LOWASSA UACHE UONGO



Na Happiness Katabazi

NIMEMTAZAMA kupitia Televisheni ya ITV ,Mzee Edward Lowassa na kuisoma neno kwa neno hotuba yake  ya kutangaza nia leo katika Uwanja wa Sheikh Abeid Mkoani Arusha ya kugombea urais wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimebaini uongo wazi katika aya ya kwanza.

Haya hiyo katika hotuba hiyo inasomeka hivi;    HOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA   KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KWA AJILI YA KUTANGAZA NIA YA KUOMBA KUTEULIWA KUWA MGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KWA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA).

Ukisoma kichwa hicho cha habari cha hotuba yake kimesema ( Hotuba ya Mheshimiwa Edward Lowassa  kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari......).

Sehemu ya hiyo aya Lowassa amedanganya  umma kuwa eti leo amezungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza nia.

Ukweli ni kwamba Lowassa leo ametangaza nia mbele ya wafuasi wake katika mkutano wa adhara ambao wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya,wasanii wa Kimasai wakiwa na mishale na silaha za jadi na mwanamuziki wa muziki wa Taarabu Hadija Kopa walitumbuiza.

Binafsi ni mwandishi wa habari kwa zaidi ya miaka 15 sasa,nimeisha shiriki  mikutano mbalimbali ya waandishi wa habari na vyanzo vya habari(source)  yaani (Press Conference).

Kitaaluma mkutano wa waandishi wa habari uhusisha waandishi wa habari na wale wanamsindikiza mtoa habari na mkutano na waandishi wa habari  katika eneo la mkutano.

Mkutano na waandishi wa habari haunaga  mbwembwe ,kualika makundi ya watu mbalimbali, wasanii,vibweka kama tulivyovishuhudia leo katika mkutano huo ,wafuasi wako kupaza sauti kusema Lowassa Rais,wanasiasa kupanda majukwaani   kumnadi mtoa habari(Lowassa), kama ulivyoshuhudia leo katika mkutano ile jinsi Kingunge Ngombale Mwilu, Kangi Lugola, Mtumishi wa Mungu Josephat Gwajima, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha,Onesmo Ole Nangolo walivyokuwa wakimpigia debe Lowassa.

Kimsingi tukubaliane Lowassa kupitia aya hiyo ya hotuba yako ya leo amedanganya umma na amejidanganya yeye mwenyewe na kujionyesha asivyo makini katika baadhi ya mambo.

Hata kama hiyo hotuba uliandaliwa na waandishi wako wa hotuba unaowaamini,kama kweli wewe ni kiongozi makini na unayetaka kuwa rais wa nchi hii kwa kila njia, ulipaswa uisome kwanza hotuba hiyo neno  na  kwa dosari hii imedhirisha na wewe siyo makini.

Hadi ulikubali kuisoma hiyo hotuba mbele ya adhara ina maana ulikubaliana na mambo yote yaliyoandikwa kwenye hiyo hotuba ambapo baada ya wewe kuisoma jukwaani leo sisi wafuatiliaji wa mambo ndani ya muda mchache tumeibaini ina kasoro hiyo ya wazi kabisa tena kwenye kichwa cha habari.

Sasa hao waandishi wa hotuba yako utawachukulia maamuzi magumu? Maana umekuwa ukijinasibu wewe ni kiongozi unayeweza kuchukua maamuzi magumu kwa haraka.

Nakushauri anza kutoa maamuzi  magumu kwa hao waandishi wa hotuba yako hii ambayo ni hotuba ya kihistoria kwani hotuba hii ni ishara ya wewe kuanza safari ya matumaini kwenda Ikulu lakini tayari nimeibaini ina dosari hiyo.

Nyie waandishi wa hotuba ya Mzee Lowassa kuweni makini na kazi yenu, au kama mmetumwa kumuandikia ujinga huo mzee Lowassa katika hotuba zake ili atolewe kasoro kuwa sio makini,mseme maana waandishi wengi hivi sasa hamuaminiki mmekuwa kama wanawake Malaya wanaouza mihili yao  ambao wana mabwana wengi ili mradi wapate fedha upitia mihili yao.

Na hili linawezekana maana aingii akili mwandishi wa habari amuandalie hotuba mtu anayemuunga mkono afanye kosa la kiufundi kama hili tena katika kichwa cha habari.

Niitimishe kwa kumtaka Lowassa aache uongo.Ule ni mkutano wa adhara aliohutubia leo wakati akitangaza nia  na siyo mkutano wake na waandishi wa habari kama alivyodai katika hotuba yake. Hongera sana Mzee Lowassa kwa mkutano wako huo uliofurika watu wengi.Ila ukumbuke  msemo usemao ' Kuzikwa  na watu wengi sio kwenda Mbinguni.

Kila la kheri katika hiyo safari yako
Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Mei 30 mwaka 2015..

HOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA YA KUTANGAZA NIA



HOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KWA AJILI YA KUTANGAZA NIA YA KUOMBA KUTEULIWA KUWA MGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KWA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


UTANGULIZI:

Ndugu zangu wana-CCM na Watanzania wenzangu,

Hii ni siku muhimu kwangu na kwa nchi yetu. Leo nimeamua kuwaita ili kuwatangazia rasmi Watanzania wenzangu azma yangu ya kutaka kuomba ridhaa ya chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), niweze kuteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nasema hii ni siku muhimu kwangu kwa sababu naamini historia yangu itainakili kama ni siku ambayo kwa mara ya pili katika maisha yangu nimejitokeza kuwania kuiongoza nchi yetu kupitia chama chetu. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini nilipojitokeza nikiwa pamoja na Rais Jakaya Kikwete; wakati ule sote tulikuwa wanasiasa vijana. Tulikwenda pamoja kuchukua fomu ndani ya Chama na baadaye tukafanya mazungumzo ya pamoja na waandishi wa habari. Tulileta hamasa kubwa pale tulipofanya jambo ambalo halikuzoeleka kwa Watanzania kwa kutangaza kwamba yeyote atakayepita kati ya wawili sisi basi mwenzake ambaye hatafanikiwa angemuunga mkono.

Ningeweza kujitokeza tena mwaka 2005 lakini nikaamua kwa dhati kabisa kumuunga mkono moja kwa moja Rais Jakaya Kikwete. Nikiwa Mwenyekiti wa Kampeni niliwaongoza wenzangu kufanikisha ushindi mkubwa wa mgombea tuliyemuunga mkono na baadaye ushindi mkubwa wa asilimia 80 wa Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa 2005.

Nitaeleza kwa nini nimeamua kujitokeza tena mwaka huu na kwa nini naamini mimi ndiye mtu sahihi wa kuiongoza nchi yetu wakati huu. Mpaka hapa itoshe tu kuwaeleza ni kwa kwa nini naamini leo ni siku muhimu kwangu.

Lakini nasema ni siku muhimu kwa nchi yetu pia. Nasema hivyokwa sababu naamini inajibu wito wa mahitaji ya sasa ya uongozi wa Taifa letu wa kumpata kiongozi imara atakayewaongoza Watanzania kujenga taifa imara. Na hili pia nitalieleza kwa kina.


HALI YA NCHI NA MATARAJIO YA WATU:

Miaka 48 iliyopita katika jiji hili la Arusha, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage alianzisha mchakato wa kujenga taifa huru kiuchumi na kupiga vita maadui umaskini, ujinga na maradhi kwakutumia silaha ya kujitegemea. Leo hii, wakati taifa likijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu ujao, hatuna budi kutafakari tulikotoka, tulipo na tunapotaka kwenda ili tuweze kubuni upya mikakati ya kuhitimisha azma aliyo kuwa nayo Mwalimu, ili tujenge taifa huru, lenye utulivu, mshikamano, amani na maendeleo.


Nchi yetu hivi sasa inapita katika kipindi kigumu cha mpito katika maeneo yote makuu ya maisha yetu – katika siasa, katika uchumi na katika maisha ya kijamii.

Kisiasa, tumeshuhudia kuongezeka kwa vuguvugu la mfumo wa vyama vingi ambapo ushindani kati ya vyama vya siasa unazidi kuwa mkali na kwa bahati mbaya kufikia sura ya kuonekana kama vile ni mapambano ya watu binafsi badala ya mapambano ya sera na dira ya kuongoza nchi. Tunashuhudia kuongezeka uhasama binafsi kati ya wanasiasa ndani ya chama kimoja kimoja na pia kati ya wanasiasa wa chama kimoja dhidi ya kingine. Kadiri siku zinavyokwenda, hali inazidi kuzorota na ikiachiwa kuendelea nchi yetu inaweza kujikuta mahali pabaya. Kukua kwa ushindani ni jambo jema linalokomaza na kurutubisha demokrasia yetu na tukiwa na ushindani wenye afya unaweza kuwa chachu ya kuleta mabadiliko mema kwa wananchi na kupelekea kuongezeka kwa kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi yetu. Kinyume chake ushindani unaochukua sura ya chuki binafsi au kukomoana na hata kulipizana visasi si ushindani wenye tija na tunapaswa kuutafutia tiba. Tunahitaji uongozi imara kusimamia kipindi cha mpito kutoka siasa muflisi za aina hii na kuelekea kwenye siasa mpya zinazoimarisha ushindani wenye tija unaojikita katika kushindana katika kuwapatia huduma bora Watanzania.

Kiuchumi, tumeshuhudia ukuaji mzuri na kuongezeka kwa mapato ya ndani ya Serikali na uimarishaji wa mfumo wa uwajibikaji na ulipaji kodi. Kwa upande mwengine, Serikali ya Rais BenjaminiMkapa na Rais Jakaya Kikwete imefanya kazi kubwa katika uendelezaji wa sekta ya mafuta na gesi asilia ambapo kiwango kikubwa cha gesi asilia kimegunduliwa. Tanzania sasa imekuwa ni miongoni mwa nchi zinazovutia uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo ambayo inatajwa kwamba inaweza kuja kubadilisha kabisa maisha ya Watanzania. Hata hivyo, kipindi hiki cha mpito kuelekea ujenzi wa uchumi wa kisasa kimeshuhudia kuongezeka kwa hofu na wasiwasi miongoni mwa wananchi kwamba hawatonufaika naukuaji huu wa uchumi na ugunduzi wa utajiri mkubwa wa gesi asilia. Kwa upande mwingine, vijana wanataka kuona ukuaji wa uchumi na ugunduzi wa utajiri huo unakwenda sambamba na uzalishaji wa ajira zenye maana ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha yao. Niliwahi kusema kwamba tatizo la ukosefu wa ajira likiachiwa bila ya kutafutiwa ufumbuzi imara ni bomu linalosubiri kulipuka. Vijana wasio na ajira hupoteza matumaini na ni rahisi kughilibiwa kuingiza nchi katika machafuko.Tunahitaji uongozi imara kuweza kuikabili hali hiyo na kuitafutia suluhisho maridhawa.

Kijamii, kipindi cha karibuni tumeshuhudia mabadiliko makubwa ya tabia miongoni mwa raia katika hali ambayo haijawahi kuwa sehemu ya utamaduni wa Watanzania. Kumekuwa na ongezeko la kutisha la matukio ya uhalifu linalokwenda sambamba na wananchi kuonyesha wanapoteza imani na taasisi zinazosimamia sheria na usalama na kuamua kujichukulia sheria mikononi mwao. Kumeripotiwa matukio mengi yakiwemo ya kuvamiwa vituo vya polisi, askari kupigwa na kuporwa silaha, matumizi makubwa ya nguvu katika utatuzi wa migogoro mbalimbali hasa ile ya kijamii, mathalani migogoro ya wakulima na wafugaji, mivutano ya kidini na pia mivutano baina ya viongozi wa dini wenyewe kwa wenyewe na baina ya viongozi wa dini na wale wa Serikali. Matokeo yakemshikamano wa taifa nao unaingia majaribuni. Mara nyingine wananchi wanatuuliza viongozi iwapo hii ndiyo nchi tuliyoachiwa na waasisi wetu. Tunahitaji uongozi imara wa kukabiliana na changamoto hizi na kurudisha mshikamano wa taifa letu na watu wake.


WATANZANIA WANATAKA MABADILIKO:

Ndugu zangu, mnaweza kujiuliza kwa nini nimeyaeleza yote hayo na yana mahusiano gani na dhamira yangu ya kutangaza nia ya kutaka kuiongoza nchi yetu kupitia CCM?

Nimeyaeleza haya kwa sababu haya na matukio mengine yanayoendelea nchini yamepelekea Watanzania kutaka mabadiliko. Watanzania wanataka mabadiliko yatakayowawezesha kuzishinda changamoto hizi na kuwaongoza kujenga Taifa imara ambalo kila mwananchi wake anaishi akiwa na uhakika wa mahitaji yake muhimu na papo hapo akijiridhisha kwamba leo yake ni bora kuliko jana yake, na kesho yake itakuwa bora zaidi kuliko leo yake. Kwa maneno mengine, Watanzania wanahitaji mabadiliko yatakayowapa uongozi imara unaoweza kuwaongoza kujenga taifaimara. Hii ndio Safari ya Matumaini.

Chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), na watangulizi wake, TANU na ASP, kimepata bahati ya kuungwa mkono na Watanzania tokea enzi za kupigania uhuru, wakati wa Uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar, na pia miaka yote tokea Uhuru, Mapinduzi na hatimaye Muungano wetu. Watanzania hawajawahi kushuhudia chama kingine kikiongoza Serikali zetu zaidi ya CCM. Wamekiamini na wanaendelea kukiamini. Hata katika yale majimbo machache ya nchi yetu ambayo hatukufanya vizuri katika uchaguzi, ukiangalia kwa undani utaona si kwamba watu wa maeneo hayo wana matatizo na CCM kama Chama bali wana matatizo na baadhi ya viongozi ambao walishindwa kukiwakilisha vyema Chama na kutambua matakwa ya wananchi hao.

