WASHITAKIWA 'KESI YA SAMAKI WA MAGUFULI' WASHINDA RUFAA





WASHITAKIWA 'KESI YA SAMAKI  WA MAGUFULI 'WASHINDA RUFAA
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Rufaa Dar es Salaam, imetengua adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela na faini ya jumla ya sh.bilioni 22 iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,Februali 23 Mwaka 2012 dhidi ya Raia wa Taiwan na China , Nahodha wa meli Hsu Chin Tai na  wakala wa meli ya Tawaliq 1, Zhao Hanquing baada ya kubaini Sheria zilikiukwa wakati wa uendeshwaji wa Kesi hiyo Katika Mahakama za chini.

Hukumu hiyo ilitolewa Jana na jopo la Majaji wa Tatu Salum Masati, Semistocles Kaijage ambao walisema dosari ya kwanza ambayo Mahakama ya Rufaa imebaini ni kwamba Kesi hiyo il ifunguliwa Katika Mahakama ya bila ya kuwepo Kibali Cha Mkurugenzi Mashitaka (DPP).

Hukumu hiyo inafuatiwana Rufaa iliyokatwa na waomba RUFAA Hao kupitia  Mawakili wao Ibrahim Bendera na John Mapinduzi  hawa kurudishwa na hukumu ya Mahakama Kuu na hivyo Februali Mwaka 2012 walikutwa RUFAA Mahakama ya RUfaa ambapo Jana Mahakama hiyo ya rufaa imekubaliana na hoja za rufaa za raia hao wa kigeni kuwa hukumu ya mahakama kuu iliyowahukumu kifungo cha jumla ya miaka 30 gerezani ilikuwA na makosa kisheria.

Hata  hivyo Mahakama Rufaa  umempatia Ruhusa ya kuwafungulia Kesi upya warufaniwa Hao na wale waliochiliwa na Mahakama Kuu, Kama ataona Ana  ya kufanya hivyo.

Kwa upande  wake Wakili wa waomba Rufaa hao , John Mapinduzi Alisema wamefurahishwa na hukumu hiyo na kwamba HIvi sasa wa najiandaa kupunguza Kesi ya Madai dhidi ya serikali wakuombwa walipwe Melissa Yao ya Tawaliq 1 ambayo imenyofolewa vifaa Vingi na sat wasiyojulikana, na pia serikali iwalipe Fedha ambazo zinathamani ya Samaki Waliokuwa wamekamatwa na serikali Katika Meli hiyo ambayo washitakiwa walk,KWA wakiiendesha.

Hata hivyo mwandishi wa Gazeti Hili aliwashuhudia raia Hao wa KIGENI saa tano Sita mchana Jana wakirejeshwa gerezani kwaajili ya Taratibu zaidi za JESHI la Magereza ili waweze kuachiliwa  Huru na mwandishi wa Habari hizi alipata fursa ya kuzungumzia na maofisa madhara wa Balozi wanazozitoa

FEbruali 23 mwaka 2012 , Jaji Agustine Mwarija alisema   washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu:Kosa la kwanza ni la kuvua samaki bila leseni kinyume na kifungu cha 18(1) cha Sheria Uvuvi katika kina kirefu cha bahari.Kosa la pili ni kuchafua bahari na kuathiri viumbe vilivyomo ndani ya bahari kinyume na kifungu cha 67 cha Sheria hiyo na kosa la tatu ni kusaidia kutenda kosa.

Jaji Mwarija alisema kwa mujibu wa maelezo ya onyo yaliyotolewa na Hsu Chin Tai (Nahodha) na Zhao Hanguin ambaye ni wakala wa meli hiyo nahodha wa meli hiyo alikiri kuwa ni kweli meli hiyo ilikuwa ikifanya shughuli za uvuvi katika ukanda huo na kwamba ni kweli meli hiyo ilivyokamatwa Machi 8 mwaka 2009 na boti ya askari wa doria wa nchi za Tanzania,Afrika Kusini,Botswana na leseni yake ilikuwa ikimaliza muda wake Desemba mosi mwaka 2008 na kwa upande wake wakala huyo wa meli alikiri kuwa kampuni yake ndiyo iliyoshughulika meli hiyo kutoka Bandari ya Mombasa kuja Tanzania.

