hiyo kwenye kampuni ya DI Abana Co Ltd kwa Stika.

Aidha alidai shitaka la tano ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kuwa tarehe hiyo washtakiwa walijipatia dola za Kimarekani 280,000 baada ya kumdanganya Stika, kwamba wamemuuzia eneo hilo ambalo limeonyeshwa kwenye hati huku wakijua wanafanya udanganyifu.

Washtakiwa wote walikana mashtaka na hakimu alisema ili mshtakiwa apate dhamana, alitakiwa awe na wadhamini wawili ambao watasaini dhamana ya dola milioni 10 na kila mshtakiwa alitakiwa kutoa fedha taslim au hati ya mali yenye thamani ya dola milioni 70.

Hata hivyo washtakiwa walishindwa kutimiza masharti na kurudishwa rumande hadi kesi hiyo itakapokujatajwa tena.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 25,2009

SERIKALI YAFUNGA USHAHIDI KESI YA MARANDA

Na Happiness Katabazi

UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya wizi wa sh bilioni 1.8 za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inayomkabili Mweka Hazina wa CCM MKoa wa Kigoma, Rajabu Maranda na Farijara Hussein, jana ulifunga ushahidi wake.

Wakili Kiongozi wa Serikali Stanslaus Boniface ambaye alikuwa akisaidiana na Vitalis Tomin aliliambia jopo la Mahakimu Wakazi wa Tatu, Cypriana William, Phocus Bambikya na Saul Kinemela jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, walisema wamefunga ushahidi huo shahidi wa tisa, Steven Mwakalukwa(54) ambaye ni Mkaguzi wa Mahesabu ya Ndani katika Benki Kuu kumaliza kutoa ushahidi wake.

“Waheshimiwa Mahakimu Wakazi leo (jana) ninayo furaha kubwa kuiambia mahakama hii tukufu kwamba sisi upande wa mashtaka tumefunga ushahidi wetu,” alieleza Boniface huku akionekana kuwa mwenye furaha.

Hata hivyo, Desemba mwaka jana, Boniface wakati akisoma maelezo ya awali ya kesi hiyo aliambia mahakama hiyo kuwa kesi ambayo alianza kusikiliwa mapema mwaka huu, watakuwa na mashahidi 22.

Kwa upande wa wakili wa utetezi, Majura Magafu, aliomba upande wa mashtaka uwapatie mwenendo wa kesi, ili waweze kutumia kifungu cha 230 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya 2002, ili mahakama iweze kuamua kwamba washtakiwa wana kesi ya kujibu au la.

Pia Magafu aliwasilisha aliomba wateja wake waruhusiwe kwenda nyumbani kwako Kigoma kwa mapumziko.

Akitoa uamuzi wa maombi hayo, Hakimu William alisema anakubalina na ombi la upande wa utetezi upewe mwenendo wa kesi mapema na kwamba anawaruhusu washtakiwa kwenda Kigoma ila ruhusa hiyo ni kwa ajili ya kesi hiyo na si kwenye kesi nyingine zinazowakabili washtakiwa hao.

“Ruhusa ya kwenda Kigoma imekubaliwa ila ni katika kesi hii peke yake kesi nyingine ruhusa hii isitumike tafadhali na hivyo naairisha kesi hii hadi April 15 mwaka huu, kesi hii itakuja kwa ajili ya kutajwa,” alisema William.

Washitakiwa hao wanadaiwa kula njama, kughushi, wizi, kuwasilisha hati za uongo na kujipatia ingizo la fedha kwa njia ya udanyifu kwenye akaunti , sh bilioni 1.8 mali ya BoT wakijaribu kuonyesha kampuni yao ya Kiloloma Brothers imepewa idhini ya kukusanya deni la kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai India.

Mapema jana akiongozwa kutoa ushahidi wake na mawakili hao wa serikali Mwakalukwa aliambia mahakama mwaka 2005 akiwa Msimamizi wa Idara ya Fedha za Nje aliliona jarada la Kiloloma &Brothers ambalo lilifika katika idara yake lilokuwa likitaka lilipwe fedha za madeni na yeye pamoja na maofisa wenzake waliidhinisha kampuni hiyo ilipwe Sh 1,864,949,294.45 kupitia benki ya United Bank of Afrika.

Maranda anakabiliwa na kesi nne za aina hiyo katika mahakama hiyo wakati Farijara anakabiliwa na kesi mbili za tatu aina hiyo mahakamani hapo na wote wapo nje kwa dhamana.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne,Machi 24 mwaka 2009

MAINJINIA UVUVI HARAMU WABURUZWA KORTINI

Na Happiness Katabazi

MAINJINIA watano ambao hivi karibuni walikamatwa kwenye meli ya Tawariq 1 wakifanya uvuvi haramu katika Bahari ya Hindi nao jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, na kusomewa shitaka lao.

Wakili wa Serikali, Biswalo Mganga, aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Cai Dong Li (44), Chen Rui Hai (34),Vu Dong Liu (39), Zhao Jong (23), Zhao Hoi Gong, wote ni raia wa China, ambao ni mainjinia wa meli hiyo.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba, Wakili huyo wa Serikali alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na shitaka moja la uvuvi haramu katika ardhi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya kuwasomea mashitaka hayo, Wakili wa utetezi, Kapteni Bendera, aliomba mahakama ilegeze masharti ya dhamana, ili wateja wake waweze kudhaminiwa.

Hata hivyo, Wakili Mganga, alieleza kuwa upande wa mashitaka hauna pingamizi, ila unashangazwa na ombi la wakili huyo kwa sababu ni lazima wakili huyo atoe uthibitisho kwamba washitakiwa hao wakidhamiwa hawatatoroka, kwa kuwa washitakiwa wote ni wageni.

Hakimu Mwaseba alisema uamuzi wa kupata dhamana au kutopatiwa dhamana kwa washitakiwa hao atauotoa leo na kuamuru washitakiwa wote waende rumande.

Mapema mwezi huu washitakiwa 32 ambao nao walikuwa kwenye meli hiyo walifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shitaka la kuvua samaki bila leseni. Walikana mashitaka na kupelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo kila mshitakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 24 mwaka 2009

FEDHA ZA EPA ZILIKUWA ZIKITUNZWA NBC-SHAHIDI

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa nane katika kesi ya wizi wa sh bilioni 1.8 za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Meneja Uhusiano wa Benki Kimataifa katika Benki ya NBC, Lyson Mwakapenda (64) ameiambia mahakama kuwa malimbikizo ya fedha za EPA awali yalikuwa yakitunzwa kwenye benki hiyo.

