VIGOGO BODI YA WATINGA KORTINI

Na Happiness Katabazi Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Watalaam wa Manunuzi na Ugavi (PSPT), Clemence Tesha na wenzake jana walijikuta wakifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa ya matumizi mabaya ya madaraka. Mbali na Tesha washitakiwa wengine ni Winfrida Igogo ambaye ni Afisa Rasilimali watu Mwandamizi na mshitakiwa wa tatu ni Amani Ngonyani ambaye ni Meneja Biashara na Maendeleo wa Bodi hiyo ambapo wanatetewa na wakili wa kujitegemea Frank Kiliani. Mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), Salha Abdallah na Sophia Gula mbele ya Hakimu Mkazi Faisa Kasamba walidai kuwa kosa la kwanza ni la matumizi mabaya ya madaraka kinyume cha na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana Rushwa ya mwaka 2007, ambapo kosa hilo linamkabili mshitakiwa wa kwanza na wa pili. Wakili Abdallah alidai Juni 22 mwaka 2010 katika ofisi za Bodi hiyo, washitakiwa walimuajiri mshitakiwa wa tatu(Ngonyani) kushika wadhifa huo wakati Ngonyani hajasajiliwa na Bodi ya Watalaamu wa Manunuzi na Ugavi,kitendo ambacho kinakwenda kinyume na kifungu cha 46(1) cha Sheria ya Bodi hiyo ya (PSPT) ya mwaka 2007. Wakili Abdallah alidai kuwa shitaka la pili ambalo linamkabili mshitakiwa wa kwanza na wapili , ni la kumwajili mshitakiwa wa tatu (Ngonyani) kushika wadhifa huo wakati wakijua mshitakiwa huyo alikuwa hajasajiliwa na bodi hiyo kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 46(1)(3) cha Sheria ya Bodi hiyo. Alidai kuwa Juni 22 mwaka 2010 Tesha na Igogo wakiwa na nyadhifa zao walimwajiri Ngonyani kama Menej wa Biashara na Maendeleo wa bodi hiyo hku wakijua Ngonyaji hakuwa amesajiliwa na bodi hiyo ya wanataaluma wa masuala ya ugavi na manunuzi. Aidha wakili Abdallah alidai shitaka la tatu ni kwa ajili ya mshitakiwa wa tatu pekee ambalo ni kujipatia ajila hiyo ya kazi za manunuzi kinyume na sheria jambo ambalo ni kinyume na kifungu cha 46(2),(3) cha sheria ya bodi hiyo kwamba Juni 22 mwaka 2010 katika ofisi ya bodi hiyo alijipatia ajira hiyo wakati akijua wazi hakuwa amesajiliwa na bodi hiyo na kuongeza kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Hata hivyo washitakiwa wote walikana mashitaka hayo na Hakimu Mkazi Kahamba alisema kesi inayowakabili ina dhamana na hivyo kumtaka kila mshitakiwa awe na wadhamini wa wiwili wanaotoka ofisi zinazotambulika na serikali ambapo watasaini bondi ya Shilingi milioni 10.Washitakiwa wote walitimiza masharti hayo na wapo nje kwa dhamana na akaiarisha kesi hiyo hadi Julai 26 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Julai 29 mwaka 2012.

KESI YA IDD SIMBA,NTAGAZWA ZA AIRISHWA

Na Happiness Katabazi KESI ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kulisababishia Shirika la Usafirishaji UDA, hasara ya Shilingi bilioni 2.3 inayomkabili Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Idd Simba jana ilitajwa mbeled Hakimu Mkazi Faisa Kahamba na kuiarishwa. Hakimu Kahamba alisema kesi hiyo iliyokuja kwaajili ya kutajwa na anaiarisha hadi Julai 19 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kupangiwa tarehe ya usikilizwaji wa awali. Mbali na Simba ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazee wa Dar es Salaam, washitakiwa wengine ni Mkurugenzi Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi ambao wanatetewa na wakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa na Said El Mamli na upande wa Jamhuri unawakilishwa na wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Ben Lincoln. Wakati huo huo kesi ya kujipatia kofia,fulana zenye jumla ya shilingi milioni 74.9 kwa njia ya udanganyifu inayomkabili aliyekuwa waziri wa zamani Arcado Arcado Ntagazwa(65) na wenzake imeairishwa mahakamani hapo hadi Julai 25 mwaka huu. Na kwamba mahakama hiyo imekubali ombi la upande wa Jamhuri la kuongezewa siku 60 kwaajili ya kuendelea kufanya uchunguzi wa kesi hiyo. Washitakiwa wengine ni Senetor Mirelya (60) na Webhale Ntagazwa wanaotetewa na Alex Mgongolwa. Aprili 23 mwaka huu, wakili wa serikali Ladslaus Komanya mbele ya Hakimu Mkazi Liad Shamshama alidai kuwa Oktoba 22 mwaka 2009 huko Msasani Mikoroshini washtakiwa hao kwania ovu walijipatia fulana 5000 na kofia 5000 zenye jumla ya thamani ya Shilingi milioni 74.9 toka kwa Noel Sevele kwa makubaliano kuwa wangemlipa Sevele kiasi hicho cha fedha katika kipindi cha mwezi mmoja tangu walipochukua vifaa hivyo lakini hata hivyo walishindwa kumlipa. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Juni 29 mwaka 2012.

KESI YA KIBANDA YAFIKA PATAMU

Na Happiness Katabazi UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima,Absalom Kibanda na wenzake jana uliwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam. Mbali na Kibanda washitakiwa wengine ni Samson Mwigamba ambaye ni mwandishi wa makala wa gazeti la Tanzania Daima na Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Theophil Makunga ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Mabere Marando ,Gabriel Mnyele, Isaya Matamba, Juvenalis Ngowi na Hohn Mhozya na Frank Mwilongo. Wakili wa serikali Elezabeth Kaganda mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema alianza kwa kuikumbusha mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilikuja kwaali ya kuwasomea maelezo ya awali na kwamba wapo tayari kwaajili ya kufanya hivyo na akaanza kuwasomea maelezo ya awali kama ifuatavyo. Kaganda alidai alidai mshtakiwa wa kwanza na wapili(Mwigamba na Kibanda) wanakabiliwa na kosa la kwanza la kuandika makala ya uchochezi iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “Waraka maalum kwa askari wote’. Alidai kuwa Mwigamba ambaye Mhasibu wa Chama Cha Demokrasi Chadema na Kibanda ambaye ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, kwa pamoja waliandika na waliruhusu makala hiyo ichapishwe kwenye gazeti hilo ambayo iliandikwa na gazeti la Tanzania Daima la Toleo Na. 2552 la Novemba 30 mwaka 2011 na makala hiyo ambayo ni ya uchochezi ikaja kuchapishwa na mshiutakiwa wa tatu (Makunga) kupitia kiwanda cha upachaji ambacho kipo chini ya uongozi wake. “Sisi upande wa jamhuri tunadai kuwa makala hiyo ni ya uchochezi na ilikuwa ikiwashawishi askari wa Jeshi la Wananchi,Polisi,Magereza na KMKM wasiitii amri za makamanda wao jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi na hata Desemba 6 na Desemba 20 mwaka jana, washitakiwa hao walipofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini na kuhojiwa ,walikiri kutenda makosa hayo ya kuandika na kuchapisha makala hiyo”alidai wakili Kaganda. Hata hivyo Hakimu Lema baada ya wakili Kaganda kumaliza kuwasomea maelezo hayo aliwataka washitakiwa hao waseme wanayakubali nini katika maelezo hayo ya awali , washitakiwa wote walikubali majina yao tu na wakayakana maelezo mengi kwa madai kuwa maelezo hayo si sahihi. Baada ya kumaliza hatua hiyo, wakili Kaganda alivitaja vielelezo watakavyovitumia wakati kesi hiyo ikianza kusikilizwa ambavyo ni makala yenyewe, maelezo ya washitakiwa na maoni ya wataalamu na hata hivyo akakataa kutaja orodha ya majina ya mashahidi ambao watawaleta kutoa ushahidi. Kwa upande wake Hakimu Lema alitoa amri ya kuutaka upande wa Jamhuri uakikishe unawapatia maelezo ya mlalamikaji wa kesi hiyo upande wa utetezi mapema iwezekanavyo na kwamba anaiarisha kesi hiyo Agosti 7 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kuanza kusikilizwa rasmi. Machi 7 mwaka huu, Wakili Kaganda akiisoma hati mpya ambayo ina mashtaka mawili tu ambapo kosa la kwanza ni la uchochezi kinyume na kifungu cha 32(1)(c) na 31(1)(a) cha Sheria ya Magazeti Sura ya 229 ya mwaka 2002 ambalo lina mkabili mshtakiwa wa kwanza na wa pili yaani Mwigamba na Kibanda. Ambapo wakili Kaganda alidai kuwa mnamo Novemba 30 mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wawili kwa makusudi na kwa nia kuvunja sheria za mamlaka ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walitenda kosa hilo la uchochezi kwa kuruhusu makala hiyo ichapishwe kwenye gazeti la Tanzania Daima la Novemba 30 mwaka 2011 iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “ Waraka Maalum kwa askari wote’ ambapo ilikuwa ikiwachochea askari hao wasitii mamlaka za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Julai 27 mwaka 2012.

