MATUKIO MAKUBWA KUTOKA MAHAKAMANI 2009

Na Happiness Katabazi

MKURUGENZI wa mashitaka(DDP),Eliezer Feleshi, kwaniaba ya serikali ya awamu ya nne chini ya rais Jakaya Kikwete, ameweka historia itakayoendelea kukumbukwa na taifa hili, kufuatia uamuzi wake wa kuwafunguliwa kesi za jinai baadhi ya waliokuwa vigogo serikali na watu maarufu kwenye jamii.


Ibara ya 59B(1) ya Katiba ya Nchi, inatamka kuwa kutakuwa na ofisi ya DPP na Ibara ya 59(2) inaeleza kazi za DPP na Ibara ya 59(3) inataja majukumu ya kiongozi huyo likiwemo jukumu la ufunguaji mashtaka kiongozi huyo.

Pia anaweza kuteua watu wa kuzifanya, Ibara ya 59(4) inasema: “DPP katika kutekeleza majukumu hayo hatakiwi kuingiliwa na mtu yeyote ili mradi majukumu anayoyafanya yawe ni ya maslahi ya umma, haki na azuie ukiukwaji wa misingi ya kisheria.”

Misingi hiyo iliyoainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kuhusu DPP pia imeainishwa kwenye kifungu cha 6 na 8 cha Sheria ya Kusimamia Mashtaka nchini ya mwaka 2008.

Kutokana na hatua hiyo ya DPP kuwafungulia kesi watu wa kada hizo, imeleta mwamko kwa wengine kuanza kudai haki zao, hakika hili ni jambo jema kwa taifa letu ambalo tumeridhia liongozwe kwa misingi ya sheria.

Ieleweke kuwa, DPP kumfunguliwa kesi mshitakiwa siyo hoja, hoja ni upande wa Jamhuri, mwisho wa siku uthibitishe pasipo shaka kesi yao ili washitakiwa waliowashitaki watiwe hatiani kwa makosa hayo na sivinginevyo.

Kwa utangulizi huo mdogo, fuatana na mwandishi wa habari za Mahakama, ili aweze kukujuza baadhi ya matukio makubwa ya kesi zilizotokea mwaka huu.
Hakimu awanya wanahabari kuripoti habari za EPA

Januari 14:
Kinara wa Richmond Kortini

HATIMAYE serikali ilimfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mtu anayetajwa kuwa kinara wa kashfa ya Richmond.Mtuhumiwa huyo, Naeema Adam Gile, alipandishwa kizimbani, kwa tuhuma za kughushi na kutoa taarifa za uongo kwa watumishi wa serikali.Hadi sasa upande wa mashitaka umekuwa ukidai upelelezi haujakamilika hali iliyopelekea mahakama hiyo hivi karibuni iuamuru upande wa mashitaka Februali mwaka huu,itakapokuja kwaajili ya kutajwa ije ieleze mahakama upelelezi wa kesi hiyo umefikia hatua gani.

Januari 20, 2009
Mahakama yaficha ukweli


KATIKA hali ya kushangaza, aliyekuwa Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya, amewapiga marufuku wanahabari kuripoti mwenendo wa kesi ya wizi wa sh milioni 207 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), inayomkabili Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Kigoma, Shaaban Maranda na wenzake watatu.

“Tumeshangazwa na uamuzi wa Hakimu Lyamuya, kwani siku zote tunashinda hapa mahakamani tunaripoti kesi mbalimbali ikiwemo kesi hizi za EPA, na moja ya kesi za EPA anaiendesha yeye, hajawahi kutuambia tusiripoti, lakini leo (jana) ushahidi unaanza kutolewa anatuambia hatuna kibali cha kuripoti, kwa kweli tumeshindwa kumwelewa....tuna mashaka hapa kuna kitu, si bure, tena tunaomba uongozi wa mahakama nchini na serikali kuingilia kati suala hili, kwani maneno mengi yamesemwa kuhusu kesi za EPA kwamba ni za kiinimacho, CCM inajiandalia mazingira ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2010, na fedha za walipa kodi zimetumika kuhakikisha watuhumiwa wa EPA wanafikishwa mahakamani, sasa kesi zinaanza kusikilizwa, sisi wanahabari ambao tuna jukumu mahususi la kuhabarisha umma kinachoendelea katika kesi hizo tunaambiwa tusiandike habari’walihoji wanahabari wanaoripoti habari za mahakama

Liyumba afunguliwa mashtaka ya matumizi mabaya pesa za umma
Januari 27, 2009:

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba na Meneja Mradi wa benki hiyo, Deogratius Kweka, wamefunguliwa mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kusababishia serikali hasara ya sh bilioni 221, baada ya kuidhinisha ujenzi wa minara Pacha ya BoT bila idhini ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu.

Zombe aanza kujitetea
Februali 10, 2009
ALIYEKUWA Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya mauji ya watu wanne,alianza kujitetea na kuieleza Mahakama Kuu na kuanza kumwaga machozi kizimbani.

Zombe alimwaga machozi mara kadhaa wakati akijitetea mbele ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Masatti kuhusiana na tuhuma hizo zinazomkabili yeye pamoja na askari wenzake tisa.

Liyumba apata dhamana ya utata
Februali 17, 2009
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala (BoT)Amatus Liyumba, amepata dhamana ya sh milioni882, huku serikali ikilalamika nje ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoridhika na hatua hiyo

Machi 12,2009
Raia 37 wa kigeni mahakamani kwa uvuvi haramu
RAIA 37 wa waliokamatwa kwenye meli ya Tawaliq 1 iliyokuwa ikifanya uvuvi haramu katika kina kirefu cha bahari ya Hindi eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , wamefikishwa mahakama ya Kisutu na kusomewa mashitaka mawili ya uvuvi haramu, walikuwa wamevua tani 70.

Machi 30,2009
Chenge kortini kwa kuendesha gari kwa uzembe
ALIYEKUWA Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge afikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni akikabiliwa na mashitaka ya kuendesha gari kwa uzembe hivyo kusababishia mauaji ya watu wawili na hadi sasa kesi hiyo inaendelea upelelezi umekamilika.

Machi 26,2009
Shahidi kesi ya Mahalu atao ushahidi kwa njia ya video


UPANDE wa mashitaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin, ulifunga ushahidi wake, ambapo siku huyo shahidi wa mwisho ambaye ni mwanasheria nchini Italia alitoa ushahidi wake kwa kutumia video ambapo siku hiyo mahakama ya Kisutu iliama na kuamia Jengo la IFM na kusikiliza kesi hiyo.

Watatu Kortini kwa kuiba bil.1/-kwa njia ya mtandao
Mei 4, 2009

WATU watatu walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka 209 kwa tuhuma za kuiba sh bilioni moja kwa njia ya mtandao wa kompyuta, mali ya Benki ya National Microfinance Bank (NMB).
Washitakiwa hao ni karani wa benki hiyo, Mtoro Midole (42), Daudi Kindamba (47) na John Kikopa (46), ambao wote ni wafanyabiashara na wakazi wa jijini.

MwanaHALISI latakiwa kumlipa Rostam bil.3/-
Mei 12, 2009


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ililiamuru gazeti la kila wiki la MwanaHALISI na washitakiwa wengine kumlipa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz fidia ya sh bilioni tatu kwa kuandika habari za kumkashifu na za uongo zilizomhusisha na umiliki wa kampuni ya Richmond.

Mbali na hilo, Mahakama Kuu katika hukumu yake ambayo inaweza kuibua mjadala mkubwa katika taaluma ya uandishi wa habari kwa siku zijazo, imeliamuru gazeti hilo, kuandika habari yenye uzito ule ule katika ukurasa wa kwanza kukanusha habari hiyo dhidi ya Rostam.

Mei 13,2009
Mahakama yakataa ombi la Dowans

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara, Dar es Salaam, ililifukuza ombi la Kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, lililokuwa likiitaka mahakama hiyo ifute maombi ya Shirika la Umeme (TANESCO) la kutaka mitambo hiyo isiuzwe kwa sababu yalikuwa na dosari za kisheria.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Robert Makaramba, ambapo alisema amefikia uamuzi wa kutupa maombi hayo kwa sababu Dowans imeshindwa kuishawishi mahakama ni vipi Tanesco ilitumia vifungu vya sheria visivyo sahihi kuwasilisha ombi lake katika mahakama hiyo.

Mei 27,2009
Liyumba afutiwa kesi
HAKIMU Mkazi Walirwande Lema, aliyekuwa akisikiliza kesi namba 27/2009 iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba na Meneja Mradi wa benki hiyo, Deogratius Kweka, afutiwa kesi baada ya kubaini hati ya mashitaka ilikuwa imekosewa, lakini muda mfupi baadaye walikamatwa tena mahakamani hapo.

Mei 28,2009
Liyumba asomewa mashtaka mapya

KUKAMATWA na kuachiwa kwa huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, iliendelea tena baada ya mshitakiwa huyo kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashitaka mapya.

Mei 31,2009
Serikali yaweweseka mgombea binafsi

KWA mara pili tena, serikali imekata rufaa dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Democrat (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, katika Mahakama ya Rufani nchini, kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ulioruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu.

Juni 8,2009
Korti kuu yambana Mahalu


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeyatupa maombi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Meneja Utawala wa Fedha, Grace Martin, wanaokabiliwa na kesi ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni 2.

Katika maombi hayo, washitakiwa hao walitaka mahakama hiyo iwaachilie huru kwa sababu mwenendo mzima wa kesi yao ya msingi, una dosari za kisheria.

Juni 9,2009
Korti Kuu yasikiliza Rufaa ya DPP vs Liyumba

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imesikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, kupinga uamuzi wa kulegezewa masharti ya dhamana

Juni 10,2009
Maranda ana kesi ya kujibu –Mahakama

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Mweka Hazina wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma Rajabu Maranda na mpwawe, Farijala Hussein, wanaokabiliwa na kesi ya wizi wa sh bilioni 1.8 za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), mali ya Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), wana kesi ya kujibu.

Mei 30,2009
Liyumba alegezewa masharti ya dhamana


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ililegeza masharti ya dhamana kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, ambaye anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.Sasa atapata dhamana kwa kuwasilisha hati ya mali au fedha taslimu sh milioni 300 badala ya Bilioni 112.

Julai 21,2009
Vigogo sita kortini kwa tuhuma za kusafirisha pembe za ndovu
VIGOGO sita wa makampuni binafsi ya kupakia na kusafirisha mizigo nchini, walifikishwa walifikishwa katika Mahakama ya Kisutu wakikabiliwa na kesi za uhujumu uchumi, kwa kusafirisha nje ya nchi jumla ya kilo 11,061 za pembe za ndovu zenye thamani ya sh 791,514,020 za meno ya tembo kwenda Hai Pong, Vietnam, na Manilla Philippiness, zenye thamani ya sh 684,827,000 mali ya Serikali ya Tanzania.

Mbele ya Hakimu Mkazi Anisetha Wambura, Wakili wa Serikali, Prosper Mwangamila, aliyekuwa akisaidiana na Michael Lwena, Shadrack Kimaro na Abubakar Mrisha, alidai kuwa kesi hiyo inamkabili Eladius Colonerio (39) ambaye ni Mkurugenzi wa Team Freight (T) Ltd, Gabriel Balua (33), Meneja Usafirishaji wa nje na ndani ya nchi wa kampuni hiyo, na Shaban Yabulula (44) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kigoma M. N Enterprises (T) Ltd.

Agosti 17,2009
Zombe ashinda kesi


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa hukumu ya kushtusha baada ya kumwaachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe na wenzake wanane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja.

Akisoma hukumu hiyo iliyochukua zaidi ya saa sita, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Salum Massati, alisema baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, amebaini kuwa serikali imeshindwa kuthibitisha mashitaka hayo.

“Katika kesi hii upande wa mashitaka licha ya kuleta mashahidi 37 na vielelezo 23, umeshindwa kuithibitishia mahakama kuwa ni kweli washitakiwa wote ndio waliowaua marehemu na kwa sababu hiyo nawaachia huru washitakiwa wote.Na kwa kuwa mahakama hii imewaona washitakiwa si wauaji, hivyo kuanzia sasa naliagiza Jeshi la Polisi liende kuwasaka wauaji wa marehemu wale, na Zombe na wenzake waachiliwe huru,” alisema Jaji Massati na kuuacha umati wa watu ukiwa umeshangaa.

Jaji Massati, alisema kamwe mahakama haiwezi kumhukumu mshitakiwa kwa ushahidi dhaifu na wa kusikia kama uliowasilishwa mahakamani hapo, kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria. Baada ya Jaji Massati kutamka kuwaachia huru washtakiwa hao, Zombe na Christopher Bageni (aliyekuwa mshitakiwa wa pili) walikumbatiana kizimbani kwa furaha na wananchi waliokuwa wamefurika katika ukumbi namba moja mahakamani hapo wakionekana kushangilia na wengine kuhuzunika.

Septemba 10,2009
IGP Mahita aumbuka


Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imemwamuru aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Omar Mahita kulipa malimbikizo ya gharama za matunzo ya kumhudumia mtoto Juma Omar Mahita (12) baada ya mahakama hiyo kujiridhisha kuwa mtoto huyo ni wake.

Oktoba 2,2009
Mtoto wa Keenja mbaroni kwa dawa za kulevya

MTOTO wa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Charles Keenja (CCM), Agatha Keenja, alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na kosa la kukutwa na dawa za kulevya zenye uzito wa gramu 6.6 zinazokadiriwa kuwa na thamani y ash 60,000.

Oktba 2,2009
Jeetu aitikisa Serikali

MAHAKAMA ya Kisutu ilitoa uamuzi wa kusimamisha usikilizaji wa kesi tatu zinazomkabili mfanyabiashara maarufu Jayantkumar Patel na wenzake,hadi pale kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na washitakiwa hao Mahakama Kuu itakapomalizika.

