UCHAGUZI MKUU BILA KATIBA MPYA?

Na Happiness Katabazi
UCHAGUZI Mkuu wa nchi ni njia kuu ya kuwashirikisha wananchi katika utawala na uongozi wa nchi.


Taifa lolote lenye uhai wa kisiasa na mategemeo ya kuwa na maendeleo shindani katika jamii ya kimataifa , uupa uchaguzi mkuu kipaumbele na uzito katika siasa na bajeti ya taifa.

Dunia ipo katika uwanja wa mashindano ya maendeleo.Mataifa yanayokimbilia fursa za kujipatia ustawi wa kasi kwa raia wake kuliko mataifa mengine.

Viongozi wa kisiasa wanaotamba duniani ni wale wanaoweza kuziongoza nchi zao kupata maendeleo makubwa na ya kasi kuyashinda mataifa mengine.

Afrika hatumo katika ulimwengu huo na kwa vyovyote vile Tanzania inashikiria nafasi za nyuma kabisa katika kasi ya maendeleo ya nyuma ya dunia.

Nchi zilizo na rasilimali duni kama Rwanda na Burundi ziko mbali kimaendeleo kuizidi nchi yetu .Mataifa yasiyo na rasilimali kama vile dhahabu ,almasi ,Tanzanite kama vile Malawi yako mbele kimaendeleo kuizidi nchi yetu.

Ni wazi kuwa hata kama yangegunduliwa mafuta ya Petroli bado Tanzania ingeendelea ‘kuchapa lapa’ katika umaskini.Kwa vyovyote vile tatizo la nchi yetu si upungufu wa rasilimali bali taifa letu ni fukara sana kiuongozi.

Hiyo ndiyo sababu kubwa ya umaskini wetu.Hatuna viongozi wenye upeo wa kuweza kuliongoza taifa kupata mageuzi ya haraka ya Sayansi na Teknolojia na kupata maendeleo ya haraka kiuchumi na kijamii.

Uchaguzi mkuu ni njia kuu ya Kikatiba ya kujikomboa katika hali kama hii ikiwa kila mwananchi analitambua hilo.

Tunaelewa fika kuwa tumeishaingia katika mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1992 .Na tumekuwa na nafasi ya kubadili serikali mara tatu sasa katika uchaguzi wa mwaka 1995,2000 na 2005.

Oktoba mwaka huu, tutapata tena fursa kwa mara ya nne kubadili uongozi wa nchi kwa njia ya kidemokrasia,kura ya kila mmoja wetu ina maana kubwa katika kuleta mabadiliko tunayoyatamani na kuyazungumzia.

Hakuna kura isiyo na thamani kwa muktadha wa hoja hii.Endapo kila mtanzania mwenye haki ya kupiga kura atapiga kura kwa kudhamilia kubadili uongozi wa nchi hii ili tuongozwe na watu wenye upeo wa kuleta maendeleo.Tutafika.

Endapo kila mwananchi mwenye upeo wa kuliongoza taifa hili kufikia maendeleo ataacha kuwa mbinafsi na badala yake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uogozi ama katika sehemu yake ya kazi akatimiza wajibu wake kikamilifu.Tutafika.

Naandika haya bila kujali kama Mtanzania atakayejitokeza ataamua kuwa mwanachama wa chama gani cha siasa. Kwa vyovyote vile, kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu ni chombo halali cha kutusaidia kupata viongozi makini.

Hakuna chama kinachoweza kudai ndicho chenye leseni ya kuliongoza taifa hili.Na wasii kukubali kubadilika na kukubali mabadiliko kama ambavyo mataifa mengine ufanya.

Wamarekani wamekiondoa chama cha Republican ambacho rais wake alikuwa George Bush.Na kwa mara ya kwanza wakampatia rais mwenye asili ya Kiafrika kupitia chama cha Democraty,Barrak Obama.

Hivi karibuni Waingereza wamekirejesha chama cha maafidhina wa kibepari kiitwacho Consecutive na kumpata Waziri Mkuu mpya aitwaye David Cameroon ambaye ni Waziri Mkuu kijana kwa kipindi cha miaka 200 iliyopita nchini Uingereza.

Siasa zilizomeleta rais Obama Ikulu ni siasa zile zililizo mleta David Cameroon madarakani.Wamarekani na Waingereza walichoshwa na uhafidhina wa kibepari usiojali utu na ustawi wa makabwera na walichoshwa na siasa za vita vyenye lengo la kupora mali asili katika mataifa kama vile Iraq na Afganistan.

Wamarekani na Waingereza walijitathimini wenyewe kama taifa na kuona ustawi wao wa kijamii na kiuchumi ukiporomoka wakati mataifa kama Japan,Taiwan,China na Korea yakisonga mbele kwa kasi ya kutisha.Na jibu la tathimini hiyo walilitoa kupitia uchaguzi mkuu wa nchi zao.

Je watanzania tunajifunza nini katika matukio hayo?Je ni mpaka taifa letu lisambaratike kama Somalia ndipo tuamke na kuanza kujua kwamba taifa limeingia mtoni?.

Hatuwezi ‘kujipiga kifua’ kwa kuwa wenyeji wa mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Duniani (World Economic Forum) wakati mwananchi wa kawaida anaishi kwa pungufu ya mlo mmoja kwa siku.

Hatuwezi kuendelea kuwa na serikali ya viongozi wabadhirifu,walio jaa hila na husuda,wababaishaji kama inavyodaiwa sasa.Kila siku kwenye kashfa zinazoibuka na zile ambazo tunazishuhudia mahakamani.

Ni vyema tujue kwamba kuna mwisho katika kila jambo.Tunaitaji viongozi wapya ambao ni waadilifu na ambao hawatufanyii usanii wa kupeleka kesi mahakamani pale ambapo wanajua moyoni mwao hakuna ushahidi ili tu wajipatie sifa za uadilifu na uchapakazi .

Tunataka viongozi wa kweli kwenye vita ya ufisadi,wizi tuambiwe ukweli.Hatuko tayari kuona watu wasiyonahatia wakibambikiziwa kesi ili kujenga umaarufu wa kipuuzi kwa watu fulani.

Tunataka mabadiliko na mabadiliko hayo yaanzie kwenye Katiba ya nchi.Mabadiliko hayo yaonekane kwenye sheria za nchi.Na mwisho yaonekane kwenye mfumo wa dola letu. Tuache ubabaishaji .Madai haya yamekuwepo kwenye meza ya serikali toka mwaka 1992.

Baadhi ya wananchi walijiunga katika Kamati ya taifa ya Mabadiliko (National Committee for Constitution Reform-NCCR).Madai yao ya mabadiliko ya Katiba ni ya kweli na ni halali hadi leo.

Hayajafanyiwa kazi na badala yake serikali imebobea katika kupeleka viraka na kuvibandika ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.Sheria za nchi zimeendelea kuwa mbaya na zinazoendekeza uonevu ,zinazowanyang’anya wananchi haki na rasilimali zao.

Na kwa kweli taifa letu haliwezi kuendelea chini ya Katiba, sheria na mfumo mbovu wa dola .Navishangaa vyama vya upinzani havigusii tena suala la mabadiliko ya Katiba, sheria na mfumo wa dola.Vinaenda kwenye uchaguzi mkuu kama wasindikizaji huku vikijua wazi Katiba, sheria na mfumo wa dola haurusu uchaguzi huru na wa haki.

Vyama hivi vya upinzani navyo vimeishia kuwa vyama vya kisanii.Vinaendeleza mchezo ule ule na kuimba wimbo ule ule wa Chama cha Mapinduzi(CCM).

Kwa muktadha huu Watanzania tusitegemee maajabu kwani vyama vya upinzani vimesambaratika au vimesambaratishwa,chonganishwa na CCM na baadhi ya viongozi wa vyama hivyo vya upinzani ambao ni mapandikizi, walafi wa madaraka na fedha hali inayosababisha vyama hivyo kuchukiana na kushindwa kuwa na umoja wa ukweli.

Kila kimoja kinajiona ndiyo chama ,kinadharau chama chenzie badala ya kuungana, kushirikiana kwa nia njema na kuleta mageuzi.Sisi tunajua hata vyama vyote vingejifuta kikabaki chama kimoja mfano CHADEMA,NCCR-Mageuzi au CUF bado kisingeweza kushindana na CCM ambacho ni chama dola.

Tatizo la udhahifu wa vyama hivyo vya upinzani umo katika mfumo wa Katiba ,Sheria na mfumo wa dola.Kama vyama vya upinzani havitaki kutambua hilo , navitakia kila la kheri katika ushiriki mwema wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.Hilo ndiyo Fukuto la Jamii.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Mei 30 mwaka 2010

LIYUMBA AKATA RUFAA KORTI KUU

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba(62) ambaye Jumatatu wiki hii, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimhukumu kwenda jela miaka miwili baada ya kumkuta na hatia la kosa la matumuzi mabaya ya ofisi ya umma, jana amekata rasmi rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akipinga hukumu hiyo.


Rufaa hiyo iliwasilisha jana saa tatu asubuhi na kupewa Na.56 ya mwaka huu,katika Mahakama Kuu na mawakili wa mrufani(Liyumba), Majura Magafu, Onesmo Kyauke, Jaji Mstaafu Hillary Mkate na Hudson Ndusyepo.

Kwa mujibu wa rufaa hiyo ambayo gazeti hili imefanikiwa kuiona nakala yake, mrufani ametaja sababu 12 za kukata rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakimu wa Kazi wawili wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa ambao ndiyo waliomtia hatiani mrufani Wakati aliyekuwa kiongozi wa jopo hilo la mahakimu hao wakazi Edson Mkasimongwa alitoa hukumu yake peke yake na akamwachiria huru mrufani na hukumu ya hakimu huyo imeifadhiwa na kwenye kumbukumbu za mahakama hiyo.

Sababu ya kwanza ya kukata rufaa, mrufani anadai mahakama ya Kisutu ilishindwa kuchambua ushahidi uliotolewa mahakamani kikamilifu na matokeo yake jopo hilo la mahakimu wakazi wa tatu likajikuta linatoka na hukumu mbili tofauti.

Sababu ya pili, mrufani anadai kwamba mahakimu hao wawili (Mla ilifanya makosa kwa kushindwa kwake kukubali mabadiliko ya ujenzi wa mradi wa ujenzi wa Minara Pacha yalifanywa baada ya Meneja Mradi huo Deogratius Kweka kuketi kwenye kikao na timu ya wataalamu wa ujenzi na kujadili shughuli za mradi huo,kwani kwa mujibu wa ushahidi uliopo kwenye rekedi za mahakama hauonyeshi Liyumba alikuwa akiudhuria kwenye kikao hicho cha wataalamu wa masuala ya ujenzi wa mradi.

Mrufani katika sababu ya tatu anadai mahakimu hao wakazi wawili(Mlacha na Mwingwa) walifanya makosa kwa kushindwa kwao kukubali kwamba shughuli zote za uendeshaji wa mradi ule zilikuwa chini ya Meneja Mradi Deogratius Kweka ambaye alikuwa akiwajibika moja kwa moja kwa Gavana na si kwa mrufani(Liyumba).

Katika sababu ya nne, mrufani anadai mahakimu hao wawili walifanya makosa kwa uamuzi wao wa kuutupilia mbali ushahidi uliotolewa na Liyumba na shahidi wake ambaye alikuwa Kaimu Katibu wa Benki Kuu, Bosco Kimela kwa maelezo kuwa mashahidi wote walikuwa wakiishi pamoja katika gereza la Keko.

“Sababu ya tano, mahakimu hao walifanya makosa kwa kusema kwamba Liyumba na Kimela ushahidi wao ulikuwa kama hadithi ya kutunga....sisi tunapinga hoja hiyo ya mahakama kwa kusema ushahidi huo haukuwa hadithi ya kutunga.

“Sababu ya sita ni mahakama ya Kisutu ilifanya makosa iliposema malipo ya mradi huo yalikuwa yakiidhinishwa na Liyumba...sisi tunapinga hoja hiyo ya mahakama kwani ni wazi kwa mujibu wa ushahidi uliopo kwenye rekodi ya mahakama hauonyeshi Liyumba alikuwa akiidhinisha malipo ya mradi huo, sasa ushahidi huo hao mahakimu wameupata wapi?alidai mrufani.

Aidha aliitaja sababu ya saba ni kwamba mahakama ya kisutu ilifanya makosa kusema Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ilipoteza mwelekeo na kwamba Liyumba na aliyekuwa Gavana marehemu Daud Balali walikuwa wakiiburuza bodi hiyo.Magafu anadai hoja hiyo ya mahakama ni ya kufikirika na hata ushahidi uliopo kwenye rekodi ya mahakama hauonyeshi mahali popote kwamba bodi hiyo ilikuwa ikiburuzwa na mrufani.

Alidai sababu ya nane ni mahakama hiyo ilifanya makosa kusema idhini za mabadiliko ya ujenzi wa mradi wa Minara Pacha zilitolewa baada ya utekelezaji kufanyika hazikubariki kisheria, wakili huyo anadai kuwa hoja hiyo ya mahakama si ya kweli kwasababu idhini zote zilizokuwa zikitolewa zinaruhusiwa na Kanuni za Fedha za Benki Kuu(BoT Financial Regulation).

“Sababu ya tisa ni kwamba mahakama ya Kisutu ilifanya makosa iliposema mrufani hakuwa na mamlaka ya kusaini zile barua ambazo zilikuwa zimeandikwa na mrufani kwaniaba ya BoT ambazo zilikuwa zikienda kwa mkandarasi ambazo ni kielelezo cha 5-12 na kwamba alifanya hivyo kinyume cha sheria....sisi mawakili wa mrufani tunasema hilo si kweli.

“Sababu ya kumi,mahakama hiyo ilifanya makosa iliposema kwamba mabadiliko ya mradi ambayo yalisababisha ongezeko la gharama katika mradi ule yalikwenda kinyume na matakwa ya bodi na kwamba bodi iliathirika”alidai mrufani.

Sababu ya 11, mrufani anadai mahakama ilikosea kusema kwamba upande wa Jamhuri katika kesi hiyo uliweza kuthibitisha kesi yake bila kuacha mashaka yoyote dhidi ya mrufani, wakili wa Liyumba anadai hilo si kweli kwani ushahidi ule wa upande wa mashtaka umeacha mashaka makubwa.

Aidha sababu ya 12, mrufani anadai mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilifanya makosa kwa kushindwa kwake kufuta taratibu zilizoainishwa kisheria katika kutoa adhabu.

Jumatatu ya wiki hii, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu yaani mahakimu wawili(Mingwa na Mlacha)ilimhukumu mrufani kwenda jela miaka miwili baada ya kumtia hatia kwa kosa la matumuzi mabaya ya ofisi ya umma.Na hadi sasa mrufani anaishi katika Gereza la Ukonga.

Lakini wakati mahakimu hao wakimtia hatiani hakimu mmoja ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa jopo la mahakama hiyo alikataa kumtia hatia mrufani na akamuachiria huru kwasababu alibaini ushahidi wa upande wa mashtaka unaning’inia.

