KASHFA YA ESCROW ISITUVURUGE

Na Happiness Katabazi
MIONGONI wa Wimbo unaotamba hapa nchini Homa ya Dengue na kile kinachoitwa eti ni vigogo wa serikali  wanaotuhumiwa kuhusika Katika kashfa  ya ufisadi  wa Sh Bilioni 200  Katika Akaunti ya Baraza la Usuluhishi la Migogoro ya Kibiashara (ESCROW) ya Benki Kuu (BoT).

Makala yangu itazungumzia Wimbo huo wa pili wa kashfa ya ESCROW ambayo  Mbunge wa Kigoma Kusini(NCCR-Mageuzi), David Kafulila amedai Kuwa ndiye yeye ameiibua kashfa hiyo  ambapo  aliwataja wahusika wakuu wa kashfa hiyo Kuwa ni  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter   Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliachim Maswi, Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Jaji  Frederick Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba.

Kafulila alisema  kuwa ufisadi huo ni lazima mbivu na mbichi zifahamike, na kwamba haungi mkono uamuzi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wa kuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza suala hili kwa kuwa linagusa mamlaka kubwa katika dola, badala yake iundwe Kamati Teule ya Bunge.

Muda mfupi baada ya Kafulila kutoa tuhuma hizo Bunge, hakukubaliana na ombi la Kafulila lililotaka iundwe Kamati Teule ya Bunge na badala yake akaiagiza TAKUKURU na OFISI ha CAG Ifanye uchunguzi wake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo.

Kwa jicho la Sheria tuhuma zilizotolewa na Kafulila zitabaki Kuwa tuhuma, na Kafulila atahesabika kwanza Kuwa yeye ni mtoa  taarifa za tuhuma hizo.Hivyo kitendo Cha Kafulila kunukiliwa na Gazeti hili toleo la Jumatano ya wiki hii Kuwa   uamuzi huo wa Pinda una Mashaka makubwa na kwamba tuhuma hizo zinahusu viongozi wakubwa wa dola hivyo eti ni Vyema  Kamati ya Teule ya Bunge iundwe uchunguze siyoni Kama Ina mantiki.

Kwani TAKUKURU imeanzishwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana Rushwa ya Mwaka 2007 Namba 11/2007.Na kifungu Cha 7 Cha Sheria hiyo kimeanisha Kazi za Takukuru na miongoni mwa Kazi za Takukuru ni kufanya uchunguzi makosa ya kula Njama Kutenda kosa, kuchunguza tuhuma za makosa ya rushwa yanayowahusu maofisa wa serikali.

Aidha OFISI ya CAG nayoilianzishwa na inayo majukumu yake mengi tu ikiwemo ya kukagua mahesabu Katika Fedha za serikali na imekuwa Ikitimiza majukumu yake na kutoa taarifa zake kwa umma.

Na Taasisi hizo zimeanzishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kafulila ni miongoni mwa wa Bunge wa Bunge Hilo.

Sasa Inashangaza  Kama siyo kutisha kusikilizwa  mtunga  Sheria Huyo Akisema uamuzi huo wa Pinda una Mashaka kwasababu yeye alikuwa akitaka Bunge iunde Kamati Teule.

Kama Kafulila alikuwa Hana Imani na Takukuru, CAG ni kwanini alitoa tuhuma hizo bungeni akitaka mbivu na mbichi sijulikane? Kumbe anaamini Takukuru, CAG ni wa chafu ni kwanini aliibua tuhuma hizo tena akitaka uchunguzi ufanyike? Hivi MWISHO wa siku alifikiri Takukuru, CAG hazitausishwa Katika uchunguzi huo

 Tuhuma hizo zinahusu Fedha za serikali , Ofisi  ya ya CAG lazima ili usiishie mAana ipo pale kwa kutazama matumizi ya Fedha za serikali zimetumika Kama iliyokusudiwa?

Maana hata Kama Kamati Teuli ya Bunge ingeundwa Mwisho wa siku ripoti hiyo ya uchunguzi wa Kamati Teuli ya Bunge Ingepelekwa Takukuru au Polisi ili zichunguze kuona je kuna ushahidi wa kutosha wa kuweza kuwafungulia Mashitaka watuhumiwa? maana Polisi  na Takukuru Ndio wenye majukumu hayo Kimsingi.

