MWANZO,MWISHO WA KESI YA JERRY MURRO


Na Happiness Katabazi


NOVEMBA 20 mwaka 2011: Jerry Murro alifunga ndoa na Jeniffer John katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Usharika wa Azani Front jijini Dar es Salaam.



Oktoba 28 mwaka huu, upande wa Jamhuri uliwaowakilishwa mwanzo hadi mwisho wa kesi hii na Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Stanslaus Boniface uliwasilisha majumuisho yao kwa njia ya maandishi ambayo yaliomba mahahakama imuone Murro na wenzake wanahatia.


Boniface alidai hoja ya Wakili wa Murro, Richard Rweyongeza inayodai kuwa Murro hakutenda makosa hayo na kwamba anashangaa ni kwanini polisi walifanya haraka kumkamata Murro wakati alikuwa hajapokea kiasi hicho cha fedha,ni dhahifu kwasababu kabla ya Murro kukamatwa tayari Wage alishafika kituo cha polisi na kutoa taarifa kuwa mshtakiwa huyo amemwomba rushwa.

“Na kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 kinasema kitendo cha kuomba rushwa ni kosa chini ya kifungu hicho ….sasa namshangaa sana wakili Rweyongeza anavyo dai ni kwanini polisi wasingesubiri Murro apokee zile Sh milioni 10 za rushwa.
Tunaiomba mahakama iipuuze hoja hiyo ya wakili Rweyongeza kwasababu haina msingi kwani sheria hiyo ya kuzuia rushwa inatamka bayana mtu yoyote atayeomba rushwa, kupokea rushwa, kula njama ni makosa matatu yanayojitegemea na kitendo cha Murro kuomba rushwa tayari alikuwa ameishatenda kosa na ndiyo maana polisi walimkamata”alidai wakili Kiongozi wa Serikali Boniface.

Aidha Wakili Boniface aliomba mahakama hiyo iikate hoja wakili wa Murro iliyokuwa ikidai kuwa Murro alikamatwa katika Hoteli ya City Garden Februali mwaka jana wakati mshatiwa huyo hotelini hapo kwaajili ya kuudhulia mkutano nma waandishi wa habari, hoja ambayo wakili hiyo wa seriakali ni ya uongo kwani siku hiyo hapakuwepo na mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika hapo na ndiyo maana si Murro wala wakili wake Rweyongeza wameweza kuleta ushahahidi unaonyesha siku hiyo hotelini hapo ulifanyika mkutano na waandishi wa habari na pia wameshindwa kumleta mtu aliyekuwa ameuitisha mkutano huo ili aje kuidhibitishia mahakama kuwa alikuwa ameitisha mkutano siku hiyo na kwamba ni yeye ndiye alikuwa amempigia simu Murro ili aje hotelini hapo kuudhulia mkutano.

“Ni rai ya upande wa Jamhuri kuwa tumeweza kuithibitisha kesi yetu na tunaiomba mahakama imuone Murro na wenzake wana hatia katika kesi hii inayowakabili kwani ushahidi, vielelezo na utetezi waliotuoa mahakamani hapa umedhibitisha kuwa washtakiwa hao walitenda makosa yanayowakabili hivyo tunaiomba mahakama hii tukufu iwatie hatiani”alidai Wakili Boniface.
Oktoba 21 mwaka huu, upande wa utetezi unaowakilishwa na mawakili wa kujitegemea Rweyongeza, Majura Magafu nao waliwasilisha majumuisho yao kwanjia ya maandishi na kuiomba mahakama iwaachilie huru washtakiwa hao kwasababu hawana hatia kwani ushahidi ulioletwa na Jamhuri ni wa kuunga unga na hautoshelezi kuishawishi mahakama kuwatia hatiani.
Wakili Rweyongeza alidai kuwa alisikilizwa kwa makini ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa Jamhuri lakini hajasikia kitu chochote kinacho muunganisha Murro na washtakiwa wengine wasiojulikana kula njama kutenda kosa hilo kama shtaka la kwanza kwanza linavyodai kuwa Murro na washtakiwa wenzake ambao ni Deo Mugassa na Edmund Kapama na watu wengine wasiyofahamika walitenda kusa la kushawishi ili wapewe rushwa Sh milioni 10 toka kwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage Karoli , Januari 20 mwaka 2010 ili asiwe kurusha tuhuma zake za ubadhilifu wa fedha za umma katika kipindi cha Usiku wa Habari kinachorushwa na Televisheni ya TBC1.

“Shtaka la kwanza katika hati ya mashtaka, linasomeka kuwa kosa lilitendeka Januari 28 mwaka 2010.Lakini ushahidi ulitolewa na Jamhuri ulionyesha kosa lilitendekea Januari 29 mwaka 2010…na hadi mapema Oktoba mwaka huu washtakiwa walimaliza kujitetea na hivyo kesi upande wa utetezi ikawa imefungwa , hati ya mashtaka ilikuwa ikisomeka Murro alitenda kosa hilo Januari 28 mwaka 2010 ndipo upande wa Jamhuri siku hiyo kabla ya utetezi kufunga kesi yao ukaamua kubadilisha hati ya mashtaka na mahakama ilikubali hati hiyo kubadilishwa kutokana na utofauti uliopo kati ushahidi na maelezo yaliyokuwa yameandikwa kwenye hati ya mashtaka.

“Kwa hali hiyo naona upande Jamhuri hauna maelezo ya uhakika yanayoonyesha mteja wangu alitenda makosa hayo na badala yake ikaamua kuleta ushahidi wa kuungaunga na matokeo yake ndiyo maana Murro aliyakana mashtaka yote yanayomkabili mahakamani hapa”alidai Rweyongeza.

Alidai kuwa kesi ya Jamhuri imesimama na kutegemea ushahidi wa shahidi wa tatu (Michael Wage) jambo linawapotosha kwa sisi upande wa utetezi tunamuona Wage siyo shahidi wa kuaminika na wanaoimba mahakama iupuuze ushahidi wake.

Wakili Rweyongeza alidai kuwa katika ushahidi mashahidi wa Jamhuri walidai kuwa shahidi wa tatu(Wage) kwakuanzia aliwapatia washtakiwa wote rushwa ya Sh 9,000,000 katika sehemu ya rushwa ya Sh milioni 10 aliyokuwa ameombwa na washtakiwa, na wakili huyo akadai kuwa kama hivyo ndivyo ni kwanini polisi wasingesubiri Murro apokee rushwa hiyo ndiyo wakamkamate na kuongeza ni kwanini polisi ilifanya haraka kumkamata Murro wakati bado hajapokea rushwa hiyo ya Sh milioni?
Kuwasilishwa kwa majumuisho hayo ya pande hizo mbili kwa tarehe tofauti yalitokana na amri iliyotolewa na Hakimu Moshi, Oktoba 4 mwaka huu, ambapo siku hiyo alizitaka pande zote kufanya hivyo.
Na siku ndiyo shahidi wa Murro alitoa ushahidi wake na washtakiwa wawili Deogratius Mugassa na Edmund Kapama nao walitoa utetezi wao na siku hiyo hiyo wakili wa utetezi Richard Rweyongeza aliambia mahakama kuwa huo ndiyo mwisho wa ushahidi wao.
Na kabla ya washtakiwa hao kuanza kutoa utetezi wao wakili wa serikali , Boniface aliwasilisha ombi la kutaka kubadilisha hati ya mashtaka ambapo ombi hilo lilikubaliwa na hakimu huyo ambapo alisema kuanzia siku hiyo hati ya mashtaka itasomeka kuwa washtakiwa waliomba rushwa Michael Wage Januari 29 mwaka jana katika hoteli ya Sea Cliff, tarehe ambayo inaoona na picha za CCTV ambazo zinawaonyesha washtakiwa hao walifika katika hoteli hiyo wakiwa na Wage.
Kabla ya kubadilisha hati hiyo,hati ya mashtaka ilikuwa ikisomeka kuwa washatkiwa hao walitenda kosa hilo Januari 28 mwaka jana, tarehe ambayo ilikuwa ikitofautiana na tarehe iliyokuwa ikionekana kwenye nakala ya picha ya CCTV kamera.
Agosti 18 mwaka 2011; Murro alipanda kizimbani na kujitetea ambapo aliiomba mahakama imuone hana hatia kwasababu kesi inayomkabili amebambikiziwa na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi.
Mei 2 mwaka 2011, kesi hiyo ilipata hakimu mpya ambaye ni Hakimu Moshi baada ya hakimu mkazi wa awali Gabriel Mirumbe aliyekuwa akiisikiliza kesi hiyo kuamishiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Machi 8 mwaka 2011, Hakimu Gabriel Mirumbe aliwaona washtakiwa wote wana kesi ya kujibu.Uamuzi huo ulitolewa ikiwa ni dakika chache baada ya shahidi wa saba wa upande wa Jamhuri D/C Koplo Lugano Mwampeta kumaliza kutoa ushahidi wake siku hiyo na Wakili wa Serikali Kiongozi Boniface kuieleza mahakama kuwa huo ndiyo ulikuwa mwisho wa ushahidi wao na kwamba wanafunga kesi yao.
Inspekta Lugano Mwambeta akitoa ushahidi wake siku hiyo alieleza kuwa yeye alisaidiana na SSP-Duwani Nyanda kupekua gari la Murro na katika upekuzi wao walikuta miwani ya kusomea ya Wage na pingu moja iliyokuwa ikimilikiwa na Murro ambapo vitu vyote hivyo viwili vilipokelewa mahakamani hapo kama kelelezo namba sita na saba.


Januari 26 mwaka huu; Shahidi wa sita ambaye ni Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Ilala, (SSP) Duwani Nyanda alitoa ushahidi siku hiyo hiyo na akaieleza mahakama jinsi alivyoongoza zoezi la upekuzi katika gari la Murro ambapo alidai alikuta pingu na miwani ya kusomea ambayo ni mali ya Michael Wage.
SSP-Nyanda alieleza kuwa Januari 31 mwaka 2010 saa 12 jioni akiwa ofisini aliamriwa na aliyekuwa Mkuu wake, Charles Mkumbo, kwenda kulipekua gari la Murro lenye namba za usajili T 545 BEH Toyota Cresta lililoegeshwa kwenye viunga vya Kituo Kikuu cha Polisi Kati(Central) Dar es Salaam.
Nyanda alieleza kuwa katika upekuzi wake alifanikiwa kupata pingu ambazo Wage alizibaini kuwa ndizo alizotishiwa nazo na Murro na miwani ya kusomea ambayo anadai ni yake aliiisahau kwenye gari hilo Januari 30 mwaka jana na kuongeza kuwa alikuwa na hato ya polisi ambayo Murro na Wage walisaini kuthibitisha kushuhudia upekuzi huo na kuitoa mahakamani kama kielelezo namba tano ambacho kilipokelewa na Hakimu Mirumbe.
Januari 25 mwaka huu; Shahidi wa tano, Mkaguzi wa Polisi, Antony Mwita(45) ambaye alitoa ushahidi wake siku hiyo hiyo alieleza mahakama kuwa kitabu cha kumbukumbu ya kupokea wageni cha Hoteli ya Sea Cliff kinaonyesha kuwa Januari 29 mwaka jana, Murro alifika hotelini hapo siku hiyo.
“Na kitabu hicho kinaonyesha mgeni wa 25 alikuwa ni Jerry Murro na alifika hotelini hapo kwa kutumia gari lake lenye namba za usajili T545 THE aina ya Cresta na mlinzi huyo aliipatia kadi Na.673 na aliingia hotelini hapo saa 7:33 na kuondoka saa 8:48 mchana. ”alidai Mkaguzi Mwita.

Aliendelea kuieleza mahakama kuwa licha ya yeye kukusanya kielelezo hicho cha kitabu pia katika upelelezi wake katika kesi hiyo alienda duka la Mizinga lililopo Upanga jijini, kujiridhisha kama ni kweli Murro alinunua pingu katika duka hilo, na upelelezi wake ulibaini kwamba ni kweli duka hilo lilimuuzia pingu hiyo Mei 26 mwaka 2009 kwa Sh 25,000 na akapewa risiti yenye kumbukumbu na. 34357410. Kwamba mahakama ilipokea risiti ya pingu hiyo kama kielelezo cha nne.
Na siku hiyo hiyo ya Januari 25 mwaka 2011; shahidi wa nne ambaye ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Issa Seleman Chabu (37) alitoa ushahidi wake ambapo aliieleza mahakama jinsi yeye na makachero wenzake walivyoweka mtego na kufanikiwa kumkamata Murro Januari 31 mwaka 2010.
Mpelelezi huyo kutoka ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala alieleza kuwa Januari 30 mwaka jana, saa nne asubuhi akiwa kwenye kazi za nje alipigiwa simu na Station Sajenti Gervas akimwarifu kuwa amepokea taarifa toka kwa Michael Wage kuwa kuna watu wamemtishia kwa silaha na kumwomba rushwa ya sh milioni 10 akanitaka nirudi ofisini.

Alidai kuwa siku hiyo Gervas alikuwa zamu ofisini kwake katika ofisi za RCO-Ilala na yeye akafika ofisini hapo saa nane mchana akamkuta Wage na Gervas wakampatia taarifa za malalamiko hayo kwa kirefu na kuongeza kuwa yeye alifikia uamuzi wa kuwasiliana na Mkuu wake wa kazi-RCO wa Ilala-Duwani Nyanda na kumueleza malalamiko hayo na kwamba mlalamikaji yupo ofisini kwao na kumuomba atupe utaratibu wa kulishughulikia tatizo hilo.
“RCO-Nyanda akanielekeza kwamba nifungue jalada la malalamiko na watuhumiwa wasakwe na wafikishwe kituoni.Na Wage alikuwa akilalamika kuwa kuna watu wawili wamejitambulisha kwake kuwa ni maofisa wawili wa (TAKUKURU )hakuwataja majina na mwingine akamtaja ni Jerry Murro ambaye ni mtangazaji ...na mimi nilitekeleza maagizo kwa kufungua jalada la uchunguzi;

“ Na nikamwelekeza afande Masika achukue maelezo ya Wage na nikamwomba Wage awapigie simu watu hao waliokuwa wakimtisha na kumwomba rushwa na akampigia mmoja wao ambaye alimtaja kuwa ni Murro na simu yake aliiweka kwenye Loud Speaker’ na Wage akamtaka Murro wakutane na Murro akamtaka Wage aje ofisini kwake TBC1 au Bamaga.”alidai Mkaguzi Msaidizi Chabu.

