WASHITAKIWA KESI YA MAUJI YA DK.MVUNGI WALALAMA MAHAKAMANI


Na Happiness Katabazi
Mshtakiwa mmoja  kati ya washtakiwa 10 wanaokabiliwa na kesi ya KUMUUA KWA makusudi  ALIYEKUWA  Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu amedai kuwa hawana imani na Mkuu wa Gereza la Segerea  kutokana na kuwahoji vitu ambavyo hawavielewi vinavyohusiana na kesi yao wakati wakiwa gerezani.

Mshtakiwa  John Mayunga (56) alitoa Madai hayo  hayo jana mara baada ya Wakili wa Serikali, Charles Anindo kuwasomea hati mpya ya shtaka la kuua  kwa kukusudia kwa lengo la kumuunganisha mshtakiwa mpya ambaye ni George Geofrey Mulugu (28) mkazi wa Vingunguti na kufanya idadi ya washtakiwa hao kufikia 11.

Akiwasomea upya hati ya Mashitaka  Wakili , Anindo alidai kuwa  washtakiwa hao kwa pamoja  Novemba 3, mwaka 2013, walifanya kosa  la mauaji ya kukusudia  kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.

Anindo  ,  siku hiyo ya  tukio katika  eneo la Msakuzi Kiswegere  lililopo eneo la Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao kwa pamoja walimuua kwa kukusudia Dk Sengondo Mvungi ambaye mjumbe  wa Katiba Mpya.

Wakili  Anindo alieleza Kuwa  upelelezi bado haujakamilika na kuomba ipangiwe tarehe ya kutajwa ili kuangalia kama utakuwa umekamilika ama la ambapo hakimu Mkazi, Geni Dudu alikubaliana na ombi hilo na kuiahirisha hadi Februari 13, 2014.

Baada ya Wakili Anindo kumaliza Kusema hayo ,  Mayunga alinyoosha  kidole na kisha kumueleza Hakimu Dudu kuwa wao wanashangazwa na hatu ya Mkuu wa Magereza kuwahoji vitu ambavyo hawavielewi kuhusiana na kesi yake.

“Hatuna imani naye  anatuhoji vitu ambavyo hatuvielewi kuhusu kesi hii, tunahojiwa mara ngapi, polisi tulikwisha hojiwa  na yeye anatuhoji  tena vitu ambavyo hatuvijui.”Alidai mashitakiwa Huyo .

Baada ya kuyatoa malalamiko hayo, Hakimu Dudu alimwambia mshtakiwa huyo kuwa anacheo fahamu upelelezi bado haujakamilika.

Kwa upande  mshtakiwa Chibago Magozi (32) alimwomba  Hakimu Dudu kumfahamisha juu ya haki za mahabusu, hawaruhusiwi kunywa maji wakiwa mahabusu na kubainisha kuwa yeye ni mgonjwa wa kifua  Kikuu anahitaji maji kwa jaili ya afya yake lakini, akiwa mahabusu kwenye mahakama ya Kisutu akinywa maji askari Magereza alimpokonya maji yake.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Dudu alimwambia kuw yeye bado ni mahabusu kosa lake bado halijathibitika hivyo ana haki zote na kumueleza askari magereza aliyekuwemo mahakamani humo ampatie maji yake.

Askari magereza huyo, naye alimwambia hakimu Dudu kuwa  wanapokuwa wanajiandaa kutoka  magereza kuwapeleka mahabusu mahakamani huwa wana andaa na maji ya kunywa  ambayo yanakuwa wamekwisha yakagua kwa ajili ya mahabusu hao kunywa.

Alieleza ,  kwa bahati mbaya mahabusu hao huyachukua  na kuyaoga na kwamba yanapoisha hawawezi kuruhusu watumie maji yoyote ambayo wao hawajayakagua.

Washtakiwa wengine  wanaokabilia na kesi hiyo ni  Chibago Magozi (32)  mfanyabiashara na mkazi wa Vingunguti Machinjioni, John Mayunga (56) mfanyabiashara na mkazi wa Kiwalani na Juma Kangungu (29)  mkazi wa Vingunguti.

Wengine ni aliyekuwa mlinzi wa marehemu Dk Mvungi, Longishu  Losingo (29) na Masunga Makenza (40) dereva na  mkazi wa Kitunda,  Paulo Mdonondo (30) mkazi wa Tabata Darajani, Mianda Mlewa (40) Mkazi wa Vingunguti, Zacharia  Msese (33)  mkazi wa Buguruni, Msungwa Matonya (30)  mkazi wa  Vingunguti  na Ahmad Kitabu (30) mkazi wa Mwananyamala wilayani Kinondoni


Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Januari 31 mwaka 2014.

KIBANDA AIBWAGA SERIKALI






Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachiria huru Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini Absalom Kibanda na wenzake waliokuwa wakikabiliwa na kesi kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi na kusema kuwa mtu yeyote aliyeisoma makala ile na mwenye akili timamu hawezi kusema makala ile ni ya uchochezi wala kuwafungulia kesi ya uchochezi.

Hukumu hiyo ya iliyokuwa ikisubiriwa kwa shahuku na wadau wa habari hapa nchini na kusababisha jana asubuhi wanahabari kufurika katika viwanja vya mahakama hiyo, Hakimu Mkazi Waliarwande Lema alisema mbali na Kibanda washitakiwa wengine walikuwa ni aliyekuwa Mwandishi wa makala hiyo ilichopishwa katika gazeti la Tanzania Daima la Novemba 30 mwaka 2011, iliyokuwa na kichwa cha habari ‘Wakala Maalum kwa askari wote’,Samson Mwigamba na  Meneja Uendeshaji  Biashara  wa kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Theophile Makunga waliokuwa wakitetewa na mawakili Isaya Matambo, Nyaronyo Kicheree, John Mhozya na Mabere Marando.

Hakimu Lema alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa hati ya mashitaka ilikuwa na jumla ya makosa mawili , kosa la kwanza likikuwa ni la kuandika makala ya uchochezi kinyume na kifungu cha  32(1) (c) na  31 (1) (a) cha Sheria ya Magazeti  sura ya 229  ya mwaka 2002 , ambalo lilikuwa likimkabili mshitakiwa wa kwanza na wa pili (Mwigamba na Kibanda) .

