MENGI AKWAA KISIKI KORTI KUU


Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa ametoa amri ya kurudishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jalada ya kesi ya madai ya kashfa ya shilingi moja iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mfanyabiashara Yusuf Manji dhidi ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Ltd, Reginald Mengi na ITV.


Jalada la kesi hiyo ambayo lilitua katika Mahakama Kuu Machi 23 mwaka huu, likitokea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na barua ya februali 23 mwaka huu, iliyoandikwa na wakili wa mdaiwa(Mengi) , Michael Ngaro kwa Jaji Mfawidhi Semistocles Kaijage ambapo ndani ya barua hiyo Ngaro alimuomba Jaji Kaijage apitie mwenendo mzima wa kesi hiyo kwani hakimu mkazi anayeisikiliza kesi hiyo Alocye Katemana ametoa maamuzi kadhaa yanaoonyesha anaupendelea upande wa mlalamikaji(Manji).

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika toka ndani ya Mahakama Kuu, vililiakikishia Tanzania Daima tayari Jaji Kaijage alishatimiza wajibu wake wa kulipitia jalada hilo na kwamba jalada la kesi na amebaini hakuna sheria zozote zilizokiukwa na Hakimu Mkazi Katemana shauri hivyo ameamuru jalada hilo lirudishwe katika mahakama ya Kisutu na liendelee kusikilizwa kwa hakimu yule yule Katemana.
“Tunakuakikishia kwamba Jaji Mfawidhi Kaijage alishatimiza wajibu wake wa kulipitia jalada hilo na amebaini kuwa Hakimu Mkazi Katemana hakupindisha sheria yoyote hivyo ameliamuru jarada hilo lirejeshwe katika katika mahakama ya Kisutu na hakimu yule yule Katemana ndiye aendelee kulisikiliza;

“Na jalada la kesi hiyo ya Manji na Mengi limeishatoka hapa mahakama kuu tangu jana (Juzi) na kupelekwa Mahakama ya Kisutu kwa hakimu Katemana…hivyo ukienda mahakama ya Kisutu utaweza kujua kesi hiyo imepangwa tarehe ipi kwaajili ya kutajwa ama upande wa mlalamikaji (Manji)kuendelea kujitetea”vilisema vyanzo vyetu.
Hata hivyo alipotafutwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,Kaijage ili aweze kuthibitisha taarifa hizo jana saa tisa mchana hakuweza kupatikana kwasababu simu yake ya kiganjani ilikuwa haipatikani.

Februali 15 mwaka huu, Hakimu Mkazi Katemana alitupilia mbali ombi la Mengi lililotaka mahakama hiyo iwapatie nakala ya uamuzi iliyotolewa na hakimu huyo Februali 11 mwaka huu,ambapo hakimu huyu alikazikataa nyaraka vivuli 14 zikiwemo nyaraka ambazo zinaonyesha ni mali ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU),Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mkataba wa kukopeshana fedha baina ya kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd na Kampuni ya Quality Finance Corporation Ltd , ili aweze kwenda Mahakama Kuu kuomba ufanyiwe mapitio kwa sababu Sheria ya Mabadiliko ya Kanuni ambazo zimeandikwa Na. 25 ya mwaka 2002, zinakataza upande wowote katika kesi yoyote kwenda mahakama ya juu kupinga amri za muda zinazotolewa na mahakama ya chini hadi kesi ya msingi itakapomalizika na kutolewa hukumu.

Hakimu Katemana alisema siyo tu sheria hiyo ina kataza maamuzi madogo kama hayo aliyoyatoa kuyakatia rufaa pia nyaraka hizo 14 haziusiani na kesi iliyopo mbele yake, ni nyaraka vivuli ambazo hazijathibitishwa kisheria na pia hazionyeshi kama ofisi hizo za serikali zimetoa kibali kwa mdaiwa kutumia nyaraka hizo katika kesi hiyo na kuongeza kuwa nyaraka hizo zimewasilishwa nje ya muda mwafaka kwani kisheria zilipaswa kuwasilishwa kabla ya mlalamikaji kupanda kizimbani kuanza kutoa ushahidi wake.

Mapema mwaka 2009, Manji anatetewa na mawakili maarufu nchini, Mabere Marando, Richard Rweyongeza, Dk.Ringo Tenga na Beatus Malima alimfungulia kesi ya madai ya kashfa Mengi na kituo cha televisheni cha ITV akitaka amlipe fidia ya shilingi moja kwa madai kuwa Mengi alitumia televisheni yake kumkashfu kwa kumuita ‘Fisadi Papa’ na kwamba mmoja wa watu wanaopora rasilimali za Tanzania.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Machi 31 mwaka 2011.

DOWANS YAWAWEKEA PINGAMIZI WANAOIPINGA MAHAKAMA

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Kampuni ya Dowans Holding SA na Dowans Tanzania Ltd,imeiwekea pingamizi Shirika Umeme (TANESCO),Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) na Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Timoth Kahoho katika kesi yake ya kuomba tuzo waliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa migogoro ya Kibiashara (ICC) isajiliwe na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Kesi hiyo ambayo jana ilikuja mbele ya Jaji Emilian Mushi katika Mahakama Kuu kwaajili ya kutajwa, wakili wa mlalamikaji(Dowans), Keneddy Fungamtama aliiambia mahakama tayari ameishawasilisha mapingamizi matatu kwa pande tatu katika kesi ambazo ni Tanesco anayetetewa na , LHRC na Kahoho ambaye anajiwakilisha binafsi

Kesi hiyo ilifunguliwa mapema mwaka huu na mshinda tuzo hiyo ambayo ni Kampuni ya Dowans ambayo inatetewa na wakili Kennedy Fungamtama dhidi ya TANESCO ambayo nayo inatetewa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju , Jamhuri Johnson, Dk.Angelo Mapunda na Florence Luoga. Na wapinga maombi ya Dowans ambao hawaja orodheshwa kwenye kesi hiyo ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kinachotetewa na Dk.Sengondo Mvungi, Harold Sungusia na Francis Kiwanga na Mwanahabari mkongwe ambaye hana wakili.

Amri hiyo ilitolewa jana na Jaji Emilian Mushi wakati kesi hiyo ya madai namba 8 ya mwaka huu,ilipokuja kwa mara ya kwanza kwaajili ya kutajwa alisema amefika uamuzi wa kutoa amri hiyo baada ya wapinga maombi (LHRC na Timoth Kahoho) kueleza kuwa hawakuwa wamepatiwa nakala tuzo hiyo na wao hawajawaipatia Dowans na Tanesco nakala za mapingamizi yao.

Jaji Mushi pia alikubaliana na maombi ya mawakili wa pande zote yaliyotaka pande zote katika kesi hiyo(Dowans na Tanesco) kuacha kufanya jambo lolote linalohusiana na maslahi ya pande hizo mbili hadi pale kesi hiyo itakapomalizika.

“Ila kama mlivyoomba nyie mawakili wa pande zote mbili kwamba endapo serikali kupitia Tanesco wakitaka kulimaliza jambo hili nje ya mahakama,mahakama hii inaziamuru pande hizo kabla ya kufikia uamuzi huo wa kumalizana nje ya mahakama au kuwasha mitambo,walete kwanza ombi mahakamani la kuomba kufanya hivyo;

“Na sioni haja ya kutoa amri ya kuwazuia wale wote wanaopiga kelele za Dowans,Dowans huko mitaani na kwenye vyombo vya habari kwasababu sheria na utaratibu unaeleweka wazi kwamba kesi ikiwepo mahakamani ni marufuku kwa mtu au vyombo vya habari kuizungumzia …lakini minanasema waache watu waendelee kupiga kelele zao huko mitaani kuhusu tuzo ya Dowans kwani napenda wajue kwamba mahakama hii aiyumbishwi na hizo kelele zao kwani siku zote inafanyakazi zake kwa kuzingatia sheria”alisema Jaji Mushi.

“Kwa sababu upungufu huo umejitokeza natoa siku 21 kwa pande mbili katika kesi hii na nyie wapingaji wawili , wenyewe kwa wenyewe muakikishe mnapeana nyaraka mlizonazo na ninaiarisha kesi hii hadi Machi 30 mwaka huu, ambapo kesi hii itakuja kwaajili ya kutajwa na kuangalia kama tayari mmeishapeana nyaraka hizo”alisema Jaji Mushi.

Awali wakili wa Tanesco, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Masaju aliomba mahakama impatie siku 21 kujibu hoja za kutaka tuzo ya Dowans isisajiliwe.Naye wakili wa Dowans, Fungamtama pia aliomba mahakama impatie siku 21 kujibu pingamizi hilo litakalowasilishwa na Tanesco.

Kwa upande wakili wa (LHRC), Dk.Mvungi aliomba apatiwe siku saba kujibu hoja kama kutakuwa na chakujibu.Na Kahoho yeye ambaye hana wakili akaeleza kuwa kama maombi yake ya kupinga Dowans isisajiliwe yatawekewa pingamizi anaomba apewe siku 14 kujibu na kuongeza kwa kuiomba mahakama itoe amri ya kuzuia watu au vyombo vya habari kuchapisha habari ambazo zinaingilia mwenendo wa kesi hiyo.

Kesi hiyo ambayo inafuatiliwa kwa karibu na umma wa Tanzania iliendeshwa chemba hali iliyobabisha mawakili na waandishi baadhi waliofika mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo ambayo jana kwa mara ya kwanza ndiyo ilitajwa kushindwa kuingia ndani ya chumba hicho na kuishia kukaa kwenye kordo za mahakama hiyo na ambapo waliushauri uongozi wa mahakama hiyo utambue kuwa kesi hiyo inagusa maslahi na hisia za watanzania wengi hivyo ni vyema siku nyingine jaji Mushi aendekusikiliza kesi hiyo kwenye mahakama ya wazi.
Januari 25 mwaka huu, Dowans iliwasilisha ombi lake lakutaka Mahakama Kuu ya Tanzania iisajili tuzo waliyopewa na Mahakama ya ICC na siku chache baadaye Tanesco, LHCR,Kahoho wakawasilisha hati ya nia ya kupinga ombi hilo la kutaka tuzo hiyo isajiliwe.

Mahakama ya ICC, ilitoa hukumu ya kesi ya Dowans dhidi ya Tanesco, Novemba 15 mwaka jana, ambapo mahakama ilitia hatiani Tanesco kwa kosa la kuvunja mkataba na Dowans na ikaimuru iilipe fidia ya shilingi bilioni 94.Hukumu ambayo imezua mjadala mkali hapa nchini kuanzia kwa viongozi wa serikali, vyama vya siasa,na makundi mengine ambapo wengine wanataka Dowans ilipwe huku wengine wakitaka kampuni hiyo isilipwe.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Machi 31 mwaka 2011.

KESI YA NG'UMBI Vs MYIKA YAPIGWA KALENDA

Na Happiness Katabazi

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya (CHADEMA), John Mnyika jana aliiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam impatie muda kwa kujibu hati ya kiapo ya mlalamikaji katika kesi ya kupinga ubunge wake iliyofunguliwa dhidi yake na aliyekuwa mgombea mwenzake kupitia (CCM), Hawa Ng’umbi kwasabu mdaiwa huyo hakuwa amempatia hati ya madai ya kesi hiyo pamoja na ombi la kuomba kupunguziwa ada ya kuendesha kesi hiyo.


Katika kesi hiyo Na. 107/2010 ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana ambayo yalimtangaza Mnyika kuwa ndiye mshindi.Hawa Ng’umbi ambaye Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ambaye anatetewa na wakili wa kujitegemea Issa Maige anamshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mnyika na aliyekuwa Msimamizi wa Jimbo la Ubungo kwamba taratibu za uchaguzi zilikiukwa na kwamba mdaiwa wa kwanza na wa tatu walishindwa kutimiza wajibu kikamilifu.

Ombi hilo lilitolewa jana na wakili wa Mnyika, Edson Mbogoro mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,Amir Msumi ambapo alidai kuwa hadi kufikia jana mteja wake ambaye ni mdaiwa wa pili katika kesi hiyo hakuwa amepatia hati ya kiapo na ombi la mlalamikaji la kuiomba mahakama impunguzie kiwango cha ada ya kuendesha kesi hiyo hivyo anaomba mahakama mahakama imwamuru mlalamikaji ampatie hati hiyo ya kiapo na ombi hilo ili aweze kujibu.

Msajili Msumi alikubaliana na ombi hilo na akamkata Mnyika awasilishe majibu ya hati hiyo ya kiapo na ombi la mlalamikaji la kuomba apunguziwe ada ya kesi Aprili 4 mwaka huu na akaiarisha kesi hiyo Mei 5 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya kutajwa.

Hata hivyo Msajili Msumi alisema licha ya Mnyika kutokabidhiwa nyaraka hizo tayari wadaiwa wenzake katika kesi hiyo ambayo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi Uchaguzi wa Jimbo la Ubungo tayari walishakabidhiwa nyaraka na mlalamikaji Hawa Ng’umbi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bukombe.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Machi 31 mwaka 2011.

MSIBA WAMKWAMISHA MURRO ASIJITETE


Na Happiness Katabazi
ALIYEKUWA Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa(TBC1) Jerry Murro jana alishindwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuanza kujitetea katika ya kula njama, kushawsishi na kuomba rushwa ya Sh milioni 10,kwasababu amesafirisha msiba wa baba yake mdogo mkoani Kilimanjaro.


Mbele ya Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka,Stanslaus Boniface aliikumbusha mahakama hiyo kwamba kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya Murro na wenzake kuanza kujitetea kutokana na uamuzi wa mahakama hiyo uliotolewa Machi 8 mwaka huu,ambao uliowaona washtakiwa wote wana kesi ya kujibu na kwamba kwa upande wa Jamhuri upo tayari kwaajili ya kusilikiza utetezi wa washtakiwa.

