ZITTO KABWE, MBONA U MSAHAULIFU?





ZITTO KABWE,MBONA U MSAHAULIFU?

Na Happiness Katabazi

SISI Wanyambo ambao ni wenyeji wa Wilaya Karagwe Mkoa wa Kagera tunamsemo mmoja maarufu usemao; “Omusheija ainduka aha Kitanda,tainduka aha lulimi’.

Kwa tasfiri ya lugha ya Kiswahili maana yake ni kwamba “Mwanaume ana geuka kitandani,habadilishi kauli aliyokwisha itoa mdomoni mwake.Yaani akisema amesema.”

Nimelazimika kutumia msemo huo kwasababu makala yangu ya leo itajadili kauli zinazokinzana zilizotolewa na mtu mmoja kwa nyakati tofauti na mtu huyo si mwingine ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia(CHADEMA), Zitto Kabwe, kuhusu mawaziri wa wanaotaka kuwania urais mwaka 2015 wafukuzwe kazi na kauli zake mwenyewe kuhusu kauli zake za kinafki na sitaki nataka wadhifa wa urais mwaka wa Tanzania. 

Gazeti la Tanzania Daima Jumapili toleo la Novemba 28 mwaka 2011, ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho ;ZITTO AWALIPUA MAWAZIRI :ASEMA HAWAFANYIKAZI ,WANAWAUWAZA URAIS.

Habari hiyo ilisomeka hivi,Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi mawaziri wake tisa wanaotaka kuwania urais kupitia  chama hicho mwaka 2015.

Bila kuwataja majina mawaziri hao, Zitto alisema hivi sasa hawafanyi kazi ya kujenga uchumi wa nchi na badala yake wamejiingiza katika ‘vita’ ya kuwania uongozi huo.

Kauli hiyo aliitoa Novemba 27 mwaka 2011  jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua mkutano wa Muungano wa vyama vya Kidemokrasia Afrika (DUA) uliojumuisha vijana kutoka katika nchi 22 ambapo Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) ndio wenyeji.

Zitto alisema uchumi wa Tanzania umeporomoka na kufikia asilimia 17, hali ambayo imesababishwa na mawaziri wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kufanya kazi kikamilifu.

Alisema kwa sasa hali ya nchi ni mbaya ukilinganisha na wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, ambapo uchumi ulishuka kwa asilimia 4.5 na mfumuko wa bei ulidhibitiwa kwa kiwango kikubwa.

Aidha Machi 1 mwaka 2012:Gazeti hili la Tanzania Daima lilikuwa na kichwa cha habari kisemacho; NIKIOMBWA NITAGOMBEA URAIS- ZITTO.

Zitto katika habari hiyo alinukuliwa akisema kuwa ikiwa chama chake kitaona kuwa anafaa kuwania nafasi ya urais ama nyingine yoyote, hatasita kupokea wajibu huo.

Lakini Gazeti la Mwananchi Jumapili la Machi 25 mwaka 2012, lilichapisha habari iliyokuwa na kichwa habari kisemacho  ZITTO: NITAGOMBEA URAIS 2015.

Katika taarifa yake aliyoituma katika gazeti la Tanzania Daima , Zitto alisema; “ KWANZA ATAKAYEKABILI CHANGAMOTO HIZI. JIMAAMINI NINAWEZA KUWAONGOZA WATANZANIA WENZANGU KUKABILIANA CHANGAMOTO HIZI". 

Alitamba anao uwezo kwa kuwa ni mzalendo, mwenye utashi wa kuleta mabadiliko stahiki kulingana na nchi inavyoongozwa. Katika taarifa hiyo ameeleza kuwa kwa sasa nchi imesahau maendeleo ya watu badala yake imejikita katika maendeleo ya vitu.

Kwa mtiririko huo hapo juu wa kauli za Zitto alizozitoa katika tarehe tofauti na magazeti tofauti ambayo nimeyanukuu hapo juu kama vielelezo na kwamba hadi leo hii naandika makala hii sijaona wala kumsikia Zitto akikanusha kauli zake hizo, ni wazi zimenipa msukumo wa kuweza kujadili kauli hizo ambazo kwa mtizamo wangu nadiriki kuziita ni kauli zinazo kinzana ambazo zinatoka kinywa cha mtu mmoja.

Kwanza Ikumbukwe kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 , inatoa haki kwa wananchi wake ya kuchagua na kuchaguliwa.

Lakini kwenye nafasi  ya Rais , Ibara ya 39(1) (b) ya Katiba hiyo inasema ‘Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano , isipokuwa tu kama; ametimiza umri wa miaka arobaini.

Kama Novemba 27 mwaka 2011,  Zitto alinukuliwa akiwatuhumu mawaziri wa serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete ambao mawaziri wote hao ni wanachama wa CCM, watimuliwe kazi bila kuwataja majina yao kwasababu hawafanyi kazi wanauwaza urais wa mwaka 2015 , halafu Machi 25 mwaka 2012, Zitto huyu huyo anaibuka na kusema anautamani urais  na kwamba anasifa za kuwa rais.