Novemba 2,2009
Kesi ya Mramba yaanza kuunguruma


KESI ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7 inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba,aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona na Katibu Mkuu Mstaafu wa Hazina, Gray Mgonja, ilianza kuunguruma kwa mara ya kwanza ambapo shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka , Nyero Matihiza (48), alitoa ushahidi wake na kudai kuwa ushauri wake wa kitaalamu alioutoa ulipuuzwa na viongozi wake.

Novemba 2,2009
DPP afuta kesi ya mfanyabishara Merey na wenzake

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Merey Ally Saleh, maarufu kwa jina la Merey Balhabou na mwenzake, Abdallah Said Abdallah, waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa dola milioni 1.08 (zaidi ya sh bilioni moja) , wamefutiwa mashitaka.Washitakiwa hao wamefutiwa mashitaka baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuwasilisha hati ya kuwafutia mashitaka washitakiwa hao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Merey na mwenzake, wameachiwa huru chini ya kifungu 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ambacho kinampa mamlaka DPP kuwaondolea mashitaka watuhumiwa.

Novemba 31,2009
Rufani ya ‘Babu seya’ yashindwa kusikilizwa

MAHAKAMA ya Rufani nchini, ilishindwa kusikiliza rufaa ya mwanamuziki mahiri wa dansi hapa nchini, Nguza Viking maarufu kwa jina la ‘Babu Seya’ na wanae watatu Papii Kocha Nguza,Nguza Mbangu na Francis Nguza ambao wanatatewa wakili wa kujitegemea Mabere Marando.Kwa sababu pande zote mbili katika kesi hizo hazikuwa tayari kuanza kusikiliza rufaa hiyo.
Babu Seya alionewa-Wakili

Desemba 3, 2009
Babu Seya alionewa-Wakili


MAHAKAMA ya Rufani nchini, ilisikiliza rasmi rufaa ya Mwanamuziki mahiri wa dansi nchini, Nguza Viking maarufu “Babu Seya’ na wanawe watatu.

Wakili wake Mabere Marando aliomba mahakama iwaachirie uhuru warufani hao kwa kuwa kesi hiyo ilikuwa imepangwa.Sambamba na hilo, mawakili hao Marando na Hamidu Mbwezeleni, walieleza kuwa tangu waanze kazi ya uwakili miaka 30 iliyopita, hawajawahi kuona hukumu ya ovyo kama hiyo.

Mawakili hao walieleza hayo mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Nataria Kimaro, walipokuwa wakiwasilisha sababu za kupinga rufaa ya Mahakama Kuu iliyolewa na Jaji Msaafu, Thomas Mihayo na hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Addy Lyamuya ambao wote walitia hatiani kwa makosa ya kubaka.Siku hiyo mamia ya watu wa kada mbalimba walifurika mahakamani hapo kwaajili ya kusikiliza rufaa hiyo.

Desemba 15,2009
Viongozi wa DECI kortini tena

HATIMAYE waliokuwa wakurugenzi wa Kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) iliyokuwa ikijihusisha na shughuli za kuvuna na kupanda fedha, kwa mara nyingine tena walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, na kusomewa mashitaka ya wizi wa sh milioni 118 mali ya DECI (Tz) Ltd.Washitakiwa hao ni Dominick Kagendi, Jackson Sifael Mtaresi, Timetheo ole Lating’ye na Samuel Sifael Mtaresi wanaotetewa na wakili wa kujitegemea, Hudson Ndusyepo.

Desemba 21,2009
Vigogo wa DECI wanyimwa dhamana


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewanyima dhamana Wakurugenzi wa taasisi ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (Deci) wanaokabiliwa na tuhuma za wizi wa sh milioni 18 kutokana na kukiuka masharti ya dhamana waliyopewa awali.

Nawatakia wasomaji wote mwaka mpya wenye mafanikio na afya njema.

0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi,(toleo maalum la matukio makubwa yaliyojitokeza mwaka huu, Desemba 31 mwaka 2009

HAPPINESS ANAKATA KEKI YAKE


Happiness Katabazi(30),nikikata keki kwaajili ya kuwalisha watoto wadogo tunaishi mtaani kwetu kwani ndiyo niliyowaalika peke yao kwenye siku hiyo ya Birthday yangu Desemba 25 mwaka 2009.

HAPPY BIRTHDAY DEAR HAPPINESS



Nikilishwa keki na mwanangu, Queen Mwaijande,siku ya Sikukuu ya Kristmas Desemba 25 mwaka huu, ambayo pia siku hiyo ni siku yangu yakuzaliwa na nilikuwa nikisherehekea kutimiza miaka 30 ya kuzaliwa kwangu iliyoambatana na tafrija fupi nyumbani kwetu Sinza C, jijini Dar es Salaam.

MSILE SAMAKI WA MAGUFULI KABLA HAWAJACHUNGUZWA

Na Happiness Katabazi

DESEMBA 10 mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ,ilikubali ombi la upande wa mshitaka katika kesi ya uvuvi haramu katika Bahari ya hindi eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakutaka samaki wawage bure.


Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Radhia Sheikh anayesikiliza kesi hiyo inayowakabili araia wa kigeni 37 wanaotetewa na wakili wa kujitegema Ibrahim Bendera na John Mapinduzi, ambapo alisema anakubaliana na ombi hilo la upade wa mashitaka na akatoa amri kwa upande huo wa jamhuri kwamba iwapo washitakiwa watashinda kesi hiyo basi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja upande wa mashitaka,uhakishe unawasilisha sh 2,074,249,000 ili kiasi hicho wapatiwe washitakiwa.

Watanzania wenzangu amri hilo ya Jaji Sheikh ilipokelewa kwa mikono miwili na pande zote katika kesi hiyo.Na kwa mujibu wa hati ya kiapo kilichoapwa na Mkugenzi wa Uvuvi ,Nanyaro na kuambatanishwa na ombi hilo la kugawa samaki bure, Mkurugenzi huyo anaeleza kuwa thamani ya samaki hao imepungua kutoka sh bilioni mbili wakati walipokamtwa samaki hao kwenye meli ya Tawariq 1, Machi 8 mwaka huu, hadi kufikia dola za kimarekani laki saba na mia saba hasmini elfu hivi sasa.

Na kwamba Mthamini toka wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi ndiye aliyefanya tathimini hiyo.Kimsingi binadamu Yoyote mwenye akili timamu atakubaliana kwamba samaki nibidhaa ambayo inaaribika.Na kisheria tunaita (Perishable Commodity).Na kawaida kwenye sheria zetu za nchi vipo vipengele vya sheria vinavyoruhusu kuiomba mahakama iwapatie kibali cha kuwauza,au kuwagawa bure samaki hao ,wakati ule ule ilipowakamata samaki wale au bidhaa yoyote ambayo inaaribika mapema.

Sasa kuhusu samaki hao maarufu kama samaki wa John Magufuli, kwanini serikali iliisinzia wakati wote huo tangu ilipowakamata?
Sisi tulitazamia serikali yetu ingeomba amri ya mahakama ya kuwauza ili wasiaribike au kupoteza ubora wake wakati ule ule ilipowakamata?

Hata umeme ungekuwapo wa uhakika bado bidhaa hiyo ya samaki isingeishi mililele bila kuaribika kwakuwa samaki siyo mawe.

Minafikiri wizara inayoongozwa na aziri john magufuri ilifanya uzembe kwakutoomba mapema kibari cha kuwauza samaki walipowakamata na kuzembea huko kumeliingiza na kunaendelea kuliingiza taifa hasara ya mamilioni na wanahousika wanatakiwa kuchukuliwa hatua .

Kwani hao wataalamu waliopo kwenye wizara ya Mifugo kwanini walizembea muda wote huo?Ama waseme ni vihiyo na taasisi husika zitathimini vyetu vyao na katika uzembe huu, hawana budi kufikishwa pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa ya uzembe na kuisababishia serikali hasara, kama walivyoshitakiwa maofisa wengine wa juu katika serikali ya awamu ya tatu ambao wengine wanaendelea kusota magerezani hadi sasa.Na hilo likishindikana kufanyika hilo tutalazimika kuamini yale madai kwamba wanaofikishwa mahakamani ni wale wasiyokuwa na kauli katika serikali hii ya awamu ya nne.

Binafsi nawashauri Watanzania wenzangu wasijaribu kula ha-o --samaki kabla ya samaki hao hawajachunguzwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), ila atakaye kubali kuwala hao samaki bila TFDA kuwachunguza na kutoa tarifa yao ya uchunguzi, ale salama na asije kumlalamikia mtu.

Na hii tabia ya serikali kuzembea hadi bidhaa feki na mbovu zinaingia nchini kwake na wananchi wanazitumia na mwisho wa siku TFDA ndiyo inakuja kutuarifu tuache kuzitumia bidhaa hizo kwani hazifahi kwa matumizi ya binadamu inakera na ndiyo inayotupelekea baadhi y watu tutilie wasiwasi wa samaki hao kama hivi sasa wanafahaa kwa matumuzi ya binadamu.

Na hii tabia ya kutupia wananchi bidhaa mbovu mbovu iache kwani imesikia watanzania wanapenda kulishwa vitu vya bure.

Tunapaswa tujiulize sana ni kwanini serikali imeamua kuwagawa bure samaki hao waliokaa kwa muda usiyojulikana tangu wavuliwe baharini na washitakiwa hao na leo hii aamue kuwagawa mahospitalini,mashuleni, hivi serikali imesikia makundi hayo ya wananchi wenzetu ni mbwa wa jamii?.Iwaombe radhi haraka.

Pia tujiulize ni kwanini serikali imeamua kuwagawa bure ,kwasababu samaki hao ni samaki wanauzwa kwenye mahoteli makubwa duniani lakini hatujasikia wala kuona mahoteli hayo au wazabuni wakipigana vikumbo kutaka kuwanunua samaki hao ili waweze kwenda kuwauza kwenye mahoteli hayo.?

Bado tungali tukikumbuka siku samaki hao walipouzwa, ni watu wachache sana walijitikeza kununua samaki hao tena tulielezwa waliojitekeza kuwanunua ni watu wa hali ya chini kama mimi.

Nayasema haya kwasababu kuna baadhi ya watumishi wa serikali kwa siri kubwa wamekuwa wakitung’ata masikio baadhi ya ndugu na jamaa zao kwamba tusiwale samaki hao pindi watakapogawiwa.Ukiwauliza maswali kwanini wanayasema hayo hawataki kutoa ufafanuzi wa kina ila wanaishia kusema wao wanafahamu nini kinaendelea.

Kauli hizi zinajenga mashaka makubwa na ndiyo maana kwa maslahi ya taifa langu na serikali inayotuongoza nimeandika makala hii iliniweze kutoa angalizo kwa mamlaka husika.

Kwani hakuna Mtanzania yoyote wala idara zetu za upelelezi ,zinauhakika samaki hao walivuliwa lini au mwaka gani na washitakiwa hao.Tunachokifahamu sote ni siku ambayo samaki hao walikamatwa Machi 8 mwaka huu.

Sasa vyovyote iwavyo naomba kutoa angalizo kwa serikali yangu ili mwisho wa siku litakapokuja kutokea la kutokea kuhusu samaki hao,ni vyema ikachukua taadhari mapema ya kuwapima samaki hao kitaalamu na taarifa ya vipimo hivyo itangazwe adharani ili ifahamike.

Kuwalisha wananchi samaki hao bila kupimwa na TFDA au taasisi huru ya kuwapima samaki hao ,kutaonyesha kumbe serikali yetu ipo tayari kuwarisha sumu wananchi wake ili mradi ijionyeshe yenyewe ina uhuruma na wananchi wake.

Mwisho nawatakia wasomaji wote siku kuu njema ya Krismas na Mwaka Mpya.Lakini pia siku ya sikukuu ya Kristmas Desemba 25 mwaka huu, binafsi nitakuwa nasherehekea siku yangu yakuzaliwa ambapo nitakuwa natimiza miaka 30.

Mungu ibariki Tanzania ,Mungu ibariki Afrika

0716 774494

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi Desemba 24 mwaka 2009

VIONGOZI WA DECI WANYIMWA DHAMANA

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewanyima dhamana Wakurugenzi wa taasisitaasisi ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (Deci) wanaokabiliwa na tuhuma za wizi wa sh milioni 18 kutokana na kukiuka masharti ya dhamana waliyopewa awali.


Katika hatua nyingine upande wa mashitaka katika kesi Na.109 ya mwaka huu, ya kuendesha na kusimamia mradi wa upatu kinyume na kifungu 111A(1,3)cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, umeiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na mahakama hiyo imepanga Januari 13 mwakani, washitakiwa watakuja kusomewa maelezo ya awali.Kesi hiyo pia iliyofunguliwa mahakamani hapo Juni 12 mwaka huu, inawakabili pia washitakiwa hao.

Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Mkazi, Alocye Katemana, alisema kwamba hakuna ibishi kuwa wshitakiw ahao ambao wanakabiliwa na kesi nyingine mahakamani hapo wamekiuka masharti ya dhamana ya kutotenda kosa lingine wakiwa nje kwa dhamana.

Washitakiwa hao ni Dominick Kagendi, Jackson Sifael Mtaresi, Timetheo ole Lating’ye na Samuel Sifael Mtaresi.

“Nakubakubaliana na pingamzi la upande wa mashitaka kwa sababu washitakiwa wazi wamekiuka masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama hii katika kesi nyingine inayowakabili, hivyo naamuru warejeshwe rumande hadi Desemba 31 mwaka huu,” alisema Hakimu Katemana.

Kesi nyingine inayowakabili washitakiwa hao ambayo imeelezwa kwua upelelezi wake umekwishakamilika itaanza kusikilizwa Januari 13 mwakani kwa washitakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Kampuni ya DECI iliyowanufaisha watu wengi hasa wale waliojiunga mwanzoni, iliibua malumbano kati ya serikali, viongozi wa kampuni hiyo na wanachama wao, waliopinga hatua ya serikali kusitisha shughuli zake kwa madai kuwa haiko kihalali.