Baada ya Boniface kuikumbusha mahakama, wakili wa kujitegemea Richrad Rweyongeza aliwasilisha ombi la kuomba kesi hiyo iairishwe kwasababu Murro hayupo mahakamani amekwenda mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kumzika baba yake mdogo na kwamba mshtakiwa huyo alileta ombi la udhuru huo juzi.

Hata hivyo ombi hilo lilikubaliwa na Hakimu Mirumbe ambapo aliairisha kesi hiyo Mei 2-3 mwaka huu, ambapo washtakiwa hao wataanza kujitetea mfululizo kwa siku hizo mbili.
Mbali na Murro, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Edmund Kapama na Deogratius Mugasa ambao wanadaiwa kuwa Februali milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo , Michael Karoli Wage.Kati ya mashtaka matatu yaliyofunguliwa dhidi ya yao,Murro anakabiliwa na mashtaka mawili.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 30 mwaka 2011.

TANZANIA IJITAZAME UPYA


Na Happiness Katabazi

Salaam! wasomaji wote wa safu hii.Leo nitaanza makala yangu kwa nukuu ya Baba wa Taifa hili, Mwalimu Julius Nyerere. Nukuu hiyo inapatikana katika hotuba zake maarufu, katika kitabu cha ‘Moyo kabla ya silaha’, aliyoitoa mwanzoni mwa miaka ya 1960. Na nitaichambua nukuu hiyo.


Jifunze wakati ni huu: “Afadhali tuwe na taifa ambalo halina silaha za kisasa, lakini tuna moyo wa ushujaa, kuliko kuwa na taifa lenye silaha, lakini vijana wake ni waoga. Tuwe taifa la binadamu, tujue wapi tunatoka na wapi tunakwenda.

“Kuwa na moyo safi ni jambo jema sana kwani tukiwa na moyo safi silaha zitafuata baadaye. Afadhali kuwa maskini, lakini tunajitegemea, kuliko kuwa matajiri kwa kuomba na kutegemea taifa jingine. “Tujiamini kwa nguvu zetu zote na tunajitegemea. Taifa linaloshiba makombo siyo taifa.

“Tuwe na tabia ya ushujaa, tusiwe waoga. Tuwe na tabia ya kujitegemea na kusaidiana. Ni afadhali kuwa na chakula kidogo, lakini tukagawana kidogo kidogo kuliko kuwa na chakula kingi na tukaanza kukigombea. Tanzania iwe na tabia mpya. Inawezekana, timiza wajibu wako.”

Aya ya kwanza ya nukuu hiyo Mwalimu Nyerere, alikuwa anaona kwamba vijana wengi walikuwa wanadai wapewe silaha, watakomboa taifa na kukomboa Bara la Afrika kutokana na ukoloni na ubeberu wa watu weupe. Wakati huo vita ya kupigania uhuru ilikuwa inarindima katika nchi za Msumbiji , Angola , Zimbambwe na kwingineko.

Nchi hizo zilikuwa chini ya ukoloni na ubeberu na Tanzania ilikuwa makao makuu ya kamati ya ukombozi ya Afrika ya Umoja wa Nchi Uhuru za Afrika. Na wakati huo ndege za Wareno zilikuwa zikivuka mpaka na kudondosha mabomu nchini mwetu.

Mwalimu Nyerere aliona upungufu katika mtazamo wa vijana wale ambao waliona silaha ndiyo njia sahihi ya kukomboa ukoloni na ubeberu.

Yeye aliona ni tofauti, kwani alichokuwa anakihitaji yeye ni ‘commitment’, uwe unaliamini hilo jambo kwa moyo wako wote na akili zako zote na ujitoe mhanga kulitetea Bara la Afrika. Hiyo ndiyo nadharia ya upambanaji na huo ndio msingi wa upambanaji wa kweli.

Mwalimu alizungumzia katika mazingira hayo. Je, leo hii kauli hiyo inatugusa vipi Watanzania, umma ambao idadi kubwa ya ni sisi vijana? Na je, tuna amini kwa moyo wote kuhusu vita dhidi ya ubeberu? Ukweli ni kwamba hatuamini.

Walio wengi hawaamini kama kuna ubeberu, wanaamini kwamba kuna utandawazi kwa maana kwamba mtaji wa kibeberu unaweza ukatumika kulikomboa taifa na kufuta umaskini.

Kwa Watanzania wengi wa leo wanatofautiana sana na Mwalimu Nyerere, hawana moyo wala ushupavu wa kupambana na udhalimu wa kila aina. Na kwa hakika kwa kiasi fulani tunashawishika kuamini sera nzima ya uwekezaji ni tamko la kukumbatia ubeberu.

Kwa msingi huo vijana hatuna budi kupambana na hata kuhitaji kuwa na moyo wa ushujaa. Tumeishakubali kwamba wageni wana haki kubwa hata kuliko wananchi kuwekeza na kuvuna rasilimali zetu.

Wajibu wetu na nafasi tuliyonayo tujiendeleze kielimu na kuomba ajira. Na katika hilo hakuna cha ushupavu wala cha woga, cha msingi ni kumpigia magoti na kumlamba miguu tajiri ili upate mradi wako.

Mwalimu Nyerere alisisitiza kwamba ili tuwe na taifa la binadamu linalostahili heshima lazima tujue wapi tunatoka na wapi tunakwenda: Kwa hilo Watanzania wa leo hatumo kwa sababu hatuna sera thabiti.

Tunachokiabudu leo hii ni kupewa misaada na wafadhili ambao sasa ndio wanatupangia mipango yetu na uchumi wa maendeleo. Miongoni mwa kazi kubwa ya baadhi ya watendaji wa serikali ni kuandika michanganuo (proposals) ili kupewa fedha, na kweli kazi hiyo inafanikiwa kwa kuandaa makongamano mbalimbali na kisha inafuatiwa na kazi kubwa ya kuandika ripoti na kuwapelekea wale mabwana zetu waliotoa fedha zao kwa nchi yetu.

Mwalimu Nyerere alisema, afadhali kuwa maskini, lakini tunajitegemea kuliko kuwa matajiri kwa kuomba kutegemea taifa jingine; kwa maana hiyo taifa linalostahili heshima ni lile linalojiamini, linalotegemea nguvu zake kwa maendeleo yake badala ya taifa linaloshiba ‘makombo,lawalawa’ linayopewa kwa jina la misaada.

Hebu tujiulize, Tanzania tunajitegemea kwa kitu gani? Vijana wetu hawajui tena kilimo wala hawapendi ufugaji, kwa hiyo chakula kilichopo sokoni na kwenye ‘supermarket’ kinaagizwa kutoka nje ya nchi.Na hatupendi kwa sababu hakuna mazingira mazuri yatayotushawishi kujikita kwenye sekta hiyo ya kilimo.

Serikali ya Tanzania haina tena viwanda vya nguo, japo inazalisha zao la pamba. Tanzania haisindiki kahawa wala matunda japo ina uwezo mkubwa wa kuzalisha mazao hayo. Tanzania haizalishi mafuta ya kula, inanunua mafuta hayo kutoka kwenye viwanda vya watu binafsi au nje ya nchi ambazo nyingine ni jangwa japo Tanzania inazalisha zao la alizeti, karanga na mbegu nyingine za mafuta ya kula.

Viwanda vyetu tumevibinafsisha tena kwa wingi, vingine vinafungwa na vilivyopo ni vya jua kali vinavyozalisha bidhaa duni zisizo na tija wala thamani kwenye masoko ya kitaifa na kimataifa.Kwa mantiki hiyo, Tanzania sasa ni jalala la kila kitu, kuanzia mitumba na kila uchafu unaotoka nje hasa nchi za Asia .

Je, kwa staili hii ni jeuri gani tunaweza kuwa nayo wakati tumeshindwa kujitegemea karibu kwa kila kitu ? Cha msingi nikuona jinsi taifa letu lilivyo taifa la waoga kiuchumi, kwani badala ya kuanzisha miradi ya kuzalisha mali , tunaanzisha miradi ya uchuuzi ya kuuza karanga na takataka kutoka nje.

Kwetu maendeleo ya uchumi ni kuligeuza taifa kuwa la wachuuzi wa aina ya wamachinga. Sasa ujasiri gani tutakuwa nao wakati karibu sote tumezama kwenye umaskini wa mali , akili,kauli, maadili na elimu na matatizo ya kiafya?.Kwani hakuna ubishi sasa kwamba taifa hili lina wagonjwa wengi sana kuliko tulivyokuwa tukifikiri hapo awali.Na ukweli huo unaendelea kujidhiirisha kule kwa Babu Loliondo(Ambilikile Mwaisapile)jinsi viongozi wetu na wananchi wanavyomiminika kwa wingi huko kupata kikombe cha dawa kinachodaiwa kutibu magonjwa sugu.Hatari sana .

Taifa la aina hii ni taifa duni ambalo litatugeuza kuwa taifa la watumwa wa mataifa mengine.Sasa hivi baadhi ya Watanzania hususani vijana wamechoka hata kufikiri, wanaogopa kufikiri na wako tayari kufuta Utanzania wao ili angalau watawaliwe na taifa lolote linalopenda kututawala.

Wengi wa Watanzania wa leo ni watu wanaopenda kutumia njia za mkato zisizo sahihi kujipatia kipato, hawapendi kufanya kazi wakatoka jasho wanapenda sana starehe na matokeo ya taifa kuwa na watu wa aina hiyo ni kuwa na taifa la matapeli, wasanii, vizabizabina,wala rushwa, wapika majungu,mafedhuli , maafiliti,mabazazi, wazandiki na watu wasioaminika kabisa na hii sasa imeanza kuwa sifa kuu ya Watanzania kimataifa.

Kwa hiyo hivi sasa ukikutana na Mtanzania awe kiongozi, mbunge,majaji,mahakimu,mawakili,maaskari,wanahabari, wapenzi,wafanyabiashara, matajiri, walemavu na wananchi wa kawaida unaanza kuwa na wasiwasi kwamba huyo si mmoja mwenye sifa kama hizo nilizozitaja hapo juu?.

Si siri tena, zile zama za Mtanzania ni kioo cha uadilifu duniani zimeanza kutoweka.Kila mmoja wetu mwenye tabia kama hizo ajirekebishe.

Mungu ibariki Tanzania , Mungu Ibariki Afrika.
0716 774494

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 29 mwaka 2011.

JAJI MWANGESI AJITOA KESI YA MAHALU

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE jaji Sivangilwa Mwangesi ambaye alikuwa akisiliza kesi ya uhujumu uchumi wa Euro zaidi ya milioni mbili inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Meneja Utawala na Fedha, Grace Martin ametangaza kujiondoa kuendelea kusikiliza kesi hiyo.


Jaji Mwangesi alitangaza umuzi huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, ambapo kesi hiyo ilikuja kwaajili ya jaji huyo kutoa uamuzi wa ama kuendelea au kujiondoa katika kesi hiyo kufuatia sababu sita zilizowasilishwa Ijumaa iliyopita na washtakiwa ambayo yalimtaka ajitoe kwasababu hawana imani nae kwasababu amekuwa akiendesha shauri hilo kwa malengo yake badala ya sheria.

“Naheshimu maoni ya washtakiwa ya kunitaka minijiondoe…ila nasema zile sababu zao sita hazina msingi msingi wowote wa kisheria kwani sababu zote za kunikataa mimi zilikwisha tolewa uamuzi na Mahakama Kuu katika ombi namba 2/2009 ililowasilishwa katika mahakama hiyo ya juu na washtakiwa hao ambapo ulilitupilia mbali ombi hilo lililotaka wafutiwe kesi ya msingi kwasababu mahakama ya Kisutu iliendesha kesi hiyo kimakosa; “Ila kwakufuata haki, washtakiwa wanahaki ya kumkataa hakimu au jaji pindi wanapokosa imani na hakimu huyo…na mimi sitaki kung’ang’ania kusikiliza kesi hii kwa misingi ya haki natangaza kujitoa kuendelea na shauri hili kuanzia leo”alisema Jaji Mwangesi na kuondoka ndani ya chumba cha mahakama ya wazi.

Lakini muda mchache baadaye Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Elvin Mugeta aliingia mahakamani na jalada la kesi hiyo ya Mahalu huku tayari wakiwa washaondoka katika eneo hilo la mahakama na kusema kuwa anaiarisha kesi hiyo hadi Aprili 28 mwaka huu, ambapo kesi hiyo itakuja kwaajili ya kutajwa na kujua ni hakimu gani amepangwa.

Machi 25 mwaka huu,wakili wa washtakiwa hao, Mabere Marando, Alex Mgongolwa, Alex Mushumbusi,Beatus Malima waliwasilisha sababu sita za kumwomba jaji Mwangesi ajitoe kwenye shauri hilo sababu ya kwanza ni ni kwamba upande wa utetezi ulishatoa mahakamani hapo Ansard ya bunge ya mwaka 2004 iliyomnukuu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali ya awamu ya tatu ambaye kwasasa ni rais Jakaya Kikwete akieleza bunge kuwa manunuzi ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia ulikidhi matakwa ya Sheria ya manunuzi ya umma na kwamba hakukuwa na wizi katika ununuzi huo lakini jaji huyo akuzingatia ansard hiyo.

“Sababu ya pili ni wewe Jaji Mwangesi ulipindisha makusudi sheria ya Ushahidi ya mwaka 2002 ukachukua ushahidi wa shahidi wa jamhuri aliyekuwa nchini Italia kwa njia ya video wakati sheria ya nchi hii inakataza na ndiyo maana hivi sasa serikali inapeleka muswaada bungeni wa kuifanyia marekebisho sheria iliyopo hivi sasa, sheria hiyo mpya ikitungwa ndiyo itakuwa ikiruhusu mahakama kuchukua ushahidi kwa njia ya video”alidai Marando.