Hali hiyo ya mahakimu kutofautiana na kusababisha kutoa hukumu mbili kulifanya mahakama hiyo kuandika historia mpya ya kesi moja iliyokuwa ikiendeshwa katika mahakama ya hakimu mkazi imekuwa na hukumu mbili tofauti.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Mei 29 mwaka 2010

LIYUMBA AFUNGWA MIAKA MIWILI JELA

*MAHAKIMU WATOFAUTIANA
*HAKIMU MMOJA AMUONA HANA HATIA
*ATOKWA MACHOZI KIZIMBANI

Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana imemuhukumu kwenda jela miaka miwili, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba baada ya kumtia hatiani kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi za umma.

Hata hivyo, mahakama hiyo iliandika historia mpya kwa jopo la mahakimu wakazi, lililokuwa likiongozwa na Edson Mkasimongwa aliyekuwa akisaidiana na Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa, kutoa hukumu mbili zilizotofautiana kimaamuzi.

Kiongozi wa jopo, Mkasimongwa alisema wakati wanaandaa hukumu ya kesi hiyo, walijikuta wanatofautiana kimtazamo. Mlacha na Mwingwa walifikia uamuzi wa kumtia hatiani mshtakiwa, wakati Mkasimongwa alikuwa na mtazamo tofauti wa kumwachia huru.

Alidai baada ya kuupitia ushahidi wa upande wa mashtaka, alibaini unaning’inia na kueleza kuwa hata hukumu itakayotumiwa na mahakama ni ile iliyoandaliwa na mahakimu wenzake wawili na aliyoiandaa yeye itahifadhiwa kwenye kumbukumbu za mahakama.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mlacha alianza kusoma hukumu hiyo iliyochukua saa tatu, ambapo alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi wanane na vielelezo 13 vya upande wa mashitaka na ushahidi uliotolewa na mashahidi wawili wa upande wa utetezi, mahakama hiyo imekubalina na upande wa jamhuri kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Alidai kuwa mahakama iliukataa utetezi uliotolewa na mshitakiwa pamoja na shahidi wake ambaye alikuwa Kaimu Katibu wa BoT, Bosco Kimela kwa sababu ushahidi wao umeonekana ni kama hadithi ya kutunga.

“Jopo hili limeona utetezi wa Liyumba na shahidi wake ni kama hadithi ya kutunga baada ya kuuchunguza, hivyo tunaukataa ushahidi wao, tulipata mashaka kuamini ushahidi wa upande wa utetezi, kwanza Liyumba na Bosco walikuwa wakiishi pamoja gereza la Keko na walikuwa wakikabiliwa na makosa yanayofanana, hivyo mahakama inakubaliana na upande wa mashtaka kwani ushahidi wake ulikuwa ni wa moja kwa moja,” alisema Mlacha.

Akichambua hoja ya Liyumba, aliyodai kwamba aliyekuwa Gavana wa BoT, marehemu Daudi Balali ndiye aliyempa madaraka kwa mdomo ya kusimamia mradi ule, Hakimu Mlacha alisema wameona kuwa taasisi ya BoT ni kubwa na nyeti, hivyo haiwezi kuendeshwa kwa maelekezo ya mdomo.

Kuhusu maelekezo ya barua zilizokuwa zinasainiwa na Liyumba kwenda kwa mkandarasi wa mradi wa majengo pacha, alisema mahakama inaona maelekezo hayo yalikuwa ni kinyume cha sheria kwani bodi ya BoT ndiyo yenye maamuzi ya kuidhinisha chochote kile kifanyike.

Akichambua ushahidi huo, alisema hakuna ubishi kwamba gharama za ongezeko la ujenzi wa mradi ziliongezeka hivyo mabadiliko hayo yalisababisha BoT itumie fedha zaidi, ambazo zingetumika kwa ajili ya shughuli nyingine.

Alisema ushahidi uliotolewa unaonyesha mabadiliko hayo yalikuwa yakifanyika kabla ya kupata idhini ya bodi na kwamba walichobaini bodi hiyo ilikuwa ikiburuzwa na mshtakiwa na marehemu Balali.

Hata hivyo, wakili wa Liyumba, Majura Magafu aliomba mahakama kabla haijafikia uamuzi wa kutoa adhabu izingatie mshitakiwa kuwa ni mgonjwa, na mtu mzima ambaye ana familia inayomtegemea.

“Tulichokibaini katika kesi hii ni kwamba Bodi ya Wakurugenzi ya BoT ilikuwa ikiburuzwa na mshtakiwa na marehemu Gavana Balali... na kwa mujibu wa ushahidi tumeona Liyumba alikuwa na uhuru sana na alikuwa hafuati sheria... hivyo, kwa kuwa nchi hivi sasa ipo kwenye vita dhidi ya wabadhirifu wa fedha za umma na kosa la matumuzi ambalo limeainishwa kwenye kifungu cha 96(1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kifungu hiki hakitaji adhabu sasa mahakama inatumia kifungu 35 cha Sheria ya Adhabu, ambacho kinaipa nguvu mahakama hii kutoa hukumu ama ya fine au kifungo.

“Sasa kwa kuwa Tanzania hivi sasa ipo kwenye vita dhidi ya wabadhirifu wa fedha za umma mahakama hii haitampatia mshitakiwa adhabu ya kulipa faini, hivyo inampatia adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela ili iwe fundisho kwa wengine,” alisema Mlacha huku Liyumba akitokwa na machozi kizimbani na baadhi ya ndugu na watoto wa mshtakiwa kububujikwa na machozi muda wote.

Nao mawakili wa utetezi, Majura Magafu, Onesmo Kyauke na Hudson Ndusyepo waliomba mahakama iwapatie nakala ya hukumu hiyo ili waende kukata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Kwa upande wa Mkasimongwa akisoma hukumu yake mbele ya umati mkubwa uliofurika ndani na nje ya mahakama, alisema yeye anamwachiria huru mshtakiwa kwa sababu ushahidi wa upande wa mashitaka unaning’inia.

Akichambua ushahidi huo alisema hakuna ubishi kwamba Liyumba alikuwa mtumishi wa BoT na barua za maelekezo kuhusu mradi ule zilizokuwa zinakwenda kwa mkandarasi alikuwa akiziandika kwa niaba ya BoT na si yeye binafsi.

Mkasimongwa alisema kwa mujibu wa hati ya mashtaka haionyeshi hayo maamuzi makubwa wanayodai Liyumba aliyafanya yeye binafsi, kwani hakuna barua zilizoletwa zikionyesha zimeandikwa na mshtakiwa binafsi kwenda kwa mkandarasi bali zilizoletwa mahakamani ni barua zinazoonyesha BoT ndiye alikuwa akimwandikia mkandarasi na mshitakiwa akawa anatia saini kwa niaba ya taasisi hiyo na kushindwa kwa jamhuri kuleta barua hizo kunaacha mashaka makubwa.

“Meneja yeyote wa BoT uteuliwa na Gavana hivyo alikuwa akifanyakazi kama anavyoelekezwa na Gavana afanye.Kama alivyoeleza na mashahidi wote kwamba mshtakiwa hakuwa na mamlaka ya kufanya mabiliko hayo na kwamba idhini zote zilitolewa na bodi na hata kama idhini zilitolewa na bodi kabla au baada ya mabadiliko hayo kutekelezwa bado idhini hizo zitakuwa idhini halali kwani zilitolewa na bodi.

“Kwahiyo mtu kusema kwamba Liyumba alivunja sheria kwa kusaini zile barua si kweli kwani Liyumba aliteuliwa na Gavana na haingii akilini kwamba alitenda mambo hayo bila maelekezo ya Gavana na Bodi.Huo ndiyo uamuzi wangu shtaka dhidi yake halijathibitshwa na ninaamuru apewe manufaa yote na ninamwachilia huru”alisema Mkasimongwa huku ndugu na jamaa wakiendelea kububujikwa na machozi na mahakama ikiwa kimya.

Hata hivyo, ilipofika saa tisa alasiri, Wakili Magafu akizungumza na gazeti hili alisema tayari ameishawasilisha kwa maandishi hati ya nia ya kukata rufaa kwa uongozi wa mahakama hiyo na kupeleka nakala katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Januari 27, mwaka huu, Liyumba na Meneja Mradi, Deogratius Kweka walifikishwa mahakamani hapo, wakikabiliwa na makosa mawili ya matumuzi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Lakini, Mei 27 mwaka jana mahakama hiyo iliifuta hati ya mashitaka baada ya kubaini ina dosari za kisheria na ikawaachia washtakiwa ingawa walikamatwa muda mfupi tu na kesho yake Liyumba peke yake ndiye alifikishwa mahakamani akikabiliwa na makosa hayo.

Aprili 9, mwaka huu, mahakama hiyo ilimfutia shitaka la pili la kusababisha hasara na kumfanya abaki na shitaka moja la matumizi mabaya.
Na kwa kipindi chote hicho alikuwa akisota katika gereza la Keko kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka atoe fedha taslimu au kuwasilisha hati ya mali yenye thamani ya sh bilioni 110.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 25 mwaka 2010

MWANZO,MWISHO WA KESI YA LIYUMBA

Na Happiness Katabazi

JANA Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, iliandika historia nyingine ya kushinda baadhi ya kesi za jinai inazozifungua katika mahakama mbalimbali nchini.


Historia hiyo ambayo ni dhahiri imeleta faraja kwenye ofisi hiyo ya DPP ambayo hivi karibuni imekuwa ikisakamwa vikali na jamii kwamba imekuwa haifanyi vyema katika baadhi ya kesi, ni kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kumhukumu kwenda jela miaka miwili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), Amatusi Liyumba (62) aliyekuwa akikabiliwa na kosa la matumizi mabaya ya ofisi ya umma baada ya kumkuta na hatia.

Liyumba alikuwa anatetewa na mawakili wa kujitegemea; Majura Magafu, Jaji Mstaafu Hillar Mkate, Onesmo Kyauke na Hudson Ndusyepo.
Kesi hii imekuwa ikivuta hisia za watu wengi wa kada tofauti.
Ufuatao ni mtiririko mzima wa kesi hii tangu ilipofunguliwa hadi jana ilipomalizika kwa kutolewa hukumu.

Januari 27, 2009:
Liyumba na Kweka walifikishwa kwa mara ya kwanza saa nane mchana mbele ya Hakimu Mkazi Hadija Msongo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, na kusomewa hati ya mashtaka Na.27/2009. Shitaka la kwanza lilikuwa ni matumuzi mabaya ya ofisi ya umma baada ya kufanya upanuzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la minara pacha la Benki Kuu (BoT) bila idhini ya Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo na shtaka la pili ni la kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Hata hivyo, Hakimu Msongo alisema ili washtakiwa wapate dhamna ni lazima kila mmoja atoe fedha taslimu au hati ya mali yenye thamani ya sh bilioni 55, kutotoka nje ya Jiji la Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na kuwasilisha hati ya kusafiria mahakamani. Walishindwa kutimiza masharti hayo.

Februari 17, 2009:
Hakimu Mkazi Msongo alimpatia dhamana iliyozua utata Liyumba peke yake ambaye aliwasilisha hati ya kusafiria iliyoisha muda wake, hati ya nyumba yenye thamani ya sh milioni 800, kinyume kabisa na masharti aliyoyatoa Januari 27. Liyumba alitoka gerezani na kurudi nyumbani kwake huku Kweka akiendelea kusota rumande kwa kushindwa kutumiza masharti ya dhamana.

Februari 20, 2009:
Hakimu Mkazi Msongo, saa nane mchana aliwaita kwa dharura wadhamini wawili wa Liyumba na kuwaeleza kuwa ameifuta dhamana ya mshtakiwa baada ya kubaini kuna dosari, na akatangaza kuufuta uamuzi wake wa kumpatia dhamana. Hata hivyo siku hiyo Liyumba hakuwepo mahakamani kwani haikuwa tarehe ya kesi yake. Hali hiyo ilisababisha wananchi na vyombo vya habari kueneza uvumi kwamba mshitakiwa huyo ametoroka.

Machi 2, 2009: Mawakili wa Liyumba waliwasilisha kwa maandishi ombi mbele ya Hakimu Mkazi Msongo la kutaka mahakama hiyo itumie kifungu cha 225(1-4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai 2002, kinachotamka kuwa, ndani ya siku 60, upelelezi kesi husika uwe umekamilika, vinginevyo ifutwe.

Machi 13, 2009:

Hakimu Mkazi Msongo aliamua kujitoa kwa madai kuwa mwenendo wa kesi hiyo umekuwa ukilalamikiwa na waendesha mashtaka na mawakili kupitia vyombo vya habari.

Machi 20, 2009:
Uongozi wa Mahakama ya Kisutu ulimpangia Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema kusikiliza kesi hiyo ikiwa ni siku chache baada ya hakimu Msongo kujiondoa.

Machi 30, 2009:
Hakimu Mkazi Lema alianza kuiendesha kesi hiyo.

Aprili 2, 2009:
Hakimu Mkazi Lema alisikiliza ombi lililowasilishwa na wakili wa utetezi, Majura Magafu lililoomba mahakama iifute kesi hiyo kwa sababu siku 60 zimepita na jamhuri haijakamilisha upelelezi wa kesi hiyo.

Aprili 23, 2009:
Hakimu Mkazi Lema alitoa uamuzi wa ombi hilo. Alisema baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili, amebaini kuwa licha ya siku 60 kupita na ni kweli upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, haoni kama haki za msingi za washtakiwa zimevunjwa, hivyo akatupilia mbali ombi hilo.

Mei 27, 2009:
Hakimu Lema aliwafutia kesi Liyumba na Kweka baada ya kukubaliana na ombi la mawakili wao kwamba hati ya mashtaka ina dosari za kisheria. Lakini wakati wakifurahia uamuzi huo, walikamatwa tena na makachero wa polisi waliofurika mahakamani hapo, muda mfupi baada ya kuachiwa na kupelekwa katika kituo cha polisi Salender.

Mei 28, 2009:
Saa nane mchana Liyumba alikifishwa peke yake mahakamani hapo na kusomewa hati mpya ya mashtaka na wakili wa serikali, Prosper Mwangamila aliyekuwa anasaidiana na Wakili Kiongozi Justus Mulokozi na John Wabuhanga mbele ya Hakimu Mkazi Nyigumalila Mwaseba ambapo alidai mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Mei 29, 2009:
Hakimu Mwaseba alitoa uamuzi wa kulegeza masharti ya dhamana kwa Liyumba. Alisema ili apate dhamana atatakiwa atoe fedha taslimu au hati ya mali yenye thamani ya sh milioni 300, wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh milioni 50 kila mmoja, kutotoka nje ya Jiji la Dar es Salaam hadi kwa kibali maalum na kusalimisha hati ya kusafiria mahakamani.

Masharti hayo ni tofauti na awali, ambapo masharti ya dhamana yake yaliangukia chini ya kifungu cha 148(5)(e) cha Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, ambayo yanamtaka mshtakiwa atoe nusu ya fedha au hati ya mali yenye thamani ya sh bilioni 110. Upande wa jamhuri haukurizika na uamuzi huo, wakakata rufaa Mahakama Kuu.