Na kwamba kwa makusudi washitakiwa hao Novemba 30 mwaka 2011 waliandika makala hiyo iliyodaiwa na upande wa jamhuri kuwa ni ya uchochezi  ambayo ilikuwa na nia ovu ya kuamasisha askari wasitii amri zinazotolewa na viongozi wao.Kosa la pili ni la kuchapisha makala hiyo iliyodaiwa kuwa ni ya uchochezi ambalo lilikuwa likimkabili Makunga peke yake, kwamba Kampuni ya Mwananchi ndiyo ilichapisha makala hiyo  na kwamba upande wa jamhuri ulileleta jumla ya mashahidi wa tatu na upande wa utetezi ulileta mashahidi wa nne.

Alisema katika haki jinai , ni jukumu la jamhuri kuthibitisha kesi yao bila kuacha mashaka yoyote na kwamba katika kesi ushahidi wote uliotolewa na jamhuri katika kesi hiyo ni wazi umeishawishi mahakama yake ione kuwa upande wa jamhuri uliokuwa ukiongozwa na mawakili wa serikali Prosper Mwangamila na Elizabeth Kaganda umeleta ushahidi dhahifu na hafifu ambao umeshindwa kuishawishi mahakama hii iwaone washitakiwa wote wana hatia katika kesi walishitakikwa nayo.

“Itakumbukwa kuwa Desemba mwaka jana washitakiwa walipomaliza kujitetea, mahakama hii ilitoa amri kwa pande zote katika kesi hii kuleta majumuisho ya mwisho kwa maandishi  lakini hadi hivi leo mahakama hii inatoa hukumu ya kesi hii ni upande wa utetezi tu ndiyo ulitekeleza amri hiyo na kuleta majumuisho yao ya mwisho na kwa masikitiko makubwa na kustaajabisha upande wa jamhuri hakutekeleza amri hiyo yaani haujaleta majumuisho yao na wala umeshindwa kuleta sababu ya kufanya hivyo lakini hilo hauzui mahakama kutoa hukumu yake”alisema Lema na kusababisha watu kushikwa  na butwaa.

Alisema ili makosa ya uchochezi ya thibitike ni lazima upande wa jamhuri ulipaswa uleta madhara yaliyotokea baada ya ile makala kuchapishwa na madhara yenyewe ni kama kulikuwa na kundi la watu lilipanga kufanya vurugu, au kuna askari kweli walikataa kutii amri za makanda wao lakini upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi wa madhara yaliyojitokeza ndani ya majeshi baada ya makala kuchapishwa na kwa mujibu wa mashahidi wa upande wa jamhuri ambao ni mlalamikaji wa kesi na mpelelezi wa kesi hiyo ofisa wa Polisi David Hizza, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, George Mwambashi walieleza mahakama hapakutokea madhara ndani ya majeshi yao yaliyosabishwa na makala hiyo kwani kuna askari wengi walikuwa hawajaisoma hiyo makala.

“Ukilisoma shitaka la kwanza ni la kuandika makala ya uchochezi linalomkabili Mwigamba na Kibanda.Na Mwigamba alivyojitetea na kueleza kuwa aliandika makala hiyo akiwa Arusha na kuituma katika chumba cha habari kinachochapisha gazeti la Tanzania Daima na upande wa jamhuri umeshindwa kuonyesha kuleta ushahidi unaonyesha makala hiyo kweli iliandikwa na Mwigamba, na alivyoiandika alikuwa na nia ovu, ya kutaka ufanyike uasi ndani ya majeshi na pia umeshindwa kuonyesha Kibanda alishiriki vipi kuiandaa makala hiyo kwa Kibanda katika utetezi wake alieleza kuwa wakati makala hiyo inachapishwa na kuhaririwa alikuwa nje ya Dar e Salaam na hakuna ushahidi wa jamhuri uliotolewa kupinga utetezi wa Kibanda”alisema hakimu Lema.

Alisema shahidi wa Jamhuri Hizza, katika ushahidi wake alidai yeye alipoisoma ile makala aliona ni ya uchochezi na akaenda kutoa taarifa kwa makamanda wake ambao nao waliisoma na kuiona ni ya uchochezi wakamtaka Hizza awe mpelelezi wa kesi na Hizza alimuita Kibanda katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kumhoji kisha baadae akawa shahidi katika kesi hiyo  lakini cha kustaajabisha shahidi huyo ameshindwa kuleta mahakamani maelezo aliyomuhoji Kibanda polisi na badala yake shahidi huyo akaeleza mahakama kuwa eti jeshi la polisi wameamua kukaa na maelezo hayo kwa manufaa yao na kwamba kisheria pale mtu zaidi ya mmoja anaposhitakiwa kwa kosa moja ni lazima upande wa jamhuri ulete ushahidi unaonyesha kila mshitakiwa alishiriki vipi kutenda kosa hilo lakini katika kesi hii upande wa jamhuri umeshindwa kufanya hivyo.

 Akilichambua kosa la pili la kuchapisha makala ya uchochezi lilokuwa likimkabili Makunga peke yake, pia hakimu Lema alisema upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi wa moja kwa moja unaonyesha Makunga ndiye aliyechapisha makala na kuongeza kuwa kwa bahati mbaya shahidi wa Jamhuri ambaye ni Msajili wa Magazeti Rafael Hokororo katika ushahidi wake alioutoa alishindwa kusema kuwa makala hiyo ni ya uchochezi na kwamba Hokororo hakuwai kumuita Kibanda ambaye alikuwa ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima lilochapisha makala hiyo kumuona kuwa makala ile ilikuwa ni ya uchochezi.

“Mimi kama hakimu ni maoni yangu kuwa washitakiwa walishitakiwa kwa hisia tu  na hisia zinakatazwa kumfungulia mtu kesi mahakamani ..kwani hata huyu mpelelezi wa kesi hii Hizza alipaswa alete ushahidi unaonyesha nani aliandika makala ,nani alihariri makala hiyo na ninani aliichapisha makala hiyo……mtu mwenye akili timamu ambaye aliisoma makala hiyo hawezi kusema makala hiyo ni ya uchochezi wala kuwafungulia washitakiwa hao kesi ya uchochezi mahakamani, ’alisema hakimu Lema.

