HEKO SERIKALI KUDHIBITI MFUMUKO WA BEI

Na Happiness Katabazi WAHENGA waliwahi kusema ‘Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni” Januari 10 mwaka huu, gazeti hili lilichapisha makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “Ugumu wa maisha utatuangamiza”. Ndani ya makala hiyo nililamikia sana ugumu wa maisha na upandaji wa bei za vyakula. Leo nimeamua kutumia msemo huo ambao naamini utasaidia kuunga mkono hoja yangu nitakayoijadili leo na makala yangu iliyochapishwa Januari 10 mwaka huu. Leo nitajadili kuhusu upunguzwaji wa bei ya bidhaa ya vyakula hapa nchini katikia masoko mbali hivi sasa ukilinganisha na kipindi cha mwanzoni mwa mwaka huu. Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa mwaka huu bei ya bidhaa za vyakula masokononi na madukani zilipanda kwa kasi hali iliyosababisha sisi waandishi wa habari kuandika makala za kukerwa na upandwaji huo wa bei na pia baadhi ya wananchi nao walipaza sauti kuonyesha kuumizwa na hali hiyo. Lakini kwa sisi wanawake ambao hasa ndiyo mashuhuda wa kuu wa upandaji na ushukaji wa bei hizo ambao ndiyo tunaoenda masokoni na madukani kununua bidhaa hizo hivi sasa mimi binafsi nadiriki kusema hali nitofauti kwani bei za nafaka kama Mchele,Unga,Maharage na Sukari zimeshuka. Bei za nafaka hizo zilipanda kwa kiasi kikubwa kilomoja ya mchele ilikuwa ni shilingi 2300-2500,Maharage Kg.sh 2,000,Unga Kg 1,000,sukari kg 2000-2500.Na itakumbukwa Sukari licha ya kupanda bei pia iliadimika sana na ikawa inasafirishwa nje ya nchi kwa magendo. Kwa wiki moja sasa nikiwa nipo likizo ya kujiandaa na mitihani nimepata fursa ya kutembelea soko la Kawe,Buguruni na Tandale na kuona bei za bidhaa hizo zikiwa zimeshuka hali iliyosababisha nishikwe na butwaa na kulazimika wauzaji ni kitu gani kimesababisha washushe bei. Ila muuzaji alitoa sababu yake wengine walisema serikali ililazimika kutumia mamlaka yake kimya kimya bila kufafanua kwa kuwataka wauzaji wakubwa wa bidhaa hizo washushe bei na wasafirishwe kwa wingi bidhaa hizo ili zipatikane kwa wahitaji tena kwa wakati na wengine. Kwanza kabisa napongeza hatua zote za wazi na za siri zilizochukuliwa ama na serikali,wauzaji wa kubwa wa bidhaa hizo hadi leo hii bei za nafaka hizo zimeshuka. Leo nii mchele kilo moja unauzwa kuanzia Sh 1,400-1,500,1,600 hadi 1,800.Sembe Sh 900,800 na maharage sh 1,500,Sukari sh 2,000. Hakika ili ni jambo jema sana kama bei ya bidhaa inapanda kwa ghafla na kisha wafanyabiashara hao hao wanakubali kushusha bei ya bidhaa hizo hizo. Hakuna haja ya kufichana ilifika mahala kupika wali katika baadhi ya familia ilikuwa ikionekana ni anasana na familia hiyo ilihesabika kuwa ina uwezo wa kifedha. Kwa uhalisia huo hapo juu leo nataka kuwaasa wanahabari wenzangu,wananchi na wale wanasiasa ambao kila kukicha wamekuwa wakipigia kelele kuhusu gharama za vyakula kupanda na kushutumu serikali,wabadilike na wawe na tabia ya kukosoa mambo fulani wanayoyaona ni vikwazo kwa taifa na pindi mambo hayo yatakapopatiwa ufumbuzi iwe na serikali au taasisi yoyote ya kirahia pia wawe wanajitokeza kupongeza. Bei za vyakula zimeshuka sisi tuliokuwa mstari wa kwanza kupigia kelele bei zishuke na leo kweli bei hizo zimeshuke, basi tusiogope tena kurudi uwanjani na kuwapongeza wale wote waliosababisha bei hizo zikashuka na huo ndiyo utakuwa uzalendo wa kweli na kuwatia moyo wale wote waliosababisha bei zishuke ili sikunyingine taifa likijakukumbwa na kadhia hiyo waweze kulitatua haraka jambo hilo. Ndiyo maana leo nimeanza makala yangu kwa kunukuu maneno yale ya wahenga yasemayo ‘Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni’. Hivyo ni kweli wananchi tuna haki na tulikuwa na haki ya kuibana serikali kuhusu upandwaji wa bei za bidhaa na leo hii bidhaa hizo zimeshuka bei,hivyo hatuna budi kuipongeza serikali na wafanyabishara wote walioshusha bei nafaka hizo hadi leo hii tunaenda masokoni kifua mbele tena bila woga. Maana zile bei za awali zilikuwa zikitutisha na kutusikitisha mno na kutukatisha tamaa ya maisha. Kwani itakumbukwa kuwa kipindi kile cha uhaba wa sukari na bei ya sukari na kwa kuwa Shida ni mwalimu sisi maskini tulilazimika kuwa tunakwenda kununua tena kwa kuviziwa sukari katika maduka ya Shoprite ,maana katika maduka hayo sukari ilikuwa ikuuzwa bei rahisi na maduka hayo yaliweka kiwango cha ununuaji wa sukari ,kwani walimtaka kila mnunuaji anununue sukari sichini ya Kilo tatu ambapo kilo moja ilikuwa ikiizwa kwa shilingi 1,900. Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika 0716 774494 www.katabazihappy.blogspot.com Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne,Agosti 21 mwaka 2012.

SERIKALI ISOME ZABURI YA 17


Na Happiness Katabazi 

 AGOSTI 9 mwaka huu, Hakimu Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Ilvin Mugeta alitoa hukumu ya kesi ya kihistoria Na.1/2007 ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin kutokana na ushahidi wa upande wa serikali kushindwa kuwatia hatiani.