Juni 1, 2009:
Jaji Geofrey Shaidi alisikiliza ombi la kupinga kulegezewa masharti dhamana kwa Liyumba lililowasilishwa mbele yake na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi, ambapo kwa mujibu wa ombi hilo, DPP alipinga masharti ya dhamana yaliyotolewa na Mahakama ya Kisutu.

Juni 15, 2009:
Jaji Shaidi alitoa uamuzi kuhusu ombi hilo la DPP na akasema anakubaliana nalo. Akaamuru kuwa mshtakiwa anapaswa apewe dhamana, akatakiwa atoe fedha au hati ya sh bilioni 110. Na akaamuru jalada la kesi hiyo lirudishwe Mahakama ya Kisutu na apangiwe hakimu mwingine. Liyumba alishindwa kutimiza masharti hayo ya dhamana hivyo kulazimika kusota jela hadi jana.

Julai 28, 2009:
Uongozi wa Mahakama ya Kisutu ulimpanga hakimu Eva Nkya kuendelea na kesi hiyo huku ikisuburi Jaji Mkuu Agustino Ramadhani aipangie jopo la mahakimu wakazi kwa ajili ya kuanza kuisikiliza kesi hiyo, na wakili kiongozi wa serikali, Justus Mulokozi aliiambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika.

Agosti 25, 2009:
Hakimu Mkazi Nkya alisema jaji mkuu tayari ameishapanga jopo la mahakimu wakazi kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba litaongozwa na Mkasimongwa atakayesaidiwa na Mlacha na Mwingwa.

Septemba 7, 2009:
Kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya upande wa jamhuri kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa, lakini hata hivyo siku hiyo hakuweza kufika mahakamani kwani alikuwa akiugua gerezani, hivyo usikilizwaji wa awali uliahirishwa.

Septemba 25, 2009: Wakili wa serikali, Mulokozi mbele ya jopo hilo, alimsomea maelezo ya awali mshtakiwa.

Oktoba 1, 2009:
Upande wa jamhuri ulianika orodha ya mashahidi wake 15 na kwamba unakusudia kuleta vielelezo 13.

Oktoba 19, 2009:
Kesi ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa mfululizo hadi Oktoba 23, lakini siku hiyo haikuweza kusikilizwa kwa sababu shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka hakuweza kutokea mahakamani kwa sababu ni mgonjwa, hivyo ikaahirishwa.

Oktoba 22, 2009:
Shahidi wa kwanza ambaye ni mchunguzi kutoka Takukuru, Seif Mohamed (50), aliiambia mahakama kuwa mabadiliko ya upanuzi wa ujenzi wa Minara Pacha (Twin Tower), yaliidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi wa BoT.

Oktoba 23, 2009:
Shahidi wa pili ambaye ni Meneja wa Masuala ya Bodi ya Wakurugenzi wa BoT, Justo Tongola (46), alieleza kuwa hajawahi kuona wala kusikia bodi hiyo ikilalamikia utendaji kazi wa Liyumba.

Novemba 18, 2009:
Shahidi wa tatu ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha BoT, Ruta Angelo (50), aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa huyo hakuwa na uamuzi wa mwisho katika mradi wa ujenzi huo.

Novemba 24, 2009:
Shahidi wa tano ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mjumbe wa bodi ya BoT, Dk. Natu Mwamba (49), alidai kuwa hana kumbukumbu ya idadi ya maombi na kiasi cha fedha za nyongeza kilichokuwa kikiletwa na menejimenti kwenye bodi ya wakurugenzi ili ipatikane idhini.

Novemba 26, 2009:
Shahidi wa saba ambaye ni mkadiriaji wa gharama za majengo, Harold Herbert Webb (78), aliiambia mahakama kuwa hapakuwepo na hasara katika ujenzi wa majengo hayo.
Webb ambaye ni raia wa Uingereza, alidai hapakuwepo hasara yoyote licha ya kuwapo kwa mabadiliko ya ujenzi na kiasi cha fedha kuongezeka kutoka dola dola 357 hadi dola milioni 756. Kiasi chote hicho kilitumika kwenye mradi wa ujenzi huo.

Januari 26, 2010:
Shahidi wa nane ambaye ni Naibu Gavana wa BoT, Juma Reli (54), alisema ameshindwa kuithibitishia mahakama kuhusu hasara iliyopatikana katika mradi huo kwa sababu hadi sasa ripoti ya mwisho ya matumuzi ya fedha za mradi huo haijakamilika. Sambamba na hilo, katika hali isiyotarajiwa, upande wa mashtaka ulisema unakusudia kupunguza idadi ya mashahidi wake kutoka 15.

Machi 15, 2010:
Kesi ilikuja kwa ajili ya mashahidi wa upande wa jamhuri kuendelea kutoa ushahidi, lakini katika hali iliyoshtusha waudhuriaji wa kesi hiyo, Wakili mwandamizi wa serikali, Juma Mzarau aliiambia mahakama kuwa baada ya wao kupitia kwa kina nakala ya mwenendo wa kesi hiyo, ulionyesha ni mashahidi wanane waliotoa ushahidi na vielelezo 13 vilitolewa mahakamani hapo na wamefikia hatua muafaka ya kuifunga kesi yao kwa mujibu wa kifungu cha 231 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Ombi hilo la kuifunga kesi yao lilikubaliwa na mahakama, na Kiongozi wa jopo, Mkasimongwa akatoa amri kwa upande wa utetezi ulete majumuisho yake kwa njia ya maandishi mahakamani Machi 22, upande wa jamhuri nao uwasilishe ya kwao Machi 29, na Aprili 9 mwaka huu, mahakama hiyo itatoa uamuzi wa mshtakiwa huyo ana kesi ya kujibu au la.

Machi 22, 2010:
Mawakili wa Liyumba waliwasilisha majumuisho yao kwa maandishi na wakaiomba mahakama imuone mteja wao hana kesi ya kujibu na imuachilie huru kwa sababu upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi yao.

Machi 29, 2010:
Mawakili wa upande wa jamhuri waliwasilisha majumuisho saa 9:21 alasiri na waliomba mahakama imuone mshtakiwa ana kesi ya kujibu kwa sababu wameweza kuithibitisha kesi yao.

Aprili 9, 2010:
Kiongozi wa jopo, Mkasimongwa kwa niaba ya wenzake alitoa uamuzi wa majumuisho hayo na alimfutia shtaka la pili ambalo ni la kusababisha hasara, na mahakama ikamuona Liyumba ana kesi ya kujibu katika shtaka la kwanza ambalo ni la matumuzi mabaya ya ofisi ya umma.

Aprili 16, 2010:
Mawakili wa Liyumba waliwasilisha mahakamani majina ya mashahidi watano wanaokusudia kuja kumtetea mshtakiwa.

Aprili 22, 2010:
Liyumba alitoa utetezi wake na akadai kuwa serikali haijui itendalo dhidi ya kesi iliyomfungulia. Na akaiomba mahakama izingatie ukweli wakati wa kutoa hukumu dhidi yake Mei 24 (jana) badala ya kuwasikiliza watu wasiojua watendalo.
Maneno hayo mawili ‘hawajui watendalo’ yanafanana na yale aliyotumia Yesu Kristo, anayeaminika kuwa ni mwokozi wa waumini wa Kikristo wakati akieleza kitendo cha Wayahudi waliokuwa wakimsulubisha (Luka 23:34).

Alipomaliza kujitetea alipanda kizimbani shahidi wake ambaye alikuwa Kaimu Katibu wa BoT na Katibu wa Bodi ya benki hiyo ambaye ni mwanasheria kitaaluma, Bosco Kimela (52), aliyeieleza mahakama kuwa shtaka linalomkabili Liyumba hastahili kushtakiwa nalo kwani hajalitenda. Na wakili Magafu akasema kutokana na ushahidi wa mashahidi hao wawili, upande wa utetezi unafunga kesi hiyo.

Hivyo hakimu Mkazi Mkasimongwa akaamuru pande zote mbili Mei 7 mwaka huu, zilete kwa njia ya maandishi majumuisho yao ya kuiomba mahakama imuone mshtakiwa ana hatia au la. Lakini hata hivyo tarehe hiyo ilipofika na kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa wakili wa serikali Ponsian Lukosi alimweleza hakimu mkazi Mkasimongwa kwamba jamhuri imeshindwa kuwasilisha majumuisho yake kwa sababu mahakama haijawapatia mwenendo wa kesi hiyo na hakimu huyo alikubaliana na ombi hilo na kuziongezea pande zote mbili muda ambapo aliziamuru ifikapo Mei 13, mwaka huu, ziwasilishe majumusho hayo.

Mei 13, 2010:
Wakili wa utetezi Onesmo Kyauke aliwasilisha majumuisho yao upande wa utetezi, ambapo waliomba mahakama imuone mshtakiwa hana hatia kwa sababu hakuwa na mamlaka ya kuamua jambo lolote lile katika mradi wa majengo pacha.
Hata hivyo, waandishi wa habari za mahakama kwa jitihada walizozifanya kwa siku mbili mfululizo za kuhakikisha wanapata nakala ya majumuisho ya upande wa jamhuri, hazikuzaa matunda baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa mawakili hao wa upande wa mashtaka ambao wakati kesi hiyo inaendelea mahakamani walikuwa wakitaka ushirikiano na waandishi wa habari za mahakama.

Mei 24, 2010:
Mahakama ya Kisuti ilimtia hatiani Liyumba kwa kosa hilo na kumhukumu kwenda jela miaka miwili.

0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 25 mwaka 2010
Mwanzo, mwisho wa kesi ya Liyumba

Na Happiness Katabazi

JANA Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, iliandika historia nyingine ya kushinda baadhi ya kesi za jinai inazozifungua katika mahakama mbalimbali nchini.
Historia hiyo ambayo ni dhahiri imeleta faraja kwenye ofisi hiyo ya DPP ambayo hivi karibuni imekuwa ikisakamwa vikali na jamii kwamba imekuwa haifanyi vyema katika baadhi ya kesi, ni kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kumhukumu kwenda jela miaka miwili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), Amatusi Liyumba (62) aliyekuwa akikabiliwa na kosa la matumizi mabaya ya ofisi ya umma baada ya kumkuta na hatia.
Liyumba alikuwa anatetewa na mawakili wa kujitegemea; Majura Magafu, Jaji Mstaafu Hillar Mkate, Onesmo Kyauke na Hudson Ndusyepo.
Kesi hii imekuwa ikivuta hisia za watu wengi wa kada tofauti.
Ufuatao ni mtiririko mzima wa kesi hii tangu ilipofunguliwa hadi jana ilipomalizika kwa kutolewa hukumu.

Januari 27, 2009:
Liyumba na Kweka walifikishwa kwa mara ya kwanza saa nane mchana mbele ya Hakimu Mkazi Hadija Msongo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, na kusomewa hati ya mashtaka Na.27/2009. Shitaka la kwanza lilikuwa ni matumuzi mabaya ya ofisi ya umma baada ya kufanya upanuzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la minara pacha la Benki Kuu (BoT) bila idhini ya Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo na shtaka la pili ni la kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.
Hata hivyo, Hakimu Msongo alisema ili washtakiwa wapate dhamna ni lazima kila mmoja atoe fedha taslimu au hati ya mali yenye thamani ya sh bilioni 55, kutotoka nje ya Jiji la Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na kuwasilisha hati ya kusafiria mahakamani. Walishindwa kutimiza masharti hayo.

Februari 17, 2009:
Hakimu Mkazi Msongo alimpatia dhamana iliyozua utata Liyumba peke yake ambaye aliwasilisha hati ya kusafiria iliyoisha muda wake, hati ya nyumba yenye thamani ya sh milioni 800, kinyume kabisa na masharti aliyoyatoa Januari 27. Liyumba alitoka gerezani na kurudi nyumbani kwake huku Kweka akiendelea kusota rumande kwa kushindwa kutumiza masharti ya dhamana.

Februari 20, 2009:
Hakimu Mkazi Msongo, saa nane mchana aliwaita kwa dharura wadhamini wawili wa Liyumba na kuwaeleza kuwa ameifuta dhamana ya mshtakiwa baada ya kubaini kuna dosari, na akatangaza kuufuta uamuzi wake wa kumpatia dhamana. Hata hivyo siku hiyo Liyumba hakuwepo mahakamani kwani haikuwa tarehe ya kesi yake. Hali hiyo ilisababisha wananchi na vyombo vya habari kueneza uvumi kwamba mshitakiwa huyo ametoroka.

Machi 2, 2009:
Mawakili wa Liyumba waliwasilisha kwa maandishi ombi mbele ya Hakimu Mkazi Msongo la kutaka mahakama hiyo itumie kifungu cha 225(1-4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai 2002, kinachotamka kuwa, ndani ya siku 60, upelelezi kesi husika uwe umekamilika, vinginevyo ifutwe.

Machi 13, 2009:
Hakimu Mkazi Msongo aliamua kujitoa kwa madai kuwa mwenendo wa kesi hiyo umekuwa ukilalamikiwa na waendesha mashtaka na mawakili kupitia vyombo vya habari.

Machi 20, 2009:
Uongozi wa Mahakama ya Kisutu ulimpangia Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema kusikiliza kesi hiyo ikiwa ni siku chache baada ya hakimu Msongo kujiondoa.

Machi 30, 2009:
Hakimu Mkazi Lema alianza kuiendesha kesi hiyo.

Aprili 2, 2009:
Hakimu Mkazi Lema alisikiliza ombi lililowasilishwa na wakili wa utetezi, Majura Magafu lililoomba mahakama iifute kesi hiyo kwa sababu siku 60 zimepita na jamhuri haijakamilisha upelelezi wa kesi hiyo.

Aprili 23, 2009:
Hakimu Mkazi Lema alitoa uamuzi wa ombi hilo. Alisema baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili, amebaini kuwa licha ya siku 60 kupita na ni kweli upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, haoni kama haki za msingi za washtakiwa zimevunjwa, hivyo akatupilia mbali ombi hilo.

Mei 27, 2009:
Hakimu Lema aliwafutia kesi Liyumba na Kweka baada ya kukubaliana na ombi la mawakili wao kwamba hati ya mashtaka ina dosari za kisheria. Lakini wakati wakifurahia uamuzi huo, walikamatwa tena na makachero wa polisi waliofurika mahakamani hapo, muda mfupi baada ya kuachiwa na kupelekwa katika kituo cha polisi Salender.

Mei 28, 2009:
Saa nane mchana Liyumba alikifishwa peke yake mahakamani hapo na kusomewa hati mpya ya mashtaka na wakili wa serikali, Prosper Mwangamila aliyekuwa anasaidiana na Wakili Kiongozi Justus Mulokozi na John Wabuhanga mbele ya Hakimu Mkazi Nyigumalila Mwaseba ambapo alidai mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Mei 29, 2009:
Hakimu Mwaseba alitoa uamuzi wa kulegeza masharti ya dhamana kwa Liyumba. Alisema ili apate dhamana atatakiwa atoe fedha taslimu au hati ya mali yenye thamani ya sh milioni 300, wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh milioni 50 kila mmoja, kutotoka nje ya Jiji la Dar es Salaam hadi kwa kibali maalum na kusalimisha hati ya kusafiria mahakamani.
Masharti hayo ni tofauti na awali, ambapo masharti ya dhamana yake yaliangukia chini ya kifungu cha 148(5)(e) cha Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, ambayo yanamtaka mshtakiwa atoe nusu ya fedha au hati ya mali yenye thamani ya sh bilioni 110. Upande wa jamhuri haukurizika na uamuzi huo, wakakata rufaa Mahakama Kuu.