Aidha alisema mwandishi wa makala hiyo Mwigamba aliandika makala hiyo kwania njema tu na alikuwa akiitumia haki yake ya kutoa maoni iliyainishwa kwenye Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977  na kwamba  makala alikuwa na nia njema ya kuyakumbusha askari wa majeshi ya Tanzania kutenda kazi zao kwa kufuata haki na kuheshimu haki za watu wengine za kushiriki maandamo ambazo na kwamba aliandika makala hiyo kwasababu alikuwa akikemea mauji yaliyofanywa na jeshi la polisi Januari 5 mwaka 2011 jijini Arusha ambapo polisi iliwaua watu watatu waliokuwa wakishiriki maandamano yaliyokuwa yameandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), hivyo nawaachiria huru washitakiwa wote chini ya kifungu cha 235 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

 Akizungumza nje ya viwanja vya mahakama, Kibanda ambaye kwa sasa ni Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari, alisema kwanza anamshukuru mungu kwa kushinda kesi hiyo ambayo imemsumbua kwa miaka miwili sasa na kwamba hukumu hiyo imeonyesha wazi kuwa kumbe ni kweli mahakama zetu zinatoa haki na kuwashukuru wanahabari na wadau wa habari waliokuwa nae bega kwa bega wakati wa kesi hiyo.

Naye wakili wa Kibanga, Nyaronyo Kichere alisema kesi hiyo ni ushindi kwa tasnia ya habari na kwamba waandishi wa habari wanayohaki ya kuandika makala za kuwakosoa askari wa majeshi yetu kwani ni kodi zetu ndiyo zinazowalipa mishahara.

Naye Meneja Maadili wa Baraza la Habari (MCT), Allan Lawa alieleza kuwa hukumu hiyo ni ushahidi tosha wa vita ya uhuru wa habari inayopiganwa na vyombo vya habari hapa nchini  ambayo imeanishwa wazi kwenye Ibara ya 18 ya Katiba ya nchi.

Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari walifurika mahakamani hapo tangu asubuhi wengine wakisali kwa imani zao na baada ya hakimu Lema kutoa hukumu yake na kuwaachiria huru waandishi hao walikumbatiana kwa furaha na kumshukuru mungu na kumpongeza hakimu Lema kwa kutoa hukumu ambayo imerejesha faraja na amani kwa tasnia ya waandishi wa habari hapa nchini.

Itakumbukwa kuwa Mwigamba,Kibanda na Makunga walifikishwa mahakamani kwa siku tofauti.Mwigamba alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Desemba 8 mwaka 2011, Kibanda alifikishwa Desemba 20 mwaka 2011 na Makunga alifikishwa Machi 6 mwaka 2012 na washitakiwa wote walikanusha mashitaka.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Januari 30 Mwaka 2014.

ALIYEZIRAI KORTINI AFUNGIWA DHAMANA NA MAHAKAMA


Aliyezirai KORTINI afungiwa dhamana
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,  imekataa kumpatia dhamana mfanyabiashara Hussein Amin Suleiman (39), mwenye asili ya Kiasia, anayekabiliwa na makosa miwili ya kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi ambaye Ijumaa iliyopita, mshtakiwa huyo alianguka na kupoteza fahamu kizimbani baada ya kumsikia Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka, akiieleza mahakama hiyo kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, amewasilisha hati ya kufunga dhamana kwa mshtakiwa.

Kesi hiyo ambayo Jana ilikuwa kwaajili ya kutajwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Issaya Arufani, Alisema Ijumaa iliyopita alisikili ombi la Wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka AMBAlo lilidai  Kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi amewasilisha hati ya KUMFUNGIA dhamana mashitakiwa Huyo chini ya kifungo Cha 148(4) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai 2002.

Hakimu pia alilisikiliza ombi la Wakili wa mashitakiwa Pascal Kamala liliomba Mahakama hiyo iipuuze hati ya DPP na badala yake impatie dhamana mashitakiwa KWA KWA makosa yanayomkabili yana dhamana na kwamba hiyo hati ya DPP haijafafanua ni Sababu zipi za Kumnyima dhamana.

Hakimu Arufani Alisema baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili anikate a ombi la Wakili wa utetezi na kwamba anakubaliana na ombi la upande wa jamhuri ya Kumnyima dhamana mashitakiwa KWA Sababu ya maslahi ya taifa na usalama.

"Kisheria pale DPP anapowasilisha mahakamani hati hiyo ya KUMFUNGIA dhamana mshitakiwa Katika Kesi yoyote ile....Mahakama inakubaliana imefungwa mkono hakiwezi kutoa dhamana KWA mshitakiwa na kwasababu hiyo mahakama hii Katika Kesi hii iliyopo Mbele yangu Mahakama hii inakubaliana ombi la DPP la KUMFUNGIA dhamana mshitakiwa na ninaamuru arejeshwe Gerezani hadi Februali 10 Mwaka huu itakapokuja kwaajili ya kutajwa" Alisema Hakimu Arufani.

Januari 24 mwaka huu. Wakili Kweka alidai kuwa kosa la kwanza linahusu kudharau amri ya mahakama kinyume na kifungu cha 124 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 kuwa Novemba 18 mwaka 2013 huko eneo la Sea View Upanga, Dar es Salaam,  alifanya marekebisho katika kiwanja  Kitalu Na. 1032 /60 LO No. 51464 huko eneo la Ocean Road  na akafanya marekebisho kitendo ambacho ni kinyume na amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi  katika kesi Na. 41 ya mwaka 2012 ya Novemba 18, 2013.

Amri hiyo ilikuwa  ikiikataza Kampuni ya Twiga  Paper  Production  Limited  au wakala wake kuvunja au kufanya mabadiliko yoyote  katika nyumba iliyopo kitalu Na. 1032/60LO No. 51464 Ocean Road.