Mimi naamini kwamba hata katika kipindi hiki ambapo Watanzania wanaonekana kutaka mabadiliko bado wanaendelea kuamini kwamba watayapata mabadiliko hayo ndani ya CCM. Lakini kama alivyotupa wasia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi hapa nchini, Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Mimi naamini kwamba CCM tunao uwezo wa kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka. Tuwape imani na imani hiyo iwe ni ya dhati na ya ukweli kwamba CCM inao uwezo wa kuwapa uongozi imara wanaouhitaji kwa ajili ya kujenga taifa imara.

Vyama vya siasa vinajumuisha watu na vinaongozwa na watu. Moja ya hulka ya binadamu ni kubadilika kulingana na mahitaji ya mazingira anayoishi. Kwa maneno mengine, binadamu ni ‘dynamic’. Kwa sababu hiyo basi, hata vyama vya siasa vinapaswa kuwa ‘dynamic’. CCM haijapata kuwa na upungufu wa sifa ya ‘dynamism’. Kwa zaidi ya miongo mitano sasa, CCM (na kabla yake TANU na ASP) iliweza kubadili dira na mwelekeo wake ili kwenda sambamba na mahitaji ya Watanzania ya wakati husika. Ndiyo maana tumepita katika vipindi tofauti vya mpito kwa mafanikio makubwa licha ya changamoto nyingi zilizotukabili. Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani licha ya kubadili mfumo wetu wa siasa kutoka ule wa chama kimoja kuja vyama vingi; licha ya kubadili mwelekeo wa uchumi wetu kutoka ule wa dola kumiliki njia zote kuu za uchumi kuja katika uchumi wa soko unaozingatia ushiriki mpana wa Watanzania wa matabaka yote; na hata karibuni kabisa katika mchakato wa kuipatia nchi yetu Katiba mpya.Tanzania tumeweza kufanya mabadiliko ya uongozi mara nne katika hali ya amani na maelewano, jambo ambalo nchi nyingi za Afrika zimeshindwa. Ni imani yangu kwamba tukijikubalisha tunaweza tena kuwapa Watanzania wanachokitaka katika zama hizi za sasa. Lakini ni lazima tuoneshe dhamira hiyo kwa dhati ili, kama alivyotuasa Mwalimu Nyerere, Watanzania wasiyatafute mabadiliko hayo nje ya CCM. Nasisitiza tena kwamba CCM inao uwezo wa kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka, lakini pia wananchi wana hiali kuchagua mabadiliko wanayoyataka.


UONGOZI UNAOHITAJIKA KULETA MABADILIKO YANAYOTAKIWA:

Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kipindi chake na kama ambavyo amekuwa akisisitiza mara kwa mara katika hotuba zake za karibuni ni kwamba yeye ametekeleza wajibu wake kwa kuweka misingi imara ya ujenzi wa Taifa la kisasa lenye uchumi madhubuti na unaoweza kukua kwa kasi. Amesema anamwachia atakayemkabidhi uongozi wa nchi yetu baada ya yeye kumaliza muda wake kuendeleza pale atakapoachia.

Kwa maoni yangu ili kuifanya kazi hiyo na kuzikabili changamoto nilizozieleza, nchi yetu inahitaji uongozi wenye sifa zifuatazo:

-    Uongozi wenye uthubutu, usioogopa kufanya kufanya maamuzi magumu;

-    Uongozi thabiti na usioyumba;

-    Uongozi makini na mahiri;

-    Uongozi wenye ubunifu na wenye upeo mkubwa;

-    Uongozi utakaozikabili changamoto kifua mbele na siyo kuzikimbia;

-    Uongozi unaoamini katika mfumo shirikishi katika ujenzi wa Taifa;

-    Uongozi unaozingatia muda katika kutekeleza majukumu yake.

Naamini pia kwamba wananchi wanataka Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awe na sifa kuu zifuatazo:

-    Aweze kuwaunganisha Watanzania (kukabiliana na viashiria vya migawanyiko ya aina mbali mbali inayoinyemelea Tanzania);


-    Aweze kuja na sera na mikakati ya kuinua uchumi wa Tanzania na kukuza pato la Mtanzania;ikiwemo kupunguza tofauti ya kipato kati ya aliyekuwanacho na wasiokuwanacho;


-     Aweze kuja na sera na mikakati ya kuzalisha ajira kwa vijana wetu;


-     Aweze kutokomeza mianya ya rushwa kwa vitendo;

-    Aweze kuwa mfano wa kuchapa kazi na kuwajibika;


-     Asimamie nidhamu ya matumizi ndani ya Serikali;


-     Aweze kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali;


-     Aweze kutumia fursa yetu ya kijiografia kibiashara


UONGOZI IMARA, TAIFA IMARA:

Naamini kwamba uongozi wa juu wa nchi katika nafasi ya Urais si kazi ya lelemama na unahitaji utashi. Kabla hata ya kutakiwa na wenzako ni lazima kwanza wewe mwenyewe uamini na uwaaminishe wenzio kwamba unao uwezo wa kuwaongoza wananchi wenzako. Na katika hilo, rekodi yako ni lazima izungumze na kulithibitisha hilo.

Binafsi nina hazina ya uzoefu na rekodi njema ya matokeo ya kazi nilizozifanya katika uongozi na utumishi wa umma ndani ya CCM na ndani ya Serikali. Nilianza kazi nikiwa Katibu Msaidizi wa CCM katika mikoa ya Shinyanga, Arusha na Moshi. Nimekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya CCM. Niliingia Bungeni mwaka 1985 na baadae mzee wangu, Rais Ali Hassan Mwinyi, akaniamini kwa kuniteua kuwa Waziri. Nimekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Ardhi, Makaazi na Maendeleo ya Miji, Waziri wa Mazingira, Waziri wa Maji na hatimaye Waziri Mkuu.

Miongoni mwa mafanikio ninayojivunia katika uongozi na utumishi wangu, na ambayo Watanzania wanayatambua na naamini wanayathamini, ni pamoja na:

-    Nikiwa Waziri wa Maji chini ya uongozi mahiri wa Rais Mkapa,tulithubutu kushawishi na kuongoza hatua za kukataa kufungika na makubaliano yaliyowekwa na wakoloni ambayo yalikuwa yanazizuia nchi zilizopakana na Ziwa Victoria zisiweze kufaidika ipasavyo na maji ya Ziwa hilo. Leo hii ndugu zangu wa Kanda ya Ziwa wanafaidika na ujasiri wetu katika kukabiliana na suala hilo zito.

-    Nikiwa Waziri wa Mazingira, tulipanda miti mingi zaidi kuliko wakati mwingine wowote tokea Uhuru na pia kuwakabili kikamilifu na kuwachukulia hatua waliochafua na kuharibu mazingira.

-    Nikiwa Waziri Mkuu, tulisimamia agizo la Rais Kikwete na kufanikisha utekelezaji wake ndani ya miaka miwili kwa kujenga shule nyingi za sekondari kuliko wakati mwingine wowote tokea Uhuru.

-    Kipindi hicho hicho, tulisimamia agizo la Rais Kikwete la kuanzisha Chuo Kikuu cha Dodoma na kuhakikisha kinakamilishwa kwa wakati. Leo hii Chuo Kikuu hicho ni fahari ya Tanzania.

Tunapomtafuta Rais wa Jamhuri ya Muungano ni lazima tukumbuke kwamba tunamtafuta mtu ambaye atakuwa pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika nchi yetu. Na kwa Chama Cha Mapinduzi tunamtafuta mtu ambaye atakuwa pia Mwenyekiti wa Chama chetu.

Naamini kwa vigezo vyote, nina kila sifa ya kubeba dhamana hizo nzito. Katika mambo ambayo najivunia na sitoyasahau katika historia yangu ni kushiriki kwangu kuilinda nchi yangu pale ilipohitajika. Nilishiriki kikamilifu katika Vita vya Kagera nikiwa miongoni askari wa mstari wa mbele wa mapambano. Nikiwa Mbunge nilipata heshima ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama. Naamini Watanzania hawatakuwa na wasiwasi wa usalama wao nikiwa Amiri Jeshi Mkuu.

Nimeeleza uzoefu wangu kwenye Chama na huo hauhitaji maelezo zaidi. Ninakijua vyema Chama Cha Mapinduzi kiasi cha kutosha kabisa kukiongoza kama Mwenyekiti wake pale wakati utakapofika. Wana-CCM wanajua nikikabidhiwa uongozi, Chama chetu kitakuwa chini ya nahodha madhubuti, mzoefu na asiyeyumba.

Kutokana na rekodi yangu hii, naamini ninazo sifa za kuwaongoza Watanzania wenzangu katika zama mpya za ujenzi wa Taifa la kisasa lenye watu wazalendo walioshikamana na lenye uchumi imara unaomnufaisha kila Mtanzania. Naamini ninao uwezo wa kuwapa Watanzania Uongozi imara kwa ajili ya ujenzi wa Taifa Imara.


DIRA YANGU NA MATARAJIO YA WATANZANIA:

Mfumo tuliojiwekea hapa nchini unaelekeza kila chama cha siasa kinachosimamisha mgombea Urais na kinachowania kuongoza nchi yetu kuja na Ilani ya Uchaguzi ambayo ndiyo inayoweka misingi ya sera zitakazofuatwa na Serikali itakayoongozwa na chama hicho pale kinapopewa ridhaa ya kuongoza nchi. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa ni cha kupigiwa mfano katika kutayarisha Ilani bora na ndiyo maana mara zote kimepewa ridhaa ya kuongoza nchi yetu. Tumefanya hivyo tokea enzi za mfumo wa chama kimoja na tumeendelea kufanya vizuri katika mfumo wa kushindanisha sera kupitia vyama vingi. Najua kwamba Ilani ya CCM ya mwaka 2015 imo katika hatua za mwisho za kukamilishwa na itakapopata baraka za vikao vya Chama itakuwa ndiyo msingi wa utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano itakayochaguliwa Oktoba mwaka huu. Hata hivyo, naamini pia kwamba mgombea mwenyewe anayetaka ridhaa ya Chama na ya Watanzania kuongoza nchi naye anapaswa kueleza dira yake.

Mimi, baada ya kutafakari kwa kina changamoto tulizo nazo na matarajio na matumaini waliyo nayo Watanzania, naamini kwamba Uongozi imara unaolenga kujenga Taifa imara unapaswa kuwa na dira yenye malengo yafuatayo:


-    Kuimarisha Muungano wetu kwa kuyashughulikia yanayotutenganisha na kuyafanyia kazi ili yasivuruge yale yanayotuunganisha ambayo ni mengi zaidi na makubwa zaidi.


-    Kushughulikia matumizi mabaya ya siasa za udini na ukabila kwa kuimarisha siasa zilizoshiba uzalendo na zenye kutuelekeza kwenye Utanzania wetu.


-    Kujenga uchumi imara na wa kisasa, na ambao ni shirikishi unaomnufaisha kila Mtanzania aliyeko mjini au kijijini. Tunapaswa kubadili hali tuliyo nayo sasa ambapo Kilimo kinaonekana kama kimesahauliwa na wakulima wetu wanaonekana wanakata tamaa.Wafugaji na wavuvi nao wanahisi sekta zao hazijapewa umuhimu unaostahiki. Tunahitaji kuondokana na hali iliyopo sasa ya kuwa Taifa linalouza malighafi na badala yake kuwa Taifa linalosindika na kusarifu mazao na kutengeneza wenyewe bidhaa zitokanazo na malighafi yake. Ndani ya miaka mitano ijayo tutahakikishatunaiondolea Tanzania sifa ya kusafirisha malighafi na badala yake kusindika mazao yanayozalishwa hapa nchini kama pamba, kahawa, chai na korosho na kuyaongezea thamani (value addition).Mkakati huu utazalisha ajira nyingi na kuongeza mapato ya fedha za kigeni nchini. Tunahitaji kujielekeza kwenye kujenga viwanda na kuleta ajira. Tuna vivutio vingi sana vya utalii lakini bado Tanzania inapitwa na nchi kama Afrika Kusini katika kuingiza idadi kubwa ya watalii. Kwa nini nchi kama Dubai iweze kuvutia watalii kwa mamilioni na Tanzania tushindwe? Tunapaswa kukabiliana kikamilifu na hisia zilizopo miongoni mwa wananchi kwamba Tanzania hainufaiki ipasavyo na utajiri wa rasilimali zake nyingi ilizo nazo. Tutajipanga zaidi kuhakikisha tunanufaika kama nchi na rasilimali zetu kama madini na gesi asilia. Hii ndio Safari ya Matumaini


-    Kukuza kipato cha wananchi na kunyanyua hali za maisha ya watu wetu. Tunapaswa kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi tunaouzungumzia unamnufaisha Mtanzania aliyeko mjini au kijijini na kwamba hali za Watanzania wa matabaka yote zinanyanyuka na kwamba wanaridhika na kuuona uhalisi wa ukuaji wa maendeleo tunayoyazungumzia.


-    Kuondokana na sifa mbaya ya kuwa Taifa ombaomba. Kwa wingi wa rasilimali tulizo nazo na neema ya ardhi, maziwa, mito na bahari Tanzania tuna kila sababu ya kuacha kuwa ‘bakuli la ombaomba’ na badala yake kuwa ‘mkoba wa neema’ katika Afrika.We can transform our nation from being the begging bowl to become the bread basket of Africa.


