MANISPAA YA KINONDONI 'MTATUUA' KWA TB




MANISPAA YA KINONDONI 'MTATUA'  KWA TB
Na Happiness Katabazi
ITAKUMBUKWA kuwa Oktoba 23 Mwaka huu, Kituo cha Dalala Cha Simu 2000 kilichopo Mtaa wa Sinza ' C' Kata ya Sinza Wilaya ya Kinondoni ,Dar es Salaam,kilichopo karibu na Shule ya Sheria kilianza kufanyakazi kwa madaladala kuanza kutoa huduma wanaotumia usafiri wa umma.

Nikiwa Kama Mwananchi na Mwandishi wa Habari mzalendo kwa taifa langu , Kituo hicho kiliapoanza kufanya kazi siku hiyo iliandika Habari ya kupongeza serikali kwa kutujengea Kituo hicho cha kisasa Katika eneo Hilo na picha nilipita na ushahidi wa Hilo, upo Humu ndani ya ukurasa wangu wa  Facebook.

Msimamo wangu wa kupongeza serikali kwa kutujengea Kituo hicho uko pale pale haujabadilika ila Leo nakuja na ombi jingine kwa Manispaa ya Kinondoni ambayo Kituo hicho kipo chini yake licha bado hakijazinduliwa rasmi.

Mapema kabisa natanga za maslahi yangu Kuwa Mimi ni miongoni mwa wakazi tunaoishi  kandokando ya Kituo hicho Cha mabasi hivyo ninavyoandika makala.  

Kituo hicho tangu kilipoanza  kufanyakazi , kweli eneo Hilo limekuwa na ongezeko kubwa la Magari na watu na Biashara mbalimbali zimeongezeka Hali inayosabaisha eneo Hilo kugeuka ni eneo la Biashara.

Pia nao matapeli waliojigeuza ni madalali  nao wameibuka kwa kuwalaghai watu wanaofika Katika eneo Hilo Kutafuta fremu kwaajili ya kupangisha ili waendeshe Biashara zao.

 Matapeli Hao wamekuwa wakiwarubuni watu wenye Shida hiyo Kuwa wao eneo Hilo wanalijua vizuri kumbe ni waongo na Kuwapeleka Katika nyumba za watu wa eneo Hilo ambao wanaendelea na ujenzi wa fremu Kuwa fremu hizo zitapangishwa na kwamba wenye nyumba wanawafahamu watawaunganisha nao ili Wawakodishe hizo fremu.

 Matapeli  wanawataka watu Hao wawapatie sh.5,000 hadi 10,000 eti kwasasa wamepewapeleka kuwaonyesha fremu hizo Kumbe ni uongo hata Wamiliki wa nyumba hizo hawa wafahamu  hata kwa sura. Kuweni makini Mnaotafuta fremu eneo Hilo.

Nirejee kwenye ajenda yangu Leo, ambayo tangu Kituo hicho kianze kufanya kazi ni wazi wakazi wa eneo na watumiaji wa kituo hicho tupo kwenye hatari kubwa ya kupata Maradhi   Ukiwemo ugonjwa wa Kifua Kikuu(TB).

Nasema hivyo kwasababu barabara  Kuu inayotumiwa madaladala barabara ,Magari madogo watembea kwa miguu Katika eneo Hilo la Kituo , Ina vumbi la kutisha Hali inayosababisha baadhi ya watembea kwa miguu wakiwa wanatembea Katika eneo Hilo kujifunika vitambaa Katika Pua zao.

Na wakazi wa eneo Hilo Ndio tumekuwa Katika wakati mgumu sana Kwani huwezi kukaa nje kwakuogopa vumbi na ukikaa ndani vumbi linaingia ndani na kusababisha nyumba Kuwa Kama kiwanda Cha Kutengenezea cimenti.

Sitanii, ni ukweli mtupu, hatuna raha tena ndani ya nyumba tunazoishi  kwasababu ya vumbi kuingia sebuleni hadi vyumbani, ukifagia ukideki ni kazi bure.

Minajiuliza hivi  Manispaa ya Kinondoni kupitia maofisa wao hawalioni hili?  Hivi Manispaa ya Kinondoni inashindwa kutoa Gari lake Moja likalijaza maji Likaja kumwagia barabara hiyo ili kupunguza vumbi Hilo Kali?

Au Manispaa ya Kinondoni inasubiri wakazi wa eneo hilo siku tuanze kujazana kwa Wingi Katika kitengo Cha ugonjwa wa TB Katika Hospitali ya Sinza Palestina na Mwananyamala tukienda kuchukua vidonge Vya TB kwasababu ya kuathiriwa na vumbi Hilo ndiyo itafurahi?

Au hiyo Manispaa ya Kinondoni ndiyo itasema  haina Fedha ya kujaza mafuta Hilo Gari na Fedha ya kununulia  maji ya kumwaga Katika barabara hiyo?

Au Manispaa hiyo italileta Gari Hilo Lije limwagie maji barabara hiyo vumbi lipungie siku kiongozi Mkuu wa Kitaifa atakapokuja kuzindua Kituo hicho?

Ebu Manispaa ya Kinondoni acheni ubahiri ,na muwathamini  wakazi wanaoishi eneo Hilo Kwani nao ni binadamu na wana Haki ya kuishi na kukingwa na Maradhi yanayokingika.

Kwa vumbi hilo linaloendelea kututesa kutokana na ongezeko la Magari kutumia barabara hiyo, nitakuwa sijakosea nikisema Kituo hicho ama ni kaburi au ugonjwa wa TB kwa wakazi wa eneo Hilo. Tuoneeni huruma wenzenu vumbi litatoa  roho zetu.

Uwepo wa Kituo  Cha Dalala Cha Simu 2000 Katika eneo Hilo ,isiwe ni Chanzo Cha wakazi wa eneo Hilo kupata TB.

Naamini Manispaa ya Kinondoni ikiamua inaweza kutoa Hilo Gari likaja kuondoa vumbi kwa kuweka utaratibu wa mara kwa mara gari hilo walau mara tatu kwa wiki kuja kumwagia maji hiyo barabara hadi mwisho siku  barabara hiyo ikaja Kujengwa Katika ngazi ya lami.

Wakati Kituo hicho kina jengwa,Manispaa ilikuwa ikitoa Gari hilo Kuja kumwagia maji barabara hiyo na vumbi Likawa linapungua.

 Lakini pia hata siku Chake Kabla ya Rais wa Marekeni Barack Obama, kuwasili nchini,tulishuhudia usafi wa Hali ya juu na barabara zilikuwa zikimwagiwa maji na Magari hayo.

Na kweli Dar es Salaam, ilikuwa safi sana.Ndiyo maana kila siku natamani Rais Obama awe anakuja hapa Tanzania ili Tanzania tuwe wasafi kweli kweli Kwani sisi ni wachafu wa makusudi na wakujitakia na uenda tuna matatizo Katika akili zetu.

Kwasababu Kama tuna akili timamu tusingekuwa tuna kubali siku zote kulea uchafu na siku tunayosikia Rais Obama ,anakuja basi ndiyo tunafanya usafi.Kumbe tunaweza Kuwa wasafi tukiamua.Mungu atusaidie sana.

Chanzo:Facebook: Happy Katabazi
Oktoba 28 Mwaka 2014.