Wakili Kweka alilitaja kosa la pili kuwa ni la kudharau pia amri ya mahakama hiyo  kuwa Novemba 18 mwaka 2013 huko eneo la See view Upanga   alivunja  nyumba aliyokuwa akiishi ofisa mwenye cheo cha juu wa serikali mwenye cheo cha  Kamishna wa Fursa Sawa ya Kibiashara na nyumba hiyo ni mali ya serikali ilioyopo kwenye kitalu Na. 1032/60LO.No.51464 iliyopo eneo la Ocean Road  kinyume na amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi katika kesi  namba 240 ya mwaka 2004 iliyotolewa mwaka 2007  kwa Kampuni ya Twiga  Paper Products  Limited  au wakala wa kampuni hiyo  ambapo mahakama hiyo ilitoa amri ya kuzitaka pande zote katika kesi hiyo kuacha nyumba hiyo Na. 3 iliyopo kitalu Na. 1032/60  ibaki kama ilivyo hadi pale kesi ya msingi itakapomalizika, lakini mshtakiwa huyo alikaidi amri hiyo ya mahakama na kuivunja.

Kweka alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wanaomba tarehe ya kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa na kwamba licha kesi inayomkabili mshtakiwa huyo ina dhamana, lakini Mkurugenzi wa Mashtaka, Dk. Feleshi amewasilisha hati ya kumfungia dhamana mshtakiwa huyo chini ya kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Kwa upande wake wakili wa mshtakiwa, Pascal Kamala, aliipinga hati hiyo ya DPP kwa sababu inakwenda kinyume na Ibara ya 13(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inasema kila mtu ana haki ya kupata dhamana.

Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi alikuwa akimtazama mshtakiwa aliyekuwa amesimama wakati akisomewa mashtaka yake na ilipofika wakili Kweka kuieleza mahakama kuwa DPP amefunga dhamana, mshtakiwa huyo aliyekuwa amesimama alikuwa akianza kufumba macho na kuhema kwa taabu na baada ya muda kidogo mshitakiwa huyo alianguka chini na kuanza kupepewa na ndugu zake.

Hali iliyosababisha hakimu atoke kwenye kiti chake cha enzi na kwenda kumshuhudia mshtakiwa alivyoanguka kizimbani huku mahakama yote ikibaki na taaruki.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Januari 29 Mwaka 2014

JAJI MKUU ARUSHA KOMBORA



Na Happiness Katabazi
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman  amesema Kesi za oparesheni tokomeza ujangili hazikufunguliwa wala kuamriwa porini bali zilifunguliwa na kusikilizwa kwa mujibu wa sheria katika mahakama.

Jaji Othman aliyasema hayo Jana Katika mkutano wake na waandishi wa Habari Dar es salaam , pamoja na mambo mengi alikuwa akizungumza kelele Cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini AMBAPO Alisema yatafanikiwa Februali 3 Mwaka huu na KWA Dar es Salaam. Yatafanyika katika Viwanja Vya jengo JIPYA la Mahakama ya Tanzania vilivyosababisha MTAA wa Chimala karibu na Hoteli ya Souther Sun AMBAPO mgeni rasmi atakuwa ni Rais Jakaya Kikwete na kwamba maudhui ya Mwaka huu ni " Utendaji Haki Kwa wakati:" " Umuhimu  wa ushiriki wa Wadau".

JAJI Othman Alisema itakumbukwa Kuwa operesheni tokomeza ujangili  ilianza Oktoba 4  na ikasitishwa Novemba MOSI Mwaka Jana,  na kwamba zaidi ya Kesi 516  zilifunguliwa mahakamani na Kati  ya hizo  Kesi 198 zilisikilizwa  na kumalizika na kwamba hiyo ni sawa na asilimia. 38.37 (38.37).
Alisema  Mashitaka mengine yalikuwa yakiitaji   Kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka(DDP), Dk.Eliezer Feleshi  na kwamba Kesi hizo zilifunguliwa kwa Sheria mbalimbali na kwamba Kesi hizo ziliendeshwa ndani ya Mahakama na siyo Porini na kwamba Kesi hizo zilisikilizwa NGOzi ya Wilaya  .

"Nataka umma utambue Kesi hizo zilizofnguliwa kutokana na operesheni tokomeza ujangili hazikusikilizwa Porini silisikilizwa na kuamtiwa mahakamani na sema hivyo kwasababu kuna baadhi ya taarifa zinaripotiwa zinaionyesha utafikiri  Kesi zilizisikilizwa Porini  wakati zilifunguliwa na kusikilizwa mahakamani....ieleweke Kuwa Mahakama ipo KWA Wakili ya kutoa Haki na kutafsiri sheria na ipo kwaajili ya kuzisikiliza pane zote mbili bila kibarua"Alisema Jaji Othman.

Aidha Alitoa onyo KWA wananchi ambao wamekuwa na tabia ya kujichukulia Sheria mkononi KWA Kuchoma mahakama na kwamba vitendo hivyo vim sana kushika Kasi tangu Mwaka 2012 na kwamba jumla ya Mahakama nne za mwanzo zimechomwa MOTO na kwamba waliousika na kitendo hicho ni uhalifu na AnAsababisha Haki za watu kupotea na kuchelewa na hukusababishi watuhumiwa kuachiwa Huru.

Hata hivyo Alisema Mahakama yake bado I naendelea na Mpango wake wa Kujenga na kukarabati Mahakama za mwanzo nchini Kwani Mahakama za mwanzo Ndio kioo Cha Mahakama.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi , Jumatano, Januari 29 Mwaka 2014

HUKUMU KESI YA KIBANDA NI LEO


Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam   Leo inatarajia kutoa hukumu Katika  kesi ya kuandika na kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na wenzake.

Mbali na Kibanda washitakiwa ni  Meneja uendeshaji  Biashara  wa kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Theophile Makunga na   mwandishi wa safu ya (Kalamu ya Makamba. Samson Mwigamba AMBAPO Makala hiyoninayodaiwa Kuwa ni a uchochezi ilikuwa na kichwani Cha Habari kisemacho  ( Waraka maalum KWA Askari wote). AMBAPO upande wa jamhuri Katika Kesi hiyo unaowakilishwa na Wakili wa serikali Prosper Mwangamila unadai Kuwa mAkala hiyo ilikuwa Inawashawishi Askari wasitii amri za viongozi wao ambayo ilichapisha Novemba 30 Mwaka 2011.