Sababu ya tatu; tangu mapema upande wa washtakiwa waliuomba upande wa Jamhuri uwatajie mlalamikaji wa kesi hiyo na upande wa Jamhuri ulishawahi kuieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo haina mlalamikaji lakini jaji huyo alishtushwa na kauli hiyo ya Jamhuri na akaiarisha kesi na kuwautaka upande wa jamhuri ukamlete mlalamikaji na mwisho wa siku jamhuri ilienda kuleta nakala ya nusu kurasa ya maelezo ya mlalamikaji ambaye ni Afisa wa TAKUKURU,na mbaya zaidi jamhuri hadi inafunga kesi yao hakuweza kumleta mlalamikaji huyo kutoa ushahidi wake mahakamani.

“Kwa hiyo sisi upande wa utetezi tunasema kwa kitendo cha wewe Jaji Mwangesi kuung’ang’ania upande wa Jamhuri walete mlalamikaji wa kesi hiyo huku upande wa Jamhuri ulishawahi kumleleza kuwa kesi hiyo haina mlalamikaji kimetunyima fursa sisi kuwasilisha ombi la kutaka kesi hiyo ifutwe kwasababu ilikuwa haina mlalamikaji”alidai Marando.

Sababu ya nne ni kwamba jaji huyo aliunyima haki upande utetezi wa kuwasilisha majumuisho ya kuwaona hawana kesi ya kujibu pale jaji huyo kwa malengo yake anayoyajua yeye siku Jamhuri ilipofunga kesi yake na ndipo siku hiyo hiyo akatoa uamuzi wa kuwaona washtakiwa wanakesi ya kujibu.

“Sababu ya tano ya kukataa jaji wewe ni kwamba wewe unasikiliza kesi hii kama hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwasababu mahakama zote zina mipaka ya ardhi ya kufanyakazi zake isipokuwa Jaji Mkuu anaweza kutoa kibali maalum kwa mahakama husika kusikiliza kesi iliyo nje ya mamlaka yake … lakini wewe mheshimiwa jaji hukupata kibali cha Jaji Mkuu na ukadiriki kupokea ushahidi wa shahidi wa Jamhuri aliyekuwa nchini Italia kwa njia ya video jambo ambalo tunaliona ulikiuka makusudi sheria za nchi kwa malengo yako binafsi.”alidai Marando.

Alitaja sababu ya sita ni kwamba alikiuka kwa makusudi sheria za Tanzania kwakukubali kwake kupokea nakala kivuli ya mkataba wa mauzo ya ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Italia kama kielelezo toka kwa shahidi wa Jamhuri ambaye ni wakili wa nchini italia ambaye alikuja hapa nchini kutoa ushahidi ambapo shahidi huyo aliambia mahakama kuwa kwa mujibu wa sheria za Italia hazimruhusu yeye kuutoa mkataba halisi na jaji huyo akakubaliana na hoja ya shahidi huyo wakati sheria za Tanzania zinakataza hilo na kwamba alikubali kupokea kielelezo hicho ambacho kiliandaliwa na shahidi huyo mwenyewe ambaye ni wakili huyo wa Italia wakati sheria za Tanzania zinakataza mkataba unaondaliwa na mwanasheria husika zisibitishwe na mwanasheria huyo huyo bali zikathibitishwe na mwanasheria mwingine.

Mapema mwaka 2006 ,Jamhuri alimfikisha Mahalu na Martin katika mahakama hiyo wakidai manunuzi ya jengo hilo hayakufuata sheria za manunuzi, na kwamba waliibia serikali kiasi hicho cha fedha kwaajili ya ununuzi wa jengo hilo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 29 mwaka 2011.

MAHALU AMKATAA JAJI

Na Happiness Katabazi
ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin ambao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ya zaidi ya Euro milioni mbili, jana walimwomba Jaji Sivangilwa Mwangesi ambaye anaendesha kesi hiyo hajitoe kwasababu amekuwa akikiusha sheria kwa makusudi kwasababu ya malengo anayoyajua yeye.

Ombi hilo limetolewa jana na mawakili wa washtakiwa haoMabere Marando aliyekuwa akisaidiwa na Beatusi Malima na Alex Mgongolwa ambapo kwakuanza waliiumbukusha mahakama hiyo kuwa wanafahamu kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya jaja huyo kupanga tarehe ya washtakiwa hao kuanza kujitetea.
Wakili Marando alidai kuwa wana sababu sita ambazo wamwomba Jaji Mwangesi ajitoe ambapo aliitaja sababu kwanza ni kwamba upande wa utetezi ulishatoa mahakamani hapo Ansard ya bunge ya mwaka 2004 iliyomnukuu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali ya awamu ya tatu ambaye kwasasa ni rais Jakaya Kikwete akieleza bunge kuwa manunuzi ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia ulikidhi matakwa ya Sheria ya manunuzi ya umma na kwamba hakukuwa na wizi katika ununuzi huo lakini jaji huyo akuzingatia ansard hiyo.

Sababu ya pili ni kwamba Mwangesi kuwa alivunja sheria ya Ushahidi ya mwaka 2002 wakati akipokea ushahidi wa shahidi wa jamhuri kwa njia ya video na kwamba shahidi huyo ambaye ni wakili wa Italia alitoa ushahidi wake katika kesi hiyo inayoendeshwa hapa nchini akiwa nchini Italia, jambo kitendo ambacho kinakiuka sheria hiyo ya ushahidi.
“Wewe Jaji Mwangesi ulipindisha makusudi sheria hiyo na kuchukua ushahidi wa shahidi huyo kwa njia ya video wakati sheria ya nchi hii inakataza na ndiyo maana hivi sasa serikali inapeleka muswaada bungeni wa kuifanyia marekebisho sheria ya sasa hili sheria hiyo mpya ikitungwa ndiyo itakuwa ikiruhusu mahakama kuchukua ushahidi kwa njia ya video”alidai Marando.

Sababu ya tatu ya kumtaka ajitoe ni kwamba tangu mapema upande wa washtakiwa waliuomba upande wa Jamhuri uwatajie mlalamikaji wa kesi hiyo na upande wa Jamhuri ulishawahi kuieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo haina mlalamikaji lakini jaji huyo alishtusha na kauli hiyo ya Jamhuri na akaiarisha kesi na kuwautaka upande wa jamhuri ukamlete mlalamikaji na mwisho wa siku jamhuri ilienda kuleta nakala ya nusu kurasa ya maelezo ya mlalamikaji ambaye ni akisa wa TAKUKURU,na mbaya zaidi jamhuri hadi inafunga kesi yao hakuweza kumleta mlalamikaji huyo kutoa ushahidi wake mahakamani.

“Kwa hiyo sisi upande wa utetezi tunasema kwa kitendo cha wewe Jaji Mwangesi kuung’ang’ania upande wa Jamhuri walete mlalamikaji wa kesi hiyo huku upande wa Jamhuri ulishawahi kumleleza kuwa kesi hiyo haina mlalamikaji kimetunyima fursa sisi kuwasilisha ombi la kutaka kesi hiyo ifutwe kwasababu ilikuwa haina mlalamikaji”alidai Marando.
Sababu ya nne ni kwamba jaji huyo aliunyima haki upande utetezi wa kuwasilisha majumuisho ya kuwaona hawana kesi ya kujibu pale jaji huyo kwa malengo yake anayoyajua yeye siku Jamhuri ilipofunga kesi yake na ndipo siku hiyo hiyo akatoa uamuzi wa kuwaona washtakiwa wanakesi ya kujibu.
“Sababu ya tano ya kukataa jaji wewe ni kwamba wewe unasikiliza kesi hii kama hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwasababu mahakama zote zina mipaka ya ardhi ya kufanyakazi zake isipokuwa Jaji Mkuu anaweza kutoa kibali maalum kwa mahakama husika kusikiliza kesi iliyo nje ya mamlaka yake … lakini wewe mheshimiwa jaji hukupata kibali cha Jaji Mkuu na ukadiriki kupokea ushahidi wa shahidi wa Jamhuri aliyekuwa nchini Italia kwa njia ya video jambo ambalo tunaliona ulikiuka makusudi sheria za nchi kwa malengo yako binafsi.”alidai Marando.
Alitaja sababu ya sita ni kwamba alikiuka kwa makusudi sheria za Tanzania kwakukubali kwake kupokea nakala kivuli ya mkataba wa mauzo ya ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Italia kama kielelezo toka kwa shahidi wa Jamhuri ambaye ni wakili wa nchini italia ambaye alikuja hapa nchini kutoa ushahidi ambapo shahidi huyo aliambia mahakama kuwa kwa mujibu wa sheria za Italia hazimruhusu yeye kuutoa mkataba halisi na jaji huyo akakubaliana na hoja ya shahidi huyo wakati sheria za Tanzania zinakataza hilo na kwamba alikubali kupokea kielelezo hicho ambacho kiliandaliwa na shahidi huyo mwenyewe ambaye ni wakili huyo wa Italia wakati sheria za Tanzania zinakataza mkataba unaondaliwa na mwanasheria husika zisibitishwe na mwanasheria huyo huyo bali zikathibitishwe na mwanasheria mwingine.
Jaji Mwangesi badala ya kusikiliza hoja hizo aliairisha kesi hiyo hadi Jumatatu Machi 28 mwaka huu, ambapo atatoa uamuzi wa kujitoa au kutojitoa katika kesi hiyo.
Mapema mwaka 2006 ,Jamhuri alimfikisha Mahalu na Martin katika mahakama hiyo wakidai manunuzi ya jengo hilo hayakufuata sheria za manunuzi, na kwamba waliibia serikali kiasi hicho cha fedha kwaajili ya ununuzi wa jengo hilo.

Chanzo Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Machi 26 mwaka 2011.

KESI YA MANJI Vs MENGI: JALADA LATUA KORTI KUU

Na Happiness Katabazi
JALADA la kesi ya madai ya kashfa ya shilingi moja iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mfanyabiashara Yusuf Manji dhidi ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Ltd, Reginald Mengi na ITV, limetua rasmi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika toka ndani ya Mahakama Kuu vililithibitishia gazeti hili kuwa jalada hilo limefika mahakamani hapo jana asubuhi likitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Vyanzo hivyo vilibainisha kuwa chanzo cha jalada hilo kuitwa katika mahakama hiyo ya juu ni kutokana na barua ya Februali 23 mwaka huu, iliyoandikwa na wakili wa mdaiwa(Mengi),Michael Ngaro kwa Jaji Mfawidhi Semistocles Kaijage ambapo ndani ya barua hiyo Ngaro anamuomba Jaji Kaijage alipitie mwenendo mzima wa kesi hiyo kwani hakimu mkazi anayeisikiliza kesi hiyo na akatolea maamuzi mbalimbali Alocye Katemana alionesha kuupendelea upande wa mlalamikaji(Manji).

“Nakukuakishia kuwa ni wakili wa Mengi ndiye aliyemuandikia Jaji Mfawidhi Kaijage barua ya malalamiko kwamba Hakimu Mkazi Katemana ameonekana kupendelea upande na jalada hilo limefika leo hapa Mahakama Kuu na hivi lipo mbioni kupelekwa kwa Jaji Kaijage ili aweze kuyafanyia kazi maombi ya wakili wa Mengi”kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo alipotafutwa wakili Ngaro ili athibitishe taarifa hizo hakuweza kupatikana kwani simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.Na gazeti hili lilipomtafuta wakili wa Manji, Mabere Marando alithibitisha kuwepo kwa taarifa hizo za wakili Ngaro kuwasilisha malalamiko hayo Mahakama Kuu lakini hata hivyo kwa upande wao wanachosubiri ni kuitwa na mahakama.

Februali 15 mwaka huu, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Katemana alitupilia mbali ombi la Mengi lililotaka mahakama hiyo iwapatie nakala ya uamuzi iliyoutoa Februali 11 mwaka huu,wa kuzikataa nyaraka 14 zikiwemo zinazoihusu kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd ambazo mdaiwa zinauhusiano na Manji, ili aweze kwenda Mahakama Kuu kuomba ufanyiwe mapitio kwa sababu Sheria ya Mabadiliko ya Sheria ambazo zimeandikwa Na. 25 ya mwaka 2002, inakataza upande wowote katika kesi yoyote kwenda mahakama ya juu kupinga amri za muda zinazotolewa na mahakama ya chini hadi kesi ya msingi itakapomalizika na kutolewa hukumu.
Mapema mwaka 2009, Manji alimfungulia kesi ya madai ya kashfa Mengi na kituo cha televisheni cha ITV akitaka amlipe fidia ya shilingi moja kwa madai kuwa Mengi alitumia televisheni yake kumkashfu kwa kumuita ‘Fisadi Papa’ na kwamba mmoja wa watu wanaopora rasilimali za Tanzania.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Machi 24 mwaka 2011.

ZUNGU:KORTI ITUPE OMBI LA TAO

Na Happiness Katabazi

MBUNGE wa jimbo la Ilala(CCM) Musa Azzan ‘Zungu’ amewasilisha pingamizi la awali katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi la aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo katika Uchuguzi Mkuu wa mwaka 2010,Hamad Tao linalotaka mahakama hiyo imsamehe kulipa dhamana ya kesi hiyo.

Katika kesi hii ya Uchaguzi Na.104/2010, Tao ambaye hana wakili anamshtaki mbunge wa Jimbo hilo Mussa Azzan anayetetewa na wakili wa kujitegemea Joseph Tadayo, aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao wanatetewa na wakili wa serikali Rashid Karimu.Katika kesi ya msingi Tao anaimba mahakama itengue ubunge wa Zungu kwasababu hakushinda kihalali na taratibu za sheria ya Uchaguzi zilikiukwa.

Kesi hiyo ambayo ilikuja jana kwaajili ya kutajwa mbele ya Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi wakili wa mdaiwa Zungu(Tadayo) aliambia mahakama amewasilisha pingamizi dhidi ya mlalamikaji(Tao) la kutaka mahakama ikatae ombi la mlalamikaji lakutaka mahakama hiyo itoe amri ya kumsamehe asilipe dhamana ya kesi hiyo ambayo ni sh milioni tano kwa kila mdaiwa;

“Tunaomba ombi la Tao litupwe kwasababu sheria ya Uchaguzi tya mwaka 2002 hairuhusu mahakama kumsamehe mlalamikaji asilipe dhamana ya kesi ya uchaguzi aliyoifungua dhidi ya wadaiwa…hivyo tunasisitiza ombi la mlalamikaji litupwe na mahakama hii imuamulu mlalamikaji huyo alipe sh milioni tano kwa kila mdaiwa aliyemshtaki”alisema wakili Tadayo.