KIKWETE: TAIFA LIMETAMBUA MCHANGO WA BALOZI MAHALU




KIKWETE: TAIFA LIMETAMBUA MCHANGO WA BALOZI MAHALU  

RAIS Jakaya Kikwete akimkabidhi cheti cha heshima Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Profesa Costa Ricky Mahalu,kwa kutambua mchango wa Mahalu  kwa taifa  katika Kutunga Katiba iliyopendekezwa , akiwa  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
 Licha ya Mahalu kuwa mjumbe wa bunge hilo pia ndiye aliyekuwa Mwenyekiti  wa Kamati ya kutunga Kanuni zilizoliongoza Bunge kufanyakazi zake na pia Mahalu  alikuwa ni mjumbe wa  Kamati ya kuandika Katiba iliyopendekezwa na Bunge Hilo kuanzia Februali 18 hadi Oktoba 4 Mwaka 2014. 
Chanzo: Facebook: Happiness Katabazi (UB)

MAREKANI KUIPIGA 'TAFU' UB






MAREKANI KUIPIGA 'TAFU'  UB

Na Happiness Katabazi
CHUO cha Southern University kilichopo  jimbo la Louisiana  nchini Marekani kimetoa tamko la pamoja na Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB) cha Tanzania  juu ya makubaliano kushirikiana .

Akizungumza na Mwandishi  wa habari hizo, Dk.Elifuraha Mtaro ambaye  ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), anayeshughulikia Fedha na Utawala, ofisini kwake Mikocheni kwa Warioba, jijini Dar es Salaam Leo alisema UB imepokea kwa Furaha tamko Hilo ambalo amelishika Katika picha inayombatana na habari hii.

Dk.Mtaro alisema tamko Hilo ambalo limesainiwa na Seneta wa Jimbo la Louisiana, Rick Gallot Jr, lilitolewa hivi karibuni Katika mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika ambapo kwa Tanzania iliwakirishwa na Rais Jakaya na   mkutano huo uliitishwa  na Rais wa Marekani, Barack Obama.

Dk.Mtaro alisema kwa mujibu wa tamko Hilo Southern University  ambalo lilipata Baraka ya Seneti hiyo ambapo Seneti hiyo ya Louisiana ilitoa tamko la kiserikali  ambalo lilisisitiza  kwamba serikali ya jimbo Hilo   itaungana na serikali ya Tanzania  Katika kuendeleza  taaluma, utafiti na huduma  za Jamii Katika vyuo vikuu hivyo viwili.

 Imetolewa: Ofisa Habari wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB)
Oktoba 21 Mwaka 2014.







WANAWAKE NA DAWA ZA KUBANA UKE Mhhhh!

WANAWAKE NA DAWA ZA KUBANA UKE Mhhhh! 
Na Happiness Katabazi
NCHI ya Tanzania ni miongoni  mwa nchi ambazo zina baadhi ya wananchi wanaugua aina Mbalimbali ya ugonjwa wa Kansa maarufu Saratani.

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi Mbalimbali za Kimataifa zimejitoa kimasomamaso Kupambana na ugonjwa huo ikiwemo kutoa elimu ya ya kujikinga na ugonjwa Huo,kuamasisha watu wajitokeze kwa Wingi Kwenye  Vituo husika kupimwa ili wajijue mapema kama wana dalili au wameishapata maambukizi ya ugonjwa wa Kansa au laa.

Kutoa   elimu kwa waathirika wa ugonjwa wa Saratani Kuwa  wanatakiwa wafanye nini,nanini wasifanye na ni wapi wanaweza kwenda kupata matibabu.

Lakini kadri siku zinavyozidi kwenda baadhi ya Watanzania wenzetu hususani wanawake wenzangu wanaona jitihada hizo ni sawa na 'kumvalisha Mbu miwani'. Tena hawataki kuzisikia na wameweka masikio pamba.Inatisha sana.

Makala yangu ya Leo nitazungumuzia jinsi baadhi ya wanawake na wasichana walivyoamua kutumia baadhi ya Madawa ambayo mengine hata hayajaandikwa   tarehe Kuwa yalitengenezwa lini,wapi, mwanamke wa aina gani anatakiwa atumie na atumie kwa muda gani na dawa hiyo itamalizika muda wake wa matumizi lini?

Dawa hizo ambazo ni Sabuni  aina Misk Attahar Soap, Misk ambacho kimetengenezwa kwa mtindo wa kimiminika ambacho kimehifadhiwa Katika kichwa ambacho hata jina halijaandikwa, wala il itengenezwa  lini, kiwanda gani , wapi na muda wake wa matumizi unaisha lini?

Ieleweke wazi makala hii haimaanishi Kuwa nimethibitisha matumizi ya dawa hizo nimezigundua  kuwa zina  madhara.Hapana. 

Lengo la makala hii ni kuziuliza  mamlaka husika za serikali je, zinafahamu uwepo wa dawa  hizo?Je serikali inafahamu Kuwa baadhi ya wananchi wake hasa wanawake ndiyo watumiaji wa Kuu wa dawa hizo?

Je dawa hizo ni salama na Hazina viambata vyenye sumu ambazo mwisho wa siku watumiaji watakuja kudhurika?

 Je Tunaruhusiwa kuzitumia dawa hizo bila kuzitilia Mashaka Kuwa mwisho wa siku zinaweza kuleta madhara kwa wanawake Kama Kansa ya shingo ya kizazi ,ngozi na madhara mengine?

Kwa Miezi Sita sasa, nilipata fursa ya kuzungumza na wanawake mbalimbali na wasichana ambao wametumia dawa hizo.

Pia nilipata fursa ya kuzungumza na wauzaji wa dawa hizo kwa Nyakati tofauti ambao kila mmoja wake alinipa maelekezo ya jinsi ya kuzitumia na kunithibitishia Kuwa ni kweli ukitumia dawa hizo sehemu ya uke wa mwanamke  ina bana yaani inageuka Kuwa ndogo.

Wauzaji wa dawa hizo walinielekeza matumizi ya dawa hizo Kuwa hiyo Sabuni, mwanamke ambaye siku Tatu Kabla  ya  kwenda kukutana  kimwili na mwanaume  ,basi mwanamke Huyo anatakiwa akishamaliza kuoga ananawaa sehemu zake za Siri kwa kutumia sabuni hiyo ya Misk Attahar Soap.

Baada ya kunawa sabuni hiyo, misuli yake  ujibana na kufanya eneo lake la uke la mwanamke   kuonekana ni dogo na hivyo siku ya kukutana na mwanamme kimwili;

Mwanaume  Huyo bila kujua nini mwanamke Huyo alitumia Kabla ya kukukutana nae, Kuwa mwanamke huyo jinsia yake ya kike ni nzuri Kwani imebana na watoto wa mjini usema ' Kitu Mnato'', na haingiliwi Mara kwa Mara na wanaume Kumbe mwanamume huyo  Tayari kaishaingizwa 'Chaka'.

Kichupa Chenye maji mekundu, hicho kichupa kwa mujibu wa watumiaji na Wauzaji wamenieleza Kuwa ,maji maji hayo mwanamke hupaka Katika sehemu zake za Siri ili aweze kuondoa harufu Mbaya na pindi apakapo dawa hiyo unukia vizuri na endapo akikutana na mwanamke kimwili,inamshawishi mwanaume Huyo Kupenda kuendelea kufanya tendo Hilo zaidi na zaidi na mwanamke huyo.

Baadhi ya wanawake  wengine Utumia majani ya chai kubana eneo Lao la uke.  Wamenielekeza Kuwa wanachukua majani ya Chai mengi wanayachemsha Kwa kuweka kiasi kidogo Cha maji,majani hayo ya chai ya nachemka hasa, yakishachemka uyaipua na kuyaacha ya Poe.

Nakisha kuyachuja halafu wanayachukua Yale majani wanayaweka Kwenye chupa safi Tayari kwaajili ya matumizi.

Wamenielekeza Kuwa mtumiaji ambaye ni mwanamke anapotaka kwenda kukutana kimwili na mwanaume siku mbili Kabla, basi ulazimika Mara mbili kwa siku kunawa Katika sehemu zake za Siri Maji Yale yaliyochemsha kwa majani ya Chai ambayo uwa ni makali sana huwezi kuyaweka mdomo na hatimaye sehemu yake ya uke ubana na Kuwa ndogo.

