DPP AKWAMISHA KESI YA VIGOGO SUMA JKT

DPP, Eliezer Feleshi
Na Happiness Katabazi 

KESI ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili Mkurugenzi wa Shirika la Kujenga Taifa (SUMA JKT), Kanali Ayoub Mwakang’ata na maofisa wengine wa jeshi hilo jana ilishindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwasababu jarada la kesi hiyo bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),Dk.Eliezer Feleshi Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Tabu Mzee mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana alieleza kuwa kesi hiyo jana isingeweza kuendelea kwasababu bado DPP haijarudisha jarada la kesi hiyo mahakamani hapo tangu ilipoliitisha jarada hilo ofisini kwake hivi karibuni. 

Hata hivyo Wakili Tabu aliomba kesi hiyo iarishwe na ipangiwe tarehe ya kuja kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao, ombi ambalo lilikubaliwa na Hakimu Katemana ambaye aliarisha kesi hiyo hadi Oktoba 26 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya upande wa Jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao. 

 Mbali na Kanali Mwakang’ata washitakiwa wengine ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na TAKUKURU, Julai 2 mwaka huu, ni Luteni Kanali Mkohi Kichogo,Luteni Kanali Paul Mayavi,Meja Peter Lushika,Sajenti John lazier,Meja Yohana Nyichi na Mkurugenzi wa Miradi ya Matrekta wa SUMA JKT-Luteni Kanali Felex Samillan wanaotetewa na wakili wa kujitegemea Majura Magafu.

Wanakabiliwa na makosa ya kula njama na matumuzi mabaya ya madaraka kuwa washitakiwa wakiwa ni wajumbe Ilidai kuwa Machi 5 mwaka 2009 katika chumba cha mikutano cha ofisi ya SUMA JKT Dar es salaam,wakiwa ni wajumbe wa bodi na Bodi ya Tenda ya SUMA JKT kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kutoa maamuzi ya bodi hiyo ambayo yaliyoonyesha yametolewa na TAKOPA kwa madhumuni ya kununua magari na vifaa vya ujenzi bila kupata idhini ya kutoka Bodi ya ya Wakurugenzi ya TAKOPA. 

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Septemba 29 mwaka 2012.

KESI YA DK.NAMALA MKOPI YAFIKA PATAMU

Na Happiness Katabazi UPANDE wa jamhuri katika kesi ya kudhalau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi inayomkabili Rais wa Chama cha Madaktari nchini(MALT), Dk.Namala Mkopi ulimsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam. Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Hakimu Mkazi Faisal Kahamba aliikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya upande wa jamhuri kumsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo anayekabiliwa na makosa mawili ya kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kinyume na kifungu cha 124 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 na kosa la pili ni kuwashawishi madaktari wagome. Wakili Kweka alianza kumsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo na kudai kuwa Dk.Mkopo daktari wa binadamu aliyeajiliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili. Alidai kuwa Dk.Mkopi ni mwanachama (MAT) ambacho kimeanzishwa na madaktari ambacho pia kinaishauri serikali katika mambo ya afya na utabibu na pia kunasimamia na kulinda maadili ya wanachama wake na kwamba mwaka 2011 mshitakiwa huyo alichaguliwa kuwa rais wa chama hicho. “Juni 2012 madaktari wanaofanyakazi katika hospitali za serikali waliingia kwenye mgomo dhidi ya mwajiri wao ambaye ni serikali na mgomo huo uliandaliwa na MAT na madaktari hao waligoma kuwahudumia wagonjwa wakati wakati mkatabao wao waajira waliongia na serikali ni kuwatibia wagonjwa”alidai Kweka. Wakili Kweka alidai kuwa wakati mgomo huo ukiendelea serikali ilipeleka maombi No.73 ya mwaka 2012 katika Mahakama Kuu Diveshini ya Kazi yaliyokuwa yakiomba mahakama hiyo itoe amri ya kuzuia mgomo huo usiendelee hadi pale ule mgogoro baina ya MAT na serikali ulifunguliwa katika Tume ya Usuluhishi wa migogoro (CMA) uliosajiliwa kwa namba CMA/DSM/ILA/145/12 mbele ya Jaji Moshi utakapomalizika. Aidha Kweka alidai kuwa Juni 22 mwaka huu,Mahakama Kuu ilitoa amri ya kuwataka madaktari waliogoma nchi nzima wasitishe mgomo na mahakama hiyo ikampatia nakala ya amri hiyo mshitakiwa (DK.Mkopi) ,Juni 25 mwaka huu. “Licha ya mshitakiwa kupatia amri hiyo ya mahakama ambayo aliipokea yeye na madaktari wenzake waliendeleza mgomo huo na Juni 26 mwaka huu, Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ilitoa amri nyingine kwa MAT iliyokuwa ikikitaka chama hicho kutekeleza kwa vitendo amri ya mahakama iliyotolewa Juni 22 mwaka huu ambayo ilimtaka Dk.Mkopi kwenda kwenye vyombo vya habari kuwatangazia madaktari wote waliogoma wasitishe mgomo huo; “Lakini Dk.Mkopi alishindwa kutekeleza amri hizo mbili za Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na matokeo yake yeye na madaktari wenzake wakaendelea na mgomo na kwamba Julai 9 mwaka huu, mshitakiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani hapa Julai 10 mwaka huu na kufunguliwa kesi hii iliyopo mbele yako Mheshimiwa Hakimu”alidai Kweka. Kwa upande wake Dk.Mkopi alidai ameyasikia maelezo hayo aliyosomewa wakili Kweka ila anakanusha kuwa yeye siyo daktari wa Hospitali ya Taifa ya Mhimbili ila anakubali kuwa ni kweli yeye ni daktari wa binadamu na anakataa kuwa madaktari hawakugoma kuwatibia wagonjwa na kwamba si kweli kuwa alidharau amri ya mahakama ya Juni 22 mwaka huu iliyomtaka aende kwenye vyombo vya habari kuwatangazia madaktari waache kugoma. Hakimu Kahamba aliarisha kesi hiyo hadi Oktoba 23 mwaka huu, ambapo siku hiyo kesi itakuja kwaajili ya mashahidi wa upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao. Julai 10 mwaka huu, ilidaiwa na wakili wa serikali Lasdiraus Komanya kuwa kati ya Juni 26 na 28 mwaka huu,Dk.Mkopi akiwa ni Rais wa MAT alidharau amri halali ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ya Juni 26 mwaka huu, ambayo ilimtaka mshitakiwa huyo kwenda kwenye vyombo vya habari kuwatangazia wanachama wa chama hicho wasitishe mgomo kwani mgomo ule waliokuwa wakitaka kuufanya ni batili kama ambayo mahakama hiyo ya Divisheni ya Kazi Juni 22 mwaka huu, ilitoa amri kama hiyo ya kuubatilisha mgomo huo, lakini mshitakiwa huyo hakufanya hivyo. Wakili Kweka pia alidai kosa la pili ni kuwashawishi madaktari wagome kinyume na kifungu 390 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kuwa Juni 27 mwaka huu, mshitakiwa huyo akiwa rais wa chama hicho aliwashawishi madaktari wasitekeleze amri hiyo ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ya Juni 22 mwaka huu,na matokeo yake madaktari hao wakagoma. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa,Septemba 28 mwaka 2012.