Juni 1, 2009:
Jaji Geofrey Shaidi alisikiliza ombi la kupinga kulegezewa masharti dhamana kwa Liyumba lililowasilishwa mbele yake na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi, ambapo kwa mujibu wa ombi hilo, DPP alipinga masharti ya dhamana yaliyotolewa na Mahakama ya Kisutu.

Juni 15, 2009:
Jaji Shaidi alitoa uamuzi kuhusu ombi hilo la DPP na akasema anakubaliana nalo. Akaamuru kuwa mshtakiwa anapaswa apewe dhamana, akatakiwa atoe fedha au hati ya sh bilioni 110. Na akaamuru jalada la kesi hiyo lirudishwe Mahakama ya Kisutu na apangiwe hakimu mwingine. Liyumba alishindwa kutimiza masharti hayo ya dhamana hivyo kulazimika kusota jela hadi jana.

Julai 28, 2009:
Uongozi wa Mahakama ya Kisutu ulimpanga hakimu Eva Nkya kuendelea na kesi hiyo huku ikisuburi Jaji Mkuu Agustino Ramadhani aipangie jopo la mahakimu wakazi kwa ajili ya kuanza kuisikiliza kesi hiyo, na wakili kiongozi wa serikali, Justus Mulokozi aliiambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika.

Agosti 25, 2009:
Hakimu Mkazi Nkya alisema jaji mkuu tayari ameishapanga jopo la mahakimu wakazi kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba litaongozwa na Mkasimongwa atakayesaidiwa na Mlacha na Mwingwa.

Septemba 7, 2009:
Kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya upande wa jamhuri kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa, lakini hata hivyo siku hiyo hakuweza kufika mahakamani kwani alikuwa akiugua gerezani, hivyo usikilizwaji wa awali uliahirishwa.

Septemba 25, 2009:
Wakili wa serikali, Mulokozi mbele ya jopo hilo, alimsomea maelezo ya awali mshtakiwa.

Oktoba 1, 2009:
Upande wa jamhuri ulianika orodha ya mashahidi wake 15 na kwamba unakusudia kuleta vielelezo 13.

Oktoba 19, 2009:
Kesi ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa mfululizo hadi Oktoba 23, lakini siku hiyo haikuweza kusikilizwa kwa sababu shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka hakuweza kutokea mahakamani kwa sababu ni mgonjwa, hivyo ikaahirishwa.

Oktoba 22, 2009:
Shahidi wa kwanza ambaye ni mchunguzi kutoka Takukuru, Seif Mohamed (50), aliiambia mahakama kuwa mabadiliko ya upanuzi wa ujenzi wa Minara Pacha (Twin Tower), yaliidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi wa BoT.

Oktoba 23, 2009: Shahidi wa pili ambaye ni Meneja wa Masuala ya Bodi ya Wakurugenzi wa BoT, Justo Tongola (46), alieleza kuwa hajawahi kuona wala kusikia bodi hiyo ikilalamikia utendaji kazi wa Liyumba.

Novemba 18, 2009:
Shahidi wa tatu ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha BoT, Ruta Angelo (50), aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa huyo hakuwa na uamuzi wa mwisho katika mradi wa ujenzi huo.

Novemba 24, 2009:
Shahidi wa tano ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mjumbe wa bodi ya BoT, Dk. Natu Mwamba (49), alidai kuwa hana kumbukumbu ya idadi ya maombi na kiasi cha fedha za nyongeza kilichokuwa kikiletwa na menejimenti kwenye bodi ya wakurugenzi ili ipatikane idhini.

Novemba 26, 2009:
Shahidi wa saba ambaye ni mkadiriaji wa gharama za majengo, Harold Herbert Webb (78), aliiambia mahakama kuwa hapakuwepo na hasara katika ujenzi wa majengo hayo.
Webb ambaye ni raia wa Uingereza, alidai hapakuwepo hasara yoyote licha ya kuwapo kwa mabadiliko ya ujenzi na kiasi cha fedha kuongezeka kutoka dola dola 357 hadi dola milioni 756. Kiasi chote hicho kilitumika kwenye mradi wa ujenzi huo.

Januari 26, 2010:
Shahidi wa nane ambaye ni Naibu Gavana wa BoT, Juma Reli (54), alisema ameshindwa kuithibitishia mahakama kuhusu hasara iliyopatikana katika mradi huo kwa sababu hadi sasa ripoti ya mwisho ya matumuzi ya fedha za mradi huo haijakamilika. Sambamba na hilo, katika hali isiyotarajiwa, upande wa mashtaka ulisema unakusudia kupunguza idadi ya mashahidi wake kutoka 15.

Machi 15, 2010:
Kesi ilikuja kwa ajili ya mashahidi wa upande wa jamhuri kuendelea kutoa ushahidi, lakini katika hali iliyoshtusha waudhuriaji wa kesi hiyo, Wakili mwandamizi wa serikali, Juma Mzarau aliiambia mahakama kuwa baada ya wao kupitia kwa kina nakala ya mwenendo wa kesi hiyo, ulionyesha ni mashahidi wanane waliotoa ushahidi na vielelezo 13 vilitolewa mahakamani hapo na wamefikia hatua muafaka ya kuifunga kesi yao kwa mujibu wa kifungu cha 231 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.
Ombi hilo la kuifunga kesi yao lilikubaliwa na mahakama, na Kiongozi wa jopo, Mkasimongwa akatoa amri kwa upande wa utetezi ulete majumuisho yake kwa njia ya maandishi mahakamani Machi 22, upande wa jamhuri nao uwasilishe ya kwao Machi 29, na Aprili 9 mwaka huu, mahakama hiyo itatoa uamuzi wa mshtakiwa huyo ana kesi ya kujibu au la.

Machi 22, 2010:
Mawakili wa Liyumba waliwasilisha majumuisho yao kwa maandishi na wakaiomba mahakama imuone mteja wao hana kesi ya kujibu na imuachilie huru kwa sababu upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi yao.

Machi 29, 2010:
Mawakili wa upande wa jamhuri waliwasilisha majumuisho saa 9:21 alasiri na waliomba mahakama imuone mshtakiwa ana kesi ya kujibu kwa sababu wameweza kuithibitisha kesi yao.

Aprili 9, 2010:
Kiongozi wa jopo, Mkasimongwa kwa niaba ya wenzake alitoa uamuzi wa majumuisho hayo na alimfutia shtaka la pili ambalo ni la kusababisha hasara, na mahakama ikamuona Liyumba ana kesi ya kujibu katika shtaka la kwanza ambalo ni la matumuzi mabaya ya ofisi ya umma.

Aprili 16, 2010:
Mawakili wa Liyumba waliwasilisha mahakamani majina ya mashahidi watano wanaokusudia kuja kumtetea mshtakiwa.

Aprili 22, 2010: Liyumba alitoa utetezi wake na akadai kuwa serikali haijui itendalo dhidi ya kesi iliyomfungulia. Na akaiomba mahakama izingatie ukweli wakati wa kutoa hukumu dhidi yake Mei 24 (jana) badala ya kuwasikiliza watu wasiojua watendalo.

Maneno hayo mawili ‘hawajui watendalo’ yanafanana na yale aliyotumia Yesu Kristo, anayeaminika kuwa ni mwokozi wa waumini wa Kikristo wakati akieleza kitendo cha Wayahudi waliokuwa wakimsulubisha (Luka 23:34).

Alipomaliza kujitetea alipanda kizimbani shahidi wake ambaye alikuwa Kaimu Katibu wa BoT na Katibu wa Bodi ya benki hiyo ambaye ni mwanasheria kitaaluma, Bosco Kimela (52), aliyeieleza mahakama kuwa shtaka linalomkabili Liyumba hastahili kushtakiwa nalo kwani hajalitenda. Na wakili Magafu akasema kutokana na ushahidi wa mashahidi hao wawili, upande wa utetezi unafunga kesi hiyo.
Hivyo hakimu Mkazi Mkasimongwa akaamuru pande zote mbili Mei 7 mwaka huu, zilete kwa njia ya maandishi majumuisho yao ya kuiomba mahakama imuone mshtakiwa ana hatia au la. Lakini hata hivyo tarehe hiyo ilipofika na kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa wakili wa serikali Ponsian Lukosi alimweleza hakimu mkazi Mkasimongwa kwamba jamhuri imeshindwa kuwasilisha majumuisho yake kwa sababu mahakama haijawapatia mwenendo wa kesi hiyo na hakimu huyo alikubaliana na ombi hilo na kuziongezea pande zote mbili muda ambapo aliziamuru ifikapo Mei 13, mwaka huu, ziwasilishe majumusho hayo.

Mei 13, 2010:
Wakili wa utetezi Onesmo Kyauke aliwasilisha majumuisho yao upande wa utetezi, ambapo waliomba mahakama imuone mshtakiwa hana hatia kwa sababu hakuwa na mamlaka ya kuamua jambo lolote lile katika mradi wa majengo pacha.
Hata hivyo, waandishi wa habari za mahakama kwa jitihada walizozifanya kwa siku mbili mfululizo za kuhakikisha wanapata nakala ya majumuisho ya upande wa jamhuri, hazikuzaa matunda baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa mawakili hao wa upande wa mashtaka ambao wakati kesi hiyo inaendelea mahakamani walikuwa wakitaka ushirikiano na waandishi wa habari za mahakama.

Mei 24, 2010:Mahakama ya Kisuti ilimtia hatiani Liyumba kwa kosa hilo na kumhukumu kwenda jela miaka miwili.

0716 774494
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 25 mwaka 2010

KESI YA AMATUS LIYUMBA HATUA KWA HATUA HADI LEO HUKUMU YAKE

Na Happiness Katabazi
KWA mara nyingine tena Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) nchini, chini ya serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete leo (Mei 24 ) itaendelea kuandika historia ya ama kushinda au kushindwa kesi zake za jinai inazozifungua na kuziendesha katika mahakama mbalimbali hapa nchini.


Leo Jopo la Mahakimu Wakazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, linaloongozwa na Edson Mkasimongwa, Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa wanatarajia kukaa kwenye viti vitatu vya enzi na kutoa hukumu kesi Na.105/2009 yenye shtaka moja tu la matumuzi mabaya ya ofisi ya umma kwamba katika kipindi cha mwaka 2001-2004 aliidhinisha mabadiliko ya ongezeko wa mradi wa ujenzi wa minara pacha ‘Twin Tower’bila idhini ya bodi ya wakurugenzi wa BoT,inayomkabili inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba(62), anayetetwa na mawakili wa kujitegemea Jaji Mstaafu Hillary Mkate, Onesmo Kyauke, Majura Magafu na Hudson Ndusyepo.

Kesi hii imekuwa ikivuta hisia za watu wengi wa kada tofauti.Hivyo ungana na mwandishi wa makala hii ambaye ni mwandishi wa habari za mahakamani ambaye aliifuatilia kwa karibu kesi hii tangu ilipofunguliwa hadi leo inatolewa hukumu ili aweze kukupa mtiririko mzima wa kesi hii tangu ilipofunguliwa hadi leo inapomalizika kwa kutolewa hukumu.

Januari 27 mwaka 2009:Liyumba na Meneja mradi wa majengo ya Minara Pacha, Deogratius Kweka walifikishwa kwa mara ya kwanza saa nane mchana mbele ya Hakimu Mkazi Hadija Msongo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, na kusomewa hati ya mashtaka Na.27/2009.Shitaka la kwanza lilikuwa ni matumuzi mabaya ya ofisi ya umma baada ya kufanya upanuzi wa mradi huo bila idhini ya bodi ya Wakurugenzi wa BoT na shtaka la pili ni la kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 221.

Hata hivyo Hakimu Mkazi Msongo siku hiyo alisema ili washtakiwa wapate dhamna ni lazima kila mmoja atoe fedha taslimu au hati ya mali yenye thamani ya sh bilioni 55, kutotoka nje ya jiji bila kibali cha mahakama, kuwasilisha hati ya kusafiria mahakamani.Walishindwa kutimiza masharti hayo siku hiyo.

Februali 17 mwaka 2009: Hakimu Mkazi Msongo alimpatia dhamana iliyozua utata Liyumba peke yake ambaye aliwasilisha hati ya kusafiria iliyoisha muda wake, hati ya nyumba yenye thamani ya Sh milioni 800, kinyume kabisa na masharti aliyoyatoa hakimu huyo huyo Januari 27 mwaka jana.Na Liyumba baada ya kupewa dhamana hiyo alitoka gerezani na kurudi nyumbani kwake huku Kweka akiendelea kusota rumande kwa kushindwa kutumiza masharti ya dhamana.

Februali 20 mwaka 2009: Hakimu Mkazi Msongo , saa nane mchana aliwaita kwa dhalula wadhamini wawili wa Liyumba na kuwaeleza kuwa ameifuta dhamana ya mshitakiwa baada ya kubaini kuna dosari na akatangaza kuufuta uamuzi wake wa kumpatia dhamana Liyumba ambao aliutia Februali 17 mwaka jana.Hata hivyo siku hiyo Liyumba hakuwepo mahakamani kwani siku hiyo haikuwa ni tarehe ya kesi yake.Hali iliyosababisha wananchi na vyombo kueneza uvumi kwamba mshitakiwa huyo ametoroka.

Machi 2 mwaka 2009: Mawakili wa mshitakiwa huyo waliwasilisha kwa maandishi ombi mbele ya Hakimu Mkazi Msongo la kutaka mahakama hiyo itumie kifungu cha 225(1-4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai 2002, kinachotamka kuwa, ndani ya siku 60, upelelezi kesi husika uwe umekamilika, vinginevyo ifutwe

Machi 13 mwaka 2009:Hakimu Mkazi Msongo aliyekuwa anasilikiza kesi hiyo aliamua kujitoa kwa madai kuwa mwenendo wa kesi hiyo umekuwa ukilalamikiwa na waendesha mashtaka na wakili kupitia vyombo vya habari.

Machi 20 mwaka 2009: Uongozi wa Mahakama ya Kisutu, ilimpangia Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema,kusikiliza kesi hiyo ikiwa ni siku chache baada ya hakimu Msongo kujiondoa kwa madai kuwa jamii kupitia vyombo vya habari , imekuwa ikilalamikia dhamana aliyompatia Liyumba..

Machi 30 mwaka 2009:Hakimu Mkazi Lema alianza kuiendesha kesi hiyo.
Aprili 2 mwaka 2009: Hakimu Mkazi Lema amesikiliza ombi lilowasilishwa na wakili wa utetezi Majura Magafu liloiomba mahakama iifute kesi hiyo kwasababu siku 60 zimepita na Jamhuri haijakamilisha upelelezi wa kesi hiyo.