Kuhusu hivyo vichupa vitatu vilivyopangana  hivyo kwa mujibu wa wauza duka na watumiaji wanasema majimaji hayo yametengenezwa na zao la  Mchaichai, na Utumiwa na mwanamke Yule ambaye sehemu zake za Siri zina majimaji hivyo , aina hiyo ya dawa inayotengenezwa kwa mchaichai ufanya sehemu zake za Siri mwanamke Huyo Kuwa kavu.

Na kichupa hicho cheupe ambacho kina Maji mazito meupe ambacho hakijaandikwa hata jina ,tarehe ambayo ingeonyesha kimetengezwa wapi na lini ambacho nacho  uitwa Misk, ambacho mwanamke anayetaka kwenda kukutana kimwili na mwanamume saa mbili Kabla  anapaka Katika sehemu yake ya uke tone Moja Kisha avaa  nguo anaenda zake kukutana kimwili na mwanaume Huyo.

Na baadhi ya watumiaji niliongea nao kwa Miezi Sita sasa wameniakikishia Kuwa ni kweli dawa hizo ukizitumia zinabana misuli ya uke na mwanamume uona mwanamke Huyo haingiliwi Mara kwa Mara na wanaume.Kumbe wizi mtupu.

Nimefanikiwa kupata aina hizo za dawa licha kuna baadhi ya wanawake wanaofanya Biashara za nguo kutoa China kuleta Tanzania ,pia wameniambia kuna kifaa kingine ambacho hapa nchini wakikileta kinauzwa Sh.35,000.

Hicho kifaa mwanamke anayetaka kwenda kukutana na mwanamume siku Moja Kabla ukiingiza ndani ya uke kifaa hicho Kwa dakika Kadhaa na Kisha ukitoa na baada ya muda uke wa mwanamke Huyo unakuwa umebana sana.

Lakini hata hivyo Hao watumiaji wa dawa hizo Kwa Nyakati tofauti pamoja na maswali mengine niliyokuwa nikiwauliza ,nilipokuwa nawauliza je tangu walipoanza  kutumia dawa hizo zimeweza kusaidia kuwazuia Waume, wapenzi wao wasiwasaliti Katika mahusiano Yao ya kimapenzi?

Wengine walipandwa na jazba na Kusema licha ya kubana uke wao kwa dawa hizo ,wanaume wao wamekuwa na mahusiano na wanawake wengine Hali iliyosabisha baadhi Yao HIvi sasa kuacha kutumia dawa hizo Kwani wamenitumia Kwa Lengo la Kuwauliza Waume zao lakini Waume zao hawatulii.

Na kwamba walichoamua hivi sasa Fedha zao wanazimalizia Katika kujipambana,kufanya vitu vinavyo starehesha nafsi zao.Lakini Hakuna hata mtumiaji mmoja aliyeniambia amewahi kupata madhara kutoka na matumizi ya dawa hizo, ila hawafahamu siku za usoni uenda wakaja kupata madhara.

Wanawake mnatumia dawa hizi naomba mnisamehe sana kwa haya nitakayoyasema Kama yatawakwaza.Maana miili ni yenu na Fedha za kununulia dawa hizo ni Zenu.

Minajiuliza HIvi hawa wanawake wenzangu ambao wameamua kujilipua na kuanza kutumia dawa hizo ,hivi wanachokitafuta hasa ni kitu gani?

Maana baadhi ya wanawake kwa makusudi tumeamua kuwa 'Maalbino wa Kutengenezwa' yaani kujipaka mikorogo ambayo inachubua ngozi na kutuaribu vibaya sana?

TDFA, Madkatari kila kukicha Maskini ya Mungu wanaelezea madhara ya mikorogo hatusikii na tunawaona wanaowakataza msitumie   mikorogo ni wanasesere na wa nawaonea wivu.

Minasema HIvi hipo siku tutawauguza Maradhi yasiyotibika kutokana na hayo matumizi ya mikorogo na Madawa ya kubana uke  kwa Lengo la kuwaahada  wanaume.

Hivi minikiwaita hawa wanaotumia  dawa hizo ni sawa tu na 'majambazi wasiyotumia  silaha' , nitakuwa nakosea?

Halafu ni wanaume gani Hao mnaowaongopea na hayo Madawa? Ni hawa hawa wanaume waliopo Kwenye kizazi hiki Cha kamasi ukipenga kamasi basi kizazi hicho kinasahaulika?

Ndiyo Mnataka Kuwahadaa kimapenzi hawa wanaume ambao Wengi wao hawana fedha, mabahiri na siku hizi wamepachikwa majina haya 'wanaume suruali,wanaume SACCOS  yaani wakopaji ,hawana Fedha' ili wawape Fedha?

Baadhi ya Wanaume wenyewe huko mitaani siku hizi wengine wanakiri kabisa Kuwa Utawala wa Rais Jakaya Kikwete umeweka mazingira mazuri kwa wanawake Kuwa na kipato na wanawake  Wengi hivi sasa wapo  Katika ngazi za uongozi ukilinganisha na Miaka ya nyuma na wengine wapo Kwenye njia Kuu za uchumi na kwamba   wanawake wengi hivi sasa wanafursa nyingi za kujipatia kipato kuliko wanaume?

Hali imebadilika HIvi sasa baadhi ya wanaume ndiyo wamekuwa mstari wa Mbele kutaka wahongwe  Fedha,mali na wasaidiwe na wanawake.

Kabla ya kuandika makala hii pia nilienda Kuwapelekea wataalamu wa Madawa Wawili wazisome dawa hizo na wazielewe, waliniambia watumiaji wa dawa hizo wanachokitafuta watakipata.

Na wakasema hao wagunduzi wa dawa hizo za kubana uke ni kwanini wasingegundua  dawa za kutibu Ugonjwa wa Ebola!.

Na waliitimisha kwa kutaka serikali kupitia dawa hizo nilizozikusanya ikazifanyie utafiti ili mwisho wa siku serikali itoe Matokeo ya utafiti huo kuwa dawa hizo Hazina madhara au zina madhara kwa watumiaji .

Naomba mamlaka husika itoe tamko kuhusu matumizi ya dawa hizo ni haramu au halali.

Na Kama ni haramu basi wale waliokuwa na fikra za kutaka kuanza kuzitumia wasi thubutu kuzitumia.

Na wale waliokwisha zitumia waendelee au wasiendelee kuzitumia na wale wenye hofu ya matumizi ya dawa hizo Kuwa ni haramu au siyo haramu ,hofu hiyo iwaondokee.

Mwisho, wanawake mjenge tabia za kujiamini na muondokane na muda wote kuwaza mawazo ya kufanya ngono.

Kuna mambo mengi sana ya kufanya ambayo ukiyafanya kikamilifu na unavyopaswa,mtaondokana na balaa hili la matumizi ya dawa hizo za kubana uke ambao Kwa  vinywa vyenu mmekiri Kuwa licha mmekuwa mkitumia dawa hizo ,wapenzi na Waume wenu wamekuwa wakisaliti mapenzi yenu na mwisho wa siku wanaokuja kupata madhara ya Kiafya ni Nyie na Hao wanaume,wapenzi watawatelekeza.

Leo hii kila kukicha tunasikia Kansa inawashambuliwa wanawake sana.Tujiulize ni kwanini inawashambulia sana wanawake tena Kansa ya shingo ya uzazi?

Isije Kuwa matumizi ya Madawa ya kubana uke yanayotumiwa na wanawake na wasichana nayo yanachangia ongezeko Hilo la maambukizi ya Kansa!

