HONGERA OFISI YA DDP,POLE MARANDA,FARIJALA


Na Happiness Katabazi

MEI 23 mwaka huu serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),Eliezer Feleshi iliandika historia mpya ya ushindi wa kesi moja kati ya jumla ya kesi 12 za wizi wa mabilioni ya Fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje(EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania .

Historia hiyo ya ushindi ilitokana na jopo la Mahakimu wakazi watatu lililokuwa likiongozwa na Saul Kinemela,Phocus Bambikya na Elvin Mugeta kutoa hukumu katika kesi ya jinai Na.1161/2008 iliyokuwa ikimkabili Mweka Hazina wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Rajabu Maranda na Binamu yake Farijala Hussein ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi wizi wa shilingi bilioni 1.8 kwa kutumia kampuni yao hewa ya Kiloloma &Brothers kuonyesha kampuni hiyo imepewa idhini ya kudai deni la Kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai India katika BoT ,huku wakijua si kweli.

Ambapo Hakimu Mugeta ambaye ndiye alikuwa akisoma hukumu hiyo alisema washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na makosa nane lakini mahakama hiyo imefikia uamuzi wa kuwatia hatiani kwa jumla ya makosa sita ya kughushi nyaraka mbalimbali na kisha kujipatia kiasi hicho cha fedha na kusema kuwa inawafutia makosa mawili ya kula njama na wizi kwasababu jamhuri ilishindwa kuthibitisha makosa hayo.Hali iliyosababisha siku hiyo mahakama hiyo kuzizima kwa vilio huku baadhi ya wananchi wakifurahia hukumu hiyo.

Kabla sijaendelea na mada ya leo, Fukuto la Jamii litawakumbusha wasomaji wake jinsi kesi hii ilitolewa hukumu ilivyokwenda hatua kwa hatua kwani mwandishi wa Fukuto la Jamii ni miongoni mwa waandishi wa habari za mahakamani na nimiongoni mwa waandishi wa habari wachache nchini ambao wameiripoti kesi hiyo na kesi nyingine tangu zilizofunguliwa hadi kutolewa hukumu.

Novemba 4 mwaka 2008, ndiyo siku ya kwanza ambayo nayo itabaki kuandikwa kwenye historia kuwa ndio siku ambayo DDP- Feleshi iliwaburuza mahakamani watuhumiwa wa wizi katika akaunti ya EPA, baada ya skendo ya wizi kuibuliwa na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utoo, kelele za wananchi na wafadhili, hali iliyosababisha Rais Kikwete kuunda Tume ya uchunguzi wa wizi huo ambayo ilimshirikisha Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP-Said Mwema, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Dk. Edward Hosea na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye kwa sasa amestaafu, Johnson Mwanyika.Tume hiyo iliwahoji watuhumiwa na hatimaye kuwafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbali na kesi hiyo Na.1161/2008 ambayo Mei 23 mwaka huu ndiyo ilitolewa hukumu, Maranda na Farijala pia wanakabiliwa na kesi nyingine tatu za EPA ambazo nazozimefikia katika hatua ya kusikilizwa, kufanywa majumuisho ya wanakesi ya kujibu au la na kujitetea.Kesi ya pili ni jinai Na.1162/2008 inamkabili tena Farijala ,Maranda ambao wa kwasasa wanatamikia kifungo chao katika Gereza la Ukonga, maofisa wa BoT ambao ni Iman Mwakosya,Ester Komu na Bosco Kimela ambapo upande wa Jamhuri wanadai washtakiwa hao waalighushi nyaraka kwa kutumia kampuni hewa ya hewa ya Rashaz T Ltd kuchota sh milioni 207 katika akaunti ya EPA.

Kesi ya tatu ni Na.1163/2008 ambayo inamkabili Maranda na Farijala ambapo walitumia kampuni yao hewa ya Money Planner kuchota fedha katika EPA.Ambapo kesi hii tayari Jamhuri imeshafunga ushahidi wake na mahakama kilichobaki sasa ni pande zote kuwasilisha mahakamani majumuisho ya kesi hiyo ambayo wataiomba mahakama iowaone washtakiwa hao wanakesi ya kujibu au la.

Kesi ya nne ni Na.1164/2008 inamkabili Farijala,Maranda,Iman Mwakosya,Ester Komu,Sophia Lalila na Ajay Somani ambao jamhuri inadai washtakiwa walikula njama,kushushi nyaraka za jina usajili, hati ya kuamisha deni,kujipatia ingizo kwa kutumia kampuni feki ya Mibale Farm kuonyesha imepewa idhini ya kudai deni la kampuni ya Raksh Mills Textile Co.Ltd ya nchini India na kisha kujipatia ingizo la shilinigi bilioni 3.8 toka kwenye akaunti ya EPA.

Kesi hii imefikia hatua ya mshtakiwa wa pili (Maranda) Juni 2 mwaka huu, kupanda kizimbani kujitetea baada ya Mei 5 mwaka huu, mshtakiwa wa kwanza Farijala Hussein kumaliza kutoa utetezi mbele ya jopo la mahakimu wakazi Sam Karua,Elvin Mugeta na Jaji Beatrice Mutungi. Tukiachana na kesi hizo tatu zinazowakabili fungwa hao.

Pia kuna kesi nyingine zinawakabili washtakiwa mbalimbali wa wizi wa EPA, na miongoni mwa kesi hizo ambayo jumla yake ni 12, kesi nne zinamkabili Mfanyabiashara maarufu nchini JayantKumar Chandubai Patel maarufu “Jeetu Patel’ na wenzake, ambapo ukilinganisha na kesi zote za EPA zilizopo mahakamani hapo kesi hizo nne za EPA ambazo nazo zilifunguliwa Novemba 4 mwaka 2008 zipo hatua ya chini kabisa yaani hata kesi moja moja ya msingi haijaanza kusikilizwa kwasababu mshtakiwa huyo na wenzake waliwasilisha maombi ya kuomba kesi zote zisiendelee kusikilizwa kwasababu amefungua kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu ya Tanzania, ya kuomba kesi zote nne zinazomkabili katika Mahakama ya Hakimu MKazi Kisutu zifutwe kwasababu Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi alimuhukumu kwa kumuita ‘Fisadi Papa’ wakati kesi anazokabiliwa nazo hazijaamliwa na mahakama na mahakama ya Kisutu ikakubali ombi lake la kusimamisha kesi hizo.

Baada Lakini hata hivyo mwaka juzi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Semistocles Kaijage aliitisha majarada la kesi hizo za Jeetu ofisini kwake na kupitia amri zilizotolewa na majopo ya mahakimu wakazi ya kusimamisha usikilizwaji wa kesi hizo ambapo Jaji Kaijage baada ya kuyapitia alitoa amri kwa mahakama ya kisutu kuendelea kusikiliza kesi hizo lakini hata hivyo mawakili wa Jeetu, Martin Matunda na Mabere Marando hakukubaliana na amri ya Jaji Kaijage kuamua kuwasilisha maombi ya mapitio ya uamuzi wa Jaji Kaijage katika katika Mahakama ya Rufaani nchini ambapo mahakama ya rufani nchini wiki mbili zilizopita ilisikiliza maombi hayo ya mawakili wa Jeetu na muda wowote kuanzia sasa itatoa uamuzi wake.

Juni 11 mwaka 2009, Kiongozi wa Jopo la Mahakimu wakazi lililokuwa likiongozwa na Cypiriana Willam ambaye kwasasa amaestaafu kwa mujibu wa sheria na nafasi yake katika kesi hiyo kuchukuliwa na Mugeta ambao alikuwa akisaidiwa na Bambikya na Kinemela walimuona Farijala na Maranda wana kesi ya kujibu katika kesi Na.1161/2008 ambayo ilitolewa hukumu Jumatatu iliyopita ambapo mwanzo mwisho upande wa Jamhuri kesi hii ulikuwa ukiwakilishwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Stanslaus Boniface akisaidiwa na Timon Vitalis, Frederick Manyanda na Shadrack Kimaro kwasababu upande wa Jamhuri umeweza kuthibitisha kesi yao.

Juni 6 mwaka 2009, Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Boniface aliwasilisha majumuisho ya kesi hiyo akiiomba mahakama hiyo iwaone washtakiwa wote yaani Farijala na Maranda wana kesi ya kujibu, kwani Jamhuri imeweza kuthibitisha kesi hiyo.

Aidha, Aprili 29 mwaka 2010, Rajabu Maranda alipanda kizimbani kutoa utetezi wake katika kesi hiyo ambayo leo inatolewa hukumu ambapo aliieleza mahakama hiyo kuwa alichokuwa akikizingatia katika mchakato wa kudai deni katika (EPA) ni kupata fedha na si kutazama nyaraka.Na Mei 23 mwaka huu, ndiyo hukumu ya kesi hiyo ilitolewa na kufanya kesi hiyo moja ya EPA kumalizika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na wahstakiwa hao kupitia wakili wao Majura Magafu wamesema hawakubaliani na hukumu hiyo na tayari wameishawasilisha katika Mahakama ya Kisutu hati ya nia ya kukataa rufaa Mahakama Kuu.

Kwa mtiririko wa kumbukumbu wa kesi ya kesi hiyo iliyokwishatolewa hukumu na kesi nyingine ambazo bado hazijatolewa hukumu zipo kwenye hatua za kusikilizwa na nyingine nne za Jeetu ambazo bado hazijaanza kusikilizwa ninaimani wasomaji wa Fukuto la Jamii mtakuwa mkielewa nini kinachooendelea katika kesi hizo.

Sasa Fukuto la Jamii linapenda kukumbusha baadhi ya matamko yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani kupitia vyombo vya habari, baadhi ya wanachama wa CCM wanajifahamu ambao walikuwa wanakebeki kesi chini chini,baadhi ya makala za waandishi wenzangu na baadhi ya wananchi ambao siwafahamu ambao kwa muda walikuwa wakinitumia mimi binafsi ujumbe mfupi wa kunitaka niache kufuatilia kesi hizo kwasababu mwisho wa siku nitamaliza soli za vitu bure kwasababu kesi hizo za EPA ni usanii wa serikali na mwisho wa siku kesi zote zitafutwa na kwamba hakuna hata mshitakiwa mmoja atakayetiwa hatiani.

Mengi yalisemwa kuhusu kesi hizo kuwa ni kesi za usanii tena hata baadhi ya mawakili walidiriki kusema hayo lakini Jumatatu ya wiki iliyopita pale katika Mahakama ya Kisutu baada ya hukumu hiyo kusomwa wale wale mawakili ambao miongoni mwao wanawatetea washtakiwa wengine wa EPA, majina yao nayaifadhi walinileza kuanzia siku hiyo wanafuta kauli yao kuwa kesi hizo ni za usanii na kwamba hukumu hiyo tayari imetoa ishara mbaya kwa kesi nyingine za EPA zinazowakabili wateja wao.Nilicheka sana.

Na mawakili wengine walidiriki kunieleza kuwa upande wa Jamhuri katika kesi za EPA zimejitahidi sana kukusanya ushahidi wa kutosha katika kesi hizo ila wanachokifanya ni kutumia mbinu chafu ya kuwasilisha mapigamizi yasiyokuwa na kichwa wa miguu mahakamani ili kasi ya usikilizwaji na umalizikaji wa kesi za EPA uchelewe ili wateja wao waendelee kubaki uraiani.

Na baadhi ya mawakili wanaofanya mchezo huo ambao majina yao nayaifadhi yalinieleza kuwa serikali imeishabaini hujuma hizo wanazozifanya kuchelewesha kesi hizo na wamekuwa wakiitwa na kuonywa na mamlaka husika na mawakili hao hivi sasa wamesema wanaachana na mchezo huo kwani mwisho wa siku wanaweza wakajikuta wananyang’anywa leseni ya uwakili kwaajili ya kesi moja tu ya kupita wakati leseni hiyo ndiyo inamfanya aendeshe maisha yake.

Lakini kama ilivyoada ya watanzania wengi kuwa na hulka ya kudhika mambo fulani,kusema sema ovyo na kutoa hukumu hata kama hawana ushahidi na hayo mambo wanayoyasema.Hadi sasa wale wanasiasa wa vyama vya upinzani ambao walikuwa wakisema kesi hizo ni usanii hata baada ya kesi hiyo moja kutolewa hukumu hadi sasa wameshindwa kujitokeza tena kwenye vyombo vya habari kufuta kauli zao na kuipongeza upande wa Jamhuri kwakushinda kesi hiyo.Lakini ingetokea upande wa Jamhuri kesi hiyo wangeshindwa ni wazi kabisa wanasiasa hao wangeibuka kutoka mafichoni na kutoa kauli za kuikebehi serikali na waendesha mashtaka wake.

Tabia hii binafsi uwa inanikera sana kwani tumekuwa taifa la wananchi tunaopenda sana kupakana matope,kuhukumiana na kushindwa kupongezana pale taasisi fulani au mtu fulani anapofanya jambo jema kwa maslahi ya nchi.Taasisi hizo zinapofanya vibaya tumekuwa vinara wakuwaramu lakini zinapofanya vizuri hatuzipongezi.Tuachane na utamaduni huo wa kijinga badala yake tujenge utamaduni wa serikali, vyama vya siasa, viongozi wetu ama wananchi wanapofanya jambo jema tuwapongeze na wanapokosea tuwakosoe kwa hoja na kuwaelekeza nini wafanye.

Na mfano wa hayo ninayo ya sema ni ile hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam(ACP),Abdallah Zombe na wenzake nane ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya mauji.Wananchi mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa na mimi mwandishi wa Fukuto la Jamii, tuliwashambulia mawakili wa serikali kwa kushindwa kesi hiyo.

Na siyo kesi ya Zombe tu, hata mimi binafsi kupitia makala zangu hapo nyuma nilikuwa nikandika makala za kuwaandama mawakili wa serikali ambao walikuwa wakiziendesha baadhi ya kesi za EPA, kwani hapo awali walikuwa wakionekana kubabaika katika uandaaji wa hati za mashtaka hali iliyokuwa ikiwalazimu kuzibadilisha hati za mashtaka mara kwa mara hali iliyokuwa ikizusha hofu kwa wananchi kuwa uenda mawakili wa serikali hawapo makini katika uandaaji wa hati hizo hali licha kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, inauruhusu upande wa jamhuri kuifanyia hati ya mashtaka marekebisho(amendment of charge).

Lakini siku zote muungwana asifiwi ushenzi, kwakuwa ni kweli serikali ilishindwa kwenye kesi ya Zombe nikaandika makala ya kuisema , na Jumatatu ya wiki iliyopita serikali Iliweza kuibuka mshindi katika kesi ya EPA, leo nimelazimika kuandika makala ya kuipongeza serikali kwa kushinda kesi hiyo.Na huu ndiyo msimamo wangu kwamba serikali ikifanya vizuri nitaipongeza na ikivurunda nitaikosoa.