-    Kujenga mfumo mpya wa elimu unaojielekeza kuwatayarisha vijana wetu waweze kuajirika, kujiajiri na kushindana katika soko la ajira. Tumepiga hatua kadhaa katika elimu lakini kiwango cha elimu bado ni hafifu. Pamoja na kuwa na shahada (degrees), bado wahitimu wetu hawawezi kushindana kwenye soko la ajira. Wakati tunazungumzia kuunganisha soko la ajira katika Afrika Mashariki,hatuna budi kujikita kubadili mfumo wetu wa elimu na kuuelekeza kwenye mafunzo ya ufundi na stadi yanayowajenga wahitimu wetu kuwa wabunifu na wenye kujiamini katika kukabiliana na changamoto za maendeleo duniani.


-    Kuhakikisha tunakabiliana ipasavyo na kulipunguza kwa kiasi kikubwa kama si kulimaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama. Ni jambo la kusikitisha kwamba tumezungukwa na mito na maziwa lakini bado watu wetu hawana maji ya kunywa hata ndani ya Dar es Salaam.

-    Kujenga na kusimamia mfumo imara wa kutekeleza sera na sheria tunazozitunga na kuzipitisha kwa lengo la kumtumikia Mtanzania na kumjengea uwezo wa kubadili maisha yake ili tuweze kwenda sambamba na viwango vya kimataifa. Tanzania imepata sera na sheria nzuri sana lakini utekelezaji wake umekuwa hafifu. Tumekuwa wepesi wa kutunga sera na sheria lakini wazito mno wa kuzitekeleza na kuzisimamia. Uongozi imara wenye kulenga ujenzi wa Taifa imara utahakikisha tunakuwa mfano wa utekelezaji wa sera na sheria tulizo nazo na mpya zitakazotungwa kukabiliana na malengo tuliyojiwekea.


Mambo haya niliyoyaeleza hapa ndiyo yatakayokuwa msingi mkuu wa utendaji wa Serikali nitakayoiongoza pale nitakapopewa ridhaa ya kubeba bendera ya CCM katika nafasi ya Urais na pia nitakapopewa ridhaa ya kuliongoza Taifa letu kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka huu.



RAMANI YA UONGOZI IMARA NINAOUAMINI (LEADERSHIP ROADMAP):

Kama nilivyotangulia kusema, kazi ya kuongoza nchi si lelemama na hasa unapoongozwa na dhamira ya dhati na msukumo wa ndani ya nafsi unaojielekeza kubadilisha maisha ya wananchi wenzako waliokuamini uwaongoze. Kwa vyovyote vile, hiyo haiwezi kuwa kazi ya mtu mmoja. Ni kazi ya pamoja. Lakini ili muweze kufanya kazi kama timu moja iliyojipanga kisawasawa kuleta mabadiliko yanayohitajika na ili muweze kweli kutoa Uongozi imara unaojikita kujenga Taifa imara hapana budi kiongozi mkuu anayeongoza timu hiyo aweke ramani anayokusudia kuifuata katika kutoa uongoziimara anaoukusudia yaani ‘Leadership Roadmap’.

Pamoja na kuwa sehemu ya uongozi huko nyuma, kutakuwa na maamuzi na matumaini mapya. Ramani ya uongozi imaraninayokusudia kuutoa kwa wenzangu na ambayo nitaitumia kuiongoza timu yangu katika kuwatumikia Watanzania wenzangu itajikita katika maeneo yafuatayo:


1. Kurejea kwenye Katiba katika kuainisha nia, dhamira na malengo yetu ya kujenga jamii inayozingatia misingi ya demokrasia, udugu na amani. Muhimu katika hili ni kukemea tabia mbaya zinazochochea mfarakano katika jamii kama vile matumizi mabaya ya siasa za udini na ukabila. Aidha moja ya misingi muhimu ya Katiba ni Muungano wetu. Itakuwa dhamira yangu kuimarisha misingi ya Muungano pamoja na udugu wa damu nahistoria ya ushirikiano iliyojengwa na waasisi wetu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Amri Abeid Karume na kuyaenzi Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.


2. Kujenga fikra mpya za kurejesha kujiamini na kufufua azma ya kujitegemea kama Taifa. Ni dhahiri kuwa pamoja na rasilimali zetu, bado Tanzania ni taifa tegemezi. Bado tunajidanganya kuwa wafadhili watatujengea nchi. Tukumbuke, nchi zinajengwa nawananchi wake. Nasi pia lazima tujikomboe kifkra na tuondokane na utamaduni wa kuwa tegemezi. Tuanze kwa kujipiga kifua kwa kujiamini kuwa tunaweza kujitegemea na kuijenga Tanzania sisi wenyewe.Kujiamini na kujitegemea ndio uhuru wa kweli.


3. Kujenga uzalendo, uadilifu ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwazi katika shughuli zote za serikali na kupambana na rushwa.Watanzania tumepoteza uzalendo kwa kiasi kikubwa. Kuna vitendo vinavyoashiria kuwa hatuipendi tena nchi yetu. Tunashabikia wizi na rushwa. Inabidi turejee kwenye misingi ya taifa letu misingi ya uadilifu na uzalendo. Tukumbuke kuwa hatuwezi kujenga uchumi wa kisasa kama tutaruhusu rushwa ishamiri. Wawekezaji hawataleta mitaji yao kwa wingi kama rushwa itaendelea kutawala katika huduma serikali na wananchi hawawezi kupata huduma bora kama rushwa itaendelea kutawala. Ni lazima tuipinge rushwa kwa vitendo sio maneno.



4. Kujenga Serikali madhubuti, makini na yenye nidhamu inayoendeshwa kwa misingi ya sheria, uwazi na uwajibikaji.Maendeleo ya watu hayawezekani bila serikali kusimamiautekelezaji sera na miradi na kuleta ufanisi katika kutoa huduma na kusimamia maendeleo. Tumekuwa wepesi wa kutunga sera lakini wazito wa kuzitekeleza na kuzisimamia.


5. Kuleta msukumo mpya wa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi katika ujenzi wa uchumi wa kisasa na unaojitegemea. Sekta binafsi ndiyo nyenzo ya uchumi imara. Inazalisha mali, ajira na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kwa kulipa kodi. Ilisekta hii itoe mchango unaotakiwa katika maendeleo ni lazima ifanye kazi na serikali kwa karibu. Tukumbuke, bila uchumi imarahakuna huduma bora!


6. Uwekezaji katika huduma za jamii. Elimu na afya bora, mazingira, makazi safi na maji salama ndiyo mihimili ya maendeleo ya watu. Hii inawezekana tu iwapo serikali itakuwa na sera na utashi wa kuutambua uboreshaji wa huduma za jamii kama ndiyo lengo kuu la maendeleo ya nchi. Serikali nitayoiongoza itahakikisha kuwa kila Mtanzania anapata elimu bora na inayogharamiwa na serikali kama mimi na wenzangu tulivyopata. Wakatitunazungumzia kuunganisha soko la ajira katika Afrika Mashariki, hatuna budi kurekebisha mfumo wetu wa elimu na kuuelekeza kwenye mafunzo ya ufundi na ustadi yanayowajenga wahitimu wetu kuwa wabunifu, wenye kujiamini, wenye uwezo kushindana katika soko la ajira na wa kujiajiri. Napenda kusisitiza kuwa elimu ndiyo muhimili wa maendeleo, ndiyo mkombozi wa kweli wa binadamu. Mimi ni mfano hai wa ukombozi wa elimu. Elimu ndiyoimenivusha kutoka kijijini kwetu Ngarash na kunipa upeo wa kitaifa. Mama akiwa na elimu atajua umuhimu wa kumpeleka mwanae shule, anapata lishe bora na chanjo stahili na kuwa anaishi katika mazingira safi. Elimu ndilo jibu la umaskini, maradhi na ujinga.Taifa lililo elimika ni taifa lenye maendeleo.




7. Kujenga uchumi shirikishi unaolenga kuondoa umaskini.Mkakati wa kuondoa umaskini Tanzania lazima ujikite kwenye nguzo za ushiriki wa kila Mtanzania katika uchumi wa taifa. Kwa misingi hii, tukiweza kupunguza umaskini, tutaweza pia kupunguzatofauti za kipato ambazo tukiziacha ziendelee kukua kwa kiasi cha sasa, zinaweza kuhatarisha utulivu na amani katika jamii yetu.Uchumi shirikishi ndio silaha dhidi ya umaskini.


8. Kuimarisha ulinzi wa nchi na usalama wa raia na ujirani mwema.Itakuwa nia yangu kuimarisha misingi iliyojengwa kulinda na kudumisha umoja na amani nchini. Kadhalika, nitahakikisha kuwa usalama wa mipaka ya Tanzania unaimarishwa kwa misingi ya ujirani mwema na kutanzua migogoro na matatatizo yoyote na nchi jirani, kwa njia ya diplomasia na mazungumzo.





HITIMISHO:

Hii ndiyo misingi na dira ya uongozi wangu. Nachelea kusema kuwa haitakuwa kazi rahisi. Lakini kwa ushirikiano wa kila mmoja na maamuzi magumu, yote yanawezekana. Tumeona nchi nyingi zilizosimamiwa na utawala thabiti wa serikali za kimaendeleo zikikabili na kupunguza umaskini katika kizazi kimoja. Kama mataifa mengine yamefanikiwa, tena bila raslimali kama zetu, kwa nini sisi tushindwe? Tuna kila sababu ya kufanya maamuzi magumu sasa ili kuwajengea Watanzania matumaini mapya ya maendeleo. Naomba nisisitize kuwa katika uongozi wangu hakutakuwa na nafasi ya majungu, na visasi. Hatutaangalia nyuma bali tutasonga mbele kwani ndicho Watanzania wanakitarajiakutoka kwa uongozi uliojengwa kwenye misingi bora.


Ndugu Watanzania:-


Ni maono yangu kuwa siku si nyingi nchi yetu itaanza safari yenye uelekeo wa matumaini na neema tele kwa wananchi.


Ni maono yangu kuwa siku si nyingi sisi kama Watanzania kwa umoja wetu tutajivunia kuishi katika nchi tunayoipenda na inayoendeshwa kwa misingi ya utawala bora, chini ya serikali ya kimaendeleo iliyojengwa kwenye fikra mpya za uzalendo, uadilifu, utendaji na uwajibikaji.


Ni maono yangu kuwa Peke yangu sitaweza, lakini kwa maamuzi magumu na ushirikiano wa kila mmoja wetu ikiwa ni pamoja na wagombea wenzangu ndani ya CCM, inawezekana kuanza safari hii ya Matumaini Mapya.

Kabla ya kumaliza hotuba yangu hii fupi, kuna mambo matatu ningependa kuyaweka wazi hapa.


La kwanza, linahusu msingi wa uongozi ninaouamini na ambao nimeusema mara kadhaa hapa. Msingi huo ni UWAJIBIKAJI.Watanzania wananifahamu mimi si mtu wa maneno, ni mtu wa vitendo. Naamini kwa dhati kabisa kwamba huwezi kuwa na Uongozi imara utakaoweza kusimamia ujenzi wa Taifa imara iwapo huna ujasiri wa kuwajibika. Mimi nimeongoza kwa mfano, na pale ilipobidi, nilikubali kuwajibika na kubeba dhamana ya uongozinilipojiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu.


La pili, mimi si mtu wa visasi. Siamini katika kuangalia ya nyuma. Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Na kwa nini tuangalie nyuma wakati kama taifa tuna kazi kubwa sana mbele yetu inayohitaji kufanywa? Mimi ni Mkristo; najifunza kutoka kwa Bwana Yesu ambaye alipoulizwa: “Nisamehe mara ngapi?” Alijibu, “Samehe mara sabini mara saba”. Nitaenzi na kudumisha utamaduni huu wenye sura ya utu na heshima.


La Tatu, natambua kwamba dhamana ya Urais ni shughuli nzito hasa kwa taifa ambalo lina changamoto nyingi. Nataka niwahakikishie Watanzania wenzangu kwamba afya yangu ni njema kuweza kuwatumikia katika jukumu hili zito. Pamoja na vijineno vinavyosemwa pembeni, mimi mwenyewe ndiye ninayejijua zaidi. Nawahakikishia kuwa nisingekuja hapa leo na kueleza nia yangu hii ingekuwa sina uhakika na afya yangu.

Natoa RAI kwa Chama changu cha CCM, nadhani umefika wakati kwamba tutende tofauti na mazoea, watu wote walionyesha nia ya kutaka kuongoza, liundwe jopo la madaktari wa ndani na nje ya nchi tupimwe afya zetu, kwa hili najitolea kuwa wa KWANZA KUPIMWA afya yangu


Safari tuianze leo, hatuna kesho nyingine.



Ahsanteni sana kwa kunisikiliza?

30/5/2015.

KATABAZI Vs.MULEMULE FBI


Happiness Katabazi na Mtunzi wa wimbo wa Ndoa ya Kisasa katika albamu ya CHUKI YA NINI  wa Bendi ya FM Academia 'Ngwasuma, Mulemule FBI.Nampenda Mulemule tangu enzi hizo hadi sasa anajua kucheza Ngwasuma na ana sauti nzito.' Biloko ya Mulemule Biloko', 30/5/2015.

NAENDELEA KUKULIA WAKILI STANSLAUS BONIFACE ' JEMBE', 2015




Na Happiness Katabazi

Leo  Mei 27 mwaka  2015, mpendwa wetu  aliyekuwa Wakili Kiongozi wa Serikali mwenye  cheo cha Mkurugenzi  Msaidizi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface Makulilo ‘Jembe’ anatimiza miaka mitatu tangu afariki ghafla  tarehe kama ya leo Mei 27 mwaka 2012 katika  Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam.

