Header Ads

MAKONGORO NYERERE AUNGANISHWA KESI YA PAPA MSOFE


Na Happiness Katabazi

MFANYABISHARA mwingine na Mkazi wa Pugu jijini Dar es Salaam, Makongoro Joseph Nyerere jana aliunganishwa kati kesi ya mauji inayomkabili mfanyabishara maarufu jijini  hapa Abubakar Marijan [50] maarufu kwa jijini  ‘Papaa Msofe chuma cha Reli akishiki Kutu mutu ya Pakee’.

Nyerere alifikishwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na askari kanzu na kabla ya wakili wa serikali   Charles Anindo kuanza kumsomea mashtaka , wakili huyo aliomba ruhusa ya mahakama ili aweze kubadilisha hati ya mashtaka, ya awali iliyokuwa ikimhusu mshtakiwa mmoja tu Papa Msofe, ili mshtakiwa huyo Nyerere awe kuunganishwa katika kesi hiyo ya mauji.

Hakimu Mkazi anayesikiliza kesi hiyo Agnes Mchome alikubaliana na ombi hilo la upande wa jamhuri , lakini akamtaka mshtakiwa huyo kuwa haruhusiwi kujibu chochote baada ya kusomewa shitaka linalomkabili kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba ni mahakama kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. 

 Wakili Anindo akimsoma shtaka alidai kuwa baada ya mahakama hiyo kukubali ombi lake la kuifanyia marekebisho hati hiyo ya mashitaka ambayo awali ilikuwa ikisomeka ni ya mshitakiwa mmoja tu(Papa Msofe), hivyo kuanzia jana kesi hiyo itasomeka kuwa inawakabiliwa washitakiwa wawili ambapo mshitakiwa wa kwanza ni  Papa Msofe na Nyerere ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Pugu jijini Dar es Salaam.

Wakili Anindo alidai kuwa washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kumua kwa makusudi   Onesphory Kituli, kinyume cha kifungu cha 196 cha Kanuni za Adhabu sura ya 19 kama kilivyorekebishwa mwaka 2002 na kwamba kosa hilo walilitenda Oktoba 11 mwaka 2011, nyumbani kwa marehemu  huko Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam na kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Baada ya mshtakiwa huyo kusomewa shtaka hilo, Hakimu Mchome aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 20 mwaka huu,itakapokuja kwaajili ya kutajwa na akaamuru Nyerere apelekwe gerezani  kwasababu kosa analokabiliwa nalo yeye na mwenzi Papa Msofe ambaye tayari yupo gerezani tangu Agosti 10 mwaka jana, halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Agosti 10 mwaka jana , Papa Msofe alipandishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza chini ya ulinzi mkali wa askari polisi  na  Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Hakimu Mchome alidai mshtakiwa huyo anakabiliwa na kosa hilo la mauji

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Februali 14 mwaka 2013.

1 comment:

Anonymous said...



Also viѕіt my wеblog payday loan,
My web site ; payday loans

Powered by Blogger.