 Hukumu hiyo inaweza kutafsiriwa kama ni kubwagwa kwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kutokana na hatua ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa Mei 7 mwaka huu, kukubali kupanda kizimbani na kumtetea Mahalu dhidi ya serikali, tukio ambalo ni la kwanza katika historia ya nchi hii. Hakimu Mugeta ambaye alikuwa akionyesha umakini wa hali ya juu wakati akiisoma hukumu hiyo alisema Mahalu na Grace waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka sita.Washitakiwa hao walikuwa wanatetewa na mawakili Mabere Marando, Alex Mgongolwa, Beatus Malima na Cuthert Tenga na upande wa Jamhuri ulikuwa ukiwakilishwa na Ben Lincoln na Vicent Haule toka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Ponsia Lukosi toka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP). Aliyaja makosa hayo kuwa ni kula njama, kutumia nyaraka za manunuzi ya jengo la ubalozi ili kumdanganya mwajiri wao serikali, wizi wa Euro milioni 2,065,827 na kuisababishia serikali hasara. ““Lakini mahakama hii imejiuliza kama serikali ilikubali kulinunulia jengo hilo,ikatoa fedha kwaajili ya ununuzi, ikampatia Mahalu nguvu ya kisheria ya kuendelea na mchakato wa manunuzi, mkataba wa kwanza ulikuwa ni rasmi na mkataba wa pili ulikuwa ni wa kibiashara. ..Na mkataba huo ndiyo ulitumiwa na ubalozi wa Tanzania kumuhamishia fedha wakala wa uuzaji wa jengo na wala muuzaji wa jengo lile akakubali kuikabidhi Tanzani lile jengo na hajalalamika kuwa fedha hazikumfikia…mahakama hii inasema washtakiwa hawana hatia katika kosa hilo la kutumia nyaraka kumdangaya mwajiri wao kwasababu ushahidi wa upande wa jamhuri unajichanganya,”alisema. Aidha alisema kwa mujibu wa ushahidi wa upande wa jamhuri kuwa taratibu za manunuzi ya jengo hilo mjini Rome haukufuatwa ni sawa na serikali kusindika risasi kwenye bastola kisha kujielekezea yenyewe kifuani. “Mahakama imebaki ikijiuliza ni kwanini Grace alishitakiwa katika kesi hiyo na kwa sababu hiyo nahitimisha kwa kusema serikali imeshindwa kuthibitisha kesi yake na hivyo ninawaachia huru washtakiwa wote,”alisema na kusababisha washitakiwa kuangua vilio Baada ya hakimu Mugeta kumaliza kusoma hukumu hiyo iliyowaliza washitakiwa na ndugu zao, Mahalu alikataa kuhojiwa na waandishi wa habari na badala yake aliwataka waandishi wa habari waende wakaisomea Zaburi ya 17 katika Biblia ya Agano la Kale ambayo inasomeka hivi: “ Ee Bwana, usikie haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya hila. Hukumu yangu na itoke kwako, Macho yako na yatazame mambo ya adili. Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku, Umenihakikisha usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose, Mintarafu matendo ya wanadamu; Kwa neno la midomo yako Nimejiepusha na njia za wenye jeuri. Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako, Hatua zangu hazikuondoshwa. “.. Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, Utege sikio lako ulisikie neno langu. Dhihirisha fadhili zako za ajabu Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia; Kwa mkono wako wa kuume Uwaokoe nao wanaowaondokea. Unilinde kama mboni ya jicho, Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako; mbali ya mashambulio ya waovu ,mbali na adui zangu hatari wanaonizunguka. Hao hawana huruma yoyote moyoni wanajua maneno ya kujigamba .Wananifuatia na kunizunguka ,wananivizia waniangushe chini.Wako tayari kunilalua kama Simba kama Simba aviziapo mawindo.Inuka e mwenyezi mungu uwakabili na kuwaporomosha kwa upanga ,uiokeo nafsi yangu kutoka kwa waovu.Kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu ambao ridhiki yao ni dunia hii tu.Uwanjaze adhabu uliyowawekea ,wapate ya kuwatosha na watoto wao .Waachie hata na wajukuu wao.Lakini mmi nitauona uso wako kwani ni mwadilifu,niamkapo nitajaa furaha kwa kukuona”. Awali ya yote naomba nieleweke kwamba kuna baadhi ya kesi serikali imeweza kufanya vizuri na kuibuka mshindi na nimekuwa nikiandika makala kuipongeza kwa ushindi huo na pindi serikali inaposhindwa kufuruka katika kesi kubwa kadhaa niliandika makala ya kukosoa na leo katika kesi ya Mahalu naandika makala hii kukosoa kwa kushindwa kuthibitisha kesi yake. Binafsi mimi ni miongoni mwa mwandishi wachache sana ambao tulianza kuiripoti kesi hii tangu ilipofunguliwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 22 mwaka 2007 hadi Agosti 10 mwaka huu ilipomalizika kwa kutolewa hukumu. Lakini nadiriki kusema mimi ni mwandishi pekee hapa nchini niliyeifahamu kesi kiundani zaidi ya kesi ilivyokuwa mahakamani na nje ya mahakama na ndiyo maana kuna wakati ilifikia mahali kukopishana kauli na baadhi ya wakili wa mmoja wa serikali ambaye nilimweleza wazi wazi kuwa wanamaliza muda wa serikali bure na fedha za walipa kodi kwa kesi hiyo hiyo isiyokuwa na kichwa wala miguu na hatimaye Hakimu Mugeta amekuta kuitimisha kwa kutupilia mbali kesi hiyo iliyofunguliwa kwa mbele na kuendeshwa na TAKUKURU.. Kupata kwangu fursa ya kuifahamu kesi hii nje na ndani ya mahakama napenda niseme wazi kuwa kumenifundisha mambo kadhaa ya msingi: Mambo hayo ni kwamba kumbe ndani ya serikali kuna baadhi ya watumishi ambao ama kwa kutaka umaarufu au waonekane ni wachapakazi wanaamua kuwazulia wenzao uongo na mwisho wa siku uongo huo unasababisha wafikishwe mahakamani na mwisho serikali inajikuta ikibwagwa kwasababu hakuna ushahidi wa kuwatia hatiani washitakiwa. Pili,Rais Jakaya Kikwete wakati mwingine anasingiziwa na kugeuzwa Mwanasesere kwani katika kesi ya Mahalu kuna baadhi ya watu wakiwemo watumishi wa umma na baadhi ya wananchi bila kumung’unya maneno walikuwa wakisema Kikwete anamchukia Mahalu kwasababu eti wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatai na Mahalu alikuwa Balozi wetu nchini Italia, alikuwa akimdharau Kikwete hivyo ndiyo maana kikwete alivyokuwa rais alianza kwa kumlipizia kisasi Mahalu kwa kuagiza kwa njia ya siri vyombo vyake vimfikishe mahakamani. Tatu;kuna watumishi wa umma ambao hawana hofu ya mungu,vibaraka wa wakuu wao wa kazi,wapo kwaajili ya kuwaumiza baadhi ya wananchi wengine wasiyo na hatia kwa kisingizio kwamba wao ndiyo wasomi wa sheria na wapelelelezi wa makosa ya rushwa na wanatumia madaraka yao vibaya kwaajili ya wakati mwingine kuwaumiza watu wanaodhani wanamagomvi nao binafsi hali hii isipothibitiwa inaweza kujenga chuki ndani ya jamii yetu. Nne;baadhi ya watumishi hao wamekuwa wakivitumia vyombo vya habari kuakikisha vinatangaza uzushi huo ili mwisho umma unaamini watu hao wanaotuhumiwa kuwa ni mafisadi na hatimaye serikali kupitia vyombo vyake vinatoa uamuzi watu hao washitakiwe.Na katika sakata hili lilopelekea kuzaliwa kesi ya Mahalu ifunguliwe kuna baadhi ya waandishi wa chache maarufu hapa nchini walitumika ama kwa kutokujua au walijua kuwa walikuwa wakitumika vibaya kuibua sakata hilo kwa kwa maslahi ya watu wachache waliokuwa na lengo la kumuangamiza Mahalu na Grace.Waandishi hao wanajifahamu na hivi sasa hawana budi kutubu mbele ya mungu wao. Haikuitaji mtu awe na taaluma ya sheria kubaini kuwa ile kesi ya Mahalu ili ni miongoni mwa kesi za kipuuzi ,majungu na iliyokuwa na lengo la kuwakomoa na kuwahalibia maisha washitakiwa hao na mwisho wa siku imekuja kuiwekea rekodi serikali yetu ya kushindwa kufurukuta katika baadhi ya kesi kubwa mahakamani. Wasomi wa sheria tunafahamu fika jukumu la kuthibitisha kesi ya jinai ni la upande wa Jamhuri.TAKUKU ambayo ndiyo ilikuwa ikiiendesha kesi hii kwa mbwembwe ,ilishindwa kuyathibitisha mashitaka yote. Na cha kushangaza wakati kesi ikiendelea mawakili wa serikali wakaibua hoja ambayo haipo katika hati ya mashitaka kuwa washitakiwa walinunua jengo kwa mikataba miwili na walikuwa wakijaliribu kutaka kuishawishi mahakama ione kununua jengo lile kwa mikataba miwili ni kosa na lakini kwakuwa Hakimu Mugeta kwale tunaomfahamu ni hakimu kijana ambaye uadilifu wake haujawai kutiliwa mashaka na ni mtu mwenye msimamo usiyoyumba katika kile anachokiamini ,katika hukumu yake alisema wazi wazi kuwa hakuna kifungu chochote cha sheria kinachokataza mikataba miwili na kwamba hoja ya mikataba miwili simiongoni mwa makosa yanayowakabili washitakiwa ,aliitupilia mbali hoja hiyo na kwamba haiwezi kumshawishi kuwatia hatiani washitakiwa. Na ikumbukwe kuwa kesi hii ni kesi kubwa ya kwanza kufunguliwa ikiwa ni mwaka mmoja baakatika serikali ya Kikwete na ilifunguliwa muda mfupi baada ya Dk.Edward Hosea kuteuliwa na rais kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na fedha za serikali zilitumika kutuma timu wachunguzi wa PCCB kwenda Italia kufanya uchunguzi,kulipigia gharama za kupokea ushahidi wa mmoja wa Marco Papi ambaye ni raia wa Italia kwanjia ya Video Conference, lakini matunda ya uchunguzi huo uliotumia kodi zetu ndiyo yale matunda yaliyooza tuliyoyavuna Agosti 9 mwaka huu, ambapo Hakimu Mugeta alimwachiria huru washitakiwa. Kwa sisi tunaofahamu kesi ya Mahalu ndani na nje ya mahakama tulikuwa tukishuhudia makundi mawili yakiwa yanapambana kimya kimya.Kundi moja lilikuwa linajitahidi washitakiwa hao wafungwe madai kuwa kesi hiyo inamkono wa rais wakati kundi jingine ambalo lilikuwa likipambana kisheria kuakikisha hawafungwi kwasababu walikuwa wakidai kuwa wanafahamu Mahalu na Grace ni wahadilifu na walibambikiwa kesi. Tujiulize kama kweli Rais Kikwete alikuwa ana mkono wake katika kesi hiyo ni kwanini walishinda kesi hiyo?Maana sote tufahamu nguvu alizokuwa nazo rais za kisheria na kimabavu na zinazoonekana na zisizoonekana kama kweli alikuwa na mkono wake katika kesi hiyo si angetumia vyombo vyake kwa njia anazozijua na angeakikisha Mahalu anafungwa?Na hakuna mtu yoyote ambaye angeweza kuleta ushahidi kuwa rais alihusika kufanya unyama huo na washitakiwa wangewekwanda gerezani. Kesi hii haikufunguliwa na rais kwasababu sisi wasomi wa sheria tunafahamu rais haina mamkala ya kufungua kesi ya jinai mahakamani ,kwa mujibu wa kifungu cha 90 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, kinasema Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP),ndiye mwenye mamlaka ya kufungua na kuendesha kesi za jinai mahakamani kwaniaba ya serikali. Hivyo uvuvi uliokuwa ukienezwa chinichini wa kwamba Rais Kikwete ndiye yupo nyuma ya kesi hiyo ni uongo mkubwa na walioanzisha uongo huo naamini walikuwa na lengo baya la kumpaka matope rais wetu na kumchonganisha na wananchi wake na uenda uongo huo ulikuwa ukitumiwa na wale wapika majungu waliosababisha kesi hiyo ifunguliwe ili waweze kumtisha Hakimu Mugeta atoe maamuzi yasiyoyahaki kwa kisingizio kesi hiyo inamkono wa rais lakini kwakuwa bado katika Mahakama zetu tuna mahakimu na majaji waadilifu akiwemo Hakimu Mugeta ambaye kwa wale tunaomfahamu Mugeta kupitia maamuzi yake kadhaa ni kwamba kama unashitakiwa mbele yake na utapata haki yako kama kwa mujibu wa sheria. Na hivyo ndivyo anavyosifika Mugeta ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwenye mhimili wa mahakama hapa nchini kwamba ni hakimu kijana ambaye na ayumbishwi na mtu wakati akitekeleza majukumu yake.Na hilo lilithibitika siku alipotoa hukumu hiyo kwani baadhi ya wananchi waliokuwa wametoka ndani ya chumba kilichokuwa kikisomewa hukumu walikuwa wakisema hakimu huyo ni jasiri kwani kesi hiyo ilikuwa na maneno mengi sana. Kama nilivyosema kesi hii imenifundisha mambo mengi sana likiwemo la kumbe hapa duniani kuna watu wana roho za ukatili wapo kwaajili ya kuwazulia wenzao uongo na kuwaaribia maisha lakini kwakuwa Mungu ni mwingi wa rehema mwisho wa siku Mungu ujiinua na kuwakumbatia watu wake walionewa na kudhalikishwa na makatili na hivyo ndivyo ilivyotokea katika kesi ya Mahalu wale wote walimuomdhulia balaa lile na kusababishia serikali iingie gharama za kuendesha kesi hii leo hii sijui wanajisikiaje katika nafsi zao. Nitoe rai kwa kuwataka wale wote walioshiriki kumfanyia madhira Mahalu, Grace waende wakaisome Zaburi 17 na wailewe na kisha kila mmoja hatubu kwa mungu wake dhambi hiyo kwani siku zote adhabu ya Mungu ni kali sana. Lakini mwisho niwakumbushe wale baadhi ya watumishi wa serikali ambao wapo serikalini kwaajili ya kutumia madaraka yao kuwaumiza wenzao na kuwazulia wenzao uongo ,wafahamu cheo ni dhamana na mwisho wa umri wa utumishi umma ni miaka 60.Baada ya hapo mnarudi uraiani mnakuja kukutana na wale mliopikia majungu wakafukuzwa kazi mnatafana au uenda yule uliyemfukuzisha kazi kabla ya umri wa kustaafu haujafika mungu akaja kumbariki akawa na maishai mazuri kuliko wewe uliostaafu kwa mujibu wa sheria,sura yako utaiweka wapi? Tumieni madaraka yenu vizuri enyi wote mliobahatika kupewa madaraka,msiumize wenzenu kwa ahadi za kupewa vyeo zaidi na wakubwa zenu kwani mkifanya hivyo mtakuwa mkikiuka maadili ya taaluma zenu na Mungu anawaona na siku atakapoanza kuwaadhibu msije kulia na mtu.Kumbukeni Mbinguni hakuna atakayekwenda na madaraka wala mali vyote tutaviacha hapa hapa. Pia wale mliowasababishia Mahalu na Grace mkawavurugia maisha yao ya utumishi wa umma na kuwaletea njaa na dhiki katika familia zao katika kipindi chote,mimi nafahamu ndugu na jamaa washitakiwa hao walikuwa wakifunga na kusali kwa mungu ,naamini maombi yale na machozi ya washitakiwa hayo hayatakwenda bure,mungu ameanza kuyajibu kama Mahalu alivyosema baada ya hukumu kutolewa kuwa ‘Mungu amemjibu maombi yake’.Siku zote tumheshimu na kumuogopa mtu anayemtumaini mungu katika jambo lake kwani mungu ni mtu wa haki. Naitimisha kwa kutoa raia kwa Rais Kikwete asifanye papara kuakikisha wale wote waliohusika kupika majungu na kumdanganya kuwa wanaushahidi mzito katika kesi hii licha kuna baadhi ya watendaji wa serikali ambao walishawahi kuishauri kwa siri serikali iifute kesi hii mapema kwani walibaini si kesi wala silolote na mwisho wa siku ni serikali ndiyo itadhalilika ,wachukuliwe hatua hatua au kubadilisha nyadhifa zao. Maana hakuna ubishi kwamba kwasisi tuofuatilia kesi mbalimbali kila siku ikiwemo kesi hii,Kikwete alikuwa akitajwa kichinichini kuwa ana mkono katika kesi hii sasa ili kuonyesha urais wako hauna ubia,na wewe ni rais wa wananchi wote na haukuchaguliwa na wanachi kwenda Ikulu kuwaumiza wananchi ni wakati sasa wakuwashughulikia au kuwaondoa madarakani wale wote walioshiriki kulizua sakata hili hadi siku ile ulipotembelea kwa mara ya kwanza Wizara ya Habari na Utamaduni ,ukalipongeza gazeti la Thise Day kwa kazi yake kubwa ya kuandika habari ya kuhusu ufisadi wa ununuzi wa jengo la Italia ambalo lilisababisha baadaye Mahalu kufikishwa mahakamani na ameshinda kesi hiyo na ukasahau tamko lako ulilolitoa Bungeni mwaka 2004 amba katika kikao cha Bajeti ambapo ulinukuliwa katika Hansard za bunge ukisema taratibu za ununuzi wa jengo hilo ulifuatwa na kwamba serikali ilituma fedha za manunuzi katika akaunti mbili za nchini Italia. Na tungali tukikumbuka hotuba yako wakati ukitangaza baraza lako jipya la mawaziri hivi karibu ambalo ulilifanyia marekebisho na kuingiza mawaziri wapya na mawaziri wengine kuwaacha, ulisema ‘kuna mawaziri wengine wamewajibika kwasababu ya makosa yaliyotendwa na wasaidizi wao na kwamba hao waliosababisha mawaziri hao wakawajibika nao haatabaki salama kwasababu kuna watu wapo serikali kazi yao ni kuwapikia majungu wenzao” Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika 0716 774494 www.katabazihappy.blogspot.com Chanzo:Gazeti la Tanzania la Daima la Jumapili,Agosti 12 mwaka 2012.