Chabu alidai hata hivyo yeye aliairisha zoezi hilo la Murro kutaka akutane na Wage ofisi za TBC1 na akamwomba RCO-Nyanda zoezi hilo la kuwamata lifanyike kesho yake ombi ambalo lilikubaliwa na mkuu wake wa kazi nakuongeza kuwa Januari 31 mwaka jana,saa nne asubuhi yeye na Wage walitoka katika ofisi za RCO-Ilala na kabla ya kutoka alimwomba Wage awapigie watu hao ili wajue wanakutana nao katika mgahawa wa City Garden.

“Wage akampigia Murro na kumweleza aje amkute katika mhagawa huo ili ampatie mzigo ambao ni sh milioni tisa na Murro akakubali na mimi nikawachukua askari wapelelezi watatu tukafanye mtego katika mgahawa huo na wapelelezi hao ni Station Sajenti Gervas, Sajenti Omary na Koplo Masawe na na tulipofika mimi nilikuwa kiongozi wao na Gervas na Masika niliweka nje ya mgahawa huo na mimi na Gervas tuliingia tuliingia na kukaa ndani ya mgahawa huo saa tano asubuhi;

“Nilipoona Murro atokeo nikamwambia Wage ampigie tena kumwarifu kwamba ameishafika na Wage akampigia huku simu yake ikiwa kwenye Loud Speaker wote tunasikia, Murro akamjibu Wage kuwa anakuja baada ya dakika tano na ndani ya muda huo Murro akafika nje ya mgahawa huo akampigia simu Wage akimtaka atoke nje ya mgahawa ili amkabidhi mzigo huo;

“Wage kabla hajatoka nje nikamkataza asitoke kwanza asubili sisi wapelelezi wawili tuko nje tukawaongezee nguvu wapelelezi wetu wawili tuliowacha nje kwaajili ya mtego, na tulivyotoka na nikamwona Murro akiwa nje ya gari lake amesimama na mimi na wale wapelelezi wenzangu tukapeana ishara zetu za Kiintelijensia na Wage ndiyo akatoka ndani ya mgahawa huo kuja nje na akakutana na Murro ambaye alikuwa akimuita kwa mkono Wage ambaye alikuwa amebeba mkoba ambapo alifungua mlango mwingine wa gari la Murro na kuingia ndani ya gari hilo.

Inspekta Chabu aliendelea kueleza kuwa baada ya Wage kuingia ndani ya gari la mshatakiwa huyo alifunga mlango haraka na kutaka kuondoka nikamweleza dereva wetu ambaye alikuwa akiendesha gari lenye namba za kiraia akaenda kulizuia gari la Murro ili lisiondoke na ndipo Murro aliposhtuka akamtaka Wage atelemke kwenye gari lake na yakazuka malumbano baina yao wawili na kutokana na hali hiyo yeye alisogea kwenye gari la mshtakiwa huyo na kumuuliza Murro kama alikuwa akimfahamu Wage, mshtakiwa huyo alikana kutomfahamu Wage.

Aidha aliieleza kuwa alimuuliza pia Wage kama alikuwa akimfahamu Murro na Wage alikiri kumfahamu mshtakiwa huyo na kusema kuwa ndiye miongoni mwa aliyemtishia kwa pisto na pingu na kumuomba rushwa y ash milioni 10 na kuongeza kuwa baada ya hapo alijitambulisha kwa Murro kuwa yeye ni ofisa wa polisi na kumweleza kuwa anakabiliwa tuhuma zinazomkabili la na kumtaka afungue gari lake ili yeye na wapelelezi wengine wapande gari lake na aliendeshe kuelekea kituo Kikuu cha Polisi Kati kwa mahojiano zaidi.

“Baada ya kumpa maelezo hayo kwanza Murro alinyamaza akasema haiwezekani kwani katika mgahawa huo yeye alifuatilia habari ya Mchina...nikapanda kiti cha mbele katika gari lake na kumtaka aendeshe gari hadi Kituo cha Kati na alitii amri hiyo na tulipofika nilimwambia afunge gari lake vizuri na anifuatwe kwenye ofisi za RCO-Ilala , tulipofika ofisini nikamuhoji kuhusu tuhuma hizo na alikana na baada ya hapo nikatoa taarifa kwa wakubwa wangu wa kazi kwamba tayari nimeishamata. Shahidi wa sita anaendelea leo kutoa ushahidi wake.
Januari 24 mwaka 2011;shahidi wa tatu ambaye alikuwa ni Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ,Michael Wage alikiri kutoa rushwa ya shilingi milioni moja baada ya kutishiwa kwa pingu na bastola.
Alidai kuwa alilazimika kutoa rushwa hiyo kwa sababu alitishwa na Murro na mshtakiwa wa pili Kapama aliyejitambulisha kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Takukuru na mshtakiwa wa tatu Deogratius Mugassa alijitambulisha kuwa ni msaidizi wa mkurugenzi huyo.

Shahidi huyo ambaye alikuwa mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kabla ya hajasimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Januari mwaka jana, alidai kuwa washtakiwa hao wote watatu Januari 31 mwaka jana, katika Hoteli ya Sea Cliff walimtaka awapatie sh milioni 10 ama sivyo wangembambikia kesi kama alivyobambikiwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, kwa kumwambukiza maradhi mpenzi wa rafiki wa Kapama ndiyo maana akabambikiziwa kesi iliyomfanya ahukumiwe kwenda jela miaka miwili.

Wage aliieleza Mahakama kuwa Januari 28 mwaka jana akiwa nyumbani kwake Bagamoyo alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa mtangazaji wa TBC1 na hakuwa hakimfahamu, akimtaka kesho yake aje Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano kwani amepata taarifa kuwa anakabiliwa na tuhuma za ufisadi katika Halmashauri ya Bagamoyo.

Katika hilo Wage alieleza kuwa alikubaliana na ombi hilo na Januari 29 mwaka jana, saa tano asubuhi alifikia katika mgahawa wa Califonia ulioko jijini hapa akiwa na dereva wake.

Alieleza kuwa akiwa njiani alimpigia simu Murro ili aje aungane naye na baada ya dakika chache Murro aliwasili katika mgahawa huo akiwa na gari ndogo na akamweleza watafute meza nyingine ili wakae mbali na dereva wake na walipohamia kwenye meza nyingine ndipo Murro alipoanza kumueleza tuhuma za ufisadi zinazomkabili na kwamba anataka kuzitangaza kwenye kipindi cha Usiku wa Habari kinachorushwa na TBC1.
“Baada ya Murro kunieleza tuhuma hizo akaniambia mahojiano kamili yangefanyika katika Hoteli ya Sea Cliff kwani huko ndiko walikokuwa mabosi wake na kunitaka nimwache dereva wangu kwenye mgahawa huo nikapande gari lake twende nae Sea Cliff na nilifanya kama alivyonielekeza nikapanda na tulipokuwa njiani akampigia simu mtu akawa anazungumza naye na akanitaja jina langu… alivyokata simu nikamuuliza ni kwa nini alikuwa akitaja jina langu akasema alikuwa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa PCCB (Kapama) naye pia atanihoji.

Wage aliendelea kueleza kuwa walipofika tu Hoteli ya Sea Cliff walipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa PCCB, anaitwa Mussa ambapo hata hivyo Wage alimtambua mtu huyo mahakamani kuwa ni Mugassa na akaongeza mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Dokta ambaye Wage jana alimtambua mahakamani kuwa ni Kapama na kuongeza kuwa baada ya hapo mahojiano yakaanza na Dokta akaanza kumueleza kuwa yeye ni fisadi mkubwa na kwamba kama alihitaji msaada wao angesema mapema ili mahojiano yao yasiweze kurushwa kwenye kipindi cha Usiku wa Habari cha TBC1.
Alisema mara baada ya kutoa taarifa hizo polisi wakamtaka ampigie simu Murro na amweleze kuwa tayari ameishafika kwenye mgahawa wa City Garden.

Wage alieleza kuwa alifanya hivyo na baada ya dakika chache Murro aliwasili kwenye mgahawa huo lakini alivyomuona Wage ameambatana na watu wengine watatu alishtuka na polisi waliwahi kuzuia gari lake lisitoke katika viwanja vya mgahawa huo na askari kanzu hao walimwamuru aendeshe gari lake na kulipeleka kituo cha polisi Kati na Murro alitii amri hiyo na wote walifika kituoni hapo.

Alisema Murro alipoulizwa kama alikuwa akimfahamu Wage alikana kumfahamu na polisi hao walipopekuwa gari la Murro walikuta bastola, pingu na miwani ya kusomea ambayo Wage alidai ni yake na aliisahau jana yake wakati alipopanda katika gari hilo wakati anapelekwa Sea Cliff.
Vitu hivyo vyote pingu, bastola na miwani ilipokelewa mahakamani hapo kama utambulisho.

Kwa upande wake wakili wa Murro, Richard Rweyongeza, na Majura Magafu, anayemtetea Kapama na Muggasa akimhoji shahidi huyo alidai kuwa shahidi huyo haoni kwamba Murro alikuwa akitangaza habari za hatari hatari za kuligusa jeshi la polisi na alikuwa akitaka kurusha tuhuma za ufisadi zinazomkabili Wage ndiyo maana alishirikiana na polisi kumbambikizia kesi mteja wake, hoja hiyo ilipingwa vikali na shahidi huyo.

Novemba 12 mwaka 2010; shahidi wa pili Kumar Aluru Pournama alitoa nakala za picha za CCTV kamera katika mtandao wa Hoteli ya Sea Cliff kama vielelezo vya ushahidi katika kesi hii zinazowaonyesha washtakiwa hao watatu pamoja na Wage ambaye wanadaiwa kumuomba rushwa,wakiwa katika eneo hilo la Hoteli ya Sea Cliff na nakala hizo za picha za CCTV zilipokelewa na mahakama kama kielelezo.

Agosti 18 mwaka 2010; shahidi wa kwanza Staff Sajenti Peter Jumamosi alidai kuwa yeye ndiye alimchukua maelezo ya onyo mshtakiwa wa tatu(Muggasa) na akaomba mahakama iyapokee maelezo hayo ya onyo kama kielelezo.
Lakini hata hivyo wakili wa mshtakiwa huyo, Majura Magafu alidai mteja wake (Mugassa) anaiomba mahakama isipokee maelezo hayo kama kielezo kwasababu Februali 3 mwaka huo ,wakati anachukuliwa maelezo hayo na mshtakiwa wa kwanza Staff Sajenti Peter Jumamosi, aliteswa na alikuwa akishinikizwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam(ZDCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo na Kamishna Kasala ambao walimtaka mshtakiwa huyo atoe maelezo yatakayomgandamiza mshtakiwa wa kwanza (Murro) ambaye jeshi la polisi limekuwa likimsaka kwa muda mrefu kwasababu amekuwa akilidhalililisha jeshi hilo kwenye vyombo vya habari..
Hali iliyosababisha Hakimu Mirumbe kutoa amri ya kusimamishwa usikilizwaji wa kesi ya msingi na akaamuru kufanyika kwa kesi ndogo (trial within a trial) ambapo ilifanyika na kila pande zikaleta mashahidi wake lakini mwisho wa siku mahakama hiyo ilitupilia mbali ombi la wakili Magafu na ikapokea maelezo hayo kama kielelezo.
Agosti 12 mwaka 2010; mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo, Deogratius Mugassa kwa mara nyingine alifikishwa mahakamani hapo kwa kesi nyingine mpya ya kujifanya ni Ofisa wa Jeshi la Polisi na kisha kujipatia shilingi milioni 19 kwa njia ya udanganyifu.,
Mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoka, Wakili wa serikali Zuberi Mkakatu alidai kuwa Mugassa anakabiliwa na mashtaka matatu.Shitaka la kwanza ni la kula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwamba mshtakiwa huyo na wenzake ambao hawapo mahakamani.

Wakili Mkakatu alidai shtaka la pili ni la Mugassa kujifanya Ofisa wa Jeshi la Polisi kwamba Aprili 28 mwaka huu, katika Bar ya Rose Garden huko Mikocheni, yeye na wenzake walijitambulisha kwa Rose Azizi kuwa wao ni maofisa wa jeshi la polisi.

Mkakatu alidai shitaka la tatu ni la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwamba kati ya Mei na Aprili mwaka huu, katika Bar hiyo ya Rose Garden walijipatia sh milioni 19 kutoka kwa Rose Azizi baada ya kujifanya wao ni maofisa wa jeshi hilo na kwamba fedha hizo walizopewa watazitumia kuweka mtego wa kuwakamata wezi walioiba matofari mawili wa madini ya dhahabu wilayani Nzega.Katika kesi hii pia alipata dhamana.
Februali 5 mwaka 2010, ndiyo siku ya kwanza washtaki
wa hao kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Gabrile Mirumbe ambapo wakili Kiongozi wa Seriakali, Stanslaus Boniface alidai Murro anakabiliwa na makosa mawili ya kula njama na kuomba rushwa ya shilingi 10 toka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamayo,Michael Karoli Wage.