Pia Itakumbukwwa kashfa ya wizi Katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), iliibuliwa Bungeni, Kamati ya Teule ya Bunge haikuundwa Matokeo yake Rais Jakaya Kikwete alitenda TIMU ya Uchunguzi wa tuhuma hizo ambayo ilishirikisha polisi, Wanasheria toka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tasisi nyingine za serikali ambayo ilikuwa na Ofisi zake Mikocheni ambapo ili fanyakazi yake vizuri  Mwisho wa siku Uchunguzi huo ulimfanya Mkurugenzi wa Mashitaka , Dk.Eliezer Felelshi Kufungua jumla ya Kesi 12 za EPA m Novemba 4 Mwaka 2008  ambapo hadi sasa jumla ya Kesi Nne zimetolewa hukumu na baadhi ya washitakiwa walipatikana na hatia za makosa waliyoshitakiwa na wengine waliachiwa Huru kwasababu ushahidi haukuwagusa.

Mfano mwingine ni tuhuma za mkataba wa kampuni ya Richmond Ambapo kelele zilipigwa na wabunge hadi Kamati Teuli ya Bunge ikaundwa Mwaka 2007 na Mwanzoni Mwaka 2008 Kamati Teuli ikabainika kilikuwa na ouzo Katika mkataba huo na kumtaka Aliyekuwa waziri makuu Edward Lowassa ajipime na Kamati hiyo ikaamuru Wamiliki wa kampuni hiyo Naeem Gire na Mohamed Gire na baadhi ya Maofisa wa serikali wawajibishwe  Hali iliyosababisha Lowassa kuwajibika KWA kujiudhuru   wadhifa  huo ambao alidumu nao KWA Kipindi  kifupi sana.

Baada ya ripoti ya Kamat hiyo kusomwa, baadhi ya wabunge kwasababu wanazozitoa wa Wakaanza kuishi nikiuza Takukuru iwashitaki watu Hao Hali iliyosababisha Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru , Dk.Edward Hosea na baadhi ya wabunge kuingia Kwenye malumbano Kwani Hosea alikuwa akitaka Takukuru iachwe ifanyekazi yake kwa  Uhuru na siyo kuingiliwa na wasiasa Hali iliyosababisha kila kukimbia wabunge Hao Kuwa wanashambulia Takukuru na Hosea kila kukicha Kumbe wabunge Hao walikuwa wananjama zao chafu za kuaribiana kisiasa.

Wananchi ambao walikuwa hawaelewi Njama hiyo waliwaunga mkono wabunge Hao wengine ambao walipachika jina la ' wabunge wanapambana na  ufisadi", Leo hii wanasiasa Hao wapo  kimya utafikiri ufisadi ndani ya nchi hii umekwisha.Dhambi sana.

Mwisho wa siku Takukuru iliamua kumfungulia Kesi ya Madai ya Kutoa taarifa za uongo Kwenye Kikao Cha Tenda Cha Tanesco kuhusu uwezo wa kampuni ya Richmond, mshitakiwa alikuwa ni Neem Gire Mwaka Juzi Hakimu Mkazi wa Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Waliarwande Lema alimuoa Gire Hana Kesi ya Kujibu  na Mkurugenzi wa Mashitaka DPP- Dk.Feleshi hakulidhika na uamuzi huo anakimbilia Mahakama Kuu Ambapo Jaji Lawrence Kaduri alitenga uamuzi huo na akaamuru jarada la Kesi hiyo lirudishwe Mahakama ya Kisutu na Gire aanze  kujitetea na Gire naye kupitia Wakili wake Alex Mgongolwa hawakubaliani na uamuzi wa Mahakama Kuu, wamekimbilia Mahakama ya Rufaa.

KWA  hiyo binafsi naweza Kusema Kuwa sikubali Kuwa tuhuma ni za kweli na sikatai Kuwa tuhuma hizo zilizoibuliwa na Kafulila  Kuwa ni za uongo Katika Hatua hii ya awali.Nasubiri   vyombo vyenye mamlaka ya kufanyia uchunguzi  itakapokuja kuandika ripoti za uchunguzi wake.