Kwa kweli baada ya kumsikia Zitto akitoa tamko hilo , binafsi nilimshukuru mwenyezi Mungu kwa kazi akae nzuri sana  ya kutuonyesha sisi waje wake ili tufumbuke macho na tuone kuwa Zitto kumbe na yeye ni jamiii ile ya baadhi ya wanasiasa wale wale wenye hulka za kinyang’au ambao wanakasumba ya kuzungumza uongo mbele ya umma, ili umma uwapende na uamini kuwa Zitto ni kiongozi   safi na mtetezi wa wanyonge, kumbe siyo kweli hata.

Kwa watu tunaofuatilia matendo na kauli za viongozi wetu wa kitaifa, uwa tunatunza akilini na maktaba zetu baadhi ya matamshi wanayoyatoa kwa lengo ya kuzisoma na kujifunza kama nitaona zina mantiki ndani yake.

Ieleweke wazi hapo nyuma Zitto alitokea kujizolea umarufu mkubwa ndani ya jamii kwa kile kilichoelezwa ni mwanasiasa kijana ambaye ana misimamo thabiti na asiyeyumba katika kile anachokiamini..

Lakini hivi sasa kadri siku zinavyozidi kwenda ule mvuto aliokuwa nao awali umeanza kutoweka kwa sababu mbalimbali ambazo binafsi bado sijazithibitisha ila baadhi ya wanananchi mitaani na wengine ni wanachama wenzake wamekuwa wakieleza kuwa Zitto hana usafi wowote,an akiisaliti  chama chake cha Chadema na kwamba yupo pale kwaajili ya kutaka kukivuruga chama.Na kwamba viongozi wa chama chake wameishamfahamu wanachokifanya ni kumpuuza.

Sisi waumini wa sheria tunasema tuhuma zitabaki kuwa tuhuma hadi pale zitakapothibitika na mahakama au vikao husika vya chama chake.Lakini kwa kuwa mungu ni mwema kadri siku zinavyozidi kwenda mbele atazidi kutuonyesha kama kweli Zitto ni mwanasiasa msafi ,mhadilifu kuliko wanasiasa wenzake wanaotoka katika vyama mbalimbali vya siasa.

Na kwa kuanzia naona mungu ameanza kutufunulia kuwa naye Zitto ana tabia ile ile ya wanasiasa wenzake ambao leo wanapinga jambo hili lisifanywe na wanasiasa wenzao lakini kesho yeye anaibuka na kufanya jambo hilo hilo na wakati akifanya jambo hilo analialalisha yeye kulifanya ni halali ila wenzie wakifanya siyo halali. Kama siyo ubinafsi,unafiki na uchonganishi nini?

Zitto alitaka mawaziri watimuliwe kazi kwa kitendo chao cha kuwaza urais wa mwaka 2015 licha hadi sasa hakuna waziri yoyote alijitokeza hadharani akatangaza nia ya kugombea au kukiri kuwa ana uwaza au anautamani urais kama alivyofanya yeye.

Tumuulize Zitto tukimuita yeye ni mbinafsi na mnafki,mzandiki mkubwa na muongo tutakuwa tu nakosa?

Maana yeye Zitto aliuambia umma kuwa kuna mawaziri tisa bila kuyataja majina yao wanautaka urais na eti watimuliwe kazi, lakini yeye muda mchache baadae  akaibuka na kusema akiombwa na chama chake agombee atagombea na baadaye katika kipindi kifupi hata chama chake hicho akijamuomba wala kumpa ridhaa akiibukia kwenye gazeti la Mwananchi na kusema anautamani urais na kwamba ana sifa.

Kama hivyo ndivyo hatuoni Zitto ana kasumba ya ubinafsi ambayo anataka apate yeye wenzie wasipate?Mawaziri wakiuwaza urais yeye kwake ni haramu ila yeye akiutamani urais tena adharani siyo haramu?

Zitto ulipendekeza mawaziri hao tisa watimuliwe kazi licha mawaziri hao hawajajitokeza hadharani kama wewe kutangaza nia, Sasa Je na wewe wafuasi wa Chandema wamuombe Mwenyekiti wako Freeman Mbowe na vikao husika wakuvue madaraka unayoyashikilia kwenye chama Chama chako kwasababu na wewe ndiyo kabisa umetangaza hadharani kuwa unautamani urais na kwa hatua hiyo hufanyikazi za kujenga chama chako?

Nimebaki kujiuliza Zitto ana ubongo wa Ndezi?.Kwani wataalamu wa viumbe hai wanatueleza kuwa Ndezi moja ya sifa yake kuu ni kusahau mambo kwa  wakati mfupi.

Kuutaka urais kwa kufuata utaratibu husika ulioanishwa kwenye Katiba ya Nchi siyo kosa la jinai na ndiyo maana sisi waumini wa sheria tulivyomsikia Zitto kwa mara ya kwanza akimtaka rais Kikwete awatimue kazi mawaziri tisa ambao hakuwa taja majina eti kwasababu wanawaza urais, tulimpuuza na kumuona ni mbumbumbu wa sheria.

