KATABAZI NA JAJI FRANCIS MUTUNGI



Kaka yangu Jaji Francis Sales Mutungi Katabazi ambaye kwasasa ndiye Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini, enzi zile akiwa na cheo cha Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Msajili wa Mahakama ya Rufaa nchini, Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, nilipata kufanyakazi nae kwa karibu ,mimi nikiwa Mwandishi wa Habari za Mahakamani na ofisa Mwandamizi wa Mhimili wa Mahakama.

Mara kwa mara Jaji Mutungi alikuwa akipenda kunieleza kuwa kiongozi mzuri au mtoaji mzuri wa maamuzi ni yule ambaye kabla ya kutolea uamuzi jambo lolote lile liloamsha hisia tofauti katika jamii au binafsi anakuwa kwanza ametulia kabisa na ameondokana na jazba na mihemko ya aina yoyote.

Kwani anaamini kutolea tamko,uamuzi jambo fulani linalohusu serikali na mamlaka zake kwa pupa unaweza kujikuta unatoa maamuzi mabovu. Na kwamba ni vema kiongozi,au mtu wa kawaida uchelewe kutoa uamuzi lakini siku ukitolea uamuzi jambo fulani au taarifa fulani ziwe zimemaliza tatizo.

Na Jaji Mutungi ni kiongozi wa aina hiyo ambaye hata lililipokuwa likitokea jambo linalohusu mhimili wa Mahakama au yeye binafsi alikuwa akurupuki kutolea msimamo.

Hata sisi 'Wambea wa Mahakamani' tulipokuwa tukimvamia ofisini kwake kumuomba atolee tamko masuala hayo alikuwa akisema tumpe muda atatolea tamko na kweli baada ya mihemko na jazba za watu kuhusu jambo fulani kupungua ndiyo alikuwa akiibuka huku akiwa na taarifa zenye takwimu na kutolea tamko.

Jaji Mutungi ambaye ni Msomi wa Sheria mwenye silika ya kujiamini, nitamkumbuka siku zote kwa mbinu hiyo aliyokuwa akinipatia,mwanzo nilikuwa simwelewi ila kwasasa nimekubaliana na mbinu yake hiyo.

Mungu akupe afya njema na maisha marefu na hekima na busara hasa katika mwaka huu wa uchaguzi Mkuu ambapo Ofisi yako ya Msajili wa Vyama vya siasa nayo inahusika kwa sehemu fulani.

Picha hii tulipiga wakati Mutungi akiwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa nchini na kabla Rais Jakaya Kikwete ajamteua kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na kisha kumteua kuwa Msajili wa vyama vya Siasa nchini.

By Happiness Katabazi, Aprili 25 mwaka 2015.

HONGERA DK.KAHANGWA KUWA MGOMBEA URAIS WA NCCR- MAGEUZI



 *Tujikumbushe mahojiano yangu na Dk.Kahangwa ya mwaka 2009.

Na Happiness Katabazi

JANA  Chama Cha NCCR Mageuzi, kilipitisha jina la Kada wake ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk.George Kahangwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

Awali ya yote naomba nitangaze maslahi yangu kwa Dk.Kahangwa.

 Dk.Kahangwa toka zamani hadi hivi sasa ni rafiki yangu,Kaka yangu kwasababu wote tunatokea Mkoa mmoja wa Kagera, Kaka yangu pia kwasababu mimi na Dk.Kahangwa na baadhi ya vijana wengine wote sisi Baba yetu mlezi ni marehemu Dk.Sengondo Mvungi ambaye  alikuwa akitulea na kutufunza pamoja mambo mbalkmbali yakiwemo siasa za kimageuzi ,sheria,kutusisitiza tujiendeleze kielimu  na mambo mengine ya kufikirisha akili  tangu mwaka 2003 hadi Dk.Mvungi anafariki Dunia Novemba 12 mwaka 2012.

Na katikati ya mwaka 2012 kaka Kahangwa alirejea nchini kutoka  masomoni  huko Ughaihuni  baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili (PhD)   na hivyo kufanya tuanze kumuita Dk.George Kahangwa na siyo George Kahangwa, licha hadi sasa imekuwa ikiniwia kumuita Dk.George namuita Kaka George kwasababu tangu akiwa ajaoa,Mwalimu wa Shule ya Green Acress,Mwanafunzi wa Shahada ya Pili ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,nikawa nakaa nae chini ya miti eneo la UDSM tunajadili mambo ya mustakabali  wa taifa letu huku tukimsubiri Dk.Mvungi arudi ofisini kwakwe ili twende tukamuone maana Dk.Mvungi nae alikuwa ni Mhadhiri wa sheria wa UDSM.

Namfahamu vizuri Dk.Kahangwa kabla ajaoa na kuajiriwa kama Mhadhiri wa UDSM alikuwa akiishi Mwananyamala nyumba moja ha uswahili ambayo mvua ikinyesha eneo la uwanja wa nyumba ile aliyokuwa akiishi ina geuka bahari hadi alipopapata ajira UDSM na kubahatika kuoa na kupata watoto wawili na kuhama Mwananyamala kuamia nyuma za UDMS zilizopo eneo la Mwenge na kwenda nchini Ughaibuni kusoma shahada ya tatu.

Dk.Kahangwa aliporejea nchini Agosti mwaka   2013 , tulikutana nae kwa mara ya kwanza katika ofisini za iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kwa aliyekuwa Mjumbe wa Tume hiyo,marehemu Dk.Mvungi ,na mimi bila kujua nilifika siku hiyo ofisini kwa Dk.Mvungi na tukakutana pale na kuongea mambo mengi na kufurahi pamoja.

Nilimpongeza kwa kutunukiwa shahada ya Udaktari kwani alikuwa ametima ndoto yake ya kuwa Daktari wa Elimu kama alivyowahi kunieleza katika mahojiano yangu niliyofanya nae ambayo ipo chini kama kielelezo cha aliyowahi kuyasema na mipango ambayo  ameanza kuitimiza hatua kwa hatua.

Kwa wale walioshiriki siku ya kuaga mwili wa marehemu Dk.Mvungi katika uwanja wa Karimjee, lazima walipatiwa nakala ya kitabu kidogo cha historia ya marehemu Dk.Mvungi ambacho kiliandikwa na Dk.Kahangwa kama mchango wa kumuhenzi mzee wetu Dk.Mvungi.

Dk.Kahangwa moja ya ndoto yake ni kuwa na PhD , kuwa mgombea urais wa Tanzania.

Na kupitia ndoto zake hizo tayari ndoto ya kupata PhD kaishaitimiza, ndoto ya kugombea urais kupitia NCCR imetimia kwani NCCR imeteua jina lake kuwa mgombea urais ambalo jina hilo litapelekwa UKAWA ambapo UKAWA itaketi na kupitisha jina moja la mgombea urais kati ya majina yaliyoletwa na vyama vjnavyounda umoja huo na kisha kupitisha jina moja la mgombea urais atakaye iwakirisha UKAWA.

Dk.Kahangwa ambaye yeye upenda kuniita mimi kwa jina Mpambanaji au First Lady wa Dk.Mvungi, ninavyomfahamu mimk Dk.Kahangwa ni kijana mwenye hofu ya Mungu,mpenda haki na asiyependa siasa chafu.

Dk.Kahangwa aamini katika siasa chafu, yeye anaamini msomi aliyefundwa kisomi anaweza kufanya siasa safi na kufanikiwa kuleta mageuzi ya kimaendeleo katika taifa letu.

Dk.Kahangwa ni msomi anayejiamini na asiyeteteleka katika kile anachokiamini, siyo mpenda makuu ila ni mtu ambaye moyo na fikra zake tangu nianze kufahamiana naye ni kijana ambaye anaipenda nchi yake na anayetaka kuitumikia zaidi kupitia ulingo wa siasa na tangu mapema amekuwa akifanya hivyo ushahidi huo ni nao na anatabia moja ya kutopenda kuonekanaonekana kwenye vyombo vya habari.

Ulipokuwa ukimsikia Dk.Mvungi au baadhi ya viongozi wa Chama cha NCCR - Mageuzi, wanazungumzia mfumo wa elimu nchi huku wakionyesha takwimu ,uzuri na ubaya wa mfumo wa elimu hapa nchini na hadi sasa ukisikia wanaongelea kuhusu hilo, ujue ni Dk.Kahangwa aliwaandikia andiko la kitaalamu linalohusu elimu na viongozi wakalisemee majukwaani.

Nakumbuka mwaka jana Dk.Kahangwa alikwazwa na kitu kimoja kilichotokea ndani ya chama chake akaanza kuingiwa na mawazo mabaya ambayo sitayataja hapa kwenye hii makala ,alinishirikisha nimsaifie ushauri.

Mimi nilimjibu kuwa asichukue uamuzi wowote wakati ana jazba, atulie akishatulia hasira zitaisha na atakumbuka nasaha na  mafunzo ya kwa sisi wanamageuzi,aliyokuwa akitufundisha mzee wetu Dk.Mvungi ya kuipambanaji na kwamba uamuzi ambao angeuchukua ni kama angekuwa amepuuza mafunzo tuliokuwa tukipewa nyumbani,na ofisini kwa  Dk.Mvungi mara kwa mara ya jinsi ya kufanya siasa za mageuzi nchini.

Alielewa na akaachana na mawazo yake akasonga mbele na hadi alipopata amefika.

Kukaa kwangu kote na Kaka Kahangwa kumenifundisha mambo mengi kwanza kumenifundisha elimu haimtupi mtu kwani maisha aliyokuwa nayo awali Kahangwa kabla ya kujiendeleza kielimu zaidi siyo maisha aliyonayo sasa, uvumilivu, kumcha Mungu, kupenda watu na kuheshimu mkubwa na mdogo na kusikiliza maoni ya watu ambao amewazidi elimu,kuwa na msimamo katika masuala ya msingi.

Kaka George na kupa hongera kwa NCCR Mageuzi kwa kuonyesha imani na wewe hadi wamepitisha jina lako uwe mgombea urais kupitia chama hicho,ni hatua nzuri.

Lakini nakutaka utambue kuwa utakuna na changamoto nyingi katika safari yako, usikate tamaa , pambana kadri ya uwezo wako utakapofikia ndiyo Mungu atakuwa alikuwa amekuandikia ufikie hapo katika  safari yako hiyo ya kuutaka urais wa taifa hili .

Kwani kumbuka wakati tulikuwa tunaketi kitako na Dk.Mvungi alikuwa akituambia kuwa yeye katika maisha yake alishaweka nia ya kuwa siku moja agombee nafasi ya Rais ili aweze kuwatumikia vyema ,na kwamba suala la kushinda au kushindwa yeye lilikuwa halimpi shida kwani ndoto yake ya kugombea urais aitimize na aliitimiza.

Namalizia kuandika makala hii kwa kusema nimefarijika kuona kijana alitengenezwa na kupitia katika mikono ya Dk.Mvungi yaani Kahangwa naye leo hii ameweza kupanda juu na kufikia hadhi aliyowahi kuipata Dk.Mvungi toka NCCR Mageuzi ya kuteuliwa kuwa  mgombea urais mwaka mwaka 2005 , jana kijana wa Dk.Mvungi ,Dk.Kahangwa nae ameweza kupata hadhi hiyo ya kuwa mgombea urais kwa tiketi ya NCCR Mageuzi.

Mungu amrehemu Dk.Mvungi kwani watu wengi walipita mikononi mwake na aliwafundisha mema na leo hii wanachomoza katika nyanja mbalimbali.

Chanzo: Blogg:www. katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Aprili 25 mwaka 2015.

******************I
(Tujikumbushe mahojiano niliyowahi kufanya na George na Kahangwa  enzi hizo mimi nikiwa Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima  ambapo makala hiyo ilichapishwa katika  Gazeti la Tanzania Daima la  Mei 27 mwaka 2009)

ELIMU, MAARIFA NA UCHUMI

Na Happiness Katabazi

Ni jinsi gani elimu inaweza kulisaidia taifa letu kiuchumi na kijamii katika ulimwengu wa sasa?

