VIGOGO SUMA JKT WAIGALAGAZA SERIKALI



HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana Imemwachiria Huru  Mkurugenzi  wa Shirika Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) Kanali Ayoub Mwakang’ata na maofisa wenzake sita wa jeshi Hilo waliokuwa wakikabiliwa na makosa Saba  ya matumizi mabaya ya madaraka.

Mbali  na Kanali Mwakang’ta washitakiwa wengine ni Kanali   Mkohi Kichogo,Luteni Kanali Paul Mayavi,Meja Peter Lushika, Sajenti John lazier,Meja Yohana Nyichi na Mkurugenzi wa Miradi ya Matrekta wa SUMA JKT- Kanali Felex Samilani.

Hukumu hiyo ya Kesi ya jinai Namba  163/2012  ilitolewa Jana asubuhi na Hakimu Mkazi Alocye Katemana ambaye Alisema alipata fursa ya kusikiliza Kesi hiyo tangu ilipofunguliwa,Wama. 2012 na hadi Jana Imefikia Tamati .

Hakimu Katemana Alisema ili kuthibitisha Kesi hiyo upande wa Jamhuri uliokuwa ukiwakilishwa na Wakili wa Taasisi ya Kuzia na Kupambanana Rushwa, Lizy  Kiwia  ulipata jumla ya mashahidi 10 na vielelezo 25 na upande wa utetezi ulileta jumla ya mashahidi Tisa na vielelezo vitano.

Hakimu Katemana alidai KWA washitakiwa wanakabiliwa na makosa ya matumizi Mabaya ya madaraka  yanayoangukia Katika Kifungu Cha 31 na 32 Cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana Na Rushwa ya Mwaka 2007 , Mahakama hiyo imejiuliza Kuwa ni kweli washitakiwa Hao walinufaina binafsi na makosa w aliyoyatenda? , Je mshitakiwa wa pili (Kichogo) na wasaba  (Samilani) walikuwa hawana madaraka ya kusaini  uamishwaji wa Fedha toka Akaunti ya Tacopa kwenda Suma JKT?, Je washitakiwa ambao ni wajumbe wa Bodi ya Tenda ya Suma JKT walikuwa hawana mamlaka ya kuidhinisha ununuzi wa vifaa Vya ujenzi? je washitakiwa hao walinufaika binafsi au watu wao wakaribu walinufaika kutokana na makosa wanaodaiwa kuyatenda?

Alisema upande wa jamhuri  umeshindwa kuleta  ushahidi unaonyesha mshitakiwa wa pili (kichogo)na Saba (Samilani) ambao  walikuwa watendaji wa TAcopa na ndiyo Waliokuwa wamepewa DHAMANA  na Tacopa ya kuidhinisha Fedha zitoke kutoka Katika Akaunti ya Tacopa Na.011103031763  kwenda Akaunti ya Suma JKT 011103017094 , hawakwa na maelekezo ya kifanya hivyo toka Bodi Suma Jkt na hawakuwa na madaraka hayo na wala siyo watendaji wa Tacopa na kwamba KWA kitendo hicho walijinufaisha binafsi au watu wenye uhusiano nao kwasababu hiyo Mahakama hiyo inawafutia kosa la Tatu, NNE, tano, Sita na Saba.

Kuhusu mshitakiwa wa kwanza, watatu, nne, tano, Sita ambao ni wajumbe wa Bodi ya SUMA JKT Kuwa  Machi 5 mwaka 2009 katika chumba cha mikutano cha ofisi ya SUMA JKT Dar es salaam,wakiwa ni wajumbe wa bodi na Bodi ya Tenda ya SUMA JKT kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kutoa maamuzi ya bodi hiyo ambayo yaliyoonyesha yametolewa na TAKOPA kwa madhumuni ya kununua magari na vifaa vya ujenzi bila kupata idhini ya kutoka Bodi ya ya Wakurugenzi ya TAKOPA.

' Hata makosa hayo pia yanayowahusu washitakiwa Hao wajumbe wa Bodi ya Suma JKT , upande wa jamhuri umeshindwa ya kuthibitisha Kuwa , je wajumbe Hao walikuwa hawana mamlaka ya kufanya hayo?Je walinufaika na maamuzi hayo binafsi? " Alisema Katemana.

Aidha Alisema KWA mujibu wa vielelezo ushahidi uliotolewa mahakamani unaonyesha washitakiwa kweli walikuwa wajumbe wa Bodi ya Tenda ya Suma JkT na kweli walikuwa vikao halali na waliidhinisha ununuzi wa vifaa hivyo wakifanya vitendo hivyo KWA kukidhi matakwa ya Sheria na siyo kuvunja Sheria Kama upande wa jamhuri ulivyodai.

Kuhusu kosa la Saba lilokuwa linawakabili washitakiwa wote   AMBAlo ni la kula Njama kinyume na Kifungu Cha 32 Cha Sheria ya TAKUKURU ya mwama2007 AMBAPO Kati ya Machi na MEI 2009 washitakiwa wakiwa wajumbe wa Tenda Bodi ya SUMA JKT, walikula Njama ya kuamisha mradi kutoka Akaunti ya Tacopa Kuja Akaunti ya suma JKT ambazo Akaunti hizo zipo Kwenye Benki ya NBC tawi la Corporate bila kufuata matakwa ya Kifungu Cha 156 Cha Sheria ya Fedha za Umma ya Kanuni zake ya Mwaka 2011 nalo limeshindwa kuthibitishwa.

" Kwa Kuwa kosa la Sita kimeshindwa kuthibitisha ni wazi kabisa kosa la Saba AMBAlo ni la kula Njama limeshindwa kuthibitika kwasababu hiyo Mahakama hii inawaachiria washitakiwa wote Katika jumla ya makosa yote Saba yanayowakabili na kuanzia sasa wapo Huru na upande ambao haujaridhika unaweza kukata RUFAA"-Alisema Hakimu Huyo na kusababisha ndugu na Jamaa kupiga makofi ya Furaha Hali iliyosababisha Hakimu awakataze ndugu na kwamba kitendo hicho ni kinyume na Sheria ya nchi.

MAKAMANDA Hao ambao waliosoma kuzungumzia hukumu hiyo, walionekana Kuwa na nyuso za Furaha na kukumbatia na ndugu na Jamaa na familia zao walifika mahakamani Hao kufuatilia hukumu hiyo.Hata hivyo wakati Hakimu Katemana Akita hukumu hiyo Wakili wa Takukuri Kiwia alikuwa akitikisa kichwa.
'
Mwaka 2012 Kesi hiyo ilipofunguliwa mahakamani hapo na kusababisha taharuki kubwa Katika Jamii , Wakili wa Serikali , Kessy alidai kosa la pili pia ni la matumuzi mabaya ya madaraka ambalo linawakabiliwa washitakiwa wote kuwa Machi 12 mwaka 2012 ,washitakiwa hao wakiwa ni wajumbe wa bodi ya Tenda ya SUMA JKT walitumia madaraka yao vibaya kwa kupitishia maazimio ya kununuliwa kwa magari na vifaa vya ujenzi ambavyo vilikuwa vimeishatumika kinyume na kifungu cha 58( 3) cha Sheria ya Mamunuzi ya Umma ya mwaka 2005.