JUGDEMENT OF CHRISTOPHER MTIKILA CASE

IN THE RESIDENT MAGISTRATES’ COURT OF DAR ES SALAAM AT KISUTU CRIMINAL CASE NO. 132 OF 2010 REPUBLIC VERSUS CHRISTOPHER MTIKILA JUDGMENT As it will be clear shortly the facts of this case are simple and straight forward. The accused person, Christopher Mtikila is charged with two counts. The first one is unlawful distribution of seditious publication contrary to section 32 (1) (c) of the News papers Act, Cap.229 R.E. 2002. The second count is unlawful possession of seditious publication contrary to section 32 (2) of the same Act. The particulars of the offence in the first count are that between 1st November, 2009 and 17th April, 2010 in the city and region of Dar es Salaam with seditious intention the accused person did distribute to the general public a seditious publication titled “Kikwete Kuangamiza Kabisa Ukristo! (Wakristo wasipoungana upesi kuweka Mkristo Ikulu)” knowing it to be seditious. In the second count the particulars of the offence are that on 16th April 2010 at Mikocheni area within the District of Kinondoni in the city and region of Dar es Salaam, without any lawful excuse the accused person was found in possession of a seditious publication. The accused person neither disputes to have possessed nor distributed the alleged seditious document which was admitted in evidence as exhibit P3. He also does not dispute to author it. As already indicated above exhibit P3 is entitled “Kikwete kuangamiza kabisa ukristo (Wakristo wasipoungana upesi kuweka Mkristo Ikulu)”. The offending exhibit P3 is a twenty four (24) pages document the contents of which, I must say, is glaringly outrageous. Even so, in his defence the accused person was emphatic that he prepared, printed, and distributed the impugnable document. The only thing he strongly disputes is the allegation that it is seditious. To him the document is an epistle based and prepared in practice of his faith. He further contended in his evidence that in preparing and distributing exhibit P3 he was proclaiming his religious faith. This is a serious allegation which needs to be taken seriously. I say so because matters of religion and faith are so complex and when they are subject of litigation and adjudication they cover a “handle with care” region. This notwithstanding I must decide this case on the facts presented by the parties. It is a noble duty I cannot abdicate. It is due to the fact that the accused person does not dispute to have possessed and distributed exhibit P3 I see no need to reproduce the evidence tendered by the parties. It suffices to say that the prosecution, in a bid to prove their case, brought in court a total of four witnesses. These are Bernette John Kipasika, Daniel David Kikunile, Isack Pingini and Ebeneza Mrema who testified as PW1, PW2, PW3 and PW4 respectively. The evidence of PW2 is to the effect that the accused person distributed exhibit P3 to them while that of PW1 and PW3 is to the effect that the house of the accused person was searched and copies of exhibit P3 were retrieved therefrom as evidenced by exhibit P1. This is a certificate of seizure. The evidence of PW4 is to the effect that he recorded the caution statement of the accused wherein he admitted to have prepared and distributed the offending document. The caution statement was admitted as exhibit P4. In a nutshell this is the gist of the prosecution evidence. As I have said the accused person does not dispute all these facts. In this judgement therefore I will concentrate on discussing the content of this document in relation to the offences charged with view to determine if it is seditious. For clarity let me say this at this juncture. That since I do not know if the accused person still stands by his words which he made in 2010 I will use the past tense when explaining and analyzing the contents of exhibit P3 in order to contectualise it. Briefly the document curses President Jakaya M. Kikwete and Islamism. The author says Honourable Kikwete and Muslims were determined to extinguish Christianity in the United Republic of Tanzania. So he was calling upon all Christian to stand up to defend their faith (Christianity) and elect a Christian God fearing president who will lead the nation to prosperity! The accused person believes he was justified to write exhibit P3 because the church and politics cannot be separated. His position on this issue is clear from his evidence. This is how the accused person ended his evidence in chief: “If the church is not indifferent in the face of the major objectives of mankind, it is required to show proof of it in practice and achievement. The church must be present at all crisis points in the human panorama. There where good and evil is being forged. During times of happiness and misery of mankind there where the future of the world is being built. So your Honour, it is needless to say that all these take place not at the pulpit but above all it takes place in the field of politics. Disengagement of the church from the administration of the country is a myth. That is why many scriptures from the holy bible and this epistle are commanding good governance of the Nation in accordance with the perfect will of God”. I have deliberately quoted this message in extenso because it expresses the reason behind the accused writing and circulating exhibit P3. In the accused person’s views he was publicizing his religion. This is what he believes, rightly or wrongly. In his evidence he even wondered why he should be charged for practicing his faith. He said: “My soul suffers much on seeing that Christ is now being challenged in court” Be as it may here in court we are doing law not theology. Conversely, I must acknowledge, the accused person’s theological virtue is mystifying. Needless to say under article 3 of the Constitution, Tanzania is a democratic secular state. It does not need a Christian leader to achieve prosperity as the accused person alleges and would want us believe. For one reason that the accused person admits possession and publication of the offending document the only issue for my determination is whether the document is seditious. Should this issue get an affirmative answer he will be automatically convicted. Then what is sedition? The Newspapers Act [Cap 229 R.E. 2002] does not define this term. However, section 31 of the Act provides for what constitutes seditious intention. It says seditious intention is an intention:- a) To bring into hatred or contempt or to excite disaffection against the lawful authority of the United Republic of Tanzania or the Government thereof; b) To excite any of the inhabitants of the United Republic to attempt to procure the alteration, otherwise than by lawful means of any other matter in the United Republic as by law established; c) To bring into hatred or to excite disaffection against the administration of Justice in the United Republic; d) To raise discontent or disaffection amongst any of the inhabitants of the United Republic; e) To promote feelings of ill-will and hostility between different categories of the population of the United Republic; It follows therefore that any publication is said to be seditious if it fits in any one of the above described seditious intentions. Besides providing for seditious intentions the Act also offers a yardstick for determination of whether act done, words spoken or document published is seditious. This is provided under section 31 (3) of the Newspaper Act which provides:- “In determining whether the intention with which any act was done any words spoken or any document was published, was or was not seditious, every person shall be deemed to intend the consequences which would naturally follow from his conduct at the time and in the circumstances in which he so conducted himself” In my view for an act, word spoken or document published to be held to be seditious such act, spoken words or publication need to be followed by certain consequences. It is my further humble view that mere publication without consequences of causing hatred, contempt, excitation of disaffection, attempt to procure alteration of any matter by unlawful means, to raise discontent and promoting feelings of ill-will cannot amount to sedition. I have reached this conclusion after reading the above provision with utmost care because a casual reading may impute an interpretation that intention without consequences makes the offence complete which view, for some reasons, I would not subscribe to. The first reason is that if the law is to be interpreted that way, the net would be cast so wide to make the law uncertain and arbitrary. Our Constitution provides and guarantees freedom of expression under article 18. In the case of Kukutia Ole Pumbun and another vs the Attorney General and another [1993] TLR 159 the Court of Appeal held that a law which seeks to limit or derogate from the basic rights of an individual must not be arbitrary and the limitation it imposes must be not more than is reasonably necessary to achieve a legitimate objective. In that regard provisions relating to the offence of sedition must be restrictively interpreted to conform to constitutional guarantee. This object cannot be achieved if a wider interpretation is given to the law relating to sedition. The uncertainty of the offence of sedition is exacerbated with lack of definition for the offence. It is my humble view that lack of definition of the offence and the vagueness with which the sections creating the offence are crafted makes one uncertain of the boundary where to stop while exercising one’s right of expression under the Constitution. Secondly in the case of Imunde vs Republic [1991] KLR, 230 it was held that the law on sedition does not punish the intention per se. It punishes when and only if it is exhibited or manifest in a manner tending to bring about disorder. I understand this case has a persuasive value only but I am convinced that is how the law should be interpreted. In that connection this idea is buttress by statements in the Commentaries on English Law where key elements of the offence of sedition are said to be:- i. Violence ii. Incitement for violence iii. Incitement for public disorder iv. Incitement for insubordination of lawful authority. It is my view that these elements are only manifest in obvious consequences which are not imaginary intention. Therefore, the outcome of the alleged seditious act must be real and vivid not mere likelihood. There is a Ugandan case which supports my above view too. This is the case of Andrew Mujuni & Another vs Attorney General, Consolidated Constitution Petitions No. 12/2005 and No. 3/2006. In this case the Constitutional Court of Uganda held that proof of the offence of sedition needs evidence as to what was the reaction of community. I fully associate myself with this view and hold that for the offence of sedition to augur well with the constitutional guarantee of freedom of speech the offence must be manifest by certain consequences like violence or preparations geared to causing disorder. So I hold that for accused person to be convicted of sedition there must be evidence about resultant disorder of the publication of the seditious material. This said did publication of exhibit P3 result into any of the above consequences which constitute seditious intentions per section 31 of the Newspaper Act? The evidence will tell us. Unfortunately the charges in all counts do not state which seditious intention was the publication intended to achieve. I think the charges had to contain such clear information for the accused person to appreciate what he pleaded to and to enable him prepares his defence with certainty. The prosecution has taken for granted that mere allegation that the material is seditious without describing a specific seditious intention is enough. This notwithstanding I will try to find out if exhibit P3 is seditious per the intentions above described. I start with the issue of causing alteration with unlawful means. I have read exhibit P3 and I am satisfied that the accused person being a Christian believes for Tanzania to prosper it must be governed by a Christian president. Therefore, under the guise of Christianity he tried to persuade his fellow Christian to remove President Kikwete in office because he is a Muslim. Exhibit P3 therefore is a call for change of state leadership from Islamic to Christianization! I have seriously pondered over this issue and I am now satisfied that such an act is an offence under section 31 (1) (b) of the Newspapers Act if two conditions are met. These are where the publication would have suggested his removal by unlawful means and attempt towards that end made. Both the conditions must exist conjunctively. Interestingly exhibit P3 does not suggest the means to be used by the Christians to remove the President from office. Further there is no evidence that there is any Christian religious sect which has ever attempted to remove the president from office. According to exhibit D1 which is newspaper with a story about the accused person’s teachings about removal of President Kikwete from office, the suggested means was the ballot box. Exhibit D1 was tendered by Mpoki Bukuku who works for the Mwananchi newspaper. Exhibit D1 was published on 6th August, 2009 and its contents tallies with the testimony of the accused person (DW1) that the offending document was issued for the first time in Mwanza during a congregation of about five hundred (500) bishops who met in Mwanza to deliberate on the state of the Christian faith in Tanzania in relation to the then forthcoming general election in the 2010. In short the accused persons urged his fellow Christians not to vote for President Kikwete and CCM in the 2010 general elections. Section 21 (2) (c) of the Newspapers Act provides:- “(2) an act, speech or publication is not seditious by reason only that it intends: a) ... b) ... c) To persuade any inhabitants of the United Republic of Tanzania to procure by lawful means the alteration of any matter in the United Republic of Tanzania as by law established. d) … It is my view that the office of the President is legally established and the President is lawfully voted in office. Therefore, in the context of the Newspaper Act Presidency and the President are “lawfully established matter”. To procure alteration (removal) of either of them is the unlawful act envisaged under section 31 (1) (b) Has the accused suggested removal of the president by unlawful means? In my view he has not. Exhibit P3 does not suggest any unlawful means to remove the President. His document is full of lamentations about his dissatisfaction on how the country is governed. Further, if exhibit D1 is something to go by the accused person suggest removal of the president through the ballot box. This cannot be an offence. Let me be explicit on this point because it is likely raise eye brows. I said from the very beginning that the language in exhibit P3 is uncouth. It tests sour in the ears. Therefore, the accused person may be guilty of trying to divide the nation on religious grounds. But the point I am trying to put across is the act by itself is not seditious Let me now test the content of exhibit P3 in line with the provisions of section 31(1)(e) of the Newspaper Act. Did it promote feeling of ill-will and hostility between Christians and Muslim? My simple answer is that no evidence to that effect can be traced on record. This said the test goes to find whether exhibit P3 meets the seditious intentions described in sections 31(1)(a), (c) and (d) of the Newspapers Act. In that regard the resultant questions are: Firstly, did exhibit P3 bring into hatred or contempt or to excite disaffection against the lawful authority? Secondly, did it bring into hatred or to excite disaffection against the administration of Justice? And finally did it raise discontent or disaffection amongst any of the inhabitants? Again there is no evidence to that effect. From the foregoing the above main issue in this case must be answered in the negative. This disposes of this case. I hold that the charges against the accused person have not been proved and I accordingly acquit him of the charges in both counts. I.C. MUGETA – SRM 25/09/2012 Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com; Septemba 25 mwaka 2012