Kila mwaka tarehe kama ya leo nimekuwa nikiandika makala ya kumbukizi ya kifo cha marehemu Boniface kwasababu wakili huyu Mwandamizi nilikuwa nikiheshimu na nitaendelea kuheshimu na kuthamini mchango wake kwa serikali kupitia taaluma yake ya sheria k hasa katika eneo la uendeshaji wa mashitaka kwa niaba ya Jamhuri.

Nilifahamiana na Boniface katika mahakama za Dar es Salaam tangu mwaka 2008.

Kilichotuunganisha mimi na Kaka Boniface ni kazi za ujenzi wa taifa tulizokuwa tukizifanya mahakamani katika mahakama hizo.

Yeye alikuwa ni wakili wa Serikali na mimi nilikuwa Mwandishi wa habari za mahakamani wa gazeti la Tanzania Daima.

Hivyo tulifanyakazi pamoja na nilipoanza safari yangu ya kuanza kusoma fani ya sheria mwaka 2009 hadi sasa Boniface naye kama walivyo baadhi ya majaji,mahakimu,wanasheria mbalimbali waliokuwa wakinipa moyo nisome fani ya sheria.

Boniface alikuwa akishiriki wakati mwingine kunifundisha baadhi ya topic na alikuwa akinipa sheria mbalimbali ambazo hadi sasa zinanisaidia katika masomo yangu ya kozi ya sheria.

Kwa wale tuliopata fursa ya kuwa karibu na Boniface kikazi na kijamii ama kwa hakika si majaji, mahakimu,wapelelezi wake na walalamikaji katika kesi za jinai,waandishi wa habari za mahakamani hakika wengi wetu tunakiri wazi wazi serikali ilipoteza Mwendesha mashitaka mahiri ambaye uenda alipokuwa hai watawala waliokuwa wameshika nyadhifa za juu serikalini walikuwa hawafahamu vizuri kipaji alichokuwa nacho Boniface cha kutumia taaluma yake ipasavyo kuipigania serikali katika kesi zake kwa ufundi wa kisheria wa hali ga juu.

Boniface nakumbuka mbwembwe zako za kiuwakili wa serikali ulizokuwa ukionyesha mahakamani na wakati ukijitambulisha mbele ya hakimu au jaji anayesikiliza kesi uliyokuwa ukiiendesha ulikuwa ukipenda kutumia neno hili ' Ikupendeze Mheshimiwa jaji,hakimu'  kisha unaweka mkono mfukoni unatoa,unendelea 'kusilisha hoja  wewe ulikuwa ukipenda kusema (una mwaga vitu) huku 'ukiswing ' kwenye 'bar'.

Yaani ukionyesha mikogo ya wanasheria  katika eneo wanalokaa mawakili kuendeshea kesi wakati kesi ikiendelea.

Boniface alikuwa ni tishio kwa baadhi ya mawakili ambao wanakuwa hawajipanga vyema kuwatetea wateja wao na alikuwa tishio kwa washitakiwa wa kesi alizokuwa akiziendesha.

Ndio maana Boniface alipo fariki kuna wengine tulilia sana kwakujua tumepoteza wakili mahiri wa serikali.

Lakini wanaopenda uhalifu na washitakiwa baadhi ambao Boniface alikuwa ni mwiba kwako walifurahia sana kwakusema kizingiti kimeondoka.

Lakini kikubwa zaidi ulipokuwa mahakamani ukiona shahidi anataka kukuchezea akili ulikuwa ukiomba kutoka nje unakwenda kwenye kordo za mahakama na kuvuta 'Fegi'  zako kisha unarudi mahakamani kutwanga shahidi kwa hoja za kisheria.

Nilivutiwa sana na umahiri wa uendeshaji wa mashitaka uliokuwa ukifanywa na kaka Boniface.

Boniface leo ukiwa unatimiza miaka mitatu tangu ulipofariki dunia ,kikubwa kilichojiri katika tasnia ya eneo la sheria katika serikali ni aliyekuwa Mkuu wako wa Kazi Mkurugenzi wa Mashitaka  DPP- Dk.Eliezer Feleshi ,Agosti 13 mwaka 2014,  Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Jaji wa  Mahakama Kuu na ofisi yake ni Kanda ya Dar es Salaam, yupo anaendelea kupiga mzigo.

Pia kijana wako Biswalo Mganga ambaye mlikuwa mkifanyaka nae kazi katika ofisi ya DPP, Oktoba 6 mwaka 2014 alipandishwa cheo baada ya  Rais Kikwete kumteua kuwa  Mkurugenzi mpya wa  mashitaka  nchini (DPP) kurithi nafasi iliyoachwa wazi ni Dk.Feleshi.

Pia Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju ,Januari 2 mwaka 2015  ,aliteuliwa na rais kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema, Disemba 16 mwaka huu,  kujiuzulu wadhifa huo kwa kile alichoeleza kuwa ushauri wake alioutoa katika Akaunti ya Tegeta  Escrow umeeleweka vibaya.

Naye AG- Masaju anafanyakazi yake vizuri ila ndiyo hivyo tena hatutamuona tena mahakamani akiendesha mashauri mbalimbali kwa niaba ya serikali kwa sababu amepandishwa cheo.

Mganga anaendelea na kazi yake hiyo vizuri tu na bado hajaanza kufanya ufisadi na nilimuaidi katika makala niliyomuandikia wakatj alipoteuliwa kushika wadhifa huo kwamba nikibaini ameanza kuwa fisadi wa kikweli kweli basi nitamuanika kupitia makala zangu bila huruma.

Kwa upande wangu mimi Happiness Katabazi, Agosti Mosi mwaka 2014 niliachakazi rasmi katika gazeti la Tanzania Daima  na kwenda kuwa Ofisa Habari wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo,Mikocheni Dar es Salaam na wakati huo naendelea kusoma kozi yangu ya Sheria kama ulivyokuwa ukiniasa.

Kwa sabababu hivi sasa sio Mwandishi tena wa habari za mahakamani kama zamani na napo majariliwa Agosti mwaka huu,nitakuwa nikienda mahakamani kufanya mazoezi ya kwa vitendo(field) kama mwanafunzi wa Shahada ya Sheria na siyo tena kwenda mahamani kwa kofia ya Uandishi wa habari. kwenda kuripoti kesi mbalimbali.

Katika Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam, kesi zenye mvuto zilizofunguliwa kuanzia mwaka jana hadi sasa ni kesi ya Ugaidi inayomkabili
Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheikh Farid  Ahmed (44).

Kesi hiyo ambayo  haina dhamana hivyo wapo gerezani na kila siku baadhi ya washitakiwa toka  Zanzibar hawaishi kutoa malalamiko yao katika Mahakama ya Kisutu kwamba watagoma kula, mara wasipoachiriwa huru watafanya kitendo ambacho kitashangaza umma, mara walivyokuwa gerezanki kule Zanzibar walilawitiwa sana gerezani hivyo wamearibika sana sehemu za siri za mihili yao na mbaya zaidi jeshi la Magereza haliwapatibabu kwani wanazidi kuaribika sehemu zao za siri  na wakiletwa mahakamani wanaletwa chini ya ulinzi mkali sana wa askari Magereza.

Kesi nyingine iliyofunguliwa na Jamhuri ni kesi dhidi ya wahitimu wa mafunzo ya JKT ambao mwaka huu ,wahitimu hao walizusha taaluki katika jamii wakishitishia wataandamana kwasababu hawajapewa ajira hali iliyosabishwa kukamatwa na kushitakiwa na DPP- Mganga akawasilisha ombi chini ya kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 la kufunga dhamana kwa wahitimu ambao hadi sasa wapo gerezani na wamekuwa na nidhamu maana walikosa nidhamu.

Kesi nyingine inayovuta hisia za watu wengi ni kesi ya uchochezi inayomkabili Sheikh Ponda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro ambayo inaendelea licha Ponda yupo gerezani kwa sababu DPP alimfungia dhamana.

Ile kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 11 inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha,Basil Mramba na wenzake ambayo ulianza kuiendesha imefikia hatua washitakiwa wameishamaliza kujitetea.

Kuhusu kesi za EPA ,Kada wa CCM, Shaban Maranda amemaliza kifungo chake katika kesi zilizokuwa zikimkabili,ila Farijala Hussein alimaliza kifungo chake na akarudi uraiani huku akiendelea na kesi zake lakini mwaka huu, amerudishwa gerezani baada ya kupatikana na hatia.

Kuhusu zile jumla ya kesi 11 za wizi katika akaunti za EPA katika Benki Kuu, ambazo wewe (Boniface)na mawakili wenzako mlikuwa mkiziendesha na hadi unakutwa na mauti uliweza kufanikiwa kushuhudia kesi moja ya EPA ya wizi wa sh.bilioni 1.3 iliyokuwa ikimkabili Rajabu Maranda na Farijala Hussein wakihukumiwa kwenda jela miaka mitano, na ulivyofariki pia tayari kuna hukumu za kesi mbili za EPA ambazo zinamhusisha Maranda ,Farijala na maofisa wa BOT watatu zilitolewa hukumu. Hivyo kesi nyingine za EPA zilizosalia bado haizajatolewa hukumu .

Ila zile kesi nne za EPA zinazomkabili mfanyabiashara maarufu Jeetu Patel  zilizofunguliwa Novemba 2008 bado hata shahidi mmoja wa upande wa jamhuri hawajaanza kupanda kizimbani kuanza kutosha ushahidi wake.

Hizo ni simulizi chache za baadhi ya kesi zilizovuta hisia katika jamii na sisi waandishi wa habari kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja ambacho wewe haupo nasi duniani.

Ila napenda nikuakikishie tu kuwa mawakili wa serikali bado wanatupatia ushirikiano wa kutosha sisi waandishi wa habari za mahakamani kama zamani.

Unakumbukwa na waandishi wa habari za mahakamani wenzangu Furaha Omary, Magai James, Tausi Ally, Faustine Kapama, Kulwa Mzee,Grace Gurisha, Frola Mwakasala ,Karama ,Hellen Mwango.

Lakini bado unakumbukwa na mawakili na Jaji Dk.Eliezer Feleshi, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Duwani Nyanda , DPP- Biswalo Mganga, Malangwe Mchungahela, Tumaini Kweka ,Sedekia Emphere,Fredrick Manyanda,Oswald Tibabyekomya, Lasdslaus Komanya, Tumaini Kweka, Ponsian Lukosi,Ben Lincoln,Arafa Msafiri, Timon Vitalis,Michael Lwena ,Bernad Kongora na wengine wengi.

Ambao kwa kadri ya uwezo wao wanafanya vizuri katika majukumu yao ya uendeshaji wa mashitaka, na wengi niliozungumza nao wanakushukuru kwa mchango wako wa kitaaluma kwani hukuwa mchoyo wa kuwafundisha kazi pale walipoitaji msaada huo.

Miongoni mwa kesi kubwa ambazo mimi binafsi nilimshuhudia  Marehemu Boniface  akiziendesha kwa zaidi ya miaka mitano katika mahakama mbalimbali hapa nchini sasa ni kesi ya wizi wa shilingi bilioni 1.8 katika EPA, iliyokuwa ikimkabili Kada wa CCM, Rajabu Maranda na Farijala Hussein ambapo mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 23 mwaka juzi, iliwahukumu kwenda jela miaka mitano, kesi ya kula njama na kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la TBC, Jerry Murro na wenzake ambapo Murro alishinda kesi hiyo mwaka juzi.

Kesi  ya Kikatiba iliyofunguliwa na mfanyabishara Jayankumar Patel “Jeetu Patel’ na wenzake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP na Reginal Mengi iliyokuwa akitaka afutiwe kesi zake nne za EPA zilizopo katika mahakama ya Kisutu kwasababu Mengi alimuhukumu kabla ya hajahukumiwa na mahakama kwa sababu alimuita ni Fisadi Papa, ambapo Boniface alimwakilisha AG na DPP na aliibuka mshindi katika kesi hiyo.

 Kesi nyingine kubwa ambayo marehemu alikuwa akiziendesha ambazo bado hadi umauti unamkuta hazijatolewa hukumu ni ile ya mauji ya Ubungo Mataa ambayo Disemba 19 mwaka 2014,Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Jaji Projestus Rugazia  alitoa hukumu ya kesi hiyo ambayo pia Boniface aliendesha na miongoni mwa Mashahidi wa upande wa Jamhuri ni Kamishna Msaidizi Duwani Nyanda .

Jaji Rugazi akitoa hukumu yake katika kesi hiyo ambayo ilikuwa na vitimbi vya kila aina alisema mahakama yake  imewahukumu kunyongwa hadi kufa  washtakiwa sita  katika kesi ya mauaji ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wa mkoani Morogoro na mfanyakazi wa Benki ya NMB.

Mauaji hayo ambayo yalipata umaarufu na kupewa jina la mauaji ya 'Ubungo Mataa 'yalifanyika Aprili 20,2006  katikati ya Ubungo Mataa jijini Dar es Salaam.

Jaji Projest Rugazia aliwataja  washtakiwa waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa kuwa ni Mashaka Pastory, John Mndasha, Martine Mndasha, Haji Kiweru,  Wycliff Imbora na Rashidi Abdikadir.

Jaji Rugazia alisema aliwatia hatiani washtakiwa hao na kuwahukumu kunyongwa hadi kufa,  kufuatia ushahidi ulitolewa na mashahidi 29 wa upande wa mashtaka pamoja na vielelezo 78 vilivyowasilishwa mahakamani hapo na ushahidi wa utetezi.