PAPA MSOFFE KORTINI KWA KESI YA MAUJI

Na Happiness Katabazi HATIMAYE mfanyabaishara maarufu jijini Dar es Salaam, mfanyabaishara maarufu jijini Marijani Abdubakari Msoffe(50) maarufu kwa jina la “Papa Msoffe chuma cha reli akishi kutu’ amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kesi ya mauji. Wakili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka alidai mbele ya Hakimu Mkazi Agnes Mchome alidai kuwa Msofe ambaye ni mkazi wa Mikocheni,anakabiliwa na kosa m
oja la mauji ambalo ni kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002. Wakili Kweka alidai kuwa Novemba 6 mwaka 2011 huko Magomeni Mapipa Papa Msoffe anayetetewa na wakili wa kujitegemea Majura Magafu alimuua Onesphory Kitoli na kwamba upelelezi wa kesi ya hiyo bado haujakamilika. Kwa upande wake hakimu Mchome alisema kesi hiyo ambayo ipo mbele yake ni mauji na mahakama yake haina mamlaka ya kuisikiliza na kwamba mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza ni Mahakama Kuu hivyo akamtaka mshitakiwa huyo asijibu chochote. “Kwa sababu hiyo naiarisha kesi hii hadi Agosti 23 mwaka huu, kesi hii itakuja kwaajili ya kujatwa na kwa kuwa kesi hii haina dhamana naamuru mshitakiwa apelekwe gerezani”alisema Hakimu Mchome. Msofe ambaye alifikishwa kwenye eneo la mahakama hii jana saa 3:30 asubuhi chini askari kanzu watatu ambao mmoja alikuwa amebeba silaha na kisha kumuingiza kwenye selo ya mahabusu hiyo kwaajili ya kumuifadhi hadi ilipofika saa tano saa asubuhi mshitakiwa huyo aliingizwa kwenye chumba namba tisa cha mahakamani hapo na kuanza kusomewa maelezo yake huku ndugu na jamaa zake walikuwa wamefika mahakamani hapo kwaajili kusikiliza kesi hiyo ya ndugu yao. Msofe ambaye jina lake limekuwa likitajwa mara kwa mara kwenye nyimbo zinazopigwa na Bendi za Miziki ya Dansi nchini ikiwemo Bendi ya FM Academia na Acudo Impact aliletwa na askari kanzu hao akitokea kwenye sero ya jeshi la polisi ambako kwa zaidi ya wiki moja sasa alikuwa akiishi ndani sero hiyo ya polisi kwaajili mahojiano na mshitakiwa huyo na hatimaye jana akafikishwa mahakamani hapo kwa kesi ya mauji. Itakumbukwa hivi karibuni mjane mmoja aishie Mbezi Beach alilalamika kupitia vyombo vya habari kuwa Papa Msofe anataka kumdhuru nyumba aliyoachiwa na marehemu mumewe wake kupitia vyombo vya habari, hali iliyosababisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuingilia kati sakata hilo na hatimaye mjane huyo akarudishiwa nyumba yake aliyokuwa akidai Msofe anataka kumdhurumu. Aidha itakumbukwa kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Papa Msofe kufikishwa katika mahakama hiyo kwa makosa mbalimbali ya jinai. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi,Agosti 11 mwaka 2012

MAHALU,MKAPA WAMBWAGA JK


*HAKIMU ASEMA KIKWETE ALITOA NGUVU YA KISHERIA 

Na Happiness Katabazi 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachilia huru aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na aliyekuwa Meneja Utawala na fedha Grace Martin waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Euro milioni mbili kutokana na ushahidi wa jamhuri kushindwa kuwatia hatiani. 

Hukumu hiyo inaweza kutafsiriwa kama ni kubwagwa kwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kutokana na hatua ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kukubali kupanda kizimbani na kumtetea Mahalu dhidi ya serikali, tukio ambalo ni la kwanza katika historia ya nchi hii. Hukumu hiyo ya kihistoria ya kesi ya uhujumu uchumi Na.1/2007 ilitolewa jana kuanzia saa 6:03 hadi 7:39 mchana na Hakimu Mwandamizi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mugeta huku akisikilizwa na umati wa ndugu jamaa,marafiki wa washitakiwa hao. 

Washtakiwa hao waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka sita walikuwa wanatetewa na mawakili Mabere Marando, Alex Mgongolwa, Beatus Malima na Cuthert Tenga na upande wa Jamhuri ulikuwa ukiwakilishwa na Ben Lincoln na Vicent Haule toka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Ponsia Lukosi toka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP). 

 Aliyaja makosa hayo kuwa ni kula njama, kutumia nyaraka za manunuzi ya jengo la ubalozi ili kumdanganya mwajiri wao serikali, wizi wa Euro milioni 2,065,827 na kuisababishia serikali hasara. Hakimu Mugeta alisema kuwa hata hivyo hati hiyo ya mashitaka haikuonyesha maelezo ya makosa hayo yanayowakabili washitakiwa. Alisema uamuzi huo ni kwa mujibu wa kielelezo cha tatu ambacho ni barua Na. FAC/0.40/58/62 ya Septemba 11 mwaka ya mwaka 2001 ambayo ni ya uamuzi wa serikali ya Tanzania wa jengo la ubalozi wake nchini Italia ambacho kilitolewa mahakamani hapo na Mahalu wakati akijitetea. Hakimu Mugeta alisema baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vyote vya pande mbili, mahakama imeona manunuzi ya jengo yalifanyika kwa njia ya mikataba miwili ambayo ilisainiwa kwa siku moja na kwa bei tofauti. Alisema mkataba wa kwanza ni ule uliosainiwa na wakili wa Serikali ya Italia (Marco Papi) ambaye alikuwa ni shahidi wa pili wa Jamhuri ambao unaonyesha jengo lile lilinunuliwa kwa Euro 1,032,913 na mkataba wa pili ambao ni kielelezo cha sita ambao uliingiwa na wakala wa uuzwaji wa jengo na Balazo Mahalu na haukushuhudiwa na wakili wa serikali ya Italia. Alisema kuwa mkataba unaonyesha jengo lilinuliwa kwa thamani ya Euro 3,098,741. Hakimu Mugeta alisema kielezo cha nne ambacho ni taarifa ya benki kinaonyesha manunuzi ya jengo hilo yalifanyika Septemba 24 mwaka 2002 katika akaunti mbili tofauti . “Kielezo cha pili kinaonyesha malipo ya ununuzi ni Euro 2,065,827 ambayo yaliingizwa kwenye akanti Na.106705 ya Monaco na malipo mengine ni Euro 1,032,913 ambayo fedha hiyo iliingizwa kwenye akaunti Na.2182/51 ya Bromitrdnor ya zote za mjini Rome,” alisema. Kwamba baada ya mikataba yote kusainiwa na fedha kupokelewa Oktoba mosi 2002,wakala aliitoa risiti ya kuthibitishia kupokea Euro 3,098,741.58 na Septemba 23 mwaka huo, ubalozi wa Tanzania iliidhinisha vocha ya malipo ambayo ni kilielezo namba tatu ya Euro milioni 3,098.741. Alifafanua kuwa siku hiyo hiyo ubalozi wa Tanzania ulimuelekeza mfanyakazi wa benki nchini Italia, ahamishe kiasi hicho cha fedha kutoka kwenye akaunti ya ubalozi wa Tanzania kwenda kwenye akaunti hizo mbili tofauti ambazo ni za wakala wa uuzaji wa jengo hilo. Hakimu huyo alisema kwa mujibu wa vielelezo hivyo hapo juu mahakama imeridhika ndivyo vilivyotumika kununulia jengo la ubalozi na kwamba washtakiwa hao walifunguliwa kesi hiyo kwa kielelezo cha 3, 6 na 8. Kilelezo cha 3 ambacho ndicho kinaunda kosa la pili wakati kielelezo cha sita kinajenga kosa la nne na utofauti wa bei ya manunuzi ni kielelezo cha 1 na sita ambacho ni Euro 2,065,827.60 ambacho kinaunda kosa la tano na sita. Kuhusu ushahidi wa jamhuri, alisema kuwa Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu,Martin Lumbanga katika ushahidi wake alidai hakumbuki kama aliidhinisha jengo lile linunuliwe kwa njia ya mikataba miwili wakati shahidi wa pili (Papi) alidai yeye alisaini mkataba mmoja wa manunuzi ulionyesha jengo lilinuliwa kwa Euro 1,032,913.80. “Shahidi wa tatu Stewart Migwano ambaye ndiye alikuwa mhasibu wa ubalozi Utalia, alieleza kuwa ni ndiye aliyeandaa na zile vocha za malipo na kuzisaini ambazo mawakili wa serikali wanadai washitakiwa hao walizitumia kumdanganya mwajiri wao,” alisema. Hakimu aliongeza kuwa shahidi wa nne, Simon Maige alitoa kielelezo cha tano ambazo ni cheki ambazo zinaonyesha jinsi fedha za manunuzi ya jengo hilo zilivyohamishwa kutoka Tanzania kwenda ubalozi wake mjini Rome,Italia. Alisema kuwa shahidi wa tano ambaye ni mchunguzi toka (Takukuru), Isidori Kyando, alidai kubaini jengo hilo lilinuliwa kwa mikataba miwili na shahidi wa sita Edwin Mikongoti ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Utawala wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa alidai yeye alikuwa akitunza rekodi za majengo yote ya ubalozi na kwamba hakushirikishwa katika ununuzi wa jengo hilo. “Shahidi wa saba Abubakar Rajabu alidai taratibu za manunuzi hazikufuatwa,” alisema. Mugeta alisema kuwa mashahidi watatu walitoa ushahidi kwa upande wa utetezi na wa pili alikuwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa ambaye alieleza mahakama yeye na serikali yake walilidhia jengo linunuliwe kwa njia ya mikataba miwili na kwamba alitoa baraka zote kwa washtakiwa wanunue jengo hilo. “Kwa maelezo hayo hapo juu kabla ya kutoa hukumu yangu nimejiuliza maswali manne ambayo ni kama kweli washitakiwa walitenda kosa la kula njama na kuiba, kama walitumia nyaraka za manunuzi ya jengo kumdanganya mwajiri wao, kama waliibia seriakali Euro 2,065,827.60, kama wwaliisababishia serikali hasara ya Euro 2,065,827.60? alisema Mugeta. Akilichambua swali la kwanza, alisema ushahidi wa upande wa jamhuri umeshindwa kuweka wazi makubaliano na mipango ya siri waliyodai imefanywa na washitakiwa kuiba fedha hizo kwamba katika kesi hiyo endapo kosa la wizi likithibitika, kosa la kula njama linakufa kifo cha asili. “Hoja hii ya kwanza inanipeleka kulijadili kosa la tano ambalo ilidaiwa Oktoba mosi mwaka 2002 katika ubalozi wa Tanzania nchini Italia, washitakiwa hao waliibia serikali Euro hizo na kwamba kosa hili la tano nilijiuliza kwenye hoja yangu ya tatu kwamba washitakiwa waliiba kiasi hicho cha fedha? “Ushahidi wa upande wa jamhuri katika kosa hili si wa moja kwa moja unaonyesha washitakiwa walitenda kosa la wizi na kwa mujibu wa ushahidi wa jamhuri ulilotelewa mahakamani una shauri kuwa washitakiwa hao wanaweza kuwa walitenda kosa hilo, hivyo ushahidi huo ni mazingira si thabiti,” alisema. Alisema Mahalu alidai kuwa kule Italia muuzaji wa jengo anaruhusiwa kuuza jengo lake kwa mikataba miwili na upande wa jamhuri katika kesi hii haukupinga hilo na mawakili wa serikali wakadai sheria za ununuzi wa jengo hazikufuatwa wakati shahidi 6 na 7 walieleza pindi serikali inataka kununua jengo na kabla. Alisema Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali anatuma timu ya wataalamu kulikagua na kisha ndiyo wanatuma fedha na kisha wizara ya Sheria na Katiba inahusishwa na katika ununuzi wa jengo hilo hayo yote yalifanyika, mahakama inakataa madai ya serikali ya kununua jengo kwa mikataba miwili kwa sababu hakuna kifungu chochote cha sheria hapa nchini kinachosema kununua jengo kwa njia ya mikataba miwili ni kosa la jinai. Alisema upande wa jamhuri ulikuwa unataka kuonyesha kuwa washitakiwa waliingia mikataba hiyo miwili bila ruhusa ya serikali wakati Mahalu katika ushahidi wake alitoa kielelezo ambacho ni nguvu ya kisheria aliyopewa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo ambaye kwa sasa ni Rais Jakaya Kikwete. “Lakini mahakama hii imejiuliza kama serikali ilikubali kulinunulia jengo hilo,ikatoa fedha kwaajili ya ununuzi, ikampatia Mahalu nguvu ya kisheria ya kuendelea na mchakato wa manunuzi, mkataba wa kwanza ulikuwa ni rasmi na mkataba wa pili ulikuwa ni wa kibiashara. ..Na mkataba huo ndiyo ulitumiwa na ubalozi wa Tanzania kumuhamishia fedha wakala wa uuzaji wa jengo na wala muuzaji wa jengo lile akakubali kuikabidhi Tanzani lile jengo na hajalalamika kuwa fedha hazikumfikia…mahakama hii inasema washtakiwa hawana hatia katika kosa hilo la kutumia nyaraka kumdangaya mwajiri wao kwasababu ushahidi wa upande wa jamhuri unajichanganya,”alisema. Aidha alisema kwa mujibu wa ushahidi wa upande wa jamhuri kuwa taratibu za manunuzi ya jengo hilo mjini Rome haukufuatwa ni sawa na serikali kusindika risasi kwenye bastola kisha kujielekezea yenyewe kifuani. “Kwa sababu mashahidi wa jamhuri walieleza mahakama kuwa serikali ilituma timu ya wataalumu wa majengo iliyongozwa na Kimweri kwenda kulikagua jengo na ikaridhika na jengo lile na ikaishauri serikali ilinunue kabla halijanunuliwa na wizara kupitia menejimenti ilishakaa vikao na kuafiki jengo linunuliwe na waziri wa mambo ya nje ndiye aliyempa Mahalu nguvu ya kisheria kununua jengo hilo na serikali ilikuwa na taarifa, mahakama hii inasema washitakiwa hawakukiuka taratibu zozote za manunuzi. “Kwa kuwa kununua jengo kwa njia ya mikataba miwili hakuundi kosa la jinai na kwa sababu hiyo hakuna ushahidi ambao unathibitisha hoja yangu ya pili, nilichokigundua ni kwamba baada ya Euro 2,065,827,59 kuhamishwa kwenye akaunti zilizopo Monaco, hakuna ushahidi kuwa washitakiwa hao walizihamisha na kuiziingiza kwenye akaunti zao. Pia jamhuri imeshindwa kuleta ushahidi kuonyesha umiliki wa akaunti zile mbili na kwamba hakukuwepo na ubishi kuwa akaunti zile kuwa hazikuwa Monaco na jamhuri haikuwahi kumhoji wakala wa uuzaji wa jengo kama hakulipwa kiasi hicho cha fedha,”alisema Hakimu Mugeta. Kuhusu hoja ya pili la nyakara hizo kuonesha jengo kununuliwa kwa Euro 3,098,741.40 na washitakiwa kumdanganya wajiri wao, hakimu huyo alisema amegundua nyaraka hizo hazina udanganyifu wowote. Kwamba kwa kuwa Jamhuri imeshindwa kuthibitisha kuwa nyaraka hizo zilikuwa za udanganyifu, kosa la kwanza la kula njama na wizi limeshindwa kuthibitishwa. “Mahakama imebaki ikijiuliza ni kwanini Grace alishitakiwa katika kesi hiyo na kwa sababu hiyo nahitimisha kwa kusema serikali imeshindwa kuthibitisha kesi yake na hivyo ninawaachia huru washtakiwa wote,”alisema na kusababisha washitakiwa kuangua vilio. Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu hukumu hiyo, Mahalu aliwataka waandishi waende wakasome Zaburi ya 17 katika Biblia huku akionekana kulengwa kwa machozi ya furaha. Mkewe Winfrida Mahalu ambaye aliogopa kuoingia ndani ya chumba ilikosomewa hukumu hiyo, alitolewa ndani ya gari na ndugu zake huku akiangua kilio baada ya hukumu hiyo na huku mshtakiwa wa pili Grace naye akiangua mahakamani hapo. Kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 22 mwaka 2007. Ili kuithibisha kesi yao, upande wa Jamhuri ilileta jumla ya mashahidi saba wakati upande wa utetezi ulileta mashahidi watatu akiwemo Rais mstaafu Benjamion Mkapa. Mei 8 mwaka huu, upande wa utetezi ulifunga ushahidi wake baada ya Grace kumaliza kujitetea. Mei 7 mwaka huu,Mahalu ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu kipya cha Bagamoyo cha jijini Dar es Salaam alimaliza kujitetea na siku hiyo ndiyo Rais Mkapa aliandika historia mpya nchini kwa upande wa marais ambapo alifika mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake katika kesi hiyo. Julai 16 mwaka 2009, Jaji Sivangilwa Mwangesi ambaye ndiye alikuwa akiisilikiza kesi hiyo tangu ilipofunguliwa mwaka 2007 alitoa uamuzi wake ambapo aliwaona washitakiwa hao wana kesi ya kujibu. Machi 25 mwaka jana. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Agosti 10 mwaka 2012.