Kwasababu Zitto akutaja majina ya mawaziri wale ,ni wazi hakutoa ushahidi unaoonyesha moja kwa moja mawaziri hao hawafanyikazi kabisa wanauwaza huo urais.Na kwakuwa rais Rais Kikwete ni msikivu aliupuuzia ombi hilo kwasababu halina mashiko na ni la kipuuzi.

Wananchi kwa kauli hizo za Zitto zimenifanya nianze kujiuliza hivi kama hali ndiyo hii. Je ahadi zote alizokuwa akizitoa jimboni kwake nyakati za kampeni atazitekeleza kweli? 

Na ndiyo maana hivi sasa ameanza kupoteza mvuto na wananchi hawampapatikii kama walivyokuwa wakimpapatikia zamani kwani wananchi walijijengea akili mwao kuwa eti huyo ndiyo ni mkombozi wao na viongozi wengine ni mafisadi na wachumia tumbo.

Na kama hivi ndivyo,Zitto ana tofauti gani na wale baadhi ya mawaziri ambao amekuwa akizikosoa bajeti zao bungeni kuwa mawaziri hao wameingiza takwimu za uongo katika bajeti zao?

Maana kiongozi au mwananchi wa kada yoyote akishaanza kuwa na tabia ya leo anaibuka na kutaka wenzake waadhibiwe kwa kufanya jambo fulani halafu kesho kiongozi huyo anaibuka na kufanya jambo lile lile linalofanywa na wenzake halafu yeye anataka umma umuone yupo sahihi ila wenzie wamekosea, kiongozi wa aina hii ni hatari kwa mustakabali wa taifa na hafai kupewa madaraka makubwa ya kuiongoza nchi yetu kwani mwisho wa siku sisi wananchi tutakachojifunza kutoka kwa kiongozi wa aina hiyo ni ubinfasi na uchonganishi.

Aidha napenda kumshauri Zitto na vijana wenzake ambao wameonyesha tamaa ya kupata madaraka makubwa kwa kutumia hoja ya umri wa kuwa rais ubadilishwe kwenye Katiba ili vijana wenye umri wa chini ya miaka 40 waweze kugombea nafasi hizo, wapunguze papara kwani wahenga walisema 'Mbio za Sakafuni uishia ukingoni'.

Kwani Watanzania wa leo siyo wale wa mwaka 1947, wanakufahamu vizuri wewe Zitto na hao vijana wenzako na hiyo kilicho nyuma ya ajenda hiyo ,msione wamewanyamazia kimya mkawaona ni majuha.

Wanafahamu fika hoja yenu hiyo ni kwa maslahi ya kikundi cha vijana wachache wenye madaraka ya kisiasa ambao hivi sasa wameanza kutuhumiwa huku mitaani kichini chini kuwa wana mali ambazo haziendani vipato vinavyotambulika na mamlaka husika na wenye tamaa ya kupata madaraka makubwa kuliko umri kwa haraka.

Kwa mtazamo wangu bado Tanzania hatujafikia hatua ya kuwa na rais kijana mwenye umri wa chini ya miaka 40 kwa kisingizio tu etu tunaenda na wakati. 

Sababu ya mimi kuwa na mtazamo huo licha mimi bado ni kijana mwenye umri wa miaka 33 ni kwamba hulka za sisi vijana wengi zinafahamika.

Lakini pia narudia kusisitiza kuwa kiti cha urais wa Tanzania, siyo kitu rahisi, rahisi kama watu wanavyodhani, ni kiti chenye heshima na hadhi ya kipekee ambacho kimebeba dhamana ya kuwaongoza watanzania wote wakubwa kwa wadogo, hivyo tusifanye majaribio katika kiti cha urais.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

Facebook. Happy Katabazi
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Aprili Mosi mwaka 2012.




KASHFA YA ESCROW ISITUVURUGE








KASHFA YA ESCROW ISITUVURUGE

Na Happiness Katabazi
MIONGONI wa Wimbo unaotamba hapa nchini Homa ya Dengue na kile kinachoitwa eti ni vigogo wa serikali  wanaotuhumiwa kuhusika Katika kashfa  ya ufisadi  wa Sh Bilioni 200  Katika Akaunti ya Baraza la Usuluhishi la Migogoro ya Kibiashara (ESCROW) ya Benki Kuu (BoT).

Makala yangu itazungumzia Wimbo huo wa pili wa kashfa ya ESCROW ambayo  Mbunge wa Kigoma Kusini(NCCR-Mageuzi), David Kafulila amedai Kuwa ndiye yeye ameiibua kashfa hiyo  ambapo  aliwataja wahusika wakuu wa kashfa hiyo Kuwa ni  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter   Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliachim Maswi, Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Jaji  Frederick Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba.

Kafulila alisema  kuwa ufisadi huo ni lazima mbivu na mbichi zifahamike, na kwamba haungi mkono uamuzi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wa kuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza suala hili kwa kuwa linagusa mamlaka kubwa katika dola, badala yake iundwe Kamati Teule ya Bunge.

Muda mfupi baada ya Kafulila kutoa tuhuma hizo Bunge, hakukubaliana na ombi la Kafulila lililotaka iundwe Kamati Teule ya Bunge na badala yake akaiagiza TAKUKURU na OFISI ha CAG Ifanye uchunguzi wake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo.

