Header Ads

HUKUMU YA KESI YA PONDA NI APRILI 18


Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema kuwa Aprili 18 mwaka huu,itaoa hukumu ya kesi ya uchochezi wizi wa malighafi za sh.milioni 59 inayomkabili  Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49.

Hakimu Mkazi Victoria Nongwa aliyasema hayo jana saa kumili alasiri muda mfupi baada ya mashahidi wa tano wa upande wa utetezi waliopanda wote jana kizimbani kutoa utetezi na hivyo kufanya upande wa utetezi weleta mashahidi 52.

Hakimu Nongwa alizitaka pande mbili katika kesi hiyo kuwasilisha kwa maandishi majumuisho ya mwisho ya kesi hiyo Aprili 3 mwaka huu, na kwamba kesi hiyo itatajwa  Aprili 4.

Kabla ya kuyasema hayo Ponda jana  alipanda kizimbani na kuanza kutoa kujitetea ambapo alidai   kuwa ni kweli yeye ndiye aliyetoa maagizo kwa maimau  wa misikiti wawatangazie waumini wao ili waje kwenye kiwanja cha Chang’ombe Markas kwaajili ya kuja kuongeza nguvu ya kujenga msikiti wa muda katika kiwanja hicho.

Itakumbukwa kuwa mashahidi watatu wa kesi hiyo ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh.milioni 59 inayomkabili Ponda na wenzake 49 jumla ya mashahidi wa tatu ambao ni viongozi wa Bakwata na mkurugenzi wa kampuni ya Agritanza, walitoa ushahidi wao na kusema kuwa awali kiwanja hicho kilikuwa kikimilikiwa na Bakwata ambayo ndiyo yenye dhamana ya kumiliki mali zote za waislamu lakini Bakwata ikaamua kuipatia kiwanja hicho Agritanza  na Agritanza ikaipatia Bakwata kiwanja kikubwa kilichopo Kisarawe kwahiyona kusema kuwa kiwanja cha Markas siyo mali ya waislamu wala Bakwata lakini washitakiwa katika utetezi wao wanadai  kiwanja hicho ni mali ya waislamu.

Sheikh Ponda aliyekuwa akiongozwa kutoa utetezi wake na wakili wake Juma Nassor na Njama mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa alieleza  ni yeye ndiye aliyetoa maelekezo hayo ya kuwataka waislamu wote wafike katika eneo hilo ili wajenge msikiti wa muda na kwamba waislamu hao waliitikia wito  na kwamba kuanzia asubuhi ya saa moja hadi saa 12 jioni ya Oktoba 12-14 yeye na waislamu hao walikuwa wakijenga msikiti huo ndani ya kiwanja hicho ambacho ni mali ya waislamu.

“Kiwanja hicho ni mali ya waislamu na kiwanja hicho tulipewa sisi waislamu na serikali ya Misri tena wakati huo waislamu wote tulikuwa chini ya East Africa Muslim Welfare,lakini baadae taasisi hiyo ilifutwa na serikali ndiyo ikaanzishwa Bakwata…kwahiyo kufutwa kwa taasisi ile hakumaanishi mali zilizokuwa chini ya taasisi zake nazo zimefutwa,kinachofanyika pale ni majukumu ya taasisi yale yanakuwa yamesimama na mali zake zinabaki kuwa ni za wanachama wake wa taasisi hiyo iliyofutwa ”alidai Sheikh Ponda

Hata hivyo alikanusha mashitaka yote yanayomkabili na kusema hafahamu ni kwanini upande wa jamhuri umemfungulia mashitaka hayo kwasababu hata hilo kosa la wizi wa malighafi ,mahakama ilipaswa iamie eneo la tukio iende kashuhudie kama wale waislamu niliokuwa nao kama walichukua malighafi za kampuni ya Agritanza kujengea msikiti wa muda.

Akielezea jinsi alivyokmatwa na askari ,Ponda alidai Oktoba 16 mwaka jana ,saa nne kasoro  wakati akiingia ndani ya msikiti wa  Tungi uliopo Temeke  kabla ya kuingia ndani alisikia sauti ya mtu ikimuita na mtu huyo alikuwa ndani ya gari, akawataka watu hao wamfuate nyuma.
“Nilipoingia msikitini nikasikia sauti ya magari nikatazama nikaona magari matatu aina ya Land Cruser  zina askari wa kikosi cha FFU  wakiwa na silaha na mabomu na wale askari walingia ndani ya msikiti wakiwa wamevaa viatu wakanivamia na kuniangusha chini na wakanitoa ndani ya msikiti kwa mtindo wa kuniteka nyara na kunikimbiza kwenye gari lao  kwa kasi”alidai Sheikh Ponda.
Alidai kisha walimepeleka katika kituo cha polisi Chang’ombe na wakanieleza kosa langu na wakaniambia mimi siyo raia wa Tanzania, na ni kwanini nisiende kufanya vurugu Burundi minikawaambia ni rais wa Tanzania’alidai Ponda.

Akijibu maswali ya wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka kuwa hakuona ni kosa kwa yeye kuita waislamu waende kujenga msikiti wa muda katika eneo lile ambalo si mali ya waislamu , Ponda alijibu kuwa ‘Sikiliza Kweka mimi nimeanza mijadala tangu enzi serikali ya rais Julias Nyerere  kwahiyo nina uzoefu na huo siyo uchochezi’alidai Ponda.

Kwa upande wake mshitakiwa wa tano, Mkadamu Abdallah akijitetea yeye alidai kuwa hafahumu hicho kiwanja kiliuzwa kwanani, na wala hajawai kutoa maelezo polisi na hafahamu kama Ponda alienda kwa Mufti wa Tanzania Sheikh Simba kumuuliza kuwa kiwanja hicho kimeuzwa.
Hata hivyo wakili Kweka alipomtaka Mkadamu areje maelezo yake aliyoyatoa polisi ambayo yamepokelewa mahakamani kama kielelezo ambapo ndani ya maelezo hayo Mkadamu alikiri kufahamu kuwa kiwanja kile kimeuzwa kwa Agritanza na Bakwata na kwamba yeye na waislamu wenzake walienda katika kiwanja hicho na kuanza kujenga msikiti wa muda, mkadamu alishia kwa kudai kuwa maelezo hayo si yake.

Oktoba 18 mwaka jana, kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapa kwa mara ya kwanza ambapo washitakiwa wanakabiliwa na jumla ya makosa matano  ambayo ni kula njama kutenda kosa, kuingia kwa jiani, kujimilikisha kwa nguvu kiwanja hicho, wizi wa malighafi zenye thamani y ash.milioni 59 na uchochezi.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa,Machi 22 mwak 2013.  




1 comment:

Anonymous said...

Hmm is anуonе else hаѵing problеms with the pictures on
this blog loаding? I'm trying to determine if its a problem on my end or if it's the
blog. Anу ѕuggеѕtions woulԁ be
gгeatly appгeсiatеd.

Here is mу blog: yookos.com

Powered by Blogger.