“Maungamo ya washtakiwa, ushahidi wa kitaalam na utambuzi wa washtakiwa kutambuliwa eneo la tukio inaonesha wazi walikuwa na nia ya kujaribu kupora takribani Sh 150 milioni mali ya benki ya NMB zilizokuwa zikisafirishwa kutoka  Dar es Salaam kwenda  Morogoro tawi la Wami.” Alisema Jaji Rugazia.

Alisema siku hiyo ya huzuni  ya Aprili 20,2006  majambazi hao walilivamia gari  hilo kwa lengo la kupora lakini  bila ya kuwa na huruma yoyote walilimiminia risasi na kuwaua  D 6866 Konstebo Abdallah Marwa na mfanyakazi wa NMB tawi la Wami Morogoro, Ernest Manyonyi.

Walifanya tukio hilo nyakati za saa 6:30 mchana, eneo la Ubungo Mataa jijini Dar es Salaam kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma.

Akiendelea kusoma hukumu hiyo, Jaji Rugazia aliwaachia huru washtakiwa Rashid Lemblisi, Philipo Mushi, Yassin Juma,

Hamisi Daud, MT 77754 Nazareth Amurike, MT 76162 Emmanuel Lameck, James Chamangwana na Hussein Idd baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi hiyo.
Kwa upande wa washtakiwa, Jackson Issawangu aliyekuwa mshtakiwa wa sita katika kesi hiyo na Mussa Mustafa aliyekuwa mshtakiwa wa 10 waliachiwa huru awali baada ya mahakama hiyo kuwaona kuwa hawana kesi ya kujibu.

Hadi wanaachiwa huru siku hiyo ya Disemba 19 2014, washtakiwa hao walikuwa wamekwisha kaa  rumande kwa muda wa zaidi ya miaka nane.

Kesi nyingine aliyokuwa akiiendesha Boniface ni rufaa ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomwona mfanyabiashara Naeem Gile ambayo inasikilizwa mbele ya Jaji Laurence Kaduri ambaye alikuwa akikabiliwa na makosa ya kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni ya kufua umeme ya Richmond LCC, kuwa hana kesi ya kujibu, rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Kisutu iliyomuona Jerry Murro hana hatia na kesi ya matumizi mabaya na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 inayomkabili waliokuwa mawaziri wa Fedha na Nishati, Basil Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja ambapo kesi hii hivi sasa imefikia hatua ya Mramba kuendelea kujitetea

Boniface alizaliwa Februali 21 mwaka 1968 ameacha mke na watoto watatu, aliitimu shahada ya kwanza ya Sheria mwaka 1995 na shahada ya pili ya sheria alimaliza mwaka 2008 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Julai Mosi mwaka 1995 aliajiriwa rasmi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kama Wakili wa Serikali, ilipofika Oktoba Mosi mwaka 2006 alipandishwa cheo na kuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi.

Oktoba Mosi mwaka 2007 alipandishwa cheo tena na kuwa Wakili Kiongozi wa Serikali.

Nyadhifa ambazo Boniface aliwahi kuzishika enzi za uhai wake ni kati ya mwaka 2003-2007 alikuwa ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Mbeya.

Kati ya Mei 2007 na Oktoba 2010 alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi Kanda ya Mwanza.

Novemba 2009 hadi Novemba 2010 alikuwa Mwanasheria Mfawidhi wa Serikali mkoani Dar es Salaam. Kutokana na utendaji kazi wake mzuri ilipofika Disemba 2010 hadi mauti yanamkuta aliteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha uendesha mashitaka na pia awaka Msimamizi wa uendeshaji kesi zenye maslahi kwa umma. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake liimidiwe.

Leo umetimiza miaka mitatu  tangu Boniface ufariki dunia Mei 27  na Mei 29 mwaka 2012 ulizikwa katika Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam mwaka 2012. Naendelea kukulia Wakili Stanslaus Boniface ' Jembe'.

Chanzo:Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Mei 27 mwaka 2015

KIKWETE: CCM KWANZA MTU BAADAE




" ....LAZIMA  tusome alama za nyakati .Kubwa zaidi tutambue watu wanataka mtu wa aina gani.Au kwa maneno mengine tutambue zaidi  wanachukizwa na mtu wa namna gani.
Tusipeleke MTU ANAYEAKISI  mambo yanayochukiza wanachi...".

Nukuu hiyo ni ya Mwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya ufunguzi wa Kikao cha NEC kilichoanza jana Mei 23 na kinatarajia kumalizika leo Mei 24 mwaka 2015.

Binafsi mimi katika haya hii isemao ' TUSIPELEKE MTU ANAYEAKISI MAMBO YANAYOCHUKIZA WATU.

 Nimeielewa kwamba Rais Jakaya Kikwete alikuwa akimaanisha wana CCM wasimteue Kada wake ambaye anaandamwa na tuhuma mbalimbali ambazo zinachukiza watu.

Na hakuna ubishi Watanzania hivi sasa wanachukizwa sana na vitendo vya utoaji rushwa na ufisadi, Hadi sasa baadhi watu wanaotajwa tajwa kugombea Urais kupitia CCM wakiwemo madata sita wansoongozwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa nwalishatiwa hatiani kwa matendo ya kuvunja Kanuni,kuanza kampeni mapema Februali mwaka 2014  na Mei 22 mwaka huu walimaliza kutumikia kifungo.Hivyo bado wana rekodi ya kifungo kwasababu hukumu ile iliyokuwa ikiwakabili haijawahi kutenguliwa na mamlaka yoyote hivyo hawa wanahesabika ni wafungwa wa CCM waliomaliza kutumikia kifungo.

Na miongoni mwa wanaotajwa tajwa kugombea urais kupitia CCM  wanaakisi mambo yanayochukiza wananchi.

Sasa kwa  kwa tafsiri nyepesi ya aya hiyo iliyopo kwenye Hotuba ya Rais Kikwete, ni kwamba Rais Kikwete kwa mamlaka aliyonayayo anawataka wajumbe wa  NEC wasimpishe mgombea yoyote wa ngazi ya urais ,udiwani,bunge ambaye anaandwa na tuhuma ,matendo yanayochukiza watu.

 Kwa nukuu hiyo wale wote wanaotaka kugombea hasa nafasi ya urais ndani ya CCM, muitafakari sana nukuu hiyo na kila mmoja wenu aone 'dongo hilo la Kikwete' linamhusu yeye binafsi kutokana na vitendo anavyovifanya yeye au genge lake?

 Na kama 'dongo ' hilo linamhusu basi haraka iwezekanavyo aachane na mpango wake wa kugombea urais maana ukimtazama Kikwete wakati akitoa haya hii isemayo ;

 'TUSIMPELEKE MTU ANAYEAKISI MAMBO YANAYOCHUKIZA WATU'  , alibadilika sura na kuonekana kuwa anachukizwa na hilo, na wale 'Dongo' hilo linalowahusu mjiandae Kisaikolojia maana niwazi hamtasalimika.

By Happiness Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blospot.com
0716 774494
Mei 24 mwaka 2015

WAFUNGWA SITA WA CCM WATOKA LUPANGO YA CCM LEO



Hongereni sana kwa kutoka gerezani ila bado mnakazi nzito mbele yenu,heshimuni kanuni msirudie kuvunja tena kanuni.Vitendo  vya kihuni vya kuvunja kanuni na mbavyo vilisababisha CCM iwafunge kifungoni.by Happiness Katabazi..

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu imepokea na kutafakari taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili ambayo ilipitia adhabu waliyopewa wanachama sita waliokiuka kanuni za Maadili na kupewa Onyo Kali, adhabu iliyodumu kwa kipindi kisichopungua miezi 12.
Wanachama hao sita ni;-
i. January Makamba
ii. Willium Ngeleja
iii. Steven Wasira
iv. Bernard Membe
v. Edward Lowassa
vi. Fredrick Sumaye
Kamati Kuu imepokea na kukubali pendekezo la Kamati ya Usalama na Maadili ya kumalizaka kwa kipindi cha adhabu kwa wanachama hawa. Kwahiyo adhabu hiyo kwa sasa imemalizika, na wanachama hao wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao katika Chama.
Hata hivyo Kamati Kuu inawataka wanachama hawa na wale wengine wenye nia ya kugombea Urais kupitia CCM Kuzisoma , Kuziheshimu na Kuzizingatia Kanuni za Maadili za CCM na kanuni zingine zinazoongoza mchakato ndani ya Chama, ili wasikumbwe na adhabu itokanayo na kuzivunja kanuni hizo.
Wale wote wanaotaka kugombea, yaani waliokuwa kwenye adhabu na wengine watakaojiingiza kwenye kampeni mapema na hivyo kukiuka maadili na miiko ya Chama, taarifa za kukiuka kwao zitatumiwa wakati wa kuchuja majina ya wagombea utakapofika.
Taarifa hizo zitatumika katika kuwapima na kuamua iwapo wana sifa za kutosha na wanafaa au hawafai katika kupata uteuzi wa nafasi wanayoiomba.

Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
22/05/2015

Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity

RAIS PIERE NKURUNZINZA, PAMBANA


Na Happiness Katabazi

MEI 13 mwaka huu, Jenerali wa zamani wa Jeshi la Burundi,Godefroid Niyombare alitangaza kumpindua Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunzinza ' Handsome Boy'.

Lakini muda mfupi baada ya kutangaza mapinduzi hayo, wanajeshi watiifu wa jeshi hilo walipambana na kuakikisha serikali ya Rais Nkurunzinza inaendelea kuwepo madarakani na inasemekana  Mtangazaji huyo wa mapinduzi Niyombare kutokomea kusikojulikana.

Awali ya yote natoa pole kwa wananchi wa Burundi kwa adha wanayoipata kutokana na machafuko ambayo haswa yanachochewa na watu wasiyo na mapenzi mema na Burundi,uchu wa madaraka na wasiotaka kuheshimu utawala wa Sheria na Demokrasia  nchini Burundi. Walaaniwe.

Nina haki ya kujadili matukio ya uvunjifu wa amani na sheria yanayofanywa na baadhi ya Wananchi wa Burundi kwasababu Burundi ni miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo pia sisi Tanzania ni mwanachama.

Hivyo madhara ya vitendo vya uvunjwaji wa sheria , Katiba yanatia doa Juimuiya ya EAC mbele ya uso wa dunia, pia Tanzania inajikuta nayo inapokea wakimbizi kutoka Burundi na nadhara mengine mengi wakati kama wananchi hao  wasingejihusisha na vitendo vya kuvunja sheria madhara hayo yasingetokea.

Nyie wananchi wa Burundi ambao mmejazwa ujinga na wapinzani mkaamua   kuingia mtaani kufanya vurugu kwanini   hamkujiulizi kwanza hao viongozi wa vyama vya upinzani vinavyowashawishi mfanye vurugu,wake na watoto wao mbona hamuungani nao mtaani kufanya vurugu na wote joto la mkondo wa sheria?

Burundi ni  taifa huru ambalo wananchi wake wameamua taifa hilo liongozwe kwa Katiba na Sheria.Na Katiba ndiyo sheria Mama.

Imeripotiwa kuwa Katiba ya Burundi inasema Rais wa Burundi atatakiwa kushika nafasi ya kiti cha urais kwa mihula mihili tu.

Katiba hiyo haitambui kipindi cha mpito.Nkurunzinza amechaguliwa mara moja tu kuwa rais wa Burundu katika uchaguzi mkuu wa kwanza uliofanyika miaka mitano iliyopita na kipindi hicho kinatambulika na Katiba ya nchi hiyo.

Kipindi cha kwanza Nkurunzinza aliingia kushika wadhifa wa rais kwa kuidhinishwa na bunge kwa kipindi cha mpito hivyo ,hakuchaguliwa katika uchaguzi mkuu .

Na Mahakama Kuu ya Burundi hivi karibuni ilitoa tafsiri yake ya kisheria na kusema Nkurunzinza ana haki Kitiba kugombea tena urais na endapo atagombea urais atakuwa hajavunja Katiba ya nchi.

Na hadi sasa uamuzi huo wa Mahakama Kuu ya Burundi haujatenguliwa na Mahakama ya Rufaa ya nchi hiyo.Hivyo bado ni uamuzi halali.

Na chama anachokiongoza Nkurunzinza   cha     hivi karibuni kilimruhusu agombee tena urais kwa muhura wa pili kupitia tiketi ya chama chao.

Kwa maana hiyo hoja ya kwamba Nkurunzinza  hatakiwi na wana Burundi wote siyo ya kweli ni hoja mfu maana kama hatawiki chama chake ndio chama tawala na kina wananchi wengi sasa inakuwaje leo hii watu wachache wadai watu wengi hawamuingi mkono.

Na hoja ya kwamba wananchi wa Burundi wamekufa katika machafuko yale kwa sababu eti Nkurunzinza hataki kutoka madarakani,ni hoja isiyo na mashiko kwani marehemu wale walivyokuwa hai wasingeshiriki vitendo vya kuvunja sheria vya kuingia mitaani na kufanya vurugu na kukaidi amri ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikiwataka watawanyike ,umauti,ulemavu usingewakuta kwani wale wananchi wa Burundi ambao walikataa kuingia mtaani hakuuwawa katika vurugu zile  wala kupata ulemavu.

Kama wana Burundi waliamua taifa lao liongozwe kwa Katiba na Sheria, kwanini sasa hawataki kuheshimu uamuzi wa  Mahakama Kuu ya Burundi ambayo ilitoa uamuzi wake hivi Karibuni na  kusema Nkurunzinza hajavunja Katiba ya Burundi?