Aidha alidai shitaka la tatu ni la matumizi mabaya ya madaraka linalomkabili mshitakiwa wa pili na wa saba( Kichogo, Samillan) ambapo Machi 16 mwaka 2009 wakiwa wajumbe wa bodi ya Tenda ya SUMA JKT waliamisha Sh 2,744,432,545 kupitia hundi Na.000010 kutoka akaunti ya TAKOPA Na.011103031753 kwa SUMA JKT akaunti Na.01110307094 ambazo akaunti hizo zote zipo katika katika Benki ya Taifa ya Biashara(NBC) bila kufuata matakwa ya kifungu cha 156 cha Sheria ya Fedha ya Umma na Kanuni zake ya mwaka 2001.

Shitaka la nne alidai linawakabili washitakiwa hao wawili yaani mshitakiwa wa pili na watatu ambalo pia ni la matumuzi mabaya ya madaraka ambalo walilitenda Aprili 3 mwaka 2009,wakiwa wajumbe wa bodi hiyo ambapo waliamisha sh 489,677,879.30 kupitia hundi Na.000011 kutoka TAKOPA akaunti Na.011103031763 kwa akaunti Na. 011103017094 ya SUMA JKT ambazo zote zipo kwenye benki ya NBC bila kufuata kanuni na matakwa ya kifungu cha 156 cha Sheria ya Fedha za Umma.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Aprili 24 Mwaka 2014

NAENDELEA KUMLILIA DITOPILE MZUZURI 2014



NAENDELEA KUMLILIA DITOPILE MZUZURI-2014
Na Happiness Katabazi

Pichani ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Marehemu Ditopile Ukiwaona Mzuzuri, ambaye Leo  April 20 mwaka 2014anatimiza miaka Sita,tangu afariki dunia Aprili 20 mwaka 2008 mkoani Morogoro.

Binafsi mimi Happiness Katabazi nitaendelea kumlilia na kumuombea kwa mungu aiweke roho yake mahala pema peponi.Sisi tulikupenda lakini mungu amekupenda zaidi.

Tujikumbushe makala iliyochapishwa na Gazeti la Tanzania Daima , Aprili 22 Mwaka 2008 iliyokuwa na kichwa Cha Habari kisemacho ".   NAMLILIA DITOPILE" na Mwandishi Happiness Katabazi 

ILIKUWA Aprili 20 Mwaka 2008,  saa 4:39, asubuhi, nikiwa nimeketi sebuleni na kunywa chai nyumbani kwetu Sinza ‘C’, nilipokea simu kutoka kwa mfanyakazi mwenzangu ambaye ni mchora katuni aitwaye, Said Michael ‘Wakudata’ akiniambia rafiki yako, Brother, amefariki dunia. 

 Nilishtuka na  ghafla mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio huku mikono ikitetemeka na kusababisha simu yangu ya kiganjani kuanguka kwenye zulia. Kwakuwa hapo sebuleni nilikuwa nimekaa na mama yangu mzazi na kaka zangu, mama yangu alishtuka, akanikaribia na kuniuliza kulikoni? Ndipo nilipomweleza kwamba nimepokea simu inayosema rafiki yangu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (60) amefariki dunia. Kwakuwa mama yangu naye alikuwa akimfahamu Ditopile, alishikwa butwaa. Kwakuwa siku hizi taarifa za kuzushiana vifo zimekuwa za kawaida ndani ya taifa hili.

 kuziamini moja kwa moja taarifa hizo, niliamua kuokota chini ile simu yangu na kuanza kupiga kupitia namba zake (Ditopile) zote nne, ambazo nilizitumia kuwasiliana naye mara kwa mara. Nilipokuwa napiga simu kwenye line zote hizo, line zote zilikuwa hazipatikani. Ndipo nilipochukua uamuzi wa kumpigia simu aliyekuwa Katibu Mkuu wa timu ya Ashanti, Arafat Said, kwa kuwa marehemu alikuwa ni mlezi wa timu hiyo, kumuuliza kuhusu tukio hilo, naye alinithibitishia ni kweli. Nikabaki nimejiinamia kwa simanzi kutwa nzima na kuishia kumwombea kwa Mungu. 

Mara ya mwisho kuwasiliana na Ditopile ilikuwa ni Ijumaa saa mbili usiku ya wiki iliyopita. Alinipigia akaanza kwa kunitania kwamba muda si mrefu nitakuwa mkwe wake kwa mtoto wake wa kiume aitwaye Ramadhani, ambaye yupo masomoni Uingereza. Nikamjibu kwa kumtania kwamba sitakuwa tayari kuwa na baba mkwe ambaye ni chakaramu kama yeye, akajibu kwamba hiyo ndiyo tabia yake tangu mdogo, hivyo hawezi kuibadili ukubwani na kwamba yeye ataongoza msafara wa wazee wa Pwani kwenda kwa mzee Katabazi kumchumbia paparazzi (yaani mimi), ili familia yake iwe na mwandishi wa habari, kwani waandishi wa habari ambao enzi za uhai wake alipenda kuwaita paparazzi, walimuandika sana kwa mabaya yake na mazuri yake. Baada ya kunieleza hayo, nilimweleza kwamba kuna mtoto wako aitwaye Ramadhani Mzuzuri, mapema wiki iliyopita alitembelea blog yangu na kuniachia ujumbe wa kupongeza kazi zangu, nami nilimuliza Ramadhani kwakutumia e- mail kwamba Ditopile ni baba yake na kama ni baba yake basi mimi rafiki yake. 

Nilivyomweleza hivyo Ditopile, akaniambia hiyo ni sababu moja wapo iliyosababisha anipigie simu siku hiyo na akanieleza kweli yule ni mtoto wake.Baada ya kumaliza hadithi hiyo akaniomba nimsaidie kufahamu kesi yake imepangwa lini na kwa jaji yupi. Nilimwambia kuwa nipe sekunde chache nitoe kitabu changu cha kumbukumbu ili niweze kukutajia tarehe, nikamweleza kwamba kesi yake itatajwa kwa mara ya kwanza Aprili 24 mwaka huu, mbele ya Jaji Njegafibili Mwaikugile. Alishukuru na kuniambia: “Eh siku hiyo mapaparazzi wenzio wamejiandaaje kuja kunipiga picha?” 