Mwakapenda alieleza malimbikizo ya madeni ya EPA yalianza mwaka 1979 na ilipofika kwamba mwaka 1985 baada ya makubaliano katika ya NBC na BoT na serikali iliridhia madeni hayo yaamishiwe BoT.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Wakili wa Serikali Vitalis Tomoni ambaye alikuwa akisaidiana na Wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus na shahidi huyo;

Wakili: Unafanyakazi wapi?
Shahidi: NBC Makao Makuu.
Wakili: Kama nani pale?
Shahidi: Meneja Uhusiano wa Benki ya Kimataifa katika benki hiyo.
Wakili: Majukumu yako nini?
Shahidi: Kufanyakazi kwa kushirikiana na benki za nje ya nchi.
Wakili: EPA ni nini ?
Shahidi: Ni malimbikizo ya madeni ya wafanyabiashara wa nje ambao serikali yetu ilishindwa kuyalipa kwa wakati ule.
Wakili: NBC ilihusika vipi na malimbikizo hayo?
Shahidi: Wafanyabishara hao wa nje walikuwa na akaunti katika benki yetu na ndipo walikuwa wanatarajia malipo yao kupitia kwenye akaunti hizo.
Wakili: NBC ilikuwa inalipaje fedha hizi?
Shahidi: Kabla ya kuwalipa nilazima NBC ilikuwa inapata kibali cha kuwalipa toka BoT.
Wakili: Nini kilifanya msilipe fedha hizo za kigeni(EPA) kwa wakati?
Shahidi: Taifa lilikuwa lina uhaba wa fedha za kigeni za kuweza kulipa madeni hayo.
Wakili: Hao wafanyabiashara/waagizaji walikuwa wanaleta fedha za aina gani?
Shahidi: Fedha za Kitanzania.
Wakili: Kulikuwa na makundi gani ya waingizaji?
Shahid: Kundi la watubinafsi, makampuni ya serikali na umma.
Wakili: Hawa waagizaji walikuwa wa njia ngapi za kulipa fedha?
Shahid: Letter for Credit,Bill of Exchange , open account.
Wakili: Tuambie ni kipindi gani malimbikizo yalianza?
Shahidi: Mwaka 1979.
Wakili: Mliwekaje kumbukumbu za malimbizo hayo?
Shahidi: Kwenye rekodi ya vitabu vya benki.
Wakili: Je kulikuwa na rejista yoyote yoyote?
Shahidi: Kwenye matawi ya benki yetu rejista ilikuwepo.
Wakili: Zilikuwa zinaitwaje?
Shahidi: LC rejister, IFBC.
Wakili: Lini hizo kumbukumbu zilipelekwa BoT?
Shahidi: Mwaka 1985.
Wakili: Kwa sababu gani?
Sahidi: Baada ya makubaliano kati ya NBC na BoT ndiyo serikali ikalidhia kwamba malimbikizo hayo yamishiwe BoT. Na baada ya makubaliano hayo kila wiki NBC ilikuwa inakusanya fedha hizo na kupeleka Benki Kuu ambapo ndipo kwenye akaunti ya EPA.
Wakili: Utaratibu huo uliendelea hadi lini?
Shahidi: Septemba 1993.
Wakili: Nini kilisababisha kusimamishwa?
Shahidi: Ulitolewa waraka na BoT kwamba NBC isipeleke fedha BoT kwani fedha za kigeni wakati huo zilianza kupatikana kutokana na kuwepo kwa soko huria.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Farijara Hussein na Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Kigoma, Rajabu Maranda ambao wanadaiwa kuiibia BoT sh bilioni 1.8. Kesi imeahirishwa hadi Jumatatu ijayo itakapoendelea kusikilizwa.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Machi 21 mwaka 2009

WANAHARAKATI WAFUNGUA KESI YA KUTETEA ALBINO

Na Happiness Katabazi

MASHIRIKA mawili yasiyokuwa ya kiserikali jana yalifungua kesi ya Kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Mwanasheria wa Serikali na wenzake kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).

Mashirika hayo ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHCR) na Chama cha Maalbino Tanzania ambao wanatetewa na mawakili Abdallah Possi,Nelly Gogley Moshi,Clarence Kipobota,Fredrick Mkatamba na Fulgence Massawe.

Kwa mujibu wa hati ya madai walalamikaji hao walidai kutokana na serikali kushindwa kuzuia mauaji hayo ni kukiuka Ibara ya 12(1),12(2),14,18(2) na 29(2) za katiba ya nchi.

“Kura za maoni zinaoendeshwa na serikali hazina nguvu ya kisheria kumkamata mtuhumiwa kwa vile anayeandika jina halazimishwi kutaja jina wala kuitwa mahakamani kama shahidi.
Aidha, katika kesi hiyo walalamikaji hao wanaiomba mahakama hiyo itoe amri ya kutungwa sheria itakayowezesha albino au walemavu kufurahia haki zilizoainishwa kwenye katiba ya nchi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Machi 21 mwaka 2009

KESI YA LIYUMBA YAPANGIWA HAKIMU

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE uongozi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imempangia Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema, kusikiliza kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba na Meneja Mradi wa BoT, Deogratius Kweka.

Hatua ya kupangiwa hakimu hiyo imekuja ikiwa wiki moja imepita, tangu hakimu Mkazi Hadija Msongo, aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, kuamua kujitoa kwa madai kuwa mwenendo wa kesi hiyo umekuwa ukilalamikiwa na waendesha mashitaka na mawikili kupitia vyombo vya habari

Wakili Kiongozi wa Serikali Stanslaus Boniface, aliyekuwa akisaidiana Prosper Mwangamila,Tabu Mzee toka Taasisi ya Kzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), alieleza kuwa, kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kupangiwa hakimu.

Hakimu Lema kwa upande wake, alisema kesi hiyo itakuja tena Aprili 2 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa maombi ya kutaka Liyumba na mwenzake waachiliwe huru kwa madai kuwa uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kufungua kesi hiyo, una dosari za kisheria.

Ijumaa iliyopita, Hakimu Msongo, alitangaza uamuzi wa kujitoa kusikiliza kesi hiyo kwa kile alichokieleza kuwa baadhi ya wananchi na mawakili wa upande wa utetezi, wamekuwa wakilalamikia mwenendo wa kesi hiyo kupitia vyombo vya habari.

Februari 17 mwaka huu, hakimu Msongo alimwachia kwa dhamana iliyozua utata Liyumba.

Utata huo, ulitokana na kauli ya wakili wa serikali, Justas Mulokozi kuonyesha kushangazwa na uamuzi wa kumwachia mtuhumiwa huyo licha ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Moja ya masharti ambayo wakili huyo alidai hayakutimizwa na Liyumba ni kuwasilisha mahakamani hati zenye thamani ya sh bilioni 55, wadhamini wawili wa serikali wakiwa na barua kutoka kwa waajiri wao na kukabidhi hati za kusafiria mahakamani hapo.

Lakini siku hiyo Liyumba aliwasilisha hati yenye thamani ya sh milioni 882, hati ya kusafiria ambayo muda wake wa matumizi umekwisha, huku wadhamini wawili wakiwa hawana barua zilizosainiwa na mwajiri wao kama masharti yalivyotolewa na mahakama.

