Na Happiness
Katabazi
OKTOBA 12 mwaka,taifa liliendelea kuandika
historia mbaya ya vurugu za kidini huko Mbagala zilizosabishwa kundi kubwa la
watu wanaodaiwa ni waumini wa dini ya Kiislamu wenye imani kali zilizoambatana na kuchomwa moto na kuharibiwa
kwa makanisa
ya Kikristo jijini Dar es
Salaam, katika kile kilichoelezwa kuchukizwa na kitendo cha mtoto wa dini ya
Kikristo ,Emmanuel Josephat (14) aliyedaiwa kukikojolea kukimwagia kitabu
kitakatifu cha Kurani.
Kundi hilo liloonekana kufura kwa hasira , lifanya uhabifu huo walichukua
hatua ya kufanya uhauribifu huo, baada ya kushindwa kwa jaribio la kukiteka
kituo kidogo cha polisi cha Mbagala wilayani Temeke kwa nia ya kumpora mtoto
huyo ambaye tayari alikuwa mikononi mwa jeshi la polisi ili waweze kumpiga.
Binafsi
nalaani uhuni huu uliofanywa
na wahuni wale ambao ni mambumbumbu wa sheria na sheria na maadili ya dini yao
ya Kiislamu kwani Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya sheria na siyo
sheria ya dini ya Kiislamu.
Aiingii akilini watu waliofanya
vurugu zile
tayari wameishaitia litia taifa
letu la mapigano ya kidini ,walielezwa
vizuri na jeshi la polisi Temeke watawanyike
na kwamba jambo hilo wanalishughulikia kisheria wao wanakaidi amri ya jeshi hilo
kisha wakaanza kufanya fujo za kuchoma
hadi makanisa.
Tuwailize hivi huo uhuni walioufanya wanayafahamu madhara yake kwa vizazi
vya sasa na baadaye?Hivi hayo majengo (Makanisa) ambayo hayana mdomo, ndiyo
yalimwagiza Josephat akakojolee kile kitabu cha Korani? Hivi nao waumini wa
makanisa yaliyochomwa nao wakikosa subira wakaamua kulipiza kisasi ,nchi hii
itakalika?
Ni maovu mangapi yanafanywa na watoto na ndugu
wetu tena ya kutisha kama
ujambazi,ushoga,usagaji,wizi lakini mbona nyie wazazi mlianzisha vurugu za
kidini Mbagala hamuonyeshi kukerwa na madhambi hayo ambayo yamekatazwa kwenye
vitabu vya dini za Kiislamu na Kikristo?
Nyie mliotaka kumchukulia hatua Josephat kwasababu ametenda
dhambi,mnauhakika kuwa nyie hamna dhambi hata chembe mbele ya binadamu wenzenu
na Mungu?Na mkae mkijia
mkijua vurugu
mlizozifanya ni dhambi mbele ya Mungu na sheria za nchi inayowaongoza.Hivyo mnapaswa
pia mtubu na serikali iwachukulie hatua za kisheria kwani serikali kuendela
kulea wa aina yenu ni hatari kwa usalama wa taifa letu huko tuendako.
Vongozi wa dini ya Kiislamu watusaidie katika hili kama Korani inawaruhusu
wauimini wake wasiheshimu mamlaka ya duniani
au wajichukulie sheria mikononi dhidi ya mtu wanayemtuhumu ameidhalilisha dini
yao?
Wote mlioenda kufanya fujo Mbagala,tuwaulize hivi ni watu wangapi tena
waumini wa dini yenu ambao wengine ni viongozi mnawafahamu wanatuhuma mbaya
wanaingia kwenye misikiti na mnakubali wawaongoze ni kwanini hata siku moja
hatujawaona mkipandwa na jazba na kuanza kushughulikia watu hao kwa madai kuwa
wanadhihaki kitabu hicho cha kurani ambacho wamekuwa wakikitumia kuombea dua
mbalimbali wakati ni watu makatili na mafisadi?
Hivi mliofanya vurugu Mbagala mnakabiliwa na umaskini,wengine hamna hata
uhakika wa kula chakula bora,umaskini umewakabili kama mimi.Ningewaona wa maana
sana siku mngeandama kwa kufuata taratibu mfikishe vilio vyenu kwa serikali
kuhusu ugumu wa maisha unaowakabili,miundo mbinu mibovu,lakini hilo
limewashinda mkaona mjiingize kwenye ujinga huu ambao chanzo chake ni watoto
wadogo kulumbana.
Imeanza kuwa ni mila na desturi sasa
katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya nne kwa baadhi ya waumini
wa dini ya kiislamu hivi sasa hasa siku za Ijumaa, kuibuka kusikojulikana na
kuanzisha vurugu
kama Mbagala, kuandamana bila taarifa hadi
Wizara ya Mambo ya Ndani, kutoa matamko ya kushinikiza Mkurugenzi Mkuu wa
Baraza la Mitihani ya Taifa, Dk.Joyce Ndelichako hajiudhuru, mara hawamtaki
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Simba,Sheikh Issa Ponda naye anawaongoza baadhi
ya waislamu kwenda kuokoa na kudai mali za waislamu huko Chang’ombe,mara wanagomea
kuhesabiwa kwenye Sensa na kisha kuwazuia watu wasiende kuhesabiwa kwenye sensa.