Tubabirike, tuache kuiga na tuache kutumia dawa ambazo mwisho wa siku zinaweza Kuja kuleta madhara Katika Afya zetu.

Wakati mwingine Huwanajiuliza ila sipati Jibu Kuwa HIvi hawa wanawake wanautumia mikorogo Kukoboa ngozi zao wakati mikorogo hiyo imekatazwa na wataalamu , HIvi ni wazima kweli kichwani au ni mahayawani?

HIvi Kama siyo uhayawani ,kutojiamini na kutojitambua ni kitu gani?Wataalamu wa Madawa wakiwemo TDFA msitumie Madawa hayo na Jeshi la Polisi inayakamata hizo cream, lotion, sabuni zenye viambata vya sumu kwasababu singlets madhara hawasikii hawa 'Maalbino wa Kutengenezwa' yaani wanawake wanaopaka mikorogo.

 Mbaya zaidi wanawake wengine ni wasomi,wanaume zao ni wasomi na wana familia zinazowategemea.

Kwa makusudi wanakaidi katazo Hilo la wataalamu na serikali ,ndiyo kwanza wanaenda kununua mikorogo na kuendelea kujichubua ngozi zao.

Mindiyo maana nasema hawa 'Maalbino wa Kutengenezwa' siyo wazima Katika ubongo wao, Kwani wanawake Wengi wanajipaka mikorogo HIvi sasa wameishakuwa watumwa wa poda kama Enjoface,Foundation ambazo ujipaka usoni muda wote ili Kuonyesha umma uso wake una rangi sawa ,Hauna mashimo na Hauna Michilizi yakuonyesha Mishipa ya Damu ambayo Mishipa hiyo uwatoka wanawake wanaozidisha matumizi ya mikorogo.

Fedha yako Mwenyewe  Kwanini uruhusu ikuletee madhara na ikutese? Au watumiaji wa mikorogo ni viziwi hawasikiagi TDFA,wataalamu ,Polisi wakiwa watu wasitu mie mikorogo? Au ni vipofu uwa hawaonagi watumiaji wa mikorogo walivyoonza madhara mbalimbali ikiwemo NGOzi zao kuaribika vibaya, kupata madhara ya Figo?

Bado hamjachelewa,acheni matumizi ya Madawa yaliyokatazwa na mamlaka husika Kwani ipo siku mtalia na kusaga meno. Watafuteni wataalamu wa Madawa watawapatia Madawa mazuri tu yasiyo na madhara Kama Lotion mtapaka na ngozi Zenu zitakuwa nzuri tu na kuondoa mikunjo usoni,alama,ngozi itakuwa nzuri.

Mwanamke Kama ni mrembo ni mrembo tu siyo lazima upake mikorogo ya kujichubua ngozi.  Mbona Mimi napaka Lotion aina ya OLAY TOTAL EFFECTS 7in one na bado nakuwa mwanamke mrembo?

Wanawake jengeni utaratibu wa Kuwa na marafiki madaktari, wataalamu wa Madawa waliobobea ambao watakaokuwa wa nawashauri nini mtumie Katika ngozi Zenu na vitu gani msitumie.

Nawaambia hili Kwani Mwenzenu nilibaini Hilo tangu Mwaka Jana, nina mtaalamu wangu wa Madawa ambaye ni mmiliki wa Madukani Pharmacy , Iliyipo Sinza Madukani, Dk.Kessy ndiyo amekuwa Mshauri wangu mkubwa Katika masuala ya Kutengeneza ngozi kwa kunielekeza kitaaluma .' Maalbino wa Kutengenezwa' . Hamjachelewa ,badilikeni sasa.

Mungu Ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Oktoba 17 Mwaka 2014.







HALIMA MDEE TULIA UZAE








HALIMA MDEE,TULIA UZAE
Na Happiness Katabazi
MAKUNGWI  na wanawake waliotuzidi umri upenda Kuwaasa watoto wa kike hususani wale walitimiza umri halali wa kuingia Kwenye mahusiano hususani  Kwenye ndoa Kuwa :

' Mwanamke yeyote aliyekamilika kuitwa mwanamke na aliyefundwa anapaswa kufanya vurugu, utundu chumbani wakati akiwa na mumewe au Mpenzi wake wakifanya tendo la ndoa '.

Nimelazimika kutumia Msemo huo wa Makungwi  kwasababu , kwa zaidi ya wiki Moja sasa tumeshuhudia Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (Bawacha) Halima Mdee (35) akifanya vurugu na kupingana na amri halali za Jeshi la Polisi Mkoa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alitangaza kuyapiga marufuku maandamano yaliyokuwa yameandaliwa na Mdee lakini Mdee na wenzake waliipuuza amri hiyo ya Kova na mwisho wa siku Oktoba 4 Mwaka huu, Mdee na wanawake wachache wa Chama hicho walijaribu kuandamana wakaishia  kusambaratishwa na Polisi na Kukamatwa kupelekwa Katika Kituo Cha Polisi Oysterbay 

Oktoba 6 Mwaka huu, Mdee na wenzake wakafunguliwa Kesi ya jinai mbele ya Hakimu Janeth Kaluyenda, Wakili wa Serikali Mkuu, Bernard Kongola alidai Mbali na Mdee washitakiwa wengine ni   Rose Moshi (45), Renina Peter ‘Lufyagila’, Anna Linjewile (48), Mwanne Kassim (32), Sophia Angel (28), Edward Julius (25), Martha Mtiko (27) na Beatu Mmari (35).

Kongola alidai kuwa washtakiwa hao Oktoba 4, 2014, wakiwa Mtaa wa Ufipa, walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi (SP), Emmanuel Tillf kwa niaba ya Jeshi la Polisi kitendo ambacho ni kinyume na Kifungu cha 124 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Katika shtaka la pili, siku hiyo ya tukio katika eneo hilo, washtakiwa hao wanadaiwa wote kwa pamoja , walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kutembea kwenda kwenye Ofisi ya Rais Ikulu .Alidai kuwa kosa hilo ni kinyume na Kifungu cha 74 na 75 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Na washitakiwa Hao walikana Mashitaka ila Masharti ya dhamana walishindwa kutimiza,Mahakama ikaamuru wapelekwe gerezani hadi Jana walipopata dhamana.

Kesi hiyo ikaairishwa  hadi Oktoba 21 Mwaka huu,itakapokuja kwaajili ya washitakiwa hao kusomewa maelezo ya awali kwasababu upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika.

Mdee ni msomi wa Sheria na nimiongoni mwa wanasiasa wachache vijana wenye ujasiri wa kujitokeza hadharani kukataa jambo ambalo yeye anafikiri jambo Hilo halina maana.

Mimi Nampongeza kwa kipaji  hicho tu Cha uthubutu wa kujitokeza hadharani Mara kwa Mara kupinga licha Mimi binafsi  wakati mwingine uwa sikubalini Sababu zake nyingine anazotumia kupinga jambo Fulani.

Lakini nitajisikia vibaya   Kama sitampongeza  Mdee ambaye ki umri tupo sawa ,kwa kuweza kuchaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa BAWACHA.

 Hakika ameandika historia ya kijana mwenye umri Kama wake kuaminiwa na Chama Chake kupewa nafasi hiyo ambayo anaongoza wanawake ambao ni wanachama wa CHADEMA ambao wengine wamemzidi yeye na mama yake umri.Hongera Mdee kwa ushindi huo.

 Maana matendo mengine anayoyatenda ya kuamasisha vurugu, uzushi ni wazi kabisa anaonekana ni mwali 'msungo'. Yaani ni mwanamke ambaye hajafundwa Mafundo ya kike au kama alifunda basi anayapuuza.