Nilimjibu huku tupo timamu na kwamba siku hiyo tutahakikisha tunazingira pembe zote za Mahakama Kuu bila yeye kujua ili kuhakikisha tunaipata sura yake.Akacheka sana, akasema mapaparazzi mna taabu kweli. Namlilia rafiki yangu Ditopile kwani tangu atoke jela nimekuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara kwa simu. Ila mara ya mwisho kuonana naye ana kwa ana na kuzungumza naye kwa takriban saa mbili ilikuwa ni Desemba 9, 2006 ndani ya Gereza la Keko alipokuwa amewekwa rumande.

 Kama inavyofahamika, waandishi wa habari huwa hawaruhusiwi kuingia magerezani, lakini mzee Ditopile alimtuma mtu anipigie simu niende kumuona gerezani, ila nikifika pale gerezani nijitambulishe kwa jina bandia la Koku Katabazi, nimetokea mkoani Kagera na kwamba nivalie mavazi ya gauni kubwa na kitambaa kichwani ili maofisa magereza wa gereza hilo wasinitambue. Kweli nilifanya hivyo na kabla ya kufikia sehemu ya kujiandikisha kwenye daftari la wageni, nilinunua maji chupa makubwa na mkate na tayari kusubiri niitwe jina la kuingia kumuona Ditopile. Nilivyoitwa jina hilo, nilishtukia nadakwa kiaina na ndugu na jamaa wa mzee Ditopile na wakanieleza nisiwe na wasiwasi watanipeleka gerezani anapolazwa.

 Kweli ilipofika zamu yangu, niliingizwa ndani ya gereza huku nikiambatana na ndugu yake mmoja ambaye ni mtu mzima kiumri, nikapandishwa sehemu ya kuzungumzia wageni ambapo ni hatua tano kutoka chumba alichokuwa akilala yeye na wenzake maarufu kwa jina la ‘Sick Bay’. Baada ya kufika na kuketi kwenye kiti, Ditopile alitoka chumbani akaja kuzungumza nami, nilishindwa kujizuia nilibubujikwa machozi. Akaniita jina langu akisema na ujanja wako wote unalia? Nilimjibu kuwa jela si kuzuri, hasa anapopelekwa mtu unayemfahamu. Akanijibu kwamba yote ni mipango ya Mungu na tumuachie Mungu.

 Nilianza kumuuliza maswali ya hapa na pale kwamba ni kweli alikuwa amemuua yule dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), alisema ni kweli Novemba 4 mwaka 2006, alimuua kwa kumpiga risasi, ila hakuwa amekusudia kufanya tukio hilo, kwani dereva wa daladala aliligonga gari lake na alipowaambia kwanini waliligonga, dereva huyo alimtukana kwa kumuonyesha ishara ya kidole cha katikati. “Happiness, kwakweli kwa utu uzima niliokuwa nao, wadhifa niliokuwa nao kweli mtu dereva alinigonga na nilipomhoji alinitusi kwa kutumia kidole cha katikati ya mkono wa kulia…kwakweli niligadhabika sana nikajikuta nachomoa silaha na kumfyatulia, licha ya kwamba halikuwa lengo langu.

 “Siwezi kukana kwamba sikumuua yule dereva, ila nilimfyatulia risasi kutokana na hayo aliyonifanyia, ila naomba Mungu na ninaendelea kumuomba Mungu anisameheme, kwani hata vitabu vya Mungu vinakataza binadamu kutoana roho…hivyo tuiachie mahakama ndiyo itaamua,” alisema Ditopile. Baada ya kumaliza mazungumzo yetu siku hiyo ambayo taifa likikuwa likisherehekea uhuru wake, nilimuaga kwamba nakwenda, akanisii nisimtupe kwa sababu yupo jela, niwe napita kumjulia hali na kumpatia taarifa mbalimbali, nikamkubalia. Baada ya kuondoka gerezani hapo, kilichofuata, alikuwa akiletwa kwa nyakati tofauti katika Mahakama ya Kisutu na hatimaye Mahakama Kuu ambapo ndipo kituo changu cha kufanyia kazi. Machi 9, mwaka jana, viwanja vya Mahakama Kuu viligeuka kuwa uwanja wa mapambano kabla na baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, kufikishwa mahakamani hapo na kutolewa kwa dhamana. Mapambano hayo yalifanywa na watu wanaosadikiwa kuwa ni ndugu wa mshitakiwa Ditopile dhidi ya waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia mwenendo wake. Nami nilikuwa mmoja wao. Machi 10, 2007 ambayo ilikuwa siku ya Jumamosi asububi, nikiwa na Mwadhiri Mwandamizi wa Sheria na Katiba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, nilipokea simu ikisema: 

“Sura yangu mnaitakia nini au mmetumwa na waganga wenu muichukue mkaniroge?” Nikamuuliza aliyenipigia alikuwa nani, akanijibu kuwa: “ Ni mimi mzee wako Ditopile.” Nilicheka. Nikacheka sana, ila nikamweleza wazi kabisa kwamba sikufurahishwa na vurugu zilizofanywa na ndugu zake, kwani zilikuwa zikizuia waandishi wasifanye kazi yao, pia lionyesha kuwa familia yake ina watu wa namna gani. Akasema tumsamehe, na nilipomhoji ni kwanini anavaa kofia kubwa ‘pama’, alisema anaivaa kwa makusudi ili wapiga picha wasiipate sura yake kwa urahisi. Akaniambia kuwa: “Wewe ni mwandishi gani umeingia gerezani kuniona ukashindwa kupiga picha mazingira ya Gereza la Keko?

” Nikamjibu kuwa nisingeruhusiwa. Akaniambia pamoja na sheria kukataza yeye alitumia mbinu zake za kijeshi na alifanikiwa kupiga picha mazingira ya gereza hilo na jinsi mahabusu wanavyolala na wala hajawahi kukamatwa na askari magereza na picha hizo amezihifadhi nyumbani kwake. Kwa wale wanaomfahamu marehemu, lazima watakubaliana nami kwamba Ditopile alikuwa ni mtoto wa mjini, mwenye kupenda masihara na mzaa, muwazi na mwongeaji kupita kiasi, na mara nyingi nilipokuwa nikionana naye au kuzungumza naye alikuwa akiniasa nipende kusali, kuishi vizuri na watu na alinisisitiza nijiendeleze kielimu, kwani elimu ndiyo mkombozi katika ulimwengu wa sasa. Pia aliniasa kufanya kazi kwa bidii na kwamba ujumbe huo niusambaze hata kwa vijana wenzagu.

Aliniambia kuwa wakati akisoma Chuo Kikuu wakati wa likizo alikuwa na ubao wa kuuza mboga na matunda katika Soko la Ilala, hivyo alikuwa akifanya biashara hiyo. Pia aliwahi kuuza magazeti ya Daily News katika mitaa ya Masaki na Oysterbay. Na alisema kazi hizo zilikuwa zinamsaidia kuongeza kipato. Baada ya kuniambia kwamba aliwai kufanya kazi hizo, nilimwangalia usoni nikajikuta naangua kicheo kwa sauti ndani ya ofisi yake ya mkuu wa Mkoa wa Pwani. 