. Nahodha na wakala nimewatia hatiani katika kosa la kwanza la kufanya uvuvi bila leseni ambapo kila mmoja atalipa faini ya Shilingi Bilioni moja au kwenda jela miaka 20 kila mmoja:

“Katika kosa la pili nimetia hatiani mshtakiwa mmoja tu ambaye ni Nahodha wa meli ambapo atapaswa alipe faini ya Shilingi bilioni 20 au kwenda jela miaka 10, na katika kosa la tatu mahakama hii inawaachiria huru washtakiwa wote kwasababu jamhuri imeshindwa kuthibitisha kosa hilo la kusaidia kutendeka kwa kosa hilo na kwamba adhabu zote hizo zinakwenda pamoja”alisema Jaji Mwarija.

Jaji Mwarija alisema kuhusu ombi la Wakili Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga liloomba meli ya Tawariq 1 ambayo ilikuwa ni kielelezo cha kwanza, itaifishwe, mahakama hiyo imekubali ombi hilo kwa sababu kifungu cha 18(1) cha Sheria ya Uvuvi katika kina kirefu cha bahari ,kinaeleza mahakama ina mamlaka ya kutaifisha chombo kilichotumika kutendea kosa na kwamba katika kesi hiyo meli hiyo ilitumika kufanya uvuvi haramu.

“Nimeangalia mazingira ya kesi hii, meli hiyo imekuwa na maji mengi tofauti na hali hiyo imenifanya niamini meli hiyo ilikuwa ikifanya uhalifu huo katika eneo la Tanzania kwa mbinu za aina yake na meli hiyo imeonyesha ilikuwa haitambuliwi na mamlaka husika: 

“….Na hili kukomesha uhalifu wa aina hii mahakama hii itatoa amri ya kuitafisha meli hiyo kuanzia sasa ili iwe fundisho kwa meli nyingine zinazokuja kufanya uhalifu katika Ukanda wa Tanzania na pia sitatoa amri yoyote kuhusu wale samaki waliokamatwa kwenye meli hiyo na kisha wakagaiwa kwenye taasisi mbalimbali za serikali na washtakiwa kama hawajalidhika wana haki ya kukata rufaa ”alisema Jaji Mwarija.

Kwa upande wake wakili wa utetezi John Mapinduzi alisema anakusudia kukata rufaa katika mahakama ya rufaa dhidi ya hukumu hiyo kwani hawajaridhishwa na hukumu hiyo.

Novemba 21 mwaka 2011, washtakiwa hao walimaliza kujitetea , ikiwa siku chache baada ya mahakama hiyo kuwaona washtakiwa hao watano wanakesi ya kujibu na kuwaachilia huru washtakiwa 31 kwasababu mahakama iliona hawana kesi ya kujibu.Kesi hiyo imekuwa ikiwahusisha wakalimani wa ligha zaidi ya nne tangu ilipofunguliwa katika mahakama hiyo ya chini hadi mahakama Kuu. 

Machi 2009 washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kisha kesi hiyo ikahamishiwa Mahakama Kuu wakikabiliwa na makosa ya kuvua samaki bila leseni, kuharibu mazingira katika kina kirefu cha ukanda wa Bahari ya Hindi eneo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusaidia kutendeka kwa kosa hilo.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi ,Machi 29 Mwaka 2014

MKENYA KORTINI KWA KUIHUJUMU TCRA


Mkenya kizimbani kwa kuiujumu TCRA
Na Happiness Katabazi
RAIA wa   Kenya, Nelson Rading Onyango Jana amefikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na  na  saba  likiwamo kosa la  kutoa huduma ya mawasiliano ya Kimataifa bila ya kuwa na leseni na kuisababishia hasara  Mamlaka ya Mawasiliano  nchini (tcra), zaidi ya Sh.ya zaidi ya Sh.bilioni  6.8 .

Wakili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka Mbele ya Hakimu Devotha Kisoka   alidai kuwa   kati ya Julai 2010 na Novemba 2013 katika eneo  la Kariakoo  mshtakiwa huyo  kwa nia ovu alifanya udanganyifu  katika  matumizi ya kimtandao kinyume cha sheria.

Wakili Kweka  alidai kuwa  Onyango   kwa nia ovu  na udanganyifu  alikuwa akifanyisha huduma za mawasiliano ya Kimataifa huku akikwepa  kutumia njia halali za maalipo  ambazo zinatolewa na ( TCRA.