Kwahiyo Fukuto la Jamii kwanza kabisa linapenda kutoa pongezi za dhati kwa serikali kupitia ofisi ya DDP-Feleshi na timu yake ambayo ilikuwa ikiongozwa na mawakili mahiri wa serikali Stanslaus Boniface,Fredrick Manyanda kwa kuweza kuleta mahakamani vielelezo,mashahidi na kutumia mifano ya kesi mbalimbali na sheria mbalimbali mahakamani hali iliyokuwa ikiufanya upande wa washtakiwa mara kwa mara wakati kesi hiyo ikiendelea kushindwa kufurukuta na mwisho wa siku upande wa Jamhuri wakaibuka washindi katika kesi hiyo ambapo mahakama ilihukumu kifungo cha miaka mitano jela na kuwataka washtakiwa warejeshe kiasi hicho cha fedha kwa mwenyewe ambaye ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hiari yao ama sivyo mali zao zitataifishwa na serikali.

Kwa wale tuliokuwa tukiudhuria kesi hii mwanzo mwisho bila kuchoka,kwanza kabisa tuliweza kujionea kuwa kumbe serikali ina mawakili wazuri wa kesi waliobobea kwenye uendeshaji wa kesi za jinai.Huwezi kuzungumzia kesi za EPA, bila kumtaja wakili mkuu wa serikali Stanslaus Boniface ambaye kwasasa amepanda cheo na kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka nchini,Wakili Mkuu wa Serikali Fredrick Manyanda, Oswald Tibabyekomya,Shadrack Kimaro, Thadeo Mwenepazi, Timon Vitalis,Biswalo Mganga,Michael Lwena na mwanadada Arafa Msafiri.

Mawakili wao muda wote wanaendesha kesi zao kwa uweledi zaidi na umakini wa hali ya juu ukilinganisha na baadhi ya mawakili wa serikali ambao tumekuwa tukiwashuhudia kwenye baadhi ya kesi wakileta ubabaishaji hali inayosababisha wakati mwingine upande wa Jamhuri kujikuta wanashindwa vibaya katika kesi walizozifungua mahakamani dhidi ya washtakiwa kadhaa hali ambayo ilisababisha jamii kuanza kuiponda serikali kuwa haina wanasheria wazuri na walisoma vizuri kama mawakili wa kujitegemea hali ambayo kwa upande mwingine ilisababisha baadhi ya wananchi kuwa na fikra kuwa ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ina mawakili mabomu ambao wameshindwa kazi.

Lakini kuna msemo maarufu usemao ‘kila zama na kitabu chake’.Hivyo alipoingia madarakani rais Kikwete alimteuwa Eliezer Feleshi kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka, na katika uongozi wake akaunda timu yake ya kufanya nayo kazi na muda mfupi baadae ikaibuka skendo ya EPA ambayo mwisho wa siku DDP mwenye akafungua kesi kwaniaba ya jamhuri na kwakuona kesi hizo zinahusisha watu wenye fedha nyingi na wenye majina makubwa kwenye jamii, kwakutambua hilo akaamua kupanga kikosi kazi chake ambacho sisi waandishi wa habari za mahakama tumekipachika jina la ’Siafu’ kwaajili ya kuendesha kesi hizo na kweli wamekuwa wakiziendesha kesi hizo kwa uweledi wa hali ya juu na uaminifu mkubwa ambao umethibittisha ndani ya serikali pia kuna mawakili wazuri tu ila huko nyuma walikuwa hawapewi nafasi na kwa wale wanaodhulia kesi za EPA mahakamani watakubaliana na hayo niliyoandika.

Pia safu hii inatoa pongezi kwa waandishi wa habari wenzangu wa habari za mahakamani jijini Dar es Salaam, ambao kwa umoja wetu bila kuchoka tulisimama imara na tunawaahidi wa watanzania kuwa tutaendelea kusimama imara kuripoti kesi zinazofunguliwa katika mahakama zetu bila kuchoka licha tumekuwa tukikutana na changamoto za hapa na pale,lakini nadiriki kusema mchango wa waandishi wa habari katika kuripoti kesi za mahakama ni mkubwa sana kwani mchango huo pia unachangia kwa kiasi kikubwa kukuza utawala wa sheria hapa nchini.

Baada ya kusema hayo, napenda kutoa pole kwa kaka yangu Maranda na Farijala ambao kwasasa wanaishi makazi mapya katika Gereza la Ukonga.Kwani kwa mara ya kwanza kufahamiana na kaka zangu hao ni siku walipofikishwa mahakamani hapo na hata siku kesi zao zilizopokuwa zikija kwaajili ya kusikilizwa,kabla ya kesi hizo kuanza kusikilizwa tulikuwa tukiketi wote pamoja kwenye mabechi mahakamani hapo na kuzungumza mambo kadha wa kadhaa na hata siku ili ya kusomwa kwa hukumu, saa mbili asubuhi hadi saa nne asubuhi kabla ya kuingia kwenye chumba cha mahakama kusikiliza hukumu yao.

Farijala,Maranda na mtuhumiwa mwingine wa EPA, Bahati Mahenge ambao walitokea majumbani kwao kuja mahakamani walikuja kunisalimu kwenye benchi nililokuwa nimekaa peke yangu na tukazungumza na kucheka lakini saa chache baadaye ndiyo mahakama iwahukumu na kuwashuhudia askari kanzu wameishawavalisha pingu mikononi na kuwapandisha gari la wazi mithili ya ‘maharusi’ na kuondoka mahakamani hapo ambapo kuanzia siku hiyo jina la watuhumiwa lilibadilika na kuuitwa wafungwa.Lakini kwakuwa bado mnakabiliwa na kesi nyingine tatu tutakuwa tukionana mahakamani hapo licha haitakuwa kama zamani kwani hivi sasa mtakuwa mkilindwa na askari wa Jeshi la Magereza. Kwa kweli inasikitisha sana hasa ukifikiria wameacha familia zao zikiwa zinawategemea.

Lakini hakuna jinsi,sisi waumini wa sheria tuna msemo usemao ‘sheria ni msumeno’ na kweli msumeno huo ndiyo umemkata Kaka yangu Farijala na Maranda.Na siku zote mimi usema hukumu mbalimbali zinazotolewa na Mahakama zetu ufunza jamii iishi kwenye mstari ulionyooka. Kwa hiyo hukumu ya Farijala na Maranda imetoa funzo kwao na sisi wananchi wengine ambao ni watuhumiwa watarajiwa kuwa tusithubutu kufanya vitendo vinavyovunja sheria za nchini kwani tukae tukijua vikitenda vitendo vya kuvunja sheria mwisho wa siku tutajikutwa tunafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwenda kuishi Magerezani.

Mwisho Fukuto la Jamii linapenda kuikumbusha ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, kuwa isilewe sifa na ushindi huo, kwani ikumbuke bado ina kesi nyingi ambazo zinafuatiliwa kwa karibu jamiii kwahiyo iongeze nguvu katika kesi hizo ili mwisho wa siku washtakiwa ambao kweli walitenda vitendo vya ufunjifu wa sheria nikiwemo kukwapua fedha za umma watiwe hatiani na mahakama.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 31 mwaka 2011.

JAMHURI YAFUNGA USHAHIDI KESI YA SAMAKI WA MAGUFURI

Na Happiness Katabazi
HATIMAYE upande wa Jamhuri katika kesi ya uvuvi haramu katika kina kirefu cha ukanda wa Bahari ya Hindi maarufu kesi ya ‘Samaki wa Magufuri’ inayowakabili raia 36 wa kigeni umefunga ushahidi wake katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Wakili Mwandamizi wa Serikali Biswalo Mganga anayesaidiwa na Prosper Mwangamila mbele ya Jaji Agustine Mwarija alieleza mahakama hiyo kuwa mashahidi wake 13 walifika mahakamani hapo kutoa ushahidi wameona ushahidi wao umetosha na hivyo wamefikia uamuzi huo wa kuifunga kesi yao.

‘Mheshimiwa jaji na mahakama yako tukufu leo tunayo furaha kuiarifu mahakama hii kuwa upane wa Jamhuri tumefunga rasmi kesi yetu kwani tumejiridhisha mashahidi 13 tuliwaleta mahakamani hapa kutoa ushahidi wanatosha kujenga kesi yetu hivyo tunaiachia mahakama iendelee na kazi yake”alisema Wakili Mwandamizi wa Serikali Biswalo Mganga.

Kwa upande wake Jaji Mwarija alisema anakubaliana na maelezo hayo na ana uamuru upande wa utetezi katika kesi hiyo unaowakilishwa na mawakili wa kujitegemea John Mapinduzi na Ibrahim Bendera kuwasilisha majumuisho ya kesi hiyo ya kuiomba mahakama iwaone wateja wao hawana kesi ya kujibu Juni 6 mwaka huu.

Aidha pia Jaji Mwarija aliuamuru upande wa Jamhuri nao uwasilishe majumuisho yao ya kuwaona washtakiwa wanakesi ya kujibu kwa njia yam domo Juni 9 mwaka huu.

Machi 2009 walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka makosa ya kukamatwa wakiwa kwenye meli ya Tawariq 1 wakifanya uvuvi katika kina kirefu bila leseni ya uvuvi na kisha kuchafua mazingira katika kina kirefu cha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Tangu kipindi hicho hadi leo washtakiwa hao wanaendelea kusota rumande kwasababu mahakama kuu imewanyima dhamana.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 31 mwaka 2011.

MSHTAKIWA RICHMOND ALIGUSHI SAINI-SHAHIDI

Na Happiness Katabazi

MTAALAMU wa maandishi toka Jeshi la Polisi, Hamad Hamad ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa kuwa hati ya nguvu ya kisheria (Power of Attoney) iliyotolewa na mshtakiwa wa kesi ya kutoa taarifa za uongo kwa Bodi ya Shirika la Umeme Tanesco kuhusu Kampuni Richmond LLC ya Marekani, Naeem Gile ilikuwa
imegushiwa.


Hamad ambaye ni shahidi wa sita wa upande wa Jamhuri ambaye alikuwa akiongozwa na Wakili Kiongozi wa Serikali Fredrick Manyanda aliyekuwa akisaidiwa Shadrack Kimaro kutoa ushahidi wake alieleza kuwa Novemba 3 mwaka 2008 alipokea hadi hiyo ya nguvu ya kisheria na barua nyingine mbili ambazo zilikuwa hazibishaniwi ili aweze kuzifanyiakazi ya kitaalamu ambayo itatoa majibu ya nyaraka ipi kati yake ilikuwa imegushiwa.

Hamad alidai kuwa nyaraka hizo mbili zilikuwa zimesainiwa katika nyakati tofauti na Mkurugenzi wa Kampuni ya Richmond LLC, Mohamed Gire anayeishi nchini Marekani na hati ya nguvu ya kisheria (Power of Attoney) ilikuwa inaonyesha kusainiwa naye hiyo yeye kama mtaalamu wa maandishi aliletewa ili aweze kuzilinganisha saini hizo mbili zilizokuwa zimesainiwa kwenye barua hizo mbili ambazo zilikuwa zimesainiwa na mtu mmoja.

Alidai kwa kuangalia tu kwa macho aligundua tofauti kati ya saini iliyokuwa kwenye barua hizo mbili na ile iliyopo kwenye hati ya nguvu ya kisheria, na alipokagua kwa kutumia kifaa maalumu ,kifaa hicho kilitoa matokeo ambayo saini hizo zilizosainiwa kwenye nyaraka hizo mbili hazikuwa zimesainiwa na mtu mmoja.

Mshitakiwa Naeem katika kesi hiyo anadaiwa pia, akifahamu na kwa ulaghai,alitoa taarifa za uongo kuhusu kampuni hiyo ya kufua umeme kwa Bodi ya Shirika la Umeme la Tanesco kuwa inauwezo wa kuzalisha umeme hapa nchini hivyo apewe tenda na kwamba alikuwa amepewa nguvu ya kisheria ya kuendesha kampuni hiyo hapa nchini na Mwenyekiti wa Kampuni ya Richmond LLC,Mohamed Gire ,inayoonyesha hati hiyo ya nguvu ya kisheria ambayo inaonyesha ilitolewa Machi 3, mwaka 2006,huku akijua si kweli.

Mshitakiwa anadaiwa Juni, 2006 jijini Dar es Salaam, alitoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa timu ya majadiliano ya serikali, kuwa Kampuni ya Richmond LLC ya Texas, Marekani, ina uwezo wa kuzalisha umeme megawati 100 ili apewe tenda hiyo.

Kabla hakimu Walialwande Lema jana kuairisha kesi hiyo baada ya kuombwa na upande wa mashitaka kwa kuwa hawakuwa na shahidi mwingine, alionya kuwa jana alikuwa ametoa ahirisho la mwisho upande wa mashitaka walete mashahidi wao hivyo wajitahidi Juni 16 mashahidi hao wafike mahakamani

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Mei 27 mwaka 2011.

AG,MAHANGA WAOMBA KESI YA MPENDAZOE IFUTWE

Na Happiness Katabazi

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali na Naibu Waziri Dk.Makongoro Maganga wamewasilisha mapingamizi matatu ya kuomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, iifute kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 wa Jimbo la Segerea iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge (CHADEMA) Fred Mpendazoe dhidi ya Mbunge wa sasa Mahanga, kwa madai kuwa hati ya madai ya kesi hiyo ina mapungufu.


Mbali na Mahanga ambaye anatetewa na wakili wa kujitegemea Jerome Msemwa,wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Segerea ambao wanatetewa na wakili wa serikali David Kamwaga.

Kesi hiyo ambayo ilikuja jana mbele ya Jaji Profesa Ibrahim Juma kwaajili ya kuanza kusikilizwa,wakili wa serikali alidai kuwa upande wa AG,una mapingamizi mawikili ambayo wanaomba ama kesi hati ya madai ya kesi hiyo ifanyiwe marekebisho au kesi ifutwe kwa kabisa kwasababu kuna baadhi ya paragrafu zimenasomeka kuwa Mpendazoe anaidi vituo 120 vya Kiwalani,vituo viwili vya Buguruni, vituo viwili vya Kipawa ambavyo vyote hivyo vilikuwa ni vituo vya kupigia kura na kura kura zake hazikuhesabiwa.

Wakili huyo wa serikali alidai pingamizi la kutaka kesi ifutwe ni kwa hati hiyo ya madai kushindwa kutaja majina ya majina ya wasimamizi wa Uchaguzi waliokiri kuwa kuna baadhi ya vituo walijumlisha kura za matokeo katka makaratasi ambayo hayakuwa yameandaliwa na Tume ya Uchaguzi kwaajili ya kujumlishia matokeo.