Kwa jicho la Sheria tuhuma zilizotolewa na Kafulila zitabaki Kuwa tuhuma, na Kafulila atahesabika kwanza Kuwa yeye ni mtoa  taarifa za tuhuma hizo.Hivyo kitendo Cha Kafulila kunukiliwa na Gazeti hili toleo la Jumatano ya wiki hii Kuwa   uamuzi huo wa Pinda una Mashaka makubwa na kwamba tuhuma hizo zinahusu viongozi wakubwa wa dola hivyo eti ni Vyema  Kamati ya Teule ya Bunge iundwe uchunguze siyoni Kama Ina mantiki.

Kwani TAKUKURU imeanzishwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana Rushwa ya Mwaka 2007 Namba 11/2007.Na kifungu Cha 7 Cha Sheria hiyo kimeanisha Kazi za Takukuru na miongoni mwa Kazi za Takukuru ni kufanya uchunguzi makosa ya kula Njama Kutenda kosa, kuchunguza tuhuma za makosa ya rushwa yanayowahusu maofisa wa serikali.

Aidha Ofisi ya CAG nayoilianzishwa na inayo majukumu yake mengi tu ikiwemo ya kukagua mahesabu Katika Fedha za serikali na imekuwa Ikitimiza majukumu yake na kutoa taarifa zake kwa umma.

Na Taasisi hizo zimeanzishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kafulila ni miongoni mwa wa Bunge wa Bunge Hilo.

Sasa Inashangaza  Kama siyo kutisha kumsikiliza  mtunga  Sheria Huyo Akisema uamuzi huo wa Pinda una Mashaka kwasababu yeye alikuwa akitaka Bunge iunde Kamati Teule.

Kama Kafulila alikuwa Hana Imani na Takukuru, CAG ni kwanini alitoa tuhuma hizo bungeni akitaka mbivu na mbichi sijulikane? Kumbe anaamini Takukuru, CAG ni wa chafu ni kwanini aliibua tuhuma hizo tena akitaka uchunguzi ufanyike? Hivi mwisho wa siku alifikiri Takukuru, CAG hazitausishwa Katika uchunguzi huo.

 Tuhuma hizo zinahusu Fedha za serikali , Ofisi  ya ya CAG lazima ilihusishwa mAana ipo pale kwa kutazama matumizi ya Fedha za serikali zimetumika Kama iliyokusudiwa?

Maana hata Kama Kamati Teuli ya Bunge ingeundwa Mwisho wa siku ripoti hiyo ya uchunguzi wa Kamati Teuli ya Bunge Ingepelekwa Takukuru au Polisi ili zichunguze kuona je kuna ushahidi wa kutosha wa kuweza kuwafungulia Mashitaka watuhumiwa? maana Polisi  na Takukuru Ndio wenye majukumu hayo Kimsingi.

Pia Itakumbukwwa kashfa ya wizi Katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), iliibuliwa Bungeni, Kamati ya Teule ya Bunge haikuundwa Matokeo yake Rais Jakaya Kikwete alitenda TIMU ya Uchunguzi wa tuhuma hizo ambayo ilishirikisha polisi, Wanasheria toka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tasisi nyingine za serikali ambayo ilikuwa na Ofisi zake Mikocheni ambapo ili fanyakazi yake vizuri  Mwisho wa siku Uchunguzi huo ulimfanya Mkurugenzi wa Mashitaka , Dk.Eliezer Felelshi Kufungua jumla ya Kesi 12 za EPA m Novemba 4 Mwaka 2008  ambapo hadi sasa jumla ya Kesi Nne zimetolewa hukumu na baadhi ya washitakiwa walipatikana na hatia za makosa waliyoshitakiwa na wengine waliachiwa Huru kwasababu ushahidi haukuwagusa.

Mfano mwingine ni tuhuma za mkataba wa kampuni ya Richmond Ambapo kelele zilipigwa na wabunge hadi Kamati Teuli ya Bunge ikaundwa Mwaka 2007 na Mwanzoni Mwaka 2008 Kamati Teuli ikabainika kilikuwa na ouzo Katika mkataba huo na kumtaka Aliyekuwa waziri makuu Edward Lowassa ajipime na Kamati hiyo ikaamuru Wamiliki wa kampuni hiyo Naeem Gire na Mohamed Gire na baadhi ya Maofisa wa serikali wawajibishwe  Hali iliyosababisha Lowassa kuwajibika KWA kujiudhuru   wadhifa  huo ambao alidumu nao KWA Kipindi  kifupi sana.

Baada ya ripoti ya Kamat hiyo kusomwa, baadhi ya wabunge kwasababu wanazozitoa wa Wakaanza kuishinikiuza Takukuru iwashitaki watu Hao Hali iliyosababisha Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru , Dk.Edward Hosea na baadhi ya wabunge kuingia Kwenye malumbano Kwani Hosea alikuwa akitaka Takukuru iachwe ifanyekazi yake kwa  Uhuru na siyo kuingiliwa na wasiasa Hali iliyosababisha kila kukimbia wabunge Hao Kuwa wanashambulia Takukuru na Hosea kila kukicha Kumbe wabunge Hao walikuwa wananjama zao chafu za kuaribiana kisiasa.