Shitaka la pili, Wakili Kweka alidai Kuwa mshitakiwa Huyo   anadaiwa kutoa huduma ya mawasiliano bila ya kuwa na leseni inayomruhusu kufanya hivyo.

Kweka  alidai kuwa  katika kipindi hicho, mshtakiwa huyo  bila ya kuwa na uhalali kisheria  alitoa huduma ya simu za Kimataifa  bila ya kuwa na leseni  inayotolewa na TCRA.

Mshtakiwa huyo  katika Shtaka la tatu anadaiwa kuwa   kati ya  Januari 2013 na Novemba 2013 akiwa katika eneo hilo la Kariakoo alitumia  kadi za simu ambazo hazijasajiliwa kama inavyotakiwa kisheria zenye  namba 0778350683,0778498179,0774395401,0774552099,0774552122,0774552138 na 0777225.

Alizitaja namba nyingine kuwa ni 07748802243,0774802250,0774802255,0774802265,07748022278,0777848892,0779579620,0779579848,0779663386,0779716796,0779716800,0779716804,0779716811,0779716812,0779716822 na 077971.

Shtaka la nne, mshtakiwa huyo   anadaiwa kuingiza nchi ni vifaa vya kielectroniki  bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya hivyo.
Akiendelea kusoma mashtaka yanayomkabili  Onyango , Wakili Kweka alidai kuwa  siku isiyofahamika   aliingiza mitambo ya mawasiliano ambayo ni SIM Boxi  bila ya kuwa na kibali.

Wakili Kweka, shtaka la tano alidai kuwa licha ya kuingiza nchini mitambo hiyo bila ya kuwa na kibali mshtakiwa huyo, alisimika mitambo mine  ya mawasiliano  na kuiendesha  ambayo ni SM Boxi  zenye namba za siri  TX 2SN5600C5/05, TX2SN48002/K21, TX2SN102335A na  wa  Cisco  Router  iliyotengenezwa Cisco AS5300 mfululizo  yenye namba ya siri ASN 050-332-940 na AP12KGCAA.

Katika shtaka la sita, wakili huyo wa Serikali Mwandamizi alidai kuwa Onyango alitumia mitambo hiyo  ya Kielectroniki ambayo ilikuwa haijathibitishwa na TCRA.

Aliongeza kudai kuwa Novemba 22, 2013 Kariakoo , akiwa na ufahamu  kuwa mitambo hiyo haijathibitishwa na TCRA aliitumia.

Shtaka la saba, mshtakiwa huyo anadaiwa kusababisha hasara kwa mamlaka  husika ya TCRA  kati ya Julai 2010 na Novemba 2013  kwa kufanya huduma hizo za mawasiliano ya Kimataifa bila ya kuwa na leseni .

Ilidaiwa kuwa kati ya Julai 2010 na Novemba 2013 mshtakiwa huyo alichepusha  mawasiliano ya simu za Kimataifa  kwa kutumia namba hizo ambazo hazijasajiliwa  na TCRA  na kwamba kutokana na kitendo hicho aliisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh 6,842,880,000.00.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa aliyakana yote na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Devotha Kisoka alimwambia mshtakiwa huyo kuwa kulingana na makosa hayo yanayomkabili dhamana ipo wazi hivyo alimtaka kutoa fedha taslimu mahakamani hapo Sh 3.4 bilioni na kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika.

Akiendelea kutoa masharti  hayo ya dhamana, hakimu Kisoka alisema mdhamini mmoja kati ya wadhamini hao wawili awe ni mtumishi wa serikali  na mwingine atakayekubalika na mahakama na kwamba wadhamini wote hao watasaini bondi ya Sh  milioni 50.

Kesi  imeahirishwa hadi Aprili 8, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa alipelekwa rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Machi 27 Mwaka 2014

TUNAPAMBANA KWELI NA DAWA ZA KULEVYA?

Na Happiness Katabazi

SERIKALI  pamoja na wananchi miongoni mwetu tumekuwa tukijinasibu kuwa tunapiga  vita matumizi ya dawa za kulevya ‘unga’  yenye mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi.

Hoja ya kupiga vita biashara hii haramu inatokana na bidhaa yenyewe kusababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji pamoja na kuichafulia sifa nzuri nchi ya Tanzania inayoonekana ni kitovu cha usafarishaji wa dawa hizo.

