MSHITAKIWA KESI YA ZOMBE AWAGEUKA WENZAKE

Na Happiness Katabazi

MSHITAKIWA wa 12 katika kesi ya mauji ya wafanyabaishara watatu na dereva taksi mmoja, inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe na wenzake tisa, Koplo Rajabu Bakari (46), amewageuka wenzake na kusema kuwa alishuhudia mauji ya marehemu hao yakifanyika msituni.

Washtakiwa wenzake katika ushahidi wao ambao tayari wamekwishautoa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mbele ya Jaji wa Mahakama ya Rufani, Salum Masati, kwa kauli moja walieleza kuwa mauji ya marehemu hao yalifanyika Sinza na ukuta wa Posta.

Koplo Rajabu ambaye jana alianza kutoa ushahidi wake saa nne asubuhi na kumaliza saa 9:58 jioni, alikuwa akiongozwa na wakili wake, Denis Msafiri ambaye aliileza mahakama kuwa mshitakiwa yeyote ambaye amewahi kuiambia mahakama hiyo kuwa mauji yalifanyika Sinza ameidanganya mahakama.

Rajabu alidai kuwa, mnamo Januari 14, mwaka 2006, yalifanyika mauji hayo katika eneo la msitu na kuongeza kuwa akiwa na marehemu Rashid Lema na Koplo Saad walikuwa ni miongoni mwa askari walioongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Kinondoni, mshitakiwa wa pili, ASP-Christopher Bageni kwenye gari aina ya Pajero mali ya Jeshi la Polisi.

Aliendelea kusema kuwa, kwa pamoja walitoka eneo la barabara ya Sam Nujoma na kuelekea msituni uliopo barabara ya Morogoro huku gari moja aina ya defender ambalo lilikuwa limewabeba marehemu ambao walikuwa hai, likiwafuata na baada ya kufika huko, Bageni na Saad walishuka kwenye gari na kuwaacha kwenye gari hilo wakiwa wamekaa.

“Baada ya kutuacha kwenye gari nikasikia mlio wa risasi nikatoka ndani ya gari na kuelekea kwenye defender lilipobaki kule msituni ili nijue kulikoni, nikaona mtu mmoja akitolewa kwenye difenda na kushushwa chini na Saad nikamshuudia akimshindilia na risasi.

“Baada ya kuona hilo nikaangalia chini na kukuta miili mingine mitatu ikiwa imelala chini kimya inavuja damu kisha Bageni akatuambia mimi na Saad twende tukapande kwenye lile Pajero tulikuja nalo na kisha kurudi kituo cha polisi Urafiki,” alidai Bakari na kufanya umati wa watu kushikwa na butwaa.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya mawakili Denis Msafiri na Rajabu Bakari:
Swali:Januari 14, 2006 unakumbuka uliingia kazini saa ngapi siku hiyo?
Jibu:Niliingia asubuhi na nilikuwa zamu.
Swali:Ulikuwa zamu na askari gani?
Jibu:Marehemu Rashid Lema na Saad ambaye hadi sasa hajakamatwa.
Swali:Unakumbuka mlipangwa kufanya doria maeneo gani na ilitakiwa muanze na mmalize muda gani?
Jibu:Kinondoni, Mwananyamala na Mikocheni.Tulitakiwa tuanze saa 12 asubuhi hadi 12 ya asubuhi ya siku inayofuata ya Januari 15, 2006.
Swali:Ulikabidhiwa silaha?
Jibu:Tulipewa silaha ila Lema na Saad walipewa SMG mimi nilipewa Bastola.
Swali:Mbali na hizo silaha mlizopewa na mlikuwa na usafiri wa aina gani?
Jibu:Tulikuwa na gari aina ya Pajero na ilikuwa ikiendeshwa na Konstebo Frank.
Swali:Mlikuwa na redio Call?
Jibu:Asubuhi unapokuwa doria hatupewi redio call ila jioni unapokuwa kwenye doria ndiyo tunapewa. Na tunapewa baada ya kutoa taarifa za matukio tulikutuna nayo mchana.
Swali:Katika hiyo doria yenu, nani alikuwa kiongozi wenu?
Jibu:Mimi.
Swali:Mlivyorudi jioni pale Oyesterbay Kituoni kutoa taarifa za doria ya mchana, taarifa hizo mlitoa kwa nani?
Jibu: Mkuu wa Upelelezi wa Kituo, ASP-Bageni.
Swali:Katika hiyo zamu yenu, nani alikwenda kwa huyo mshitakiwa wa pili kutoa taarifa hizo?
Jibu:Mimi.
Swali:Hiyo taarifa ulitoa kwa njia gani?
Jibu:Mdomo na wakati nikienda ofisini kwa Bageni nilikutana naye anashuka ngazi akaniambia twende nae tulipoegesha gari akaniambia tuingie kwenye gari na tukiwa njiani akaniambia tunaanzia barabara ya Sam Nujoma.
Swali:Alikwambia Sam Nujoma kuna nini?
Jibu:Aliniambia kuna tukio la ujambazi watu wameibiwa.
Swali:Mlivyofika hapo Sam Nujoma mlikuta nini?
Jibu:Tulikuta lori tani tatu mali ya kampuni ya BIDCO likiwa katika barabara hiyo na ndani yake ilikuwa na watu wanne, majina yao siku yafahamu ila mmoja alisema yeye ni dereva mwingine ni kuli (mbeba mizigo), na tulifika eneo hilo jua rasmi likiwa limeisha na giza lilikuwa halijaanza kuingia.
Swali:Wewe ulinzungumza na hao watu?
Jibu:Hapana ila Bageni ndiye alikuwa akiwahoji.
Swali:Ulisikia mahojiano yao?
Jibu:Nilisikia wakisema wao ni wafanyakazi wa BIDCO na waliporwa fedha zao siku hiyo na kabla ya kuporwa walitishiwa bastora na walisema waliporwa sh milioni tano.
Swali:Baada ya Bageni kuambiwa hayo nini kilifuata?
Jibu:Bageni alisogea pembeni kidogo akaanza kuongea nasimu yake ya kiganjani na siyo redio call ambayo alikuwa ameshika mkononi.
Swali:Baada ya kumaliza kuongea na simu nini kilifuata?
Jibu:Gari aina ya Pick Up la Kituo cha Polisi Chuo Kikuu lilikuja pale Samnujoma tulipokuwa tumesimama na ndani yake ilikuwa imebeba watu wanne ukiacha polisi ambapo watu hao walikuwa wamekalishwa chini na askari wamesima.
Swali:Unaweza kufahamu idadi ya askari walikuwemo kwenye hiyo Pick Up?
Jibu: Sajent James, PC Noel ambaye alikuwa mshitakiwa mwenzetu ila mahakama hii ilimuachilia huru.
Swali:Hao watu wanne waliokuwa wamekalishwa chini ulikuwa una wafahamu?
Jibu:Hapana.
Swali:Hiyo Pick Up iliambatana na na gari jingine?
Jibu:Ndiyo iliambana na gari jingine aina ya Saloon yenye rangi ya Daki blue.
Swali:Kulikuwa na gari jingine?
Jibu:Baada ya muda kidogo ilikuja gari jingine aina ya Saloon ,nyeupe.
Swali:Baada ya hao watu wanne kuja na hayo magari manne kusimama hapo Samnujoma, nini kilifuata?
Jibu:Nilimtambua mshitakiwa wa tatu, Makele ambaye alikuwa mkuu wa Upelelezi Kituo cha Urafiki, ,Koplo Abeneth na mwanamke ambaye sikumtambua kwa sura.
Swali:Hao waliokuwepo kwenye hiyo Saloon nyeupe walishuka kwenye gari?
Jibu:Ndiyo maana niliwatambua, walishuka kwenye gari.
Swali:Hiyo saloon ya daki blue ilikuwa ikiendeshwa na askari?
Jibu:Ndiyo.
Swali:Wale watu wanne walikuwa kwenye Pick Up ya polisi walishushwa kwenye gari?
Jibu:Hapana.
Swali:Ulipata kufahamu wale walikuwa wanakosa gani?
Jibu:Nilipata taarifa kuwa walikuwa wamekamatwa kwenye tukio la ujambazi na walikamatwa wakiwa na bastora na briefcase ye yenye milioni tano.
Swali:Baada ya maelezio hayo nini kiliendelea?
Jibu:Bageni alienda tena pempeni kuzungumza na simu na wakati huo mimi na Frank tulienda pembeni kidogo tulipokuwa tumeegesha gari ili tusubiri afande amalize kuongea na simu.
Swali:Wale watu wa BIDCO mliwashirikisha kuwatambua wale watu wanne?
Jibu:Bageni aliwashirikisha na dereva wa BIDCO aliwatambua na kusema wale ndiyo waliowafanyia uhalifu.
Swali:Baada ya Bageni kumaliza kuzungumza na simu alitoa maagizo gani?
Jibu:Niliona Defenda ya Osytebay imekuja pale na tayari giza lilikuwa limeishaingia kidogo na waliokuwa kwenye hiyo hiyo gari ni mshitakiwa Abeneth, Koplo John na Koplo Abubakar na gari hilo lilikuwa na namba za usajili TZR 6559.
Swali:Nini kilifuata?
Jibu:Bageni aliamuru wale watu wanne washushwe kenye Pick Up waingizwe hilo kwenye Defenda.
Swali:Hiyo amri ilitekelezwa?
Jibu:Ilitekelezwa wale watu wakaingizwa kwenye hilo gari na baadhi ya askari wa Chuo Kikuu wakapanda kwenye hiyo gari.
Swali:Baada ya watu wale kuamishiwa humo kulitolewa maelekezo gani tena?
Jibu:Dereva wa Chuo Kikuu PC Noel aliambiwa aende kituo cha Urafiki na yule dereva wa defenda aliingia kwenye gari na kuelekea njia ya ubungo.
Swali:Nyie mlielekea wapi?
Jibu:Bageni alikuwa akiongea na simu kwa mara ya tatu pale na baada ya bapo alituambia tusukume gari lililotuleta pale ,tukalisukuma likawaka tukaingia kwenye gari na akamtaka dereva tuelekea Ubungo na kweli tulielekea huko.
Swali:Wakati mkielekea Ubungo yale magari mengine yaliyotangulia kuondoka mlikuwa mkiyaona?
Jibu:Hapana kwani yaliondoka dakika kumi zilikuwa zimeishapita.
Swali:Mlipofika ubungo mataa mlielekea wapi?
Jibu:Dereva aliambiwa aelekee Kimara tukaingia kwenye kisima kimoja cha mafuta afande Bageni akatoa fedha mfukoni akalipa tukawekewa mafuta, tukaendelea na safari hadi Kituo cha polisi Mbezi Lous.
Swali:Mlipofika katika kituo hicho cha polis?
Jibu:Dereva wetu aligeuza gari akaliangaliza usawa wa kurudi mjini, Bageni akaingia ndani ya kituo kile, mimi na Lema tukabaki kwenye gari.
Swali:Alivyorudi ikawaje?
Jibu:Alirudi na askari mmoja aliyekuwa amevalia sare ya Jeshi la Polisi, ambaye alimpata pale kituoni na kisha askari huyo alipanda kwenye lile gari letu.
Swali:Yale mageri manne mliyokuwa nayo pale Samnujoma mlipofika hapo Mbezi Louis, uliyaona?
Jibu:Siku yaona.
Swali:Baada ya Bageni kurudi kwenye gari mlielekea wapi?
Jibu:Akamwamuru dereva tuelekee mbele kama tunaenda Morogoro, yaani kule msituni tulipoendaga na mahakama mwaka jana na na kabla hatujafika katika msitu huo kuna kituo cha mabasi.
Swali:Hukumuuliza Bageni mnakwenda wapi?
Jibu:Nashukuru mungu niliuliza dereva akaniambia tunaenda Mbezi Makabe, nikamuuliza swali la pili tunaenda kukamata, dereva akanijibu hajui, nikanyamaza kimya.
Swali:Unasema Bageni alionhea na simu , je alirudi kwenye gari?
Jibu:Hakurudi ila sekunde chache niliona defenda ng’ambo ya pili ya barabara ikiwa imepaki na sikuelewa ilikuwa imetokea kituo gani wala namba zake.
Swali:Baada ya Defenda hiyo kuja nini kiliendelea?
Jibu:Bageni alimuuliza yuke askari aliyevalia sare tunaelekea wapi,akamjibu mbele kule tulikokwendaga na mahakama siku hili na defenda ikawa inatufuata.
Swali:Uliweza kumuuliza Bageni mnakwenda wapi?
Jibu:Ni kosa kubwa kumuuliza afande ,aswali, tuliendelea na safari hadi tukamaliza nyumba zote zilizokuwa zinaonekana kisha tukaingia porini.
Swali:Mlivyonigia porini mlifanya nini?
Jibu:Yule askari aliyevaa sare alimwambia Bageni eneo lenyewe ndilo hili ila lina Chui sana.
Swali:Baada ya askari huyo kusema maneno hayo mlifanya nini?
Jibu:Tulienda mbele kidogo na gari letu na dereva akasimamisha gari.
Swali:Ilikuwa muda wa saa ngapi?
Jibu:Sikumbuki ila giza tayari lilikuwa limeishaingia.
Swali:Baada ya dereva wenu Frank kusimamisha gari nini kilifuata hapo msituni?
Jibu:Aligeuza gari na lile defender likageuzwa baada ya hapo Bageni,Lema na Saad walishuka kwenye gari.
Swali:Wewe je?
Jibu:Mimi na dereva na yule askari tuliyemchukua Mbezi hatukushuka kwenye gari.
Swali:Wakati wameshuka ile redia call ilikuwa wapi?
Jibu:Nilibaki nayo mimi nikaifungua nikasikia tukio la ujambazi la Kijitonyama.
Swali:Kule porini wakati Bageni , Saad na marehemu Lema walivyoteremka walisema wanaenda kufanya nini?
Jibu:Hawakusema.
Swali:Kutoka Pajero yenu ilipokuwa imesimama na ile defenda ni umbali gani kwa kukadilia?
Jibu:Kama mita 15-20.
Swali:Ulivyokuwa kule msituni hukuweza kutambua ni watu gani waliokuwa wamepakizwa kwenye ile defenda?
Jibu:Sikuweza kutambua.
Swali:Wakati unasikiliza redio call kule porini ulisikia nini?
Jibu:Nilisikia mlio wa bunduki ambapo mlio huo ulisika eneo lililokuwepo ile defenda na baada ya kusikia hivyo nilishuka kwenye gari nikajue kulikoni, ndipo nilikuta mtu mtu mmoja anashuka kwenye ile defenda na Saad akamtwangwa risasi na pia chini nikaona tayari kuna watu watatu wameishapigwa risasi.Hivyo yule nileyemuona akipigwa risasi ndiye alikuwa akimaliziwa.
Swali:Ulipita muda gani wewe kusikia mlio huo?
Jibu:Dakika moja haijapita.
Swali:Baada ya zoezi hilo la kupigwa risasi wale watu kukamilika nini kiliendelea?
Jibu:Miili ya watu wale ilipandishwa kwenye defenda na nilishuhudia kwa macho yangu ikipakizwa,mimi, Bageni ,Lema na Saad turiduni kwenye Pajero letu na yule askari aliyevalia sare alionekana kuchanganyikiwa na kile kitendo , tukamshusha njiani badala ya Kituo cha polisi Mbezi Lous.
Swali:Baada ya kumshusha mliekea wapi?
Jibu:Urafiki polisi, Bageni akaingia kituoni pale na sisi tulibaki kwenye gari na tulikaa kwa muda mrefu na alirudi akatuambia tuondoke turudi ofisini Oystebay, tukamshusha na sisi askari wa dogo tukaendelea na doria.
Swali: Miili ya marehemu ilipelekwa wapi?
Jibu:Bageni alimuru ipelekwe Muhimbili na kweli ilipelekwa.
Swali:Siku ya pili yake yaani Januari 15, 2006, mlifanya nini?
Jibu:Mimi na Rashid tulirudisha zile silaha ofisini na Saad akafungua jarada.
Swali:Shahidi 30,31 na 36 walisema kuwa tukio la kupigwa risasi Bunju, wewe unalifahamu?
Jibu:Ni kweli nalifahamu, tarehe sikumbuki ya tukio hilo ila tulilifanyabaada ya Januari 16.
Swali:Nani alienda kupiga risasi bunju?
Jibu:Siku hiyo nilifika ofisini na kukuta Lema na Saad wameishaingia kwenye gari , nikaambiwa niongozane nao nikafyatue risasi kwani afande Bageni anataka maganda haraka sana.
Swali:Baada ya kupokea hayo maelekezo mlikwenda Bunju?
Jibu: Tulielekea huko na kabla ya kuondoka nilishauri kwamba ni kwanini tusiende pale FFU Ukonda kwenye uwanja wa Range , ila nikalazimishwa zoezi la kutafuta maganda hayo likafanyike bunju.Kweli tulikwenda bunju tukapiga risasi tukarudi na maganda na nikamkabidhi yale maganda Bageni, akaniambia asante sana.
Swali:Ulivyokuwa msituni ukona maganda na na mkiwa njiani kutoka bunju hukuuliza maganda hayo ni kwanini yanatakiwa?
Jibu:Sikufahamu ni kwanini yanatakiwa na wala sikuona maganda kule msituni.
Swali:Unaikumba Tume ya Jaji Mussa Kipenka?
Jibu:Ndiyo kwani nilienda kuhojiwa na leo nasema ukweli maelezo niliyotoa kwenye tume hiyo ni tofauti kabisa naniliyotoa polisi kwani maelezo niliyotoa kwa Tume ya Kipenka tulipewa maelekezo tutoe maelezo ya uongo.
Swali:Nani aliwapa maelezo ya nini mkaongee kwenye tume hiyo?
Jibu:Zombe na maelekezo hayo ni kwamba tunakaseme kuwa mauji yalitokea Sinza ukuta wa posta na siyo msituni na binafsi sifahamu kama siku hiyo kulitokea tukio la ujambazi eneo la sinza ukuta wa posta.
Swali:Je kulikuwa na sababu yoyote ya nyie kutakiwa mtoe maelezo ya uongo kwenye Tume hiyo?
Jibu:Tuliambiwa maelezo yale ya uongo ndiyo msimamo wa jeshi la polisi hivyo atakaye saliti maelezo yale msalaba wote atabebeshwa yeye.