Kwa upande wake Msajili Msumi alimtaka Machi 28 na akaiarisha kesi hiyo Aprili 5 mwaka huu , ili mahakama hiyo ije kusikiliza pingamizi hilo la awali lilowasilishwa jana asubuhi na mdaiwa ambaye ni mbunge wa Ilala Azzan.

Wakati huo huo ; kesho mahakama hiyo itaanza kusikiliza ombi la aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha NCCR-Mageuzi,James Mbatia linaloiomba mahakama hiyo impangie kiwango nafuu cha fedha za kuweka dhamana mahakamani kwaajili ya kesi ya kupinga ubunge mbunge wa sasa wa jimbo jilo Halima Mdee(Chadema) na wenzake.

Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi ambaye amepangwa kusikiliza katika hatua za awali kesi za uchaguzi wa majimbo ya mkoa wa Dar es Salaam,alisema kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kupangiwa tarehe ya mahakama kusikiliza ombi la mlalamikaji(Mbatia) anayetetewa na wakili wa kujitegemea Mohamed Tibanyendera, pia alimwamuru wakili wa Mdee, Edson Mbogoro ambaye jana ndiyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuudhuria kesi hiyo tangu ilipofunguliwa aakishe hadi saa tisa jioni jana awe amewasilisha mahakamani majibu ya kiapo cha Mbatia.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 23 mwaka 2011.

KUBADILI SHERIA,KUNUNUA MITAMBO YA DOWANS NI KUTOHESHIMU UTAWALA WA SHERIA

Na Happiness Katabazi

KUBADILISHA Sheria ya Manunuzi Umma ya mwaka 2004 ili serikali iweze kuinunua mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, ndiyo ufisadi wenyewe na kutoheshimu utawala na dhima nzima ya utawala wa sheria(Rule of Law).

Wahenga walisema ni bora kuchakaza nguo kuliko kuchakazi akili.Sasa ni wazi kuwa baadhi ya viongozi wetu na wataalamu wetu waliopo serikalini wamechaka akili zao.

Na hilo linadhibitisha jinsi miongoni mwao wanavyong’ang’ania ufisadi na kujaribu kwa kila namna kuupa rangi au kuubatiza jina jipya kila siku,.

Kila mtu mwenye akili timamu za kung’amua mambo na akashuhudia kashfa ya Richmond , hanajua kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliunda Kamati maalum ya kuchunguza jambo hilo iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk.Harrison Mwakyembe na kamati hiyo hatimaye iliwasilisha ripoti yake na bungeni.

Na ilipojadiliwa kwa mapana na ikadhihirika wazi kwamba Richmond ni kikundi feki ambacho wala hakikuwa kampuni yenye hisa Marekani wala Tanzania na kwamba tenda ya serikali ya kufua umeme wa dharula ilitolewa kwa kikundi kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004.
Mara baada ya bunge kumaliza kuijadili ripoti ya Kamati ya Dk.Mwakyembe, maamuzio yake yalipelekea aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo Edward Lowassa, waliokuwa mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti, Nazir Karamagi na Dk.Ibrahim Msabaha walijiudhuru nafasi ya uwazi.

Lakini wajanja walio nyuma ya kampuni hizo wanadaiwa kuwa walijitahdi kuilazimisha Tanesco ama iridhie mrithi wa mkataba wa Richmond na Tanesco ajulikanae kwa jina la Dowans apewe uhalali.

Juhudi hizo zilishindikana kwa kipindi fulani mbunge wa Kigoma Kaskazini. (Chadema),Zitto Kabwe alijitokeza adharani na kutoa maoni yake kwamba mitambo ya Dowans inunuliwe kwa maslahi ya umma.Zitto hakulieleza taifa lina maslahi gani katika kununua mitambo hiyo ambayo inadaiwa kuwa ilishakwishatumika(used).

Cha msingi ni kwamba mitambo ya kufua umeme wa dharula inaundwa mipya viwandani na mnunuzi kuchagua kununua mitambo chakavu na uchagauzi wake ambao labda unasababishwa na ufukara wa kutokuwa na fedha za kununulia mitambo mipya.

Kumbe ikiwa mitambo mipya inauzwa sokoni na hakuna sababu ya taifa letu kununua mitambo iliyokwishatumika.Hivyo maslahi ya umma aliyokuwa anayazungumzia Zitto hatuyajui ni yapi.

Leo hii imezuka hoja kuhusu mitambo ya Dowans.Wanasema iwashe wanaangalia hali ya sasa ya kutokuwepo umeme wa kutosha.Hao hawajali kuwa hali ya mgao wa umeme imekuwa ikitokea kila mwaka hata kabla ya mitambo ya kufua umeme ya Dowans kuingizwa hapa nchini.

Hivi megawati 100 za Dowans zinaweza kusaidia nini kuondoa tatizo hili la katizo la umeme hapa nchini?Tukubali kwamba sekta ya nishati imeendeshwa vibaya na baadhi ya watu wasiyo na upeo ambao hawatangulizi maslahi ya taifa mbele.
Hivi kweli tangu mwaka 2006 serikali imeshindwa kununua hata mitambo mipya kumi tu, hadi inasubiri hicho kibiriti cha Dowans?

Sasa tujadili ambalo limezuka sasa ambalo linadaiwa kuwa serikali ipo mbioni kupeleka mswaada bungeni ili sheria ya Manunuzi ya Umma ibadilishwe ili iweze kuinunua mitambo hiyo.Sheria hiyo ya sasa inaizuia serikali kununua mitambo au bidhaa zilizokwishakutumika.Na hiyo ni kuakikisha inaziba mianya ya rushwa.

Binafsi nachelea kusema serikali iununue mtambo huo kwasababu zifuatazo;
Utawala wa Sheria hauruhusu sheria itungwe inayomlenga mtu mmoja au kikundi cha watu.Sheria ya namna hiyo ni mbaya(Bad Law).Mabadiliko hayo yakifanywa yatakuwa yanalenga mitambo ya kufua umeme iliyopo Ubungo ambayo ni mali ya Dowans.

Je! baada ya kuitunga sheria hiyo, tutatunga sasa sheria ya kuifuta hiyo sheria mpya ili turejee kwenye sheria yetu nzuri ambayo inakataza kununua vitu ambavyo vimekwishatumika?

Na ikiwa ni hivyo hao baadhi ya maofisa wa serikali akili zao ni nzuri?Kimsingi wana jamii wanasema watu wengine si lazima wafanyekazi serikali kama akili zao haziwatoshi .Waache kazi serikali wasitualibie nchini.

Ikiwa watang’ang’ania hayo tutaendelea kuwanyoshea vidole kwa haki na kwamwe wasidhani wanajamii wa taifa hili hatujui utawala bora nini.

Mungu Ibariki Tanzania , Mungu Ibariki Afrika.
0716 774494


Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 22 mwaka 2011.

KESI YA WIZI WA GARI LA DPP:SITA WAFUTIWA SHITAKA LA UNYANG'ANYI

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imewafutia shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha washtakiwa sita katika kesi unyanganyi wa kutumia silaha, kupokea mali za wizi na wizi wa gari na kompyuta mali ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DDP) vyenye jumla ya thamani ya shilingi sh 111,500,000.


Sambamba na hilo Hakimu Mkazi Jenevitus Dudu ambaye ndiye anasikiliza kesi hiyo ambayo ina jumla ya washtakiwa 12, pia amewaachilia huru washtakiwa watatu ambao walikuwa wakikabiliwa na kosa la kupokea mali za wizi baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.

Hakimu Mkazi Dudu alisema baada ya kuuchambua ushahidi wa uliwasilishwa na wakili mwandamizi wa serikali Timon Vitals amebaini kuwa ushahidi huo umeshindwa kuthibitisha kuwa washtakiwa sita , Ally Mustapha,Haji Mwanga,Bakari Makala,Deogratius Chuwa, Philipo Jose na Abubakar Kamugisha ambao ndiyo walikuwa wakikabiliwa na shtaka moja la unyang’anyi wa kutumia silaha ambalo kwa mujibu wa sheria halina dhamana kuwa hawakutenda kosa na hivyo akawafutia kosa hilo na kufanya washtakiwa hao wakibaki wakikabiliwa na makosa mawili ya wizi na kupokea mali za wizi.

Hakimu Dudu alisema baada ya kupitia ushahidi wa Jamhuri pia amefikia uamuzi wa kuwaona washtakiwa wanne, Antony Mengi, Wilfred Maleko,Alex Kimaro na Hajat Kileo waliokuwa wakikabiliwa na kosa la wizi wa mali hizo kuwa hawana kesi ya kujibu chini ya kifungu cha 291 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.Na hivyo kuwaona washtakiwa wawili, Mary Lyimo na Jacob Mosha kuwa wana kesi ya kujibu katika kosa wizi wa mali hizo hivyo wanapaswa wajitete.

“Mahakama hii imefikia uamuzi huo kama nilivyouanisha hapo juu kwenye kesi hii iliyokuwa ikiwakabili jumla ya washtakiwa 12 kwasababu jamhuri imeshindwa kuthibitisha shtaka la unyang’anyi kwa washtakiwa sita, bila limeshindwa kuthibitisha shtaka la kukutwa na mali za wizi kwasababu mahakama hii imeona washtakiwa hao wanne ambao walikuwa wakikabiliwa na kosa hilo la kukutwa na mali za wizi hawakuwa wakifahamu mali hizo ni za wazi na pia mahakama hii imewaona washtakiwa nane wana kesi ya kujibu katika shtaka la wizi na kukutwa na mali za wizi.

Baada ya Hakimu Dudu kutoa uamuzi huo , Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP), Eliezer Feleshi aliwasilisha mahakamani hapo hati ya kuzuia dhamana kwa washtakiwa sita walifutiwa shtaka la unyang’anyi kwa kutumia silaha ambalo kwa mujibu wa sheria za mwenendo wa makosa ya Jinai ya mwaka 2002, shitaka hilo halina dhamana na Wakili wa Serikali Zuberi Mkakati naye akawasilisha mahakamani hapo hati ya kusudio ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu dhidi ya uamuzi wa hakimu huyo.

Aidha kwa upande wake Hakimu Dudu baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha hati hizo mbili, alisema leo kesi hiyo ilikuja kwaajili washtakiwa sita kutimiza masharti ya dhamana lakini kwakuwa DPP amewasilisha hati ya kufunga dhamana kwa washtakiwa hao akasema anaiarisha kesi hiyo hadi Aprili nne mwaka, ili kuipa nafasi ya hati hiyo ya DPP ambayo inazuia washtakiwa hao wasipewe dhamana na na akaamuru washtakiwa hao kurejeshwa rumande.

Hata hivyo baadhi ya ndugu na jamaa wa washtakiwa ambao wamesota rumande tangu mapema mwaka 2009 hadi sasa,waliokuwa wamefika mahakamani hapo kwaajili ya kukamilisha taratibu za kuwadhamini washtakiwa, walijikuta wakiangua vilio baada ya kusikia jamhuri imewasilisha hati ya kukataa rufaa na DPP kuwasilisha hati mahakamani ya kuzuia washtakiwa hao wasipewe dhamana.

Mapema mwaka 2009 mahakamani hapo Inspekta Emma Mkonyi alidai kuwa Machi 5 mwaka huo, huko Tabata Liwiti CCM, Kamugisha aliiba gari STK 5002 Toyota Hiace modeli mpya lenye thamani ya sh 56,972,000, komyuta sita zenye thamani ya sh 4,250,000, printa zenye thamani ya sh 7,435,000, seti ya UPS, laptop na vitabu vya sheria mali ya ofisi ya DPP na vitu vyote hivyo vikiwa na jumla ya thamani ya sh 111,500,000.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Machi 19 mwaka 2011.

SHAHIDI:DECI WALIKUWA WAKIWEKA FEDHA UVUNGUNI

Na Happiness Katabazi

MRAKIBU wa Polisi(SP) Suleiman Nyakulinga ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa katika upelelezi wao Jeshi la polisi liligundua viongozi wa matawi ya mikoani ya Taasisi ya Entrepreneurship for Community Initiative(DECI)walikuwa wanaifadhi fedha za wananchama uvunguni na kwenye droo za ofisi badala ya benki.

SP-Nyakulinga ambaye ni mpelelezi toka Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ni shahidi wa sita wa upande wa Jamhuri na aliyatoa maelezo hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Stewart Sanga wakati akihojiwa na mawakili wa utetezi Onesmo Kyauke na Hudson Ndusyepo.

Shahidi huyo alieleza mahakama kuwa Juni 2009, Jeshi la Polisi ndiyo serikali ilizikamata akaunti zote za DECI na hapo ndipo jeshi la polisi lilipanza uchunguzi wake kwa matawi ya DECI kote mikoani na kubaini kuwa matawi ya mikoani yalikuwa yakiifadhi fedha hizo za mchezo haramu wa upatu zilikuwa zikiifadhiwa uvunguni na kwenye droo za ofisi na kuongeza kuwa pia uchungizi wao ulibaini kuwa DECI haikuwa na leseni ya biashara hivyo haikuwa imealalishwa kama kampuni.

Akijibu swali la wakili wa utetezi Kyauke lilitaka kufahamu ni kwanini polisi walifikia uamuzi wa kuwakamata washtakiwa hao badala ya kuishtaki kampuni hiyo , shahidi huyo alidai kuwa yeye ndiye aliyemhoji mshtakiwa wa kwanza na wapili na kwamba hawajawahi kumweleza kwamba ni mawakala wa DECI hivyo ndiyo maana polisi wakamaamua kuwakamata.

