MAHAKAMA:MARANDA,FARIJALA WANAKESI YA KUJIBU

Na Happiness Katabazi
KWA mara nyingine tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemuomwona Kada wa CCM, Rajabu Maranda na mpwa wake Farijala Hussein kuwa wanakesi ya kujibu katika kesi ya pili inayowakili ya wizi wa Sh bilioni 2.2 katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania.


Uamuzi huo ulitolewa jana na jopo la Mahakimu wakazi watatu wanaoongozwa na jaji Fatma Masengi anayesaidiwa na mahakimu wakazi Projestus Kahyoza na Katarina Revocate ambao walisema kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya jopo hilo kutoa uamuzi wake utakaowaona washtakiwa hao wanakesi ya kujibu au la.

Hakimu Mkazi Recovate ndiye aliyesoma uamuzi huo kwaniaba ya jopo hilo ambapo alisema jopo hilo baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa jamhuri na vielelezo, majuisho ya upande wa utetezi na majumuisho ya kesi hiyo yaliyowasilishwa na wakili wa serikali Arafa Msafiri, jopo hilo kwa kauli moja limefikia uamuzi wa kuwaona washtakiwa wote wanakesi ya kujibu.

Revocate ambaye alisoma uamuzi huo kwa kifupi kwa kutumia takribani dakika tano, na bila kuweka wazi vigezo vilivyotumiwa na jopo hilo kufikia uamuzi huo, alisema jopo hilo limetosheka na kuridhika na hoja zilizotolewa na upande wa jamhuri kwani ndiyo zimeweza kuilishawishi jopo hilo lifikie uamuzi wa kuwaona washtakiwa wote wanakesi ya kujibu.

“Jopo hili kwa kauli moja linasema limeridhishwa na ushahidi wa upande wa jamhuri kwani ushahidi huo umefanya mahakama hii uweze kukukubali kuwa jamhuri imeweza kuthibitisha kesi yao hivyo mahakama hii imewaona washtakiwa wote wanakesi kesi ya kujibu hivyo hawana budi kupanda kizimbani kuanza kujitetea”alisema Hakimu Revocate.

Kwa upande wake wakili wa washtakiwa hao, Majura Magafu alieleza mahakama wanakubaliana na uamuzi huo wa mahakama na kwamba wateja wake watajitetea kwa njia ya kiapo na kwamba wanakusudia kuleta jumla ya mashahidi sita.Mashahidi sita hao miongoni mwao ni washtakiwa wenyewe.

Aidha Hakimu Revocate alisema washtakiwa hao wataanza kujitetea katika kesi hiyo mfululizo kuanzia Novemba 7,8,9 na 10 mwaka huu na kuamuru washtakiwa hao warejeshwe gerezani kwasababu wanaendelea kutimikia adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela, baada ya Mei 23 mwaka huu, mahakama hiyo kuwatia hatiani katika kesi ya kujipatia ingizo la sh bilioni 1.6 isivyohalali kutoka katika akaunti ya EPA.

Novemba 4 mwaka 2008, Jamhuri ilidai mahakamani hapo kuwa Maranda na Farijala wanadaiwa kuiibia BoT , Sh 2,266,049,041.25 baada ya kudanganya kuwa kampuni yao ya Money Planners & Consultant imepewa idhini ya kudai deni BoT na kampuni ya B. Grancel ya nchini Ujerumani huku wakijua si kweli. Kwa sasa jumla ya kesi tatu zinawakabili washtakiwa hao ndiyo bado hazijatolewa hukumu wakati kesi moja tu ndiyo ilikwishatolewa hukumu.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Julai 26 mwaka 2010.

JUBILEE YA MIAKA 50 YA KITIVO CHA SHERIA UDSM


*WALIMU,WANAFUNZI KUKUTANISHWA

Nappiness Katabazi
KITIVO cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,ambacho hivi sasa kinaongozwa na mwandishi wa habari na mwanasheria mbobevu , Profesa Paramaganda John Kabudi ni kitivo maarufu ndani na nje ya nchi yetu.

Umaarufu wake unatokana na umahiri wake wa kuwapika wasomi wengi wa upika wasomi wengi wa sheria ambao hivi sasa wameshika nyadhifa za juu serikalini, sekta binafsi na taasisi za kimataifa karibu kote duniani.

Lakini umaarufu mwingine wa kitivo hicho ni kwamba Kitivo hicho ndiyo kitivo cha kwanza kuanzishwa Oktoba 25 mwaka 1961 na ilipofika mwaka 1970 kitivo hicho ndicho kilichopelekea kuanzishwa rasmi kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika makala hii, Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kabudi anaanza kwa kusema kuanzishwa kwa kitivo hicho ni alama moja ya wapo ya uhuru wa Tanganyika. Kwani kitivo kilianzishwa kwanza halafu Desemba 9 mwaka 1961 Tanganyika ikapata uhuru wake.

“Ndiyo maana nasema kuanzishwa kwa kitivi hiki ni ala moja wapo ya uhuru wa Tanganyika “alisema Profesa Kabudi ambaye ni mbobevu katika sheria za mazingira na mwandishi wa Habari Kitaaluma.

Pofesa Kabudi anasema Oktoba 25 mwaka 1961 , Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Nyerere alisema maneno yafuatayo alipokubali kuanzishwa kwa kitivo hicho cha Sheria;

“…my Government is so pleased that the law faculty is open even before Independence Day. Dar es Salaam..is the only place where East Africans can get training in law. Its is not by accident that we started with a law college. An essential part of our national philosophy must be a legal profession of great integrity which not only knows the formalities of law but also understands the basic philosophy which underlies our society”

Kwa tafsiri yangu isayo rasmi kuhusu nukuu hiyo , mwalimu Nyerere alisema uamuzi wake wa kuruhusu kuanzishwa kwa kitivo hicho haukuwa ajali , ulikuwa ni uamuzi sahihi kwani Dar es Salaam, ndiyo ilikuwa ni eneo pekee la kwa wananchi wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki kupata mafunzo ya sheria .Na kwamba taifa lilikuwa likiitaji kuwa na wasomi wa sheria ambao wanasimamia maadili na miiko ya sheria.

Akielezea historia ya kitivo hicho na maandalizi ya kuazimisha Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 , anasema Kitivo hicho ni Kitivo cha kwanza kuanzishwa hapa Tanzania na nchini za Jumuiya ya Afrika Mashariki na ndicho kitivo kilichosababisha kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Profesa Kabudi anasema kwanza kabisa anaanza kwa kuwataka waadhili wastaafu, wahitimu wa fani ya sheria waliowahi kuhitimu kozi ya cheti na shahada mbalimbali za fani ya sheria katika kitivo hicho, wananchi na viongozi mbalimbali kushiriki kwenye maazimisho hayo yatakayofanyika chuo hapo.

Profesa Kabudi anasema Kitivo cha Sheria ndiyo kilikuwa kitivo cha kwanza kanzishwa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika ya Kati pia ndiyo kitivo cha kwanza kuanzishwa UDSM Oktoba 25 mwaka 1961 ambacho kuanzishwa kwa kitivo hicho ambacho kuanzishwa kwa kitivo hicho ndiyo kikaja kusababisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuzaliwa mwaka 1970.

Profesa Kabudi ambaye ni Mwenyekiti Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo ya nusu karne anasema wiki ya maazimisho hayo yataanza rasmi Oktoba 17-25 mwaka huu na kwamba maazimisho hayo wameyapatia jina la ( Golden Jubilee Celebrations of The Faculty of Law October 25,1961-October 25,2011).

Anasema Kamati ya maandalizi ya maazimisho hayo inaongozwa na yeye mwenyewe, Profesa Gamalie Mgongo Fimbo, Profesa Leonard Shaidi, Profesa B.Rutinwa, Profesa F.Luoga, Dk Khoti Kamanga, Asina Omari, Ebenezer Mshana ,Consolata Lyimo, Reginald Mhango, Joaqine de Mello.

Aidha anasema siku hiyo ya kilele cha Jubilee ya dhahabu ya miaka 50,yatafanyika mahafali ya wanafunzi wa sheria wa kitivo tu katika ngazi ya cheti, shahada ya kwanza, ya pili na shahada ya uzamivu(PhD) ukilinganisha na mahafali ya miaka iliyopita.