GRATIAN MKOBA NI KIBWETERE WA WALIMU WALIOGOMA?


Na Happiness Katabazi 

KIFUNGU cha 8 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya mwaka 2012,kinasomeka hivi; ‘kutofahamu sheria siyo kinga ya kutokuadhibiwa’. 

Nimelazimika kutumia nukuu ya kifungu hicho kwasababu hivi karibuni baadhi ya walimu wa shule za serikali hapa nchini kupitia chama chao CWT waliendesha mgomo ambapo kupitia Rais wa chama hicho,Gration Mkoba ndiye aliyeuitisha na mara kwa mara kiongozi huyo alikuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akijigamba kuwa mgomo huo ambao hauna kikomo upo halali kisheria na baadhi ya walimu ambao naweza kusema akili zao zimeshikiliwa na Mkoba walianza kugoma tangu Julai 30 mwaka huu. Lakini Julai 26 mwaka huu, Katibu Mkuu Kiongozi, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Ufundi na Mwanasheria Mkuu wa serikali kupitia mawakili wa serikali Obadia Kamea na Pius Mboya dhidi ya CWT waliokuwa wakitetewa na wakili wa kujitegemea Gabriel Mnyele. Walalamikaji hao walifungua maombi madogo Mahakama Kuu Divesheni ya Kazi yaliyopewa Na.96/2012 chini ya hati ya dharula chini ya kanuni ya 25(1) ya Kanuni za Mahakama ya Kazi ya mwaka 2007,wakiomba mahakama itoe amri ya zuio la muda la kuzuia kufanyika kwa mgomo wa walimu kwasababu mgomo huo ni batili na haujakithi matakwa ya Kanuni ya 43(1) ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 na kifungu cha 80(1) vya sheria hiyo. Hivyo Wakili Kamea alidai endapo mgomo huo ukifanyika utailetea wakati mgumu serikali ,kuvuruga mitaala ya elimu na muda wa vipindi vya masomo,wanafunzi na wazazi watapata madhara ambayo hayatalipika endapo mgomo huo ukifanyika na wakaiomba mahakama imwamuru Mkoba aende kwenye vyombo vya habari kuutangazia umma mgomo ule ni batili na kwamba mgomo huo uliadhishwa kwa dhamira mbaya. Wakati wakili Mnyele alipokuwa akiwasilisha hoja zake mbele ya Jaji Sophia Wambura alidai kuwa CWT iliendesha zoezi lake la kupiga kuunga mkono ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho za kufundishia kwa walimu wa Sayansi asilimia 55 na walimu wa Sanaa kwa asilimia 50 na posho ya mazingira magumu ya asilimia 30 kwa kufuata sheria hivyo mgomo ule hauna mawaa. Ilipofika Agosti 2 mwaka huu saa tisa alasiri minilikuwa miongoni mwaandishi wa habari waliofuatilishia shauri hilotangu linafunguliwa hadi linatolewa uamuzi siku hiyo, Jaji Wambura katika uamuzi wake ambayo nakala yake ninayo alisema anakubaliana hoja ya wakili wa serikali, Kamea kuwa mgomo huo ni batili kwa mujibu wa Kanuni ya 43(1) ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ambapo aliinukuu kanuni hiyo kama ifuatavyo; “Kama kuna mgogoro wa kimaslahi umeshindikana kusuluhishwa na msuruhishi,msuruhishi atajaribu kuzipatia pande zinazolumbana kanuni za kuitisha mgomo,kanuni hizo zitatangazwa kwa utaratibu,utaratibu wakuendesha mgomo huo,kutolewa noti yakuonyesha mgomo utaanza lini,eneo,muda,mazingira ya mgomo huo na utangazwe kwa wafanyakazi hao kabla mgomo kuanza,usalama wa wafanyakazi katika kipindi cha mgomo’ Jaji Wambura akasema wakati CWT ikijiandaa kuingia kwenye mgomo huo,pia ilikuwa haijakamilisha masharti ya kifungu cha 80(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini,kwasabababu amebaini kuwa wakati inaendesha zoezi la upigaji kula za kuunga mgomo ,iliwapotosha wanachama wake kuwa zoezi hilo liliitishwa rasmi na limekidhi matakwa ya kisheria, upigaji kula ule ni batili kwani walimu walikuwa hawajahalifiwa vizuri madhara yatakayojikoze kwenye mgomo ule,zoezi halikufuata taratibu za kisheria,hati ya nia ya kusudia la kugoma la CWT ambalo walimpelekea Katibu Mkuu Kiongozi Julai 27 saa tisa Alasiri wakati taratibu za upigaji kula hazijafanyika pia nayo iliuwa ni batili,kushindwa kwa CWT kutekeleza matakwa ya Kanuni ya 42 na 43 ya Shera ya Ajira na Mahusiano Kazini. “Mahakama hii inasema taratibu zote zilizofanywa na CWT kuitisha mgomo zilifanywa kwa dhamila mbaya kwasababu ni CWT ndiyo ilikata kuendelea na majadiliano kuhusu madai yao na mwajiri wake,tangu mwanzo CWT ilikuwa na majadiliano na serikali kuhusu maslahi yao lakini CWT akaamua kuyakacha mazungumzo hayo na kwenda njia anayoijua yeye,Julai 27 mimi nilitoa amri katika shauri hili la kuzitaka pande zote kubaki kama zilivyo hadi maombi haya yatakapokuja kusikilizwa baada ya siku hiyo pande mbili kutoka mahakamani hapo CWT saa tisa jioni ilienda kutoa notisi ya kuitisha mgomo na kwasababu hiyo mahakama hii inasisitiza CWT ilikuwa na dhamira mbaya ya kuitisha mgomo huu na ninaamuru walimu wote warejee kazini na wawalipe wanafunzi fidia”alisema Jaji Wambura. Kwanza napenda nitoe pongezi kwa Jaji Wambura kwa kuweza kutoa uamuzi huo mzuri kisheria na ambao umeudhiirishia umma kuwa walimu waliogoma ambao rais wao ni Mkoba ni mambumbumbu wa sheria ambao akili zao zimeifadhiwa ndani ya mkoba anaotembea nao Rais wa CWT,Gration Mkoba. Walimu mliogoma napenda mrejee tukio hili la mauji ya aina yake yaliyohusisha zaidi ya wafuasi wa dini "Movement for the Restoration of the Ten Commandments" 1,000 walioyokuwa wakiongozwa na kiongozi wao wa kidini Joseph Kibwetere, ambapo Machi 17 mwaka 2000 wafuasi zaidi ya 500 wa kanisa hilo waliingia kwenye jengo dogo lisilo na madirisha huko Kangngu small church in Kangngu,Magharibi mwa Uganda. Wafuasi hao waliimba sana nyimbo za kumtukuza mungu kabla jengo hilo dogo kuanza kuteketea kwa moto ambapo moto huo uliwashwa kutokea ndani ya jengo hilo kwa madai kuwa mwisho wa dunia ulikuwa umefika na kwamba wakifa wanaenda kuonana na mungu.Machi 19 mwaka 2002,serikali ya Uganda ndiyo ikaja kugundua watu hao wamefariki duniani ndani ya jengo hilo.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na serikali ya Uganda baadaye zilidai mwaka 1998 Kibwetere ambaye naye alifariki katika mauji hayo na ndugu zake waliweza kuugundua mkono wake, aliwai kulazwa hospitalini akisumbuliwa na maradhi ya akili bila hao wafuasi wake kutofahamu kuwa kiongozi wao huyo aliwahi kuugua maradhi ya akili wakaendelea kumuamini na kumtii. Kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyotokea kwa wafuasi waliokuwa wakimtii Kibwetere ambaye aliwaaminisha mwaka 2000 ni mwisho wa duania na amewasiliana na mungu, basi walimu wa shule za serikali hapa nchini ambao wanayafuata maagizo ya Mkoba yanayowataka wagome wakati maagizo hayo ni batili kisheria na mwisho wa siku mahakama inakuja kusema mgomo ni batili, wajiulize je hawaoni ipo siku Mkoba anaweza kuwafanya kama Kibwetere alivyowafanyia wafuasi wake na wao wakakubali ? Kokote duniani mwalimu anaonekana ni mtu anayefahamu mambo na anayependa kujisomea wakati wote ili anapoingia darasani kufundisha akiulizwa maswali na wanafunzi wake aweze kuwapatia majibu. Lakini hapa Tanzania hivi sasa walimu wetu wengi hasa wa shule za serikali kwa mara ya pili sasa wameingia kwenye migomo batili ambayo inatenguliwa na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi.Mgomo wa kwanza ni ule uliofanyika mwaka 2008, ambapo serikali ilifungua kesi Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ambapo Jaji wa Mahakama ya Rufaa hivi sasa William Mandia,aliutangaza mgomo ule wa walimu ni batili na akawataka warejee kazini na wakarejea na mgomo wa pili ni huu uliobatilishwa na Jaji Wambura Alhamisi ya wiki iliyopita. Hivi walimu waliowafundisheni nyie hadi leo na nyie mmekuwa walimu nao kipindi wanawafundisha wangegoma kuwafundisha leo hii mngekuwa walimu? Baadhi ya wanafunzi katika mgomo wa wiki iliyopita wamedai kulikuwa na walimu waliokuwa wakiwafundisha wanafunzi kuandamana kuunga mkono madai ya walimu hao.Hili jambo limenisikitisha sana na ndiyo maana napendekeza uchunguzi ufanyike ilikuwabaini walimu waliokuwa wakiwafundisha wanafunzi kufanya ufedhuli huo kwani leo walimu wameweza kuwafundisha ufedhuli huo wanafunzi kesho wanawaweza kuwafundisha wanafunzi wawe wanawadhau watawala na hata wazazi wao. Na kwasababu hiyo sisi watu tunaofikiri sawa sawa tumeanza kuhoji umakini, ufahamu na usomi wa walimu hao wanaojiingiza kichwa kichwa kwenye migomo hiyo bila kwanza kujiridhisha kama migomo hiyo imekithi matakwa ya kisheria kama wana akili timamu au akili zao wameshikiwa na Mkoba kwani haingii akilini, Mkoba akiitisha mgomo haramu baadhi ya walimu bila kujifikiria wanakubaliana naye na kugoma kutokwenda kazini wakati kila mwalimu anafahamu adha na machungu ya kufukuzwa kazi,kushitakiwa mahakamani,kushushwa cheo au kuamishiwa vijijini pindi unapobainika umeshiriki mgomo huo na mwajiri wako? Nilitegemea walimu wale waliogoma hasa wa Shule za Dar es Salaam,kabla ya kukubali kuingia kwenye mgomo wa juzi wangeukumbuka ule mkutano wao walioufanya pale ukumbi wa Dimond Jubilee , Oktoba 14 mwaka 2008 ambapo siku hiyo walimu walioudhuria pale walikuwa wameazimia kuanza mgomo lakini ilipofika mchana wa siku hiyo Mkoba alisema yeye haungi mkono kuanza kwa mgomo huo hali iliyosababisha kuzuka kwa tafrani kubwa baina ya walimu hao na Mkoba ambao walimu hao waligeuza chupa za maji ya kunywa,soda na viti kurusha meza kuu ambapo alikuwa ameketi Mkoba na viongozi wenzake wakimtuhumu kuwa amewasaliti hali iliyosababisha Makachero wa polisi kutumia mbinu zao za kijeshi kumwokoa Mkoba ambaye alikuwa amevalia vazi la suti na kumpitisha mlango wa dhalura na kisha kumpandisha kwenye gari la polisi na kumuondoa kwenye eneo hilo ili asidhulike na walimu hao kwa hasira wakatoka nje ya ukumbi na kuanza kulilirushia mawe gari la polisi hali iliyosababisha polisi hao kuanza kurusha risasi hewani kuwatawanya walimu hao ambao walitawanyika kwa kuogopa risasi na kesho yake baadhi ya walimu waligoma. Halafu leo hii Mkoba kanukuliwa na gazeti hili akijigamba kuwa aogopi kujeruhiwa kama alivyojeruhiwa Dk.Steven Ulimboka.Kwa kweli nilisikia hasira baada ya kuisoma habari hiyo kwani ni huyu huyu Mkoba siku ile ya Oktoba 14 mwaka 2008, pale Dimond Jubilee,mimi binafsi nilikuwepo katika mkutano ule na nilimshuhudia Mkoba alivyokuwa amehamaki na kutweta na kujikuta akitumbukia kwenye mtalo wa nyuma ya ukumbi huo wakati akipandishwa gari la polisi baada ya kuponyeshwa kipigo cha walimu hao ambao wengi wao walikuwa ni wanawake. Sasa Mkoba anataka kuhadaa umma kuwa yeye ni shujaa na siyo mwoga. Kwakuwa nilimshuhudia Mkoba siku ile akiloana jasho,woga na kukumbwa na taaruki kwa bahati nzuri polisi ndio waliomwokoa, nasema hana ushujaa,ujasiri na anaogopa kufa na kudhulika hivyo siyo mwanaharakati wala mpiganaji wa kweli kama walivyo wanaharakati wa nchi za wenzeti kama Somalia, Syria,Afghanistan,Libya . Mkoba anajaribu kutaka kuhadaa walimu na umma kuwa ni mwanaharakati na yupo tayari kufa kwaajili ya madai ya