Hakimu Waliarwande Lema Leo Ndio anatarajiwa kutoa  hukumu hiyo ambayo inasubiri wa KWA shahuku kubwa na WADAU wa Habari nchini.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Januari 29 Mwaka 2014









AZIRAI KIZIMBANI BAADA DPP KUMFUNGIA DHAMANA







Mahakama ya Hakimu Mkazi KisutuMFANYABIASHARA Hussein Amin Suleiman (39), mwenye asili ya Kiasia, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na makosa mawili ya kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi.
Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, mshtakiwa huyo alianguka na kupoteza fahamu kizimbani baada ya kumsikia Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka, akiieleza mahakama hiyo kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, amewasilisha hati ya kufunga dhamana kwa mshtakiwa.
Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Issaya Arufani, wakili Kweka alidai kuwa kesi hiyo ni mpya na kwamba mshtakiwa huyo anakabiliwa na makosa mawili.
Wakili Kweka alidai kuwa kosa la kwanza linahusu kudharau amri ya mahakama kinyume na kifungu cha 124 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 kuwa Novemba 18 mwaka 2013 huko eneo la Sea View Upanga, Dar es Salaam,  alifanya marekebisho katika kiwanja  Kitalu Na. 1032 /60 LO No. 51464 huko eneo la Ocean Road  na akafanya marekebisho kitendo ambacho ni kinyume na amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi  katika kesi Na. 41 ya mwaka 2012 ya Novemba 18, 2013.
Amri hiyo ilikuwa  ikiikataza Kampuni ya Twiga  Paper  Production  Limited  au wakala wake kuvunja au kufanya mabadiliko yoyote  katika nyumba iliyopo kitalu Na. 1032/60LO No. 51464 Ocean Road.
Wakili Kweka alilitaja kosa la pili kuwa ni la kudharau pia amri ya mahakama hiyo  kuwa Novemba 18 mwaka 2013 huko eneo la See view Upanga   alivunja  nyumba aliyokuwa akiishi ofisa mwenye cheo cha juu wa serikali mwenye cheo cha  Kamishna wa Fursa Sawa ya Kibiashara na nyumba hiyo ni mali ya serikali ilioyopo kwenye kitalu Na. 1032/60LO.No.51464 iliyopo eneo la Ocean Road  kinyume na amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi katika kesi  namba 240 ya mwaka 2004 iliyotolewa mwaka 2007  kwa Kampuni ya Twiga  Paper Products  Limited  au wakala wa kampuni hiyo  ambapo mahakama hiyo ilitoa amri ya kuzitaka pande zote katika kesi hiyo kuacha nyumba hiyo Na. 3 iliyopo kitalu Na. 1032/60  ibaki kama ilivyo hadi pale kesi ya msingi itakapomalizika, lakini mshtakiwa huyo alikaidi amri hiyo ya mahakama na kuivunja.
Kweka alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wanaomba tarehe ya kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa na kwamba licha kesi inayomkabili mshtakiwa huyo ina dhamana, lakini Mkurugenzi wa Mashtaka, Dk. Feleshi amewasilisha hati ya kumfungia dhamana mshtakiwa huyo chini ya kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.
Kwa upande wake wakili wa mshtakiwa, Pascal Kamala, aliipinga hati hiyo ya DPP kwa sababu inakwenda kinyume na Ibara ya 13(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inasema kila mtu ana haki ya kupata dhamana.
Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi alikuwa akimtazama mshtakiwa aliyekuwa amesimama wakati akisomewa mashtaka yake na ilipofika wakili Kweka kuieleza mahakama kuwa DPP amefunga dhamana, mshtakiwa huyo aliyekuwa amesimama alikuwa akianza kufumba macho na kuhema kwa taabu na baada ya muda kidogo mshitakiwa huyo alianguka chini na kuanza kupepewa na ndugu zake.
Hali iliyosababisha hakimu atoke kwenye kiti chake cha enzi na kwenda kumshuhudia mshtakiwa alivyoanguka kizimbani huku mahakama yote ikibaki na taaruki.
Kuona hivyo hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 28 mwaka huu, itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na kuamuru mshitakiwa apelekwe hospitali.
Hata hivyo, ndugu mmoja wa mshtakiwa huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika alikuwa akimzonga mwandishi wa habari hizi asimpige picha mshtakiwa na kumtaka asiandike habari hiyoiShare

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Januari 25 Mwaka 2014


BRAVO RAIS KIKWETE KWA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI





Na Happiness Katabazi
NAMPONGEZA Rais Jakaya Kikwete  KWA kutangaza Baraza la mawaziri Jana.Nampongeza Kwasababu licha ya kelele, majungu ,fitna za watu kupaka Matope baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri waliokuwa Kwenye Baraza la mawaziri la awali Kuwa ni mizigo tena bila kuainisha ushahidi unaonyesha mawaziri na manaibu wale Kuwa ni mizigo.

Rais Kikwete amepuuza kelele hizo Kwani ana mamlaka ya kufanya hivyo pindi anapoona Madai hayo hayana  Msingi  na ni maneno ambayo yaliolewa na watu waliokuwa na ajenda zao

Kwa uamuzi huo wa Rais Kikwete wa kupuuza tuhuma hizo, ni ushahidi sasa Rais Kikwete amekomaa kisiasa na kiuongozi na kwamba hayumbushwi tena na  tuhuma zinazoelekezwa  kwa baadhi  ya watendaji wake ambazo wakati mwingine tuhuma hizo zimekuwa size kweli.

Nawapongeza mawaziri na mawaziri walioteuliwa na ninawaomba wafanyakazi kwa mashahidi ya taifa.Nawapa pole wale manaibu na mawaziri waliochwa Katika Baraza jipya.Wakubaliane na halisi na wa shukuru MUNgu kwa kila jambo.

Mwisho nawaasa waandishi we zangu Kuepuka kuandika Habari zinazowataja  Hao mawaziri walioteliwa Jana Kuwa ni mizigo kwasababu, anaweza kutokea waziri mmoja anatatutwa  Wakili akalifungulia Kesi ya Madai Gazeti husika akitaka adai alipwe mabilioni ya Fedha kwa kuchapisha Habari ya kumdhalisha Kwa kumuita waziri Mzigo.

Nina huakika itaviwia vigumu vyombo va Habari kupelekea ushahidi mahakamani wa Kuonyesha waziri Huyo ni Mzigo,mtaishia Kusema Kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ndiye aliyetaja  Majina ya mawaziri mizigo na sijui Huyo Nape Kama atakubali Kuwa shahidi wenu Katika Kesi hizo.
Vyombo Vya Habari Tujiepushe kuziamini na kuzialalalisha kauli za baadhi wanasiasa wanazozitoa bila kuziamini mAana Mwisho wa siku Gazeti ndilo litakalopata madhara.