Februali 24 mwaka huu, Liyumba alifika mahakamani hapo na hakimu Msongo alisema hati 10 za wadhamini zenye thamani ya sh bilioni 55, ndizo zilizotumika kujaribu kumdhamini mshitakiwa huyo mara ya kwanza, lakini zilikataliwa baada ya kubainika kuwa zilikuwa na kasoro za kisheria, huku nyingine zikidaiwa kuwa ni za kughushi.

Kutokana na kasoro hizo, hakimu Msongo aliagiza hati hizo zipelekwe Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na tayari Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, aliliambia Tanzania Daima kuwa hati hizo uchunguzi wa hati hizo, umeanza.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Machi 21 mwaka 2009

MSHITAKIWA KESI YA ZOMBE AHAMISHIWA OCEAN ROAD

Na Happiness Katabazi

MSHITAKIWA wa 11 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja, Rashid Lema amehamishiwa katika Taasisi ya Saratani, Ocean Road, jijini Dar es Salaam kwa matibabu, imefahamika.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka ndani ya Gereza la Keko na Ocean Road, vimeihakikishia Tanzania Daima kuwa Lema alifikishwa hospitalini hapo tangu juzi.
Vyanzo hivyo vilieleza kuwa Lema amelazimika kuhamishiwa katika hospitali hiyo baada ya kubainika kuwa ana kansa ya ngozi.

“Nakuhakikishia Lema amelazwa Ocean Road tangu juzi, kwa kweli hali yake inazidi kuwa mbaya kadiri siku zinavyozidi kwenda, cha msingi tuombe Mungu ampe nafuu,” kilieza chanzo hicho.

Aidha, vyanzo hivyo vilisema kuwa tayari serikali imeimalisha ulinzi kwa mgonjwa huyo tangu alipolazwa katika Hospitali ya Muhimbili na sasa Ocean Road.
Hata hivyo jitihada za gazeti hili za kumtafuta Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Twalib Ngoma, hazikuzaa matunda.

Hivi karibuni Lema alizidiwa gerezani na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke, lakini siku chache baadaye alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwa ajili ya matibabu zaidi ambako alilazwa kwa zaidi ya wiki tatu sasa.

Februari 19 mwaka huu, Jaji wa Mahakama ya Rufaa ambaye anasikiliza kesi inayomkabili mshitakiwa huyo na wenzake 12, alilazimika kuahirisha kusikiliza kesi hiyo baada ya mshitakiwa huyo kushindwa kufika mahakamani kutokana na afya yake kuwa mbaya.

Lema anaelezwa kuwa ndiye shahidi muhimu kwa sababu ndiye alibadilisha sura ya kesi hiyo, kwani baada ya kutoka mafichoni alikokuwa amejificha, alimweleza mlinzi wa amani aliyechukua maelezo yake kwamba mauaji ya watu hao, yalifanyika kwenye msitu wa Pande.

Mbali na Lema, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe, SP Christopher Bageni, SP Ahmed Makelle, Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Koplo Abeneth Saro, Bakari na Festus Gwasabi.

Washitakiwa hao wanadaiwa Januari 14 mwaka 2006, eneo la Mbezi Luis, katika msitu wa Pande, waliwaua, Ephraim Chigumbi, Sabinus Chigumbi na Mathias Lukombe, ambao ni wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Ulanga na Juma Ndugu, ambaye ni dereva teksi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Machi 20 mwaka 2009

MRAMBA AZUIWA KUSAFIRI,MGONJA ARUHUSIWA

Na Happiness Katabazi

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Basil Mramba na wenzake wawili ambao wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7, wamewasilisha maombi ya ruhusa ya kutoka nje ya Dar es Salaam na kurejeshewa hati zao na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Mbali na Mramba, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.

Maombi hayo ambayo yamewasilishwa na mawakili wao mbele ya Hakimu Mkazi, Henzron Mwankenja kwa tarehe tofauti, Mramba anaomba aruhusiwe kwenda jimboni kwake Rombo kuanzia Machi 4 mwaka huu na atarejea siku ya karibu na kesi.

Pia aliiomba mahakama imrudishie hati ya kitalu 446 Kawe, iliyondikwa jina la Basil Mramba na hati ya kitalu 294 iliyoandikishwa kwa jina la H.K. Senkoro ambazo zilitumika kumdhamini.

Kwa upande wa Yona ambaye maombi yake yaliwasilishwa na wakili wake, Joseph Thadayo, Februari 10 mwaka huu, anadai kutokana na amri iliyotolewa Februari mosi mahakamani hapo kwamba kiwango cha dhamana kimepunguzwa hivyo anaomba mteja wake aruhusiwe kupewa hati yake yenye namba CT57467 ya kitalu 745 na CT 57230 ya kitalu namba 745, zote zimeandikishwa kwa jina la Daniel Yona, ambazo zote zipo Block A, Makongo Juu.

“Na kwa kuzingatia masharti ya sasa ya dhamana mahakama hivi sasa inashikilia hati yenye namba CT 59935 kwa ajili ya kitalu 744 iliyopo Makongo Juu yenye thamani ya sh bilioni 2.2, ambayo inakidhi masharti ya dhamana iliyowekwa na mahakama.

Kwa upande wa Mgonja, wakili wake kutoka kampuni ya uwakili ya Kisarika, Malimu Mlola, aliwasilisha ombi la ruhusa Machi 12 mwaka huu, akiomba mteja wake aruhusiwe kwenda Kilimanjaro na Arusha kwa ajili ya kuwatembelea wazazi wake na atarejea jijini Aprili 15.

Hakimu Mwankenja alisema amekubaliana na maombi ya kurejeshewa hati Yona na Mramba, ila amelikataa ombi la Mramba la kutaka aruhusiwe kwenda jimboni kwake kwa sababu katika ombi hilo mshitakiwa huyo hajaonyesha tarehe ya kurejea.

Hata hivyo alisema licha ya kukubali ombi la Yona na Mramba kurejeshewa hati, alisema hati hizo zitarejeshwa mikononi mwao Aprili 17 mwaka huu, wakati kesi yao itakapotajwa.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi,Machi 19 mwaka 2009

WALIOSHTAKIWA KWA UVUVI HARAMU WAPATA MAWAKILI

Na Happiness Katabazi

MAWAKILI wawili raia wa Tanzania, wamejitosa kuwatetea raia 32 wa kigeni ambao hivi karibuni walikamatwa kwenye meli ya Tawariq 1 wakifanya uvuvi haramu katika Bahari ya Hindi.

Mawakili hao ni Elasimus Buberwa ambaye anamtetea mshitakiwa 7 na wa tisa wakati Elias Nawera anawateta washitakiwa 30 katika kesi hiyo ambayo ilifunguliwa Ijumaa iliyopita katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali Rose Chilongola ambaye alikuwa akiwasaidiana na Prospa Mwangamila mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi Addy Lyamuya waliambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo aujakamilika ila wanaiomba mahakama hiyo imruhusu mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Naodha wa meli hiyo , Chin Tai Hsu(61),aruhusiwe kutoka gerezani kwa siku mbili ili aweze kwenye Kituo Polisi Kati kwaajili ya mahojiano.