Wakati Mugassa na Kapama wanakabiliwa mashtaka hayo kama yanayomkabili Murro na shtaka jingine la tatu ambalo ni la kujifanya wao ni maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), jambo ambalo si la kweli.Na kwa kipindi chote hicho washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

0716- 774494

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 30 mwaka 2011.

HUKUMU KESI YA JERRY MURRO LEO

Na Happiness Katabazi


HAKIMU Mkazi wa Mkazi ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Frank Moshi leo anatarajia kuketi kwenye kiti cha enzi na kumsomea hukumu aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa(TBC 1),Jerry Murro(30) na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya kula njama na kuomba rushwa ya shilingi milioni 10.




Kusomwa kwa hukumu hiyo leo hii kunatokana na amri iliyotolewa na Hakimu Moshi, Oktoba 31 mwaka huu mahakamani hapo ambapo siku hiyo kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa na kupangiwa tarehe ya kusomwa hukumu ya kesi hiyo ambayo inasubiriwa kwa shahuku kubwa.

Februali 5 mwaka 2010, ndiyo siku ya kwanza washtaki
wa hao kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mirumbe ambapo Wakili Kiongozi wa Serikali Stanslaus Boniface ambapo alidai Murro anakabiliwa na makosa mawili ya kula njama na kuomba rushwa ya shilingi 10 toka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamayo,Michael Karoli Wage.

Wakati Mugassa na Kapama wanakabiliwa mashtaka hayo kama yanayomkabili Murro na shtaka jingine la tatu ambalo ni la kujifanya wao ni maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), jambo ambalo si la kweli.Na kwa kipindi chote hicho washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 30 mwaka 2011.

NHC GHOROFA SIO LAZIMA ZIJENGWE UBUNGO

Na Happiness Katabazi


IELEWEKE wazi kuwa si lengo langu kupingana na baadhi ya hatua za maendeleo zinazoendelewa kupigwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), chini ya Mkurugenzi Mkuu Nehemiah Mchechu.



La hasha kwanza napongeza baadhi ya hatua za kimaendeleo zilizopigwa katika kipindi cha muda mfupi na NHC ikiwemo cha kuwaumbua adharani wadaiwa sugu, na pia mikakati yako ya kuwabana wadaiwa sugu hadi hivi sasa tunaona baadhi ya wapangaji wanaoishi kwenye nyumba hizo wameanza kufuata utaratibu wa kwenda kulipa kodi ya pango kila muda unapofika.

Na kwale wanaosikiliza Redio Clouds kikamilifu, watakuwa wameishalisikia liletangazo NHC linalovutia na kuacha maswali mengi kwa wasikilizaji ambalo limekuwa likiwataka watu wanaotaka kununua nyumba za kisasa zilizopo katikati ya mji, madhali nzuri ambazo wamezipa jina la Ubungo Residential.

Kwa mara ya kwanza niliposikiliza tango hilo ndani ya gari na wenzangu tulibaki tukijiuliza maswali yafuatayo kuwa hayo majengo yako wapi?Je yameishajengwa?yapo ubungo eneo gani ambalo mimi silifahamu?. Na ili kupata ukweli wa hilo nilimtafuta rafiki yangu mmoja anayeishi kwenye maghorofa ya Ubungo-NHC na kumuuliza kwa undani kuwa nimelisikia tango hilo je hayo majengo yapo eneo gani?

Ndiyo huyo rafiki yangu akaanza kunieleza kuwa kwanza hayo majengo hayajaanza hata kujengwa na yanajengwa katikati ya maeneo ya maegesho ya magari na njia ya wapitao kwa miguu ambayo yapo ndani maghorofa ya NHC-Ubungo.Kwakweli nilichoka kabisa na kuamua kwenda kutembelea eneo hilo.

Nilipofika nikakuta mabati yamezungushwa katika eneo hilo ambalo ni kati ya ghorofa na ghorofa za awali ambazo watu wanaishi tangu miaka ya 1970 hali inayosababisha wakazi wa maeneo hayo hivi sasa kukosa hewa ya kutosha , eneo la kuegesha magari yao na watembea kwa miguu kushindwa kupita katika eneo hilo kama zamani.

Baada ya kukutana na hali hiyo kwakweli nilijiuliza hivi kama kweli serikali inania ya dhati ya kupanua mji ni kwanini imeruhusu NHC ijenge majengo hayo katika eneo finfu kama lilele?

Kama kweli NHC imeona biashara ndiyo bora zaidi kuliko afya za watu ni kwanini isingeiomba serikali maeneo makubwa tu ikaenda kujenga nyumba zake hizo inazodai ni sasa kisasa ili watu wanaotaka kuzinunua waende kuzinunua na kwenda kuishi huko?

Ni serikali hii hii ya Rais Jakaya Kikwete ilituhadi kuwa itakuza michezo, sasa ni michezo gani inayokuza wakati maeneo ya wazi katika maghorofa ya NHC-Ubungo ambayo utumiwa na watoto wadogo kucheza michezo mbalimbali, leo hii yanachukuliwa na NHC na kubadilishwa matumuzi na matokeo yake kwasasa yanajengwa makazi ya watu?

Basi NHC kama haiyataki maghorofa yake ya zamani ya hapo Ubungo ambayo bado watu wanaishi na shirika hilo linaendelea kupokea kodi zao, ni vyema basi shirika hilo lingewataka wapangaji wake wote wanaoishi hapo waame ili maghorofa hayo yavunjwe na kisha shirika hilo ndiyo lije na ramani ya kujenga hayo majengo ya kisasa kwa nafasi zaidi?

Aiingii akilini kwa watu waliofika eneo hilo linalotaka kujengwa maghorofa hayo ambayo yanatangazwa kana kwamba tayari majengo hayo ujenzi wake umeishamalizika, kuona watu wakiendelea kuishi katika eneo hilo wakati ujenzi wa majengo hayo mapya tunayoambiwa ni ya kisasa ambayo eti yatakuwa na eneo kubwa la kuegesha magari lakini kwa watu tunaofahamu eneo hilo la maghorofa ya NHC-Ubungo tunaishia kuchekea moyoni, ukikaribia kuanza.

Tanzania bado ina maeneo mengi tu yanaitaji kuendelezwa ama na mtu mmoja mmoja, serikali yenyewe, wawekezaji au hata hilo shirika la nyumba NHC.Kwa hiyo siyo lazima NHC ijenge majengo hayo ya kisasa ndani ya eneo ya maghorofa ya NHC-Ubungo ambapo watu wanaishi na kwa ukweli kabisa maeneo yaliyosalia katika si vyema yangepaswa kujengwa maghofa mapya.

NHC achaneni na tamaa ya kupata fedha za chap chap, kama kweli NHC mmpo kwaajili ya kukikisha mnaisaidia wananchi wa taifa hili kupata nyumba za kuishi iwe kwa kuwapangisha au kujenga na kisha kuziua, ni vyema mngewasiliana na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka awapatie maeneo makubwa tu ili muweze kujenga hayo majengo ya kisasa ambayo yatakuwa na hewa zaidi ya hasili kuliko ilivyo hivi sasa maghorofa hayo mnayokusudia kuyajenga pale Ubunge, wakazi wa maghorofa hayo ya kisasa watategemea zaidi hewa ya isiyo ya halisi kwa kulazimika kutumia AC na Feni.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

0716 774494

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 29 mwaka 2011.

WAZIRI AONGEZA MUDA KESI YA MBATIA,MDEE

Na Happiness Katabazi


HATIMAYE Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani ameongeza muda wa miezi sita kuanzia jana katika kesi ya kupinga matokeo yaliyomtangaza mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee(Chadema), kuwa mshindi kama alivyokuwa ametakiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuongeza muda huo.


Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2010 iliyofunguliwa na aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya (NCCR-Mageuzi), James Mbatia anayetetewa na wakiliwa Mohamed Tibanyendera dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mdee na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kawe.

Hayo yalisemwa jana na Jaji John Utamwa jana wakati kesi hiyo ilipokuja kwaajili ya kutajwa na kuangalia kama waziri huyo tayari ameishatekeleza amri hiyo ya mahakama ya kuongeza muda wa usikilizwaji wa kesi hiyo kwasababu kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi inataka kesi yoyote ya uchaguzi iwe imemalizika ndani ya miezi 12 , na kesi hiyo ya Mbatia na Mdee anayetetewa na Edson Mbogoro muda wa miezi 12 imeishapita na bado haijamalizika.

Jaji Utamwa alisema kwakuwa tayari muda umeishaongezwa, maelezo ya awali yatasomwa mahakamani hapo Desemba 6 mwaka huu na kwamba kesi hiyo itaanza kusikilizwa rasmi kuanzia Februali 7-10 mwakani.

Novemba 25 mwaka 2010, Mbatia alifungua kesi hiyo ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo ambayo yalimtangaza Halima Mdee(CHADEMA) kuwa mshindi.

Na kwa mujibu wa hati yake ya madai, Mbatia anadai kuwa katika mikutano ya kampeni, Mdee alimwita yeye kuwa ni fataki anayefanya mapenzi na watoto wa shule, kibaraka wa CCM na kila wiki analipwa sh milioni 80 na chama hicho, hivyo kuwataka wapiga kura wa jimbo la Kawe wasimchague Mbatia.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 29 mwaka 2011.

KESI YA WANAFUNZI UDSM YAPIGWA KALENDA

Na Happiness Katabazi


UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya maandamano na kufanya mkusanyiko haramu inayowakabili wanafunzi 50 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, jana ulishindwa kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao kwasababu ya mshtakiwa mmoja kuongezwa katika kesi hiyo na mshtakiwa mmoja kushindwa kufika mahakamani hapo.



Wakili wa Serikali Ladiuslaus Komanya mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema,alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa lakini haitawezekana kwasababu wanamuongeza mshtakiwa mmoja Fred Hatari na hivyo kufanya idadi ya washtakiwa kufikia 51 hivi sasa.

Wakili Komanya alidai sababu ya pili ni mshtakiwa mmoja Said John ameshindwa kufika mahakamani hapo na kulazimika kuomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa huyo na mdhamini wake aitwe mahakamani, maombi ambayo yalikubaliwa na hakimu Lema
Hata hivyo mshtakiwa aliyeongezwa, Hatari alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na amepelekwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hakimu Lema aliarisha kesi hiyo hadi Desemba 20 mwaka huu itakapokuja kwaajili ya kutajwa na kwamba upande wa Jamhuri uje kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali Januari 10 mwakani.

Novemba 14 mwaka huu, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na wakili wa serikali Komanya alidai kuwa katika eneo la Mlimani la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walifanya mkusanyiko usio wa halali na kusababisha uvunjifu wa amani katika eneo hilo.

Na kwamba shtaka la pili ni kwamba washtakiwa hao wakiwa kwenye mkusanyiko huo haramu kwa lengo la kufanya mgomo, askari wa Jeshi la Polisi waliwataka wanafunzi hao watawanyike lakini hata hivyo wanafunzi hao walikahidi amri hiyo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 29 mwaka 2011.

MHASIBU WA TRA KORTINI KWA UDANGANYIFU

Na Happiness Katabazi


MHASIBU wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Sangu John alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jana na kusomewa mashitaka 132 akidaiwa kujipatia zaidi ya Sh milioni 944 mali ya mwajiri wake kwa njia za udanganyifu pamoja na kulipa mishahara hewa.


Mashitaka hayo aliyosomewa mbele ya Hakimu Aloyce Katemana na mawakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincon, Osward Tibabyekomya wakisaidiana na wakili wa serikali Shadrack Kimaro. Mashitaka yalikuwa ni ya kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri wake, kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kusababisha hasara kwa mamlaka hiyo Sh 944,169,330.

Shitaka la kwanza alidaiwa June 19, 2006 katika ofisi za TRA makao makuu yaliyoko wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya alighushi orodha ya malipo ya mshahara kwa mwezi huo, akionyesha wafanyakazi hewa tisa wa shirika hilo walitakiwa walipwe Sh 12,000,000 akijua si kweli.

Katika mashitaka ya kutumia nyaraka kumpotosha mkuu wake wa kazi, alidaiwa moja wapo alidaiwa June 20, 2006 ofisi za TRA akiwa mwajiriwa aliwasilisha orodha hiyo kwa mkuu wake wa kazi akidai kwamba wafanyakazi hao walitakiwa kulipwa fedha hizo huku akijua sio kweli.

Mashitaka mengine alidaiwa kwa nia ya kudanganya alijipatia kutoka benki ya NBC fedha hizo akijidai kuwalipa watu hao kwa mshahara wa mwezi June 2006.
Katika mashitaka mengine alidaiwa kudai malipo hayo hewa miezi mingine kuanzia June 2006 hadi Augost 2009.

Mashitaka mengine John alidaiwa alighushi nyaraka kuonyesha mishahara ya wafanyakazi wa TRA mwezi Novemba ni Sh 2,207,122,430 akijua sio kweli, alidaiwa kuendelea kumdanganya mwajiri wake katika miezi mingine katika kipindi hicho akionyesha mishahara tofauti na iliyokuwa ikistahili wafanyakazi wa TRA kwa mwezi.

Aidha mshitakiwa huyo alishitakiwa pia kwa kufanya mchezo huo aliisababishia hasara mamlaka ya Mapato Tanzania ambayo ndio ilikuwa mwajiri wake Sh 944,169,330.

John alikana mashitaka yote na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kutoa nusu ya fedha hiyo ambayo ni Sh 472,084,665. Kesi hiyo imepangwa kutajwa Desemba 5 mwaka huu na upelelezi haujakamilika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Novemba 24 mwaka 2011.

DAVID MATTAKA KIZIMBANI




Na Happiness Katabazi


ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATLC), David Emmanuel Mattaka jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na makosa matatu likiwemo kosa la matumizi mabaya ya madaraka kinyume na Sheria na kifungu 31 Na.11 ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007.