Kwa upande wake wakili Mahanga, Msemwa alianza kwa kudai kuwa yeye alikuwa na jumla ya mapingamizi mawili yakutaka kesi hiyo ifutwe lakini pingamizi moja kwa hiari yake ameamua kuliondoa na badala yake akawasilisha pingamizi moja ambalo linaomba kesi ifutwe kwasababu mlalamikaji alifungua kesi hiyo moja kwa moja kwa jaji wakati kesi hizo za usajili zinatakiwa katika hatua za awali zianze kusikilizwa na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Akipangua mapingamizi hayo, wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatara aliomba mahakama hiyo iyatupilie mbali mapingamizi hayo kwasababu hayana msingi.Akichambua mapingamizi ya wakili wa serikali ,alidai kuwa kama kweli walikuwa wakitaka kufahamu majina ya vituo ambavyo kura zao hazikuhesabiwa na majina ya wasimamizi wa uchaguzi ambao walikiri kuwa walijumla kura katika karatasi ambazo hazijatolewa na Tume ya Uchaguzi, wadaiwa hao walipaswa wawasilishe maombi mahakamani ya kuomba upande mlalamikaji(Mpendazoe)awapatie majina ya vituo na majina ya wasimamizi hao na kuongeza kuwa Sheria ya Kesi za Madai ya mwaka 2002, inawataka wafanye hivyo na kwamba anashangaa wameshindwa kuwasilisha maombi hayo mahakamani badala yake wanakimbilia kuomba kesi ifutwe.

Wakili Kibatara akijibu pingamizi la Msemwa, alidai pingamizi hilo pia halina msingi kwani kiutaratibu siku zote mlalamikaji anayefungua kesi za madai jukumu lake nikuwasilisha hati yake ya madai katika masijala ya kesi za madai mahakamani na uongozi wa masijala hiyo ndiyo wenye jukumu la kupeleka hati hiyo ya madai kwa mamlaka husika ambapo mwisho wa siku mamlaka husika za mahakama ndiyo umpanga jaji wa kusikiliza kesi husika na kuongeza kuwa wao walifuata taratibu zote za kufungua kesi hiyo katika masijala ya madai mahakamani hapo na wakalipia ada kufungulia kesi na mwisho wa siku mahakama hiyo ndiyo iliyowapatia jina la jaji wa kusikiliza kesi hiyo.

Kwa upande wake Jaji Profesa Ibrahim Juma ambaye awali alipanga kuanza kusikiliza kesi mfululizo kuanzia jana hadi kesho, alisema amesikiliza hoja zote zilizowasilishwa na pande mbili na anaiarisha kesi hiyo hadi Juni 6 mwaka huu, ambapo siku hiyo atatoa uamuzi kuhusu hoja hizo.

Novemba mwaka jana Mpendazoe alifungua kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Jimbo hilo ambayo yalimtangaza mbunge wa sasa Dk.Mahanga kuwa ndiye mshindi kwasababu uchaguzi huo ulikiuka matakwa ya sheria ya Uchaguzi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Mei 26 mwaka 2011.

HUKUMU KESI YA EPA :YAMETIMIA


.MARANDA,FARIJALA JELA MIAKA MITANO
.WASHTAKIWA WENGINE WA EPA MATUMBO MOTO
.HUKUMU YAWALIZA NDUGU,JAMAA
Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ilitoa hukumu ya kwanza katika kesi ya wizi wa sh bilioni 1.8 zilizochotwa kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), mali ya Benki Kuu (BoT).


Hukumu hiyo ilizusha vilio na kuifanya mahakama hiyo kuzizima kwa muda baada ya Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma Rajab Maranda na binamu yake Farijala Hussein kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Katika kesi hiyo, ndugu hao makada wa CCM wanadaiwa kughushu nyaraka na kujipatia sh bilioni 1.8 isivyo halali kutoka kwenye akaunti hiyo. Hiyo ni miongoni mwa kesi 14 za EPA zilizopo mahakamani.

Jopo la mahakimu wakazi likiongozwa Saul Kinemela lilianza kusoma hukumu hiyo kwa saa moja ndani ya ukumbi namba mbili wa mahakama hiyo.

Mahakimu wengine ni Phocus Bambikya Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani na Elvin Mugeta, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akisoma kwa kujiamini Hakimu Mugeta alisema kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo Novemba 4, 2008 ambapo jumla ya mashahidi tisa upande wa Jamuhuri walitoa ushahidi wao.

Hakimu Mugeta aliikumbusha mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao walikabiliwa na makosa nane ambayo ni kula njama kwa nia ya kutenda kosa, wizi wa sh bilioni 1.8 na kughushi hati ya kuhamisha deni (deed of asssigment) inayoonyesha kampuni hewa ya Kiloloma & Brothers imepewa idhini ya kukusanya deni la kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai ya India.

Makosa mengine ni kughushi hati ya jina la biashara la kampuni hiyo inayoonyesha imetolewa na Msajili wa Makampuni (BRELA), kuwasilisha nyaraka zilizoghushiwa BoT, kuwasilisha nyaraka hizo kwenye Benki ya Afrika (BOA), kufungua akaunti na kujipatia ingizo la kiasi cha sh 1,864,949,294.45 isivyo halali.

“Baada ya kupitia hati ya makosa hayo, kupitia ushahidi na utetezi uliotolewa na pande zote mbili, jopo hili limefikia uamuzi wa kuwatia hatiani washtakiwa hao kwa kosa la pili, tatu, nne, tano, sita na saba.

“Na kwamba mahakama imeshindwa kuwatia hatiani kwa kosa la kwanza ambalo ni kula njama na kosa la nane ambalo ni wizi kwa sababu upande wa jamuhuri umeshindwa kuthibitisha kwamba washtakiwa hao walikula njama na kuiba katika BoT,” alisema Hakimu Mugeta huku ndugu na jamaa wakijifuta machozi ndani ya chumba cha mahakama.

Hakimu huyo alisema jopo hilo linakubalina na ushahidi wa jamuhuri kuwa washtakiwa hao walighushi nyaraka hizo kwa sababu mashahidi watatu ambao ni Ofisa wa Polisi Salum Kisai, Mkurugenzi Mtendaji wa BRELA, Esteriano Mahingira, na Neema Kitambi Ofisa wa Benki ya BOA.

Katika ushahidi wao, waliithibitishia mahakama hiyo kuwa nyaraka na saini iliyokuwa kwenye hati hiyo na jina la biashara ya Kampuni ya Kiloloma&Brothers vilighushiwa.
“Kwa mujibu wa utetezi wa Maranda na Farijala, nyaraka hizo hazikuandaliwa na wao bali ziliandaliwa na Charles Issack Kissa… sasa mahakama hii imejiuliza kwa nini washtakiwa hao wasingemleta huyo Kissa kama shahidi wao ili awatetee?

“Kwa kuwa hawakumleta Kissa mahakama hii inakubaliana na upande wa jamuhuri kuwa huyo ni mtu wa kufikirika na kwamba Kissa ndiyo Farijala aliyeghushi nyaraka hizo,” alisema Hakimu Mugeta aliyekuwa anavuta pumzi kwa kunywa maji.

Akiendelea kuichambua hukumu hiyo, Mugeta alisema katika utetezi wao washtakiwa walikiri kwa hiyari yao ni wamiliki wa kampuni ya Kiloloma & Brothers na kwamba walifungua akaunti ya pamoja katika Benki ya Afrika na kujipatia kiasi hicho cha fedha kutoka BoT.

Kwa upande wake Maranda alikiri pia kuhusika na mchakato wa kudai deni hilo na kweli alipewa idhini na kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai, India kudai deni hilo kwa kuwa alichokizingatia ni fedha, sio uhalali wa nyaraka zilizotumika kupata fedha hizo.

Hakimu huyo alisema jopo hilo limeukataa utetezi wa washtakiwa kwa kuwa hauna msingi hivyo Mahakama inakubalina na upande wa Jamuhuri kwamba washtakiwa hao na watu wengine wasiyofahamika ndani ya jiji la Dar es Salaam mwaka 2005 walighushi nyaraka hizo na kujipatia mabilioni ya fedha.

Baada ya kuwatia hatiani washtakiwa hao, jopo hilo lilitoa fursa kwa upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali Stanslaus Boniface wakati upande wa utetezi uliwakilishwa na Wakili wa kujitegemea Majura Magafu, kusema lolote kabla ya adhabu kutolewa.

Wakili Boniface aliyekuwa akisaidiwa na Wakili Shadrack Kimaro, aliieleza Mahakama kuwa kwa kumbukumbu zinaonyesha hii ni mara ya kwanza kwa washtakiwa hao kutiwa hatiani hivyo ione haja ya kuwapa adhabu kali kwa kuzingatia kiasi kikubwa cha fedha kilichopotea.

Aidha, aliiomba mahakama kutumia kifungu cha 358 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 ili itoe amri kwa washtakiwa kurejesha kiasi hicho cha fedha kwa mwenye mali ambaye ni serikali ama wafilisiwe mali zao.

Kwa upande wake wakili Magafu aliiomba mahakama kuwaonea huruma washtakiwa kwa kuwa ni mara ya kwanza kutiwa hatiani, pia ni wagonjwa wa figo, wanategemewa na familia zao na kwamba makosa mengine waliyatenda bila kujua au kutoelekezwa vema na taasisi husika.

Magafu pia aliiomba mahakama kutumia kifungu cha 38 (1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 kinachoeleza kuwa pamoja na mahakama kumtia hatiani mshtakiwa, inaweza kumwachilia huru kwa masharti hivyo kuliomba jopo hilo kuzingatia kifungu hicho litakapotoa adhabu.

Akisoma adhabu baada ya kusikiliza maombi ya mawakili wa pande zote, Hakimu Mugeta alisema jopo hilo limezingatia maombi yao mawakili na uzito wa makosa hivyo limewatia hatiani katika kosa la pili ambalo washtakiwa wote watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Kwa mujibu wa hakimu huyo, kosa la tatu ambalo washtakiwa wote wametiwa hatiani kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka mitano jela wakati kosa la nne washtakiwa hao watatumikia miaka mitano jela.

Aidha, katika kosa la tano Maranda amepatikana na hatia hivyo atatumikia miaka miwili jela huku kosa la sita ambalo washtakiwa wote wametiwa hatiani, kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela na shtaka la saba lililowatia hatiani wote, watatumikia kifungo cha miaka miatatu jela.

Hivyo watuhumiwa hao walihukumiwa kifungo cha miaka 21 adhabu itakayokwenda kwa pamoja ambapo watatumikia miaka mitano jela.

Baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo jopo la mahakimu liliondoka na kufanya ndugu, jamaa na marafiki wa watuhumiwa hao wakiangua vilio kwa sauti ya juu kisha askari polisi waliwatoa kizimbani washtakiwa hao na kuwapeleka mahabusu ya mahakama hiyo kusubiri taratibu za kiutawala ili wapelekwe kuishi makazi mapya katika Gereza la Ukonga.

Tangu saa 5:22 asubuhi washtakiwa hao walihifadhiwa kwenye mahabusu ya mahakama hiyo huku Tanzania Daima ikishuhudia jamaa zao wakihaha huku na kule na wengine kununua maji, dawa za miswaki, sabuni na maziwa kwa ajili ya wafungwa hao ambao waliondolewa mahakamani hapo saa 9:30 alasiri kwa gari aina ya Toyota Land Cruser lenye namba za usajili SCN 9008K mali ya Jeshi la Polisi.

Wakati Farijala na Maranda wanaondolewa katika eneo la mahakama hiyo, askari kanzu na waliovalia sare wakiwa na silaha kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na wafungwa hao walipandishwa kwenye gari la wazi na kuketi nyuma mithili ya ‘maharusi’ huku wakiwapungia mikono watu waliofurika mahakamani hapo.

Baadhi ya wananchi waliotoa maoni yao walisema adhabu hiyo ni ndogo ikilinganishwa na kiasi cha fedha kilichochukuliwa na kuipongeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kazi nzuri ya kutoa ushahidi ulioiwezesha mahakama kuwatia hatiani wafanyabiashara hao.

Kwa mwingine baadhi ya mawakili wa kesi nyingine za EPA walisema hukumu hiyo ni ishara mbaya kwa wateja wao na kwamba kesi hizo sio usanii kama ilivyokuwa ikidhaniwa na wengi.

Jumla ya kesi 14 za EPA zilifunguliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka, Eliezer Feleshi, Novemba 4, 2008 dhidi ya washtakiwa mbalimbali wakiwemo mfanyabiashara maarufu nchini Jayantkumar Chandubhai Patel ‘Jeetu Patel na wenzake na baadhi ya maofisa wa BoT ambao kesi zao zinaendelea mahakamani hapo.

Jumla ya kesi 14 za EPA zilifunguliwa na DDP- Feleshi kwa kishindo kwa mara ya kwanza Novemba 4 mwaka 2008 dhidi ya washtakiwa mbalimbali wakiwemo mfanyabiashara maarufu nchini Jayantkumar Chandubhai Patel ‘Jeetu Patel na wenzake na baadhi ya maofisa wa BoT ambao bado kesi zao zinaendelea kusikilizwa mahakamani hapo.

Mbali na kesi hiyo Na.1161/2008 ambayo jana ilitolewa hukumu, Maranda na Farijala pia wanakabiliwa na kesi nyingine ya wizi wa Sh milioni 207 ambapo anashtakiwa yeye na maofisa wa BoT, Mkuu wa Idara ya EPA, Iman Mwakosya na Kaimu Mkurugenzi wa idara hiyo Ester Komu, na Katibu wa Benki Bosco Kimela.

Katika kesi hiyo ya wizi Maranda anadaiwa kutumia nyaraka za kughushi kuonyesha kampuni yake ya Rashaz Tanzania kuwa imepewa idhini ya kudai deni la kampuni ya Rashaz T Ltd na kisha kujipatia ingizo hilo la Sh milioni 207 huku akijua si kweli.

Kesi ya tatu ya jinai ni kesi Na. 1164/2008 ya wizi wa shilingi bilioni 3.8 katika akaunti hiyo ambayo inasikilizwa mbele ya jaji Beatrice Mutungi, Hakimu Mkazi Samwel Karua na Elvin Mugeta. Katika kesi hiyo, washitakiwa Farijala, Maranda, Iman Mwakosya, Ester Komu, Ajay Somani na Sophia Lalika walitumia kampuni ya Mibale Farm kuonyesha imepewa idhini ya kudai deni la kampuni ya Lakshmi Textile Mills co. Limited ya India huku wakijua si kweli.

Juni 11 mwaka 2009, mahakama hiyo ilimuona Maranda na Farijala ambao wanakabiliwa na jumla ya kesi nne za wizi katika EPA, kuwa wana kesi ya kujibu katika kesi Na.1161/2008 ambayo ilitolewa hukumu jana na kwamba upande wa Jamhuri unaowakilishwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Stanslaus Boniface aliyekuwa anasaidiwa na Timon Vitalis, Frederick Manyanda na Shadrack Kimaro umeweza kuthibitisha kesi yao.

Juni 6 mwaka 2009, Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Boniface aliwasilisha majumuisho ya kesi hiyo akiiomba mahakama hiyo iwaone washtakiwa wote hao wana kesi ya kujibu, kwani Jamhuri imeweza kuthibitisha kesi hiyo na kwa hiyo washtakiwa hao wana kila sababu ya kujibu kesi inayowakabili.