Akauliza: “Unacheka hizo kazi?” Akaniambia mwanangu hadi leo hii mnatuaona tunateuliwa kushika nyadhifa mbalimbali, mkae mkijua tumetoka mbali.” Hatukuishia hapo, tuliendelea kuwasiliana kwa simu na hata Januari 6 mwaka huu, baada ya yeye kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba waandishi wa habari, Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage, wamemwagiwa tindikali, alinipigia simu akasema yupo mkoani Lindi, akasema amesikitishwa na tukio hilo na kwakuwa haishi utani aliniambia wakati umefika sasa mapaparazzi tuanze kuvaa ‘pama’ kama yeye ili watakapotumwagia tindikali isituingie machoni. “Mapaparazzi anzeni kuvaa pama kama mimi ili mkimwagiwa tindikali isiwaingie machoni au wasilianeni na mimi niwaonyeshe duka niliponunua pama langu,” alisema. 

Niliishia kucheka. Ndugu msomaji mapema mwaka huu, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kwamba Ditopile alikuwa akiuza asali, na kweli hadi anafariki dunia alikuwa akifanya biashara hiyo, ambayo aliwahi kunieleza kwamba inamuingizia kipato kizuri. 

Baada ya taarifa hizo kutangazwa, alinipigia simu akiniambia kwamba: “Waandishi hamna dogo, mimi kuuza asali imekuwa nongwa?” Akaniambia mbona Mwenyekiti wenu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Reginald Mengi, anauza soda za Coca Cola amuandiki? Mbona bosi wako Freeman Mbowe anauza pombe kwenye ukumbi wake wa Billicanas auandiki? Nilishindwa kumjibu kwani nilicheka sana, akaniambia usicheke. Katika viongozi wa CCM hakika naweza kusema kiongozi ambaye nilikuwa naye karibu kikazi na aliyekuwa akinipa ushauri mbalimbali alikuwa ni Ditopile, alinichukulia kama mwanawe, hakika Ditopile nakulilia. 

Hakuwa na majivuno kama walivyo viongozi wengine, hata wakati alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani nilipokuwa nikipata nafasi, nilikuwa nikipita kumsalimia ofisini kwake. Ni Ditopile huyu huyu, siku moja kabla ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika utawala wa Awamu ya Tatu, Jakaya Kikwete, kwenda kujitangaza rasmi kugombea urais katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Pwani, Kibaha, alinipigia simu saa tatu usiku akiniambia: “Wewe si unataka ‘scoop’” (habari moto), akaniambia kesho saa mbili asubuhi panda gari kisha shuka stendi ya mabasi Kibaha. Nilipomuuliza kuna habari gani mbona hataki kuniambia, akaniambia Nimwamini yeye na kwamba kesho yake nifike bila kukosa.

 Kwakuwa nilikuwa nikimuamini na kumheshimu, kesho yake ambayo ilikuwa ni siku ya Jumapili, nilifanya hivyo nikapanda gari la kwenda Kibaha pale Ubungo, na kabla ya gari kuondoka Ubungo, alinipigia simu akiniuliza nilikuwa nimefika wapi, nikamweleza ndiyo tunaondoka Ubungo, akasema sawa.

 Lile gari lilipofika stendi ya Kibaha, ghafla nilipokea simu nyingine kutoka kwake akiniuliza nilikuwa nimefika wapi, nikamwambia nimefika stendi ya Kibaha, ilikuwa saa 3 asubuhi. Akaniambia nikodishe teksi nimwambie dereva anipeleke CCM Mkoa wa Pwani, nilifanya hivyo. Nilipoanza kuingia ile njia ya vumbi kuelekea kwenye ofisi hizo, nikaona kumepambwa bendera za CCM. 

Nikamuuliza yule dereva kulikoni? Akaniambia kuwa hata yeye alikuwa anashangaa. Nilipofika kwenye ofisi hizo za CCM saa nne asubuhi nikakuta wafuasi na viongozi wa CCM wametanda huku viti vikiwa vimepangwa na nikabahatika kumkuta mpiga picha wa TvT, sasa TBC, Chris, nikamuuliza kulikoni? 
Akaniambia Kikwete siku hiyo anakuja kujitangaza rasmi kwamba atagombea urais. 

Aidha, baada ya dakika chache, Ditopile akaniambia: “Umekwishafika?” Nikamjibu, ndiyo. Akasema: “Eh umekuta nini au umesikia nini?” nikamwambia nimeambiwa kwamba muda mfupi ujao Kikwete atatangaza rasmi azima yake ya kugombea urais, akasema ni kweli na akaniambia hiyo ndiyo ‘surprise’ yake kwangu na kamwe sitakuja kumsahau kwani tukio lile lilikuwa ni la kihistoria. Ni kweli sitamsahau. Wana CCM walitutangazia kwamba Kikwete angefika pale saa tano kujitangaza lakini alifika saa saba na nusu mchana.

 Na ilipofika saa sita Ditopile na alinitafuta na kunitambulisha kwa mkewe aitwaye Tabia, kasha tulisalimiana. Nakumbuka enzi za uwahi wake aliwahi kuniambia kwamba alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari akawa anasema anafuata masharti yote ya daktari. Na alikuwa aishi utani, nakumbuka kuna siku nikiwa ofisini kwake Pwani nilimkuta anakunywa chai na mkate wa kumimina nikamuuliza kulikoni na mikate ya kumimina asubuhi, akasema ni miongoni mwa kitafunio anachokipenda. Nasema tukio hili sitalisahau kwakuwa lilihudhuriwa na wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam na walianza kufika eneo hilo saa tano hadi saa saba. 

Baadhi ya wahariri walionikuta hapo walishikwa butwaa na kuniambia wewe umepataje taarifa hizo, nikawaambia kwa njia zangu hasa ukizingatia kipindi hicho nilikuwa bado mwandishi mchanga sana na hata nilivyoandika habari ya tukio lile nakumbuka habari ile nilinyimwa ‘by line’ na mhariri wangu bila sababu za msingi. Nakulilia Ditopile ambaye haupo tena nasi duniani, ila mazuri uliyoachia tutayafuata na kuyatekeleza kwa vitendo.

Hata hivyo Ditopile kama walivyo binadamu wengine alikuwa na upungufu na udhaifu na mabaya yake, hatutayafuata. Mwanasiasa wa siku nyingi Ditopile amefikwa na mauti Jumapili iliyopita. Alifikwa na mauti katika Hoteli ya Hilux ya mjini Morogoro. Nimemfahamu Ditopile kwa miaka sita sasa na hadi sasa kuna baadhi ya watu ukiwaeleza kwamba Ditopile ana elimu ya chuo kikuu wanakukatalia kutokana mzaha wake.

