RUFAA YA BABU SEYA SASA KESHOKUTWA

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Rufani nchini, jana ilishindwa kuanza kusikiliza rufaa ya ya mwanamuziki mahiri wa dansi hapa nchini, Nguza Viking maarufu kwa jina la ‘Babu Seya’ na wanae watatu ilishindwa kuanza kusikilizwa kwasababu pande zote mbili katika kesi hizo hazikuwa tayari kuanza kusikiliza rufaa hiyo.


Mbali na Babu Seya, warufani wengine ni Papii Kocha Nguza,Nguza Mbangu na Francis Nguza ambao wanatatewa wakili wa kujitegemea Mabere Marando.

Jaji Nataria Kimaro,Salum Massati na Mbarouk Mbarouk walisema wanakubaliana na maombi yaliyowasilishwa na mawakili wa pande zote yaliyotaka shauri hilo liairishwe ili waweze kupata muda wa kupitia nakala ya rufaa hiyo.

“Jopo limeyakubali maombi yenu ya kutaka usikilizwaji wa rufaa hii uairishwe ili mpate muda wa kujiandaa, hivyo tunaairisha rufaa hii hadi Desemba 3 mwaka huu, siku hiyo itaanza kusikilizwa” alisema Jaji Nataria Kimaro ambaye ni kiongozi wa jopo la majaji wanasikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo ukumbi Na.2 wa Mahakama ya Rufani, jana ulifurika watu waliofika mahakamani hapo kwaajili ya kusikiliza rufaa hiyo ambayo imekuwa ivuta hisia za watu wengi.

Awali kabla ya kuairishwa kesi hiyo wakili wa warufani Marando, aliiambia mahakama kuwa ameajiriwa kuendesha kesi hiyo wiki iliyopita na akabaini kichwa cha habari cha rufaa hicho kimeandikwa rufaa ya jinai Na.59/2009 badala ya kuandikishwa rufaa ya jinai Na.59/2005, hivyo akaomba kichwa hicho cha habari kiafanyiwe marekebisho na isomeke rufaa ya jinai Na.59/2005, ombi ambalo alikupingwa na upande wa mashitaka.

Aidha alieleza mahakama kuwa anatarajia kuongeza sababu nne katika rufaa hiyo na kisha kuziondoa sababu nne kati ya sababu 19 zilizowasilishwa awali na wakili wenzake Hurbet Nyange na kuongeza kuwa amechelewa kuwasilisha sababu hizo mapama kutokana na ukubwa wa nyaraka zilizomo ndani rufaa hiyo.

Akijibu hoja hizo Wakili Mkuu wa Serikali Justus Mulokozi aliambia mahakama kuwa waliopokea nyongeza ya sababu za kukata rufaa Ijumaa wakati muda wa kazi ulikuwa umekwisha hivyo naye akaomba wapewe muda ili waweze kuzipitia kwa kina ili wakati rufaa hiyo ikianza kusikilizwa wawe na majibu ya uhakikika.

Januari 27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25 mwaka 2004.

Waomba rufani hao wanakabiliwa na makosa kumi ya kubaka watoto wa kike wenye umri kati ya miaka sita na nane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri kama huo na kwamba wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya April na Oktoba 2003 eneo la Sinza kwa Remmy, jijini.

Aidha katika kesi hiyo mwalimu wa shule ya Msingi Mashujaa, Sigirinda Ligomboka, alishitakiwa kwa makosa mawili ya kumsaidia Babu Seya kutenda makosa ya kubaka na kulawiti kwa kuwaruhusu baadhi ya watoto hao kutoka madarasani.

Upande wa mashitaka ulileta mashahidi 24, ambao upande wa utetezi ulipinga vikali kutenda makosa hayo na uliita mashahidi nane.Katika hukumu yake Hakimu Lyamuya alitupilia mbali na utetezi wa Babu Seya na wanawe na akawatia hatiani kwa makosa hayo na hivyo kuwafunga kifungo cha maisha gerezani.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Desemba mosi mwaka 2009

TUMSIHI MKAPA AENDELEE KUKAA KIMYA

Na Happiness Katabazi

MOJA ya mambo ambayo nina hakika yanaleta faraja kwa Serikali ya Awamu ya Nne ni ukimya wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kuhusu tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, pamoja na malumbano ya hapa na pale ya kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili aweze kufikishwa mahakamani kukabiliana na tuhuma hizo.


Pamoja na kufurahia jambo hilo, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hivi sasa tumeanza kuwa na wasiwasi kwamba kiongozi huyo mstaafu ataendelea kukaa kimya?

Ni lazima wananchi watafakari kwa kina juu ya tuhuma za Mkapa, kwa nini zimeshamiri zaidi katika Awamu ya Nne?

Bila shaka jibu ni rahisi kuwa kulikuwa na uratibu maalumu wa kutangaza mabaya ya Mkapa ili watu watumie muda mwingi kufikiria na kuyazungumza mabaya yaliyofanywa na kiongozi huyo huku Serikali ya Awamu ya Nne ikiendelea kupumua na kufanya ufisadi kwa kadiri iwezavyo.

Ukitazama kwa kina utabaini kuwa mgawanyiko na malumbano ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiyo uliozaa haya tunayoyaona hapa nchini ambapo baadhi ya mambo ya maendeleo yanakwamisha kwa sababu ya chuki binafsi, kukomoa kunakofanywa na viongozi waliopo ndani ya chama tawala.

Hatuhitaji kuficha mabaya yaliyofanywa na kiongozi aliyetangulia lakini ni lazima tujiulize, je, ni kweli yatatusaidia kuziba nyufa zilizojitokeza au ndiyo yatabomoa kabisa nyumba tuliyoijenga kwa miaka mingi chini ya utawala wa Mwalimu Julius Nyerere?

Kwa nini hatujipi muda wa kutafakuri kwa nini viongozi na watendaji waliotenda maovu katika utawala wa Awamu ya Nne hawafikishwi mahakamani kama inavyoshinikizwa kwa Mkapa?

Si tunajua wapo watendaji na wanasiasa walishiriki katika kashfa za Richmond EPA, rada na nyinginezo lakini bado wanaendelea na nyadhifa zao pasi na aibu na uchungu kwa kutafuna rasilimali za taifa, tuna sababu gani la kumdhalilisha, kumuaibisha na kumkejeli Mkapa wakati tunajua fika kuwa hata Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, na yule wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, kuna makosa walifanya na mengine tunayajua waliyafanya kwa masilahi binafsi au familia zao, mbona hatujawaandama kama tunavyofanya kwa Mkapa?

Ni upumbavu kujadili makosa ya kiongozi mmoja mmoja alivyotumia vibaya madaraka yake akiwa Ikulu badala ya kujadili mfumo mzima uliomuwezesha kuingia madarakani pamoja na kufanya biashara zake akiwa Ikulu.

Kama tusipobadilika na kuuangalia mfumo huo kamwe hatutatua tatizo na kila kukicha tutakuwa tunawaandama viongozi wastaafu kwa sababu ya kutumia vibaya madaraka yao kwa misingi ile ile ya malumbano ya kutoa ahueni kwa serikali ya nne ambayo mpaka sasa imeshindwa kuleta maisha bora iliyowaahidi wananchi katika ilani yao ya uchaguzi ya mwaka 2005.

Mfumo uliopo wa wizi kutendeka kitaasisi ni hatari zaidi kuliko kuanza kushughulikia makosa ya mtu mmoja mmoja kama tunavyofanya sasa, tujiulize ni lini kulindana ndani serikali na chama tawala kutamalizika?

Kwa nini tusichukue hatua za kusafisha mfumo huu mbovu uliozaa EPA, rada, Richmond kuliko kumng’ang’ania Mkapa?

Si tumeshasikia fedha zilizoibwa Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited kuchota kiasi cha sh bilioni 40 katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) iliyokuwapo chini ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilivyoisaidia CCM katika kampeni na hatimaye ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Leo hii tunawezaje kutoka mbele za watu na kudai tunapambana na ufisadi wakati wamiliki wa Kagoda hawajafikishwa mahakamani wakati wao ndio waliochota kiwango kikubwa cha fedha kulinganisha na wengine? Tutafakari tuchukue hatua.

Nani anayeweza kujitokeza hadharani na kuueleza umma kuwa ufisadi anaotuhumiwa kuufanya Mkapa aliufanya peke yake pasi na kushirikiana na wengine? Inawezekana vipi baraza la mawaziri lisijue kile kinachofanywa na kiongozi mkuu wa nchi? Bunge lilikuwa wapi mbona hawakupiga kura ya kutokuwa na imani na rais?

Waliamua kufunika kombe mwanaharamu apite kwa kuwa walijua wazi kuwa mfumo wa serikali na chama tawala ni kulindana na wao kuna maeneo wanafaidika.

Tunapohoji nafasi ya Rais wa Awamu ya Tatu (Mkapa) kufanyabiashara akiwa madarakani, Serikali ya Awamu ya Nne inajiondoa vipi katika tuhuma kwamba wengi wa watendaji na viongozi ni wanatumia madaraka yao kufanyabiashara?

Kwa bahati mbaya wananchi wamekuwa vipofu wenye kupenda kushabikia kila kinachosemwa na wanasiasa ambao wanajua waseme au wafanye nini kwa wakati gani, wananchi wanapaswa wakae chini na kuchambua utekelezaji wa ahadi moja moja zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Nne badala ya kushabikia mambo ambayo mwisho wa siku hayana tija kwa taifa zaidi ya kuzidisha ugumu wa maisha.

Wananchi wana kitu gani cha kuipongeza Serikali ya Nne katika mapambano ya ufisadi wakati hata kesi zilizopo mahakamani nyingi zinaonekana zimepelekwa kwa ushabiki wa kisiasa au chuki binafsi?

Mfumo ndiyo chanzo kikuu cha kuzalisha kiongozi mzuri au mbaya, kama mfumo utakuwa mzuri kwa hakika hata viongozi watafanyakazi katika mfumo huo, utendaji wao utakuwa safi na uliojaa uadilifu lakini kama mfumo utakuwa mbaya hata aje kiongozi safi kama malaika hataweza kuubadilisha, kwani atamezwa na mfumo na mwisho wa siku naye atakuwa mchafu kama matope.

Kuna mifano mingi duniani ambapo serikali zilizoundwa na kuingia madarakani kwa mifumo mibovu imezivuruga nchi zao, Tanzania kabla ya kupata uhuru wake mwaka 1961 mfumo uliokuwapo kwa kiasi kikubwa ulikuwa ukitoa upendeleo kwa wakoloni lakini mara baada ya kupata uhuru Mwalimu Nyerere na viongozi wengine walijaribu kuboresha mfumo wa kiutawala kuanzia katika elimu, afya, miundombinu na huduma nyinginezo.

Lakini kwa bahati mbaya utawala wa Mwalimu Nyerere kuna baadhi ya mambo alishindwa kuyaweka katika mfumo uliokuwa unatakiwa, ulipoondoka madarakani na kuingia utawala wa mzee Mwinyi ‘Ruksa’ hatukusikia mabaya ya Nyerere kwa kiwango kikubwa kama tunavyosikia ya Mkapa hivi sasa, hivyo hivyo hata alipoingia Mkapa pia hatuyumbishwa na mabaya aliyoyafanya Mwinyi kwa sababu yaliyofanyika huko nyuma yalishapita, tulikuwa tukihitaji kujipanga vizuri pale tulipokosea ili maendeleo ya wananchi yapatikane.

Ni jambo la kusikitisha sana hivi sasa nchi ina wasomi wengi zaidi lakini maadili ya viongozi ndiyo yanazidi kumeguka siku hadi siku tofauti ilivyokuwa kwa Mwalimu Nyerere na Mwinyi, kila mtu sasa ni muongeaji, mtendaji na kiongozi.

Tuulizane inawezekana vipi zaidi ya miaka 45 ya uhuru taifa halijitoshelezi kwa umeme kiasi cha kuingia katika mgawo wa kutisha, ni taifa gani linaweza kuendelea iwapo umeme haupo wa kutosha pamoja na kukatikatika hovyo hata katika hafla kubwa kama ile ya marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutiliana saini ya kuanzisha soko la pamoja pale kwenye ukumbi wa AICC Arusha wiki chache zilizopita.

Kwa nini nchi iwe maskini wakati kuna madini mengi ambayo kama yakitumika ipasavyo nchi haiwezi kutembeza bakuli la kuomba misaada ya wahisani katika bajeti yake, mbona utawala wa Rais Kikwete umeshindwa kusimamia madini kwa faida ya Watanzania?