ELIAS GOROI : SULUHU YA VITA YA KOO,WIZI WA MIFUGO RORYA


Na Happiness Katabazi

WILAYA ya Rorya iliyopo Mkoani Mara  ni miongoni mwa wilaya mpya hapa nchini ambayo pamoja na mambo mengine imekuwa ikisifika kwa baadhi ya wananchi wake kushiriki katika matukio ya wenyewe kwa wenyewe, wizi wa mifugo  n.k
Fuatana na Mwandishi wa makala hii   ambaye mapema mwaka huu alifika katika ofisi ya  Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Elias .G. Goroi , iliyopo Ingri Juu, Kata ya Mirare  Tarafa  ya Girango wilayani Rorya na kufanya nae mahojiano kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu wilaya hiyo

Swali: Hali ya ulinzi na usalama katika Wilaya ya Rorya ikoje kwasasa ukilinganisha  na miaka ya nyuma?

Jibi:Wilaya ya Rorya ni moja ya Wilaya tano (5) za Kiutawala Mkoani Mara na ni Halmashauri ya Wilaya miongoni mwa Halmashauri saba (7) zilizopo Mkoani Mara.  Mazingira ya Wilaya ya Rorya yanashabihiana na Wilaya nyingine na tabia za wakazi ni zile zile.  Hata hivyo kumekuwepo na matukio ya uhalifu unaolingana kwa muda mrefu, Wilaya ya Rorya na Tarime ni Wilaya zilizokuwa na matukio mengi na makubwa ya uhalifu huko nyuma kama vile; vita vya Kikabila na Koo, Wizi wa kupora mifugo kwa kutumia silaha za moto (Bunduki) na mauaji ya kisingizio cha ushirikina. 

Hali hii ilisababisha Serikali kulitangaza eneo hii la Tarime/Rorya kuwa Kanda Maalum ya Kipolisi.  Hii inamaanisha ongezeko la huduma za Kipolisi na kuimarika kwa hali ya Ulinzi na Usalama unalenga kupunguza matukio hayo ya kihalifu,  ukilinganisha na huko nyuma. 

Swali:Mmejipanga vipi kutokomeza  matukio ya mauaji?
Jibu:Wilaya imejipanga kutokomeza matukio ya mauaji kwa njia tatu (3) kubwa.Mosi; uhakikisha kuwa Ulinzi unaimarika katika ngazi zote kwa kutumia Kamati za Ulinzi na Usalama ngazi husika.Pili Kuimarisha upashaji wa habari za matukio na taarifa za kiintelijensia.Tatu ni Kusimamia utawala wa Sheria na utoaji haki pamoja na kuimarisha Utawala Bora.

Swali:Hali ya uporaji  wa mifugo  kwa kutumia  silaha ikoje kwa sasa?
JIbu:Kama Wilaya majibu ya hapo juu, hakuna matukio makubwa.  Hali ya uhalifu mkubwa na hasa wizi na uporaji wa mifugo kwa kutumia silaha za moto nzito (bunduki) na silaha  za jadi naweza kusema umeisha.  Wizi wa kawaida wa kutumia silaha nao umepungua sana na wizi wa mifugo wa kawaida nao unaelekea kwisha na pale unapotokea unakuwa ni wizi wa ndani na mara nyingi umedhibitiwa na vyombo vya Dola.  Mifugo inayoibiwa kwa njia ya kawaida karibu yote imefanikiwa kukamatwa na kurejeshwa kwa wenyewe.  Watuhumiwa wengi hufikishwa mahakamani na kwa ujumla uhalifu hasa wizi wa mifugo, kwa kipindi cha miaka miwili (2012/2013), niliyokuwa hapa, umeonyesha kupungua kwa asilimia (82%) tofauti na miaka ya 2004 – 2011.  kwa miaka miwili hiyo hapajatokea uporaji wowote wa mifugo kwa kutumia silaha.  Haya ni mafanikio makubwa katika kipindi kifupi.

Swali:Hali ya ugomvi  kati ya Koo na Koo  iliyokuwa ikijitokeza huko  nyuma  ikoje?Mlitumia mbinu gani hadi mkafanikiwa kupungumza matukio hayo?

Jibu:Katika Wilaya za Rorya na Tarime, ukiweza kuthibiti wizi wa mifugo, kwa kiasi kikubwa, umethibiti vita na ugomvi wa Kikabila na Koo.  Kwa Wilaya ya Rorya, baada ya kuthibitiwa wizi wa Mifugo, ugovi wa Koo na Kikabila umepungua sana.  Pia ugomvi huu husababishwa pia na kugombea mipaka na Ardhi ya malisho na kilimo kati ya majirani ambao nao umeshashughulikiwa na kupungua sana.  Kwa miaka miwili hii hakujatokea vita vya ugomvi wa kikabila wa Koo.
Suala hili ni pana sana na siyo rahisi kuainisha mikakati yote tuliyotumia kama Serikali   na Mbinu zote tulizotumia hadi kufanikisha/kupunguza matukio hayo.  Hata hivyo nitaelezea machache ya msingi;-Mosi; Ushirikiano kati ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na vyombo vya Dola hasa Polisi na nyenzo Kuu iliyosaidia kupunguza matukio.  Hii iliongeza usimamizi wa pamoja na wa karibu.
Pili;Dhana ya ushirikishwaji wa Jamii, Vikundi vya Ulinzi na Ulinzi shirikishi ilipewa Mkazo wa hali ya juu.  Hii iliimarishwa doria za pamoja kati ya Polisi na Jamii (Polisi Jamii).  Hii imesaidia sana kuimarisha Amani na Utulivu katika Wilaya ya Rorya na kwa kutumia mpango wa Komandi za Wilaya, matukio makubwa yamethibitiwa kwa kiwango kikubwa sana.  Kupitia mpango huu makosa yote yamethibitiwa kwa zaidi ya asilimi 85% kulinganisha na asilimia 15% ya hapo awali (2004 – 2010).