Aprili 23 mwaka 2009: Hakimu Mkazi Lema alitoa uamuzi wa ombi hilo na alisema baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili, amebaini kuwa licha ya siku 60 kupita na ni kweli upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, haona kama haki za msingi za washtakiwa
zimevunjwa, hivyo akatupilia mbali ombi la mawakili wa utetezi lilotaka kesi hiyo ifutwe.

Mei 27 mwaka 2009:Hakimu Lema aliwafutia kesi washtakiwa wote wawili baada ya kukubaliana na ombi la mawakili wa washtakiwa kwamba hati ya mashtaka ina dosari za kisheria.Lakini wakati Liyumba na mwanzeke wakifurahia uamuzi huo, walikamatwa tena na makachero wa polisi waliofurika mahakamani hapo, muda mfupi baada ya kuachiwa na kupelekwa katika kituo cha polisi Salender.

Mei 28 mwaka 2009:Saa nane mchana Liyumba alikifishwa peke yake mahakamani hapo na kusomewa hati mpya ya mashtaka Na.105/2009 na wakili wa serikali Prosper Mwangamila aliyekuwa anasaidiana na Wakili Kiongozi Justus Mulokozi na John Wabuhanga mbele ya hakimu mkazi Nyigumalila Mwaseba ambapo alidai mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya matumuzi na mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 221.

Mei 29 mwaka 2009:Hakimu Mwaseba alitoa uamuzi wa kulegeza masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo.Alisema ili apate dhamana atatakiwa atoe fedha taslimu au hati ya mali yenye thamani ya Sh milioni 300, wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh milioni 50 kila mmoja,kutotoka nje ya jiji hadi kwa kibali maalum na kusaliminisha hati ya kusafiria mahakamani.

Masharti hayo ni tofauti na awali, ambapo masharti ya dhamana yake yaliangukia chini ya kifungu cha 148(5)(e) cha Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, ambayo yanamtaka mshtakiwa atoe nusu ya fedha au hati ya mali yenye thamani ya Sh bilioni 110.Upande wa Jamhuri haukulizika uamuzi huo wamekata rufaa Mahakama Kuu.

Juni 1 mwaka 2009:Jaji Geofrey Shaidi alisikiliza ombi la kupinga kulegezewa masharti dhamana mshtakiwa huyo liliwasilishwa mbele yake na Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP),Eliezer Feleshi dhidi ya Liyumba, ambapo kwa mujibu wa ombi hilo, DPP anapinga masharti ya dhamana yaliyotolewa na Mahakama ya Kisutu.

Juni 15 mwaka 2009:Jaji Shaidi alitoa uamuzi kuhusu ombi hilo la DPP na akasema anakubalina na ombi la DPP la kutaka mahakama hiyo itengue masharti ya hakimu Mwaseba na akaamuru kuwa mshtakiwa anapaswa apewe dhamana yatakayoangukia kwenye kifungu cha 148(5)(e) cha sheria ya Makosa ya jinai ya mwaka 2002 ambao Liyumba alitakiwa atoe fedha au hati ya bilioni 110.Na akaamuru jarada la kesi hiyo lirudishwe Kisutu na apangiwe hakimu mwingine.Na Liyumba alishindwa kutimiza masharti hayo ya dhamana hivyo kulazimika kusota jela hadi leo.

Julai 28 mwaka 2009:Uongozi wa mahakama ya Kisutu ulimpanga hakimu mwingine Eva Nkya kuendelea na kesi hiyo huku ikisiburi Jaji Mkuu Agustino Ramadhani aipangie jopo la mahakimu wakazi kwaajili ya kuanza kuisikiliza kesi hiyo.Na wakili kiongozi wa serikali Justus Mulokozi aliambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Agosti 25 mwaka 2009: Hakimu Mkazi Nkya alisema jaji mkuu tayari ameishawapanga jopo la mahakimu wakazi kwaajili ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba jopo hilo litaongozwa na Mkasimongwa atakayesaidiwa na Mlacha na Mwingwa.

Septemba 7 mwaka 2009: Kesi hiyo ilikuja kwaajili ya upande wa jamhuri kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa lakini hata hivyo mshtakiwa siku hiyo hakuweza kufka mahakamani kwani alikuwa akiugua gerezani,hivyo usikilizwaji wa awali uliarishwa.

Septemba 25 mwaka 2009: Wakili wa serikali Mulokozi mbele ya jopo hilo, alimsomea maelezo ya awali mshtakiwa.

Oktoba 1 mwaka 2009: Upande jamhuri ulianika orodha ya mashahidi wake 15 na kwamba inakusudia kuleta vielelezo 13.

Oktoba 19 mwaka 2009: Kesi ilikuja kwaajili ya kuanza kusikilizwa mfululizo hadi Oktoba 23 ,lakini siku hiyo haikeweza kusikilizwa kwasababu shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka hakuweza kutokea mahakamani kwababu ni mgonjwa hivyo ikaairishwa.

Oktoba 22 mwaka 2009:Shahidi wa kwanza ambaye ni Mchunguzi kutoka(TAKUKURU), Seif Mohamed (50), aliambia mahakama kuwa mabadiliko ya upanuzi wa ujenzi wa Minara Pacha (Twin Tower), yaliidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi wa BoT.

Oktoba 23 mwaka 2009: Shahidi wa pili ambaye ni Meneja wa Masuala ya bodi ya Wakurugenzi wa BoT, Justo Tongola (46),alieleza kuwa hajawahi kuona wala kusikia bodi hiyo ikilalamikia utendaji kazi wa Liyumba.

Novemba 18 mwaka 2009:Shahidi wa tatu ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha BoT, ruta Angelo(50),aliambia mahakama kuwa mshtakiwa huyo hakuwa na uamuzi wa mwisho katika mradi wa ujenzi ‘Twin Tower”.

Novemba 24 mwaka 2009: Shahidi wa tano ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mjumbe wa bodi ya BoT, Dk.Natu Mwamba(49), alidai kuwa hana kumbukumbu ya idadi ya maombi na kiasi cha fedha za nyongeza kilichokuwa kikiletwa na menejimenti kwenye bodi ya wakurugenzi ili ipate idhini.

Novemba 26 mwaka 2009: Shahidi wa saba ambaye ni mkadiliaji wa gharama za majengo,Harold Herbert Webb(78),aliambia mahakama kuwa kuwa hapakuwepo na hasara iiyopatikana katika ujenzi wa majengo pacha katika benki kuu.

Webb ambaye ni raia wa Uingereza, alidai hapakuwepo hasara yoyote licha ya kuwapo kwa mabadiliko ya ujenzi na kiasi cha fedha kuongezeka kutoka dola milioni 73 hadi dola 357,568, kiasi chote hicho kilitumika kwenye mradi wa ujenzi huo.

Januari 26 mwaka 2010:Shahidi wa nane ambaye ni Naibu Gavana wa Benki Kuu (BoT), Juma Reli (54), alisema ameshindwa kuithibitishia mahakama hiyo kuhusu hasara iliyopatikana katika mradi huo kwa sababu hadi sasa ripoti ya mwisho ya matumuzi ya fedha za mradi huo haijakamilika.Sambamba na hilo, katika hali isiyotarajiwa, upande wa mashitaka katika kesi hiyo ulisema unakusudia kupunguza idadi ya mashahidi wake kutoka 15.

Machi 15 mwaka 2010:Kesi ilikuja kwaajili mashahidi wa upande wa Jamhuri kuendelea kutoa ushahidi lakini katika hali iliyoshtusha waudhulaji wa kesi hiyo Wakili mwandamizi wa serikali, Juma Mzarau aliambia mahakama kuwa baada ya wao kupitia kwa kina nakala ya mwenendo wa kesi hiyo ulionyesha ni mashahidi wanane waliotoa ushahidi na vielelezo 13 vilitolewa mahakamani hapo na wamefikia hatua muafaka ya kuifunga kesi yao kwa mujibu wa kifungu cha 231 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Ombi hilo la kuifunga kesi yao lilikubaliwa na mahakama na Kiongozi wa jopo Edson Mkasimongwa akatoa amri kwa upande wa utetezi yake kwa njia ya maandishi mahakamani Machi 22 , upande wa Jamhuri nao uwasilishe majumuisho yake mahakamani Machi 29 na Aprili 9 mwaka huu, mahakama hiyo itatoa uamuzi wa mshtakiwa huyo ana kesi ya kujibu au la.

Machi 22 mwaka huu: Mawakili wa Liyumba wawasilisha majumuisho yao kwa maandishi na wameiomba mhakama imuone mteja wao hana kesi ya kujibu na imuachirie huru kwasababu upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi yao.

Machi 29 mwaka huu: Mawakili wa upande wa jamhuri uliwasilisha majumuisho saa 9:21 alasiri na uliomba mahakama imuone mshtakiwa ana kesi ya kujibu kwasababu wameweza kuithibitisha kesi yao.

Aprili 9 mwaka huu:Kiongozi wa jopo Edson Mkasimongwa kwaniaba ya wenzake alitoa uamuzi wa majumuisho hayo na alimfutia shtaka la pili ambalo ni la kusababisha hasara na mahakama ikamuona Liyumba ana kesi ya kujibu katika shtaka la kwanza ambalo ni la matumuzi mabaya ya ofisi ya umma.

Aprili 16 mwaka huu:Mawakili wa Liyumba waliwasilisha mahakamani majina ya mashahidi watano wanaokusudia kuja kumtetea mshtakiwa.

Aprili 22 mwaka huu: Amatus Liyumba alitoa utetezi wake na akadai kuwa serikali haijui itendalo dhidi ya kesi iliyomfungulia.Na akaiomba mahakama izingatie ukweli wakati wa kutoa hukumu dhidi yake Mei 24 (leo)badala ya kuwasikiliza watu wasiojua watendalo.

Maneno hayo mawili ‘hawajui watendalo’ yanafanana na yale aliyotumia Yesu Kristo, anayeaminika kuwa ni Mwokozi wa waumini wa Kikristo wakati akieleza kitendo cha Wayahudi waliokuwa wakimsulubisha (Luka 23:34).

Alipomaliza kujitetea alipanda kizimbani shahidi wake ambaye alikuwa Kaimu Katibu wa BoT na Katibu wa Bodi ya benki hiyo ambaye ni mwanasheria kitaaluma, Bosco Kimela (52), aliieleza mahakama kuwa shitaka linalomkabili Liyumba hastahili kushtakiwa nalo kwani hajalitenda.Na wakili Magafu akasema kutokana na ushahidi wa mashahidi hao wawili , upande wa utetezi unafunga kesi hayo.

Hivyo hakimu Mkazi Mkasimongwa akaamuru pande zote mbili Mei 7 mwaka huu, zilete kwa njia ya maandishi majumuisho yao ya kuiomba mahakama imuone mshtakiwa ana hati au la.Lakini hata hivyo tarehe hiyo ilipofika na kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa wakili wa serikali Ponsian Lukosi alimweleza hakimu mkazi Mkasimongwa kwamba Jamhuri imeshindwa kuwasilisha majumuisho yake kwasababu mahakama haijawapatia mwenendo wa kesi hiyo na hakimu huyo alikubaliana na ombi hilo na kuziongezea pande zote mbili muda ambapo aliziamuru ifikapo Mei 13 mwaka huu, ziwasilishe majumusho hayo.

Mei 13 mwaka huu: Wakili wa utetezi Onesmo Kyauke aliwasilisha majumuisho yao upande wa utetezi ambapo waliomba mahakama imuone mshtakiwa hna hatia kwasababu hakuwa na mamlaka ya kuamua jambo lolote lile katika mradi wa majengo pacha.

Hata hivyo waandishi wa habari za mahakama kwa jitihada walizozifanya kwa siku mbili mfululizo za kuakikisha wanapata nakala ya majumuisho ya upande wa jamhuri, hazikuzaa matunda baada ya kukosa ushirikiano kutoka kwa mawakili hao wa upande wa mashtaka ambao wakati kesi hiyo inafunguliwa , inaendelea mahakamani walikuwa wakiwaatia ushirikiano waandishi wa habari za mahakama.

Mei 24 mwaka huu:Ambayo ni leo ndiyo mahakama ya kisutu inaitimisha jukumu lake la kisheria la litakalobaki kuwa historia kwa watanzania la kutoa hukumu ya kesi hiyo ambayo ilidumu mahakamani hapo kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi minne sasa.

0716 774494
Chanzo;Gazeti la Tanzania Daima la Jumatatu,Mei 24 mwaka 2010

UTAWALA BORA TANZANIA U WAPI?


Na Happiness Katabazi
WAPENZI wasomaji wa makala zangu napenda kuwaarifu kuwa kuanzia Jumapili ya leo na Jumapili zijazo nitakuwa na safu yangu ambayo itatambulika kwa jina la FUKUTO LA JAMII, hivyo mtakuwa mkizisoma makala zangu kupitia safu hiyo.Karibuni.

Serikali ya awamu ya nne ,imejivika joho la utawala bora .Katika matendo yake ndani na nje ya nchi serikali hii imekuwa ikidai kwamba imebobea katika utawala bora.

Ieleweke wazi kwamba utawala bora siyo tu utawala wa kufuata Katiba na sheria,uwazi na uwajibikaji bali kutenda mambo na kuendesha serikali kwa ufanisi na uweledi unaostahili.

Inapokuwa kwamba sheria inatoa haki au kupiga marufuku jambo fulani , ni wajibu watendaji wa serikali kuakikisha haki hiyo ina wafikia wadau wake.Haki kutowafikia wadau inaweza ikasababishwa na serikali kutowaamasisha wadau kutojua haki zao kwa kutumia elimu ya uraia au serikali kwa chombo kikuu cha uvunjaji wa haki.

Pale ambapo sheria inapiga marufuku jambo fulani lisitendeke , ni wajibu wa serikali kupitia elimu ya uraia kwa kuwaamasisha raia wake wasitende jambo hilo na pia ni wajibu wa serikali kuweka mfumo wa watendaji wenye taaluma na weledi wa kutosha ili kuwawajibisha wakiukaji wa sheria hizo.

Hapa nchini hayo yote hayafanyiki ,serikali haina mfumo wa elimu ya uraia wala haina utaratibu unaofaha wa kuajiri watendani wenye taaluma na weledi wa kutosha.

Kwa hiyo ukienda mahakamani utakutana na waendesha mashtaka wasio na weledi wa kutosha wa kuweza kuandaa hati za mashtaka na kuyawasilisha mahakamani.

Kesi nyingi ushindwa kwasababu baadhi ya waendesha mashtaka wanaanda hati mashtaka vibaya au wameendesha mashtaka vibaya.Katika kesi nyingi mtu wa kawaida ambaye ajasomea sheria anaona wazi mshitakiwa kaonewa au kabambikiwa kesi.Kila mara serikali inaposhindwa kesi katika kesi hiyo ni aibu kwa dola la Jamhuri ya Muungano.

Ukienda mahakamani utakutana na baadhi ya majaji na mahakimu, hao hawatakiwi kabisa kuamua kesi bila shinikizo, upendeleo,wanatakiwa wawe waaminifu na wenye weledi wa kutosha.Lakini huko huko mahakamani tunashuhudia baadhi ya watuhumiwa wakipatikana na hatia pasipo stahili au wahusika kwenye kesi za madai kupoteza haki zao ama kwasababu jaji au hakimu hana utaalamu na weledi wa kutosha au kapokea rushwa.