walimu kumbe si kweli kwani kama ni kweli angekataa kuokolewa na polisi siku ile ya Oktoba 14 mwaka 2008 na angekubali kupokea kipigo cha walimu wengi wa kike ambao walikuwa wanataka kumtia adabu. Nawaomba wale baadhi ya walimu ambao ni bendera fuata upepo msitekeleze maagizo yanayovunja sheria za nchi yanayotolewa na Mkoba kwani mwisho wa siku mtakaopata madhara ni nyie walimu na familia zenu ,na Mkoba wala hapati madhara zaidi jina lake linazidi kujiandika katika historia ya viongozi wa CWT wanaoitisha migomo inayobatilishwa na mahakama,cheo chake cha urais na posho zinazotokana na cheo chake zinaendelea kuwepo,kwenye meza ya majadiliano na mwajiri wenu anaenda yeye na huko atakunywa na chai na mikate yenye Blue Band na Soseji na nyie walimu mazuzu amtoambulia chochote mtaendelea kufanyabiashara zenu za kuwalazimisha wanafunzi wanunue bagia, ubuyu na ice cream zenu za Ukwaju madarasani. Na jinsi ninavyoifahamu serikali yetu makini ni wazi kabisa hivi sasa imeishatuma wachunguze mashuleni ni mwalimu gani alikuwa Chakubimbi ,kimbelembele wa kuamasisha mgomo na kuwafundisha wanafunzi waingie barabarani kuandamana na kwakuwa sisi Watanzania tunanyimana matonge ya ugali lakini habari tunapeana, watajulikana na watachukuliwa hatua za kiutumishi kimya kimya na msije kulia na mtu na wakati hatua zikianza kuchukuliwa dhidi yenu Mkoba yeye bado atendelea kuwa rais wenu na wala hatapata madhara makubwa kama ya nyie walimu mambumbumbu msiokuwa tofauti na Misukule. Ifike mahali walimu wa shule za serikali ambazo serikali ina shule nyingi zaidi, mjiulize ni kwanini walimu wa shule binafsi ambao hawalipwi pesheni pindi wanapostaafu baadhi ya walimu wa shule binafsi licha wanalipwa vizuri hawana ajira za uhakika,huduma ya matibabu hawagomi? Ila nyie walimu wa shule za serikali ajira zenu ni za uhakika, mnaruhusiwa kupata mikopo, wengine ni walimu wa ngazi ya cheti(voda Fasta),mnapata pesheni mnapostaafu, pesheni mnapostaafu lakini mnagoma? Sikatai kuwa ndani ya sekta ya walimu wa serikali kuna matatizo yake kwani kuna malalamiko ya baadhi ya walimu ambao walikuwa wakifundisha kisha wakaamua kwenda kujiendeleza vyuoni na wanavyorudi na vyetu kwa mwajiri wao,mwajiri wao amekuwa akichelewa kuwapandisha madaraja na kuwabadilishia mishahara yao,uhaba wa nyumba za walimu,mishahara midogo ambayo haitoshelezi kwani gharama za maisha zimepanda hali inayosababisha wafanyakazi kuwavunja moyo lakini matatizo hayo yasiwe kigezo cha walimu wasifuate sheria wakati wanapodai madai yao. Siasa ifuate sheria siyo sheria ifuate siasa.Na hapo ndipo Vyama vya wafanyakazi vinapokosea katika kudai madai yao kwani wanataka sheria ifuate siasa badala ya siasa ifuate sheria kitendo ambacho hakikubaliki katika dola letu ambalo linaongozwa kwa utawala wa sheria. Baada ya Jaji Wambura kutoa uamuzi huo ,baadhi ya wasomi wa sheria na wananchi wa kawaida walikuwa wakinipigia simu wakiubeza uamuzi huo kwasababu jana yake Rais Jakaya Kikwete alilihutubia taifa na akasema serikali yake haiwezi kuyalipa madai ya walimu kwani hayalipiki.Wasomi hao walikwenda mbali na kuongeza kuwa jaji huyo alikuwa ameandika uamuzi huo kwa maelekezo ya serikali kwasababu jana yake kabla hajatoa uamuzi huyo Rais Kikwete alishazungumzia mgomo huo. Kwa kweli nilisikitishwa na kauli hizi kwani zilikuwa zikitolewa na wasomi wa sheria ambao awali nilikuwa na waheshimu sana na siku sita kuwahoji ni kwanini wamefikia hatua ya kutoa shutuma hizo wakati hata nakala ya uamuzi huo hawajaipata na kuisoma, hawakuwepo mahakamani wakati shauri hilo linasikilizwa na kuamriwa na niliwataka wanipe ushahidi wa jaji huyo aliandikiwa uamuzi huo na Rais Kikwete,walishindwa kufanya hivyo na kusema Tanzania hivi sasa ina majaji wana ojikomba kwa serikali. Wakati baadhi ya wanasheria hao wakitoa tuhuma hizo kwangu wakili wa CWT ,Mnyele aliwaeleza waandishi wa habari kuwa yeye kama wakili amekubaliana na uamauzi wa Jaji Wambura.Na kwa wale wanaofahamu sheria wasomi wa sheria wanaelewa kuwa amri za muda zinazotolewa na mahakama hazikatiwi rufaa hivyo hata uamuzi huo wa Jaji Wambura,CWT haiwezi kuukatia rufaa katika mahakama yoyote ile hadi kesi ya msingi itakapotolewa hukumu. Kadri siku zinavyozidi kwenda Tanzania imekuwa na wananchi tena wengine wasomi na sisi baadhi ya waandishi wa habari kuropoka au kuandika habari tusizokuwa na ushahidi nazo na kwa bahati mbaya wananchi wengine wanaziamini taarifa zinazochapishwa katika vyombo vya habari hata kama sisi wanahabari tunajua habari hiyo ina mapungufu ya kitaaluma. Nimalizie kwa kuwaasa wananchi wenzangu kila mtu katika eneo lake la kazi afanyekazi kwa bidii kwani nchi yetu bado inaitaji kuletewa maendeleo na sisi wenyewe na ndiyo uchumi wetu utaimarika na kamwe uchumi wa taifa hili hautaweza kukukua kwa kila kukicha kuzuka kwa migomo ya kipumbavu ya wanafunzi wa vyuo na wafanyakazi. Tulishuhudia jinsi ya migomo ya vyuo vya elimu ya juu ilivyokuwa imeshika kasi lakini hatimaye serikali iliamka usingizini na kuanza kuwasaka wanafunzi wanaoshiriki kwenye mikusanyiko haramu na kuwafikisha mahakamani na hatimaye tunaweza kusema hivi sasa hali ni shwari katika vyuo vikuu vingi hapa nchini.Mwaka huu zaidi ya wanafunzi 50 wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, walifunguliwa kesi pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kufanya mkusanyiko haramu na hadi sasa kesi hiyo inaendelea kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema na baadhi ya waadhiri wa UDSM wanasema hatua hiyo ndiyo imesababisha mitihani ya kufunga mwaka wa masomo uliomalizika Julai mwaka huu kufanyika kwa amani bila ghasia. Aidha Januari,Machi na Julai mwaka huu tulishuhudia mgomo wa Madaktari hapa nchini hali iliyosababisha wananchi wenzetu wasiona hatia kupoteza maisha kwa kukosa huduma kwa kile kilichodaiwa na madaktari wanaitaka serikali iwaongezee mishahara,posho na iweke mashine za citscan amasivyo hawatarejea kazini. Lakini mwisho wa siku Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikwenda kufungua ombi dogo Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi dhidi ya Chama cha Madaktari akiomba mahakama isema mgomo ule ni batili na mahakama ilitamka mgomo ni batili na ilimtaka Mwenyekiti wa chama cha Madaktari Dk.Namala Mkopi kwenda kuutangazia umma kuwa mgomo huo ni batili lakini hakufanya hivyo hadi Julai 10 mwaka huu, Dk.Mkopi alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Faisal Kahamba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa mawili ya kudharau amri ya mahakama iliyomtaka akatangaze mgomo ule ulikuwa ni batili na kosa la pili ni kuwashawishi wanachama wake wagome,kesi hiyo imekuja jana kwaajili ya kutajwa. Na hatimaye madaktari wameamua kufyata mkia na kurejea kazi kimya kimya ,wengine wamesimamishwa kazi licha madaktari hawa walikuwa wakijiapiza kuwa hawatarejea makazini hadi madai yao yatekelezwe na Citscan zinunuliwe,lakini wamerejea kazini bila kuboroshewa hayo maslahi wala mazingira ya kazi na cha ajabu hawa madaktari waliokuwa wakijifanya wanamsimamo thabiti wamebaki wakitushangaza ni kwanini wameamua kurejea kazini wakati pia walieleza hawatalejea kazini hadi mwenzao Dk.Steven Ulimboka apone. Pia tujikumbushe katika miaka ya nyuma hapa nchi kulikukwa na kikundi cha baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu waliochoma mabucha yaliyokuwa yakiuza nyama ya Nguruwe pale Manzese, wananchama wa chama cha CUF walikuwa wakipambana na Jeshi la Polisi enzi hizo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Alfred Gewe wakati Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Omar Mahita,wafuasi wa chama cha NCCR-Mageuzi kilichokuwa kikiongozwa na Agustine Mrema. Serikali kupitia vyomvo vyake vya dola iliweza kupambana na makundi hayo ya waandamanaji waliokuwa wakikiuka sheria za nchi na hatimaye ikafanikiwa kuwasambaratisha na ndiyo maana leo hii chama cha CUF,NCCR,TLP na wale waislamu waliokuwa wakivunja mabucha ya nyama ya nguruwe na kuendesha mazoezi ya kareti misikitini hawafanyi tena vitendo hivyo kwani miongoni mwao walipata vilema katika mapambano hayo akiwemo marehemu Sheikhe Magezi. Nimelazimika kwa kusema hapa Tanzania hakuna waandamanaji wa kweli wala wanaharakati.Kuna waandamanaji ‘kunguru’ yaani waoga.Waandamanaji au wagomaji gani kutwa wapo kwenye bar wanakunywa pombe na nyama choma na vimada pembeni wakiburudika kwenye kumbi za starehe na wanawakimbia polisi wanaokuja kutawanya maandamano yao? Waandamanaji,wagomaji na wanaharakati wa kweli wapo nchi za wenzetu huko kama Misri,Libya, Afghanistan,Syria na Somalia ambapo waandamanaji wa huko siyo wanafki,wachumia tumbo tofauti na wanaharakati wapuuzi wa Tanzania ambao miongoni mwao wanadiriki kutoa matamko yao mbalimbali mbele ya waandishi wa habari huku wakinuka Konyagi. Hivyo kimsingi tukubaliane hapa Tanzania hakuna wagomaji na wanaharakati wa kweli kuna wauza sura na masharobalo na wanaotaka kujijenga kisiasa ili mwisho wa siku wawanie nafasi za kisiasa. Na mfano mzuri wala si wa kutafuta ni enzi zile Rais wa CWT alikuwa Magreth Sitta.Sitta alijipambanua kama mtetezi wa maslahi ya walimu na enzi hizo Joseph Mungai ndiyo alikuwa waziri wa Elimu, kila kukicha mwana mama huyu alikuwa akitoa matamko ya kukosoa utendaji wa wizara ile iliyokuwa ikiongozwa na Mungai. Lakini mwaka 2005 Sitta naye aliingia kwenye ulingo wa siasa na kugombea ubunge wa viti maalum na kufanikiwa kupata na Rais Jakaya Kikwete alivyoapishwa Desemba 21 mwaka 2005 na alipounda baraza lake la mawaziri alimteua mama huyo kuwa Waziri wa Elimu, alivyompatia wadhifa huo hadi leo hii sijamsikia tena mama huyo akiendeleza harakati zake za wazi wazi kama zamani za kumtetea mwalimu wa nchi hii. Natoa rai kwa serikali kuanza uchunguzi makini wa vyeti vya taaluma vya walimu wote walioshiriki mgomo ule batili kwani siamini mwalimu aliyesoma kwa kutumia akili zake pasipo kugelezea mitihani au kununua vyetu angekubali kushiriki mgomo wa kipuuzi kama ule. Hivyo nimalizie kwa kuunga mkono kauli iliyotolewa bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema kuwa kazi ya kichwa sio kufuga nywele,ni kufikiri hivyo wafanyakazi wenzangu ambao mnaingizwa kichwa kichwa kwenye migomo hiyo batili mnatakiwa mjiulize na mtafakari kwanza kabla ya kuunga mkono mgomo kwani mwisho wa siku walimu mmejidhalilisha kuwa mmeunga mkono mgomo ambapo mlikuwa hamfahamu kama taratibu za kuitisha zilifuatwa.Niitimishe kwa kuuliza swali je Mkoba ni Kibwetere wa walimu waliogoma? Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika 0716 774494 Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com, Agosti 8 mwaka 2012