MTIKILA AMWANGUSHA KIKWETE KORTINI

Na Happiness Katabazi HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ,imemfutia kesi ya uchochezi ya kuchapisha na kumiliki waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete iliyokuwa ikimkabili Mwenyekiti wa Chama cha Democratic(DP), Mchungaji Christopher Mtikila badaa ya upande wa jamhuri kushindwa kuleta ushahidi wa kuthibitisha kesi hiyo. Hukumu hiyo ya kesi hiyo ya jinai Na.132/2010 ilitolewa jana mchana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,Elvin Mugeta ambapo alianza kwa kuikumbusha mahakama hiyo kuwa mshitakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na makosa mawili.Kosa la kwanza ni kusambaza waraka wa uchochezi kinyume na kifungu cha 32(1),(c) cha Sheria ya Magazeti ya mwaka 2002 na kosa la pili ni la kumiliki waraka huo wa uchochezi kinyume na kifungu cha 32(2) cha sheria hiyo. Hakimu Mugeta aliyasoma maelezo ya makosa hayo kuwa ilidaiwa na wakili wa serikali mwaka 2010 mahakamani hapo kuwa Novemba 1 mwaka 2009 na April 17 mwaka 2010 jijini Dar es Salaam, akiwa na nia ya kutenda kosa la uchochezi ,Mtikila alisambaza kwa umma waraka huo uliokuwa na kichwa cha habari kisemacho (Kikwete Kuangamiza Kabisa Ukristo!(Wakristo wasipoungana upesi kuweka Mkristo Ikulu),huku akijua kufanya hivyo ni uchochezi. Na maelezo ya kosa la pili ni kwamba katika ya Aprili 16 mwaka 2010 huko Mikocheni alikutwa akimiliki waraka huo wa uchochezi. Akianza kusoma hukumu yake Hakimu Mugeta ambaye alisema kwanza Mtikila katika utetezi wake alikiri kuaanda waraka huo na alikiri pia alikuwa akiumiliki waraka huo na kwamba waraka huo ulitolewa mahakamani hapo kama kielezo cha tatu na jumla ya mashahidi wanne waliletwa na upande wa Jamhuri kuthibitisha kesi hiyo wakati Mtikila akuleta shahidi,alijitetea yeye mwenyewe kwa madai hakuona haja ya kuwaleta mashahidi kwasababu endapo angefanya hivyo angekuwa anamaliza fedha za mahakama na kupoteza muda wa mahakama bure. Hakimu Mugeta alisema kufuatia mashitaka yanayomkabili mshitakiwa kabla ya kutoa hukumu yake alijiuliza maswali yafuatayo kuwa je ni kweli waraka huo ni wa uchochezi?Je waraka huo ulileta madhara katika jamii?Je waraka huo wa mshitakiwa ulikuwa ukitaka kumpindua rais Kikwete kinyume na sheria za nchini kwani ofisi ya Rais imeanzishwa kwa sheria husika? “Mimi nimeusoma waraka huo unaodaiwa na upande wa Jamhuri kuwa ni uchochezi na nimebaini kuwa waraka huo si wa uchochezi kwani Mtikila licha ni mwanasiasa pia ni kiongozi wa kidini na waraka ule ulikuwa umejaa maneno ya kidini ambayo ndani yake Mtikila alikuwa akiwataka wakristo wenzake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 watumie haki yao ya msingi ya kumpigia kura mgombea ambaye ni mkristo … na kumng’oa madarakani rais Kikwete kwa njia ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu siyo kosa la jinai: “Kitendo ambacho mahakama hii kwa kauli moja imeona upande wa Jamhuri imeshindwa kuleta ushahidi unaonyesha Mtikila alikuwa anataka wakristo wamuondoe rais Kikwete Ikulu kwa njia haramu na pia kusambazwa kwa waraka huo na mshitakiwa kulileta madhara na kwamba wameshindwa kuleta ushahidi unaonyesha waumini wa dini ya kikristo walishawishika na waraka huo na wakajaribu kumuondoa Rais Kikwete madarakani kwa njia haramu”alisema Hakimu Mugeta. Alisema mshitakiwa angeweza kukutwa na hatia kama ingethibitika kuwa alikuwa akitumia karata ya dini kuligawa taifa na kuongeza kuwa mahakama hiyo imejiridhisha kuwa waraka huo haukuibia chuki mbaya baina ya waumini wa dini ya kiislamu na Kikristo na kwasababu hiyo mahakama hii imemuona Mtikila hajatenda kosa la uchochezi kwasababu hakuna madhara mabaya yaliyojitokeza katika taifa kupitia waraka huo na kwasababu hiyo mahakama hii inamwachiria huru mshitakiwa. Baada ya Hakimu Mugeta kumwachiria huyu Mtikila, Mtikila alisimama kizimbani akipaza sauti akisema “Haleluya,Haleyula…kesi hii ni ya mungu na hakuna binadamu yoyote anayeweza kushindana na mungu na kuwataka Watanzania wakasome Bibilia ,Waraka wa pili wa Timotheo Sura :4:2 ambao unasema ‘fanyakazi yako wewe Mhubiri wa Injili onya,karipia na kemea dhambi’ . Mtikila akasema yeye alichokifanya katika waraka ule ni kukemea dhambi na kutangaza neno la mungu lakini cha kusganga serikali ikamfungulia kesi hiyo ambayo ni jumla ya kesi ya jinai ya 43 amefunguliwa na serikali tangua aanze harakati zake za ukombi wa wanchi hii na kwamba kati ya kesi hiyo serikali ilimfunga kesi mmoja tu ambayo ilikuwa ni yakutoa maneno ya uchochezi ambapo alisema CCM, ndiyo ilimuua aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho,Horace Korimba ambapo alipokuwa Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Stella Mwandu alimfunga mwaka mmoja jela Kabla ya Hukumu kusomewa Mtikila alizungumza na waandishi wa habari nje ya viwanja vya mahakama ambapo alijigamba kuwa ni lazima atashinda kesi hiyo kwani alichokifanya kutangaza injili na kesi hiyo ni ya mungu na haogopi kufungwa. Baada ya Mtikila kushinda kesi hiyo hali ilikuwa ni tofauti karibu na mahabasu ya mahakama hiyo ambapo alikuja mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa mfanyabiashara anaitwa Gotem Ndunguru akiwaamrisha askari polisi wamkamate Mtikila kwa madai kuwa ana taarifa ya Kumkamata iliyotolewa na kituo cha polisi Kimara yenye namba RB/10482/12 ambapo alidai Mtikila alimtishia kumuua kwa maneno. Hata hivyo askari polisi na Ndunguru walishindwa kumkamata Mtikila kwasababu Mtikila alianza kumfokea askari polisi mmoja ambaye hatukuweza kufanikiwa kulipata jina lake ambaye alikuwa na cheo cha Koplo akimwambia kwa ukali kuwa hana hadi ya kumkamata yeye ana hadhi ya kukamatawa na polisi mwenye cheo cha Mrakibu wa Polisi na kwamba Nduguru ni mwizi mkubwa. “We askari huyo Ndunguru kakuonga uje unifanyie fujo hapa kwa taarifa yako mimi najua sheria ,wewe huna mamlaka ya kunikamata na huwezi kunikamata kiuni hivi…hata huyo bosi wako IGP-Said Mwema kabla ya kunikamata ananipigia simu kwa adabu na mimi mwenyewe ndiyo naenda polisi…sasa nawaambia hivi hauna hadhi ya kunikamata.”alifoka Mtikila na kusababisha askari huyo kunyewa na kuitwa na maaskari wenzake ambao walimtaka amwache Mtikila aende zake na maaskari hao wakimtaka Ndunguru anyamaze asiwafundishe kazi na baadae Ngunguru aliondoka mahakamani hapo kimya kimya na kuelekea nyumbani kwake. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano,Septemba 26 mwaka 2012