Swali:Siku Bageni anatoa ushahidi wake Februali mwaka huu, alidai kuwa alifahamu tukio hilo kupitia redia call na kwamba, wewe unasemaje katika hilo?
Jibu:Mtukufu Jaji, afande bageni ni muongo sana kwani yeye ndiye aliyetupeleka mimi na wenzake kule msituni mauji yalipofanyika.
Swali:Kumbuka kama uliwahi kumweleza Bageni kwamba mapambano ya risasi na marehemu hao yalitokea Sinza ukuta wa Posta?
Jibu:Nasema hivi sijui na wala sijawahi kumweleza hilo.
Jaji Massati aliairisha kesi hiyo hadi leo ambapo mshitakiwa wa 13, Festus Gwasabi ataanza kutoa ushahidi wake.
Mbali ya Zombe na Lema, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka wilayani Ulanga, Morogoro, na dereva teksi mmoja, ni pamoja na SP Christopher Bageni, SP Ahmed Makelle, Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Koplo Abeneth Saro, Rajabu Bakari na Festus Gwasabi..

Zombe na wenzake,wanadaiwa kufanya mauaji hayo Januari 14 mwaka 2006, eneo la Mbezi Luis, katika msitu wa Pande, ambapo waliwaua, Ephraim Chigumbi, Sabinus Chigumbi na Mathias Lukombe, ambao ni wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Ulanga na Juma Ndugu, ambaye ni dereva teksi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano,April 29,2009

WIZARA,NECTA ELIMU INAELEKEA WAPI?

Na Happiness Katabazi

SERIKALI kupitia Baraza lake lenye dhamana na mitihani (NECTA) imeshindwa kudhibiti uadilifu wa watendaji wake. Ithibati inajidhihirisha katika vitendo vilivyotamalaki vya uvujaji wa mitihani.

Pamoja na kwamba hiyo ni aibu na kashfa kwa kuwa uozo huo unahatarisha mfumo wa elimu na ubora wake kwa kuwaandaa watu mbumbumbu, hakuna hata mmoja aliyewajibika na anayeonekana kuwa na uelekeo wa kufanya hivyo, si Waziri mwenye dhamana wala viongozi wa NECTA, wote kimya, hali inayotoa uashirio kuwa mambo ni barabara.

Labda tujiulize, je, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, inaongozwa na mwanazuoni, Profesa Jumanne Maghembe, ambaye haoni wala kujua hatari ya kuvuja kwa mitihani?

Ingekuwa Tanzania ni taifa linaloendelea au linalotamani kupiga hatua kutoka katika hali yake ya sasa, Prof. Maghembe angelazimika kuwajibika pamoja na kufuatiwa kwa karibu zaidi na watendaji.

Lakini kwa kuwa Tanzania ni taifa limeamua kuishi gizani, waheshimiwa hao wanaendelea kupeta kwa kiburi kwa kuwa hata aliyewaitia kazi hiyo amenyamaza na hasemi jambo.

Sasa kana kwamba kashfa hiyo ya kuvuja kwa mitihani haitoshi, imeibuka kashfa nyingine kubwa zaidi na hadi sasa hakuna msimamo wala ufafanuzi wowote uliokwishatolewa.

Si nyingine, ni ile ya wahitimu wa kidato cha nne ambao walifaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza kutochaguliwa kuingia kidato cha tano katika shule za serikali kwa visingizio mbalimbali.

Kinachonishangaza zaidi ni kuona kuwa waliofauli kwa kiwango cha madaraja ya chini ya lile la kwanza (II na III) ndio wanaofanikiwa kupata shule hizo.

Viongozi wa wizara wamekuwa wakiwapatia wazazi wa wanafunzi hao majibu yasiyoridhisha, kwamba kuna awamu ya pili hivyo wametakiwa waandike barua kuomba nafasi za kuchaguliwa.

Sasa tatizo la jibu kama hili, linageuza kero kuwa kanuni. Mosi, hakuna tangazo lililotolewa nchini linalowataka wale ambao hawajachaguliwa waandike barua wizarani kuomba nafasi hizo.

Pili, utaratibu wa kujaza fomu za kuomba kuchaguliwa ‘selection form’ ambao umekuwa ukitumika, umetupwa, tumeamua kwamba watoto wawe wanaomba kuendelea na masomo kwa barua, tena shule za serikali, je huo ndio Utawala Bora ama Bora Utawala?

Hii njia iliyoamuliwa na Wakuu wa Baraza ni ya kifisadi na ni moja ya kero ya taifa katika awamu hii ya Rais Jakaya Kikwete. Iweje aliyefaulu daraja la kwanza alazimike kuomba kwa barua kuendelea na masomo licha ya kujaza selection form?

Wakati wenye daraja la pili, tatu na nne walichaguliwa kupitia selection form, iweje mtu akifaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza iwe tena ni adhabu, au ndiyo tumeamua kupalilia ujinga?

Hayo ni machache kati ya mengi yanayoashiria kuporomoka kwa kiwango cha elimu hapa nchini. Ni Wizara hiyo hiyo ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ndiyo inayosimamia mikopo ya wanafunzi, huko pia kuna vioja.

Mwanafunzi maskini ananyimwa mikopo wakati wale wanafunzi waliotoka kwenye familia tajiri wakipewa. Wakati huo huo wanafunzi ambao tayari maombi yao ya mikopo yameishadhibitiwa na kupewa mikopo mara moja, hujikuta wamekatwa na hawapelekewi tena mikopo bila maelezo yoyote.

Katika Bodi ya Mikopo ambapo fomu ya kuomba mikopo hutozwa fedha si chini ya sh 10,000-30,000, hivi hizo fedha wanalipa maskini au matajiri?

Tunaamini kuwa kutokana na matumizi yasiyo ya ulazima, kiasi kikubwa kinachotumiwa na bodi hiyo, kinaelekeza ndani ya bodi hiyo na kusahau maudhui ya kuundwa kwa chombo hicho.

Je, kwa aina hii ya matumuzi Watanzania tutafika?