Kwani tuna Mifano hai  ambayo inafunza kupitia wanasiasa wetu ambao Walijifanya ni mabingwa wa kuibua kile wanachokiita ufisadi  wakati Sheria zote za Tanzania ikiwemo  Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002 , haina kosa linaloitwa ufisadi. Sijui wenzetu hawa kosa la ufisadi wanaotaka watu washitakiwa nalo sijui wa alipata Katika Kifungu kimya Cha Sheria.

Mbunge Zitto Kabwe aliuaminisha umma Kuwa Ana ushahidi kuhusu Majina na namba za Akaunti za watu walioficha  Fedha nje ya nchi na baadhi ya watu waliomua mini, lakini siku zote njia ya muongo ni Fupi, Mwanasheria  Mkuu wa Serikali Jaji Werema aliliambia  Bunge Kuwa Zitto ni muongo aliwasilisha kumuita  Ofisini kwake akitaka atoe ushahidi chini ya kiapo , Zitto  akasema hana ushahidi, na hadi Leo kimya kabisa utafikiri Zitto  siyo yeye aliyekuwa akisimama  majukwaa akijinadi anaoushahidi wa Hilo.

Pia kuna wanasiasa wengine ambao Walijitapa ndani na nje ya Bunge Kuwa wanaushahidi wa Majina ya watu walioiba  Fedha za EPA kupitia kampuni a Kagoda hadi Leo hawajaenda kutoa ushahidi thabiti Katika vyombo husika, Wanaishia kubwatuka majukwaani na kuwataka Ujinga huo baadhi ya waandishi wa Habari ambao hawajui kilichopo nyuma ya tuhuma zinazoibuliwaga na baadhi ya wanasiasa wa naandika Habari za kutoa hukumu  za upande mmoja.

Wiki iliyopita Spika Anna Makinda  Mara Tatu wakati akiendesha Bunge aliwataka baadhi ya wabunge waache kutumiwa  na baadhi ya watu walionje ya Bunge Kuja bungeni  Kusemea maslahi binafsi ya watu wakiwa tuma na kuwataka wabunge Hao watumie akili zao.

Ushauri  huu ni mzito sana kutolewa na Spika Kwa wabunge na Hakuna Shaka Makinda alikuwa anasababu anayoifahamu  ndiyo mAana Akaamua kutoa ushauri huo licha Spika Makinda hakutaja jina la Mbunge anayetumiwa.

Hivyo ushauri wangu kwanza kwa waandishi wa Habari wenzangu  kuhusu tuhuma hiyo iliyoibuliwa na Kafulila tuwe makini na tusimame Katika Maadili ya taaluma yetu.Kafulila tumemsikia, serikali kupitia Pinda imeishachukua Hatua  KWA kuanzia Pinda ameagiza Taasisi hizo mbili zifanyie Kazi tuhuma za Kafulila. 

Hivyo ni vyema sasa tuziachie Taasisi hizo zifanyie kazi yake Kwa Uhuru na Mwisho wa siku zije zitoe ripoti yake.Tusikubali ama kutumiwa na wafanyabiashara, wanasiasa, Wanasheria kuwachafua watu wengine wanaotuhumiwa Katika tuhuma hizo na Kafulila isivyohalali Kwani Tayari naona kuna Dalili za wazi ambazo ni chafu za miongoni mwetu kuanzia kutumiwa na Makundi yanayoasimiana Katika kashfa hii.

Pili, Takukuru, CAG visikubali kuingiliwa kufanyakazi yake na Makundi yenye Hira Katika Sakata hili Kwani endapo watakubali kufanyakazi KWA shinikizo la wanasiasa Mwisho wa siku watajikuta wanaumbuka Mbele ya safari Kama serikali ilivyoumbuka Mara mbili Kwenye Kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Ricky Mahalu na Grace Martin Kwani Chanzo kikubwa Cha Kesi hii kilianzia  pale Bungeni Mwaka 2004 ambalo  mwanasiasa mmoja alijitapa Kuwa Balozi Costa Mahalu  aliwafungulia  Fedha za ujenzi wa Jengo  la ubalozi Wa Tanzania nchini Italia kumbe ni uzushi.