MTIKILA AMBWAGA KIKWETE KORTINI

Na Happiness Katabazi HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ,imemfutia kesi ya uchochezi ya kuchapisha na kumiliki waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete iliyokuwa ikimkabili Mwenyekiti wa Chama cha Democratic(DP), Mchungaji Christopher Mtikila badaa ya upande wa jamhuri kushindwa kuleta ushahidi wa kuthibitisha kesi hiyo. Hukumu hiyo ya kesi hiyo ya jinai Na.132/2010 ilitolewa jana mchana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,Elvin Mugeta ambapo alianza kwa kuikumbusha mahakama hiyo kuwa mshitakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na makosa mawili.Kosa la kwanza ni kusambaza waraka wa uchochezi kinyume na kifungu cha 32(1),(c) cha Sheria ya Magazeti ya mwaka 2002 na kosa la pili ni la kumiliki waraka huo wa uchochezi kinyume na kifungu cha 32(2) cha sheria hiyo. Hakimu Mugeta aliyasoma maelezo ya makosa hayo kuwa ilidaiwa na wakili wa serikali mwaka 2010 mahakamani hapo kuwa Novemba 1 mwaka 2009 na April 17 mwaka 2010 jijini Dar es Salaam, akiwa na nia ya kutenda kosa la uchochezi ,Mtikila alisambaza kwa umma waraka huo uliokuwa na kichwa cha habari kisemacho (Kikwete Kuangamiza Kabisa Ukristo!(Wakristo wasipoungana upesi kuweka Mkristo Ikulu),huku akijua kufanya hivyo ni uchochezi. Na maelezo ya kosa la pili ni kwamba katika ya Aprili 16 mwaka 2010 huko Mikocheni alikutwa akimiliki waraka huo wa uchochezi. Akianza kusoma hukumu yake Hakimu Mugeta ambaye alisema kwanza Mtikila katika utetezi wake alikiri kuaanda waraka huo na alikiri pia alikuwa akiumiliki waraka huo na kwamba waraka huo ulitolewa mahakamani hapo kama kielezo cha tatu na jumla ya mashahidi wanne waliletwa na upande wa Jamhuri kuthibitisha kesi hiyo wakati Mtikila akuleta shahidi,alijitetea yeye mwenyewe kwa madai hakuona haja ya kuwaleta mashahidi kwasababu endapo angefanya hivyo angekuwa anamaliza fedha za mahakama na kupoteza muda wa mahakama bure. Hakimu Mugeta alisema kufuatia mashitaka yanayomkabili mshitakiwa kabla ya kutoa hukumu yake alijiuliza maswali yafuatayo kuwa je ni kweli waraka huo ni wa uchochezi?Je waraka huo ulileta madhara katika jamii?Je waraka huo wa mshitakiwa ulikuwa ukitaka kumpindua rais Kikwete kinyume na sheria za nchini kwani ofisi ya Rais imeanzishwa kwa sheria husika? “Mimi nimeusoma waraka huo unaodaiwa na upande wa Jamhuri kuwa ni uchochezi na nimebaini kuwa waraka huo si wa uchochezi kwani Mtikila licha ni mwanasiasa pia ni kiongozi wa kidini na waraka ule ulikuwa umejaa maneno ya kidini ambayo ndani yake Mtikila alikuwa akiwataka wakristo wenzake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 watumie haki yao ya msingi ya kumpigia kura mgombea ambaye ni mkristo … na kumng’oa madarakani rais Kikwete kwa njia ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu siyo kosa la jinai: “Kitendo ambacho mahakama hii kwa kauli moja imeona upande wa Jamhuri imeshindwa kuleta ushahidi unaonyesha Mtikila alikuwa anataka wakristo wamuondoe rais Kikwete Ikulu kwa njia haramu na pia kusambazwa kwa waraka huo na mshitakiwa kulileta madhara na kwamba wameshindwa kuleta ushahidi unaonyesha waumini wa dini ya kikristo walishawishika na waraka huo na wakajaribu kumuondoa Rais Kikwete madarakani kwa njia haramu”alisema Hakimu Mugeta. Alisema mshitakiwa angeweza kukutwa na hatia kama ingethibitika kuwa alikuwa akitumia karata ya dini kuligawa taifa na kuongeza kuwa mahakama hiyo imejiridhisha kuwa waraka huo haukuibia chuki mbaya baina ya waumini wa dini ya kiislamu na Kikristo na kwasababu hiyo mahakama hii imemuona Mtikila hajatenda kosa la uchochezi kwasababu hakuna madhara mabaya yaliyojitokeza katika taifa kupitia waraka huo na kwasababu hiyo mahakama hii inamwachiria huru mshitakiwa. Baada ya Hakimu Mugeta kumwachiria huyu Mtikila, Mtikila alisimama kizimbani akipaza sauti akisema “Haleluya,Haleyula…kesi hii ni ya mungu na hakuna binadamu yoyote anayeweza kushindana na mungu na kuwataka Watanzania wakasome Bibilia ,Waraka wa pili wa Timotheo Sura :4:2 ambao unasema ‘fanyakazi yako wewe Mhubiri wa Injili onya,karipia na kemea dhambi’ . Mtikila akasema yeye alichokifanya katika waraka ule ni kukemea dhambi na kutangaza neno la mungu lakini cha kusganga serikali ikamfungulia kesi hiyo ambayo ni jumla ya kesi ya jinai ya 43 amefunguliwa na serikali tangua aanze harakati zake za ukombi wa wanchi hii na kwamba kati ya kesi hiyo serikali ilimfunga kesi mmoja tu ambayo ilikuwa ni yakutoa maneno ya uchochezi ambapo alisema CCM, ndiyo ilimuua aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho,Horace Korimba ambapo alipokuwa Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Stella Mwandu alimfunga mwaka mmoja jela Kabla ya Hukumu kusomewa Mtikila alizungumza na waandishi wa habari nje ya viwanja vya mahakama ambapo alijigamba kuwa ni lazima atashinda kesi hiyo kwani alichokifanya kutangaza injili na kesi hiyo ni ya mungu na haogopi kufungwa. Baada ya Mtikila kushinda kesi hiyo hali ilikuwa ni tofauti karibu na mahabasu ya mahakama hiyo ambapo alikuja mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa mfanyabiashara anaitwa Gotem Ndunguru akiwaamrisha askari polisi wamkamate Mtikila kwa madai kuwa ana taarifa ya Kumkamata iliyotolewa na kituo cha polisi Kimara yenye namba RB/10482/12 ambapo alidai Mtikila alimtishia kumuua kwa maneno. Hata hivyo askari polisi na Ndunguru walishindwa kumkamata Mtikila kwasababu Mtikila alianza kumfokea askari polisi mmoja ambaye hatukuweza kufanikiwa kulipata jina lake ambaye alikuwa na cheo cha Koplo akimwambia kwa ukali kuwa hana hadi ya kumkamata yeye ana hadhi ya kukamatawa na polisi mwenye cheo cha Mrakibu wa Polisi na kwamba Nduguru ni mwizi mkubwa. “We askari huyo Ndunguru kakuonga uje unifanyie fujo hapa kwa taarifa yako mimi najua sheria ,wewe huna mamlaka ya kunikamata na huwezi kunikamata kiuni hivi…hata huyo bosi wako IGP-Said Mwema kabla ya kunikamata ananipigia simu kwa adabu na mimi mwenyewe ndiyo naenda polisi…sasa nawaambia hivi hauna hadhi ya kunikamata.”alifoka Mtikila na kusababisha askari huyo kunyewa na kuitwa na maaskari wenzake ambao walimtaka amwache Mtikila aende zake na maaskari hao wakimtaka Ndunguru anyamaze asiwafundishe kazi na baadae Ngunguru aliondoka mahakamani hapo kimya kimya na kuelekea nyumbani kwake. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Septemba 26 mwaka 2012.

MWANAMKE KUPENDEZA

Happiness Katabazi nikiwa kwenye pozi tofauti

MWANAMKE KUPENDEZA

Happiness Katabazi nikiwa kwenye pozi tofauti

MATUKIO YALIYOPITA YAWEFUNZO KWA WANAHABARI TANZANIA

Na Happiness Katabazi

SEPTEMBA 2 mwaka huu, Mwandishi wa habari wa Kituo cha utangazaji cha Chanel Ten, Daudi Mwangosi alifariki dunia katika vurugu zilizotokea katika mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), na Polisi wilayani Mufindi Mkoani Iringa.

Vyombo vya habari na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo hilo la tukio waliueleza umma kupitia vyombo vya habari kuwa ni Jeshi la Polisi ndiyo waliomua Mwangosi kwa kipigo na bomu.

Baada ya vyombo vya habari kuaminisha umma hilo, umma uliamini hilo na baadhi taasisi ya kiraia na vyama ya siasa vikatoa matamko ya kulaani mauji hayo na kulihukumu moja kwa moja kuwa jeshi la polisi ndiyo lililomua na baadhi ya vyombo vya habari vilichapisha picha iliyokuwa ikionesha askari mmoja akiwa ameshika bunduki na kumuelekezea Mwangosi na wengine walifikia hatua ya kusema huyo askari aliyeonekana kwenye picha hiyo ambaye walishindwa kumtaja jina lake ndiye aliuemua marehemu huyo.

Aikuishia hapo Jumanne ya wiki hii, baadhi ya waandishi wa habari waliandama wa mikoa kadhaa waliandamana kulaani mauaji hayo na wale wa Mkoa wa Dar es Salaam, waliandamana na kuweka mkutano pale Viwanja vya Jangwana huku wakiwa na mabango yaliyosomeka hivi ‘Polisi wakaoge, polisi wauji’.

Pia walimtimua na kumtolea maneno ya kebei katika mkutano huo Waziri wa Mambo ya Ndani,Dk.Emmanuel Nchimbi kwa madai kuwa hawakumualika licha kuna taarifa za chini chini ambazo bado hazijathibitishwa zinadai kuwa miongoni mwa wahariri walimualika Dk.Nchimbi katika mkutano huo.Ni suala la muda tu ukweli utakuja kujulikana.

Kwani kwa watu tunaofikiri sawa sawa tumekuwa tukijiuliza hivi inawezekanaje Waziri Dk.Nchimbi kwa madaraka aliyonayo anawezaje kufunga ofisi yake na kuja kwenye eneo hilo bila kuarikwa?. Je waandishi waliomfikia hatua hiyo ya kumfukuza Dk.Nchimbi kwa madai kuwa siyo mwanahabari na hawajamwalika katika mkutano huo lakini ni wanahabari hao hao walimpatia nafasi Dk.Exavely Rwaitama ambaye si mwanahabari nafasi ya kuhutubia kwenye mkutano huo.

Baadhi ya wanahabari waliomtimua Dk.Nchimbi pale Jangwa na kutoa maneno ya kulipa matope jeshi la polisi wakati waliomfanyia unyama ule Mwangosi ni askari wachache ambao siyo jeshi zima, kuwa Nchimbi ni kiongozi wa nchi na amekuwa akishirikiana kwa karibu na vyombo vya habari na ujio wake pale Jangwani haukuvunja sheria zozote za nchi kwani Katiba ya Nchi inatoa haki kwa kila mtu kwenda kokote anakotaka idi mradi asivunje sheria na pia yeye ni binadamu anastahili heshima mbele ya jamii hivyo kitendo cha kumzomea wakati si yeye aliyetenda kosa hilo na tayari alikwishachukua hatua ya kuunda Kamati ya kuchunguza chanzo cha mauji hayo hakikua cha kiungwa katika jamii iliyostaharabika kwani sisi waandishi wa habari ni kioo cha jamii hivyo tunapaswa kutenda matendo, kuandika na kutangaza mambo ambayo yanastaha na kuifundisha vyema jamii.

Tendo la kumzoea Dk.Nchimbi tukae tukijua baadhi ya watoto wetu na makundi mengi wanaweza kulichukulia kuwa ni sawa na mwisho wa siku nao wanaweza kuja kumzoea kiongozi mwingine yoyote au watu wazima waliowazidi umri kwa kigezo kuwa hata wanahabari walishawahi kumzoea Waziri Nchimbi na hawakuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu.

Kumbukeni Dk.Nchimbi ,jeshi la polisi lipo chini yake na polisi ambalo tumelihukumu kuwa limemuua mwenzetu bila hata mahakama bado haijatoa hukumu kuwa ni jeshi hilo ndilo,na ni polisi hao hao ambao leo hii tumewatoea maneno ya kuwakashfu licha jeshi hilo limeunda tume ya kuchunguza chanzo cha mauji hayo ndiyo lenye mamlaka ya kupeleza kesi za jinai hususani kesi hiyo mauji ya Mwangosi,na tukumbuke nao ni binadamu na wanamshikamano wa kweli kuliko sisi waandishi wa habari ambao kwanza hatupendani,wanauwezo pia wakutumia madaraka yao vibaya ya kupeleleza kesi kwa kualibu ushahidi na mwisho wa siku upande wa jamhuri wakashindwa kesi hiyo, hivyo mmemtukana Mamba wakati Mto hamjavuka.

Turejee kwenye mada yangu ya leo ambayo ninataka umma hususani wanahabari wenzangu tujenge utaratibu wa kujifunza kutokana na matukio mbalimbali na maamuzi mbalimbali yanayotolewa na mahakama.

Nasema hivyo kwasababu ni wazi kuwa vyombo vya habari hapa nchini tunaonekana ni watu wa kusahau matukio mapema na hatutaki kujifunza kutokana na matukio yaliyopita.