Rais Kikwete aliunda tume ya kupitia mikataba ya madini ili itoe mapendekezo ya kuboresha kile kinachopatikana lakini mbona mpaka sasa kimya? Ripoti ile ilitolewa mapema sana lakini mbona imegeuka godoro la watu kuchapa usingizi?

Inawezekanaje mpaka leo hii nchi ikose dawa katika zahanati, hospitali, vituo vya afya wakati kuna mamilioni ya fedha yanatafunwa na viongozi kwa miradi ya uongo na ukweli, barabara mbovu, maji tabu, vyote hivi ni Mkapa kavisababisha?

Hapana huu ni mfumo mbovu wa chama tawala (CCM) bila kupigania kuuondosha kamwe maisha bora hayatapatikani, tutakuwa tukiyasoma, kuyasikia na kuyaangalia kwenye runinga, redio na magazeti kupitia kwa wenzetu.

Ni jukumu la Watanzania kuamka ili viongozi wasiendelee na utaratibu wa kufikiri wao ndio wenye akili zaidi kuliko wengine, tunahitaji mabadiliko lakini hayawezi kuja kama tutaendeleza woga, unafiki na chuki.

Tusipofanya hivyo tutakuwa tupo kwenye sala moja na uongozi wa Awamu ya Nne ya kumsihi Rais mstaafu Benjamin Mkapa aendeleze ukimya wake ili awape unafuu wa kutawala kwa kuwa tayari wameshaonyesha kushindwa kiuchumi, kimaadili, kiutawala na mengineyo.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania la Jumapili, Novemba 29 mwaka 2009

CCM YAGEUKA BENDI YA TAARABU?

Na Happiness Katabazi

MALUMBANO yakipuuzi yanayoendelea katika makundi yayohasimiana ndani ya chama cha mapinduzi yanathibitisha maneno ya mwenyekiti wa chama hicho rais Jakaya Kikwete,alipowaambia wananchi kwamba ndani ya ccm kuna makundi yanayochukiana na kuasimiana kiasi kwamba mtu anashindwa kuacha glasi yake ya maji kwa kuhofu uenda akawekewa sumu.


Kile ambacho CCM ilikipanda ndani ya vyama vya upinzani sasa kimewageukia na kinawatafuna sasa.

Hapo zamani ilikuwani shangwe na vigelegele kuwacheka wapinzani na kuwaita ni mabingwa wa mitafaruku lakini ssa CCM leo hii tuwaite ni vingunge wa ufisadi na umbeya au mapaka shume ,manyani au magwiji wa mipasho?

Kile wanachokifanya wabunge wa CCM kwenye Kamati ya Rais Hassan Mwinyi ,ni ukweli wa mambo na uchafu ulio ndani ya chama hicho tawala.Ni sawa na wachawi waliokengeuka wanapoanza kuloga mchana na kuanza kuweweseka na kuwataja watu waliowaua na kuwala nyama.

Habari toka ndani ya kamati hiyo zinatisha na kusikitisha.Lakini tunajua zote zina ukweli.La msingi kwa watanzania ni kujua hawa wote hawafahai kuwa viongozi wetu hivyo tusiwachague tena .

Haijalishi kwamba kundi moja linajitetea na kujikosha mbele za watu lakini ukweli ni kwamba kujikosha huku kunaandaliwa makusudi kwaajili ya uchaguzi mkuu ujao.

Una watu ambao wanataka kutumia mwanya huo na taasisi za umma kujisafisha ili wagombee na kuwa tena wabunge, marais wajao.

Inakuwa kana kwamba nchi hii wameumbiwa wao na hakuna Mtanzania mwingine mwenye sifa za kuongoza isipokuwa wao.Kama mtu alipewa nafasi ya kuongoza akawa fisadi anataka kurudi kufanya nini tena?Hanataka kujakufanya ufisadi kipeuo cha pili?

Ni vizuri na tunamsifu Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete kwa kuunda kamati ya ‘umbeya’ ikiongozwa na mwenyekiti mstaafu wa chama hicho rais mwinyi.

Lakini tukumbuke kwamba kila umbeya una unaupande.Tutakuja kujua huyu Mwinyi yupo kundi lipi nay eye mwenyekiti wa sasa Kikwete yupo kundi lipi.

Kwasababu makundi hayo yanayoendelea kuparulalana na kuvuana nguo adharani huwa yanageuka nyuma kuangalia wapambe waona katika hili hakuna moja ndani ya ccm awe kiongozi mstaafu au aliypo madarakani hauisiki kwa njia moja ama nyingine kwa kashfa zinazozungumziwaaua hazijazungumziwa.

Kwani tumeona na kusikia kashfa zile zile wakati ambapo kashfa mpya zinazaliwa kila siku.kwani kuna usemi usemao mlani mla leo mla jana kala nini.

Kashfa ya Richmond ,ndege ya rais,helkopta za JWTZ,mitambo ya IPTl,mikataba ya migodi,BoT,mifuko ya pesheni,kila moja ya hizo ina Mapapa ambao wapo ndani ya serikali na wengine wamestaafu na watanzania hawatakuja kujua ukweli wake kwasababu wengi walioopo madarakani wana mizizi katika kashfa hizo kwani watuhumiwa wa kashfa hizo ni ndugu zao au maswahiba zao .

Kamati ya ‘umbeya’ inayoongozwa na Mwinyi haina tija kwa taifa wala ccm ukiacha ukweli kwamba inafurahisha ‘manyani’ na kuwakela binadamu.Mtasemana,mtapalulana lakini walioshika nyadhifa wataendelea kuzishikilia ang’oki mtu ng’o na wasiojua watazani ccm itakayoibuka baada ya kmati hiyo kumaliza muda wake itakuwa safi zaidi.

Licha ya udhahidi huu mkubwa ,hakuna dalili kwamba vyama vya upinzani vitajifunza na kuwa na sifa zaidi kuizidi CCm.Inavyoonekana ama ni vishiriki katika ufisadi ama vinakosa nafasi ya kuwa mafisadi.

Madhara ya kuwa na makundi ndani ya vyama, mkundi yenye rangi ya ukabila, udini,tayari yapo katika vyama vikuba vya upizani na hivyo haviwezi kuinyoshea ccm kidole.

Kama kipo chama cha upinzani kitakachojifunza somo la haya yanayotokea ndani ya ccm hivi sasa ,hiyo itakuwa ni neema kubwa kwa taifa letu.

Mungu ibariki Tanzania ,Mungu ibariki Afrika

0716 774494

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Novemba 18, 2009

SHAHIDI:UJENZI BOT HAUKUSABABISHA HASARA

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa saba wa upande wa mashitaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, amedai kuwa hapakuwapo na hasara iliyopatikana katika ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo.


Shahidi huyo ambaye ni mkadiriaji wa gharama za majengo kitaaluma, Harold Herbert Webb (74), raia wa Uingereza, alitoa maelezo hayo jana wakati akijibu maswali ya wakili wa utetezi, Onesmo Kyauke, mbele ya kiongozi wa jopo la mahakimu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Webb alidai hapakuwepo hasara yoyote licha ya kuwapo kwa mabadiliko ya ujenzi na kiasi cha fedha kuongezeka kutoka dola milioni 73 hadi dola 357,568, kiasi chote hicho kilitumika kwenye mradi wa ujenzi huo.

“Hakuna hasara ya fedha iliyopatikana kwenye ujenzi huo, kwa sababu kiasi hicho kilichotengwa awali na kilichokuja baadaye baada ya BoT kuagiza yafanyike mabadiliko ya nyongeza ya maghorofa, kiasi hicho chote kiliingizwa kwenye mradi huo,” alidai Webb.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano baina ya mawakili wa utetezi Onesmo Kyauke, Majura Magafu, Hudson Ndusyepo na shahidi huyo:

Wakili: Nani alikuteua kufanya kazi ya ukadiriaji wa gharama za ujenzi wa mradi huo?

Shahidi: Kampuni ya ukandarasi ya Design & Services Ltd, kampuni ambayo ndiyo iliyopewa kazi ya kuchora majengo ya BoT.

Wakili: Ni mazoea katika shughuli za ujenzi kufanyika kwa mabadiliko?

Shahidi: Ni mazoea na inaruhusiwa.

Wakili: Katika mkataba wa awali kabla mabadiliko hayajafanyika ulikadiria mradi uwe wa gharama kiasi gani?

Shahidi: Dola za Marekani milioni 73.

Wakili: Kama kiasi hicho cha fedha kilitumika chote kwenye mradi, unafikiri kilisababisha hasara?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Nani alikuambia BoT imefanya mabadiliko ya mradi huo?

Shahidi: Nilipata maelekezo kutoka Kampuni ya D&S Ltd.

Wakili: Kwanini BoT ilifanya mabadiliko ya mradi?

Shahidi: Si kazi yangu kujua.

Wakili: Hicho kielelezo ulichokitoa ni ripoti ya mradi mzima?

Shahidi: Mmh! Siyo ripoti ila ni sehemu ya ripoti (watu wakaangua kicheko).

Wakili: Nani alikuambia uandae ripoti ya mradi huo?

Shahidi: Kampuni ya D&S.

Wakili: Lini ulimaliza kazi uliyopewa katika mradi huo?

Shahidi: Mwishoni mwa Februari 2008.

Wakili: Ulipata sababu za kufanyika kwa mabadiliko ya mradi?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Utakubaliana na mimi mabadiliko ya mradi yalitokana na matakwa ya mteja wenu ambaye ni BoT?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Wakati ukifanya kazi hiyo, uliwahi kuwasiliana moja kwa moja na Liyumba?

Shahidi: Hapana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 10 na 24 itakapokuja kwa kutajwa na kuendelea kusikilizwa mfululizo kuanzia Januari 26 – Februari 6 mwakani.

Liyumba anakabiliwa na makosa ya kuidhinisha mradi wa ujenzi wa majengo pacha BoT bila idhini ya bodi ya wakurugenzi, hivyo kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Novemba 27 mwaka 2009

SHAHIDI MWINGINE ABANWA KESI YA LIYUMBA

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa tano wa upande wa mashitaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, ameieleza mahakama kuwa hana kumbukumbu ya idadi ya maombi na kiasi cha fedha za nyongeza kilichokuwa kikiletwa na menejimenti kwenye bodi ya wakurugenzi ili ipate idhini.


Liyumba, anakabiliwa na tuhuma za matumuzi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Shahidi huyo ambaye ni mhadhiri kutoka Idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Dk. Natu Mwamba (48), alitoa amelezo hayo jana wakati akijibu maswali ya jopo la mahakimu wakazi, Edson Mkasimongwa, anayesaidiana na Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa, baada ya kuhojiwa na mawakili wa utetezi na upande wa mashitaka.

“Kwanza, sikumbuki menejimenti ilileta maombi mara ngapi kwenye bodi yetu ya kutaka idhini ya matumizi ya nyongeza ya mradi…vile vile siwezi kukumbuka hayo maombi yaliletwa mara ngapi na menejimenti, pia sikumbuki ni kiasi gani cha fedha kilichokuwa kimeainishwa kwenye maombi hayo.

“Na kuniuliza hilo ni changamoto kubwa kwangu,” alidai Dk. Mwamba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi.

Yafuatayo ni mahojiano kati ya mahakimu wakazi na shahidi huyo:

Hakimu: Ulisema maombi ya nyongeza ya kutaka bodi yenu iyaidhinishe yalikuwa yakiegemea kwenye vikao vya dharura, je, dharura za menejimenti za kuitaka bodi ikutane zilitokea mara ngapi?

Shahidi: Siwezi kukumbuka.

Hakimu: Kwanini hukushtuka? Ni menejimenti iliyoomba vikao vya dharura vya bodi mara kwa mara?

Shahidi: Kwakuwa mwenyekiti wa bodi, yaani gavana, alikuwa ana kofia mbili, yaani pia ndiye aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, naweza kusema alikuwa anatu ‘over power’ wajumbe.

Hakimu: Unaweza kukumbuka bodi ililetewa na menejimenti mara ngapi maombi hayo ya matumizi ya nyongeza ya mradi wa ujenzi wa minara pacha?

Shahidi: Sikumbuki.

Hakimu: Ni kiasi gani kikubwa wewe kilikushtua katika maombi hayo ya matumizi yaliyowasilishwa na menejimenti katika bodi yenu?

Shahidi: Sikumbuki kiasi sahihi, ila ni kama mabilioni.

