WAFUASI WA PONDA WAPUNGUZIWA ADHABU



Na Happiness Katabazi
MAHAKAM A Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetengua adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam Machi 21 mwaka huu,dhidi ya wafuasi 52 wa Sheikh Ponda Issa Ponda  kwasababu adhabu hiyo ilitolewa kinyume na sheria husika.

Hukumu ya Rufaa hiyo ilitolewa jana asubuhi na Jaji Salvatory Bongole ambaye alisema  Agosti 12 mwaka huu alisikiliza  hoja za wakili wa waomba rufaa(Mohamed Tibanyendera) na hoja zilizotolewa na mawakili wa serikali Peter Njike  ambapo wakili        Wakili Tibanyendera alikilichambua kosa la kula njama kutenda kosa kinyume na kifungu 384 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kosa la pili ni la kufanya mkusanyiko haramu kinyume na kifungu cha 74 na 75 cha sheria hiyo  ambavyo vinasomwa pamoja na kifungu cha 43(2)(4) na 46 cha Sheria ya Jeshi la Polisi ya mwaka 2002.

‘Kwa masikitiko makubwa tu   nasema kosa la kula njama halikuthibitika, na hakimu Fimbo alikosea kuwatia hatiani kwa kosa la kula njama kwa kutumia kifungu hicho cha 384 cha sheria ya Kanuni ya adhabu. Na kwa mujibu wa kifungu cha 46 cha Sheria ya Jeshi la Polisi ya mwaka 2002,inasema wazi kabisa mtu anayekutwa na hatia ya kutenda kosa la mkusanyiko haramu atapaswa alipe faini ya Sh.50,000 au kwenda jela miezi mitatu au vyote pamoja:

‘Lakini tunashangaa huyu hakimu Fimbo ameto adhabu ya juu kabisa ya mwaka mmoja jela..sijui hiyo sheria ameipata wapi?Tunaomba mahakama hii itengue hukumu hiyo kwani inadosari nyingi za kisheria na hakukuwa na ushahidi wowote wakuweza kuishawishi mahakama hiyo iwatie hatiani waomba rufaa”alidai wakili Tibanyendera.

Kwa upande wake wakili wa serikali Njike aliiomba mahakama isitengue hukumu hiyo kwasababu hukumu ile ya Mahakama ya Kisutu ilikuwa sahihi kisheria na kwamba upande wa jamhuri ulileta ushahidi mzito ambao uliishawishi mahakama ya Kisutu kuwatia hatiani washitakiwa hao kwa makosa matatu ya kula njama, kufanya maandamano haramu na kukaidi amri ya jeshi la Polisi.

Akitoa hukumu ya Rufaa hiyo jana Jaji  Bongole alisema anakubaliana na wakili wa waomba rufaa kuwa hakimu Fimbo alikosoea kuwatia hatiani katika kosa la kwanza la kula njama, kwani hakukuwepo na ushahidi unaonyesha washitakiwa walitenda kosa hilo la kuja njama kutenda kosa hivyo mahakama yake inawaachiria huru washitakiwa hao katika kosa hilo la kwanza la kula njama kwasababu hakukuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani.

Aidha jaji Bongole alisema hakubaliani  na ombi la waomba rufaa lilotaka mahakama iwaachiriwe katika kosa la pili la kufanya maandamano haramu kwenda katika ofisi za Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi kushinikiza DPP amwachirie huru Ponda aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya wizi wa malighafi na uchochezi katika Mahahakam ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambayo ilimhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja.

“Mahakama hii imekataa kuwaachiria huru katika kosa la pili la kufanya maandamano haramu kwenda ofisi ya DPP na pia imekataa kuwaachiria huru katika kosa la tatu na kukaidi amri ya jeshi la polisi iliyowataka watawanyike kwasababu  , upande wa jamhuri uliweza kuleta ushahidi ambao umedhibitisha waomba rufaa walitenda makosa hayo mawili na kwamba Mahakama Kuu inawatia hatiani kwa makosa hayo na kusema kuwa mahakama ya Kisutu ilikuwa sahihi kuwatia hatiani katika makosa hayo”alisema Jaji Bongole.