Kwani leo hii vyombo vya habari vimeuaminisha umma kuwa ni polisi ndiyo walioua Mwangosi.Lakini waandishi hao wanasahau kuwa jeshi la polisi ni taasisi na inaafanyakazi wake ambao ni polisi na watumishi raia.

Hivyo vyombo vya habari tunavyoshinikiza aliyemua Mwangosi wakamatwe na kufikishwa mahakamani bila kusema mtu anayetuhumiwa kumua Mwangosi akamatwe tunakosea kwani mwisho wa siku tukumbuke Ibara ya 13(6)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema; ‘Ni marufuku kwa mtu aliyeshitakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo’.

Pia tukumbuke kifungu cha 7(1)(B) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 inasema hivi; “ Kila mtu analojukumu la tarifa polisi kuhusu tukio la kifo cha binadamu mwenzie cha kawaida au kilichosababishwa na vurugu au umemkuta mtu mwili wa marehemu bila kujua chanzo cha kifo chake unatakiwa ukatoe taarifa polisi”.

Pia kifungu cha 10 cha sheria ya hiyo kinatoa mamlaka kwa ofisa wa polisi kupeleleza matukio ya uhalifu.Na kifungu cha 60(1) cha Sheria hiyo kinasema ofisa yoyote msimamizi wa kituo au ofisa yoyote wa mpelelezi wa makosa ana mamlaka ya kuendesha gwaride la utambuzi lengo likiwa mashahidi wa kesi inayokusudiwa kufunguliwa mahakamani waweze kumtambua mtu anayetuhumiwa kutenda kosa husika”.

Kwa matakwa ya vifungu hivyo vya sheria hapo juu, ni wazi sisi waandishi wa habari hususani wale waandishi wenzetu waliokuwepo kwenye vurugu zilizosababisha Mwangosi kufariki hawajatekeleza kwa vitendo vitendo matakwa ya vifungu hivyo.

Yaani hawajaenda kutoa taarifa za kifo hicho kwenye kituo cha polisi wala kwa ofisa wa polisi, hawajaitwa kwenye gwaride la utambuzi kumtambua mshitakiwa aliyetenda kosa hilo la mauji hadi Septemba 12 mwaka huu, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi kumfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23).Ambapo wakili wa Serikali Michael Lwena alidai mshitakiwa huyo anakabiliwa na kosa la mauji ya Mwangosi na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.



Nawakumbusha waandishi wenzengu tuache kuongea sana bila kuitenda na kujifunza,tuongee na kuandika kwa kuwa na vielelezo ambavyo mwisho wa siku vitaisaidia mahakama kuwatia hatiani watuhumiwa wa makosa mbalimbali.

Leo hii tunasema kabisa ni polisi ndiyo walioua lakini tunashindwa kutaja jina la polisi aliyeua.Nisisi waandishi waandishi wa habari enzi zile za tukio la mauji ya wafanyabiashara wanne wa wilayani Mahenge mkoani Morogoro.Tulishupalia na kushikia bango kuwa ni polisi na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaa,Abdallah Zombe ndiyo waliowaua wafanyabiashara hao bila ya kuwa na ushahidi na mwisho wa siku Mahakama Kuu chini ya Jaji wa Mahakama ya Rufani hivi sasa Salum Massati aliwaachiria huru kwa maelezo kuwa jamhuri imeshindwa kuthibitisha kesi hiyo na akalitaka jeshi la polisi likawatafute wauaje na kwamba Zombe na wale washitakiwa wenzie siyo wauaji wa wafanyabiashara wale.

Na baada ya kuachiriwa huru Zombe aliyashitaki baadhi ya magazeti likiwomo gazeti la Uhuru, Tanzania Daima, Dar Leo kwa madai kuwa lilimhukumu kabla hajahukumiwa na kesi zipo mahakamani isipokuwa gazeti la Uhuru lilikwenda kumwomba msamaha Zombe na hatimaye Zombe akaiondoa kesi hiyo mahakamani wakaenda kumalizana nje ya mahakama.

Pia ningali nikikumbuka tukio la uvamizi katika ofisi za gazeti la Mwanahalisi ambapo watu wasiyojulikana walimjeruhi Mwandishi Saed Kubenea na Ndimara Tigambwage na sisi waandishi wa habari na jamii kwa ujumla tulifanya maandamano na kupiga kelele kutaka wahusika wakamatwe wafikishwe mahakamani na kweli polisi iliwafikisha mahakamani watuhumiwa hao pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Oktoba 2012 ,mahakama hiyo iliwaachilia huru kwa madai kuwa jamhuri imeshindwa kuleta ushahidi wa kuthibitishia mahakama kuwa ni kweli washitakiwa hao ndiyo waliyemjeruhi Kubenea na Ndimara.

Tukio jingine ni kuhusu mkataba wa kampuni ya kufua umme ya Richmond, tuliandika na kufikia hatua ya kujipa mamlaka ya kusema mkataba huo uliingiwa kwa misingi ya Rushwa na kuandika makala za kumdhihaki Mkurugenzi Mkuu wa (TAKUKURU), Dk.Edward Hosea ambaye alisema hakukuwa na tuhuma za rushwa katika mkataba huo na mwisho wa siku DPP-Dk.Feleshi alimfikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mfanyabiashara Naeem Gile aliyekuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa kwa makosa ya kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni hiyo ya Richmond, lakini mwaka jana Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, alimwachiria huru baada ya kumuona hana kesi ya kujibu.

Tukio jingine ambalo sisi wanahabari,wanasiasa na waharakati ni lakupinga hukumu ya mahakama ya kimataifa ya ICC, iliyoipa kampuni ya Dowans Tanzania, tuzo ya dola za kimarekani milioni 56, ambapo tulisema ni rushwa na haiwezekani la mwisho wa siku Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilikubali tuzo hiyo isajiliwe hapa nchini na wiki iliyopita mahakama hiyo tena ilitupilia mbali ombi la Tanesco lilokuwa linataka mahakama itoe amri ya kuzuia utekelezwaji wa hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyoruhusu tuzo hiyo ya Dowans isajiliwe.

Kwa mifano hai hiyo hapo juu, nataka kuwaasa sisi wanahabari tusiwe watu wenye kasumba ya kupayuka payuka bila kuwa na ushahidi kwani tukumbuke yale tunayoyaandika ndiyo umma wanayoyaamini na kuyafuata.

Pia kama tunaandika fulani ni muuaji,mla rushwa bila ya kuwa na ushahidi na hilo tukae tukijua wananchi wengi wanaamini hivyo.Na kama tunaandika hivyo basi tuakikishe tunakwenda pia kutoa taarifa hizo za Fulani ni mharifu kwenye mamlaka husika ili ziweze kufanyiwa kazi kwani matukio hayo ya kesi hizo yamenifundisha kuwa sisi waandishi na umma tunapenda sana kuamini vitu vya kusikia bila kuwa na ukweli na ushahidi thabiti ambao kama ushahidi huo tungewapelekea waendesha mashitaka wetu wangeweza kuutumia kuijenga kesi yao kwani ikumbukwe kuwa Kifungu cha 90(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, inaeleza majukumu ya DPP na moja ya jukumu lake ni kuendesha kesi za jinai mahakamani kwaniaba ya serikali.

Na DPP huyo huyo ndiyo mwenye madaraka ya kugawanya madaradaka yake kwa mawakili hao wa serikali kwenda mahakamani kwaniaba yake kuendesha kesi za jinai kama ilivyo kwenye kesi hiyo ya mauji ya Mwangosi ambapo DPP,anawakilishwa na Lwena.

Sasa wakili huyo aweze kufanya miujiza yoyote ya kushinda kesi hiyo kama mashahidi wa kesi hiyo hawatailetea vielelezo na ushahidi kwa polisi ili yeye aweze kuviwasilisha mahakamani.Na tukumbuke sisi waandishi wa habari kama tunataka mauji kwa wanahabari wenzetu na raia wenzetu wasiyona hatia licha siwezi kusema nini kilisababisha waliompiga na kuumua Mwangosi nini kwasababu sijui nini kilisababisha wampigie hadi kuumua , nilazima tuwe wepesi wa kushirikiana na polisi na waendesha mashitaka kwa kupeleka ushahidi mzuri ambao utaifikisha mahakama iwaone washitakiwa wanahatia.

Aidha nawaasa baadhi ya waandishi wa habari wenzangu tusimame kwenye maadili ya kazi yetu,tusiingize hisia na mapenzi ya vyama kwenye kazi kwani mwisho wa siku tunaoumia ni sisi na siyo hao viongozi wa vyama wala watoto wao wala wake zao kwani kwenye maandamano haramu viongozi hao hawaji na wake zao na watoto ila wakati wanaapishwa kushika madaraka viongozi hao wa siasa ndiyo uenda na wake zao na ndugu zao kwasababu huko hakuna virugu vya polisi.

Kwani hata Mwenyekiti wa Baraza la Habari (MCT), Kajubi Mkajanga wiki, hii amewataka waandishi wa habari kuacha kuwa wasemaji wa vyama siasa jambo ambalo binafsi namuunga mkono Mkajanga kwani hivi sasa baadhi ya waandishi hapa nchini wanaingiza mapenzi ya vyama vyao,na urafiki wa baadhi ya viongozi katika taaluma jambo ambalo linachafua heshima ya taaluma hii ambayo ni muhimu sana katika kuliletea maendeleo taifa letu. Naomba kutoa hoja.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

0716 774494

Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com ; Septemba 16 mwaka 2012.

KESI YA KIBANDA YASHIKA KASI

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE upande wa Jamhuri katika kesi ya kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, uliupatia upande wa utetezi nakala ya mlalamikaji katika kesi hiyo kama ulivyokuwa umeamriwa na mahakama hiyo kufanya hivyo.


Sambamba na hilo Mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi , Wakili Mwandamizi wa Serikali Prosper Mwangamila aliikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya mashahidi wa upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi na kwamba wamekuja na mashahidi wa wawili ambao ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza(ACP), George Mwampashi na Rafael Hokororo na wapo tayari kwaajili ya kuanza kutoa ushahidi.

Lakini hata hivyo Hakimu Moshi alisema hakimu anayesikiliza kesi hiyo Waliarwande Lema amepata hudhuru hivyo yeye amepewa kesi hiyo jana kwaajili ya kuiarisha na hivyo anaiarisha hadi Oktoba 22 mwaka huu, nakuwataka mashahidi wote wafike bila kukosa.