Hakimu: Hayo malipo ya matumuzi ya nyongeza kabla ya bodi kuyapa idhini, yalikuwa yanapitishwa na nani?

Shahidi: Gavana.

Hakimu: Bodi yenu iliiyaidhinisha malipo hayo?

Shahidi: Tuliyaidhinisha, kwani tulikuwa hatuna jinsi.

Hakimu: Kwa mujibu wa maelezo yako umeieleza mahakama bodi iliyaidhinisha malipo kwa sababu mlikuwa hamridhishwi na utaratibu huo, sasa kwanini hamkufikiria kujiuzulu ujumbe wa bodi?

Shahidi: Mmh! Hilo la kujiuzulu tulilifikiria ila tuliona tumekabidhiwa jukumu la kitaifa, tukashindwa kujiuzulu.

Hakimu: Mahakama imepokea ripoti inayoonyesha imeandikwa na wajumbe wa bodi, je, ieleze mahakama hii ripoti ni ripoti ya bodi?

Shahidi: Hapana siyo ripoti ya bodi, hiyo ripoti tuliandika sisi wajumbe wa bodi wa kuchaguliwa na ambao tulikuwa tunamaliza muda wetu na tuliweka saini zetu, wala haikumhusisha gavana, naibu gavana na Katibu wa Benki, ambao nao hao ni wajumbe wa bodi na wanaingia kwenye bodi hiyo kwa mujibu wa nyadhifa zao katika benki hiyo na tulivyomaliza kuiandika tuliikabidhi kwa bodi mpya.

Kwa hiyo naomba ieleweke hiyo taarifa siyo ya bodi, wala bodi ndogo, ni ya sisi wajumbe wa bodi ambao tulichaguliwa na tulikuwa tunamaliza muda wetu.

Yafuatayo ni mahojiano baina ya mawakili wa utetezi, Hudson Ndusyepo, Jaji mstaafu Hillary Mkate, Onesmo Kyauke na Majura Magafu kwa shahidi huyo:

Wakili: Bajeti ya BoT zilikuwa zinaidhinishwa mara ngapi?

Shahidi: Mara moja.

Wakili: Baada ya bajeti hiyo, kwa mwaka kulikuwa na bajeti nyingine?

Shahidi: Mara nyingine zilikuwa zinakuja bajeti za nyongeza (supplementary bajeti).

Wakili: Umeieleza mahakama mara nyingi menejimenti ilikuwa inaleta maombi kwenye bodi, wakati inakuwa tayari imeishatekeleza nyongeza ya matumuzi?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Aliyekuwa anawasilisha taarifa ya maombi ya matumizi ya nyongeza kwenye bodi ni nani?

Shahidi: Meneja Mradi (Deogratius Kweka), na alikuwa anafanya hivyo baada ya Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Liyumba kuomba idhini kwa mwenyekiti wa bodi ili meneja mradi atoe taarifa hiyo.

Wakili: Taarifa hiyo ya maombi ya nyongeza ilikuwa imetayarishwa na nani?

Shahidi: Menejimenti ya BoT.

Shahidi: Bodi kupitisha ombi la nyongeza ya matumuzi wakati tayari matumizi yameishafanyika ni sahihi?

Shahidi: Kiutaratibu siyo sahihi.

Wakili: Bodi kupitisha ombi la nyongeza ya matumuzi baada ya matumuzi kuwa yameishafanyika kisheria, mnaweza?

Shahidi: Bodi inaweza, ila ni kinyume cha taratibu.

Wakili: Taratibu zipi hizo?

Shahidi: Kimya.

Awali akiongozwa na Wakili wa Serikali, Juma Mzarau, kutoa ushahidi wake, aliiambia mahakama kuwa wajumbe wa bodi walikuwa hawalidhishwi na menejimenti jinsi ilivyokuwa ikiwaletea maombi ya nyongeza ya bajeti wakati tayari matumizi yameishafanyika, lakini bodi haikuwa na jinsi, ikawa inaidhinisha maombi hayo.

Aidha, kiongozi wa jopo, Edson Mkasimongwa, aliahirisha kesi hiyo hadi leo, ambapo shahidi wa sita wa upande wa mashitaka anatarajiwa kuanza kutoa ushahidi wake.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 25 mwaka 2009.

SHAHIDI:BODI BoT HAIKUWAHI KUMLALAMIKIA LIYUMBA

Na Happiness Katabazi

MENEJA wa Masuala ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Justo Tongola (45), ambaye ni shahidi wa pili katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa BoT, Amatus Liyumba, ameieleza mahakama kuwa hajawahi kuona wala kusikia bodi hiyo ikilalamikia utendaji kazi wa Liyumba.


Akitoa ushahidi huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, pia alidai hajawahi kushuhudia bodi hiyo ikikataa kuidhinisha maombi ya menejimeti ya benki hiyo wala aliyekuwa Gavana wa BoT, marehemu Daudi Balali, akilalamikia mradi wa ujenzi wa minara pacha.

Shahidi huyo alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa maswali na mawakili wa utetezi Majura Magafu, Hudson Ndusyepo, Hillary Mkate, na Onesmo Kyauke mbele ya Jopo la Mahakimu Wakazi linaloongozwa na Edson Mkasimongwa anayesaidiana na Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa.

Sehemu ya mahojiano ya mawakili wa utetezi na shahidi huyo yalikuwa kama ifuatavyo:

Wakili: Nani alitoa kibali cha Kurugenzi ya Utumishi na Utawala iliyokuwa ikiongozwa na Liyumba, iratibu mradi huo?

Shahidi: Sina hakika, ila miradi yote inayoangukia kwenye eneo la Capital Expenditure inaratibiwa na ofisi hiyo.

Wakili: Umesema ofisi iliyokuwa ikiongozwa na mshtakiwa (Liyumba) ilikuwa ikiratibu mradi huo, ilikuwa ikifanyakazi hiyo kwa niaba ya Benki Kuu?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Taarifa za uaandaaji wa mabadiliko ya upanuzi wa ujenzi zilikuwa zinaratibiwa na ofisi ya mshtakiwa na nani?

Shahidi: Ofisi ya Liyumba na Meneja Mradi, Deogratius Kweka, ambaye aliajiriwa na Benki Kuu kwa mkataba.

Wakili: Nani mwingine alihusika katika uandaaji wa taarifa hiyo ya mabadiliko ya ujenzi ukiacha Kweka?

Shahidi: Hilo sina taarifa.

Wakili: Taarifa ikishaandaliwa inapelekwa kwenye bodi?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Ulisema mradi ulikuwa kwenye Capital Expenditure katika kipindi chote bodi ilikuwa hairidhiki na mabadiliko?

Shahidi: Kuna kipindi bodi baada ya kupokea maombi kadhaa ilikuwa hairidhiki na ilikuwa inarudisha baadhi ya maombi kwa menejimenti, ili zifanyiwe marekibisho kisha zinarejeshwa tena kwenye bodi na bodi inatoa idhini.

Wakili: Kuna kipindi chochote bodi iliwahi kumlalamikia Liyumba kama Liyumba?

Shahidi: Hilo sijawahi kusikia wala kuliona kwenye vikao ila kuna wakati menejimenti ilikuwa inaondolewa kwenye vikao.

Wakili: Ina maana Gavana na Naibu Gavana waliondolewa kwenye vikao vya Menejimenti?

Shahidi: Hapana, kwani hao ni kwa vyeo vyao ni sehemu ya bodi ila baadhi ya watendaji waliondolewa.

Wakili: Kuna sehemu uliona Gavana aliwahi kulalamika kuhusu mradi huo?

Shahidi: Mimi binafsi sijawahi kuona hilo.

Wakili: Ni kweli kwamba hakuna hata siku moja kikao cha menejimenti hakijawahi kujadili mradi huo hata mara moja?

Shahidi: Sikumbuki kama menejimenti iliwahi kuzungumzia mradi huo.

Wakili: Inawezekana kurugenzi ya utawala ipewe jukumu la kuratibu mradi halafu isiujadili?

Shahidi: Menejimenti ipo katika sehemu mbili. Mosi, Gavana ndiye mwenye mamlaka ya kusimamia menejimenti na halazimiki kupeleka kila jambo kwenye menejimenti.

Wakili: Nitakuwa sijakosoe, mambo yanayofanywa na utawala lazima Gavana awe na taarifa?

Wakili: Utakubaliana na mimi jukumu la bodi ni kulinda maslahi ya BoT na serikali kwa ujumla yasihujumiwe?

Shahidi: Ni kweli na hilo ni jukumu la kisheria.

Awali, akihojiwa na wakili wa serikali, Juma Mzarau, shahidi huyo alidai alianza kujishughulikia masuala ya bodi kwa kumsaidia katibu wa Benki ambaye alikuwa na majukumu ya kuratibu maandalizi ya mikutano ya bodi na menejimenti na kuhakikisha wajumbe wanapata madokezi yote na maazimo yote yanawekwa kwenye maandishi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 28 itakapotajwa na kupangwa siku ya kuendelea kusikiliza.

Chanzo:Gazerti la Tanzania Daima la Jumamosi, Novemba 24,2009

KESI YA RADA BADO YAPIGWA KALENDA

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kwa mara nyingine imeendelea kuahirisha kesi ya rushwa katika ununuzi wa rada ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) inayomkabili Seileth Vithlani kutokana na mshitakiwa huyo kutokamatwa hadi sasa.


Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 4 mwakani, baada ya wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo kutokana na sababu hiyo.

Tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo, Novemba mwaka 2007 mahakamani hapo, imekuwa ikiahirishwa kwa kuwa mshitakiwa hiyo ambaye alikuwa wakala wa ununuzi wa rada hiyo kutokamatwa.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, mshitakiwa huyo anadaiwa kusema uongo kuhusiana na Kampuni ya Envers Trading Corporation iliyokuwa ikimilikiwa na Pablo Espino na Adelina Estriby,tofauti na maelezo hayo, mtuhumiwa ndiye aliyekuwa mmiliki halali wa kampuni hiyo akiwa kama mkurugenzi na kwamba alipokea kiasi cha asilimia 31 ya uwakala wa mauzo ya rada ambayo ni sawa na dola 12,391,459.50 chini ya mkataba uliokuwa kati ya Red Diamond Trading Corp na Enves Trading Corp.

Katika shitaka la pili, inadaiwa Julai 28 mwaka jana, akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mtuhumiwa alitoa maneno ya uongo kuwa alilipwa dola 390,000 za Marekani na Kampuni ya British Aero Space (BAE System) ambayo ni sawa na asilimia moja ya manunuzi ya rada ambayo ilinunuliwa na Tanzania wakati ukweli ni kwamba alipewa asilimia 31.

Mtuhumiwa huyo pia anakabiliwa na shitaka la kutoa taarifa za uongo kwa ofisa wa TAKUKURU, Kassim Ephrem, Desemba 27, mwaka jana, eneo la Kinondoni, Dar es Salaam kuwa alilipwa asilimia moja ya manunuzi ya rada huku akijua taarifa hiyo itaharibu upelelezi wa suala hilo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima Novemba 20, 2009

SHAHIDI WA SERIKALI AMTAKASA LIYUMBA

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa tatu katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221, inayomkabili Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala mstaafu wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba, ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa huyo hakuwa na uamuzi wa mwisho katika mradi wa ujenzi wa majengo pacha.


Shahidi huyo Julius Ruta Angelo (49) ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha BoT, alitoa madai hayo mbele ya jopo la mahakimu wakazi; Edson Mkasimongwa, Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakati akihojiwa na wakili wa utetezi, Majura Magafu.

Angelo aliieleza mahakama kuwa, Bodi ya Wakurugenzi ya BoT, ndiyo ilikuwa na uamuzi wa mwisho wa nini kifanyike na nini kisifanyike katika mradi wa ujenzi wa majengo ya Minara Pacha.

“Waheshimiwa, mshitakiwa (Liyumba) kwa wadhifa wake kipindi kile hakuwa na uamuzi wa mwisho katika mradi huo, bali bodi ya wakurugenzi ndiyo ilikuwa na uamuzi wa mwisho wa nini kifanyike na nini kisifanyike,” alidai Angelo.

Yafuatayo ni mahojiano baina ya mawakili wa utetezi Majura Magafu, Hudson Ndusyepo, Jaji Mstaafu Hillary Mkate, Onesmo Kyauke dhidi ya shahidi Anjelo:

Wakili: Nani alikuwa na majukumu ya kusimamia ujenzi wa mradi huu?