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, April 29, 2009

SERIKALI YATETEA ADHABU YA KIFO

Na Happiness Katabazi

UPANDE wa Serikali katika kesi ya Kikatiba ya Kupinga adhabu ya kifo iliyopo katika Mahakama ya Kuu Kanda ya Dar es Salaam, umepinga kufutwa kwa adhabu hiyo kwasababu adhabu hiyo haivunji Katiba ya nchi.

Mlalamikaji katika kesi hiyo namba 67/2008 ni Chama Cha Wanasheria Tanganyika(TLS), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC),Sahringon-Tanzania Chapter dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegema Alex Mgongolwa, Fulgence Masawe, Chacha Boke na Julias Rugazi.

Pingamizi hilo liliwasilishwa juzi na Mkurugenzi wa Haki za Binadamu katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Methew Mwaimu mbele ya jopo la majaji wa tatu wanaongozwa na Jaji Robert Makaramba, Razia Shehke na Projest Rugazia.

Kwa mujibu wa hoja za upande wa serikali zinadai kuwa wanaomba adhabu hiyo iendelee kutumika kama sheria za nchi na kwamba adhabu si ya kiudhalilishaji na kamwe haitwezi utu wa binadamu hivyo kuimba mahakama hiyo itupilie mbali kesi hiyo ambayo imefunguliwa na mlalamikaji.

Baada ya upande wa serikali kuwasilisha pingamizi hilo kesi hiyo ilialishwa hadi Julai 22 mwaka huu , ambapo kesi hiyo itakuja kwaajili ya kutajwa.

Kwa mujibu wa hati ya madai, walalamikaji wanaiomba mahakama hiyo itamke kuwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa ni kinyume cha Ibara 4(2),12(2),13(1),13(6)a,d,e,14,26(2),64(5) na 107(a) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani inazalilisha utu wa binadamu ambao unakatwa katika Katiba.

Ombi la pili ni kwamba sheria husika ya adhabu hiyo inailazimisha mahakama inapomkuta mtu ana hatia ni lazima anyongwe na wala haitoa adhabu mbadala kwa mahakama wakati Katiba inasema kazi ya utoaji wa haki na adhabu zake ni kazi ya mahakama.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, April 28, 2009

WAMILIKI MTANDAO WA ZE UTAMU WASAKWE

Na Happiness Katabazi

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Chama cha Mapinduzi, karibu wakati wote imekuwa na kasumba ya kutotaka kupokea mawazo na changamoto zinazotolewa na wananchi wake, hata kama mawazo hayo yakifanyia kazi, yataleta tija kwa taifa.

Ni serikali hii kwa miaka kumi sasa, imekataa kabisa kufanyia kazi mawazo ya wasomi na wananchi wa kawaida waliokuwa wakiitaka kwamba, kabla haijakubali kujiingiza kwenye mfumo wa Utandawazi, kwanza ni lazima ihakikishe inaandaa wananchi wake kikamilifu kuingia kwenye mfumo huo.

Miongoni mwa viongozi waliokuwa wakishupalia taifa letu kuingia kwenye mfumo huo, ambao nadiriki kusema ni mzuri, ila haukustahili kuja kabla wananchi kuandaliwa.

Alikuwa, ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa na vingozi wa serikali yake ya Awamu ya Tatu na wale chama chake cha CCM.

Naamini, wakati waking’ang’ania jambo hili kuingia nchini bila ya kuwaandaa wananchi kikamilifu kumudu mfumo huo, hawakujua kwamba ipo siku, kunaweza kusababisha kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili, viongozi na wananchi kudhalilishwa utu wao na pengine kuhatarisha usalama wa nchi. Hii inasikitisha mno.

Lakini, Watanzania tukumbuke wakati serikali imeridhia kwenye mfumo huo wa utandawazi, lakini mwaka juzi wakati Dk.Willbroad Slaa alipowasilisha hoja bila mafanikio ya kutaka kuwataja mafisadi uliofanyika katika Benki Kuu ya Tanzania.

Serikali kwa upande wake, ilisimama kifua mbele na kusema kuwa kamwe haifanyiikazi taarifa zinazopatikana katika mtandao.

Baada ya kuona Dk. Slaa amakomalia hoja hiyo na kuamua kwenda kuimwaga pale viwanja vya Mwembe Yanga-Temeke na moto kusambaa nchi nzima na hatimaye serikali ikaunda tume kuchunguza ubadhilifu nayo ikagundua na kisha leo hii tunaona baadhi ya wahusika wa kashfa hiyo wamefikishwa mahakamani.

Sasa basi, wiki hii katika mtandao wa www.zeutamu.com mtandao ambao umejipambanua kwaajili ya kupachika picha za utupu za watu wa kada zote na wanaotembelea mtandao huo uchangia mawazo yanayohusu maisha binafsi ya faragha za watu, hakika hivi sasa umepata umaarufu kutokana watoto, hata watu wazima wenye heshima zao na baadhi ya viongozi kuutembela japo kwa kujificha.

Na wakati mtandao huo ukiendelea kujipambanua mamlaka husika zimekuwa zikiukenulia meno mtandao huu hadi wiki hii ulipotundika picha ya kumdhalilisha rais wetu, ndipo mtandao huo umedhibitiwa kwani hivi sasa hata ukiufungua aufunguki.

Mtandao huo wiki hii ulitundika picha chafu yenye sura ya Kikwete, ambayo picha hiyo inamdhalilisha rais wetu, sisi wananchi anaotuongoza na familia yake kwa ujumla.

Na tayari wataalamu wa masuala ya kompyuta wametanabaisha kuwa picha ile chafu ni ya kutengeneza.

Binafsi, nimekuwa ni miongoni mwa wananchi ambao tumekuwa tukitofautiana kimsimamo na rais na serikali yetu na tumekuwa tukipingana nao kwa kutoa maoni yetu kwa njia sahihi.

Na tumekuwa tukifanya hivyo lengo likiwa moja tu kuikumbusha serikali majukumu yake kwani kuna mambo mengine yanafanyika mitaani na serikali inakuwa haina habari.

Lakini, Watanzania tujiulize hadi kufikia hatua hii ya siyo rais peke yake anadhalilishwa kwenye mitandao huo na wananchi wengine wamekuwa wakidhalilishwa, mamlaka husika zinakuwa wapi ?

Kweli Idara yetu ya Usalama wa Taifa, Interpol na wale wataalamu wa masuala ya kompyuta ambao wamesomeshwa na kodi zetu wanashindwa kudhibiti mfumuko huu wa kutundika picha za utupu kwenye mitandao, halafu tunaendelea kuwacheka.

Aingii akilini kabisa Makachero wetu ambao wamesomea fani ya Sayansi ya Teknolojia wanashindwa kutambua mitandao ya aina hii inamilikiwa na wa kina nani je ni watanzania wenzetu au raia wa kigeni wameamua sasa kuanza kutufanyia chokochoko kuanza kudhalilisha viongozi wetu na wananchi wake au makachero wetu wanashindwa kutumia teknolojia kuidhibiti mitandao ya aina hii?

Katika hili la mfumuko wa mitandao inayotundika picha chafu niwe mkweli kwamba Njagu namba moja IGP-Said Mwema na Shushushu namba moja Othman Rashid mnatuangusha, lakini hamjachelewa bado mnayonafasi ya kuakikisha mnapambana na tatizo hili ama kwakushirikiana na wataalamu wa nchi marafiki wa taifa letu au kuwapeleka vijana wenu kusoma.

Tusinyoshee vidole tu mitandao hiyo,pia kuna baadhi ya magazeti na redio hivi sasa vimevuka mipaka na kuchapicha picha na kutangaza mambo yasiyofaha mbele ya jamii, na mamlaka husika wanafumbia macho.

Nasema kuna haja gani ya kuruhusu mfumo kuingia nchini wakati hatujaandaa watalaamu wakuweza kukabiliana na mfumo huo pindi unapotaka kuleta madhara kwa jamii yetu?

Kikwete siyo kiongozi mkuu wanchi peke yake ambaye amekumbwa na kadhia hiyo, hata Rais mstaafu Mkapa akiwa madarakani mwaka 2005, gazeti hili liliwahi kutoa picha ya kutengeneza ilichotwa kwenye mmoja wa mtandao ilikuwa ikimuonyesha Mkapa amekaa kizimbani na hakimu akimuuliza maneno haya.

“Mr. Mkapa, this is the 3rd time I see you in this court for the same crime, that is asking for loan and not repaying, You should be hanged to death.

Rais Mkapa kwa mujibu wa picha hicho iliyomwonyesha kaketi kizimbani, alimjibu hakimu huyo maneno yafuatayo: “Don’t you give discount to your Regular Clients?
Picha hii iliiponza gazeti hili la Tanzania Daima na kusababisha Idara ya Habari Maelezo, kulifunga kwa siku kadhaa.

Lakini yote hii inatokana mfumo wa mzima wa uongozi, jamii kukosa uzalendo, wameishiwa uwezo wa kufikiria na pia ile zana ya uwajibikaji wa pamoja hakuna tena.

Naamini kama serikali yetu ingekuwa ikiwajibika kwa pamoja na wakaondokana na makundi, visasi na uchumia tumbo mambo yangeenda vizuri na yote haya ingekuwa ni historia.

Leo hii kukaa na watoto au wazazi wako kusikiliza redio, kuangalia Tv imekuwa ni wasiwasi unakutana na matangazo ambayo unasikia na kuona aibu.

Hivyo, napenda kutoa pole kwa Rais Kikwete,na watanzania kwa ujumla kwani ni kiongozi wetu amedhalilishwa, lakini achukulie kitendo hicho kichafu ni changamoto vyombo vya ulinzi na usalama wa vya nchi.

Kwamba, viamke usingizini na viache ubinafsi wa kutumia ujuzi waliyoupata kwa manufaa yao badala ya taifa.

Hata kama kiongozi wetu ana udhaifu wake kiutendaji au ule wa kibinaadamu kwa mambo kadhaa yanayohusu taifa hili, hatupaswi kumdhalilisha kiasi hiki.

Kitu cha msingi ni kuendeleza utamaduni wetu wa kupingana kwa hoja na vielelezo na si vurugu na kutundikana picha za utupu kwenye mitandao.

Kama tutakataa kubadilika sisi wenyewe wananchi tukae tukijua tunaipeleka nchi yetu kuzimu kwasababu, watoto wa sasa wanatumia huduma ya kompyuta kwaajili ya kupataa taarifa mbalimbali za kimasomo au burudani lakini endapo tutaacha kutumia uhuru huu wa kuwa mtandao kujadili matatizo yanayoikabili tukajiingiza kwenye upuuzi huu niwazi hatufiki kokote.

Huru wa kujieleza ambao umeanishwa kwenye Katiba ya nchi yetu kila mtanzania kwa nafasi yake autumie vizuri na si vinginevyo kwani hakuna uhuru usiyo na mipaka.

Wakati tujadili hayo yote, tujiulize je yale madhambi yaliyokuwa yakifanywa na kundi la wanamtandao katika mchakato wa kutafuta mgombea urais mwaka 2005,dhambi ya kupakana matope, kuzuliana kashfa miongoni mwa wagombea, kumuundia Dk.Salim Ahmed Salim picha iliyokuwa ikionyesha yeye aliwahi kuwa mwanachama wa Hizbu,Je ndiyo zimeanza kumtafuna rais wetu?

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, April 26, 2009

MAHAKAMA YARUHUSU MKUTANO TLP KESHO

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana iliruhusu uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), ufanyike kama ulivyopangwa.

Amri hiyo ilitolewa jana jioni na Jaji Geofrey Shaidi baada ya kusikiliza ombi la mwanachama wa chama hicho, Stanley Ndamugoba, anayetetewa na wakili Alex Makulilo, dhidi ya Baraza la Udhamini la TLP, linalotetewa na Desidely Ndibalema.

Kwa mujibu wa hati ya madai, mwombaji alifungua kesi ya madai na kuwasilisha maombi hayo ya zuio la muda juzi na katika ombi hilo, aliomba mahakama hiyo itoe amri ya kuzuia kufanyika kwa mkutano mkuu wa TLP, unaotarajiwa kufanyika kesho.

Jaji Shaidi alisema baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili za kuhusu kukubali au kutokubaliwa kwa ombi hilo, amebaini kuwa ombi la mlalamikaji halina msingi, kwa sababu mkutano utakaofanyika kesho, tayari chama kilishatumia gharama kuuandaa.