Kwa mujibu wa nakala ya maelezo ya mlalamikaji wa kesi hiyo ambaye ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi(SSP), David Hizza ambaye anafanya kazi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi nchini, alidai kuwa moja ya majukumu yake ni kufuatilia matishio ya uhalifu pamoja na matukio ya uhalifu a kwamba anakumbuka Novemba 30 mwaka 2011 alipata nakala ya gazeti la Tanzania Daima toleo la Namba 2553.

Hizza alidai katika kulisoma nilikuta makala iliyokua katika ukurusa wa 14 ambayo ilisomeka ‘Kalamu ya Mwigamba’ na ikaonyesha kuwa imeandikwa na mtu aitwaye Samson Mwigamba ambaye ni mdaiwa wa kwanza na makala hiyo ilisomeka ‘Waraka maalumu kwa askari wote’ na katika kuisoma makala hiyo alibaini kuwa mwandishi alionyesha kuwaandikia askari wanaofanya kazi katika majeshi ya Jeshi la Polisi,Jeshi la Kujenga Taifa,Kikosi maalum cha Kuzuia Magendo,Jeshi la Magereza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

“Katika kuusoma waraka huo yapo maeneo ambayo niliyaona kuwa ni uchochezi kwa askari hao kuwafanya wasiwatii viongozi wao jambo ambalo linaweza kuleta uasi jeshini.Maneno niliyoyaona kuwa ni uchochezi ni haya; “Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kila ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya’

“Na pia kulikuwa na maneno yanayochochea chuki kwa askari dhidi ya serikali yao ambayo ameitaja kuwa inawategemea wao lakini huku ikiminya haki zao na wazazi wao ‘Lakini wale wa Tanzania wako tayari kung’oa uhai wa raia wengi ili mradi kuzuia nguvu ya umma inayodai haki na wanafanya hivyo kwa sababu ya hofu ya kung’oka madarakani jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia.Na ndugu zangu askari napenda kuwaambia kwamba yote yanafanywa na watawala wetu kwa kuwategemea ninyi.Wanaminya haki zenu ninyi wenyewe,haki za wazazi wenu,marafiki zenu,jamaa zenu na majirani zenu”alidai SSP-Hizza.

Hizza alidai maneno kwamba askari wako tayari kung’oa uhai ili kuzuia nguvu ya umma yanaashiria uchonganishi kati ya raia kung’oa uhai ili kuzuia nguvu ya umma yanaashiria uchonganishi kati ya raia wa kawaida na askari kuonyesha jinsi askari wasivyojari utu wa raia jambo ambalo linachochea chuki dhidi ya majeshi yetu kwa raia na kwamba kitendo cha kuwaambia askari wasiwatii viongozi wao wanaowaamuru katika shughuli zao ni kuwashawishi wasitii kiapo cha utii walichofanya wakati wanaajiriwa kama askari ‘kinachomtaka kila askari kuwa mwaminifu na mtii kwa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa uaminifu kuitumikia na kuilinda jamhuri wakati wote wa utumishi wao na kutii amri zote za rais na viongozi walio juu yao’.

“Ushawishi huo alioufanya mwandishi wa makala hiyo ni uvunjaji wa sheria za nchi na baada ya kuusoma waraka huo niliwasiliana na viongozi wangu katika idara na wote baada ya kuupitia walikuwa na maoni kuwa una taarifa za kiuchochezi hivyo ni vema waliohusika wahojiwe na hatua stahiki zichukuliwe na nilimtafuta naye mahojiano na hatua stahiki zichukuliwe na nilimtafuta mwandishi wa makala hiyo(Mwigamba) na kufanya naye mahojiano na akakiri kuwa ndiye aliyeandika waraka huo lakini akadai alifanya hivyo kwa lengo la kuelimisha”alidai Hizza.

Aliendelea kueleza kuwa maelezo ya Mwigamba yaliandikwa kisha akapelekwa mahakamani hapo pia alimwita Mhariri Mtendaji wa gazeti hili Absalom Kibanda ambaye naye alimhoji juu ya uhalali wa gazeti lake kutoa waraka huo ambao ni wa kichochezi lakini naye akadai waraka huo ni wa kawaida na siyo wa uchochezi kwa askari hivyo naye alipelekwa mahakamani na kwamba alimwita na kumhoji Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwananchi Communication ambaye ni mshitakiwa wa tatu, Theophil Makunga ambaye kampuni yake ndiyo ilichapa gazeti hilo na kumhoji.

Aidha alidai kuwa kwa upande wa Makunga alidai anao mkatana na kampuni ya Freemedia ambyo nio watoaji wa gazeti hilo unaonyesha kuwa jukumu la kisheria la yaliyomo katika katika gazeti hilo anayewajibika ni Free Media na sio wao.Ili kulithibitisha hilo kisheria nilifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Raphael Hokororo ambaye alidai jukumu la uchapaji haliondolewi na mkataba huo bali linabaki kwa kampuni hiyo ya uchapaji na alikusanya ushahidi na kisha kulipelekea jalada kwa maoni ya kisheria.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Septemba 11 mwaka 2012.





MPENDAZOE AMGWAYA DK.MAHANGA

Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman ameliondoa Mahakama ya Rufani nchini,ombi la kusudio la kukata rufaa iliyowasilishwa Mahakama hapo, na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredy Mpendazoe.


Mei 7 mwaka huu, Mpendazoe aliwasilisha mahakamani hapo taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam katika kesi yake ya uchaguzi wa jimbo la Segerea na Julai 12 mwaka huu,wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatara aliwasilisha ombi la kutaka kuiondoa taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa.

Katika kesi hiyo namba 98 ya mwaka 2010, Mpendazoe alikuwa akipinga matokeo yaliyomtangaza Dk.Makongoro Mahanga (CCM) kuwa mbunge wa jimbo hilo la Segerea.
Jaji wa Mahakama Kuu Profesa Ibrahim Juma alitoa hukumu ya kumtangaza Dk.Mahanga kuwa ndiye mbunge halali wa jimbo hilo na kwamba matokeo yaliyompa ushindi hayakukiuka taratibu za sheria na akawa ameitupilia mbali kesi hiyo iliyokuwa imefunguliwa na Mpendazoe.

Hata hivyo Jaji Mkuu Othman alimuru taarifa hiyo iondolewe mahakamani hapo chini ya Kanuni ya 89 (1) ya Kanuni za Mahakama ya Rufani za mwaka 2009.
Jaji Mkuu Othman alitoa amri hiyo Agosti 2, 2012, baada Mpendazoe kuamua kuondoe nia yake hiyo ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Katika kesi ya msingi aliyoifungua Novemba10, 2010, Mpendazoe alikuwa akipinga ushindi wa Dk. Mahanga akidai kuwa haukuwa huru na wa haki kwa kuwa taratibu na kanuni za Sheria ya Uchaguzi zilikiukwa, katika hatua ya kuhesabu, kujumlisha na kutanga matokeo.

Hivyo aliiomba mahakama itengue matokeo hayo na kuamuru uchaguzi mdogo uitishwe katika jimbo hilo ama imtangaze yeye kuwa mshindi.
Wadaiwa katika katika kesi hiyo walikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi wa majimbo yaliyoko katika manispaa hiyo likiwemo Segerea na Dk. Mahanga.

Dk. Mahanga alikuwa akitetewa na mawakili wakili, Jerome Msemwa, na Aliko Mwamanenge, AG na RO walikuwa wakitetewa na Mawakili Waandamizi wa Serikali David Kakwaya na Seth Mkemwa.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Septemba 11 mwaka 2012.

MAWAKILI WA TANESCO KESI YA DOWANS WAMETUSAIDIA NINI?


Na Happiness Katabazi 

SEPTEMBA 6 mwaka huu, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Dk.Fauz Twaib alitupilia ombi la shauri la madai Na.8/2011 lilofunguliwa mahakamani hapo Oktoba mwaka jana na Shirika la Umeme(Tanesco) dhidi ya kampuni ya Dowans Hodlings SA(Costa Rica)Dowans Tanzania LTD,lilokuwa likiomba mahakama hiyo itoe amri ya kuzuia utekelezwaji wa hukumu ya mahakama kuu iliyotolewa Septemba 28 mwaka jana ambayo iliruhusu tuzo iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya (ICC) ya dola za Kimarekeni 65,812,630.03 kwa Dowans isajiliwe. 