Shahidi: Ulikuwa unaratibiwa na Kurugenzi ya Utumishi na Utawala iliyokuwa ikiongozwa na Liyumba.

Wakili: Ni nani alikuwa na maamuzi ya mwisho ya hili lifanyike na hili lisifanyike katika mradi huu?

Shahidi: Bodi ya Wakurugenzi ya BoT.

Wakili: Nitakuwa sijakosea nikisema aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala (Liyumba), asingeweza kusema ili lifanyike au ili lisifanyike bila kupitishwa na Bodi ya Wakurugenzi?

Shahidi: Nakubaliana na wewe.

Wakili: Maoni au mapendekezo yaliyotolewa na kurugenzi iliyokuwa ikiongozwa na mshitakiwa kuhusu mradi huo yalikuwa yanatoka wapi. Kwenye Menejimenti, Utawala?

Shahidi: Mmh! Naomba uniulize kuhusu mambo ya fedha, hayo mengine siyajui.

Wakili: Masuala ya fedha kwenye mradi huo yalikuwa yanaanzia wapi?

Shahidi: Yalikuwa yanaanzia kwa Meneja wa Mradi (Deogratius Kweka), na yakitoka kwake yanaenda kwenye ofisi ya Liyumba, kisha yanapelekwa kwa Gavana (Daud Balali) ambaye yeye ndiyo anaidhisha.

Wakili: Kwa kifupi, Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, hakuwa na kauli ya mwisho kwenye ujenzi wa mradi huo?

Shahidi: Ni kweli kabisa, hakuwa na kauli ya mwisho.

Yafuatayo ni mahojiano kati ya jopo la Mahakimu Wakazi na shahidi huyo:

Hakimu: Liyumba kama Liyumba aliwahi kuidhinisha malipo?

Shahidi: Kimya.

Hakimu: Ulisema Bodi ya Wakurugenzi iliikemea menejimenti, tueleze bodi hiyo ilikemea mambo gani hayo?

Shahidi: Mengi iliyoyakemea ni malipo yaliyoidhinishwa na gavana na mengine iliyokemea siyakumbuki.

Hakimu: Bodi ilimkemea Liyumba?

Shahidi: Hapana, ilikemea malipo makubwa yaliyoidhinishwa na gavana na malipo madogo yaliyoidhinishwa na Liyumba kabla ya kupata kibali cha bodi.

Kesi hiyo ilipangwa ianze kusikilizwa mfululizo kuanzia jana hadi Novemba 26, lakini hata hivyo wakili wa serikali, Mzarau aliomba iahirishwe hadi Jumatatu hiyo kwa sababu aliyepanga kutoa ushahidi leo ni mgonjwa na anatibiwa nchini Kenya.

Alidai kuwa mashahidi wengine, wanakaa mbali na wanatarajia kuongeza idadi ya mashahidi na watawasilisha ombi hilo kwa maandishi.

Hata hivyo, ombi hilo lilipingwa na wakili Magafu, akidai kuwa hoja kwamba mashahidi wapo mbali si ya msingi kwani wanafahamu baadhi ya mashahidi wa upande wa mashitaka Bosco Kimela, yupo gereza la Keko, Profesa Semboja yupo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wanapatikana kwa urahisi.

“Naomba tuwe makini na kesi hii, mteja wetu anaendelea kuteseka rumande na ni mgonjwa, anahitajika kwenda kutibiwa nje ya nchi, lakini inashindikana kwa sababu yupo rumande, kama upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kesi yao useme,” alidai Magafu.

Liyumba alifikishwa mahakamani hapo Januari 27 mwaka huu, akikabiliwa na makosa ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma na kuidhinisha ujenzi wa mradi huo bila idhini ya Bodi ya BoT, hivyo kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Liyumba anaendelea kusota rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka atoe fedha taslimu au hati yenye mali yenye thamani ya sh bilioni 111.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 19,2009

MAPYA YAIBUKA KESI YA MRAMBA,YONA

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa pili katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7, inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na wenzake, Betha Msoka (44), ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa hakuna mahali popote panapomlazimisha Waziri wa Fedha kuomba ushauri wa kutoa msamaha wa kodi Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Sambamba na hilo, pia Msoka ambaye ni mwanasheria kitaaluma, amesisitiza kuwa hana ushahidi kwamba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali haikushirikishwa kwenye mchakato wa kuitafuta Kampuni ya ukaguzi wa madini ya Alex Stewart Government Business Corporation.

Wakati shahidi huyo akitoa maelezo hayo, kwa mujibu wa hati ya mashitaka inasomeka kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na kosa la kukaidi ushauri wa TRA uliotaka kampuni hiyo isipewe msamaha wa kodi, lakini kwa nafasi zao waliamua kutoa msamaha huo.

Shahidi huyo wa upande wa mashitaka alitoa madai hayo jana mbele ya jopo la mahakimu wakazi; John Utamwa, Saul Kinemela na Sam Rumanyika wakati akihojiwa na mawakili wa utetezi; Hurbet Nyange, Peter Swai, Elias Msuya, Cuthbet Tenga na Profesa Shahidi.

Yafuatayo ni mahojiano baina ya mawakili hao na shahidi huyo:

Wakili: Ulishawahi kufanya kazi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Mwanasheria wa Serikali?
Shahidi: Ndiyo.
Wakili: Ulifanya kazi katika ofisi hiyo kwa muda gani?
Shahidi: Sikumbuki ila nilifanya kazi kwa muda mfupi kwani nilipata barua toka Ofisi ya Utumishi ikiniarifu nahamishiwa Wizara ya Fedha.
Wakili: Hiyo barua ya Utumishi ilikuwa ni ya kukubadilisha kazi au kituo cha kazi?
Shahidi: Kituo cha kazi.
Wakili: Unayo hiyo barua inayokuonyesha umebadilishiwa kazi?
Shahidi: Sina.
Wakili: Tangu 1992 ulipohamishiwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, uliwahi kurudi katika ofisi hiyo kufanya kazi za ofisi hiyo?
Shahidi: Sikuwahi kurudi kwa sababu niliajiriwa na Wizara ya Fedha.
Wakili: Baada ya kutoka katika ofisi ya AG uliwahi kuwa na access ya majalada ya AG?
Shahidi: Sikuwahi kuwa na access ya kushika majalada ya ofisi hiyo.
Wakili: Je, nitakosea kama wewe ukiwa mtumishi wa serikali kama wakili wa serikali, ulikuwa ni daraja kati ya Wizara ya Fedha na ofisi ya AG?
Shahidi: Kuna masuala ambayo ofisi hizo mbili zilikuwa zikishirikiana.
Wakili: Nitakuwa sahihi nikisema masuala ya kisheria mnayoshirikiana na AG, ni Wizara ya Fedha ilikuwa inahusika moja kwa moja?
Shahidi: Mengi ni yale yaliyokuwa yanahusu Wizara ya Fedha moja kwa moja na mengine ambayo yana commontiment na wizara.
Wakili: Ulisema uliitwa BoT kujadili rasimu ya mkataba wa Alex Stewart, na ulibaini vipengele viwili vya kodi na ada, kipi kilikuwa kinahusu wizara yako?
Shahidi: Kipengele cha kodi kilikuwa kinahusu Wizara ya Fedha.
Wakili: Kipengele cha ada wewe akikukusumbua kama mwanasheria wa Wizara ya Fedha?
Shahidi: Ili msamaha wa kodi utolewe, ni lazima Waziri wa Fedha atoe idhini.
Wakili: Je, uliwasiliana na ofisi ya AG kuhusu hicho kipengele cha kodi?
Shahidi: Hatukuwasiliana na AG.
Wakili: Hivi Mramba, Yona na Mgonja wakati wakiwa na nyadhifa walikuwa ni wanasheria?
Shahidi: Hawakuwa na hadi sasa hawana taaluma ya sheria.

Wakili:Juzi uliieleza mahakama hii kwamba tangu uondoke ofisi ya AG ujawahi kurudi kufanyakazi hapo na nikakuuliza unasema uongo ,ukakataa.Kama unakumbuka dokezo la aliyekuwa Waziri wa Nishati(Yona)alilomwandikia Rais Benjamin Mkapa la Mei 11 mwaka 2003 linasomeka “Baada ya kukubali dokezo langu la Machi 3 mwaka 2003 kuhusu umuhimu wa kuanzisha ukaguzi wa dhahabu inayochimbwa na kuuzwa nchi za nje ,majadiliano kati ya Wizaya Nishati,Fedha,BoT na AG yanaenda vizuri’.Nikikwambia Wizara ya Nishati ilikuwa inawasiliana na na AG utasemaje?
Shahidi:Siwezi kujua.
Wakili:Kwahiyo wewe ulikwenda kwenye timu ya majadilio ya rasimu ya mkataba kama mwanasheria wa umma kwani sijakusikia wewe kama unataaluma ya uchumi?
Shahidi:Ndiyo nilikwenda kama mwanasheria.
Wakili:Wewe mwenyewe ulisema ulikuwa ni daraja kati ya Wizara ya Fedha na AG ,wewe uliona kuna haja katika timu hiyo kuletwa mwanasheria toka ofisi ya AG?
Shahidi:Watakuja watu wa ofisi ya AG watasema wenyewe.
Wakili:Una uhakika kama Wizara ya Nishati na Madini haikutafuta ushauri wa AG katika mchakato mzima wa kutafuta kampuni hiyo?
Shahidi:Sina uhakika.
Wakili;Jana ulisema uliandika barua TRA kuomba ushauri kuhusu kipengele cha msamaha wa kodi wa kampuni hiyo ,ebu ionyeshe mahakama hiyo barua?
Shahidi:Sina.
Wakili:Hiyo barua uliyoiandikia TRA kuhusu kipengele cha msamaha wa kodi , inamuweka Mramba kwenye nafasi nzuri.
Shahidi:Ndiyo inamuweka kwenye nafasi nzuri katika kutoa msamaha wa kodi.
Wakili: Una weza kujua ni kwanini upande wa mashitaka umeshindwa kukupa hiyo barua ili uitoe mahakamani kama kielelezo?
Shahidi:Sijui.
Wakili:Nikikwambia upande wa mashitaka umeiacha hiyo barua makusudi ili kumkandamiza mshitakiwa wa kwanza(Mramba)?
Shahidi:Sijui.
Wakili:Ulisema wizara ya Fedha inapotengeza matangazo ya serikali(government Notice) ni kwanini inashirikiana na ofisi ya AG?
Shahidi:Kwasababu matangazo hayo ya serikali ni nyaraka za kisheria.
Wakili:Je Gorvement Notice yakiakikiwa na AG halafu yakasainiwa na waziri wa Fedha, Je waziri akasini matangazo hayo ya serikali,kiongozi huyo anashtahili kulaumiwa?
Shahidi:Hastahili kulaumiwa.
Wakili: Ulisema ofisi ya AG haikuwa na mwakilishi kwenye timu yenu?
Shahidi:Ndiyo.
Wakili:Je hukumaanisha mchakato mzima haukurikisha ofisi ya AG?
Shahidi:Sikumaanisha hivyo.
Wakili:Utakubaliana namimi kwamba mchakato mzima ulishirikisha ofisi ya AG?
Shahidi:Sina hakika na hilo.
Wakili:Una fahamu kuwa Mei 2 mwaka 2003,AG alijibu barua ya Yona aliyomwandikia Machi 3 mwaka 2003?
Shahidi:Sifahamu.
Wakili:Nikikwambia barua hiyo ya AG ipo unaweza kubisha kwani?
Shahidi:Siwezi kubisha.
Wakili:Unaweza kutoa ushahidi kwamba hakukuwepo mawasiliano kati ya Wizara ya Nishati na ofisi ya AG katika mchakato wa kutafuta kampuni hiyo ya ukaguzi wa madini?
Shahidi:Sina.
Wakili:Timu yenu ilikuwa inawajibika kwa nani?
Shahidi:Gavana(Marehemu Daud Ballali).
Wakili: Unafahamu mchakato mzima ulitakiwa kusimamiwa na BoT kwa niabaya ya serikali?
Shahidi:Siwezi kujua.
Wakili:Juzi ulisema Gavana alisaini mkataba mkataba wa serikali na kampuni hiyo, mwingine aliyesaini huo mkataba ni nani?
Shahidi:Katibu wa BoT, Bosco Kimela na huyu Edwin Frolence alisaini kwaniabaya kampuni hiyo na mkataba ulisainiwa Juni 14 mwaka 2003.
Wakili:Timu yenu ya majadiliano ndiyo ilipelekea mkataba huo kusainiwa?
Shahidi:Ndiyo.
Wakili:Timu yenu ilikuwa huru kufanyakazi na wala haikuingiliwa na mtu?
Shahidi:sikumbuki.
Wakili:Hawa washitakiwa walishawahi kuingilia timu yenu?
Shahidi:Sijawahi kuwashuhudia wakiingilia timu yetu.
Wakili:Mkataba uliosaini ni matokeo ya timu yenu, Je ndiyo ulioweka kipengele cha kodi?
Shahidi:Siyo kwasababu kipengele katika timu yetu tulikiwa kando na pia isingewezekana kwani waziri hakuwa ameishatoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo.
Wakili:Timu yenu ndiyo iliyopitisha ada ya kampuni hiyo iwe asilimia 1.9 na mkaiweka kwenye ule mkataba?
Shahidi:Ndiyo tuliweka ada hiyo.
Wakili:Unafahamu Juni 4 mwaka 2003 timu yenu ilimjulisha Yona kwamba suala la ada limeishamalizika na barua hiyo iliandikwa na Gavana?
Shahidi:Hilo silifahamu.
Wakili:Nikikwambia barua hiyo ipo?
Shahidi:Sibishi.
Waliki:Ulisema waziri ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya kutoa msamaha wa kodi sasa kwanini wewe ulipeleka barua TRA kuomba ushauri?
Shahidi:Ieleweke hakuna mahala popote panapomlazimisha waziri wa Fedha aombe ushauri wa msamaha wa kodi kwa kampuni yoyote kwa TRA.
Wakili:Mkataba huo ulikuwa unasemaje?
Shahidi:Ulisema Alex Stewart itasamehewa kodi zote.
Wakili:Jukumu la Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye matangazo ya serikali nini?
Shahidi:Ni kuakikisha matangazo ya serikali linakubalika kisheria.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Desemba 15-18 mwaka huu, itakapokuja kwa ajili ya shahidi wa tatu wa upande wa mashitaka kuanza kutoa ushahidi wake.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Novemba 6,2009