Takribani nyakati zote katika historia ya mwanadamu, elimu imekuwa ya manufaa sana kwa mtu mmoja mmoja anayeipata na kwa jamii ambayo mpata elimu anaishi. Leo hii zinapoendelea jitihada za kihimizana katika ngazi ya familia na taifa kwamba hapana budi kuwekeza sana katika suala la elimu bila suluhu, kimsingi sababu kuu ni hilo kwamba elimu ina manufaa kwa mtu binafsi (private returns) na kwa jamii (social returns). Ni dhahiri basi kwamba anapoelimika mtanzania mmoja ananufaika yeye na linanufaika taifa zima la Tanzania.

Katika ulimwengu wa sasa unaouzungumzia, manufaa hayo ya elimu yanazidi kutambulika na kuongezeka kiasi kwamba katika mataifa mbali mbali hususan ya ulimwengu wa kwanza elimu inatazamwa kuwa ndilo tumaini la kipekee kiuchumi na kimaendeleo kwa sasa na kwa siku nyingi za usoni.

Utakumbuka kwamba uchumi wa nchi moja moja una msingi wake, matharani hapa Tanzania kwa miongo kadhaa tunazungumza kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa taifa,kwa maneno mengine msingi mkuu wa uchumi wetu ni kilimo. Utakuwa unafahamu pia kwamba mataifa kadhaaa yaliyoendelea kiviwanda yanazungumzia uzalishaji wa viwandani kuwa ndio msingi mkuu wao kiuchumi (industrial economy)
Mtazamo wa kidunia sasa hivi ni kwamba uchumi wa ulimwengu hususan wa mataifa yanayoitwa yaliyoendelea unahama katika kutegemea zaidi viwanda na sekta nyinginezo za uzalishaji, tegemeo kubwa sasa ni maarifa ambayo chimbuko lake ni elimu. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa dunia ya leo na kesho inaelekea zaidi katika uchumi wa maarifa (knowledge economy)

Nchi za ulimwengu wa tatu, ikiwemo Tanzania yetu zimedumu katika kutegemea kilimo, zikashindwa kuingia katika uchumi wa viwanda. Kwa sasa nchi hizi zinayo fursa ya kujikwamua na kutoka katika maendeleo duni endapo zitajielekeza katika kuutafuta uchumi wa maarifa. Kwa mantiki hiyo nchi yetu inayo fura ya kuingia katika ulimwengu wa kwanza, bila kulazimika kutafuta ufalme wa viwanda mama, yatosha tukiuendea sasa kwa udi na uvumba uchumi wa maarifa. Elimu ndio chombo pekee cha kutupeleka huko.

Ni nini hasa unachokimaanisha kwa kusema uchumi wa maarifa na una uhakika gani kwamba kwa kuutafuta uchumi huo taifa letu litaondoka katika ulimwengu wa tatu?

Ndugu mwandishi, upo ushahidi usiotiliwa shaka kutoka katika mataifa mbali mbali ambayo awali hayakufanikiwa sana katika uchumi wa viwanda yakaja kupata maendeleo makubwa sana kutokana na maarifa. Tuchukulie kwa mfano nchi ya Finland, kwa miongo kadhaa taifa hilo lilikuwa halina mafanikio makubwa kiuchumi, wafinland walitegemea sana zao la mbao na mara kwa mara uchumi wao uliyumba. Lakini tokea serikali ya nchi hiyo ilipofunguka macho ikawekeza kwa nguvu katika maarifa, Finland kwa sasa limekuwa taifa lenye mafanikio makubwa sana kiuchumi kwa kiasi kilichoushangaza ulimwengu. Kwa sasa finland ni moja ya nchi chache sana duniani zinzoweza kutoa kwa raia wake elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vikuu. Mataifa yaliyoko katika umoja wa nchi za Ulaya yanaendelea kujifunza kwa bidii kile ambacho finland imekifanya, wakijua fika kuwa katika ulimwengu wa utandawazi ni maarifa pekee yatakaloliwezesha taifa kuwa na nguvu kubwa kiuchumi.

Kwa ufupi uchumi wa maarifa ni uchumi unaotegemea maarifa kama raslimali kuu. Unajua maliasili kama madini na ardhi ni rasilimali, fedha ni rasilimali hali kadhalika watu ni raslimali. Hizo ni raslimali zinazoshikika na kuonekana wazi (tangible resources) lakini maarifa ni tofauti kidogo maana ni intangible. Viel vile wakati rasilimali tangible hutumika na kuisha, rasilimali ya maarifa haiwezi kuisha bali huwa bora zaidi na kuongezeka kadiri inavyotumika.
Uchumi huu wa maarifa unaeleweka zaidi unapochanganuliwa katika zile zinazoitwa nguzo zake kuu nne. Hizo nguzo ni Elimu na uendelezi wa rasilimali watu; pili, Utafiti, uvumbuzi na ubunifu; tatu, Tekinolojia na mawasiliano; na nne ,ni Mfumo wa utawala na nyenzo sahihi.

Katika nguzo ya elimu na uendelezi wa rasilimali watu, ili taifa liufikie uchumi wa maarifa linatakiwa kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa ina ubora wa hali ya juu na watu wa nchi husika wanaendelezwa kwa wingi, kama sio wote ili wafikie viwango vikubwa vya elimu na kuyapata maarifa watakayoyatumia kuujenga uchumi wao.

Taifa halina budi kuhakikisha si tu kwamba halina raia yoyote mjinga bali pia asilimia kubwa ya raia ni wahitimu wa vyuo vikuu katika fani mbali mbali na ni wasiokoma kutafuta maarifa hata wawapo kazini na katika maisha yao yote ili wazidi kupata ujuzi wa kazi, wawe wazalishaji zaidi na washindani.

Katika nguzo ya utafiti, uvumbuzi na ubunifu taifa linatakiwa kuwa na mchakato endelevu wa kufanya tafiti zinazolenga kugundua maarifa mapya, suluhu za matatizo mbalimbali, ugunduzi wa nyenzo na uboreshaji wa zana za kazi. Tafiti za namna hiyo zitalifanya taifa kuboresha kila sekta ya uzalishaji na zaidi sana zitalinufaisha taifa kwa njia ya kuuza maarifa yaliyogunduliwa kwa mataifa mengine. Nadhani unafahamu ni kiasi gani wagunduzi wa vitu mbali mbali wanazinufaisha nchi zao kwa kile wanachokigundua.

 Chukulia mfano wa ugunduzi wa simu za mkononi unavyozinufaisha nchi zinazozalisha simu hizo. Ni wazi kuwa elimu yetu inapaswa kuwa na mkono katika hili, tunatakiwa kuwa na elimu inayomfanya mwanafunzi awe na uwezo wa kutafiti na kugundua maarifa mapya au kuwa mbunifu hata akaboresha yale yaliyopo.

Kuhusu nguzo yya teknolojia na mawasiliano, taifa linapaswa kuwa la watu wenye kupata kwa wingi habari sahihi na zenye manufaa, wawe na mawasiliano ya kutosha tena ya haraka na wawe watumiaji wazuri wa teknolojia ya habari na mawasiliano kiasi kwamba njia hizo zinawasaidia kuzalisha mali zaidi, na kwa wakati muafaka. Fikiria kwa mfano, unapokuwa na mkulima au mfanya biashara anayeweza kupata mtandao unaomwezesha kupata habari za soko la mazao yake au bidhaa zake kutoka ulimwengu mzima, ni dhahiri mtu huyu akitumia habari hizo vizuri kamwe hatakuwa sawa na yule anayejua tu habari za soko la kijijini kwake. Hata katika hili elimu ina jukumu muhimu kwani ni kupitia katika elimu watu hujifunza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Nguzo ya nne ya mfumo wa utawala na nyenzo sahihi. Katika hili taifa linahitaji kuwa na mfumo unaowezesha maarifa yanayopatikana yanatumika vilivyo katika sekta za uzalishaji. Ili kufanikisha hilo hapana budi kuwe na uhusiano wa maana kati ya taasisi za elimu na sekta mbali mbali za uzalishaji. Matharani, kuwepo kwa uhusiano wa vyuo vikuu na sehemu za ajira ili kinachofunzwa vyuoni kiwe ni chenye manufaa mahali pa uzalishaji. Vile vile kuwe na mfumo unaowezesha maarifa kuzalishwa na kutumika katika nchi. Mfumo huo uwezeshe mambo kadhaa kama vile upatikanaji wa nyenzo za kufanyia tafiti, uhuru wa kujiendeleza kimaarifa mahali pa kazi na uhuru wa watu kufanya ugunduzi majaribio na ubunifu.

Unafikiri nguzo hizo za uchumi wa maarifa ziko katika hali gani hapa nchini, taifa letu linawezesha hayo unayoyasema?

Nchi yetu Tanzania, kwa kweli ina hali mbaya sana katika nguzo zote nne. Laiti kama tungekuwa vizuri katika japo nguzo mbili, uchumi wetu ungekuwa na hali nzuri kiasi chake. Elimu yetu imeendelea kuyumbisha na kuwa na hali duni kuanzia kile tunachokiamini na kukitekeleza kama falsafa ya elimu nchini, sera za elimu, mitaala, mchakato wa kufundisha na kujifunza, uwezeshaji wa watendaji katika elimu na suala zima la utadhimini wa elimu.

Ukiangalia katika takwimu zilizotolewa hivi karibuni na benki ya dunia, Tanzania ina alama 7 kwa mia katika elimu na uendelezaji wa rasilimali watu, asilimia 17 katika utafiti na ugunduzi, asilimia 8 katika teknolojia ya habari na mawasiliano, na asilimia 34 katika mfumo na nyenzo. Kwa hiyo uchumi wetu unaitegemea rasilimali ya maarifa kwa asilimia takribani 17 tu, wakati yapo mataifa yamekwisha kufikia asilimia 90 na zaidi.

Unaweza kung’amua kwa takwimu hizo jinsi taifa letu lilivyo na elimu isiyokidhi. Vile vile licha ya kwamba watanzania sasa tunakadiriwa kuwa milioni 39 watu wetu wengi hawajaendelezwa kiasi cha kulinufaisha taifa kiuchumi, tunayo rasilimali watu ya kutosha lakina bahati mbaya iliyokosa maarifa. Mwalimu Nyerere aliwahi kutuambia kwamba, ili nchi iendelee inahitaji pamoja na vitu vingine, watu wake. Lakini watu bila maarifa ni hasara tupu.
Kwa upande wa tafiti nako hatuko vizuri kwa sababu nyingi, kwanza matharani katika vyuo vikuu, utakuta tafiti zinafanyika ndio, lakini si kwa maslahi ya taifa bali kwa wafadhili wan je wanaotoa fedha kwa ajili ya tafiti hizo. Ninachosema hapa ni kwamba watafiti wachache tulionao badala ya kutumiwa na taifa wanatumiwa na mashirika ya nje kufanya tafiti ambazo hao wageni wana maslahi nazo, na watafiti wetu wanakubali maana wanataka pesa. Laiti kama Taifa letu, hususan serikali kuu, ingeona haja ya kuwekeza katika utafiti na kuwawezesha watafiti wetu kutumia umahili wao katika kutafuta maarifa mapya, na kutafiti suluhu za matatizo yetu yote sisi wenyewe.

Kibaya zaidi hata tafiti chache zilizokwisha fanyika nchini, matokeo ya tafiti hizo ni nadra kusikia yakitumiwa vilivyo katika sekta za uzalishaji. Ripoti nyingi za tafiti zimeishia kujaa vumbi katika shelf za maktaba za vyuo vikuu bila kutumiwa.

Ama kwa suala la teknolojia ya habari na mawasiliano, licha ya kwamba hatujamudu kuingiza jambo hili katika shule zetu za sekondari, wengi miongoni mwa vijana wanaojua kutumia intertnet na vitu kama simu za mkononi bahati mbaya hawazitumii katika kiwango kizuri cha kuwanufaisha . Kwa walio wengi internet ni kwa ajili ya kutumiana ujumbe wa kirafiki, kuangalia picha za pono, hali kadhalika simu ni kusalimiana tu. Wachache sana wanaotumia mawasiliano kujiendeleza kielimu, kutafuta maarifa na au kupata habari za masoko na biashara.