Lipo jambo linalosikitisha zaidi unaposikia tetesi kwamba katika kesi fulani baadhi ya vigogo wa serikali wametoa maelekezo kwa wakili wa serikali au mahakama kesi iamuliwe kwa misingi ya kulinda maslahi ya serikali au watu fulani badala ya misingi ya haki.

Tunaona wazi mambo hayo yakifanyika, wafanyakazi wakinyimwa haki za ajira kwa kuwa serikali imeagiza maslahi ya wawekezaji yalindwe.Kwa maana hiyo wafanyakazi,wafugaji,wakulima au wananchi kwa ujumla wamepoteza haki zao ama za ajira, maeneo waliyokuwa wakiyamiliki kwa kuwa serikali imeagiza mslahi yalindwe.

Kaumua kesi kwa misingi hiyo ya ‘vimemo’ siyo sawa na kuamua kesi kutokana na vishawishi vya rushwa na inawezekana baadhi ya mahakimu na majaji wanaotenda hivyo wanajua wazi hawatendi haki kwa kuwa tu ni waoga wa kupoteza kazi au wameaidiwa vyeo na marupurupu mengine.

Aina hii ya uendeshaji wa serikali si utawala bora na ni chanzo cha wananchi kukosa imani na mhimili wa mahakama,dhuruma inayoletea wananchi umaskini.

Tumesikia na ni kweli kwamba kunaucheleweshwaji wa kesi wa makusudi wakati mwingine ni wa makusudi jambo ambalo linasababisha kero na umaskini mkubwa.

Wahusika katika kesi za madai na jinai ushindwa kuendeleza shughuli zao kwasababu ama wapo rumande ama mahakama haijaamua kesi husika kwasababu upelelezi haujakamilika au mashahidi hawatokei mahakamani .Yote hayo ukwamisha shughuli zinazowaingizia vipato kwa watu ambao mwisho wasiku mahakama inawaona hawana hatia.

Serikali haina budi kurekebisha ali za wananchi hao auhata kuwafidia hasara waliyoipata maishani mwao.Tayari zipo kesi ambazo zimefuguliwa kwa mbwembwe kama kesi ya EPA,matumizi mabaya ya ofisi ya umma inayomkabili aliyekuwa mkurugenzi wa utumishi na utawala wa Benki, Amatus Liyumba ambayo hukumu yake itatolewa Mei 24 mwaka huu, kesi ya mauji inayomkabili Ramadhani Mussa na mama yake mzazi ambapo Ramadhani anadaiwa kukutwa na kichwa cha mtoto marehemu Salome Yohana iliyopo mahakama ya Kisutu, na kila kukicha waendesha mashtaka wamekuwa wakidai jarada la kesi hiyo lipo kwa DPP hivyo kesi inapigwa kalenda, utafikiri ofisi ya DPP ipo mbinguni ambapo kufika kwake lazima mtu afe kwanza.

Kesi ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma inayomkabili Mkurugenzi wa BoT, Simon Jengo ,Kisima Mkango,Bosco Kimela na Ally Bakari na wenzake wawili, ambapo hata hivyo vigogo hao walifunguliwa kesi ya kusababisha hasara y a Sh bilioni 104 katika Mahakama ya Ilala, Septemba mwaka jana.

Lakini Mei 7 mwaka huu, DPP aliwasilisha hati ya kuifuta kesi hiyo lakini muda mfupi washitakiwa watatu kati ya wanne walikamatwa tena na kufunguliwa kesi nyingine mpya ya matumizi mabaya, na aliyekuwa mshitakiwa watatu Bosco Kimela aliachiriwa huru baada ya DPP kusema hana nia tena ya kumshtaki.Washtakiwa wote watatu wanaendelea kusota rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Utaratibu rufaa katika kesi zilizokwisha amliwa mara zote ni mgumu hasa ule wa kukata toka Mahakama Kuu kwenda Mahakama ya Rufaa nchini.Ilivyo hivi sasa kanuni za uendeshwaji wa rufaa katika mahakama ya rufaa ni za kiufundi mno kuliko za utendaji wa haki.

Mfano hai ni Mahakama Kuu imekuwa ikisoma hukumu yenye tarehe isiyoendana na tarehe ya siku iliposomwa hukumu husika na kwa dosari hiyo tu waombaji rufaa wengi zilizokosewa tarehe , mahakama hiyo ya juu nchini inazitupa na inabidi sasa waombaji wa rufaa waanze upya mchakato wa kupata hukumu na amri yenye tarehe sahihi na na kuwasilisha ombi la kuongezewa muda wa kukata rufaa, zoezi hilo kwa pamoja linaweza likachukua hadi kipindi cha mwaka mmoja.

Je kwa utaratibu huo haki iliyochelewa hivyo ni haki?Na hao waomba rufaa hawatafilisika kweli.?

Mfano wa mahakamani ni mmoja tu katika mifano mingi ambayo tunaweza kutoa katika utendaji wa serikali yetu .Tunachotaka kusema kwamba nchi yetu ina miaka 46 toka ilivyopata uhuru , na nchi yetu inawataalamu wa kutosha.

Ni wakati sasa wa kutathimini utendaji kazi wa serikali yetu,ubora wa sheria zetu, ubora wa mifumo ya utawala na sheria an utendaji haki kwa ujumla ili turekebishe na kujenga upya dola la Kikatiba na Sheria zilizobora.

Mungu ibariki Tanzani, Mungu Ibariki Afrika.

0716 774494:
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili la Mei 23 mwaka 2010

LIYUMBA HANA HATIA-WAKILI

Na Happiness Katabazi

MAWAKILI wa upande wa utetezi katika kesi ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatusi Liyumba umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imuone mteja wao hana hatia kwasababu hakuwa na mamlaka ya kuamua jambo lolote ile katika mradi wa ujenzi wa mradi wa majengo pacha.


Ombi hilo ambalo ni majumuisho kesi hiyo yaliwasilishwa jana saa sita mchana mahakamani hapo kwa njia ya maandishi na mawakili hao Onesmo Kyauke, Majura Magafu na Hudson Ndusyepo na Jaji Mstaafu Hillary Mkate.Kuwasilishwa kwa majumuisho hiyo kunatokana na utekelezaji wa amri iliyotolewa Mei 7 mwaka huu, na Kiongozi wa Jopo la Mahakimu wakazi wanaosikiliza kesi hiyo Edson Mkasimongwa ambaye aliutaka upande wa Jamhuri na utetezi jana uakikishe kila upande unawasilisha majumuisho yao.

Lakini katika hali isiyotarajiwa hadi saa 10:40 jioni waandishi wa habari za mahakamani waliokuwa wameshinda mahakamani hapo tangu saa mbili asubuhi kwaajili ya kufuatilia kesi mbalimbali ikiwemo majumuisho ya kesi hiyo hawakufanikiwa kuwaona mawakili wa serikali wanaondesha kesi hiyo kuwasilisha majumuisho hayo hali iliyowalazimu waandishi hao kwenda ofisini kwa Hakimu Mkuu Mkazi Elvin Mgeta ili waweze kuthibitishiwa kama upande wa Jamhuri umeleta au haujaleta majumuisho hayo, lakini Mgeta ambaye ndiye mkuu wa mahakama hiyo alisema yeye hawezi kuthibitisha kama wameleta au hawajaleta na kuwaomba waandishi wa habari wafike leo asubuhi ofisini kwake atakuwa tayari ana taarifa kamili kuhusu jambo hilo.

Kwa mujibu wa nakala ya majumuisho ya upande utetezi ambapo Tanzania Daima ina nakala yake, wanaiomba mahakama imuone mshtakiwa hana hatia hivyo imuachirie huru kwani Liyumba kama Liyumba hakuwa na mamlaka ya kuamua jambo lolote kuhusu mradi huo kwani mradi ulikuwa ukiratibiwa na Meneja Mradi Deogratius Kweka ambaye ndiye alikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na Gavana Daud Balali kuhusu masuala yanayohusu mradi ule.

“Liyumba kazi yake ilikua nikuakikisha ule mradi hauwezi kukosa vitu kama usafiri, steshenali na maitaji mengine muhimu...na kwamba mshitakiwa alikuwa anawajibika kujibu barua zilizokuwa zinatoka kwa mkandarasi zinazohusu mradi kama alivyokuwa akielekezwa kuzijibu barua hizo na Gavana baada ya Gavana kuwa ameishajadiliana na Meneja Mradi;

“Kwani Meneja Mradi ndiye aliyekuwa anakaa na wakandarasi na wanajadiliana nini kifanyike na kisha Meneja Mradi anapeleka mapendekezo hayo kwa Gavana na kisha gavana anatoa maamuzi ...hivyo Liyumba hausiki kabisa na kosa hili la matumuzi mabaya ya ofisi ya umma ambalo upande wa Jamhuri umedai alijichukulia madaraka bila idhini ya bodi ya wakurugenzi kwa kufanya mabadiliko ya ongezeko za mradi wa ujenzi huo”alidai Wakili Onesmo Kyauke.

Hakimu Mkazi Edson Mkasimongwa anayesaidiana na Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa Mei 24 mwaka huu, watatoa hukumu ya kesi hii ambayo inavuta hisia za wanchi wengi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Mei 14 mwaka 2010

MKURUGENZI BoT AFUTIWA KESI

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam,imemuachiria huru aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Benki Kuu(BoT), Bosco Kimela aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 104 ambaye amesota rumande kwa miezi nane sasa kwaajili ya kesi hiyo.


Mbali na Kimela aliyekuwa akikabiliwa na kesi hiyo washtakiwa wengine ni Mkurugenzi wa BoT,Simon Jengo, Naibu Mkurugenzi wa Fedha za Nje, Kisima Mkango, Kaimu Mkurugenzi na Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki , Ally Bakari.Ambao nao walifutiwa kesi hiyo ila baada ya muda mfupi washtakiwa hao watatu walikamatwa na kufunguliwa kesi mpya ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma.

Uamuzi huo wa kumuachilia huru Kimela ulitolewa mwishoni mwa wiki na Hakimu Mfawidhi ,Joyce Minde ambapo alisema amefikia uamuzi wa kumuachiria huru mshitakiwa huyo kwasababu Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Eliezer Feleshi aliwasilisha mahakamani hapo hati ya kumfutia kesi hiyo hivyo mahakama hiyo inamuachiria huru.

“DPP amewasilisha hati ya kumfutia kesi Kimela peke yake hivyo mahakama hiyo haina pingamizi na hati hiyo ya DPP hivyo inamwachiria huru mshitakiwa wa tatu, Bosco Kimela “alisema Hakimu Mfawidhi Minde.

Septemba mwaka jana, washitakiwa hao walifunguliwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka manne matumuzi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ambapo kosa la kwanza walilifanya mwaka 2004, walichapisha noti zenye thamani y ash milioni 500.Shitaka la pili linafanana la kwanza ambapo wanadaiwa kutumia nyaraka hizo kumdanganya mwajiri ili aweze kuongeza gharama za uchaopishaji wa noti zenye thamani hiyo kwa mwaka 2005.

Aidha ,wakili alidai shtaka la tatu, ni la kutumia madaraka yao vibaya, ambapo watuhumiwa hao kwa pamoja wakiwa na nafasi zao, waliongeza gharama za uchapishaji wa noti zenye thamani ya Sh bilioni 1.4 mwaka 2007.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Mei 9 mwaka 2010

TUCTA ,KAMA MGOMO NI HALALI KWANINI MMEUSITISHA?

Na Happiness Katabazi

BABA wa Taifa mwalimu Julias Nyerere aliwahi kusema kwamba; “Ukweli unatabia moja nzuri sana ,kwani haubagui rafiki wala adui”.

Leo nimelazimika kutumia nukuu hiyo ya muhasisi wa tiafa letu kwani naamini kabisa nukuu hiyo itasaidia kuunga mkono makala yangu ambayo itajadili azimio la TUCTA liloitisha mgomo usiokuwa na kikomo kwa wafanyakazi wote nchini waliokuwa wamepanga uanze Mei 5 mwaka huu, tena kwa tambo kali, hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati akizungumza na wazee wa Dar es salaam, hiv karbuni ambapo alitoa msimamo wa serikali yake kuhusu azimio hilo , na pia nitajadili uamuzi wa Tucta wa kusitisha mgomo walioutoa jumanne wiki hii ikiwa ni siku moja baada rais kikwete kutangaza msimamo wa serikali kuhusu azimio hilo.

Kwa zaidi ya kipindi cha mwezi mmoja sasa TUCTA imekua ikitaja sababu nyingi zinazosababisha wao watangaze mgomo ‘shindwa’ kwenye vyombo vya habari hivyo sioni sababu ya kuzirudia rudia katika makala hii ila sababu moja wapo walikuwa wakiishinikiza serikali iwaongezee mshahara watumishi wake hadi kufikia kiasi cha sh 315,000.

Itakumbukwa na watanzania wote waliokuwa wakifuatilia sakata hilo, TUCTA ilikuwa ikijinasbu kupitia vyombo vya habari kwamba mgomo waliouandaa una baraka zote za kisheria na kwamba hakuna kiongozi yeyote wa serikali ambaye angeweza kuwazuia kugoma.

Kwa kauli hiyo ya TUCTA ambayo hadi sasa hawajaikana, nadiriki kuwaita TUCTA walikuwa hawajajiandaa kikamilifu na mgomo , mipango yao ilikuwa ni ya kiubabaishaji na kinafiki pasipo na mfano kwani ilikuwa ikijua wazi kauli hiyo ilikuwa imefurika uongo ,yakizandiki, na ya kuwahaada wafanyakazi wasio na upeo wa kuchambua mambo na walikuwa wakijua fika walikuwa wakivunja sheria za nchi ila walichokuwa wanakifanya ni kutikisa kibiriti.

Wamekuta njiti zimejaa kwenye kibiriti.Rais Kikwete ni namba saba agawanyiki.Viongozi wa TUCTA walitaka kumgeuza Kikwete babu yao kumbe wamekuta bado wamo. Na endapo TUCTA itakana tuhuma hizo hapo juu, basi ijitokeze hadharani na iseme ni kwani imesitisha azimio lake na mgomo siku moja baada ya rais Kikwete kutoa msimamo wa serkali yake, kwani sote tuna fahamu si Rais wetu wala mwananchi yeyote yule hayupo juu ya sheria.

Sote tuliisikia TUCTA ikijitapa kuwa mgomo wao upo halali kisheria ,ni kwanini imeshindwa kuendeleza msimamo wao wa mgomo kama si unafki, uzandiki na inataka kuleta mvurugano kwenye taifa letu ambapo kwani uchumi wa taifa letu utasambaratika.?

Kwasababu hakuna mtu aliye juu ya sheria , hivyo kamwe Rais hawezi kuzuia maamuzi yao ambayo walidai ni halali mbele ya sheria,sasa TUCTA itueleze ni kwanini wamesitisha mgomo wao wakati mgomo wao walidai upo halali kisheria kama walivyokuwa wakijinasibu?