Tatu, Kwa kuwa kiini kikubwa cha migogoro, ugomvi na vita ulijikita katika wizi na uporaji wa mifugo, Wilaya ilibuni dhana ya mazizi ya pamoja, ambapo Wananchi walishauriwa kuweka mifugo pamoja kwenye zizi la pamoja ili kurahisisha na kuimarisha Ulinzi, jumla ya mazizi takribani 20 yaliungana hasa katika Tarafa ya Girango (Kata za Bukwe, Koryo, Mirare, Goribe, Ikoma na Kitembe).

Nne; Kwa matukio mengi ya ugomvi na mapigano isiyo ya wizi wa mifugo, kwa kutumia dhana ya usuluhishi wa migogoro (Conflict Resolution) mapigano yamepungua sana.  Vita vya mwisho vya Kikabila/Koo ulitokea Kata ya Ikoma mwishoni mwa mwaka 2011 na kuisha kabisa mwaka 2012.
Mbinu hii pia imetumika kuelimisha watu juu ya madhara ya ushirikina, kuchomeana nyumba moto kwa madai hayo na kujichukulia sheria mikononi.  Hii imeenda sambamba na kutoa elimu juu ya Katiba,  sheria na kanuni za Utawala bora ili kupambana na tabia ya matumizi ya nguvu na kujichukulia sheria mkononi.  Shughuli ya utatuzi wa migogoro ni endelevu na inayohitaji mbinu mbali mbali na uzoefu ikiwepo kushauriana na kuelekezana na matunda yake ili yawe ya kudumu yanahitaji muda.  Kwa juhudi czote hizi Wilaya ya Rorya (Kata ya Bukwe) ilitunukiwa cheti cha kuwa Wilaya Salama Nchini mwaka 2012/2013, na I.G.P. SAID MWEMA.

Swali:Wilaya ya Rorya  ipo mpakani na nchi ya Kenya .Je kuna tatizo  la wahamiaji haramu  kutoka nchi jirani?

Jibu:Kama zilivyo Wilaya zote za Mipakani, Rorya nayo inayo majirani na mahusiano mazuri kati yao.  Katika mahusiano hayo inakuwa sio rahisi kutambua au kubaini nani mhamiaji na ni wakati gani uhamiaji na mahusiano yanapoanzia na kukomea.  Kwa uchunguzi uliofanywa na Idara ya Uhamiaji,Wilaya ya Rorya, wapo wahamiaji wapatao 107 Kata ya Ikoma pekee; (58 Kijiji cha Kogaja; Kijiji cha Ikoma wapo 31, na Kijiji cha Nyamasanda wapo 18) imebainika wahamiaji wengi waliingia Nchini muda mrefu uliopita na wengine kukaribishwa na jamaa zao kuishi nao bila kufuata taratibu za Nchi.  Tathimini inaendelea kubaini wengine sehemu nyingine.

Pamoja na ujirani, undugu na mahusiano ya Kijamii watu waliyonayo au wengine kuishi kwa muda mrefu, kwa mujibu wa sheria ya Uraia Na. 6 ya mwaka 1995 kipengele cha 7, hatua zifuatazo za uhamiaji zinachukuliwa.

Mosi ni kuwaandisha  raia wote wa Kenya waishio Kata ya Ikoma kwenye daftari la wageni wakazi (kwa mujibu wa sheria).

Pili ni kuwafikisha mahakamani na kuwafungulia mashtaka baadhi ya raia wa Nchi mbali mbali walioingia bila Vibali.

Tatu,kuwafukuza raia wote wasio Watanzania walioingia hivi karibuni bila kibali kwa kuwapatia “Prohibited Immigrant Notice”.  Kazi hizi zote zinafanyika pamoja.  Kwa kazi inayoendelea,  pamoja na changamoto yake, hatujafikia kusema kuwa tunapata matatizo katika hili kwa sasa na tunaomba uzalendo utumike kwa wenyeji ili kufanikisha, kubaini watu hao.  Changamoto kubwa ni ushirikiano duni tunaopata kutoka kwa viongozi ngazi mbalimbali katika kuwafichua wahalifu wa uhamiaji.  Idara ya Uhamiaji Wilaya ikisaidiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inaendelea kubaini wote wasio raia wa Tanzania.

Swali:Kuna madai kuwa baadhi ya wavuvi wa samaki katika Ziwa Victoria eneo la Rorya   wanatumia  nyenzo  haramu  ikiwemo  sumu kuvulia  samaki,hili unazungumziaje madai haya?

Jibu:Ndio, madai hayo ni ya kweli. Kama ilivyo tabia ya wavuvi wote kutaka kupata samaki wengi na kwa urahisi, tatizo hili linakabili sana uvuvi wa Ziwa Victoria ikiwepo Wilaya ya Rorya, kwa Mfano; katika doria “Operesheni Maalum” ya mwezi wa Desemba, iliyofanywa Mkoani Mara kwa ajili ya kuondoa zana zote harama za uvuvi zinazotumika kwenye maji ya Ziwa Victoria, katika Wilaya za Bunda, Butiama, Musoma na Rorya,  jumla ya zana haramu za uvuvi 11620 kamba (Kokoro) zenye urefu wa mita 53020, samaki wachanga kilo 1830, na jora moja la wavu wa dagaa  vilikamatwa.  Kwa Rorya pekee, zilipatikana kokoro 32, Timba 1139, nyavu za Makila 1240, nyavu za Tupa tupa 29, majora ya wavu wa dagaa 9, na kamba za kuvuta kokoro mita 11920.  katika doria ya Operehsni hiyo samaki wachanga  aina ya Sangara wa Rorya walikamata kilo 120 na Sato kilo 21.

Takwimu kama hizi zinaonyesha uwepo wa tatizo lakini pia rasilimali ya uvuvi kuwa katika hatari ya kutoweka iwapo hatua za maksudi hazitachukuliwa haraka kukabiliana na hali hiyo hatari.  Natoa  wito kwa kila mdau wa tathnia ya uvuvi wa walaji kushirikiana kuchukua hatua stahiki na endelevu.  Hii ni pamoja na kupambana na matumizi ya sumu (mabomu) katika uvuvi Ziwani ambao pia ni hatari kwa Afya ya walaji.  Kikosi cha Askari Wanamaji, kushirikiana na Askari Polisi wa kawaida na nyakati mbali mbali kushirikisha vikundi vya “Beach Management Units” (BMU) kwa nyakati tofauti hufanya doria Ziwani,  ingawa hukabiliwa na ukosefu wa nyenzo za kazi kama vile mafuta ya Boti.