Unafikiri ni nini kifanyike?
Yapo mengi ya kufanya, labda mimi nizungumze kupitia jicho la taaluma yangu. Hatuna budi kuwa na sera za elimu zitakazotuhakikishia kwamba kila mwenye uwezo wa kupata elimu ya juu anaipata bila vikwazo vya karo, nafasi kidogo na kadhalika. Tunatakiwa kuongeza fursa kwa gharama yoyote ile, huo ni uwekezaji utakaotuletea manufaa makubwa sana kiuchumi kama nilivyoeleza.

Hatuna budi pia kuwa na mitaala inayomwezesha mwanafunzi kuwa wa manufaa kabisa katika ulimwengu wa kisasa. Tunahitaji wahitimu wanaoajirika, tuahitaji elimu ituzalishie wagunduzi na wabunifu mahiri, watafiti wachapa kazi na watu wanaodumu katika kuyatafuta maarifa kwa bidii katika maisha yao yote.

Kadri tutakavyoendelea na sera za kukopesha watu wachache waingie vyuo vikuu ndivyo tutakavyolididmiza taifa. Kadri tutakavyoipuuza taaluma ya ualimu ndivyo tutakavyo dunisha elimu yenyewe na kubaki kuwa wasindikizaji katika ulimwengu wa utandawazi.

Hujazungumzia manufaa ya elimu kijamii, unasemaje hapo?

Nimetaja jambo la social returns, lakini kwa upande mwingine elimu inapaswa kuinufaisha jamii kwa kuzalisha wahitimu waadilifu.kwa sasa mitaala yetu haijakaza sana suala la maadili na shule nyingi hazionekani zikiwaadilidha watanzania. Yamkini ndio sababu tuanpata wingi wa watumishi na viongozi wala rushwa, wabadhilifu na mafidsadi.

Laiti kama mitaala yetu yote kuanzia elimu ya awali hadi vyuo ingesisitiza vya kutosha elimu ya maadili. Tunatakiwa kuwa waadilifu katika mahusiano, katika kazi, katika utunzaji wa mazingira, katika utumiaji wa rasilimali na katika mwenendo kwa ujumla. Elimu inalojukumu la kutuhakikishia hilo.

Nini historia yako kwa ufupi?

Mimi ni mzaliwa wa mkoa wa Kagera. Umri wangu ni miaka 39 sasa. Nimesoma elimu ya msingi katika shule ya Omurushenye na baadaye Bilele ya mjini Bukoba. Nilipata elimu ya sekondari katika shule ya Sekondari Bukoba. Nilisomea ualimu katika chuo cha ualimu Korogwe. Kwa miaka kadhaa nilikuwa mwalimu wa elimu ya Msingi. Baada ya kujiendeleza na kupata shahada ya kwanza ya ualimu katika chuo kikuu cha Dar es salaam, nilifungisha kwa miaka miwili mara hii elimu ya sekondari. Nilifanikiwa pia kusoma shahada ya uzamili katika elimu, hapa hapa chuo kikuu cha Dar es salaam, na hatimaye kuajiriwa na chuo hiki katika kitivo cha elimu, ambapo kazi yangu ni unadhiri katika masuala ya utawala wa elimu, mipango na sera. Nimepata pia mafunzo ya elimu na Utandawazi katika chuo Kikuu cha Oulu nchini Finland. Nimeoa na tuna watoto wawili.

Ni nini matarajio yako ya baadaye?

Kwa taaluma yangu, inanipasa kujiendeleza zaidi na zaidi katika kuyatafuta maarifa. Natarajia kuanza masomo ya shahada ya juu ya falsafa huko ughaibuni mwishoni mwa mwezi huu. Bila shaka ninalo jukumu la kuitumia elimu yangu katika utumishi kwa taifa langu.

 Ndoto yangu ni kupata fursa pana za kuwahudumia na kuwatumikia watanzania wengi zaidi kama sio wote kwa kadri Mungu atakavyonipa kibali.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Mei 27 mwaka 2009 .

0716 774494

FRANCIS HOZA DHIDI YA EDWARD LOWASSA




MTAZAME FRANCIS HOZA,MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI WA BARAZA LA UVCCM ,MOROGORO AKIENJOY HAKI YAKE YA KIKATIBA YA KUTOA MAONI YAKE ILIYOAINISHWA KATIKA IBARA YA 18(a) YA KATIBA YA NCHI..

MANGULA: KANUNI ZITAWAMEZA




Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula amesema kanuni za uchaguzi  za chama hicho zitawameza makada wake wanaotumia fedha kuwanunua wapigakura kama maandazi.

Mangula alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanaCCM wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam katika ziara yake katika majimbo mawili ya Ukonga na Segerea.

Mangula alisema wapo wagombea wanaodhani kuwa wao ni maarufu na wanasahau kuwa fedha walizotanguliza mbele ndiyo maarufu na siyo wao wenyewe, hivyo wanajidanganya.

“Unatawanya fedha kila kona, kwa kila kundi, halafu unajiita maarufu badala ya kuona fedha zako ndiyo maarufu... unajidanganya ukijua kuwa unajidanganya,” alisema.

Aliwataka wanachama hao kuwa makini na watu wenye tamaa ya kwenda Ikulu, huku akinukuu alichowahi kukisema Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuwa; “mtu yeyote anayetafuta kwenda Ikulu kwa fedha muogopeni kama ukoma.”

Akifafanua maadili na kanuni za wagombea wa CCM, Mangula anayeongoza pia Kamati Ndogo ya maadili, alisema, “Yeyote anayekukuruka kuutafuta uongozi kwa kutumia fedha, kununua wanachama ili apigiwe kura au apitishwe, akiona jina lake halikutoka ajue limemezwa na kanuni na sheria za uchaguzi.”

Kauli hiyo ya Mangula imekuja wakati kamati ya maadili anayoiongoza ikiendelea kuwachunguza makada sita wa chama hicho kwa madai ya kuanza kampeni mapema na kufanya vitendo vinavyokiuka maadili.

Alisema CCM ni umoja, hivyo wanaoleta migogoro ni watu waliopotoka ambao wanashindwa kutekeleza sheria walizojiwekea na wenye tamaa ya madaraka.

Mangula alisisitiza kuwa anayowaeleza makada hao si hadithi, bali ni ya kweli na yaliwahi kufanyika huko nyuma akitolea mfano mwaka 2000 akiwa Katibu Mkuu wa CCM walipowasimamisha wagombea wa majimbo ya Morogoro ambao wagombea sita walihonga, uchunguzi ukafanyika ilipobainika walisimamishwa wote na wahusika wakapigwa marufuku kugombea.

Alisema hata mkoani Singida makada waliobainika kusambaza fedha ili wachaguliwe walitimuliwa na nafasi ikatangazwa upya.

“Wakalalamika demokrasia ipo wapi, tukawajibu hakuna cha demokrasia, unalazimisha vipi demokrasia kwa kutumia fedha?” alisema.

Alisema kutumia fedha kwenye uchaguzi ni tatizo sugu, hadi watendaji wanakula rushwa kwa wagombea mpaka wanafikia kupanga hadi bei ya hongo.

“Ni aibu, watu wanajua kabisa watapata shilingi ngapi, wamepanga hadi bei ya hongo na wanachukua kila upande, wanasema ndiyo wakati wao wa kuvuna, wamekuwa malaya wa kisiasa, kutokana na kutokuwa na maamuzi wala kufuata kanuni za chama,” alisema Mangula. Alisema kutokana na kukithiri kwa tabia ya utovu wa nidhamu kwa wagombea wa CCM, hivi sasa kadi za chama ni kama keki ya moto, kila mtu anazitaka, wagombea wanawanunulia kadi wanachama, wanawalipia kadi za Jumuia ya Wazazi ili waje kuwachagua baadaye, jambo ambalo ni kosa.

Chanzo: Mwananchi7 zitawameza makada wake wanaotumia fedha kuwanunua wapigakura kama maandazi.

Mangula alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanaCCM wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam katika ziara yake katika majimbo mawili ya Ukonga na Segerea.

Mangula alisema wapo wagombea wanaodhani kuwa wao ni maarufu na wanasahau kuwa fedha walizotanguliza mbele ndiyo maarufu na siyo wao wenyewe, hivyo wanajidanganya.

“Unatawanya fedha kila kona, kwa kila kundi, halafu unajiita maarufu badala ya kuona fedha zako ndiyo maarufu... unajidanganya ukijua kuwa unajidanganya,” alisema.

Aliwataka wanachama hao kuwa makini na watu wenye tamaa ya kwenda Ikulu, huku akinukuu alichowahi kukisema Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuwa; “mtu yeyote anayetafuta kwenda Ikulu kwa fedha muogopeni kama ukoma.”

Akifafanua maadili na kanuni za wagombea wa CCM, Mangula anayeongoza pia Kamati Ndogo ya maadili, alisema, “Yeyote anayekukuruka kuutafuta uongozi kwa kutumia fedha, kununua wanachama ili apigiwe kura au apitishwe, akiona jina lake halikutoka ajue limemezwa na kanuni na sheria za uchaguzi.”

Kauli hiyo ya Mangula imekuja wakati kamati ya maadili anayoiongoza ikiendelea kuwachunguza makada sita wa chama hicho kwa madai ya kuanza kampeni mapema na kufanya vitendo vinavyokiuka maadili.

Alisema CCM ni umoja, hivyo wanaoleta migogoro ni watu waliopotoka ambao wanashindwa kutekeleza sheria walizojiwekea na wenye tamaa ya madaraka.

Mangula alisisitiza kuwa anayowaeleza makada hao si hadithi, bali ni ya kweli na yaliwahi kufanyika huko nyuma akitolea mfano mwaka 2000 akiwa Katibu Mkuu wa CCM walipowasimamisha wagombea wa majimbo ya Morogoro ambao wagombea sita walihonga, uchunguzi ukafanyika ilipobainika walisimamishwa wote na wahusika wakapigwa marufuku kugombea.

Alisema hata mkoani Singida makada waliobainika kusambaza fedha ili wachaguliwe walitimuliwa na nafasi ikatangazwa upya.

“Wakalalamika demokrasia ipo wapi, tukawajibu hakuna cha demokrasia, unalazimisha vipi demokrasia kwa kutumia fedha?” alisema.

Alisema kutumia fedha kwenye uchaguzi ni tatizo sugu, hadi watendaji wanakula rushwa kwa wagombea mpaka wanafikia kupanga hadi bei ya hongo.

“Ni aibu, watu wanajua kabisa watapata shilingi ngapi, wamepanga hadi bei ya hongo na wanachukua kila upande, wanasema ndiyo wakati wao wa kuvuna, wamekuwa malaya wa kisiasa, kutokana na kutokuwa na maamuzi wala kufuata kanuni za chama,” alisema Mangula. Alisema kutokana na kukithiri kwa tabia ya utovu wa nidhamu kwa wagombea wa CCM, hivi sasa kadi za chama ni kama keki ya moto, kila mtu anazitaka, wagombea wanawanunulia kadi wanachama, wanawalipia kadi za Jumuia ya Wazazi ili waje kuwachagua baadaye, jambo ambalo ni kosa.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi,April 22 mwaka 2015.

FM ACADEMIA WANAREKODI NYIMBO MPYA

 MuleMule FBI
Kingombe Blaise 'KingBlaise'





FM ACADEMIA WANAREKODI NYIMBO MPYA

Na Happiness Katabazi
BENDI ya FM Academia (Wazee wa Ngwasuma) ,hivi sasa wapo Studio  wanarekodi nyimbo mpya .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mhasibu wa bendi hiyo Calvin Mkinga alisema nyimbo ambazo zimeanza kurekodiwa ni wimbo wa Watabiri uliotungwa na Mulemule FBI na Bodaboda Kariakoo ulitungwa na Kingombe Blaise'Kingblaise'   na kwamba wanarekodi nyimbo hizo katika studio ya Metro, watunzi wa nyimbo hizo ni hapo pichani.


Mkinga alisema Redio na Televisheni zimetoa masharti kwa bendi za muziki wa dansi nchini kuwa ili ziwe zinapiga nyimbo za bendi za muziku wa dansi ni lazima bendi hizo zitunge nyimbo zitakazoimbwa kwa dakika chache kwani mifumo ya utangazaji iliyofungwa katika vituo vya redio na Televisheni ni mfumo wa kisasa ambao hautaki kupiga wimbo  wenye dakika nyingi,unaitaji wimbo uwe ni wa dakika nne tu.