KESI YA HASSANOL YADODA

Na Happiness Katabazi MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ilishindwa kuanza kusikiliza kesi ya wizi wa madini ya shaba yenye thamani ya sh milioni 400, inayomkabili Katibu wa zamani wa Simba, Hassan Hassanol (43) na wenzake watatu. Hiyo imetokana na wakili wa serikali aliyekuwa akiindesha kesi hiyo tangu awali, Elizabeth Kaganda kuwakabidhi jukumu hilo mawakili wengine kwani yeye ametingwa na majukumu mengine. Mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, mawakili wapya wanaoendesha kesi hiyo, Theophil Mtakyawa na Ester Kyala, waliieleza mahakama kuwa, kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya mashahidi wa upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi. Hata hivyo, walisema hilo halitawezekana kwa sababu wakili wa serikali (Kaganda), aliyekuwa akiendesha kesi hiyo amewakabidhi wao kuiendesha kwa kipindi chote kutokana yeye kupewa majukumu mengine ya kiserikali. “Na leo (jana) asubuhi ndiyo tumekabidhiwa jalada la kesi hii, hivyo hatujajiandaa kabisa, tunaomba mahakama itupatie muda ili twende tukalisome jalada hii tufahamu vizuri kesi hii,” alidai wakili Mtakyawa. Hakimu Kisoka alikubaliana na ombi hilo na akaahirisha kesi hiyo hadi Julai 25, maka huu itakapokuja kutajwa na Agosti 6-7 itaanza kusikiliziwa. Katika hati ya mashitaka, wanadaiwa Agosti 28 mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao kwa pamoja, walipanga njama ya kuiba mali hizo. Shitaka la pili, tarehe hiyo hiyo, washitakiwa hao waliiba tani 26 za madini ya shaba yenye thamani ya fedha hizo yaliyokuwa yanasafirishwa kutoka Zambia kuja nchini. Ilidaiwa kuwa, madini hayo yalikuwa yanasafirishwa kwenye lori lenye namba za usajili T 821 BCL na tela namba T 566 BCL ambayo ni mali ya Kampuni ya Liberty Express. Katika shitaka la tatu, wanadaiwa washitakiwa hao walipokea mali hiyo huku wakijua kuwa ni ya wizi. Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Wabura Magenga (32), Dk. Najim Msenga na Salim Shekibala. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Julai 27 mwaka 2012.

HUKUMU YA MARANDA YAYEYUKA TENA

Na Happiness Katabazi KWA mara ya pili sasa, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imejikuta ikishindwa kutoa hukumu katika kesi ya wizi wa sh bilioni 2.2 kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu inayomkabili kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Maranda na binamu yake, Farijala Hussein kwa sababu baadhi ya mahakimu waliokuwa wakiisikiliza wana matatizo ya afya. Jana kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutolewa hukumu ambayo ilishindikana kutolewa Mei 17 mwaka huu, kwa sababu ya kuugua kwa Hakimu Mkazi Catherine Revocate ambaye anaunda jopo jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo, pamoja na Jaji Fatma Masengi na Projest Kahyoza. Hakimu Mkazi Kahyoza aliyefika mahakamani hapo jana, ambapo ukumbi wa mahakama ulikuwa umefurika ndugu wa washitakiwa hao na waandishi wa habari, alianza kwa kusema kuwa ni kweli kesi hiyo ilikuja jana kwa ajili ya kutolewa hukumu, lakini haitawezekana kwa sababu mwanajopo mmoja bado afya yake haijatengamaa na ndio amerudi nchini akitokea nje ya nchi kwa ajili ya matibabu. “Kwa sababu hiyo, napenda kusema kuwa hukumu ya Maranda leo haitasomwa na badala yake itasomwa Julai 24 mwaka huu, na tutajitahidi wanajopo wote tuwepo ili tuweze kuisoma kwani tayari tumeishaindaa hukumu yetu, ipo na hatutaki tukae nayo sana kwani haya makaratasi yasije yakatuzoea,” alisema. Baada ya Hakimu Kahyoza kusema hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Oswald Tibabyekomya alisema hana pingamizi na amri hiyo ya mahakama. Hadi sasa washitakiwa wanatumikia kifungo katika Gereza la Ukonga, na kumalizika kwa kesi hiyo kutawafanya wabakiwe na nyingine tatu ambazo zimefikia hatua ya kuendelea kusikilizwa. Mei 23 mwaka jana walitiwa hatiani na mahakama hiyo kwa makosa ya kughushi, kula njama na kujipatia ingizo la sh bilioni 1.8 za EPA. Wakati huo huo, upande wa jamhuri unaowakilishwa na wakili wa serikali, Prosper Mwangamila katika kesi ya kuendesha upatu inayowakabili viongozi wa Taasisi ya DECI, ulifunga kesi hiyo baada ya mashahidi wake 16 kumaliza kutoa ushahidi wao. Hakimu Mkazi Stewart Sanga aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 17 mwaka huu, ambapo siku huyo atakuja kutoa uamuzi wa ama washitakiwa wana kesi ya kujibu au la. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Julai 27 mwaka 2012.

DK..BILAL ATUA BRAZIL KUSHIRKI RIO +20 JUMATANO

Na Happiness Katabazi,Brazil TANZANIA na mataifa mengine mbalimbali dunia Jumatano hii inaanza kuudhulia mkutano wa Rio+20 unaofanyika jijini Rio Je Neiro nchini Brazil. Mkutano huo ambao utamalizika Juni 22 mwaka huu na washiriki wa mkutano huo kutoa maazimio yao ya nini kifanyike kuhusu kuhusu uharibu wa misitu na mazingira kwa ujumla, unaudhuliwa na marais wa nchi,wawakilishi wa marais hao, wataalamu wa masuala ya mazingira duniani. Kwa upande wa Tanzania, makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal ambaye amefuatana na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira, Teresa Uvisa, Mshauri Mwandamizi wa rais Jakaya Kikwete wa masuala ya Kidiplomasi, balozi Liberata Mulamula na maofisa wengine waandamizi wa serikali ndiye aitaiwakilisha nchi na tayari jana mchana aliwasili nchini hapa tayari kwaajili ya kuudhuria mkutano huo. Mwandishi wa habari hizi ambaye ni miongoni mwa waandishi wa habari anayeudhulia mkutano huo wa kihistoria ameshuhudia maofisa ubalozi wa Tanzania nchini hapa wakimlaki Dk.Bilal na pia kuwashuhudia baadhi ya wakuu wa mataifa mbalimbali duniani waliofuatana na watendaji wa serikali zao wakiwasili mjini hapa Rio de Jeneiro kwaajili ya kuudhulia mkutano huo. Pia mwandishi wa habari ambae ameweza kutembelea katikati ya mji wa Rio De Jeneiro ameishuhudia wananchi wa mataifa mbalimbali wakiwa wamekodi katika mahoteli hao kwaajili ya kuishi kwa muda wakati wakiidhulia mkutano. Katika mkutano huo wa mazingira duniani maarufu kama Rio +20 ,wanakusudia kujadili matatizo ya uharibu wa mazingira yaliyojitokeza kwa ghafla katika karne ya 21 kwani uharibu wa misitu utabakia kuwa ajenda ya juu ya mkutano huo wa mwaka huu 2012.