Kila siku ya Ijumaa ni siku ya Kuabudu kwa ndugu zetu wa dini ya kiislamu
lakini hivi karibuni hususani hapa jijini Dar es Salaam, tumeanza kuona baadhi
ya waumini wa dini hiyo wamekuwa wakiitumia siku hiyo kufanya mambo yao hayo
ambayo wakati mwingine hayapendezi kusikika kwa watu wanaopenda amani.
Ikumbukwe kuwa Ibara ya 19(1),(2),(3) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977, ambazo zinatoa haki kwa mtu uhuru wa mawazo,imani na uchaguzi wa
mambo ya dini,shughuli za uendeshaji
wa
jumuiya za dini
zitakuwa nje ya shughuli
za mamlaka ya nchi.
Lakini Ibara ya 19(3) ya Katiba ya Nchi inasomeka hivi; “Hifadhi ya haki
zilizotajwa kwenye ibara hii itakuwa chini ya taratibu
zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu
katika jamii ya kidemokrasia kwa ajili
ya usalama wa jamii,amani katika
jamii,maadili
ya jamii na umoja wa wa
kitaifa”.uhuru kwa mtu kwa mtu kuabudu.
Sasa vurugu hizi zinazoendelewa kufanywa na baadhi ya waislamu wachache
kwa kisingizio cha kuipigania dini yao,pia
vurugu hizo zinakwenda kinyume na matakwa ya Ibara ya 19(3) ya Katiba ya Nchi.
Naweza kusema jeuri hii waliyonayo
baadhi ya waumini wa dini hiyo wanaoshiriki kiufanya vitendo vya uvunjifu wa
amani uenda ni kwasababu kipindi kile baadhi yao walivyokamatwa kwa makosa ya
kuwazuia watu wengine wasiende kuhesabiwa,wenzao wakaamua kuandamana tena bila
kutoa taarifa polisi hadi wizara ya Mambo ya Ndani na hawakuchukuliwa hatua
zozote na baada ya muda mfupi tukasikia wale waliokuwa wakishikiliwa na jeshi
la polisi wakaachiwa, ndiyo maana uenda inayosababisha hata wafikie hatua sasa
ya kujichukulia sheria mkononi kwasababu wameishajiona wao wapo juu ya sheria.
Leo hii taifa letu bado linakabiliwa na changamoto nyingi za kujiletea
maendeleo ,tunashindwa kuzitafutia ufumbuzi na kufanyakazi kwa bidii lakini
wachache wetu wameanza kuleta vurugu za kidini kwa sababu za kiupuzi kabisa
ambazo mwisho wa siku zitakuja kutuletea madhara wote.
Napenda kuwashauri wale wote wanaotamani waione Tanzania leo hii ikiingia
kwenye machafuko ya kidini, kisiasa,kikabila waame nchi waende kwenye nchi
zenye machafuko ya kisasa,dini na ukabila wakaishi huko kwani huko ndiko hasa
kunakowafaa wao ambao wamechoka kuishi kwenye nchi yetu yenye amani.
Mwisho naomba nimshauri Rais
Kikwete
na viongozi wengine wote walioshirikia nyadhifa za juu za uongozi wa
kiserikali wawaeleze hao baadhi ya wauimini wa dini ya kiislamu kuwa sheria ni
msumeno
na kwamba hakuna aliyejuu ya
sheria na kwamba Tanzania haiongozwi na sheria ya dini ya Kiislamu wa Kikrito inaongozwa
na sheria za nchi na kwamba kitendo cha serikali ya awamu ya nne kuwa na rais
Kikwete,Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman, Makamu wa Rais Kikwete,Mkuu wa Idara
ya Usalama wa Taifa Rashid Othman,Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali
Said Mwema, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Suleman Kova ni waislamu, isihakiwapi
uhalali wa wao kufanya vitendo vya uvunjifu
wa sheria kwa hisia kwamba waislamu wenzao wameshika madaraka ya juu nchini
watawatetea.
Ninachofahamu mimi hao viongozi hao enzi za ujana wao walifanya juhudi
wakajiendeleza kielimu wakasoma kwa shida,wakapata ajira na wakaonyesha
jutuhudi katika utendaji kazi wao huko kwenye majeshi,na kwenye ulingo wa siasa
hadi leo hii wameweza kupata madaraka hayo ya juu ambayo kwa ujinga wenu tu
nyie mnaofanya vurugu mnaanzisha vurugu kwa mwamvuli wa kutetea dini ya
kiislamu na mkikaa vijiweni baadhi yenu mnajitapa kuwa hakuna wakuwachukulia
hatua kwasababu hivi sasa viongozi wa juu wa nchi ni Waislamu wenzenu.
0716 774494
Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com
; Oktoba 17 mwaka 2012