Ambapo katika wiki hiyo ya maadhimisho kutafanyika kongamano mdahalo, kujadili mada ya Ukatiba na ujenzi wa Katiba mpya ya Tanzania, kusikiliza hotuba za wanafunzi 12 wa kwanza waliohitimu sheria katika kitivo hicho, pia hotuba zitakazotolewa waadhili wa kwanza wa kitivo hicho, pia wasomi wa sheria mbalimbali ambao wamewai kusomea fani hiyo katika chuo kikuu cha UDSM.

“Kitivo cha Sheria kimepata kutoa wasomi mbalimbali wa fani hiyo ambao leo hii wanafanyakazi katika ngazi mbalimbali duniani na Oktoba 25 mwaka huu, kitivo cha Sheria ndiyo kinatimiza miaka 50 tangu kilipoanzishwa na tunawataka umma utambue uanzishwaji wa kitivo hicho ni harama ya kwanza ya uhuru wa nchi yetu ambapo Desemba 9 mwaka huu, taifa linaazimisha miaka 50 ya uhuru hivyo utaona kitivo kilianza halafu miezi mitatu baadaye taifa likapata uhuru”alisema Profesa Kabudi.

Baadhi ya wanafunzi waliowai kusoma sheria katika kitivo hicho ni hivi leo wameshika nyadhifa za juu za kitaifa na kimataifa, Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, Jaji Mkuu Othaman Chande, majaji wakuu wastaafu Agustino Ramadhani,Barnabas Samatta, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa, Dk.Edward Hosea na Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP), Elizer Feleshi.

Naibu Waziri Mkuu wa kwanza na Waziri wa wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa serikali ya Uganda, Eriya T.Kategaya, Jaji Mkuu wa Kenya Evan Johnston Gicheru,Jaji Mkuu wa Uganda, Benjamin J.Odoki,Jaji Mkuu wa Zanzibar, H.M.Hamid,marehemu jaji Mkuu wa Kenya
ZZ.S. Chesoni .

Majaji wanawake wa mahakama ya rufaa ya Tanzania, ambao walihitimu fani ya sheria katika kiito hicho ni, Jaji Eusebio Mnuo, Engela Kileo,Nataria Kimaro, Sauda Mjasiri na Katherine Oriyo.
Wanasheria wakuu waliowakusoma fani ya sheria katika kitivo hicho ni Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Amos Wako, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Jaji Frederick Werema, Mwanasheria Mkuu wa zamani wan chi ya Gambia, H.B. Jallow, wanasheria wakuu wastaafu wa hapa nchini, Andrew Chenge na Johnson Mwanyika na mwanasheria mkuu wazamani wa Zanzibara Iddi Pandu Hassan.
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Samwel Sitta na Spika wa zamani wa Bunge la Uganda, marehemu J.F.W. Wapakabulo.
Watumishi katika taasisi za kimataifa ambao walipikwa na kitivo cha Sheria ni Dk. Asha-Rose Migiro ambaye kwasasa ni Naibu Katibu Mkuu wa (UN), Lee C.Muthoga, S.h.Sekule ambao ni Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya Rwanda na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama hiyo ya mauji ya Rwanda S.H.Sekule na Balozi James Kateka ambaye kwasasa ni Jaji wa Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya bahari.
Waziri wa Elimu ya Juu wa Malawi Peter Mutharika, Waziri wa Wizara ya Ulinzi A.Mbabazi na Waziri Sheria ya Katika wa Kenya Mutula Kilonzo.
Wanafunzi waliowai kusoma kitivo na mwisho wa siku wakawa wakuu wa majeshi yetu hapa nchini ni Meja Jenerali mstaafu, L.G.O. Mang’enya ambaye pia alikuwa jaji wakili wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi(JWTZ), Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema na mkuu wa jeshi la polisi mstaafu, Haruni Mahundi na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mstaafu O.E. Malisa.
Wahitimu wengine ambao wamewahi kuwa makatibu wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Amanya Mushenga na Juma Mwapachu.
Wahitimu wengine ambao wamekuwa na nyadhifa za wenyeviti, maofisa watendaji wakuu katika makambuni na mashirika mbalimbali ni Mwenyekiti wa Benki ya Barclays(Kenya), Francis Okoma-Okello, Deo Mwanyika ambaye ni Makamu wa Rais wa Barrick Gold Afrika, aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam,Dk.Hamis Kibola na afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Breweries Ltd na Shirika la Maendeleo Tanzania(NDC), Anold Kilewo.

Mbali na majina wahitumu hao, Profesa Kabudi anasema tangu kitivo hicho kianzishwe, wasomi mbalimbali wa sheria waliwai kuchaguliwa kuwa wakuu wa kitivo hicho.

Mkuu wa kwanza kitivo hicho ni Profesa Arther Brain Weston,wapili ni Profesa y.Ghai , watatu D.Bishota,wa nne ni P.L.U. Cross,wa tano ni Profesa J.L Kanywanyi, wa sita ni Profesa Gamaliel Mgongo Fimbo, wa saba ni Profesa Costa Ricky Mahalu, wa nane, Profesa Zebron Stephen Gondwe, wa tisa ni Dk.Wilbert Kapinga,wa kumi ni Dk.Sengondo Mvungi, wa 11 ni Profesa Jaji Ibrahim Hamis Juma, wa 12 ni Profesa Sifuni Mchome na Profesa Kabudi ambaye ndiyo Mkuu wa kitivo hicho kikongwe kwa sasa.

Profesa Kabudi ambaye amewahi kuwa Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Gazeti la Uhuru na Mzalendo, anasema maandalizi ya maamizisho hayo ambayo yatausisha wasomi mbalimbali wa sheria toka pande zote za dunia yamekamilika.

Na kwamba anawaomba wasomi wa fani hiyo na umma kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika wiki hiyo kuudhulia maazimisho hayo kwani watajifunza mengi hasa ukizingatia kitivo hicho ndiyo kitivo cha kwanza kaunzishwa na kitivo hicho ndiyo kilichopelekea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzishwa.

0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Julai 21 mwaka 2011.

UAMUZI KESI YA MARANDA WAKWAMA

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ilishindwa kutekeleza ahadi yake ya kuutoa uamuzi katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 2.2 katika akaunti ya madeni ya Nje katika Benki Kuu, inayomkabili Kada wa CCM, Rajab Maranda na mpwa wake Farijala Hussein wa ama washtakiwa hao wanakesi ya kujibu au la.


Julai 4 mwaka huu, Jaji Fatma Masangi aliyekuwa akisaidiwa na Hakimu Mkazi Projestus Kahyoza na Catherine Revocati walijigamba mahakama hapo kuwa jana ndiyo wangekotoa uamuzi wa ama washtakiwa wanakesi ya kujibu au laa ikiwa ni saa chache siku hiyo wakili wa serikali Arafa Msafiri kumaliza kuwasilisha majuisho yake ambayo yaliomba mahakama hiyo iwaone washtakiwa wote ambao wanatumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa ya kuibia BoT, sh bilioni 1.6.

Kesi hiyo jana ilikuja mbele ya Hakimu Mkazi Ritha Tarimo ambapo alisema kuwa amepata maelekezo toka kwa jopo hilo kuwa hawataweza kutoa uamuzi huo jana na akaiarisha kesi hiyo hadi Julai 25 mwaka huu, ambapo siku hiyo ndipo jopo hilo litatoa uamuzi wa ama washtakiwa wanakesi ya kujibu au.

Katika kesi hii ya wizi wa sh bilioni 2.2, washtakiwa hao wanaotetewa na wakili Majura Magafu wanakabiliwa na makosa ya wizi, kughushi nyaraka na kisha kujipatia kiasi hicho cha fedha kutoka katika akaunti ya EPA.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Julai 19 mwaka 2011.

JAJI MKUU AONGOZA KUSIKILIZA RUFAA YA MOKIWA

Na Happiness Katabazi
KANISA la Anglikana Tanzania, limeiomba Mahakama ya Rufaa Tanzania kutengua amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliyoamuru Askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk.Valentino Mokiwa akamatwe na ashtakiwa kwa sababu ametenda kosa la jinai la kudharau amri ya mahakama.


Katika kesi ya madai ya msingi iliyofunguliwa na waumini wa kanisa hilo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ni Lothi Oilevo ,Godfrey Mhone na Frank Jackob ambao wanatetewa na Meinrad D’ Souzer.