Anachokifahamu yeye ni Mafunzo ya darasani na siasa chafu za ugomvi  ambazo zinazidi  kumshushia heshima yake Kwa Wapiga kura wake wa jimbo la Kawe, Jamii ya wapenda ustaharabu, Amani na Utawala wa Sheria na wasomi.

Kinachonikera kwa Mdee hii tabia yake ya kufanya 'Usela Mavi' wakati amelelewa Katika familia ya wasomi Kwani baba yake ni msomi na Mdee  Mwenyewe amepata fursa ya kusoma shule lakini tunamshangaa anatenda matendo ambayo hawapaswi kutendewa na mtu Kama yeye.

Mdee ni msomi wa Sheria na msomi yoyote wa Sheria, Mwaka wa kwanza wa shahada ya kwanza ni lazima ufundishwe  somo la Criminal Law ambalo somo Hilo mwalimu pamoja na mambo mengine anatumia Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya Mwaka 2002 ( Penal Code).

Na hiyo Sheria inaweka wazi makosa mbalimbali kwa Kifungu kwa Kifungu Mdee amelisoma na kufaulu somo Hilo na anafahamu Kuwa ndani ya Sheria Hilo Kuwa kuna kosa la kukaidi amri ya Jeshi la Polisi, kufanya mkusanyiko haramu Adhabu zake ni zipi.

Lakini Mdee ambaye amekuwa akijitapa eti yeye ni Mwanasheria mzuri ndiyo amekuwa miongoni mwa wasomi wa Sheria ambao ameshitakiwa Kutenda  matendo ya kuvunja Sheria wazi wazi kwa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikimtaka asiandamane kwa Kigezo eti Rais Jakaya Kikwete amealika  Ikulu.

Nimuulize Halima hivi Rais Kikwete ni Hawara yako,ndigu yako hadi mkutane sehemu huyo Kikwete akupe mualiko uende Ikulu ,wewe na hao wafuasi wako bila Katibu wa Rais kujua mualiko huo?

Rais ni Taasisi kwa wale tunaofahamu, hivyo huwezi kujikurupukia tu ukaamka Leo ukachukua  kundi la wahuni wenzio na mabango juu ukasema unaenda Kumuona Rais Ikulu eti Rais Kikwete amekupa Mwaliko?

Kama siyo kumsingizia Rais na kumchonganisha Rais Kikwete na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ni kitu gani? 

Maana Kama Rais Kikwete alikualika kweli.Si haraka sana Rais angetengua amri ya Kamanda Kova ya kuwazuia msiende kumuona Ikulu?

Unafikiri ni kwanini amri ya Kova iliendelea kubaki Kama ilivyo? 

Jibu ni Jepesi tu ,Halima ni muongo, Mzushi na aliyekuwa anataka kujipatia umaarufu wa kijinga Kuwa eti Mwaliko wa Rais Kikwete amemwalika Ikulu. 

Alichokuwa akikitafuta Mdee ni kutaka kujionyesha yeye ndiyo Mwenyekiti Mpya wa BAWACHA na kwamba ni ngangari kweli kweli kuliko Mwenyekiti aliyepita Suzan Lyimo na hivyo anaushawishi mkubwa wa kuweza kuwashawishi wanachama wanawake wa Chama hicho waweze kuandamana mwisho wa siku sifa anapata Mdee Kuwa ni mwanamke Shujaa na aliogopi jeshi la polisi, Kumbe ni Ujinga mtupu.

Kama Mdee kweli wewe uliogopi Jeshi la Polisi kwanini ile Oktoba 4 Mwaka huu, mlivyo andamana ,Polisi ilivyo watawanya ,kwanini wewe uliogopa KISAGO ukakimbia Kwenda kujificha ili kukwepa kipondo Cha Polisi?

Kama wewe ni Shujaa kweli kwanini Oktoba 7 Mwaka huu, ulipofikishwa Katika Mahakama ya Kisutu  kwanini uliyakana hayo Mashitaka?

Maana Kabla hujafikishwa mahakamani ulikuwa ukijigamba kupitia vyombo Vya Habari Kuwa kuandamana ni Haki yako na hutakiwi kuomba Kibali?

Kama wewe ni Shujaa kwanini ulikubali kupewa dhamana?

Shujaa au kamanda gani anaogopa kukaa gerezani kweli licha ni kweli dhamana ni Haki yako ?

Ningekuona Wewe ni Shujaa  kweli usingeomba dhamana ungesema upo Tayari kwenda kukaa gerezani ili ukiwa kule gerezani pia huweze  kutoa hoja zako kwa mahabusu wa kike zinazohusu  msimamo wako na Chama Chako Cha kuipinga Katiba iliyopendekezwa Bunge na kujua matatizo yanayowakabili.

Kamanda  gani akiona kilungu Cha Polisi na Gari za Maji ya kuwasha'Kikojozi' Ana kimbia?

Unatakiwa ukae upambane na Polisi Kwani ulijigamba licha Polisi imekataza maandamano yenu ,wewe na wanachama wako mtaandamana na nauogopi Polisi.

Mdee Tanzania hii unayoiona hivi sasa watu wanaishi kwa amani tofauti na nchi za wenzetu , Elewa Kuwa  watu walipoteza Uhai wao,Jasho Lao wakaijenga nchi hadi Leo hii wewe umeikuta,ukasoma, umepata madaraka ambayo ya nakulevya hadi unaanza jeuri ya kukaidi amri ya Jeshi la Polisi.

 Mamlaka husika hazitakuacha ufanye huo uhuni wako ambao mwanamke yeyote mwenye haiba  ya kike hawezi kufanya .

Na Mbaya zaidi ulichokuwa ukikipigania Cha kutaka Rais Kikwete asipokee Katiba iliyopendekezwa na Bunge hujafanikiwa Kwani Jana jioni Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk.Mohamed Shein wameipokea Katiba kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta na tumemshuhudia Rais alishindwa kuficha hisia zake na akajikuta akitamka zaidi ya Mara mbili kwamba anayofuraha sana sana kuona tendo Hilo la Kihistoria ilifanyika chini ya uongozi wa serikali yake na akasema kabisa Katiba  ile ni nzuri sana na awashawishi Watanzania waipigie kura ya ndiyo.

Ila Kwa mwanamke ambaye Hana haiba ya kike  na Mwanamke ambaye hajithamini na hatambui mambo yapi  mwanamke afanye na mengine asifanye ,atayafanya Kama wewe Mdee ambaye tunakuhesabu ni msomi,kiongozi lakini unashiriki hadharani Kutenda matendo ya kuvunja Sheria. 

Kiongozi yoyote mzuri anatakiwa awe ni mfano wa kuwaongoza wafuasi wake wafikie malengo waliyoyakusudia.

 Sasa  Mdee  ambaye ni kiongozi lakini unawaongoza wafuasi wako waende njia isiyo sahihi kwa kushiriki vitendo vya uvunjifu wa sheria na matokeo yake mmeishia kushitakiwa na kulala Gerezani na kujitia nuski.

Halima  tambua kuwa hata kama mwanamke awe na fedha ,mali ,madaraka kiasi gani bado mwanamke anatakiwa hajiheshimu na afanye matendo ambayo mwanamke anatakiwa atende .

Siyo mwanamke asimame hadharani atende matendo ya kihuni huni  ambayo tumezoea kuona yanatendwa wanaume wahuni wahuni au wanawake wahuni wahuni tu ,Kama wewe ulivyotenda.

Labda ni mwambie Mdee  vitendo hivyo vya ukahidi na Kauli ambazo hazipaswi  kutolewa kwenye kinywa Cha mwanamke mwenye haiba ya kike,Hupaswi kujifanya.