Ombi hilo lilikubaliwa na Lyamuya na kuairisha kesi hiyo hadi Machi 27 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa na kuagiaza upande wa mashtaka uhakikishe tarehe hiyo wakalimani wote wanafika bila kukosa kwasababu jana alifika mkarimani mmoja toka ubalozi wa China.

Ijumaa iliyopita Wakili wa Serikali, Biswalo Mganga akisaidiana na Michael Lwena, Prospa Mwangamila aliwataja baadhi ya majina ya washtakiwa huku majina mengine yakitajwa na wakalimani kutoka Ubalozi wa China na Indonesia.

Mbali na Naodha wa meli washtakiwa wengine ni mabaharia, Jiojwen Chang (34), Jia Yin Zhao 26), Gexi Zhao (36), Zongmin Ma (36), Dong Liu (25), Yongiao Fang (22), Nguyen Tuan(23), Hsu Sheng Pao (55), Zhao Hanquing (39), Zho Hanging (39) ambaye wote ni wakala na raia wa China.

Wengine ni Tran Van Phuon (33), Pham Dinn Suong (31), Tran Van Thanh (23), Cao Vuong (27), Kristofer Padilla (29) raia wa Vietnam. Wengine ni Mohamed Kiki (61), Anul Mani (24) raia wa Taiwani.

Aidha, Wakili Mganga alisema washtakiwa wengine ni Jejen Priyana (22), Kuntoto Suratno (27), Tusi Ame (25), Ifan Herman Pandi (21), raia wa Indonesia, Silvano Garanes (32), Benjie Rosano (34), Ignacio Dacumos (31), Marlon Maronon (33), Jhoan Belano (34), Rolando Nacis (35) raia wa Philipins, Wakati Ali Ali Mkota (32), Juma Juma Kumu (40), Jackson Toya(39) raia wa Kenya.

Wakili Mganga alidai washtakiwa wote wanakabiliwa na mashtaka mawili, shitaka la kwanza ni kuvua samaki bila leseni kinyume na sheria ya Uvuvi wa Samaki katika kina kirefu ya mwaka 2009.

Alidai Machi 8 mwaka huu, washtakiwa wote kwa pamoja, saa sita usiku katika ukanda wa bahari ya Hindi ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walikamatwa wakiwa wakivua samaki bila leseni.Na washtakiwa wote walikana mashtaka na wapo rumande kwaajili ya wameshindwa kutimiza masharti dhamana.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 11 mwaka 2009

Ghafla viongozi wa CCM wanawaangukia wananchi
Na Happiness Katabazi
GHAFLA Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wanawaangukia wananchi kumbe msimu wa kura umewadia.

Mwaka 2005, CCM ilinadi wagombea wake kwa kuwaaidi wananchi maisha bora kwa kila Mtanzania.Msemo huo ulichapishwa kila gazeti, ulitangazwa kila redio,Televisheni,fulana, kanga na vipeperushi mbalimnali kwa wingi kwa wapiga kura.

Ukiacha thamani ya vipepelushi yenyewe ambayo ilighalimu mamilioni ya fedha , viongozi wa chama hicho waliomba kura kwa kila njia, mbinu ikiwa ni pamoja na kutoa takrima ambayo mwaka 2006 Mahakama Kuu,iliitangaza kuwa ni rushwa , fedha, chakula, vinywaji nk.

Kwa hakika msemo wa kasi mpya ari mpya na nguvu mpya uliambatana na nguvu hizo za fedha ambazo leo tumejua ni hizi za EPA na mikataba ya manunuzi ya umma na madini.

Tunao uhakika sasa kwamba wapiga kura wengi wa nchi hii walidanganywa kwa usanii huo mkubwa.Leo hakuna kiongozi wa kuachaguliwa awamu ya nne anayeweza kukwepa tuhuma za kuwa alichaguliwa kwa kutumia mbinu hizi chafu.

Hakuna aliyeyaona maisha bora hayo miaka mitatu sasa baada ya uchaguzi ule wa mwaka 2005, wala hakuna matumani kwamba maisha hayo bora kwa kila mtanzania yatapatikana katika kipindi cha miaka miwili iliyosalia.

Kwa mara ya kwanza katika histoaria ya nchi yetu serikali iliyoingia madarakani kwa mara ya kwanza ili kumba na mfululizo wa kashfa za wizi wa mali za umma, rushwa na ubadhilifu hata ikibidi serikali ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, kujiudhuru.

Tatizo ni kwamba serikali hiyo iliyojiudhuri kwa tuhuma za rushwa na shetani hilo la rushwa limo ndani ya serikali hiyo hadi sasa.Serikali iliyochaguliwa kwa rushwa kamwe aisafishiki.

Leo ilibidi wananchi waikabe koo serikali hiyo iteme donge la Dowans.Wananchi wasingesimama kidete siku chache zilizopita, donge hilo lingeishamezwa na serikali yetu.

Kipindi kilichopo tunashuhudia mawaziri , wabunge na madiwani wakimimika kwenye majimbo yao ya uchaguzi.Mawaziri wakitumia nyenzo za kiserikali za magari na misaada kupelekea wapiga kura katika majimbo yao.

Ghafla tumeshuhudia lugha nyenyekevu kutoka kwa viongozi na kwa mara ya kwanza tumeanza kuwasikia wabunge wakitetea wananchi wao wanaodhurumiwa haki zao kupitia sera mbalimbali za serikali.

Kuanzia kwa Rais Jakaya Kikwete, tumeanza kusikia utetezi kwa wananchi wanaobomolewa makazi na kunyang’anywa ardhi zao ili kuwapisha wawekezaji na miradi mbalimbali ya maendeleo bila malipo ya fidia.

Hiki ni kilio cha wananchi kila mahali nchini.Serikali yetu haijali maslahi yao bala inajali maslahi ya wawekezaji na maslahi ya miradi .

Umaskini wa raia binafsi unasababishwa na serikali yenyewe kwa kuwa kila mara wapolazimika kuama makazi na ardhi mbadala na wala fidia haitoshi kujenga makazi mapya.

Tungetegema kama wananchi wangelitambua hilo na kusimama kidete kushika fimbo kumchapa kila kiongozi wa CCM anayejaribu kuwoamba kura.Ni usanii mtupu.

Kwa upande mwingine tumeona sasa baadhi ya viongozi wanaotoka maeneo ya wafugaji wakianza kufurukuta kutetea haki za wafugaji , hili wanalifanya japo wakijua kwamba serikali ya CCm haina sera ya wafugaji japo ina sera ya mifugo.

Hiki ni kiini macho kwa taifa kuwa na sera ya mifugo bila kuwa na sera ya kuendeleza wafugaji.Hakuna kikundi cha Watanzania kilichozalaulika na kunyimwa haki za kibinadamu kama wafugaji.