“Kwa sababu hiyo, nalitupa ombi la mwombaji na ninaagiza uchaguzi huo ufanyike kama ulivyopangwa na kesi ya msingi iliyopo mahakamani, itaendelea pindi mtakapopewa tarehe,” alisema Jaji Shaidi na kufanya umati wa wanachama waliokuwa wakiongozwa na Mwenyekiti wa TLP anayemaliza muda wake, Augustine Mrema, kuripuka kwa shangwe.

Awali, wakili wa mwombaji, Makulilo aliwasilisha hoja ya kutaka uchaguzi huo uzuiwe hadi kesi ya msingi iliyopo mahakamani itakapomalizika.

Akijibu hoja hizo, wakili wa utetezi, Ndibalema, alidai ombi hilo halina msingi wa kisheria kwa kuwa limeletwa chini ya kifungu kisicho sahihi cha Sheria ya Madai, kwani hakiiruhusu mahakama kutoa amri zilizoombwa na mlalamikaji.

Ndibalema aliendelea kudai kuwa, hata hivyo mlalamikaji si mwanachama wa TLP na kwamba kadi yake ya uanachama imeghushiwa na katika kumbukumbu za chama, hazionyeshi kama waliwahi kuwa na mwanachama mwenye jina hilo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, April 25, 2009

JENERETA NI MUHIMU MAHAKAMANI

Kulia ni Wakili wa Serikali Biswalo Mganga na wakili mwenzake Michael Lwena,wakifurahia jambo muda mfupi baada ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Addy Lyamuya kuairisha kesi ya wizi wa sh milioni 207 za Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania, kwasababu ya umeme kukatika.Kukatika kwa umeme kunasababisha kesi za EPA kushindwa kuendelea kwasababu kompyuta maalum na vinasa sauti zimekuwa zikitumika kurekodi mwenendo mzima wa kesi hizo.(Picha na Happiness Katabazi)

UMEME WAKWAMISHA KESI YA EPA

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ilishindwa kuendelea kusikiliza ushahidi katika kesi ya wizi wa sh milioni 207 wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) inayomkabili Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Kigoma, Rajabu Matanda na wenzake watatu kutokana na kukatika kwa umeme.

Hakimu Mkuu Mkazi wa mahakama hiyo, Addy Lyamuya, jana alialazimika kuahirisha kesi hiyo baada ya kukatika umeme wakati shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka katika kesi hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Sifael Mkonyi, alipokuwa akitoa ushahidi wake.

Alisema analazimika kuahirisha kesi kwa kuwa mwenendo wa kesi hiyo hautaweza kurekodiwa kutokana na kukatika kwa umeme.

Awali akitoa ushahidi wake, Mkonyi aliyekuwa akiongozwa na Wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus Boniface, alidai alimfahamu Maranda Machi 7 mwaka jana alipofika katika Ofisi ya Kikosi Kazi Mikocheni na kumchukua malezo yake.

Alidai alifuata taratibu zote wakati akichukua maelezo ya Maranda na kuiomba mahakama ipokee maelezo hayo kama kielelezo katika kesi hiyo.

Hata hivyo, ombi hilo lilipingwa na Wakili wa utetezi, Magura Magafu, kutoyapokea maelezo hayo kwa sababu katika maelezo hayo kuna sehemu inayomtaka mshitakiwa asaini pindi anapomaliza kuchukuliwa maelezo yake, lakini mteja wake hakusaini.

Wakati Magafu akiendelea kupinga suala hilo ndipo umeme ulikatika, hali iliyomlazimu Hakimu Lyamuya kuahirisha kesi hiyo.

Mbali na Maranda, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Farijala Hussein na maofisa wa BoT, Iman Mwakosya, Ester Komu na Bosco Kimela.

Hii ni mara ya pili kwa kesi hiyo kuairishwa kutokana na kukatika kwa umeme.

Maofisa wa mahakama wakizungumza na Tanzania Daima kwa masharti ya kutotajwa majina, walisema hata wao wanakerwa na uongozi wa mahakama kushindwa kufunga jenereta katika mahakama hiyo hasa ikizingatiwa kuwa ni mahakama kubwa na inapokea kesi mbalimbali.

“Hii ni aibu na uongozi wa mahakama unapaswa utambue hiki ni chombo cha serikali ambacho kipo kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wake…..yaani huko mitaani saluni zina jenereta, lakini mahakama kama hii haina ni aibu kwa kweli,” alisema mmoja wa maofisa hao.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, April 25, 2009

MAHAKAMA YAMNG"ANG"ANIA LIYUMBA

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imekataa kufuta kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba na Meneja Miradi wa benki hiyo, Deogratius Kweka.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Walirwande Lema, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutolea uamuzi wa ama kuifuta au la.

Uamuzi huo ulitokana na ombi la wakili wa Liyumba, Majura Magafu ambaye Machi 2, mwaka huu, aliwasilisha mahakamani hapo ombi la kutaka mahakama hiyo itumie kifungu cha 225(1-4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai 2002, kinachotamka kuwa, ndani ya siku 60, upelelezi kesi husika uwe umekamilika, vinginevyo ifutwe.

Lema alisema baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili, amebaini kuwa licha ya siku 60 kupita na upalelezi wa kesi hiyo kutokamilika, haoni kama haki za msingi za washitakiwa zimevunjwa.

“Kwa sababu hiyo, natupilia mbali ombi la wakili wa utetezi la kutaka niifute kesi hii na ninatoa amri ya kuuongezea muda upande wa mashitaka ili waweze kukamilisha ushahidi, na tayari ulishaleta ombi la kuongezewa muda,” alisema Lema na kuahirisha kesi hiyo kwa nusu saa.

Mbali ya kusikiliza ombi hilo na kulitupilia mbali, mahakama hiyo pia ilisikiliza ombi lingine la upande wa utetezi la kutaka washitakiwa waachiliwe huru kwa madai kuwa hati ya mashitaka ina kasoro.

Wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus Boniface ambaye alikuwa akisaidiana na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Frederick Manyanda na Wabuhanga, Beni Likoni, Prosper Mwangamila na Tabu Mzee, alidai kuwa waombaji walileta ombi lao la kutaka mahakama hiyo itupilie mbali hati ya mashitaka pamoja na kibali cha DPP cha kufungua kesi hiyo kwa madai kuwa ina dosari za kisheria.

Aliendelea kudai kuwa, kifungu cha 135 walichokitumia mawakili wa utetezi, kingeweza kutumika endapo tu wangeainisha ni kifungu gani kidogo ndani ya kifungu sentensi katika kifungu hicho, lakini wao wametumia kifungu hicho kavu.

“Kutumia kifungu kisichohusika na kutochagua kifungu kwa ukamilifu, kisheria hakuna suluhu, hivyo upande wa mashitaka unaiomba mahakama hii itambue kuwa ombi la utetezi ni mfu na yanatakiwa yatupiliwe mbali haraka iwezekanavyo kwa sababu wametumia vifungu visivyo sahihi,” alidai Boniface.

Aidha, Wakili Magafu aliyekuwa akisaidiana na Profesa Gamalieli Mgongo Fimbo, Hurbet Nyange na Hudson Ndyusepo, aliinuka na kuanza kujibu hoja hizo na kudai kuwa pingamizi la Boniface halina msingi na lina lengo la kuchelewesha kesi hiyo na kwamba amezitoa ili kupima upepo wa mahakama unavyovuma.

Magafu alidai kuwa, nao upande wa mashitaka umeshindwa kuonyesha ni kifungu gani wameshindwa kukitumia kuwasilisha maombi yao na kuongeza nao upande wa mashitaka umeonyesha haujui kifungu hicho na kusisitiza kuwa, maombi hayo yameletwa kwa njia sahihi na kuiomba mahakama itupilie mbali pingamizi la upande wa mashitaka.

Baada ya kusikiliza malumbano hayo makali ya kisheria, yaliyodumu kwa saa moja na nusu, Lema aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 31, ambapo itakuja kwa ajili ya kutolea uamuzi maombi hayo.

Machi 30, mwaka huu, Lema alianza kuendesha kesi hii baada ya Hakimu Mkazi, Hadija Msongo ambaye ndiye alikuwa nayo tangu ilipofunguliwa Januari 27, mwaka huu,
kujiondoa baada ya jamii kupitia vyombo vya habari kulalamikia dhamana ya Liyumba.

Februari 17, mwaka huu, hakimu Msongo alimwachia kwa dhamana iliyozua utata Liyumba.

Moja ya masharti ambayo hayakutimizwa na Liyumba, ni kuwasilisha mahakamani hati zenye thamani ya sh bilioni 55, wadhamini wawili wa serikali wakiwa na barua kutoka kwa waajiri wao na kukabidhi hati za kusafiria mahakamani hapo.

Lakini siku hiyo, Liyumba aliwasilisha hati yenye thamani ya sh milioni 882, hati ya kusafiria ambayo muda wake wa matumizi umekwisha, huku wadhamini wawili wakiwa hawana barua zilizosainiwa na mwajiri wao kama masharti yalivyotolewa na mahakama.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, April 24, 2009

WASHTAKIWA KESI YA NBC UBUNGO WANA KESI YA KUJIBU

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema washtakiwa 11 wanaokabiliwa na kesi ya wizi wa kutumia silaha na kupora sh milioni 1.6 mali ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Tawi la Ubungo, wana kesi ya kujibu.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Pelagia Khaday, alisema hayo jana wakati akitoa uamuzi wake baada ya pande zote mbili katika kesi hiyo kuwasilisha hoja za washtakiwa iwapo wana kesi ya kujibu au la.

Khaday alisema licha ya ushahidi katika kesi hiyo kutolewa kwa vipande vipande, mahakama hiyo imeona ni vema ikawapatia nafasi washtakiwa hao kujitetea.

“Kwani baadhi ya mashahidi waliwatambua baadhi ya washtakiwa katika gwaride la utambulisho kwamba siku ya tukio walikuwepo na baadhi ya vielelezo vimeonyesha kuwa vinawahusu washtakiwa hivyo nimeona ni vema washtakiwa nao wakapewa nafasi ya kujitetea,” alisema Hakimu Khaday.

Wakati akisema hayo ghafla ndege wawili walifika kwenye jarada la kesi hiyo alilokuwa akilisoma na kufanya hakimu huyo kutaharuki hali iliyosababisha wananchi waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo kushtuka lakini hakimu huyo alisema yupo salama na kwamba hilo ni jambo la kawaida.

Kutokana na uamuzi huo, alisema washtakiwa hao wataanza kujitetea Mei 21.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Februari 2, mwaka 2006 saa tatu asubuhi katika NBC tawi la Ubungo, waliiba sh milioni 168,577.84 mali ya benki hiyo.

Wakati huohuo, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Victoria Nongwa amemhukumu kifungo cha maisha jela, muosha magari wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Robert Daudi(29) baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka tisa.

Nongwa alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote ameridhika kuwa mshtakiwa huyo alifanya kitendo hicho.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo Wakili wa Serikali, Ntuli Mwakahesya, aliomba mahakama hiyo itoe adhabu kali dhidi ya mshtakiwa, kwani vitendo vya namna hivyo vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku hali inayosababisha kuwaharibu kisaikolojia watoto waliotendewa vitendo hivyo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, April 24, 2009

ROGER MUZUNGU

Kilio chetu cha kurejeshwa tuzo za Kili kimesikika
*Tumefanikiwa kutwaa tuzo ya wimbo bora wa mwaka huu

Na Happiness Katabazi

“TIMU ya taifa, hatutaki zaidi, tunatosheka na afadhali.”

Si kila mwanamke anaye kwenda baa ni malaya, si kila mwanamke anayeingia baa anajiuza, wengine waenda baa ni kwa starehe zao binafsi, kwenye pochi zao wana fedha zao za matumizi. Fedha za kula, fedha za kunywa na usafiri wa kurudi majumbani eh, kwao.

“Eh nashindwa kuelewa juu ya nini binadamu twakuwa na imani potofu? Hasa kwa dada zetu twawafikiria vibaya. Mwanamke akienda kazini hawamsemi lakini akienda kuangalia FM Academia , tu wanachonga chonga na kumuona malaya why…kwanini”?