HUKUMU YA MAHALU LEO

Na Happiness Katabazi HAKIMU Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Ilvin Mugeta leo anatarajia kuketi kwenye kiti cha enzi na kutoa hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi Na.1/2007 inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia,Profesa Costa Mahalu na aliyekuwa Meneja Utawala na Fedha wa ubalozi huo, Grace Martin. Hukumu hiyo ambayo inasubuliwa kwa shauku kubwa na watu wa kada mbalimbali wakiwemo wasomi wa sheria ,waadhili wa vyuo vikuu,na wanadiplomasia mbalimbali duniani, inatokana na amri iliyotolewa na Hakimu Mugeta Juni 16 mwaka huu, ambapo alizitaka pande mbili katika kesi hiyo Juni 11 mwaka huu, kuwasilisha kwa maandishi maombi yao kuwana washitakiwa wana hatia au la na pande zote zilitekeleza amri hiyo na akaipanga tarehe ya leo kuwa ndiyo siku atakayotoa hukumu ya kesi hiyo ambayo imedumu mahakamani hapo kwa miaka saba sasa ambapo ilifunguliwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Januari 22 mwaka 2007. Awali Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Ben Lincoln, Ponsia Lukosi na Vicent Haule walidai kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa sita ambayo ni kosa la kula njama, wizi wa Euro milioni mbili ,kugushi vocha za manunuzi ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia,kutumia risiti za manunuzi ya jengo hilo kuidanganya serikali na kuisababishia serikali hasara ya Euro milioni mbili. Ili kuithibisha kesi yao,upande wa Jamhuri ilileta jumla ya mashahidi saba ambao ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali ya awamu ya tatu,Martin Lumbanga, Stewart na nyaraka mbalimbali. Wakati upande wa utetezi nao ulileta mashahidi wa tatu ambao ni Mahalu, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Grace Martin ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Mabere Marando, Alex Mgongolwa, Beatus Malima na Cuthbet Tenga na kuwasilisha nyaraka mbalimbali za serikali. Mei 8 mwaka huu, upande wa utetezi ulifunga ushahidi wake baada ya Grace kumaliza kujitetea. Mei 7 mwaka huu,Mahalu ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu kipya cha Bagamoyo cha jijini Dar es Salaam alimaliza kujitetea na siku hiyo ndiyo Rais Mkapa aliandika historia mpya nchini kwa upande wa marais ambapo alifika mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake katika kesi hiyo. Julai 16 mwaka 2009, Jaji Sivangilwa Mwangesi ambaye ndiye alikuwa akiisilikiza kesi hiyo tangu ilipofunguliwa mwaka 2007 alitoa uamuzi wake ambapo aliwaona washitakiwa hao wana kesi ya kujibu. Machi 25 mwaka. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Agosti 9 mwaka 2012.

HAKIMU KESI YA KIBANDA ACHARUKA

Na Happiness Katabazi MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,imetoa amri ya mwisho kwa upande wa Jamhuri katika kesi ya kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima,Absalom Kibanda na wenzake inayoutaka upande wa jamhuri kuwapatia nakala ya maelezo ya awali ya mlalamikaji katika kesi hiyo ili washitakiwa waweze kujiandaa na utetezi. Amri hiyo ilitolewa jana Hakimu Mkazi Waliarwande Lema muda mfupi baada ya wakili jopo la mawakili wa utetezi linaloongozwa na Mabere Marando anayesaidiwa na Isaya Matamba, Juvenalis Ngowi na Hohn Mhozya na Frank Mwilongo kuieleza mahakama hiyo kuwa licha ya Juni 26 mwaka huu kutoa amri iliyoutaka upande wa jamhuri kuwapatia maelezo ya mlalamikaji washitakiwa na kwamba leo kesi hiyo ilikuwa inakuja kwaajili ya mashahidi wa upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao,bado upande wa jamhuri ulikuwa haujawapatia maelezo hayo. “Leo natoa amri ya mwisho kwa upande wa jamhuri uakikishe unawapatia maelezo hayo washitakiwa na ninaiarisha kesi hii hadi Septemba 10 mwaka huu, kesi hii itakapokuja kwaajili ya kuanza kusikilizwa”alisema Hakimu Lema. Awali wakili wa serikali Ester Kyala aliambia mahakama kuwa wakili wa serikali Elizabeth Kaganda ambaye ndiye alikuwa akiendesha kesi hiyo yupo mkoani Arusha kikazi na kwamba yeye jana ndiyo alikuwa amekuja kuiendesha kesi hiyo hivyo akaiadi mahakama kuitekeleza amri hiyo na kukiri kuwa ni kweli hadi kufikia jana upande wa jamhuri ulikuwa haujawapatia maelezo hayo ya mlalamikaji washitakiwa. Mbali na Kibanda washitakiwa wengine ni Samson Mwigamba ambaye ni mwandishi wa makala wa gazeti la Tanzania Daima na Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Theophil Makunga ambapo Desemba mwaka jana ilidaiwa mahakamani hapo na wakili Kaganda kuwa K mshtakiwa wa kwanza na wapili(Mwigamba na Kibanda) wanakabiliwa na kosa la kwanza la kuandika makala ya uchochezi iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “Waraka maalum kwa askari wote’. Alidai kuwa Mwigamba ambaye aliwahi kuwa Mhasibu wa Chama Cha Demokrasi Chadema na Kibanda ambaye ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, kwa pamoja waliandika na waliruhusu makala hiyo ichapishwe kwenye gazeti hilo ambayo iliandikwa na gazeti la Tanzania Daima la Toleo Na. 2552 la Novemba 30 mwaka 2011 na makala hiyo ambayo ni ya uchochezi ikaja kuchapishwa na mshiutakiwa wa tatu (Makunga) kupitia kiwanda cha upachaji ambacho kipo chini ya uongozi wake. “Sisi upande wa jamhuri tunadai kuwa makala hiyo ni ya uchochezi na ilikuwa ikiwashawishi askari wa Jeshi la Wananchi,Polisi,Magereza na KMKM wasiitii amri za makamanda wao jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi na hata Desemba 6 na Desemba 20 mwaka jana, washitakiwa hao walipofika katika Wakili Kaganda alidai kosa la kwanza kosa la kwanza ni la uchochezi kinyume na kifungu cha 32(1)(c) na 31(1)(a) cha Sheria ya Magazeti Sura ya 229 ya mwaka 2002 ambalo lina mkabili mshtakiwa wa kwanza na wa pili yaani Mwigamba na Kibanda. Ambapo wakili Kaganda alidai kuwa mnamo Novemba 30 mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wawili kwa makusudi na kwa nia kuvunja sheria za mamlaka ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walitenda kosa hilo la uchochezi kwa kuruhusu makala hiyo ichapishwe kwenye gazeti la Tanzania Daima la Novemba 30 mwaka 2011 iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “ Waraka Maalum kwa askari wote’ ambapo ilikuwa ikiwachochea askari hao wasitii mamlaka za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Agosti 8 mwaka 2012.