VIONGOZI WA BAKWATA MMEKOSEA

Na Happiness Katabazi TAYARI kuna baadhi ya Watanzania wenzetu ambao wameanza kuonyesha dalili ya kuichoka amani iliyopo hapa nchini hivyo sasa kila kukicha wanatamani kushuhudia machafuko ya kidini yakitokea hapa nchini. Uenda wamefikia hatua ya kutamani hayo kwasababu uenda wamechoka kuona machafuko hayo kupitia kwenye Televisheni na kusikia kwenye redio yakitokeo kwenye nchi za wenzetu ambao zimekumbwa na machafuko yanayosababishwa na udini,ukabila na madaraka. Nimelazimika kusema hayo kwasababu hivi karibuni tumeshuhudia viongozi wa Kikundi cha Uamsho kule Zanzibar wakileta machafuko kwa kuchoma kanisa na kuchoma moto maduka kwa kisingizio wanapinga Muungano lakini navishukuru sana vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama vimeweza kuwashughulikia kimya kimya waasisi wa vurugu zile na ndiyo maana leo hii wale viongozi na wafuasi wa Kikundi cha Uamsho kimefyata mkia na hatuwasikii tena wakijinasibu kwenye vyombo vya habari. Lakini Jumatano ya wiki hii tena tumelisikia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na viongozi wa jumuiya za Kiislamu 31,walitangaza kulisusia zoezi la kuhesabu watu na makazi linalotarajia kufanyika Agosti mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bakwata kwa niaba ya Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa bin Shaaban Simba, Amir Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu nchini, Musa Kundecha alisema waislamu hawakusikilizwa ndiyo maana wamesusia . “Kama kukataliwa ni vyema basi tukataliwe sote,kwa kitendo cha Kanisa Katoliki kufanya sense na kuweka mitandaoni ni lazima pia watakuwa wanashirikiana na sense,hivyo basi kwa nini na wailasmu wasiruhusiwe hivyo”alisema Kundecha. Wengi wetu tuliosikia kauli hiyo ya Bakatwa tulishtuka na kuanza kutafakari na kuanza kujiuliza maswali yafuatayo hivi sensa imeanza kufanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu? Mbona miaka yote huko nyuma serikali imekuwa ikiendesha zoezi la Sensa na Bakwata na jumuiya zake zilikuwepo lakini hatukuwahi kuzishuhudia zikijitokeza adharani kutangaza kususia sensa kwa kigezo kuwa serikali imekataa ombi lao la kutaka kipengele cha udini kiingizwe kwenye sensa? Inaeleweka wazi kuwa lengo moja wapo la serikali kufanya sensa kwa wananchi wake ni kutaka kufahamu takwimu halisi la wananchi wake waliopo kwaajili ya kuwaletea maendeleo na kupanga mipango yake ya kimaendeleo hata kwa vizazi vijavyo. Kamwe taifa lolote haliwezi kupanga mipango yake ya kimaendeleo au kuwaletea maendeleo wananchi wake kupitia maeneo wanayoishi bila kufahamu eneo fulani lina idadi ya wakazi wa ngapi kwahiyo hata kama serikali inataka kujenga hospitali katika eneo hilo basi itajenga hospitali ambayo itaweza kutumiwa na idadi fulani ya wakazi wa eneo hilo. Sasa inashangaza kuona leo hii Bakatwa na hizo jumuiya zake zinajitokeza adharani na kuwataka waumini wa dini ya kiislamu wasusie sensa. Hivi tuiulize hii Bakwata na jumuiya zake zinaitii serikali ipi? Maana kama kweli inaitii serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama sheria za nchi zinavyotutaka wanachi na taasisi zote zilizopo hapa nchini kuiitii serikali iliyopo madarakani, wasingetoa tamko la aina hiyo kwani tamko hilo walilolitoa ni wazi kabisa linaamasisha waamuni wa dini ya kiislamu wakatae agizo la serikali linalowataka wananchi wote wajitokeze kuhesabiwa katika zoezi la sensa. Hivi mtu yoyote anayekaidi agizo lolote la serikali ,si sheria zinatueleza mtu au taasisi inayokaidi agizo la serikali anapaswa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria? Uenda Sheikh Kundecha wakati anatoa tamko hilo hakuwa hakifahamu madhara na uzito wa tamko hilo.Angefahamu madhara na uzito wa endapo tamko hilo litatekelezwa na waumini wake kama ni kweli kiongozi huyo wa dini ana uzalendo wa kweli na serikali yake asingethubutu kutoa tamko hilo. Kwani tamko hilo linaweza kusababisha baadhi ya waumini wa kiislamu ambao wanawatii kikamilifu viongozi wao dini kweli wasusie sensa, watakuwa wamekwamisha malengo ya serikali ya kufahamu idadi sahihi ya wananchi wake. Na kama serikali itapata takwimu zisizo sahihi za wananchi wake, mwisho wa siku serikali itajikuta ikitenga bajeti za kimaendeleo kwa takwimu zisizosahihi na matokeo yake wananchi wengine ambao walijitokeza kuhesabiwa nao watajikuta wakikosa au kupata mgao finyu wa kimaendeleo kwasababu ni wazi serikali itakuwa imetenga bajeti ya watu wachache lakini wakati mwisho wa siku watumiaji watakuwa wengi wakiwemo wale waliosusia sense. Na hilo likitokea hiyo Bakwata na jumuiya zake itapata faida gani? Na mbona hiyo Bakwata haisemi wazi lengo hasa la kutaka kipengele cha udini kiingizwe kwenye sense?Maana serikali tayari imeshaweka wazi lengo la kufanya sensa kwa wananchi wote. Hivi kwani Bakwata wakiamua kufanya sensa yao na ikishapata takwimu za waumini wao ikaziifadhi kwenye taasisi hizo kuna ubaya gani?Ni kwanini basi wanang’angania kipengele hicho cha udini kiingizwe kwenye sensa ya serikali? Kundecha amenukuliwa akisema wao wamefikia uamuzi huo kwasababu wahawajasikilizwa ombi lao hilo.Hivi jamani kila anayewasilisha ombi lake kwa mamlaka husika ni lazima ombi hilo likubaliwe? Kundecha amenukuliwa akisema haoni sababu ya serikali kugoma kuingiza kipengele cha dini ilhali wenzao wakristo (Kanisa Katoliki) wameruhusiwa kuingiza takwimu hizo mitandaoni bila kujulikana walikozipata.Tumuulize kiongozi huyo hivi Kanisa katoliki ndiyo waumini wote wa dini ya Kikristo hapa nchini?Jibu ni hapa. Na kama hivyo ndivyo hizo Takwimu za Kanisa Katoriki ndiyo imekuwa sensa ya Taifa au imebaki kuwa sensa ya kanisa hilo? Ibara ya 19(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inasema “ Kazi ya kutangaza dini, ,kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi”. Kwa maana hiyo ombi hilo la Bakwata kwa serikali linapingana na matakwa ya ibara hiyo. Ikumbukwe kuwa taifa letu haliendeshwi kwa misingi ya kidini wala kikabila.Linaendeshwa kwa misingi ya sheria na Katiba hivyo ni vyema basi viongozi hao wa kidini na wale wa dini nyingine wakatambua kuwa Katiba na serikali kwa ujumla ina heshimu dini na imani za watu na ndiyo maana Ibara ya 19(1) ya Katiba imetoa uhuru wa mtu kuamini dini atakayo. Leo hii serikali ikiiruhusu kuingizwa kipengele cha udini katika sensa, kesho kutwa na sisi watu wa kabila la Wanyambo tutaibuka na kushinikiza kipengele cha ukabili kiingizwe kwenye sensa ili sisi wanyambo tujifahamu tupo kiasi gani.Mwisho wa siku tutajikuta sasa tuanza kusigana katika udini na ukabila, ambao hautusaidii lolote katika taifa. Kuna mambo mengi sana ya kimaendeleo viongozi wetu wa dini wanatakiwa wawe wanayasemea kwa kauli nzito ,lakini cha kushangaza hawayasemi wala kutoa maagizo mazito kama hayo. Ningeona busara sana kama Kundecha na wenzake wangetangaza kuwataka waumini wao wenye umri wa kwenda shule ambao wazazi wao hawana huwezo wa kifedha wa kuwalipia ada,wajiorodheshe majina yao na wafike katika ofisi za Bakwata kwani tayari wameishawatafutia wafadhali wakuwasomesha,ningeona hilo ni jambo jema sana lenye manufaa kwa baadhi ya waumini. Hivyo basi misioni haja ya leo hii ya viongozi wetu wa dini kuingia kwenye malumbano hayo ambayo ni wazi hayailetei tija taifa kwani hivi sasa wananchi wanachokitaka ni kuletewa maendeleo wao wenyewe na serikali yao . Na taifa hivi sasa linashahuku ya kufahamu idadi mpya ya watanzania wanaishi hapa nchini ili waweze kuzitumia takwimu hizo katika shughuli mbalimbali. Ikumbukwe kuwa kiongozi ni mtu anayepaswa kuwaongoza watu wake katika kufanya mambo fulani ili waweze kufikia mafanikio ya malengo waliyojiwekea sasa inapotokea baadhi ya kiongozi anashindwa kuwaongoza waumini au wafuasi wake kufikia maendeleo waliojiwekea ni wazi kiongozi huyo hatastahili kuendelea kuwa kiongozi. Tayari tumeshuhudia nchi za wenzetu zikiingia kwenye machafuko yaliyosababishwa na udini, ukabila na ung’ang’aniaji wa madaraka na watu wakajikuta wakipoteza maisha ,sasa maagizo kama haya yanaweza kusababisha baadhi ya waumini wa kiislamu kuanza kuwachukia wakristo(Katoliki) na wakatoriki kuanza kuwachukia waislamu. Hatutaki tufike huko na ninaamini ndugu zetu waislamu ambao tunaishi nao vizuri na kwa upendo na wanaofahamu nini maana ya kuhesabiwa watalipuuza agizo hilo lilotolewa na viongozi wao wa Bakwata. Kwasababu siyo siri viongozi wao wa Bakwata hawana mvuto,ushawishi na huwezo wa kuwashawishi waislamu wote wakakubali kutekeleza agizo hilo lao la kususia sensa kwani kuna baadhi ya waislamu akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Ghari Bilal ,watendaji wa Taasisi ya Takwimu ya Taifa na wale waumi wa kawaida wa dini wa kiislamu hawawezi kususia sensq kwani wameridhia lifanyike na hadi sasa wanaendelea kushiriki kikamilifu katika kuakikisha sensa inafanyika kwa umakini wa hali ya juu. Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika 0716 774494 Email:katabazihappy@yahoo.com www.katabazihappy.blospot.com Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Juni 17 mwaka 2012.