Hayo ni baadhi ya mashairi yanayopatikana katika kibao cha ‘Heshima kwa Wanawake’ toka Bendi ya FM Academia ‘wazee wa ngwasuma’ ambacho kimewapatia heshima ya kutwaa tuzo ya wimbo bora wa mwaka, katika mashindano ya muziki hapa nchini maarufu kama ‘Kill Awards Tanzania’.

Kufuatia hatua hiyo, gazeti hili liliamua kumtafuta mtunzi wa kibao hicho, Roger Muzungu, ambapo hakuna ubishi kuwa kadiri siku zinavyosonga mbele kinazidi kujipatia umaarufu na kubadili mtazamo wa jamii kwa mtoto wa kike.

Tangu enzi za mababu zetu ilijengeka dhana kwamba mtoto wa kike ni dhaifu na kwamba hawezi kufanya jambo lolote bila kupata msaada wa mwanamume.

“Nathubutu kusema dhana hii ilikuwa ikirutubisha mfumo dume lakini katika karne hii wanaharakati, wanawake wenyewe wamesimama kidete kuhakikisha dhana kama hizo, mfumo dume unatokomezwa na kwa kiasi fulani tunaanza kuona mafanikio ya vita hiyo kwani hivi sasa wanawake wengi wameteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali na wamekuwa wakiendesha familia zao bila kutegemea msaada wa mwanamume,” alisema Muzungu.

Kwa wale wanaofuatilia bendi za muziki wa dansi za hapa nyumbani, utakubaliana nami kuwa Muzungu ni miongoni mwa wanamuziki wanaojiheshimu, na mwenye subira, hali iliyomfanya hata kupata mafanikio kwenye fani hiyo ya muziki kutokana na vibao vyake kutamba.

Kwa wale msiomjua Muzungu, mwanamuziki huyo alianza kutumikia bendi ya Dimond Sound ‘Ikibinda Nkoi,’ waliokuwa na maskani yao ukumbi wa Silent Inn, wakati huo akiwa mwanamuziki na mwalimu wa wanenguaji wa bendi hiyo lakini kwa bahati mbaya kuna baadhi ya nyimbo alizitunga akiwa na bendi hiyo hazikuweza kurekodiwa hadi bendi hiyo iliposambaratika.

Roger Muzungu a.k.a ‘mutu ya zamani’, ambaye ni mwanamuzi wa FM Academia, anasema anajisikia ni mwenye furaha wimbo alioutunga kupata tuzo ya wimbo bora wa mwaka 2009.
Anasema amefurahi sana kwani imethibitisha ni jinsi gani Watanzania kwa ujumla wamekubali mashairi yaliyomo kwenye wimbo huo ambao anasema ulimchukua miaka miwili kukaa chini na kuutunga na kisha kuukabidhi kwenye bendi yake na kufanyiwa mazoezi na wanamuziki wenzake na kisha kurekodiwa na kuanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya utangazaji.

“Nawashukuru wapenzi wa bendi yetu ya FM Academia ambao tumekuwa nao bega kwa bega na wote walioupigia kula wimbo huo hadi kula zikatosha na hatimaye wimbo huu ukapata tuzo na tunawaahidi kuwa muda si mrefu tutatoa vibao vipya vikali hivyo mkae mkao wa kula,” anasema Roger Muzungu kwa kujiamini.
Anasema huo ni wimbo wake wa pili kuutunga akiwa na bendi hiyo, wimbo wa kwanza ulikuwa, ‘Heinken Ngwasuma’ uliopigwa kwa mtindo wa sebene.”

Muzungu anasema Juni mwaka huu, bendi yake inatarajia kukamilisha albamu na nyimbo zipo tayari na moja ya nyimbo hizo ni Heshima kwa Wanawake, Vuta nikuvute uliotungwa na Elombee, Jusmine wa Nyoshi El Saddat, Fadhira kwa Mama wa Katumbi Jesus, Matatizo ya Yangu wa Toscanie na Generique ambao umetungwa kwa kushirikisha wanamuziki wote wa bendi hiyo na utakuwa na maadhi ya sebene.

Anasema baadhi ya nyimbo nyingine ambazo zitaingia kwenye albamu hiyo, bado hazijapangiwa majina.

Kuhusu bendi yao kuondolewa kwenye mashindano ya Kill Awards mwaka jana kwa sababu bendi yao ni ya Wakongo, anasema walilamikia wazi wazi kipengele hicho na kwa sababu bendi hiyo haina Wakongo peke yao pia ina wanamuziki Watanzania.

“Tunashukuru kilio chetu kimesikika hatimaye katika mashindano ya mwaka huu, Kill Award iliondoa kipengele hicho hivyo kufanya bendi yetu kushiriki mwaka huu, na mungu akasaidia tukafanya vizuri” anasema Munzungu.

Anasema wimbo wake unapendwa hata na wanaume wamekuwa wakiunga mkono mashahiri yake na kwamba aliamua kutunga wimbo huo kwani jamii ilikuwa na mtazamo hasi kwa wanawake kwamba wakienda baa au kumbi za starehe wanaonekana ni wanawake wasi na maadili mema na ni malaya.

Kumbe hali sasa ni tofauti kwani wanawake hivi sasa wengine wamepata elimu, wanajibidiisha kwenye biashara za kuwaingizia vipato halali, hivyo baadhi ya wanawake siku hizi utawakuta wanakutana pamoja kwenye kumbi za starehe kubadilishana mawazo na kuagiza vinywaji kwa gharama zao bila ya kutegemea wanaume, hatua hii ni muhimu katika harakati za kusaka usawa kijinsi barani Afrika.

Muzungu anawahasa wanamuziki wenzake kuwa waache chuki zisizo na maendeleo bali wawe wabunifu katika fani ya muziki ili wanamuziki wote waweze kukuza muziki wa Tanzania.

Akizungumzia mchakato wa Kill Awards Tanzania, mwaka huu, Muzungu anasema yeye binafsi anaona haki imetendeka kwa sababu hata yeye alikuwa ana fikira kuwa bendi zenye wanamuziki kutoka Kongo, zingebaguliwa, lakini hilo halikutokea kwani mambo yamekwenda vizuri kama yalivyopangwa.

Aidha, anatoa changamoto kwa waandaaji wa Kill Awards kwamba wajitanue zaidi kwa kushirikisha bendi na nyimbo za wanamuziki kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EA), kwasababu kushirikisha nchi hizo kutaimarisha mahusiano mema kwa wanamuziki kutoka nchi hizo.

Pia kutaitangaza Kill Awards na pia kuwafanya wanamuzi na bendi kutoka nchi hizo kuongeza bidii katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Hata hivyo anazitaka zile bendi au wanamuziki ambao hawajabahatika kupata tuzo katika mashindayo yaliyopita wasikate tamaa, bali waongeze bidii na waendelee kushiriki, kwani ipo siku nao watapata tuzo, kwani tuzo haziwezi kutolewa kwa wanamuziki na bendi zote zilizoshiriki katika shindao hilo kwa wakati mmoja.

Muzungu ambaye hujivuma vilivyo awapo jukwaani, anamaliza kwa kutoa shukrani zake za dhati kwa wale wote waliofanikisha FM Academia waliotwaa Tuzo ya wimbo bora wa mwaka.

Hii ni mara ya pii kwa FM Academia ambayo imejizolea mashabiki ndani na nje ya nchi kutwaa tuzo za Kill Awards, mwaka juzi katika mashindano ya Kill Awards, bendi hiyo kupitia albamu yake ‘Dunia Kigeugeu’ ilipata tuzo ya albamu bora.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, April 18, 2009

MRAMBA AMLIPUA MKAPA

*Adai Ikulu ndiyo iliyotoa vibali vya Alex Stewart
* Wakili wake adai alikuwa mtumishi mwaminifu

Na Happiness Katabazi

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Basil Mramba, amekiri kutoa vibali vya msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart, baada ya Ofisi ya Rais Ikulu kuridhia afanye hivyo.

Mramba ambaye ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7, alikiri hilo wakati akisomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Mramba ambaye ni mteja wake, Wakili Hurbet Nyange mbele ya Hakimu Mkazi, Henzron Mwankenja, alidai mteja wake alikuwa mwaminifu na kusisitiza kuwa, alitoa vibali hivyo baada ya kuagizwa kufanya hivyo na Ikulu.

Nyange ambaye alikuwa akizungumza kwa ukali, alikiri Mramba kumuandikia barua Gavana wa Benki Kuu ya kumtaka iilipe Kampuni ya Alex Stewart, lakini alifanya hivyo baada ya Ikulu kuridhia, kwani mteja wake hakuwa na mamlaka ya kuidhinisha malipo hayo.

“Kwa faida ya mpelelezi wa kesi hii, nakubali mteja wangu alitoa vibali vya msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo, ila nataka ieleweke hivyo kuwa alitoa vibali hivyo baada ya Ikulu kuridhia.

“Pia nakataa serikali haijapata hasara kwa sababu hasara hiyo imetokana na mkataba wa kijinga wa Kampuni ya Alex Stewart.

“Kwa hiyo, maelezo mengine yaliyosalia hatuyakubali kabisa kwa kuwa yamejaa sukari na chumvi na uongo na ukweli…hatuyakubali, sasa kuna hatari nikiyakubali tutakuwa tunakubali yale ya ukweli na uongo. Kwa usalama wetu tunakataa maelezo yote,” alidai Nyange kwa sauti ya ukali na kusababisha mawakili wenzake kumkatisha mara kwa mara bila mafanikio.

Akisoma maelezo hayo, Mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Joseph Holle ambaye alikuwa akisaidiana na Tabu Mzee kutoka Takukuru na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Fredrick Manyanda, alidai Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali ya awamu ya tatu, Daniel Yona, na Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Uchumi na Fedha, Gray Mgonja, walikuwa watumishi wa umma na wenye nyadhifa za juu serikalini, maelezo ambayo washitakiwa wote waliyakubali.

Holle alidai washitakiwa hao wakiwa na nyadhifa hizo, walikuwa na jukumu la kuwa waaminifu na makini katika majukumu waliyokabidhiwa kisheria.

Alidai Machi 3, mwaka 2003 mshitakiwa wa pili (Yona), aliandika barua yenye kumbukumbu namba CDA 111/338/01 inayotaka kibali cha rais, ili wizara yake iweze kuingia mkataba wa kuikodi kampuni ya kutafiti madini ya dhahabu.

Alidai barua hiyo ilikuwa ikimshawishi rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kwamba endapo kampuni hiyo itakodishwa, itakuwa ikisimamiwa na Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania na kwamba inatakiwa kitafutwe chanzo mbadala cha mapato kwa ajili ya kukodisha kampuni hiyo kwa sababu mradi huo haukuwapo kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2003/2004.

Holle alidai wakati mchakato huo ukiendelea baina ya Wizara ya Nishati na Madini, Fedha na Benki Kuu Mei 11 mwaka 2003, Yona alimuandikia tena barua rais, yenye kumbukumbu namba CDA/111/338/01 kumkumbushia ombi lake la kutaka kibali cha kampuni hiyo ya utafiti wa madini kuanza kufanya kazi.

Aliendelea kudai kuwa, Juni 12, 2003, Mramba katika barua yake namba TYC/M/30/2 alimtaarifu Yona kuwa ukodishaji wa kampuni huru ya utafiti wa dhahabu umekuja wakati bajeti ya mwaka wa fedha wa 2003/2004 imeishafungwa na kwamba makusanyo ya mrahaba unaotokana na sekta ya madini tayari umeishaingizwa kwenye matumuzi mengine.

Alidai Mramba alimshauri Yona kwamba, bajeti ya mradi huo itaingia kwenye bajeti ya nyongeza ya mwaka 2003-2004 na kwamba atapeleka pendekezo hilo bungeni kuwa, chanzo mbadala cha fedha za kukodisha mradi huo kitatokana na mrahaba wa madini.

“Lakini mshitakiwa wa kwanza hakupeleka ombi hilo kwenye Baraza la Mawaziri, ili lijadiliwe bungeni na badala yake alimuuliza Mgonja amshauri ni jinsi gani anaweza kuisamehe kodi Kampuni ya Alex Stewart,” alieleza mwanasheria huyo.

Aidha, alidai Mei 15, mwaka 2003, aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Alhaji Abdisalaam Khatib, alimshauri Yona kwamba taratibu za ukodishaji wa kampuni huru ya utafiti wa dhahabu, usubiri hadi wataalamu toka Sekretarieti ya Commonwealth iishauri Serikali ya Tanzania kama itatumia mtindo gani wa kufanya kazi na aina gani ya madini itatafiti.