Aidha alipotakiwa ajibu swali ni kabla ya polisi kuzifunga akaunti za DECI, kuna mwanachama wa DECI alishafika polisi kulalamika kwamba wamedhulumia fedha zao taasisi hiyo, shahidi huyo alidai kuwa hawakuwai kupokea malalamiko ya wanachama wa taasisi hiyo kudhulumiwa fedha zao.Kesi hiyo iliairishwa hadi leo ambapo shahidi wa saba wa upande wa Jamhuri ataanza kutoa ushahidi wake.

Mwaka 2009, washtakiwa katika kesi hiyo ni Jackson Mtares, Dominic Kisendi, Timotheo ole Loitgimnye, Samuel Mtares, Arbogast Kipilimba na Samuel Mtalis,walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na Jamhuri ilidai kuwa washtakiwa wanamakosa ya kuendesha na kusimamia mradi wa upatu kinyume na sheria pamoja na kupokea amana za umma bila leseni na Na upande wa Jamhuri unawakiliwa na Mwanasheria wa Kanda ya Dar es Salaam, Justus Mulokozi na Prosper Mwangamila.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Machi 18 mwaka 2011.

GULAM DEWJI ABURUZWA KORTINI

Na Happiness Katabazi

SHIRIKA la Nyumba la Taifa(NHC), imeiburuza katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ,Bodi ya Udhamini ya Federation of Khoja Ithna-Asheri Jamaats of Afrika na mfanyabiashara maafuru nchini Gulambhai Dewji wakiomba mahakama hiyo itamke jengo lililopo kitalu Na.39 mtaa wa Chuma-Chang’ombe jijini hapa ni mali halali ya shirika hilo na si la wadaiwa hao.

Kesi hiyo ya madai namba 23 ya mwaka huu na tayari imeishapangwa kuanza kusikilizwa mbele ya Jaji Chingilwe Machi 24 mwaka huu, mlalamikaji(NHC) anatetewa na wakili wa kujitegemea Jerome Msemwa na tayari mahakama hiyo imeishatoa hati za wadaiwa kuitwa mahakamani siku hiyo.

Kwa mujibu wa hati ya madai ambayo gazeti hili inayo nakala yake, mlalamikaji ambaye amefungua kesi hiyo chini ya hati ya hati ya dharula , na Mwanasheria wa Shirika hilo la Nyumba nchini, Martin Mdoe ndiye amekula kiapo kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa (NHC), anaiomba mahakama hiyo itamke kuwa jengo hilo ambalo lina thamani ya zaidi ya bilioni mbili ni mali ya shirika hilo.

Shirika hilo linadai jengo hilo ni mali yake na si mali ya mdaiwa wa kwanza kama mdaiwa huyo wa pili alivyojiingiza kwenye umiliki wa jengo hilo Oktoba 23 mwaka jana kwa njia ya udanganyifu na kughushi.

“Tunaiomba mahakama hii itamke wadaiwa hao siyo wamiliki halali wa jengo lile kwani hata mwaka 1971 serikali ilipotoa amri ya kuyataifisha majengo hapa nchini jengo hilo lilikuwa likimilikiwa na Albai Punja Khoja Shia Education Trust na hata lilipotaifishwa mmiliki huyo Albai Punja Khoja Shia Education Trust ndiyo April 27 mwaka 1992 ndiyo aliyeandika barua kwa rais wa awamu ya pili, All Hassan Mwinyi awarejeshee jengo hilo;

“Lakini ilipofika Januari 1996 serikali ya Tanzania kupitia aliyekuwa Waziri Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi , alibatirisha agizo la rais Mwinyi lilokuwa limekubali maombi ya baadhi ya waliokuwa wamiliki wa majengo hayo yaliyotaifishwa na serikali na kuongeza kuwa mdaiwa wa kwanza hakuwai kuwa miongoni mwa waliopeleka maombi kwa Mwinyi wala wizara ya Ardhi yakuomba arejeshewe jengo kwasababu hakuwahi kuwa mmiliki wa jengo hilo”alidai Msemwa.

Aidha alidai kuwa Oktoba 23 mwaka jana , mdaiwa wa kwanza alikwenda wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kubadilisha hati inayoonyesha jengo hilo ni mali yake na mdaiwa huyo akamteua mdaiwa wa pili Gulambahi Dewji kwa barua ya Agosti 4 ya mwaka jana ambayo imesainiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Federation of KLhoja Ithna-Asheri Jamaats of Afrika, Anwaralui Dharamsi ya kumtoa kwenye jengo hilo mpangaji ambaye alikuwa amepangishwa kihalali na NHC, ambaye ni M/S FAZAL&CO.LTD agizo ambalo mdaiwa wa pili mdaiwa wa pili alilitekeleza kwa vitendo.

Aidha Msemwa katika hati hiyo ya madai anaeleza kuwa sababu nyingine iliyosababisha mteja wake kuamua kuwaburuza mahakamani wadaiwa hao ni kwamba mdaiwa wa kwanza ambayo ni bodi ya wadhamini ni kigeni na kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Tanzania inakataza kampuni ya kigeni kumiliki ardhi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Machi 17 mwaka 2011.

FAILI KESI YA MANJI,MENGI LAITWA KORTI KUU

Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeitisha jalada la kesi ya madai ya kashfa ya shilingi moja iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na mfanyabiashara Yusuf Manji dhidi ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Ltd, Reginald Mengi na ITV kwaajili ya kulipitia upya.


Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana wakili wa Manji, Dk.Ringo Tenga alisema kesi hiyo ambayo ilipangwa kuendelea kusikilizwa juzi na jana ilishindikana kusikilizwa na Mahakama ya Kisutu kwasababu wao wamepata taarifa kuwa jalada la kesi ya msingi limeitishwa Mahakama Kuu kwaajili ya kulikagua jarada hilo.


“Kama mlivyoona juzi na jana sisi mawakili wa mlalamikaji na nyie waandishi wa habari tulikaa sana pale mahakama ya Kisutu kusubiri mteja wetu (Manji)aendelee kutoa ushahidi wake lakini baadaye tukaja kupata taarifa kuwa jalada la kesi hiyo limeitishwa Mahakama Kuu na hatujui limeitwa kwaajili ya nini ila kwa mujibu wa sheria za nchi Mahakama Kuu ina mamlaka ya kuitisha jalada la kesi inayoendeshwa katika mahakama za chini….hivyo tunasubiri taarifa zaidi”alisema Dk.Tenga.

Alipotafutwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Semistocles Kaijage ili aweze kulizungumzia hilo alisema yupo safarini hivyo hayupo kwenye nafasi nzuri ya kulizungumzia hilo.


Februali 15 mwaka huu, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Alocye Katemana alitupilia mbali ombi la Mengi lililotaka mahakama hiyo iwapatie nakala ya uamuzi iliyoutoa Februali 11 mwaka huu,wa kuzikataa nyaraka 14 zikiwemo zinazoihusu kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd ambazo mdaiwa zinauhusiano na Manji, ili aweze kwenda Mahakama Kuu kuomba ufanyiwe mapitio.


“Nataka ieleweke kwamba mahakama inaongozwa na kutenda kazi zake kwa mujibu wa sheria na hivyo basi mahakama hii inatupilia mbali ombi la mdaiwa (Mengi) lililotaka apatiwe nakala ya uamuzi wangu ili aweze kuomba upitiwe na Mahakama Kuu kwa sababu Sheria ya Mabadiliko ya Sheria ambazo zimeandikwa Na. 25 ya mwaka 2002, inakataza upande wowote katika kesi yoyote kwenda mahakama ya juu kupinga amri za muda zinazotolewa na mahakama ya chini hadi kesi ya msingi itakapomalizika na kutolewa hukumu.


“Sababu hiyo ya kimsingi na kisheria niliyoitoa hapo juu ndiyo imenisukuma kulitupilia mbali ombi hilo la mdaiwa (Mengi) la kutaka kwenda kuiomba Mahakama Kuu iupitie uamuzi wangu niliokwisha utoa kwa maana hiyo kesi hii itaendelea kusikilizwa katika mahakama hii ya Kisutu na hata sasa niko tayari kwa ajili ya kuanza kuisikiliza na imeamriwa hivyo na mahakama hii,” alisema Hakimu Mkazi Katemana kwa kujiamini.


Mapema mwaka juzi, Manji alimfungulia kesi ya madai ya kashfa Mengi na kituo cha televisheni cha ITV akitaka amlipe fidia ya shilingi moja kwa madai kuwa Mengi alitumia televisheni yake kumkashfu kwa kumuita ‘Fisadi Papa’ na kwamba mmoja wa watu wanaopora rasilimali za Tanzania.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 16 mwaka 2011.

KWA HILI,JESHI LA POLISI LINASTAHILI SIFA

Na Happiness Katabazi

SALAAM! Wasomaji na wapenzi wote wa safu yangu ya FUKUTO LA JAMII ambayo awali ilikuwa ikitoka kila siku ya Jumapili katika gazeti hili ila kwasababu zisizoweza kudhuhirika na zilizokuwa nje ya uwezo wangu,nimelazimika kuamishia safu hii kwenye gazeti letu litokalo kila kila siku ya jumanne hivyo.


Februali 23 mwaka huu, Serikali ilifikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, watu wanne wakiwemo raia wawili wa Pakstan wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama na kusafirisha kilo 179 za dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6.2. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Biswalo Mganga, mbele ya Hakimu Mkazi, Agustina Mmbando, aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Freddy Chonde na Kambi Zubery ambao ni Watanzania na Abdul Ghan Peer Bux na Shahbaz Malik ambao ni raia wa Pakstan, Februari 21, mwaka huu, maeneo ya Mtaa wa Jogoo, Mbezi Beach kwa pamoja washitak
iwa wote waliingiza nchini dawa za kulevya zenye uzito na thamani hiyo ya fedha.

Machi 7 mwaka huu, Jamhuri ilifikisha raia wengine wa nne wa kigeni katika mahakama hiyo wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kula njama na kuingiza dawa za kulevya zenye uzito wa aina gramu 81 zenye thamani ya Sh bilioni 2.8.

Mustapher Siyani wakili mwandamizi wa serikali Biswalo Mganga aliyekuwa akisaidiwa Prosper Mwangamila na Theophili Mtakyawa aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Dinnis Chukwudi Okechukwu,Paul Ikechukwu Obi ambao ni raia wa Naigeria, Stani Hycenth raia wa Afrika ya Kusini na Shoaib Mohammed Ayazi ambaye ni raia wa Pakstani.

Machi 9 mwaka huu, tena Jamhuri ilimfikisha kwa hakimu huyo , raia mwingine wa Nigeria , Luvinus Ajina Chime akikabiliwa na kosa la kuingia dawa za kulevya hapa nchini aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 810 na zina thamani ya Sh milioni 28.3.Mahakimu wote wanaosikiliza kesi hizo kwa nyakati tofauti waliwaeleza washtakiwa hawapaswi kujibu chochote kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hizo.

Kesi hizo tatu za dawa za kulevya ni miongoni mwa kesi kadhaa zilizokwishafunguliwa katika mahakama mbalimbali hapa nchini.

Hakuna ubishi kwamba uzito wa dawa huo ni mkubwa na kama watuhumiwa wangefanikiwa kuziingiza dawa hizo sokoni hapa nchini bila kukamatwa na askari wa Jeshi la Polisi wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya kinachoongozwa na Kamanda mzalendo, Godfrey Nzowa ni wazi washtakiwa hao wangepata fedha nyingi na baadhi ya vijana wetu wangezidi kualibiwa na dawa hizo.

Na hapa naomba ieleweke kwamba mada ya leo haitaingilia mwenendo wa kesi hizo tatu kwani mwandishi wa habari hizi si maamuma kihivyo wa sheria kwani ana fahamu vyema kesi ikishafikishwa mahakamani hakuna mtu yoyote anayepaswa kuizungumzia na kwamba mtuhumiwa atabaki kuwa mtuhumiwa hadi pale mahakama ikapotoa hukumu dhidi yake.

Hivyo kilichonisukuma kuandika mada hii ni kutaka kukipongeza Kitengo hicho kinachoongozwa na Kamanda Nzowa pamoja na askari wa kitengo hicho nchi nzima, kwani hivi sasa tunashuhudia kasi ya watu wanaotuhumiwa kuingiza dawa za kulevya nchini wakikamatwa na kufikishwa mahakamani ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Licha watu hao ambao ukamatwa na askari wa kikosi hicho hawana majina makubwa wala wafanyabishara wakubwa nchini,kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na wengi kwamba baadhi ya matajiri na wafanyabiashra wa kubwa ndiyo wanaongoza kuuza dawa hizo lakini sisi tusiopenda ‘longolongo’ , tunaziamini taarifa zinazotolewa na Kitengo hicho ambazo utolewa muda mchache baada ya kuwakamata watuhumiwa hao na dawa na si uvumi unaozagaa mitaani.

Pili, natoa pongezi kwa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)-Elizer Feleshi kwa kufanyakazi kama timu na kitengo hicho cha polisi kwa kuwafungulia mashtaka washtakiwa wanaokabiliwa na kesi za aina hiyo.Kwa kuwa sote tunafahamu kuwa hivi sasa polisi kazi yake ni kuchunguza na kukamata na ofisi ya DDP ni kuwafungulia mashtaka washtakiwa, tofauti na zamani kwani polisi ndiyo waliokuwa wanapeleleza,wanakamata na wanaendesha kesi mahakamani .

Ni kweli hayo ni majukumu yanapaswa kufanywa na kitengo hicho na ofisi ya DDP.Lakini safu hii inasema kwamba licha hayo ni miongoni mwa majukumu yao inapenda kuwapongeza kwani kama askari wa kitengo hicho kinachoongozwa na Kamanda Nzowa wangekuwa ni wachumia tumbo na wanatamaa ni wazi wangechukua rushwa kwa washtakiwa na wangewaruhusu washtakiwa hao kuondoka na dawa hizo na mwisho wa siku huyo Nzowa,Feleshi na sisi wananchi tusingejua kilichokuwa kikiendelea.