Kusimamishwa kwa shughuli za kampuni hiyo, kulitokana na uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kutoa taarifa ya kuwatahadharisha Watanzania waliojiunga na upatu huo kuwa, taasisi hiyo haiko kisheria na wanaweza kupoteza fedha zao walizopanda.

Shughuli za kupanda na kuvuna mbegu DECI zilisitishwa baada ya serikali kusimamisha akaunti za kampuni hiyo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika, hali ambayo baadaye ilisababisha uvunjifu wa amani katika ofisi za kampuni hiyo, baada ya wanachama wake kuamua kuchukua sheria mkononi kwa kuvunja vioo vya magari ya viongozi, wakitaka warejeshwe fedha zao.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Desemba 22 mwaka 2009

SHAHIDI AZUA JAMBO KESI YA MRAMBA

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa tatu katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh biliono 11.9 inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Mramba na wenzake, ja alisababisha watu wanaoudhuria kesi kuangua vicheko baada ya kuieleza mahakama kwamba yeye yupo tayari kupanda kizimbani kutoa ushahidi wake.


Mbali na Mramba washitakiwa wengine ni Katibu Mkuu Mstaafu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Hurbet Nyange,Peter Swai,Profesa Leonard Shahidi,Cuthbert Tenga.

Kesi hiyo ambayo jana ilikuwa imekuja kwaajili ya kuendelea kusikilizwa ambapo shahidi huyo wa tatu ndiyo alikuwa anatakiwa aanze kutoa ushahidi wake asubuhi lakini hata hivyo jopo la Mahakimu Wakazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu John Utamwa, Sam Rumanyika na Saul Kinemela lilifika lilingia mahakamani hapo saa 6:28 mchana kwaajili ya kuandelea kusikiliza kesi hiyo.

Shahidi huyo ni Geogre Mtigiti aliyasema hayo baada ya kuulizwa na jopo la mahakimu hao ambao walimweleza wamefikia uamuzi wa kumuuliza kwamba kama anaweza kupanda kizimbani kutoa ushahidi kwakuwa muda mchache uliopita Wakili Kiongozi wa Serikali, Stanslaus Boniface aliambia mahakama kuwa wanaomba kesi hiyo iairishwe hadi leo kwakuwa shahidi huyo alifika mahakamani hapo tangu asubuhi na mchana huo amewaeleza kuwa anaumwa maralia.

“Waheshimiwa mahakimu minipo tayari kupanda kizimbani kutoa ushahidi wangu”alidai shahidi huyo wakati alipoitwa mahakamani na mahakimu hao na kusababisha mahakimu na wananchi walifika kwenye kesi hiyo kuangua vicheko.
Hata hivyo wakati Hakimu Mkazi Utamwa na Sam Rumanyika wakimuuliza shahidi huyo kama yupo tayari, wakili wa serikali Boniface alikuwa akijaribu kuingilia kati lakini hata hivyo mahakamani hao walimweleza Boniface kuwa mahakama hiyo pia ina mamlaka ya kumhoji shahidi huyo kuhusu hilo hali iliyosababisha pia watu mahakimu na watu wanaoudhuria kesi kuendelea kuangua vicheko.

Kiongozi wa Jopo hilo ambaye pia ni Msajili wa Mahakama Kuu nchini, John Utamwa alisema. “Kwa kuwa pande zote mbili hazipingi kuairishwa kesi hiyo ….na kwakuwa Boniface aliambia mahakama shahidi wake anaumwa maralia lakini shahidi huyo jopo lilipomhoji akasema yupo tayari kuanza kutoa ushahidi wake ,tunaairisha kesi hii kesho(leo) asubuhi”alisema Utamwa huku akicheka.

Tayari mashahidi wawili walishatoa ushahidi wao na kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa jana hadi Ijumaa wiki hii.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima Jumatano, Desemba 16 mwaka 2009

VIGOGO DECI KIZIMBANI TENA

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE waliokuwa wakurugenzi wa Kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) iliyokuwa ikijihusisha na shughuli za kuvuna na kupanda fedha, jana walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, na kusomewa mashitaka ya wizi wa sh milioni 118 mali ya DECI (Tz) Ltd.

Washitakiwa hao ni Dominick Kagendi, Jackson Sifael Mtaresi, Timetheo ole Lating’ye na Samuel Sifael Mtaresi wanaotetewa na wakili wa kujitegemea, Hudson Ndusyepo.

Wakili wa Serikali Mutalemwa Kishenyi mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana alidai kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa mawili.

Kishenyi alidai shitaka la kwanza ni kwamba washitakiwa wote hao kati ya Desemba 1 na 8 mwaka huu katika sehemu isiyofahamika walikula njama kwa nia ya kulaghahi umma ili kuiba sh 118,440,000.

Alidai shitaka la pili ni la wizi kwamba Desemba 8 mwaka huu, katika Benki ya Standard Chartered tawi Kariakoo jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote waliiba kiasi hicho cha fedha mali ya DECI (Tz) Ltd. Na washitakiwa wote walikana mashitaka hayo.

Hata hivyo, wakili huyo wa serikali Kishenyi alisema upande wa mashitaka unapinga washitakiwa hao wasipewe dhamana kwa sababu wametenda kosa hilo wakati wapo nje kwa dhamana katika kesi ja jinai Na.109 ya mwaka huu, inayoendelea mahakamani hapo.

Juni 12, mwaka huu, washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na kesi Na.109 ya mwaka huu, ya kuendesha na kusimamia mradi wa upatu kinyume na kifungu 111A(1,3) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kampuni ya DECI iliyowanufaisha watu wengi hasa wale waliojiunga mwanzoni, iliibua malumbano kati ya serikali, viongozi wa kampuni hiyo na wanachama wao, waliopinga hatua ya serikali kusitisha shughuli zake kwa madai kuwa haiko kihalali.

Kusimamishwa kwa shughuli za kampuni hiyo, kulitokana na uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kutoa taarifa ya kuwatahadharisha Watanzania waliojiunga na upatu huo kuwa, taasisi hiyo haiko kisheria na wanaweza kupoteza fedha zao walizopanda.

Shughuli za kupanda na kuvuna mbegu DECI zilisitishwa baada ya serikali kusimamisha akaunti za kampuni hiyo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika, hali ambayo baadaye ilisababisha uvunjifu wa amani katika ofisi za kampuni hiyo, baada ya wanachama wake kuamua kuchukua sheria mkononi kwa kuvunja vioo vya magari ya viongozi, wakitaka warejeshwe fedha zao.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano,Desemba 16 mwaka 2009

VIONGOZI WA DECI WAPANDISHWA KIZIMBANI

Na Happiness Katabazi

KWA mara nyingine tena viongozi watano wa kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) iliyokuwa ikijihusisha na shughuli za kuvuna na kupanda fedha, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka ambayo bado hayajafahanika.


Vigogo hao ni Jackson Sifael Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo Saigaran ole Loitginye, Samwel Sifael Mtares, Arbogast Francis Kipilimba na Samwel Mtalis ambao walifikishwa, Juni 12 mwaka huu, mahakamani hapo wakikabiliwa na kesi ya kuendesha na kusimamia mradi wa upatu kinyume na kifungu 111A(1,3) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 inayoendelea mahakamani hapo na wanatetewa na mawakili wa kujitegemea, Hudson Ndusyepo, na Simon Kitulu.

Waandishi wa habari za mahakama waliwashuhudia watuhumiwa hao wakifikishwa mahakamani hapo saa nane mchana wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari kanzu kutoka jeshi la polisi na kupelekwa moja kwa moja katika ofisi moja inayotumiwa na mawakili wa serikali mahakamani hapo.

Hata hivyo wakati waandishi wa habari wakiwasubiri wapandishwe kizimbani watuhumiwa hao, waliwashuhudia maaskari kanzu wakiondoka nao na kwenda kuwapandisha kwenye magari yenye namba za usajili T 515 BBH aina ya Mistubishi Pajero na T833 BDU aina Toyota Carina mali ya jeshi hilo bila watuhumiwa hao kupandishwa kizimbani.

Jana Tanzania Daima iliwasiliana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, ili athibitishe ni kweli jeshi lake linawashikilia vigogo hao tangu Desemba 8, mwaka huu; alipokea simu na kumtaka mwandishi wa habari kuwasiliana na msemaji wa jeshi hilo Abdallah Msika ili kupata taarifa zaidi.

Lakini kwa mujibu habari za kuaminika kutoka ndani ya jeshi hilo, watuhumiwa hao walikamatwa Desemba 8, mwaka huu, katika benki moja (jina linahifadhiwa) wakipokea malipo yao ya sh milioni 120 kutoka kwa mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika ambapo kabla ya serikali kuifunga DECI, mtu huyo aliwauzia nyumba watuhumiwa hao kwa thamani ya sh milioni 260 na watuhumiwa hao walimlipa kwa awamu sh milioni 120.

“Ndiyo, siku hiyo pande zote zilikutana ndani ya benki hiyo na kiasi hicho cha fedha walichokuwa wakirejeshewa kilikuwa kipitie kwenye akaunti ya watuhumiwa....nafikiri unakumbuka akaunti za DECI zote na fedha zote zinashikiliwa na serikali na akaunti hiyo waliyokuwa wakiitaka kupitishia kiasi hicho cha fedha tulikuwa hatuifahamu na raia wema wakaijulisha polisi ndipo tukaenda kuwamata na kiasi hicho cha fedha mkononi,” kilidai chanzo chetu.

Shughuli za kupanda na kuvuna mbegu DECI, zilisitishwa baada ya serikali kuifunga kampuni hiyo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika hali ambayo ilisababisha uvunjifu wa amani katika ofisi za kampuni hiyo eneo la Mabibo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Desemba 15 mwaka 2009

DK.HOSEAH UNAMTISHIA NYAU DPP?


Na Happiness Katabazi

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), inashughulikia makosa ya rushwa lakini taasisi hiyo si Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai hapa nchini.


Alhamisi wiki hii, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, ameuambia umma kupitia vyombo vya habari kwamba kesi zaidi ya 60 zinazohusu rushwa kubwa zilizochunguzwa na taasisi yake ziko katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Eliezer Feleshi.

Dk. Hoseah anasema utaratibu wa kesi za jinai kupitia kwa DPP, kabla ya kupelekwa mahakamani, unachelewesha kesi nyingi za rushwa na kwamba angetamani kesi zote za rushwa zilizochunguzwa na Takukuru ziruhusiwe kwenda mahakamani bila kupitia kwa DPP, kwa kuwa taasisi yake ina wanasheria waliobobea katika kuchunguza matukio ya rushwa.

“Utaratibu huu unatukwaza, tungependa kila mtu ampande farasi wake kama anajiamini kuwa farasi ni wa kwake, tuna wanasheria wetu waliobobea na wanaojiamini, hivyo tungependa zetu ziende mahakamani bila kupitia kwa DPP na kazi yetu ingeonekana, lakini hatuna mamlaka zaidi ya hapo...ila sipingi utaratibu wa kesi kupitia kwa DPP kwa kuwa uliwekwa kisheria na lazima tuufuate,” anasema Dk. Hoseah.

Dk. Hoseah kupitia matamshi hayo anatuonyesha na kutaka kuuaminisha umma kuwa wanachapa kazi kuliko taasisi nyingine; ikumbukwe cheo cha DPP ni cheo cha Kikatiba na ndiyo maana anateuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivyo hata rais wa nchi hawezi kumlazimisha DPP amshtaki mtu ambaye hajajiridhisha kisheria kama kuwepo kwa kesi hiyo ni kwa mujibu wa sheria.

DPP anaruhusiwa kushtaki, kutoshtaki na pia kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 pia kinampa mamlaka kuiondoa mahakamani kesi wakati wowote pindi atakapoona hana haja ya kuendelea na kesi hiyo na hapaswi kuhojiwa na mtu yeyote.

Ibara ya 59B(1) ya Katiba inatamka kuwa kutakuwa na ofisi ya DPP na Ibara ya 59(2) inaeleza kazi za DPP na Ibara ya 59(3) inataja majukumu ya kiongozi huyo likiwemo jukumu la ufunguaji mashtaka kiongozi huyo pia anaweza kuteua watu wa kuzifanya na Ibara ya 59(4) inasema: “DPP katika kutekeleza majukumu hayo hatakiwi kuingiliwa na mtu yeyote ili mradi majukumu anayoyafanya yawe ni ya maslahi ya umma, haki na azuie ukiukwaji wa misingi ya kisheria.

Misingi hiyo iliyoainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kuhusu DPP pia imeainishwa kwenye kifungu cha 6 na 8 cha Sheria ya Kusimamia Mashtaka nchini ya mwaka 2008.

Hivyo basi tukianza kumwendesha DPP kwa ‘rimoti’ tutakuwa tunavunja Katiba ya nchi. Na kwa madaraka hayo makubwa aliyopewa DPP katika Katiba na sheria hizo ambazo tumeziridhia wenyewe zituongoze na tuzitii, ndiyo maana kila mara Mwalimu wangu wa habari za uchunguzi, ambaye pia ni mwandishi mwandamizi nchini, Ndimara Tegambwage, huishia kusema DPP ni ‘Mungu’ wa Tanzania.

Kwanza DPP anatakiwa ajiridhishe na ushahidi ulioletwa mbele yake na vyombo vya upelelezi; upelelezi unaotosha kuweza kuthibitisha kesi, ndipo anaporidhia kesi ifunguliwe mahakamani kwani DPP atapotoa kibali cha kufunguliwa kesi ya jinai mahakamani kisha mwisho wa siku ushahidi hakuna, hali hiyo inapelekea serikali kushindwa kesi hiyo.