Serikali na taasisi mbalimbali za umma zimekuwa zikiibuka pale wanapokamatwa watuhumiwa wa dawa hizo wakiwa na uzito mkubwa au kuwahusisha watu wenye majina makubwa.

Wakati huo ndiyo huonekana mwanasiasa fulani akijinasibu kuwa kinara wa kupinga usafirishaji, uuzaji na utumiaji. Tambo zake huungwa mkono na vyombo vya habari kwa muda baada ya hapo mambo huendelea kwa utaratibu wa kimazoea.

Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kinachoongozwa na Kamanda, Godfrey Nzowa, kimejitahidi katika kupambana na dawa hizo lakini tatizo kubwa ni sheria, nia thabiti na utekelezaji wa wadau mbalimbali.

Licha ya serikali kupambana na biashara hiyo haramu, tujiulize ni kwanini serikali hii tangu Agosti  mosi mwaka jana, hadi leo imeshindwa kumteua Kamishna mpya wa Tume ya Kuzuia na Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini?

Aliyekuwa Kamishna wa tume hiyo, Christopher Shekiondo, amestaafu kazi, Agosti mosi mwaka jana, hadi leo hatujasikia ameteuliwa kamishna mpya.

Tume iliyokuwa ikiongozwa na Shekiondo ilianzishwa kisheria na taratibu za kiuendeshaji zilikuwa zikifuata mkondo huo huo.

Moja ya jukumu la tume hiyo ni kutoa thamani ya dawa za kulevya alizokamatwa nazo  mtuhumiwa katika kesi fulani zilizofunguliwa  Katika mahakama tofauti, ikiwemo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Kesi nyingine za dawa za kulevya zilizofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi  zimefunguliwa kwaajili ya kuandaliwa kisha zihamishiwe Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kwa ajili ya kusikilizwa kwa sababu Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya ambazo thamani yake imezidi sh milioni 10.

Hivyo kisheria ni lazima zifunguliwe Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuandaliwa (committal proceedings) kisha zihamishiwe Mahakama Kuu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Nimekuwa nikiandika matukio na mienendo ya kesi mbalimbali zikiwemo kesi za dawa za kulevya katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Nimefanya utafiti na nimekuwa nikihudhuria na kuandika kesi mbalimbali ikiwa pamoja na kuzungumza nje ya mahakama na washitakiwa wa kesi hizo, askari, mahakimu na wadau wengine wa mahakama, umeonyesha    mwaka 2012 , Jamhuri ilifungua kesi za dawa za kulevya mahakamani hapo 19.

Mwaka 2013 , Jamhuri ilifungua mahakamani hapo kesi za dawa za kulevya 13 na kuanzia Januari 2 mwaka huu hadi Februari  27 mwaka huu, upande wa jamhuri ulifungua kesi za dawa za kulevya  nane.

Na washitakiwa wa kesi hizo wapo gerezani kwa sababu ya kutokuwapo kwa dhamana kwenye makosa au tuhuma za aina hiyo,  kila zinapokwenda mahakamani hapo upande wa Jamhuri umekuwa ukidai upelelezi wa kesi hizo haujakamilika.

Kesi nyingine zinaongezewa milolongo isiyo na sababu kwakuwa wahusika hukamatwa viwanja vya ndege ama wamebeba au wamemeza dawa husika. Wanaomeza hulazimishwa kuzitoa kwa njia ya haja kubwa.

Watuhumiwa wa aina hii wanahitaji upelelezi wa aina gani? Wapo baadhi yao walishakutwa na vidhibiti eneo la tukio lakini kesi zao zina miaka miwili zikifanyiwa upelelezi.

Upelelezi wa aina hiyo ndio unaolisababishia taifa hasara kubwa ya kuwalisha mahabusu pamoja na kufurika kwa magereza yetu.

Kuchelewa kukamilisha upelelezi kunasababisha mashahidi waliokusudiwa kufariki dunia, ugonjwa, kuacha kazi, kusafiri au sababu zozote zile zinazokwamisha au kufifisha kesi.

Gharama za kuwasafirisha mashahidi wa aina hii ni kubwa sana, sioni sababu kwanini Kesi za dawa za kulevya aina chukua muda mrefu kumalizika wakati serikali inasema ipo Kwenye vita dawa za kulevya? 