Wanaopaswa kufanya matendo Kama hayo ni baadhi ya wanawake kama Asha Ngedere,  na wanawake wengine ambao kufanya vitendo vya kihuni, kusutana na wengine hadi wameunda vikundi vinavyokodisha kwaajili ya kuchamba watu, ambao wanawake hao wanaofanya vitendo hivyo vya kihuni wanapatikana sana huko uswahili mitaa ya Mburahati Madoto, Kigogo Luhanga, Mburahati kwa Binti Kahenga ,vurugu ndiyo sifa zao tena wanaona fahari kuona watoto wao wanafuata nyayo za mama zao za kufanya vitendo Vya kihuni na kishenzi.

 Mdee Hupaswi kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria na vya kihuni huni, waachie wakina Asha Ngedere  , wewe unapaswa hivi sasa ukae katika ofisi mpya ya Bawacha ,  ubuni mipango yako yakuwaletea wanachama wako na taifa maendeleo kwa njia amani.

Una mambo mengi ya kufanya siyo kuanzisha maandamano haramu .

Hivi kweli unashindwa kuketi kitako ukaanzisha hata taasisi yako binafsi ,Ukaanda harambee za kuchangia kutokomeza mimba za utotoni, au kufanya utafiti wa ni kwanini wanawake wengi wanashambuliwa na ugonjwa wa UTI na mambo mengine,ukaalika watu wenye Fedha zao wakashiriki harambee wakachangia Fedha utapata za kuendesha Programu hizo?

Lakini umeama kujigeuza Kituko Mbele ya Jamii ya wanawake wastaarabu ya kushiriki kushinikiza kufanya maandamano haramu. 

Kama Fedha, madaraka unayo.Tatizo Lako nini  Mdee  hadi unaamua kushiriki vitendo hivyo Vya kihayawani ambayo vinakushushia heshima?

Umri ndiyo huo una unazidi kukutupa mkono na ukae ukijua  hivyo vitendo vya 'Usela Mavi' unavyofanya vina mwisho  wake.

Mwanamuziki Banza Stone aliwahi kuimba ' upatapo fahamu ujue Umepotea'.

Ebu Mdee  achana na usela Mavi , anza kuweka fikra na matamanio ya siku Moja na wewe uitwe mama wa Fulani.

Mshirikishe Mungu Katika matamanio hayo ,Mungu atakupa mtoto na ukishampata mtoto ni wazi utakuwa busy sana na kuangaika na mambo ya mtoto na familia yako kwa ujumla na utajikuta unaoendokana na vitendo hivyo Vya kihuni  ambavyo mwanamke mkorofi akisha bahatika kupata mtoto wake anaachana navyo  Kwani anaona akiendelea  anavyo anakuwa kama anamdhalilisha mtoto wake.

Achana na wazimu huu unaoufanya wa kujifanya wewe ni jike dume, umesababisha watu kuanza kuhoji Kuwa Mdee ni mwanamke kweli?Anaujua uchungu wa Mwana?Na je Halima amebahatika kupata mtoto?

Na Wengi wanahoji hivyo kwasababu wanasema wanashangaa na kujiuliza kuwa hivi Mdee alishawahi kubeba mimba na akalea mtoto na kuitwa mama hawezi kufanya hayo anayoyafanya? 

Wanajiuliza   Mdee  ni mwanamke wa aina gani ambaye hana uchungu hadi anaamasisha wanawake wa Chadema  waandamane Katika maandamano  haramu ambayo wanaenda kupigwa ma Polisi na kufunguliwa Kesi mahakamani na hadi wakalala gerezani siku Moja?

Na wengine wanadiriki Kusema Mdee pamoja na usomi wake na madaraka aliyonayo ,anaitaji kutafutiwa Makungwi kama Bibi Hindu, Bibi Chau wamfunde ili ajue mwanamke anatakiwa aweje ,avae mavazi gani, na vitendo gani afanye Mbele za watu na yapi asifanye.

Maana licha ya madaraka na usomi aliyonayo,wakati mwingine tunamshuhudia akitenda na kuongea mambo ambayo mwanamke aliyefundwa kuwa mwamke na kuwa kiongozi , hapaswi kuyatenda Kama ya kupayuka payuka ovyo ovyo tena wakati mwingine kwa hoja zisizo na mashiko utafikiri hayawani.

Kuna wanawake wako Tanzania  mashughuli dini Kama Dk.Asha Rose Migiro, Profesa Anna Tibaijuka na wengine Wengi, huwezi kuwasikia wakifanya vitendo Vya kihuni huni na vya kuamasisha watu Wavunje Sheria.Wao ubishina Kwa hoja, ustaarabu.

Bado namkumbuka   aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya  Chama cha Tanzania Labour(TLP), Getrude Pwila  Enzi zile Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP- Omar Mahita.

Kwa mama huyu alikuwa ni rafiki yangu nalilikuwa naandika Habari za Chama Cha TLP kinachoongozwa na 'mume wangu wa zamani', Agustine Mrema.

Pwila alikuwa ni mwanamke machachari sana kila uchao alikuwa akiwaamasisha wanawake wa TLP waandamane Katika maandamano haramu hadi Wizara ya Mambo ya Ndani huku wakiwa wamevua  Fulana wamebaki na Sidiria tu na walikuwa wakiaa nje ya ya Wizara ya mambo ya ndani tangu asubuhi hadi jioni wakitoa maneno ya kulikashfu Jeshi la Polisi, Rais aliyekuwa madarakani, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Msajili wa Vyama Vya Siasa, Mahundi.Na zoezi Lao la kubaki NA Sidiria walijifanya zaidi ya Mara tano Kipindi kile Cha Miaka 2002- 2004.

Mimi ,Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Jocye Mmasi tulikuwa ni miongoni mwa waandishi tuliokuwa tukishiriki maandamano hayo na kuandika Habari.

Leo hii Pwila amepotea Katika ulingoni wa siasa, hasikiki tena na ukizungumza naye anajutia kitendo kile alichokuwa akijifanya cha kuongoza wanawake wa TLP kuvua nguo na kubaki  na Sidiria pale nje ya Makao makuu ya Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Sasa na wewe Mdee ukae ukijua wewe ni Kama una beep tu, hata hujamfikia Pwila Kwani Pwila alikuwa anaushawishi mkubwa kwa wafuasi wake walishapigwagwa sana Polisi lakini mwisho wa siku walipokuja kutambua uhuni ule waliokuwa wakiufanya kwanza ulikuwa ukiwadhalilisha  wao wenyewe binafsi.

Walipokuja  kubaini wao kama wanawake wa TLP walichokuwa wakikipigania kwa njia  ya maandamano haramu eti jeshi la Polisi lina mnyanyasa Mrema ni batiri .

Waliachana na vitendo hivyo na ndiyo ikawa Chanzo Cha umoja wa wanawake TLP kusambaratika na wanawake Wengi kaumua kuiama  TLP  kwasababu ya kubaini Pwila alikuwa alikuwa alikuwa akiwaongoza Kutenda vitendo Vya Uvunjifu wa Sheria ambavyo mwisho wa siku walikuwa wakaishia kupigwa virungu na Polisi ,kufunguliwa Kesi mahakamani na kupelekwa gerezani.

Sasa wanawake wenye akili timamu ambao mnaoamini Katika Utii wa Sheria bila shuruti  wa  Bawacha  ,mfano huo hapo  juu wa Pwila msiuupuze Kwani sote ni mashahidi Enzi za mtangulizi wake Mdee, Suzan Lyimo akiwa Mwenyekiti wa Bawacha, hatukuwa hi kumshuhudia Lyimo akiwaamasisha  wanawake washiriki vitendo Kama hivyo Vya kuvunja  Sheria Kama afanyavyo Mwenyekiti Mpya wa Bawacha ,Mdee  ambaye hata Ofisi mpya ya Bawacha ajaikaa vizuri, ajaeleza kwa vitendo vipaumbele vyake ni nini.