MTALAAMU:NILISHAURI YONA KUACHANA NA ALEX STEWART

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma, inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na wenzake, Godwin Nyero (48), ameendelea kuiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kuwa, waziri akiona ushauri uliotolewa na mtaalamu haufahi, anaweza kuukataa.


Nyero ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Masuala ya Uchumi katika Wizara ya Nishati na Madini, alitoa maelezo hayo jana mbele ya jopo la mahakimu wakazi; John Utamwa, Saul Kinemela na Sam Rumanyika wakati akijibu maswali aliyokuwa akihojiwa na Wakili Cuthbet Tenga na E. Msuya ambao wanamtetea mshitakiwa wa pili, Daniel Yona na Profesa Leonard Shahidi, anayemtetea mshitakiwa wa tatu, Gray Mgonja.

Shahidi huyo ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya kuandaa mchakato wa kuileta kampuni ya ukaguzi wa madini nchini ya Alex Stewart Government Business Corporation, alidai kuwa baada ya kumalizika kwa mchakato huo, alimpelekea dokezo aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Yona kutaka serikali isiipe kazi kampuni hiyo.

Hata hivyo, mawakili hao wa mshitakiwa wa pili walilazimika kuiomba mahakama isitishe kuendelea kumhoji shahidi huyo kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuleta nyaraka za mkataba wa serikali na kampuni hiyo ambazo walidai zingeletwa mahakamani hapo ili zitumike kumuuliza maswali.

Ombi hilo lilikubaliwa na jopo hilo ambalo liliuamuru upande wa mashitaka ulete nyaraka hizo Novemba 16 mwaka huu ili shahidi huyo aendelee kuhojiwa na mawakili hao.
Mahojiano kati ya shahidi huyo na mawakili hao yalikuwa hivi:

Wakili: Kwanini mapendekezo yako ya kuikataa kampuni hiyo hukutoa nakala kwa Katibu Mkuu na Kamishna wa Madini?
Shahidi: Katibu Mkuu nilimpatia taarifa kwa mdomo na Kamishna wa Madini sikumpatia taarifa.
Wakili: Ieleze mahakama mantiki ya kumpa waziri taarifa kwa maandishi, kamishna wa madini usimpatie taarifa na katibu mkuu umpatie kwa mdomo.
Shahidi: Mh! Ni taarifa tu ambayo nilimpa ushauri waziri (Yona) autumie yeye kama ataona unafaa na akiona haufahi pia kiongozi huyo wa wizara alazimiki kuniambia mimi mtaalamu.
Wakili: Waziri akiona ushauri wako wewe mtaalamu haufahi anakuwa amekosea?
Shahidi: Hajakosea.
Wakili: Kamishna wa Madini kama ulimwambia ushauri huo kwa mdomo alikujibu nini?
Shahidi: Alinijibu nimwandikie dokezo waziri wangu.
Wakili: Ni kweli kwamba kulikuwa na ulazima wa serikali kuleta mkaguzi wa dhahabu hapa nchini kufuatia malalamiko ya wabunge na wananchi kwamba madini yetu yanaibwa?
Shahidi: Ni kweli.
Wakili: Malalamiko ya wabunge yalijitokeza bungeni?
Shahidi: Ndiyo.
Wakili: Serikali ilivyoanza mchakato wa kuipata kampuni hiyo ilikuwa inatekeleza matakwa ya Bunge?
Shahidi: Hilo sifahamu.
Wakili: Kamati yenu ya watu wanne iliteuliwa rasmi lini?
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili: Yawezekana ilikuwa Septemba 12, 2002?
Shahidi: Yawezekana.
Wakili: Mwenyekiti wa kamati yenu alikuwa nani?
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili: Katibu Mkuu wa kamati hiyo alikuwa nani?
Shahidi: Sikumbuki ila najua wajumbe wenzangu watatu walitoka BoT.
Wakili: Hao wajumbe watatu walikuwa wataalamu wa mambo gani kwenye hiyo kamati yenu kwa sababu wewe ulishaiambia mahakama ulikuwa mtaalamu wa madini?
Shahidi: Sifahamu.
Wakili: Kabla ya kwenda kwenye hiyo kamati mlipewa mwongozo wa kufanya kazi?
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili: Mlikuwa mnatumia utaratibu gani wa kufikia uamuzi?
Shahidi: Consensus.
Wakili: Ni kweli kwamba na wewe ulikuwa unafikia consensus hiyo?
Shahidi: Ndiyo.
Wakili: Consensus inafikiwa baada ya majadiliano ya wajumbe wanne?
Shahidi: Ndiyo.
Wakili: Juzi uliiambia mahakama kwamba masuala yenye utata mliyapeleka kwa gavana na yasiyo na utata kwenye kamati yenu yaliendelea kujadiliwa?
Shahidi: Ndiyo.
Wakili: Hiyo kamati yenu ilifanya kazi yake kwa uhuru bila kuingiliwa na washitakiwa waliopo kizimbani?
Shahidi: Ndiyo.
Wakili: Kwanini ulipeleka mambo msiyokubaliana kwa Waziri Yona badala ya Gavana?
Shahidi: Kwa maelekezo ya waziri alivyonituma kazi, nikitoka kwenye kamati hiyo niwe namletea taarifa.
Aidha, shahidi wa pili, Betha Msoka (44), ambaye ni mwanasheria kitaaluma na kati ya mwaka 1992-2003 alikuwa ni ofisa mwandamizi msimamizi wa fedha toka Wizara ya Fedha, aliiambia mahakama kuwa mwaka 2003 alipewa maelekezo na mkuu wake kitengo cha huduma ya sheria wizarani hapo, Agness Bukuku ambaye sasa ni Msajili wa Hazina, akaiwakilishe wizara katika majadiliano ya mkataba wa kampuni hiyo ya ukaguzi wa madini na wizara yake.
Soka alidai aliudhuria majadiliano hayo yaliyoshirikisha wataalamu toka wizara ya Fedha,Nishati na Benki Kuu na majadiliano yalihusu mkataba wa mkaguzi wa madini ya dhahabu katika ya serikali ya Tanzania na Alex Stewart Gorvement Corporation ya Marekani na kwamba vikao vilijadili rasimu ya mkataba huo na baada ya kupitia walibaini vipengele vingi vya kitaalamu vinavyohusu Kodi na Ada.

Yafuatayo ni mahojiano kati ya Shahidi huyo na Wakili Mkuu wa Serikali Stanslaus Boniface:
Wakili:Hayo mambo mawili yalishughulikiwa vipi katika majadiliano yenu?
Shahidi:Suala la Ada lilishughulikiwa na Wizara ya Nishati.Na mkataba huo kwangu ulikuwa ni mgeni kwangu kwasababumimi nilikuwa natokea Wizara ya Fedha ,nilitizama kipengele cha kodi kwa makini.
Wakili:Baada ya kutizama kwamikini vipengele hivyo vilisema nini?
Shahidi:Vilikuwa vinatoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo na wataalamu wake.
Wakili:Wewe ulishughulikia vipi jambo hilo?
Shahidi:Mimi niliwaeleza wajumbe wenzake kwamba mwenye mamlaka ya mwisho ya kusamehe kodi ni Waziri wa Fedha kwahiyo hadi tupate ridhaa toka kwa waziri.
Wakili:Baada ya kuwaeleza hilo, wenzio majibu yao yalikuwaje?
Shahidi:Ni kitu ambacho waliamua kukiweka kando hadi Waziri atoe idhini.
Wakili:Wewe kama mwakilishi wa wizara ya Fedha ulifanyanini?
Shahidi:Nilimjulisha mkuu wangu wa kazi(Agnes Bukuku) kwa njia ya maandishi na baada ya kumueleza alikubaliana nami na barua ikaandikwa kwenda TRA kwaajili ya kuhusu vipengele vile viwili yaani vya ada na kodi.
Wakili:Namna gani ulishughulikana na kampuni hiyo ya ukaguzi?
Shahidi:Sikushiriki majadiliano tangu siku barua ya ushauri ilipopelekwa TRA wala sikujua nini kiliendelea kwani sikuitwa tena kwenye kikao.
Wakili:TRA walijibuje hiyo barua?
Shahidi:Ilisema kampuni hiyo haistahili kusamehewa kodi.
Wakili:Katika Timu yenu ya majadiliano ya mkataba huo alikuwepo mwakilishi toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali?
Shahidi:Hakuwepo.
Wakili:Soma hiki kielelezo cha kwanza, katika aya ya tano inasomekaje?.
Shahidi:Kielelezo hiki ni dokezo la Yona alilomwandikia Rais Mkapa,Machi 3 mwaka 2003,kinasomeka: ‘Kabla ya BoT haijachagua kampuni inayofaha itazingatia mapato ya serikali yasipungue na wawekezaji wasiumie kiasi cha kukata tama kuwekeza zaidi kwenye madini .Aidha tutapa ushauri toka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wakili:Soma tena na kielelezo hiki cha tatu kinasomekaje?
Shahidi:Hiki ni barua aliyoiandika Yona kwenda kwa rais Mkapa Mei 11,2003 na kinasomeka hivi: ‘Baada ya kukaandikia dokezo langu Machi 3 mwaka 2003 kuhusu umuhimu wa kuanzisha ukaguzi wa dhahabu inayochimba na kuuzwa nchi za nje , majadiliano kati ya Wizara ya Nishati.Fedha,BoT na Mwanasheria Mkuu wa Serikali yanaendelea vizuri.

Kesi hiyo inayovuta hisia za wengi, inaendelea tena ambapo mawakili wa utetezi wataanza kumhoji shahidi huyo wa pili.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi Novemba 5,2009

KESI YA MRAMBA,YONA YAIBUA MAPYA

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma, inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na wenzake, Godwin Nyero (48), ameendelea kuiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kuwa, waziri akiona ushauri uliotolewa na mtaalamu haufahi, anaweza kuukataa.


Nyero ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Masuala ya Uchumi katika Wizara ya Nishati na Madini, alitoa maelezo hayo jana mbele ya jopo la mahakimu wakazi; John Utamwa, Saul Kinemela na Sam Rumanyika wakati akijibu maswali aliyokuwa akihojiwa na Wakili Cuthbet Tenga na E. Msuya ambao wanamtetea mshitakiwa wa pili, Daniel Yona na Profesa Leonard Shahidi, anayemtetea mshitakiwa wa tatu, Gray Mgonja.