WAZIRI MKANGARA UMESEMA KWELI

Na Happiness Katabazi MAPEMA wiki hii Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na MIchezo Dk.Fenella Mkangara aliwataka maafisa Habari wa serikali kuachana na tabia ya kuficha habari za serikali kwasababu kufanya hivyo ni kuwanyima wananchi haki ya Kikatiba ya kupata habari. Dk.Mkangara aliyasema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa maafisa habari wa serikali ambapo alisema kitendo pia kinasababisha serikali ionekane haifanyi kazi kwasababu wao wanashindwa kuwapatia taarifa za shughuli za kimaendeleo zilizofanywa na serikali kwa wananchi. Binafsi nilimshuhudia Dk.Mkangara akitoa maneno hayo kupitia Televisheni na lilinufurahisha mno kwasababu ameongea ukweli mtu bila kuwaonea haya maofisa habari ambao wengi wao kadri siku zinavyozidi kwenda tunawaona wameishasahau majukumu yao kitaalum. Awali ya yote naomba ieleweke kuwa siyo kila taarifa za serikali zinapaswa kutolewa kwa umma.Kuna baadhi ya mambo yanayofanywa na serikali kwa maslahi ya taifa yetu hayapaswi kuwekwa adharani kwasababu ya unyeti wake na ndiyo lakini kuna baadhi ya mambo yanatakiwa umma uelewezwe. Lakini hayo mambo ambayo umma unatakiwa uelezwe na serikali kupitia maofisa habari hao, wamekuwa hawayaelezi kila wakati kama wanavyotakiwa wafanye hivyo. Ni maofisa Habari wachache sana wa serikali wamekuwa wakijiamini na kutekeleza moja ya jukumu hilo la kuubadilisha umma bila ugumu wowote.Lakini maofisa habari wengi wa serikali hapa nchini wamekuwa ni wazito kutoa taarifa mbalimbali kwa umma kwa kisingio kuwa mawaziri ,wakuu wa wilaya,makatibu wakuu, wakuu wa mikoa wamekuwa wakiwazuia kichinichini kutoa taarifa kwa umma na matokeo yake maofisa habari hao wameamu kukaa kimya. Minajiuliza hivi ofisa habari ambaye alisoma vizuri chuoni ni lazima atakuwa anaifahamu vyema kazi yake na kamwe hatakubali kuyumbishwa na mtu ambaye hana taaluma ya habari. Lakini cha kushangaza baadhi ya maofisa wa habari wa serikali hawako hivyo kabisa na uenda labda ni kwasababu waliajiriwa moja kwa katika nafasi hizo bila kwanza kufanyakazi katika vyumba vya habari? Lakini mwandishi wa habari ufanyakazi kwenye vyombo vya habari kwanza inaweza isiwe sababu ya msingi ya kusababisha afisa wa habari wa serikali kushindwa kutoa taarifa kwa umma, kwani kuna baadhi ya maofisa habari wa serikali leo hii hapo nyuma walishawahi kuwa waandishi wa habari katika vyumba kadhaa vya habari lakini waliteuliwa au walivyoajiriwa kuwa maofisa wa habari wa serikali ndiyo wamekuwa mstari wa mbele leo hii kushindwa kutoa taarifa za serikali kwa umma, kubagua vyombo vya habari katika kuvipa taarifa, wameshindwa kuwabunifu katika ofisi zao za habari huko serikalini. Ieleweke kuwa hivi sasa hapa ulimwengu umuhimu wa watu kupashana habari za aina yoyote unazidi kuongezeka na hali hiyo isaidia wananchi kujua nini kinaendelea hapa nchini na duniani kwa ujumla. Ndiyo maana makala yangu ya leo nimelazimika kuunga mkono hoja ya Waziri Mkangara ya kuwasema wazi wazi maofisa hao waache tabia ya kuficha habari bila sababu za msingi. Bila serikali kutoa taariza zake kwa umma ni wazi wananchi walioiweka serikali hiyo madarakani wataishia kulalamika kila siku kuwa serikali yao haiwatimizii matakwa yao na ushahidi wa hilo ni hivi sasa wananchi wengi wamekuwa wakiishutumu serikali kuwa haijawafanyia lolote jambo ambalo si kweli kwani kuna baadhi ya mambo ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, nafuu ya upatikanaji wa umeme ukilinganisha na miaka mitatu nyuma hapo taifa lilikuwa likikabiliwa na mgao wa umeme, sera ya watoto wa chini ya miaka mitano kutibiwa bure katika hospitali za serikali na mambo mengine mengi lakini mambo hayo ya kimaendeleo hayasemwi kwa mapana na maofisa habari hao. Ukiachilia mbali hilo pia kuna baadhi ya maofisa habari wa serikali wamekuwa na kasumba mbaya ya kubagua vyombo vya habari vya kuvipatia taarifa bila sababu za msingi jambo ambalo linatufanya sisi waandishi wa jeuri tukiwa na shida ya kupata taarifa za taasisi fulani kuamua kwenda moja kwa moja ama kwa waziri,wakurugenzi, mkuu wa wilaya au wakuu wa mikoa watupatie hizo hizo kwa maslahi ya nchi. Na maofisa wa habari wenye tabia hii waache hiyo tabia kwani wakae wakijua cheo ni dhamana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inakataza ubaguzi wa aina yoyote ile. Ina kera sana tabia hiyo kwani wakati mwingine mwandishi wa habari anataka kuandika habari au makala kuhusu eneo fulani anaitaji kupatia taarifa za kiserikali kutoka kwa maofisa habari lakini cha kusikitisha hapewi ushirikiano na baadhi ya maofisa hao wa serikali hali inayosababisha baadhi ya waandishi wa habari wanaofanya kazi katika vyombo vya habari kuandika taarifa au makala isiyokuwa na taarifa rasmi za kiserikali au mwandishi mwingine anaamua kuachakuandika makala au habari ya eneo lile alilokuwa amekusudia kuliandikia ili aweze kuubadilisha umma. Nimalizie kwa kuwataka hao maofisa habari wanaokalia habari waache tabia hiyo, wabadilike na waige mfano maofisa habari wenzao ambao ni Shy Rose Banji wa Benki ya Makabwera(NMB), na Badra Masoud wa Tanesco na wengine wachache ambao kwakweli hawa ni maofisa habari hao ni wachapakazi, wanajiamini kitaaluma na katika ofisi zozote wanapoenda kufanyakazi mchango wao unaonekana hata kwa watu wasio na taaluma ya habari. Mfano hai ni kipindi kile Banji na Badra katika nyakati tofauti walivyowai kushika wadhifa wa Afisa Uhusiano wa DAWASCO , sote tuliwashuhudia maofisa hao walivyokuwa wakichapakazi yao na kutoa taarifa za kwa umma bila upendeleo na hadi sasa wamekuwa wakifanya hivyo.Igeni mfano wao. Nimalizie kwa kuwaasa wale maofisa habari wanaokalia habari na wasiotaka kutoa ushirikiano ,wazingatie funzo walilopewa na Dk.Mkangara kwani kama wasipotaka kubadilika ipo siku viongozi wao ambao wanataka umma upewe taarifa watawachoka na watawaondoa kwenye hizo nafasi na kuwaweka maofisa habari wasiowababaishaji ili waweze kushika nyadhifa hizo. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika 0716 774494 www.katabazihappy.blogspot.com Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Juni 14 mwaka 2012.