Swali:Wewe Kama Mkuu wa Wilaya ya Rorya , tueleze ni kwanini  baadhi ya watu wa wilaya yako wamekuwa wakisifika kwa kujichukulia sheria mkononi  kwa kuwaua wenzao. Je  hilo linasababishwa na umbumbumbu wa sheria?

Jibu: Nimekaa Rorya kwa muda mfupi (miaka mmoja na nusu) muda ambao hautoshi kuzoea na kuzifahamu tamaduni zote za watu.  Lakini ni na kubaliana nawe kuwa Rorya, kama Wilaya nyingine Mkoani Mara, zipo tabia za baadhi ya watu kujichukulia sheria mikononi na kusababisha mauaji ya binadamu.

Kwamba ni umbumbumbu wa sheria yaani ni kutofahamu sheria ni suala la kutafakari na utafiti wa kina.  Rorya ni Wilaya ya Vijiji (Rural District) kama Wilaya nyingi Tanzania.  Tabia hii unayoulizia, kama ingekuwa ni kutojua sheria, basi ligekuwa ni tatizo la Nchi nzima yaani Wilaya nyingi. 

Sikatai kuwa umbumbumbu wa sheria unachangia, bali siyo sababu pekee.  Wakati mwingine tatizo hili linachangiwa na ushiriki au hamasa toka kwa baadhi ya viongozi.  Ikitokea hivyo hatuwezi kusingizia umbumbumbu wa kutojua sheria.  Lakini pia linaweza kuchangiwa na imani mbalimbali hasa zile za kishirikina na hapa ndipo kazi ya elimu inapotakiwa kuhimizwa ili watu waelimike waache imani hizi za kipuuzi na hatari.  Ili tuondokane na hali hii vizuri kila kiongozi kupiga vita tabia hii na sote kufuata na kusimamia Utawala Bora na Utawala wa sheria.

Swali: Hivi karibuni  pametokea  mgongano  kati ya viongozi  wa serikali na viongozi wa kisiasa  hapa Rorya , tatizo nini?

Jibu: Migogoro ya kazi na uelewa duni wa majukumu lazima unaleta matatizo  mahali popote pa kazi.  Matatizo yanayosababisha aina za migogoro ni mengi yakiwemo, labda, ufahamu mdogo wa mipaka ya kazi na wajibu wa kila mmoja.  Lakini pia yanaweza kusababishwa na pale maslahi ya watu, (siyo ya Chama/Vyama) yanapo hatarishwa kwa njia moja ama nyingine.  Lakini pia migongano ya mifumo kati ya Utawala bora na mifumo ya ubabe katika Uongozi vinaweza kuwa tatizo kisiasa.  Hivyo siyo rahisi mimi kueleza tatizo linalopelekea kuwepo migogoro mpaka nijue ni kati ya nani na nani, katika ngazi gani na uhalisia (nature) wa mgogoro. Kubwa hapa ni kuwataka viongozi kujua mipaka ya kazi na majukumu yao.

Swali:Rekodi zinaonyesha  mapato ya Halmashauri  ya Rorya  yalikuwa  chini ,lakini  hivi sasa yanaonekana kuongezeka .Je mlitumia  mbinu  gani kuongeza  mapato?

Jibu:Ni kweli mapato ya ndani (Proper Own Source) ya Halmashauri ya Wilaya ya Rorya yalikuwa chini kwa mfano; mwaka 2011/2012 ongezeko lilianza kuonekana ambapo makusanyo yalikuwa Sh. 282,988,921/= mwaka 2012/2013 mapato yakafikia Sh. 327,964,125/=.  Hii ni ongezeko la Sh. 44,975,284/= ongezeko hili ni kubwa ukichukulia kuwa linatokana na mbinu ya muda mfupi (mwaka mmoja) mbinu iliyotumika ni kuthibiti ukusanyaji wa mapato hasa kwenye Mialo ya Samaki.  Wilaya ilifanya tathimini upya ya vyanzo vyake vya mapato vyote na kubaini kwamba baadhi ya vyanzo vilikuwa vilitozwa ushuru aidha mdogo au chini ya uhalisia, hivyo viwango vilirekebishwa.  Pia ilionekana kuwa vipo vyanzo ambavyo havijabainishwa hivyo viliongezwa kama vyanzo vipya.

Kwa mikakati hii, pamoja na kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, mwaka huu katika kipindi cha nusu mwaka Julai – Desemba,2013/2014 makusanyo yamefikia Sh. 201,838,652/= ongezeko la Sh. 81,150,269/=. Ili kuongeza mapato zaidi tunatarajia kuimarisha vyanzo vingine kama vile Minada ya Mifugo na kumpata mtalaam Mshauri aliyebobea katika masuala ya ukusanyaji mapato atufanyie tathimini ya jinsi ya kuboresha vyanzo vya mapato ya ndani kwa kupata uhalisia wa mapato na vyanzo.  
Swali: Hali ya kisiasa wewe kama Mkuu wa Wilaya  ya Rorya  na mjumbe  wa Kamati ya siasa ya wilaya.Vipi  hali  ya Kisiasa ya Rorya ikoje?

Jibu: Ni kweli mimi ni mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Chama cha Mapinduzi kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Kama Mjumbe mimi siyo msemaji wa Kamati wala wa Chama (CCM). 
Lakini kama mwanachama na Kada mzoefu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), nami nitahitaji pia kuuliza kwa wasemaji wa Chama  Wilaya, Jee hali ya kisiasa Rorya ikoje? (Kama Mkuu wa Wilaya, hawezi kusema kuwa, hali ya Kisiasa kwa ujumla ndani ya Halmashauri ya Wilaya ni nzuri.  Upo ushirikiano wa Viongozi wa vyama vyote , hasa Waheshimiwa Madiwani, katika uendeshaji wa shughuli za maendeleo.  Kwa ufupi, tukiacha mambo ya ndani ya vyama vyenyewe, ambayo yana wasemeji wa kila Chama, hali ya jumla ya Kisiasa imekuwa shwari muda mrefu.


Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Januari 19 Mwaka 2014.