Aliendelea kudai kuwa, Mei 26, mwaka 2003, Godwin Nyero ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria ya Wizara ya Madini na Nishati, ambaye alikuwa ni mjumbe katika timu ya majadiliano ya serikali, alimshauri Yona kuwa, kampuni hiyo haikuwa wazi kwenye timu yao ya majadiliano na kwamba inakwenda kinyume na mawazo ya Alex Stewart (Assayers) ya mkataba.

Alidai kuwa, Septemba 11, mwaka 2002 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini na Nishati, B. Mrindoko naye alimshauri Yona afuate Sheria ya Manunuzi ya Umma katika kuingia mkataba na kampuni hiyo.

Licha ya ushauri huo, Juni 12, mwaka 2003 Mramba alimuelekeza aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, marehemu Daudi Balali kupitia barua namba TYC/M/30/2 kuilipa malipo ya awali Kampuni ya Alex Stewart dola milioni moja.

Aliendelea kueleza kuwa, Juni 23, mwaka 2003, Mamlaka ya Mapato (TRA) katika barua yake namba TRA/SB/E/1.3/Vol.XVII/32 ilimtaarifu Mgonja kwamba, kampuni hiyo haimo kwenye orodha ya makampuni yanayosamehewa kodi.

Katika barua nyingine namba TRA/E/1.3/Vol.XVII/31 ya Oktoba 7, mwaka 2003 kwenda kwa Mgonja, ilieleza kuwa kampuni hiyo inatakiwa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria za nchini.

“Kwa masikitiko makubwa, licha ya maagizo hayo ya TRA, Mgonja alimshauri Mramba kuendelea na mchakato wa kusaini vibali vya serikali vya kuisamehe kodi kampuni hiyo, ambapo vibali hivyo vimesababisha serikali kupata hasara ya sh 11,752,350,148,” alidai Holle.

Kwa upande wa wakili wa mshitakiwa wa pili, Joseph Tadayo, alidai mteja wake anakubali jina lake na kwamba alikuwa Wazini wa Madini na Nishati na malezo mengine anayakata.

Kwa upande wa wakili wa mshitakiwa wa tatu, Profesa Shaidi, naye alikubali mteja wake alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na kwamba alikamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani.

Baada ya kusoma maelezo hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Manyanda alidai upande wa mashitaka utakuwa na mashahidi 13 na miongoni mwa mashahidi hao, ni aliyekuwa Naibu wa Waziri wa Fedha wa serikali ya awamu ya tatu, Alhaji Abdisalaam Khatib.

Hata hivyo, Manyanda alidai wamepunguza idadi ya mashahidi kwa sababu upande wa utetezi umekataa sehemu kubwa ya maelezo ya awali.

Baada ya kutoa orodha hiyo ya mashahidi, Nyange alitaka upande wa mashitaka utaje vielelezo watakavyovitumia kwenye kesi hiyo na kwamba sheria inawataka wafanye hivyo.

Hoja hiyo ilipingwa na Manyanda na kueleza hawawezi kutaja vielelezo vya kesi hiyo, na badala yake vielelezo hivyo watavitoa wakati kesi itakapokuwa ikiendelea kusikilizwa, majibu ambayo hayakumridhisha Nyange, ambaye alisimama tena na kushinikiza watajiwe idadi ya vielelezo hivyo.

Ndipo Hakimu Mwankenja aliingilia kati na kumtaka Nyange aonyeshe ni kifungu gani cha sheria kinataka hilo lifanyike. Nyange alishindwa kutaja sheria hiyo.

Akiahirisha kesi hiyo jana, Hakimu Mwankenja alisema kesi itaanza kusikilizwa Mei 18, mwaka huu na kuutaka upande wa mashitaka uhakikishe unakuwa na mashahidi siku hiyo.
Wakati huo huo, Mwankenja amekubali ombi la Mramba la kutaka aruhusiwe kwenda Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge na kumtaka arudi Dar es Salaam Mei Mosi, mwaka huu.

Novemba 25 mwaka jana, washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, wakikabiliwa na mashitaka 12 ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia hasara ya sh bilioni 11.7

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, April 18, 2009

JEETU AGONGA MWAMBA KORTINI

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imekataa kutoa uamuzi wa kumruhusu au kutomruhusu mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya wizi wa sh bilioni 2.5 za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania BoT), Jayantkumar Chandubhai Patel, maarufu Jeetu Patel, kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Uamuzi huo ulitolewa jana na kiongozi wa jopo la mahakimu wakazi, Rwaichi Meela, anayesaidiana na Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, John Kayohza na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, Grace Mwakipesile, ambaye alisema licha ya jana kesi hiyo kuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi wa ombi hilo la mshitakiwa, wameona ni muhimu, ila linahitaji umakini.

Meela alisema mahakama hiyo ni chombo cha serikali, hivyo haiwezi kupokea taarifa za ugonjwa wa mshitakiwa kutoka hospitali binafsi, na kumtaka kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuonana na mtaalamu wa ugonjwa huo, ambaye atamchunguza na kuandika ripoti, kisha kupelekwa mahakamani hapo.

“Ombi la mshitakiwa tumelichukulia kuwa ni muhimu, ila jopo hili leo (jana) haliwezi kupokea taarifa za ugonjwa wake kutoka hospitali binafsi, hivyo tunamwamuru mshitakiwa aende Muhimbili na kuonana na mtaalamu wa ugonjwa unaomsumbua, ili naye aandike ripoti yake kisha iletwe mahakamani, ndipo sisi tutakapotoa uamuzi kuhusu ombi lake,” alisema Meela.

Baada ya kueleza hayo, Meela aliahirisha kesi hadi Aprili 28, itakapotajwa.
Jumatano wiki hii, Wakili Mabere Marando anayemtetea mshitakiwa huyo, aliwasilisha ombi hilo akidai mteja wake anasumbuliwa na maradhi ya moyo, na amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Hindu Mandal.

Marando alidai hospitali hiyo imeandika taarifa mbili za uchunguzi wa ugonjwa unaomsumbua mteja wake, na kupendekeza akatibiwe nchini India, kwani hospitali hiyo haina uwezo wa kumtibu.

Marando alidai licha mteja wake kukabiliwa na kesi nne mahakamani hapo, anaomba aruhusiwe kwenda India kuanzia Aprili 20 hadi Mei 14, kwa ajili ya matibabu.

Mbali na Jeetu Patel, washitakiwa wengine katika kesi hiyo namba 1154/2008 ni Devendra Patel na Amit Nandy, ambao wote wanatetewa na mawakili wa kujitegemea; Marando, Joseph Tadayo na Martin Matunda.

Novemba 16, mwaka jana, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, washtakiwa wote kwa pamoja bila ya halali yoyote, walitumia kampuni yao ya Nobel Azania Investment Ltd kuonyesha kuwa kampuni ya nje ya Bencon Investment, imewapatia idhini ya kurithi deni lake la sh bilioni 2.5.

Wakati huo huo, shahidi wa tisa katika kesi ya wizi wa sh milioni 207 za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) inayomkabili Rajabu Maranda na maofisa wa BoT, Iman Mwakosya, Ester Komu na Bosco Kimela, jana alishindwa kuanza kutoa ushahidi wake baada ya upande wa mashitaka kubadilisha hati ya mashitaka na kumuongeza mshitakiwa Farijala Hussein.

Hussein ambaye kwa sasa atakuwa anakabiliana na kesi nne za EPA mahakamani hapo, aliunganishwa jana baada ya upande wa mashitaka uliokuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Vitalis Timon, kuwasilisha ombi la kubadilisha hati na kumsomea mashitaka sita, likiwamo shitaka la kula njama, wizi na kujipatia ingizo isivyo halali.

Jopo la mahakimu wakazi, lililokuwa likiongozwa na Hakimu Mkuu Mfawidhi, Addy Lyamuya na Kitusi, waliahirisha kesi hiyo hadi Jumatatu asubuhi ambapo siku hiyo washitakiwa watasomewa maelezo ya awali.

Mshitakiwa alidhaminiwa baada ya kuwasilisha hati yenye thamani ya sh milioni 20.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, April 18,2009

KESI YA TANESCO DHIDI YA DOWANS YAKWAMA

Na Hapiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara Dar es Salaam, jana ilishindwa kuanza kusikiliza kesi ya kutaka mitambo ya Kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, isiuzwe, iliyofunguliwa na Shirika la Umeme (TANESCO) dhidi ya Dowans, kwa sababu ya kukosekana jaji wa kuisikiliza.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, Katarina Revocati, alisema kesi hiyo ambayo jana ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa haitaweza kusikilizwa kwa sababu aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Catherine Oriyo amehamishwa katika mahakama hiyo hivi karibuni, baada ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Revocati alisema kwa sababu hiyo, uongozi wa Mahakama nchini utampanga jaji mwingine ambaye atasikiliza kesi hiyo na hivyo kuiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 24, mwaka huu.

“Kesi hii ambayo leo (jana) ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, haitaweza kusikilizwa, kwa sababu Jaji Mfawidhi, Orriyo, ambaye ndiye alikuwa akisikiliza kesi hii hivi karibuni ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, kwa sababu hiyo naahirisha kesi hii hadi tarehe hiyo,” alisema Naibu Msajili Revocati.

Katika kesi hiyo namba 19/2008, mlalamikaji ni Tanesco, inayotetewa na kampuni ya uwakili ya Rex Attoneys, dhidi ya Dowans Tanzania Ltd, ambayo inatetewa na Kampuni ya uwakili ya Amicus Attorneys.

Kwa mujibu wa hati ya madai, TANESCO inaiomba mahakama kutoa amri ya kuizuia Dowans asiuze mitambo yake hadi kesi ya msingi iliyopo mahakamani hapo itakapomalizika na endapo mahakama haitakubali kutoa amri hiyo, iamuru Dowans kuweka mahakamani asilimia kumi ya dola za Marekani 109,857,686.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima,April 18, 2009

MAHAKAMA:MAHALU ANA KESI YA KUJIBU

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imesema kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin, wana kesi ya kujibu.

Uamuzi uliotolewa jana na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani nchini, Sivangilwa Mwangesi, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili kutolewa uamuzi wa ama washitakiwa wana kesi ya kujibu au la.

Akitoa uamuzi huo, Naibu Msajili Mwangesi alisema washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka sita.

Alitaja mashitaka hayo kuwa ni kula njama kwa nia ya kutenda kosa, shitaka la pili, tatu na la nne ni la kutumia hati zenye maelezo yasiyo sahihi kwa lengo la kumdanganya mwajiri wao, ambaye ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shitaka la tano ni la wizi na shitaka la sita ni kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni mbili.

Alisema mahakama imejiridhisha kwamba watuhumiwa hao wana kesi ya kujibu baada ya upande wa mashitaka kuleta mashahidi saba na vielelezo tisa.

“Mahakama hii baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi saba na vielelezo tisa, imeshawishika kuona washitakiwa wana kesi ya kujibu na kuwahoji mawakili wa utetezi kwamba wateja wao watatoa ushahidi wao kwa njia gani,” alisema Mwangesi.

Wakili wa utetezi, Bob Makani na Alex Mgongolwa, walidai kuwa wateja wao watajitetea kwa njia ya kiapo na kwamba mshitakiwa wa pili, Grace ataleta mashahidi watatu wakati Profesa Mahalu ataleta mashahidi kadiri kesi itakavyoanza kusikilizwa.
Aidha, Mwangesi alisema washitakiwa hao wataanza kujitetea mfululizo kuanzia Mei 4 mwaka huu na kutaka mashahidi wafike bila kukosa.

Mapema Januari mwaka juzi, washitakiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya sh bilioni mbili, mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Ijumaa, April 19, 2009

JK APANGUA WAKUU WA MIKOA 11

*Kandoro ahamishwa Dar na kwenda Mwanza
*Mabadiliko yawagusa ma-RC walio wabunge
*William Lukuvi amrithi Kandoro Dar es Salaam

Na Happiness Katabazi

SIKU chache baada ya kufanya mabadiliko makubwa ya wakuu wa wilaya nchini, Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko mengine madogo ya wakuu wa mikoa.