Ambapo wadaiwa kwenye kesi hiyo ya msingi ambayo inayosikilizwa na Jaji Kakusulo Sambo ni Bodi ya Wadhamini ya kanisa hilo(So 4757) na Stanley Hotay ambaye ni askofu mteule ambao wanatetewa na wakili Joseph Thadayo na Albert Msando.

Ambapo katika madai hayo ya msingi waliwasilisha kwa Jaji Sambo ambapo waliomba mahakama yake itoe amri ya kuzuia uchaguzi wa askofu wa dayosisi Mount Kilimanjaro usifanyike na askofu mteule wa dayosisi hiyo asiapishwe ambapo mahakama kuu baadaye ilitoa amri ya Mhashamu Dk.Mokiwa akamatwe na ashtakiwa na adhibiwe kwa sababu amedharau amri ya mahakama kwani amemwapisha mdaiwa wa pili (Hotay) wakati mahakama hiyo bado haijatoa maamuzi yake.

Ombi hilo la kanisa la Anglikana la kutaka amri hiyo itenguliwe liliwasilishwa jana wakili wa kanisa hiyo Joseph Thadayo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Chande Othman aliyekuwa akisaidiwa na majaji wa mahakama ya rufaa William Mandia na Steven Bwana.

Kusikilizwa kwa ombi hilo jana na Jopo hilo la majaji liloongozwa na Jaji Mkuu Othman, kulitokana hatua ya Mahakama ya Rufaa yenyewe kwa mamlaka iliyonayo (sue moto) kuliitisha jalada la kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuletwa katika Mahakama ya Rufaa ili mahakama hiyo ya juu nchini iweze kusikiliza pande mbili katika kesi hiyo, kutazama amri zilizotolewa na Jaji Sambo na kisha itatoa maamuzi yake.

Wakili Thadayo aliiomba mahakama hiyo itengue amri hiyo kwasababu hadi sasa hakuna amri ya mahakama iliyopuuzwa na wateja wake kwani hadi sasa Dayosisi hiyo bado haijapata askofu ila kilichofanyika ni mdaiwa wa pili (Hotay) kwa mujibu wa taratibu za kiimani za Kanisa la Anglikana walimweka wakfu na baada ya kuwekwa wakfu aliwekwa kwenye kiti na kisha kuzungukwa na maaskofu wa kanisa hilo.

Thadayo alieleza kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Kanisa hilo, askofu anaapishwa na Msajili wa Kanisa hilo ,Profesa Paramaganda Kabudi, na kwwamba Hotay akakuapishwa kuwa askofu na ndiyo maana hakuna mahali kokote mahakama na hao walalamikaji wanaweza kupata ushahidi kuwa mdaiwa huyo wa pili ameapishwa kuwa askofu wa dayosisi hiyo wakati tayari kulikuwa na kesi mahakamani ya kupinga kuapishwa.

“Watukufu majaji wa mahakama ya rufaa ,shauri hili limejikita kwenye imani za ya dini na kila kanisa linataraibu na kanuni zake jamani….Hotay ajaapishwa kuwa askofu kilichofanyika ni Hotay aliwekwa katika inada ya wakfu…sasa tumesikitishwa sana amri ya jaji Sambo inayotaka Mokiwa akamatwe kwa kudharau amri ya kwa kitendo cha kumuapisha Hotay kuwa askofu wa dayosisi hiyo wakati ukweli ni kwamba Hotay hajaapishwa kuwa askofu wa dayosisi hiyo kilichofanyika ni Kanisa lilimuandaliwa misa kumsimika Wakfu.

“Pia tumesikitishwa na amri hiyo ambayo sisi tunaiita ni batili kwani hata huyo Mokiwa siyo mdaiwa katika hii kesi…na kupitia amri ile ni wazi Jaji Sambo alishamhukumu Mokiwa kuwa ametenda kosa la kuidharau mahakama na kwamba anastahili kupatiwa adhabu ambapo kisheria mtu anayepatikana na kosa hilo atapaswa kwenda jela miezi sita ….sasa wakati jaji huyo anatoa amri hiyo alimnyima fursa ya askofu Mokiwa kujielezea”alidai Wakili Thadayo.

Kwa upande wake wakili wa walalamikaji Meinrad D’ Souzer aliliomba jopo hilo la majaji watatu kutupilia mbali pingamizi hilo la wakili wa wadaiwa kwa maelezo kuwa amri ya kukamatwa kwa askofu Mokiwa ni sahihi kisheria na kwamba tangu amri ile ilipotolewa, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alipaswa kumfungulia mashtaka Mokiwa.

Aidha Jaji Mkuu Othman alisema jopo lake limesikiliza hoja za pande zote za kesi hiyo ya madai Na. 1/2011 na kwamba tarehe ya uamuzi huo kutolewa, pande zote mbili zitaarifiwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaani.

Juni mwaka huu, Jaji Sambo alitoa amri hiyo ya kiongozi huyo mkuu wa kanisa la Anglikana kukamatwa kwasababu jaji huyo alikuwa amesikiliza hoja za pande zote mbili ambapo kabla hajatoa uamuzi wa maombi ya kuzuia au kutozuia kufanyika kwa uchaguzi na ibada kumsimika uaskofu, kanisa hilo likadaiwa kabana ibada ya kumsimika uaskofu wa dayosisi hiyo mdaiwa wa pili kitendo kilichotafsiriwa na mahakama hiyo kuwa ni kuidharau mahakama hiyo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Julai 16 mwaka 2011.

31 WAACHIWA 'KESI YA SAMAKI WA MAGUFULI"

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imewaachilia huru raia wa kigeni 31 kati ya 36 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uvuvi haramu bila leseni maarufu kama “kesi ya samaki wa Magufuli”katika ukanda wa Tanzania, baada ya kuwaona hanawana kesi ya kujibu.


Sambamba na hilo,mahakama hiyo imemwamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na taasisi nyingine za serikali kuandaa haraka iwezekanavyo utaratibu wa usafiri ambao ni salama wa kuwarejesha katika nchi zao raia 31 wa kigeni iliyowaachilia huru ili waweze kwenda kuungana na familia zao.

Wakili wa Serikali waandamizi Biswalo Mganga na Prosper Mwangamila waliikumbusha kuwa kesi hiyo ilikuja kwaajili ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wa ama washtakiwa hao ambao wanatetewa na wakili wa kujitegemea Ibrahim Bendera na John Mapinduzi ama wana kesi ya kujibu au la.

Jaji Agustino Mwarija ambaye alisoma uamuzi huo kwa saa mbili, alisema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 13 wa upande wa ujamhuri, vielelezo kadhaa,hoja za mawakili wa pande zote mbili, mahakama hiyo imefikia uamuzi wa kuwaona washtakiwa watano yaani mshtakiwa 1,7,9,33 na 34 kati ya 36 ndiyo wana kesi ya kujibu na washtakiwa 31 hawana kesi ya kujibu.

Jaji Mwarija aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Nahodha wa meli hiyo ya Tawariq 1 ambayo ilikuwa ikivua bila leseni na kuaribu mazingira ya ukanda wa Tanzania, Hsu Chin Tai,mawakala wawili wa meli hiyo ya Tawariq 1, Zhao Hanguing,Hsu Shang Pao na mainjinia wawili Ca’ Dong Li na Chen Rui Hai.

Jaji huyo alisema anakubaliana na hoja moja ya mawakili wa utetezi kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja uliotolewa na upande wa Jamhuri kwamba washtakiwa wote walikuwa wakivua samaki katika ukanda huyo, ambapo alisema anakubaliana na hoja huyo kwamba upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kuwa washtakiwa wote walikuwa wakifanya shughuli za uvuvi kwani baadhi ya washtakiwa wengi walikuwa ni wapishi, wafagizi hivyo makosa ya uvuvi haramu wanayodaiwa kutenda, hayawahusu.

“Kwa kuwa upande wa Jamhuri umelete kielelezo cha leseni inayoonyesha kutumiwa na meli ya Tawariq 2 ambayo shahidi mmoja aliambia mahakama kuwa leseni hiyo ilikutwa kwa mshtakiwa wa kwanza ambaye alimweleza mpelelezi wa kesi hii kuwa meli ya Tawariq 1 ilikuwa ikitumia kibali cha Tawariq 2…hivyo mahakama hii inaona anayepaswa kuzungumzia suala hilo la leseni ni nahodha wa meli, mawakala wa meli na mainjinia siyo wapishi, wahudumu wa meli hiyo.