Maana Mahakama ndio chombo pekee cha kutoa haki na kutafsiri sheria na Mahakama Kuu ya Burundi ilishatoa tafsiri kuhusu je kipindi cha mpito kinatambulika Katika Katiba ya Burundi ,ikasema hakitambuliki.

Kikubwa zaidi hatusikia wakazi wa Burundi wakilalamika Nkurunzinza ameshindwa kuwaletea maendeleo , kila kukicha tunawasikia wakilalamika  Nkurunzinza amevunja Katiba tena wameanza kulalamika hilo baada ya kusikia chama cha Nkurunzinza kimempitisha tena kugombea nafasi ya urais ?

Halafu kama sio nongwa na choyo ni kitu gani? Kama kweli nyie baadhi ya watu wa Burundi hammtaki Nkurunzinza si msubiri siku ya tarehe ya kupiga kura katika Uchaguzi  Mkuu wa nchi yenu, ndiyo mmpigie kura nyingi za hapa ili ashindwe kutetea nafasi ya kiti cha urais?

Mnafikiri vurugu ni njia sahihi na nzuri?Binafsi mimi ni muumini wa amani na sheria na nilitangaza  maslahi yangu tangu wiki mbili zilizopita kuwa napinga vitendo vya uvunjwaji wa sheria na vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wa Burundi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Haya jaribio la kumpindua Rais Nkurunzinza limekwama, nyie wananchi mliokuwa mkijitanguliza mstari wa mbele kuingia mtaani kushiriki vitendo vya uvunjwaji wa sheria vya kushinikiza rais wenu atoke madarakani leo hii sura zenu mtaziweka wapi?

Maana yule Meja Jenerali Niyombare  aliyetimuliwa kazi na Nkurunzinza Februali mwaka huu,ambaye juzi alitangaza mapinduzi ameishatokomea kusikojulikana,  Nkurunzinza ndiyo katuna pale Ikulu mnafikiri nini kitawakuta nyie wote mlioshiriki wazi na kwa  siri kuanzisha machafuko kwa siku kadhaa hapo Burundi ?

Na ninatoa rai kwa baadhi Watanzania tena wengine ni viongozi wa vyama vya upinzani ambao walikuwa wakiunga mkono vitendo vya kihuni hadharani wengine ndani ya Bunge akiwemo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema ambaye jana bungeni bila aibu alizungumza ndani ya bunge kuwa anawapongeza wananchi wa Burundi kwa kumpindua rais wao  hali iliyosababisha Mwenyekiti wa Bunge,Idd Azzan Zungu kumtaka asindelee kuzungumzia mambo hayo.

Vitendo vya uvunjifu wa sheria mitaani  vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya wananchi kuwa Burundi, waache hiyo tabia kwasababu hao wanaojifanya wanawaunga mkono wananchi wa Burundi ni wazandiki na  majuha.

Nasema ni wanafki kwasababu kama wanawapongeza kwa kutenda vitendo vile vya kidharimu kwanini huyo Lema na hao Watanzania wanaowaunga mkono wananchi wale ambao miongoni mwao hivi sasa wapo mikononi mwa vyombo vya dola na wengine wamekimbia kwanini hawaendi Burundi au  kule kule Kigoma kwenda kuwapa misaaada?

Wakazi wa Burundi sijui kwanini hamtaki kujifunza kuwa vita hainaga  macho na kwamba vita hii mnayoitaka miaka ya nyuma iliwaletea madhara makubwa sana?

Burundi ilishakumbwa na vita mkapoteza wapendwa wenu alipoingia Nkurunzinza kwa kipindi chake chote hicho hakuna vita iliyotokea ila sijui mmnaamu vita tena irudi nchink kwenu?

Acheni ujinga huo wakutumiwa ovyo ovyo na baadhi watu wenye uchu wa  madaraka na wenye dhamira mbaya na husuda na Burundi.

Na mtambue sio kila ushauri unaotolewa na wananchi kwa rais wao ,rais halazimiki kuufuta wala kuuzingatia kama ushauri huo auzingatii matakwa ya Katiba na sheria ya taifa husika.

Mfano mzuri ni Ibara ya 37(1) ya  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1979 , inasomeka hivi ;

   "37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba
hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na
shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata
ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale
anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya
jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka
yoyote.".

Kwa minajiri ya Ibara hiyo tunaona kuwa Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa  na mtu yeyote,isipokuwa tu pale  anapotakiwa na Katiba au sheria nyingine yoyote  kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na  mtu au mamlaka yoyote.

Na nina imani viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hawatakubali kuona machafuko yanaendelea nchini Burundi,watatumia njia za kidemokrasia na njia nyingine za siri kuakikisha Burundi inakaa sawa na wahuni wanashughulikiwa haraka.

Na leo Rais Nkurunzinza amewasili nchini Burundi akitokea Tanzania na amepokelewa shangwe na nderemo na maelfu ya wafuasi wake.Yupo Ikulu anachapakazi na walioshiriki kufanya mapinduzi baadhi yao wamekamatwa na watafikishwa kwenye vyombo vya dola.

Niitimishe kwa kumpa pole Nkurunzinza kwa niaba ya taifa lake kwa changamoto inazopitia ninaimani Mungu atalivusha salama taifa la Burundi na mtendeneane haki kwa mujibu wa sheria na sio misukumo ya uchu wa madaraka wa kutaka madaraka kwa njia haramu ambazo wana Afrika  Mashariki hatutaki wananchi wenzetu kutoka katika nchi zinazounda Jumuiya ya EAC watumie njia za mapinduzi kuingia madarakani.

Jumuiya ya  EAC bado ni changa ukilinganisha na Jumuiya za  mataifa mengine makubwa duniani,hivyo bado tunaitaji kuwa na Jumuiya imara ambayo moja ya nchi yake hatutairuhusu kirahisi kiingie kwenye vita kwani njia za kidiplomasia za kusuluhisha migogoro zipo na Wanadiplomasia wazuri tu wapo katika EAC na historia inaonyesha Wanadiplomasia hao wameishawahi kusuluhisha  migogoro katika baadhi ya nchi ikiwemo  mgogoro nchini Kenya inayotokea nyakati za uchaguzi ambao ni  Rais Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na wengine.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494

Mei 15 mwaka 2015.

LUSINDE 'AICHANA' UKAWA BUNGENI LEO


" NI kweli serikali ya CCM imechoka kwasababu imefanyakazi kubwa sana ya kujenga barabara,mahospitali,madaraja,kuleta maendeleo kwa taifa.

Hata gari likitembea umbali mrefu linachoka linaitaji kufanyiwa sevisi halafu linaendelea na safari. 

Kwani hata gari la Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe na Tundu Lissu magari yakitembea umbali mrefu yakichoka  hawayatupi wanachokifanya ni kuyafanyia sevisi kisha magari hayo yanaendelea na safari.

Ndio maana nakiri CCM imechoka kwasababu imefanyakazi nzito ya kuleta maendeleo katika nchi ni lazima ichoke ipumzike halafu ndio maana kwenye kampeni za Oktoba mwaka 2015 ,CCM itaomba tena ridhaa ya wananchi ili irudi kuendelea kufanyakazi kubwa zaidi.

UKAWA hawajachoka kwasababu haijafanyakazi ngumu ,UKAWA imekuwa ikifanyakazi nyepesi sana na kazi hiyo ina herufi sita tu ambayo ni kusimama na kusema neno hili(HAPANA). Sasa mtu ambaye ana kazi moja tu ya kusema neno HAPANA kama UKAWA na Chadema ni wazi hawawezi kuchoka maana hawajafanya kazi nzito.Kusema HAPANA kwa kila kitu siyo kazi nzito ndiyo maana UKAWA hawajachoka.

UKAWA wamekuwa wakisema CCM imechoka kwasababu imekaa muda mrefu madarakani, mimi na waambia hivi Chadema wakati mwingine wanajitukana wenyewe kwasababu Mzee Mtei , Dk.Wilbroad Slaa ni wazee lakini ndiyo wanaiongoza Chadema na UKAWA ndio wanamtegemea Slaa awe mgombea urais wakati Slaa ni mgombea urais mzee kuliko wagombea wote na amechoka.

Jamani  Ikulu sio wodi ya wagonjwa,Ikulu watu wanatakiwa kwenda kufanyakazi sio kulazwa.

Nasema sumu haionjwi , Ukawa ni sumu na watanzania sio wajinga hawapo tayari kuona sumu kwa kuiweka UKAWA madarakani kwanza UKAWA una sera gani  na ni chama kilichosajiliwa wapi na nani?

Maana hili Chama kichaguliwe lazima kiuze sera zake kwa wananchi,wananchi waulizeni Ilani na sera za UKAWA ni zipi maana hakuna chama kilichosajiliwa kinaitwa UKAWA?

CCM ukawa wasitutishe ,hawana wameishakwisha mapema na ninawaakikishia UKAWA mtashindwa vibaya katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

Eti Mbunge wa Iringa Mjini (Peter Msigwa), anasema CCM ya CCM ni hatari kwa usalama wa Taifa  kwasababu Hazina hailipi madeni ya makandarasi na serikali ina madeni makubwa sana .

Kwanza amenishangaza sana huyu Msigwa,anajifanya kushangaa madeni inayodaiwa serikali lakini anashindwa kujishangaa kwanza yeye binafsi maana na yeye ana madeni alikopa hapa bungeni.

Mbona hashangai madeni tunayodaiwa sisi wabunge humu ndani maana kuna wabunge humu ndani tulikopa mikopo zaidi ya Sh.Milioni 200".

Maneno hayo ni miongoni mwa maneno yaliyozungumzwa na Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM), Livingstone Lusinde wakati akichangia hoja zake katika Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu ,leo saa sita mchana,Mei 13 mwaka 2015.

Nampenda sana Lusinde kwa ubunifu wake wa maneno na kupambana na mahasimu wa kisiasa wa chama chake cha CCM na kupigania maendeleo ya wananchi.

Mungu ampe maisha marefu na afya njema ana arudi tena bunge lijalo aendeleze kazi aliyoianza katika Jimbo la Mtera.

Imendaliwa na Happiness Katabazi, Mei 13  mwaka 2015.
0716 774494
Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com

HIVI DAVID KAFULILA NI MZIMA KWELI?





Na Happiness Katabazi

MEI 11 mwaka huu, katika kipindi 45 kinachorushwa na Televisheni ya ITV alihojiwa Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara, David Kafulila ambapo alizungumzima mambo mbali mbali likiwemo suala la akaunti ya Tegeta Escrow.

Mbali na kuhojiwa katika kipindi hicho pia katika taarifa ya habari  ya ITV , Kafulila alihutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alisema akubaliani na ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za kashfa ya sakata la Escrow iliyotolewa Mei 8 mwaka huu na Katibu Mkuu Kiongozi ,Balozi Ombeni Sefue ambayo ilimuona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospiter Muhongo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi kuwa hawana hatia.

Kafulila kupitia taarifa ya habari hiyo akiwajaza ujinga wakazi wa Shinyanga ambapo alisema hakubaliani na taarifa hiyo ya Ikulu na kwamba taarifa hiyo imewasafisha vigogo hao ambao hawakustahili kusafishwa na kwamba anaenda kulianzisha upya bungeni jambo hilo la Escrow kwasababu eti pia kwenye Escrow kuna nyaraka zilizoghushiwa na serikali iwataje waliokula fedha za Escrow kupitia benki ya Stanbic.

Katika kipindi DK 45 , baadhi ya mambo aliyoyazungumza alizungumzia pia  suala la Escrow kwamba linahusisha vigogo wengi  na serikali kwakuwa haina utawala bora haijawashughulikia ipasavyo vigogo hao na kwamba suala la Escrow lilisababisha shilingi kuporomoka na kuwa kuna nyaraka za serikali zilighulishiwa ili wapate fedha za Escrow na cha ajabu mtoaji rushwa kwa maofisa hao wa serikali, mahakama   na mtoaji rushwa James Lugemalira  hajakamatwa.

Itakumbukwa kuwa Bunge liloketi mwishoni mwa mwaka jana ndio lilofunga mjadala wa sakata la Escrow baada ya kutoa maazimio yaliyotokana na uchunguzi uliofanywa na Kamati ya PAC iliyokuwa ikiongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA),Zitto Kabwe  ambaye alijizulu nafasi ya uenyekiti wa PAC na ubunge baada ya kufukuzwa uanachama na chama chake cha awali cha Chadema.

Katika makala yangu ya Mei 10 mwaka huu, iloyokuwa na kichwa cha habari kisemacho: ( ZITTO,KAFULILA NA WAZANDIKI WENZENU MMESHUSHUKA  SHUU!!!)

Moja ya aya makala hiyo niliaidi kuwa sitaacha Kafulila aendelee kuzungumzia suala la Escrow ndivyo sivyo na kwamba nitatumia karamu yangu kumhoji hivyo na leo tena nimetumia kalamu yangu kumhoji Kafulila kuhusu mambo ya Escrow aliyoyajadili jana.

Itakumbukwa pia Kafulila wakati alipokuwa mwanachama wa Chadema, wakati akiwa Chadema na kudaiwa kuleta chokochoko, Katibu Mkuu wa Chadema,Dk.Wilbroad Slaa alipohojiwa na vyombo vya habari kuhusu taarifa za Kafulila kuleta chokochoko ,Slaa alimfananisha Kafulila na sisimizi lakini pia wakati sakata la Escrow limeshika kasi aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema ambaye alijiuzulu kwa kile alichokieleza kuwa ushauri wake umeeleweka vibaya alimfananisha Kafulila na Tumbili.Werema na Slaa walikuwa na sababu za kumpachika  majina hayo ambayo hayapendezi.