Tatu , Kafulila kwa Kuwa Tayari umeishanukuliwa ukisema uamuzi wa Pinda una Mashaka nao , ni wazi hata vyombo hivyo va uchunguzi vikitoa Matokeo ya uchunguzi ambao wewe hutapendezewa nao, hutatakubaliana nao.

 Basi minakushauri Kafulila tumia    Kifungu Cha 99 Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002, kuomba uwe mwendesha Mashitaka Binafsi(Private Prosecutor), ili uweze kuendesha Kesi hiyo mahakamani mAana Tayari umejinasibu Kuwa una ushahidi wa kutosha kuhusu tuhuma hizo.

Ni sisi wenyewe wananchi wa Tanzania Tulitaka nchi yetu iongozwe na Utawala wa Sheria, kwahiyo Takukuru, CAG, Cheo Cha Waziri wa Mkuu na Spika vimeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Hivyo tuheshimu wanapokuwa wanatimiza majukumu Yao na anayeona Hana Imani na vyombo Vya dola, aende kuishi nchi ambazo anaamini vyombo vyao Vya dola vinaaminika.

Na wananchi huko vijiweni Tusikubali kutoa hukumu Kuwa. Fulani n fisadi , hafai kuongoza, afukuzwe Kazi eti tu mwanasiasa Fulani kajitapa kuibua tuhuma za ufisadi.Kwani ni hawa hawa wanasiasa Ndio wamekuwa wakituingiza Kwenye ushabiki wa mambo ya kijinga Mwisho wa siku wanatoa na soremba.

Ni hawa hawa wanasiasa walijiapiza Kuwa kampuni ya Richmond ni ya Kitapeli na ni kampuni ya mfukoni .Wananchi  tukaamini  Kumbe walikuwa nalo jambo.

 Mwisho wa siku kampuni hiyo ikabadilishwa jina ikaitwa  Dowans, kelele zikadhidi hadi kufikishana mahakamani na Mwisho wa siku Tanesco ikashindwa Kesi iliyoishitaki   Dowans kule katika Baraza la Usulushi wa Migogoro ya Kibiashara ya Kimataifa (ICC), Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Kampuni ya Richmond tuliyoaminishwa na wasasiasa uchwara Kuwa ni kampuni ya mfukoni ilibadilishwa toka jina la Richmond Kuja Dowans, na Mwishoe HIvi sasa inaitwa Sympion Power Na inatoa huduma zake kama kawaida na huduma ha kampuni hiyo inatumika .

Na mwaka jana   Rais wa Marekani Baraka Obama alivyokuja Tanzania  aliizindua  kampuni hiyo,na Hao wanasiasa waliotuaminisha uongo kuhusu uwezo wa kampuni hiyo Kuwa ni ya mfukoni nao walikuwepo Kwenye msafara wa ziara hiyo ya Obama kuzindua Sympion .Na leo wanasiasa hAo, sanaharakati waliokuwa wakishabikia kuiponda kampuni hiyo leo wapo kimya utafikiri wamefariki.

Tujifunze kutokana makosa, tusiwe wepesi kuamini   kila kitu kinachoibuliwa na baadhi ya wanasiasa wetu uchwara Kwani wengine ni Mavuvuzera wa wafanyabiashara, makampuni  na wanasiasa,na makuadi wa Makundi yanayoasimiana Katika magomvi Yao ama ya Kugombea Tenda Fulani, Biashara , vyeo na magomvi mengi.

Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Mei 18 mwaka 2014





MAHALU HURU TENA


Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemfutia Rufaa  ya jinai iliyokuwa ikimkabili Aliyekuwa  Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin kwasababu Mkata rufaa ambaye ni Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi  han haja ya kuendelea na rufaa hiyo.