Aidha, Aprili 29 mwaka 2010, Rajabu Maranda alipanda kizimbani kutoa utetezi wake katika kesi hiyo ambayo leo inatolewa hukumu ambapo aliieleza mahakama hiyo kuwa alichokuwa akikizingatia katika mchakato wa kudai deni katika (EPA) ni kupata fedha na si kutazama nyaraka.

Itakumbukwa kuwa serikali kupitia Mkurugenzi wa Mashtaka (DDP) Feleshi iliwaburuza mahakamani watuhumiwa wa wizi katika akaunti ya EPA, baada ya tuhuma kuibuliwa na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utoo, kelele za wananchi na wafadhili, hali iliyosababisha Rais Kikwete kuunda Tume ya uchunguzi wa wizi huo ambayo ilimshirikisha Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP-Said Mwema, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Dk. Edward Hosea na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye kwa sasa amestaafu, Johnson Mwanyika.Tume hiyo iliwahoji watuhumiwa na hatimaye kuwafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 24 mwaka 2011.

WANAHABARI TUJITAZAME UPYA


Na Happiness Katabazi

WIKI iliyopita Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari(MCT), Kajubi Mkajanga alinukuliwa na vyombo vya habari akikemea tabia ya baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuchapisha na kutangaza habari ambazo zinaleta misuguano ya viongozi wa dini na taasisi hizo.


Kajubi pamoja na mambo mengi alikemea pia taabia ya wanahabari kushindwa kusimama kwenye maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na matokeo yake wamekuwa wakitangaza na kuchapisha habari ambazo zinaleta madhara katika baadhi ya taasisi za kidini, wananchi na jamii kwa ujumla hali iliyodai haipo kwenye utamaduni wa nchi yetu.

Fukuto la Jamii linaunga mkono hoja ya Mkajanga ambaye naye pia ni mwanahabari kitaaluma kwamba hivi sasa umezuka uandishi wa kuleta uchochezi wa kijaami.Lakini kwa wale wanaomfahamu Mkajanga kufuatilia matamko yake watakubaliana nami yeye ni miongoni mwa wanahabari wa zamani ambao wamekuwa wakitoa matamko ya kukemea aina ya uandishi unapofanywa hivi sasa na wanahabari na waandishi wa kizazi hiki ambao kwa kiasi fulani usipodhibitiwa mwisho wa siku unaweza kulitumbukiza taifa shimoni.

Mkajanga kupitia Baraza la Habari (MCT) kila kukicha wamekuwa wakikemea hali hiyo lakini cha kusikitisha baraza hilo Fukuto la Jamii leo linadiriki kutamka bayana baraza hilo halina meno na linaitaji kupatiwa meno hili liweze kung’ata vyombo ya habari ambavyo vinatangaza au kuchapisha habari ambazo zinakwenda kinyume na miiko ya taaluma.

Baraza hilo kila kukicha kulalamika mbele ya jamii au kuwaita wahariri ambao vyombo vyao vimechapisha habari zisizo na maadili au kufanyakazi za usuluhishi,haitoshi kabisa.Tunataka Baraza hilo ama liiambie serikali au limweleze mfadhili wake kwamba wakati umefika sasa wakuifanyia mabadiliko ya muundo na sera ya baraza hilo ili kipengele cha kuweza kuvibana vyombo vya habari na kutoa adhabu kali kwa mhariri,chombo na mwandishi waliohusika kuandika habari zisizokidhi viwango vya kitaaluma.

Mbona taaluma zingine kama mawakili, madaktari,wahandisi wana mabaraza yao na Kamati za Maadili ambapo pindi mwanataaluma wake anapokiuka miiko ya taaluma yake uweza kumshughulikia kikamilifu?Kwanini sisi wanahabari hatuna chombo chenye meno cha kuweza kutushughulikia hadi tumsubiri Waziri wa Habari ndiyo atoe amri ya kufungia gazeti?

Hiyo ni sura moja ya mada ya leo ,sura ya pili ya makala ya leo inajumuisha waandishi wa habari,wahariri, yombo vya upelelezi, mahakama na wananchi wenyewe.

Dhima nzima ya ujumla ya makala ya leo ninazungumzia aina ya uhandishi wa habari na jinsi ya wananchi wengi wakati mwingine wasiyofahamu ajenda iliyopo kwenye hizo habari au makala wanazosishabikia.Kila siku binafsi napenda kuipongeza serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete kwani katika utawala wake uhuru wa wananchi kujieleza na vyombo vya habari umekuwa ukikua kila kukicha na katika hili katika maisha yangu yote nitaikumbuka serikali ya awamu ya nne.

Lakini pia nitaendelea kuilaumu serikali inayoongozwa na rais Kikwete kwa kushindwa kuchukua hatua kwa baadhi ya vyombo vya habari ambavyo wakati mwingine vimekuwa vikichapisha habari kiushabiki, za uongo na za kuleta uchochezi wazi wazi.Na mifano hayo ninayoisema ni mingi lakini Idara ya Habari ,Vyombo vya Upelelezi, Mahakama,mahakama vipo kwenye lindi la usingi mzito sana kana kwamba hawazisomi habari hizo.

Mfano mzuri ni miongoni mwa waandishi wa habari za mahakama,kuna wenzetu ambao kwa ujinga wao hawataki kujifunza wala kuuliza maofisa wa mahakama,kusoma majalada ya kesi ili kufahamu kilichoandikwa kwenye jarada hilo wamekuwa wakiandika habari kuhusu kesi fulani zikiwa na makosa makubwa na upotoshaji.

Mfano hakimu ametoa uamuzi(ruling)- mwandishi anasema hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Flora Mushi ametoa hukumu(Judgment),hakimu ameifuta kesi ya kuvunja na kuiba katika ghala Kampuni inayozalisha kinywaji cha Konyagi,Tanzania Distillers Limited ,inayowa wakabili walinzi wa Kampuni ya KK Security,chini ya kifungu cha 225 cha Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Waandishi wengine walioripoti kufutwa kwa kesi hiyo bila woga waliliropiti kuwa hakimu huyo ametumia kifungu cha 225 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Huku ukweli ni kwamba kifungu hicho kipo ndani ya Sheria ya Makosa ya Jinai ambacho kinampa mamkala hakimu hakimu kuifuta kesi isipokuwa kesi ya kughushi na kinataka ndani ya siku 60 upelelezi wa kesi uwe umekamilika.

Sasa upotoshwaji wa aina hiyo tena wa mwenendo wa kesi za mahakama unaofanywa na baadhi ya waandishi tena waandamizi wasiotaka kuuliza, kujifunza na matokeo yake mwisho wa siku heshima ya gazeti ndiyo inayoporoka mbele ya wasomi wa sheria na wale wanaofahamu kifungu cha 225 cha Sheria ya makosa ya jinai, kinasema nini na kwamba kifungu hicho si cha Katiba.

Wakati uongo na ujuha huo ukiendelea kufanywa na baadhi ya wanahabari ambao unasababisha jamii kukaririshwa na kuaminishwa vitu vya uongo,hatujasikia uaongozi wa mahakama au hakimu husika anayeendesha kesi kukemea upotoshwaji huo wazi na mwisho wa siku baadhi ya wanahabari wasiyo makini wanaendelea na mchezo huo kwa kuzipotosha habari za kimahakama.

Kuhusu habari za kisiasa, baadhi ya wanahabari ambao hivi sasa wengi wao wameanza kushindwa kudhibiti mihemko yao kuhusu mapenzi yao na vyama fulani au ushabiki wa wanasiasa fulani,miongoni mwao wamekuwa wakiandika habari ambazo kwa maslahi yao binafsi na siyo ya taifa wamekuwa wakiandika habari ama wakiwanukuu au kuficha majina ya wanasiasa wanaowapenda wao au chama wanachokipenda wao ambazo mwisho wa siku zimekuwa zikileta misuguano baina ya vyama na jamii.

Baadhi ya vyombo vya habari wakati mwingine vimejikuta vinachapisha habari ambazo zinaisu taasisi fulani au mtu fulani bila hata ya kutoa nafasi kwa mhusika aliyetuhumiwa na taarifa hizo ambazo wakati mwingine hazionyeshi chanzo cha taarifa hizo ni nini, kujieleza.

Na baadhi ya wananchi hao wanaokumbwa na kadhia hiyo ya habari zinazowahusu kuchapishwa bila wao kupewa fursa ya kueleza anachokijua, wamekuwa wakikimbilia mahakamani kufungua kesi za kudai fidia za kashfa dhidi ya baadhi ya magazeti na wengi wao wamekuwa wakishinda kesi hizo lakini cha kusikitisha mwandishi wa habari za mahakama ambao uzipata nakala za hukumu za wananchi hao walioshinda kesi hizo unapofika kwenye chumba cha habari na kumweleza mwariri wako kuwa kuna mwananchi mmoja ameshinda kesi dhidi ya gazeti fulani,baadhi wahariri ukataa habari hiyo isichapishwe kwa kigezo kuwa wahariri walishafanya makubaliano yao ya siri ambayo yanakataza gazeti jingine lisiandike habari kuhusu gazeti jingine ambalo limetiwa hatiani na mahakama kwa kuchapisha habari fulani ya uongo.

Mfano huo hapo juu ni wa kweli na nimeushuhudia mimi binafsi.Na nina diriki kusema wazi kwamba kama kweli nyie wahariri wetu mliingia makubaliano hayo ya kifedhuli ambayo ni wazi kabisa yanakwenda kinyume na Ibara ya 18(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; ambayo inasema ‘kila mtu anayohaki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii;’.

Lakini kwa watu tunaotunza kumbukumbu kichwani ,tunajiuliza ni kwanini vyombo vingine vya habari vikifikishwa mahakamani,baadhi ya vyombo vingine ulipoti kesi hizo hadi zinapotolewa hukumu lakini ni kwanini vyombo vingine vinaripoti habari za kesi hizo tena hao hao wahariri wanaosema kuna azimio wamelipitisha la kutoandikana,wanaziruhusu habari za kesi hizo zichapishwe na gazeti analoliongoza?

Na kama hilo ni kweli wananchi tuwaulize hao wahariri wetu nani amewapa madaraka ya kuvunja ibara hiyo ya sheria?Kwa hiyo ni haki kwa vyombo vya habari kuchapisha habari zinazowashushia heshima na kuwaletea usumbufu baadhi ya wananchi zichapishwe lakini si haki kwa wananchi walioshuhiwa heshima habari zao za kulifungulia kesi gazeti kuchapishwa gazetini?

Sasa kumbe tunailaumu nini serikali kuwa inalindana wakati sisi vyombo vya habari ndiyo tunalindana katika kuficha makosa yetu ambayo tena mahakama ndiyo imeuanika udhahifu wetu kupitia hukumu mbalimbali?

Wakati baadhi ya vyombo vya habari vikichapisha na kutangaza habari ambazo hazina maadili,upotoshaji na uchochezi tunavishuhudia vyombo vya upelelezi vikishindwa kufurukuta kuvichukulia hatua vyombo hivyo ambavyo hali ilivyo hivi sasa wananchi wengi wamekuwa wakiamini kila kinachoandikwa na magazeti hata kama ni cha uongo kwani wazi hivi sasa watu wengi hawaudhulii mikutano ya adhara ya vyama vya siasa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma wakati vyama vingi vimeanzishwa hapa nchini na badala yake wamekuwa wakifuatia mikutano hiyo kupitia vyombo vya habari.

Sasa inapotokea na sisi vyombo vya habari tunashindwa kuripoti habari kwa usahihi bila kuweka ushabiki ,unakuta wananchi hao wakiamini habari hiyo.Lakini kwa sisi wajanja ambao tumeishang’amua uwendawazimu huo wa upotoshwaji unaofanywa na baaadhi ya wanataaluma wenzetu tena kwa maslahi binafisi, tumekuwa na utaratibu kuzichambua sana habari hizo na pia kuwauliza waandishi zaidi ya wanne walioudhulia ama mkutano huo ili kujua ukweli ni upi.

Ikumbukwe kuwa karibu nchi nyingi zilizowahi kukumbwa na machafuko ama ni wanasiasa au vyombo habari vilishiriki kikamilifu kuchochea machafuko hayo ambayo yalileta maafa.Na mfano mzuri ni machafuko yaliyotokea nchini Rwanda miaka ya 1990.Lakini baada ya vita kumalizika nchi hiyo ikapata kiongozi wa nchi ambaye ni Rais Paul Kagame ambaye aliahidi na akatekeleza kuwafikisha mahakamani waandishi,wanasiasa na wanajeshi waliohusika na machafuko hayo.

Na kweli tumeshuhudia wanajeshi ,waandishi wa habari waliochochea mauji ya Rwanda wakifikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu dhidi ya Binadamu iliyopo mkoani Arusha wakipatikana na hatiani ya makosa ya uchochezi na hivi ninavyoandika makala hii wapo magerezani wanatumikia adhabu zao.Na kutokana na hukumu hizo ,inaelezwa waandishi wa Rwanda hivi sasa wanaheshimu na wanazingatia utaifa na maadili ya taaluma zao.

Hapa Tanzania bado hilo la vyombo vya habari vinavyochaposha habari za kichochezi kufikishwa kortini halijafanyika na siku likifanyika nitafurahi sana. Kwani hata Baba wa Taifa Hayati Julias Nyerere alishawahi kusema ; ‘ Uhuru bila nidhamu ni sawa na uwendawazimu na nidhamu bila uhuru ni sawa na utumwa’.

Nyerere hakuwa mpumbavu kutamka maneno hayo alikuwa anasema anachokimaanisha ambacho katika utawala huu wa Rais Kikwete ni kweli uhuru wa kutoa maoni,vyombo vya habari umepanuka lakini baadhi ya vyombo vya habari,wanasiasa na wananchi wameshindwa kabisa kuutumia uhuru huo kwa nidhamu na vyombo vya upelelezi, na taasisi nyingine za serikali zenye dhamana ya kukomesha hali hiyo vimelala usingizi wa pono hali inayosababisha taratibu baadhi ya vyombo vya habari na waandishi kujifanya vipo juu ya sheria.

Siku Jeshi la Polisi chini ya IGP-Said Mwema litakapashirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtka(DDP),Eliezer Feleshi kumfungulia kesi ya jinai mwandishi na mwariri kwa kosa la kuandika na kuchaposha habari za uchochezi mahakamani naamini na mwisho wa siku kama ushahidi wa jamhuri utaweza kuishawishi mahakama kuwatia hatiani watu hao, nafikiri ndiyo itakuwa mwanzo na mwisho wa wahariri,wanahabari wanaoandika habari za uchochezi ,uongo na zinaleta ,misuguano isiyoyalazima ndani ya jamii yetu.