“Hata hivyo nakubaliana na upande wa jamhuri kuwa ushahidi waliouleta umeweza kuwagusa washtakiwa hao watano …na ndiyo maana mahakama hii imefikia uamuzi wa kuwaona washtakiwa hao yaani mainjinia, mawakala wa meli na nahodha kuwa wana kesi ya kesi ya kujibu na inawaachiria huru washtakiwa wengine ambao ni wapishi, wahudumu wa meli hiyo kwani ni wazi kabisa mpishi, mhudumu wa meli hawezi kufahamu masuala ya leseni na kibali cha meli husika…mwenye jukumu la kujua hilo ni nahodha …hivyo kuanzia sasa washtakiwa 31 nawaachiria huru baada ya kuwaona hana kesi ya kujibu”alisema Jaji Mwarija na kusababisha raia hao wa kigeni kulipuka kwa furaha na wengine kuangua vilio.

Jaji Mwarija alisema kutokana uamuzi wake wa kuona washtakiwa hao watano wana kesi ya kujibu, watapaswa wapande kizimbani kujitetea na akasema wataanza kujitetea katika kikao kingine cha Mahakama ambapo uongozi wa mahakama utapanga tarehe rasmi ya kesi hiyo kuendelea na mahakama itazijulisha pande zote kwa njia ya maandishi tarehe hiyo ambayo itakuwa imepangwa.

Aidha Jaji Mwarija alikubaliana na ombi la wakili wa utetezi John Mapinduzi lilioiomba mahakama hiyo itoe amri kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ya kuandaa usafiri wa kuwasafirisha raia 31 wa kigeni chini na jaji huyo alitoa amri hiyo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashilikiane na idara nyingine za seriakali kuwarudishi hati za kusafiria raia hao walioachiwa huru na kisha waandalie utaratibu wa usafiri salama ambao utawafikisha katika nchi zao.

Mabalozi , maofisa ubalozi wa balozi mbalimbali walifika mahakamani hapo kwaajili ya kusikiliza uamuzi huo ambao muda mfupi baada ya jaji Mwarija kumaliza kusoma uamuzi huo walionekana kupeana mikono ya pongezi na kufurahi na raia hao na sekunde chache baadaye Tanzania Daima liliwashuhudia makachero toka Kituo cha Kikuu cha Polisi Kati, wakiingia moja kwa moja ndani ya ukumbi namba moja ambapo kesi hiyo ilikuwa ikiendeshwa na kuwachukua raia hao 31 waliochiwa huru na kisha kuondoka nao na washtakiwa watano ambao walikutwa na kesi ya kujibu waliendelea kubakia mikononi mwa maofisa wa Jeshi la Magereza.

Itakumbuka kuwa Februali 25 mwaka huu, jaji wa awali aliyekuwa akisiliza kesi Razia Sheikhe alitoa uamuzi wa kuwanyima dhamana washtakiwa hao na kusema makosa yanayowakabili washtakiwa yanadhamana ila kutokana na mazingira ya kesi hiyo mahakama hiyo imetumia mamlaka yake kuwanyima dhamana.

Uamuzi ambao ulipingwa vikali na mawakili wa wastakiwa Bendera na Mapinduzi ambapo walimwomba jaji huyo ajitoe kusikiliza kesi hiyo kwasababu hawana imani naye hali iliyosababisha Machi 3 mwaka huu, Jaji Sheikh kutangaza uamuzi wa kujitoa katika kesi hiyo hali iliyosababisha uongozi wa mahakama hiyo siku chache kumpanga jaji mpya ambaye ni Mwarija kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Machi 8 mwaka 2009 washtakiwa hao walikamatwa na askari wa doria wakiwa kwenye meli ya Tawariq 1 na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kisha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uvuvi katika kina kirefu katika Ukanda wa bahari ya Tanzania,kufanya shughuli za uvuvi bila leseni na kuaribu mazingira ya ukanda huo.Tangu wakamatwe washtakiwa hao walikuwa wakiishi magerezani.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Julai 15 mwaka 2011.

MPENDAZOE ADAI AG ANANJAMA NA KESI YAKE

Na Happiness Katabazi

ALIYEKUWA mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea(Chadema), Fred Mpendazoe amwandikia barua Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ya malalamiko kwamba mapingamizi yanayoondelewa kuekwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wenzake katika kesi yake yana njama ya kuchelewesha kesi hiyo ya kupinga matokeo ya jimbo hilo isimalizike kwa wakati.


Katika kesi ya kupinga matokeo ya jimbo hilo Na.98/2010. Mpendazoe anamshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mbunge wa jimbo hilo Dk.Makongoro Mahanga(CCM) na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo ambalo wanatetewa na David Kakwaya, Patience Ntinwa na Jerome Msemwa ambapo mlalamikaji anataka ushindi huo utenguliwe kwasababu kanuni na taratibu za sheria ya uchaguzi zilikiukwa.

Barua hiyo hiyo iliandikwa Julai 5 mwaka huu, na wakili wa mlalamikaji, Peter Kibatala yenye sababu saba ambayo inaanza kwa kumuomba Msajili huyo aifikishe barua hiyo kwa Jaji Profesa Ibrahim Juma ambaye ndiye anasikiliza kesi hiyo ya msingi.

Wakili Kibatala anaeleza kuwa Juni 6 mwaka huu, Jaji Juma alitoa uamuzi wa kutaka hati ya madai iende ikafanyiwe marekebisho baada ya kutaka vituo vinne vya kupigia kura vya Kata ya Buguruni, vituo 2 vya Kata ya Tabata, na vituo 4 vya Kata ya Kipawa viondolewe katika hati ya madai ya awali.

Wakili huyo anasema baada ya uamuzi huo wa mahakama, Juni 20 mwaka huu, mlalamikaji aliwasilisha hati ya madai iliyofanyiwa marekebisho mahakamani hapo, na upande wa wadai Julai 4 mwaka huu, nao waliwasilisha majibu ya hati ya madai iliyofanyiwa marekebisho.

“Lakini siku hiyo wakati wadaiwa wanawasilisha majibu yao kwa maandishi, mdaiwa wa kwanza (AG) na mdaiwa wa tatu ambaye ni Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Segerea, waliwasilisha mapingamizi mawili wakitaka mahakama hiyo iifute hati ya madai iliyofanyiwa marekebisho kwasababu ni batili na imeongeza lalamiko jipya kinyume na amri ya mahakama iliyotolewa Juni 6 mwaka huu, ambayo ilimwamuru mlalamikaji kwenda kuifanyia marekebisho hati ya madai kwa kuviondoa vituo hivyo vya kupigia kula katika hati hiyo.

“Naandika barua hii kwako mheshimiwa kwa masikitiko makubwa na uamonifu mkubwa licha hatuna jinsi ya kuizuia mahakama hii isikilize pingamizi hilo la wadaiwa ila pingamizi hilo linatufanya tuwe na hisia mbaya kwamba wadaiwa hao wameliwasilisha mbele yako kwa lengo la kuchelewesha kesi hii isimalizike ndani ya muda wa mwaka mmoja ambao umewekwa na Sheria ya Uchaguzi…kwa kuwa tunaamini kabisa hati yetu yetu tuliyoifanyia marekebisho siyo batili kama inavyodaiwa na hao wenzetu ” alidai Wakili Kibatala.

Hivyo wakamuomba Jaji Juma kuwazuia wadaiwa kuwasilisha mapingamizi ambayo yanarudisha nyuma kasi ya uendeshwaji wa kesi hiyo ya Uchaguzi ambayo kwa mujibu wa Kanuni na Sheria ya Uchaguzi inataka kesi ya uchaguzi imalizike ndani ya mwaka tangu ilipofunguliwa wakati kesi hiyo imefunguliwa Novemba mwaka jana, na hadi sasa bado ushahidi haujaanza kutolewa.

Aidha kesi hiyo ilikuja jana mbele ya Jaji Juma kwaajili ya kupanga tarehe za kuanza kusikiliza kesi hiyo lakini jaji huyo alishindwa kupanga tarehe hizo kama alivyoahidi Juni 6 mwaka huu, kwa sababu ya wadaiwa wawili kuwasilisha mapingamizi mawili ambapo kisheria mahakama inapaswa iyasikilize kwanza na kuyatolea uamuzi mapingamizi hayo ndiyo ije ipange tarehe za kuanza kupokea ushahidi.