Yapaswa tutafakari kwa kina juu ya vita hii na dhamira ya serikali, inakuwaje kesi za dawa za kulevya zichukue muda mrefu ilhali kesi za maandamano kama ile iliyokuwa ikiwakabili wafuasi 52 wa Sheikh Ponda Issa Ponda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitolewa hukumu haraka?

Kesi hiyo ya maandamano ilifikishwa mahakamani Februari mwaka jana na ikatolewa hukumu Machi  20 mwaka jana, kesi hii ilimalizika ndani ya mwezi mmoja.

Hukumu zinapotolewa mapema watu hupata muda wa kuendelea na masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Kama serikali imedhamiria kutokomeza biashara haramu ya ‘unga’, kwanza imteue Kamishna mpya wa Tume ya Kuzuia Dawa za Kulevya.

Kamishna huyu ni muhimu, kwakuwa ndiye anayetoa thamani za dawa zinazokamatwa kama moja ya kielelezo mahakamani, naamini kuna Watanzania wengi  wana sifa za kushika wadhifa huo.

Kama serikali haipo tayari kutafuta kamishna mwingine, basi wamrudishe Shekiondo na wampe mkataba mwingine. Tangu Agosti mosi mwaka jana hadi leo tume hiyo haina kamishna.

Mungu Ibariki Tanzania.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Machi 23 Mwaka 2014

MASKINI SHEIKH PONDA



Na Happiness Katabazi
JITIHADA za Mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu,, Sheikh Ponda Issa Ponda za kuiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaaam, ikubali ombi lake lililokuwa Linaomba Mahakama hiyo Ifanyie mapitio uamuzi wa awali wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro , umegonga Mwamba baada ya Mahakama, hiyo kutupilia Mbali ombi lake.

KORTI Kuu yamliza sheikh Ponda
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia  Mbali ombi la kuomba Mahakama hiyo Ifanyie Marejeo uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Oktoba Mosi Mwaka Jana, ambalo liliwasilishwa Mbele yake na Sheikh Ponda Issa Ponda.
Uamuzi huo ilitolewa Jana asubuhi na Jaji Agustino Mwarija ambaye alisema Mahakama yake imesikiliza hoja za pande zote mbili  na Imefikia uamuzi wa kukubaliana na pingamizi la awali liliwasilishwa mahakamani na mjibu  Maombi ambaye ni MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Dk.Elizer Feleshi,   Februali Mwaka huu mahakamani hapo AMBAlo liliomba ombi la Ponda litupwe kwasababu linakiuka matakwa ya Kifungu cha 372(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 ambacho kinakataza amri za MUDa ,awali zinazotokana na Mahakama za chini zisikatiwe RUFAA katika Mahakama za juu Kama Ponda aliyofanya kukata rufaa amri hiyo ya MUDa ambayo uamuzi wa Oktoba Mosi Mwaka Jana haumalizi Kesi ya Msingi inayomkabili Ponda Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.

Jaji Mwarija Alisema anashangazwa na Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassor kushindwa kuelewa kuwa Kifungu hicho cha 372(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 , kinakataza amri za MUDa, awali ambazo hazimalizi Kesi za Msingi na ambazo zinatolewa na Mahakama za chini, hazitakiwi Kupatiwa rufaa Mahakama za juu.

Jaji Mwarija Alisema ombi Hilo la Ponda Na.14/2013 liloletwa Mbele yake lilitokana  na amri  ya awali iliyotolewa na Mahakama ya Ya Hakimu Mkazi Morogoro ,Oktoba Mosi Mwaka Jana, AMBAPO Mahakama hiyo Iliikataa hoja ya Wakili wa Ponda , Nassor iliyokuwa ikidai Mahakama ya morogoro haina mamlaka ya  kusikiliza kosa la kwanza Katika Kesi ya Msingi Na. 128/2013  AMBAPO kosa la kwanza linalomkabili Ponda ni kutotii amri  halali ya JESHI la POLISI  kinyume na Kifungu cha 124 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002 , na kwamba alitenda kosa Hilo  AGOSTI  10 Mwaka Jana, Katika eneo la Kiwanja cha Ndege Wilayani Morogoro Kitendo ambacho ni kukiuka amri ya Hukumu ya Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotolewa Mei 9 mwaka jana, ambayo ilimtaka asitende makosa na awe mtunza amani.