Kwanza walinyang’anywa ardhi yao ya kufugia ,nyumba zao kuchomwa moto katika wilaya ya Hanang’.Huko serikali ilianzisha mashamba makubwa ya kilimo cha nga’no.

Wafugaji wale hawakupata fidia wala ardhi mbadala na sasa wamesambaa kila mahala nchini Mvomero , Ihefu na kwingineko.Kama vile hiyo haitoshi mahakama za nchi hazikuwasaidia wafugaji hao walipo kwenda kudai haki zao mahakamani.

Hii inaonekana kwamba kwa ujumla wake sera na sheria za nchi kwa ujumla wake zinalinda na kutetea wakuliwa na haziwalindi wafugaji.

Kule Mkomazi, wafugaji waliokuwa wakiongozwa na Lakei Faru Parutu walifukuzwa ndani ya hifadhi na bila fidia wala ardhi mbadala.Leo hii wanatangatanga bila kujua wapi walishie mifugo yao.

Lakini tumemsikia Mbunge wao Anna Kilango akiwatetea na kutaka watafutiwe maeneo mbadala ya kulisha mifugo yao na wejengewe huduma za kijamii ili jamii yao iweze kujisikia kuwa ni binadamu kama wengine.

Tukizungumiza suala zima la maendeleo , Wakulima maskini wa nchi hii ambao ndiyo waliowengi kuliko kundi lolote nchini,wamesahauliwa, kule vijijini hatuoni miradi ya umwagiliaji maji ikizinduliwa wala hatuoni wagani wa kilimo ambao wangewaongoza na kuwashauri wakulima kuhusu kilimo bora na cha kisasa.

Ama kwa hakika kila aliyewahi kutembelea vijijini siku za hivi karibuni atakuwa ameshuhudia jinsi jembe la mkono linavyowadidimiza wakulima wetu na kuwakatisha tama.

Kilimo cha kutumia jembe bila pembejeo na kutegemea mvua kimewaweka wakulima katika maisha magumu na wala wimbo huu wa maisha bora hauna maana kwao.

Tungetamani kama wakulima kwa umoja wao wangetambua hilo na kuwanyima kura hawa viongozi matapeli wa kisiasa wanaojipitisha pitisha sasa na kuwalambalamba miguu huku wakiwamwagia sifa na zawadi lukuki.

Ni vyema wakulima wajue kwamba hakuna kiongozi atakaye wakomboa kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakabili ila wao wenyewe.

Watambue pia kwamba kila wanapopokea rushwa inayoletwa kwa sura ya ukarimu wanapunguza uhuru wao kwa kujitia minyororo na kujilaani wenyewe na kubaki maskini wenyewe.

Kwa upande wa Wafanyakazi, kipindi cha serikali ya awamu ya nne kimekamilisha mzunguko wa gurudumu la Utandawazi kwa maana kwamba uporaji wa rasilimali za viwanda na migodi sasa umetimia kwa kuwa sekta hizo zimetekwa na wageni.

Pamoja na hilo licha wafanyakazi wengi kustaafishwa kwa masurufu ‘kiduchu’, sekta ya ajira sasa inaendelea kutegemea wataalamu wageni kuliko wataalamu wenyeji.

Na hiyo sasa kwa kadri itakavyokuwa tabaka la wafanyakazi litaendelea kufifia kipato chake kitaendelea kuwa kidogo kwakuwa serikali imeshindwa kuwa na sera inayoboresha taaluma ya kazi na sera inayoboresha uongozi wa Vyama vya Wafanyakazi.

Vyama vya Wafanyakazi vipo kama havipo au kwa lugha nyingine ‘vipo vipo tu’.Kule migodini zipo taarifa za unyanyasaji kwa wachimbaji na mainjiinia wazawa na tunajua kwamba nafasi nyeti kwenye maeneo ya madini yanapokusanywa ili kupakiwa na kusafirishwa zipo mikono mwa wageni na hakuna mwenyeji anayeruhusiwa kuzisogelea.

Tunajua vile vile wenyeji hawana ushiriki wowote katika uuzaji na usafirishaji wa madini na kwamba takwimu za madini ni uongo na wizi mtupu.

Basi ni vyema wakati tukijadili hoja za kuwadia kwa uchaguzi wa Serikali za Mtaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani,tuangalie pia nafasi ya vyombo vya habari.

Katika uchaguzi mkuu uliopita , vyombo vya habari viliwashawishi wananchi kuchagua viongozi wa awamu ya nne.Vilifanya hivyo kwa ushawishi mkubwa na kila kalamu na ulimi ulitumika kumsifia Jemedali wa awamu ya nne, Kikwete, alivyobora, alivyo ‘Hand Some boy’ ,alivyo kijana, anavyopendwa na anavyotufaa kutuongoza.

Hata ikafikia pahala baadhi ya viongozi wa dini wakaitimisha kwa kusema hilo ni chaguo la mungu. Sasa tujiulize kama vyombo hivi vya habari viliwatendea Watanzania haki?

Hayo maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi?Mbona vyombo hivi hivi vya habari haviulizi maswali magumu kujua kama wizi unaotokea sasa ndiyo yale maisha bora tuliyoaidiwa?

Lakini hivi sasa kwa namna moja au nyingine tumegundua baadhi ya vyombo na waandishi wa habari tayari wameishaweka sawa kuanzisha kampeni ya kuirejesha serikali ya awamu ya nne madarakani.

Sasa tujiulize hilo wanalifanya kwa maslahi ya nani?Ni vyema tuayeseme haya sasa kwani taaluma ya uandishi wa habari ipo matatani,tukifanya yale baadhi yetu waliyofanya mwaka 2005,taaluma hii itakufa.

Tutaonekana ni wahuni, wazandiki na wabababishaji malaya.Kama ni njaa basi njaa yetu aiwezi kumalizwa kwa hivyo vijisumni tunavyopewa na wanasiasa kama mbwa koko.

Ni afadhali tukajiheshimu na kuheshimu taaluma yetu hata kama itatulazimu kufa njaa.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 18 mwaka 2009

GHAFLA VIONGOZI WA CCM WANAWAANGUKIA WANANCHI

TUWASHANGAE VIONGOZI WETU NA BAKORA MKONONI

Na Happiness Katabazi

GHAFLA, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameanza kuwaangukia wananchi. Ni jambo lililotarajiwa na wengi kutokea wakati kama huu tunapokaribia msimu wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Mwaka 2005, CCM ilinadi wagombea wake kwa kuwaahidi wananchi maisha bora kwa kila Mtanzania. Msemo huo ulichapishwa katika kila gazeti, ulitangazwa katika kila redio, kwenye maTV, fulana, kanga na vipeperushi mbalimbali.

Ukiacha thamani ya vipeperushi ambavyo haina shaka viligharimu mamilioni ya shilingi, viongozi wa chama hicho waliomba kura kwa kila mbinu ikiwamo ya kutoa takrima ambayo mwaka 2006 Mahakama Kuu iliitangaza kuwa ni rushwa.