Hata hivyo jaji huyo alisema Julai 27 mwaka huu, ndiyo atayasikiliza mapingamizi hayo mawili na kuwataka mawakili wa pande zote mbili wafike mahakamani hapo bila kukosa.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Julai 13 mwaka 2011.

MAHAKAMA YA KISUTU ,HII NI AIBU

Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, ni miongoni mwa mahakama za hadhi hiyo yenye umaarufu kuliko nyingine zote hapa nchini.


Naweza kusema umaarufu wa Mahakama ya Kisutu unatokana na baadhi ya mambo kadha wa kadha kama waandishi wa habari za mahakama kila siku tano za juma kuweka kambi mahakamani hapo kwa ajili ya kufuatilia kesi mbalimbali na kisha kuziripoti.

Baadhi ya watu wenye umaarufu katika jamii, maofisa wa serikali, taasisi za kidini na michezo wamefunguliwa kesi katika mahakama hiyo na baadhi kufungwa jela baada ya kukutwa na hatia na wengine kushinda kesi zao.

Mambo mengine yanayoifanya mahakama hiyo iwe maarufu ni kwa sababu mahakama hiyo ipo katikati ya Jiji la Dar es Salaam na sifa nyingine ni kwamba hivi sasa mahakama hiyo ipo katika hatua za mwisho za ukarabari wa majengo yake.

Napongeza kukarababitiwa kwa mahakama hiyo.

Leo nazungumzia kuhusu uchafu wa vyoo vitatu vya nje vya mahakama hiyo ambavyo vinashusha heshima na hadhi ya uongozi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kwa wale wenzangu ambao tunapata fursa ya kufika mahakamani hapo kwa siku tano za juma, au wale wananchi wanaofika mahakamani hapo kwa ajili ya shida mbalimbali na kupata fursa ya kuingia kwenye vyoo vitatu vilivyopo nyuma ya mgahawa wa mahakama hiyo, watakubaliana na mimi kuwa vyoo hivyo vinatia kinyaa na kichefuchefu kwa ajili ya uchafu na aviwekwi maji kwa ajili ya watumiaji.

Binafsi ninachokizungumza hapa nimekuwa nikikishuhudia kwa macho yangu na mara ya mwisho ni Ijumaa iliyopita, nilipoingia ndani ya vyoo hivyo nikiwa na mwandishi mmoja, sote tukashuhudia kadhia hiyo iliyotukera.

Kwa kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii chini ya Waziri Dk. Haji Mponda kila mara imekuwa ikitusisitiza wananchi tuweke mazingira yetu safi na tunapotoka vyooni tunawe mikono ili kujiepusha na magonjwa ya milipuko na kuweka vyoo vyetu safi, lakini msisitizo huo wa wizara hiyo naona unapuuzwa na wahusika wa usafi wa Mahakama ya Kisutu ambao wamepewa jukumu la kuhakikisha vyoo hivyo vitatu vinakuwa visafi.

Sote tunafahamu mahakamani ni sehemu ambayo watu wengi wanakuja na kama watu wengi wanakuja ni dhahiri taasisi hiyo inapaswa iwe na vyoo safi ili kuepusha magonjwa ya milipuko.

Katika mgahawa wa Mahakama ya Kisutu nyuma yake ndiyo hivyo vyoo.

Watu wanapata vyakula na vitafutwa wakati wakisubiri kesi zao na wengine huwa wanakwenda kwenye vyoo hivyo ambavyo hivi sasa vimebadilika rangi kwaajili ya uchafu.

Hatuoni kwamba kama uongozi wa mahakama unaohusika na masuala ya usafi wa mazingira ya eneo hilo usipojirekebisha na kuvifanyia usafi vyoo hivyo mwisho wa siku vinaweza kuleta magonjwa ya mlipuko mahakamani?

Au ni kwa sababu vyoo hivyo havitumiwi na waheshimiwa mahakimu ndiyo maana havisafishwi ipasavyo na kuwekwa maji? Au kwakuwa vyoo hivyo vinatumiwa na watu wa kawaida ambao si mahakimu?

Siku hizi karibu kote barabarani dawa za kusafisha vyoo zinauzwa tena kwa bei ndogo.

Sasa kinachowashinda ni kitu gani kumwajiri mtu atayekuwa akisafisha vyoo hivyo kwa uhakika, kujaza maji na kutoa mabaibui yaliyotanda kwenye vyoo hivyo?

Mbona hali sivyo kwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama ya Rufani? Au ndiyo mahakama ya Kisutu itajitetea kuwa inapewa fungu dogo la fedha hivyo haliwezi kutosha kununua dawa za choo, kumlipa msaficha vyoo hivyo?

Lakini katika hilo la uchafu kuhusu vyoo hivyo vitatu sishangai sana, kwani ningali nikikumbuka miaka mitatu nyuma vyumba vya wazi vinne vya kuendeshea kesi vya mahakama hiyo vilivyokuwa vimekithiri kwa uchafu wa tanda bui, feni ambazo zilikuwa zimechakaa na kulika na kutu na ndege kujenga jumba zao(viota) kwa majani katika feni hizo zilizokuwa zimeharibika, pamoja na kunuka kwa harufu ya mikojo kutoka ndani ya mahabusu ya mahakama hiyo.

Licha ya matatizo hayo ya miaka ya nyuma kutatuliwa kutokana na kufunguliwa kesi 12 za wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania (EPA) Novemba 4 mwaka jana, baada ya waandishi wa habari za mahakama kuziripoti kesi hizo kikamilifu pamoja na kuyageukia matatizo hayo kuyaandika katika vyombo vya habari na hatimaye mwisho wa siku matatizo hayo yakatatuliwa na feni mpya zikanunuliwa na kufungwa.

Lakini kwa sasa feni hizo zimeanza kuwa na vumbi na hazionyeshi dalili za kufutwa vumbi hilo mara kwa mara.

Nayaandika haya kwa nia njema ya kujenga na si kuboboma.

Kupitia mtazamo huu naamini wahusika kama ni wasikivu na wapenda changamoto wataifanyia kazi kero ya uchafu wa vyoo ambao unaipa sifa mbaya mahakama hiyo yenye mahakimu wakazi wanaoongozwa na Hakimu Mkuu Mfawidhi Elvin Mugeta, watanashati wanaovalia suti na majoho safi, lakini vyoo vitatu vilivyopo ndani ya mahakama wanayoiongoza ni vichafu.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

0716 774494.
www.katabazihappy.blogspot.com
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Julai 12 mwaka 2011.

WAHITIMU UDSM WAHAMASISHWA KUSHIRIKI JUBILEE YA MIAKA 50


Na Happiness Katabazi

KITIVO cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimewataka waadhili wastaafu, wahitimu wa fani ya sheria waliowahi kuhitimu kozi ya cheti na shahada mbalimbali za fani ya sheria katika kitivo hicho kushiriki kwenye maadhimisho ya jubilee ya miaka 50 yatayofanyika Oktoba 25 mwaka huu, chuoni hapo.


Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Paramaganda Kabudi alitoa wito huo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jana chuoni hapo ambapo alisema lengo la mkutano huo wa waandishi wa habari ni kuitambulisha Kamati ya Maandalizi ya maazimisho ya miaka 50 ya kitivo hicho na jinsi maadhimisho hayo yatakavyoazimishwa.

Profesa Kabudi alisema Kitivo cha Sheria ndiyo kilikuwa kitivo cha kwanza kanzishwa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika ya Kati pia ndiyo kitivo cha kwanza kuanzishwa UDSM Oktoba 25 mwaka 1961 ambacho kuanzishwa kwa kitivo hic ambacho kuanzishwa kwa kitivo hicho ndiyo kikaja kusababisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuzaliwa mwaka 1970.

Kabudi ambaye ni Mwenyekiti Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo ya nusu karne alisema wiki ya maazimisho hayo yataanza rasmi Oktoba 17-25 mwaka huu, ambapo katika wiki hiyo ya maadhimisho kutafanyika kongamano mdahalo, kujadili mada ya Ukatiba na ujenzi wa Katiba mpya ya Tanzania, kusikiliza hotuba za wanafunzi 12 wa kwanza waliohitimu sheria katika kitivo hicho, pia hotuba zitakazotolewa waadhili wa kwanza wa kitivo hicho, pia wasomi wa sheria mbalimbali ambao wamewai kusomea fani hiyo katika chuo kikuu cha UDSM.