Wananchi ambao walikuwa hawaelewi Njama hiyo waliwaunga mkono wabunge Hao wengine ambao walipachika jina la ' wabunge wanapambana na  ufisadi", Leo hii wanasiasa 'Mgambo uchwara' hao wapo  kimya utafikiri ufisadi ndani ya nchi hii umekwisha.Dhambi sana.

Mwisho wa siku Takukuru iliamua kumfungulia Kesi ya Madai ya Kutoa taarifa za uongo Kwenye Kikao Cha Tenda Cha Tanesco kuhusu uwezo wa kampuni ya Richmond, mshitakiwa alikuwa ni Neem Gire Mwaka 2012,  Hakimu Mkazi wa Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Waliarwande Lema alimuoa Gire Hana Kesi ya Kujibu  na Mkurugenzi wa Mashitaka DPP- Dk.Feleshi hakulidhika na uamuzi huo anakimbilia Mahakama Kuu Ambapo Jaji Lawrence Kaduri alitengua  uamuzi huo na akaamuru jarada la Kesi hiyo lirudishwe Mahakama ya Kisutu na Gire aanze  kujitetea na Gire naye kupitia Wakili wake Alex Mgongolwa hawakubaliani na uamuzi wa Mahakama Kuu, wamekimbilia Mahakama ya Rufaa.

Kwa  hiyo binafsi naweza Kusema Kuwa sikubali Kuwa tuhuma ni za kweli na sikatai Kuwa tuhuma hizo zilizoibuliwa na Kafulila  Kuwa ni za uongo Katika Hatua hii ya awali.Nasubiri   vyombo vyenye mamlaka ya kufanyia uchunguzi  itakapokuja kuandika ripoti za uchunguzi wake.

Kwani tuna Mifano hai  ambayo inafunza kupitia wanasiasa wetu ambao Walijifanya ni mabingwa wa kuibua kile wanachokiita ufisadi  wakati Sheria zote za Tanzania ikiwemo  Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002 , haina kosa linaloitwa ufisadi. Sijui wenzetu hawa kosa la ufisadi wanaotaka watu washitakiwa nalo sijui wa alipata wapi  Katika Kifungu kipi Cha Sheria.

Mbunge Zitto Kabwe aliuaminisha umma Kuwa Ana ushahidi kuhusu Majina na namba za Akaunti za watu walioficha  Fedha nje ya nchi na baadhi ya watu waliomua mini, lakini siku zote njia ya muongo ni Fupi, Mwanasheria  Mkuu wa Serikali Jaji Werema aliliambia  Bunge Kuwa Zitto ni muongo aliwashawahi kumuita  Ofisini kwake akimtaka  atoe ushahidi chini ya kiapo , Zitto  akasema hana ushahidi, na hadi Leo kimya kabisa utafikiri Zitto  siyo yeye aliyekuwa akisimama  majukwaa akijinadi anaoushahidi wa watu walioficha Fedha nchini Uswiss.

Pia kuna wanasiasa wengine ambao Walijitapa ndani na nje ya Bunge Kuwa wanaushahidi wa Majina ya watu walioiba  Fedha za EPA kupitia kampuni a Kagoda hadi Leo hawajaenda kutoa ushahidi thabiti Katika vyombo husika, Wanaishia kubwatuka majukwaani na kuwataka Ujinga huo baadhi ya waandishi wa Habari ambao hawajui kilichopo nyuma ya tuhuma zinazoibuliwaga na baadhi ya wanasiasa wa naandika Habari za kutoa hukumu  za upande mmoja.

Wiki iliyopita Spika Anna Makinda  Mara Tatu wakati akiendesha Bunge aliwataka baadhi ya wabunge waache kutumiwa  na baadhi ya watu walionje ya Bunge Kuja bungeni  Kusemea maslahi binafsi ya watu wakiwa tuma na kuwataka wabunge Hao watumie akili zao.

Ushauri  huu ni mzito sana kutolewa na Spika Kwa wabunge na Hakuna Shaka Makinda alikuwa anasababu anayoifahamu  ndiyo mAana Akaamua kutoa ushauri huo licha Spika Makinda hakutaja jina la Mbunge anayetumiwa.

Hivyo ushauri wangu kwanza kwa waandishi wa Habari wenzangu  kuhusu tuhuma hiyo iliyoibuliwa na Kafulila tuwe makini na tusimame Katika Maadili ya taaluma yetu.Kafulila tumemsikia, serikali kupitia Pinda imeishachukua Hatua  KWA kuanzia Pinda ameagiza Taasisi hizo mbili zifanyie Kazi tuhuma za Kafulila. 

Hivyo ni vyema sasa tuziachie Taasisi hizo zifanyie kazi yake Kwa Uhuru na Mwisho wa siku zije zitoe ripoti yake.Tusikubali ama kutumiwa na wafanyabiashara, wanasiasa, Wanasheria kuwachafua watu wengine wanaotuhumiwa Katika tuhuma hizo na Kafulila isivyohalali Kwani Tayari naona kuna Dalili za wazi ambazo ni chafu za miongoni mwetu kuanzia kutumiwa na Makundi yanayoasimiana Katika kashfa hii.