Hakika msemo wa ari, kasi na nguvu mpya uliambatana na nguvu hiyo ya fedha ambazo leo tunaambiwa ni hizi za EPA na mikataba ya manunuzi ya umma na madini. Haina shaka kwamba wapiga kura wengi walidanganywa. Leo hakuna kiongozi wa kuchaguliwa wa awamu ya nne anayeweza kukwepa tuhuma kuwa alichaguliwa kwa kutumia mbinu hizi chafu.

Hakuna mwananchi aliyeyaona maisha bora miaka mitatu sasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2005, wala hakuna matumani kwamba maisha bora kwa kila Mtanzania yatapatikana katika kipindi cha miaka miwili iliyosalia.

Kwa mara ya kwanza katika histoaria ya nchi yetu, serikali iliyoingia madarakani kwa mbwembwe za kuchaguliwa ‘kwa kishindo’, viongozi wake kukumbwa na kashfa za wizi wa mali za umma, rushwa na ubadhilifu.

Kinachoonekana hapa ni kwamba serikali iliyoingia madarakani kwa rushwa haiwezi kujisafisha au kusafishika. Hii ni kwa sababu shetani anayejulikana kwa jina la rushwa aliyeweka maskani yake serikalini hawezi kuiachia pasipo serikali yenyewe kumfukuza yeye pamoja wafuasi wake kutoka serikalini.

Njia za kumfukuza shetani huyo ni pamoja na kuomba msaada wa wananchi kuikemea serikali kila pepo huyo mchafu anapoipanda kichwani kama walivyofanya katika ‘issue’ ya serikali kutaka kununua mitambo ya kuvua umeme ya kampuni ya Dowans.

Tunayoyaona sasa ya mawaziri, wabunge na madiwani kumiminika kwenye majimbo yao ya uchaguzi wakitumia nyenzo za kiserikali kupelekea misaada kwa wapigakura katika majimbo yao hayatuondoi katika hali tuliyonayo ya kuandamwa na rushwa rushwa.

Lugha za unyenyekevu kutoka kwa viongozi na kasi ya wabunge kuwatetea wananchi wao wanaodhulumiwa haki zao kupitia sera mbovu za serikali navyo havituondoi katika hali tuliyomo.

Ukitaka tushangae pamoja. Sikiliza kauli hii ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwatetea wananchi wanaobomolewa makazi yao na kunyang’anywa ardhi zao ili kuwapisha wawekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo bila malipo ya fidia. Rais anaibuka leo kuanza kuwatetea wapiga kura wake wakari tatizo hili analijua kabla hata hajaingia madarakani.

Anajua fika kuwa hiki ni kilio cha wananchi kila mahali nchini. Na kwa muda mrefu, serikali yetu imekuwa haijali maslahi ya wananchi wake bala ya wawekezaji na miradi yao.

Anajua kuwa umaskini wa raia unasababishwa na serikali yenyewe kwa kuwa kila mara kwa kuwalazimisha wananchi wake kuhama hama makazi yao pasipo kuwalipa fidia ya kutosha kwa ajili ya kujenga makazi mapya.

Lakini katika hali ya kushangaza, sasa wananchi wanatetewa na serikali hiyo hiyo iliyowasababishia matatizo hayo. Ili kuisadia kuondokana na shetani huyo wa kuwatesa, wananchi hawana budi kusimama kidete sasa na kushika bakora mkononi ambazo wasisite kuzitumia kuwacharaza wanaopita sasa kuwaomba kura wakati msimu wa kufanya hivyo haujafika.

Tukiwa na bakora zetu mikononi, tunapaswa kuwashangaa pia baadhi ya viongozi wanaotoka maeneo ya wafugaji walioanza kufukuta sasa kutetea haki za wafugaji, huku kukiwa na taarifa kuwa kauli zao zinatokana na baadhi yao kuwa wamiliki wa mamia ya mifugo inayoshughuliiwa sasa na serikali.

Tuwashangae kwa sababu licha ya kufahamu kuwa serikali ya CCM haina sera ya wafugaji bali ya mifugo, wao sasa wameanza kupiga kelele wa kuwatetea haki za wafugaji, hawa nao ni wasanii, ili kuwasaidia tunapaswa kucharaza bakora kama alivyofanya Albert Mnali.

Hawa ni lazima tuwacharaza kwa hasira kwa sababu wanatufanya kiini macho, ni wao waliohusika kulifanya taifa kuwa na sera ya mifugo pasipo kuwa na sera ya kuendeleza wafugaji.

Ni hawa waliosababisha kundi hili la jamii wa wafugaji kudharaulika kama ilivyo sasa, wanapojitokeza leo wakilia lia kuhusu hali za wafugaji, tujue kuwa wanalenga uchaguzi mkuu wa 2010.

Hawa wanaowalilia wafugaji leo walikuwapo wakati serikali ikiwanyang’anya wafugaji ardhi yao huko Hanang na kuanzisha mashamba makubwa ya kilimo cha ngano pasipo kuwalipa fidia wala ardhi mbadala kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao. Ni hao ambao hivi sasa wamesambaa kila mahali huko Mvomero, Ihefu na kwingineko.

Kama kushangaa, kwa wafugaji tutashangaa hadi kesho, kwa sababu tukimaliza ya huko Mvomero, tushangae ya kule Mkomazi ambako wafugaji wa eneo hilo chini ya kiongozi wao, Lakei Faru Parutu, walifukuzwa ndani ya hifadhi bila kulipwa fidia wala ardhi mbadala. Leo wanatangatanga bila kujua wapi watalisha mifugo yao.

Hawa nao tumemsikia Mbunge wao, Anna Kilango, akiwatetea na kutaka watafutiwe maeneo mbadala ya kulisha mifugo yao na wejengewe huduma za kijamii ili jamii yao iweze kujisikia kama nyingine zinavyojisikia.

Kundi jingine la jamii yetu linalopaswa kuanza kujipanga sasa na bakora zao mikononi ni la wakulima. Hili ni kundi la Watanzania wengi lakini lililosahaulika likiwa limeachwa likiishi katika lindi la umaskini wa kutupa.

Watanzania wa kundi hili kwa miaka makumi manne wamekuwa wakiahidiwa kupelekewa zana za kisasa za kilimo na katika siku za usoni, tumewasikia watawala wetu wakihubiri kuwapelekea miradi ya umwagiliaji ili waweze kuboresha kilimo chao, jambo ambalo kama limetekelezwa, sijui kama inafika asilimia 20.

Sote ni mashihidi wa jinsi hali zilivyo katika maeneo ya vijijini, hawa wanaochangia kwa kiasi kikubwa kuwaweka watawala madarakani, bado wanasota na kilimo cha jembe la mkono.