“Kitivo cha Sheria kimepata kutoa wasomi mbalimbali wa fani hiyo ambao leo hii wanafanyakazi katika ngazi mbalimbali duniani na Oktoba 25 mwaka huu, kitivo cha Sheria ndiyo kinatimiza miaka 50 tangu kilipoanzishwa na tunawataka umma utambue uanzishwaji wa kitivo hicho ni harama ya kwanza ya uhuru wa nchi yetu ambapo Desemba 9 mwaka huu, taifa linaazimisha miaka 50 ya uhuru hivyo utaona kitivo kilianza halafu miezi mitatu baadaye taifa likapata uhuru”alisema Profesa Kabudi.

Aidha alisema maandalizi ya maamizisho hayo ambayo yatausisha wasomi mbalimbali wa sheria toka pande zote za dunia yamekamilika na kwamba wanawaomba wasomi wa fani hiyo na umma kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika wiki kuudhulia maazimisho hayo kwani watajifunza mengi hasa ukizingatia kitivo hicho ndiyo kitivo cha kwanza kaunzishwa na kitivo hicho ndiyo kilichopelekea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzishwa.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatatu, Julai 11 mwaka 2011.

KESI YA MAHALU,MWENZAKE YAPIGWA KALENDA

Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa mara nyingine jana ilishindwa kuanza kusikiliza utetezi wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa zaidi ya Euro milioni mbili kwasababu mawakili wa utetezi walikuwa na udhuru.


Wakili Mwandamizi wa Serikali Ponsian Lukosi mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Elvin Mugeta aliambia mahakama kesi hiyo ilikuja jana kwaajili ya washtakiwa hao kuanza kujitetea na kwamba upande wa jamhuri upo tayari kwaajili ya kuendelea na kesi hiyo.

Lakini wakili wa utetezi mmoja Beatus Malima aliambia mahakama hiyo kuwa upande wa utetezi jana haupo tayari kwaajili ya kuendelea na kesi hiyo kwasababu wakili kiongozi wa utetezi Mabere Marando yupo Mahakama ya Rufani kuudhulia kesi nyingine na Alex Mgongolwa anaugua hivyo wanaomba kesi hiyo iarishwe.

Ombi hilo lilikubaliwa na hakimu huyo ambaye aliairisha kesi hiyo hadi Agosti 5 ba 26 mwaka huu, ambapo washtakiwa hao watapanda kizimbani kutoa ushahidi wao.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi,Julai 9 mwaka 2011.

KESI YA JERRY MURRO YAPIGWA KALENDA

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kwa mara nyingine jana ilishindwa kuanza kusikiliza utetezi wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), Jerry Murro na wenzake wawili wanaokabiliwa na kesi ya kula njama, kushawishi na kuomba rushwa ya sh milioni 10 kutokana na wakili wa utetezi, Majura Magafu kushindwa kutokea mahakamani.


Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Stanslaus Boniface mbele ya Hakimu Mkazi, Frank Moshi, aliieleza mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea na kwamba upande wa jamhuri upo tayari kuendelea na kesi hiyo.

Hata hivyo, Wakili wa Jerry, Pascal Kamala, aliimbia mahakama kuwa wakili wa mshtakiwa wa pili na watatu ambaye ni Magafu hajafika mahakamani, hivyo wanaomba kesi iairishwe.

Hakimu Moshi alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Agosti 3 mwaka huu washtakiwa hao watakapoanza kujitetea.

Mbali na Murro, washitakiwa wengine ni Edmund Kapama na Deogratius Mugasa ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 15 mwaka 2010.

Washitakiwa haop wanadaiwa kula njama, kushawishi na kuomba rushwa ya sh milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Karoli Wage. Kati ya mashitaka matatu yaliyofunguliwa dhidi yao, Murro anakabiliwa na mashitaka mawili.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Julai 7 mwaka 2011.

MAHANGA ATAKA KESI YA MPENDAZOE IFUTWE


Na Happiness Katabazi

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Mbunge wa Jimbo la Segerea(CCM) na Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 wa jimbo hilo, wanaokabiliwa na kesi ya madai kupinga matokeo ya uchaguzi huo, wamewasilisha majibu katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na wameomba kesi hiyo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo (CHADEMA), Fred Mpendazoe ifutwe kwa gharama.


Sambamba na hiyo wadai wawili AG, na Msimazi wa Uchaguzi wa jimbo hilo wamewasilisha mapingamizi mawili ambapo pingamizi la kwanza wanadai kuwa hati ya madai iliyofanyiwa marekebisho na kuwasilishwa na Mpendazoe Mahakamani ni batili kwasababu imekiuka amri ya mahakama iliyomtaka mlalamikaji huyo akaifanyie marekebisho tu hati hiyo ya madai lakini cha kustaajabisha mlalamikaji huyo amewasilisha hati hiyo iliyofanyiwa marekebisho huku akiwa ameongeza dai jipya ambalo halikupaswa kuwekwa kwenye hati hiyo hivyo wakaomba hati hiyo iliyofanyiwa marekebisho nayo itupwe.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo na wanatetewa na mawakili wa serikali David Kakwaya na Patience Ntwina wakati Mahanga ambaye ni Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Maendeleo ya Vijana anatetewa na wakili wa kujitegemea Jerome Msemwa waliwasilisha majibu hayo ya hati ya madai iliyofanyiwa marekebisho kumetokana na amri iliyotolewa na Jaji Profesa Ibrahim Juma, Juni 22 mwaka huu kwa wadai hao kuwa ifikapo jana wawe wamewasilisha majibu ya hati ya madai iliyofanyiwa marekebisho.

Kwa mujibu wa majibu hayo ambayo yamewasilishwa mahakamani kwa njia ya maandishi na Tanzania Daima inayo nakala yake, wadaiwa hao wanaiomba mahakama iifute kesi hiyo kwasababu madai ya mlalamikaji yanayodai taratibu za sheria ya Uchaguzi zilikiukwa katika uchaguzi ule ambao ulimtangaza mdaiwa wa pili(Mahanga) kuwa ndiyo mshindi hayana msingi.

“Sisi tunasema uchaguzi ule ulifuata taratibu zote za Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010 na ndiyo maana Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilimtaka Dk.Mahanga kuwa ndiyo mshindi kati ya wagombea wote walioshinda na hivyo kufanya Mahanga kuwa mbunge….kwa hiyo sisi tunashangazwa na hayo madai ya mlalalamikaji kuwa sheria na taratibu za uchaguzi zilikiukwa na ndiyo maana tunaiomba mahakama hii tukufu iifute kesi hii tena kwa gharama”alidai Wakili Kakwaya.

Kuwasilishwa mahakamani kwa hati hiyo iliyofanyiwa marekebisho, kulitokana na utekelezaji wa amri iliyotolewa na Jaji Profesa Juma, Juni 6 mwaka huu, ambapo aliamuru hati ya madai ya awali ikafanyiwe marekebisho kwa kuviondoa vituo 10 vya kupigia kura ambavyo mlalamikaji hakuvitaja kwa majina.

Baada ya kufanyiwa marekebisho, Wakili wa mlalamikaji Peter Kibatala alieleza hivi sasa hati hiyo inasomeka kuwa wamebakiwa na vituo vya kupigia kura 249 ambapo vituo 120 ni vya Kata ya Kiwalani na vituo 129 ni vya Kata ya Vingunguti.

Jaji Juma aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 12 mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa na kupanga tarehe ya kuanza kusikilizwa.

Novemba mwaka 2010 Mpendazoe alifungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo ambayo yalimtangaza mbunge wa sasa Dk. Mahanga kuwa ndiye mshindi kwa sababu uchaguzi huo ulikiuka matakwa ya sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano,Julai 6 mwaka 2011.

POLEPOLE LOWASSA


Na Happiness Katabazi

HIVI karibuni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, alisema mengi yenye tija bungeni na kuwataka viongozi wachukue maamuzi magumu.