 Ditolipe ndiye mwasisi wa msemo wa ‘halo halo’. Ambaye amekuwa akisema yeye si mtu wa kuja, bali yeye ni mzaliwa wa jiji hili na amezaliwa wodi ya ‘Makuti’ enzi hizo ilikuwa ndani ya Hospitali ya sasa Taifa ya Muhimbili. Ditopile aliitimu shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1973, aliajiriwa na Chama cha TANU kama Katibu Msaidizi, Makao Makuu.

 Na kutokana na utendaji wake mwaka 1980 alikwishafikia cheo cha Katibu Msaidizi Mkuu Daraja la Kwanza. Machi 1983, aliteuliwa kuwa Katibu wa Wilaya wa CCM katika wilaya za Serengerema na Tabora mjini. Nyota yake ilianza kung’ara, na mwaka 1982 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM .Mwaka 1996 hadi 1997, aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara. Ditopile alikuwa ni miongoni mwa vijana sita waliokuwa wameamua kujiunga na utumishi wa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) mara baada ya kuhitimu masomo ya chuo kikuu mwaka 1973. 

Baada ya kujiunga na utumishi wa TANU , Ditopile alijiunga na Chuo cha Itikadi na Propaganda Kivukoni, wakati ule kikiitwa Chuo cha Chama. Baada ya kumaliza mafunzo ya Itikadi na Propaganda, alirudi makao makuu ya chama, na hapo alipewa jukumu la kuanzisha maktaba ya CCM ambayo hadi leo ni ya chama tawala. Pia alikuwa ni mtumishi mwaminifu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Wakati wa utumishi wake alikwenda katika Chuo cha Maofisa Monduli, alikochukua mafunzo ya uafisa wa jeshi. 

Pamoja na nyadhifa hizo , Ditopile aliwai kuwa mbunge wa Jimbo la Ilala katika miaka ya 1980. Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Naibu Waziri wa Mawasiliano. Pia alipata kuwa mkuu wa Mkoa wa Pwani, Kigoma, Lindi, Dar es Salaam na Tabora. Ditopile alizaliwa Machi 7, mwaka 1948 katika Wilaya ya Ilala, mkoani Dar es Salaam. 

Alisoma  Shule ya Msingi Mchikichini, Dar es Salaam kati ya mwaka 1956 na 1959. Mwaka 1960 hadi 1963, alisoma Shule ya Kati Magomeni, Dar es Salaam. Kati ya mwaka 1964 hadi 1967, alisoma Shule ya Sekondari ya Aga Khan, ambayo kwa sasa inajulikana kama Tambaza. Mwaka 1968 hadi 1969, alihitimu Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Tanga. Julai 1970, alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1973. Lakini makala hii haita kamilika kama sitaandika kwamba marehemu Ditopile alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia ya Rais Kikwete. 

Na hakuna ubishi kwamba katika uhai wake marehemu alikuwa ni miongoni mwa watu waliopigana kufa na kupona ili Kikwete ateuliwe na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Na kweli hilo walifanikiwa. Lakini naweza kusema bahati haikuwa upande wake, kwani ndani ya miaka miwili na miezi minne, tangu kijana wake Kikwete ashike kiti cha urais, Ditopile alikumbwa na kesi ya kuua bila kukusudia, na kusababisha kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wa mkuu wa Mkoa.

 Pia katika kipindi hicho kifupi cha utawala wa kijana wake, Ditopile amekumbwa na mauti. Hivyo hakuweza kufaidi matunda ya utawala wa kijana wake. Ditopile anatarajiwa kuzikwa leo katika shamba lake lilipo Kinyerezi, Dar es Salaam. Ditopile sisi tulikupenda, lakini Bwana amekupenda zaidi. Mungu ailaze roho yako mahala pema peponi. Amina. Namlilia Ditopile. 

0716 774494 www.katabazihappy.blogspot.com 

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne.April 22,2008



Sent from my 

BUNGE LA KATIBA NI 'KOMEDI'?

BUNGE LA KATIBA NI " KOMEDI" 

Na Happiness Katabazi
HAKUNA Ubishi kuwa siku hizi ukitaka kucheka, kukereka na kupunguza msongo wa mawazo uliyonayo, ukitaka kujifunza maneno machafu mapya, huna budi kufungulia Televisheni ya Taifa (TBC1), na kuanza kuangalia mijadala ya Bunge la Katiba la Tanzania linavyoendeshwa na jinsi wajumbe wa bunge hilo wanavyochangia kwa kutumia lugha za matusi, zisizonastaa na zinazopolomosha heshima ya bunge hilo na jamii yetu ya Tanzania.

Na Baadhi wananchi wengine wamekuwa wakisema uenda kabla ya bunge hilo kuanza , baadhi ya wajumbe wanakunywa kwanza ‘viroba’ ndiyo wanaingia ndani ya bunge na kuanza kuchangia mjadala kwa kutoa lugha za kejeli, uzushi, kuzomea na kugonga meza ovyo.

Nimeyasema hayo kwasababu tayari baadhi ya wananchi wameisha lipachika bunge la Katiba kuwa ni ‘Komedi’. Kwa wajumbe wa bunge hilo ambao ni watu wazima wenye umri wa zaidi ya miaka 18 , baadhi yao wameshindwa kujiheshimu na kuchunga kauli zao wakati wakichangia mjadala wa mchakato wa kupata Katiba Mpya

Kila kukicha tumesikia wabunge hao wengine wakiwa na umri mdogo wamekuwa wakiwatolea maneno ya ‘shombo’ wajumbe wenzao ambao wamewazidi umri kwa kisingizio kuwa wajumbe hao wenye umri unaowazidi na kuwapita hata wazazi hao wamekuwa wakilidanganya bunge, na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo ambao wanaumri mkubwa nao wamekuwa wakiwatolea maneno yasiyofahaa wajumbe wenzao wenye umri mdogo wachangiapo mjadala huo.

Mila na tamaduni zetu ni mkubwa anamheshimu mdogo na mdogo anamheshimu mkubwa lakini kupitia bunge letu la Katib a’Komedi’, niwazi wajumbe wa bunge hilo wanauzika utamaduni huo na kufanya sasa jamii ya watanzania waanze kuishi kwa kutumia utawawa Kambare kwani baba,mama ,mtoto wa kambare wote wanandevu hakuna wa kumbabaisha mwenzie.

Nia ya Rais Jakaya Kikwete ya kutaka Tanzania iandike Katiba mpya ni njema, ila sasa tunashuhudia baadhi ya wajumbe wa bunge hilo hawataki nia hiyo ikamilike kwa kila siku kuibua mapingamizi na hoja zisizokuwa na kichwa wa miguu hali inayosababisha hivi sasa  heshima ya bunge hilo kuporomoka na kuona ni kheri tubakie na Katiba ya zamani ya mwaka 1977 licha ina mapungufu yake kuliko kuletewa Katiba mpya ambayo inaendelea kuandikwa na baadhi ya wajumbe waliokosa adabu, wanatumia lugha za matusi, uzushi kwa kisingizio kuwa eti wanataka serikali mbili wengine wanataka serikali tatu.