Tunachokishuhudia sasa ni baadhi ya wananchi wanaodhani wamechafuliwa majina yao na vyombo vya habari ndiyo wamekuwa wakifungua wao wenyewe mahakamani kudai fidia.Hatua ambayo hivi sasa baadhi ya wahariri na waandishi hawaiogopi kabisa kwani wamekuwa wakisema mwisho wa siku mahakama ndiyo itaitia hatiani kampuni ,gazeti na mchapishaji na kuimaru imlipe fidia mlalamikaji huyo na siyo mwandishi aliyeandika habari iliyoleta madhara kwa mwananchi mwengine na ndiyo maana kila kukicha baadhi ya habari ambazo hazikidhi matakwa ya kitaaluma zimekuwa zikiendelea kuchapishwa na hakuna mamlaka ya serikali inayochukua hatua.

Fukuto la Jamii linapenda kuona Taifa la Tanzania linakuwa na wanataaluma wanaoheshimu taaluma zao na wanaofanyakazi zao kwa kuzingatia maadili na kanuni za taaluma zao.Hivyo sisi vyombo vya habari tuamke na kusimama kwenye misingi ya haki,ukweli na taaluma.Kwani tukae tukijua tunavyochapisha kwa makusudi habari ambazo hazijakidhi vigezo vya kitaaluma tunawaumiza wananchi wenzetu.

Tukumbuke viongozi wa madhebu ya dini zetu wamekuwa wakituasa kwa kutumia vitabu vya dini kwamba tutendeane yaliyomema na wengine hivi sasa wamekuwa wakituambia malipo ya matendo mema au mabaya tunayoyafanya tutalipwa hapa hapa duniani.Hivyo ni kheri mwenyezi mungu atulipe mema kutokana na matendo mema tunayowafanyia wenzetu.

Kwani kupitia habari zetu za uongo, majungu, fitna ambazo miongomini mwetu wamekuwa wakiziandika wakati mwingine zimekuwa zikisababisha watu kupoteza maisha, kufukuzwa kazi,kuamishwa vituo vya kazi ama kufukuzwa kazi hata kusambaratisha ndoa zao.

Kwa hiyo ni vyema na haki kila mwanahabari kwa nafasi yake akawa na hofu ya mungu, kuzingatia maadili ya taaluma yake, kuepuka kutumika na baadhi ya wanasiasa au maofisa wa seriakali ambao wamekuwa na magomvi binafsi maofisini kwao bila siye kujua sasa wanaona njia ya kumkomesha mbaya wake ni kwenye vyombo vya habari.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 24 mwaka 2011.

KESI YA SAMAKI WA MAGUFULI-MELI HAIKUWA NA KIBALI CHA UVUVI-SHAHIDI

Na Happiness Katabazi

KAMISHNA Msaidizi wa Polisi(ACP) Charles Mkumbo(46) ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuwa ndugu wawili wa raia wa kigeni 36 wanaokabiliwa na kesi ya uvuvi haramu katika Bahari ya Hindi katika kina kirefu cha Ukanda wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walimpatia kibali cha uvuvi cha meli ya Tawariq 1 ambacho kilikuwa kimeisha muda wake.


ACP-Mkumbo alitoa maelezo hayo wakati akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili Mwandamizi wa Serikali Biswalo Mganga na Prosper Mwangamila alidai kuwa yeye ndiye aliyeongoza timu ya makachero wa Jeshi la Polisi kufanya upekuzi wa meli na washtakiwa hao alidai kuwa Machi 10 mwaka 2009 ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam(ZDCO) siku hiyo alikuwa bandarini na timu yake.

Mkumbo ambaye hivi sasa anafanyiakazi Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai siku hiyo raia wawili China ambao ni Zhao na Xhu ambao nao ni washtakiwa walimfuata na kujitambulisha kwake kuwa wao ni mawakala wa Tawariq 1 ambao wametokea Mombasa na wakamtaka awaachie mara moja raia hao wa kigeni kwa madai kuwa walikuwa wakipita katika Bahari ya Hindi ukanda wa Tanzania kuelekea Mombasa nchini Kenya.

“Minilikataa kuwachiria huru na kuwaeleza nilipata taarifa za kipelelezi kuwa raia hao wakigeni walikuwa wakivua bila leseni kwenye eneo la Tanzania na kitendo hicho ni kosa ....na washtakiwa hao wakanijibu kuwa walikuwa na kibari cha kuvua na nikawataka wathibitishe hilo ndio Zhao leseni inayoirusu meli hiyo ivue;

“Niliisome hiyo leseni ambayo inayoonyesha imetolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa meli ya Tawariq 1 na kwamba leseni hiyo ilimalizika muda wake wa matumuzi Desemba 22 mwaka 2008.Ndipo nikaanza kutilia mashakata kauli hizo mbili wale ndugu zao wawili walisema washtakiwa hao walikuwa wakipita njia na meli yao wakielekea Mombasa na leseni hiyo inayonyesha imekwisha muda wake na mimi kama mpelelezi mkuu nilifikia uamuzi wa kuwakamata hata hao ndugu wawili na kuwaunganisha na washtakiwa hao wengine ambao jumla yake sasa wapo 36.

Aidha Mkumbo alidai kuwa hadi yeye na timu yake wanamaliza upelelezi kuhusu kesi hiyo hajawahi kupata mawasiliano toka ofisi za balozi zozote za kigeni wala Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa nchi kuhusu ukamatwaji wa meli hiyo.Jaji Agustine Mwarija aliairisha kesi hiyo hadi Jumatatu shahidi wa 13 atakapoanza kutoa ushahidi wake.Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mfululuzio hadi Mei 31 mwaka huu.

Machi 9 mwaka 2009 washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya uvivu haramu katika kina kirefu cha habahari ya Hindi Ukanda wa Tanzania na kuharibu mazingira ya ukanda huo.Hadi sasa washtakiwa wanaendelea kusota rumande kwa kukosa dhamana.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi,Mei 21 mwaka 2011.

GAZETI LA MTANZANIA LATAKIWA LIMPE MIL.45 ALIYESANIFU JENGO LA SOKO LA KARIAKOO

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemuamuru Mhariri wa gazeti la Mtanzania na Kampuni ya Habari Corporation kumlipa fidia ya jumla ya sh milioni 45 Msanifu wa Majengo ambaye ndiye alichora ramani ya jengo la Soko la Kariakoo Dar es Salaam,Beda Jonathan Amuli kwa kumkashfu kuwa hana taaluma ya usanifu majengo.


Wadaiwa katika kesi hiyo ya madai kashfa Na 29/2008 iliyofunguliwa na Amuli dhidi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Kariako Kuboja Ng’ungu,Mwariri wa Gazeti la Mtanzania na Kampuni ya Habari Coporation inayochapisha magazeti la Bingwa,The African, Rai,Dimba na Mtanzania ambapo mlalamikaji huyo alikuwa anaomba alipwe sh bilioni tano kama fidia ya kuchafuliwa jina lake kutokana na habari iliyochapishwa na gazeti hilo la Na 4214 la Novemba 23 mwaka 2007 iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho;

“Soko kuu la Kariakoo lipo katikati ya eneo la Kariakoo Dar es Salaam, Kitalu namba 32,limepakana katika maungano ya mitaa mine ya Nyamwezi,Mkunguni, Swahili, Sikuuu na Tandamti. Meneja Mkuu wa Soko ,Kuboja N’ungu anasema mchoro wa jengo hili ulibuniwa na Mtanzania ambaye hakwenda shule kwa ajili ya usanifu wa majengo (Local Architect)anaishi maeneo ya Kigamboni, Dar es Salaam”.

Hukumu hiyo imetolewa hivi karibuni na Jaji Profesa Ibrahim Juma ambapo alisema baada ya kupitia utetezi na vielelezo viliwasilishwa na pande zote mbili amefikia uamuzi wa kukubaliana na hoja za mlalamikaji(Amuli) kwamba habari hiyo ilimshushia heshima, haina ukweli wowote na ili mletea madhara mbele ya jamii kwani habari hiyo ilikuwa ni ya uongo kwani mlalamikaji huyo ni kweli ana taaluma ya usanifu wa majengo na shahada ya usanifu majengo aliipata katika Taasisi ya Teknolojia nchini Israel mwaka 1964.

Jaji Juma alisema mlalamikaji huyo Amuli alifaulu kwa kiwango cha juu kabisa kozi yake hiyo na kwamba ndiye alikuwa Mwafrika wa kwanza toka Tanganyika kupata shahada hiyo ya usanifu majengo na kwamba baada ya kuitimu kozi hiyo msanifu huyo alijiunga na kampuni Zevet International Architect and Engineers of Tel Aviv na kuwa kampuni hiyo ndiyo ilikuwa imeshinda tenda ya kuchora mchoro wa ujenzi wa Hoteli ya Kilamanjaro ambayo sasa inatambulika kwa jina la Kempinski.

Jaji huyo alisema kampuni ya Usanifu Majengo ya ZEVET ilimtuma mlalamikaji (Amuli) jijini Dar es Salaam kama mwakilishi wake ambapo aliweza kusimamia ujenzi wa jengo la iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro ambapo kampuni ilifanyakazi na mlalamikaji kwa miaka mitano na kisha mlalamikaji alimia katika kampuni nyingine ya usanifu majengo ya BJ AMULI na kwamba moja ya kazi kubwa kampuni hiyo iliyopata ni mradi wa ujenzi wa jengo la Soko la Kariakoo kati ya mwaka 1972-1974 na kisha mlalamikaji ndiye pia aliyechora mchoro wa jengo la Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) na Chuo cha Mafunzo cha Benki ya Taifa ya Biashara(NBC) ambacho kwa sasa ndicho Chuo Kikuu cha Ruaha mkoani Iringa.

“Kwa kazi hizo za usanifu majengo ambazo zilitolewa mahakamani hapa na mdaiwa kama vielelezo kuwa yeye ni msomi wa fani ya usanifu majengo na miongoni mwa kazi alizowahi kuzifanya kupitia taaluma yake ni hizo hapo juu na upande wa wadaiwa wameshindwa kuthibitisha madai ya mlalamikaji ,mahakama hii pia imengalia haki itendeke kwa pande zote mbili licha ni kweli habari hiyo ni kweli ilichapwa na mdaiwa wa pili na wa tatu na likasambazwa mikoa yote ya Tanzania na ni kweli ilimletea usumbufu mlalamikaji…mahakama hii inatoa hukumu ya kukubalina na madai ya mlalamikaji na ina mwamuru mdaiwa wa kwanza na wapili kumlipa fidia ya jumla ya milioni 45 pamoja na riba mlalamikaji kuanzia siku ambayo hukumu hii imesomwa badala ya bilioni tano .”alisema Jaji Profesa Juma.Hukumu imetolewa Mei 5 mwaka 2011.

Chanzo:katabazihappy.blogspot.com

MELI YA TAWALIQ 1 HAIKUWA NA BENDERA-SHAHIDI

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa 11 wa Upande wa Jamhuri katika kesi ya uvuvi haramu katika Bahari ya Hindi katika kina kirefu cha Ukanda wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayowakabili raia 36 wa kigeni maarufu kama ‘kesi ya samaki wa Magufuli’,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi(SSP), Hussein Kashinde ameileza Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alikutaka mkoba mweusi kwenye chumba cha naodha wa Meli ya Tawariq 1, kilichokuwa na nyaraka za meli ya Tawariq 2.


SSP Kashinde ambaye alikuwa mpelelezi wa kesi hiyo na ndiyo alitoa hati ya ukaguzi wa meli hiyo, alitoa maelezo hayo wakati akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili mwandamizi wa serikali Biswalo Mganga,Prosper Mwangamila na kuhojiwa na wakili wa utetezi Ibrahim Bendera alidai kuwa wakati wanafanya ukaguzi walimshirikisha naodha wa meli hiyo na pia walipoikagua meli hiyo walibaini meli hiyo pia haikuwa na bendera inayoonyesha meli hiyo ya Tawariq 1 ilikuwa ikitokea nchi gain na kuelekea nchi ipi na kwamba hakuwa na nyaraka zozote zinazoonyesha meli hiyo ilikuwa imebeba mzigo gain.

“Baada ya kuipekua meli hiyo ya Tawariq 1 kwenye chumba cha naodha nilikuta mkoba mweusi wenye nyaraka za meli ya Tawariq 2 na nilipomhoji naodha alikiri kuwa nyaraka hizo ni zao na ni za meli nyingine ambazo zinamilikiwa na mtu mmoja na kwamba wanaruhusiwa kuzitumia katika meli ya Tawariq 1 ambayo imekamatwa ambaye hakumtaja kwa jina na pia tulibaini meli hiyo hakikuwa ikipeperusha bendera ya nchi iliyokuwa ikitoka na hilo ni kosa kisheria na pia hatukukuta nyaraka ambazo zingeonyesha meli hiyo ilikuwa imebeba mzigo gani na wenye uzito gani”alidai SSP-Kashinde.

Aidha alidai alipofika Bandari jijini Dar es Salaam, ambapo meli hiyo imetia nanga hapo kwaajili ya upekuzi alikadhibiwa jumla ya hati 32 za kusafiria wakati jumla ya washtakiwa hivi sasa ni 36 na kwamba wengi hawakuwa wamempatia hati zao za kusafiria kitendo ambacho alidai kuwa washtakiwa wengine ambao hawakuwa wamemkabidhi hati zao ina maana hawakuwa na hati hizo za kusafiria.

Hata hivyo wakili wa utetezi Ibrahim Bendera alimtaka shahidi huyo akisome kielelezo cha 22 ambacho ni hati ya upekuzi ambayo imesainiwa na shahidi huyo na nahodha ambapo Bendera aliiomba mahakama imruhusu mkarimani wa lugha ya Kichina kusoma kilichosainiwa na naodha huyo kwenye hati hiyo ambapo mkarimani huyo alisoma na kuieleza mahakama hiyo kuwa naodha huyo ambaye ni mshtakiwa wa kwanza aliweka saini yake na chini ya saini yake aliandika kuwa hafahamu lugha ya kiingereza hali iliyosababisha watu kuangua kicheko.

Wakili Bendera aliendelea kumuuliza shahidi huyo ni utarabu gani aliokuwa akiutumia kuwasiliana na mshtakiwa huyo ambapo shahidi huyo alidai kuwa alikuwa akitumia mtindo wa kumweleza nahodha ambaye ni raia wa china kupitia mkarimani wa lugha ya Kichina, Rahma Mohamed na kwamba hata alipomaliza kupekua alimpatia hati hiyo nahodha aisaini na kweli aliisani na kwamba mkarimani huyo Rahma Mohamed alimsomea shahidi huyo kuwa nahodha huyo alikuwa ameweka saini yake na kwamba hilo andishi la chini ya saini ya nahodha hiyo ambayo limetafsiriwa jana na mkarimani mwingine wa lugha ya kichina kuwa kilichoandikwa na naodha chini ya saini yake kuwa ‘hafahamu lugha ya kiingereza’ ni kigeni kwake.