Mwaka 2012  DPP-Dk.Feleshi kupitia Wakili mwandamizi wa serikali Oswald Tibabyemkomya alikata  rufaa Mahakama Kuu Kapinga hukumu iliyotolewa na Aliyekuwa Hakimu Mkuu Mfawidhi Elvin Mugeta, Agosti 9 Mwaka 2012 Katika Kesi ya uhujumu uchumi Na.1/2007 iliyokuwa ikiwakabili wajibu rufaa  ambapo Hakimu Mugeta alimwachiria Huru Mahalu na grace baada ya kuwaona hawana Hatia  Katika Kesi iliyokuwa ikiwakabili.

Amri ya kuondolewa rufaa hiyo ilitolewa Jana na JAJI John Utamwa ambaye Alisema Mahakama yake inatumia Ibara ya 108 (2)ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 , kukubali ombi la DPP ambapo DPP aliwasilisha ombi la kuiandika rufaa yake dhidi ya wa jibu rufaa chini ya Kifungu Cha 386(1) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002.

Ibara ya 108(2) ya Katiba ya nchi inasomeka HIvi: ' Iwapo Katiba hii au Sheria nyingine  yoyote  haikutamka wazi kwamba shauri  la aina iliyotajwa. Mahususi litasikilizwa  kwanza Katika Mahakama ngapi iliyotajwa  mahususi  kwaajili hiyo, basi Mahakamu Kuu  itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kila shauri  la aina hiyo.Hali Kadhalika  Mahakama Kuu itakuwa na uwezo  wa kutekeleza  shughuli  yoyote  ambapo kwa mujibu  wa mila  za kisheria  zilizotumika  Tanzania  shughuli ya aina  hiyo  kwa kawaida  hutekelezwa  na Mahakama Kuu.
Isipokuwa  kwamba Masharti  ya Ibara hii ndogo  yatatumika  bila ya kuathiri  mamlaka Mahakama ya Rufaa  ya Tanzania  Kama ilivyoelekezwa  Katika Katiba  hii au Katika Sheria nyingine".

Jaji Utamwa alisema Kwakuwa Kifungu Cha 386(1) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 ikampa madaraka DPP , kuondoa rufaa wakati wowote Kabla ya rufaa, Mahakama yake inalikubali ombi Hilo la DPP la kuondoa rufaa hiyo mahakamani na kwamba kuanzia sasa Mahalu na wenzake wapo huru.

Amri ambayo ilipokelewa kwa Furaha na Grace na wakili wao Beatus Malima licha Mahalu ambaye Mjumbe wa Bunge la Katiba hakuwepo mahakamani , ambapo Wakili Malima Alisema amefurahishwa na amri hiyo ya MahakamA na pia amepongeza uamuzi huo wa DPP. Dk.Feleshi  kwa kuwaondolea rufaa hiyo wateja wake na kwamba kwa amri hiyo ya Mahakama ni wazi sasa wateja wake wanakuua Huru kulitumikia taifa Lao kwa kasi mpya baada ya kukumbuka na Kesi hiyo kwa  Miaka Saba sasa.

Agosti  9 Mwaka 2012 Aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Elvin Mugeta alimwachishakazi Huru Baloz Mahalu na Grace  waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Euro milioni mbili kutokana na ushahidi wa jamhuri kushindwa kuwatia hatiani.

Hukumu hiyo hiyo ilitqfsiriwa  i kama ni kubwagwa kwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kutokana na hatua ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kukubali kupanda kizimbani na kumtetea Mahalu dhidi ya serikali, tukio ambalo ni la kwanza katika historia ya nchi hii. Hukumu hiyo ya kihistoria ya kesi ya uhujumu uchumi Na.1/2007 .

Washtakiwa hao waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka sita walikuwa wanatetewa na mawakili Mabere Marando, Alex Mgongolwa, Beatus Malima na Cuthert Tenga na upande wa Jamhuri ulikuwa ukiwakilishwa na Ben Lincoln na Vicent Haule toka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Ponsia Lukosi toka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Aliyaja makosa hayo kuwa ni kula njama, kutumia nyaraka za manunuzi ya jengo la ubalozi ili kumdanganya mwajiri wao serikali, wizi wa Euro milioni 2,065,827 na kuisababishia serikali hasara.

Kesi  hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 22 mwaka 2007.