Wanavuja jasho kila uchao kwa kilimo hicho cha jembe la mkono pasipo kusaidiwa hata pembejeo za uhakika, walichabakiza ni kutegemea kudra za mwenyezi mungu ili mazao yao yaweze kustawi.

Kama wafugaji, hawa nao natamani kusikia kuwa wako tayari na bakora zao mikononi wakiwasubiri hao wanaokwenda kuwaomba kura sasa, bila kujali staili wanayoitumia kuwaendea, kama ni ya kuinama au kupiga magoti kama ishara ya kuwasihi wadodoshe chini bakora zao.

Kwa upande wa wafanyakazi, sina wasiwasi kwa sababu ninaamini wapo ambao wamekwishaanza kuwacharaza bakora wanasiasa wa aina hii, kisa ni hasira walizo nazo za kukamilika kwa mzunguko wa gurudumu la utandawazi, kwa maana ya kukamilika kwa zoezi la kurahisisha uporaji wa rasilimali zetu, viwanda na migodi na kuzimilikisha kwa wageni.

Wafanyakazi wanajitahidi hata kuicharaza bakora serikali, kwa kudai mafao zaidi kuliko kidunchu wanayolipwa kama masurufu wakati wa kustaafu.

Ninafurahi kwa sababu ninatambua wanasiasa ambao wameanza zoezi la kuwahadaa wapiga kura sasa kwa visingizo mbalimbali vikiwamo vya kuwatetea na kuwapekelea vijizawadi, huko kwa wafanyakazi hawatathubutu hata kunusa kwa vile hawa tayari wanazo bakora mikononi mwao.

Watu wa hatari ambao jamii haina budi kuwaangalia kwa macho mawili ni waandishi wa habari ambao katika uchaguzi mkuu uliopita, baadhi yao waliwalazimisha Watanzania kuamini kuwa Rais Kikwete ndiye aliyechaguliwa na Mungu kuwa rais wa Tanzania.

Walifanya hivyo baada ya kulidaka tamko la viongozi wa dini kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu, wakatumia kalamu na ndimi zao kulihuburi hilo kwa Watanzania wote, wakafanikiwa kusaidia kwa kiasi kikubwa kumpeleka Ikulu.

Lakini ni waandishi hawa hawa ambao hivi sasa wameanza kumgeuka Rais Kikwete kwa kumkosoa karibu kwa kila hatua anayoichukua katika kutekeleza majukumu yake kama kiongozi mkuu wa nchi. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa baadhi ya vyombo vya habari na waandishi wa habari wameshawekwa sawa kuanza kampeni za kuirejesha serikali ya awamu ya nne madarakani.

Hawa tunapaswa kujiuliza, wanalifanya hilo kwa maslahi ya nani? Kwa nini wasijielekeza katika kazi ya kuelimisha umma zaidi na kusuburi muda wa kumpigia kampeni utakapowadia ndipo waanze kazi hiyo?

Hawa nao hawana budi kushikiwa bakora kwa sababu mapito yao katika taaluma hii si sahihi. Kinachoonekana kwao ni kuichafua taaluma hii na kuifanya w atu wanaoweza kununuliwa kwa kibaba cha unga na kumpigia chapua mwanasiasa yoyote hata asiye faa kushika madaraka makubwa ya nchi yetu.

Hawa tunapaswa kuwaambia mapema kuwa kitakachowanusuru na bakora za umma ni kujiheshimu na kulinda maadili ya taaluma ya uandishi wa habari hata ikibidi kufa njaa.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 18 mwaka 2009

MABAHARIA WA MELI YA UVUVI HARAMU WASOMEWA MASHTAKA

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE raia 32 wa kigeni ambao wiki iliyopita walikamatwa kwenye meli ya Tawariq 1 wakifanya uvuvi haramu katika Bahari ya Hindi, jana walipandishiwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Wakili wa Serikali, Biswalo Mganga akisaidiana na Michael Lwena, Prospa Mwangamila na Wakili Kiongozi wa Serikali Stanslau Boniface, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Addy Lyamuya aliwataja baadhi ya majina ya washtakiwa huku majina mwengine yakatajwa na wakalimani kutoka Ubalozi wa China na Indonesia.

Washtakiwa hao ni Naodha wa Meli hiyo, Chin Tai Hsu(61), wengine ni mabaharia, Jiojwen Chang (34), Jia Yin Zhao 26), Gexi Zhao (36), Zongmin Ma (36), Dong Liu (25), Yongiao Fang (22), Nguyen Tuan(23), Hsu Sheng Pao (55), Zhao Hanquing (39), Zho Hanging (39) ambaye wote ni wakala na raia wa China.

Wengine ni Tran Van Phuon (33), Pham Dinn Suong (31), Tran Van Thanh (23), Cao Vuong (27), Kristofer Padilla (29) raia wa Vietnam. Wengine ni Mohamed Kiki (61), Anul Mani (24) raia wa Taiwani.

Aidha, Wakili Mganga alisema washtakiwa wengine ni Jejen Priyana (22), Kuntoto Suratno (27), Tusi Ame (25), Ifan Herman Pandi (21), raia wa Indonesia, Silvano Garanes (32), Benjie Rosano (34), Ignacio Dacumos (31), Marlon Maronon (33), Jhoan Belano (34), Rolando Nacis (35) raia wa Philipins, Wakati Ali Ali Mkota (32), Juma Juma Kumu (40), Jackson Toya(39) raia wa Kenya.

Wakili Mganga alidai washtakiwa wote wanakabiliwa na mashtaka mawili, shitaka la kwanza ni kuvua samaki bila leseni kinyume na sheria ya Uvuvi wa Samaki katika kina kirefu ya mwaka 2009.

Alidai Machi 8 mwaka huu, washtakiwa wote kwa pamoja, saa sita usiku katika ukanda wa bahari ya Hindi ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walikamatwa wakiwa wakivua samaki bila leseni.

Mganga ambaye wakati akisoma shitaka alilazimika kuwapatia hati ya mashtaka wakalimani, ili waweze kuwasomea washtakiwa kwa lugha za nchi zao, alidai kuwa shitaka la pili ni kuvua samaki katika kina kirefu kinyume na sheria hiyo ya uvuvi.

Hata hivyo, washtakiwa hao ambao walikuwa awali wote walikana kutojua kiingereza miongoni mwao baada ya kuulizwa kama ni kweli au si kweli kwamba walitenda kosa hilo, walikana mashtaka yote.

Baada ya kukana mashtaka Wakili Kiongozi, Boniface alisema upande wa serikali hauna pingamizi la dhamana na aliomba mahakama iwapatie kibali cha washtakiwa wote leo wapelekwe kituo cha polisi Kati, ili wakahojiwe zaidi na Jeshi la Polisi na kuomba wafikishwe kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 12 jioni.