Pili, lazima DPP ajiridhishe kwamba kumshtaki mtu ni kwa maslahi ya nchi. Kwa hiyo hapo anaweza kupeleka kama ushahidi unatosha; sidhani kama DPP ni mjinga wa kukurupuka na kukimbilia mahakamani halafu kesho yake serikali inashindwa na kuingia kwenye aibu.

Ni vyema vyombo vya dola vinapofanya kazi zake vizingatie Katiba na sheria za nchini. Pindi viongozi wa vyombo hivyo wanapoona wanataka kutoa malalamiko au mapendekezo yao ya nini kifanyike ili taifa lisonge mbele ni vyema wayafikishe kupitia vikao rasmi.

Hivyo, matamshi hayo ya Dk. Hosea hayapaswi kupewa nafasi mbele ya jamii ya kistaarabu, jamii ikifikia hatua hiyo ya kuamini maneno ya kushutumiana yatolewayo na viongozi wa taasisi nyeti hukosa imani kwa chombo husika jambo ambalo huleta dharau na kupunguza imani dhidi ya chombo hicho.

Cha kujiuliza kwa nini Dk. Hoseah anatumia vyombo vya habari badala ya kupeleka malalamiko yake kwa rais ambaye ndiye amemteua? Kwa nini asiandike mapendekezo yake ili Bunge lipelekewe lifanye mabadiliko katika sheria?

Lakini pia kauli kama hizo ni sawa na kushtakiana au upande fulani kutaka upate sifa ya kuwa unafanya kazi nzuri kuliko mwingine mbele ya Rais Jakaya Kikwete na jamii.

Bado tungali tukikumbuka mapema mwaka huu ni Dk. Hoseah huyuhuyu ambaye alijitokeza hadharani na kuishutumu mahakama kuwa inaendesha kesi za ufisadi taratibu, hivyo kupunguza kasi ya taasisi hiyo kushughulikia watuhumiwa wa rushwa.

Hivi tumuulize Dk. Hoseah malalamiko kama haya alishawahi kuyawasilisha kwenye vikao husika na yakapuuzwa? Je, ni kwa nini kiongozi anayeongoza taasisi inayochunguza kesi za rushwa tu na si Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, ambaye ofisi yake ndiyo imetwishwa mzigo mzito wa kupeleleza kesi zote za jinai, iwe kesi za ujambazi, kughushi, wizi wa kuku, ubakaji, mauji, nk?

Ni kwa nini hata siku moja DCI- Manumba hatujamuona wala kumsikia akijitokeza hadharani na kubwabwaja kwamba ameishapeleleza idadi kadhaa ya kesi za jinai na amezifikisha ofisini kwa DPP na DPP ameshindwa kuzifikisha mahakamani?

Hivi ni kwa nini Takukuru ina papara ya kutaka kesi nyingine za rushwa zipelekwe mahakamani kwa wakati mmoja badala ya kusubiri matokeo ya kesi za rushwa zinazoendelea mahakamani ili wajipime?

Si siri baadhi ya kesi za rushwa zilizopelelezwa na Takukuru ambazo zinahusisha baadhi ya vigogo zinazoendelea kuunguruma mahakamani, tayari upande wa mashtaka katika kesi hizo umekuwa ukipata wakati mgumu kwa sababu upelelezi wa kesi hizo ulifanywa hovyohovyo na hao wachunguzi ambao tumeelezwa wamebobea katika nyanja hiyo na matokeo yake mashahidi wa upande wa mashtaka wanapofika mahakamani kutoa ushahidi katika kesi hizo, wanatoa ushahidi ambao unawatakasa washtakiwa.

Hali inayosababisha hata mambumbu wa sheria kung’amua utumbo huo na kuishia kusema bila kificho kwamba kesi hizo ni sinema na kwamba siku kesi hizo zinapokuja kwa ajili ya kusikilizwa utawasikia wananchi hao wakisema, “Leo tunaenda kurekodi sinema katika kesi ya mshtakiwa fulani mahakamani!”

Hali hiyo inatia hasira kwa walipa kodi wanaojionea madudu hayo pale mahakamani na kufuatilia kesi hizo kupitia vyombo vya habari kwani fedha za walipa kodi zinateketea bure kwa ajili ya upelelezi wa kesi hizo, muda wa mahakama unapotea na serikali yetu inashushiwa heshima mahakamani kwa sababu ya baadhi ya wachunguzi wa kesi hizo wamekuwa wakifanya kazi kwa kukurupuka.

Napenda kumuasa DPP (Feleshi), kwamba afanye kazi yake kwa mujibu wa sheria na Katiba ambazo ndizo zimempa madaraka, kamwe asikubali kufanya kazi kwa maslahi ya watu wachache ambao hivi karibuni tumewabaini kwamba kipindi chote cha kesi hizo za vigogo zilivyoanza kufunguliwa Novemba mwaka jana na hadi sasa pale katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

Na kesi mpya zinazowahusu watu wenye nyadhifa serikalini na kwenye jamii, kwa mbwembwe nyingi zinazochagizwa na kamera za waandishi wa habari tunaokuwepo siku zote za juma mahakamani hapo, inakuwa ni mtaji kwao na kujitapa mitaani na kwa baadhi ya viongozi wenzao wa serikali kwamba ofisi zao zinafanya kazi kwa ari, kasi na nguvu mpya.

Hata kama ni kweli kesi hizo 60 zimepelekwa ofisini kwa DDP, ni vema akaepuka kukurupuka kuzipeleka mahakamani kuliko kukurupuka kuzipeleka huko ambapo mwisho wa siku ikishindwa inakuwa ni aibu kwa ofisi hiyo nyeti pamoja na kuingiza nchi katika hasara.

DDP ni lazima ujue kuwa kama usipokuwa makini katika kazi yako na kuendeshwa na watu kama kina Hoseah utaondoka kwenye wadhifa huo ukiwa na sifa moja mbaya ya wewe “Feleshi ni DDP pekee uliyefungua kesi nyingi kwa kipindi kifupi na serikali ikashindwa mahakamani”. Tumuulize Feleshi je, yuko tayari kutunukiwa sifa hiyo?

Dk. Hoseah huko ni kutojua utendaji wa umma. Inawezekana kwamba humtishii DPP ila hujui vyema maadili katika taasisi ya serikali katika mamlaka aliyonayo au unayajua vyema umeamua kufyatuka kwenye vyombo vya habari.

Mkurugenzi wa Takukuru, Dk. Hoseah, ni miongoni mwa viongozi wa juu wa serikali, anatakiwa kufahamu maadili ya utendaji wa serikali. Sasa namshauri kiongozi huyo arejee (Civil Service Regulation), ataona wazi kwamba serikali yetu haiendeshwi hivyo.

Kwani siku zote tujuavyo, serikali inatoa taarifa kwa vyombo vya habari kwani huo ni wajibu wake, lakini kamwe serikali haiendeshwi kupitia vyombo vya habari. Naomba kutoa hoja!

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika

0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Desemba 13,2009

MAPAPARAZI TUKISAKATA NGOMA ZA OTTU JAZZ


Kulia ni mpiga picha wa Gazeti la Tanzania Daima, Francis Dande,na mpiga Picha wa Gazeti la Mwananchi, Kassim Mbarouk na kusho ni Happiness Katabazi, tukisaka kibao cha Nitakazamoyo,kilichokuwa kikiporomoshwa na bendi ya OTTU Jazz katika Bonanza hilo la Waandishi wwa Habari katika ukumbi wa Msasani Beach Club jijini, Desemba 5 mwaka 2009

HAPPINESS VS KILAJI



Nikiwa na Waandishi wa Habari wa Gazeti letu la Tanzania Daima katika Bonanza hili, tukipata kilaji.

HAPPINESS Vs PANGAMAWE


Nikiwa na mpiga solo wa bendi ya Msondo Ngoma(OTTU JAZZ,Abdul Ridhiwan 'Pangamawe",katika Bonanza la Waandishi wa habari wa vyombo tofauti lilofanyika Desemba 5, mwaka 2009,katika Ukumbi wa Msasani Beach Club Dar es Salaam.

NKESHIMANA JOHN 'DIONE'



strong>KUTOKA HUKUMU YA KIFO HADI KUACHIWA HURU
*ASOTA JELA KWA MIAKA 12, ASIMULIA MATESO YA JELA

Na Hapinnes Katabazi

ADHABU ya kifo ni miongoni mwa adhabu zinazopingwa vikali na baadhi ya watu wanaotetea haki za binadamu kwa madai kuwa inakiuka haki ya kuishi ambayo kila mtu anastahili.

Nkeshimana John ‘Dione’, kamwe hawezi kusahau namna alivyonusurika na adhabu hiyo aliyopewa mwaka 2005 kwa kosa la mauaji ya Tatu Kuyamba, kosa lililomfanya akae gerezani kwa miaka 12 ambapo kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani mwaka 1997.

Tanzania Daima Jumapili, imefanya mahojiano kwa njia ya video na Nkeshimana ambaye amenusurika adhabu kifo ya kifo baada ya kushinda rufani yake aliyokuwa ameikata ambako alikuwa akitetewa na Shirika la Msaada wa Sheria (Nola) kupitia wakili wake Mugaya Mtaki.

Historia ya kilichompata Nkeshimana ni ndefu sana lakini kifupi anasema hakutenda kosa hilo na chanzo cha kesi hiyo ni ugomvi wa kiitikadi za siasa ulioanzia nchini kwao (Burundi) kwani kabla ya kuimbia nchi yao kwa sababu ya vurugu za kisiasa baina yake ya wakimbizi wenzake akiwamo marehemu ambaye alikuwa mfanyabiashara mwenzake wa vitenge.

Anasema na aliingia nchini kwa mara ya kwanza mwaka 1996 na kuendelea kuishi nchini akiendelea kujipatia kipato kwa kufanya biashara hiyo ya vitenge akishirikiana na wakimbizi wenzake.

anabainisha kuwa siku ya tukio, alikuwa yeye na wakimbizi wengine akiwemo marehemu walikuwa katika Kijiji cha Mwikigo wakifanyabiashara ya vitenge, lakini ghafla waliona watu wenye silaha na kuanza kuwakimbiza ambapo walianza kukimbia kwa lengo la kuokoa nafsi zao.

anabainisha kuwa jitihada zake za kujiokoa kutoka katika hatari hiyo iliyokuwa ikimkabili ilizaa matunda kwani alifanikiwa kujinasua pamoja na kunusuru kiasi cha sh 50,000 alichokuwa nacho kisiporwe na watu hao.

Anasema siku iliyofuata ilikuwa ni Jumapili ambapo alikwenda katika Kanisa la Sabato Manyovu na ibada ilipokuwa ikiendelea yeye na mwenzake walikamatwa na polisi walioingia katika kanisa hilo kwa madai kuwa anafanya kazi bila kibali na alipelekwa kituo cha polisi ambako alinyang’anywa fedha na polisi huku mkimbizi mwingine aliyekuwa amekamatwa naye akafanywa shahidi.

Alibainisha kuwa marehemu Tatu alionekana siku ya nne akiwa amekufa na kutumbukizwa kwenye shimo huku akiwa amefungwa kamba shingoni katika kijiji cha Mwikigo. Marehemu huyo alikuwa mfuasi wa chama cha Rais Burundi, Piere Nkurunzinza.

Anasema kisheria kesi hiyo ilikuwa haina dhamana hivyo mahakama ilimwamuru apelekwe gerezani Bangwe na baada ya miezi sita alifunguliwa kesi ya jinai Na. 478/1997 ya wizi wa kuiba kwa kutumia nguvu.

Anaongeza kuwa kesi hiyo mwisho wa siku ilifutwa kwa sababu mashahidi walikuwa hawatokei mahakamani hivyo akawa anakabiliwa na kesi moja ya mauaji ambayo ilikuwa ya kupikwa.

Anaeleza kuwa Desemba 1998 alihamishiwa Gereza la Uyui Tabora ambako alikaa hadi mwaka 2000, mwaka 2005 ndipo alihukimiwa adhabu ya kifo ambayo ilimfanya asote gerezani kwa miaka 12 kabla ya hivi karibuni kufutiwa adhabu hiyo. Adhabu ya kifo alianza kuitumikia Gereza la Uyui baadaye akaamishiwa kutumia kifungo hicho kwenye gereza la Bangwe-Kigoma.

Akizungumzia maisha ya gerezani baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifo, anasema alikataa tamaa na kuona adhabu hiyo ndiyo mwisho wa maisha yake ila alikuwa anajua ameonewa lakini kilichokuwa kikimsikitisha zaidi ni nguo za bluu alizokuwa akizivaa.

Anasema wafungwa wanaosubiri kunyongwa angalau wanakula vizuri na wana uangalizi maalumu chini ya askari wa Jeshi la Magereza pamoja na kulala wafungwa watatu katika chumba kimoja kidogo.

“wakati mwingine chakula kilikuwa kinanishinda kula, niliugua mara tatu gerezani nusura nife ila nashukuru Mkuu wa gereza alinipenda sana, kwa kweli maisha ya adhabu ya kifo yanatisha sana ..tulivyokuwa tukiwasikia wabunge na wanaharakati kwenye redio na televisheni wakisema walioua nao wauawe basi siku hiyo sisi hatulali wala kula.

“Tulikuwa tunalala saa tisa alasiri kuamka hadi kesho yake saa moja asubuhi na tunapokuwepo chumbani tunakuwa tunazungumza kimya kimya ....gerezani kuna watu walikuwa wakijiita marehemu ...tukawa tunajiuliza lini tutanyongwa na kuhoji ni kwanini rais hanyongi,” anasema.

Anabainisha kuwa gerezani kuna sehemu ya kunyongea ambayo walikuwa wakiiona hivyo kuwafanya wachanganyikiwe na kujiona ni wafu wasio na mwelekeo.