KESI YA DK.MKOPO,BADWEL ZAPIGWA KALENDA

Na Happiness Katabazi UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na kuwashawishi madaktari wagome inayomkabili Rais wa Chama cha Madaktari nchini(MALT), Dk.Namala Mkopi ulieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Wakili wa serikali Mwanaisha Komba mbele ya Hakimu Mkazi Faisal Kahamba aliikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa lakini wanaomba kesi hiyo iairishwe kwa sababu upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Hakimu Kahamba alikubaliana na ombi hilo na akaiarisha kesi hiyo hadi Septemba 3 mwaka huu. Julai 10 mwaka huu, ilidaiwa na wakili wa serikali Tumaini Kweka kuwa kati ya Juni 26 na 28 mwaka huu,Dk.Mkopi akiwa ni Rais wa chama cha Madaktari alidharau amri halali ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ya Juni 26 mwaka huu, ambayo ilimtaka mshitakiwa huyo kwenda kwenye vyombo vya habari kuwatangazia wanachama wa chama hicho wasitishe mgomo kwani mgomo ule waliokuwa wakitaka kuufanya ni batili kama ambayo mahakama hiyo ya Divisheni ya Kazi Juni 22 mwaka huu, ilitoa amri kama hiyo ya kuubatilisha mgomo huo, lakini mshitakiwa huyo hakufanya hivyo. Wakili Kweka alilitaja kosa la pili kuwa ni kuwashawishi madaktari wagome kinyume na kifungu 390 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kuwa Juni 27 mwaka huu, mshitakiwa huyo akiwa rais wa chama hicho aliwashawishi madaktari wasitekeleze amri hiyo ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ya Juni 22 mwaka huu. Wakati huo huo ,kesi ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni moja toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jonathan Liana inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Bahi(CCM), Omary Ahmed Badwel (43) ambayo ilikuja jana mbele ya Hakimu Mkazi Kahamba kwaajili ya kuanza kusikilizwa iliarishwa kwasababu mshitakiwa huyo hakuwepo mahakamani kwasababu amekwenda kuudhulia msiba wa dada yake hivyo hakimu huyo aliarisha kesi hiyo hadi Septemba 3 mwaka huu. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Agosti 7 mwaka 2012.

MAHAKAMA YASEMA MGOMO WA WALIMU NI BATILI

Na Happiness Katabazi MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Kazi jijini Dar es Salaam, imesema mgomo wa walimu ni batili kwasababu haukuzingatia matakwa ya kifungu cha 84(1),(2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazi ya mwaka 2004 na uliandaliwa kwa dhamila mbaya. Jaji Sophia Wambura wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo jana saa 9:14-37 alasiri huku ukumbi wa wazi wa mahakama hiyo ukiwa umefurika walimu ambapo katika uamuzi wake huo pia aliwataka walimu wote kurejea mara moja kazini. Jaji Wambura alisema asikiliza kwa makini hoja za mawakili waandamizi wa serikali Pius Mboya na Obadia Kameya ambao walikuwa wakiwawakilisha walalamikaji katika maombi hayo madogo namba 96/2012 yaliyoletwa chini ya hati ya dharula na Katibu Mkuu Kiongozi,Katibu Mkuu Ofisi ya rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ya mdaiwa ambaye ni Chama cha Walimu Tanzania(CWT) ambao walikuwa wakiwakilishwa na wakili wa kujitegemea Gabriel Mnyele. Jaji Wambura alisema mgogoro uliowasilishwa mbele yake na walalamikaji ni kwamba wanaiomba mahakama hiyo itamke kuwa mgomo wa walimu ni batili wakati wakili wa CWT ,Mnyere alidai mgomo huo ni halali kwa sababu umekidhi matakwa ya sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini. Jaji huyo alisema mahakama yake imefikia uamuzi wa kutofautiana na zoezi la upigaji kura za kuunga mkono mgomo ambalo liliendeshwa na CWT ambapo asilimia 97 ya walimu waliinga mkono kuanza kwa mgomo kwasababu zifuatazo: “Mosi, zoezi lile la upigaji kula lilikuwa likiwadanganya wanachama wa CWT kuwa zoezi hilo limeendeshwa rasmi na kwa mujibu wa sheria,zoezi lile halikukidhi matakwa ya sheria kwasababu wanachama wake walikuwa hawajaelewa na viongozi wa chama hicho madhara ya kufanya mgomo huo,zoezi lile halikufuata taratibu; “Noti ya kugoma iliyotolewa na CWT Julai 27 mwaka huu saa tisa alasiri wakati zoezi la upigaji kura zile lilikuwa bado halijafanyika na kwasababu hiyo zoezi lile likikuwa batili: “Kwa mdaiwa(CWT) kushindwa kufuata matakwa ya kifungu cha 42 na 43 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini,ni wazi taratibu zote walizozifanya za kupiga kura ya kuunga mkono mgomo na kugoma mdaiwa alizifanya akiwa na dhamila mbaya kwani wajumbe wa chama hicho hakuwa na makubaliano ya jinsi mgomo utakavyoendeshwa na kusimamiwa”alisema Jaji Wambura huku baadhi ya walimu wakiwa wamejiinamia. Alisisitiza kuwa CWT imeitisha mgomo huo ikiwa na dhamira mbaya kwasababu ni CWT ndiyo alikataa kuendelea na mazungumzo na mwajiri wake badala yake akaanzisha mgomo wakati Julai 27 mwaka huu, pande zote katika hizo zilifika mbele yake kuomba na upande wa mlalamikaji ukaomba mahakama itoe amri ya kutaka pande zote zisiendelee na jambo lolote hadi mahakama itakapowasilikiliza lakini cha kushangaza siku hiyo hiyo saa tisa alasiri CWT ilienda kutoa noti ya kuanza mgomo kwa walimu nchi nzima ndani ya saa 48 wakati kulikuwa na amri ya mahakama iliyozitaka pande zote kutoendelea kufanya jambo lolote linalohusiana na kesi hiyo ambapo mgomo huo batili ulianza rasmi nchi nzima kuanzia Jumatatu ya wiki hii na hadi sasa unaendelea. “Kwa maelezo hayo hapo juu nasisitiza mgomo huo ni batili kwani haujakidhi matakwa ya kifungu cha 84(1),(2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka,na mgomo uliondeshwa kwa siku tatu sasa ni batili na ninaamuru mgomo huo usitishwe mara moja na walimu wote warejee kazini na kwa kuwa mdaiwa aliitisha mgomo huo kwa mkutumia taarifa kwa vyombo vya habari pia naamuru kiongozi aliyetoa taarifa hiyo ya mgomo aende tena kwenye vyombo vya habari akatangaze kuwa mgomo waliokuwa wakiufanya ni batili na kuwataka walimu warejee kazini mara moja na mahakama hii imemshangaa sana wakili Mnyere kwa kushindwa kuwashauri wateja wake mapema kwamba mgomo waliokuwa wakiundesha ulikuwa umekiuka sheria” alisema Jaji Wambura. Aidha pia naiamuru CWT kulipa gharama na fidia kwa kipindi chote ambacho wanafunzi wamekosa vipindi kwaajili ya mgomo huo batili na kama pande zote zinaona kuna hata ya kurudi meza ya majadiliano zilirudi kwenye meza ya majadiliano na zimualike mtaalamu wa sheria za kazi awasaidie kufikia mwafaka. Baada ya hukumu kutolewa,baadhi ya viongozi wa CWT waliwaomba waandishi wa habari waje nje ya mahakama kwani kutakuwa na mkutano lakini hata hivyo waandishi walipofika nje ya viwanja hivyo mahakama walimkuta Rais wa chama cha walimu,Gration Mkoba akiwa amenyongonyea na hata alipotakiwa atoe tamko ni lini atatekeleza amri ya mahakama iliyomtaka aende kwenye vyombo vya habari autangazie umma kuwa mgomo alioutisha ni batili na awatake walimu warudi kazini alishia kusema leo atafanya mkutano na waandishi wa habari na kwa upande wa wakili wao Mnyere alisema amekubaliana na uamuzi huo wa mahakama. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa,Agosti 3 mwaka 2012

KESI YA VIGOGO WA SUMA JKT YAIVA

Na Happiness Katabazi MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kusutu Dar es Salaam, imesema Agosti 30 mwaka huu, upande wa jamhuri katika kesi ya kula njama na matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili Mkurugenzi wa Shirika Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) Kanali Ayoub Mwakang’ata na maofisa wenzake sita utawasomea maelezo ya awali. Hayo yalisemwa jana hakimu Mkazi Aloyce Katema jana muda mfupi baada ya wakili wa serikali Liz Kiwia kuikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kutajwa na kwamba wanaoiomba mahakama iwapangie tarehe ya kuja kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa. Mbali na Kanali Mwakang’ta washitakiwa wengine ni Luteni kanali Mkohi Kichogo,Luteni Kanali Paul Mayavi,Meja Peter Lushika,Sajenti John lazier,Meja Yohana Nyichi na Mkurugenzi wa Miradi ya Matrekta wa SUMA JKT-Luteni Kanali Felex Samillan. Mawakili toka ofisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa(TAKUKURU) wanaotetewa na wakili wa kujitegema Majura Magafu. Julai 2 mwaka huu, mawakili wa taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Dominsian Kessy na Ben Lincoln waliwafikisha washitakiwa hao mahakamani hapa kwa mara ya kwanza wakidaiwa kutenda kosa la kwanza ni la matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007, inayowakabili washitakiwa wote. Wakili Kessy alidai kuwa Machi 5 mwaka 2009 katika chumba cha mikutano cha ofisi ya SUMA JKT Dar es salaam,wakiwa ni wajumbe wa bodi na Bodi ya Tenda ya SUMA JKT kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kutoa maamuzi ya bodi hiyo ambayo yaliyoonyesha yametolewa na TAKOPA kwa madhumuni ya kununua magari na vifaa vya ujenzi bila kupata idhini ya kutoka Bodi ya ya Wakurugenzi ya TAKOPA. Wakili Kessy alidai kosa la pili pia ni la matumuzi mabaya ya madaraka ambalo linawakabiliwa washitakiwa wote kuwa Machi 12 mwaka 2012 ,washitakiwa hao wakiwa ni wajumbe wa bodi ya Tenda ya SUMA JKT walitumia madaraka yao vibaya kwa kupitishia maazimio ya kununuliwa kwa magari na vifaa vya ujenzi ambavyo vilikuwa vimeishatumika kinyume na kifungu cha 58( 3) cha Sheria ya Mamunuzi ya Umma ya mwaka 2005. Katika hatua nyingine Mkuu wa Gereza la Kuu la Ukonga, Kamishina Msaidizi wa Magereza Estimi Mkwavi(58), alikuja kutoa ushahidi wake katika kesi ya kukutwa na simu gerezani inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba ambapo alidai Julai 27 mwaka 2011 akiwa na wadhifa huo aliletewa taarifa na Supretendant John, kuwa liyumba ambaye alikuwa mfungwa katika gereza hilo amekutwa na simu gerezani. Mawakili wa serikali Humphrei Maricky na Tumaini Kweka ambao walikuwa wakimuongoza ACP-Mkwavi kutoa ushahidi wao alidai kuwa baada ya kupata taarifa hizo aliagiza Liyumba aletwe ofisini kwake ili aweze kumhojia na Liyumba alipofika ofisini kwake walimhoji na alikiri kutenda kosa hilo ila akasema hajisikii vizuri hivyo anaomba atoe maelezo yake kwa njia ya maandishi na aliyatoa maelezo hayo ambayo yanonyesha Liyumba alikiri kukutwa na simu hiyo lakini hata hivyo wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama iisipokee karatasi hilo kwani ungamo hilo halijakidhi matakwa ya kifungu cha 48 na 58 cha Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 ,ambapo vifungu hivyo vinatoa mamlaka kwa mlinzi wa amani na afisa wa polisi kuchukua ungamo la mshitakiwa yoyote na kwamba ungamo hilo halikuchukuliwa na mlinzi wa amani na ofisa wa polisi, hivyo Magafu akaomba mahakama isiipokee hiyo nyaraka inayoonyesha Liyumba alikiri kosa kwasababu ni batili kisherioa. Baada ya mvutano huo wa kisheria hakimu Mkazi Stewart Sanga aliarisha kesi hiyo hadi leo ambapo atakuja kutolea uamuzi wake wa amana nyaraka hiyo ipokelewe kama kielelezo au isipokelewe. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Agosti 2 mwaka 2012.