NG'UMBI AKIMBILIA MAHAKAMA YA RUFAA

Na Happiness Katabazi ALIYEKUWA mgombea Ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), Hawa Ng’umbi amewasilisha hati ya kusudio la nia ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa nchini, akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambayo ilitupilia mbali kesi yake ya uchaguzi ambayo ilikuwa ikipinga ubunge wa mbunge wa jimbo hilo John Mnyika(Chadema). Nia hiyo iliwasilishwa Mahakama ya Rufaa na wakili wa Ng’umbi , Issa Maige kwa njia ya maandishi ikiwa ni siku chache baada ya Jaji wa Mahakama Kuu Upendo Msuya kutupilia mbali kesi ya uchaguzi Na.107 ya mwaka 2010 iliyofunguliwa na Ng’umbi dhidi ya Mnyika. Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima jana, Ng’umbi alithibitisha kuwasilisha kusudio hilo la kukata rufaa na kwamba tayari nakala ya kusudio hilo imeishapelekewa Mnyika. Mei 24 mwaka huu, jaji Msuya alitoa hukumu ya kesi ya kupinga ushindi wa Mnyika iliyofunguliwa na Ng’umbi ambapo jaji huyo aliitupilia mbali kesi hiyo kwa maelezo kuwa madai ya Ng’umbi dhidi ya Mnyika ambayo yalikuwa ni kuiomba mahakama itamke kuwa uchaguzi wa Jimbo la Ubungo ulikuwa ni batiri kwasababu haukuwa huru na haki, taratibu za uchaguzi zilikiukwa kwani kuna baadhi ya fomu hazikujumlisha matokeo, pia Mnyika aliingiza Laptop kwenye chumba cha kuhesabia kura na kwamba alizitumia laptop hizo kujiongezea kula, Mnyika aliingiza watu watano katika chumba cha kujumlishia kura wakati watu hao hawakuwa na kibali cha kuingia ndani ya chumba hicho,pia Mnyika alimtolea maneno ya alimkashifu kwa kumita fisadi kwani alipokuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake(CWT) Kinondoni, aliuza kifisadi nyumba za jumuiya hiyo na kwamba kuna baadhi ya kula zimeongezeka, halishindwa kuleta ushahidi wa kuthibitisha. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Juni 14 mwaka 2012.

MAHALU ANA HATIA-SERIKALI

Na Happiness Katabazi UPANDE wa Jamhuri katika kesi wizi wa Euro milioni mbili inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin wamiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, iwaone washitakiwa hao wana hatia kwa sababu washitakiwa wameshindwa kuleta ushahidi mathubuti ambao unaonyesha hawakutenda makosa hayo. Ombi hilo la upande wa Jamhuri limewasilishwa kwa maandishi na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Ben Lincoln na mawakili wa serikali Vicent Haule na Ponsian Lukosi ikiwa ni utekelezaji wa amri ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mugeta aliyoitoa kwa pande zote katika kesi hiyo Mei 16 mwaka huu, ambapo alizitaka pande zote ziwasilishe maombi hayo ya kuwaona washitakiwa wana hatia au la. Kwa mujibu wa ombi hilo la upande wa Jamhuri ambalo gazeti hili inayo nakala yake, wakili Lincoln anaiomba mahakama hiyo iwakute na hatia washitakiwa wote wawili yaani Mahalu na Grace Martin kwasababu upande wa jamhuri umeweza kuleta mashahidi saba, vielelezo ambavyo ni nyaraka mbalimbali ambavyo vimethibitisha washtitakiwa hao wanaokabiliwa na makosa sita ilikiwemo kosa la kula njama, wizi wa Euro milioni mbili ,kugushi vocha za manunuzi ya jengo la Ubalozi,kutumia risiti za manunuzi kuidanganya serikali,kuisababishia serikali hasara ya Euro milioni tatu kuwa walitenda makosa hayo. Wakili Lincoln alidai kuwa wakati Mahalu akitoa utetezi wake alishindwa kutoa ushahidi mbadala ambao ungeonyesha ni kweli serikali ya Tanzania ilimruhusu anunue jingo la Ubalozi kwa njia ya mikataba miwili na kwa maana hiyo ameshindwa kuipangua hoja ya upande wa jamhuri ambayo inadai kuwa serikali haikuwa ikifahamu wala haikumpa idhini Mahalu ya kununua jengo hilo kwa njia ya mikataba miwili kitendo ambacho kina kwenda kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2001 ambayo inakataza mali yoyote ya serikali isinunuliwe kwa njia ya mikataba miwili na endapo kutakuwa na ulazima wa kununua mali ya serikali kwa njia mikataba miwili ni lazima ipatikane kwanza idhini toka katika mamlaka husika. Wakili Lincoln alidai kwa mujibu wa shahidi wa pili wa upande wa Jamhuri ambaye ni wakili wa Italia ambaye ndiye asiyesaini mkataba wa manunuzi wa jengo hilo Marco Papi ambao mkataba huo ulionyesha jengo hilo lilinuliwa kwa thamani ya Euro milioni moja na kwamba huo mkataba ndiyo unatambuliwa kisheria na ule mkataba wa pili ambao unaonyesha jengo hilo limenunuliwa kwa jumla ya thamani ya Euro milioni tatu autambuliki kisheria na endapo mtu atanunulia kitu au jengo kwa mtindo wa mikataba miwili serikali ya Italia itamhesabu mtu huyo amekwepa kodi. “Na katika utetezi wao washitakiwa hao wawili wameshindwa kutoa ushahidi mbadala unaopinga ushahidi huo wa Papi pamoja na kutoa vielelezo vinavyoonyesha mamlaka au sheria za Tanzania ziliwaruhusu kutenda tendo hilo la kununua jengo hilo kwa njia ya mikataba miwili na kwa sababu hiyo ndiyo maana tunaiomba mahakama iwaone wanahatia”alidai wakili Lincoln. Wakili Lincoln akiuchambua ushahidi wa shahidi wa pili wa upande wa utetezi, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ,wakili huyo alidai Mkapa alieleza kuwa yeye aliruhusu jengo hilo linunuliwe na kwamba malipo yalipwe kupitia akaunti mbili tofauti lakini Mahalu alishindwa kumweleza Mkapa kuwa jengo lile litanunuliwa kwa njia ya mikataba miwili. “Kwa sababu hizo tulizozitaja hapo juu, tunaiomba mahakama hii tukufu iwaone washitakiwa hao wanatia na iwahukumu vifungo kama sheria inavyosema na wairudishie serikali jumla ya Euro milioni mbili ambazo waliziiba kwa kisingizio cha kununua jengo la ubalozi kwa njia ya mikataba miwili”alidai Lincoln”alidai Lincoln. Kesi hiyo itakuja kutolewa hukumu na Hakimu Mfawidhi Mugeta, Julai 11 mwaka huu. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Julai 13 mwaka 2012.

MAHALU HANA HATIA-MAWAKILI

Na Happiness Katabazi ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu na Meneja Utawala na Fedha, Grace Martin wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, isiwaone wanahatia katika kesi ya wizi wa Euro Milioni tatu kwasababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi wa kutenda makosa hayo. Balozi Mahalu aliwasilisha maombi hayo ya jana mchana kupitia mawakili wake Mabere Marando, Beatus Malima ,Alex Mgongolwa na Cuthbert Tenga kwa njia ya maandishi mahakamani hapo kama walivyoamriwa kufanya hiyo na Hakimu Mfawidhi Ilvin Mugeta Mei 16 mwaka huu, ambapo hakimu huyo alizitaka pande zote kuwasilisha jana majumuisho hayo ya kuiomba mahakama iwaone washtakiwa wana hatia au la. Kwa mujibu wa maombi hayo ya Mahalu ambapo Tanzania Daima ina nakala yake, mawakili wamewaanza kuikumbusha mahakama kuwa washtakiwa hao wanakabuliwa na makosa sita likiwemo kosa lakula njama, wizi wa Euro milioni mbili ,kugushi vocha za manunuzi ya jengo la Ubalozi,kutumia risiti za manunuzi kuidanganya serikali,kuisababishia serikali hasara ya Euro milioni tatu. Kwa mujibu wa hoja zao tano muhimu ambazo wamezitumia kuwasilisha ombi hilo, hoja ya kwanza mawakili hao wa utetezi Serikali ya Tanzania ilimruhusu Mahalu kununua jengo la ubalozi kwa njia ya mikataba miwili kwa bei ya Euro 3,098,741.58 na kwamba Mahalu alileta vielelezo kadhaa ambavyo viliweza kuithibitishia mahakama hiyo kuwa serikali ililidhia jengo hilo linunuliwe kwa njia ya mikataba miwili na kwa thamani hiyo…na kwamba hakuna ushahidi wowote ulioletwa na upande wa Jamhuri kuwa washtakiwa walifanya siri na kutenda kosa la wizi”alidai wakili Marando. Hoja ya pili, mawakili hao wanadai kuwa upande wa Jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi unaonyesha muuzaji wa jengo hilo la ubalozi hakupokea fedha za manunuzi ya jengo hilo ambazo ni Euro milioni tatu..na kwamba wameshindwa kuleta ushahidi ambao ungethibitisha muuzaji huyo wa jengo hakulipwa kiasi hicho cha fedha na washtakiwa. Aidha hoja ya tatu ni kwamba ripoti tatu za thamani ya majengo zilizoandaliwa na Wizara ya Ujenzi, muuzaji na ubalozi wa Tanzania nchini Rome hazikuandika jengo hilo lilikuwa na thamani ya chini ya Euri milioni tatu, kwani ripoti zote ziliandika jengo hilo lilikuwa na thamani ya zaidi ya Euro milioni tatu na kwamba upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi unaonyesha unaonyesha wakati huo jengo linanunuliwa lilikuwa na thamani ya kiasi gani na kwa maana hiyo jamhuri ilikuwa haifahamu thamani ya jengo hilo wakati serikali inalinunua. “Hoja ya tano sisi tunadai kuwa upande wa Jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi ambao ungeonyesha nani ni mmiliki wa akaunti mbili ambazo Euro milioni tatu ambazo zilitumwa na ubalozi wa tanzania nchini Rome kwenye akaunti hizo: “Kwa hoja hizo tano tulizozitaja hapo juu, tunaiomba mahakama hii iwaone washtakiwa hawana hatia kwasababu upande wa jamhuri wameshindwa kuleta ushahidi ambao utaishawishi mahakama iwaone washtakiwa hao wana hatia katika makosa wanashitakiwa nayo” alidai wakili Marando. Hata hivyo mahakama hiyo Julai 11 mwaka huu, ndiyo itakuja kutoa hukumu katika kesi hii ambayo ilifunguliwa rasmi mwaka 2007. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Julai 12 mwaka 2012.