Pili, Takukuru, CAG visikubali kuingiliwa kufanyakazi yake na Makundi yenye Hira Katika Sakata hili Kwani endapo watakubali kufanyakazi kwa shinikizo la wanasiasa Mwisho wa siku watajikuta wanaumbuka Mbele ya safari Kama serikali ilivyoumbuka Mara mbili Kwenye Kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Ricky Mahalu na Grace Martin Kwani Chanzo kikubwa Cha Kesi hii kilianzia  pale Bungeni Mwaka 2004 ambapo wanasiasa uchwara waliliaminisha Bunge na Takukuru  Kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Costa Mahalu  alitafuna  Fedha za ujenzi wa Jengo  la ubalozi Wa Tanzania nchini Italia kumbe ni uzushi na leo hii wale wanasiasa na baadhi ya wachunguzi wanaona haya.

Tatu , Kafulila kwa Kuwa Tayari umeishanukuliwa ukisema uamuzi wa Pinda una Mashaka nao , ni wazi hata vyombo hivyo va uchunguzi vikitoa Matokeo ya uchunguzi ambao wewe hutapendezewa nao, hutatakubaliana nao.

 Basi minakushauri Kafulila tumia    Kifungu Cha 99 Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002, kuomba uwe mwendesha Mashitaka Binafsi(Private Prosecutor), ili uweze kuendesha Kesi hiyo mahakamani mAana Tayari umejinasibu Kuwa una ushahidi wa kutosha kuhusu tuhuma hizo.

Ni sisi wenyewe wananchi wa Tanzania Tulitaka nchi yetu iongozwe na Utawala wa Sheria, kwahiyo Takukuru, CAG, Cheo Cha Waziri wa Mkuu na Spika vimeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Hivyo tuheshimu wanapokuwa wanatimiza majukumu Yao na anayeona Hana Imani na vyombo Vya dola, aende kuishi nchi ambazo anaamini vyombo vyao Vya dola vinaaminika.

Na wananchi huko vijiweni Tusikubali kutoa hukumu Kuwa. Fulani n fisadi , hafai kuongoza, afukuzwe Kazi eti tu mwanasiasa Fulani kajitapa kuibua tuhuma za ufisadi.Kwani ni hawa hawa wanasiasa Ndio wamekuwa wakituingiza Kwenye ushabiki wa mambo ya kijinga Mwisho wa siku wanatoa na soremba.

Ni hawa hawa wanasiasa walijiapiza Kuwa kampuni ya Richmond ni ya Kitapeli na ni kampuni ya mfukoni .Wananchi  tukaamini  Kumbe walikuwa nalo jambo.

 Mwisho wa siku kampuni hiyo ikabadilishwa jina ikaitwa  Dowans, kelele zikazidi hadi kufikishana mahakamani na Mwisho wa siku Tanesco ikashindwa Kesi iliyoishitaki   Dowans kule katika Baraza la Usulushi wa Migogoro ya Kibiashara ya Kimataifa (ICC), Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na Mahakama ya Rufaa Tanzania.Na Tayari Serikali ya Tanzania imeishailipa fidia Dowans.

Kampuni ya Richmond tuliyoaminishwa na wasasiasa uchwara Kuwa ni kampuni ya mfukoni ilibadilishwa toka jina la Richmond Kuja Dowans, na Mwishoe HIvi sasa inaitwa Sympion Power Na inatoa huduma zake kama kawaida na huduma ha kampuni hiyo inatumika .

Na mwaka jana   Rais wa Marekani Baraka Obama alivyokuja Tanzania  aliizindua  kampuni hiyo,na Hao wanasiasa waliotuaminisha uongo kuhusu uwezo wa kampuni hiyo Kuwa ni ya mfukoni nao walikuwepo Kwenye msafara wa ziara hiyo ya Obama kuzindua Sympion .Na leo wanasiasa hao, sanaharakati waliokuwa wakishabikia kuiponda kampuni hiyo leo wapo kimya utafikiri wamefariki Dunia.

Tujifunze kutokana makosa, tusiwe wepesi kuamini   kila kitu kinachoibuliwa na baadhi ya wanasiasa wetu uchwara Kwani wengine ni Mavuvuzera wa wafanyabiashara, makampuni  na wanasiasa,na makuadi wa Makundi yanayoasimiana Katika magomvi Yao ama ya Kugombea Tenda Fulani, Biashara , urais Mwaka 2014 na kulipizana visasi vitendo ambavyo havina maslahi ya taifa zaidi ya kutaka kuvuruga umoja wetu.Tusiwape nafasi wahuni hawa.

Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Mei 18 mwaka 2014
0716 774494
www.katabazihappy.blospot.com

Facebook: Happy Katabazi





SHYROSE BANJI JIEPUSHE NA TUHUMA CHAFU










SHYROSE BANJI JIEPUSHE NA TUHUMA CHAFU
Na Happiness Katabazi
WASWAHILI wanamsemo wao mmoja usemao ' anaye jamba lazima atakunya tu'.