Kwa wale tuliopata kuisoma rasimu ya pili ya Katiba, mtakubaliana na mimi rasimu hiyo imeandikwa vitu vingi sana siyo Muungo wa Serikali mbili, Serikali tatu, wala hati ya Muungano pekee.Imeandikwa vitu vingi lakini hatuoni kama baadhi ya wajumbe wanajipa muda wa kuisoma rasmi hiyo yote na kufahamu kilichoandikwa.

Leo hii baadhi ya wajumbe wanaibuka wanasema hati za Muungano mara zimegushiwa, mara hazipo kwa sababu hiyo hakuna muungano.Na mbaya zaidi wanaongea uzushi ndani ya bunge hilo hawatoi vielelezo.Tuwaulize wajumbe wa aina hii hivi siku hati za Muungano zilivyokuwa zinatengenezwa na waliozitengeneza na zikasainiwa na Marehemu Baba wa Taifa Julias Nyerere na Rais wa Zanzibar, Abeid Aman Karume walikuwepo?

Mapema wiki hii  Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alifanya mkutano wake na waandishi wa habari na kuwaonyesha hati za Muungano na kusema hati hiyo ni halisi na kwamba Rais Jakaya Kikwete amesikitishwa na uzushi huo kwamba hati hazipo, na lugha za kejeli na matusi.

Minashangaa sana huyo Balozi Sefue anavyosema Rais Kikwete eti amesikitishwa na vitendo hivyo.

Naye Rais Kikwete amenukuliwa juzi akisema kuwa anakerwa na lugha za kejeli , matusi nakuwakejeri waasisi wa taifa hili.

Ni najiuliza Kwa hiyo rais Kikwete akishasikitika ndiyo hao wajumbe wazushi, wanaotoa lugha za kejeli ndiyo wataacha tabia hiyo ambalo linaporomosha heshima ya bunge hilo mbele ya jamii?

Kwa hiyo Rais Kikwete akisikitishwa na lugha hiyo za kejeli zinazotolewa na Hao  baadhi ya wabunge la Katiba, ambao watu tunaofikiri sawa sawa HIvi sasa kutokana na vitendo Vya kishenzi na kijani  vinavyofanywa  ndani ya Bunge na Hao wajumbe  HIvi huo mchakato wa kuwapata wajumbe wale ulifanywa na watu wenye akili timamu  au wahuni tu?

Maana aingii akilini kabisa kuna baadhi ya wajumbe ambao tangu serikali hii iingie madarakani Desemba 21 mwaka 2005 , wamekuwa wakipinga kila kinachofanywa na serikali hii kiwe kizuri au kibaya na wazushi wakubwa, lakini cha ajabu Rais Kikwete akawateua baadhi ya wanasiasa hao sijui akidhani kwa kuwateua ndio atawafurahisha na wataacha kuzua uongo?

Matokeo yake wajumbe hao wenye tabia hiyo baada ya kufika ndani ya bunge hilo ndiyo kwanza wameendelea na tabia zao ya uzushi, kulazimisha mambo wanayoyataka wao tu na wanataka watu wote waamini yale wanayoyaamini wao na kuzua taftari ma maneno ya shombo ndani ya bunge jambo linalosababisha hivi sasa heshima ya bunge hilo kuanza kuporomoka kwasababu ya vitendo vya kiuni kufanywa na baadhi ya wajumbe ambao wengine ni wateuli wa rais Kikwete.

Wahenga waliwahi Kusema " Mtoto umleavyo ndivyo akuwavyo". Msemo huu umethibitika kwamba Katika Utawala wa serikali awamu ya nne imekuwa ikiwa lea na wakiwa kukumbatia baadhi ya wanasiasa na wanaharakati ambao wamekuwa wakitoa maoni Yao kupitia vyombo Vya Habari, mikutano ya adharani kuzulia uongo na kuwachafua mahasimu wao kisiasa, vyama Vya siasa na wakati mwingine serikali.

Sasa tabia hiyo chafu ya kuzua maneno ya uongo ndiyo Imefikia mahali sasa wajumbe wa Bunge la Katiba kufikia Hatua ya Kusema Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mara imegushiwa Mara haipo wakati ipo.

Kwa hiyo tabia hii Chafu iliyoota mizizi sasa Kwenye vinywa na Fikra Kwa baadhi ya wanasiasa wetu uchwara ya uzishi, upotoshaji kwa kiasi kubwa nadiriki Kusema imelelewa na kukumbatia sana na Utawala wa serikali awamu ya NNE ambayo Katika Utawala awamu ya NNE ndiyo wanasiasa Wengi uchwara hapa nchini ndiyo wamekuwa walitumia mbinu hiyo ya uzishi na uongo Katika hotuba zao kuwadanganya wananchi Katika Mashaka mbalimbali.

Na uthibitisho wa hili ni kitendo Cha baadhi ya wajumbe wa Bunge Hilo kusimama ndani ya Bunge Kusema eti hati ya Muungano haipo , wengine imegushiwa Kumbe hati hiyo ipo.

Mbona serikali hii imeishawahi kuyafungia baadhi ya magazeti kwa kile ilichodai kuwa magazeti hayo yamekuwa yakiandika habari ambazo zinaleta uchochezi na uhasama katika jamii?.

 Kwanini baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kwa ushabiki wao wa kijinga tu wa kundi moja linataka serikali mbili jingine linataka serikali tatu lifikie sehemu ya kufanya vitendo vya kulidhalilisha bunge letu mbele ya walipa kodi?

Hata kama hati zilizotolewa na Balozi Sefue ni halisi au zimegushiwa hao walisema hati za muungano hazipo na zimeghushiwa  wanaweza kuzitambua? .Tukubaliane kimsingi si kila nyaraka ya serikali inatakiwa kuwekwa wazi.Nyaraka zingine hazistahili kuwekwa adharani.

Siku zote wananchi wataendelea kuzieheshimu na kuziogopa mahakama licha mahakama zetu nyingi hazina mazingira mazuri ya ofisi kwasababu mahakimu na majaji wanaoendesha kesi wanajiheshimu wawapo mahakamani wakiendesha kesi.Wakati kesi zikiendeshwa hutakuta mtu akipokea simu, wala kuchati wala kupigana picha na kisha picha kuweka kwenye simu wakati kesi zikiendelea.

Lakini hivi sasa tunashuhudia baadhi ya wajumbe wa bunge la Katiba wakati bunge hilo likiendelea wakitumia Ipad na simu zao kuchati na kupigana picha.Hivi tujiulize muda wa kufuatilia kwa makini hoja zinazotolewa na wajumbe wenzao wanaupata wapi?Maana muda wote wapo bize na simu?