Endapo itajitetea kuwa wameamua kuairisha mgomo kwasababu hawataki kubishana na rais au wanamstahi rais la nchi.Swali je wakati wote iivyokuwa ikiandaa mgomo ilikuwa ikifikiri kiongozi huyo wa nchi na wasaidizi wake watanyamaza kimya?

Na ikiwa endapo sababu iliyosababisha TUCTA kusitisha mgomo wao ghafla ni kuogopa msimamo wa serikali uliotolewa na rais kikwete mapema wiki hii, kwamba hawezi kuongeza mshahara kwa kiasi hicho na asiyetaka kazi aache na atakayegoma atakutana na mkono wa dola,basi kuanzia sasa nadiriki kuita TUCTA ni chui wa karatasi.

Ni TUCTA hii kwa nguvu zote wamejitahidi kuuaminisha umma wa wafanyakazi wa serikali kwamba ifikapo Mei 5 mwaka huu,watagoma na baadhi ya wafanyakazi ambao ni bendera fuata upepo wasiyofahamu kuwa viongozi wa jumuiya hiyo hawana ujasiri wa kupambana na dola mwisho ,waliwaamini msimamo huo wa viongozi wao.

Tuwaulize hawa viongozi wa taifa wa TUCTA ,Kaimu Katibu Mkuu, Nicholas Mgaya na Rais wa TUCTA, Omary Ayoub,ambao ndiyo walikuwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha mgomo ‘shindwa’unafanikiwa , hawaoni kwamba kwa ubabaishaji wao katika uandaaji wa suala nyeti kama mgomo wafanyakazi na mgomo huo ukashindwa kufanyika kwa maelezo ambayo hayana kichwa wa miguu,na kuudanganya kwao umma kwamba vikao vya vya serikali vimeshindwa kuafikiana huku wakati ikijua Mei 8 mwaka huu, TUCTA ilikuwa imekubali kuudhulia mkutano wa majadiliano na serikali ambayo wameiituhumu haijali maslahi ya wafanyakazi na kwakuwa tucta walimeishaituhumu hivyo serikali ni kwanini inakubali tena kwenda kufanya mazungumzo na serikali isiyowajali?

Kama hili la kuandaa mgomo usiokoma limewashinda TUCTA , watanzania na vyombo vya ulinzi na usalama kwani tusiwe na hofu na shirikisho hilo kwamba kwa ubabaishaji wake wa kuandaa mambo mbalimbali yanayohusu wafanyakazi wa umma ,hatuoni ipo siku wanaweza kulipeleka taifa kuzimu?

Na wakilishalipeka taifa kuzimu, mwisho wa siku watakaoathirika moja kwa moja na haraka zaidi ni watoto,wanawake, wazee na wagonjwa ambao wamelazwa tayari mahospitalini na wagonjwa watarajiwa kwani ni wazi wasingepata huduma ya matibabu kwasababu wauguzi wangedai wapo kwenye mgomo,wanafunzi mashuleni na vyuoni wangekosa kufundishwa na walimwa na taifa kwa ujumla lingepata hasara.

Wanajeshi wa wapo vitani mkuu wa Majeshi huwa aendi vitani bali uteua mabrigedia jenerali kuongoza brigedi tofauti vitani.Hivyo inapobainika kiongozi wa brigedi vitani hana msimamo katika kupiganisha vita, mara moja kiongozi huyo hurudishwa nyuma na nafasi yake inachukuliwa na mmoja wa wafuasi wake na unyanganywa silaha na hurudisha nyuma na na nafasi yake uchukuliwa na mwanajeshi mwingine na kisha kiongozi huyo ambaye alionesha kutokuwa na msimamo uchukuliwa hatua na yule aliyepewa jukumu la kushika nafasi ya kiongozi huyo, huendelea na jukumu la kupiganisha vita.

Sasa kwa mtindo huo unaotumiwa na wanajeshi wote duniani wakati wa wapo vita, ni wazi kabisa mtindo huo leo hii ungetumiwa na wanachama wa TUCTA ni wazi wange wanyang’anya madaraka viongozi wao kwasababu wameonekana hawana msimamo katika kupiganisha vita ‘harakati’ya kudai kuboreshewa maslahi ya wafanyakazi wa umma.

Kwa sababu viongozi wa TUCTA wamekuwa ni chui wa karatasi , kwani kwa kipindi chote hicho wametumia muda wa serikali kuketi katika vikao vyao vya kujadili masuala ambayo hatimaye wameshindwa kuyatekeleza kama walivyoadi, na katika kuketi katika vikao hivyo lazima walilipana posho ambazo ni uenda ni michango ya wanachama, walijaza mafuta kwenye magari kwaajili ya usafili wa kuudhulia vikao hivyo ambapo,sasa wanayakazi wa umma ni kwanini wasianze kuhoji matumuzi hayo ya vikao hivyo ambavyo maazimio yake viongozi hao wameshinmdwa kutekeleza ni kwanini wasiwalazimishe viongozi hao walipe gharama zote walizotumia kuendesha vikao hivyo ambavyo havijazaa matunda waliyohahidiwa?

TUCTA imekuwa ikivuma wakati inapofika wakati wa kudai kuboreshewa maslahi yao, lakini TUCTA hatuisiki kabisa ikitoa ripoti kwa umma kwamba imeweza kushirikiana kikamilifu na waajiri kuwachukulia hatua wafanyakazi wazembe, watoro na wakosefu wa nidhamu makazi au kutoa matamko ya kuwaasa wafanyakazi wake wafanyakazi kwa bidii ili ili kuongeza tija kwa taifa.

Hivi si ni wafanyakazi hawa hawa wa umma ndiyo nao waliochangia kwa kiasi kikubwa kwa marais wetu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kukubali kuruhusu sera ya uwekezaji nchini, kwasababu viongozi hao walishabaini wazi kwamba baadhi ya wafanyakazi wa umma wamechangia kuyaua mashirika ya umma kama KAMATA, UDA na ATC kwa kushindwa kuzalisha kikamilifu na wakati makampuni hayo ya umma yalikuwepo, hakukuwa na makampuni mengine shindani lakini wafanyakazi hao walishindwa kuyaendeleza na matokeo yake yakafa kifo cha mende.

Leo hii tunawashuhudia watanzania wakijitumbukiza kwenye biashara ya huduma za usafirishaji (daladala) na wamekuwa wakipata faida na kila kukicha wamekuwa wakiagiza daladala nyingi mitaani kwaaji ya kuuendelea kutoa huduma hiyo ambayo inatumiwa na wananchi wengi.

Na wamikili wa magari hayo wamekuwa wakiwalipa ujira mdogo makonda na madereva wa magari hayo.Itakumbukwa enzi mashirika ya umma ya UDA,wafanyakazi waliokuwa wakifanyakazi kwenye mashirika hayo walikuwa wakilipwa mishahana usalama wa ajira zao na mishahara ya uhakika lakini walishindwa kuliendesha shirika hilo .

Kwahiyo wafanyakazi wa umma mnapodai kuboreshewa maslahi yenu haraka lazima mjiulize mara mbili kwenye nafsi zenu kama nyie wenyewe kwanza mnatimiza wajibu wenu ipasavyo na utendaji wenu huo unaliletea taifa tija ipasavyo?Maana msiwe mstari wa mbele kulalamikia kuboreshewa maslahi yenu wakati miongoni mwenu hamtimizi wajibu wenu kikamilifu.

Kwani siyo siri kuna wafanyakazi wa umma wanaenda ofisini siku wanazojisikia wao na ndiyo wamekuwa mabingwa kughushi ruhusa fupi za mapuziko ya ugonjwa(ED) zinazoonyesha zimetolewa na madaktari wa hospitali,au wakiingia ofisini basi hawakai ofisini hadi muda wa mwisho wa serikali unamtaka mfanyakazi wa umma atoke ofisini, au akiwahi ofisini basi muda mwingi atautumia kufanya mambo yake binafsi tena kwa kutumia rasilimali za serikali kama simu, nukushi, internate, printer au wakati mwingine wanaamua kupiga soga,na wengine wanajibu wagonjwa kuwa dawa hazipo katika hospitali na baada ya kumtolea kauli hiyo umvuta pembeni mgonjwa huyo na kumwambia kama atampa fedha ya chai anaweza kumpatia dawa hiyo ambayo ataitoa hapo hospitalini.

Na ninapenda kuishauri TUCTA ikipata wasaa ikaisome vyema ibara ya 37(1) ya Katiba ya Nchi , inasema “Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakapewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushahuri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote’.

Na hapo ndipo nipomweleza rais Kikwete kwamba uzi ni ule ule uliouonyesha Jumatatu wiki hii wakati akizungumza na wazee hapa jijini.Na ninamtaka atambue kuwa kushindwa kwake kutoa kukemea na kuwachukulia hatua katika matukio mbalimbali ambayo yanalihusu taifa hili toka alipoingia madarakani naweza kusema ndiko hasa kulikosababisha miongoni mwetu tuanze kuamini Tanzania ina ombwe la uongozi kwasababu ya rais aliyepo maradakani uenda ameshindwa kutumia vyema madaraka yake yaliyopewa katika Sura ya pili ya Ibara ya 33-46 B za Katiba ya Jamhuru ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Hisia kali ulizozionyesha siku hiyo zimedhiirisha kwamba kaya ya Tanzania ina mwanamme(rais) na hivyo ndivyo mwanamme ndani ya nyumba anavyopaswa aonyeshe kuwa mwanamme ambaye ndiyo kichwa cha familia.Kwani hapa nchini hivi sasa ilifika mahali hajulikani rais ni nani kwani kila mtu anaropoka anachoweza kuropoka hata kama anazungumza uongo hakuna wakumchukulia hatua.

Kwa sisi tunaotamani nchi yetu izidi kupiga hatua za kimaendeleo tungependa kumuona kiongozi wa nchi akiwa mkali kuwachukulia hatua kwa wafanyakazi au mwananchi yeyote anayetaka kurudisha nyuma jitihada za kuliletea tiafa letu maendeleo.

Ieleweke kuwa huu si wakati wa rais wetu kuendelea kuwaonea haya watendaji wa serikalini ,wabunge wake na mawaziri ambao miongoni mwao wana hulka za kinyang’au,wababaishaji,ambao siku za hivi karibuni wamekuwa vinara wa kuvujisha kwenye vyombo vya habari siri za vikao vya chama tawala na baraza la mawaziri, na kumgeuza rais kama ‘ mwanasesere’ katika masuala mbalimbali mfano Sheria ya Gharama za Uchaguzi, kumkabidhi hundi zilizokosewa tarakimu, kumpatia taarifa za uongo ambazo mwisho wa siku mzigo wa fedhea una muungukia kiongozi huyo wa nchi.

Mwisho na waasa wafanyakazi wa umma wasiwe kama vifurushi vinavyobebwa kwenye mifuko laini (Rambo)maana vifurushi hivyo huwa havijui vinapelekwa wapi.

Mungu Ibariki Tanzania ,Mungu ibariki Afrika

0716 774494

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne Mei 11 mwaka 2010

WAZIRI DAFTARI ASHINDA KESI

Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemfutia kesi ya madai ya kashfa iliyokuwa ikimkabili Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Dk.Maua Daftari kwasababu hati ya madai ina dosari za kisheria.


Uamuzi huo umetolewa na Jaji Agustine Mwarija ambapo alisema amefikia uamuzi wa kuifuta kesi hiyo kwasababu amekubaliana na pingamizi la awali lilowasilishwa mbele yake na wakili wa mdaiwa, Peter Swai liloiomba mahakama hiyo iifute kesi hiyo kwasababu mlalamikaji kupitia hati yake ya madai ameshindwa kuonyesha maneno ya nini alichokuwa akikilalamikia.

“ Mahakama imepitia kwa kina hoja za pande zote mbili na linakubaliana na pingamizi la wakili wa utetezi Peter Swai kwamba hati ya madai ina dosari za kisheria kwa mujibu wa hati hiyo ya mlalamikaji hajataja sababu ya kufungua kesi hiyo na na kwa mujibu Kanuni 11(a) amri ya VII ya Sheria ya Madai ya mwaka 2002 inamtaka mlalamikaji ataje sababu za kufungua kesi;

“Na kwa mujibu Amri ya VII Kanuni 11(a) ya Sheria ya Madai ya mwaka 2002 inaipa mahakama mamlaka ya kuifuta hati ya madai ambayo mamlalamikaji ajataja sababu ya kulalamika….na kwa mamlaka hayo niliyopewa na kanuni hiyo, naifutilia mbali hati ya madai kwasababu nimebaini ina dosari za kisheria na niaamuru mlalamikaji alimpe mdaiwa(Dk.Daftari)gharama zote alizozitumia kwaajili ya kuendesha kesi hiyo”alisema Jaji Mwarija.

Kesi hiyo ya madai Na.34 ya mwaka 2008 ilifunguliwa mahakamani hapo na mlalamikaji Fatma Salmin ambaye kwa mujibu hati hiyo ya madai iliyofutwa, alikuwa akidai kuwa mdaiwa ambaye ni Dk.Maua Daftari Novemba 14 mwaka 2007 katika ofisi za Bunge mjini Dodoma ,muda mfupi baada ya kupokea taarifa toka kwa wakili wake Peter Swai ambaye ofisi zake zipo Dar es Salaam, alizungumza na waandishi wa habari ambapo alikuwa akipinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, dhidi yake katika kesi nyingine ya madai Na.21 ya mwaka 1999 iliyofunguliwa na mlalamikaji Fatma Salim ambapo mahakama ilimtaka naibu waziri huyo alimpe fidia ya Sh milioni 100.

Kwa mujibu wa hati hiyo Salmin alidai kuwa mdaiwa(Dk.Daftari) siku hiyo alikuwa akihoji uhalali wa hukumu hiyo ile ya Mahakama Kuu katika kesi hiyo Na.21 ya mwaka 1999, na kwamba wakati akihoji alimuita yeye ni ‘tapeli mkubwa’na kuuongeza kuwa tamshi hilo limemletea limemshushia hadhi kwenye jamii na kumfanya onekane siyo mwaminifu hivyo akaomba mdaiwa amuliwe kumlipa sh milioni 500.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 11 mwaka 2010

VIGOGO BoT WAACHIWA,WAKAMATWA

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, jana iliwafutia mashtaka ya uhujumu uchumi yaliyokuwa yakiwakabili wakurugenzi wanne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Licha ya kuwafutia mashtaka, wakurugenzi hao walijikuta wakikamatwa tena baada ya kutuhumiwa mashtaka matatu ya matumizi mabaya ya ofisi za umma.

Washtakiwa hao ni Mkurungezi wa BoT, Simon Jengo, Naibu Mkurugenzi wa Fedha za Nje, Kisima Mkango, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kitengo cha Sheria, Bosco Kimela, na Mkurugenzi wa Huduma za Benki, Ally Bakari, waliondolewa jalada lao baada ya
mahakama kupokea ombi lililowasilishwa na Mkuregenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Agnes Mchome, wakili wa Serikali, Sedekia, alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa ya matumizi mabaya ya ofisi za umma wakiwa waajiriwa BoT.