MKUTANO WA MAZINGIRA UTUBADILISHE TABIA

Na Happiness Katabazi MAKAMU wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal ataliwakilisha taifa katika mkutano wa dunia wa mazingira utakaofanyika Rio De Jeneiro nchini Brazil kuanzia Juni 20-22 mwaka huu. Wataalamu wa masuala ya Geographia wanaeleza mkutano huo maarufu kama mkutano huo , utatoa fiursa kwa viongozi wa mataifa mbali mbali kujadili na kufikia muafaka kuhusu masuala ya mazingira na kutoa dira ya nini kifanyike baada ya mkutano huo kumalizika kufanyika. Itakumbukwa kuwa Juni 5 kila mwaka Watanzania huungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, na kwa mwaka huu tayari Tanzania ilishazindua maazimisho hayo katika mikoa mbalimbali. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa,hivi karibuni alinukuliwa akisema maadhimisho hayo ni kumbukumbu ya mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira uliofanyika mwaka 1972 mjini Stockholm, Sweden. Dk.Huvisa alisema kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni ‘Uchumi Kijani; Unakuhusu’. Anasema ujumbe huu unahimiza kuwajibika katika uzalishaji endelevu kwa kupunguza uzalishaji wa gesijoto hususani gesi ,mkaa na matumizi bora ya rasilimali. Anasema kitaifa ujumbe unaoongoza maadhimisho hayo ni hifadhi ‘Hifadhi Mazingira; jikite kwenye uzalishaji endelevu’. Kwa mujibu wa waziri huyo wa mazingira, changamoto za mazingira zinazoikabili nchi ni nyingi, mojawapo ni zaidi ya asilimia 60 ya nchi inakabiliwa na hali ya jangwa na ukame. Anasema changamoto nyingine ni kwamba takriban hekta 220,000 za misitu huangamia kila mwaka kwa mahitaji ya nishati, kilimo kisicho endelevu na kwa mahitaji ya ujenzi, uwezo wa malisho katika mikoa mingi umezidiwa na wingi wa mifugo hivyo kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira pamoja na uvamizi katika vyanzo vya maji. Kwa maelezo hayo hapo juu, kwanza nampongeza Dk.Huvisa uthubutu wake wa kuanika ukweli wa vyanzo vya uharibu wa mazingira unavyoathiri maeneo fulani katika taifa letu na kushauri nini kifanyike. Hakuna ubishi kuwa kadri siku zinavyozidi kwenda uhalifu wa mazingira umekuwa ukishika kasi hapa nchini kana kwamba waliopewa dhamana ya kuakikisha wanawathibiti wahalifu hao wameacha kazi, au wale wanaojihusisha na vitendo vya uharibu huo wa mazingira wanafikiri madhara ya uharibu wa mazingira hautakuja kuwaathiri kwa nanma yoyote ile. Ukitembelea baadhi ya maeneo ya mikoa ya nchi hii hivi sasa na ukilinganisha na miaka iliyopita utabaini kuwa tayari kuna wananchi au viwanda vimejihusisha na utendaji kazi katika maeneo hayo ambayo matokeo yake yanasababisha ukame, mikiti kukaukwa na kukatwa kwasababu ya shughuli hizo za binadamu ambazo zimesababisha uharibifu wa mazingira. Ukitembelea mito inayotililisha maji hapa jijini na mfano mzuri ni Mto Ng’ombe ,Bonde la Mto Msimbazi na mingine utaona kuna baadhi ya watu wamejenga makazi yao kando kando ya mito hiyo na wengine wamekuwa wakitupa takataka katika maeneo hayo na wengine wametililisha mabomba ya maji machafu yanayotoka kwenye vyoo vyao kuingia kwenye mito hiyo ili kuweza kuhebuka gharama za kulipia magari ya kuja kuchonya maji taka katika majumba yao. Hali hiyo imekuwa ikisabisha nyakati za mvua , mito hiyo kufurika sana na maji yanayopita kwenye mito hiyo ulazimika kupita kwa shida hali inayosababisha maji hayo kupita kwenye mkondo wake maji ambapo mkondo huo mara nyingine ndiyo nyumba za watu waliojenga mabondeni na mwisho wa siku Desemba 21 na 22 mwaka huu, nyumba za watu na wananchi kadhaa kupoteza maisha kwa kutoka na mvua kubwa iliyonyesha. Hivyo mkutano huo wa mazingira , Tanzania inayoenda kuwakilishwa na Dk.Bilal tuutumie vizuri kwa kuwasilisha hoja mathubutu na kuibua mjadala wenye mashiko sambamba na kila mwananchi kuanza kuchukia kutenda matendo yanayoleta uharibu wa mazingira. Hivi sasa kunazana ya kijinga iliyotawala katika vichwa vya baadhi ya watu hapa nchini kwamba kutunza mazingira ni kwa wale waliojariwa kuwa na vipato vikubwa kutengeneza bustani za mauwa ya kila aina majumbani kwao. Kwani Taifa hili na dunia hii ni yetu sote hivyo yanapotokea madhara ya uhalifu wa mazingira,anga tunaoathirika ni sisi binadamu tunaondelea kuishia humu duniani na vizazi vyetu. Na mataifa maskini pia yatumie mkutano wa Rio De Jeneiro kuakiskisha yanasimama kidete kuyakemea mataifa tajiri ambayo yamekuwa yakituhumiwa kuwa ni chanzo cha kusabisha uhalifu wa mazingira katika anga kwani kila kukicha yamekuwa yakitengeneza vifaa na kemikali ambazo wataalumu wa masuala ya mazingira wamedai yanasababisha mabadiliko ya tabia ya nchi. Nimalizie kwa kuwauliza wasomi wa masuala ya Geografia na wadau wa mazingira na taifa kwa ujumla wamejipangaje na mkutano wa mazingira duniani wa Rio De Jeneiro-Brazil ? Naomba kutoa hoja. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania 0716 774494 www.katabazihappy.blogspot.com Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Juni 10 mwaka 2012.