' Wanamuziki wetu walizoea kutunga wimbo unaopigwa kwa dakika 15 sasa hivi sharti linataka watunge nyimbo zenye dakika nne na tayari wanamuziki wetu wameishatunga nyimbo kadhaa nazimeishaanza kurekodiwa na kwamba jumla wanatarajia kurekodi jumla ya nyimbo sita.alisema Mkinga.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Aprili 20 mwaka 2015.

NAMLILIA DITOPILE


*LEO NI MIAKA SABA YA KIFO CHAKE

Na Happiness Katabazi

LEO Aprili 20 mwaka 2015 , rafiki  yangu Marehemu ,Ukiwaona   Ditopile Ramadhan Mwinshehe Wa Mzuzuri  anatimiza miaka saba tangu afariki dunia Aprili 20 mwaka 2008, Mkoani Morogoro.

Binafsi kila tarehe kama ya leo uwa namuenzi Swahiba wangu Ditopile kwa kuandika makala yakumbukizi ya kifo chake ukiwa ni mchango wangu kwake.

Leo nikikumbuka siku ya kufariki kwa Brother Ditopile ,napenda kumsimulia  Ditopile ambaye alikuwa Kada wa CCM baadhi ya yanayoendelea hapa nchini kama ifuatavyo;

Ditopile ,Oktoba mwaka 2015 ,Tanzania itafanya uchaguzi  Mkuu wa nafasi ya Rais,Ubunge na Udiwani.

Hadi sasa vyama vyote vya siasa kikiwemo chama chako cha CCM bado hakijatangaza ratiba ya vikao husika kumpata mgombea urais.

Ditopile ,minyukano ya kisiasa ndani ya CCM imezidi kuliko ulivyoicha, makundi yamekuwa mengi,chuki,uzushi,matumizi ya fedha yametawala ,ukiukwaji wa Kanuni ,baadhi ya makada wa wamekuwa wakidharau  maagizo ya viongozi wao wa juu wa chama.

Kamati ya Maadili ya CCM ,Februali mwaka 2014  ilitoa hukumu yake ya kifungo cha mwama mmoja na kukaa chini ya uangalizi baada ya kuwakuta na   hatiani kwa makosa kuvunja kanuni ya CCM ya mwaka 2010 na kuanza kampeni mapema za urais kifungo cha mwaka mmoja  Makada wake sita wakiwemo Bernad  Membe, January  Makamba,Edward Lowassa,  na wengine.

Lakini Machi 31 mwaka huu, Kamati Kuu ya CCM iliagiza kifungo hicho ambacho kilikuwa kinatakiwa kimalizike Februali mwaka huu, lakini kwa agizo hilo la Kamati Kuu la Machi 31 mwaka huu, niwazi kifungo hicho ni endelevu.

Hata hiyo agizo hilo la Kamati Kuu, limesababisha kambi za watu wanaotajwa kugombea urais ambao bado kifungo kinaendelea kubaki na hali ya sintofahamu kuwa je ,wagombea wanaowaunga mkono kweli wataruhusiwa na CCM kugombea?.

Tusubiri maamuzi ya vikao vya juu vya  CCM wakati ukifika maana ndio vyenye mamlaka ya kutupatia mgombea wa urais ambaye wataona amekidhi vigezo walivyojiwekea.

Rafiki yako Rais Jakaya Kikwete ,Oktoba mwaka huu, atamaliza atamaliza muda wake wa miaka 10 ya kuwa Rais wa Tanzania.

Pia hivi sasa Tanzania imekumbwa na jinamizi la ajali,na kule ,tishio la Ugaidi na kule nchini Afrika Kusini ,baadhi ya wananchi wa taifa hilo wameamua kujichukulia sheria mkononi kwa kutumia silaha kuwatoa roho na kuwafukuza nchini kwao wageni wanaoishi humo na kusababisha wageni mali zao kuchomwa moto,kuuwawa kikatiri hali iliyosababisha baadhi ya mataifa mengine kufunga balozi zake zilizopo Afrika Kusini.

Lakini pia hapa nchini mwaka jana, baadhi ya vyama vichache vya upinzani vimeanzisha umoja wao unajulikana kwa jina la Umoja wa Katiba ya Wananchi ( UKAWA).

Umoja huo umeazimia kumsimamisha mgombea umoja wa kiti cha Rais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Pia umoja huo wakati mwingine umekuwa ukiitoa jasho CCM na serikali yako lakini mwisho wa siku mambo yanakwenda sawa.

Serikali yako ya CCM imekumbwa na changamoto nyingi lakini zimekuwa zikitatuliwa .

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa dini za kikristo,kiislamu wameamua kujiingiza kwenye siasa waziwazi hali inayosababisha mvurugano katika jamii na baadhi ya waumini kupunguza imani kwa baadhia ha viongozi wa dini.

Hivi sasa baadhi ya makada wa chama chako cha CCM wamezidisha tabia ya unafki,uzandiki,hawana mapenzi ya kweli na chama  chao,wavujisha siri wazuri wa  siri za serikali na CCM kwa wapinzani na wapo ndani ya CCM kwaajili ha kupata madaraka wao binafsi au watu wanaowaunga mkono .

Leo hii ni nadra sana kuona viongozi wa ngazi ya Tawi,Kata,Wilaya,Mkoa,Taifa kufanya mikutano ya hadhara ya CCM kama kipindi kile Rais Benjamin Mkapa alipokuwa Mwenyekiti wa CCM wakikipigania chama kufa na kupona na kuuza sera za chama hicho.

Tunamuona Katibu Mkuu wa CCM, Abdruhman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ndio waliokuwa wakifanya mikutano ya hadhara katika mikoa mbalimbali.

Lakini binafsi nilipata fursa ya mahojiano na baadhi ya makada wa CCM kuwa ni kwanini CCM ya sasa viongozi wa ngazi hizo hatuwaoni mitaani wakienda kanadi sera za CCM majukwaani kama enzi Rais Mkapa, walikuwa na majibh tofauti.

Wengine waliniambia chama hakiwawezeshi kiuchumi vya kutosha kufanya mikutano hiyo, wakati mwingine watendaji wa CCM wanachelewa kulipwa mishahara na CCM, makundi ndani ya chama hicho kwani unakuta kuna kiongozi mmoja wa CCM ngazi fulani ana moyo wa dhati wa kukitumikia chama hicho ikiwa ni pamoja kunadi hadharani sera za CCM lakini anawekewa mikingamo na kundi ambalo linaona akinadi sera za chama atajipatia umaarufu.

Na siyo siri leo hii kuna baadhi ya wanachama wa CCM wanahofia kuvaa nguo zenye sare za CCM na kutembea nazo mtaani kwasababu wanaogopa kuzomewa.

Wanachama wengi wa CCM hivi sasa jukumu la kuisemea na kuipigania CCM wamemuachia Rais Kikwete, Kinana,Nape na baadhi ya viongozi wengine wachache wa CCM.

Ukiwauliza kwanini wanashindwa kujibu tuhuma mbalimbali zinazoelekewa kwa CCM tena wakati mwingine ni habari za uzushi wa wazi ,wanasema wanaogopa kutukanwa na wafuasi wa vyama vya upinzani.

Na huu ndiyo ukweli na hata Februali Mosi mwaka huu, Rais Kikwete alipokuwa akihutubia katika mkutano wa sherehe za kukumbuka kwa CCM ,pamoja na mambk mengi alikemea hali hiyo na alisema baadhi ya wananchi hawawafahamu viongozi wa CCM Mkoa,wilaya,Kata,Tawi kwasababu viongozi hao hawaendi kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara .Hicho alichokisema  Kikwete ni ukweli.

Wosia wako ulioniachia wakuwa na subira,kujiendeleza kielimu,kuheshimu dola na kuheshimu mkubwa na mdogo ,uzalendo kwa taifa langu nauzingatia kwa vitendo na faida yake nimeanza kuziona.

 Nilikupenda ila Mungu alikupenda zaidi.


(TUJIKUMBUSHE MAKALA YANGU NILIYOIANDIKA APRILI 22 MWAKA  2008 ,TAREHE AMBAYO DITOPILE ALIZIKWA.)

NAMLILIA DITOPILE

Happiness Katabazi

ILIKUWA juzi saa 4:39 asubuhi, Aprili 20 mwaka 2008 , nikiwa nimeketi sebuleni na kunywa chai nyumbani kwetu Sinza ‘C’, nilipokea simu kutoka kwa mfanyakazi mwenzangu ambaye ni mchora katuni aitwaye, Said Michael ‘Wakudata’ akiniambia rafiki yako, Brother Ditopile, amefariki dunia.


Nilishtuka na ghafla mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio huku mikono ikitetemeka na kusababisha simu yangu ya kiganjani kuanguka kwenye zulia.

Kwakuwa hapo sebuleni nilikuwa nimekaa na mama yangu mzazi na kaka zangu, mama yangu alishtuka, akanikaribia na kuniuliza kulikoni? Ndipo nilipomweleza kwamba nimepokea simu inayosema rafiki yangu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (60) amefariki dunia.

Kwakuwa mama yangu naye alikuwa akimfahamu Ditopile, alishikwa butwaa. Kwakuwa siku hizi taarifa za kuzushiana vifo zimekuwa za kawaida ndani ya taifa hili, sikutaka kuziamini moja kwa moja taarifa hizo, niliamua kuokota chini ile simu yangu na kuanza kupiga kupitia namba zake (Ditopile) zote nne, ambazo nilizitumia kuwasiliana naye mara kwa mara.

Nilipokuwa napiga simu kwenye line zote hizo, line zote zilikuwa hazipatikani. Ndipo nilipochukua uamuzi wa kumpigia simu aliyekuwa Katibu Mkuu wa timu ya Ashanti, Arafat Said, kwa kuwa marehemu alikuwa ni mlezi wa timu hiyo, kumuuliza kuhusu tukio hilo, naye alinithibitishia ni kweli. Nikabaki nimejiinamia kwa simanzi kutwa nzima na kuishia kumwombea kwa Mungu.

Mara ya mwisho kuwasiliana na Ditopile ilikuwa ni Ijumaa saa mbili usiku ya wiki iliyopita.
Alinipigia akaanza kwa kunitania kwamba muda si mrefu nitakuwa mkwe wake kwa mtoto wake wa kiume aitwaye Ramadhani, ambaye yupo masomoni Uingereza.


Nikamjibu kwa kumtania kwamba sitakuwa tayari kuwa na baba mkwe ambaye ni chakaramu kama yeye, akajibu kwamba hiyo ndiyo tabia yake tangu mdogo, hivyo hawezi kuibadili ukubwani na kwamba yeye ataongoza msafara wa wazee wa Pwani kwenda kwa mzee Katabazi kumchumbia paparazzi (yaani mimi), ili familia yake iwe na mwandishi wa habari, kwani waandishi wa habari ambao enzi za uhai wake alipenda kuwaita paparazzi, walimuandika sana kwa mabaya yake na mazuri yake.

Baada ya kunieleza hayo, nilimweleza kwamba kuna mtoto wako aitwaye Ramadhani Mzuzuri, mapema wiki iliyopita alitembelea blog yangu na kuniachia ujumbe wa kupongeza kazi zangu, nami nilimuliza Ramadhani kwakutumia e- mail kwamba Ditopile ni baba yake na kama ni baba yake basi mimi rafiki yake.

Nilivyomweleza hivyo Ditopile, akaniambia hiyo ni sababu moja wapo iliyosababisha anipigie simu siku hiyo na akanieleza kweli yule ni mtoto wake.Baada ya kumaliza hadithi hiyo akaniomba nimsaidie kufahamu kesi yake imepangwa lini na kwa jaji yupi.


Nilimwambia kuwa nipe sekunde chache nitoe kitabu changu cha kumbukumbu ili niweze kukutajia tarehe, nikamweleza kwamba kesi yake itatajwa kwa mara ya kwanza Aprili 24 mwaka huu, mbele ya Jaji Njegafibili Mwaikugile.

Alishukuru na kuniambia: “Eh siku hiyo mapaparazzi wenzio wamejiandaaje kuja kunipiga picha?” Nilimjibu huku tupo timamu na kwamba siku hiyo tutahakikisha tunazingira pembe zote za Mahakama Kuu bila yeye kujua ili kuhakikisha tunaipata sura yake.Akacheka sana, akasema mapaparazzi mna taabu kweli.