“Chumba hicho kilikuwa kimefungwa ndani kilikuwa na minyoro, kwa kusmea ukweli lilikuwa jambo la kutisha na la kusikitisha sana kila nikikumbuka natawaliwa na huzuni,” anasema Nkeshimana.

Anasema adhabu hiyo imemfunza mambo mengi ambapo kwa muda mrefu alikuwa muhalifu halafu mfungwa na sasa yu huru, anabainisha kuwa sheria za Tanzania ni nzuri hasa zikimpata mtoa haki wenye kujali na kufuata misingi yake.

Anabainisha kuwa adhabu ya kifo haifai kabisa kwani wafungwa wa adhabu hiyo akili zao huwa si za binadamu wa kawaida kwa kuwa mtu hujua amepangiwa kufa na binadamu mwenzake jambo ambalo ni baya asana.

Aidha, anashauri sheria ibadilishwe ili kesi kubwa za mauaji angalau zipitie kwa mahakama zisizopungua tatu kuliko ilivyo hivi sasa ambapo kesi za mauaji zinasikilizwa katika Mahakama Kuu na mahakama ya Rufaa.

Anasema mfumo huo unahitaji umakini wa jaji na asipokuwa makini hutoa adhabu ya kifo kwa mshitakiwa asiyefanya kosa jambo ambalo ni sawa na kuminya haki ya msingi ya mtu mwingine.

Anasema kama ilivyo kwenye makosa mengine tofauti mauaji ambapo makosa ya wizi, kughushi na mengineyo yanaanzia kwenye mahakama za chini na kama mtu hajaridhika anakata rufaa mahakama za wilaya mkoa, Mahakama Kuu na Rufaa.

Nkeshimana ambaye anaendelea kuishi kwenye kambi ya Mtabira Kasuru, mkoani Kigoma anasema hivi sasa anaanza masiaha mapya lakini yenye furaha hasa baada ya kukwepa kitanzi kilichokuwa kikimkabili.

Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani lililokuwa likiongozwa na Jaji Natharia Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk ndilo lilosikiliza rufaa ya mkimbizi huyo ambapo Oktoba 26 mwaka huu, ilitengua adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

Shirika hilo la Nola linakodisha mawakili wa kuwatetea wakimbizi wanaokabiliwa na kesi mbalimbali hapa nchini chini ya mradi wa kutoa msaada wa kisheria kwa wakimbizi na jamii inayoizunguka (CPSP) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Mrufani huyo alikata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyotolewa mwaka 2005 na Hakimu Mkuu Mkazi Kigoma, Awasi ambaye alipewa mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya mauji (Extended Jurisdiction) na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora na alimhukumu kunyongwa hadi kufa mrufani ambaye alikuwa akidaiwa kumuua mkimbizi mwenzake aitwaye Tatu Kuyamba.

Nakala ya rufaa hiyo ambayo Tanzania Daima ina nakala yake, Jaji Mbarouk anasema upande wa mashitaka ulidai marehemu aliuawa na mwili wake ulikutwa na kamba shingoni, lakini ulishindwa kuleta kamba hiyo mahakamani ili iwe kielelezo, akasema upande wa mashitaka kushindwa kupeleka mahakamani kamba hiyo kunaacha shaka kubwa kama ni kweli marehemu aliuwawa kwamba na kuongeza kuwa kanuni za uendeshaji wa kesi za jinai upande wa mashitaka unatakiwa udhibitishe kesi yake bila kuacha shaka lolote na katika hilo umeshindwa kuthibitisha mashaka.

Jaji Mbarouk anasema kwa mujibu wa nakala ya hukumu ile Hakimu Awasi alitoa hukumu ya kifo kwa mrufani na kisha akapeleka nakala ya hukumu Mahakama Kuu, anasema kitendo hicho kimeonyesha wazi asivyojua vyema marekebisho ya Sheria Na.

32 ya mwaka 1994.Kwa mujibu wa kifungu cha 173(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002,ambacho kinasema Hakimu Mkazi anayepewa mamlaka ya Mahakama Kuu ya kusikiliza kesi ya mauji kabla ya kutoa hukumu hiyo hakimu huyo anatakiwa kupeleka rekodi ya uamuzi wake Mahakama Kuu ili uwakikiwe.

“Sasa kwa kitendo kile cha Hakimu Awasi kumhukumu mrufani bila kwanza kupeleka rekodi ya hukumu yake Mahakama Kuu ambayo ndiyo ilimteua na kumpa mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya mauji, jopo hili linasema hukumu ile ni batili kisheria.

“Na kwamba ushahidi wa mazingira ambao Hakimu Awasi alisema ulitosha kumtia hatiani mrufani, jopo hili tunasema hiyo siyo hoja ya msingi ya kumuona mrufani ana hatia hiyo mahakama ya rufaa inatengea uamuzi wa Mahakama Kuu uliomhukumu mrufani kunyongwa hadi kufa na pia tunaamuru mrufani aondolewe gerezani,” anasema Jaji Mbarouk.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Desemba 6 mwaka 2009.

WAKILI ATAKA WATUHUMIWA EPA WAFUTIWE KESI

Na Happiness Katabazi

UPANDE wa utetezi katika kesi ya wizi wa sh bilioni 1.8 fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje, katika Benki Kuu, inayomkabili mfanyabiashara Bahati Mahenge na wenzake wanne, umeiomba mahakama iwaone washtakiwa wote hawana kesi ya kujibu.


Ombi hilo lilitolewa jana na wakili wa utetezi Majura Magafu wakati akiwasilisha majumuisho ya ushahidi ili mahakama iwaone wateja wake wana kesi ya kujibu au laa kulingana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka mbele ya jopo la Mahakimu Wakazi, Sekela Mosha, Lameck Mlacha na Sam Rumanyika.

Wakili Magafu alieleza kuwa anataka shtaka hilo lifutwe kwa sababu kifungu hicho hakipo kabisa kwenye sheria za nchi na badala yake kifungu sahihi kilichopo ni cha 305(a,b,c,d) cha sheria hiyo ya kanuni ya adhabu.

“Kwa hiyo mahakama haiwezi kuendeshwa kwa kifungu hicho cha 305(1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu na kosa kama hilo la kujipatia ingizo kwa njia ya udanganyifu hapa nchini halijawahi kutumiwa na kifungu hicho na kwa sababu hiyo leo hii upande wa mashtaka hauwezi kutumia kifungu cha 334(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, kufanyia marekebisho kwa sababu kifungu hiki kinataka makosa yaliyofanywa yaangukie kwenye vifungu vilivyopo kwenye sheria za nchi…sasa katika kesi hii upande wa mashtaka umewashtaki katika kifungu ambacho hakipo kwenye sheria za nchi,”alidai Magafu.

Akizungumzia shtaka la wizi wa sh bilioni 1.8, anadai katika mashahidi wote waliopelekwa na upande wa mashtaka , hakuna hata shahidi mmoja aliyetamka waziwazi kwamba washtakiwa waliiba kiwango hicho toka BoT.

“ASP-Mataba ameshindwa kudhibitisha fedha hizo ziliibwa; na suala jingine la kujiuliza fedha hizo zilizoibwa ni za nani? Sisi tunasema hakuna fedha zilizoibwa kwa sababu BoT yenyewe haijalalamika kuibiwa fedha na kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan ambayo ndiyo iliyotoa idhini kwa kampuni ya Changanyikeni Residential Complex ya hapa nchini kukusanya deni lake ndiyo yenye zile fedha.”

Pia alidai kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha hati ya kuhamisha deni ya Marubeni ya Japan ilighushiwa kwani hati hiyo haikupelekwa moja kwa moja kwa Mahenge bali ilipelekwa moja kwa moja BoT na kampuni hiyo ya Japan na kuongeza kuwa ushahidi unaonyesha kampuni hiyo ya nje siyo mara yake ya kwanza kufanya kazi na Changanyikeni Residential Complex.

“Kwa kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wala mazingira, tunaomba mahakama ifikie uamuzi wa kuwaona washtakiwa Mahenge, Manase Makalle, Davis Kamungu na Edda Makalle, hawana kesi ya kujibu,” alidai Magafu.

Hakimu Mkazi Sekela Mosha aliairisha kesi hiyo hadi Desemba 21 mwaka huu, ambapo upande wa upande wa mashitaka nao utakuja kuwasilisha majumuisho yake.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Desemba 12 mwaka 2009

BABU SEYA ALIONEWA-WAKILI

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Rufani nchini, imeombwa kumwachiria huru mrufani mwanamuzi mahiri wa muziki wa dansi nchini,Nguza Viking maarufu kwa jina la ‘Babu Seya’ na wanaye watatu kwani hukumu zilizowatia hatiani zimejaa kubwa za kisheria.


Mbali na Babu Seya, warufani wengine ni Papii Kocha Nguza,Nguza Mbangu na Francis Nguza ambao wanatatewa wakili wa kujitegemea Mabere Marando na Hamidu Mbwezeleni toka Zanzibar.

Sambamba na hilo pia wakili wa warufani, Mabere Marando na Hamidu Mbwezeleni wamedai kuwa kesi hiyo ni ya kupangwa na kwamba hawajawahi kuona hukumu ya ovyo ya aina hiyo tangu waanze kufanyakazi ya uawakili kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Ombi hilo lilitolewa jana mawakili hao wawarufani wakati wakiwasilisha sababu nne za kupinga rufaa ya Mahakama Kuu iliyotolewa na Jaji mstaafu, Thomas Mihayo na hukumu ilioyotolewa na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Addy Lyamuya, ambao wote walitia hatia washitakiwa kwa makosa ya kujamiana na hivyo kuwafunga kifungo cha maisha jela.

Mawakili hao wa utetezi ambao walianza kuwasilisha sababu hizo tangu saa 3:38 asubuhi hadi saa 7:27 mchana, mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa Jaji Nataria Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk, huku mamia ya wananchi wakiwemo raia wa nchi ya Kongo wakifurika ndani na nje ya mahakama hiyo kwaajili ya kufuatilia kesi hiyo ambayo inavuta hisia za watu wengi na huku wananchi wengine wakati Marando akiwasilisha hoja zake wengine walikuwa wakibubujikwa machozi kwa uchungu.

Marando alianza kwa kueleza mahakama kuwa sababu ya kwanza, pili, tatu,tano,sita,saba,nane, 11,14 na 15 ambazo zinasomeka kwenye hati ya rufaa yao ameamua kuziacha na kwamba anatawasilisha sababu ya tisa ambayo inahusu mahojiano ya awali ya shahidi ambaye ni mtoto mdogo kama ilivyoeleza na katika rufaa ya Jaji Mihayo jinsi Lyamuya alivyowahoji mashahidi ambao ni watoto wadogo katika kesi hiyo.

Marando anachambua kuwa mstari wa 7-9 ukurasa wa 645 katika rufaa ya Mahakama Kuu, Jaji Mihayo anasema “Hakimu Lyamuya alitumia utaratibu wenye makosa na hatimaye alimalizia kwakusema kwamba hakimu huyo kwamba ‘kisheria na ukweli hakufanya mahojiano kihalali na hao watoto(mashahidi) kabla ya watoto hao kuanza kutoa ushahidi wao”;

Akadai kuwa lakini mwishowe katika ukurasa wa 647 mstari wa 25-27 Jaji Mihayo anasema pamoja na makosa hayo ushahidi ulitolewa na mashahidi hao unakubalika.

“Washimiwa na majaji wa mahakama ya rufani sisi tunasema jaji na hakimu huyo kwakusema hayo hakitaka hukumu zao walikosea kisheria kwani sheria inaitaka mahakama kabla haijaanza kuchukua ushahidi wa mtoto ni lazima ijiridhishe mtoto huyo anaakili timamu na anaelewa maana ya kiapo na kisha irekodi hayo kwenye jarada la kesi lakini Hakimu Lyamuya hakufanya hivyo wala kuandika rekodi ya hayo”alida Marando.

Marando akiwalisha sababu hizo kwa kujiamini alidai kuwa kwa makosa hayo ya kisheria yaliyofanywa na hakimu na Lyamuya huyo hadi wakafikia uamuzi wa kufunga kifungo cha maisha warufani, ni wazi kabisa walikuwa wanapinga na sheria za nchi na maamuzi yaliyotolewa na majaji wa mahakama za hapa nchini kwenye kesi mbalimbali , ambazo alizitumia jana kusapoti hoja zake.

“Mashahhidi 10 ambao ni watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 6-8 ambapo upande wa mashitaka ulidai ndiyo walibakwa na kulawitiwa na warufani,walipofika mahakama ya Kisutu kutoa ushahidi wao hawakuhojiwa na wala mahakama aikujiridhisha kama wana akili timamu kwasababu hiyo tunasema kwamba ushahidi wa watoto hao ni batili na tunaliomba jopo lenu lisiukubali”alidai Marando.

Alionyesha ukurasa 661 ukurasa wa 20,Jaji Mihayo alisema Hakimu Lyamuya aliangalia kwa makini ushahidi wa upande wa mashitaka na utetezi.Marando alidai katika hilo jaji huyo hakutenda haki kwasababu mahakama ya chini iliangalia ushahidi wa upande wa utetezi kwa namna isivyolidhisha.

Akiwasilisha sababu 16,17 na 19 kwa pamoja Marando alionyesha kuwa katika ukurasa 661 haya 20,Mihayo aliendelea kusema mahakama ya Kisutu ilizingatia ushahidi wa upande wa utetezi lakini katika hukumu ya iliyotolewa na Lyamuya katika ukurasa wa 529 mstari wa 15, alidai hakimu huyo aliandika maoni yake binafsi ambayo yanapishana na mashahidi wa upande wa utetezi kitu ambacho kinapingana na sheria za nchi.