Katika mabadiliko hayo, rais ameendelea kuziacha sura zile zile za wakuu wa mikoa na badala yake akawahamisha kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kusainiwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Aggrey Mwanri inaonyesha kuwa mabadiliko hayo ambayo yalikuwa yakitarajiwa, yamehusisha wakuu wa mikoa 11 kati ya 21 wa Tanzania Bara pekee.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, ambayo yameelezwa kuwa na lengo la kusukuma utendaji serikalini, wakuu wote wa mikoa ambao ni wabunge wa majimbo na mmoja wa viti maalum, wameguswa, jambo ambalo linaweza kuibua maswali kuhusu utendaji na pengine ufanisi wao wa kazi.
Miongoni mwa mabadiliko makubwa ni uamuzi wa Rais Kikwete kumhamisha kutoka Dar es Salaam, Abbas Kandoro na kumpeleka mkoani Mwanza.
Kandoro anaondoka Dar es Salaam akiwa ameuongoza mkoa huo kwa miaka mitatu baada ya kuteuliwa mwaka 2006, kuchukua nafasi ya Luteni Yussuf Makamba aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika mabadiliko hayo, nafasi ya Kandoro sasa itachukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, William Lukuvi.
Kuondoka kwa Kandoro, kunakuja siku chache tu baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kufanya ziara ya kikazi jijini Dar es Salaam kukagua mazingira na shughuli za usafi na kuibua maswali kuhusu masuala mbalimbali.
Aidha, kuhamishiwa Dar es Salaam kwa Lukuvi, kada wa CCM ambaye amepata kufanya kazi na Rais Kikwete zama wakiwa viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana enzi ikijulikana kama UVT miaka ya 1980, kunaweza kukawa kuridhishwa kwake na namna alivyoweza kuuongoza Mkoa wa Dodoma katika kipindi cha miaka takriban minne sasa.
Wakati Lukuvi ambaye ni Mbunge wa Isimani mkoani Iringa akihamishiwa Dar es Salaam, nafasi yake ya Dodoma imekwenda kwa Dk. James Msekela ambaye kama ilivyo kwa Lukuvi, ni Mbunge wa Tabora Kaskazini.
Wengine waliohamishwa kutoka vituo vyao ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Enos Mfuru ambaye anakwenda Mara kuchukua nafasi ya Issa Machibya anayehamia Morogoro.

Katika mabadiliko hayo madogo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Meja Jenerali Said Kalembo anahamia Tanga anakokwenda kuchukua nafasi ya Mohamed Abdulaziz.
Aziz ambaye naye ni Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini, amehamishiwa katika Mkoa wa Iringa akimrithi, Hajaat Amina Mrisho, anayekwenda mkoani Pwani.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dk. Christine Ishengoma ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum amehamishiwa Mkoa wa Ruvuma.

Katika mlolongo huo huo wa mabadiliko, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Monica Mbega ambaye naye ni Mbunge wa Iringa Mjini, amehamishiwa mkoani Kilimanjaro akichukua nafasi ya Mohammed Babu anayekwenda Kagera.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi 16, 2009

JEETU PATEL AOMBA AKATIBIWE INDIA

Na Happiness Katabazi

MSHTAKIWA wa kwanza katika kesi ya wizi wa sh bilioni 2.5 za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jayantkumar Chandubhai Patel, maarufu Jeetu Patel, ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, impe ruhusa ya siku 30 kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo namba 1154/2008 ni Devendra Patel na Amit Nandy, ambao wote pamoja na Jeetu Patel wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Mabere Marando, Joseph Tadayo na Martin Matunda.

Mbele ya jopo la mahakimu wakazi wa mahakama hiyo, linaloongozwa na Hakimu Rwaichi Meela anayesaidiana na Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, John Kayoza na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, Grace Mwakipesile, wakili Marando aliwasilisha ombi hilo kwa niaba ya mteja wake, Jeetu Patel, muda mfupi baada ya Meela kusema kuwa, wasingeweza kusikiliza maelezo ya awali jana, kwani ni wapya katika kesi hiyo na bado hawajapatiwa nakala ya kesi hiyo.

Awali, kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na hakimu mmoja, lakini sasa imefikia hatua ya kuanza kusikilizwa, na imepangiwa jopo la mahakimu wakazi watatu.
Marando aliiambia mahakama hiyo kuwa, Jeetu Patel anasumbuliwa na maradhi ya moyo na amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Hindu Mandal.

Alidai kuwa, hospitali hiyo imeandika taarifa mbili za uchunguzi wa ugonjwa unaomsumbua mteja wake, na kupendekeza akatibiwe nchini India kwani hospitali hiyo haina uwezo wa kumtibu.
Marando alidai kuwa, licha mteja wake kukabiliwa na kesi nne mahakamani hapo, anaomba aruhusiwe kwenda India kuanzia Aprili 20 hadi Mei 14, mwaka huu kwa ajili ya matibabu.

Kwa upande wa mashitaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa serikali, Vitulis Timon ambaye alikuwa akisaidiana na Fredrick Manyanda, Oswald Tibabyekoma na Stanslaus Boniface, ulidai kuwa hawana pingamizi na ombi hilo.

Hata hivyo, kiongozi wa jopo hilo la mahakimu wakazi, Meela alisema watatoa uamuzi wa ombi hilo leo kwani watakuwa wameshapitia nakala za kesi hizo kwenye majalada yao.
Novemba 16, mwaka jana, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, washtakiwa wote kwa pamoja bila ya halali yoyote, walitumia kampuni yao ya Nobel Azania Investment Ltd kuonyesha kuwa kampuni ya nje ya Bencon Investment, imewapatia idhini ya kurithi deni lake la sh bilioni 2.5.

Wakati huo huo, kesi nyingine ya EPA ya wizi wa sh bilioni 1.8 inayomkabili Bahati Mahenge, Manase Makale, Eda Makale na Davis Kamungu, itasikilizwa na jopo la mahakimu wakazi wawili wapya.

Kiongozi wa jopo hilo ni Sekela Mosha anayesaidiana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Lameck Mlacha ambaye alisema kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa Mei 13-15, mwaka huu.
Katika hatua nyingine, kesi ya matumuzi mabaya ya ofisi za umma na kusababisha hasara ya sh bilioni 220, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba na Meneja Mradi wa benki hiyo, Dogratius Kweka, jana ilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Walirwande Lema alisema, Aprili 23, mwaka huu, atatoa uamuzi kuhusu ombi la mawakili wa utetezi waliokuwa wakitaka washtakiwa hao wafutiwe kesi kwa kuwa siku 60 za upelelezi wa kesi hiyo, zimepita, lakini haujakamilika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, April 16, 2009

WAKILI WA WATUHUMIWA EPA ABANWA

Na Happiness Katabazi

WAKILI maarufu wa kujitegemea, Majura Magafu, ambaye anawatetea baadhi ya watuhumiwa wa kesi za wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT) na ile ya matumizi mabaya ya ofisi za umma, jana alijikuta akipatwa na wakati mgumu, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kumbana kwa maswali.

Majura alijikuta kwenye hali hiyo, baada ya sekunde chache kuwasilisha ombi lake mbele ya jopo la mahakimu wakazi, lililokuwa likiongozwa na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Addy Lyamuya, kuiomba mahakakama hiyo kumruhusu leo aweze kuendelea na kesi ya mauaji, iliyotokea Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Wakili huyo leo atakuwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuendesha kesi ya mauaji ya Ubungo mataa, ambapo ameteuliwa na mahakama hiyo ya juu kuwatetea baadhi ya washtakiwa.

Katika kesi hiyo, inayohusisha wizi wa sh milioni 207, inayowakabili Kada wa CCM, Rajabu Maranda na Imani Mwakosya, Ester Komu na Bosco Kimela, ambao wote ni maofisa wa BoT, jana shahidi wa tisa aliendelea kutoa ushahidi wake.

“Unaomba kesi hii iahirishwe kwa sababu unakwenda kwenye kesi ya mauaji Mahakama Kuu, hivi hapo ofisini kwako hakuna mawakili wengine ambao wanaweza kuja kuendelea na kesi za wateja wako zilizopo katika mahakama hii, hivi huoni kwenda kwako Mahakama Kuu mara kwa mara kunasababisha wateja wako kuchelewa kujua hatima zao kwenye kesi zinazowakabili katika mahakama hii?” Hakimu Lyamuya alimhoji Magafu.

Yafuatayo ni maswali kati ya Lyamuya na Magafu:

Lyamuya: Umeomba kesi hii iahirishwe kwa sababu wewe kuanzia kesho (leo) utakuwa Mahakama Kuu kwa kipindi cha mwezi mmoja, kutetea watuhumiwa wa kesi ya mauaji, je, ni kwanini ofisi yako isimtume wakili mwingine aje aendeshe kesi hii badala yako?
Magafu: Wakili aliyepo ni mgonjwa wa kisukari, hawezi kuja kusimama hapa mahakamani.

Lyamuya: Hapa mahakamani si lazima wakili asimame, je, hakuna wakili zaidi ya huyo mgonjwa?

Magafu: Yupo Maregesi, ila kwa mazingira ya kesi hizi za EPA hawezi kuja kuendesha kesi hizi, kwa sababu kwa namna moja ama nyingine naye anahusishwa kwenye tuhuma hizi za wizi wa EPA.

Lyamuya: Zaidi ya Maregesi, hakuna tena wakili mwingine katika ofisi yenu?
Magafu: Mwingine ni wakili Makubi, ila kwa sasa anauguliwa na mzazi wake na amekwenda likizo na sina uhakika ni lini atakuja ofisini.

Lyamuya: Hiyo summons ya wewe kuitwa kwenye hiyo kesi ya mauaji Mahakama Kuu, uliipata lini?

Magafu: Niliipata wiki mbili zilizopita.

Lyamuya: Ulivyoipata hiyo summons, kwanini hukutoa udhuru Mahakama Kuu kwamba una kesi zaidi ya tatu unazozitetea hapa Kisutu na zote zimeishaanza kusikilizwa?

Magafu: Sikufahamu kikao cha mauaji kingepangwa kwa muda mrefu wa mwezi mmoja, hivyo naomba mahakama hii iniruhusu nikaudhurie kwenye kikao cha Mahakama Kuu.

Lyamuya: Magafu unafahamu kwamba kesho (leo) katika mahakama hii kwenye kesi nyingine ya EPA, mbali na hii iliyopo mbele yetu sasa inayomkabili Maranda ambaye ni mteja wako, inakuja kwa ajili ya upande wako kuwasilisha hoja kuwa wateja wako wana kesi ya kujibu au la?

Magafu: Sijui. Ninavyofahamu, kesi hiyo inakuja kwa ajili ya kupangiwa tarehe ya upande wangu kuwasilisha hoja ya kwamba wateja wangu wana kesi ya kujibu au la.

Lyamuya: Ndiyo nakwambia sasa kwa mujibu wa rekodi za mahakama zinaonyesha kesho (leo) kesi nyingine ya EPA inayomkabili mteja wako Maranda na wenzake inakuja kwa ajili ya kuwasilisha hoja kuwa kuna kesi ya kujibu.

Lyamuya: Wewe unatetea kesi nyingi za EPA, huoni kwenda kwako Mahakama Kuu, kutasababisha wateja wako kuchelewa kupata haki zao katika kesi zinazowakabili?

Magafu: Off recod, kama ni hivyo waheshimiwa naomba niwasiliane na wakili mwenzangu ambaye anauguliwa na mzazi wake aje aendelee na kesi moja ya EPA ambayo nilikuwa naiendesha mimi na mimi pia nitawasiliana na Mahakama Kuu ili iweze kuniondoa kwenye orodha ya mawakili watakaowatetea washtakiwa wa kesi ya mauaji ya Ubungo, ili niweze kuendelea na kesi za EPA.

Kitusi: Hakuna cha off record hapa kila kitu kinarekodiwa, unataka tuandike nini kwenye rekodi ya mahakama?

Magafu: Naomba irekodiwe kwamba nitawalisiliana na wakili mwezangu ambaye anauguliwa na mzazi wake ili aje kuendesha kesi moja, pia nitawasiliana na Mahakama Kuu ili iweze kuniondoa kwenye orodha ya mawakili wa kuwatetea watuhumiwa wa kesi ya mauaji iliyopo Mahakama Kuu.