Na nina mshangaa sana huyu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,Samuel Sitta ambaye ni msomi wa sheria anashindwa kupiga marufuku ufedhuli huu ambao nao  unaporomosha heshima ya bunge hilo ambalo hivi sasa huku mitaani limepewa jina la utani la ‘Komedi’.

Kwa uhuni huu unaofanywa na baadhi ya wajumbe wa bunge la Katiba wa kuibua hoja za uzushi, kejeli,matusi ambazo zimesababisha baadhi ya wajumbe hao wamekosa adabu wanaacha bila kuchukuliwa hatua, kunanifanya sasa nione ni kheri tuendelee kutumia Katiba ya zamani ya mwaka 1977 ambayo ni kweli ina mapungufu ambayo yanaweza kurekebishwa kuliko kuja kutumia hiyo Katiba mpya ambayo  inaendelea kutengenezwa na hawa baadhi wajumbe ambao wakati wanaitengeneza walikuwa wakitumia lugha chafu na uzushi.

Katiba Mpya sio itaji muhimu sana kama lilivyoitaji la serikali kutoa hela kununua madawa mengi kuweka mahospitalini, kujenga miundombinu,kutengeneza wodi za kuzaliwa wa kinamama, kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa UTI ambao hivi sasa umeanza kuwa tishio kubwa hapa nchini.

Kama kweli tunataka kutengeneza hiyo Katiba mpya, wale wajumbe wa bunge hilo ambao kisheria sisi tunasema wao siyo wa mwisho wa kutengeneza Katiba mpya ,wajiheshimu na watimize jukumu lao hilo kwa nidhamu bila kuvunja heshima ya bunge hilo na kupotosha jamii.

Ni ajabu sana wajumbe wa bunge la Katiba kutaka kuparurana kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya, wakati sisi tuliosoma somo la Katiba tumefundishwa kuna hatua kadhaa za kufikia kutengeneza Katiba mpya. Hatua ya kwanza ni Tume kukusanya maoni ya wananchi, tume kuyaweka kwenye maandishi maoni hayo(rasimu), Bunge la Katiba kuijadili rasimu husika kama bunge linavyofanya sasa, kisha yaliyojadiliwa na Bunge yapelekwe kwa  kwa wananchi wayapigie kura za ndio au hapana.

Sasa nyie wajumbe mnaotaka kuparulana kwa kisingizio cha kutaka serikali mbili, mara tatu make mkijua bunge siyo chombo cha mwisho ya kutengeneza Katiba mpya.

0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com
Aprili 19 Mwaka 2014.

UB YAWAASA WAHITIMU





Na Happiness Katabazi
CHUO KIkuu Cha Bagamoyo(UB) Dar es Salaam, kimewataka wahitimu walioitimu kozi ya utetezi wa Haki za binadamu na Haki za kijamii kutumia taaluma hiyo waliyoipata Katika nchi za Afrika Mashariki bila woga ili waweze Kuwatetea wananchi ambao Haki zao zinafunjwa na hawajui jinsi ya kuzidai.

 Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitivo Cha Sheria Cha Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Dk.Natujwa Mvungi juzi katika mahafali ya kuwakabidji jumla ya wahitimu 10 w yaliyofanyika Katika Ukumbi wa chuo hicho uliopo KAWE Beach Da es Salaam, AMBAPO Mafunzo hayo yalifadhiliwa na taasisi ya Akiba Uhaki  Foundation ya nchini Kenya.

Dk.Natujwa ambaye pia ni Mratibu wa kozi hiyo Alisema kozi hiyo Ulianza Septemba Mwaka Jana na kumalizika Machi mwaka huu, ambapo wahitimu Hao ambao ni raia  toka nchini za Afrika Mashariki  wakiwa fursa ya kafundishwa na Wanasheria toka vyuo mbalimbali jinsi ya kuwaza Kuwa watetezi wa Haki za binadamu kila kila nchi zao Kwani ni wazi kuna baadhi ya watu wanakunyana Haki za binadamu na wanaovunjiwa Haki hizo hawana uelewa wa jinsi kuzidai Haki hizo.

"UB imewafundisha jinsi ya kufahamu Haki za binadamu ni zipi?na wa jibu wa binadamu wa serikali na Jamii yake ni upo na Jinsi ya kuzidai Haki hizo....tu naimani mnavyorudi nchini kwenu Mtaenda kutumia elimu hii mliyoipata KWA vitendo ili wale ambao hawajafanikiwa Kuipata elimu hiyo waweze kunufaika na elimu mliyoipata" Alisema Dk. Natujwa.

Kwa upande wake Rais wa Chama Cha Tanganyika Law Society(TLS)" Charles Rwechungura, akipongeza UB, na Taasisi ya Akiba Uhaki KWA kuendesha Mafunzo hayo kutoka Kwa wahitimu Hao wanaogombea nchi za EAC Kwani licha ya swaps mwanga wahitimu Hao w kufahamu Haki za binadamu pia zimeimaimalisha mahusiano Mema haina a kataifisha hayo na kuwataka wahitimu Hao wakaitumie vyama elimu waliyoipata Katika Jamii zinazowazunguka.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Aprili 16 Mwaka 2014

WAHANDISI JWTZ WATUMIKE WAKATI WOTE



Na Happiness Katabazi

JUKUMU mojawapo la msingi la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa amani, ni kusaidia mamlaka za kiraia kulinda usalama wa wananchi na mali zao na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo kutoa misaada ya uokoaji wakati wa majanga na kukarabati miundombinu inapoharibika.

Katika kusaidia shughuli za kijamii, JWTZ kwa muda wote wa uhai wake, imeweza kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi mkubwa na kujizolea sifa nyingi  kutokana na mchango wake, hasa katika uokoaji na urejeshaji miundombinu ya barabara na madaraja wakati wa mafuriko na Majanga mengine.

Jukumu hilo limekuwa likifanywa na wanajeshi wote, wakiongozwa na wahandisi wa medani wa JWTZ wenye makao makuu yao eneo la Sangasanga -Ngerengere mkoani Morogoro, ambao wamebobea katika fani hiyo.

Wahandisi wa medani ndio watalaamu ambao wakati wa vita huwezesha vikosi kusonga mbele kwa kuonyesha njia, kwa kufanya doria na kuchagua sehemu nzuri ya kupitisha vikosi, zana na vifaa. Wao pia husafisha njia kwa kutegua mabomu, kujenga barabara, madaraja na viwanja vya ndege.

Kwa misingi hiyo basi, binafsi naona bado  kuna haja kwa taifa letu kuanzisha utaratibu wa kuwatumia wahandisi wa JWTZ wakati wa amani ili taifa liweze kupiga hatua ya maendeleo katika sekta ya miundombinu.

Jeshi letu hivi sasa lina hazina ya wataalam wa kila fani, lakini baadhi yao taaluma zao hawazitumii ipasavyo kutokana na serikali kutowapa fursa ya kutumia ujuzi wao wakati wa amani.