“Ukurasa wa 532 katika hukumu iliyoandikwa la hakimu huyo, utaona wazi hakimu huyo anabisahana na shahidi baada ya kumbishia shahidu huyo kwamba siyo Mzaramu,wakati shahidi huyo aliambia mahakama mama yake ni mzaramu na baba yake ni Mkongo....haya ni mambo madogo lakini yanaonyesha ni jinsi gani Hakimu Lyamuya alivyopuuza ushahidi wa upande wa utetezi.

“Waheshimiwa majaji na mahakama hii tukufu, sijawahi kuona hukumu kama hii kwa miaka 30 tangu zinaanze kazi yangu ya uwakili ...kwani sote tunachujua maoni ya hakimu katika hukumu yanaandikwa pembeni lakini katika hukumu hii hakimu ameweka maoni yake”alidai Mrando na kusababisha watu kuangua vicheko.

Akichambua ukurasa 541 mstari wa 15-16 katika hukumu ya Kisutu, mrufani wa pili, Papi Kocha anaeleza alivyokuwa mikoani akifanyaziara ya kikazi ya kimuziki, lakini hakimu Lyamuya katika hukumu yake akaweka mawazo yake kwakusema hata kama alikuwa safari anaweza kutenda makosa hayo ‘possibility crime’ aliporudi kutoka safari.

“Lakini majaji katika rufaa ya Mahakama Kuu hakuna ushahidi ulitolewa unaonyesha warufani walibaka...hayo yalikuwa ni mawazo ya hakimu kwamba lazima Babu Seya na watoto wake waende gerezani....narudia tena sijawahi kuona hakimu wa aina hii na hukumu ya aina hii ambayo hakimu aliamua kuweka maoni yake binafsi kwani kinachowatia hatiani washitakiwa katika kesi zote ni ushahidi nasiyo maoni ya hakimu”

“Ni wajibu wa mahakama kutafakari ushahidi wa utetezi hata kama hauana uzito sasa huyu Lyamuya katika hukumu yake amewataja mashahidi wa utetezi waliokuja kutoa ushahidi bila kueleza mashahidi kwa mapana walieleza nini”

“Kwa mkanganyiko huu uliofanywa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Lyamuya siyo tu alikosea kisheria nasema alifanya makusudi na alikuwa ameshaamua kuwapeleka jela warufani” alidai Marando kwa hisia kali.

Akichambua ushahidi wa shahidi wa upande wa mashitaka Azah Hassan(7) ambaye akuapishwa,alidai shahidi huyo alifundishwa kusema uongo wa dhahiri kwani mtoto aliiambia mahaka walikuwa wakifundishwa Kiingereza na aliyekuwa mshitakiwa wa tano ambaye ni mwalimu wa shule ya Msingi Mashujaa, Sigirinda Ligomboka ambaye aliachiriwa huru.

“Watukufu majaji swali je kwanini watoto wote waseme uongo?Azah alisema alikamatwa na watoto wa Babu Seya,bila ya kutaja ni watoto gani kwa majina wala kuwatambua mahakamani ,sasa ushahidi wake siyo sahii.

“Ni Azah huyo huyo katika ushahidi wake alidai Babu Seya alimbaka lakini hakuna rekodi yoyote inayoonyesha shahidi huyo alimtaja mrufani pili,tatu na wanne.Na katika ukurasa114-115,shahidi huyo ametaja majina ya vijana waliomkamata ni Cheupe na Sembe na katika warufani wote hao hakuna mrufani mwenye majina hayo ya Cheupe na Sembe na upande wa mashitaka wala hawakuwaleta mahakamani watu hao ili wawe mashahidi.”alidai Marando na kusababisha wananchi kubaki vinywa wazi.

Akiendelea kuuchambua ushahidi wa Azah,unaonyesha shahidi huyo alikuwa akibakwa hata siku za shule na moja ya tarehe ni Oktoba 11,2004 tarehe ambayo ilikuwa ni siku ya Jumamosi ,wanafunzi hawaendi shule na kwamba tarehe hiyo tayari Babu Seya alikuwa ameishakamatwa nakuhoji kuwa sijui babu seya siku hiyo alitoka rumande na kwenda kumbaka shahidi huyo?.

Akichambua kwa ujumla ushahidi wa watoto hao ,alidai kuwa hakuna shahidi wa upande wa mashitaka aliyeiambia mahakama kuwa makosa hayo yalitendekea April,Mei,Juni,Julai,Agosti,Septemba na Oktoba isipokuwa hati ya mashitaka inasomeka kwamba makosa yote yalitendeka kati ya Septemba na Oktoba lakini Jaji na hakimu huyo wakaridhia.

Akiuchambua ushahidi wa shahidi wa 14 wa upande wa mashitaka,Days Safari ambaye aliambia mahakama ya Kisutu, kwamba hamfahamu Babu seya wala Papi na kwamba hawapo mahakamani na hata angeonyeshewa kisu asingeweza kuwatambua lakini hati ya mashitaka inasomeka shahidi huyo alibakwa warufani hao na Hakimu Lyamuya katika hukumu yake akasema kuwa upande wa mashitaka umethibitisha kesi hiyo pasipo shaka yoyote na Jaji Mihayo akamuunga mkono.

Kuhusu shahidi 11 wa upande wa mashitaka, Yasinta Mbegu katika ukurasa wa 26 wa hukumu ya Hakimu Lyamuya, aliambia mahakama hakufanywa chochote wala kubakwa na warufani,Marando alidai kwakuwa Lyamuya alikuwa ameishapanga warufani awapeleke jela akawahukumu kifungu cha maisha kwa ushahidi dhahifu na wakutunga kama huyo.

Akiendelea kuchambua ushahidi wa shahidi wa mtoto mwingine aitwaye Gift ambaye alidai mahakamani kuwa alibakwa Babu Seya na akamuambukiza Kisonono, na licha ya mrufani huyo kutaka akapimwe kama anaugonjwa huo ili ushahidi upatikane upande wa mashitaka ulikataa kwenda kumpima Babu Seya na hata hivyo ripoti ya daktari wa Hospital baada ya kumpima mtoto huyo ilibaini mtoto huyo hajaambukizwa ugonjwa huo na upande wa mashitaka ulikataa ripoti hiyo ya daktari itolewe kama kielelezo mahakamani.

Kuhusu ushahidi ulitolewa na shahidi wa tatu wa upande wa mashitaka Alocia Longino kwamba alitokwa damu baada ya kubakwa lakini taarifa ya daktari ikaja kusema shahidi huyo bado ni bikra na wala haonyeshi aliwahi kubikiriwa wala kuingiliwa kinyume na maumbile.

“Longoni alidai alikuwa anakamatwa chooni na alizishuhudia manii za Babu Seya ni nyeupe na zilikuwa zinaruka hewani kama nzi...jamani majaji huu ni uongo wa hali ya juu natunaomba jopo Hakimu Lyamuya alipata jazba wakati akitoa hukumu hiyo”alidai Marando na kufanya watu kushikwa na butwaa

Alihoji ni kilichofanya upande wa mashitaka kuficha ripoti ya daktari aliyewafanyia uchunguzi watoto hao wanaodaiwa walibakwa na warufani na kushindwa kuleta mashahidi ambao ni wanamuziki wa Bendi ya Achigo, mama wa Babu Seya na Mke wa Babu seya kwasababu waliona mashahidi hao wangewaumbua.

“Kesi hii ni ngumu kweyu sote na kama mahakama na sisitunaona warufani walifanya haya makosa tuwalaani ila mimi Marando nasema nimejiridhisha hawajafanya hayo makosa:

“Hivi tujiulize Kibaiolojia kweli inawezekana mtoto wa miaka sita apakwe na wanaume hawa(warufani)nyuma na mbele halafu mtoto wa umri huo aweze kutembea?Aiingii akilini hata kidogo nasema kesi hii ni ya kutunga kwani hata mwanamke mwenye umri wa utu uzima akifanyiwa unyama huo hawezi kutembea.”alidai Marando na kusababisha umati uliofurika kuendelea kuacha vinywa wazi kwa mshangao.

Akijibu hoja za mrufani, wakili Mkuu wa Serikali Justus Mulokozi ambaye alitumia nusu saa kujibu hoja hizo alidai kuwa kitendo cha shahidi kushindwa kumtambua mshitakiwa mahakamani siyo sababu inayopeleka ushahidi wa shahidi huyo kuonekana hauna thamani, jibu lilosababisha umati wa watu kuangua vicheko.

Mulokozi alidai pia mahakama ikiamini upande mmoja, halazimiki kuangalia upande mwingine lakini hata hivyo hoja hiyo ilipingwa vikali na Marando ambaye alidai kuwa hoja hiyo haikupaswa kutolewa na wakili mwandamizi kama Mulokozi kwani hoja hiyo inatofautiana na sheria za nchi na kauli hiyo ya wakili wa serikali imedhiirisha sasa ni kweli Lyamuya aliegemea uegemea ushahidi wa upande wa mashitaka tu.

Jaji Nataria Kimaro alisema jopo hilo tayari imeishamaliza kusikiliza rufaa hiyo na akasema jopo lake litatoa taarifa ya hukumu.

Baada ya kuairishwa kwa kesi hiyo umati wa wananchi waliofurika kufuatilia kesi hiyo walimrukia na kumkumbatia wakili Mabere Marando kwa furaha na kumpachika jina la ‘Simba wa Vita” huku wangeni wakilisukuma gari ambalo lilikuwa linawabeba warufani kuwarudisha gerezani na huku wengine wakiimba nyimbo mbalimbali za kujifari kwamba wanaimani na mahakama ya rufani chini ya jopo hilo litatenda haki.

Januari 27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25 mwaka 2004.

Waomba rufani hao wanakabiliwa na makosa kumi ya kubaka watoto wa kike wenye umri kati ya miaka sita na nane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri kama huo na kwamba wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya April na Oktoba 2003 eneo la Sinza kwa Remmy, jijini.

Aidha katika kesi hiyo mwalimu wa shule ya Msingi Mashujaa, Sigirinda Ligomboka, alishitakiwa kwa makosa mawili ya kumsaidia Babu Seya kutenda makosa ya kubaka na kulawiti kwa kuwaruhusu baadhi ya watoto hao kutoka madarasani.

Upande wa mashitaka ulileta mashahidi 24, ambao upande wa utetezi ulipinga vikali kutenda makosa hayo na uliita mashahidi nane.Katika hukumu yake Hakimu Lyamuya alitupilia mbali na utetezi wa Babu Seya na wanawe na akawatia hatiani kwa makosa hayo na hivyo kuwafunga kifungo cha maisha gerezani.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Desemba 4 mwaka 2009












o

KORTI YAKATAA SAMAKI WA MAGUFULI KUGAWIWA BURE

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imelikataa ombi la upande wa mashitaka katika kesi ya uvuvi haramu inayowakabili raia 37 wa kigeni waliokamatwa kwenye meli ya Tawariq 1, la kutaka uruhusiwe kugawa samaki hao bure.


Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Razia Shekhe baada ya kubaini hati ya kiapo kilichoambatanishwa na ombi hilo kuwa na dosari za kisheria.

Jaji Shekhe alizitaja dosari hizo kuwa ni upande wa mashitaka kushindwa kueleza kampuni au mtu aliyefanya tathimini ya samaki hao pamoja na kutotaja thamani yake.
“Kwa sababu ya dosari hizo, mahakama hii inatupilia ombi la upande wa mashitaka ulioiomba mahakama iwaruhusu kugawa bure samaki wale ambao ni kielelezo,” alisema Jaji Shekhe.

Awali, wakili wa utetezi Ibrahimu Bendera alipinga ombi hilo kwa madai kuwa samaki hao ni kielelezo na kwamba kinachotakiwa kisheria ni samaki hao wauzwe na fedha zitakazopatikana zihifadhiwe mahakamani.

Kabla ya upande wa mashitaka kuwasilisha ombi hilo mwishoni mwa mwezi ulipita, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli alikaririwa kwenye vyombo vya habari akiutangazia umma kwamba samaki hao watagawiwa bure na kwamba taratibu za kuwagawa zinafanyika.

Wakati Magufuli akitoa taarifa hiyo kwa umma, upande wa mashitaka ulikuwa haujawasilisha ombi la kutaka samaki hao wagawiwe bure na wala mahakama haikuwa imetoa uamuzi wa samaki kugawiwa.

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kuwa kuwa Machi 8 mwaka huu, majira ya saa sita usiku katika ukanda wa Bahari ya Hindi, ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walikamatwa wakivua samaki bila leseni.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Desemba 4 mwaka 2009

RUFAA YA BABU SEYA SASA KESHOKUTWA

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Rufani nchini, jana ilishindwa kuanza kusikiliza rufaa ya ya mwanamuziki mahiri wa dansi hapa nchini, Nguza Viking maarufu kwa jina la ‘Babu Seya’ na wanae watatu ilishindwa kuanza kusikilizwa kwasababu pande zote mbili katika kesi hizo hazikuwa tayari kuanza kusikiliza rufaa hiyo.


Mbali na Babu Seya, warufani wengine ni Papii Kocha Nguza,Nguza Mbangu na Francis Nguza ambao wanatatewa wakili wa kujitegemea Mabere Marando.

Jaji Nataria Kimaro,Salum Massati na Mbarouk Mbarouk walisema wanakubaliana na maombi yaliyowasilishwa na mawakili wa pande zote yaliyotaka shauri hilo liairishwe ili waweze kupata muda wa kupitia nakala ya rufaa hiyo.

“Jopo limeyakubali maombi yenu ya kutaka usikilizwaji wa rufaa hii uairishwe ili mpate muda wa kujiandaa, hivyo tunaairisha rufaa hii hadi Desemba 3 mwaka huu, siku hiyo itaanza kusikilizwa” alisema Jaji Nataria Kimaro ambaye ni kiongozi wa jopo la majaji wanasikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo ukumbi Na.2 wa Mahakama ya Rufani, jana ulifurika watu waliofika mahakamani hapo kwaajili ya kusikiliza rufaa hiyo ambayo imekuwa ivuta hisia za watu wengi.