Jaji Mwarija aliairisha usikilizaji wa kesi hiyo hadi leo ambapo shahidi wa 12 wa upande wa Jamhuri atapanda kizimbani kuanza kutoa ushahidi.Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mfululizo hadi Mei 31 mwaka huu.

Machi 9 mwaka 2009 washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya uvivu haramu katika kina kirefu cha habahari ya Hindi Ukanda ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuharibu mazingira ya ukanda huo.Hadi sasa washtakiwa wanaendelea kusota rumande kwa kukosa dhamana.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Mei 20 mwaka 2011.

KESI YA SAMAKI WA MAGUFURI YAZIDI KUUNGURUMA

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa 10 wa Upande wa Jamhuri katika kesi ya uvuvi haramu katika Bahari ya Hindi katika kina kirefu cha Ukanda wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayowakabili raia 36 wa kigeni maarufu kama ‘kesi ya samaki wa Magufuli’, Mwanaidi Mndolwa ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,walipokagua Meli ya Tawariq 1 waliwakuta samaki wakiwa hawana vichwa.


Mndolwa ambaye ni Mtaalamu wa Uchakataji wa Samaki toka Wizara ya Maendeleo na Uvuvi ambaye pia ndiyo alikuwa ni miongoni mwa timu ya maofisa wa serikali na Jeshi la Polisi ambao ndiyo walipewa jukumu ya kuipekuwa meli ya Tawariq 1 ambayo ndiyo ilikamatwa ikivua samaki na kuaribu mazingira katika ukanda huo wa bahari ya Hindi, alitoa maelezo hayo wakati akiongozwa na wakili mwandamizi wa serikali Biswalo Mganga,Prosper Mwangamila na Mango kutoa ushahidi wake jana mbele ya Jaji Agustine Mwarija.

Mndolwa aliieleza mahakama kuwa zoezi upekuzi na upakuaji samaki toka ndani ya meli kuja kwenye majokofu lilichukua siku tisa ambapo samaki walianza kupakuliwa Machi 10-18 mwaka 2009 na wakati wanapekuwa Keptaini wa meli hiyo ambaye naye ni miongoni mwa washtakiwa alikuwepo ambapo walifanikiwa kupakua jumla ya makontena 19 na kila kontena moja lilikuwa kiifadhi zaidi ya samaki 900 na hivyo kufanya uzito huo kuwa ni wa tani 55.

“Na kufuatia upekuzi na upakuaji tuliwakuta samaki ndani ya meli hiyo ya Tawariq 1 ambao hawana vichwa na kitaalamu kutambua samaki aliyekwisha ondolewa vichwa kuwa wamevuliwa lini , huwezi kujua na samaki ambao tayari wameishaondolewa vichwa kitaalamu uweza kuishi bila kuaribika ndani ya miezi 18”alidai Mndolwa.

Mndolwa aliendelea kudai kuwa upekuzi wao ndani ya meli hiyo ulibaini meli hiyo ilikuwa na sehemu kwaajili ya kuifadhi utumbo,vichwa, mikia na kuongeza kuwa kwa mujibu wa kitaalamu meli ya uvuvi inatakiwa kuwa na eneo la kutunzia utumbo,mikia na kwamba walikuja majokofu yote yalikuwa yameifadhiwa samaki ambao wengi wao walikuwa ni aina ya Jodari, changu,vibua na ngisi na kwamba hawakukuta majokofu yaliyokuwa yameifadhi uchafu wa samaki hao.

Jaji Mwarija aliairisha usikilizaji wa kesi hiyo hadi leo ambapo shahidi wa 11 wa upande wa Jamhuri atapanda kizimbani kuanza kutoa ushahidi.Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mfululizo hadi Mei 31 mwaka huu.

Machi 9 mwaka 2009 washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya uvivu haramu katika kina kirefu cha habahari ya Hindi Ukanda ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuharibu mazingira ya ukanda huo.Hadi sasa washtakiwa wanaendelea kusota rumande kwa kukosa dhamana.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Mei 19 mwaka 2011.

MBATIA ALIPA DHAMANA MIL.9/-

Na Happiness Katabazi
HATIMAYE aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama cha (NCCR)-Mageuzi, James Mbatia atekeleza amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa vitendo, iliyomtaka alipe shilingi milioni tisa kama dhamana ya kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 dhidi ya mbunge wa sasa wa jimbo hilo kwa tiketi ya (Chadema) , Halima Mdee kuwa ndiye mbunge alishinda.

Wakili wa walalamikaji hao watatu yaani Mbatia na wapiga kula wake Hemed Manoni na Solomoni Mfunda, Mohamed Tibanyendera aliliambia Tanzania Daima jana kwenye viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alisema tayari mteja wake(Mbatia) ameishalipa kiasi hicho cha fedha katika ofisi ya Mhasibu wa Mahakama na kwamba kiasi hicho cha fedha alikkiwasilisha yeye mahakamani kwaniaba ya mteja wake.

“Mahakama hii ilitupunguzia nafuu ya kiasi cha kulipa fedha kama dhamana ya kesi iliyofunguliwa na mteja wangu hapa mahakamani ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, mlalamikaji anapaswa awe dhamana mahakamani ya shilingi milioni tano kwa kila mdaiwa hiyo mteja wangu asingeomba nafuu ya kunguziwa angepaswa kulipa jumla ya milioni 15 lakini kwakuwa aliomba apunguziwe mahakama hii ilimpunguzia kutoka kiwango hicho na kumtaka alipe jumla ya shilingi milioni kwa wadaiwa wote ambapo hapo sasa utaona kila mdaiwa anamuwekea dhamana ya shilingi milioni tatu badala ya milioni tano ya awali na kesi hiyo itakuja kwaajili ya kutajwa Mei 31 mwaka huu.”alisema Tibanyendera.

Mbali na Mdee wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo.Novemba 25 mwaka 2010 Mbatia alifungua kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo ambayo yalimtangaza Halima Mdee(CHADEMA) kuwa ndiye aliyeshinda na ataliongoza jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitano.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Mei 19 mwaka 2011.

KESI YA RICHMOND:SHAHIDI WA JAMHURI AIGEUKA JAMHURI

Na Happiness Katabazi

SHAHIDI wa tano wa upande wa Jamhuri Ruabangi Luteganya(52) ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa kampuni ya Richmond Development Company kupitia nyaraka za kuomba tenda ya kuleta mashine ya kuzalisha umeme hapa nchini ungezalisha umeme wa megawati 110.


Luteganya ambaye wakati kampuhi ya Richmond alikuwa ni Meneja Usafirisha na kwa sasa ana cheo cha Meneja Usafirishaji na Manunuzi wa Shirika la Umeme(Tanesco), aliyasema hayo jana wakati akijibu swali la wakili wa utetezi Richard Rweyongeza na Alex Mgongolwa ambao walimuuliza ni kwanini yeye anasema Richmond ilisema itazalisha umeme wa megawati 110 wakati kwa mujibu wa hati ya mashtaka Jamhuri inadai kampuni hiyo ilidanganya kuwa inauwezo wa kuzalisha megawati 100.

Shahidi huyo alieleza kuwa Machi 20 mwaka 2006 alipewa jukumu na mkuu wake wa kazi la kusimamia ufunguzi wa waombaji tenda ambapo kwa mujibu wa orodha ya makampuni yaliyoomba tenda yalikuwa jumla 23 lakini siku hiyo makampuni yaliyoudhulia kwenye kikao hicho ni kampuni 16 na kampuni ya Richmond ilikuwepo na ilikiwakilishwa na mshtakiwa Naeem Gile ambaye alikuwa amepewa nguvu ya kisheria ya kumwakilisha Mwenyekiti wa kampuni hiyo Mohammed Gile.

‘Mimi ndiyo nilikuwa nimefungua kikao cha waombaji tenda siku hiyo ambapo kampuni ya Richmond iliwakilishwa na mshtakiwa ambaye alileta kitabu ya kampuni yao kuomba tena na kwa mujibu wa kitabu cha kampuni hiyo kinaonyesha kuwa kampuni hiyo ilisema ilikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 110;

‘Sasa kuhusu hati ya mashakta ilitumika kufungulia kesi hii hapa mahakamani inadai kuwa kampuni hiyo ilidai ilikuwa ina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 100…mimi sijui walikuwa wamepata wapi hilo kwani kilichoandikwa kwenye kitabu cha kampuni hiyo na kuwasilishwa kwenye kikao uombaji tenda na ndicho hiki kitabu kimetolewa mahakamani hapa kama kielelezo kinaonyesha kampuni hiyo ilisema ina uwezo wa kuzalisha megawati 110 na siyo 100”alidai Luteganya.

Aidha shahidi huyo alieleza kuwa siku hiyo ya ufunguzi wa kikao cha uombaji tenda, mshtakiwa hakuzungumza wala kutoa taarifa yoyote kwa maneneo na kuongeza yeye akiwa kama msimamizo wa kikao cha ufunguaji tenda hakuwa amepata malalamiko toka kwenye kampuni ya Richmond kuwa mshtakiwa alikuwa ameiwakilisha kampuni hiyo vibaya na kusema kuwa kikao cha ufunguzi wa tenda uwa kumbukumbu zake urekediwa na kwamba rekodi za kikao hicho zipo.

Wakati shahidi huyo Lutenganya akijibu swali hilo la wakili wa utetezi (Rweyongeza) kuwa mshtakiwa siku ya kikao cha ufunguzi wa tenda hakuzungumza chochote, lakini katika kosa moja linalomkabili mshtakiwa huyo (Naeem) upande wa Jamhuri unadai kuwa mshatakiwa huyo siku hiyo alitoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa timu ya majadiliano ya serikali , kuwa kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha umeme kwa kiwango cha megawati 100 ili apewe tenda hiyo.

Kwa upande wake Hakimu Mkazi Waliarwande Lema aliarisha shauri hilo hadi Mei 23-26 mwaka huu ambapo litakuja kwaajili ya mashahidi wa upande wa Jamhuri kuendelea kutoa ushahidi na akautaka upande wa jamhuri unaowakiliwa na Wakili mwandamizi wa Serikali Fredrick Manyanda na Shadrack Kimaro kuleta mashahidi wao kwa wingi bila kukosa.

Februali 2009 ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Juni, 2006 jijini Dar es Salaam, mshitakiwa (Naeem) alitoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa timu ya majadiliano ya serikali, kuwa Kampuni ya Richmond LLC ya Texas, Marekani, ina uwezo wa kuzalisha umeme kwa kiwango hicho ili apewe tenda hiyo.Aidha, alidai katika shitaka jingine mshtakiwa akifahamu na kwa ulaghai, alitoa hati ya nguvu ya kisheria iliyotolewa Machi 3, mwaka 2006 iliyokuwa ikimuonyesha kuwa ameruhusiwa na Mwenyekiti wa Kampuni, Hemed Gile ambaye ni kaka yake kufanya kazi za kampuni hiyo hapa nchini.

Aliendelea kudai kuwa, shitaka la jingine linalomkabiri mtuhumiwa huyo ni kutoa taarifa za uongo kwa watumishi wa umma na kwamba Julai 20, 2004 eneo la Ubungo Umeme Park, alitoa taarifa ya uongo kwa wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Shirika la Umeme (TANESCO). Kwamba Richmond LLC ya Texas, Marekani, ina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 100 kwa Tanzania ili wajumbe wa bodi hiyo waweze kumpendekeza kupewa tenda ya kutoa huduma hiyo.

Gile amefikishwa mahakamani ikiwa ni takriban mwaka mmoja sasa baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na mwenzake aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha, walilazimika kujiuzulu nyadhifa zao kwa kashfa hiyo ya Kampuni ya Richmond.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Mei 11 mwaka 2011.

KORTI YAMTAKA ZOMBE KUMJIBU AG KWA MAANDISHI

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemwamuru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe kujibu kwa maandishi hoja za Mwanasheria wa Serikali (AG) ifikapo Mei 23 mwaka huu.


Amri hiyo ilitolewa jana na Jaji Upendo Msuya wakati kesi hiyo namba 35/2011 ya madai ya fidia ya sh bilioni tano iliyofunguliwa na Zombe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilipofika kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo Zombe anawakilishwa na wakili wa kujitegemea Nyaronyo Kichere wakati upande wa mdaiwa haukuwa na mwakilishi.

“Kesi hii ilikuja leo kwa ajili ya kutajwa hivyo upande wa mdaiwa ulishawapatia majibu ya hati yenu ya madai, hivyo mahakama inauamuru upande wa mlalamikaji kujibu na kuyaleta majibu yenu Mei 23 na kesi hii itakuja kutajwa tena Juni 20 mwaka huu,” alisema Jaji Upendo.

Hati ya majibu ya mwanasheria mkuu inadai kwamba Zombe hana anachomdai kwa sababu Oktoba 7, 2009 Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliwasilisha rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ya Agosti 17 mwaka 2009 ambayo ilimwachia huru Zombe na wenzake nane waliotuhumiwa kwa mauji na kwamba rufaa hiyo bado haijatolewa maamuzi.

Machi 18 mwaka huu, Zombe alifungua kesi hiyo mahakamani hapo akiomba mdaiwa amlipe sh bilioni tano na riba ya sh milioni 200 kwa sababu polisi ilikiuka sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 wakati wanamkamata.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 17 mwaka 2011.

WATANZANIA TUSITUHUMIANE HOVYO,TUFUATE SHERIA


Na Happiness Katabazi

KIFUNGU cha 7(1)(a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002; kinasema ni wajibu wa kila mwananchi anayefahamu taarifa za kutendeka au kuna mtu anania ya kutenda uhalifu au mauji,analazimika kutoa taarifa hizo kwenye mamlaka husika za dola.


Na endapo mtu huyo atashindwa kutimiza waibu huo anaweza kushtakiwa kwa kosa la kusaidia kutendeka kwa kosa kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code R:E;2002).

Kifungu cha 99(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 ,kina mruhusu hakimu kutoa kibali kwa mwananchi aliyeomba mahakama impatie kibali cha kuendesha kesi binafsi si bali kuhusisha waendesha mashtaka wa serikali.
Na kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Pili iliyochapishwa na Oxford Universty Press, inatoa maana ya neno Fisadi .Ina sema Fisadi maana yake ni “Mtu mbaya ,mtongozaji,mharibifu,mpotevu,mwasherati;-guberi”.

Fukuto la Jamii limelazimika kuanza kwa kunukuu vifungu hivyo vya sheria na Kamusi hiyo ni kwasababu limeona kadri siku zinavyozidi kwenda hapa nchini baadhi ya wanasiasa,vyombo vya habari,viongozi wa dini na wananchi wamekuwa wakirushiana maneno kuwa huyu,yule ni fisadi.

Hivi sasa hapa nchini kumekuwa na upumbavu miongoni mwa pande mbili za baadhi ya wanasiasa wa chama tawala na wale wa vyama vya upinzani,baadhi ya vyombo vya habari, viongozi wa dini ambao wamekuwa wakionyesha dhahiri kuegemea upande mmoja katika pande hizo mbili.