Katika sakata la Escrow , Kafulila alikuwa ni mtoa taarifa tu, Kamati ya PAC ikafanyia kazi taarifa yake na ikasoma bungeni matokeo ya uchunguzi wake na bunge liliibuka na maazimio yake ambayo iliitaka serikali iyafanyie kazi.

Na kweli serikali kupitia vyombo vyake vikaanza kufanyia kazi ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), ikawafikisha mahakamani baadhi ya maofisa wa serikali kwa makosa ya kupokea rushwa tu  kutoka kwa James  Lugemalila na kesi hizo zinaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.

Pia watuhumiwa wengine ambao makosa yao hayaangukii katika jinai ,yameangukia katika makosa ya ukiukwaji wa maadili ya watumishi wa umma,wamefunguliwa mashauri katika Tume ya Sekretarieti ya Maadili ambao ni Professa Anna Tibaijuka, Andrew Chenge, Mnikulu  Shabani Gurumo na bado mashauri yao hayajatolewa weuamuzi.

Katika kuonyesha serikali imeyafanyia kazi kwa vitendo maazimio yale ya bunge ,pia ilimsimamisha kazi Maswi ili kupisha uchunguzi, Rais alimtimua kazi aliyekuwa Waziri wa Ardhi na Makazi Professa Tibaijuka , Muhongo alijiuzulu wadhifa wake na pia ikaunda timu ya kuchunguza tuhuma kama Profesa Muhongo,Maswi wanahusika  au la.

Ripoti ya uchunguzi iliyoyolewa na Mei 8 mwaka huu na Balozi Sefue imesema uchunguzi umebaini Muhongo na Maswi ni watu safi kwani hakuna ushahidi ulionyesha walishiriki kutenda makosa ya jinai au utovu wa maadili katika sakata la Escrow.

Hivyo  wapo huru na siyo mafisadi wa Escrow kama tulivyoamishwa na Kafulila,Zitto na wazushi wengine.

Kwa kuwa serikali imeishatekeleza maazimio ya bunge kwa sehemu kubwa,iweje leo hii suala la Escrow ambalo limeishamalizika, Kafulila ambaye alikuwa ni mtoa taarifa tu aibuke kwenye majukwaa ajiapize kuanzisha upya sakala la Escrow?

Inakuwaje tena Kafulila aibuke aseme kwenye Escrow kulikuwa na nyaraka zilizoghushiwa?

Kuonyesha Kafulila hivi sasa ni kama mtu aliyechanganyikiwa anapanda majukwaani na kufunga safari hadi kwenye TV kwenda kusema eti nyaraka zilighushiwa bila kuonyesha nyaraka hizo anazodai zimegushiwa.

Hilo suala la kughulishi ulilitolea taarifa katika vyombo husika?Kama ulilitolea taarifa mbona katika maazimio ya Bunge hatukusikia kuwa uchunguzi wao ulibaini nyaraka za serikali zilighushiwa  na vigogo wa serikai ili wapate fedha za Escrow?

Uchunguzi uliofanywa na Takukuru,Polisi,CAG haujabaini kuwepo makosa ya nyaraka za serikali kughushiwa ndiyo maana hakuna aliyeshitakiwa kwa makosa ya kughushi, wizi na ndiyo maana nasema nanitaendelea kusema wewe,Zitto na wazandiki wenzenu ni mlizushia watu na kuwaundia makosa ya wizi wakati hakuna makosa ya wizi waliyoyatenda.

Chombo chenye mamlaka ya kuchunguza na kuthibitisha kuwa nyaraka fulani imeghushiwa ni kitengo cha utambuzi wa Maandishi na ofisi yake ipo chini ya ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai(DCI) ,pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam.

Tumuulize huyu Kafulila hayo mamlaka ya kuthibitisha nyaraka za Escrow eti zilighushiwa ameyapata wapi?

Maana hakuna mamlaka yoyote wala mtu yoyote yenye mamlaka ya kuthibitisha eti nyaraka fulani imeghushiwa au laa isipokuwa Kitengo hicho cha Utambuzi wa Maandishi kilichopo ndani ya Jeshi la Polisi(Forensque Bureu).

Labda mwenye ubongo wa sisimizi ndio anaweza kujitapata anayo mamlaka hayo ya kusema nyaraka fulani imeghushiwa wakati akijua hana mamlaka hayo.

Kuhusu hoja ya Kafulila jana kuwa serikali hii haina utawala bora; binafsi niliposikiliza jana kwenye Televisheni ,kwanza kauli yake ya kuiomba serikali iwataje majina ya vigogo waliochukuwa fedha za Escrow kwa kutumia Benki ya Stanbic ni wazi anaimani na serikali kuwa inauwezo wa kufanyakazi na ina utawala bora isipokokuwa ujinga wake ndio unamfanya aongee maneno ambayo ni hayawani anaweza kuyaongea ya kusema serikali haina utawala bora.

 Kama serikali haina utawala bora kitu gani kinakuwasha wewe Kafulila uombe serikali iwataje kwa majina vigogo unaodai waliiba fedha za Escrow kwa kutumia akaunti ya E
scrow?

Jana katika  kipindi Dk.45 jana, alitambulishwa kama Waziri Kivuli  wa Wizara ya Viwanda na Biashara.Katika mahojiano yake kwa wale tuliyoyafuatilia mwanzo hadi mwisho Kafulila hakuzungumzia mambo mengi yanayohusika na Wizara yake.

Mengi sana amenzungumzia mambo yanayohusu wizara za wenzie mfano sakata la Escrow linaangukia Wizara ya Nishati na Madini, suala la Mabehewa linaangukia wizara ya Uchukuzi.

Je alienda kuhojiwa kwaajili ya kuwafulaisha Tembo waliomtuma  maana yeye Dk.Slaa alimpachika jina la Sisizimi? Ameumbuka kwani ndio alienda kuvurunda kabisa.Kafulila umefirisika kisera na kimkakati .

Na hayo uyalopokayo ni miongoni mwa tabia aliyonayo Sisimizi.

Maana Sisimizi anaweza kuingia kwenye Gunzi  la Mahindi  au mfupa  akalamba ,gunzi na mfupa huo ukikauka sisimizi huyo uondoka kesho yake anasahau kama jana alililamba lile gunzi na mfupa  anarudi kulamba katika gunzi na mfupa ule alioulamba jana ukakauka akifikiri ni gunzi na mfupa mpya.

Sasa Kafulila  ametuambia anataka kuibuka upya   na sakata la Escrow wakati mamlaka husika zimeishamaliza suala la Escrow.

Ndio maana nauliza hivi Kafulila ni mzima kweli au amechanganyikiwa?

Inavyonekana sasa Kafulila  ubunge kwake ni Escrow.Uchaguzi mkuu ukikaribia utakuwa unaibuka na Escrow?Ndio kampeni zako hizo?umeishiwa huna hoja kijana.

Ni wazi sasa Kafulila akafanyiwe maombi na kupewa ushauri wa Kisaikolojia haraka maana huwezi kuwa Mbunge mwenye akili timamu ambaye unafahamu zana nzima ya mgawanyo wa madaraka(Separation of Power) , halafu ukaamua kujitokeza hadharani kuzungumza ujinga kama anaouzungumza Kafulila ambaye ni wazi sasa ajitambui kuwa yeye katika sakata hili alikuwa ni mtoa taarifa na alipotoa taarifa ina maana alikuwa anaimani zitafanyiwa kazi na vyombo hivyo vya dola sasa imefika zamu ya dola kufanyia kazi maazimio ya mhimili wa bunge ambako Kafulila ndiko anakotokea na ukatoa taarifa yake, Kafulila anapinga.Hivi huyu Kafulila ni Mzima kweli?

Mbona wakati bunge linafanyia kazi sakata la Escrow mbona mhimili wa serikali wala Mahakama haukiliingilia bunge?Hivi Kafulia ni Mzima kweli?

Kuhusu hoja ya Kafulila aliyoitoa jana kuwa ataanzisha upya sakata la Escrow Bungeni.Minamuuliza Kafulila hivi lile bunge ni la mjomba au bibi yake?

Bunge letu limeanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 62 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Hivyo bunge ni chombo kinachojiendesha kwa kanuni,sheria na taratibu.

Sasa katika Bunge lililoanza leo ,tayari bunge hilo limeishajipangia ratiba zake za kikao hicho sasa huyu Kafulila alivyosimama kule Shinyanga na kuwadanganya wakazi wa Shinyanga eti ataenda kulianzisha sakata la Escrow bungeni wakati ratiba iliyotolewa na Bunge mwishoni mwa wiki haionyeshi mahali popote kuwa bunge hilo limetenga nafasi kwa Kafulila ili awasilishe hoja mpya ya Escrow .

Ratiba ya kikao cha Bunge hili imesema wazi hili ni bunge la Bajeti siyo bunge la kujadili Escrow.

Wakazi wa Shinyanga mlipaswa mmsute Kafulila kwa kutumia ratiba hiyo ya bunge ni wazi Kafulila angekoma kuendelea kuwadanganya na kwa kifupi hana hayo mamlaka ya kufufua upya sakata la Escrow kwasababu tayari sakata hilo limeishafanyiwa kazi na sisi wasomi wa sheria tunasema mtu hawezi kushitakiwa mara mbili kwa makosa yale yale ambayo yameishatolewa uamuzi(Res Judicater ).

Ni wazi Kafulila ni mbumbumbu wa sheria na wananchi wa Jimbo la Kigoma Kusini kwa vitendo hivi unavyofanya binafsi sioni tena kama wanasababu ya kukuamini tena uendelee kuwa Mbunge wao .

Mbaya  zaidi bunge hili ni bungela Bajeti  siyo bunge la akaunti ya Tegeta Escrow  na  kuna dalili za wazi kabisa hili ni bunge  la mwisho kwako.

Nakutakia maisha mema uraini,karibu sana uraini,kule uraini Kigoma Kusini kuna Migebuka na Mawese hakuna nyama choma kama  Chakonichako Bar iliyopo Dodoma.

Kafulila  ni wazi bado unaota ndoto za Escrow,ukilala ukiamkia unaota ndoto kuhusu Escrow, basi nenda kaonane na wakazi wa eneo la Tegeta wakupe eneo ujenge nyumba ili uishi hapo Tegeta ambako kutwa unataja Tegeta,Tegeta,Tegeta.

Ukurasa wa Escrow umefungwa na mamlaka husika ,PAC iliitimisha bungeni suala la Escrow,serikali imeshafanyiakazia sasa kuanza kuzungumzia tena jambo hilo ni kuwadharau wabunge wenzio ambao uliwaamini sana  na bunge kwa ujumla  likafanyakazi yake na PAC ikatoa ripoti yake.

Unaonekana sasa unapenda sana kupewa medani(Tuzo) zilizotengenezwa  na Sufulia (Shaba).Maana hao wanaharakati wenzio walikupa tuzo ya kufanikisha Escrow kwa pupa bila kusubiri kwanza  ripoti ya uchunguzi ya Ikulu ambayo imemuona Maswi na  Muhongo hawana hatia.

Kama unapenda sana kupewa medani nakushauri anachana na medani  ya sufulia (Shaba) nenda kasake  medani  za dhahabu kwa kushindana na mkimbiaji bingwa duniani wa riadha wa mbio fupi  ,Bolt  wa  nchini Jamaica  ili utunukiwe medani ya dhahabu .

Maana medani ile ya Shaba(Sufulia) uliyopewa na wanaharakati ambayo imepewa jina huku mitaani kuwa ni "Medani ya wajinga Duniani.

Hivi wewe Kafulila hiyo medani ya Shaba(sufulia) sijui ilitengenezwa pale Gerezani au Makoroboi mkoani Mwanza uliyopewa ,Hivi ulishawahi kujiuliza taasisi hiyo ilishawahi kumtunikiaga nani tuzo kama hiyo ambayo sasa inaonekana inakupa kiwewe?

Niitimishe kwa kumshauri kijana mwenzangu Kafulila acha kuchekesha walionuna, ajitambue ana mke na wakwe.

Sasa inapotokea leo hii unazungumza mambo hayo ya Escrow ambapo sisi wasomi wa sheria na wajuzi wa mambo tunamuona ni kama mtu aliyechanganyikiwa na hivyo heshima yako kushuka mbele ya watu wanaofikiri sawasawa.

Kafulila acha kudanganya umma, kisheria huna mamlaka ya kuanzisha upya sakata la Escrow, huna hayo mamlaka zaidi zaidi unachokifanya ni kujitutumua mbele ya  umma ambao wengine tunaofahamu huna mamlaka hayo tunaokuona ni mtu uliyokumbwa na kiwewe na kiwewe hicho kimesababishwa na ripoti ya Ikulu iliyomuona Professa Muhongo na Maswi hawana hatia.

Kafulila acha kudanganya umma na kufanya umma wa Tanzania wote hauna akili timamu,uzushi wako huo wa kuzusha uongo kipindi kile kuwa fedha za Escrow zimeibwa na vigogo wa Escrow ,zimeleta madhara makubwa kwa taifa kwani huo mdomo wako unaoendelea kuuchonga kama Samaki aina ya Chuchungi ndio ulisababisha wafadhili wasuse kutoa misaada na hivyo kuwa ni moja ya sababu ya shilingi kuporomoka na matokeo yake upatikanaji wa fedha kwa wananchi kumekuwa kugumu.

Hivi Kafulila unachokitafuta hasa ni kitu gani? Naona kuna kitu ambacho wewe unakijua sirini  unakitafuta basi hicho unachokitafuta kwa bidii hivi ipo siku utakipata.