Namlilia rafiki yangu Ditopile kwani tangu atoke jela nimekuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara kwa simu. Ila mara ya mwisho kuonana naye ana kwa ana na kuzungumza naye kwa takriban saa mbili ilikuwa ni Desemba 9, 2006 ndani ya Gereza la Keko alipokuwa amewekwa rumande.

Kama inavyofahamika, waandishi wa habari huwa hawaruhusiwi kuingia magerezani, lakini mzee Ditopile alimtuma mtu anipigie simu niende kumuona gerezani, ila nikifika pale gerezani nijitambulishe kwa jina bandia la Koku Katabazi, nimetokea mkoani Kagera na kwamba nivalie mavazi ya gauni kubwa na kitambaa kichwani ili maofisa magereza wa gereza hilo wasinitambue.

Kweli nilifanya hivyo na kabla ya kufikia sehemu ya kujiandikisha kwenye daftari la wageni, nilinunua maji chupa makubwa na mkate na tayari kusubiri niitwe jina la kuingia kumuona Ditopile.

Nilivyoitwa jina hilo, nilishtukia nadakwa kiaina na ndugu na jamaa wa mzee Ditopile na wakanieleza nisiwe na wasiwasi watanipeleka gerezani anapolazwa.

Kweli ilipofika zamu yangu, niliingizwa ndani ya gereza huku nikiambatana na ndugu yake mmoja ambaye ni mtu mzima kiumri, nikapandishwa sehemu ya kuzungumzia wageni ambapo ni hatua tano kutoka chumba alichokuwa akilala yeye na wenzake maarufu kwa jina la ‘Sick Bay’.

Baada ya kufika na kuketi kwenye kiti, Ditopile alitoka chumbani akaja kuzungumza nami, nilishindwa kujizuia nilibubujikwa machozi. Akaniita jina langu akisema na ujanja wako wote unalia? Nilimjibu kuwa jela si kuzuri, hasa anapopelekwa mtu unayemfahamu.
Akanijibu kwamba yote ni mipango ya Mungu na tumuachie Mungu.

Nilianza kumuuliza maswali ya hapa na pale kwamba ni kweli alikuwa amemuua yule dereva wa daladala, Hassan Mbonde (33), alisema ni kweli Novemba 4 mwaka 2006, alimuua kwa kumpiga risasi, ila hakuwa amekusudia kufanya tukio hilo, kwani dereva wa daladala aliligonga gari lake na alipowaambia kwanini waliligonga, dereva huyo alimtukana kwa kumuonyesha ishara ya kidole cha katikati.

“Happiness, kwakweli kwa utu uzima niliokuwa nao, wadhifa niliokuwa nao kweli mtu dereva alinigonga na nilipomhoji alinitusi kwa kutumia kidole cha katikati ya mkono wa kulia…kwakweli niligadhabika sana nikajikuta nachomoa silaha na kumfyatulia, licha ya kwamba halikuwa lengo langu.

“Siwezi kukana kwamba sikumuua yule dereva, ila nilimfyatulia risasi kutokana na hayo aliyonifanyia, ila naomba Mungu na ninaendelea kumuomba Mungu anisameheme, kwani hata vitabu vya Mungu vinakataza binadamu kutoana roho…hivyo tuiachie mahakama ndiyo itaamua,” alisema Ditopile.

Baada ya kumaliza mazungumzo yetu siku hiyo ambayo taifa likikuwa likisherehekea uhuru wake, nilimuaga kwamba nakwenda, akanisii nisimtupe kwa sababu yupo jela, niwe napita kumjulia hali na kumpatia taarifa mbalimbali, nikamkubalia.

Baada ya kuondoka gerezani hapo, kilichofuata, alikuwa akiletwa kwa nyakati tofauti katika Mahakama ya Kisutu na hatimaye Mahakama Kuu ambapo ndipo kituo changu cha kufanyia kazi.

Machi 9, mwaka jana, viwanja vya Mahakama Kuu viligeuka kuwa uwanja wa mapambano kabla na baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, kufikishwa mahakamani hapo na kutolewa kwa dhamana.

Mapambano hayo yalifanywa na watu wanaosadikiwa kuwa ni ndugu wa mshitakiwa Ditopile dhidi ya waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia mwenendo wake. Nami nilikuwa mmoja wao.

Machi 10, 2007 ambayo ilikuwa siku ya Jumamosi asububi, nikiwa na Mwadhiri Mwandamizi wa Sheria na Katiba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, nilipokea simu ikisema: “Sura yangu mnaitakia nini au mmetumwa na waganga wenu muichukue mkaniroge?”
Nikamuuliza aliyenipigia alikuwa nani, akanijibu kuwa: “ Ni mimi mzee wako Ditopile.” Nilicheka.

Nikacheka sana, ila nikamweleza wazi kabisa kwamba sikufurahishwa na vurugu zilizofanywa na ndugu zake, kwani zilikuwa zikizuia waandishi wasifanye kazi yao, pia lionyesha kuwa familia yake ina watu wa namna gani. Akasema tumsamehe, na nilipomhoji ni kwanini anavaa kofia kubwa ‘pama’, alisema anaivaa kwa makusudi ili wapiga picha wasiipate sura yake kwa urahisi.

Akaniambia kuwa: “Wewe ni mwandishi gani umeingia gerezani kuniona ukashindwa kupiga picha mazingira ya Gereza la Keko?”

Nikamjibu kuwa nisingeruhusiwa. Akaniambia pamoja na sheria kukataza yeye alitumia mbinu zake za kijeshi na alifanikiwa kupiga picha mazingira ya gereza hilo na jinsi mahabusu wanavyolala na wala hajawahi kukamatwa na askari magereza na picha hizo amezihifadhi nyumbani kwake.

Kwa wale wanaomfahamu marehemu, lazima watakubaliana nami kwamba Ditopile alikuwa ni mtoto wa mjini, mwenye kupenda masihara na mzaa, muwazi na mwongeaji kupita kiasi, na mara nyingi nilipokuwa nikionana naye au kuzungumza naye alikuwa akiniasa nipende kusali, kuishi vizuri na watu na alinisisitiza nijiendeleze kielimu, kwani elimu ndiyo mkombozi katika ulimwengu wa sasa.

Pia aliniasa kufanya kazi kwa bidii na kwamba ujumbe huo niusambaze hata kwa vijana wenzagu.Aliniambia kuwa wakati akisoma Chuo Kikuu wakati wa likizo alikuwa na ubao wa kuuza mboga na matunda katika Soko la Ilala, hivyo alikuwa akifanya biashara hiyo.

Pia aliwahi kuuza magazeti ya Daily News katika mitaa ya Masaki na Oysterbay. Na alisema kazi hizo zilikuwa zinamsaidia kuongeza kipato. Baada ya kuniambia kwamba aliwai kufanya kazi hizo, nilimwangalia usoni nikajikuta naangua kicheo kwa sauti ndani ya ofisi yake ya mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Akauliza: “Unacheka hizo kazi?” Akaniambia mwanangu hadi leo hii mnatuaona tunateuliwa kushika nyadhifa mbalimbali, mkae mkijua tumetoka mbali.”

Hatukuishia hapo, tuliendelea kuwasiliana kwa simu na hata Januari 6 mwaka huu, baada ya yeye kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba waandishi wa habari, Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage, wamemwagiwa tindikali, alinipigia simu akasema yupo mkoani Lindi, akasema amesikitishwa na tukio hilo na kwakuwa haishi utani aliniambia wakati umefika sasa mapaparazzi tuanze kuvaa ‘pama’ kama yeye ili watakapotumwagia tindikali isituingie machoni.

“Mapaparazzi anzeni kuvaa pama kama mimi ili mkimwagiwa tindikali isiwaingie machoni au wasilianeni na mimi niwaonyeshe duka niliponunua pama langu,” alisema.
Niliishia kucheka.

Ndugu msomaji mapema mwaka huu, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kwamba Ditopile alikuwa akiuza asali, na kweli hadi anafariki dunia alikuwa akifanya biashara hiyo, ambayo aliwahi kunieleza kwamba inamuingizia kipato kizuri.


Baada ya taarifa hizo kutangazwa, alinipigia simu akiniambia kwamba: “Waandishi hamna dogo, mimi kuuza asali imekuwa nongwa?” Akaniambia mbona Mwenyekiti wenu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Reginald Mengi, anauza soda za Coca Cola amuandiki? Mbona bosi wako Freeman Mbowe anauza pombe kwenye ukumbi wake wa Billicanas auandiki? Nilishindwa kumjibu kwani nilicheka sana, akaniambia usicheke.

Katika viongozi wa CCM hakika naweza kusema kiongozi ambaye nilikuwa naye karibu kikazi na aliyekuwa akinipa ushauri mbalimbali alikuwa ni Ditopile, alinichukulia kama mwanawe, hakika Ditopile nakulilia.

Hakuwa na majivuno kama walivyo viongozi wengine, hata wakati alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani nilipokuwa nikipata nafasi, nilikuwa nikipita kumsalimia ofisini kwake.

Ni Ditopile huyu huyu, siku moja kabla ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika utawala wa Awamu ya Tatu, Jakaya Kikwete, kwenda kujitangaza rasmi kugombea urais katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Pwani, Kibaha, alinipigia simu saa tatu usiku akiniambia: “Wewe si unataka ‘scoop’” (habari moto), akaniambia kesho saa mbili asubuhi panda gari kisha shuka stendi ya mabasi Kibaha.

Nilipomuuliza kuna habari gani mbona hataki kuniambia, akaniambia Nimwamini yeye na kwamba kesho yake nifike bila kukosa.

Kwakuwa nilikuwa nikimuamini na kumheshimu, kesho yake ambayo ilikuwa ni siku ya Jumapili, nilifanya hivyo nikapanda gari la kwenda Kibaha pale Ubungo, na kabla ya gari kuondoka Ubungo, alinipigia simu akiniuliza nilikuwa nimefika wapi, nikamweleza ndiyo tunaondoka Ubungo, akasema sawa.

Lile gari lilipofika stendi ya Kibaha, ghafla nilipokea simu nyingine kutoka kwake akiniuliza nilikuwa nimefika wapi, nikamwambia nimefika stendi ya Kibaha, ilikuwa saa 3 asubuhi.

Akaniambia nikodishe teksi nimwambie dereva anipeleke CCM Mkoa wa Pwani, nilifanya hivyo. Nilipoanza kuingia ile njia ya vumbi kuelekea kwenye ofisi hizo, nikaona kumepambwa bendera za CCM. Nikamuuliza yule dereva kulikoni? Akaniambia kuwa hata yeye alikuwa anashangaa.

Nilipofika kwenye ofisi hizo za CCM saa nne asubuhi nikakuta wafuasi na viongozi wa CCM wametanda huku viti vikiwa vimepangwa na nikabahatika kumkuta mpiga picha wa TvT, sasa TBC, Chris, nikamuuliza kulikoni? Akaniambia Kikwete siku hiyo anakuja kujitangaza rasmi kwamba atagombea urais.

Aidha, baada ya dakika chache, Ditopile akaniambia: “Umekwishafika?” Nikamjibu, ndiyo.
Akasema: “Eh umekuta nini au umesikia nini?” nikamwambia nimeambiwa kwamba muda mfupi ujao Kikwete atatangaza rasmi azima yake ya kugombea urais, akasema ni kweli na akaniambia hiyo ndiyo ‘surprise’ yake kwangu na kamwe sitakuja kumsahau kwani tukio lile lilikuwa ni la kihistoria. Ni kweli sitamsahau.

Wana CCM walitutangazia kwamba Kikwete angefika pale saa tano kujitangaza lakini alifika saa saba na nusu mchana. Na ilipofika saa sita Ditopile na alinitafuta na kunitambulisha kwa mkewe aitwaye Tabia, kasha tulisalimiana.

Nakumbuka enzi za uwahi wake aliwahi kuniambia kwamba alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari akawa anasema anafuata masharti yote ya daktari. Na alikuwa aishi utani, nakumbuka kuna siku nikiwa ofisini kwake Pwani nilimkuta anakunywa chai na mkate wa kumimina nikamuuliza kulikoni na mikate ya kumimina asubuhi, akasema ni miongoni mwa kitafunio anachokipenda.