Dawa za kulevya ni miongoni mwa jinamizi kubwa linaloangamiza taratibu kizazi na nguvu kazi ya taifa hili.Kwakuwa sote ni mashahidi tunapopita mitaa ya Kinondoni, Buguruni, Manzese-Shidele, Mananyamala, Shekilango, Temeke,Ubungo Standi na huko mikoani utawakuta vijana wetu ambao ni watumiaji wa dawa hizo haramu wakiwa wamelewa hata asubuhi hawajitambui, sura zao zimegeuka kuwa kama mababu wanaoishi Mwituni.Inasikitisha sana na kukera pia.
Lakini taifa wakati nguvu kazi yake hiyo ikizidi kuangamia kwa dawa hizo, watu wazima ambao ndiyo wafanyabiashara wa dawa hizo ndiyo vipato vyao vinazidi kukukua kutokana na vijana hao kununua dawa hizo kwa wingi.Inasikitisha sana.

Ndiyo maana nilivyoona kasi ya hivi karibuni ya kukamatwa kwa watuhumiwa wa dawa za kulevya na kuburuzwa mahakamani inaongezeka,nikalazimika kuandika makala ya kupongeza kitengo hicho na ofisi ya DPP .Naamini kasi ya ukamataji ikiongezeka naye DPP akaaongeza kasi ya kuwafungulia kesi na sisi wanahabari wa habari za mahakama nchini tukaongeza nguvu ya kuripoti kesi hizo, ni wazi watuhumiwa wengine wanaofanyabiashara hiyo wataogopa kama sikuiacha kabisa.

Ikumbukwe kwamba wahalifu nao kila kukicha wana buni mbinu mbadala za kukabiliana na mkono wa dola wakati wa kuingiza na dawa hizo nchini.Na biashara hiyo haramu wameigeuza kuwa ndiyo ajira yao rasmi ambayo inawaingizia kipato cha kuishi na kuwaliopia ada watoto.Hivyo ni vyema serikali sasa iamke na ikatae nchi yake kugeuzwa shamba la bibi na baadhi ya wageni ambao wakuwa wakiingiza dawa za kulevya ambazo zinakuja kuteketeza kizazi cha taifa hili.Kwa kukiongezea fedha , mafunzo kwa askari wa kikosi cha kuzuia dawa za kulevya.
Kwakuwa inauma kuwaona vijana wadogo wakikatisha masomo yao kwaajili ya kuharibiwa na dawa hizo.Siku zote minaamini taifa ambalo wananchi wake hawana elimu ni wazi taifa hilo litakuwa ni taifa tegemezi.

Baada ya kuyasema hayo napenda kutoa angalizo kwa Kitengo hicho kwamba wasiishie kuwakamata waingizaji wa dawa za kulevya tu , bali pia wawageukie wauzaji wadogo ‘wazungu wa unga,mapusha’ , hao uishi mitaani kwetu na hao ‘mateja’ uenda kwa hao kununua kete hizo za dawa na kisha kubwia au kujidunga.Na kama hamjui wanapatikana mitaa gani ni vyema mkaunda urafiki na mateja waliozagaa kwenye vituo vya basi watawaonyesha ni wakinanani wanawauziaga dawa hizo.Tunachokishuhudia sasa mmeelekeza nguvu nyingi katika kuwakamata wanaoingiza dawa hizo nchini.

Kingine ambacho ningependa kifanywe na kitengo hicho nikuwakamata mateja wote wanaorandaranda mitaani hasa kwenye vituo vya mabasi na baadhi ya wanamuziki hawa muwapeleke hospitali wakachukuliwe vipimo ili kuona kama kweli ulevi wao una tokana na matumuzi ya dawa hizo za kulevya na kama hakuna sheria ya kuwashughulikia walaji wa dawa hizo basi sote tuone haja ya bunge letu kutunga sheria ya kuwabana walaji wa dawa hizo maarufu kama kwa majina ya ‘mateja,wala unga’.

Kama ripoti za madaktari zitathibitsha ulevi wao unatokana na dawa za kulevya, hivi hatuoni haja sasa ya Sheria ya Kuzuia Dawa za Kulevya ya mwaka 2002; inaongezewa makali ya kuwabana vilivyo hata walaji dawa hizo kwa siri lakini adharani wanaonekana wamelewa?Kwani hivi sasa tunachokishuhudia wanaokamatwa ni waingizaji na wasafirishaji, walaji wa dawa hizo hawakamatwi na wengine wanafahamika kabisa kwamba ni walaji wazuri wa dawa hizo.

Nasema hivyo kwasababu wala unga kwa kificho halafu wanalewa adharani hatuwaoni, ulevi wao huo mwisho wa siku vijana ambao ni wepesi kurubunika wanatajikuta wanarubunika kwa kutamani kutumia ulevi huo?.

Angalizo jingine nalitoa kwa mawakili wetu wa serikali mtakapowea jukumu la kuendesha kesi hizi za dawa za kulevya, nanyi tunaomba mziendeshe kesi hizi kwa kutanguliza haki na siyo tamaa za kupenda kuhongwa fedha na ndugu wa washtakiwa ili muweze kuzivuruga hizo kesi mwisho wa siku washtakiwa waokoke kwenye mkono wa dola.

Kwani tayari kuna malalamiko ya chini chini toka kwa baadhi ya askari polisi kwamba wao wamekuwa wakijitahidi kufanyakazi yao ya upelelezi vizuri tu lakini baadhi ya mawakili wa serikali wenye hulka za kifisadi wamekuwa wakiziaribu kesi hiyo kwaajili kupokea rushwa.Narudia tena sitaki kuingilia kazi ya mahakama lakini napenda kuona haki inatendeka na kila mmoja wetu anatimiza majukumu yake ipasavyo katika kuakikisha taifa hili linapambana na biashara hii haramu ya dawa za kulevya.

Hapa Dar es Salaam, sasa hivi imeanza kuwa sifa moja wapo ajira ya kupiga debe lazima uwe ‘teja’ na yote hayo tunayaona hakuna mamlaka inayochukua hatua.Kama ilivyoongezwa makali makosa ya utakatishaji fedha haramu ndivyo tunavyotaka sheria ya kuzuia dawa za kulevya iongezewe makali.Kwani adhabu nyepesi kama kifungo au faini za wanazopewa watuhumiwa wa kesi hizo pindi wanapitiwa na mahakama ndiko kunako wapa jeuri ya kutoogopa ya kuendelea kufanya biashara hiyo haramu ambayo inatuharibia nguvu kazi ya taifa.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 15 mwaka 2011.

MPENDAZOE ALIPA KORTINI SH MIL 15/-

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE aliyekuwa Mgombe Ubunge wa Jimbo la Segerea (Chadema),Fred Mpendazoe amelipa sh milioni 15 katika Idara ya Fedha ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam ikiwa ni dhamana ya kesi yake ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa jimbo uliofanyika mwaka jana ambayo yalimtangaza Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk.Makongoro Mahanga (CCM) kuwa ndiye mbunge wa jimbo hilo.

Mbali na Dk.Mahanga wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo na katika madai yake mlalamikaji ambaye ni Mpendazoe anataka mahakama kuu itengue ushindi wa Dk.Mahanga kwakuwa taratibu za sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010 hazikufuatwa.

Wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala jana ndiye aliyekwenda idara ya hiyo ya fedha iliyopo ndani ya jengo la Mahakama ya Rufani nchini kulipa kiasi hicho cha fedha na kuwaonyesha waandishi wa habari risiti ya malipo hayo.

“Hii ndiyo risiti ya kiasi hicho cha fedha nilicholipa mahakamani kama dhamana ya kesi iliyofunguliwa na mteja wangu ….na kwakuwa tayari tumeishalipa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya kuupata udhibitisho wa malipo haya ndiyo atapanga tarehe ya kesi ya mteja wangu kuanza kusikilizwa rasmi kwani taratibu zote za kisheria tumeishazikamilisha”alisema wakili Peter Kibatala.

Machi nane mwaka huu, Jaji Profesa Ibrahimu Juma alitupilia mbali pingamizi la wakili Jerome Msemwa anayewatetea wadaiwa liloiomba mahakama hiyo imzuie Mpendazoe asiruhusiwe kuweka kiasi hicho cha fedha mahakamani kwasababu muda wa kuwasilisha fedha hizo ulikuwa umeishapita kwakuwa halikuwa limekidhi matakwa ya kisheria na badala yake akalikubali ombi la Mpendazoe kuweka mahakama kiaisi hicho cha fedha kama dhamana.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Machi 12 mwaka 2011

JERRY MURRO ANA KESI YA KUJIBU

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imemuona aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la TBC1, Jerry Murro na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya kula njama, kushawishi na kuomba rushwa ya sh milioni 10, kuwa wana kesi ya kujibu.


Uamuzi huo wa kushtua ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe ikiwa ni muda mfupi baada ya shahidi wa sita wa upande wa Jamhuri, D/C Koplo Lugano Mwampeta kumaliza kutoa ushahidi wake na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Stanslaus Boniface kueleza kuwa wamefunga ushahidi.

Baada ya Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Boniface kueleza hayo, Hakimu Mirumbe alisema anaahirisha kesi hiyo kwa dakika kumi, ili aweze kupitia jalada la kesi hiyo na ushahidi wote uliokwishatolewa na mashahidi sita wa upande wa jamhuri kisha atarudi kutoa uamuzi wa ama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la.

Ilipofika saa 6:47 mchana Hakimu Mirumbe aliingia kwenye chumba cha mahakama hiyo na kutoa uamuzi wake ambapo alisema baada ya kulipitia jalada la kesi hiyo mahakama imeona upande wa jamhuri umeweza kuthibitisha kesi yake na hivyo mahakama hiyo imewaona washtakiwa wote wana kesi ya kujibu.

“Baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri katika kesi hii mahakama imewaona washtakiwa wote mna kesi ya kujibu na ninaaharisha kesi hadi Machi 29 ambapo washtakiwa mtaanza kukjitetea,” alisema Hakimu Mirumbe.

Awali, shahidi wa sita, D/C Koplo Lugano Mwampeta akiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Boniface, kutoa ushahidi wake, alidai Januari 31, 2010 alikuwa ofisini katika ofisi za Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ambapo mkuu wake wa kazi ambaye ndiye mkuu wa upelelezi wa mkoa huo(RCO)-Duwani Nyanda alimpatia kazi.

Mwampeta alieleza kuwa RCO-Nyanda alimpatia kazi ya kumsaidia kulikagua gari la Murro ambapo kiongozi wake huyo ndiye aliyekuwa mkaguzi mkuu, ambapo katika ukaguzi kwenye gari hilo walipata miwani na pingu na wakati wakifanya upekuzi huo Murro alikuwa akishuhudia.

Mbali na Murro, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Edmund Kapama na Deogratius Mugasa ambao wanadaiwa Februari 15 mwaka jana walikula njama kushawishi na kuomba rushwa ya sh milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Karoli Wage. Kati ya mashtaka matatu yaliyofunguliwa dhidi yao, Murro anakabiliwa na mashtaka mawili.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 9 mwaka 2011.

ZOMBE AISHIKA PABAYA SERIKALI

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Mohamed Zombe(57),amemfungulia kesi ya madai ya fidia ya Sh bilioni tano serikali kwasababu ilimnyanyasa, kumdhalilisha,kumbakizia kesi na ilikiuka sheria na Katiba ya nchi wakati ilipomkamata na kumfungulia kesi ya mauji ya watu wa nne.

Zombe kupitia wakili wake Richard Rweyongeza aliifungua kesi hiyo juzi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na tayari imeishapewa namba 35 ya mwaka 2011.Ambapo mdaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa mujibu wa hati ya madai yenye kurasa tisa ambayo Tanzania Daima imefanikiwa kupata nakala yake, Zombe ametoa sababu 21 za kufungua kesi hiyo ya madai ya fidia ya kutaka alipwe sh bilioni tano na riba ya Sh milioni 200.

Zombe anadai Jeshi la Polisi lilikiuka sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 inayotaka kabla ya mtu kukamatwa ni lazima aelezwe anakamatwa kwa sababu gani na akifikishwa kituo cha polisi ni lazima ahojiwe na kuchukuliwa maelezo yake ambayo baadaye hutumika mahakamani kama kielelezo.

“Jeshi la polisi lilikwenda kinyume na sheria hiyo kwani ilinikamata, na kunifungulia kesi hiyo ya mauji bila ya hata ya kunihoji na kunichukua maelezo …kwahiyo utaona kitendo hicho cha polisi walichonifanyia kilininyang’anya haki yangu ya msingi iliyoainishwa kwenye Katiba ya nchi inayosema kila mtu ana haki ya kusikilizwa;

“Mimi licha nilikuwa ni mshtakiwa lakini nilikuwa ninafahamu vyema sheria za nchi hivyo kitendo hicho cha ukiukwaji wa sheria nilichofanyiwa na polisi ambapo nilifikishwa mahakamani bila ya kuchukuliwa maelezo na polisi kiliniathiri kisaikolojia”alidai Zombe.

Aidha Zombe kwa sasa anafanya shughuli zake zinazomuingizia kipato huko mkoani Morogoro na Rukwa,anadai kuwa sababu nyingine ilisababisha afungue kesi hiyo ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi(IGP)-Said Mwema kushindwa kulijibu kusudio lake la kuishtaki serikali ambapo kusudio hilo lilikuwa linatakiwa lijibiwe na Mwema ndani ya siku 90.

Anaeleza kuwa Septemba 27 mwaka huu, ndiyo alikabidhi barua hiyo ya kusudio kwa IGP-Mwema na ilionyesha kupokelewa na kiongozi huyo na kwamba siku hizo 90 zilikuwa zikimalizika Desemba 25 mwaka jana.Katika barua yake ya kusudio mlalamikaji huyo alimweleza Mwema kuwa atakwenda mahakamani iwapo masharti hayo ya kuombwa radhi na kulipwa fidia hayatatekelezwa.