Ili kuithibisha kesi yao, upande wa Jamhuri ilileta jumla ya mashahidi saba wakati upande wa utetezi ulileta mashahidi watatu akiwemo Rais mstaafu Benjamin  Mkapa.

Mei 8 mwaka 2012, upande wa utetezi ulifunga ushahidi wake baada ya Grace kumaliza kujitetea. Mei 7 mwaka 2012,Mahalu ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu kipya cha Bagamoyo cha jijini Dar es Salaam alimaliza kujitetea na siku hiyo ndiyo Rais Mkapa aliandika historia mpya nchini kwa upande wa marais ambapo alifika mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake katika kesi hiyo. Julai 16 mwaka 2009, Jaji Sivangilwa Mwangesi ambaye ndiye alikuwa akiisilikiza kesi hiyo tangu ilipofunguliwa mwaka 2007 alitoa uamuzi wake ambapo aliwaona washitakiwa hao wana kesi ya kujibu. Machi 25 mwaka 2011.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Mei 10 Mwaka 2014.

MAPYA YAIBUKA KESI YA GHOROFA DAR



Na Happiness Katabazi
MAWAKILI wa upande wa utetezi Katika kesi ya Mauji yaliyosababishwa na kuangukiwa na ghorofa lilikuwa MTAA wa Indra Gandhi Dar es Salaam, inayomkabili Mkurugenzi wa zamani wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime(61) na wenzake wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ,ilifutwa Kesi hiyo kwasababu hati ya Mashitaka Ina dosari za kisheria.

Mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka Mawakili wa Washitakiwa John Mhozya na Ndurumah Majembe Jana waliwasilisha ombi Hilo Jana  hoja zao jana ambapo Wakili , Mhozya aliomba  mahakama kuiangalia kwa umakini hati ya mashtaka inayomkabili mteja wake , Fuime  kwa madai ni batili kwa kuwa haikidhi matakwa ya sheria.
 
Wakili Mhozya alidai Kuwa Sheria   inaitaka hati ya mashtaka  kuwa na viashiria vya kosa  ambalo mshtakiwa anashtakiwa nalo, na kwamba mteja wao ameshtakiwa na Kesi ya Mauji  ila hati ya mashtaka iliyopo mahakamani haina viashiria vinavyoonyesha  kosa hilo Hali nayoifanya hat hiyo ionekane ni Batiri kisheria.
 
Awali Kabla ya Wakili Mhozya kuwasilisha hoja hiyo, Hakimu Kisoka alimweleza Wakili Huyo  kuwa jalada halisi la kesi hiyo limeitwa Mahakama  Kuu hata hivyo wakili huyo aliieleza mahakama kitu ambacho kimesababisha liitwe huko akimuhusu mteja wake na kuomba kuendelea kuwasilisha hoja yake.
 
Hakimu Kisoka alimpa nafasi hiyo ya kumsikiliza lakini Wakati wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongola  alipinga  kwa madai kuwa  mahakama hiyo ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza wala kusuluhisha chochote kwa sababu kesi ipo hapo kwa ajili ya taratibu za awali tu na kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza Kesi ya Mauji.
 
Baada ya kutoa maelezo hayo, Hakimu Kisoka alimtaka wampe nafasi ya  kumsikiliza Mhozya, kitendo ambacho Kongola alikataa na kudai kuwa hata jibu chochote na  na wakili huyo wa serikali alidai kuwa atatoka   nje ya mahakama wakati kesi hiyo ikiendelea
 
Hata hivyo Hakimu Kisoka alimtaka wakili Kongola kutulia ili aweze kumsikiliza Wakili Mhozya anaongea nini.
 
Kutokana na kitendo hicho, Wakili Majembe  aliiomba mahakama kuzuia uvunjifu wa sheria kwa watu wa kawaida na  wale wa serikali mahakamani  na kuongeza kuwa katika kusoma kwake  na uzoefu aliokuwa nao hajawahi kuona mahali popote  hicho kinachodaiwa na upande wa mashtaka.
 