Awali kabla ya kuairishwa kesi hiyo wakili wa warufani Marando, aliiambia mahakama kuwa ameajiriwa kuendesha kesi hiyo wiki iliyopita na akabaini kichwa cha habari cha rufaa hicho kimeandikwa rufaa ya jinai Na.59/2009 badala ya kuandikishwa rufaa ya jinai Na.59/2005, hivyo akaomba kichwa hicho cha habari kiafanyiwe marekebisho na isomeke rufaa ya jinai Na.59/2005, ombi ambalo alikupingwa na upande wa mashitaka.

Aidha alieleza mahakama kuwa anatarajia kuongeza sababu nne katika rufaa hiyo na kisha kuziondoa sababu nne kati ya sababu 19 zilizowasilishwa awali na wakili wenzake Hurbet Nyange na kuongeza kuwa amechelewa kuwasilisha sababu hizo mapama kutokana na ukubwa wa nyaraka zilizomo ndani rufaa hiyo.

Akijibu hoja hizo Wakili Mkuu wa Serikali Justus Mulokozi aliambia mahakama kuwa waliopokea nyongeza ya sababu za kukata rufaa Ijumaa wakati muda wa kazi ulikuwa umekwisha hivyo naye akaomba wapewe muda ili waweze kuzipitia kwa kina ili wakati rufaa hiyo ikianza kusikilizwa wawe na majibu ya uhakikika.

Januari 27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25 mwaka 2004.

Waomba rufani hao wanakabiliwa na makosa kumi ya kubaka watoto wa kike wenye umri kati ya miaka sita na nane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri kama huo na kwamba wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya April na Oktoba 2003 eneo la Sinza kwa Remmy, jijini.

Aidha katika kesi hiyo mwalimu wa shule ya Msingi Mashujaa, Sigirinda Ligomboka, alishitakiwa kwa makosa mawili ya kumsaidia Babu Seya kutenda makosa ya kubaka na kulawiti kwa kuwaruhusu baadhi ya watoto hao kutoka madarasani.

Upande wa mashitaka ulileta mashahidi 24, ambao upande wa utetezi ulipinga vikali kutenda makosa hayo na uliita mashahidi nane.Katika hukumu yake Hakimu Lyamuya alitupilia mbali na utetezi wa Babu Seya na wanawe na akawatia hatiani kwa makosa hayo na hivyo kuwafunga kifungo cha maisha gerezani.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Desemba mosi mwaka 2009

TUMSIHI MKAPA AENDELEE KUKAA KIMYA

Na Happiness Katabazi

MOJA ya mambo ambayo nina hakika yanaleta faraja kwa Serikali ya Awamu ya Nne ni ukimya wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kuhusu tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, pamoja na malumbano ya hapa na pale ya kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili aweze kufikishwa mahakamani kukabiliana na tuhuma hizo.


Pamoja na kufurahia jambo hilo, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hivi sasa tumeanza kuwa na wasiwasi kwamba kiongozi huyo mstaafu ataendelea kukaa kimya?

Ni lazima wananchi watafakari kwa kina juu ya tuhuma za Mkapa, kwa nini zimeshamiri zaidi katika Awamu ya Nne?

Bila shaka jibu ni rahisi kuwa kulikuwa na uratibu maalumu wa kutangaza mabaya ya Mkapa ili watu watumie muda mwingi kufikiria na kuyazungumza mabaya yaliyofanywa na kiongozi huyo huku Serikali ya Awamu ya Nne ikiendelea kupumua na kufanya ufisadi kwa kadiri iwezavyo.

Ukitazama kwa kina utabaini kuwa mgawanyiko na malumbano ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiyo uliozaa haya tunayoyaona hapa nchini ambapo baadhi ya mambo ya maendeleo yanakwamisha kwa sababu ya chuki binafsi, kukomoa kunakofanywa na viongozi waliopo ndani ya chama tawala.

Hatuhitaji kuficha mabaya yaliyofanywa na kiongozi aliyetangulia lakini ni lazima tujiulize, je, ni kweli yatatusaidia kuziba nyufa zilizojitokeza au ndiyo yatabomoa kabisa nyumba tuliyoijenga kwa miaka mingi chini ya utawala wa Mwalimu Julius Nyerere?

Kwa nini hatujipi muda wa kutafakuri kwa nini viongozi na watendaji waliotenda maovu katika utawala wa Awamu ya Nne hawafikishwi mahakamani kama inavyoshinikizwa kwa Mkapa?

Si tunajua wapo watendaji na wanasiasa walishiriki katika kashfa za Richmond EPA, rada na nyinginezo lakini bado wanaendelea na nyadhifa zao pasi na aibu na uchungu kwa kutafuna rasilimali za taifa, tuna sababu gani la kumdhalilisha, kumuaibisha na kumkejeli Mkapa wakati tunajua fika kuwa hata Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, na yule wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, kuna makosa walifanya na mengine tunayajua waliyafanya kwa masilahi binafsi au familia zao, mbona hatujawaandama kama tunavyofanya kwa Mkapa?

Ni upumbavu kujadili makosa ya kiongozi mmoja mmoja alivyotumia vibaya madaraka yake akiwa Ikulu badala ya kujadili mfumo mzima uliomuwezesha kuingia madarakani pamoja na kufanya biashara zake akiwa Ikulu.

Kama tusipobadilika na kuuangalia mfumo huo kamwe hatutatua tatizo na kila kukicha tutakuwa tunawaandama viongozi wastaafu kwa sababu ya kutumia vibaya madaraka yao kwa misingi ile ile ya malumbano ya kutoa ahueni kwa serikali ya nne ambayo mpaka sasa imeshindwa kuleta maisha bora iliyowaahidi wananchi katika ilani yao ya uchaguzi ya mwaka 2005.

Mfumo uliopo wa wizi kutendeka kitaasisi ni hatari zaidi kuliko kuanza kushughulikia makosa ya mtu mmoja mmoja kama tunavyofanya sasa, tujiulize ni lini kulindana ndani serikali na chama tawala kutamalizika?

Kwa nini tusichukue hatua za kusafisha mfumo huu mbovu uliozaa EPA, rada, Richmond kuliko kumng’ang’ania Mkapa?

Si tumeshasikia fedha zilizoibwa Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited kuchota kiasi cha sh bilioni 40 katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) iliyokuwapo chini ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilivyoisaidia CCM katika kampeni na hatimaye ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Leo hii tunawezaje kutoka mbele za watu na kudai tunapambana na ufisadi wakati wamiliki wa Kagoda hawajafikishwa mahakamani wakati wao ndio waliochota kiwango kikubwa cha fedha kulinganisha na wengine? Tutafakari tuchukue hatua.

Nani anayeweza kujitokeza hadharani na kuueleza umma kuwa ufisadi anaotuhumiwa kuufanya Mkapa aliufanya peke yake pasi na kushirikiana na wengine? Inawezekana vipi baraza la mawaziri lisijue kile kinachofanywa na kiongozi mkuu wa nchi? Bunge lilikuwa wapi mbona hawakupiga kura ya kutokuwa na imani na rais?

Waliamua kufunika kombe mwanaharamu apite kwa kuwa walijua wazi kuwa mfumo wa serikali na chama tawala ni kulindana na wao kuna maeneo wanafaidika.

Tunapohoji nafasi ya Rais wa Awamu ya Tatu (Mkapa) kufanyabiashara akiwa madarakani, Serikali ya Awamu ya Nne inajiondoa vipi katika tuhuma kwamba wengi wa watendaji na viongozi ni wanatumia madaraka yao kufanyabiashara?

Kwa bahati mbaya wananchi wamekuwa vipofu wenye kupenda kushabikia kila kinachosemwa na wanasiasa ambao wanajua waseme au wafanye nini kwa wakati gani, wananchi wanapaswa wakae chini na kuchambua utekelezaji wa ahadi moja moja zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Nne badala ya kushabikia mambo ambayo mwisho wa siku hayana tija kwa taifa zaidi ya kuzidisha ugumu wa maisha.

Wananchi wana kitu gani cha kuipongeza Serikali ya Nne katika mapambano ya ufisadi wakati hata kesi zilizopo mahakamani nyingi zinaonekana zimepelekwa kwa ushabiki wa kisiasa au chuki binafsi?

Mfumo ndiyo chanzo kikuu cha kuzalisha kiongozi mzuri au mbaya, kama mfumo utakuwa mzuri kwa hakika hata viongozi watafanyakazi katika mfumo huo, utendaji wao utakuwa safi na uliojaa uadilifu lakini kama mfumo utakuwa mbaya hata aje kiongozi safi kama malaika hataweza kuubadilisha, kwani atamezwa na mfumo na mwisho wa siku naye atakuwa mchafu kama matope.

Kuna mifano mingi duniani ambapo serikali zilizoundwa na kuingia madarakani kwa mifumo mibovu imezivuruga nchi zao, Tanzania kabla ya kupata uhuru wake mwaka 1961 mfumo uliokuwapo kwa kiasi kikubwa ulikuwa ukitoa upendeleo kwa wakoloni lakini mara baada ya kupata uhuru Mwalimu Nyerere na viongozi wengine walijaribu kuboresha mfumo wa kiutawala kuanzia katika elimu, afya, miundombinu na huduma nyinginezo.

Lakini kwa bahati mbaya utawala wa Mwalimu Nyerere kuna baadhi ya mambo alishindwa kuyaweka katika mfumo uliokuwa unatakiwa, ulipoondoka madarakani na kuingia utawala wa mzee Mwinyi ‘Ruksa’ hatukusikia mabaya ya Nyerere kwa kiwango kikubwa kama tunavyosikia ya Mkapa hivi sasa, hivyo hivyo hata alipoingia Mkapa pia hatuyumbishwa na mabaya aliyoyafanya Mwinyi kwa sababu yaliyofanyika huko nyuma yalishapita, tulikuwa tukihitaji kujipanga vizuri pale tulipokosea ili maendeleo ya wananchi yapatikane.

Ni jambo la kusikitisha sana hivi sasa nchi ina wasomi wengi zaidi lakini maadili ya viongozi ndiyo yanazidi kumeguka siku hadi siku tofauti ilivyokuwa kwa Mwalimu Nyerere na Mwinyi, kila mtu sasa ni muongeaji, mtendaji na kiongozi.

Tuulizane inawezekana vipi zaidi ya miaka 45 ya uhuru taifa halijitoshelezi kwa umeme kiasi cha kuingia katika mgawo wa kutisha, ni taifa gani linaweza kuendelea iwapo umeme haupo wa kutosha pamoja na kukatikatika hovyo hata katika hafla kubwa kama ile ya marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutiliana saini ya kuanzisha soko la pamoja pale kwenye ukumbi wa AICC Arusha wiki chache zilizopita.

Kwa nini nchi iwe maskini wakati kuna madini mengi ambayo kama yakitumika ipasavyo nchi haiwezi kutembeza bakuli la kuomba misaada ya wahisani katika bajeti yake, mbona utawala wa Rais Kikwete umeshindwa kusimamia madini kwa faida ya Watanzania?

Rais Kikwete aliunda tume ya kupitia mikataba ya madini ili itoe mapendekezo ya kuboresha kile kinachopatikana lakini mbona mpaka sasa kimya? Ripoti ile ilitolewa mapema sana lakini mbona imegeuka godoro la watu kuchapa usingizi?

Inawezekanaje mpaka leo hii nchi ikose dawa katika zahanati, hospitali, vituo vya afya wakati kuna mamilioni ya fedha yanatafunwa na viongozi kwa miradi ya uongo na ukweli, barabara mbovu, maji tabu, vyote hivi ni Mkapa kavisababisha?

Hapana huu ni mfumo mbovu wa chama tawala (CCM) bila kupigania kuuondosha kamwe maisha bora hayatapatikani, tutakuwa tukiyasoma, kuyasikia na kuyaangalia kwenye runinga, redio na magazeti kupitia kwa wenzetu.

Ni jukumu la Watanzania kuamka ili viongozi wasiendelee na utaratibu wa kufikiri wao ndio wenye akili zaidi kuliko wengine, tunahitaji mabadiliko lakini hayawezi kuja kama tutaendeleza woga, unafiki na chuki.

Tusipofanya hivyo tutakuwa tupo kwenye sala moja na uongozi wa Awamu ya Nne ya kumsihi Rais mstaafu Benjamin Mkapa aendeleze ukimya wake ili awape unafuu wa kutawala kwa kuwa tayari wameshaonyesha kushindwa kiuchumi, kimaadili, kiutawala na mengineyo.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania la Jumapili, Novemba 29 mwaka 2009

CCM YAGEUKA BENDI YA TAARABU?

Na Happiness Katabazi

MALUMBANO yakipuuzi yanayoendelea katika makundi yayohasimiana ndani ya chama cha mapinduzi yanathibitisha maneno ya mwenyekiti wa chama hicho rais Jakaya Kikwete,alipowaambia wananchi kwamba ndani ya ccm kuna makundi yanayochukiana na kuasimiana kiasi kwamba mtu anashindwa kuacha glasi yake ya maji kwa kuhofu uenda akawekewa sumu.


Kile ambacho CCM ilikipanda ndani ya vyama vya upinzani sasa kimewageukia na kinawatafuna sasa.

Hapo zamani ilikuwani shangwe na vigelegele kuwacheka wapinzani na kuwaita ni mabingwa wa mitafaruku lakini ssa CCM leo hii tuwaite ni vingunge wa ufisadi na umbeya au mapaka shume ,manyani au magwiji wa mipasho?

Kile wanachokifanya wabunge wa CCM kwenye Kamati ya Rais Hassan Mwinyi ,ni ukweli wa mambo na uchafu ulio ndani ya chama hicho tawala.Ni sawa na wachawi waliokengeuka wanapoanza kuloga mchana na kuanza kuweweseka na kuwataja watu waliowaua na kuwala nyama.