Kwamba  uamuzi huo wa Oktoba Mosi Mwaka Jana iliusiana na kosa Hilo Moja tu licha Anakabiliwa na jumla ya makosa matatu na makosa hayo matatu hayahusiaji na Maombi hayo yaliyotolewa uamuzi Jana.

" KWA Kuwa Ponda Anakabiliwa na Mashitaka matatu Katika Kesi ya awali kule Morogoro na uamuzi wa wa Oktoba Mosi Mwaka Jana, sio uamuzi wa kumaliza Kesi ile ya jinai ni uamuzi wa MUDa tu,....Mahakama hii inakubaliana na pingamizi la awali la Wakili wa serikali Kongola Kuwa ombi Hilo la Ponda limevunja matakwa ya Kifungu hicho na kwasababu hiyo inalitupilia Mbali ombi Hilo la Ponda lililokuwa Linaomba Mahakama yangu Ifanyie Marejeo uamuzi wa awali wa Mahakama ya awali ya Morogoro" Alisema Jaji MwAarija.

Nje ya Mahakama wafuasi  wake na ndugu zake walikuwa wakisikika wakisema huku wakimpungia mkono " Takibiri' na Kisha kuondolewa eneo la Mahakama Chini ya Ulinzi Mkali wa jeshi la Polisi na Magereza. 

Ilipofika saa Sita mchana Wakili wa Ponda, Nassor aliwasilisha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ombi la kuomba Mahakama hiyo itoe amri ya kusimamisha usikilizwaji wa Kesi Na.124/2013 inayomkabili Ponda mjini  Morogoro hadi Rufaa Na.89/2013 iliyokuwa na Ponda Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam , Kapinga hukumu ya Mahakama ya Kisutu iliyotolewa MEI 9 Mwaka Jana, Ambayo ilimfungankifungo cha Nje Ponda itakaposikilizwa na kuamriwa.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 19 Mwaka 2014












UPELELEZI KESI YA MADABIDA WAKAMILIKA



Na Happiness Katabazi 

UPANDE wa jamhuri Katika Kesi ya kusambaza dawa za kupunguza MAKALI ya ugonjwa wa ARVs inayomkabili  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam Kuwa upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika.


Wakili wa serikali Jacline Nyantori adai Mbele yaHakimu Mkazi  Nyigulila Mwaseba, 
Kuwa upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika na wa naomba wapangiwe tarehe ya kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa.

Hakimu Nyigulila aliarisha kesi hiyo hadi Aprili 23 Mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya upande wa jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa.

Mbali na Madabida washitakiwa wengine  ni Seif Salum Shamte ,Simon Msoffe, Fatma Shango ,Sadiki Materu na Evance Mwemezi na kwamba hati ya mashitaka ina jumla ya mashitaka matano.

Februali 10 Mwaka huu, washitakiwa Hao walifikishwa wa Mara ya kwanza Mahakamani hapo wakikabiliwa makosa matano yakiwemo makosa ya    la kusambaza dawa za ARVs zilizokwisha muda wa matumizi kinyume na kifungu cha 76(1) cha Sheria ya Taifa ya Vyakula, Madawa na Vipodozi ya mwaka 2003 na kuisababishia Bohari yaMadawa Hasara  ya sh 148,350,156.48

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 19  Mwaka 2014.


MMILIKI JENGO LILILOANGUKA DAR ABADILISHIWA SHITAKA


MMILIKI JENGO LILILOANGUKA DAR ABADILISHIWA SHITAKA
Na Happiness Katabazi
MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi Amemfutia Kesi ya KUUA bila kukusudia mmiliki  wa jengo liloanguka  Katika MTaawa INdra gandi mwenye asili ya kiasia,  Raza Hussein Raza na Wenzie  11 akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,  Gabriel Fuime  na  kisha kuwafungulia Kesi mpya ya Mauaji   ya watu 27.

Wakili Kiongozi wa Serikali Bernad Kongora  akisaidiwa na Joseph Mahugo,Inspekta Jackson Chidunda,Peter Njike, Tumaini Kweka Mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoki , alianza KWA Kudai Kuwa awali washitakiwa 11 walikuwa wakikabiliwa na Kesi KUUA bila kukusudia ambayo il ifunguliwa Mwaka Jana mahakamani hapo na walikuwa nje KWA DHAMANA, isipokuwa Fuime ambaye alifunguliwa Kesi ya Mauaji  hivi karibuni mahakamani na Kuwa akiishi gerezani.