Majembe alidai kuwa Mahakama inauwezo wa kuangalia kwa umakini kosa ili kujiridhisha  kwa kuwa uhuru wa mtu ni muhimu  na jela ni mbaya,  leo mteja wetu, Fuime ameshtakiwa kwa kosa la mauaji kesho anaweza kubadilishiwa likawa la kutakatisha fedha na baadaye hata kubaka.

Aidha Hakimu Kisoka aliarisha Kesi hiyo hadi  Mei 19 Mwaka huu, AMBAPO Atakuja kutolea uamuzi wa ombi lilowasilishwa na Mhozya.
 
Fuime na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 27 ya mauaji  yaliyotokea katika mtaa wa Indira Gandh, yaliyotokana na kuporomoka jengo la ghorofa 16.Washtakiwa wengine ni mfanyabiashara na mmiliki wa jengo hilo Radha Hussein Radha, Diwani katika Manispaa ya Kinondoni,  Ibrahim Mohamed maarufu kama Kisoki (59),  Mhandisi Charles Salu (48), Mhandisi wa Majengo Godluck Sylivester (35)  na Mkurugenzi Mkuu wa Mkaguzi wa Majengo, Willibrod Wilbard (42).

Washtakiwa wengine ni Mhandisi Mohamed Swaburi (61), Mhandisi Mshauri, Zonazea Oushoudada (60), Mkadiriaji Majenzi, Vedasto Nziko (59), Msanifu Majengo, Michael Hema (59), Msajili Msaidizi AQRB, Albert Mnuo na Ofisa Mkuu Mtekelezaji OJoseph Ringo.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Mei 7 Mwaka 2014
 
 
 
 
 
 
 
 
 

WAKILI RUTAGATINA ASHINDA RUFAA YAKE

WAKILI RUTAGATINA ASHINDA RUFAA
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama ya Rufaa nchini, imetengua hukumu ya Mahakama Kuu Kanda a Dar es Salaam, ya Septemba 6 Mwaka 2006 ambayo ilitupilia Mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na Wakili wa kujitegemea Christian  Rutagatina Kapinga Kapinga uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Mawakili ambayo Kamati hiyo ilimwondoa Kwenye orodha ya Mawakili nchini.

Hukumu ya rufaa hiyo Na.46/2012 ilitolewa jopo la Majaji wa Tatu wa Mahakama ya Rufaa Stephen Bwana, Sauda Mjasiri na Januari Msoffe .Rufaa hiyo Iliikatwa na Rutagatina aliyekuwa akitetewa na wakili George Kilindu dhidi ya Kamati ya Maadili ya Mawakili na Clavery Ngalapa Mwaka 2012.

jaji Bwana Alisema Rutagatina aliwasilisha jumla ya Sababu Sita za Kapinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyotupa RUFAA yake,AMBAPO Sababu ya kwanza ni kwamba Majaji wa Mahakama Kuu waliopo sea kisheria na kimaelezo kukubali mamlaka yasiyosahihi  ambayo yaliyotolewa na mrufani(Rutagatina).

Sababu nyingine ni mahakama Kuu  Walikosea kisheria kukata kukubali Haki ya Msingi ya mrufani, kwamba Mahakama Kuu ilikosea kisheria Kwa kushindwa kutoa hukumu yake kutumia ushahidi thabiti wa tuhuma zilizokiwa zinamkabili mrufani bila kuachakazi mashaka, na kwamba Mahakama ile ilikosea kisheria Kwa kushindwa kutumia ushahidi unaonyesha Majina ya wa maofisa wa Mahakama ambao mdaiwa  wa pili ( Ngalapa) alidai Kuwa mrufani alimtaka ampatie Fedha ili akawape maofisa wa Mahakama Kama rushwa ili wamsaidie Kwenye Kesi yake. Na kwamba adhabu aliyopewa mrufani ya kuondolewa Kwenye orodha ya Mawakili nchini ni kubwa.