Pwila hakuwa na elimu kama Mdee  ila alikuwa na ushawishi na Tayari alikuwa ni Mzima , Mdee  ni kijana na bado    ana Muda mrefu Mungu akimjalia  wa kulitumikia taifa hili  na kujiandalia rekodi safi.

Sasa kwa mtindo huu wa Mdee  tena mtoto wa kike kutaka Kupambana na Polisi kwa jeuri ya kijinga na Mbaya zaidi unawaamasisha wanawake wachama Chake washiriki vitendo hivyo ,vitamsababishia kumporomosha au kumfuta  Kwenye Medani za siasa nchini Kwani Watanzania ni watu wasiyopenda ni wapenda Amani na utulivu.

Tambua Mdee  wewe ni kiongozi kijana ,unapofanya mambo mazuri au Mabaya sifa hizo unazipata wewe na vijana wenzako kwa ujumla.

Hujachelewa  unaweza kubadilika licha Tayari umeishaingia Kwenye rekodi Mbaya ya Watanzania Kuwa Mdee  ni kiongozi ambaye analazimisha maandamano ambayo yamekatazwa na Polisi hivyo wewe ni Mpenda Vurugu.

Na Kwa taarifa yako Mdee  ,siasa hizo unazotaka kuzileta hapa  Tanzania, haziwezekani,ndiyo maana wewe na Chama Chako kila mlipokuwa mkijaribu  kufulukuta kuhusu kutaka kufanya maandamano  yenu mliyosema mtaandamana nchi nchi nzima bila kikomo, hamjafanikiwa kwasababu Watanzania na vyombo Vya dola havitaki aina ya siasa mnavyotaka kulileta hapa nchini .

Kwasababu mbinu yenu ya kufanya siasa ilikuwa haina  kheri zaidi ya kutuletea vurugu na mbinu yenu ya kufanya maandamano imeshadoda sijui mnabuni mbinu gani nyingine ili iwarejeshee umaarufu kwasababu Tayari Chama chenu kinashuka Kwa kasi Umaarufu kwasababu mmoja tu ya kulazimisha matendo yanayovunja Sheria Kama maandamano haramu.

Mdee tambua hapa Tanzania  kuna wanawake wameshika   nyadhifa kubwa na nyeti nchini,lakini wanaojiheshimu na niwatiifu wa Sheria za nchi Yao, watiifu na Kamwe hutawaona wafanya vioja Kama unavyofanya wewe Vya kushiriki vitendo Vya Uvunjifu wa Amani kwa makusudi.

Wanawake Hao wengine wapo Kwenye majeshi yetu ,serikalini na taasisi mbalimbali za kiraia wametulia tulia.

Na wana uwezo wa kusaliti nchi,au kuanzia vurugu na wanaushawishi  na mvuto mkubwa sana kuliko wewe lakini wametulia wanaipenda nchi Yao na wanatii Sheria za nchi bila shuruti.

Iweje wewe Mdee ambaye umedhiirisha wazi Huna Nguvu wala karama  ya kushawishi wanawake wote wa Chadema wakatii agizo  Lako la kuwataka wanawake wa Chadema waandamane kupinga Katiba iliyopendekezwa na Bunge Kwani  tulishuhudia siku ulipo ulipoandamana ukashughulikiwa.

Ni idadi   ndogo sana ya wanawake  wa Chadema waliitikia agizo Lako  na wanawake wengine wa Chadema ambao tuna wafahamu ambao tupo nao mitaani, wasomi na wamama watu wazima wenye akili timamu na wenye utashi walikataa kushiriki   Walisema hawawezi kukubali kuingizwa kwenye  matatizo na Mdee, kwasababu wanamfahamu Mdee ni mtu wa aina gani na mwisho wa siku watakuja kuonekana wao ni mahayawani Kwani wasingekuwa mahayawani wasingeitikia wito haramu wa Mdee  wa kwenda kushiriki maandamano haramu na kweli hawakwenda. 

Ona sasa ukahidi wako kwa Jeshi la Polisi umekufanya wewe na wafuasi nane muingie Kwenye orodha ya washitakiwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwasabu hiyo Tayari mmeishakuwa  ni Kama watumwa wa Mahakama hiyo ambao mtatakiwa   mfike tarehe itakayopangwa wakati ulikuwa na uwezo  kabisa wa kujizua  usitende makosa unayoshitakiwa nayo.

Sasa  utajikuta badala ya kwenda kutimiza majukumu mengine ,unakwenda kushinda Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia hatima  ya Kesi yako.

Muulize Mzee Mabere Marando,Agustine Mrema ,Samson Mwigamba na wengine wanafahamu  vizuri madhara ya kushitakiwa kesi za aina hiyo uliyoshitakiwa nayo hadi leo wamekoma kushiriki vitendo kama hivyo ulivyoshitakiwa nayo.

Mimi napenda sana kukaa nyuma ya wanasiasa wa vyama vyote na kufualitia matamko wanayoyatoa na uchapaji Kazi wao.Ila nachukizwa mwanasiasa yoyote ambaye anaamasisha wafuasi wake watende matendo ya kuvunja Sheria za nchi na kuhatarisha Amani ya nchi kwa makusudi.

Hii tabia sipendi Kwani mwisho wa siku wanatumia ni wafuasi siyo viongozi Hao wakuu na hata wanapopelekwaga gerezani wanasiasa wenye vyeo Vya juu  huifadhiwa  Kwenye vyumba vyenye hadhi wale wafuasi wa kiongozi Huyo uwekwa Kwenye selo ya 'Kajambanani'.

Mdee Jana Oktoba 8 Mwaka huu,  wakati unaondoka Katika Mahakama ya Kisutu ulitamka baadhi ya maneno Kuwa ulivyolala gerezani Juzi wala hawajakukomoa.

Hivi kwani kuna mamlaka ilikuwa imepanga kukukomoa ulalae gerezani kwa makusudi?Kwani ulivyokuwa gerezani ' ulikula Bata'.

Huo uongo wadanganye watu ambao Hawajawahi kutembelea magezera na kupata Habari za Magereza wanayolala mahabusu na hawajawahi kuona picha za magereza yetu.Kama kule gerezani ulikolala  Juzi ulikuwa 'unakula Bata', kitu gani sasa kimekufanya urudi uraiani?

Hayo ni maneno ambayo umejitutumua  tu Mbele za watu ila naimani ukipata wasaa na kukaa peke yako,HIvi sasa utakuwa unajua ni kwanini ulitenda makosa   yaliyosababishwa ufunguliwe Kesi mahakamani maana hata Askari Magereza wenyewe wanaowalinda  Wafungwa,mahabusu lakini  kila siku wanasema  gerezani siyo sehemu nzuri ya Mtu kupelekwa na ndiyo Mtu yoyote akitoka gerezani Kama ni muumini wa dini ya Kiislamu anaenda kufanya Kisomo na Kama ni Mkristo anaenda kufanya Misa Maalum ya kumshukuru kumalizana na Mkosi wa kulala gerezani na kushitakiwa mahakamani lakini ajabu wewe mwanamke wenzetu unashangilia jambo hilo. Ni ajabu sana.

Sasa namshangaa Mdee ,anavyotuambia 'amekula bata' gerezani.Kwa hiyo Ana Ana maanisha Kuwa HIvi sasa  Magereza yetu ni mazuri sana hadi watu tuanze kuvunja Sheria kwa makusudi huku uraiani ili tupelekwe gerezani nasisi 'Tukale Bata? 

Nijuavyo Mimi Hakuna bingwa wa Shida na Mara kwa Mara mahabusu wamekuwa wakinilalamikia Kuwa gerezani siyo kuzuri na taarifa nilizo nazo ni kwamba baadhi ya mahabusu wa gereza la Keko wanaokabiliwa na Kesi za Madawa,Mauaji wamegoma.