Shahidi huyo ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya kuandaa mchakato wa kuileta kampuni ya ukaguzi wa madini nchini ya Alex Stewart Government Business Corporation, alidai kuwa baada ya kumalizika kwa mchakato huo, alimpelekea dokezo aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Yona kutaka serikali isiipe kazi kampuni hiyo.

Hata hivyo, mawakili hao wa mshitakiwa wa pili walilazimika kuiomba mahakama isitishe kuendelea kumhoji shahidi huyo kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuleta nyaraka za mkataba wa serikali na kampuni hiyo ambazo walidai zingeletwa mahakamani hapo ili zitumike kumuuliza maswali.

Ombi hilo lilikubaliwa na jopo hilo ambalo liliuamuru upande wa mashitaka ulete nyaraka hizo Novemba 16 mwaka huu ili shahidi huyo aendelee kuhojiwa na mawakili hao.
Mahojiano kati ya shahidi huyo na mawakili hao yalikuwa hivi:

Wakili: Kwanini mapendekezo yako ya kuikataa kampuni hiyo hukutoa nakala kwa Katibu Mkuu na Kamishna wa Madini?
Shahidi: Katibu Mkuu nilimpatia taarifa kwa mdomo na Kamishna wa Madini sikumpatia taarifa.
Wakili: Ieleze mahakama mantiki ya kumpa waziri taarifa kwa maandishi, kamishna wa madini usimpatie taarifa na katibu mkuu umpatie kwa mdomo.
Shahidi: Mh! Ni taarifa tu ambayo nilimpa ushauri waziri (Yona) autumie yeye kama ataona unafaa na akiona haufahi pia kiongozi huyo wa wizara alazimiki kuniambia mimi mtaalamu.
Wakili: Waziri akiona ushauri wako wewe mtaalamu haufahi anakuwa amekosea?
Shahidi: Hajakosea.
Wakili: Kamishna wa Madini kama ulimwambia ushauri huo kwa mdomo alikujibu nini?
Shahidi: Alinijibu nimwandikie dokezo waziri wangu.
Wakili: Ni kweli kwamba kulikuwa na ulazima wa serikali kuleta mkaguzi wa dhahabu hapa nchini kufuatia malalamiko ya wabunge na wananchi kwamba madini yetu yanaibwa?
Shahidi: Ni kweli.
Wakili: Malalamiko ya wabunge yalijitokeza bungeni?
Shahidi: Ndiyo.
Wakili: Serikali ilivyoanza mchakato wa kuipata kampuni hiyo ilikuwa inatekeleza matakwa ya Bunge?
Shahidi: Hilo sifahamu.
Wakili: Kamati yenu ya watu wanne iliteuliwa rasmi lini?
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili: Yawezekana ilikuwa Septemba 12, 2002?
Shahidi: Yawezekana.
Wakili: Mwenyekiti wa kamati yenu alikuwa nani?
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili: Katibu Mkuu wa kamati hiyo alikuwa nani?
Shahidi: Sikumbuki ila najua wajumbe wenzangu watatu walitoka BoT.
Wakili: Hao wajumbe watatu walikuwa wataalamu wa mambo gani kwenye hiyo kamati yenu kwa sababu wewe ulishaiambia mahakama ulikuwa mtaalamu wa madini?
Shahidi: Sifahamu.
Wakili: Kabla ya kwenda kwenye hiyo kamati mlipewa mwongozo wa kufanya kazi?
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili: Mlikuwa mnatumia utaratibu gani wa kufikia uamuzi?
Shahidi: Consensus.
Wakili: Ni kweli kwamba na wewe ulikuwa unafikia consensus hiyo?
Shahidi: Ndiyo.
Wakili: Consensus inafikiwa baada ya majadiliano ya wajumbe wanne?
Shahidi: Ndiyo.
Wakili: Juzi uliiambia mahakama kwamba masuala yenye utata mliyapeleka kwa gavana na yasiyo na utata kwenye kamati yenu yaliendelea kujadiliwa?
Shahidi: Ndiyo.
Wakili: Hiyo kamati yenu ilifanya kazi yake kwa uhuru bila kuingiliwa na washitakiwa waliopo kizimbani?
Shahidi: Ndiyo.
Wakili: Kwanini ulipeleka mambo msiyokubaliana kwa Waziri Yona badala ya Gavana?
Shahidi: Kwa maelekezo ya waziri alivyonituma kazi, nikitoka kwenye kamati hiyo niwe namletea taarifa.
Aidha, shahidi wa pili, Betha Msoka (44), ambaye ni mwanasheria kitaaluma na kati ya mwaka 1992-2003 alikuwa ni ofisa mwandamizi msimamizi wa fedha toka Wizara ya Fedha, aliiambia mahakama kuwa mwaka 2003 alipewa maelekezo na mkuu wake kitengo cha huduma ya sheria wizarani hapo, Agness Bukuku ambaye sasa ni Msajili wa Hazina, akaiwakilishe wizara katika majadiliano ya mkataba wa kampuni hiyo ya ukaguzi wa madini na wizara yake.
Soka alidai aliudhuria majadiliano hayo yaliyoshirikisha wataalamu toka wizara ya Fedha,Nishati na Benki Kuu na majadiliano yalihusu mkataba wa mkaguzi wa madini ya dhahabu katika ya serikali ya Tanzania na Alex Stewart Gorvement Corporation ya Marekani na kwamba vikao vilijadili rasimu ya mkataba huo na baada ya kupitia walibaini vipengele vingi vya kitaalamu vinavyohusu Kodi na Ada.

Yafuatayo ni mahojiano kati ya Shahidi huyo na Wakili Mkuu wa Serikali Stanslaus Boniface:
Wakili:Hayo mambo mawili yalishughulikiwa vipi katika majadiliano yenu?
Shahidi:Suala la Ada lilishughulikiwa na Wizara ya Nishati.Na mkataba huo kwangu ulikuwa ni mgeni kwangu kwasababumimi nilikuwa natokea Wizara ya Fedha ,nilitizama kipengele cha kodi kwa makini.
Wakili:Baada ya kutizama kwamikini vipengele hivyo vilisema nini?
Shahidi:Vilikuwa vinatoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo na wataalamu wake.
Wakili:Wewe ulishughulikia vipi jambo hilo?
Shahidi:Mimi niliwaeleza wajumbe wenzake kwamba mwenye mamlaka ya mwisho ya kusamehe kodi ni Waziri wa Fedha kwahiyo hadi tupate ridhaa toka kwa waziri.
Wakili:Baada ya kuwaeleza hilo, wenzio majibu yao yalikuwaje?
Shahidi:Ni kitu ambacho waliamua kukiweka kando hadi Waziri atoe idhini.
Wakili:Wewe kama mwakilishi wa wizara ya Fedha ulifanyanini?
Shahidi:Nilimjulisha mkuu wangu wa kazi(Agnes Bukuku) kwa njia ya maandishi na baada ya kumueleza alikubaliana nami na barua ikaandikwa kwenda TRA kwaajili ya kuhusu vipengele vile viwili yaani vya ada na kodi.
Wakili:Namna gani ulishughulikana na kampuni hiyo ya ukaguzi?
Shahidi:Sikushiriki majadiliano tangu siku barua ya ushauri ilipopelekwa TRA wala sikujua nini kiliendelea kwani sikuitwa tena kwenye kikao.
Wakili:TRA walijibuje hiyo barua?
Shahidi:Ilisema kampuni hiyo haistahili kusamehewa kodi.
Wakili:Katika Timu yenu ya majadiliano ya mkataba huo alikuwepo mwakilishi toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali?
Shahidi:Hakuwepo.
Wakili:Soma hiki kielelezo cha kwanza, katika aya ya tano inasomekaje?.
Shahidi:Kielelezo hiki ni dokezo la Yona alilomwandikia Rais Mkapa,Machi 3 mwaka 2003,kinasomeka: ‘Kabla ya BoT haijachagua kampuni inayofaha itazingatia mapato ya serikali yasipungue na wawekezaji wasiumie kiasi cha kukata tama kuwekeza zaidi kwenye madini .Aidha tutapa ushauri toka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wakili:Soma tena na kielelezo hiki cha tatu kinasomekaje?
Shahidi:Hiki ni barua aliyoiandika Yona kwenda kwa rais Mkapa Mei 11,2003 na kinasomeka hivi: ‘Baada ya kukaandikia dokezo langu Machi 3 mwaka 2003 kuhusu umuhimu wa kuanzisha ukaguzi wa dhahabu inayochimba na kuuzwa nchi za nje , majadiliano kati ya Wizara ya Nishati.Fedha,BoT na Mwanasheria Mkuu wa Serikali yanaendelea vizuri.

Kesi hiyo inayovuta hisia za wengi, inaendelea tena ambapo mawakili wa utetezi wataanza kumhoji shahidi huyo wa pili.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi Novemba 5,2009

MKAPA ALIPULIWA MAHAKAMANI

.YADAIWA ALITOA IDHINI KULETWA ALEX STEWART
.SHAHIDI ADAI YONA ASINGEKATAA AGIZO LA RAIS
Na Happiness Katabazi

RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa anadaiwa kuandika barua iliyomtaka aliyekuwa Waziri wa NiShati na Madini, Daniel Yona kuharakisha mchakato wa kuileta Kampuni ya Alex Stewart Government Business Corporation kuja nchini kufanya ukaguzi wa dhahabu.


Yona ni mshitakiwa wa pili katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7. Pamoja nae washitakiwa wengine ni aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gray Mgonja.

Kuhusika kwa Mkapa kulibainishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, na shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri, Godwin Nyero (48) mbele ya jopo la mahakimu wakazi; John Utamwa, Saul Kinemela na Sam Rumanyika, wakati akihojiwa na wakili wa utetezi, Hurbet Nyange.

Nyero, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Masuala ya Uchumi katika Wizara ya Nishati na Madini, alitoa maelezo hayo baada ya wakili Nyange kumtaka asome kwa sauti kielelezo namba 10 kilicholetwa mahakamani hapo na upande wa mashitaka, ambacho ni barua iliyotoka kwa Mkapa akimjibu Yona.

“Kwa mujibu wa barua ya Rais Mkapa aliyomjibu Yona, inasomeka kama ifuatavyo: Nakubaliana na ombi lako Waziri Yona na ninataka wizara yako iendelee na mchakato huo haraka,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo.

Shahidi huyo, jana alionekana kuzungumza baadhi ya maelezo mapya yaliyokuwa yakitofautiana na aliyoyatoa juzi wakati akiongozwa na wakili wa mashitaka. Alidai kuwa licha ya yeye kumpatia mapendekezo yaliyokataza serikali isifanye haraka kuikubali Kampuni ya Alex Stewart kwa sababu haikuwa na mtaji wa kutosha, Yona asingeweza kukataa maagizo ya Rais Mkapa yaliyomtaka kuendelea na mchakato wa kuileta kampuni hiyo nchini.

Aidha, mahojiano kati ya shahidi huyo na wakili wa utetezi yalikuwa kama ifuatavyo:

Wakili: Juzi ulitamba hapa mahakamani kwamba wewe ulikuwa mtaalamu na ulitoa ushauri wako kwa Yona wa kuikataa hiyo kampuni, lakini mshitakiwa alipuuza. Je, ilikuwaje serikali ilikubali wewe ujiuzulu na isikatae ombi lako kwa gharama yoyote?

Shahidi: Sijui. Ninachofahamu mimi nilijiuzulu.

Wakili: Katika kamati yenu, wewe ulishauri nini kuhusu Alex Stewart?

Shahidi: Nilishauri isipewe tenda.

Wakili: Kuna andiko lolote uliloandika kwenye kamati hiyo kwamba hukubaliani na kampuni hiyo kupewa tenda?

Shahidi: Mh! Sina andiko la kuthibitisha hilo.

Wakili: Tutaamini vipi kama ushauri huo wa kitaalamu ndiyo huo huo ulimshauri Yona?

Shahidi: (Kimya)

Wakili: Sasa Yona alikosea nini kama si wewe ndiye uliyeisaliti kamati yako?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Kwa hiyo unataka kusema walioisababishia serikali hasara ni wajumbe wenzako wa kamati?

Shahidi: Siwezi kusema hilo.

Wakili: Hii asilimia 1.9 ya malipo ya ada kwa kampuni hiyo, kamati yenu iliikubali?

Shahidi: Hatukuipitisha, tulifanya ulinganisho.

Wakili: Mlipitisha kampuni hiyo ilipwe ada asilimia ngapi?