Tunaosoma Kwenye vyuo HIvi sasa   ni mashahidi Kwani Wanajeshi Wengi na wanausalama toka vyombo mbalimbali Vya dola wamejiandikisha vyuoni humo ili wajiendeleze kielimu Katika fani mbalimbali.

Sote ni mashaidi kwamba inapotekea maafa, wahandisi wa JWTZ wamekuwa wakisukumizwa kutengeneza barabara, kuokoa majeruhi nk., lakini hali hiyo ya pilikapilika hawaipati wakati wa amani.

Pamoja na kuwa na fani ya uhandisi, lakini wanajeshi wote wamefundishwa ukakamavu , nidhamu ya Hali ya juu na  kazi zao huzifanya ndani ya muda unaotakiwa na kwa uaminifu na uzalendo.

Ni barabara, madaraja mengi tunayashuhudia yamejengwa na raia wa kawaida, tena kwa gharama kubwa, yakiaribika mapema kwasababu yamejengwa chini ya kiwango na wakandarasi waliokosa vifaa na uzalendo. Pia yamekuwa  yakichukua muda mrefu kukamilika, na mara nyingine tunaambiwa serikali ndiyo imekuwa ikichelewesha fedha za kuwalipa makandarasi na wakati mwingine tunaambiwa makandarasi hao ni wazembe.

Hakika habari kama hizi hazipendezi kusikiwa maskioni mwa mwananchi yeyote mpenda maendeleo, kwani sote tunafahamu taifa lisilo na miundombinu ya uhakika ni wazi litakuwa linajirudisha nyuma kimaendeleo kwani shughuli za uzalishaji zitakwama kwa kuwa mazao au mawasiliano hayasafirishwi kwa wakati muafaka, hivyo kufanya pato la wananchi na taifa kwa ujumla kukosekana na bidhaa kukosekana sokoni.

Wakati  umefika kwa serikali ya awamu ya nne ambayo kwa bahati nzuri inaongozwa na Rais Jakaya Kikwete ambaye kabla ya kuingia kwenye ulingo wa siasa alikuwa ni ofisa wa jeshi hili,  ione jinsi ya kuwashirikisha wahandishi wa JWTZ  kwenye ujenzi wa miundombinu ya taifa hata wakati wa amani.

Kwani hivi sasa serikali inatumia fedha nyingi kuleta makandarasi toka nje ya nchi kwa ajili ya ujenzi wa barabara wakati jeshi lina wahandisi wengi tu wasiotumiwa ipasavyo. Endapo serikali itakubali kuwatumia wahandisi medani, ni wazi kwamba serikali itatumia fedha kidogo kwa ajili ya kulipa gharama za uhuduma hiyo.

Yawezekana wakawapo watakaosema kuwa jeshi halina vifaa vya kutosha vya kuweza kufanya shughuli hiyo, sawa, lakini hatuoni sababu ya JWTZ kutowezeshwa ili waweze kununua vifaa hivyo ambavyo vitakuwa ni mali yetu ya kudumu na tutakuwa tukivitumia muda wowote tunapovihitaji kuliko hali ilivyo hivi sasa ambako tunatoa tenda kwa wahandisi wa nje ambao huongeza gharama kwa kuingiza vifaa vya ujenzi na bado hujinufaisha kwa kuviuza mara wanapomaliza kazi zao.

Tujiulize kipi bora, kuendelea kuwatumia makandarasi toka nje ya nchi kwa gharama kubwa ambao wakimaliza kazi wanaondoka na vifaa vyao au taifa lijinyime na kununua vifaa vyake na kutumia wahandisi wake katika ujenzi wa miundombinu ya taifa letu?

Lengo langu si kupiga vita makandarasi wa nje ili wasipewe tenda, la hasha! Ila kwa kuwa serikali kila kukicha imekuwa ikidai  kuwa haina fedha za kutosha kutokana na bajeti ya taifa kuwa tegemezi kwa wafadhali, sasa kwanini hicho kidogo tulichonacho kisizunguke humu ndani ili wananchi na taasisi nyingine za serikali ziweze kufaidika nacho?

Naamini fedha za kununulia vifaa vya ujenzi wa miundombinu kote nchini tukiwa na nia ya dhati tunaweza kuzipata, kwani nchi yetu ina utajiri mwingi wa rasilimali, ambao tukiutumia vizuri, unaweza kutupatia haraka fedha hizo.

Nitoe pia changamoto kwa JWTZ , chini ya Mkuu wa Jeshi hilo , Jenerali Davis Mwamunyange kwamba, kama kweli nayo ina nia njema na taifa hili na inapenda kuona miundombinu ya taifa lao ikiimarika, pia nayo ina jukumu la kuiomba serikali iiwezeshe na kisha iwaruhusu kufanya kazi za kuboresha miundombinu wakati wa amani.

Huu ni wakati wa zama za maendeleo ya sayansi na teknolojia na hivyo vinapaswa kuikumbuka JWTZ  pia na njia mojawapo ya kulifanya liende sambamba na maendeleo hayo, ni kupanua wigo wa utendaji wake na ninafikiri njia mojawapo ni kwa kujishughulisha katika ujenzi wa taifa kwa kutumia wataalamu lililonao.

Hizi si zama za wanajeshi wetu kutembea na silaha wakati wote au kushinda messi wakinywa Pombe za JWTZ ambazo zinauzwa KWA bei rahisi au kunyang'ang'Anyana wanawake na raia mitaani, bali kubadilika ili liwe jeshi la ujenzi wa taifa, huku likihakikisha amani na usalama kwa nchi yetu.

Rais Kikwete haitoshi kuona ukiteua baadhi ya maofisa wa JWTZ kuwa wakuu wa mikoa na wilaya. Tunataka  kuona wahandisi medani wa jeshi hilo wakitumiwa na serikali yako katika shughuli za ukarabati na ujenzi wa miundombinu ili taifa lipate maendeleo kwa haraka  kama sote tunavyotamani.

Wanajeshi madaktari na fani nyingine ndani ya jeshi hilo, tunaona hivi sasa wamekuwa wakitumia fani zao vizuri kwa sababu kuna hospitali zinazoeleweka ndani ya jeshi hilo  na hasa ukizingatia Baada ya mgomo wa madaktari , serikali iliipandisha hadhi Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam , Kuwa Hospitali ya Rufaa,  zimekuwa zikitoa uhuduma ya matibabu hata kwa raia.

Ni vyema tutambue kuwa, mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe, hivyo basi Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe na si wageni. Sote kwa pamoja tujifunge mkanda bila kubaguana katika kushiriki kwenye shughuli za ujenzi wa taifa na naamini tutafanikiwa.Waandisi wa JWTZ watumike wakati wote hapa nchini, siyo tu kuwatumia wakati wa mafaa na Kuwapeleka Katika nchi zenye vita Kama Darfur, Congo na kwingineko.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Aprili 4 Mwaka 2014.