Mbali na Mattaka anayetetewa na wakili wa kujitegemea Peter Swai, washtakiwa wengine ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Elisaph Mathew Ikomba na Mkazi Mkuu wa Mahesabu ya Ndani, William Haji anayetetewa na wakili Alex Mgongolwa walifikishwa mahakamani hapo jana saa nne asubuhi na makachero wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa(TAKUKURU), chini ya ulinzi mkali wa makachero hao.

Wakili wa Takukuru, Ben Lincoln aliyekuwa akisaidiwa na wakili wa serikali Oswald Tibabyekomya mbele ya Hakimu Mkazi Ritha Tarimo aliyasoma mashtaka hayo
Kuwa ni kosa la kwanza ambalo linawahusu washtakiwa wote ni kwamba washtakiwa wote kwa pamoja walishindwa kutunza kumbukumbu za mawasiliano ya manunuzi waliyokuwa wakifanya na mtoa huduma kinyume na kifungu cha 55(3),87(1)(f) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 21 ya mwaka 2004 na kanuni ya 17(1) ya Sheria ya Manunuzi (Goods,Works,Non-Consultant Services and Disposal of Public Asets by Tender) Regulation,G.N. No.97 of 2005.

Wakili Lincoln alidai shtaka la pili ambalo pia linawakabili washtakiwa wote ni la kushindwa kutimiza matakwa ya vifungu vya Sheria ya Manunuzi ya Umma na Kanuni zake kinyume na kifungu cha 87(1)(f) cha Sheria ya Manunuzi ya umma ya mwaka 2004.
Na shtaka la tatu lina mkabili Mattaka peke yake ni matumuzi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa ya mwaka 2007.

Lincoln alidai kuwa maelezo ya shtaka la kwanza kuwa Juni 2007 na JUlai 2007 ndani ya jiji la Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja kupitia nafasi zao wote kwa pamoja walishindwa kutunza rekodi ya tangazo la tenda idadi ya magari 26 waliyoyanunua ambapo magari hayo yalinunuliwa na shirika hilo yakiwa tayari yamekwishatumika(magari mitumba) kutoka kwa kampuni ya Bin Dalmouk Motors Co.Ltd yenye ofisi zake nchini Dubai katika Falme za Kiarabu, kampuni ambayo ilipewa tenda shirika hilo kuleta magari hayo 26 ambayo ni mitumba.

Wakili Lincoln alidai kuhusu shtaka la pili ambalo ni la kushindwa kutimiza masharti ya sheria hiyo ya Manunuzi ya mwaka 2004 kuwa kati ya Julai 2-Agosti 23 mwaka 2007 wote kwa walishindwa kutimiza matakwa ya kifungu cha 87(1)(f) cha Sheria ya manunuzi ya umma na Kanuni ya 58(3) sheria hiyo kwa kutumia kampuni ya umma ya ATLC walinunua magari ya mitumba 26 toka kwa kampuni ya Bin Dalmouk Motors Co.Ltd ya Dubai kinyume na kifungu hicho ambacho kinakataza ofisi yoyote ya serikali kununua bidhaa ambazo zilizokwishatumia.

Wakili Lincoln alidai shtaka la tatu la matumizi mabaya ya madaraka linalomkabili Mattaka peke yake ambaye amestaafu hivi karibuni utumishi wa umma, alitumia madaraka yake vibaya kwa makusudi na kuagiza magari hayo ya mitumba 26 huku akijua kufanya hivyo ni kwenda kinyume na vifungu hivyo vya sheria ya manunuzi.

Hata hivyo washtakiwa wote walikana mashtaka hayo na wakili wa serikali Tibabyekomya alidai kuwa upelelezi bado unaendelea na kwamba makosa yanayowakabili washtakiwa yanadhaminika na hivyo akaiomba mahakama iwapatie dhamana washtakiwa kwa kutumia kifungu cha 148(5)(e) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002,ambayo yanamtaka mshtakiwa atoe mahakamani nusu ya fedha taslimu au hati ya mali isiyoamishika yenye thamani ya nusu ya kiwango anachotuhumiwa kuiba, kuharibu au kusababisha hasara.

Hata hivyo hoja hiyo ilipingwa vikali na mawakili wa utetezi Peter Swai na Alex Mgongolwa ambao walidai kimsingi mashtaka yanayowakabili wateja hao si ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma, kusababisha hasara wala wizi hivyo kamwe dhamana ya washtakiwa hao haiwezi kuangukia chini ya kifungu hicho na kuiomba mahakama ikatae hoja hiyo ya mawakili wa jamhuri.

Akitoa uamuzi wake Hakimu Tarimo alisema anakubaliana na hoja ya mawakili wa utetezi kuwa mashtaka yanayowakabili washtakiwa hayo hayahusiani na fedha, kusababisha hasara, wizi wala uharibu wa mali ya umma.

“Hivyo masharti yangu ya dhamana ni haya hapa kuwa ili kila mshtakiwa apate dhamana ni lazima awe na wadhamini wawili wa kuaminika ambapo kila mdhamini atapaswa asaini bondi ya milioni 10 kila mmoja na kwa anaiarisha kesi hiyo hadi Desemba 5 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa”alisema Hakimu Tarimo.

Washtakiwa wote walitimiza masharti ya dhamana ambapo Mattaka alitolewa ndani ya chumba hicho cha mahakama kwa kasi huku akisindikizwa na ndugu zake na maaskari na kisha kuondoka ndani ya eneo hilo la mahakama.
Hivi karibuni Mattaka alistaafu kwa mujibu wa sheria utumishi wa umma akiwa na cheo cha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ndege nchini.

Rais Jakaya Kikwete alipochaguliwa kuwa rais wa Tanzania Desemba 21 mwaka 2005 muda mchache baadaye alimteua Mattaka kuwa mkurugenzi wa shirika hilo la ATCL na kisha baadaye kumteua Mattaka kuwa Mjumbe wa Tume ya Rais ya Kikosi Kazi cha Kurekebisha Shirika la Bima la Taifa.

Wakati Rais Kikwete akimteua Mattaka kushika nyadhifa hizo katika kipindi cha Serikali ya awamu ya nne, wananchi mbalimbali walilaani uteuzi huo bila mafanikio.

Na kabla ya Rais Kikwete kumteua Mattaka kushika nyadhifa hizo,Rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alikuwa amemstaafisha Mattaka kwa manufaa ya umma.Na wakati Mkapa anamstaafisha mshtakiwa huyo kwa manufa ya umma alikuwa akishikilia cheo cha Ukurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa Mashirika ya Umma(PPF).

Chanzo:Gazeti la Tanzania Jumatano, Novemba 23 mwaka 2011.

LEMA USITUNYIME UHURU WANAHABARI




Na Happiness Katabazi

INASHANGAZA kuona uandishi wa habari za mahakamani licha ya kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu kesi za wananchi na viongozi, mchango wake bado haujatambuliwa.

Nadiriki kusema hivyo kutokana na kitendo kilichofanywa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Waliarwande Lema, Novemba 14 na 16 mwaka huu.

Nasema jamii na serikali haina budi kuthamini mchango wetu waandishi wa habari za mahakamani kwani tukiamua kuziripoti kesi hizo mara moja tu wakati zinafunguliwa mahakamani na kisha tukaacha kuripoti mwendelezo wake, matokeo yake si serikali, wakuu wa vyombo vya habari wala jamii watakao kuwa wakifahamu kesi hizo zimefikia hatua gani.

Lakini kwa uzalendo wetu na kwa kupenda kuripoti habari za mahakamani tumekuwa tukiziripoti kesi hizo mwanzo - mwisho na tunauhakikishia umma wa Watanzania kuwa tutaendelea kuziripoti kesi hizo bila kuchoka.

Novemba 14 mwaka huu, wanafunzi 50 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), walifikishwa mahakamani hapo wakidaiwa kutenda makosa mawili ya kufanya mkusanyiko haramu Novemba 11, na kosa la pili ni kukaidi amri ya Jeshi la Polisi lililowataka wanafunzi hao kutawanyika.

Siku zote hizo mbili kesi hiyo ilipokuja kwa mara ya kwanza kwa ajili ya washitakiwa kusomewa mashitaka, waandishi wa habari tuliingia ndani ya chumba cha mahakama kwa ajili ya kuanza kusikiliza kesi hiyo lakini ghafla Hakimu Lema aliwatimua waandishi ambao tulitii amri yake tukatoka nje na kesi ilipokwisha tulitumia mbinu zetu za kujua kilichoeendelea ndani ya chumba hicho.

Kesho yake tukaenda kuiripoti kesi hiyo kwenye vyombo vya habari bila kukosea.

Aidha, Novemba 16 katika hali isiyotarajiwa Hakimu Lema aliendeleza kasumba yake ya kutufukuza waandishi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya wanachuo hao 41 kuja kupata masharti ya dhamana.

Kweli tuliitii amri yake na kutoka nje na kwakuwa tuliona hakimu huyo hakututendea haki kwakuwa kesi hiyo ilikuwa ikiwahusu watu waliozidi miaka 18, si kesi ya kulawiti wala kubakwa, tuliamua kwenda kumripoti kwa mkuu wake wa kazi, Hakimu Elvin Mugeta, ambaye alitupokea na kututaka tuwe na subira na kwamba atakwenda kuzungumza na Hakimu Lema kujua ni kwanini alifikia uamuzi huo wa kutufukuza.

Na wakati Lema akitufukuza tusiingie kwenye chumba alichokuwa akiendeshea kesi, wanausalama mbalimbali wanaoshinda mahakamani hapo walikuwa wakijitahidi kadiri ya uwezo wao kuwasaidia waandishi wa habari kuingia ndani ya chumba hicho ili waweze kusikiliza kesi hiyo bila mafanikio.

Si siri, kitendo alichotufanyia Hakimu Lema si tu kinanyima haki ya waandishi wa habari kupata habari, pia kilitudhalilisha waandishi wa habari tuliokuwa tumefika hapo kwa ajili ya kuripoti habari hiyo na nyingine.

Pia kitendo hicho kimeibua maswali mengi yasiyo na majibu kuwa hakimu huyo ana nini anachotaka kukificha katika kesi hiyo?

Au Hakimu Lema alidhani sisi ni wafuasi wa kikundi cha wanamgambo wa Kisomali cha Al - Shabaab tuliobeba mabomu kwenye pochi zetu kwenda kumlipua?

Tumuulize Hakimu Lema ana masilahi gani binafsi katika kesi hiyo hadi atuzuie kuripoti kesi hiyo?

Kwa upande wa pili wa shilingi, binafsi namuona Hakimu Lema ni miongoni mwa mahakimu wanawake wachache wenye uzoefu wa kazi hiyo na wanaojiamini katika kutoa maamuzi yao ukilinganisha na baadhi ya mahakimu wengine wanawake ambao si jasiri.

Na katika hili nampongeza Hakimu Lema, kwani kupitia kesi mbalimbali anazoziendesha ambazo mimi nimekuwa nikihudhuria, nimeweza kulibaini hilo.

Hivyo basi, ni rai yangu kwa Hakimu Lema atambue kuwa tunaheshimu uhuru wa mahakama na utawala wa sheria na tunakuza utawala wa sheria kupitia uandishi wetu wa habari hizo za mahakamani na tunafahamu vema miiko na mipaka ya taaluma yetu.

Tunamwakikishia Hakimu Lema kuwa tutaendelea kuiripoti kesi hiyo ya wanafunzi wa UDSM na nyingine kwa njia tunazozijua sisi, hata kama atatuzia kuripoti kesi hiyo.

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 22 mwaka 2011.

WASHTAKIWA KESI YA 'SAMAKI WA MAGUFULI'WAMALIZA KUJITETEA

Na Happiness Katabazi


HATIMAYE washtakiwa watano raia wa China wanaokabiliwa na kesi ya uvuvi haramu katika ukanda wa Tanzania kwa kutumia meli ya Tawariq 1 maarufu kama ‘Kesi ya Samaki wa Magufuli’ wamemaliza kujitetea katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Washtakiwa hao Hsu Chin Tai, Zhao Hanguing, Hsu Shang Pao, Ca’ Dong Li na Chen Rui Hai wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Ibrahim Bendera na John
Mbele mbele ya Jaji Agustine Mwarija.

Novemba 14, mwaka huu, washtakiwa hao walijitetea kwa lugha ya Kichina na kusaidiwa na mkalimani Mtanzania; walisema: “Mheshimiwa Jaji wateja wetu hao watano wamemaliza kujitetea na tumeona utetezi wao unatosha hivyo hatuhitaji kuleta mashahidi ili waje kuwatetea na kwa hiyo upande wa utetezi katika kesi hii tumefunga ushahidi wetu na tunaiachia mahakama iendelee na taratibu zingine za kisheria,” alisema Wakili Bendera.

Kwa upande wake Jaji Mwarija alikubaliana na ombi hilo na akaahirisha kesi hiyo hadi Novemba 29 ambapo siku hiyo pande zote katika kesi hiyo, ule wa jamhuri unaowakilishwa na wakili mwandamizi wa serikali Biswalo Mganga na wa utetezi unaowakilishwa na mawakili tajwa hapo juu, zinatakiwa kufika mahakamani hapo na kuwasilisha majumuisho yao kwa njia ya mdomo.

Machi 2009 washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kisha kesi hiyo ikahamishiwa Mahakama Kuu wakikabiliwa na makosa ya kuvua samaki bila leseni, kuharibu mazingira katika kina kirefu cha ukanda wa Bahari ya Hindi eneo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 22 mwaka 2011.