Nasema tukio hili sitalisahau kwakuwa lilihudhuriwa na wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam na walianza kufika eneo hilo saa tano hadi saa saba.

Baadhi ya wahariri walionikuta hapo walishikwa butwaa na kuniambia wewe umepataje taarifa hizo, nikawaambia kwa njia zangu hasa ukizingatia kipindi hicho nilikuwa bado mwandishi mchanga sana na hata nilivyoandika habari ya tukio lile nakumbuka habari ile nilinyimwa ‘by line’ na mhariri wangu bila sababu za msingi.

Nakulilia Ditopile ambaye haupo tena nasi duniani, ila mazuri uliyoachia tutayafuata na kuyatekeleza kwa vitendo.Hata hivyo Ditopile kama walivyo binadamu wengine alikuwa na upungufu na udhaifu na mabaya yake, hatutayafuata.


Mwanasiasa wa siku nyingi Ditopile amefikwa na mauti Jumapili iliyopita. Alifikwa na mauti katika Hoteli ya Hilux ya mjini Morogoro.

Nimemfahamu Ditopile kwa miaka sita sasa na hadi sasa kuna baadhi ya watu ukiwaeleza kwamba Ditopile ana elimu ya chuo kikuu wanakukatalia kutokana mzaha wake.

Ditolipe ndiye mwasisi wa msemo wa ‘halo halo’. Ambaye amekuwa akisema yeye si mtu wa kuja, bali yeye ni mzaliwa wa jiji hili na amezaliwa wodi ya ‘Makuti’ enzi hizo ilikuwa ndani ya Hospitali ya sasa Taifa ya Muhimbili.


Ditopile aliitimu shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1973, aliajiriwa na Chama cha TANU kama Katibu Msaidizi, Makao Makuu. Na kutokana na utendaji wake mwaka 1980 alikwishafikia cheo cha Katibu Msaidizi Mkuu Daraja la Kwanza.

Machi 1983, aliteuliwa kuwa Katibu wa Wilaya wa CCM katika wilaya za Serengerema na Tabora mjini. Nyota yake ilianza kung’ara, na mwaka 1982 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM .Mwaka 1996 hadi 1997, aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara.

Ditopile alikuwa ni miongoni mwa vijana sita waliokuwa wameamua kujiunga na utumishi wa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) mara baada ya kuhitimu masomo ya chuo kikuu mwaka 1973.

Baada ya kujiunga na utumishi wa TANU , Ditopile alijiunga na Chuo cha Itikadi na Propaganda Kivukoni, wakati ule kikiitwa Chuo cha Chama. Baada ya kumaliza mafunzo ya Itikadi na Propaganda, alirudi makao makuu ya chama, na hapo alipewa jukumu la kuanzisha maktaba ya CCM ambayo hadi leo ni ya chama tawala.


Pia alikuwa ni mtumishi mwaminifu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Wakati wa utumishi wake alikwenda katika Chuo cha Maofisa Monduli, alikochukua mafunzo ya uafisa wa jeshi.

Pamoja na nyadhifa hizo , Ditopile aliwai kuwa mbunge wa Jimbo la Ilala katika miaka ya 1980. Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Naibu Waziri wa Mawasiliano.

Pia alipata kuwa mkuu wa Mkoa wa Pwani, Kigoma, Lindi, Dar es Salaam na Tabora.
Ditopile alizaliwa Machi 7, mwaka 1948 katika Wilaya ya Ilala, mkoani Dar es Salaam. Alisoma Shule ya Msingi Mchikichini, Dar es Salaam kati ya mwaka 1956 na 1959.


Mwaka 1960 hadi 1963, alisoma Shule ya Kati Magomeni, Dar es Salaam.
Kati ya mwaka 1964 hadi 1967, alisoma Shule ya Sekondari ya Aga Khan, ambayo kwa sasa inajulikana kama Tambaza.

Mwaka 1968 hadi 1969, alihitimu Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Tanga. Julai 1970, alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1973. Lakini makala hii haita kamilika kama sitaandika kwamba marehemu Ditopile alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia ya Rais Kikwete.

Na hakuna ubishi kwamba katika uhai wake marehemu alikuwa ni miongoni mwa watu waliopigana kufa na kupona ili Kikwete ateuliwe na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Na kweli hilo walifanikiwa.

Lakini naweza kusema bahati haikuwa upande wake, kwani ndani ya miaka miwili na miezi minne, tangu kijana wake Kikwete ashike kiti cha urais, Ditopile alikumbwa na kesi ya kuua bila kukusudia, na kusababisha kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wa mkuu wa moka.

Pia katika kipindi hicho kifupi cha utawala wa kijana wake, Ditopile amekumbwa na mauti. Hivyo hakuweza kufaidi matunda ya utawala wa kijana wake.

Ditopile anatarajiwa kuzikwa leo katika shamba lake lilipo Kinyerezi, Dar es Salaam.

Ditopile sisi tulikupenda, lakini Mungu  amekupenda zaidi.

Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi. Amina.

Namlilia Ditopile

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne.April 22,2008

Blog:www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494


MAHABUSU CHE MUNDUGWAO AFARIKI DUNIA








*TUJIKUMBUSHE KESI YAKE ILIVYOANZA

Na Happiness Katabazi

KWA wapenzi wa muziki wa asili  na watayarishaji wa vipindi va Redio Leo tume pokea kwa masikitiko taarifa za mwanamuziki  wa muziki wa asili nchini, Chingwale Che Mundugwao  (48) ambaye alikuwa akiishi gerezani kwasababu alikuwa akikabiliwa na Kesi ya wizi wa Passpot mali ya serikali tangu Aliposhitakiwa rasmi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,Juni 2 Mwaka 2013 na wenzake.

Makosa waliyokuwa wakishitakiwa nayo yaliyokuwa na dhamana kwa mujibu wa Sheria licha Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwendendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 , kinampa mamlaka kumfungia dhamana mshitakiwa yoyote anayekabiliwa na kesi ambayo Mashitaka yanayomkabili yanadhamana pindi atakupoona kunasa babu zenye maslahi ya taifa.

Kwahiyo tangu Juni 2Mwaka 2013, Che Mundugwao alikuwa Ni mahabusu na alikuwa  akiishi Katika Gereza la Keko . 

Na wakati akiishi gerezani Che Mundugwao alifiwa  na Mtoto wake lakini hakuweza kushiriki msiba wa mwanae Huyo kwasababu alikuwa gerezani chini ya Ulinzi , hivyo Che Mundugwao ,Leo amemfuata mwanae mavumbini.Huzuni.

Binafsi Che Mundugwao nilianza kumfahamu tangu Kipindi kile akiwa mwanamuziki wa muziki wa asili na Aliwahi kupiga Wimbo wake mmoja uliompatia  Umaarufu unaitwa 'TUMETOKA KWETU MAHENGE....TUMEKUJA  DAR ES SALAM KUJA KUCHEZA SINDIMBA '. Mwaka 2000.

Wimbo huu ulitamba Katika Miaka ya katikati ya miaka 1990 na Katika Wimbo huu miongoni mwa wanamuziki waliocheza Katika Wimbo huo ni Luiza Mbutu ambaye ni kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta hivi sasa na dansi machachari wa Enzi hizo za Mwakambaye ambaye ni Mkazi wa Ubungo NHC, Lucas Mapunda 'Kimavi' ambaye alisoma shule ya Msingi Ubungo NHC , Dar es Salaam, na wakati huo Mimi nikisoma shule ya Msingi Mugabe na Tution nilikuwa nikisoma shule ya Msingi Ubungo NHC, hivyo tulikuwa tukikutana Mara kwa Mara Che Mundugwao Na Lucas Mapunda

Kwa mtakaoenda kutaza video ya Wimbo hiyo mtakubaliana na Mimi Kuwa  Luiza Mbutu ametoka mbali katika fani ya muziki na amebadilika sana.

Aidha Che Mundugwao aliendesha Kipindi cha Muziki wa Asili  Katika Redio Tumaini na hatimaye mwisho wa siku Juni 3 Mwaka 2013, Mimi nilipokuwa Mwandishi wa Habari  za Mahakamani wa Gazeti la Tanzania Daima, nilishuhudia Che Mundugwao aniletwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu siku hiyo kwa Mara ya kwanza mchana, akiwa chini ya Ulinzi wa Askari kanzu na kupandishwa kizimbani na kushitakiwa kwa Kesi iliyokuwa ikimkabili.

Nilisikitika sana  kuona Che Mundugwao kuwa mikononi mwa dola ila nilikuwa sina jinsi ya kumsaidia kwasababu licha alikuwa ni rafiki yangu, lakini Sheria ni Msumeno inakata kote kote na Mimi Kama Mwandishi wa Habari za mahakamani na waandishi wenzangu licha tulikuwa tukimfahamu Che Mundugwao ,bila woga tulikuwa tukitimiza jukumu letu la ku hatarisha umma ikiwa ni pamoja kwa kuripoti Kesi mbalimbali ikiwemo Kesi ya Che Mundugwao.
Mungu aiweke roho ya marehemu mahali panapostahili.Amina.


NOVEMBA 14 MWAKA 2013

UPELELEZI  KESI YA CHE MUNGUGWAO WAKAMILIKA

Na Happiness Katabazi

NOVEMBA  14 Mwaka 2013 upande wa jamhuri Katika Kesi hii ulieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ,Dar es Salaam, Kuwa upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika.


JULAI  18 MWAKA 2013

KESI YA CHE MUNDUGWAO YAZIDI KUSOMBA WATU

Na Happiness Katabazi

WAKAZI wawili wa Dar es Salaam,jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kwaajili  ya hapo baadae kuja kuunganishwa katika kesi ya wizi wa Paspoti 26 inayomkabili Msainii wa Muziki wa asili, Chingwele Che Mundugwao na wenzake wanne.

Wakili wa serikali  Aidah Kisumo mbele Hakimu Mkazi Sundi Fimbo aliwataja washitakiwa hao walifikishwa jana kwa mara ya kwanza mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa yanayofanana ambayo yanamkabili Chemundugwao na wenzake ni  Rajab Momba na Haji Mshamu.

JULAI 24 mwaka 2013 

WANNE WAONGEZWA KESI YA CHE MUNDUGWAO

Na Happiness Katabazi
 WAHUDUMU  wa wawili wa Idara ya Uhamiaji jana walifikishwa kalifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, nakuunganishwa katika kesi ya wizi wa Paspoti 26 inayomkabili Mwanamuziki wa muziki wa Asili nchini, Chingwele Che Mundugwao na wenzake  ambapo hadi kufikia jana kesi hiyo imefanya kuwa na jumla ya washitakiwa tisa akiwemo raia mmoja wa Uingereza.

Wakili wa Serikali Lasdsalaus Komanya mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo 
alidai kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kujatwa lakini,pia upande wa jamhuri imekusudia kufanya mabadiliko ya hati ya mashitaka ambapo jana imeweza kuwaunganisha washitakiwa wawili wapya ambao ni wahudumu wa Idara ya uhamiaji Adam Athuman na Abdallah Salehe  na washitakiwa wengine wawili ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Julai 18 mwaka huu ambao ni  Rajab Momba na Haji Mshamu katika kesi hiyo ya Che Mundugwao ambao inawashitakiwa watano na hivyo kufanya sasa kuwa na jumla ya washitakiwa tisa.

Washitakiwa wengine ni Che Mundugwao, Raia wa Uingereza Ahsan Iqbal au Ali Patel, Ofisa  Ugavi wa  Idara ya Uhamiaji Shemweta Kiluwasha, Injinia Keneth Pius wa Kikosi  cha Zimamoto na Uokoaji na mfanyabiashara Ally Jabir.

Hata hivyo washitakiwa hao walikanusha mashitaka hayo na kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika na hivyo hakimu Fimbo aliarisha kesi hiyo hadi Agosti 5 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa na akaamuru washitakiwa hao warejeshwe rumande kwasababu bado Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi hajaondoa hati yake ya kuwafungia dhamana mahakamani.


Akiwasomea mashitaka wakili Komanya alidai kuwa tarehe isiyofahamika washitakiwa walikula njama ya kutenda kosa. Aidha tarehe tofauti Dar es Salaam, Momba aliiba hati ya kusafiria yenye namba AB 651926 mali ya serikali.