Agosti 17, mwaka 2009,Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitoa hukumu ya kushtusha baada ya kumwachilia huru Zombe na wenzake wanane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja.

Serikali ilikata rufaa Oktoba 7 mwaka 2009 katika Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachilia Zombe na wenzake.

Akisoma hukumu, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Salum Massati, alisema baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, alibaini kuwa serikali ilishindwa kuthibitisha mashitaka na kuwa kamwe mahakama haiwezi kumtiha hatiani mshitakiwa kwa ushahidi dhaifu na wa kusikia kama uliowasilishwa mahakamani hapo, kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria.Kwamba washitakiwa hao si wauaji na aliliagiza Jeshi la Polisi liwatafute wauaji halisi wa marehemu wale.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 9 mwaka 2011.

KORTI YAKUBALI OMBI LA MPENDAZOE,LISSU KIDEDEA

Na Hapiness Katabazi

HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imekubali ombi la aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea(Chadema), Fred Mpendazoe la kutaka mahakama hiyo imruhusu aweke sh milioni 15 mahakamani kama dhamana.

Dhamana hiyo ni sh milioni tano kwa kila mdaiwa ambapo wadaiwa katika kesi hiyo ni Mbunge wa Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk. Makongoro Mahanga (CCM), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi anazotakiwa kuzitoa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

Katika kesi ya msingi Mpendazoe anapinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 jimbo la Segerea yaliyomtangaza Dk. Mahanga kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Uamuzi huo ulitolewa jana asubuhi na Jaji Profesa Ibrahimu Juma ambapo alisema anakubaliana na ombi lilowasilishwa na wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala liloiomba mahakama hiyo iwaruhusu kuweka kiasi hicho cha fedha kwa sabababu ombi hilo limekidhi matakwa ya kifungu cha 111(2) cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

Kwani kifungu hicho ndicho kinachomruusu mlalamikaji wa kesi za uchaguzi kuwasilisha fedha mahakamani na kwamba mlalamikaji katika ombi hilo hakutaka apunguziwe kiasi cha kulipa bali alikuwa anaomba ridhaa ya kulipa kiasi chote cha fedha anachotakiwa alipe kwa mujibu wa sheria.

“Kwa maana hiyo mahakama hii inakubaliana na ombi la mlalamikaji(Mpendazoe) na linalitupilia mbali pingamizi la mdaiwa(Dk.Mahanga) na wenzake kwasababu kifungu cha sheria walichokitumia kuwasilisha pingamizi hilo si sahihi na hakiendani na ombi la mlalamikaji…na kwa maana hiyo mahakama hii imemruhusu mlalamikaji kuwasilisha kiasi hicho cha fedha ndiyo kesi ipangwe tarehe ya kuanza kusikilizwa”alisema Jaji Profesa Juma.

Februali 28 mwaka huu, wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala aliwasilisha ombi jipya la kuomba mteja wake aruhusiwe kuweka kiasi hicho cha fedha kwani tayari mteja amepata kiasi hicho cha fedha.Hata hivyo wakili wa wadaiwa hao Jerome Msemwa alilipinga ombi hilo na kuiomba Mahakama isimruhusu hadi pale mlalamikaji atakapopeleka ombi rasmi mahakamani la kuiomba impangie kiwango cha kuweka mahakamani hapo.

Wakili Msemwa aliongeza kuwa kifungu cha 111(3) cha Sheria ya Uchaguzi, kinamtaka mwombaji anayeiomba mahakama imsamehe kulipa dhamana hiyo au kumpunguzia kiwango cha kulipa, anatakiwa awasilishe ombi hilo ndani ya siku 14 tangu alipofungua kesi ya msingi ya kupinga matokeo ya Ubunge.

Akipangua hoja hiyo wakili wa Mpendazoe, Kibatala aliambia kuwa kifungu hicho kilichotumiwa na Msemwa hakiendani na ombi lao waliloliwasilisha kwa kuwa ombi lao ni Mahakama imruhusu mlalamikaji aweke kiasi hicho cha fedha na si vinginevyo.Februali 15 mwaka huu, Jaji Juma alitupilia mbali ombi la Mpendazoe la kuitaka Mahakama hiyo imsamehe kulipa fedha hizo kwa sababu hana uwezo wa kupata fedha hizo na kwamba amebaini hati ya kiapo cha maombi hayo kina dosari za kisheria.

Katika katua nyingine; Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imetupilia mbali maombi ya kuondoa ama kusamehewa dhamana za gharama za uendeshaji kesi za uchaguzi, yaliyofunguliwa na wanachama wawili wa CCM dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki, Tindu Lissu (Chadema).
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Silivangira Mwangesi na kuongeza kuwa Lissu ameshinda kesi hiyo kutokana na kutofuatwa kwa utaratibu wakati wa kufungua kesi hiyo.

Hata hivyo, hukumu hiyo ilitolewa wakati Lissu hakuwepo mahakamani. Mlalamikiwa huyo aliwakilishwa na ndugu yake aliyejitambulisha kwa jina la Samson Mkotya ambaye alidai alifanya hivyo kwa kuwa Lissu aliharibikiwa na gari mkoani Morogoro.

Maombi hayo yaliwasilishwa na wanachama wawili wa CCM, Shaban Itambu na Pascal Hallu ambao wamewafungulia kesi ya kupinga matokeo ya ubunge jimbo la Singida Mashariki, Tindu Lissu, Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria wa Serikali.

Hata hivyo, Lissu alipinga maombi hayo kwa sababu waombaji hawakuwasilisha maombi ya kutaka kupangiwa dhamana ya gharama za uendeshaji kesi za uchaguzi.

Lissu aliwasilisha hukumu za kesi tatu ambazo mahakama kuu iliwahi kuzitupa baada ya walalamikaji kutowasilisha kwanza maombi ya kupangiwa dhamana hiyo.

Hukumu zilizowasiliswa na Lissu ni ya John Mnyika na Charles Keenja, Joyce Chitende na Zainabu Gama, John Jomba Koyo na Christopher Ole Sendeka. Akipinga pingamizi hilo, wakili wa walalamikiwa hao ni Abdallah Possi, alisema si lazima Jaji akubaliane na hukumu hizo ambazo zimetolewa na majaji wenzake wa mahakama hiyo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 9 mwaka 2011.

VIONGOZI ACHENI KUMSINGIZIA MUNGU

Na Happiness Katabazi

LEO Machi 8 ni Siku ya Wanawake Duniani. Hivyo wanawake tunasherehekea siku hii kwa njia mbalimbali.


Binafsi naisherehekea siku hiyo kwa kutumia kalamu yangu kuandika makala hii.

Heko wanawake duniani, kwani naamini katika dhana hii isemayo: “Katika mafanikio ya mwanamume, basi mwanamke yuko nyuma yake.”

Wanawake tunaweza sana, licha ya kuwepo baadhi ya wanaume wasiopenda mabadiliko na wenye chuki binafsi sehemu za maofisini, majumbani na mitaani ambao wamekuwa wakiwagandamiza wanawake makusudi.

Leo wakati tukisherehekea siku yetu, wanawake tutiane moyo katika kuvitokomeza kwa nguvu zote vikwazo hivyo tunavyowekewa na baadhi ya wanaume ambao ama wana madaraka mahali pa kazi, biashara, vyama vya siasa na kwenye ngazi ya familia.

Lakini nitakuwa sijatenda haki kama wanawake Watanzania leo tunavyoungana na wenzetu duniani hatuna budi kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwani katika serikali ya awamu ya nne ni wazi ameweza kuwateua wanawake wengi kuwa majaji, wakurugenzi, mawaziri na manaibu waziri.

Nimeshuhudia wanawake wengi wakiwemo katika vyombo vyetu vya dola kama ulinzi na usalama.Heko Kikwete katika hilo. Nirejee kwenye mada yangu ya leo.

Taifa linalochakachua elimu, taifa linalochakachua mfumo wake wa elimu, taifa hilo ama halipo au limo njiani kuangamia.
Kwa sababu ufahamu ni mfumo wa akili za binadamu kutambua mambo, ukweli na vitu vinavyomzunguka. Ufahamu ndiyo elimu yenyewe na ndiyo moyo wa elimu. Kwa maana kwamba hakuna kitu binadamu anakijua bila ufahamu. Ukiondoa ufahamu binadamu tutakuwa hakuna kitu tutakachokuwa tunakijua.

Kwa hiyo mambo tunayoyajua na tunathibitisha kuwa ni kweli ndiyo ambayo tunayafundisha kuwa ni ya kweli. Kwa hiyo elimu msingi wa kwanza ni ukweli.

Sasa ukishajua ukweli, binadamu anaweza kuanza kujitambua.
Sasa hatuwezi kujitambua kama viumbe hai wenye ufahamu ikiwa kile tunachotambua ni ukweli kimechakachuliwa.

Katika kipindi hiki mambo yameharibika kutokana na baadhi kujitambulisha kuwa ni wahandisi kumbe vyeti wameghushi; na watu huo wanapewa kazi ya kujenga daraja ambalo usiku linabomoka kwa kusombwa na maji kisha wananchi wanashindwa kupita, fedha za walipa kodi zilizotolewa kujenga zimeteketea kwa sababu si mtaalamu wa fani ya uhandisi; hakika yote yanatokana na watu kutokuwa wakweli.

Baba au mama anahonga fedha ili walimu wamuuzie mitihani aweze kumpatia mwanae kabla ya kuingia kwenye chumba cha mtihani ili aweze kufaulu.

Na mtoto huyo anajikuta anafaulu na kupata daraja la kwanza. Je, kweli elimu aliyoipata mtoto huyo ni sawa ya kufaulu daraja la kwanza?

Na mtoto huyo atazuia watoto wenzake waliopata daraja la pili kwa akili zao. Mtoto huyo aliyepata daraja la kwanza ataenda chuo kikuu na huko nako atapata shahada ya mtindo wa kununuliwa mitihani na wazazi wake na mwisho wa siku anahitimu na kuwa daktari wa binadamu; je, wewe mwananchi au wewe mzazi utaridhika kutibiwa na daktari wa aina hiyo?

Kumbe basi, viongozi wetu wanaokimbilia nje ya nchi kutibiwa mara kwa mara, wanajua ni kitu gani walikifanya kwenye mfumo wetu wa elimu.

Mambo yote mabaya yanayotokea serikalini raia wanalalamika, chimbuko lake ni mfumo wa elimu. Kuna mawaziri hawajui a,b,c za hizo wizara walizopewa kuziongoza.

Hiyo mikataba mibaya inayopingwa sasa, ni matokeo mabaya ya mfumo wa elimu. Hao wanasheria wanaoiandika hiyo mikataba si ni wanasheria wetu? Baadhi ya mawakili wetu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wamekuwa wakiandaa hati za mashitaka zenye dosari za kisheria, hali inayosababisha mahakama kuwafutia mashitaka washitakiwa.

Baadhi ya mahakimu na majaji nao wamekuwa wakiandika hukumu zenye makosa ambazo mwisho wa siku hutenguliwa na mahakama za juu.

Tangu mwaka 2006 mgawo wa umeme ulikuwepo, sasa huo umeme wa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 utatusaidia nini?

Siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), kutoa hukumu katika kesi ya Dowans na Shirika la Umeme nchini (TANESCO); iliamuru Tanesco iilipe fidia Dowans ya sh bilioni 94 pamoja na riba.

Tulimsikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema, akisema hatuna budi kuilipa Dowans,Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akasema tusiilipe. Halafu wote hao ni wanasheria kitaaluma.

Hivi karibuni Brigedia Jenerali mstaafu, Yahya Ali Adawi, alikuja hapa nchini na kujitangaza kuwa yeye ndiye mmiliki mwenye hisa nyingi wa Kampuni ya Dowans, halafu inaibuka Kamati ya Bunge ya Nishati inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba inasema isipowashwa mitambo hiyo mgawo wa umeme hautakoma.

Watanzania tunataka umeme wa zaidi ya megawati 5,000. Serikali ya awamu ya nne tangu mwaka 2006 inagombania umeme wa megawati 100 wa Dowans!
Hivi tuwaulize viongozi wetu, elimu yao waliipata wapi?
Aliyewaambia kuna uhusiano kati ya ukame na uzalishaji umeme ni nani? Hiyo elimu mliipata wapi? Hivi mbona baadhi ya viongozi wetu mnasingizia Mungu?

Hivi nchi zenye ukame kama Saudi Arabia, Somalia na nyingine zilizo kwenye majangwa mbona hawana mgawo wa umeme? Hoja hiyo ya ukame ni dhaifu, ni ya taifa lisilo na elimu.

Taifa la Tanzania lina upepo, makaa ya mawe na gesi kwa miaka mingi tu, nishati zote hizo hazitegemei mvua. Na zipo hapa nchini miaka nenda rudi.

Kwa hiyo dhiki hii ya maisha tunayoipata inayotokana na mgawo wa umeme haina maelezo katika maelezo ya kudra za Mwenyezi Mungu?

Tunamlaumu Mungu bure kumbe sisi wenyewe ni wazembe na wataalumu wetu wa masuala ya nishati ambao wana moyo wa kizalendo hatuwapi nafasi ya kututatulia tatizo hili la umeme ambalo ni wazi litayumbisha pato la taifa.

Sasa hakuna mtu aliyewajibika matokeo mabaya ya wahitimu wa kidato cha nne yalivyotoka hivi karibuni, hakuna mtu anayewajibika tunavyosema mitahala imekosewa. Tumefika mahala hakuna watu wa kuwajibika.

Lakini ni Mungu huyo ndiyo anatuambia tuchukue fedha za walipa kodi tuilipe Dowans? Hizi ndimi mbili zinazotolewa na viongozi wetu wanazipata wapi?

Nchi hii kwa kuwa imeondokana kwenye misingi ya kusema ukweli na hata baadhi ya viongozi wetu wengi hivi sasa wamejifanya mahiri sana wa kutotoa taarifa za ukweli katika baadhi ya mambo. Kwa hiyo lazima taifa letu siku moja litaangamia.