Katika uamuzi wake huo ambao ninayo nakala yake Jaji Dk.Twaib alisema amefikia uamuzi wa kukataa ombi hilo la mawakili wa Tanesco ambao ni Richard Rweyongeza, Lugano Mwandambo,Dk.Eve Hawa Sinare,Dk.Alex Nguluma na Majura Magafu na badala yake ikakubaliana na hoja zilizotolewa na wakili wa Dowans, Kennedy Fungamtama kwasababu mahakama yake haina mamlaka ya kusikiliza ombi hilo kwakuwa ni Tanesco hao ambao waliwasilisha ombi hilo la kutaka mahakama yake izuie utekelezwaji wa hukumu iliyotolewa na jaji wa mahakama Kuu Emilian Mushi Septemba 28 mwaka huu, ndiyo Tanesco hao hao pia tayari wameishawasilisha taarifa ya kusudia la kukata rufaa kupinga hukumu ya iliyotolewa na jaji Mushi katika Mahakama ya Rufani nchini. “Mahakama Kuu ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza na kulikubali ombi la Tanesco la kuzuia Dowans isitekeleze hukumu ya Jaji Mushi kipindi kile wakati Tanesco hawajawasilisha taarifa ya kusudio la kukatia rufaa hukumu iliyotolewa na Jaji Mushi, Septemba 28 mwaka jana,katika Mahakama ya Rufani,kwa kuwa tayari Tanesco wameishawasilisha taarifa hiyo mahakama ya rufani,mahakama hii inakubaliana na hoja za wakili wa Dowans,Fungamtama kuwa mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza na kukubali ombi hilo la Tanesco’alisema Jaji Dk.Twaib. Itakumbukwa kuwa Septemba 28 mwaka 2011 jaji wa Mahahakama Kuu Emilian Mushi ambaye alikuwa akisiliza ombi la Tanesco lililokuwa likiomba Tuzo iliyotolewa na mahakama ya ICC kwa Dowans isisajiliwe hapa nchini,jaji Mushi alitupilia mbali ombi hilo la Tanesco na makundi mengine ya wakanaharakati ambao ni Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu na akaruhusu tuzo hiyo isajiliwe hapa nchini kwasababu uamuzi wa mahakama ya ICC ulioipatia tuzo Dowans ulikidhi matakwa ya kisheria. Aidha Novemba 15 mwaka 2010 mahakama ya ICC ilipatia tuzo ya ushindi kampuni ya Dowans ya dola za kimarekani 65,812,630.03 baada ya Tanesco kukutwa na hatia ya kuivunjia mkataba Dowans kinyume na mkataba wao na ikaiamuru tanesco ilimpe dowans kiasi hicho cha fedha. Lakini Tanesco haikulidhika na uamuzi huo na kuamua kuja Mahakama kuu ya Tanzania mbele ya Jaji Mushi kuipinga hukumu hiyo ya ICC wakati ikifahamu wazi makubaliano ya Dowans na tanesco katika mkataba wao walioingia walikubaliana endapo wakigombana wataenda kusuluhishwa katika Mahakama ya ICC pekee na siyo mahakama Kuu wala Mahakama ya rufaa. Hukumu hiyo ya ICC ilizusha malumbano hapo nchini na kusababisha baadhi ya watu kutaka Dowans isilipwe kiasi hicho na wengine wakishauri serikali ieheshimu utawala wa sheria na iilipe Dowans fedha zake kwani tanesco ndiyo waliovunja mkataba na Dowans. Oktoba 2 mwaka 2011 gazeti hili lilichapisha makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “Tanesco imevuna ilichopanda Dowans”.Ndani ya makala hiyo nilizungumzia hukumu ya iliyotolewa na Jaji Mushi na kuwasema sana Tanesco na wale wanaharakati waliokuwa wakipinga tuzo ya Dowans isisajiliwe kwasababu lengo hanawana hoja za msingi. Na leo tena narudia kusema hivi kuwa nyie mawakili mnaoitetea Tanesco kwanini lakini hamtaki kurejea zile notisi mlizofundishwa chuoni wakati mnasoma sheria na kupitia kwa makini sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai(Civil Procedure Act:RE,2002 na Sheria ya Mikataba ya mwaka 2002 na maamuzi ya kesi mbalimbali(Precedent). Naamini kama mngezisoma kwa makini na mngeheshimu maadili ya taaluma yenu na kuogopa kuumbuliwa na Mahakama ICC na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa zaidi ya mara mbili sasa, msingekuwa mnathubutu hata siku moja kuwasilisha hayo maombi yenu yaliyotaka tuzo ya Dowans isisajiliwe na lile ombi la kutaka mahakama itoe amri ya kuzuia Dowans isitekeleze hukumu ya jaji Mushi. Aiingii akili kabisa kwa mawakili hao wa Tanesco ambao wanauzoefu wa kazi hiyo wanakubalije kila mara kwenda kusimama mbele ya mahakama nakuwasilisha maombi yao yasiyonakichwa wala miguu ambayo mwisho wa siku mahakama kuu imekuwa ikiyakataa maombi yao. Na cha kustaajabisha kama siyo cha kushangaza Tanesco hii hii ambayo kila siku imekuwa ikilia haina hela ila inapata fedha za kuwalipa mawakili hao wawatee kwenye kesi hiyo na matokeo yake wanashindwa tena kwa uzembe tu kwasababu wanawasilisha hoja dhaifu ambazo zinabaki kuwaduwaza watu kuwa inakuwaje hoja dhahifu kama hizo zinaweza kuwasilishwa na mawakili hao wenye majina makubwa kama hayo? Nimeifuatilia kesi hiyo mwanzo hadi mwisho upande wa Dowans umekuwa ukiwakilishwa na wakili mmoja tu Fungamtama lakini Tanesco wamekuwa wakiwakilishwa na lundo la mawakili ambao mwisho wa siku maombi yao yanatupiliwa mbali na mahakama.Kwanini hamjisikii aibu. Ni kweli mawakili kazi yenu ni kuisadia mahakama ikifikie hatua ya kutenda haki na pia mziwakilishe pande mbili katika kesi na mambo mengine lakini hivi inakuwaje wakili anayeheshimu taaluma yake na mwenye weledi wa taaluma ya sheria anawezaje kuwa anawasilisha hoja dhaifu kama hizi zinazowasilishwa na mawakili wa Dowans? Kwa wale waliopata fursa ya kuusoma mkataba baina ya Tanesco na Dowans wataona ndani ya mkataba huo kunakipengele cha (POA) pande hizo zilikubaliana kuwa endapo utatokea mgogoro baina yao basi mmogoro huo utasuluhishwa kwenye Mahakama ya ICC na siyo mahakama nyingine. Sasa ni kitu gani kila kukicha hawa mawakili wanaitetea Tanesco wanashindwa kukubaliana na hilo na matokeo yake wanakimbilia katika Mahakama Kuu huku wakifahamu fika mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo yasiyonakichwa wala miguu na wala haiwezi kutengua hukumu ya ICC isipokuwa tu pale kama Tanesco ingeweza kuleta ushahidi kuwa majaji wale wa ICC waliipendelea,au walihongwa na Dowans na Tanesco hilo wameshindwa kuthibitisha. Nafahamu kasumba ya baadhi ya wananchi wa taifa hili akitokea mtu au mwandishi akiandika ukweli ambao unawakera wao wanaishia kumuhukumu mwandishi huyo kaongwa na Dowans,mawazo ambayo ni ya kipuuzi. Na mwanasheria Mkuu wa Serikali jaji Fredrick Werema alishawahi kusema hatuwezi kukwepa kuilipa Dowans lakini wanaharakati uchwara na makundi mengine ambayo hata hukumu ya ICC,mkataba wa Tanesco na Dowans ulivunjwa hawakuwai kuusoma walimkebei sana lakini leo hii maana ya maneno yake yamenza kuonekana kupitia maamuzi mbalimbali ya Mahakama Kuu. Tanzania ni nchi inayoheshimu utawala wa sheria na pia inaitambua Mahakama ya ICC.Pia Tanzania ni nchi ambayo ina sera ya kuwakaribisha wawekezaji waje kuwekeza hivyo kwa mchezo huu wa kiuni unaofanywa ama na serikali kupitia njia hii ya kuwatumia mawakili kwenda kuweka mapingamizi mahakamani kuzuia Dowans isilipwe mara kuzuia hukumu ya Jaji Mushi isitekelezwe kwa njia ya kuchelewesha malipo ya Dowans,tukae tukijua mwisho wa siku utakuja kulighalimu taifa hili. Kwani tunavyozidi kuchelewa kuilipa Dowans kwa hoja hizi dhaifu zinazowasilishwa na mawakili wa Tanesco ambazo kwa mara tatu sasa mahakama za ICC,na mahakama kuu inazikataa zinasababisha deni hilo kuongezeka thamani kila kukicha na kuwachukiza wamiliki wa kampuni hizo na kuwadhalilisha kitaaluma hao mawakili wanaoitetea Tanesco mbele ya wasomi wenzao wa sheria maana kama walikuwa na uweledi mathubuti wa taaluma ya kisheria wasingethubutu kuwa wanawasilisha hoja hizo dhaifu ambazo zinakataliwa na mahakama. Na ninapenda ieleweke wazi uenda hii kesi ya Tanesco dhidi ya Dowans uenda imegeuzwa mgodi wa baadhi ya watu kujipatia fedha nyingi toka serikali kwa kisingizio kuwa wataiwasilisha fedha mahakamani Tanesco na mwisho wa siku watashinda kumbe ni uongo mtupu. Nimalizie kwa kuikumbusha serikali kuwa nchi yetu inatawaliwa kwa utawala wa sheria hivyo ni vyema ikaheshimu maamuzi ya mahakama na pia kama kweli wameamua kutumia njia hii ya kuchelewesha malipo ya dowans basi wasitumie njia hii ya kuwasilisha mapingamizi mahakamani kila kukicha kwani mbinu hiyo haifai na ndiyo kwanza inaidhalilisha serikali kupitia Tanesco kwani hata hao mawakili mapingamizi wanayoyawasilisha hayana mashiko kabisa. Na dawa ya deni ni kulipa kwani ni sisi ndiyo tulivunja mkataba na kama ndivyo hivyo lazima tukubali Dowans ilipata madhara na usumbufu wa Tanesco kumvunjia mkataba.Tulipe deni la watu ili tuendelee na mambo mengine kwani ujanja ujanja una mwisho. Na mwisho wake ndiyo huu wa Mahakama ya ICC na Mahakama Kuu ya Tanzania kuyatupilia mbali maombi ya Tanesco.Na wale wanasiasa akiwemo Samwel Sitta, Dk.Harrison Mwakyembe na wanaharakati wengine waliotufikisha leo kuhusu Dowans wamekaa kimya utafikiri hawapo wakati nao ni chanzo cha balaa lote hili. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika 0716 774494 www.katabazihappy.blogspot.com Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Septemba 9 mwaka 2012.

DOWANS YAIBWAGA TENA TANESCO KORTINI


Na Happiness Katabazi 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia ombi la Shirika la Umeme (TANESCO) lilolokuwa likiomba mahakama hiyo itoe amri ya kuzuia utekelezwa wa ukazaji wa hukumu ya mahakama hiyo ambayo iliruhusu tuzo ya Dola za Kimarekani 65,812,630.03 iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa migogoro ya Kibiashara (ICC) Novemba 15 mwaka 2010 kwa kampuni ya Dowans Hodlings SA(Costa Rica)Dowans Tanzania LTD isajiliwe hapa nchini. 