Upumbavu huo ni ule wa miongoni mwao wa kumhukumu mwanasiasa fulani kuwa ni fisadi wakati kumbe naye huyo anayemhukumu kwa maneno mwanasiasa mwenzie kumbe naye ana ananukia halufu ya ufisadi.

Hadi sasa hakuna hata kundi moja hapo juu lililokwenda mahakamani kumfungulia mwanasiasa mmoja anayemtuhumu kufanya ubadhirifu wa rasilimali za taifa au kwenda kituo chochote cha polisi kutoa taarifa za mwanasiasa au ofisa yoyote wa serikali kuomba achunguzwe kwani ana ushahidi mkononi unaonyesha mwanasiasa au ofisa wa serikali ni mbadhilifu(fisadi) wa mali za umma ,chama na amegushi vyeti(fisadi wa elimu) ndiyo maana amekuwa akimtaja kwa jina mwanasiasa huyo majukwaani kuwa ni fisadi na siyo mtuhumiwa wa ufisadi.

Tunachokishuhudia sasa ni kwa baadhi ya wanasiasa au wafanyabiashara kumfungulia kesi mwanasiasa fulani au mfanyabiashara fulani kuwa amemkashfu binafsi mbele ya jamii kwa kumuita yeye ni fisadi.Na mfano wa hili ni zile kesi za madai ya kashfa zilizowahi kufunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na mfanyabiashara Yusuf Manji dhidi ya Reginald Mengi na ile kesi ya madai ya kashfa ya shilingi moja iliyoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyofunguliwa na Yusuf Manji na Reginald Mengi ambapo mahakama hiyo imetoa amri ya kuzuia vyombo vya habari visiripoti kesi hiyo.

Inashangaza sana kuona ni sisi wananchi tumekuwa na ujasiri na wepesi sana wa kuwakamata wale tunaowatuhumu kuwa wametuibia simu,pochi,mikufu, majumbani kwetu na kuwapiga,kuwachoma moto au kuwapeleka vituo vya polisi ili sheria zichukue mkondo wake lakini siku za hivi karibuni nimekuwa nikijiuliza ni kwanini ni sisi wananchi tunaojitapa kuwa tunachukia ufisadi na tuna uchungu wa mali ya umma tumekuwa vinara wa kusimama majukwaani na kwenye vyombo vya habari kuwataja fulani na fulani tena kwa majina kuwa wanafuja rasilimali za nchi lakini tunashindwa kwenda vituo vya polisi vilivyopo karibu yetu kutoa taarifa hizo za wale mliowahukumu kwenye majukwaa kuwa wamekuwa wakifuja rasilimali za taifa ili polisi waweze kuzifanyia kazi?
Mbona tumekuwa taifa la watu wanaopenda kuzungumza sana,majungu,kuchafuana kuliko kuchukua hatua?Kusema fulani ana mali nyingi basi ni fisadi wakati wewe uliyeanzisha tuhuma hizo hadharani unashindwa kuisaidia polisi kuwa mali za mtu huyo ni zake kweli?Mali hizo zipo maeneo gani?Kweli amezipata kwa haramu?

Kwani hapa nchini hatuna kipimo kinachoonyesha mwenye mali kiasi hiki ni tajiri au bilionea na wala hakuna sheria inayomkataza mtu kumiliki mali.

Hakika huo ni udhaifu mwingine wa wajenga hoja wanaowatuhumu wenzao kuwa wana mali nyingi.Mwisho wa siku hata hilo jeshi la polisi au Takukuru zitapata wakati mgumu wa kuanzia uchunguzi wao dhidi ya mtu huyo.

Lakini ikumbukwe kuwa nao hao mnaowataja hadharani kuwa ni mafisadi kuwa wana mbinu sana tena kuliko hata nyie mnaowataja.Na hili ninalolisema hata IGP-Said Mwema, Mkurugenzi Mkuu wa (TAKUKURU),Dk.Edward Hosea walishawahi kukiri kwenye vyombo vya habari kuwa mafisadi ni watu wenye mbinu sana.

Wewe raia mwema ambaye kweli unadai una uchungu sana na rasilimali za taifa hili na mnawachukia mafisadi wa mali za umma mnatamba kuwa mna mnataarifa za uhakika kuwa mwanasiasa,ofisa wa serikali ni mbadhilifu fulani wabadhilifu, sasa ni kwa nini mnashindwa kupeleka taarifa hizo kwenye vyombo vya dola ili muweze kusaidiana na vyombo hivyo ili hizo taarifa za ubadhilifu ziweze kufanyiwa kazi?

Kama tulivyokwisha elezwa na IGP-Mwema, Dk.Hosea kuwa mafisadi wana mbinu sana, hamuoni mnavyowaanika majukwaani ndiyo nao wanaibuka na mbinu nyingine mbadala tena kimya kimya za kuvuruga ushahidi wa hizo tuhuma mnazozielekeza kwao.?

Sasa kwa muktadha huo nyie mliojipa jukumu la kuwasema wenzenu ni mafisadi mtakuwa hamuisaidii serikali badala yake mtakuwa mnazidi kuwapa mbinu hao mnaowahukumu kuwa ni mafisadi kubuni mbinu mpya za kuiba, kubadilisha umiliki wa mali wanazozimiliki, kuhamisha fedha kwenye akaunti zao na kwenda kuzihifadhi kwenye akaunti zenye majina ya watu wengine na mwisho wa siku vyombo vya upelelezi vitajikuta vinashindwa kukusanya ushahidi mathubutu dhidi ya wao na hivyo kujikuta wanashindwa kuwafikisha mahakamani?

Kuna watanzania wengi sana wenye mapenzi ya kweli na taifa lao tena wala hawana mpango wa kujikomba ili wapatiwe madaraka,wala hawabwatuki majukwaani pindi wapatapo taarifa za kutendeka au kuna watu wanataka kutenda uhalifu wamekuwa wakienda kimya kimya kwenye mamlaka husika kutoa taarifa na taarifa hizo zimekuwa zikifanyiwa kazi na mwisho wa siku waliohusika vitendo hivyo wamekuwa wakikamatwa na kufikishwa mahakamani?

Lakini hilo miongoni mwa wanasiasa wetu tena wa pande mbili yaani wa chama tawala na upinzani hilo la kwenda kutoa taarifa katika taasisi husika kuhusu ubadhilifu mkubwa kutendeka limewashinda kabisa matokeo yake hivi sasa wamegeuza hilo la kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola za kuhusu kutendeka kwa uhalifu kuwa ni ngazi ya kupandia kupata umaarufu wa ‘chee’ katika jamii yetu lakini Uchaguzi mkuu unapofika wananchi wale wale waliokuwa wakimshangilia mwanasiasa huyo aliyejipa jukumu la kuwahukumu wenzao kuwa ni mafisadi, wanamnyima kura za ndiyo wanampatia kura za ndiyo yule aliyehukumiwa majukwaani kuwa ni fisadi.

Ikumbukwe kwamba nchi hii ni ya watanzania wote walio wanachama wa vyama vya siasa na siyo wanachama wa vyama vya siasa kwahiyo sote tuna uhuru wa kutoa taarifa za kutendeka au kutaka kutendeka kwa uhalibifu au ubadhirifu wa rasilimali za umma, kulinda rasilimali za nchi yetu kwa kushirikiana na serikali iliyopo madarakani kwa sasa.Sasa inapotokea kikundi cha watu fulani kikaanza kukwepa uhuru huo na majukumu hayo ambayo yameainishwa hata kwenye Katiba na sheria ya makosa ya Jinai ya mwaka 2002,inashangaza sana.

Pia ikumbukwe hata Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)Elizer Feleshi ambaye ndiye mwenye dhamana ya kufungua kesi mahakamani kabla ya kufungua kesi za jinai mahakamani anapaswa kukusanya na kujiridhisha na baadhi ya vielelezo vilivyowasilishwa kwake na pia ajiridhishe kwa kuona baadhi ya maelezo ya mashahidi ambao anatarajia kuwatumia kujenga kesi atakayoifungua mahakamani na siyo ‘blaa blaa’ zitolewazo na baadhi wanasiasa,wananchi na baadhi ya vyombo vya habari.

Na matokeo yake vikundi hivyo vya wanasiasa vikaamua kutumia njia inazozijua kusema serikali iliyopo maradakani imeshindwa kutimiza wajibu hivyo iondoke madarakani na wakati wakitoa madai hayo vikundi hivyo vinakwenda kuomba ruhusa ya kufanya mikutano ya hadhara na kuomba ulinzi kwa jeshi la Polisi ambalo jeshi la polisi linaongozwa na IGP-Mwema ambaye naye ameteuliwa kushika wadhifa huo na Rais Jakaya Kikwete ambaye naye baadhi ya wanasiasa wa upinzani wanamuita ni fisadi ,kwakweli huwanapata shida kuwaelewa wanasiasa wa aina hiyo ambao wanakataa kula nyama ya nguruwe lakini wanakunywa supu yake!

Mbona hatujawasikia hao wanasiasa vinara wa kuwasema wenzao ni mafisadi kwamba walishapeleka kituo chochote cha polisi,Takukuru au mamlaka nyingine za dola taarifa kuhusu watu kadhaa kutenda au kuwa nania ya kutenda uhalifu halafu taarifa hizo hazikufanyiwa kazi na mamlaka hizo?

Na mbona hatujawasikia hao wanasiasa vinara wa kuwahukumu wenzao kuwa ni mafisadi kwamba walishawahi kufika mahakamani na kuomba kibali cha mahakama cha kuendesha kesi binafsi bila kuwashirikisha mawakili wa serikali halafu mahakama ikawafukuza au kuwanyima kibali hicho?

Nadiriki kusema kwa sasa tulipofika hao baadhi ya wanasiasa toka CCM na vyama vya upinzani waliokuwa mstari wa mbele wa kuwataja wanasiasa wenzao kuwa ni mafisadi bila kupeleka taarifa na ushahidi wa tuhuma hizo katika mahakama husika, wanatuharibia nchi taratibu.

Leo hii makala hii itadharauliwa sana na majuha lakini nawataka wananchi tuamke na kuwahoji hao viongozi wetu wa siasa siku wakikosa kile wanachokiita kuibua ufisadi watatueleza nini sisi wapiga kura wao na wananchi kwa ujumla?
Maana ninachokiona hivi sasa na baadhi ya viongozi wa Chadema na CCM,baadhi ya vyombo vya habari kuhusu kuwahukumu wenzao kuwa ni mafisadi, hakitofautiani sana na kile kilichokuwa kikifanywa Mbunge wa Vunjo(TLP),Agustine Mrema wakati akiwa Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi lakini mwisho wa siku alipoishiwa ajenda hizo tuna muona hivi sasa ameachana na mtindo huo na badala yake anafanyakazi zake vyema za kibunge.

Je tuwaulize hao vinara wa sasa siku watakapopata nyadhifa fulani kubwa kule serikalini kama alioupata yule mwanasiasa aliyekuwa na ushawishi mkubwa Zanzibar kwa chama cha (CUF) cha Makamu wa Pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad,ndiyo watapunguza kasi ya maandamano na mikutano ya hadhara na kusimama majukwaani kudai serikali iliyopo madarakani imeshindwa kazi?
Wanasiasa wengi tabia na hulka zao wengi zinaeleweka, kama hawajapata kile wanachokitaka wao binafsi huwa wana hulka ya kubwatabwata majukwaani lakini pindi wanapopata nyadhifa walizokuwa wakizinyemelea,huamua kuvisaliti hata vyama vyao na kuamua kusalimu amri katika kile ambacho awali walikuwa wakikiita ni mapambano dhidi wabadhilifu wa rasilimali za umma na serikali iliyopo madarakani.

Nina uzoefu na hili kwani Uchaguzi wa mwaka 1995 na 2000,2005 na 2010 nili bahatika kuzishuhudia chaguzi hizi.Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 na 2005 ulitawaliwa na vurugu za hhapa na pale.Viongozi wa vyama upinzani wakati huo walikuwa wakiwatanguliza mstari wa mbele vijana kushiriki na kuongoza maandamano ambayo serikali ilikuwa imeyapiga marufuku na mwisho wa siku vijana hao wakajikuta wanaangukia kwenye mikono ya polisi kwa kupigwa na wengine kupoteza maisha yao na wengine kupata ulemavu wa kudumu huku wale viongozi wao waliokuwa wakiwatuma kukwepa vipigo na wengine hivi sasa wamerudi CCM tunawajua, ambao ndiyo walikuwa wakituhadaa sisi wananchi kuwa ni chama kilichochoka na wamepewa madaraka na wapo wengi tu.

Sasa ni rai yangu kwa wanasiasa na sisi wote tunao watuhumu wenzetu kwenye jamii kuwa ni vinara wa ufisadi ,tukasoma kwanza maana ya neno ‘Fisadi’ kisha kila mmoja kwa wakati wake ajiulize kimya kimya kuwa yeye siyo fisadi?

Maana kwa mujibu wa Kamusi hiyo inasema Fisadi ni ‘ Mtu mbaya, mtongozaji, mharibifu, mpotevu, mwasherati;-guberi”.Sasa nyie wanasiasa mnaowasema wenzenu ni mafisadi Je tuwaulize hakuna hata mmoja ambaye ajihusishi na vitendo vya uasherati? Je hakuna hata mmoja wenu ambaye hadi leo hii amewahi kuisaliti ndoa yake kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na vimada nje ya ndoa yake?.Miongoni mwenu nanyi mmekuwa mkituhumiwa kuwa ni vinara wa uasherati. Na uasherati umetajwa kwenye maana nzima ya neno fisadi.Je hamuoni na nyie mnapaswa kuitwa adharani ni mafisadi pia?

Na tukumbuke hao tunaowahukumu mbele za familia zao na jamii kuwa ni mafisadi wakati mwingine hakuna ushahidi wa madai hayo mkae mkijua wanafamilia na wana watoto, wanawasikia na watoto wao wanawatazama,wana chukia,wanakasirika na kuwaweka kwenye kumbukumbu zao na dhambi hiyo itawatafuna .Mwisho wa siku watoto hao watakuja kulipiza visasi tu.Sasa hatutaki kujenga taifa la vijana wenye visasi dhidi ya vijana ambao hapo nyuma baba zao waliwaumiza baba zao kwa kuwadhalilisha mbele ya umma na familia zao.Na huko ndipo taifa la Tanzania lilipo na linapoelekea.Tukomeshe upuuzi huu,haraka sana.

Tunataka kuwa na wanasiasa wa chama tawala,upinzani ambao wanatoa hotuba zinazotoa dira kwa taifa na kufundisha wananchi na siyo kama ilivyo hivi sasa kwa baadhi ya wanasiasa wengi kutoa matamko au hotuba zenye lengo la kuumbuana,kushushiana heshima na kuchafuana badala ya kutoa hotuba za kuwaelekeza wananchi na wanachama wao dira ya taifa na vyama vyao ni ipi.