Ombi hilo lilikubaliwa na Hakimu Lyamuya ambaye alisema endapo washitakiwa hao wana wadhamini wawili kila mmoja wajitokeze, ili wadhaminiwe sharti ambalo lilishindwa kutimza na washtakiwa hao na kusababisha kwenda rumande. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 17 mwaka huu, itakapotajwa.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Machi 14 mwaka 2009

HAKIMU KESI YA LIYUMBA AJITOA

Na Happiness Katabazi

BAADA ya kelele nyingi kupigwa kuhusu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kupamtia dhamana yenye utata aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT), Amatus Liyumba, hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi amejitoa.

Hakimu Mkazi, Hadija Msongo ambaye ndiye alikuwa akisikiliza kesi hiyo, alitangaza uamuzi huo jana, wakati kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa kwa ombi la mawakili wa utetezi uliokuwa ukiongozwa na wakili wa kujitegemea Profesa Gamaliel Mgongo Fimbo ya kutaka Liyumba na mwenzake waachiliwe huru kwa sababu uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wa kuwashtakiwa una dosari za kisheria.

Hata hivyo, ombi hilo halikuweza kusikilizwa kutokana na hakimu huyo kutangangaza kujitoa kusikiliza kesi hiyo.

Hakimu Msongo alitoa uamuzi huo muda mfupi baada ya wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus Boniface, Prospa Mwangamila na mawakili wa utetezi Profesa Fimbo, Hurbet Nyange, Hudson Ndusyepo, Majura Magafu kujitambulisha kwake na kumweleza wapo tayari kwa ajili ya kesi hiyo kuendelea.

Baada ya mawakili hao kujitambulisha hakimu huyo alisema kutokana na mwenendo wa kesi hiyo kulalamimikiwa baada ya mshitakiwa Liyumba kupewa dhamana, anaona ni busara kujitoa kuendesha kesi hiyo.

“Kutokana na mwenendo wa kesi hii kulalamikiwa wazi wazi na Watanzania na waendesha mashtaka wa kesi hii kupitia vyombo vya habari na mbele ya jamii mahakma imeonekana imekosea.

“Na ili haki ionekane imetendeka, najitoa kwenye kesi hii na jalada la kesi nitampelekea kwa Hakimu Mfawidhi wa mahakama hii, ili aweze kumpangia hakimu mwingine,” alisema hakimu Msongo.

Baada ya kutoa uamuzi huo, Profesa Fimbo aliinuka kudai kuwa washtakiwa kwa kuwa wapo kizimbani aliomba kesi hiyo jana ile ile ipangiwe kwa hakimu mwingine, ili waweze kujua tarehe ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Hata hivyo, Msongo alisema kesi hiyo itatajwa Machi 20 mwaka huu, ambapo itakuwa imeshapangiwa hakimu mwingine wa kuiendesha kesi hiyo.

Februari 17 mwaka huu, Msongo alimwachia kwa dhamana iliyozua utata Liyumba na utata huo ulitokana na kauli ya wakili wa serikali Justas Mulokozi, kuonyesha kushangazwa na uamuzi wa kumwachia mtuhumiwa huyo licha ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Moja ya masharti ambayo wakili huyo alidai hayakutimizwa na Liyumba ni kuwasilisha mahakamani hati zenye thamani ya sh bilioni 55, wadhamini wawili wa serikali wakiwa na barua kutoka kwa waajiri wao na kukabidhi hati za kusafiria mahakamani hapo.

Lakini siku hiyo Liyumba aliwasilisha hati yenye thamani ya sh milioni 882, hati ya kusafiria ambayo muda wake wa matumizi umekwisha, huku wadhamini wawili wakiwa hawana barua zilizosainiwa na mwajiri wao kama masharti yalivyotolewa na mahakama.

Februali 24 mwaka huu, Liyumba alifika mahakamani hapo na hakimu Msongo alisema hati 10 za wadhamini zenye thamani ya sh bilioni 55, ndizo zilizotumika kujaribu kumdhamini mshitakiwa huyo mara ya kwanza, lakini zilikataliwa baada ya kubainika kuwa zilikuwa na kasoro kubwa za kitaalam, huku nyingine zikidaiwa kuwa ni za kughushi.

Aidha alisema kutoka na hati hizo kuwa na kasoro hizo aliagiza zipelekwe Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na tayari Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) Robert Manumba aliliambia Tanzania Daima kuwa hati hizo ameishazipokea na tayari wameishaanza kuzifanyia uchunguzi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Machi 14 mwaka 2009

ALIYEMPIGA MWINYI AFUNGWA MWAKA MMOJA

*Asema adhabu aliyopewa ni sahihi

Na Happiness Katabazi

KIJANA Ibrahimu Said Sultani ‘Ustaadhi’ (26), aliyempiga kofi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi, Neema Chusi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya mshitakiwa huyo juzi kukiri kutenda kosa hilo.

Alipopewa nafasi ya kujitetea kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Sultani alisema kuwa, anaamini hukumu atakayopewa ni sahihi na itakuwa inatokana na mapenzi ya Mungu.

“Hakimu nashukuru kwa kunipa nafasi hii, mimi nakiri kwamba nimetenda kosa na ninaamini hukumu nitakayopewa na mahakama hii ni sahihii na itakuwa imetokana kwa mapenzi ya Mungu.

“Hata hivyo, naomba nipunguziwe adhabu, mimi ni kiumbe dhaifu wa Mwenyezi Mungu…kama adhabu hii nitapunguziwa Mungu ndiye atakuwa amepanga,” alieleza Sultani baada ya hakimu kumpa nafasi ya kujitetea kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo.

Awali, Sultani alianza kuomba dua kwa kutumia lugha ya Kiarabu, lakini Hakimu Chusi alimweleza kuwa haelewi na ndipo mshitakiwa huyo alipotaka atafutwe mkalimani.

Hata hivyo, hakimu alimweleza kuwa hawezi kufanya hivyo na kumtaka kusali kimyakimya.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Chusi alisema kwa kuwa mshitakiwa hajaisumbua mahakama kwa kuleta mashahidi na kwa kuzingatia kuwa ni kosa lake la kwanza, anamhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela.

“Kwa kuwa Sultani umekiri kosa mapema na kukiri kwako kumesaidia mahakama kutopata usumbufu wa kuletwa kwa mashahidi, na pia ni kosa lako la kwanza, nakuhukumu kwenda jela mwaka mmoja,” alisema Hakimu Chusi.

Mshitakiwa huyo alihukumiwa baada kukiri maelezo yote ya kosa aliyosomewa na Wakili wa Serikali, Monica Mbogo.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa, mshitakiwa huyo alionekana ni mtu mwenye huzuni, huku mama yake akiangua kilio.

Juzi, mshitakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza akikabiliwa na shitaka moja la shambulio la kudhuru mwili.
Ilidaiwa kuwa Machi 10, mwaka huu, katika ukumbi wa Dimond Jubilee alimpiga kibao shavu la kushoto Rais Mstaafu Mwinyi, ambaye siku hiyo alikuwa akihutubia kwenye Baraza la Maulid.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Machi 14 mwaka 2009.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi,Machi 14 mwaka 2009