ADAM MBOGO 'NYENGO"APATA JIKO


Mdau Adam Mbogoro'NYENGO"akiwa tafakari mpya baada ya kupata mke Matrida mwishoni mwa wiki na kufuatiwa na tafrija la kukata na shoka katika ukumbi wa Land Mark jijini Dar es Salaam.
Nawatakieni furaha na uvumilivu katika safari yenu mpya ya maisha ya ndoa mliyoianza na mungu awatangulie.

SHAHIDI:MINTANGA HAKUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA



Na Happiness Katabazi


SHAHIDI wa nne upande wa Jamhuri katika kesi ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya Kilo 4.8 inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Ngumi la Ridhaa Tanzania (BFT), Alhaji Shaban Mintanga, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Charles Ulaya amedai mshtakiwa huyo alistahili kushtakiwa kwa kosa moja tu la kula njama na siyo kosa la kusafirisha dawa hizo.

SSP Ulaya, ambaye ndiye mpelelezi mkuu wa kesi hiyo na aliyeongoza askari wenzake kupekua makazi na ofisi mbili za mshtakiwa (Mintanga), alitoa maelezo hayo jana mbele ya Jaji Dk. Fauz Twaib wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakati akijibu swali la wakili kiongozi wa utetezi Jerome Msemwa anasaidiwa na Majura Magafu na Yassin Membar.

Swali hilo lilimtaka shahidi huyo, aieleze mahakama kama, kutokana na upelelezi wake aliyoufanya na vielelezo alivyovikusanya, alikuwa anaona Mintanga anastahili kushtakiwa kwa makosa mawili ya kula njama na kusafirisha kiasi hicho cha dawa za kulevya.

“Mtukufu Jaji na mimi ndiyo mpelelezi mkuu wa kesi hii na mimi ndiyo niliyemhoji mshtakiwa na nikaongoza askari wengine kufanya upekuzi. Mimi na askari mwenzangu mmoja, tulikwenda hadi nchini Mauritius kufanya upelelezi wa kesi hii na kuwahoji wale Watanzania sita, ambao ulikuwa ni msafara wa mabondia wa hapa Tanzania waliokwenda Mauritius kushiriki mashindano ya ngumi za ridhaa na nilivyowahoji hao Watanzania sita na mwanamke mmoja raia wa Kenya, walinieleza kuwa dawa zile hawakupewa na Mintanga, bali dawa zile walipewa na mtu mmoja ambaye anaitwa Mika, ambaye hadi sasa Jeshi la polisi halijafanikiwa kumkamata.

“Hivyo basi, kwa vielelezo vyote na ushahidi wote niliyoukusanya hapa Tanzania na kule Mauritius, nasema wazi kuwa mshtakiwa hakustahili kabisa kushtakiwa kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya, badala yake mawakili wa serikali walipaswa kumshtaki mshtakiwa huyo kwa kosa moja la tu la kula njama,” alieleza SSP Ulaya na kusababisha watu kuangua vicheko vya chini chini mahakamani.

Aidha, SSP Ulaya alieleza kuwa, kimsingi kilichofanya mshtakiwa huyo afikishwe mahakamani ni simu yake yenye namba 0754 284887, kuonekana ilikuwa ikitumika kuwasiliana na kampuni ya usafirishaji ya Antelops Tours Agency kwa ajili ya kuwakatia tiketi mashabiki watatu, ambao nao waliongozana na msafara huo uliokamatwa nchini Mauritius. Lakini hata hivyo alivyotakiwa na mawakili wa utetezi kutoa kielelezo hicho kinachoonyesha simu hiyo ilikuwa ikiwasiliana na kampuni hiyo ya ukatishaji tiketi, shahidi huyo alidai kuwa, yeye katika upelelezi wake alikwenda katika kampuni ya simu ya Vodacom, akapewa kielelezo hicho (print out) na kwamba, alishakikabidhi kwa mawakili wa serikali, lakini hadi shahidi huyo anamaliza kutoa ushahidi wake, hakuweza kukitoa ili kiweze kupokelewa na mahakama.

Shahidi huyo akijibu maswali aliyoulizwa kwa mpigo na mawakili wa utetezi, Msemwa na Magafu, kuwa katika maelezo ya nyongeza aliyomchukua Mintanga katika mahojiano yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, eneo la Kilwa Road jijini Dar es Salaam, Juni 20 mwaka 2008, kuwa, alimhoji mshtakiwa huyo kuhusu matumizi ya simu ya mkononi Na. 0754 284887 inayodaiwa kuwa ni ya mshtakiwa na alikuwa akiitumia kwa mawasiliano na kampuni Antelope Tours Agency, shahidi huyo alidai hakuwahi kumuuliza swali hilo mshtakiwa huyo.

Yafuatayo ni mahojiano baina ya mawakili wa utetezi Msemwa na Magafu na SSP Ulaya:

Wakili:
Tazama haya maelezo ya mshtakiwa aliyoyatoa mbele yako wakati unamhoji, kuna sehemu yoyote inaonyesha wewe ulimuuliza mshtakiwa matumuzi ya hiyo simu ambayo mnadai ni yake, alikuwa anaitumiaje?

SSP Ulaya: Hakuna sehemu inayoonyesha kuwa nilimuuliza swali hilo.

Wakili: Soma haya maelezo yako wewe shahidi, kuna sehemu yanaonyesha ulimhoji mshtakiwa kuhusu matumuzi ya namba hiyo ya simu?

SSP Ulaya: Mhhh! pia sikumuuliza swali hilo.

Wakili: Utakubaliana na mimi hiyo simu namba 0754 284887 unayodai ni ya mshtakiwa siyo mali ya mshtakiwa, bali ni simu ya ofisini kwa mshtakiwa?

SSP Ulaya: Mimi nilivyokuwa nikimchukua maelezo ya nyongeza, mshtakiwa huyo alinieleza simu hiyo ni yake.

Wakili: Soma hii ni Barua ya BFT inakwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa?

SSP Ulaya:Juu ya barua hiyo inaonyesha anwani ya BFT ni Box-15558 namba binafsi ya Mintanga ni 0773-257547, kazi na ofisi ni +255 0754-284887 .

Wakili:Kwa mujibu wa hizo nyaraka, si zinaonyesha simu hiyo ya Vodacom +255 0754-284887 si ni ya ofisini kwa Mintanga?

SSP Ulaya: Ndiyo (watu wakacheka).
Wakili:Ulivyooenda katika kampuni ile ya Antelope kufanya upelelezi wako, ulimhoji nani?

SSP Ulaya:Nilimhoji shahidi wa tatu, Godfrey Mroso na akaniambia namba hiyo ndiyo alikuwa akiwasiliana nayo na ikamtaka awakatie watu hao watatu, licha mwenye namba hiyo hajawahi kumtajia jina lake.

Wakili:Kama hivyo ndivyo, wewe ulisema kigezo pekee kilichokufanya upendekeze mshtakiwa afunguliwe kesi ni simu hiyo?

SSP Ulaya:Ndiyo, kwani nilikwenda hadi Vodacom nikaprint out mawasiliano ya namba hiyo.

Wakili: Hiyo print out umekuja nayo hapa mahakamani ili tuione?
SSP Ulaya:Sijaja nayo ila nakumbuka niliikabidhi kwa mawakili wa serikali.

Wakili:Utakubaliana na mimi hadi sasa hizo dawa za kulevya zilizokamatwa Maurtius hazijaletwa hapa nchini na kesi inayomkabili mshtakiwa ni kula njama na kusafirisha dawa hizo za kulevya Kg.4.8, na hatuoni kuwa hapa tunazungumzia hewa na kucheza mchezo wa kuigiza, kwani kielelezo ni dawa za kulevya na wewe kama mpelelezi mkuu pia hizo dawa za kulevya leo hujazileta hapa mahakamani kama kielelezo?

SSP Ulaya: Mmh! siwezi kusema hii ni kesi hewa na ninavyofahamu mimi hizo dawa bado hazijaletwa nchini.

Wakili:Katika upelelezi wenu, mliweza kubaini katika kipindi hicho cha mgogoro huo kama mshtakiwa aliwahi kwenda nchini Mauritius?

SSP Ulaya:Hatujagundua kama Mintanga aliwahi kwenda Mauritius.
Wakili:Huu uzito wa Kg. 6 wa dawa za kulevya uliupata?

SSP Ulaya: Mauritius ambapo walipowakamata Watanzania wale walilitumia jeshi la Polisi Tanzania kuwa, dawa za kulevya zenye Kg. 6.

Wakili:Unamfahamu mtu mmoja anaitwa Christopher Shekiondo?

SSP Ulaya: Namfahamu, huyo ni Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, ambaye yeye alitoa hati yake inayoonyesha dawa hizo zina uzito wa Kg.4.8 na zina thamani ya sh. milioni 120 na hati inaonyesha ilitolewa na Kamishna huyo Julai 6, 2010.

Wakili:Utakubaliana na mimi kuwa, Kamishna Shekiondo aliyapima madawa hayo na kutoa uzito na thamani ya dawa hizo wakati dawa hizo hazijaletwa bado nchini?

SSP Ulaya: Ndiyo.

Wakili: Huoni kitendo hicho cha Shekiondo kupima dawa hizo wakati dawa hizo bado haziletwa hapa nchini, ndiyo kumemsababisha mshtakiwa afunguliwe kesi hii na hadi sasa anaendelea kusota gerezani?

SSP Ulaya:Kimya.

Wakili:Hivi hizo kilo 6 za dawa hizo ambazo jeshi la polisi la Tanzania lililetewa kwa maandishi na serikali ya Mauritius zinafanana na kilo 4.8 zilizotajwa katika hati ya Shekiondo?

SSP Ulaya:Ni tofauti.

Wakili: Inakuwaje hati ya mashtaka inasomeka mshtakiwa alisafirisha Kg.4.8 kwenda Mauritius na taarifa za kipelelezi za Mauritius walizolitumia jeshi letu la polisi, zinaonyesha waliukamata msafara ule ukiwa na kg. 6 za dawa za kulevya, sasa ieleze mahakama usahihi ni upi?

SSP Ulaya:Kimya.

Wakili: Kwa hiyo utakubaliana na mimi tuhuma kuhusu usafirishaji wa dawa hizo zilikuwa zinamhusu Mika na siyo Mintanga?

SSP Ulaya:Ni kweli, kwani tulipata taarifa hizo toka Mauritius na ndiyo maana tukawa tunamtafuta sana Mika, kwani Petro Mtagwa, Elia Nathaniel, Ally Msengwa na Emilian Patrick ndiyo waliokamatwa na dawa hizo wakiwa wamemeza tumboni na mimi nilipowafuata katika gereza moja nchini humo na kuwahoji, walinieleza kuwa aliyewapatia dawa hizo ni mtu mmoja anaitwa Mika na aliwamezesha dawa hizo katika hoteli moja iliyopo Manzese na aliwapatia dola 100 za kimarekani kwa kila mmoja na Agosti 10 mwaka 2008, walianza safari kuelekea Maurtius wakiwa wamememeza tumboni dawa hizo.

Yafuatayo ni mahojiano baina ya wazee wa baraza na SSP Ulaya:

Swali:Kuna ushahidi gani katika upekuzi unahusiana na makosa yanayomkabili mshtakiwa?
SSP Ulaya: Hakuna.

Swali:Ulisema ulivyofika Mauritius wale Watanzania waliokamatwa walikuambia ni Mika ndiyo aliyekuwa amewapatia zile dawa za kulevya, sasa kwanini Jamhuri inamfungulia kesi hii Mintanga peke yake?
SSP Ulaya:Kimya.

Swali:Una uhakika gani kama mshtakiwa hausiki katika kesi hii?
SSP Ulaya: Naamini ushahidi niliyotoa na upelelezi niliyofanya, mshtakiwa anahusika katika kesi hii kwenye kosa moja tu la kula njama.

Swali:Kwani wale Watanzania waliokamatwa kule Mauritius ulivyowahoji, walikueleza kuwa Mintanga ana husika kusafirisha dawa zile za kulevya walizokutwa nazo?
SSP Ulaya:Walinieleza kuwa Mintanga hausiki kabisa na dawa hizo.

Jaji Dk.Fauz Twaib aliarisha kesi hiyo hadi leo, ambako shahidi wa tano anatarajiwa kupanda kizimbani kutoa ushahidi wake.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Novemba 18 mwaka 2011.

SHAHIDI:SIMU YA MINTANGA ILITUMIKA



Na Happiness Katabazi


HATIMAYE Mahakama Kuu Dar es Salaam jana ilizipokea tiketi tatu za ndege kama vielelezo vya upande wa Jamhuri katika kesi hiyo ambazo tiketi hizo zilitumiwa na msafara wa Timu ya Taifa ya Ngumi, ambao ulitiwa mbaroni nchini Mauritius kwa tuhuma za kuingiza dawa za kulevya zenye uzito wa Kg.4.8 nchini humo.


Jaji Dk.Fauz Twaib alisema anazipokea tiketi hizo kama vilelezo kwasababu vimekidhi matakwa ya kisheria na uamuzi alioutoa juzi ambao ulikataa kuzipokea tiketi hizo kama vielelezo hadi upande wa jamhuri utakapokwenda kuzifanyia marekebisho tiketi hizo ambazo zilikuwa ni nakala na kisha jana wazirejeshe mahakamani hapo, amari ambayo ilitekelezwa na mawakili wa upande wa Jamhuri.

Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani hap na hivyo vielelezo vilivyopokelewa jana na Jaji Dk.Twaibu, kunaonyesha kuwa aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania Alhaji Shabani Mintanga ambaye ndiye mshtakiwa pekee katika kesi hiyo kuwa ndiye aliyehusika kuwatafutaia tiketi watu waliokutwa na dawa hizo huko Mauritius ambao hata hivyo hawajashtakiwa katika Mahakama za Tanzania.