Shahidi: Sikumbuki.

Wakili: Baada ya kamati yenu kuandaa ‘proposal’, kulifanyika tathimini ya kuipata kampuni hiyo, je, wewe ulishiriki kufanya tathimini kwa kampuni hizo mbili?

Shahidi: Nilishiriki.

Wakili: Tathimini ilionyesha Alex Stewart Government Business Corporation ilipata pointi ngapi?

Shahidi: Sikumbuki.

Wakili: Nakukumbusha, kampuni hizo mbili mlizipa alama za ushindi, Alex Stewart mliipa asilimia 92.9 na Walker & World mliipa asilimia 73.3.

Shahidi: Ni kweli.

Wakili: Ukiwa mtaalamu wa masuala ya madini, ni kampuni gani hapo ilikuwa na mafanikio zaidi ya kupata tenda?

Shahidi: Alex Stewart.

Wakili: Kamati ilipendekeza ni kampuni gani ipewe kazi ya kukagua dhahabu?

Shahidi: Alex Stewart.

Wakili: Wewe ulikuwepo kwenye kamati wakati pendekezo hilo linatolewa?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Kwa mujibu wa kielelezo cha kumi, baada ya kamati yenu kutoa pendekezo hilo kwa serikali, wewe uliwazunguka wajumbe wa kamati yako na ukaenda peke yako kwa Yona na ukamwambia kampuni hiyo isipewe kazi, si ndiyo?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Wewe unajua Yona ni mtu mmoja katika serikali hii, ni kwa nini ulifanya hivyo?

Shahidi: (Kimya)

Wakili: Huu mkataba wa serikali na kampuni hiyo si ulitokana na mapendekezo ya kamati yenu?

Shahidi: Sikumbuki.

Wakili: Ndiyo maana awali wakati naanza kukuhoji nilikwambia wewe wakati unafanya kazi Wizara ya Nishati na Madini ulikuwa hupikiki chungu kimoja na wenzio. Mwanzo uliiambia mahakama kamati yenu ilipendekeza kampuni ipewe kazi, sasa hivi unasema ilikataa isipewe kazi.

Shahidi: Kimya( wananchi wanaoudhuria kesi hiyo wakaangua vicheko).

Wakili: Kwa hiyo shahidi umeanza siyo kubadili maelezo yako kwamba kamati yenu ilipendekeza kampuni hiyo ipewe tenda?

Shahidi: Sikumbuki kamati kwamba tulipendekeza au tulisema imeshindwa kutimiza vigezo.

Wakili: Ni mapendekezo gani mlipeleka kwa Gavana marehemu Daud Balali kuhusu kampuni hiyo?

Shahidi: Mapendekezo kwamba Alex Stewart ilishinda.

Wakili: Baada ya kamati yenu kumpelekea mapendekezo hayo, mlitegemea gavana afanye nini?

Shahidi: Sijui (watu wakaangua vicheko)… Tulichotegemea aiite kampuni hiyo na aieleze imeshinda tathimini na wakubaliane namna ya kufanya kazi na makubaliano hayo yawekwe kwenye mkataba.

Wakili: Ndugu shahidi, ulishawahi kufanya utafiti wa madini katika nchi nyingine?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Unajua hupaswi kuzungumzia kitu kama hujakifanyia utafiti, sasa ni kwanini unadai uliandika pendekezo kwa Yona kwamba tenda ya kampuni hiyo isitishwe na badala yake ufanyike utafiti katika nchi nyingine kwanza?

Shahidi: (Kimya)

Wakili: Kuna mahali popote wewe binafsi uliwahi kutoa taarifa kwa gavana kwamba hukubaliani na wajumbe wenzio?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Mapendekezo yenu yaliyopelekwa kwa gavana uliwahi kuyaona?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Wewe ulimshauri Waziri Yona kwamba hakuna haraka ya kuingia mkataba na kampuni hiyo. Nakuuliza akiambiwa na wakubwa wake aruhusu kampuni hiyo ije nchini kufanya kazi angekataa?

Shahidi: Hapana asingeweza kukataa.

Wakili: Nakwambia sasa Yona alimuandikia barua rais wa wakati huo Benjamin Mkapa akimuarifu kuhusu serikali kuitaka kampuni hiyo ije ifanye kazi ya ukaguzi hapa nchini na rais alimjibu barua hiyo ambayo naomba uisome kwa sauti.

Shahidi: Inasomeka kwamba. “Nakubaliana na taarifa yenu na endeleeni na mchakato wa kuipata kampuni hiyo haraka.”

Wakili: Sasa kama Rais Mkapa alimuagiza Yona aendelee na mchakato, waziri angeendelea kusikiliza ushauri wako wa kukataa serikali isitishe tenda na kampuni hiyo wakati wewe ni mdogo kimadaraka?

Shahidi: Ni kweli Yona asingeweza kukataa agizo la Mkapa.

Wakili: Uliwahi kuusoma ule mkataba?

Shahidi: Hapana, nilisoma rasimu ya mkataba na wala sikuona kipengele kilichonitatiza isipokuwa kipengele cha ada ya asilimia 1.9.

Wakili: Unavifahamu hivi vitabu?

Shahidi: Ndiyo, ni kumbukumbu ya majadiliano katika Bunge.

Wakili: Majadiliano ya Bunge mwaka 2004 uliyafuatilia?

Shahidi: (Kimya)

Wakili: Chukua hiki kitabu kimoja fungua ukurasa wa 25, kisha usome kwa sauti ili mahakama ijue unasema nini.

Shahidi: Unasomeka miswaada ya sheria ya nyongeza na matumizi ya fedha mwaka 2004.

Wakili: Kwa hiyo kuna uwezekano wa kufanyika ‘supplementary’ bajeti kabla ya mwaka wa fedha kuisha?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Juzi uliiambia mahakama bajeti ya mwaka 2003/2004, haikutengwa bajeti ya malipo ya kampuni hiyo na kwamba Benki Kuu na wizara ilitumia njia zake kutafuta fedha kuilipa kampuni hiyo. Je, nikikwambia hii hansad inasema bajeti hiyo ilikuwa na nyongeza ya bajeti?

Shahidi: Ukisema hivyo ina maana hauna bajeti.

Wakili: Kwa hiyo ukipata nyongeza ya bajeti unakuwa hauna bajeti?

Shahidi: Unakuwa na bajeti.

Wakili: Zoezi la kuileta kampuni hiyo nchini lilikuwa halina faida yoyote?

Shahidi: Kifedha halina faida na kule kuthibitisha hakuna wizi wa madini yetu ni faida.

Wakili: Na nikikwambia sababu ya kampuni hiyo kushindwa kufanya kazi yao sawasawa ilitokana na kampuni za uchimbaji wa madini kukataa kukaguliwa?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Unakumbuka aliyekuwa Waziri wa Fedha (Mramba) aliziita kampuni za uchimbaji wa madini nchini akazionya na kuzitaka zikubali kukaguliwa na kampuni hiyo?

Shahidi: Sawa kabisa Waziri wa Fedha alitenda hilo.

Wakili: Unakumbuka kampuni hiyo ilikataa taarifa za mahesabu za kampuni zinazochimba dhahabu hapa nchini zilizoonyesha zimepata hasara?

Shahidi: Hiyo sikumbuki.

Wakili: Unakumbuka sababu za serikali kuongeza mkataba na kampuni hiyo mwaka 2005 hadi 2007 ili iwezeshe kampuni hiyo kumaliza kazi yake ya ukaguzi iliyocheleweshwa na kampuni zilizokataa kukaguliwa?

Shahidi: Ni kweli.

Wakili: Kwa hiyo serikali iliingia hasara miaka miwili kwa sababu kampuni hizo zilikataa kukaguliwa, halafu wewe leo hii unatetea kampuni hizo hazijaitia hasara serikali?

Shahidi: Hiyo ni sababu mojawapo.

Wakili: Unajua nyaraka 6,000 zilifichwa na kampuni hizo za uchimbaji ili Kampuni ya Alex Stewart isizikague?

Shahidi: Ni zaidi ya 6,000.

Wakili: Hivi una habari hizo nyaraka zaidi ya 6,000 zilifichwa kwa ajili ya kukwepa kodi?

Shahidi: Hilo nalijua.

Wakili: Kama hilo unalijua asante sana kwani hizo nyaraka zilizofichwa ziligunduliwa na Kampuni ya Alex Stewart.

Shahidi: (Kimya)

Wakili: Unaifahamu Kampuni ya Plaser Dom na Resolut zilikuwa zinachimba madini, na katika ukaguzi Kampuni ya Alex Stewart iligundua zimeshindwa kuthibitisha matumizi ya dola 160 kwa sababu nyaraka zilikuwa Makao Makuu ya kampuni zao na si hapa nchini, nje ya nchi?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Unajua nyaraka za kampuni za madini zinatakiwa zibaki hapa hapa nchini?

Shahidi: Najua.

Wakili: Wataalamu wenzio wametoa taarifa serikalini, wamesema takwimu za upatikanaji wa dhahabu ni za uongo, lakini wewe unasema takwimu za upatikanaji ni sahihi, tuamini lipi?

Shahidi: (Kimya)

Wakili: Hapa ninalo dokezo lililopokelewa na Spika wa Bunge kwamba Alex Stewart iligundua upungufu mkubwa katika uchimbaji na usafirishaji dhahabu, sasa unataka kusema kamati ilikosea?

Shahidi: Najua, ila siwezi kulisemea hilo.

Wakili: Juzi, uliiambia mahakama hii tukufu kwamba Alex Stewart haikutoa mafunzo kwa Watanzania?

Shahidi: Ni kweli ila kwa upande fulani.

Wakili: Una ushahidi wa hilo unalosema?

Shahidi: Sina hakika.

Wakili: Kama huna uhakika ni kwanini unadai kampuni hiyo haikutoa mafunzo kwa Watanzania?

Shahidi: (Kimya, watu wakaangua vicheko)

Wakili: Sasa tumepokea taarifa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi, kupitia gazeti la The Citizen aliuambia umma kwamba hivi sasa Tanzania inatumia wataalamu Watanzania waliopata mafunzo ya ukaguzi wa madini toka Kampuni ya Alex Stewart. Je, utabisha?

Shahidi: Sibishi.

Hata hivyo, kiongozi wa jopo la mahakimu wakazi, Utamwa, aliahirisha kesi hiyo hadi leo na kumtaka shahidi huyo wa kwanza afike mahakamani ili endelee kuhojiwa na mawakili wa utetezi kwa kuwa jana kwa saa nne mfululizo alihojiwa na wakili Nyange, ambaye anamtetea Mramba.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 4,2009

KESI YA MRAMBA YAANZA KUUNGURUMA

na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7 inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na wenzake wawili, Nyero Matihiza (48), ameieleza mahakama kuwa ushauri wake wa kitaalamu alioutoa ulipuuzwa na viongozi wake.


Mbali na Mramba washitakiwa wengine ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu Mstaafu Gray Mgonja.Wanaotetewa na mawakili wa kujitegemea Hurbet Nyange, Peter Swai, Profesa Leonard Shaidi, Cuthbert Tenga.

Matihiza ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Masuala ya Uchumi katika Wizara ya Nishati na Madini wakati huo ikiongozwa na mshitakiwa wa pili, Daniel Yona, alitoa madai hayo jana mbele ya jopo la mahakimu wakazi John Utamwa, Saul Kinemela na Sam Rumanyika wakati alipokuwa akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Fredrick Manyanda na Stanslaus Boniface.

Matihiza alidai kitaalum yeye ni Diolojia alieleza yeye alikuwa mmoja wajumbe wa Kamati iliyopewa jukumu la kuaandaa mchakato wa kutafuta kampuni ya nje itakayokuja nchini kwaajili ya kukagua thamani na kiasi cha dhahabu kinachopatika kwasababu jamii ilikuwa ikitilia shaka takwimu ya dhahabu inayopatikana nchini haina ukweli wowote.

“Kamati yeti ilifanyakazi yake vyema na nilitoa mapendekezo kwa waziri wangu enzi hiyo(Yona)kwamba Kampuni ya Alex Stewart Gorvenment Bussiness Corporation imeshindwa kazi na ilikuwa imelenga kuficha ukweli na pia nikapendekeza kuwa ada ya asilimia 1.9 inayolipwa kampuni hiyo ni kubwa sana na zabuni itangazwe upya.”alidai Matihiza.

Ifuatayo ni mahojiano kati ya wakili wa serikali Manyanda na shahidi huyo.