Alidai washitakiwa hao wa nne na wanadaiwa tarehe isiyofahamika Dar es Salaam, walighushi hati ya kusafiria yenye namba hiyo, kuonesha ni halali na imetolewa na Idara ya Uhamiaji ya Tanzania jambo ambalo si kweli.


JUNI 2 Mwaka 2013 

CHE MUNDUGWAO KORTINI KWA WIZI WA PASPOTI 26

*DPP AWAFUNGIA DHAMANA

Na Happiness Katabazi

MSANII wa muziki nchini, Chigwele Che Mundugwao 46, ofisa Manunuzi  wa Idara ya Uhamiaji, Shemweta Kilwasha (31), Mhandisi wa Idara ya Zimamoto na Ukoaji, Keneth Pius 37 na mfanyabiashara, Ally  Jabir ( 34) jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na jumla ya mashitaka manne likiwemo kosa la wizi wa jumla ya Pasipoti 26.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Ladslaus Komanya  mbele ya Hakimu Mkazi  Aloyce Katemana wanakabiliwa na kosa la kula njama kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha  384 cha Sheria ya Kanuni ya adhabu ya mwaka 2002.
Wakili Komanya alieleza kuwa kati ya Aprili 16 na Mei 10, mwaka huu , Shimweta akiwa ni mtumishi wa umma,  katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji aliiba paspoti 26, mali ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Komanya alidai kuwa washitakiwa  Chigwele, Keneth na Ally, Mei 30, mwaka huu, huko Yombo Makangarawe jijini Dar es Salaam ,walikamatwa wakiwa na pasipoti hizo 26 za wizi.

Kuhusu  Che Mundugwao,wakili Komanya alidai kuwa mshitakiwa huyo kuwa Aprili 22, mwaka huu alikamatwa akimiliki  paspoti 12  za watu wengine bila ya kuwa na sababu yoyote ya msingi .

Wakili huyo wa Serikali, aliendelea kudai kuwa Mei , mwaka huu  Che Mundugwao pia alikamatwa na maofisa wanausalama akimiliki pasipoti nyingine mbili  zenye majina ya watu wengine sababu yoyote ya msingi. 
Komanya aliendelea kuwa Aprili 24 mwaka huu, mshitakiwa Ally , alighushi paspoti yenye namba AB 65196 akionyesha kuwa ilikuwa ni halali na kwamba ilitolewa na Idara ya Uhamiaji wakati akijua kuwa si kweli.

Wakili Komanya alidai kuwa kati ya mwaka 2007 na 2011 Dar es Salaam,   Shemweta alighushi nyaraka ya serikali ambayo ni muhuri akijaribu kuonyesha kuwa nyaraka hizo zilikuwa ni halali na kwamba zimetolewa na Idara ya Uhamiaji wakati si kweli.

Baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka hayo, walikana na upande wa jamhuri ukadai  kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Wakili Komanya alidai kuwa kutokana na asili ya makosa hayo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP),Dk.Eliezer Feleshi aliwasilisha hati ya kuzuia dhamana chini ya kifungu cha 148 (4) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 na ataiondoa hati hiyo pale atakapoona hipo sababu ya kufanya hivyo ila kwasasa amefunga dhamana ya washitakiwa hao. 

Kiongozi wa jopo  la mawakili wanaowatetea washtakiwa hao, Peter Kibatala aliiomba mahakama kuwapa dhamana washtakiwa hao kwa sababu mashtaka yao yanadhaminika na kwamba hayapo katika vifungu ambayo vinazuia dhamana.

Hata hivyo Hakimu Katemana  aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 5, mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi juu ya hoja hizo zilizowasilishwa mahakamani hapo na akaamuru washitakiwa wote wapelekwe gerezani na kwamba Mahakama yake haina mamlaka ya kutoa dhamana kwasababu Kifungu hicho kilichotumiwa na DPP kimeifunga mkono mahakama kutoa dhamana kwa washitakiwa.

 Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Aprili 16 Mwaka 2015.


WAFANYABIASHARA ACHENI KUTUMIWA NA WANASIASA KUENDESHA MIGOMO YA KUFUNGA MADUKA




Na Happiness Katabazi
KWA zaidi ya miezi nane sasa baadhi ya wafanyabiashara wenye   maduka katika mikoa mbalimbali wamekuwa wakigoma kufungua maduka yao kwa madai mapya kila awamu wanayogoma.

Mgomo wa kwanza walivyogoma walidai kuwa mashine za EFDS wanauziwa kwa gharama kubwa na kwamba hawawezi kuzinunua,kodi ni kubwa.

Mara wafanyabiashara wakazusha mgomo mwingine ambao wakaja na madai mapya kuwa hawana elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya mashine ua EFDS hivyo wanaitaji elimu.

Hivi sasa wameibuka tena kivingine katika mikoa tofauti eti wakitaka  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja  ambaye Machi 25 mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kwasababu alikiuka masharti ya dhamana aliyopewa ikiwemo ya kutowazuia wafanyabiashara kufunga maduka yao wakati kesi yake ikiendelea aachiliwe huru ndipo watafungua maduka yao.

Akitoa taarifa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Dodoma, Rebecca Mbilu, Mwendesha mashtaka wa serikali Rose Shio amesema kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo umeshakamilika na kuiomba mahakama kutengua dhamana ya mshtakiwa kutokana na kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa.
Amesema kuwa pamoja na hilo Mwenyekiti huyo amekuwa akiendelea kufanya mikutano na wafanyabiashara kwa ajili ya kuwahamasisha wasiendelee kulipa kodi kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFDS kitendo alichosema kuwa ni kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa.

Hata hivyo wakili wa mshtakiwa, Godfrey Wasonga ameiambia mahakama kuwa tangu mteja wake apewe dhamana hajawahi kuitisha mikutano na wafanyabiashara kwani hata juzi hakuwa na mkutano bali wafanyabiashara waliokuja mjini Dodoma kusikiliza kesi ya mwenyekiti huyo, waliposikia kuwa yupo Dodoma walikwenda kumsalimia baada ya kupata taarifa kuwa yuko katika hoteli ya Image Hill.

Hata hivyo hakimu Mbilu alisema kuwa ameridhika na hoja za upande wa mashtaka na hivyo akatengua dhamana ya Minja na kumtaka kubaki rumande hadi April Mosi mwaka huu ambapo kesi yake itakuja kwaajili ya kutajwa.

Watanzania ikumbukwe kuwa Tanzania ni nchi iliyojiamliwa kuongozwa kwa Katiba na sheria.

Na Ibara ya 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, nanukuu:

" 107A.-(1) Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano
itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya
Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali
wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar
kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.
 (2) Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa
kuzingatia sheria, Mahakama zitafuata kanuni zifuatazo, yaani:
(a) kutenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya mtu kijamii Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaau kiuchumi;
(b) kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi;
(c) kutoa fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika kutokana
na makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheria
mahususi iliyotungwa na Bunge;
(d) kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wahusika na katika migogoro; na
(e) kutenda haki bila kufungwa kupita kiasi na masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha haki kutendeka.

Minja amefunguliwa kesi hiyo ya jinai na kwa makusudi ameamua kukiuka masharti ya dhamana upande wa jamhuri ukawasilisha ombi la kuomba afutiwe dhamana kwababu amekiuka masharti na mahakama ikakubaliana na ombi hilo kwasababu ina mamlaka ya kufanha hivyo.

Sasa haya madai ya kiuwendawazimu yaani yanayotolewa na  baadhi ya wafanyabiashara ambao wamedai wameamua kuanzisha mgomo wa kutofungua maduka eti  kushinikiza Mwenyekiti wao Minja aachiriwe uhuru hayo mamlaka ya kiuwendawazimu lazima watakuwa wameyapata kwa wendawazimu wenzao ambao ni baadhi ya  wanasiasa wanaowatumia wafanyabiashara hao wa maduka kufanya vitendo vya uwendawazimu vya kugoma kufungua maduka yao.

Nimelazimika kuwaita hawa wafanyabiashara wanaogoma wanafanya vitendo vya kiuwendawazimu na kweli kitendo chao hicho cha kugoma kufungua maduka kwasababu wanataka Minja aachiriwe huru ni cha kiuwendawazimu.

Kwababu mtu mwenye akili timamu ,anateheshimu sheria za nchi na anayejitambua,mwenye uchungu na taifa lake na asiyekubali kutumiwa na wanasiasa uchwara kama wanavyotumika hawa wafanyabiashara uchwara wanaogopa kufungua maduka yao kwa kutumia njia za kiuni hawezi kufanya hivyo.

Wasomi wa sheria wanamsemo mmoja usemao ' Haki yako inapoishia ndiyo haki ya mwenzako inapoanzia'.

Yaani kwa  maana ya msemo huo hapo juu kuwa wafanyabiashara wana haki ya kupata maslahi na wananchi wanaotaji kupata huduma kutoka kwa wafanyabiashara matokeo yake hawapati haki hiyo na serikali haipati haki yake ya kupata mapato.

Sasa hawa wafanyabiashara uchwara ambao minawaita wafanyabiashara ucharwa na wanaotumiwa na wanasiasa kwa lengo moja la kuakikikisha serikali inashindwa kupata mapato kwasababu ya mgomo huo na matokeo yake serikali itajikuta inakosa fedha za kuendesha mahospitali,huduma za kijamii muhimu kwasababu itakuwa haina fedha na mwisho wake wananchi kuichukia serikali yao na kuanza kuingia barabarani kufanya vurugu kushinikiza serikali itoke madarakani kwasababu imeshindwa kuwapatia  huduma muhimu.

Na mpango huo ndiyo ulioratibiwa na baadhi ya wanaisasa  hapa nchini kwa siri kwa kuwatumia hao wafanyabiashara uchwara ambao wengi wa wafanyabiashara wanatokea Mkoa mmoja wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kufanya migomo hiyo kwa njia dhalimu.

Hata kama wafanyabiashara hao wana madai ya msingi lakini ni wazi baadhi ya wafanyabiashara hao wanatumia njia ambazo hazikubariki kisheria kudai haki zao.

Haya basi tufanye ni kweli mashine hizo hawawezi kuzinunua kwasababu bei yake ipo juu, wamepandishiwa kiwango kikubwa cha kodi na hawawezi kukimudu.

Nawauliza wafanyabiashara hawa hivi Mahakamani au kwenye Baraza la Rufaa la Kodi hawapajui?

Maana huko ndiko sehemu sahihi kwao kwenda kulalamikia hayo mambo mawili wanayoyapinga matokeo yake hawajaenda kulalamika huko wameishia kulalamika kwenye vyombo vya habari,serikalini na kwa hao mabwana zao wanasiasa wanaowatumia vibaya.

Ibara ya 13(6)(a) ya   Katiba ya nchi ,ninanukuu;

'Wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji
kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo
kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na
haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na
pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya
kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au
chombo hicho kingenecho kinachohusika'.

Kwa lugha nyepesi ibara hiyo nyie wafanyabiashara uchwara ibara hiyo  inatoa haki ya kukata rufaa katika mahakama ya juu kupinga uamuzi uliotolewa na mahakama ya chini kama unaona una sababu na haki (Locus of stand) ya kukata rufaa katika Mahakama ya juu.

Kwahiyo  nyie wafanyabiashara uchwara hamna haki ya kukata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama wa kumfutia dhamana Minja ,mwenye mamlaka hayo ni  Minja mwenyewe na siyo nyie wafanyabiashara wala wanasiasa uchwara waliopayuka ndani ya bunge akiwemo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kutaka Minja apewe dhamana nje ya mahakama na siku zote mahakama inafanyakazi ndano ya mahakama siyo maneno ya kihuni uhuni yanayotolewa na wahuni huni nje ya mahakama kutaka apewe dhamana.

Na mtambue uhuni wenu huo wa shinikizo la kutaka Minja apatiwe dhamana,nyie siyo watu wa kwanza uufanya, aliiufanya Mwenyekiti wa Chama Cha CUF, Professa Ibrahim Lipumba wakati Sheikh Ponda Issa Ponda alipokamatwa Agosti mwaka 2012 na kufunguliwa kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini alimfungia dhamana kwa mujibu wa kifungu cha 148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 na Ponda kweli alikaa gerezani hadi  Mei 8 mwama 2013 alipofungwa kifungo cha mwaka mmoja nje.