Tiketi hizo tatu zilitolewa jana na shahidi wa tatu, Godrey Mroso ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Anvelope Travel Agency, ambaye alidai yeye ndiye aliyekatisha tiketi hizo mwaka 2008 ambapo tiketi hizo zilikuwa ni za Nathaniel, Msengwa na Mutagwa.

Nathaniel na Msengwa waliambatana na timu hiyo nchini Mauritius kwa madai kuwa ni mashahabiki ambao kwa mujibu wa ushahidi walitambulishwa kwa kocha wa timu hiyo Nassoro Michael Irenge na Mintanga.


Akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili wa Serikali Ntuli Mwakahesya, Mroso aliitaja namba ya simu ya kiganjani aliyokuwa akipigiwa na mtu aliyekwenda ofisini kwao kufanya maandalizi na kulipia tiketi hizo nne kwa ajili ya safari hiyo kuwa ni 0754 284887.

Hata hivyo wazee wa baraza Wazee wa Baraza, Zeshta Lyimo na Msakala Tambaza walipomuuliza shahidi huyo swali kuwa mtu ambaye alikwenda kukata tiketi hizo kama alijitambulisha jina, shahidi huyo alijibu kuwa mtu huyo hakujitambulisha jina na hawezi kumtambua kwa sura.

Lakini kwa mujibu wa ushahidi uliokwisha tolewa na shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ambaye alikuwa ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi la Taifa, Christopher Mtabarukwa,mapema Jumatatu wiki alieleza mahakama hiyo kuwa mwenye namba hiyo ya hi namba hiyo 0754 284887 ni mshtakiwa Mintanga.

Mutaburukwa alidai kuwa alikuwa akiwasiliana na rais wake (Mintanga) kwa kutumia simu hiyo kuhusu maendeleo ya kambi ya timu hiyo wakati ikiwa kambini.
Irenge na bondia Patrick Emilian pia walikuwa wameshikiliwa nchini Mauritius kwa tuhuma hizo lakini wao wameshaachiwa baada ya kuonekana kuwa hawahusiki na uingizaji wa dawa hizo nchino humo, lakini Bondia Mutagwa, Nathaniel na Msengwa bado wanashikiliwa nchini humo.

Akitoa ushahidi wake juzi shahidi wa pili upande wa mashtaka kocha wa zamani wa timu hiyo ya ngumi Nassoro Michael Irenge alidai kuwa dawa hizo za kulevya anazoshtakiwa nazo Mintanga zilikutwa kwenye begi la Bondia Petro Mutagwa.

Irenge aliieleza mahakama kuwa katika msafara wa timu hiyo ulikuwa na mabondia wawili Patrick na Mutagwa na yeye kocha na kwamba ndio wlaioagwa.

Hata hivyo alidai kuwa baada ya kuagwa aliambiwa na Mintanga kuwa kuna watu wengine ambao ndio waliomdhamni bondia Mutagwa tiketi ya kusafiri, pia watakuwa nao katika msafara huo.

Alidai kuwa walipofika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, alikutana na watu wengine aliowataja kwa majina ya Nathaniel na Msengwa ambao walijitambulisha kuwa ni mashahabiki.

Alidai kuwa wakiwa katika hoteli waliyofikia Mauritius, siku ya pili akiwa chumbani kwake na mabondia wake waliingia askari wa Mauritius wakiwa na wale mashahabiki pamoja na begi lilioandikwa Tanzania likiwa na jina la Petro Mutagwa.
Alidai askari wale waliwaweka chini ya ulinzi kwa tuhuma za kukutwa na dawa zaa kulevya ambazo walizitoa kwenye begi lile na kuzimwaga chini.

Irenge aliendelea kudai kuwa Mutagwa alikubali kuwa begi lile ni lake na kwamba liliazimwa na mmoja wa wale mashahabiki kuwa kuna vitu alikuwa anakwenda kuvinunua.Kesi hiyo inaendelea tena leo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Novemba 17 mwaka 2011.

HAKIMU AZUIA WAANDISHI KURIPOTI KESI YA WANAFUNZI WA UDSM

Na Happiness Katabazi



HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Waliarwande Lema kwa mara ya pili jana aliendelea tabia yake kwa kuwazuia waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali vya wasiingie kusikiliza kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali inayowakabili wanafunzi 50 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Kesi hiyo ambayo jana ilikuja kwaajili wanafunzi 41 kati ya 50 kuja kupatiwa dhamana na hakimu huyo, ambapo waandishi hao wa habari walifika mahakamani hapo tangu saa mbili asubuhi na kuhudhuria kesi mbalimbali lakini ilipofika saa 6.30 mchana wanafunzi hao waliingizwa kwenye ofisi ya hakimu Lema kwaajili ya kuanza kutimiza masharti ya dhamana.

Wakati wanafunzi hao wakiongozwa na askari wa Jeshi la Magereza na Polisi kuingia ndani ya chumba hivyo, pia askari polisi walikuwa wakiwasaidia waandishi wa habari ili waweze kuingia ndani ya chumba hicho ili waweze kusikiliza kesi hiyo lakini ghafla hakimu Lema alipoona sura za waandishi wa habari akatoa sauti ya ukali na ya juu ya kuwafukuza waandishi wa habari wa habari watoke ndani ya chumba hicho bila kutoa sababu zozote.

“Nimesema nyie waandishi wa habari tokeni haraka ndani ya ofisi yangu, na hii ni amri nataka mtoke upesi ili nianze kuendesha kesi hii ya wanafunzi wa Chuo Kikuu”alifoka Hakimu Lema kwa sauti ya juu na kuwafanya waandishi wa habari akiwemo mwandishi wa habari hii kuondoka ndani ya chumba hicho bila kujua kesi hiyo iliendeleaje.

Hata hivyo waandishi hao wa habari za mahakama walionyesha kukerwa na tabia hiyo ya Hakimu Lema ya kuwazuia kuripoti kesi hiyo kwa mara ya pili sasa hali iliyowazimu kwenda kwa kushtaki kwa Hakimu Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Elvin Mugeta ambaye aliwaomba waandishi wa habari kuwa wapole na akaidi hilo swala kulifuatili ili kujua ni sababu gani iliyosababisha hakimu huyo kufia uamuzi huo wa kuwakataza waandishi wasiingie kusikiliza kesi hiyo.

Mara ya kwanza hakimu huyo kuwatimua waandishi wa habari kuripoti kesi hiyo ni Novemba 14 mwaka huu,wanafunzi hao 50 walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza mbele ya hakimu huyo na kusomewa mashtaka mawili kwamba Novemba 11 mwaka huu,katika eneo la Mlimani la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walifanya mkusanyiko usio wa halali na kusababisha uvunjifu wa amani katika eneo hilo.

Wakili Komanya alidai kosa la pili ni kwamba washtakiwa hao wakiwa kwenye mkusanyiko huo haramu kwa lengo la kufanya mgomo, askari wa Jeshi la Polisi waliwataka wanafunzi hao watawanyike lakini hata hivyo wanafunzi hao walikahidi amri hiyo na kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Novemba 17 mwaka 2011.

MARANDA AFUNGULIWA KESI MPYA YA EPA



Na Happiness Katabazi


KADA wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda jana alifikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na kesi mpya ya kugushi na kujipatia ingizo la jumla ya Sh bilioni 5.9 toka Benki Kuu ya Tanzania, mali ya benki hiyo kinyume cha sheria.


Maranda na mpwa wake Farijala Hussein ambao kwa sasa wanatumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kutiwa hatiani na mahakama hiyo Mei mwaka huu, kwa makosa ya kughushi na kujipatia ingizo la shilingi bilioni 1.8 toka katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), na hadi sasa anakabiliwa na kesi tano za aina hiyo katika mahakama hiyo ambazo bado hazijatolewa hukumu.

Wakili Mwandamizi wa serikali Fredrick Manyanda mbele ya Hakimu Mkazi Alocye Katemana, alidai kesi hiyo kwa sasa itakuwa na jumla ya washtakiwa watano ambapo washtakiwa wapya ni Maranda,aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Idara ya Madeni ya Nje(EPA), Ester Komu na Kaimu Katibu BoT, Bosco Kimela na wafanyabiashara Ajay Somani na Jai Somani.

Wakili Maranda alidai Maranda anakabiliwa na makosa matano ya kula njama, kugushi, kuwasilisha hati ya kuamisha deni iliyogushiwa, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kujipatia ingizo la kiasi hicho cha fedha toka Benki Kuu.

Alidai kuwa Desemba 15 mwaka 2004 alighushi hati ya kuamisha mali kati ya Philip Sceman of Societe Alsociene de Construction De Machines Textile 146-148,Ruedaboukir 75002 ya Paris Ufaransa na Maulid Kaasa wa kampuni ya Liquidity Services Ltd kuonyesha kwamba mauled wa kampuni ya Liquidity Services Ltd amepewa idhini ya kudai deni la shilinigi bilioni 5.9 mali ya kampuni ya M/S Societie Alsacienne De Cpnstruction De Machines Textile ya Ufaransa.

Kwa upande wa Komu na Kimela alidai wanashtakiwa kwa kosa moja la kuisababishia BoT hasara ya kiasi hicho cha fedha kwani wao walikuwa watumishi wa benki hiyo na wakashindwa kutimiza majukumu yao hivyo kuisababishia benki hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Hata hivyo washtakiwa wote walikana mashtaka hayo na Maranda akadai juzi jioni alipigiwa simu akiwa katika gereza la Ukonga anakoishi kwa sasa akitakiwa jana afike mahakamani hapo bila kujua afike kwaajili ya jini na kwamba hata wakili wake hana taarifa kama amefunguliwa kesi hiyo mpya ila anaiomba mahakama hiyo impatie dhamana kwa mashtari yatakayowekwa na mahakama hiyo.

Hakimu Katemana alisema Komu na Kimela wanakabiliwa na kosa la kusababisha hasara hivyo ili wapate dhamana ni lazima kila mmoja wao awe na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya bilioni 1.5.

Wakati Maranda anayekabiliwa na makosa ya kula njama, kugushi na kujipatia ingizo atapaswa awe na wadhamini wawili ambao watatoa fedha taslimu au kuwasilisha hati yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.6.Hata hivyo Maranda ameshindwa kutimiza masharti hayo ya dhamana na kesi hiyo imearishwa Desemba mosi mwaka huu na watasomewa maelezo ya awali watasomewa Januari 16-20 mwaka 2012.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Novemba 17 mwaka 2011.

VIELELEZO VYAKWAMISHA KESI YA MINTANGA

Na Happiness Katabazi


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana ililazimika kusitisha kuendelea ushahidi wa shahidi wa tatu na wanne katika kesi ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 4.8 inayomkabili Rais wa zamani wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (TFB) Alhaji Shabani Mintanga baada mahakama hiyo kuvikuta vielelezo vitatu vya upande wa Jamhuri kuwa vina mapungufu.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Dk.Fauz Twaib kufuatia shahidi wa tatu Godfrey Mroso ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Anvelope Travel Agency kutoa sehemu ya ushahidi wake ambapo alidai kuwa yeye ndiye alitengeneza tiketi tatu ambazo aliomba zipokelewe na mahakama kama vielelezo ombi ambalo lilipingwa vikali na mawakili wa utetezi Jerome Msemwa na Yassin Memba kwa madai kuwa tiketi hizo ni nakala badala risiti halisi.

Wakili Msemwa aliomba mahakama isipokee tiketi hizo vivuli kama vielelezo kwasababu tayari upande wa Jamhuri upo kwenye nafasi nzuri ya kuleta tiketi halisi na kompyuta iliyotumiwa na kampuni kutengeneza tiketi hizo ambapo hata hivyo Jaji Dk.Twaibu alikubaliana na pingamizi la wakili Msemwa na akautaka upande wa Jamhuri uende kuondoa neno linalosomeka kuwa tiketi hizo si nakala halisi na akaamuru shahidi huyo aruhisiwe kwenda nyumbani na pindi marekebisho hayo yatakaponywa upande wa Jamhuri umulete tena shahidi huyo ili aweze kuja kumalizia kutoa ushahidi wake na kutaka shahidi wa nne apande kizimbani aanze kutoa ushahidi wake.

Wakati Jaji Dk.Twaibu huyo akitolea uamuzi kuhusu vielelezo hivyo vilivyokuwa vikitaka kutolewa na shahidi wa tatu wa upande wa Jamhuri,Wakili Mwandamizi wa serikali Prudence Rweyongeza alimleta shahidi wa nne, ambaye ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi(SSP), Charles Ulaya ili atoe ushahidi wake lakini hata hivyo wakili huyo alieleza mahakama kuwa kutokana na uamuzi wa mahakama ulitolewa wakati shahidi wa tatu anataka kutoa vile vielelezo vitatu.

Shahidi huyo wan ne (SSP) Ulaya , vielelezo vyake anavyokusudia kuvitoa wakati akitoa ushahidi wake ni kama vya shahidi wa tatu ambavyo vimetengenezwa kwa teknolojia ya kielekroniki na nikala siyo halisi hivyo wakaiomba mahakama shahidi huyo asitoe ushahidi ili upande wa jamhuri uende kuvifanyia marekebisho vielelezo vyote hivyo kwenye kompyuta na leo wataviwasilisha mahakamani na mashahidi hao wataendelea kutoa ushahidi wao.

Aidha Jaji Dk.Twaibu alikubaliana na ombi hilo la wakili wa serikali Rweyongeza la kuarisha kesi hiyo hadi leo na akaamuru vielelezo hivyo ambavyo hata hivyo bado havikuwa vimepokelewa na mahakama hivyo haikuweza kujulikana mara moja ndani ya vielelezo hivyo vimeandikwa nini, hadi leo asubuhi.