Hayati Julias Nyerere,viongozi wengine wa kisiasa barani Afrika na wanasiasa makini hapa nchini kabla ya vyama vyao kushika hatamu na wakati ni viongozi wa kuu wa serikali wamekuwa na walikuwa wakitoa hotuba zenye kuonyesha dira na mwelekeo kwa wananchi na wanachama wao na hadi leo ukizitafuta hotuba zao na kuzisoma kuna mambo utajifunza kutokana na hotuba zao, lakini siyo kama ilivyosasa kwa baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani na baadhi ya CCM kutwa wamekuwa wakitoa matamko ambayo hata vizazi vyetu havitafaidika na hotuba hizo zaidi zaidi watakachoambulia ni kujivunza tabia mbaya ya kuzulia maneno na kupakana matope.Mmbadilike.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 17 mwaka 2011

HEKO SPIKA MAKINDA,NDUGAI,DK.KASHILILAH


Na Happiness Katabazi

HIVI karibuni Spika wa Bunge Anne Makinda, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah na Naibu Spika Job Ndugai kwa wakati tofauti waliviambia vyombo vya habari kuwa wabunge wengi kutofahamu kanuni za uendeshaji wa Bunge ndiyo ilikuwa chanzo cha mivutano katika kikao cha 10 cha Bunge.


Wameyasema hayo kutokana na wananchi mbalimbali pamoja na taasisi za kiraia kujitokeza kukosoa mambo yaliyofanyika katika kikao cha Bunge lililopita.
Dk. Kashililah anasema uwepo wa wabunge vijana kumelifanya Bunge hilo kuonekana kama ni la wanafunzi.

Katika Bunge hilo, baadhi ya wabunge walionekana kwenda kinyume na kanuni za Bunge na kuzusha malumbano na kurushiana vijembe bila kuheshimu nyadhifa zao.
Baadhi ya wabunge hao walikwenda mbali na kutaka milango ya ukumbi ifungwe ili waweze kuchapana makonde.

Kwa upande wake Makinda ambaye amefiwa na mama yake mzazi na Fukuto la Jamii linampa pole kwa kuondokewa na mama yake, aliunga mkono hoja ya Kashililah kuwa wabunge wengi hawajui kanuni.

Anasema Bunge limeshatenga muda fulani katika Bunge lijalo kwa ajili ya kuwapatia mafunzo wabunge hao ili waweze kuzifahamu kanuni za Bunge.

Naye Naibu Spika, Job Ndugai, anasema kuna baadhi ya wabunge wanawake wanavaa nguo fupi, zisizoendana na utamaduni wa Bunge hilo.

Naamini hilo likifanyika la kuwapatia mafunzo wabunge matatizo hayo yatakwisha.

Binafsi nilibahatika kuzunguka Mikoa yote nchini na Zanzibar kwaajili ya kampeni.
Awali kulikuwa na lundo la tuhuma kutoka kwa baadhi ya wananchi na wanachama wa chama alichotoka mbunge husika kuwa amepitishwa kwenye kura za maoni na chama chake kwa mbinu chafu.

Leo Fukuto la Jamii linapenda kutoa pongezi kwa Spika Makinda na Katibu wa Bunge Dk. Kashililah kwa ujasiri wao wa kuzungumza kile kilichomo ndani ya akili na mioyo yao kwamba wabunge ambao tumewachagua wakatuwakilishe bungeni na wakatutungie sheria, wengi wao hawataki kujisomea.

Na kwamba viongozi hao wa Bunge wanawaongoza baadhi ya wabunge ambao hawafahamu kanuni ingawa walishapewa. Ni aibu sana.

Nasema hawataki kujisomea, kwa sababu tumeambiwa na Dk. Kashililah kwamba muda mrefu Ofisi ya Bunge ilishawapatia wabunge kanuni za Bunge ili wazisome na wazielewe.

Lakini tulichokishuhudia katika kikao cha 10 ni wazi kabisa baadhi ya wabunge hawana ule utamaduni wa kupenda kujisomea na kuelewa kanuni au taratibu zinazopaswa ziwaongoze wao katika shughuli za kibunge.

Ushahidi wa hilo ni vile vitendo vya ubwatukaji ovyo na kutoa kauli za kuchochoea uvunjifu wa amani bungeni, vitu vilivyokuwa vikitolewa na baadhi yao.
Siku zote viongozi wetu na wasomi wamekuwa wakieleza jamii kuwa elimu haina mwisho na binafsi nakubaliana na msemo huo.

Sasa inapotokea Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye hajui kanuni za kumuongoza yeye akiwa bungeni na jinsi Bunge linavyoongozwa, hivi ataweza kusimama mbele ya wapiga kura wake na kuwataka wasome kwa bidii kwa sababu elimu haina mwisho?
Ndiyo maana Fukuto la Jamii linatoa pongezi kwa Spika Makinda na Dk. Kashililah kwa kutueleza ukweli kwamba wale wabunge wanaowaongoza wengi hawafahamu kanuni.

Ni nadra sana kwa viongozi wa taasisi fulani kuandika udhaifu wa wafanyakazi wao au watu wanaowaongoza lakini viongozi hao wamekuwa wakweli.

Hivi ndivyo viongozi wa taasisi nyingine wanatakiwa wawe pindi wanapobaini watendaji wao wana udhaifu katika eneo fulani na kisha kutafuta njia ya kuweza kuutokomeza udhaifu huo.

Kwa sisi waumini wa fani ya sheria tumekuwa tukijiuliza maswali mara kwa mara, ni kwanini huu utaratibu wa kuwaruhusu wabunge wetu ambao wengi hawajasoma sheria kutunga sheria?

Na ndiyo maana sheria nyingi zilizotungwa na Bunge, huku zikisainiwa na rais zimekuwa zikilalamikiwa kuwa ni sheria mbaya na baadhi ya vipengele vyake vinakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Baadhi ya taasisi za kutetea haki za binadamu na wanaharakati wamekuwa wakilalamikia vipengele hivyo Mahakama Kuu, ambayo imekuwa ikivitengua.

Sasa tutegemee tutungiwe sheria zisizo kandamizi wakati tayari Spika Makinda na Katibu wa Bunge wameishatueleza kwamba wabunge wengi hawajui kanuni ingawa Bunge lilishawapa vitabu vya kanuni ili wajisomee?

Hivi wananchi watamsikiliza kweli mbunge huyo au watapuuza mafundisho yake? Wananchi wamewachagua wabunge wao wakawawakilishe bungeni kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na mambo mengi ya msingi lakini hakuna mpiga kura aliyempigia kura mbunge wake ili aende bungeni kwa ajili ya kwenda kubwatuka na kutaka milango ifungwe ili wapigane makonde.

Mbunge anayeshindwa kusema matatizo na kero za wananchi wake ndani ya Bunge ili serikali isikie kilio hicho na kisha iziweke kero hizo kwenye mpango wa kuzitatua, mbunge wa aina hiyo hafai tena kupewa kura na wananchi.
Bunge ni eneo linaloheshimiwa na wananchi, kwani sheria zote hutungwa na kurekebishwa huko.

Ifike mahala wapiga kura tujiulize, zile kero zote tulizowapatia waliokuwa wagombea ubunge kwenye majimbo yetu na sasa wabunge, wanaziwasilisha sehemu husika zitatuliwe?
Maana hivi sasa ninachokiona kuna fasheni mpya imeanza kutumiwa na baadhi ya wabunge wanaotaka umaarufu wa ‘chapuchapu’, wa kujitapa kuwa Bunge lijalo atawasilisha hoja binafsi au kuuliza swali kuhusu ufisadi wa mfano wa Kampuni ya Meremeta na Kagoda ambapo ukiitazama hiyo hoja haimo hata kwenye vipaumbele vyake.

Na maswali hayo ya kuhusu ufisadi wa kampuni hizo yalishatolewa majibu na serikali bungeni kuwa upelelezi bado unaendelea.

Sasa basi, mbunge huyo anaacha kuwasilisha kero za wananchi wake kwanza anapewa nafasi ya kuchangia na Spika, yeye anauliza swali kuhusu ufisadi huo, wakati mbunge huyo pia alikuwa ana nafasi kabla ya vikao vya Bunge kuanza mjini Dodoma au kumalizika kwenda kuonana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba au kumwandikia barua ya kumuuliza swali hilo na angejibiwa kwa sababu hivi sasa Jeshi la Polisi nchini lina mabadiliko makubwa ya kiutendaji, linaendeshwa kisomi na urasimu uliokuwapo unaendelea kutokomezwa.

Ni haki yao wabunge kuuliza maswali ya aina hiyo kuhusu kile wanachodai kuwa ni ufisadi mkubwa, lakini tunawaomba wakumbuke yale waliyoyaahidi wakati wa kampeni kwamba watahakikisha wanafikisha matatizo ya wapiga kura wao kama uhaba wa maji, kukosekana dawa hospitalini, matatizo ya walimu, huduma mbovu kwa wajawazito, ujenzi wa barabara na madaraja na maji.

Maana matatizo hayo ndiyo yamekuwa yakiwakabili wapiga kura lakini hivi sasa tunachokishuhudia baadhi ya wabunge utawasikia wakiuliza maswali ya nyongeza yasiyo na tija katika majimbo yao au kuwasilisha hoja binafsi ambazo binafsi nadiriki kusema hazina faida kabisa kwa wapiga kura wao ambao kura zao ndizo zilimfanya mbunge anayeuliza maswali ya aina hiyo kuingia bungeni.

Si dhamira yangu kutaka kuwafunga midomo wabunge wetu, la hasha! Napendekeza sasa hayo maswali kuhusu ufisadi katika kampuni fulani fulani wabunge mliochaguliwa na wananchi muwaachie wabunge walioteuliwa na rais au wabunge wa viti maalumu ambao hawana majimbo, wakijisikia waulize maswali ya aina hiyo na nyie wabunge mliochaguliwa na wananchi muwe mnauliza maswali yanayohusu majimbo yenu ili serikali iweze kusikia kwa mapana kero za wananchi na kuzitatua.

Binafsi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 na ule wa mwaka 2010 nilibahatika kuzunguka majimbo yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, nilijifunza mengi na kujionea mengi lakini kikubwa nilichojifunza ni kwamba wabunge ambao mara kwa mara wamekuwa vinara ndani ya Bunge kuuliza maswali ambayo wakati mwingine hayahusu majimbo yao au kuwasilisha hoja ambazo hazina masilahi kwa taifa, majimbo yao yapo nyuma sana kimaendeleo.

Na wale wabunge wenye hulka ya kukaa kimya bungeni majimbo yao yamepiga hatua za kimaendeleo.

Mfano mmoja wapo wa wabunge ambao hawana hulka ya kuzungumza bungeni ni Mbunge wa jimbo la Igunga (CCM), Rostam Aziz, lakini ukilizunguka jimbo lake utakubaliana nami kwamba licha ya kukaa kimya bungeni, lakini jimbo lake limeendelea sana kwa mawasiliano ya simu, nguzo za umeme ambazo zimetanda katika vijiji vingi; pamoja na kujengwa shule nyingi za msingi na sekondari, ukilinganisha na baadhi ya majimbo yanayoongozwa na wale wabunge wazungumzaji wazuri bungeni.

Ikumbukwe kuwa wapiga kura walivyowapigia kura wabunge wao walikuwa wana imani wabunge hao ndio watakwenda bungeni na sehemu nyingine kuwasemea matatizo yao.

Sasa inapotokea wabunge mnasahau mlichotumwa na wananchi wenu, matokeo yake mkajiingiza kwenye ile fasheni mpya ya kuomba Bunge liwaruhusu kuwasilisha hoja binafsi kuhusu ufisadi fulani ambao si kero ya wananchi, kwakweli inatia kichefuchefu na kutukera.

Msifikiri hatuwaoni mnayoyatenda huko bungeni, tunayajua na tunayaweka kwenye fikra zetu.
Hakika Uchaguzi Mkuu ujao sisi wananchi tutawahoji, ni kwanini mmeshindwa kutusemea kero zetu bungeni na kwenye mabaraza ya madiwani.

Tunataka wabunge wa vitendo na wanaotanguliza masilahi ya wapiga kura wao mbele kuliko fasheni mpya ya kuomba kuwasilisha hoja binafsi kuhusu ufisadi.

Utakuta mbunge anauliza swali kuhusu uchunguzi wa ufisadi katika kampuni fulani kwamba umefikia wapi wakati mbunge huyo huyo katika kampeni zake za Uchaguzi Mkuu alitumia ufisadi wa kugawa rushwa na mbinu nyingine chafu hadi akashinda ubunge.

Na wabunge waliotumia mbinu chafu, dhalimu na dhuluma hadi wakafanikiwa kuupata ubunge tunawafahamu na tunasikia kichefuchefu kuwaona wakiwa ndani ya Bunge na kujigeuza vinara wa kuuliza maswali kuhusu ufisadi wakati naye anajua na wapiga debe wake wanajua vema walitumia mbinu chafu kuhakikisha mbunge wao anapata ubunge. Ina kera sana.

Nimalizie kwa kumtaka Spika Makinda atambue kuwa yeye ndiye mwanamke pekee tangu nchi hii ilipopata uhuru Desemba 9, 1961 kuteuliwa kuwa Naibu Spika na sasa Spika wa Bunge.
Kwa hiyo atambue wadhifa wake huo ni kielelezo kuwa wanawake wanaweza wakipewa nafasi.
Hivyo endapo atashindwa kuthibitishia umma na Afrika kuwa yeye ni Spika mwanamke na anaweza, ajue hiyo haitakuwa aibu yake bali itakuwa ni aibu kwa wanawake wote.

Spika Makinda anapaswa awe Spika anayesimamia sheria na kanuni za Bunge bila kutetereka, aachane na tabia ya kuwaona wabunge wakishindwa kusimamia kanuni na kutoa maneno yanayohatarisha amani ndani ya Bunge akaishia kusema: “Wabunge vitendo mnavyovifanya mjue mnajidhalilisha,” hii kauli hatutaki tena kuisikia.

Wabunge ni watu wa kupita, hivyo wanapotokea baadhi ya wabunge wanatoa maneno yasiyotakiwa bungeni, wanapaswa kuchukuliwa hatua ili liwe fundisho kwa wengine.

Wito kwa Spika Makinda ni kwamba tunaomba ulifanyie kazi tamko la Naibu Spika Ndugai, linalosema kuna baadhi ya wabunge wanawake wanavaa nguo fupi.
Madai hayo ni mazito, kwani inaonyesha wabunge wa kike wameshindwa kudhibitiwa kuhusiana na suala la kuvaa nguo fupi.

Hivyo baadhi ya wabunge wa kike wanaovaa nguo fupi ndani ya Bunge letu tukufu, Fukuto la Jamii linasema kama kazi ya ubunge imewashinda ni vema mjivue ubunge, kwani kamwe hatuwezi kukubali kuona Bunge letu heshima yake inaporomoshwa na baadhi ya wabunge wachache kwa mavazi yao.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne,Mei 10 mwaka 2011.