Na siyo Lipumba peke yake bali baadhi ya waislamu wenzake nao walikuwa wakikesha misikitini na mahakamani kushinikiza aachiwe lakini wapi.

Sasa Minja ninani hadi na yeye mahakama ipindishe sheria ili impendelee?

Hivi Minja na Ponda nani mwenye nguvu ya watu na mwenye wafuasi wengi na akiamua kufanya jambo lake vyombo vya dola vinakesha macho kumsaka kama siyo Ponda lakini serikali imemdhibiti?

Mbinu yenu hiyo ya kijinga ndiyo itasababaisha Minja aendelee kusota gerezani.

Ndio maana minashawishika kuwafananisha nyie wafanyabiashara mliogoma hivi sasa kwa sababu eti mnataka Minja aachiriwe huru kwa  sawa  na wendawazimu kwababu zifuatazo:

Mosi , hamna haki ya kisheria nyie wafanyabiashara mambumbu wa sheria wa kuilazimisha mahakama ifanye mnavyotaka nyie.

Pili, mnaingilia majukumu ya kimahakama  ya kusikiliza na kutolea maamuzi kesi.

Tatu, nyie wafanyabiashara uchwara mliogoma hamna haki ya kwenda kukata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma wa kumfutia dhamana  Minja kwasababu nyie siyo washitakiwa katika kesi hiyo.

Sasa kihelehele hiki cha kusema Minja kaonewa wakati hata usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo haujafanyika  kinatoka wapi kama siyo ushambenga na ukosefu wa akili na kuipaka matope mhimili wa mahakama na kuleta fujo katika jamii yetu?

Watanzania wangapi wanafutiwa dhamana na  Mahakama mbona hamjawahi kuwa na umoja kiasi hiki na kufunga maduka?

Kwanini Minja tu? Kwa hiyo ikitokea mahakama isitengue amri yake ya kumfutia dhamana hadi mwakani ,nyie wafanyabiashara uchwara mtaendelea hadi mwakani na mgomo wenu  wa kutofungua madukani yenu hadi atakapopatiwa dhamai hapo mwakani?

Hivi zile leseni za biashara mlizopewa na serikali kwaajili ya nyie kuendesha biashara kuna mahali kokote zimeandikwa siku Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara akifutiwa dhamana basi ni ruksa kwa wafanyabiashara kugoma kufungua maduka?

Hivi hizo leseni za biashara zenu kuna sehemu yoyote  inaonyesha wafanyabiashara wataruhusiwa kisheria kugoma kufungua maduka yao kwasababu ya kupinga gharama za manunuzi ya mashine ya EFDS? Jibu ni hakuna.

Nawauliza nyie wafanyabiashara uchwara haya mamlaka  ya nyie baadhi ya wafanyabiashara ya kukaidi kununua mashine hiyo, kushiriki migomo isiyofuata taratibu za kisheria mmeyapata wapi na kwa mujibu wa sheria zipi hali inayosababisha wananchi kukosa huduma na kulipa kodi kwa serikali yao na serikali kushindwa kupata mapato?

Halafu tujiulize ni kwanini wafanyabiashara wenye asili ya Kiarabu na Wahindi hawagomi na wote wapo pale pale Kariakoo kwa hapa jiji la Dar es Salaam?

Na ni kwanini kila kukicha mfano Dar es Salaam, wanagoma wafanyabiashara wenye maduka eneo la Kariakoo tu?

Mbona wafanyabiashara wenye maduka yenye bidhaa zilizokidhi viwango kupita bidhaa zinazoouzwa katika maduka ya wafanyabiashara wagomaji katika maeno ya Posta Mpya, Sinza,Manzese, Mbezi ,Masaki na Kimara mbona hajuwasikia wakigoma na kufunga ofisi zao?

Kila kukicha ni wafanyabiashara wa Kariakoo.Kwanini? Maduka mengi ya Kariakoo inadaiwa yanamilikiwa  na watu wenye asili ya Kabila la Wachaga na Wakinga.

Iweje baadhi ya wafanyabiashara hawa wagomaji wadai hawana feha za kununulia mashine ya EFDS lakini wafanyabiashara hawa hawa wanamitaji inayowapa fursa ya wenda nchini Uturuki, China ,Kenya na Dubai kwenda kuchukua  mzigo  na kuuleta Tanzania na kisha kuuza?

Kwanza badhi ya wafanyabiashara wenye maduka hapo Kariakoo mnatuuzia bidhaa mbazo hazina ubora .

Lakini upole Watanzania ndio unawaa kiburi nyie wafanyabiashara kufanya uhuni we huu lakini mtambue kila jambo lina  mwisho wake.

Na uchunguzi wangu nilioufanya kabla sijaandika makala hii unaonyesha kuna baadhi ya wafanyabiashara wapo tayari kufungua maduka yao ila wanaogopa kushughulikiwa na wafanyabiashara wenzao ambao wanaendesha mgomo huo kwa maelekezo ya baadhi ya wanaisasa toka baadhi ya vyama ya upinzani hapa nchini.

Licha pia kuna baadhi ya wafanyabiashara wengine hapo Kariakoo wamefunga mlango wa mbele wa duka hilo anakaa mbele ya hilo duka na endapo anahisi anayepita mbele yake ni mteja anamuuliza kama anaitaji huduma na mteja yule akikubali, muuzaji wa duka hilo anampitishia mlango wa nyuma mteja yule na kisha anaenda kumpatia huduma bila kumpatia risiti hali inayosababisha serikali kuendelea kukosa mapato kutokana na uhuni huu unaofanywa na wahuni hawa yaani wafanyabiashara.

Ebu tujiulize mfanyabiashara wa ukweli na  mweye akili timamu na tujuavyo sisi wafanyabiashara wengi wanamikopo ya kuendeshea biashara zao na wanadaiwa kodi za pango, anakubalije kugoma kufanyabiashara na asiingize fedha  kwa sababu dhaifu kama hizo?

Nalazimika kuanza kukubaliana na Mwanasayansi ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB) Dk.Elifuraha Mtaro ambaye kila siku anasema mitafaruku inayoendelea kuibuka kila kukicha ni Jiopolitiko Agenda, akiwa anamaanisha mtafuruku inayobuka kila kukicha ni ajenda chafu za baadi ya mataifa ya kigeni yasiyotaikia mema Tanzania, wanataka kuakiikisha siku watanzania tunachinjana  amani yetu inatoweka.

Uenda hawa wanaoendesha mgomo wa kutofungua maduka tayari wameishapatiwa fedha za uhakika na wabaya wa taifa hili ndio maana hata wasipoyafungua maduka yao hawana hasara kwasababu tayari walishapeww fedha za kutosha toka kwa  kwa mabwana zao wanaowatuma waanzishe migomo hiyo kila kukicha.

 Maana aingii akilini mfanyaboashara anayeendesha biashara ya duka lake kwa mkopo ,anatakiwa kila  baada ya muda fulani akarudishe  marejesho, anadaiwa kodi ya pango akubali kushiriki mgomo wa kugoma kufungua duka lake.

Maana Tanzania hivi sasa kila kukicha inaibuka mitafaruku ya kutikisa nchi na kuacha  makovu hali inayosababisha nchi hii hivi sasa ya kuibua na mitafaruku na siyo furaha tena.

Serikali nayo katika mgogoro huu wa wafanyabiashafa ,haiwezi kukwepa lawama hii kwamba imekuwa ikichelewa sana kuchukua maamuzi ya maana ambayo yangesebabisha hawa wafanyabiashara kurudia kugoma goma.

Nimekuwa nikijiuliza maswali bila majibu kwamba ni kwanini serikali inabembelezana sana na wafanyabiashara hawa ambao tangu mwanzo wanavunja sheria za nchi na kusababisha wananchi kukosa huduma na serikali kushindwa kupata mapato?

Je ni kwasababu baadhi ya viongozi wa serikali nao wanamgongano wa kimaslahi yaani wanatajwa wao binafsi ,familia zao kumiliki maduka katika maeneo hayo kama Kariakoo?

Maana aiingii akilini serikali yoyote ambayo kamwe haipotayari kuona inakoseshwa kupata mapato yake na wahuni wachache yaani hawa wafanyabiashara halafu iendelee kuwakumbatia  na kuwa kenulia meno.

Hawa wafanyabiashara wamekuwa na jeuri  kila wanapojisikia wanagoma  kwasababu uenda  wanadhani  serikali hii ni 'mhuni' mwenzao haiwezi kuwafanya chochote na ndio maana hata jana tumeshuudia madereva wa daladala kule  mjini Songea Mkoani Ruvuma nao waligoma utoa huduma kwa madai kuwa wanaunga mkono mgomo wa wafanyabaishara na wanashinikiza Minja aachiliwe huru.

Huu  mi nasema ni wazimu unaofanywa  na hao wenye madaladala na wafanyabiashara kwani kadri siku zinavyozidi kusoga mbele ndiyo mnavyodhiirisha huu siyo mgomo wa wafanyabiashara bali wafanyabiashara hao na madereva hao wa madaladala wanatekeleza kwa vitendo maelekezo ya wanasiasa uchwara ambao mara kwa  mara wamekuwa wakijiapiza nchi haitatawalika na kuiosesha mapato serikali.

Watu wenye akili timamu na wachunguzi wa  mambo tumelibaini hili.

Nawashauri wafanyabiashara mnaogoma  acheni kugoma rudini mfanyekazi na kama kweli mnafiriki mnamadai ya msingi basi fuateni njia utaratibu wa kisheria na kiungwana kudai madai yenu na siyo njia hii ya kihuni na kidhalimu mnayofanya.

Hao wanasiasa  wanaowatumia minawafananishaga na  Maibilisi kwani nyie siyo watu wa kwanza kuwatumiwa kutekeleza ajenda zao chafu  ambazo mwisho siku mtaumia nyie siyo wao.

Kawaulizeni baadhi ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Madaktari,wakazi wa Mtwara kuzuia bomba la gesi lisijengwe, baadhi ya  wahitimu wa JKT .

Wanasiasa hao wenye tabia za kishetani waliyatumia makundi kikamilifu na mwisho wa siku makundi hayo ndiyo yaliyoathirika wale vinara wa JKT wapo gerezani, yule kinara wa mgomo wa madaktari kilichomkuta sote tunakifahamu nakilichowakuta wale baadhi ya wakazi wa Mtwara waliokuwa wakileta vurugu kuhusu bomba la gesi lisijengwe kilichowafika sote tunakifahamu na sio wanaisasa hao.

Bila shaka na nyie wafanyabiashara   mnawashwa mno mnaitaji mmpatiwe dawa ili muache kujikuna huo upelele unaowawasha hadi unasababaisha mnavunja sheria za nchi kwa makusudi na mtapatiwa dawa na wenye uchungu na nchi hii kama msipoacha huo uhuni wenu wa kuikosesha  mapato serikali na kutusabishia wananchi tukose huduma.

Sasa na nyie wafanyabiashara mnachokitafuta mtakipata kwasababu ushahidi uliopo wazi mmevuka mipaka sasa na mna ajenda  chafu nyuma pazi ya mgomo wenu siyo  mashine ya EFDS na huo ndiyo
 ukweli mchungu fungueni maduka mfanyebiashara kama biashara imewawashinda fungeni maduka ingieni kwenye ulingo wa siasa tuwajue kuliko kucheza na uchumi wa taifa letu kwa sababu za kipuuzi tu.

Kama kweli Tanzania ni taifa linalotaka kupiga  hatua za kimaendeleo kweli ,minashauri nyie wanasiasa uchwara wetu acheni tabia zenu chafu za kuingiza siasa zenu chafu katika masuala ya uchumi,mnaangamiza taifa kiuchumi kwa akili zenu mbovu na tamaa zenu za madaraka kwa kuuingiza siasa chafu katika mambo nyeti kama masuala ya uchumi,amani na usalama wa taifa letu.

Na serikali iache tabia ya kulealea ushetani huu kwa kuacha madhara yasambae ndiyo iibuke usingizini ijifanye inaanza kuchukua hatua.Ina kera sana.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Aprili Mosi Mwaka 2015.