Ule umati uliofika Jana mahakamani kukulaki ukitokea gerezani, Kwani miongoni mwao ni wanaume, kwanini usingewauliza ni kwanini wanaume wale walishindwa kuwaruhusu wake ,wapenzi zao washiriki  kwenye yale maandamano haramu  ambayo yamesababisha ufunguliwe kesi na ulale gerezani?

Baadhi ya wanachama waliofika mahakamani Kisutu Jana nawafahamu na wengine wana vyeo Vya udiwani nilivyowauliza kwanini ni wanafki wakamshangilia Mdee Kinafki uwa eti ni Shujaa lakini Oktoba 4 Mwaka huu,walizuia wake na wapenzi wao wa kike wasishiriki maandamano haramu yaliyokuwa yameandaliwa na Mdee walinijibu wake zao wana watoto na watoto wao bado wanaitaji kulelewa NA mama zao  ,ila Mdee kwakuwa bado hajajaliwa na Mwenyezi Mungu kupata mtoto ,maandamano Yale yanamfaaa Kwani hata akiumizwa na kupoteza Maisha Hana Hasara.

Jibu hili liliniuma sana na Kusema kweli mla nawe hafi nawe.Misina ushahidi Kama Mdee Hana mtoto na Kamwe siwezi kumsimanga mwanamke mwenzangu ambaye haja bahatika kupata mtoto. 

Na ni lilitimisha kwa kuwaona wanaume wale na baadhi ya wanawake wa Chama hicho ni wanafki ,wakamshangilia Mdee kinafki na Kumbe hawampendi Mdee kwa dhati.

Hadharani wanajifanya wanamshangilia Mdee ,ila wakikaa vipembeni wanamkebehi Mdee.Ni unafki na dhambi ya Haki ya juu.

Mdee unapaswa utambue ndani ya vyama Vyama Vya siasa vina Siri nzito zilizofichwa kwa baadhi ya viongozi wa vyama hivyo ambao hata wewe uwenda hufahamu Kama wana siri hizo.Siku ukija kufahamu ,utatayari.

Kama una akili timamu unapaswa ujiulize ni kwanini wewe na baadhi ya wanachama mmetuhumiwa kutenda   makosa hayo Jumamosi iliyopita chap chap mmefikishwa mahakamani  lakini Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe alitoa maneno mazito ya kutaka viongozi wake wanaandaa maandamano yasiyo na kikomo na wasiombe Kibali Polisi ,  Septemba   14 Mwaka huu.

Siku chache baadae aliitwa Polisi akahojiwa na Polisi wakamsindikiza hadi Uwanja wa Ndege akasafiri kwenda Nchini Afrika Kusini na hadi Leo kimya bado hajafikishwa mahakamani  Licha anaweza kufikishwa muda wowote DPP akiona Ana Haja ya kumshitaki.

Rais Kikwete kila siku anasema ' akili za kuambiwa changanya na za kwako'. Hivi vyama vya upinzani vijana wenzangu msiviingilie kwa pupa sana ,vina siri nzito ndani yake na hivi vyama tutake tusitake vinawenyewe na hao wenyewe walivyovianzisha walivianzisha kwa malengo maalum ambayo siyo yale yaliyowekwa kwenye Katiba za vyama.

Sisi wenye bahati  ya kuteta siku moja moja na baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wanatuelezaga mengi na tumeishaona mengi sana.Minakutazama  tu .Shauri yako. .Nenda Taratibu, Wazaire wanasema ' Malembe Malembe'

Mdee hayo madaraka uliyopewa yasikutie wazimu, wakiamua walioviunda vyama hivyo ambayo hata siku Moja huwaoni Kwenye vikao Vya vyama hivyo Vya upinzani, wao wanakaa Mbali ,wanaviendesha vyama hivyo wakiwa Gizani, wakiamua siku kukung'oa madarakani , watakusukia ajenda Moja iliyosimama na watakunyang'anya hayo madaraka na utakuwa Huna la kufanya .

Na hao wanaokuvimbisha  kichwa Leo maana  Tayari wameisha kufahamu  Kuwa wewe ni kiongozi unayependa sifa ,kusifiwa hata ukifanya Ujinga  ndiyo watakuwa wa kwanza kukugandamiza Kuwa ulikuwa ukikiua Chama. Nayasema haya nimeyaona na siku ya kikufika ndiyo akili itakuwa sawa.

Mdee bado hujafikia kipaji Cha ushawishi wanawake wakuunge mkono Kama kipaji alichokuwaga nacho wanasiasa wanawake wa Enzi  zile TANU, BIbi Titi Mohamed, Lucy  Lameck. Bado sana.

Nimalize  kwa kumwambia Halima  Mdee Tulia uzae .Mdee nakushauri zingatia  maneno ya Makungwi Kuwa 'mwanamke anapaswa kufanya vurugu chumbani' siyo barabarani Kama ufanyavyo . 

Achana na tabia ya kufanya vitendo vya kihuni ambavyo unafikiri vitakupa umaarufu wa sifa mbaya. 

Na hao Leo  wanaojifanya kukushangilia wengine kupitia mitandao ya kijamii mwisho wa siku ndiyo watakwa wa kwanza kukuangamiza. 

Hata waliokuwa wafuasi 52 wa Kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda ,walipofikishwa mahakamani mwaka jana kwa makosa kama yako,wao na wapambe wao walikuwa na vibweka sana tena zaidi ya wewe na hadi walikuwa wakitaka kutupiga waandishi wa Habari ndani ya mahakama lakini kesi Yao ilipoanza kushika kasi akili iliwakaa sawa,walikuwa wapole na Wakaanza kujikomba kwa waandishi wa Habari ,mapolisi, askari magereza na watumishi wa Mahakama.

Sasa na wewe Mdee Jana ilikuwa ni Haki yako kupayuka Yale maneno uliyopayuka pale Mahakamani, lakini Kesi ikianza kushika kasi lazima utatulia tu , wale wafuasi wako walikuja kwa Wingi mahakamani Jana hutauona, idadi ya umati ule utapungua. Tumeyaona haya.Tusubiri wakati.

Haya Bunge Maalum la Katiba limemaliza muda wake Marais wetu Wawili wa pande zote wamekabidhiwa  Katiba iliyopendekezwa na Bunge ,NA wameisifu Kuwa ni Katiba bora  na wamesema wa awashawishi wananchi waipigie kura za Ndio nyingi.

Sijiu sasa kijana mwenzangu Mdee unajipanga 'atoke vipi' ,maana  ndiyo basi tena Katiba ya Samuel Sitta imeishapatikana , na Biashara yenu ya kufanya maandamano haramu ndiyo haina Soko tena maana Polisi wameacha tena kuwadekeza.

Na Joto hili sijui kombati mtazivalia wapi,sizitawavuka?

Mdee nakushauri ongoza wanawake wenzako wa Bawacha ambao Wengi nawafahamu ni wanawake na wasichana wanaojiheshimu Kama wakina Ester Wasira kufikia Malengo mliyojiwekea .Usiwaongoze wanawake wenzako kwenda kufanya matendo ambayo yamekatazwa na Sheria.

Naendelea kutoa rai kwa  Jeshi la Polisi chini ya IGP- Ernest Mangu, liendelee kufanya Kazi zake kwa mujibu wa Sheria na lisimuonee haya wala huruma Mtu yoyote hata akiwa ni mwanamke.

Kama mwanamke anashiriki maandamano haramu basi mwanamke Huyo ni wazi amejizatiti Kupambana na Polisi, Polisi na Nyie pambaneni naye  Kwani Sheria ni Msumeno.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Oktoba 9 Mwaka 2014