Sipendi tufike huko. Nyie viongozi wetu na sisi wananchi kwa ujumla tujirekebishe na tuwe na hofu ya Mungu.

Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Afrika.

0716- 774494

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 8 mwaka 2011.

RAIA WA KIGENI KORTINI KWA DAWA ZA KULEVYA

Na Happiness Katabazi

KWA mara nyingine tena serikali imewaburuza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, raia wanne wa kigeni wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kula njama na kuingiza dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 81 zenye thamani ya Sh bilioni 2.8.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mustapher Siyani wakili mwandamizi wa serikali Biswalo Mganga aliyekuwa akisaidiwa Prosper Mwangamila na Theophili Mtakyawa aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Dinnis Chukwudi Okechukwu,Paul Ikechukwu Obi ambao ni raia wa Naigeria, Stani Hycenth raia wa Afrika ya Kusini na Shoaib Mohammed Ayazi ambaye ni raia wa Pakstani ambao wanatetewa na wakili wa kujitegemea Brigson Sheiyo.

Wakili Mganga alidai kuwa washtakiwa wote wanakabiliwa na mashtaka mawili.Shtaka la kwanza ni la kula njama kuingiza dawa za kulevya nchini Tanzania katika kipindi cha Machi 4 mwaka huu na Septemba 26 mwaka jana,katika maeneo tofauti bila kibali cha serikali ya Tanzania washtakiwa hao ambao ni raia wa Nigeria, Pakstani na Afrika Kusini kwa pamoja walitenda kosa hilo la kula njama na kuingiza dawa za kulevya hapa nchini.

Mganga alidai kuwa shtaka la pili ni la kusafirisha dawa hizo kuja hapa nchini kinyume na kifungu cha 16(11)b(i) cha Sheria ya Kuzuia dawa za Kulevya ya mwaka 2002 , kuwa Machi 4 mwaka huu, huko Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote waliingiza nchini gramu 81,000 aina ya Heroin yenye thamani ya Sh 2,835,000,000.

Hata hivyo washtakiwa hao hawakutakiwa kusema chochote kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo kwani Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi.

Kwa upande wake wakili wa washtakiwa hao, Sheiyo aliomba mahakama itoe amri ya kuwataka polisi warejeshe simu za washtakiwa ili washtakiwa hao ambao ni raia wa kigeni waweze kuzitumia kuwasiliana na ndugu zao.

Hata hivyo hoja hiyo ilipingwa vikali na wakili wa serikali Biswalo Mganga ambaye alidai kuwa ombi hilo alijaletwa chini ya kifungu chochote cha sheria na kuongeza kuwa kifungu cha 38 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, inawaruhusu polisi kushikilia vitu vya mshtakiwa ambavyo wanaamini vinaweza kuwasaidia kwenye upelelezi wa kesi husika na kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri wakusikiliza kesi hiyo.

Akitoa uamuzi wake kuhusu ombi hilo la wakili wa washtakiwa, Hakimu mkazi Siyani alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba na ndiyo maana baada ya upande wa Jamhuri ulivyomaliza kuwasomea mashtaka washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote na kumhoji wakili huyo wa washtakiwa kuwa kama washtakiwa hao wanahitaji simu hizo ili waweze kuwasiliana na ndugu zao ,Je washtakiwa walimpataje yeye aje kuwatetea mahakamani wakati tayari simu zao zilikuwa zimeishaanza kushikiliwa na jeshi la polisi na akaairisha kesi hiyo hadi Machi 21 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa.

Februali 23 mwaka huu, serikali ilifikisha mahakamani hapo raia wanne wakiwamo raia wawili wa Pakstan wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama na kusafirisha kilo 179 za dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6.2.

Wakati huo huo;Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Gabriel Mirumbe jana alishindwa kuendelea kusikiliza kesi ya kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 inayomkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa(TBC1), Jerry Murro na wenzake kwasababu ya Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Boniface Stanslaus kushindwa kutokea mahakamani hapo kwasababu alikuwa akiiudhulia kesi nyingine Mahakama Kuu.

Hakimu Mirumbe alisema kesi hiyo ilikuwa imepangwa kuanza kusikilizwa jana na leo na akaiarisha hadi leo ambapo Jamhuri italeta mashahidi wake ili waweze kuendelea kutoa ushahidi wake.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Machi 8 mwaka 2011.

MGIMWA ATAKA KUTUNISHA MFUKO WA JIMBO

Na Happiness Katabazi

MBUNGE wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa (CCM), amewataka wananchi wa jimbo wanaoshi jijini Dar es Salaam na Pwani kushiriki kuchangia mfuko wa maendeleo wa jimbo hilo.


Mgimwa alitoa rai hiyo juzi katika mkutano wake na wananchi wa jimbo hilo wanaoishi mkoani hapa Dar es Salaam na Pwani uliofanyika katika Hoteli ya Travetine, alisema lengo la kuwashirikisha wananchi hao ili waweze kuchangia katika mfuko huo ni kutaka kuleta maendeleo.

“Wananchi wa Mufindi Kaskazini siyo tu wanaishi jimboni humo tu wengine ndiyo kama nyie mmetawanyika mikoa mingi ya Tanzania kutokana na majukumu ya kikazi... sasa nimewaita hapa ili niwashirikishe katika uanzishwaji wa mfuko huo ambao wananchi mkihamasika kuuchangia ni wazi jimbo letu litapata maendeleo kwa kasi kwani sio lazima tusubiri serikali ituletee hata sisi wananchi kwa michango yetu tunaweza kuleta maendeleo,” alisema Mgimwa.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Machi 8 mwaka 2011.

KESI YA MBATIA Vs MDEE:MBATIA ONGEZA MSHTAKIWA MWINGINE

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imekubali ombi la aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Kawe kwa tiketi ya (NCCR-Mageuzi) James Mbatia lilokuwa likitaka mahakama hiyo imruhusu kuondoa mahakamani hati yake ya madai ili aende kuifanyia marekebisho na kisha kuirejesha upya mahakamani hapo.

Mbatia katika kesi hii ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya jimbo la Kawe,ambayo imepewa Na.111/2010.Mbatia anamlalamikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mbunge wa jimbo hilo Halima Mdee (CHADEMA) ambaye hata hiyo Mdee hakuwepo mahakamani jana ila Mbatia alikuwepo.

Amri hiyo ya kukubali ombi la Mbatia ilitolewa jana na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,Amir Msumi ambapo alisema anakubaliana na ombi kuibadilisha hati ya madai lilowasilishwa na mawakili wa Mbatia, Mohamed Tibanyendera na Alocye Komba na akawataka wawasilishe hati mpya Machi 8 na kesi hiyo itakuja kutajwa Machi 10 mwaka huu.

Awali mapema jana asubuhi wakili Tibanyendera na Komba waliambia mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa ila mlalamikaji (Mbatia) anawasilisha ombi la kuomba kuiondoa hati ya madai ili aende kuifanyia marekebisho kwani kwa mujibu mabadiliko ya Kanuni za kesi uchaguzi yaliyofanyika mwaka 2010,yanalazimisha Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo husika naye afunguliwe kesi jambo ambao katika hati yao ya madai hawakuwa wamemshtaki.

Tibanyendera alieleza kuwa kwa mujibu wa kanuni za zamani za sheria ya uchaguzi ya mwaka 2002 kabla hazijafanyiwa mabadiliko mwaka jana mlalamikaji alikuwa akiruhusiwa kumshtaki mbunge aliyeshinda katika jimbo husika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali mbapo huyo mwanasheria mkuu wa serikali ndiyo aliyekuwa akishtakiwa kwaniaba ya msimamizi wa uchaguzi wa jimbo.

“Kwa maelezo hayo ya kisheria mteja wetu(Mbatia) anaomba abadilishe hati yake ya madai ya awali ili aweze kumuongeza Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kawe kwahiyo katika hati hiyo mpya tutakayoiwasilisha Jumatatu ijayo wadaiwa watakuwa ni watatu na si wawili tena;

“Na sababu ya pili ya mteja wetu kuiondoa hati hiyo akaifanyie marekebisho ni kuna wapiga kura wawili wa jimbo hilo wamejitokeza na wametaka kuungana na Mbatia katika kesi hiyo kuwashtakiwa wadaiwa hao.Na wapiga kura hao ni Hemed Manoni na Solomoni Mfunda na hivyo wataifanya hati mpya kuwa na walalamika watatu ambao ni Mbatia,Manoni na Mafundi dhidi ya AG,Mdee na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kawe”alidai Wakili Tibanyendera.

Novemba 25 mwaka 2010 Mbatia alifungua kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo ambayo yalimtangaza Halima Mdee(CHADEMA) kuwa ndiye aliyeshinda na ataliongoza jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitano.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Machi 5 mwaka 2011.

JAJI AJITOA KESI YA SAMAKI WA MAGUFULI

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE jaji Razia Sheikh anayesikiliza kesi ya uvuvi haramu katika Bahari ya Hindi ukanda wa Tanzania inayowakabili ryaia 34 wa kigeni maarufu kama ‘kesi ya samaki wa Magufuli’ amejitoa kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Jaji Sheikh alitoa uamuzi huo jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kufuatia ombi la washtakiwa hao walioliwasilisha mbele yake Ijumaa iliyopita ambapo washtakiwa walimwomba ajitoe kwasababu hawana imani naye.

Jaji Sheikh alisema anajitoa kusikiliza shauri hilo si kwasababu ya hoja zilizowasilishwa na wakili wa washtakiwa John Mapinduzi na Ibrahim Bendera bali anajitoa ili haki ionekane inatendeka na kwamba jalada la kesi hiyo atalipeleka kwa Jaji Mfawidhi Semistocles Kaijage ili aweze kumpanga jaji mwingine.

Alisema mawakili wa washtakiwa waliwasilisha maombi ya kutaka yeye ajitoe kusikiliza kesi hiyo hayana msingi mantiki ya kisheria na kwamba waliyatoa kwa nia mbaya dhidi yake kufuatia uamuzi wake alioutoa Ijumaa iliyopita ambao uliwanyima dhamana washtakiwa.

Jaji Sheikh alisema sababu za kumtaka ajitoe alizozitoa wakili Mapinduzi hazikidhi matakwa ya sheria yaliyowekwa na Mahakama ya Rufani na ya kumlazimu jaji au haki aweze kujitoa katika kesi na kwamba sababu zilizowasilishwa na wakili Mapinduzi wiki iliyopita zilikuwa anatakiwa akazitumie siku atakapoukatia rufaa uamuzi wake katika Mahakama ya Rufani na siyo pale Mahakama Kuu.

“Miongoni mwa sababu zinazoweza kumfanya jaji au hakimu ajitoe kusikiliza kesi ni pamoja na kuonesha upendeleo kwa upande mmoja…hivyo naamua kujitoa kwenye kesi hii siyo kwasababu ya hoja za mawakili wa utetezi ila najitoa ili haki ionekane inatendeka”alisema Jaji Sheikh.

Aidha alisema tuhuma zilizotolewa na wa washtakiwa (Mapinduzi) dhidi yake hazina ushahidi kwani hata mawakili wa washtakiwa walishindwa kuzithibitisha tuhuma hizo ikiwemo tuhuma ya yeye kuichelewesha kesi hiyo kwa makusudi hali iliyosababisha mshtakiwa mmoja kufia jela.

Jaji huyo akiipangua tuhuma kwamba washtakiwa hao hawana imani naye ,alisema tuhuma hiyo haina msingi kwani kumbukumbu za mwenendo wa kesi hiyo unaonyesha kuwa ucheleweshwaji wa kesi hiyo umekuwa ukichangiwa na mawakili hao wa utetezi hasa wakili John Mapinduzi.

“Wakili Mapinduzi kwa mujibu wa kumbukumbu ya jalada ya kesi hii ndiyo anaonekana amekuwa mara nyingi haudhulii kesi hii tena hata bila kutoa taarifa”alisema Jaji huyo Aidha Jaji Sheikh aliwashambulia vikali mawakili wa utetezi katika kesi hiyo kwa kusema kuwa licha mawakili hao ni maofisa wa mahakama nchini ambao wanajukumu la kuisaidia kufikia maamuzi ya haki na sahihi lakini cha kushangaza mwenendo wao umekuwa siyo mzuri kwa mahakama hususani wakili Mapinduzi.

Februali 25 mwaka huu, washtakiwa ho kupitia kwa wakili wao Mapinduzi walimtaka jaji huyo ajitoe ikiwa ni saachache tu baada ya jaji huyo kutoa uamuzi wa kuwanyima dhamana licha makosa yanayowakabili yanadhamana kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 ila akasema kwa mazingira ya kesi hiyo mahakama hiyo imetumia mamlaka yake kuwanyima dhamana.

Uamuzi huo uliwafanya baadhi ya washtakiwa hao kumwaga machozi baada ya wakalimani wao kuwatafisiriwa uamuzi wa jaji huyo na ndipo kupitia kwa mawakili wao wakamtaka ajiondoe katika kesi yao. Katika sababu zao za kumkataa jaji huyo mmoja wa mawakili wao John Mapinduzi walidai kuwa hawana imani naye kwa kuwa kesi yao imechukua muda mrefu kiasi kwamba hata mwenzao mmoja amefariki akiwa mahabusu.

Pia walidai kuwa hakuna ushahidi kuwa wakipewa dhamana watatoroka kama ambavyo jaji alisema huku wakipinga kuwa wao si wahamia haramu kwa kuwa hawakuwa na mpango wa kuja Tanzania bali walikuja baada ya kutiwa mbaroni na kikosi cha doria cha maafisa wa uvuvi. Walikamatwa Machi 9 mwaka 2009 na kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu Machi 12 mwaka huo kabla ya kesi yao kuhamishi Mahakama Kuu mbele ya Jaji Sheikh.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Machi 4 mwaka 2011.