Msemo huo una una Tafsiri nyingi tu ikiwemo Kuwa unawaweza Kuwa unapenda matendo maovu lakini kwasababu una Nguvu za aina fulani unatumia kujisafisha Mbele ya hadhara Kuwa hujatenda maovu hayo lakini ukae ukifahamu ipo siku ukweli utaanikwa hadharani na itabainika Kuwa ni kweli MTu Yule aliyekuwa akikanusha tuhuma zile ni muongo na kwamba ni kweli alitenda makosa hayo anayekabili nayo.

Nimeamua kuanza na Msemo huo kwasababu nafikiri kila kukicha sasa baadhi ya vyombo Vya Habari vimekuwa vikiandika baadhi ya Habari mbaya zinazomuhusu Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji.

Banji ambaye licha ni Mbunge wa Bunge hilo, pia Mwandishi wa Habari Kitaaluma wa muda mrefu.

Miongoni mwa tuhuma zisizopendeza ambazo zinaelekezwa moja kwa Moja Banji,Moja ni ile tuhuma ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya Kijamii Kuwa ni za utovu wa nidhamu kwamba Banji alitoa lugha ya matusi dhidi ya baadhi ya wabunge wenzake wa Afrika Mashariki akiwa eti amelewa Pombe ndani ya Ndege Hali iliyosabisha baadhi ya wabunge wa Bunge Hilo kutaka ashughulikiwe.


Tuhuma nyingine ni kwamba tulimshuhudia Banji mapema Mwaka Mwaka huu akirushiana vijembe na Waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta ' Mzee Sugu' , ambaye Sitta aliibuka na kusema Banji Hana mamlaka ya kumnyoshea kidole wala Wizara yake kwa Sababu Banji ni miongoni wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ni Mtoro  yaani ahudhurii  ipasavyo vikao Vya Kamati na Bunge Hilo.

Tuhuma Nyingine ambayo imeibuka HIvi sasa ni kwamba Banji ampiga mbunge mwenzie wa Bunge Hilo kutoka Tanzania, Ndelakindo Kessy.

Ibara ya 13 (5) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 , inasema mtuhumiwa anayetuhumiwa  Kutenda makosa ya jinai asichukuliwe au kutendewa Kama Ana hatia hadi pale Mahakama itakapokuja kumkuta na hatia.

Hivyo na Mimi Katika makala hii niliyomwandikia dada yangu, mwanahabari mwenzangu Banji imezingatia matakwa ya Ibara hiyo, hivyo simchukili  Banji Kuwa Ana hatia Katika tuhuma hizo zote zinazomkabili hadi pale mamlaka husika zitakapokuja kumuona Ana hatia.

Namfahamu Banji tangu enzi zile 'tunasaka Nyoka' wote mtaani yaani kusaka Habari, pia namfahamu Banji Enzi zile akiwa Kiongozi wa Timu ya Waandishi wa Habari Wanawake (Taswa Queen), Ofisa Uhusiano wa City Water na Benki ya NMB.

Ni mwanamke ambaye ameangaika hadi kufika hapo alipofikia ,Nampongeza Katika Hilo.

Leo Banji Kama nitakukwaza naomba nisamehe  bure Kwani Mimi siyo mnafki na siogopi Kusema kile ninachokiona Kina faida kwa wahusika .

Banji Utakumbuka ulivyoanza harakati zako za kutaka uongozi ndani ya CCM ,Ubunge wa Jimbo Kinondoni na nafasi nyingine nyingi tu lakini kura hazikutosha na hukufanikiwa kupata nafasi hizo.

Kumbe Mungu aliruhusu ukose hizo nafasi ili uje uchaguliwe Kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.Wanahabari wenzako tunapokutakia Mema tulifurahi kwa kuchaguliwa kwako Kuwa Mbunge wa Bunge la EAC siyo tu ni sifa kwa Familia yako pia ni sifa kwa waandishi wa Habari ,wanawakd Kuwa miongoni mwa wa wabunge wa Bunge la EAC ni mwanahabari na mwanamke mwenzetu ambaye ni Banji.

Sasa inapotokea tena tuhuma Kama hizi zinakuandama mfululizo ,watu tunaofikiri sawa sawa lazima tushituke na tuliulize Kulikoni Banji?Mbona unaandamwa na tuhuma mpya mfululizo kiasi hicho?

Ni kweli Banji amekuwa akijitokeza hadharani kuzinaka tuhuma hizo.Lakini Mimi binafsi SINA ushahidi unaonyesha Tuhuma hizo ni za ukweli au uongo.

Ila najiuliza ni kwanini basi Banji kila kukicha anaandamwa na tuhuma mpya? Je ni kweli Banji anatenda matendo hayo machafu ila amekuwa ni mahiri kukanusha tuhuma hizo pindi zinapovujishwa kwenye vyombo Vya Habari na mitandao ya kijamii?

Tumuulize Banji ,je ana Mpango wa kutaka Kugombea Urais, Ubunge au Udiwani ?.