Septemba 28 mwaka 2011 jaji wa Mahahakama Kuu Emilian Mushi ambaye alikuwa akisiliza ombi la Tanesco lililokuwa likiomba Tuzo iliyotolewa na amahakama ya ICC kwa Dowans isisajiliwe hapa nchini,jaji Mushi alitupilia mbali ombi hilo la Tanesco na akaruhusu tuzo hiyo isajiliwe hapa nchini kwasababu uamuzi wa mahakama ya ICC ulioipatia tuzo Dowans ulikidhi matakwa ya kisheria. Uamuzi huo wa shauri la madai Na.8/2011 lilofinguliwa la Tanesco dhidi ya kampuni hizo mbili za Dowans ambapo nipigo tena kwa TANESCO ulitolewa jana na Jaji Dk.Fauz Twaib ambapo alisema baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili anakubaliana na hoja za wakili wa wadaiwa(Dowans),Kennedy Fungamtama wakati Tanesco ilikuwa ikiwakilishwa na mawakili wa kujitegemea Richard Rweyongeza, Lugano Mwandambo,Dk.Eve Hawa Sinare,Dk.Ale nguluma na Majura Magafu . Ya kwamba mahakama hiyo haiwezi kusikiliza ombi hilo kwasababu tayari Tanesco walikishwa wasilisha Mahakama ya Rufani taarifa ya kusudio la kupinga hukumu iliyotolewa na jaji Mushi Septemba 28 mwaka 2011 ambayo iliruhusu tuzo hiyo isajiliwe. Jaji Twaib alisema katika kesi hiyo mahakama kabla ya kutoa uamuzi huo ilijiuliza maswali mawili ambayo ni katika mazingira ya kesi hiyo kama mahakama ina mamlaka ya kukubali ombi la Tanesco lilotaka mahakama hiyo izuie utekelezwaji wa ukazaji hukumu wa mahakama hiyo kwasababu tayari Tanesco walishawasilisha hatia ya nia ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani ya kupitia hukumu ya Jaji Mushi iliyoruhusu Dowans isajiliwe? Pia amejiuliza kama mlalamikaji(Tanesco) ombi lake la kutaka Dowans izuiliwe kutekeleza hukumu ya Jaji Mushi wakati tayari ni Tanesco huyo huyo ambaye akliwasilisha ombi hilo mbele yake pia amewasilisha ombi la kukatia rufaa hukumu ya Jaji Mushi katika Mahakma ya Rufani? Jaji Dk.Twaib katika uamuzi wake ambapo gazeti hili linayo nakala yake alisema mahakama yake kwanza haina mamlaka ya kusikiliza ombi hilo la Tanesco lilotaka mahakama hiyo izuie Dowans wasitekeleze hukumu iliyotolewa na Jaji Mushi ambapo hukumu hiyo ya Jaji Mushi iliruhusu Dowans waanza kukaza hukumu kwa kuanza kuidai Tanesco iilipe tuzo waliyopewa na mahakama ya ICC ambayo ni Dola za Kimarekani 65,812,630. Akichambua hoja zilizowasilishwa na wakili Fungamtama ,Jaji Twaib alisema Fungamtama aliikumbusha mahakama kuwa Tanesco waliwasilisha ombi hilo kwa kutumia kanuni 1192) na 47 ya Kanuni za Mahakama ya Rufani Tanzania ya mwaka 2009. Fungamtama aliendelea kueleza kuwa kanuni ya 47 pia inatumika kwenye ombi hilo ambapo Mahakama ya Rufaa na Mahama Kuu inayomamlaka sawa na kwamba ombi hilo la kuizuia Dowans isitekeleze hukumu ya mahakama Kuu halikuwa limetajwa na tanesco katika maombi yale waliyoyafungua Mahakama ya Rufani. Alidai wakili Fungamtama alidai kuwa ombi hilo la Tanesco la kutaka Dowans izuie kukazia hukumu lingekubaliwa na Mahakama ya Rufani kwa mujibu wa Kanuni ya 11(2)(B) ya Kanuni za Mahakama ya Rufani nchini ya mwaka 2009 na kwamba Fungamtama alidai neno mahakama lilotajwa katika kanuni ya 11(2) ina maanisha Mahakama ya Rufani na siyo Mahakama Kuu na kwasababu hiyo ni Mahakama ya Rufani pekee ndiyo inaweza kukubali ombi mlalamikaji(Tanesco) la kuwazuia wadaiwa (Dowans )wasikaze hukumu ya mahakama kuu. Na kuwa wakili wa tanesco Lugano Mwandambo katika hoja zake mbele ya Jaji dk.Twaib alieleza mahakama kuwa Kanuni ya 11(2)(b) ya Kanuni za mahakama ya Rufani nchini ya mwaka 2009,inaipa mamlaka mahakama na mabaraza kutoka kwenye rufaani zote zinazowasilishwa mahakama ya rufani zitoe amri ya utekelezwaji wa ukazaji hukumu na kwamba kwamujibu wa kanuni hiyo kuna masharti mawili ambayo ni kuwasilisha hatia ya kusudio la kukata rufaa na uwepo wa sababu mathubiti za kushinda hiyo rufaa. Jaji Dk.Twaib alisema mahakama yake hainabwi na maamuzi ambayo yalishawai kutolewa zamani na mahakama hiyo kwa kuwa mahakama hiyo ipo huru katika kufanyazi zake. Jaji Dk.Twaib alisema kwa mujibu wa amri xxxix Kanuni ya 5(1),(2) ya Sheria ya Madai,Sura ya 33 ya mwaka 2002 inayoonyesha majukumu na mahakama kuu na mahakama rufani na kwamba kwa mazingira ya kesi hiyo mahakama yake ilikuwa na mamlaka ya kulikubali ombi hilo la Tanesco kipindi kile kabla ya tanesco haijawasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika mahakama rufaa kupinga hukumu ya mahakama kuu iliyoisajli tuzo ya Dowans. “Kwakuwa tayari Tanesco walishawasilisha mahakama ya rufani taarifa ya kusudia la kukata rufaa kupinga hukumu ya mahakama kuu iliyotolewa Septemba 28 mwaka 2011 na Jaji mstaafu Mushi ambayo iliruhusu tuzo ya Dowans isajiliwe ….mahakama kuu hapo mamlaka yake ya kukubali ombi hilo la Tanesco la kutaka Dowans isikaze hukumu hiya ya Jaji Mushi nguvu hizo zinakufa na kwa maana hiyo maamuzi yale jaji Mushi hadi leo hii bado hayajatenguliwa: “Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili ,mahakama hii imekubaliana na hoja za wakili Dowans,Fungamtama kuwa mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza ombi hili liloletwa na Tanesco mbele yake lilotaka mahakama hiyo itoe amri ya kuizuia Dowans isikazie hukumu ya mahakama kuu iliyotolewa na Jaji Mushi ,Septemba 28 mwaka 2011 ambayo ilikubali tuzo ya Dowans isajiliwe hapa nchini na Dowans ianze kudai Tanesco dola za kimarekani 65,812,630.03,hivyo inatupilia mbali ombi hilo la Tanesco na sitatoa amri ya ya kuitaka Tanesco ilipe gharama’alisema Jaji Dk.Twaib. Itakumbukuzwa kuwa Septemba 28 mwaka 2011 mahakama Kuu kanda ya dar es salaam ilitoa hukumu yake katika kesi iliyokuwa imefunguliwa na tanesco dhidi ya Dowans na ikatupilia mbali ombi la Tanesco lilotaka tuzo ya Dowans isisajiliwe. Aidha Novemba 15 mwaka 2010 mahakama ya ICC ilipatia tuzo ya ushindi kampuni ya Dowans ya dola za kimarekani 65,812,630.03 baada ya Tanesco kukutwa na hatia ya kuivunjia mkataba Dowans kinyume na mkataba wao na ikaiamuru tanesco ilimpe dowans kiasi hicho cha fedha. Lakini Dowans haikulidhika na uamuzi huo na kuamua kuja Mahakama kuu ya Tanzania mbele ya Jaji Mushi kuipinga hukumu hiyo ya ICC wakati ikifahamu wazi makubaliano ya Dowans na tanesco katika mkataba wao walioingia walikubaliana endapo wakigombana wataenda kusuluhishwa katika Mahakama ya ICC pekee na siyo mahakama Kuu wala Mahakama ya rufaa. Pia itakumbukwa hukumu hiyo ya ICC ilizusha malumbano hapo nchini na kusababisha baadhi ya watu kutaka Dowans isilipwe kiasi hicho na wengine wakishauri serikali ieheshimu utawala wa sheria na iilipe Dowans fedha zake kwani tanesco ndiyo waliovunja mkataba na Dowans. Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Septemba 7 mwaka 2012.

SERUKAMBA AIBWAGA CHADEMA

Na Happiness Katabazi MAHAKAMA ya rufaani nchini, imetupilia mbali kwa gharama maombi ya kufanyiwa mapitio ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora Machi 28 mwaka huu, ambayo ilisema kuwa taratibu za sheria ya uchaguzi na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 yaliomtangaza Peter Serukamba (CCM), kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, hayakukiuka sheria. Agosti mwaka huu, aliyekuwa mgombea wa CHADEMA katika jimbo hilo, Ally Mleih, aliwasilisha Mahakama ya Rufaa, ombi la kuiomba ifanye mapitio ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora iliyotolewa na Jaji Stella Mgasha. Uamuzi huo wa jana ulitolewa na majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, Jaji Edward Rutakangwa, Bernard Luanda na Salum Massati, baada ya kusikiliza hoja za pande mbili katika shauri hilo. Jaji Rutakangwa alisema jopo lake limekubaliana na hoja zilizowasilishwa mbele yao na wakili wa Serukamba, Kennedy Fungamtama, kuwa mrufani alipaswa afungue rufaa katika mahakama hiyo na si kuwasilisha ombi linalotaka mahakama hiyo ifanyie mapitio ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora. “Baada ya kupitia hoja za pande zote mbili, mahakama hii imekubaliana na hoja za Wakili Fungamtama na kwamba imebaini mrufani alipitia mlango wa nyuma kuwasilisha ombi lake hilo, jambo ambalo ni kinyume cha sheria na Katiba ya nchi. Kwa sababu hiyo inatupilia mbali kwa gharama,” alisema. Jaji Rutakangwa alisema kuomba rufaa ni haki ya kikatiba na haki hiyo imeainishwa bayana katika ibara ya 83 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977. Alisema kwa mujibu wa matakwa ya ibara hiyo mrufani, Mleih ana haki ya kukata rufaa na si kuwasilisha ombi la mapitio kama alivyofanya hivi sasa. Mapema Machi 28 mwaka huu, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Mgasha alitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya mwaka 2010 ya Kigoma Mjini yaliyomtangaza Serukamba kuwa mshindi kwa maelezo kuwa mlalamikaji alishindwa kuthibitisha madai aliyoyafungua mahakamani. Chanzo:Gazeti la Tanzania la Alhamis Septemba 6 mwaka 2012.