Habari toka ndani ya kamati hiyo zinatisha na kusikitisha.Lakini tunajua zote zina ukweli.La msingi kwa watanzania ni kujua hawa wote hawafahai kuwa viongozi wetu hivyo tusiwachague tena .

Haijalishi kwamba kundi moja linajitetea na kujikosha mbele za watu lakini ukweli ni kwamba kujikosha huku kunaandaliwa makusudi kwaajili ya uchaguzi mkuu ujao.

Una watu ambao wanataka kutumia mwanya huo na taasisi za umma kujisafisha ili wagombee na kuwa tena wabunge, marais wajao.

Inakuwa kana kwamba nchi hii wameumbiwa wao na hakuna Mtanzania mwingine mwenye sifa za kuongoza isipokuwa wao.Kama mtu alipewa nafasi ya kuongoza akawa fisadi anataka kurudi kufanya nini tena?Hanataka kujakufanya ufisadi kipeuo cha pili?

Ni vizuri na tunamsifu Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete kwa kuunda kamati ya ‘umbeya’ ikiongozwa na mwenyekiti mstaafu wa chama hicho rais mwinyi.

Lakini tukumbuke kwamba kila umbeya una unaupande.Tutakuja kujua huyu Mwinyi yupo kundi lipi nay eye mwenyekiti wa sasa Kikwete yupo kundi lipi.

Kwasababu makundi hayo yanayoendelea kuparulalana na kuvuana nguo adharani huwa yanageuka nyuma kuangalia wapambe waona katika hili hakuna moja ndani ya ccm awe kiongozi mstaafu au aliypo madarakani hauisiki kwa njia moja ama nyingine kwa kashfa zinazozungumziwaaua hazijazungumziwa.

Kwani tumeona na kusikia kashfa zile zile wakati ambapo kashfa mpya zinazaliwa kila siku.kwani kuna usemi usemao mlani mla leo mla jana kala nini.

Kashfa ya Richmond ,ndege ya rais,helkopta za JWTZ,mitambo ya IPTl,mikataba ya migodi,BoT,mifuko ya pesheni,kila moja ya hizo ina Mapapa ambao wapo ndani ya serikali na wengine wamestaafu na watanzania hawatakuja kujua ukweli wake kwasababu wengi walioopo madarakani wana mizizi katika kashfa hizo kwani watuhumiwa wa kashfa hizo ni ndugu zao au maswahiba zao .

Kamati ya ‘umbeya’ inayoongozwa na Mwinyi haina tija kwa taifa wala ccm ukiacha ukweli kwamba inafurahisha ‘manyani’ na kuwakela binadamu.Mtasemana,mtapalulana lakini walioshika nyadhifa wataendelea kuzishikilia ang’oki mtu ng’o na wasiojua watazani ccm itakayoibuka baada ya kmati hiyo kumaliza muda wake itakuwa safi zaidi.

Licha ya udhahidi huu mkubwa ,hakuna dalili kwamba vyama vya upinzani vitajifunza na kuwa na sifa zaidi kuizidi CCm.Inavyoonekana ama ni vishiriki katika ufisadi ama vinakosa nafasi ya kuwa mafisadi.

Madhara ya kuwa na makundi ndani ya vyama, mkundi yenye rangi ya ukabila, udini,tayari yapo katika vyama vikuba vya upizani na hivyo haviwezi kuinyoshea ccm kidole.

Kama kipo chama cha upinzani kitakachojifunza somo la haya yanayotokea ndani ya ccm hivi sasa ,hiyo itakuwa ni neema kubwa kwa taifa letu.

Mungu ibariki Tanzania ,Mungu ibariki Afrika

0716 774494

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Novemba 18, 2009

SHAHIDI:UJENZI BOT HAUKUSABABISHA HASARA

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa saba wa upande wa mashitaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, amedai kuwa hapakuwapo na hasara iliyopatikana katika ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo.


Shahidi huyo ambaye ni mkadiriaji wa gharama za majengo kitaaluma, Harold Herbert Webb (74), raia wa Uingereza, alitoa maelezo hayo jana wakati akijibu maswali ya wakili wa utetezi, Onesmo Kyauke, mbele ya kiongozi wa jopo la mahakimu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Webb alidai hapakuwepo hasara yoyote licha ya kuwapo kwa mabadiliko ya ujenzi na kiasi cha fedha kuongezeka kutoka dola milioni 73 hadi dola 357,568, kiasi chote hicho kilitumika kwenye mradi wa ujenzi huo.

“Hakuna hasara ya fedha iliyopatikana kwenye ujenzi huo, kwa sababu kiasi hicho kilichotengwa awali na kilichokuja baadaye baada ya BoT kuagiza yafanyike mabadiliko ya nyongeza ya maghorofa, kiasi hicho chote kiliingizwa kwenye mradi huo,” alidai Webb.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano baina ya mawakili wa utetezi Onesmo Kyauke, Majura Magafu, Hudson Ndusyepo na shahidi huyo:

Wakili: Nani alikuteua kufanya kazi ya ukadiriaji wa gharama za ujenzi wa mradi huo?

Shahidi: Kampuni ya ukandarasi ya Design & Services Ltd, kampuni ambayo ndiyo iliyopewa kazi ya kuchora majengo ya BoT.

Wakili: Ni mazoea katika shughuli za ujenzi kufanyika kwa mabadiliko?

Shahidi: Ni mazoea na inaruhusiwa.

Wakili: Katika mkataba wa awali kabla mabadiliko hayajafanyika ulikadiria mradi uwe wa gharama kiasi gani?

Shahidi: Dola za Marekani milioni 73.

Wakili: Kama kiasi hicho cha fedha kilitumika chote kwenye mradi, unafikiri kilisababisha hasara?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Nani alikuambia BoT imefanya mabadiliko ya mradi huo?

Shahidi: Nilipata maelekezo kutoka Kampuni ya D&S Ltd.

Wakili: Kwanini BoT ilifanya mabadiliko ya mradi?

Shahidi: Si kazi yangu kujua.

Wakili: Hicho kielelezo ulichokitoa ni ripoti ya mradi mzima?

Shahidi: Mmh! Siyo ripoti ila ni sehemu ya ripoti (watu wakaangua kicheko).

Wakili: Nani alikuambia uandae ripoti ya mradi huo?

Shahidi: Kampuni ya D&S.

Wakili: Lini ulimaliza kazi uliyopewa katika mradi huo?

Shahidi: Mwishoni mwa Februari 2008.

Wakili: Ulipata sababu za kufanyika kwa mabadiliko ya mradi?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Utakubaliana na mimi mabadiliko ya mradi yalitokana na matakwa ya mteja wenu ambaye ni BoT?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Wakati ukifanya kazi hiyo, uliwahi kuwasiliana moja kwa moja na Liyumba?

Shahidi: Hapana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 10 na 24 itakapokuja kwa kutajwa na kuendelea kusikilizwa mfululizo kuanzia Januari 26 – Februari 6 mwakani.

Liyumba anakabiliwa na makosa ya kuidhinisha mradi wa ujenzi wa majengo pacha BoT bila idhini ya bodi ya wakurugenzi, hivyo kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Novemba 27 mwaka 2009

SHAHIDI MWINGINE ABANWA KESI YA LIYUMBA

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa tano wa upande wa mashitaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, ameieleza mahakama kuwa hana kumbukumbu ya idadi ya maombi na kiasi cha fedha za nyongeza kilichokuwa kikiletwa na menejimenti kwenye bodi ya wakurugenzi ili ipate idhini.


Liyumba, anakabiliwa na tuhuma za matumuzi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Shahidi huyo ambaye ni mhadhiri kutoka Idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Dk. Natu Mwamba (48), alitoa amelezo hayo jana wakati akijibu maswali ya jopo la mahakimu wakazi, Edson Mkasimongwa, anayesaidiana na Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa, baada ya kuhojiwa na mawakili wa utetezi na upande wa mashitaka.

“Kwanza, sikumbuki menejimenti ilileta maombi mara ngapi kwenye bodi yetu ya kutaka idhini ya matumizi ya nyongeza ya mradi…vile vile siwezi kukumbuka hayo maombi yaliletwa mara ngapi na menejimenti, pia sikumbuki ni kiasi gani cha fedha kilichokuwa kimeainishwa kwenye maombi hayo.

“Na kuniuliza hilo ni changamoto kubwa kwangu,” alidai Dk. Mwamba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi.

Yafuatayo ni mahojiano kati ya mahakimu wakazi na shahidi huyo:

Hakimu: Ulisema maombi ya nyongeza ya kutaka bodi yenu iyaidhinishe yalikuwa yakiegemea kwenye vikao vya dharura, je, dharura za menejimenti za kuitaka bodi ikutane zilitokea mara ngapi?

Shahidi: Siwezi kukumbuka.

Hakimu: Kwanini hukushtuka? Ni menejimenti iliyoomba vikao vya dharura vya bodi mara kwa mara?

Shahidi: Kwakuwa mwenyekiti wa bodi, yaani gavana, alikuwa ana kofia mbili, yaani pia ndiye aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, naweza kusema alikuwa anatu ‘over power’ wajumbe.

Hakimu: Unaweza kukumbuka bodi ililetewa na menejimenti mara ngapi maombi hayo ya matumizi ya nyongeza ya mradi wa ujenzi wa minara pacha?

Shahidi: Sikumbuki.

Hakimu: Ni kiasi gani kikubwa wewe kilikushtua katika maombi hayo ya matumizi yaliyowasilishwa na menejimenti katika bodi yenu?

Shahidi: Sikumbuki kiasi sahihi, ila ni kama mabilioni.

Hakimu: Hayo malipo ya matumuzi ya nyongeza kabla ya bodi kuyapa idhini, yalikuwa yanapitishwa na nani?

Shahidi: Gavana.

Hakimu: Bodi yenu iliiyaidhinisha malipo hayo?

Shahidi: Tuliyaidhinisha, kwani tulikuwa hatuna jinsi.

Hakimu: Kwa mujibu wa maelezo yako umeieleza mahakama bodi iliyaidhinisha malipo kwa sababu mlikuwa hamridhishwi na utaratibu huo, sasa kwanini hamkufikiria kujiuzulu ujumbe wa bodi?

Shahidi: Mmh! Hilo la kujiuzulu tulilifikiria ila tuliona tumekabidhiwa jukumu la kitaifa, tukashindwa kujiuzulu.

Hakimu: Mahakama imepokea ripoti inayoonyesha imeandikwa na wajumbe wa bodi, je, ieleze mahakama hii ripoti ni ripoti ya bodi?

Shahidi: Hapana siyo ripoti ya bodi, hiyo ripoti tuliandika sisi wajumbe wa bodi wa kuchaguliwa na ambao tulikuwa tunamaliza muda wetu na tuliweka saini zetu, wala haikumhusisha gavana, naibu gavana na Katibu wa Benki, ambao nao hao ni wajumbe wa bodi na wanaingia kwenye bodi hiyo kwa mujibu wa nyadhifa zao katika benki hiyo na tulivyomaliza kuiandika tuliikabidhi kwa bodi mpya.

Kwa hiyo naomba ieleweke hiyo taarifa siyo ya bodi, wala bodi ndogo, ni ya sisi wajumbe wa bodi ambao tulichaguliwa na tulikuwa tunamaliza muda wetu.

Yafuatayo ni mahojiano baina ya mawakili wa utetezi, Hudson Ndusyepo, Jaji mstaafu Hillary Mkate, Onesmo Kyauke na Majura Magafu kwa shahidi huyo:

Wakili: Bajeti ya BoT zilikuwa zinaidhinishwa mara ngapi?

Shahidi: Mara moja.

Wakili: Baada ya bajeti hiyo, kwa mwaka kulikuwa na bajeti nyingine?

Shahidi: Mara nyingine zilikuwa zinakuja bajeti za nyongeza (supplementary bajeti).

Wakili: Umeieleza mahakama mara nyingi menejimenti ilikuwa inaleta maombi kwenye bodi, wakati inakuwa tayari imeishatekeleza nyongeza ya matumuzi?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Aliyekuwa anawasilisha taarifa ya maombi ya matumizi ya nyongeza kwenye bodi ni nani?

Shahidi: Meneja Mradi (Deogratius Kweka), na alikuwa anafanya hivyo baada ya Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Liyumba kuomba idhini kwa mwenyekiti wa bodi ili meneja mradi atoe taarifa hiyo.

Wakili: Taarifa hiyo ya maombi ya nyongeza ilikuwa imetayarishwa na nani?

Shahidi: Menejimenti ya BoT.

Shahidi: Bodi kupitisha ombi la nyongeza ya matumuzi wakati tayari matumizi yameishafanyika ni sahihi?

Shahidi: Kiutaratibu siyo sahihi.

Wakili: Bodi kupitisha ombi la nyongeza ya matumuzi baada ya matumuzi kuwa yameishafanyika kisheria, mnaweza?

Shahidi: Bodi inaweza, ila ni kinyume cha taratibu.

Wakili: Taratibu zipi hizo?

Shahidi: Kimya.

Awali akiongozwa na Wakili wa Serikali, Juma Mzarau, kutoa ushahidi wake, aliiambia mahakama kuwa wajumbe wa bodi walikuwa hawalidhishwi na menejimenti jinsi ilivyokuwa ikiwaletea maombi ya nyongeza ya bajeti wakati tayari matumizi yameishafanyika, lakini bodi haikuwa na jinsi, ikawa inaidhinisha maombi hayo.

Aidha, kiongozi wa jopo, Edson Mkasimongwa, aliahirisha kesi hiyo hadi leo, ambapo shahidi wa sita wa upande wa mashitaka anatarajiwa kuanza kutoa ushahidi wake.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 25 mwaka 2009.