Lowassa aliwashambulia viongozi wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwa wana ugonjwa wa kuogopa kufanya maamuzi magumu. Bila kufafanua, alisema ni bora kiongozi uhukumiwe kwa kufanya maamuzi magumu kuliko kuogopa.

Pamoja na mambo mengine, alisema wakati taifa likiadhimisha miaka 50 ya Uhuru, serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imefanya mambo mengi ambayo si vema watu kuyabeza.

Binafsi nakubaliana na hoja ya Lowassa kwamba wakati taifa likiadhimisha miaka 50 ya Uhuru wake, serikali ya CCM imefanikiwa kuleta maendeleo kwa kiwango fulani katika sekta ya elimu, teknolojia hasa ya habari, nishati na barabara.

Anayebisha katika hili ni wazi hajapata fursa ya kuizunguka Tanzania Bara na Zanzibar, kamwe sitamlazimisha mtu akubaliane nami kwamba katika kipindi hiki cha miaka 50 ni wazi kuna hatua za maendeleo taifa limepiga.

Lakini kuhusu hoja ya Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli kwamba hivi sasa viongozi wana ugonjwa wa kutochukua maamuzi magumu, binafsi kauli hii imeniachia na maswali mengi kuliko majibu.

Mimi ni miongoni mwa wanahabari tunaofuatilia mambo yanayohusu mustakabali mwema wa taifa hili, matamshi na matendo yanayofanywa na baadhi ya wanasiasa wetu, huwa nayaweka kwenye kumbukumbu zangu.

Itakumbukuwa kuwa Rais Kikwete aliapishwa Desemba 23 mwaka 2005 kuliongoza taifa hili akiwa ni rais wa awamu ya nne, siku chache baadaye aliliteua jina la Lowassa likapelekwa bungeni ili kuidhinishwa kuwa waziri mkuu.

Kweli Lowassa alianza kazi hiyo kwa kishindo, na mpongeza kwa kazi nzuri ya kushupalia ujenzi wa shule za sekondari kila kata licha ya changamoto kadha wa kadha zilizopo kwenye shule hizo, zimesaidia kuwapa tamaa wazazi wengi kuwapeleka watoto wao ili wapate elimu.

Lakini ningali nikimkumbuka kwa jengo la Hoteli ya Chang’ombe Village lililoanguka na kuua mtu mmoja, Lowassa alitembelea eneo hilo na kuamuru mhandishi wa Manispaa ya Temeke na mainjia wake wakamatwe.

Agizo lake lilitekelezwa na wahusika walifikishwa mahakamani, kwa kosa la kuua bila kukusudia. Mwisho wa siku mainjinia wa manispaa hiyo walishinda kesi hiyo na wakaachiliwa huru.

Pia ningali na kumbukumbu ya majengo mawili ya ghorofa yaliyopo Masaki jijini Dar es Salaam ambapo ulizuka utata kuwa wamiliki wa majengo hayo walijenga eneo hilo bila kibali cha Manispaa ya Kinondoni.

Utata ulikuwa kwamba kuna baadhi ya watumishi wa manispaa hiyo waliwapatia kibali cha ujenzi kilichoghushiwa.

Mgambo walitekeleza agizo la Lowassa na kuyabomoa majengo hayo ambayo ujenzi wake ulikuwa umekamilika.

Hata hivyo wamiliki wa majengo yale walikimbilia Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na kuifungulia kesi serikali na walishinda, mahakama ikaamuru wenye majengo walipwe mamilioni ya fedha.

Ikumbukwe wakati Lowassa ni mwana CCM na Ibara ya 18(a) ya Katiba ya nchi ya mwaka 1977 inasema kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni na kueleza fikra zake hivyo Lowassa wakati akizungumza alikuwa akiitumia haki yake hiyo ya kikatiba.

Lakini anapotuambia viongozi wengi hivi sasa wana ugonjwa wa kutochukua maamuzi magumu, kwanini hajatutajia viongozi walioshindwa kuchukua maamuzi hayo?

Maana hata ndani ya majeshi yetu kuna viongozi,kwenye dini,serikalini na bungeni kuna viongozi pia. Swali nililonalo ni je, hata viongozi walio kwenye majeshi yetu nao wanasumbuliwa na ugonjwa na kushindwa kuchukua maamuzi magumu?

Namtaka Lowassa atambue kuwa kuna baadhi ya viongozi huko kwenye serikali inayoongozwa na chama chake, kwenye majeshi yetu na kwenye mhimili wa mahakama ni wachapakazi na waaminifu, wenye uthubutu wa kuchukua uamuzi wa haki na si wa jazba.

Wanachukua uamuzi mgumu wenye masilahi kwa taifa letu na kamwe viongozi hao hawajitokezi hadharani wakitamba kuwa wamechukua uamuzi mgumu.

Viongozi wa aina hii binafsi nawafahamu na wengine wamekuwa wakiingia ofisini saa 12 asubuhi lakini hata siku moja sijawaona wakipita mitaani na kujitapa.

Kama ni kweli Lowassa anasema viongozi wa serikali ya awamu ya nne wanasumbuliwa na ugonjwa huo, kwa nini wananchi wengi katika Uchaguzi wa mwaka 2010 waliipatia tena kura za ndiyo CCM ikashinda na kisha ikaendelea kutawala?

Ugonjwa huo ameubaini lini? Ni baada ya kuwa nje ya utumishi wa serikali tangu alipojiuzulu kwa kashfa ya Richmond mwaka 2008? Na kama kweli ugonjwa huo ameubaini, anakusudia kutumia dawa ipi ili kuwatibu viongozi hao?

Nimalizie kwa kusema, Watanzania tunahitaji kuwa na viongozi makini wasio na jazba.
Viongozi wanaochukua uamuzi wakati wana jazba, mara nyingi viongozi wa aina hiyo huigharimu serikali, kwani walioonewa na hukimbilia mahakamani, fedha za walipa kodi ndizo zinazotumika kuwalipa fidia walioonewa.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Julai 5 mwaka 2011.

'MARANDA,FARIJALA WANAKESI YA KUJIBU"

Na Happiness Katabazi
UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya wizi wa sh bilioni 2.2 katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania, inayomkabili Kada wa (CCM), Rajabu Maranda na Farijala Hussein umejigamba kuwa umeweza kuithibitisha kesi hiyo na umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, iwaone washtakiwa wote wana kesi ya kujibu.


Wakili Mwandamzi wa Serikali Arafa Msafiri aliyekuwa akisaidiwa na Oswald Tibabyekomya mbele ya Jaji Fatma Masengi aliyekuwa akisaidiwa na Hakimu Mkazi Catherine Revocati na Projestus Kahyoza aliwasilisha majumuisho hayo jana ambapo aliiomba mahakama hiyo iwaone washtakiwa wana kesi ya kujibu katika makosa yote saba wanayokabiliwa nayo.

Washtakiwa wote wanaishi gerezani baada ya Mei 23 mwaka huu, mahakama ya Kisutu kuwa hukumu kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa ya kughushi na kisha kujipatia ingizo la sh bilioni 1.6 toka BoT na hivi wanakabiliwa jumla ya kesi tatu za EPA ambazo bado hazijatolewa hukumu.

Wakili Msafiri alikuwa akiwasilisha majumuisho hayo kwa mtindo wa kuchambua kosa moja moja huku akitumia ushahidi na vielelezo vilivyokwishatolewa na upande wa Jamhuri mahakamani hapo na kupokelewa, alidai kosa la saba ni la kughushi hati ya usajili wa jina biashara la Money Planners and Consultant ambacho ni kielelezo cha tatu ambayo walionyesha imetolewa na kusainiwa na shahidi wa kwanza wa Jamhuri ambaye ni Msajili Msaidizi wa Makampuni(BRELA).

Msafiri alidai kwa mujibu wa ushahidi wa shahidi huyo wa kwanza aliutoa hapa mahakamani,ambapo alikanusha kutoa jina hilo la biashara kwa washtakiwa hao na kwamba saini iliyodaiwa na washtakiwa kuwa ni ya kwakwe si yake na ripoti ya mtaalamu wa maandishi ilitolewa mahakamani hapa na shahidi mwingine ilidhibitisha washtakiwa hao waligushi jina la biashara,majina wa miliki na saini ya Naibu Msajili wa BRELA.