Hata hivyo Jaji Bongole alisema pamoja na mahakama yake kuwatia hatiani katika makosa hayo mawili ambapo kwa mujibu wa Sheria ya polisi , mtu anayepatikana na hatia katika makosa hayo anapewe adhabu ya  ya kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela na faini ya Sh. 50,000 na kwamba mahakama yake inawapatia adhabu  kwasababu ndiyo adhabu iliwekwa na Sheria ya Jeshi la Polisi hivyo hakimu wa Mahakama ya Kisutu alikosoea kuwapatia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja.\

Aidha Jaji Bongole alisema licha mahakama yake imewapatia adhabu hiyo, pia mahakama yake imeona washitakiwa ambao walikuwa wakitumikia adhabu ya mwaka mmoja gerezani tayari wameishakaa gerezani muda mrefu na adhabu ya kisheria kwa mujibu wa makosa hayo ya miezi mitatu imeishapita , hivyo mahakama yake inawaachiria huru ila kama waomba rufaa hao wanakesi nyingine, waendelee kushikiliwa na mamlaka nyingi.

Hata hivyo gazeti hili saa nne asubuhi lilishuhudia waomba rufaa hao wakipakizwa kwenye basi la jeshi la Magereza  na kurudishwa gerezani hadi pale mahakama itakapopelekea hati inayoonyesha waomba rufaa hao wameachiwa na Mahakama hiyo.Hata hivyo ulinzi ulikuwa umeimalishwa na hapakuwepo na vurugu zozote.

Kesi hiyo ya kihistoria ilifunguliwa  rasmi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,  Februali 18 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, na siku hiyo hiyo upande wa  jamhuri ukasema upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na  Februali 19 mwaka huu,upande wa jamhuri uliwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao na shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri ambaye ni Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Hemed Msangi alianza kutoa ushahidi wake hadi Februali 26 mwaka huu, upande wa jamhuri ulipofunga ushahidi wake ,washitakiwa wakaanza kujitetea na Februali 19 mwaka huu,Na Machi 21 mwaka huu, Mahakam a hiyo ilimaliza kusikiliza kesi hiyo kwa Mahakama hiyo kutoka hukumu yake ambapo iliwahukumu kwenda jela mwaka mmoja kwa makosa hayo ya kula njama, kufanya maandamano haramu na kukaidi amri ya jeshi la polisi iliyowataka watawanyike.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Oktoba 22 mwaka 2013.