Awali Wakili Mwandamizi wa Serikali, Fredrick Manyanda aliyekuwa akisaidiana na Vitalis Timon aliwasilisha ombi la kutaka kesi hiyo iahirishwe kwa sababu wanataka kumuongeza mshitakiwa mwingine kwenye kesi hiyo na kwamba endapo mshitakiwa huyo angekuwa kwenye eneo la mahakama jana, wangemuunganisha.

Aidha, Manyanda aliieleza mahakama kwamba, kwakuwa kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa, upande wa mashtaka ulikuwa umemleta shahidi wao aitwaye Emmanuel Boaz, ambaye jopo hilo lilimtaka aingie mahakamani na akashindwa kutoa ushahidi wake, baada ya kutokea mabishano na maombi ya kuombwa kuahirishwa kwa shauri hilo.

Hata hivyo Lyamuya aliahirisha kesi hiyo hadi keshokutwa ambapo kesi hiyo hiyo itaendelea kusikilizwa. Mara ya mwisho, kesi hii iliahirishwa Septemba 9, mwaka huu.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, April 15, 2009

SOKOINE,HIVI NDIVYO TUNAVYOKUENZI

Na Happiness Katabazi

MIAKA 25 iliyopita, Watanzania walifikwa na msiba mkubwa, kwa kumpoteza mmoja wa viongozi aliyeipigania nchi yake bila woga.

Kiongozi huyo si mwingine bali ni aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, Edward Moringe Sokoine, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari jioni ya Aprili 12, 1984 katika eneo la Wami, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.

Sokoine alifariki dunia wakati nikiwa na umri wa miaka mitano, lakini nakumbuka nilikuwa nikilisikia jina lake kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kabla na baada ya kifo. Hakika, nyingi zilikuwa zimebeba ujumbe wa kumtukuza kutokana na mchango wake, nilimsikia Radio Tanzania na kumsoma kupitia vitabu mbalimbali.

Nikiri kuwa sikubahatika kumtia machoni kiongozi huyu, hadi Mwenyezi Mungu alipomtwaa. Ila nimetokea kuwa muumini mzuri tu wa mtindo wake alioutumia kutenda kazi katika ofisi za umma.

Kwa mujibu wa vitabu na watu waliowahi kufanya kazi naye, wanamuelezea kuwa ni kiongozi aliyejawa na uzalendo kwa nchi yake, hakupenda makuu, aliyewashughulikia wote waliohujumu uchumi wa taifa hili, hakuwa mwoga, alimkemea na kumchukulia hatua yeyote aliyekwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.

Hakuwa mchumia tumbo kama walivyo viongozi wengi wetu wa sasa. Hakuingia madarakani kwa kubebwa na vyombo vya habari wala kupenda sifa na kuwagawa wanachama wa CCM kama ilivyo sasa. Alipenda umoja.

Lakini leo tukiwa tunakumbuka kifo chako Sokoine, mambo maovu ambayo wewe na Baba wa Taifa, Julius Nyerere, kila kukicha mliyapiga vita kwa vitendo, leo maovu hayo ndiyo yamekuwa kigezo cha kupata uongozi na kupata umaarufu ndani ya jamii.

Mlipinga rushwa kwa ngazi zote, lakini leo hii hospitalini, polisi, kwenye ajira na kwenye michakato ya uchaguzi, ziwe chaguzi za ndani ya chama chako, Chama Cha Mapinduzi (CCM), au chaguzi za kiserikali, ni rushwa tu ndiyo imetamalaki. Hutolewa na kupokewa kwa wazi.

Si kwenye sekta hizo tu, bali hata katika vyombo vya habari rushwa nayo imo kwani, wanahabari ni miongoni mwa wala rushwa wazuri tu.

Tunapewa na baadhi ya viongozi manyang’au ili tusiweze kuripoti machafu yao kwenye jamii. Manyang’au wamekuwa wakitupatia fedha tuwachafua mahasimu wao kisiasa, ili wao ndio waonekane wasafi mbele ya jamii.

Na kazi hiyo tukiishaikamilisha husherehekea na kutamba kuwa hakuna aliye msafi.
Sisi waandishi wa habari za mahakamani hasa pale, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baadhi yetu tunakuenzi kwa kupokea rushwa kutoka kwa baadhi ya washtakiwa wenye fedha, wenye umaarufu, na wenye asili ya Kiasia, wanaofikishwa hapo kwa makosa mbalimbali.

Lengo lao ni kutaka tusiripoti kesi zinazowakabili kwa sababu tukiwaandika kwenye vyombo vya habari, watadhalilika mbele ya jamii na shughuli zao za kitapeli zitakwama. Hivyo, tunaamua kuchukua fedha zao na kisha hatuandiki kesi zinazowakabili.

Hakika sisi ni majasiri kuliko mafisadi kwani, kila siku tunashinda mahakamani hapo na kuona watu mbalimbali wakihukumiwa kwenda jela lakini wala hatuogopi kuwa kupokea rushwa ni kosa la jinai, linaloweza kumpeleka mtu jela.

Hili hufanyika mara kwa mara pale Kisutu, mchana kweupe! Baadhi ya askari polisi wanalifumbia macho, kwani nao ni miongoni mwa wanaofaidika na vipato hivyo haramu vinavyotolewa ndani ya jengo la mahakama, chombo kinachopaswa kuwa kimbilio la haki za wananchi.

Hivyo ndivyo tunavyokuenzi kwenye suala la rushwa kwa sisi wanahabari, na mhimili huu wa nne (usio rasmi), sasa umeanza kuwa na nguvu.

Ulipigana kufa na kupona na wahujumu uchumi lakini leo hii, baadhi ya wafanyabiashara wachafu wamejipenyeza kwenye CCM yako.

Wanatoa misaada ya fedha chafu na serikali yetu inawapa nafuu ya kodi na kupitisha mizigo yao inayoingia nchini bila kukaguliwa na mamlaka husika, kwa sababu ya kile kinachoelezwa kuwa wafanyabiashara hao wana rekodi nzuri.

Nafuu hiyo haiwatoshi, wafanyabiashara wengine sasa wamejitumbukiza kwenye CCM na kugombea nyadhifa mbalimbali. Dhamira yao si kukisaidia chama bali ni kukitumia chama kutimiza haja zao, mathalani kupata upendeleo katika zabuni za serikali na kinga ya kidiplomasia (Diplomatic Immunity), ili wanapopitisha mizigo yao haramu pale uwanja wa ndege wasikaguliwe wala kutiliwa shaka na wana usalama.

Ulisisitiza kwa vitendo maendeleo ya kilimo nchini, leo wakulima wetu hakuna anayewajali.

Fedha nyingi hutengwa katika kugharamia shughuli za kisiasa. Wanasiasa wanajilipa malupulupu makubwa na ndiyo maana hivi sasa Watanzania wengi, hata ambao hawana sifa za uongozi, wanakimbilia kuhonga fedha nyingi ili wapate uongozi.

Viongozi wetu wa leo wamegeuka kuwa manyapara, kazi yao ni kutoa amri bila kuonyesha njia.

Majukwaani wanasema kilimo ni uti wa mgongo, lakini hakuna kiongozi ambaye ameonyesha mfano kwa vitendo, hata kwa wananchi wanaomzunguka, kwamba na yeye hushika jembe na kulima.

Wamekuwa ni mahiri na wajanja wa kucheza na maneno na hotuba. Kabla ya kuzitoa, hutuma mashushushu wao sehemu husika, kupeleleza wananchi wa eneo hilo wanakabiliwa na tatizo gani kisha hurudi ofisini na kuandaa hotuba ya matumaini kuhusu kero hizo.

Kiongozi huyo anapotembelea eneo hilo huzungumzia kero au matatizo hayo na kuahidi kuyatafutia ufumbuzi. Kumbe ni danganya toto!

Kwa upande wa wafugaji, Serikali haijali masilahi yao bali inajali masilahi ya wawekezaji wakubwa.

Baadhi ya viongozi wanaotoka maeneo ya ufugaji hufurukuta kutetea haki za wafugaji, hata hivyo wanalifanya hilo huku wakijua kwamba serikali ya CCM haina sera nzuri ya ufugaji.

Hiki ni kiini macho kwa taifa kuwa na sera ya mifugo bila kuwa na sera ya kuendeleza wafugaji.

Hakuna kikundi cha Watanzania kilichodharaulika na kunyimwa haki za kibinadamu kama wafugaji.

Kwanza, walinyang’anywa ardhi yao ya kufugia na nyumba zao kuchomwa moto katika Wilaya ya Hanang’. Huko serikali ilianzisha mashamba makubwa ya kilimo cha ngano.

Wafugaji wale hawakupata fidia wala ardhi mbadala na sasa wamesambaa kila mahala nchini, Mvomero, Ihefu na kwingineko hali ni hiyo hiyo.

Kama vile hiyo haitoshi, mahakama za nchi hazikuwasaidia wafugaji hao walipo kwenda kudai haki zao mahakamani.

Hii inaonekana kwamba sera na sheria za nchi kwa ujumla wake, haziwalindi wafugaji.

Kule Mkomazi, wafugaji waliokuwa wakiongozwa na Lakei Faru Parutu, walifukuzwa ndani ya hifadhi bila kufidiwa fedha, au ardhi mbadala. Leo hii wanatangatanga bila kujua wapi walishie mifugo yao. Hivyo ndivyo tunavyokuenzi.

Kwa bahati mbaya uliaga dunia wakati nchi yetu haijaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, mfumo wa vyama vingi ulianza rasmi 1992.

Sasa tuna zaidi ya vyama vya upinzani 15, lakini ni vyama vichache mno vinavyoonyesha kuwa na upinzani wa ukweli.

Ndani ya vyama hivyo kuna mamluki wa kisiasa, wachumia tumbo na walafi wa madaraka.
Pindi wanapokosa fursa hizo ndani ya vyama vyao, hurudi CCM au huanzisha vyama vyao binafsi. Sasa, siasa na uongozi imekuwa ni biashara.

Tanzania uliyoiacha mwaka 1984, si hii ya leo kwani, imepiga hatua za kimaendeleo katika sekta mbalimbali japo maendeleo hayo hayawiani na wakati tulionao. Wananchi wengi wanapata elimu za msingi katika shule nyingi za serikali, lakini elimu hiyo haina ubora wa kutosha.

Watanzania hivi sasa wameanza kujua haki zao na kuzidai, wameanza kuwa majasiri na kuwakosoa viongozi na serikali wazi wazi pindi inapofanya kinyume. Uhuru wa kutoa maoni hata katika Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete unazidi kuongezeka.

Hata hivyo, baadhi yetu tumekuwa tukiutumia uhuru huo vibaya, kwa kuwapaka matope wenzao na kutundika picha za utupu kwenye mitandao, vitendo vinavyochochea mmomonyoko wa maadili kwa kizazi hiki na kijacho.

Tunapoadhimisha miaka 25 ya kifo cha Sokoine, viongozi wetu na wananchi kwa ujumla tujitazame upya. Maadili yetu je, ni sawa na ya viongozi wa awamu ya kwanza ya kina Nyerere, Sokoine, Karume na wengine?

Sokoine, hivi ndivyo tunavyokuenzi kinafiki. Machafu uliyoyapiga vita, leo tunayakumbatia. Serikali, chama chako, na vyuo vikuu havijishughulishi kuandaa hata mijadala ya kukumbuka mchango wako.

Tunashuhudia serikali ikilipia matangazo ya sherehe za muungano kwa takriban wiki tatu sasa, miaka kadhaa ya Kikwete tangu aingie madarakani, maadhimisho mbalimbali lakini haijadiriki kutoa matangazo ya kuonyesha kuwa Aprili 12 mwaka huu, taifa linakumbuka kifo chako.

Hukuwa fisadi, ulikuwa mchapakazi na mpenda haki, hivi unafikiri nani atakukumbuka?
Pengo kati ya tajiri na maskini limeongezeka, hivi matajiri waliotajirika na kuneemeka baada ya enzi ya uongozi wako wewe na Mwalimu, watakukumbuka?

Tuache unafiki wa kuzungumza kuwa tunamuenzi Sokoine mdomoni wakati kivitendo hatumuenzi. Tutakuwa tunachuma dhambi bure, mwisho wa siku tuje kuwa kuni kwenye moto wa milele. Mungu aipumzishe roho yako mahala pema peponi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, April 15, 2009