“Naibu Msajili wa BRELA katika ushahidi wake alieleza katika kampuni hizo hakukuwa na mabadiliko ya majina ya wamiliki wala jina la biashara la Money Planers kama ilivyodaiwa na upande wa utetezi na kwamba mtu anapotaka kubadili jina la biashara au wamiliki nilazima BRELA itampatia hati ya kubadilisha wamiliki au jina (Certificate Change of Particular) na washtakiwa hawana hati hiyo.

“ Na sisi Jamhuri katika kuthibitisha kosa hili tunasema kuna vielelezo viwili ambavyo ni maelezo ya onyo washtakiwa hao ambapo Farijala alikiri kuwa yeye ndiyo aliyeandaa fomu ya kujaza majina ya wamiliki wa kampuni yao ya Money Planers and Consultance BRELA kwa kutumia majina ya Fundi Kitunga na Thobias Nyingo ambao wanaonekana ndiyo wamiliki wa kampuni kwa maelekezo aliyoepewa na Maranda na kwamba yeye hawafahamu watu hao na hajawahi kuwaona.

“Na kwa mujibu wa maelezo ya onyo ya Maranda mshtakiwa huyo wa kwanza naye anadai hamfahamu Fundi na Nyengo ila akadai kuwa Fundi ni mtu wa karibu wa Farijala ….kwa maelezo hayo sisi upande wa Jamhuri tunasema washtakiwa hao ndiyo walitenda kosa hilo kwani nyaraka hizo za kughushiwa zimekutwa mikononi mwao wakizimiliki na sheria iko wazi kuwa anayekamatwa akimiliki nyaraka za kughushi ndiyo anayeshtakiwa kwa kosa la kughushi” alidai wakili Msafiri.

Akichambua kosa la tatu, ambalo ni la kuwasilisha nyaraka hizo zilizoghushiwa kwenye Benki ya Umoja wa Africa(UBA) ambao kwa sasa inatambulika kama BOA Benki, wakili huyo alidai kuwa washtakiwa hao ndiyo walikwenda kufungua akaunti yao Na.10913790010 kwa majina yao ya Farijala, Maranda kupitia nyaraka hizo zilizoghushiwa ambazo zilikuwa na majina ya kufikirika ya Fundi na Nyengo na kisha kujipatia ingizo la bilioni 2.2 toka kwa BoT.

Alidai kosa la nne, ni kughushi hati ya kuamisha deni (deed of assignment) ambapo ni kielelezo cha kumi ambacho kinaonyesha kampuni ya B.Grancel and Company ya Ujerumani iliyowakilishwa na Jones Bach na kampuni ya Money Planers iliwasilishwa na Fundi katika kuandaa hati hiyo ya kuamisha deni na kwamba kuna ushahidi wa mazingira wa kutosha kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo.

“Jamhuri tunasema huyo Fundi ni mtu wa kufikirika washtakiwa walimtunga kwa lengo la kuibia Tanzania, kwani katika maelezo ya onyo mshtakiwa wa pilisi Farijala alidai amfahamu Fundi wala Nyengo…na Fundi hajausika kwenye utoaji fedha kwenye akaunti, kuifungua akaunti hiyo…waliofungua akaunti, kuchuchukua fedha hizo ni washtakiwa wenyewe.

“Na ukiitaza hati hiyo ya kuamisha deni ambayo sisi upande wa Jamhuri tunasema imeghushiwa, utaona hati hiyo ilisainiwa Ujerumani baina ya kampuni hizo mbili Septemba 8 mwaka 2005, ukiangalia folio ya pili utaona kampuni ya B Grancel ya Ujerumani tarehe hiyo hiyo waliituma hapa nchini kwa Gavana wa BoT na Folio tatu inaonyesha siku hiyo hiyo , Fundi alimtumia hati hiyo Gavana wa wakati huo marehemu Daud Balali….sasa inawezekanaje hati hiyo isainiwe Ujerumani halafu siku hiyo hiyo ikatumwa kwa gavana na hati ya Fundi inaonyesha hati hiyo ameituma akiwa hapa nchini “alidai wakili Msafiri.

Aidha akilichambua shtaka la tano ambalo ni la kuwasilisha hati hiyo ya kuamisha deni ambayo imegushiwa na kwamba wameweza kuthibitisha kosa hilo kwasababu ushahidi uliopo unaonyesha ni washtakiwa hao ndiyo waliwasilisha hati hiyo ya kuamisha deni ambayo imegushiwa katika BoT na kisha kujipatia ingizo la Sh bilioni 2.2.

Wakili Msafiri alidai shtaka la sita ni la wizi, ambapo alidai pia kuwa wameweza kulithibisha kwani kwa mtiririko wa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa jamhuri ni ambao unaonyesha washtakiwa walikula njama, wakaghushi nyaraka mbalimbali na kisha wakatumia nyaraka hizo kufungua akaunti na kisha washtakiwa hao walikiri mahakamani hapo waliingiziwa fedha hizo kihalali na BoT.

Wakili huyo alidai shtaka la kwanza ni la kula njama, ambapo alidai wameweza kuthibitisha kosa hili kwani kupitia maelezo ya onyo ya washtakiwa hao na yalipokelewa na mahakama hii kama vielelezo,yanadhiirisha wazi washtakiwa hao walipanga kwa pamoja kuibia BoT kiasi hicho cha fedha.

Kwa upande wake kiongozi wa jopo la mahakimu wakazi wanaosilikiza kesi hiyo Jaji Fatma Masengi alisema wamesikiliza kwa makini majumuisho yaliyotolewa na upande wa Jamhuri jana na majumuisho yaliyotolewa na upande wa utetezi siku za nyuma na kwamba Julai 18 mwaka, watakuja kutoa uamuzi wa kuwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu au la.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne,Julai 5 mwaka 2011.

UAMUZI KESI YA SAMAKI WA MAGUFURI JULAI 14/2011

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imesema Julai 14 mwaka huu itatoa uamuzi wake wa ama kuwaona washtakiwa katika kesi ya Uvuvi haramu ukanda wa Tanzania katika bahari ya Hindi inayowakabili raia 36 wa kigeni ama wanakesi ya kujibu au la.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Jaji Agustine Mwarija muda mfupi baada ya wakarimani wanne wa lugha za kigeni katika kesi hiyo kumaliza kutoa tafsiri ya hoja zilizowasilishwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Biswalo Mganga na Prosper Mwangamila kumaliza kuwasilisha majumuisho yao ambayo yaliiomba mahakama hiyo iwaone washtakiwa wote wanakesi ya kujibu kwani wanaamini wameweza kuleta ushahidi thabiti ambao utaishawishi mahakama iwaone washtakiwa wanakesi ya kujibu.

“Nimesikiliza hoja za pande zote mbili zilizowasilishwa na mawakili wa pande zote mbili,hivyo naairisha kesi hii hadi Julai 14 mwaka huu ambapo siku hiyo nitakuja kutoa uamuzi wa kuwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu au la”alisema Jaji Mwarija.

Juni 16 na 17 mwaka huu, mawakili wa utetezi Ibrahim Bendera na John Mapinduzi waliwasilisha majumuisho ya kesi hiyo ambayo waliiomba mahakama hiyo iwaone washtakiwa wote hawana kesi ya kujibu kwasababu upande wa Jamhuri umeleta ushahidi dhaifu na kwamba wakati wateja wao wanakamatwa Machi 7 mwaka 2009, Tanzania haikuwa na Sheria ya Uvuvi wa Samaki katika kina kirefu cha Bahari(The Deep Sea Fishing Authority Regulation, 2009).

Wakati Juni 20 na 21 mwaka huu, mawakili wa serikali Mganga na Mwangamila nao waliwasilisha majumuisho yao kwa njia ya mdomo ambao walijigamba kuwa wameweza kuthibitisha kesi na hivyo wanaiomba mahakama iwaone washtakiwa wote wanakesi ya kujibu.Ambapo jana wakarimani wanne wanaotafsiri yote yanayozungumzwa mahakamani hapo kwa lugha za washtakiwa hao walimaliza kutoa tafsri ya majumuisho hayo ya serikali.

Machi 2009 ilidaiwa na upande wa Jamhuri kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa matatu ambayo kufanya uvuvi katika bahari ya Hindi ukanda wa Tanzania bila leseni na pia kufanya uharibifu wa mazingira katika eneo la ukanda huo.

Chanzo:Happiness Katabazi Juni 25 mwaka 2011.