Wakili Kongora alidai Kuwa upande wa jamhuri unaomba kutumia Kifungu cha 234(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 , kubadilisha hati ya Mashitaka ya Kesi Kuua  bila kukusudia kwasababu wanamuunganisha mshitakiwa mpya (Fuime) Katika Kesi mpya ya Mauji ya kukusudia ya watu 27  kinyume na Kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu  ya Mwaka 2002, ombi AMBAlo lilikubaliwa na Hakimu Huyo.

Akisoma hati hiyo , Kongola aliyetaja Majina ya washitakiwa Kuwa ni RAZA ambaye ni mmiliki  wa Jengo lililoanguka Mtaa  wa Indra Gandi na KUUA watu 27, Goodluck Silvester,Wilbroad Mugya, Ibrahim  Mohamed ,Charles  Salum  Ogare ,Zonazea Anange,Oushao Udada,Vedasto Frednand Ruhele,Michael Leth,Albert Mnuo ,Joseph Ringo na Gabriel Fuime wanaotetewa na Wakili John Mhozya.

 Kongora alidai makosa hayo 27 ya Mauaji   ya watu 27 waliyatenda  Machi  29 Mwaka  2013  Katika Mtaa wa INDRAGANDI  na kwamba upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika.

KWA upande Wake Hakimu Kisoki  ambaye ndiye hakimu ALIYEKUWA akiisikili za Kesi ya awali ya KUUA bila kukusudia iliyokuwa ikiwakabili washitakiwa Hao,  ambayo Jana ilifutwa na kufunguliwa Kesi mpya ya Mauji ambayo pia amepangwa  kusikiliza  yeye.

 Hakimu Huyo Alisema KWAKUWA upande wa jamhuri umebadilisha hati ya Mashitaka na kuwafungulia washitakiwa Kesi mpya ya Mauji ha watu 27 , kesi ya zamani ya KUUA bila kukusudia na dhamana zinakuwa zimetutwa na hivyo HIvi sasa washitakiwa watakuwa wanaokabiliwa  na Kesi  mmoja ya Mauji ambayo haina dhamana na Mahakama hii hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza Kwani ni  Mahakama Kuu ndiyo Ina mamlaka ya kuisikiliza  , hivyo akaamuru washitakiwa wapelekwe Rumande hadi Machi 26 Mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa.

Baada ya Hakimu Kisoki Kutoa Amri hiyo ndugu na Jamaa wa washitakiwa Hao akisemo Mtawa (sister ) wa Kanisa Katoriki, aalijikuta wakiingia Bilioni Katika Viwanja Vya Mahakama hiyo wakiwa hawaamini Kama ndugu zao HIvi sasa washitakiwa kwa Kesi ya Mauji  ambayo haina dhamana na kwamba HIvi sasa watakuwa wakiishi gerezani.

hata hivyo washitakiwa Hao ambao walikuwa wakilindwa chini ya Ulinzi MKALI wa kaka hero wa JESHI la POLISI, mshitakiwa wa kwanza  Raza ambae ana asili ya Kiasia Kabla ya Hakimu kuingia mahakamani mwandishi wa Habari hizi alimshuhudua Akiwa amesimama wakati washitakiwa wenzie  wamekaa Kwenye mabenchi wakisubiri Hakimu aingie akiwa ameshika (tasibiri) mkononi anaibesabu  na mara Hakimu Alipoingia walk panda kizimbani na wakati wakisomewa Mashitaka alikuwa amesimama akiende lea kuiesababu  na Muda mchache aalijikuta alishindwa kuendelea kusimama na akaomba ape we Kiri akae ambao ambapo  alikaa Kwenye Kiti kilichoketi nyuma ya washitakiwa.

Machi  Mwaka Mwaka Jana washitakiwa Hao 11 ,walifikishwa mahakamani hapo KWA Kesi na KUUA bila kukusudia na Hakimu Huyo aliwapatia DHAMANA, lakini Jana DPP aliwafutia Kesi hiyo na kuwafungulia Kesi mpya ya Mauji ambayo kisheria haina dhamana.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Machi 13 Mwaka 2014.