Wakili:Wakati ukiwa na wadhifa huo, majukumu yako yaliyokuwa yapi?
Shahidi:Kuishauri wizara ya Nishati na Madini katika masuala ya sheria ya madini,uwekezaji katika sekta hiyo na mfumo wa kodi katika eneo hilo.
Wakili:Unajua nini kuhusu Mineral Assayers?
Shahidi:Ni ufuatiliaji wa madini yaliyo katika sampuli tofauti,mfano katika miamba dhahabu inapatikana kiasi gani.
Wakili:Unafahamu nini kuhusu Gold Asseyers Tanzania?
Shahidi: Mwaka 2002 nakumbuka kulikuwa na suala la wasiwasi kwa wananchi,wabunge kwamba makampuni yanayochimba madini yanaficha takwimu za ukweli kwahiyo kwahiyo majibu ya wakaguzi wa madini yalikuwa yakitiliwa wasiwasi.
Wakili:Kwanini kulikuwa na wasiwasi wa takwimu hizo?
Shahidi:Suala la uchimbaji wa madini katika taifa letu lilikuwa ni geni nandiyo maana wananchi walikuwa wanawasiwa kwamba madini yanayopatikana nimengi kuliko takwimu zonazotajwa.Na wizara iliamua kutafuta mkaguzi wa dhahabu ili kujua kitu gani kinaendelea kwenye sekta ya madini na baada ya hapo wizara kwa kushirikiana na BoT walipewa jukumu la kutafuta mkaguzi wa kutafiti dhahabu nchini.Wizara iliunda timu ya watu wanne na mimi nilikuwa mmoja wao ,tukafanyakazi yakuandaa maombi ya kutafuta mkaguzi wa dhahabu.
Wakili:Timu yenu ilitoa mapendekezo gani katika zoezi hilo la utafiti?
Shahidi:Tulipendekeza uwepo mifumo ya usimamizi ya uchimbaji wa madini,kukiaki taarifa za upatikanaji wa dhahabu na tukaweka vigezo kwamba kampuni ya ukaguzi wa madini tunayoitafuta isitokee kwenye nchi ambayo wachimbaji wa hapa nchini wametokea.
Wakili:Ni makampuni yapi mlipata baada ya kutangaza hiyo tenda?
Shahidi:Tulipata makampuni matano ambayo yalijitokeza ila ni kampuni moja ya Alex Stewart Asserys ndiyo ilishinda zabuni.
Wakili:Ni nani hao Alex Stewart Asseys?
Shahidi:Ni kampuni ambayo inafanya shughuli za ukaguzi wa madini Uingereza pia inatawi Marekani Na hiyo kampuni ya marekani ambayo ndiyo ilipewa kazi hapa nchini inaitwa Alex Stewart Government Bussiness Corporation.
Wakili:Alex Stewart Asseys na Alex Stewart Gorvement Bussiness Corporation zinahusiano gani?
Shahidi:Alex Stewart Asseys ni kampuni mama na hiyo nyingine ambayo inadaiwa inafanyakazi na serikali mbalimbali duniani na ndiyo maana serikali yetu ikaitafuta.Na ilitimiza vigezo vingi ila kigezo cha mtaji kilichomtaka alete vifaa(mahabara )hapa nchini kilimshinda na ndiyo maana kamati yetu tukaona hicho ni kikwazo kwetu.
Wakili:Mlifanya nini baadaya kuona haitimizi kigezo hicho?
Shahidi:Sisi kama kamati tulipeleka mapendekezo kwa Gavana marehemu Daudi Balali kwani nyiyo aliyekuwa anatusimamia.Na nimi nilipeleka dokezo kwa aliyekuwa waziri wa Nishati, Yona.
Wakili: Baada ya majadiliano yenu na kampuni hiyo nini kilifuata?
Shahidi:Uliandaliwa mkataba na ofisi ya Gavana.Waandaaji wa mkataba misikushiri ila nilishiriki kutoa mapendekezo.
Wakili;Mapendekezo ya kuikataa kampuni hiyo ya ukaguzi wa dhahabu uliandika lini?
Shahidi:Kabla ya mkataba kusainiwa na mapendekezo yangu niliyatoa wakati draft ya mkataba.
Wakili;Ni mapendekezo gani hayo?
Shahidi:Ada ya asilimia 1.9 kwa kampuni hiyo ilikuwa ni kubwa sana ikataliwe kwasababu taifa linapata mrahaba wa dhahabu wa asimilia 3.Hivyo nasisitiza mapendekezo yangu ya kitaalamu niliyompelekea Yona hakuzingatiwa.
Wakili:Utendaji wa Kampuni ulitakiwa uweje kwa mujibu wa mkataba?
Shahidi:Kuimarisha udhibiti na usimamizi na tulika kampuni hiyo itusaidie lakini haikuweza kutusaidia,eneo jingine ni ambalo utendaji wake haukulidhisha ni eneo la takwimu kwani katika mkataba kampuni hiyo iliaidi kupandisha takwimu za ukaguzi hadi asilimia 50 lakini ilishindwa kutimiza hilo,eneo jingine ni mafunzo kwa wataalum wa nchini ili kampuni hiyo ikimaliza muda wake na kuondoka wataalamu wetu waweze kuendelea.
Wakili:Bajeti ya 2003-2004 malipo ya mkaguzi huyo yalikuwemo?
Shahidi:Halikuwemo.

Kiongozi wa Jopo la mahakimu wakazi John Utamwa, aliairisha kesi hiyo hadi leo ambapo upande wa utetezi utakuja kumhoji shahidi huyo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 3,2009

MEREY BALHABOU AFUTIWA KESI

Na Happiness Katabazi

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Merey Ally Saleh, maarufu kwa jina la Merey Balhabou na mwenzake, Abdallah Said Abdallah, waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa dola milioni 1.08 (zaidi ya sh bilioni moja) , wamefutiwa mashitaka.


Washitakiwa hao wamefutiwa mashitaka baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuwasilisha hati ya kuwafutia mashitaka washitakiwa hao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Merey na mwenzake, wameachiwa huru chini ya kifungu 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ambacho kinampa mamlaka DPP kuwaondolea mashitaka watuhumiwa.

Kuachiliwa kwa washitakiwa hao kunafanya washitakiwa katika kesi hiyo kwa njia ya mtandao wa kompyuta, mali ya Benki ya Barclays kubaki tisa.

Washitakiwa waliobaki katika kesi hiyo ni Winford Mwang’onda, Shubira Mutungi, Naima Saria, Upendo Mushi, Magreth Longway, Emmanuel Mukoni na Ramadhani Khamis, ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo na mfanyabiashara, Justice Rugaibura.

Washitakiwa hao Oktoba 29-30 mwaka jana, walikula njama katika eneo lisilofahamika jijini Dar es Salaam, walifanya udanganyifu na kuiibia benki hiyo fedha hizo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 3,2009

TAKUKURU ISIWATISHE WABUNGE

Na Happiness Katabazi

BABA wa Taifa, hayati Julius Nyerere, aliwahi kusema kwamba ‘ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo , haujali adui wala rafiki’.


Kuwahoji wabunge wakati Bunge linangojea kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa serikali kuhusu maazimio ya Kamati Teule yaliyotokana na uchunguzi wa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond ni ufisadi wa kupindukia.

Katika malumbano kati ya wabunge na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), taasisi hiyo imeungwa mkono na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kujaribu kuwahoji wabunge eti kuhusu sakata la kupokea posho mbilimbili.

Ukweli umeibuka kwamba zipo njama za kulizuia Bunge lisiwe na msimamo wa kuikataa taarifa itakayotolewa na serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya mkataba wa kampuni ya mfukoni ya Richmond.

Ni kweli kwamba katika ripoti aliyoiwasilisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuchunguza kashfa ya mkataba huyo, Dk. Harrison Mwakyembe, Februari mwaka jana, ilikubaliwa na kupitishwa na Bunge. Ndani ya ripoti hiyo liko pendekezo la kuwajibika kwa Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hosea.

Mtu huyo (Dk.Hosea) sasa amechukua jukumu la kutaka kuwahoji wabunge hasa Dk.Mwakyembe.

Ni zuzu gani asiyekuwa na hata chembe ya uelewa wa sheria za nchi hata ashindwe kugundua kwamba Takukuru inatumia vibaya mamlaka yake kulitisha Bunge kwa jambo ambalo halina maslahi kwa taifa letu?

Kama wabunge watakubali vitisho hivyo vya kitoto na wakashindwa kujadili kikamilifu taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu Richmond, hapo itakapowasilishwa ili kuifurahisha Takukuru, hilo litakuwa ni janga la kitaifa na vita dhidi ya ufisadi vitakuwa vimeshindwa na mafisadi wanaweza kushangilia kwa nderemo na vifijo na kugonganisha glasi za mvinyo!

Sheria ya rushwa haina kipengele chochote kinachozuia takrima na wala wabunge kupokea posho mbili, hivyo kupokea posho mbili si kuvunja sheria za nchi ambazo tumeridhia zituongoze.

Kumhoji mtu kwenye jambo ambalo halijakatazwa kisheria ni kumtisha, kumfunga mdomo, kumkera na kumdhalilisha na pia ni upotevu wa rasilimali za taifa.

Labda Takukuru pekee ndiyo isiyojua kwamba muda watakaoutumia kuwahoji wabunge kwa jambo la ajabuajabu na kuchekesha, unalipiwa na walipakodi hivyo ni hasara kwa taifa?

Waziri Mkuu alipojiingiza katika jambo hili kwa kuruhusu mahojiano hayo baina ya wabunge na Takukuru yafanyike, hakuzingatia kwamba taasisi inayohusika inatuhumiwa mbele ya Bunge kwa hiyo kuiruhusu iwahoji wabunge ni kutojua sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Tunasema tumechoka sasa kwani ni miaka miwili serikali inasuasua na kujikanyagakanyaga kutekeleza maazimio ya Bunge! Kuna nini ndani yake?

Ikiwa kikao hiki cha Bunge kitashindwa kuiwajibisha serikali na kulimaliza suala hilo, basi ni wajibu wa sisi wananchi kuiadhibu serikali na wabunge wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Kwa upande wa Takukuru ni wazi kuwa sasa taasisi hii imepoteza heshima yake kwa kuparamia baadhi ya mambo bila kufanya utafiti wa kina.

Imekuwa ikipeleka baadhi ya kesi mahakamani bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha na inazingatia zaidi majungu na mizengwe ya kisiasa kuliko maslahi ya taifa.

Yawezekana kwamba baadhi ya viongozi wakuu wa taasisi hiyo hivi sasa ni sehemu ya ufisadi na ni wala rushwa, makuwadi siasa za uporaji wa rasilimali za wananchi.

Ndiyo maana sintashangaa wavuja jasho kuiita taasisi hiyo taasisi ya kuhamasisha rushwa na siyo kuzuia.

Nimalizie kwa kuwaasa wabunge kwamba katu wasikubali kuhojiwa na Takukuru kwa sababu hakuna sheria ya nchi yoyote waliyoivunja, na ninawataka Takukuru na wale wote ambao wanakerwa na wabunge kupata posho mbilimbili, waone wakati umefika sasa wa kuibana serikali ili ipeleke muswada bungeni ambao utazuia wabunge na wafanyakazi wa taasisi nyingine iwe kwenye sekta binafsi na serikalini kupokea posho mbili.

Sasa kama hilo tukishindwa kulifanya, tutabaki kubwatabwata na kubwabwaja mitaani na kwenye vyombo vya habari.

Ieleweke itakuwa ni sawa na kumvalisha mbu miwani. Wabunge waliopokea na wanaoendelea kupokea posho mbili hawajavunja sheria za nchi na Takukuru inalijua hilo vizuri tu ila kwa sababu imeamua kutumia vibaya taasisi yetu hiyo kwa maslahi ya watu wachache inaamua kufanya kama ifanyavyo.

Takukuru inataka kuwahoji wabunge ili kuwahamisha fikra wananchi na wabunge kuacha kufuatilia hoja kuu ya ufisadi inayosababisha umaskini wa kutupwa kwa wavuja jasho.

Nataka Takukuru na Waziri Mkuu Pinda mfahamu kwamba sisi baadhi ya wananchi na waandishi wa habari wenye misimamo thabiti na upeo wa kuona mbali, tunaofahamu vyema kusoma alama za nyakati ‘hatudanganyiki’! Hii imekula kwenu na si kwa wavuja jasho!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

0716 774494

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Novemba 1, 2009