WAHUNI NDIYO WALIOFANYA UHALIFU ZANZIBAR

Na Happiness Katabazi JUNI 26-27 mwaka huu, huko kwenye Jiji la Zanzibar viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu maarufu kwa jina la Uamsho, walileta katika mkoa wa mjini Magharibi ,Unguja iliyosababisha uvunjifu wa amani na kuchoma makanisa mawili , maduka ya watu kuvunjwa na mali zao kuibiwa kwa madai kuwa wanapinga Muungano. Taasisi hiyo imeanzishwa kwa madhumuni ya kidini, lakini hivi sasa viongozi wake wanaonekana wazi kuyaacha madhumuni hayo na kubeba ajenda za siasa. Awali ya yote kwanza nataka ieleweke wazi waliofanya uhuni,uhalifu huu sio Wazanzibari wote na wala siyo waislamu kama baadhi ya watu wanavyotaka kuamini waliofanya uhuni ule ni wazanzibar na waislamu wote. Ni genge la waharifu tu ambalo limevaa sura ya jumuiya ya kidini ndiyo limefanya uhalifu huo kwa kuwa limefanya uhalifu na linataka liiungwe mkono likajaribu kutaka kuonyesha kuwa ni waislamu na wazanzibar wote wapo nyuma yao na wanakerwa na muungano,jambo ambalo si la kweli na ninawashukuru wale viongozi wa dini ya Kiislamu waliojitokeza kukanusha hilo na pia kuwashukuru viongozi wa dini ya Kikristo kuwa na moyo wa uvumilivu kwa vurugu hizo. Ni wahuni hao ambao uenda wametumwa na kupewa ujira na maadui zetu wanaotuonea wivu na amani tuliyonayo ili waanzishe vurugu mwisho wa siku amani yetu tuliyoirinda kwa miaka mingi itoweke. Kwa sababu haingii akilini kabisa jumuiya ya kidini ambayo moja ya jukumu lake ni kuamasisha amani ndiyo inakuwa mstari wa mbele kutofuata taratibu za kisheria kudai hayo madai yao matokeo yake wanatumia njia za kihalifu kudai madai yao jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi. Nasisitiza waliofanya uhalifu ule ni wahuni kwasababu wameshindwa kuheshimu mamlaka iliyopo duniani kwani hata vitabu vya dini vinatutaka tuheshimu mamlaka zilipo duniani. Hivi hii Jumuiya ya Uamusho ni Muungano kweli ndiyo unawakera hadi wanachoma makanisa na maduka na kuleta vurugu kweli? Kwa sisi tuliofika Zanzibar zaidi ya mara nne tumeweza kushuhudia baadhi ya vitendo vichafu ambavyo vinapingwa na vitabu vya dini.Mfano vitendo vya watu wa jinsi moja kujamiana yaani vitendo vya ushoga na usagaji,matumuzi ya dawa za kulevya.Licha matendo hayo pia hata huku Tanzania Bara yapo. Kwahiyo hayo matendo machafu hayaikeli hiyo jumuiya ya uamsho?Maana jumuiya hiyo ni ya kidini na inajumuku la kuyakemea kwa nguvu zote lakini hatuisikii ikielekeza nguvu zake zote kukemea uchafu huo ambao unaipaka matope Zanzibar yetu. Binafsi sipingi Muungano wetu usijadile,napenda ujadiliwe kwa amani na wanaojadili wawe na nia safi mioyo mwao na watoe maoni yao kwa njia ya amani tu bila vurugu.Na kero za Muungano kisiwe chanzo cha kuleta vurugu. Tunapaswa kujiuliza kwanza hivi huo Muungano umeanza kuikera kwa sana hivi karibuni jumuiya hiyo hadi wafikie kufanya uhalifu huo? Tuiulize hiyo jumuiya njia ile ya vurugu ya kupinga muungano wiki iliyopita,ndiyo imewasaidia kutatua shida yao? Jibu ni kwamba tatizo lao halijatatuliwa. Nilichokiona mimi njia hiyo haramu waliyoitumia sana sana imewafanya wajikute wakiangukia kwenye mikono ya dola kwa kufunguliwa kesi mahakamani na kutokana na hali hiyo waliofikishwa mahakamani ndiyo wameanza kuwa watumwa wa mahakama hadi pale mahakama itakapotoa maamuzi yake. Kwa wale tuliofika Zanzibar, tutakubalina kuwa eneo waumini wa dini ya Kiislamu ndiyo wanaoishi kwa wingi huko.Lakini kuishi kwao huku kwa wingi hakuwazui wakristo kuishi wala kufanyakazi na kushirikiana pamoja katika masuala ya kijamii na kiserikali. Wazanzibar ni wenzetu na Muungano wetu utabaki kuwa ni wa kipekee hapa duniani kwani tangu uundwe haujawahi kuvunjika wala kuleta maafa makubwa. Lakini wakati machafuko hayo yametokea siyoni wanawake,vyama vya siasa na vile vyama vya kiraia vikijitokeza kulaani vurugu hizi,wamekaa kimya utafikiri Zanzibar ikitokea maafa makubwa hawataathirika.Makundi hayo yamekuwa mabingwa ya kuchangia mada za kisiasa,ufisadi na maandamano lakini kwenye mambo kama haya yanayoatharisha usalama wa wenzetu kule Zanzibar wamekaa kimya.Inashangaza sana. Napenda kuisa Idara ya Usalama wa Taifa(TISS), Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi(JWTZ), bila kufanya papara wachunguze kwa undani kuhusu chanzo cha vurugu hizo na mwisho wa siku waweze kubaini Je ni kweli hao viongozi wa jumuiya walifanya vurugu hizo kwa utashi wao au kuna watu wanawatumia kuanzisha vurugu hizo ili mwisho wa siku Zanzibar na Tanzania Bara tujikute tukingia kwenye vita ya udini na uzanzibari na utanzania Bara. Maana tayari tumeishapata funzo toka kwenye nchi ambazo ziliwahi kukumbwa na vita,baadhi ya mataifa yenye fedha yalikuwa yakiwatumia baadhi ya wananchi wanayoishi kwenye taifa wanalokusudia kulisambaratisha au kumng’oa rais aliye madarakani kuleta chokochoko na mwisho wa siku wakafanikiwa. Na matokeo yake wanaokuja kuteseka ni sisi wakina mama na watoto. Naamini mfumo wa upelelezi wa hapa nchini bado ni thabiti licha ya hivi sasa umekuwa ukikosolewa na wakosoaji kuwa umelegalega,ila binafsi naamini bado upo imara. Mwisho nimalizie kwa kusema ni Jeshi la Polisi hapa Tanzania Bara na Zanzibar ndiyo wamekuwa wakivilea vikundi hivyo ambapo hapa Dar es Salaam, pale viwaja vya Bakhresa Manzese kila siku jioni ndiyo wamekuwa wakitoa miadhara na wakati mwingine mkihadhara hiyo imekuwa ikitoa maneno ya kukashifu dini ya Kiislamu au Kikristo na polisi wala hawachuki hatua kwani nakumbuka waandishi wa habari nikiwemo mimi miaka ya nyuma tulishaandika habari za kulitaka jeshi la polisi kudhibiti matamshi yanayotolewa katika mihadhara hiyo bila mafaniko. Na Wahenga walisema ‘Mazoea ujenga tabia’. Mungu ibariki Tanzania ,Mungu Ibariki Afrika 0716 774494 www.katabazihappy.blogspot.com Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Juni 7 mwaka 2012.

MBUNGE WA CCM KORTINI KWA RUSHWA

Na Happiness Katabazi MBUNGE wa Jimbo la Bahi(CCM), Omary Ahmed Badwel(43) jana alijikuta akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), kwa makosa ya rushwa ya shilingi Milioni moja toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Jonathan Liana. Wakili wa Takukuru,Janeth Machullia na Ben Lincoln walidai mbele ya Hakimu Mkazi Faisal Kahamba kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na makosa mawili ya rushwa. Wakili Machullia alidai kuwa kosa la kwanza ni la rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007, kuwa kati ya Mei 30 na Juni 2 mwaka huu katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam , Badwel akiwa ni Mbunge wa Bahi na Mjumbe Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) na wakati huo akiwa ni ofisa wa serikali kwa maana ya sheria ya Takukuru, alitenda kosa la kushawishi ili apewe rushwa ya jumla ya Shilingi milioni nane toka kwa Sipora Liana ili kiasi hicho cha fedha aweze kuwapelekea wajumbe wenzake wa Kamati hiyo ya Bunge ili waweze kuipitisha ripoti ya fedha ya mwaka 2011/2012 ya Halmashauri hiyo. Wakili Machullia alidai shitaka la pili ni kwamba kati ya Juni 2 mwaka huu, katika Hoteli ya Peacock,mshitakiwa akiwa na nyadhifa zake zote hizo alipokea rushwa ya Milioni moja kutoka kwa Liana ili aweze kwenda kuwashawishi wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kuipitisha ripoti ya fedha ya Halmashauri ya Mkuranga huku akijua kufanya hivyo ni kosa. Hata hivyo mshitakiwa huyo anayetetewa na wakili wa kujitegemea Mpare Mpoki alikanusha mashitaka yote na wakili wa Machullia alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika. Kwa upande wake Hakimu Mkazi Kahamba alisema ili mshitakiwa apate dhamana ni lazima awe na wadhamini wawili wa kuaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya shilingi milioni nne na kusalimisha hati zao za kusafiria mahakamani, sharti ambalo lilitimizwa na mshitakiwa huyo na akapata dhamana. Hakimu Kahamba alialishisha kesi hiyo hadi Juni 18 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya kutajwa na kupangiwa tarehe ya kuja kumsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Juni 5 mwaka 2012.