Wakili Sedekia, alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu, ambapo kosa la kwanza walilifanya 2004, kwa kuchapisha noti zenye thamani ya sh milioni 500.

Wakili Sedekia, alidai shtaka la pili linafanana na la kwanza ambapo wanadaiwa kutumia nyaraka hizo kumdanganya mwajiri wao ili aweze kuongeza gharama za uchapishaji wa noti zenye thamani hiyo mwaka 2005.

Aidha, wakili alidai shtaka la tatu ni la kutumia madaraka yao vibaya, ambapo watuhumiwa hao kwa pamoja wakiwa na nafasi zao, waliongeza gharama za uchapishaji wa noti zenye thamani ya sh bilioni 1.4 mwaka 2007.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Mei 8 mwaka 2010

SIMBA KUCHAGUANA LEO

.KORTI KUU YABATILISHA AMRI YA KISUTU

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana jioni ilibatilisha amri ya muda ya kuzuia uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba unaofanyika leo ambayo ilitolewa Alhamisi wiki hii na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kubaini dosari katika amri hiyo.


Amri hiyo ilitolewa jana saa 1:10 jioni na Jaji Agustine Mwarija baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili zilizokuwa zinavutana katika kesi iliyokuwa imefunguliwa na Michael Wambura dhidi ya mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan Dalali, kuruhusu uchaguzi huo kuingiliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Jaji Mwarija ametoa uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za walalamikaji Othuman Hassan ‘Hassanoo’ na Aden Rage ambao ni wagombea wa nafasi ya uenyekiti katika uchaguzi huo waliokuwa wakitetewa na mawakili wa kujitegemea, Richard Rweyongeza na Peter Swai, dhidi ya Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali, aliyekuwa akitetewa na wakili Majura Magafu na Wambura ambaye hakuwa na wakili.

Baada ya Jaji Mwarija kusikiliza hoja za pande zote kwa zaidi ya saa mbili mfululizo, aliahirisha shtaka hilo kwa muda ili kuandaa uamuzi kabla ya kurejea saa 1 usiku na kutoa uamuzi wake.

Akisoma uamuzi huo ambao ulichukua dakika zisizozidi tano na bila kuchambua, alisema amebaini mwenendo wa kesi iliyofunguliwa Kisutu ambayo ilisababisha hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Aniceth Wambura, kutoa amri ya muda ya kusitishwa kwa uchaguzi huo, ulikuwa batili.

“Nimepitia kwa kina hoja za pande zote mbili, mahakama hii kwanza imekubaliana na ombi la waombaji (Rage na Hassanoo) kutaka mahakama hii itoe amri ya kutengua uamuzi wa Mahakama ya Kisutu.

“Hivyo mahakama hii inatengua amri ya mahakama hiyo ya chini na inaagiza jalada la kesi hiyo lirudishwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na ipangiwe hakimu mwingine,” alisema Jaji Mwarija na kusababisha Wakili Swai na Rweyongeza kukumbatiwa kwa furaha na wafuasi walalamikaji.

Awali, majira ya saa 10 jioni, wakili Rweyongeza akiwasilisha hoja zake, aliomba mahakama itengue uamuzi wa Kisutu kwa sababu wateja wake hawakuwa wamepewa haki ya kusikilizwa na uamuzi huo tayari umeishawaathiri kwa sababu hawawezi kugombea nafasi hiyo ya uenyekiti kwani uchaguzi umesimamishwa wakati wao hawakushtakiwa, isipokuwa mwenyekiti wa Simba ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Simba, aliyepaswa kushtakiwa ni Bodi ya Wadhamini ya klabu hiyo.

Kwa upande wake Magafu aliyekuwa akimtetea Dalali alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba anayepaswa kushtakiwa ni mwenyekiti wa Simba na kwamba katika kesi iliyofunguliwa Kisutu aliyeshtakiwa ni mwenyekiti, waombaji wala hawakuwa wameshtakiwa, hivyo hakimu Wambura asingeweza kuwasikiliza waombaji hao kwa sababu hawakuorodheshwa kwenye hati ya kiapo katika kesi ya msingi.

“Mheshimiwa Jaji Mwarija, naomba siasa isiletwe hapa mahakamani katika kuamua kesi hii, msimamo wangu ni kwamba Hakimu Mkazi wa Kisutu, Wambura, alikuwa sahihi, hajakosea mahali popote na ndiyo maana waombaji katika hati yao ya madai hawajaonyesha hakimu huyo amekosea wapi na ikumbukwe sheria inataka anayelalamikia uamuzi wa mahakama ya chini ni lazima aonyeshe mapungufu yaliyofanywa na hakimu husika, lakini msomi mwenzangu (Rweyongeza) ameshindwa kuainisha mapungufu.....tusilete siasa katika masuala ya kisheria,” alidai Magafu.

Kwa upande wake Wambura ambaye hakuwa na wakili, alidai kuwa yeye anaiomba isitengue uamuzi wa Kisutu kwa sababu haki zake zimevunjwa na uchaguzi huo haukufuata katiba.

Naye wakili Swai alisema anasikia furaha ombi lao kukubaliwa ila hataisahau kesi hiyo kwani tangu aanze kazi ya uwakili hajawahi kukumbana na kesi kama hiyo ambayo imewatesa mno; walitumia muda kidogo mno kujiandaa na kesi hiyo.

Kwa upande wake Hassan Hassanoor aliliambia gazeti hili mahakamani hapo kwamba amefurahishwa na uamuzi wa mahakama hiyo na anawaomba mashabiki wake wafike kwa wingi katika uchaguzi na wampigie kura za ndiyo ili aweze kushinda na kuiongoza klabu hiyo na kuongeza kuwa endapo atapata fursa ya kuchaguliwa kuiongoza Simba atahakikisha analeta maendeleo katika klabu hiyo kongwe hapa nchini.

Juzi, Jaji Mfawidhi Njengafibhili Mwaikugile aliitisha jalada la kesi iliyofunguliwa Mahakama ya Kisutu na kesi iliyokuwa imefunguliwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kupokea lalamiko la Rage na Hassanoo kwa ajili ya upekuzi na alimuagiza Naibu Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Lameck Mlacha, Jumatatu, ayapeleke kwa Jaji Agustine Mwarija ili aweze kupanga tarehe ya kuziita pande zote mbili na kuzisikiliza.

Hata hivyo, juzi usiku uongozi huo wa mahakama ulitoa maelekezo kwa watendaji wake kuandaa hati za kuziita pande zote mahakamani hapo jana saa sita mchana na pande zote zilipata hati za wito wa mahakama na jana saa tatu asubuhi zilifika mahakamani hapo.

Wakati huo huo, uchaguzi wa klabu hiyo unafanyika leo katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oyesterbay jijini Dar es Salaam kwa jumla ya wagombea 16 kushindana katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Akizungumza na waandishi wa habari hata kabla ya uamuzi wa Mahakama Kuu, Ndumbaro alisema maandalizi yalikuwa yamefikia asilimia 99 na uchaguzi utaanza saa tatu asubuhi.

Wagombea nafasi ya mwenyekiti ni Hassan Othman ‘Hassanoo’ na Ismail Aden Rage huku Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akiwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Nafasi ya ujembe wa kamati ya utendaji itawaniwa na Joseph Kinesi, Francis Waya, Yassin Mwete, Damian Manembe, Hassan Mnyenye, Said Juma, Maulid Said, Hamis Mkoma, Sued Nkwambi, Boniface Wambura, Suleiman Kigodi, Ibrahim Masoud na Hassan Mtenga.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Mei 9 mwaka 2010

MAJUMUISHO YAKWAMISHA KESI YA LIYUMBA

Na Happiness Katabazi

UPANDE wa mashitaka katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kwamba wameshindwa kuwasilisha majumuisho ya kesi hiyo kwa sababu mahakama haijawapatia majumuisho sahihi ya mwenendo wa kesi hiyo.


Wakili wa serikali, Ponsian Lukosi alidai mbele ya kiongozi wa jopo la mahakimu wakazi, Edson Mkasimongwa, kuwa wameshindwa kuwasilisha majumuisho hayo jana kama walivyoamriwa na endapo watapatiwa watawasilisha mara moja.

Hakimu Mkazi Mkasimongwa alikiri kuwa nakala halisi ya mwenendo wa kesi hiyo bado haijatolewa na kwamba mahakama hiyo itafanya jitihada, ili Jumatatu ijayo pande zote zipatiwe mwenendo wa kesi hiyo na kuwa ifikapo Mei 13 mwaka huu, pande zote ziwasilishe mahakamani majumuisho yao.

Alisema kutokana na hali hiyo, kesi hiyo itatajwa Mei 21 na hukumu itatolewa Mei 24 mwaka huu.

Januari 26, mwaka jana, Liyumba na Meneja Mradi wa Benki Kuu, Deogratius Kweka, walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza na kusomewa mashitaka hayo ya kuidhinisha mradi wa majengo ya minara pacha bila idhini ya bodi ya wakurugenzi na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Mei 8 mwaka 2010

KULIKONI DUKA LA VITABU LA SERIKALI?

Na Happiness Katabazi
DUKA la Vitabu la serikali ambalo wajibu wake ni kuuza nakala za sheria zinazotungwa na Bunge , halitekelezi wajibu wake ipasavyo.
>Duka hili la serikali kwanza linatakiwa liwe na matawi wilaya zote na mikoa yote ya hapa nchini, kwasababu msingi mkuu wa sheria za nchi yetu ni kwamba kila raia ana wajibu wa kujua sheria na kutojua sheria siyo utetezi.

Kwa hiyo wajibu wa kuchapisha sheria na kuzisambaza kwenye maduka yote ya serikali nchini ni wajibu wa kwanza wa dola linaloendeshwa kwa mujibu sheria.

Hii ina maana gani?Moja;Ina maana kwamba kwana gazeti la serikali na taarifa za sheria zinazotungwa na bunge litoke kila mwezi , hili halifanyiki ipasavyo kwani wakati mwingine linachelewa kutoka.Na hii ina maana kwamba serikali yetu haizingatii msingi wa uwazi ambao ni msingi mkuu wa utawala bora.

Pili; sheria zinazotungwa na bunge hazipatikani ,kila tunapokwenda kwenye duka la vitabu la serikali lililopo Mtaa wa Jamhuri jijini Dar es Salaam, unaambiwa sheria hizo zimekwisha na hawajui lini zitachapwa na ofisi ya Mpigachapa wala lini zitafikishwa dukani hapo.

Mfano mzuri ni nakala Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya 2002,Sheria ya Madai,Katiba kwa kipindi cha miezi mitatu sasa hazipo na haijulikanizitapatikana lini.

Tatu;duka hilo halina matawi nchi nzima bali lina maduka madogo Iringa,Mwanza,Arusha,Zanzibar na kwingineko , hii inamaanisha hata duka hilo lingekuwa na nakala za kutosha,mtandao wa maduka ya vitabu vya serikali ni finyu mno.Je !haiyumkiniki mwananchi kutoka kijiji cha Nyakayanja Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, kusafiri kutoka huko kuja Dar es Salaam kununua sheria za nchi?

Kwa mujibu wa dhana ya sheria kwamba kila mwananchi ana wajibu na haki ya kujua sheria , basi ni wajibu wa serikali kuwa na maduka ya vitabu vya serikali katika kila wilaya.

Ikiwa hili halifanyiki ni makosa na ikiwa wananchi hawajatambua ni haki yao kupata nakala za sheria basi ni matokeo ya ujinga.Ama sivyo kama utaratibu huu utaendelea itabidi kutunga msingi mpya wa sheria unaomwezesha raia kujitetea kwamba hajui sheria kwa kuwa hazipatikani madukani kwa wakati.

Wanasheria waliobobea na mahakimu , majaji hata waendesha mashtaka waliofanyakazi mikoani,wanasemaga huko hakuna sheria kwa kuwa hata baadhi ya mahakimu wenyewe hawana nakala za sheria wanazotakiwa wazitumie kuamria baadhi ya kesi.

Baadhi ya Waendesha mashitaka hawana nakala ya sheria anayoitumia kuendeshea mashtaka kwa maana hii watendaji wote hawa wanajikuta ni wababaishaji wasiyo na uhakika na kile wanachokifanya au wanaishia kuazima sheria hizo.Kwa mantiki hiyo wapo wananchi wengi ambao wamejikuta wakipoteza haki zao au hata kutumikia vifungo jela kwa makosa ambayo hayamo kwenye sheria za nchi.

Na mfano hai ambao si wa kutafuta ni kesi ya ubakaji na kulawiti watoto wa shule ya msingi inayomkabili Mwanamuziki mahiri wa dansi nchini Nguza Viking(Babu Seya) na wanawe watatu ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, iliwahukumu kutumikia kifungo cha maisha jela baadaya kuwatia hatiani kwa makosa hayo.Lakini mapema mwaka huu, Majaji watatu wa mahakama ya rufaa nchini , Jaji Nataria Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati iliwafutia washitakiwa mashitaka yote sita ya kulawiliti na kubakiza mashitaka matano ya ubakaji.

Jopo hilo la majaji wa tatu lilisema limefikia sababu ya kuyawafutia mashtaka hayo ya kulawiti kwasababu Tanzania haitambui kosa la kulawiti kwa kushirikiana(gang sodomie).Kwa uamuzi huu wa mahakama ya rufani ambao uliwaachiria huru mrufani wa tatu na wanne na kuwatia hatiani mrufani wa kwanza na wapili, mtakubaliana nami kwamba mahakama hizo za chini ziliwahukumu warufani adhabu hiyo kwa makosa hayo ya kulawiti ambayo hayapo kwenye sheria za nchini yetu.

Kwa hiyo maduka ya serikali ni muhimu mno katika kufanikisha utawala bora.Maduka hayawezi kuachwa holela holea lazima sasa itungwe sheia itakayotawala uendeshaji wa maduka ya serikali kwa dhana nzima ya utawala itategemea ufanisi wake.

Dhana dhima ya haki itategemea ufanisi wa maduka hayo.Wananchi hawawezi kujua wana haki gani kama hawana nakala za sheria kwasababu eti hazipatikani .Hataishiwa kuonewa tu.

Sasa sheria za uendeshaji wa maduka ya vitabu vya serikali iweke masharti ya maduka hayo, yatengewe fedha katika bajeti ya kutosha ya serikali kila mwaka ili kuakikisha sheri zote zinachapishwa na zinapaikana kwa urahisi kote nchini.

Ieleweke kwamba kuendeleza hali hii ya uahidimu wa machapisho ya sheria za nchi ni kichocheo kikubwa cha rushwa kwa kuwa mwananchi anajikuta hajui hazi zake kila mara.Pia kukosekana kwa machapisho ya sheria za nchi ni chanzo cha utawala usiojali haki na sheria kwa kuwa watawala wanajificha maovu yao katika ujinga wa wananchi.

Hicho pia ni chanzo cha umaskini wetu kwasababu kwa kutojua sheria haki za wananchi zitaporwa kila siku na baadhi ya watendaji wa serikali ni manyang’au na miungu watu na kuwasababishia wananchi umaskini.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Mei 2 mwaka 2010