'VIROBA' VYA WAFIKISHA KORTINI


 Na Happiness Katabazi

WAFANYABIASHARA Wawili Jana walifikishwa Katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam , wakikabiliwa na kosa Moja la kuuza Katoni 216 za Pombe halisi Maarufu "Viroba" zinazoonyesha zimetengenezwa na kampuni ya Mega Trade Ltd , jambo AMBAlo sio kweli.

Wakili Mwandamizi wa serikali, Joseph Mahugo  ya Hakimu Mkazi Augusta Mbando akiwa taja washitakiwa Hao Kuwa ni Elizabeth Masawe na Frank Rudika  na kwamba Novemba Mwaka 2011 walikamatwa na Viroba hivyo huko eneo la Keko Magurumbasi Jijini Dar es Salaam  kinyume na Sheria Ya Bidhaa  iliyofanyiwa marekebisho No.5 ya Mwaka 2005 na kwamba  Kwamba upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika na washitakiwa walikanusha Shtaka 

Hakimu Mbando Alisema ili mshitakiwa speed DHAMANA nilazima awe na mdhamini wa huakika atakaye SAINI BONDO ya sh. Milioni tano, Shari AMBAlo lilitimizwa na washitakiwa Hao na wakapata DHAMANA na Kesi hiyo imearishwa hadi Aprili  4 Mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutaka.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Machi 13 Mwaka 2014

KORTI YAMRUHUSU MRAMBA,YONA KWENDA INDIA KUTIBIWA


Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Da es Salaam, imemtuhusu waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba na Waziri wa Nishati na Madini wa zamani, Daniel Yona, WANAOKABILIWA na Kesi ya matumizi Mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali Hasara ya sh Bilioni 11.7, kwenda nchini India kutibiwa.

Ruhusa hiyo ilitolewa Jana na Jaji John Utamwa, MUDa mfupi baada ya Wakili wa serikali Shadrack Kimaro kuiambia Mahakama hiyo upande wa jamhuri Hakuna pingamizi na ombi Hilo liliwasilishwa na Wakili wa washitakiwa Juzi Peter Swai liloomba Mahakama iwapatie Ruhusu wateja wake warned nje ya nchi kutibiwa.

JAJI  Utamwa Alisema licha Amearuhusu washitakiwa waende kutibiwa India, pia Amekataa washitakiwa watakapo rejea nchini waakikishe wanatetewa hati zao za kusafiria mahakamani hapo na akaairisha Kesi hiyo hadi Aprili 21 hadi 25 kwaajili ya kuendelea kusikilizwa.

Wakati huo huo, Kesi ya Mauji nayomkabili Mfanyabashara Maarufu Papa MSOFFE imearishwa tena mahakamani hapo baada ya Wakili wa serikali Leonard  Chalo Kudai Kuwa jarada la Kesi hiyo bado lipo kwa MKURUGENZI wa Mashitaka na Hakimu Hellen Liwa akaiairisha hadi Machi 25 Mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutaka.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 12 Mwaka 2014

MARANDA MGONJWA KALAZWA MOI


Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,Jana ilishindwa kuendelea kusikiliza utetezi wa Kesi ya wizi wa sh.milioni 400 Katika Akaunti ya Madeni ya Nje Katika Benki Kuu , inayomkabili Kada wa CCM, Rajabu Maranda na wenzake kwasababu Maranda ni mgonjwa na Amelazwa Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Eva Nkya, mshitakiwa Farijala Hussein  aliomba Mahakama Kesi hiyo Kuwa Kesi hiyo Jana ilikuwa KWAAJILi ya washitakiwa KUJITETEA lakini anaomba wasijitetee kwasababu mshitakiwa mmoja(Maranda) ambaye ni mfungwa Katika GEREZA Ukonga HIvi sasa Amelazwa Katika Hospitali ya Muhimbili kwaajili ya matibabu.
Ombi Hilo lilikubaliwa na Hakimu Nkya na akaairisha Kesi hiyo hadi MACHI 10  Mwaka huu.

Maranda na Farijala hadi sasa wameishahukumiwa Katika Kesi Tatu tofauti za EPA na WANAISHI gerezani huku Kesi zao nyingine zikiendelee mahakamani hapo.

Katika Hatua nyingine Mahakama hiyo Imeiatisha Kesi ya matumizi Mabaya ya madaraka inayomkabili ALIYEKUWA MKURUGENZI wa TBS, EKEREGE hadi Aproli 8 Mwaka huu.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima Machi 7 Mwaka 2014