Mwaka 2008, Mwintanga alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi hiyo ambayo haina dhamana ambapo kisheria Mahakama ya Hakimu Mkazi haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kesi hiyo iliamishiwa mahakama Kuu mwaka jana na juzi ikaanza kusikilizwa rasmi ambapo imepangwa kusikilizwa mfululizo hadi Novemba 25mwaka huu.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 16 mwaka 2011.

KESI YA ALHAJI MINTANGA:SHAHIDI:DAWA ZA KULEVYA ZILIKUTWA KWENYE BEGI LA BONDIA PETO MTAGWA



Na Happiness Katabazi


ALIYEKUWA Kocha wa timu ya Taifa ya Ngumi , Nassoro Michael Irenge aliyeachiliwa huru na Serikali ya Mauritius kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya , ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuwa dawa hizo zilikutwa na wanausalama zikiwa ndani ya begi la Bondia Petro Mutagwa.

Irenge ambaye ni shahidi wa upande wa Jamhuri aliingia nchini hapa wiki iliyopita akitokea kwenye gereza moja nchini Mauritius alikokuwa akishikiliwa kwa kosa tuhuma hizo , alitoa madai hayo jana wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Dk.Fauz Twaibu katika kesi kesi ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa Kg 4.8 toka Tanzania kwenda Mauritus kukutwa na dawa za kulevya ambayo inamkabili Rais wa zamani wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (TFB) Alhaji Shabani Mintanga anayetetewa na wakili Jerome Msemwa na Yassin Memba ilikuja kwaajili ya kuanza kusikilizwa.

Irenge ambani askari wa Jeshi la Wananchi Watanzania(JWTZ), pamoja na mabondia wawili, Patrick Emilian na Petro Mutagwa walikuwa wakishikiliwa nchini Mauritus kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya wakati walipokwenda kwenye mashindano ya Champion mwaka 2008 nchini humo.Bondia Mutagwa bado anashikiliwa nchini Mauritus wakati bondia Emilian na Irenge waliachiliwa huru na serikali hiyo.

Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa Mwandamizi wa Serikali Pridence Rweyongeza ,Irenge ambaye ni shahidi wa pili katika kesi hiyo alidai kuwa msafara wao ulikuwa na mabondia wawili Mutagwa na Emuilian na kwamba bondia wa tatu Abdallah Kimwaga hakufanikiwa kusafiri kwasababu alikosa tiketi lakini akadai kuwa siku ya kuondoka Mintanga alimweleza kuwa katika msafara wao watakuwepo mashahabiki watatu na kwamba hao mashabiki ndiyo ndio walimdhamini Bondia Mutagwa.

Alidai kuwa wakiwa uwanjwa wa Ndege wa Mwalimu Julia Nyerere alionana na watu wengine watatu ambao ni Phiris Kesi, Nathaniel na Ali Msengwa ambao walijitambulisha kwake kuwa wao ni mashabiki ambao wanajiunga kwenye msafara wake, kama awali alivyokuwa ameishaelezwa na na Mintanga.

“Mheshimiwa jaji mimi na mabondia wangu tulipofika Mauritus tulilala chumba kimoja katika tuliyokuwa tumeandaliwa na wenyeji wetu lakini cha kushangaza kesho yake usiku walikuja askari kutugongea mlango kwa nguvu minikamtaka Mutagwa aende kuwafungulia mlango na baada ya kufungua mlango waliingia askari wakiwa na silaha na kutuambia kuanzia wakati huo tupo chini ya ulinzi na baadae wakawaingiza na wale mashahabiki wakiwa na begi ambalo walilifungua na kutoa dawa ambazo walisema ni za kulevya,” alidai.

Awali akihojiwa na wakili Msemwa , Irenge alidai kuwa begi lile lilikuwa limeandikwa jina la Bondia Mutagwa lakini wakati akihojiwa na Wakili Msemwa akisaidiana na Wakili Memba na kuoneshwa maelezo yake aliyoaandika Polisi, Irenge alidai kuwa begi lile liliandikwa Tanzania.

Aidha katika maelezo ya Irenge alidai kuwa mashahabiki wale walikiri kutenda kosa hilo na kwamba dawa hizo walikuwa wamezimeza tumboni.

Akijibu maswali ya wakili Msemwa, Irenge alieleza kuwa Muntanga kuwa dhidi ya tuhuma zinazomkabili akidai kuwa yeye hakuwahi kukaa naye na kupanga njama kutenda kosa hilo na kwamba Mintanga hakuwai kusafiri na timu hiyo.

Alidai kuwa ingawa walifanyiwa upekuzi mkali katika viwanja vya ndege Dar es Salaam, Nairobi Kenya walikopotia na Mautius ambako walivuliwa hata nguo, lakini hakuna katika msafara wake ambaye alikutwa na dawa au kitu chochote kisicho cha kawaida.

Kw upande wake shahidi wa kwanza Christopher Mutabarukwa ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa BFT alisema kuwa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo ambayo ndio huidhinisha watu wa kuambatana na timu haikuwahi kuwaidhinisha mashahabiki hao.

Hata hivyo akihojiwa na wakili wa Mintanga, Mutabarukwa alidai kuwa hajui lolote kuhusu mahali zilikokamatwa dawa hizo huko Mauritius, aliyewakamata wala waliokamatwa nazo.

Kesi hiyo itaendelea tena leo ambapo shahidi wa tatu upande wa mashtaka ataendelea kutoa ushahidi wake.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 15 mwaka 2011.

WANACHUO UDSM 50 KORTINI KWA MAANDAMANO HARAMU

Na Happiness Katabazi

JUMLA ya Wanafunzi 50 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa mawili ya kufanya mkusanyiko usihalali na kukaidi amri ya Jeshi la Polisi liliwataka watawanyike.


Mawakili wa Serikali Ledslaus Komanya na Shadrack Kimaro walidai mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema waliwataja washtakiwa hao kuwa ni Mwambapa Elias,Evalist Elias, Baraka Monesi, Hellen Mushi, Alphonce Lusako, Matrona Babu, Rolana Wilfred, Godfrey Deogratius , Munisi Denis,Evanos Gumbi na wenzao 40.

Wakili wa Serikali Komanya alidai kuwa mnamo Novemba 11 mwaka huu,katika eneo la Mlimani la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walifanya mkusanyiko usio wa halali na kusababisha uvunjifu wa amani katika eneo hilo.

Wakili Komanya alidai kosa la pili ni kwamba washtakiwa hao wakiwa kwenye mkusanyiko huo haramu kwa lengo la kufanya mgomo, askari wa Jeshi la Polisi waliwataka wanafunzi hao watawanyike lakini hata hivyo wanafunzi hao walikahidi amri hiyo na kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Hata hivyo washtakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, walikana mashtaka hayo na Hakimu Lema alisema ili mshtakiwa apate dhamana ni lazima kila mshtakiwa awe na mdhamini mmoja wa kuaminika ambaye atasaini bondi ya Sh milioni moja.

Hata hivyo ni washtakiwa tisa tu kati ya 50 ndiyo waliotimiza masharti na kupata dhamana na wengine waliosalia walijikuta wakipelekwa gerezani kwa kushindwa kutimiza masharti hayo ya dhamana.

Washtakiwa hao waliopata dhamana ni Rehema Mnuo, Grory Masawe, Happy Amulike, Elisia Mpangala, Frida Timoth , Stela Msofe, Betwel Martin, Mmasi Stephano na Lugemalila Venance.

Hakimu Lema aliarisha kesi hiyo Novemba 28 mwaka huu, ambapo siku hiyo itakuja kwaajili ya upande wa jamhuri kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Novemba 11 mwaka huu, Jeshi la polisi liliwatanya baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho ambao walianzisha mgomo kwa kile walichodai ni kuishinikiza bodo ya Mikopo iwapatie mikopo wanafunzi wenzao.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 15 mwaka 2011.

MSHTAKIW KESI YA 'SAMAKI WA MAGUFULI'AIBUA MAPYA

Na Happiness Katabazi


WAKALA wa Meli ya Tawariq 1, Zhao Qinj(41) ambayo inadaiwa kukamatwa kwenye ukanda wa bahari ya Hindi ya Serikali ya Tanzania ikivua bila leseni na kuharibu mazingira, ameileza Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuwa meli hiyo iliingia nchini Kenya na Tanzania tayari ikiwa na Tani 110 za Samaki ambazo ilizivua kwenye eneo la bahari kuu ambalo halimilikiwi na nchi yoyote duniani.


Zhao ambaye pia ni raia wa China, alitoa maelezo hayo jana wakati alipokuwa akitoa utetezi wake mbele ya Jaji Agustine Mwarija huku akiongozwa na wakili wake Ibrahim Bendera kutoa utetezi wake ambapo alidai kuwa wamiliki wa meli hiyo ambao hakuwataja majina yake ndiyo waliompa jukumu ya kuitafutia leseni Meli ya Tawariq 1 hapa Tanzania ili ije kuvua samaki na kwamba walimteua yeye kuwa wakala wa meli hiyo, maombi ambayo aliyakubali na akayatekeleza kwa vitendo kupitia mamlaka husika za Kenya na Tanzania.

Mshtakiwa huyo alidai Septemba 22 mwaka 2009 aliiandika barua ya Idara ya Uvuvi ya Zanzibar akiomba meli ya Tawariq 1 iruhusiwe kuvua kwenye eneo la Ukanda wa Uchumi, kwa muda wa miezi mitatu na nakala ya ombi hilo naitoa kama kielelezo na Zanzibar ilikubali ombi hilo na kisha nikawajulisha wamiliki wa hiyo meli kwa njia ya mtandao ambapo wakati nawajulisha kuwa kibali hicho kimepatikana Meli ya Tawariq 1 ilikuwa katika eneo la Bahari Kuu ambalo eneo hilo halimilikiwi na nchi yoyote hapa duniani.

Alidai kuwa ilipofika Desemba 2008 wamiliki wa meli hiyo walimtaarifu wamewatuma manahodha wa tatu wa meli hiyo wanaotokeo katika eneo hilo Bahari Kuu kuja mjini Mombasa ambapo anaishi mshtakiwa huyo ili waje kuchukua kibali hicho na Januari 1 mwaka 2009 manahodha hao waliwasili kwenye bandari ya Mombasa na akawapatia kibali hiyo na kisha akawapandisha kwenye meli iitwayo Tuosoun kwaajili ya kuanza safari.

“Machi 8 mwaka 2009 ndiyo meli ya Tawariq 1 ilifika bandari ya Mombasa ikitokea eneo la Bahari Kuu na ndani ya meli hiyo kulikuwa na tani 110 za samaki ambazo zilitakiwa kusafirishwa nje na kwamba walinitajia tani hizo za samaki ili yeye kama wakala wa meli hiyo aweze kwenda kufanya bokingi ya makontena ya kuifadhia samaki hao na kuandaa ilani ya meli hiyo na bandari ya Mombasa iweze kufahamu meli hiyo imebeba mzigo wa uzito gani;

“Lakini Machi 9 mwaka 2009 nikiwa Nairobi nikapigiwa simu na nahodha wa meli hiyo ambaye ni mshtakiwa wa tisa,Hsu Shang Pao kuwa kuna meli nyekundu imezingira meli yao ya Tawariq 1 baharini na kuikataza meli yao isiende Mombasa bali meli hiyo iende Dar es Salaam, na kwamba yeye baada ya kupokea taarifa hizo Machi 10 mwaka huo, alilazimika kupanda ndege kutoka Mombasa kuelekeza Zanzibar na kisha akachukua boti ya Sea Bus na kuisha kuingia Marine Polisi ya Dar es Salaam na alipofika hapo akakutana na askari mmoja ambapo yeye alijitambulisha kwa askari huyo kuwa yeye ndiye wakala wa meli hiyo iliyokamatwa”alidai Zhao.

Kesi hiyo imearishwa hadi leo ambapo washtakiwa wengine wataendelea kutoa utetezi wao.Mbali za Zhao washtakiwa wengine ni manahodha wa meli hiyo Hsu Shang Pao na Ca’ Dong Li na Chen Rui Hai.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima, Novemba 15 mwaka 2011.

MDOGO WA ROSTAM AZIZ KIZIMBANI KWA DAWA ZA KULEVYA

Na Happiness Katabazi


ASSAD Aziz Abdulasul ambaye ni mdogo wa mwanasiasa maarufu nchini, Rostam Aziz, anayetuhumiwa kusafirisha kilo 92.2 za dawa ya kulevya aina ya heroine yenye thamani ya sh bilioni 2, jana alifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu Kanda ya Tanga na kusomewa maelezo ya awali.


Mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Kipenka Mussa, wakili mwandamizi wa serikali Biswalo Mganga aliieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ya jinai Na.1/2011 ilikuja mahakamani hapo kwa mara ya kwanza jana ikitokea Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Tanga kwa ajili ya maandalizi ya kuhamishiwa katika mahakama hiyo ya juu ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na jana upande wa jamhuri uliwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali.

Wakili wa mganga aliwataja washtakiwa hao mbali na Assad kuwa ni Kileo Bakari Kileo, Yahya Makame, Mwamadali Podadi ambaye ni raia wa Iran, Salum Mparakesi, Saidi Ibrahim Hamis na Bakari Kileo ‘Mambo’ ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Richard Rweyongeza na Edward Chuwa.

Akiwasomea maelezo hayo ya awali, Wakili Mganga alieleza kuwa washtakiwa wote kwa pamoja kati ya Januari mwaka 2009 hadi Machi 8 mwaka 2010 walikula njama na kusafirisha kiasi hicho cha dawa za kulevya na kuziingiza nchini.

Aidha wakili Mganga alidai kuwa kosa la pili linalowakabili washtakiwa hao ni kusafirisha dawa hizo za kulevya na kukamatwa na askari wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya cha Jeshi la Polisi, mkoani Tanga, Machi 8, 2010.