VIONGOZI ACHENI TABIA HII

Na Happiness Katabazi BABA wa taifa aliwahi kusema ‘ukweli una tabia moja nzuri sana kwani auchagui rafiki wala adui’. Na kwa mara yingine leo nalazimika kutumia nukuu hilo kwasababu mada yangu nitakayoijadili leo kwa asilimia kubwa itagemea sana kuhusu suala zima la ukweli. Itakumbukwa kuwa Mei 29 mwaka huu, mwili wa gwiji la uendeshaji wa mashitaka nchini ambaye alikuwa na wadhifa wa Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha uendesha mashitaka na pia ndiye aliyekuwa Msimamizi mkuu wa uendeshaji kesi zenye maslahi kwa umma, Stanslaus Boniface Makulilo (44),uliagwa na kuzikwa katika nyumba yake ya milele pale katika Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam. Jamii ya wasomi wa fani ya sheria wakiwemo majaji,mahakimu, mawakili wa serikali na kujitegemea na wananchi wengine wa kada tofauti walishiriki katika mazishi mazishi hayo na wengi wao walikuwa na huzuni na wengine kushindwa kujizuia na kujikuta kila mara wakibubujikwa na machozi kutoka na majonzi ya kumpoteza gwiji hilo la mashitaka ambalo lililikuwa ni mwiba mkali,ambaye alikuwa akiisaidia kwa hali na mali kitaaluma mahakama kufikia maamuzi ya haki na aliyekuwa ametanguliza maslahi ya taifa kwanza. Binafsi niliudhulia msiba huu mwanzo hadi mwisho yaani kuanzia siku aliyokufa yaani Mei 27 alfajiri katika Hospitali ya Regency pale nyumbani kwa mdogo wa marehemu Dk.Alexander Makulilo tangu hadi siku Mei 29 siku tuliyoenda kumzika Boniface makaburi ya Kinondoni. Ni kweli mimi nimwandishi wa habari za kimahakama na nilikwenda msibani kwanza kama mfiwa kwasababu Boniface na mawakili wengine wa serikali na kujitegema kila siku tumekuwa tukifanya nao kazi pamoja,pia nilikwenda msibani pia kama mwandishi wa habari kwaajii ya kutazama na kurekodi matukio yote yaliyokuwa yakiendelea katika msiba huo ili niuabarishe umma. Ama kwa hakika kwa siku zote hizo miongoni mwa viongozi wa chache ambao nilikuwa nikiwashuhudia wakifika msibani hapo na wanakaa hadi usiku ni Mwanasheria Mkuu wa serikali Fredrick Werema na Naibu wake George Masaju ,Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Eliezer Feleshi,Mkuu wa Chuo cha Sheria(Law School) Gerad Ndika, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sheria(UDSM),Profesa Paramaganda Kabudi ,Mbunge wa Kigoma Mjini,Peter Serukamba,maofisa wa jeshi la polisi ,waandishi wa habari za mahakamani mawakili wakujitegemea na wale wa serikali na kada nyingine na siku ya mazishi kule makaburini ndiyo Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe alikuja. Kwanza naomba ieleweke wazi kuwa wale wote ambao hawakuhudhulia msiba wa Boniface hawajatenda kosa la jinai na wala siyo deni.Na pia kuzikwa na watu wengi siyo kwenda mbinguni. Lakini mimi binafsi na baadhi ya watu walioudhulia msiba huo tumebaki tukijiuliza ni kwanini viongozi wa juu kabisa wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal,Waziri Mkuu Mizengo Pinda.Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye, Katibu Uenezi wa Chama Cha Demokrasi Chadema, john Mnyika na vyama vingine na vile vyama vya kiraia, wale wapambanaji wa ufisadi walishindwa kabisa kuudhulia msiba huo au hata kutuma salamu za pole kutokana msiba wa Boniface? Ieleweke wazi kuwa tangu Kikwete apishwe kuwa rais wa taifa hili Mei 21 mwaka 2005, serikali yake ndiyo imeandika historia ya kuwafikisha vigogo mahakamani kwa kesi mbalimbali na hatua hiyo ilitokana na kelele nyingi zilizokuwa zikipigwa na wananchi zilizotaka watuhumiwa wa ufisadi wa wizi wa fedha za EPA,Richmond,UDA,Shirika la Ndege(ATCL) wafikwe mahakamani haraka.Na walifikishwa mahakamani na DPP-Dk.Feleshi na Boniface na wenzake ndiyo waliokuwa wakiziendesha kesi hizo kwa nguvu zao zote hadi kufikia hatua ya kutishiwa usalama wao na watu wasiojulikana mara kwa mara. Ni huyu Rais Kikwete Pinda na huyo Nnauye na wabunge wengine wa ccm kwa mara kadhaa tumekuwa tukiwashuhudia katika majukwaani wakijinasibu kuwa serikali ya awamu ya nne imefanya mengi ikiwemo kuwafikisha mahakamani vigogo. Ni kweli serikali hiyo hilo imelifanya lakini cha kushangaza viongozi hao kupitia wasaidizi wao wameshindwa hata kuandika taarifa kwa umma kwamba wameupokeaje msiba huo.Ni ajabu sana. Uenda Boniface aina ya mchango wake kwa taifa hili ulikuwa hauthamini na hautiliwi maanani sana na makundi hayo kuliko mchango uliokuwa ukitolewa na watanzania wenzetu kama wasanii na wanasiasa waliotangulia mbele za haki ambao vifo vyao vilisababisha CCM na serikali yake vilijifanya kuonyesha kutaharuki hadi rais Kikwete,Dk.Bilal kwenda kwa zaidi ya mara mbili kwenye msiba mmoja.Katika msiba mmoja ambao sitalitaja jina la marehemu hao, Rais Kikwete na viongozi wenzake licha marehemu hao hata hawakuwa watumishi wa serikali waliofariki mwaka huu waliudhulia tena hadi usiku lakini viongozi hao wakashindwa kutenga hata siku moja kuja kuudhuria msiba wa Boniface. Niwe mkweli kabisa tabia hii imeanza kuwafanya baadhi ya watu kuamini kuwa viongozi wetu wa kisiasa wanachagua misiba ya kwenda.Wakifikiri msiba fulani kama wa Boniface ambao ulisheheni wasomi wa sheria hawatapa upenyo wa kujigenga kisiasa hawaudhurii wala kutoa salamu za pole na msiba fulani wakishapiga hesabu wakabaini wakiudhulia msiba huo watapata upenyo wa kujitangaza kisiasa basi haraka sana wanaudhuria msiba huo na kutoa salamu za pole. Hii ni tabia isiyopendeza na kukatisha tamaa watendaji hususani wale wa serikali ambao ni waadilifu na wachapakazi kwa viongozi hao kwani miongoni mwao waliniuma sikio msibani wakisema msiba wa Boniface ndiyo ungekuwa ni msiba wa msanii basi Ikulu ingeamia katika msiba huo na kutoa misaada mingi.Kauli kama hizi hazipendezi kwani zinaonyesha kutolewa na wafanyakazi wa serikali walioanza kukatishwa tamaa na viongozi wao.Badilikeni. Hivi katika hali ya kawaida leo nyie viongozi hao nyie vyama vya upinzani,CCM na wanaharakati na nyie baadhi ya wabunge mliokuwa mmejipambanua kupambana na ufisadi mnaweza kuwa na jeuri ya kusimama majukwaani na kutuleeza nini kuhusu kesi za ufisadi, wakati hata kutoa salamu za pole kwa marehemu Boniface aliyekuwa akiongoza dawati la kuendesha kesi zilizokuwa na maslahi ya umma mmeshindwa?Kutwa kutoa matamko kuhusu ufisadi, maandamano na kupikiana majungu na kufukuzana kazi na kusuka makundi ya kugombea urais mwaka 2015. Ndiyo maana kuna baadhi ya majaji ,maofisa wa serikali waliniuma sikio wakiambia kuwa miongoni mwao muda mrefu walichaacha kuudhulia sherehe za kitaifa kwani wao wakifa vingozi hao wa juu wa serikali hawaudhulii madhishi yao. Boniface alipenda sana kazi ya Uwakili wa Serikali na hasa kuendesha mashtaka.Alikuwa tayari kuendesha kesi yoyote bila woga.Alikuwa msaada kwa mahakama katika kufikia maamuzi ya haki. Hii inadhiirika kwa kusoma hukumu na maamuzi ya mahakama ya mashauri ambayo aliiwakilisha serikali. Mfano mzuri ni hukumu ya Mahakama ya Rufaa Na. 250/2006 katika kesi ya Silivester Hillu Dawi na wenzake dhidi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ambapo jaji Edward Rutakangwa alimwelezea Boniface aliyekuwa akiiwakilisha serikali katika shauri hilo kuwa ni mkweli na mpenda haki. Jaji Rutakangwa aliweka kanuni ya washitakiwa wanaokabiliwa na shitaka kuchangia nusu ya thamani ya mali inayohusika shtaka husika ili kupata dhamana badala ya kila mshitakiwa kutoa nusu ya thamani hiyo. Kesi nyingine ni ya Mwenyekiti wa Timu ya Simba, Ismail Aden Rage dhidi ya Jamhuri katika Mahakama ya Rufaa Na. 286/2005, ambapo Jaji Mroso alieleza wazi kuwa Jamhuri iliyokuwa ikiwakilishwa na Boniface,ilikuwa imewakilishwa na mtu mwenye uwezo na msaada pale alipotamka. Kwa hukumu hizo mbili,ni wazi zimeuthibitishia umma kuwa hata Mahakama ya Rufaa Tanzania ilikuwa ikiheshimu na kumtambua Boniface kuwa ni wakili mahiri wa serikali.Na sisi watu tunaofikiri sawa sawa na wale wasomi wa sheria tutaendelea kuuenzi mchango wa marehemu na kumkumbuka daima katika tasnia ya sheria nchini. Mungu ailaze roho ya Boniface mahali pema peponi.Amina. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika 0716 774494 www.katabazihappy.blogspot.com Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Juni 3 mwaka 2012.