Maana nchi hii hivi sasa wanasiasa wetu Wengi wamefilisika kimkakati ,kimbinu za kuwadhohofisha maadui wao wa kisiasa hasa wale wanaotaka Kugombea pamoja Katika Ngazi ya urais, Ubunge na udiwani kwa kuamua kwatumia baadhi ya wapambe ambao wabambwe wao wamekuwa na kazi Moja tu ya Kutengeneza fitna,uzushi,majungu dhidi ya hasimu wao na Kisha wapambe Hao wamekuwa wasambaza majungu hayo kupitia Mtandao ya kijamii na kwatumia baadhi ya waandishi wa Habari wasiyojua ajenda iliyopo nyuma ya Habari hizo kuwachafua wenzao.

Nasema Hilo kwasababu ndiyo wanasiasa wetu na sisi wanahabari tulipolifikisha taifa letu hapa lilipo kwa baadhi ya watu Kuwa na tabia za kishenzi za kuzushiana taarifa za uongo na kuchafuliana majina Lengo likiwa ni Moja kuaminisha umma Kuwa Fulani aliyechafuliwa kwenye mitandao na magazeti na wakati mwingine ni Habari za uongo tu, Kuwa hafai kupewa madaraka Fulani hata kidogo kwasababu Hana nidhamu, mwizi na fisadi.Dhambi sana na ni ukatiri pia.

Kama ni kweli Banji unafanya Vituko HIvi Leo hii ni Mara ya pili nakushauri, achana na vitendo HIvi Kwani kaa chumbani peke yako, jitafakari ulipo toka, ulipo sasa na unakokwenda. 

Nayafahamu baadhi ya mapungufu yako  wewe na Ndelakindo Kessy na Mimi Kama binadamu kuna watu wanayafahamu mapungufu yangu sikatai. 

Nakushauri Banji jiepushe kukaliabia ya kufanya mambo ambayo yataendelea Kuwa Chanzo Cha wewe kuibuliwa tuhuma mpya kila kukicha.

Maana sikufichi huku mitaani kuna baadhi ya watu wameanza kuziamini hizo tuhuma Kuwa ni za kweli kwasababu eti wa nafahamu baadhi ya rekodi ya matendo yako.

 Sijapendezwa na mtazamo huu Kwani pia unahusishwa Moja kwa Moja na taaluma ya wanahabari Kuwa Banji ni mwanahabari amepewa nafasi hiyo ya Ubunge lakini anafanya vitendo Vya kihuni.

Binafsi naamini Kama ulitenda vitendo hivyo ,ulitenda Kama wewe binafsi na siyo kwa Kofia ya Ubunge, Uandishi wa Habari. 

Wanawake Watanzaia ni miongoni mwa wanawake Dunia ambao tumekuwa tukipigania Usawa Katika madaraka na kweli Katika Utawala wa serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, wanawake wengine wameshika nafasi nyingi za uongozi ndani na nje ya serikali ni jambo la kujivunia sana kwa wanawake sasa inapotokea Nyie baadhi ya viongozi wanawake mnaanza kutuhumiwa Kuwa mnatenda matendo yasiyofaaa Mkae mkijua mnawapa nafasi ya wanaume Kusema kuendeleza kasumba ya kumuona Mwanamke hafai kupewa madaraka kwasababu Hao waliopewa madaraka wameonyesha kushindwa kujiheshimu. 

Banji  jitambue Kuwa wewe ni kiongozi  na kukubali Kuwa kuna baadhi ya mambo Unatakiwa usifanye hadharani.

Mfano kiongozi aliyefundwa akafundika huwezi kumkuta akivaa nguo za ovyo ovyo barabarani, kujihusisha na ulevi wa vilevi vilivyopigwa marufuku na sheria za nchi, kutoa lugha chafu Mbele za watu ,kupigana hadharani na mambo mengine yasiyofaha. 

Ieleweke Kuwa hayo matendo simaanishi yanafanywa na Banji.
Mwisho nimalizie kwa kumuasa dada yangu Kitaaluma Banji ajitambue Kuwa yeye ni kiongozi  Kama kweli  anatenda matendo aache kwani yatamletea madhara makubwa sana  na kuporomosha heshima yake na ninamshauri afanye utafiti ni kwanini anaandamwa na tuhuma hizo mfululizo na ni wakina nani wanasambaza taarifa hizo  kwa Malengo gani.

Je ni baadhi ya wabunge wenzake wake Bunge la Afrika Mashariki wanaotoka Tanzania au ni wabunge wenzake wa Bunge la Afrika Mashariki wanaotokea nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki? 
Na ujiulize  ni kwanini wakuandame wewe tu   kila kukicha kwa tuhuma na wabunge wenzako  wanawake wa Bunge Hilo toka Tanzania Kama Angella Kiziga na wengine hawaandamwi na tuhuma Kama hizo?  Kwanini ni wewe Banji  tu? Kumbuka  Msemo usemao ' Mke wa Mfalme hata kiwi kutuhumiwa'.

Pole sana Banji kwa kupitia Kipindi hicho kigumu ila rejea Msemo huu ' aliye jamba atakunya tu'.  Hivyo Kama kweli Banji unafanya upuuzi huu halafu unajitokeza hadharani mapema unakanusha , basi tambua ipo siku ukweli utajulikana Kuwa ni kweli Banji anatenda matendo hayo na tutakupuuza.

Chanzo: Facebook.Happy Katabazi,
Novemba 20 Mwaka 2014