DPP AMWANGUSHA ZOMBE KORTINI





Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam,imekubali ombi la mkurugenzi wa mashitaka lililokuwa linaiomba mahakama hiyo iwaongezee muda wa kupata rural katika mahakama ya rufani nchini kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu kanda ya dar es salaam Agosti 17 mwaka 2009 ambayo ilimwachiria huru aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa dar es salaam, kamishna msaidizi wa polisi, Abdalah zombe na wenzake ambayo walikuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji.
Uamuzi huo ulitolewa jana na JAJI Aloyisius Mujuluzi ambapo Alisema Dpp aliwasilisha ombi la kuomba mahakama umwombe zee muda wa kukata rufani kwa sababu muda wa kupata rufaa ulikuwa umeishapita kwa sababu April 22 mwaka huu, mahakama ya rufaa ili panga kuanza kusikiliza rufaa hiyo ya Dpp lakini mahakama hiyo ilijikuta ikishndwa kuanza kuisikiliza kwa sababu siku hiyo mahakama ilibaini hati ya kukatia rufaa ilimtambulisha jaji aliyekuwa ameitoa hukumu hiyo ni jaji wa mahakama ya rufaa,na hivyo ikafutwa rufaa hiyo na kuelekeza Dpp akaombe ombi la kuomba kuongoza wa muda wa kukatia rufaa pindi wanapoona wanataka kukata rufaa.
JAji mujulizi alisema rufaa ni haki ya kila mtu na nina haki ya umma na haki hiyo imeanishwa wazi katika ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, na kwamba umma katika katika kesi za jinai unawakilishwa na Dpp, hivyo mahakama hiyo kwa kuzingatia mazingira ya kesi hiyo ya zombe kwa ina maslahi ha taifa, watu walichuku loa tofauti hukumu ile iliyowaachilia huru na kwamba kesi hiyo ina tofauti na kesi nyingine kwani kesi hiyo ilisababisha Rais Jakaya kikwete kuunda tume ya ku chunguza mauji ya watu wanna ambao zombe na wenzake watalisaidia kuwaua.
"Hivyo mahakama hii I naona ni Vyema itatoka ruhusa kwa Dpp skate rufaa katika mahakama ya rufaa ili hayo mahakama ya rufaa hayo hukumu yake kwani hukumu ya kuwa choirs huru iliyotolewa na mahakama kuu ilibua maneno na hisia tofauti"alisema JAJI mujulisi.
Aidha jaji mujulisi alisema mahakama yake impatia Dpp nyongeza ya siku 14 za kukata rufaa ambazo siku hizo zinaanza kuhesabika yangu jana.
Hata hivyo JAJI mujuluzi alitupilia mbali pingamizi la awali lililowasilishwa na wakilk Denis Msafiri ambapo liliomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi Hilo la Dpp la kuomba aongezewe muda wa kukata rufaa kwa sababu hati za viapo vilivyoapwaa na wakili Alexander mzikila kwaniaba a ofisi a Dpp haionyeshi mzikila anawadhifa gani katika ofisi ya Dpp na kwamba hati hiyo Imeonyesha mhuri unaonyesha mzikila alikuwa ikapoteza chini ya ofisi wa mahakama mwenye nyadhifa mbili yaani kamishna wa Kiapo na hakimu mkazi hivyo Kiapo hicho ni batiri.
JAJI mujuluzi alisema suala la kuthibitisha Kiapo hicho kuwa ni batiri au la lilikuwa linahitaji kutokuwa ushahidi na wakili Msafiri ambao ungeishawishi mahakama ions hati hiyo ina kasoro hiyo lakini wakili Msafiri alishindwa kuleta ushahidi unaonyesha hati hiyo ni batiri na haistahiri kupokelewa na mahakama hivyo JAJI huyo anatupilia mbali pingamizi Hilo.
Katika hatua nyingine mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, imeshindwa kumtoa hukumu ya kesi ya mauji patia fedha kwa njia ya udanganyifu inayomkabili waziri wa zamani, Arcado Ntagazwa kwa sababu upande wa jamhuri ulichelewa kuwasilisha majumuisho yake ya mwisho kama walivyotakiwa na mahakama hiyo wawasilishe majumuisho yao oktoba 3 na baraka yake wake wasioliona Leo majumuisho hayo wakati Leo kesi hiyo ilikuja kuwasajili ya kutokuwa hukumu na hivyo hakimu mkazi Gene Dudu akasema hataweza kumtoa hukumu hiyo kwa sababu hajaindaa na hivyo anaiarisha kesi hiyo hadi oktoba 25 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kumtoa hukumu.
Wakat huo huo upande wa jamhuri katika kesi ya kutaka kumdhuru mhariri wa Gazeti la mwanza nchi Denis Msaki inayomkabili kiongozi wa chadema,Wilfred Rwakatare umesema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na mawakili wanaomtetea lwakatare wameiambia mahakama kuwa lwakatare bado ni mgonjwa ndio maana ameshindwa kufika mahakaman na hakimu allocate Katemana aliairisha kesi hiyo hadi Oktoba 15 mwaka huu,itakapokuja kwaajili ya kutajwa,.
Chanzo;Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa,Oktoba 18 mwaka 2013