Baada ya washtakiwa hao kusomewa maelezo hayo ya awali, walikana mashtaka hayo yanayowakabili na badala yake walikubali majina tu kuwa ndiyo yao.

Kwa upande wake Jaji Kipenka aliahirisha kesi hiyo hadi kikao kingine cha Mahakama Kuu na akaamuru washtakiwa wote kurudi mahabusu kwa sababu kisheria, makosa yanayowakabili washtakiwa hao hayana dhamana.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Novemba 12 mwaka 2011.

WATANZANIA TUACHE UNAFIKI




Na Happiness Katabazi

WIKI iliyopita Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon alihutubia mkutano wa marais wa nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika nchini Austalia. Tanzania tuliwakilishwa na rais wetu Jakaya Kikwete na msafara wake.

Imeripotiwa kuwa katika mkutano huo Waziri Mkuu wa Uingereza, Cameroon aliwahutubia viongozi hao mambo mengi likiwemo agizo la kuzitaka nchi za Afrika kwenda kutunga sheria itakayoruhusu ndoa za jinsi moja la sivyo nchi yake itazinyima misaada nchi za Afrika.

Tangu kuripotiwa na vyombo vya habari agizo hilo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe amejitokeza hadharani kutoa tamko kwa niaba ya serikali kuhusu agizo hilo ambapo alisema msimamo wa serikali yetu, ni kwamba haitakaa itekeleze agizo hilo kwasababu siyo utamaduni wetu na kwamba heri watanzania wafe masikini kuliko kutunga sheria hiyo.
Wananchi kupitia njia mbalimbali za mawasiliano wanaendelea kutoa maoni yao kuhusu agizo hilo ambapo wananchi wengine wanataka sheria hiyo itungwe huku wengine wakitaka isitungwe.

Ieleweke wazi kuwa hadi sasa sheria na Katiba ya Tanzania haitambui ndoa za jinsia moja.

Licha ya vitendo vya ushoga, usagaji na vya baadhi ya wanawake kupenda kufanyiwa matendo ya ngono kinyume na maumbile kwa hiari yao au wengine siyo kwa hiari yao vinazidi kushika kasi kila kukicha na baadhi viongozi wa serikali, wananchi wakiwemo wazazi na viongozi wa dini wanafahamu fika hilo ila kwa unafiki wetu tulifumbia macho ubazazi huu kwa kukataa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola wale wote wanaofanya ufilauni huo.

Lakini leo hii Camerron ametoa agizo hilo mbele ya marais wetu, ndiyo serikali yetu,wananchi,viongozi wa dini nao wanaibuka nakutoa matamko ya kupinga utekelezwaji wa agizo hilo.

Nakubaliana na matakwa ya Ibara 18(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inampa uhuru kila mwananchi kutoa maoni na kutoa fikra zake;

Lakini huu ni unafki wa kujitokeza kupinga agizo hilo wakati tayari kuna baadhi ya Watanzania wenzetu wameishakubuhu na wamegeuza vitendo hivyo ndiyo ajira yao inayowapatoa riziki.Na inaelezwa hata baadhi ya wanaume waliofunga ndoa uamua kuwasaliti wake zao na kuamua kuwatafuta mashoga kwa siri ili wawapatie huduma hiyo ya ngono kinyume cha maumbile.

Leo hii hapa Dar es Salaam, zile sherehe maalum za kumfunda bibi harusi mtarajiwa(Kitchen Party), kwenye kumbi hasa zinazopiga muziki wa Taarabu hata dansi ni kawaida kabisa kuwakuta mashoga wakiwa wametamalaki na ‘kutamba,kujishebedua’ bila wasiwasi.

Kitchen Party nyingi siku hizi mashoga hukodishwa kwaajili ya kuja kusasambua sanduku analotuzwa bibi harusi mtarajiwa, kucheza muziki wa mwambao na mashoga hao ama kwa hakika uchangamsha sherehe hizo. Na wakati mashoga hao wakifanya vitendo hivyo wazazi wa bibi harusi mtarajiwa na ndugu wa mwanaume ambao mtoto wao wa kiume siku chache zijazo anatarajia kumuoa bibi harusi huyo, wanakuwepo ukumbini na kushuhudia hali hiyo na wala hawakemei au kususia sherehe hizo na ndiyo huwa wa kwanza kuwatunza fedha mashoga hao.

Baadhi Maustaadhi wa dini ya Kiislamu nao wamekuwa wakilalamikiwa kichini chini na wengine kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kuwalawiti watoto wa kiume ambao ufika ‘Chuoni’ kufundishwa mafundisho ya dini ya Kiislamu.

Nao baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo hasa wale Roman Katoliki nao wamekuwa wakituhumiwa kuwanajisi watoto wa kiume ambao hufika makanisani kujifunza dini na wengine pia wakafikishwa mahakamani kwa makosa ya kulawiti.

Malalamiko hayo ya mapadri kuwanajisi watoto wa kiume ambayo yamezaaga karibu dunia nzima, hivi karibuni yalimlazimu Kiongozi wa Kanisa hilo la Katoriki Papa Benedict akiwa kwenye ziara yake nchi moja , kuomba radhi kwa vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya mapadri kwaniaba ya kanisa hilo.

Kwa muktadha huo hapo juu, sioni sababu ya kupinga utekelezwaji wa agizo la Uingereza licha tayari serikali yangu imetoa tamko la kulipinga.

Kwani hakuna ubishi kwamba Tanzania licha inautajiri mkubwa tu, taifa letu limeamua kuwa tegemezi kwa nchi zilizoendelea.Na siyo tu serikali yetu imeamua kuwa tegemezi pia hata vyama vya siasa si CCM,Chadema, CUF na vingine navyo vimegeuka kuwa omba omba ‘Matonya’ kwa ama wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya nchi au vyama vya siasa vya nchi zilizoendelea kikiwemo cha huyo David Cameroon na vimekuwa vikipatiwa misaada ya kifedha, mafunzo na vifaa mbalimbali.

Ukizigeukia hizo taasisi binafsi zinazojiita taasisi za wanaharakati uchwara ambazo kila kukicha zimekuwa zikiishutumu bajeti ya serikali kutegemea wafadhili, wakati kumbe taasisi hizo nazo zinaendeshwa kwa kutegemea fedha hizo hizo za wafadhili.

Tumuulize huyo Bernad Membe ni kwanini asingepinga agizo hilo pale pale wakati Swahiba wetu Cameroon anaongea kule Australia?

Membe kasubiri amefika hapa nchini kwa sisi malofa wenzie ndiyo anajifanya mwamba kwa kutoa tamko la kupinga agizo hilo?Ananichekesha sana.

Binafsi nazifahamu fika hulka za wanasiasa wa Tanzania, wengi wao ni wanafiki na wazandiki wakubwa, kwani wanachokisema adharani siyo wanachokifiria wala kukitenda.

Ieleweke wazi ule mshikamano na umoja wa kweli wa nchi za Jumuiya ya Afrika haupo tena.Kila nchi inaangalia maslahi yake kwanza tofauti na awali.Hivyo katika utekelezwaji wa agizo hilo mwisho wa siku msije mkashangaa nchi zingine za Afrika ikiwemo Tanzania zikaridhia kutekeleza agizo hilo kwa kigezo kwamba wanaogopa kunyimwa misaada.

Wanasiasa kama mnakataa sheria hiyo isitungwe hapa nchini basi hata wakati wa Uchaguzi mkatae kupigiwa kura za ndiyo na hao mashoga, wasagaji.

Katika mawazo yangu nitabaki nikiamini kuwa David Cameroon hakutoa agizo lile kwa bahati mbaya ndani ya mkutano ule maana hatukuona hata rais yoyote ndani ya mkutano ule aliyejitutumua kunyosha kidole kupinga agizo hilo la Bwana Mkubwa “Cameroon’ ambaye nchi yake imekuwa ikitupatia misaada kila wakati, kulipinga.

Nimalizie kwa kuwataka watanzania watambue misemo hii yenye maana kubwa ndani yake kuwa “Maskini hana kiapo, Hakuna bingwa wa shida,na ukijua kupokea ujue na kutoa.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
0716 774494:www.katabazihappy.blogspot.com

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 8 mwaka 2011.

SUMATRA,HAWA WAENDESHA PIKIPIKI POSTA MPYA VIPI?



Na Happiness Katabazi


NAANZA kuandika mtazamo huu kwa kuwaomba radhi waendesha Pikipiki maarufu ‘Boda boda”wanaoendesha pikipiki hizo katikati ya jijini la Dar es Salaam,kwa lengo la kutoa huduma ya usafiri kwa abiria wanaopenda kutumia huduma hiyo.

Nasema nawaomba radhi kwakuwa mtazamo huu wa leo unaweza kuwakwaza kwa njia moja au nyingine kwasababu nafahamu fika nyie waendeshapikipiki mliofurika kwa kasi maeneo ya Posta Mpya na maeneo mingine ya katikati ya mji, mnatafuta riziki ili mkono uende kinywani.

Itakumbukwa kuwa ni Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu(SUMATRA), ilizipiga marufuku daladala(Hiace) maarufu kwa jina la Vipanya kuingia katikati ya mji na badala yake ikaruhusu madaladala makubwa (DCM)ndiyo yatakuwa na kibali cha kuingia katikati ya mji na kutoa huduma hiyo ya usafiri kwa abiria.

Kweli amri hiyo ilitekelezwa kwa vitendo na hadi sasa Vipanya havitoi huduma ya usafiri katikati ya mji na badala yake vipanya vimekuwa vikitoa huduma ya usafiri katika barabara ambazo haziingii katikati ya jiji.

Lakini cha kushangaza hivi sasa takribani miezi minne sasa sisi tunaofanyakazi maeneo ya Posta mpya, tumeshuhudia idadi kubwa ya waendeshapikipi wakitoa huduma ya usafiri wa pikipiki bila ya hata SUMATRA kuutangazia umma kuwa imeziruhusu pikipiki hizo kutoa huduma katika ya mji.

Na mbaya zaidi waendesha pikipiki hao wamekuwa waziegesha pikipiki hizo kwenye vituo vinavyopaki daladala hali inayoleta usumbufu mkubwa kwa abiria wanasuburi kupanda daladala na watembea kwa miguu na kufanya abiria washindwe kutofautisha kituo cha kusubiria daladaka ni kipi na kituo cha kusubilia pikipiki ni kipi?

Wakati waendesha pikipiki wakiendelea kutamalaki katikati ya mji,hatujasikia Sumatra ikiutaarifu umma kuwa huduma ya pikipiki ndiyo imekuwa mbadala wa daladala (Vipanya).

Sumatra basi jitokezeni muueleze umma kama ni kweli usafiri wa pikipiki ndiyo umekuwa mbadala wa vile Vipanya mlivyovipiga marufuku ili tuelewe, kwani huo ukimya wenu unatukera na mwisho wa siku utakuja kusababisha madhara kwa abiria wanaosubiri madaladala vituoni na wanatemba kwa miguu.

Kwa sababu hivi sasa tunachoona kwenye vituo vya mabasi ni mashindano ya kuporana wateja baina ya makonda wa daladala na waendesha pikipiki.

Na kama ni kweli pikipiki ndiyo zimeruhusiwa kuja kutoa huduma ya usafiri badala ya Vipanya, basi huu utakuwa ni uwendawazimu wa hali ya juu, kwani huwezi kukataza vipanya visiingie katikati ya mji kutoa huduma ya usafiri wakati kinauwezo wa kubeba abiria wengi kuliko hizo pikipiki halafu ukaruhusu pikipiki ndiyo zitoe huduma.

Ieleweke wazi Mtazamo huu hauna lengo la kuharibu biashara ya usafiri wa pikipiki la hasha, unalengo la kuhoji Je ni halali kukataza vipanya siingine katikati ya mji kutoa huduma ya usafiri ambapo vipanya hivyo vinauwezo wa kubeba abiria wengi kuliko pikipiki halafu mamlaka husika zikaruhusu pikipiki ndiyo ziingie katikati ya mji kutoa huduma hiyo ya usafiri tena bila abiria anayepanda pikipiki hapewi risiti?

Ifike mahala mamlaka husika za serikali ziache mzahaa katika utendaji kazi na zitimize majukumu yake kwa maslahi ya taifa hili na siyo ubabaishaji kama huu, kama mamlaka husika ilisema uwepo wa Vipanya katikati ya mji ni uchafu, iweje leo hii iruhusu pikipiki ndiyo ziingie katikati ya mji kutoa huduma hiyo ?

Hakuna ubishi kuwa madai kuwa waendesha pikipiki wengi hivi sasa hawana mafunzo ya kutosha kuhusu uendeshaji wa pikipiki hizo hali inayosababisha kila kukicha ajali za pikipiki kuongeza na kusababisha majeruhi wa ajali za pikipiki kuleta msongamano mkubwa pale Taasisi ya Mifupa(MOI) yanaongezeka.

Sasa kama hivyo ndiyo serikali imejipanga vipi kuakikisha inawashughulikia madereva uchwara wa pikipiki ili wasiweze kuendesha pikipiki hizo?

Nimalizie kwakusema kuwa kuna ulazima wa SUMATRA kutolea tamko kuwa limewaruhusu waendesha pikipiki kutoa huduma hiyo katikati ya mji na kama imewaruhusu basi waendesha pikipiki hao wawekewe utaratibu wa maalum ili tuweze kuitambua kuwa pikipiki hii iliyopakwa rangi fulani ubavu inafanya safari zake mfano Sinza hadi Posta na abiria wanaotumia usafiri huo wapewe risiti na waendesha pikipiki hao wapangiwe kiwango cha nauli cha kuwatoza abiria hao.

Kinyume cha hapo utakuwa ni uwendawazimu tu uliowekewa baraka za mamlaka husika inayoshughulika na huduma ya usafiri mjini.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne,Novemba mosi,mwaka 2011.