Jaji Bwana Alisema amepitia hoja za pande zote mbili ambapo mdaiwa wa kwanza awatete wa na Wakili Mwandamizi wa serikali Vicent  Tangho , mahakama yake imeamua kukubaliana na hoja za mrufani kwamba utaratibu uliotumika kuendesha shauri Hilo Katika Kamati ya Maadili ya Mawakili na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ulikiuka Sheria na Kanuni inayotaka     
Mahakama au Kamati ya Maadili Imtie Mtu hatiani KWA makosa anayokabiliwa nayo bila Kaacha Mashaka yoyote lakini KWA mazingira ya shauri Hilo, Kamati ya Maadili ya Mawakili na Mahakama Kuu ilishindwa kuzingatia kanuni hiyo ambayo inakataza kumtia MTu hatiani wakati kuna Mashaka.

"Mahakama hii inatamka Kuwa  mrufani (Rutagatina),ameathirika  kwa Miaka Tisa sasa  kutokana na hukumu hizo mbili ambazo ni hukumu ambazo zimevunja Sheria  na kwasababu hiyo Mahakama hii inakubali RUFAA yake na inatambua hukumu ya Mahakama Kuu" Alisema Jaji Bwana.

Novemba 18 Mwaka  2005 , Kamati ya Maadili ya Mawakili  nchini, ilimvua  uwakili Rutagatina , baada ya kumkuta na hatia ya kosa kuvunja  Maadili ya uwakili.
Clavely Ngalapa , alikuwa ni mteja wa mrufani , ndiye  aliyewasilisha  malala ipo  Kwenye Kamati hiyo. Ngalapa  alidai Kuwa Wakili Huyo (Rutagatina) alimtaka atoe  rushwa  kwa  jaji  na maharani wa Mahakama Kuu  Katika Kesi ya Madai Namba 393/1998 ambayo Wakili Huyo alikuwa akimtetea  mteja Huyo.

Septemba 6 Mwaka 2006 , jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, lilokuwa likiongozwa na Jaji Augustine Shangwa, Jaji Juxon Mlai (Mstaafu),  Na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Kwa sasa William Mandia , Alisema yeye  Kuwa yeye  na wenzake wamepitia Kwa kina ombi la Rufaa ya Rutagatina kuhusu hukumu iliyotolewa Novemba 18 Mwaka 2005  na Kamati ya Maadili ya Mawakili , na wameikataa  Rufaa yake Kwasababu wamebaini Mrufani alivunja mabadili ya uwakili.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 6 Mwaka 2014.



VIGOGO BARCLAYS WATINGA KIZIMBANI



Na Happiness Katabazi
WATU saba wakiwemo wafanyakazi wawili  wa benki ya  Barclays
Jana wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Da es Salaam, kwa kesi ya  sh. milioni 390.2 kwa kutumia silaha.

WAkili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka akisaidiwa na Mwanaamina Kombakono mbele Hakimu Mkazi Nyigulila Mwaseba aliwataja washitakiwa Hao Kuwa ni   Alune Kasililika (38), Neema Batchu (26) wafanyakazi wa
benki, Kakame Julius (38), Iddy Khamis (32), Sezary Msolopa (31), Boniphace na Muumba (29) na Ruth Macha (30) wafanyabiashara.

Wakili Kweka alidai kuwa washitakiwa hao  wanakabiliwa na mashtaka mawili.
Alidai Kuwa  kuwa katika tarehe tofauti tofauti zisizo fahamika washtakiwa  wakiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam walikula njama ya kwa nia ya kutenda kosa la wizi.

Wakili Kweka akili taja SHITAKA la pili washitakiwa Hao   Aprili 15 mwaka huu, wakiwa Katika eneo la  benki hiyo tawi la Kinondoni, Dar es Salaam waliiba fedha tasilimu sh.
milioni 390.2, Dola za Marekani 55, 000 na Euro 2150 mali ya Barclays na  Kuwa Kabla ya kufanya wizi huo walimtishia kwa silaha
Anifah Ahmad na Anna Tegete ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo ili kuweza
kujipatia na kumiliki fedha hizo.

hata hivyo washitakiwa hao walikana mashitaka na Wakili Kweka  alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na wa naomba  tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Mwaseba alisema kwa mujibu wa sheria shtaka la pili halina dhamana,
kwa hiyo washtakiwa wapelekwe gerezani  na Kesi hiyo itaalishwa hadi   Mei 15 Mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Mei  3 Mwaka 2014.