UAMUZI KESI YA MGOMO WA WALIMU KESHO

Na Happiness Katabazi MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Kazi Dar es Salaam, jana ilishindwa kutoa uamuzi wake kama ilivyoaidi katika maombi madogo yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu Kiongozi na wenzake dhidi ya Chama cha Walimu(CWT), yaliyooiomba mahakama hiyo itoe amri ya muda ya kuzuia mgomo wa walimu unaoendelea chini nzima kwasababu mgomo huo ni batili. Mbali na Katibu Mkuu Kiongozi walalamikaji wengine ni Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Na.1/2012 dhidi ya CWT wanaowakilishwa na mawakili wa waandamizi wa serikali Pius Mboya na Obadia Kameya. Ambapo wakili Kameya ambapo walalamikaji hao wanaomba mambo mawili ambayo wanaomba mahakama itamke mgomo huo ni batili kwasababu haujakidhi matakwa ya kifungu cha 26(1) cha Sheria ya Usuluhishi wa migogoro ya mwafanyakazi Na.6 ya mwaka 2003 ,ambapo kifungu hicho kinatoa utaratibu wa mtumishi wa umma azifuate kabla hajaanza kugoma ambapo zinataka mfanyakazi anayetaka kugoma kwanza atoe hati ya kukusudio la mgomo wa serikali siku 60. Jambo ambalo CWT hawakulizingatia kabla ya kutangaza nia yao ya mgomo ambayo waliitangza Julai 27 mwaka huu tena bila kuwapatia nakala ya kusudio hilo walalamikaji. Ombi la pili wakili Kameya anaomba mahakama hiyo itoe amri ya kuzuia kuendelea kwa mgomo batili kwasababu unaathiri wanafunzi na kuleta mashadhara makubwa ambayo hayalipiki kwani serikali imeweka mitaala ya elimu mashuleni na shule zimeweka muda wa vipindi kufundishwa hivyo kuendelea kuwepo kwa mgomo ni wazi kuna vuruga malengo ya mitaala na muda wa vipindi mashuleni. Wakili Kameya pia aliomba mahakama imumzuei Rais wa CWT,Gration Mukoba na wenzake kutoka kwenda tena kwenye vyombo vya habari kuelezea kesi ya msingi iliyopo mahakamani hapo kwani juzi walienda kwenye vyombo vya habari na kuizungumizia kesi hiyo jambo ambalo ni kinyume cha sheria na pia wanaiomba mahakama itoe amri ya kumtaka Mkoba kwenda kwenye vyombo vya habari kuuutangazia umma kuwa mgomo huo ni batili na awataka walimu wote warejee makazini. Mawakili hao wa serikali na wakili wa utetezi Gabriel Mnyele walianza kuwasilisha hoja zao tangu saa sababa mchana hadi saa kumi jioni, ambapo kwa upande wake Mnyele alidai mgomo huo wa walimu haujakiuka sheria zozote za nchi kwani umekithi matakwa ya Sheria Na. 4 ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2006, ambayo inamruhusu mfanyakazi wa serikali au sekta binafsi kutoa hati ya kusudio la kutaka kugoma ndani ya 48 kama walivyofanya CWT. Na kwa mujibu wa madai ya msingi wanayoyadai walimu hao ambayo ndiyo yamesababisha wagome ni kutaka kuishinikiza serikali iwaongezee mshahara kwa asilimia mia moja. Baada ya mawakili hao kumaliza kuwasilisha hoja zao saa 10:45 jioni katika mahakama ya wazi ndipo Jaji Sophia Wambura alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili na akaairisha shauri hilo kwa nusu saa na kwamba akirejea tena ndiyo atatoa uamuzi wake kuhusu hoja hizo. Ilipika saa 12:6 jioni huyo aliingia kwenye ofisi yake badala ya ukumbi wa wazi wa awali aliokuwa akisikilizia kesi hiyo na kusema kwa kifupi tu ‘uamuzi wa malumbano hayo ya kisheria atautoa kesho saa nane mchana. Baada ya jaji huyo kumaliza kusema maneno hayo kwa kifupi, baadhi ya walimu waliokuwa wamefika mahakamani hapo walisikika wakisema na kuwapigia simu wenzao kwakuwa mgomo huko pale pale kwani mahakama haijatoa amri ya kuzuia mgomo wao. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Agosti Mosi mwaka 2012.

BALALI ATAJWA TENA KESI YA EPA

Na Happiness Katabazi MSHTAKIWA wanne katika kesi ya wizi wa zaidi ya sh.bilioni 3.9 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania, Imani Mwakosya (54) jana ameileleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salama, kuwa aliyekuwa gavana wa wakati huo marehemu Daudi Balali ndiye aliyeidhinisha kiasi hicho cha fedha kilipwe kwa kampuni ya Mibare Farm kwakuwa ilionekana ni deni halali. Mwakosya anayetetewa na wakili wa kujitegemea Majura Magafu alitoa maelezo hayo mbele ya jopo la majaji Samuel Kalua,Beatrice Mutungu na Hakimu Mfawidhi Ilvin Mugeta wakati akitoa utetezi wake Mshtakiwa huyo ambaye alikuwa kifanya kazi idara ya Madeni BoT,alidai kuwa nyaraka mbalimbali vilizowasilishwa BoT na kampuni hiyo wakati ikiombwa kulipwa fedha hizo,zilionekana ni halali baada ya kupitiwa na maofisa mbalimbali wa benki hiyo. Mwakosya alizitaja baadhi ya nyaraka hizo kuwa ni pamoja na hati ya makabidhiano ya kuamisha deni hilo baina ya Kampuni ya Mibare Farm na Kampuni ya Lackshim Textile Mills Ltd ya India. Alidai kuwa deni hilo pia lilionekana katika mtandao wa BoT huku taarifa zake zikionekana kulingana na vielelezo zilivyowasilishwa na kampuni ya Mibare Farm wakati wakidai deni hilo. "Napenda mahakama ielewe kuwa malipo yalifanyika kihalali kwasababu vithivitisho vyote vilivyotakiwa kuthibitisha deni vililetwa BoT na vilitiwa na vikaonekana halali na ndipo gavana alipitisha malipo hayo"alidai Mwakosya. Alidai kuwa katika mchakato wa ulipwaji wa deni hilo yeye aliwahi kuandika dokezo la kulipwa kwa deni hilo kwenda kwa gavana. Alidai kuwa kampuni ya Kampuni ya Lackshmi Textile Mills Ltd ya India ilikuwa inaidai serikali ya Tanzania Yeni milioni 307,595,400 pamoja na fedha za india rupia milioni 29,220,686.92 ambazo ni sawa na sh.bilioni 3,868,805,737.13 Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kada wa CCM Rajabu Maranda,Farijala Hussein ambao tayari wameishafungwa jela jumla ya miaka nane katika kesi mbili tofauti za EPA, Ajay Somani, Ester Komu na Sophia Lalika. Katika kesi hiyo washitakiwa hao wanadaiwa kula njama,kugushi na kuiba zaidi ya Shbilioni 3 .8 kutoka BoT, baada kudanganya kuwa imepewa deni na Kampuni ya Lackshim Textile Mills Ltd ya India na kujipatia inginzo hilo. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Julai 31 mwaka 2012

KAKOBE AKWAA KISIKI MAHAKAMANI

Na Happiness Katabazi HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBC) Zakaria Kakobe dhidi ya wachungaji wa tatu wa kanisa hilo waliomfungulia kesi ya ubadhirifu wa fedha za kanisa hilo. Kesi hiyo namba 79/2011 ilifunguliwa Mei 26 mwaka 2011 na wachungaji watatu wa kanisa hilo, Mchungaji Deuzidelius Patrick, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma. Wachungaji hao wanamtuhumu Askofu Kakobe kuwa amekuwa akifanya ubadhirifu wa fedha wa kanisa hilo Sh.bilioni 14 14 na anakiuka matakwa ya Katiba ya kanisa hilo. Kakobe kupitia kwa wakili wake Miriamu Majamba aliwawekea pingamizi la awali walalamikaji hao akidai kuwa hawana haki ya kisheria kumfungulia kesi hiyo Kakobe kwasababu si wachungaji wa kanisa hilo kwasababu Bodi ya Wadhamini wa Kanisa hilo ilishawafunguza uchungaji tangu mwaka 2010. Hata hivyo mahakama baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili , Kakobe kupitia kwa wakili wake, Majamba na walalamikaji kupitia kwa wakili wao Barnaba Luguwa zilizowasilisha kwa njia ya maandishi, ilitupilia mbali pingamizi la Kakobe na kulikubali ombi la walalamikaji . Katika uamuzi wake dhidi ya pingamizi hilo la awali, alioutoa Julai 16 na Jaji Agustine Shangwa alisema kuwa hati ya madai ya walalamikaji haioneshi sababu za madai na kwamba hawana haki ya kisheria kumfungulia mashtaka Askofu Kakobe . Jaji Shangwa alisema kuwa anakubaliana na wakili wa walalamikaji, Luguwa, kuwa hati ya madai ya walalamikaji hao inabainisha cause of action kwa maana ambayo kinadharia ina madai ambayo walalamikaji watapaswa kuyathibitisha. Aliyataja baadhi ya mambo ambayo walalamikaji hao watapaswa kuyathibitisha na kwamba kama yakithibitika Kakobe atawajiba kwayo kuwa ni pamoja na mabilioni ya fedha za kanisa hilo ambayo wanamtuhumu Kakobe kuyatafuta. Mengine ni mahubiri ya uwongo kwa waumini wa kanisa hilo kuwa kwa kufunga pamoja naye watakingwa dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi au kwamba wanaweza hata kuponywa kwa jina la Yesu anayemwabudu. Katika hilo Jaji Shangwa alisema kuwa walalamikaji watapaswa kuthibitisha kwamba mahubiri hayo ya uwongo ni makosa wanapaswa kulipwa fidia au kuadhibiwa. Madai mengine ni kuwa Askofu Kakobe amekuwa akiwafungisha ndoa waumini wake bila kuwapa vyeti vya ndoa na kwamba kwa kufanya hivyo ni kosa ambalo watapaswa kulipwa fidia au mlalamikiwa kuadhibiwa. BAADA YA KUSOMA UAMUZI Baada ya kutoa uamuzi huo Jaji Shangwa alipanga shauri hilo kuendelea Agosti 6, 2012, kwa ajili ya hatua ya usuluhishi huku akiwataka walalamikaji katika kesi hiyo kuwatafuta maaskofu wengine kutoka madhebu tofauti tofauti ili kutoa ushauri wa masuala ya kidini na kiimani ambayo mimi siyajui . Hata hivyo alisema hiyo ni hiyari yao wakiona ni vema kufanya usuluhishi na kuongeza kuwa kama hatakuwa tayari naye atalipeleka jalada hilo kwa Jaji Mfawidhi ili wapangiwe jaji wa kuanza kuisikiliza rasmi kesi yao. Jaji Shangwa alisema kuwa kesi hiyo ni kubwa na kwamba ndio maana alishauri mapema wahusika katika kesi hiyo wapatane kwanza wenyewe kwa kuwa ni hatari kwa upande ambao utashindwa. Mkithibitisha kuwa hatoi vyeti wakati anapofungisha ndoa hili litakuwa ni kosa kubwa kisheria na uthibitisho wa kwanza utoke kwenu wenyewe.”, alisem Jaji Shangwa. Katika hati ya madai yao, walalamikaji hao wanamtuhumu Kakobe kuwa amekuwa akikusanya pesa nyingi kutoka kwa waumini wake kwa madai ya kufanyia shughuli na miradi mbalimbali ya kanisa na kuzitumia kinyume cha malengo. Mbali na kuzitumia fedha hizo isivyo kama vile kugharimia kampeni za kisiasa kinyume cha katiba ya kanisa hilo, pia wanadai kuwa Kakobe amekuwa hatoi taarifa ya mapato ya pesa anazozikusanya wala matumizi yake. Kuhusu ukiukwaji wa Katiba ya kanisa hilo, walalamikaji hao wanadai kuwa katiba inataka kuitishwa kwa mkutano mkuu kila baada ya miaka mitano ambao ndio chombo cha juu cha maamuzi lakini Kakobe hajawahi kuitisha mkutano huo tangu mwaka 1989. Pia wanadai kuwa katiba hiyo inaelekeza kuwa kanisa liwe na Katibu Mkuu na Mweka Hazina ambao ndio watakaolinda mali za kanisa lakini Kakobe ndio amekuwa akifanya maamuzi na shughuli zote yeye mwenyewe. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Julai 19 mwaka 2012.