Maana hata ukiendelee kulalama mithili ya mtu anayetaka kukata roho ,huna mamlaka ya kutengua uamuzi uliotolewa na Ikulu ambao ulimuona Muhongo na Maswi ambao uliwashupalia sana hawana hatia.Na pia huna mamlaka ya kuliamuru bunge lianze upya kushughulikia sakata la Escrow sasa ni vyema ufunge huo mdomo wako.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com

Facebook: Happy Katabazi
0716 774494

Mei 12 mwaka 2015.

ZITTO,KAFULILA NA WAZANDIKI WENZENU MMESHUSHUKA SHUUU!!



Na Happiness Katabazi
' GWIJI la muziki wa dansi Duniani, Koffi Olomide ' Mopao' , aliwahi kusema hivi hivi:'' Uongo unapanda lifti na ukweli unapanda ngazi'.

Koffi Olomide  alikuwa ana maanisha taarifa za uongo uwa tabia ya kusambaa haraka sana  na kwamba ukweli unachukua muda mrefu kufika yaani kujulikana  kwasababu ni kama mtu anayetumia lifti hufika haraka kule aendako na yule anayepanda ngazi kwa kutumia miguu uchelewa kufika kule aendako licha ni lazima atafika aendako .

Sisi watu wa Kabila la Wanyambo toka Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera tuna msemo usemao  hivi; "Kabambone, " ahemuka omu mbaga. 
Kwa tafsiri ya lugha ya Kiswahili manaake ni ; ' Atakaye kutamba hadharani ,aibu zake huanikwa juani.'.


Nimelazimika kutumia nukuu hiyo ya Koffi kwasababu Mwaka Jana Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Zitto Kabwe, Mbunge wa Njombe,Deo Filikunjombe na wabunge wengine wazushi walimzushia uongo aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliakim Maswi .

Kuwa ni wezi wameiba Fedha za Tegeta Escrow na kuwa  Fedha za Escrow ni Fedha za umma na kuwa viongozi hao wameziiba uzushi ambao uliaminiwa na watu wasiyopenda kufikiri na kufanya utafiti lakini watu wenye akili timamu na tunaopenda kufanya utafiti Kama Mimi niliipingana wazi wazi na Kamati ya Zitto na Kafulila na wale wote waliokuwa wakisema Fedha za Escrow ni mali za umma, na kwamba Muhongo na Maswi walioshiriki kuiba Fedha hizo na ushahidi Kuwa nilipinga uzushi na fitna zilizokuwa zimefanywa na wabunge ni makala mbalimbali .

 Desemba 23 Mwaka 2014 , Rais Jakaya Kikwete Katika mkutano wake na  wazee wa Dar es Salaam Katika hotuba yake alisema Fedha za Escrow Si mali ya umma na Kama siyo mali ya umma  hawezi  kuwashitaki kwa mashitka ya wizi wa fedha hizo Kama tulivyokuwa tumeaminishwa Ujinga na baadhi ya wabunge na Kamati ya Zitto na Kafulila Kuwa Fedha za Escrow ni mali ya umma na zimeibwa kwa Magunia watu waliotajwa kwenye ripoti ya PCA kwakutumia Benki ya Mkombozi mali ya Kanisa Katoliki.

Itakumbukwa pia Professa   Muhongo Katika hotuba yake wakati akijiuluzu  nafasi ya uwaziri wa Nishati na Madini alisema anajiuzulu   kwasababu ya fitna, majungu, Chuki za kisiasa na wafanyabiashara ila anaimani aliifanya Kazi yake kuitumikia taifa kwa uzalendo wa Hali ya juu na ipo siku ukweli utajulikana.Na ukweli imejulikana Juzi Kuwa waliozushiwa tuhuma zile na wanasiasa manyang'au.. Ni suala la muda tu, tuipe Mahakama nafasi ifanyekazi yake.


Baada ya Sakata la Escrow kushika kasi na wananchi Wengi wakajenga Chuki na viongozi hao na serikali kwa ujumla, Balozi Sefue alitangaza kumsimamisha Kazi Maswi ili kupisha uchunguzi, Muhongo na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema walijuzulu nafasi zao  huku wakiitwa ni mafisadi wa fedha za Escrow, Rais Jakaya Kikwete alimtimua Kazi aliyekuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mbunge William Ngeleja, Andrew Chenge walivuliwa madaraka yao katika CCM na kushitakiwa katika Sekretarieti ya Maadili ya Umma na hadi sasa bado chombo hicho hakijatoa uamuzi wake dhidi ya mashauri yao.

Baada ya viongozi Hao waliotuhumiwa Katika Sakata la Escrow kujiuzulu , Mtandao wa Watetezi  wa Haki za Binadamu unaunganisha asasi  za kiraia zinazotetea Haki za binadamu ( THIRD- Coalition), wakimpata Tuzo Kafulila na Kafulilia akasema hivi  " Naamini 'scandal'  ya Escrow itaiondoa CCM madarakani Kama Goldenburg ilivyoiondoa  KANUNI madarakani' alisema Kafulila.


Mei 8 Mwaka huu,  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitoa ripoti za uchunguzi kuhusu Maswi na Profesa Muhongo ambapo alisema baada ya Kamati ya Maadili ya Sekretarieti ya Umma kuwachunguza imebainika Maswi,Muhongo hawakuhusika Kutenda makosa ya jinai ,ukiukwaji wa Maadili Katika Sakata la Escrow hivyo hawana hatia.

Pia Sefue alitoa ripoti nyingine ya uchunguzi kuhusu Sakata la Operesheni  Tokomeza Ujangili ,Mawaziri wote waliojiuzulu kwa sakata hilo hawana hatia kwa kuwa waliwajibika kisiasa tu.Kisheria tunaita ( Ministerial Responsibility).


Mawaziri waliojiuzulu kutokana na Sakata la Tokomeza ni Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk.Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa Waziri wa Maliasili, Balozi  Khamisi Kagasheki, aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Chakula Dk.Mathayo David  na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Vuai Nahodha.

Sakata la Tokomeza lilivaliwa njuga na mbunge James Lembeli na wenzake.

Kabla sijaenda Mbali ,napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ( Baba Careen)  kwa kazi nzuri aliyoifanya yeye na timu yake ya uchunguzi ambayo ilichunguza tuhuma dhidi ya Muhongo na Maswi na mwisho wa siku juzi;

Balozi   Sefue alitoka  hadharani na kukata mzizi wa fitna na kutoa ripoti ya uchunguzi wa sakata la Escrow ambapo alisema timu yake ya uchunguzi imebaini Muhongo, Maswi hawana hatia ya jinai wala ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma .

 Umma uliaminishwa na wanaisiasa uchwara aina ya Zitto  na wazushi wenzake Kuwa maofisa hao wa serikali kuwa ni mafisadi wa Escrow na walinufaika na Fedha za Escrow na Fedha za Escrow na mali ya umma licha Muhongo alisema siyo Fedha za umma.

Sasa ni wazi tuhuma dhidi ya Muhongo na Maswi zilikuwa ni tuhuma   za kizushi na visasi vya kisiasa ,biashara na ambazo zilizushwa na wanasiasa uchwara yaani baadhi ya wabunge ambao walitumia Bunge letu kuendesha uzushi huo .

Hali iliyosababisha wananchi kuichukia serikali, CCM, na viongozi lakini hatimaye Juzi vyombo vya uchunguzi vya serikali vimewaona hawana hatia na ripoti hiyo ni wazi Kafulila, Zitto Kabwe na wazandiki wenzako mmeshushuka shuu.

 Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Mei 18 mwaka 2014, lilichapisha makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho ( KASHFA YA ESCROW  ISITUVURUGE).

Miongoni mwa haya za makala hiyo ni haya if upatapo hapa chini ; 
Tujifunze kutokana makosa, tusiwe wepesi kuamini   kila kitu kinachoibuliwa na baadhi ya wanasiasa wetu uchwara Kwani wengine ni Mavuvuzera wa wafanyabiashara, makampuni  na wanasiasa,na makuadi wa Makundi yanayoasimiana Katika magomvi Yao ama ya Kugombea Tenda Fulani, Biashara , urais Mwaka 2015  na kulipizana visasi vitendo ambavyo havina maslahi ya taifa zaidi ya kutaka kuvuruga umoja wetu.Tusiwape nafasi wahuni hawa.

Disemba  23 Mwaka 2014 nilichapisha makala yangu iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho ; (   WALIOMUITA PRO.MUHONGO NI MUHONGO KAMA JINA LAKE AIBU YAO).

Miongoni mwa haya zilizokuwa Katika Katika makala hii ni hizi hapa ; 

WALE wazushi,Visarata Mtaa,Washambenga,wenye nongwa Kama ndugu wa mume ambao Katika zogo la Escrow,walimu hukumu Waziri wa Nishati na Madini, Professa Sospiter Muhongo Kuwa ni Muhongo kama jina lake na kwamba ni fisadi wa Escrwo Leo hii wameziweka wapi sura zao? 


Licha ya Profesa Muhongo kutoa utetezi wake kupitia hotuba yake ndani Bunge ambapo pamoja na mambo mengine ,msomi Huyo alisema Fedha za Escrwo siyo za umma watu wakiwemo wanasiasa uchwara ambao ni wabunge walimpinga na kumuhukumu Kuwa ni Muongo mkubwa Kama jina lake na kwamba Fedha za a Escrow ni za umma. 

Lakini Jana Baba mwenye nyumba nyumba, Profesa Jakaya Kikwete katika hotuba yake alikubaliana na Muhongo Kuwa Fedha zile siyo za umma ni za IPTL na hazijaibwa wala Kubebwa kwa Magunia Kama Zitto Kabwe wakati akisoma ripoti ya PAC bungeni alisema Fedha za Escrow zilibebwa kwa Magunia bila kufuata Taratibu ya Sheria ya Benki Kuu. 

Waswahili wanamsemo wao usemao ' Mnafki hafi hadi ameumbuka'. Hivyo wanafki,Majaji mama DDP ,DCI ,majaji ,Mashushushu wa 'Kichina' ,mabush Lawyer ,wazushi na mahakimu uchwara ambao mlijipachika majukumu yasiyo ya kwenu ya kuhukumu Watu na kuwaita wakina Muhongo ni wezi ,wamekula Rushwa ,wamechota Fedha ya umma ya Escrow hotuba ya jana imewaumbua. 

Naendelea kusisitiza tuache tabia ya kuhukumu au kushabikia jambo wakati Hatuna vielelezo Vya kutosha Kwani tukae tukijua uzushi unaumuiza watu wasiyo na hatia Katika baadhi ya mambo machafu wasiyo yatenda. 

Leo hii kila kona watu wamepandikizwa chuki Mbaya sana ambapo baadhi ya wananchi ambao wao wakisikia jambo hawataki kilifanya utafiti wanaliamini, wanaamini Muhongo ni fisadi, kaiba Fedha za Escrow Kumbe ni uzushi tu unafanywa na wahuni wachache kwa Malengo Yao binafsi. 

PAC ilipotosha umma Katika ripoti yake ilisema Kiwango Cha Fedha kilichokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni Sh.Bilioni 306.7. Wakati ukweli ni kwamba kiasi kilichokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ni Bilioni 202.9. PAC ilisema Fedha za Escrow ni za umma, Rais amewaumbua amesema siyo za umma ni za IPTL. 

Mnaolazimisha kuwa fedha za Escrow ni za umma endeleeni kulazimisha, ila haitawasaidia maana tayari mjadala huo Baba mwenye nyumba yaani Rais Kikwete aliufunga mjadala huyo kwa kusema fedha za Escrow siyo za ummma. 

Waliomuita Profesa Muhongo ni Muhongo Kama jina lake kwasababu eti alisema Fedha za Escrow Si za umma, ni dhahiri shahiri hotuba ya jana imewaumbua. Mabingwa wa fitna kajipageni upya ili tukianza Mwaka mmoja 2015 muibuke na jungu jingine mAana shughuli kubwa mnayoifahamu ni kuwazushia wenzenu uongo. 

Binafsi naamini ipo siku ushauri wa kisheria uliotolewa na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji Werema utakuja kueleweka ,ni suala la muda. Mungu ibariki Tanzania. 

Disemba 12 Mwaka 2014 niliandika Makala yangu iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho ; (KIKWETE USIWASIKILIZE  'BUSH LAWYER' KATIKA ESCROW).

Baadhi ya haya zilizomo Katika makala hii nikimfuata zao; 

Sakata la Escrow  pamoja nalo limeibua au kuwezesha mambo mengi sana. Limekuwa kama mtego wa panya ambao waliokuwemo na wasiokuwemo wote wanaingia na baadhi ya watu wakauchukulia huu mwanya kutimiza  haja na matakwa yao ya kisiasa. 

Januari 24 Mwaka 2015, niliandika makala kupitia ukurasa wangu wa Facebook na Blogg yangu ya www.katabazihappy.blogspot.com. ,iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho ; (MUNGU AKULINDE  SOSPETER MUHONGO )

Baadhi ya haya za Makala hii ni hizi hapa ;

LEO  saa tano asubuhi,Januari 24 Mwaka 2015 , aliyekuwa  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alitangaza rasmi kujiuzulu nafasi hiyo ya uwaziri kwasababu ya zogo  la Escrow.

Tangu mwanzo kupitia makala yangu msimamo wangu niliweka wazi Kuwa naunga mkono Utendaji kazi wa Profesa Muhongo na hata Leo hii ninavyoandika makala hii sitabadilisha msimamo wangu Kuwa Kwangu Profesa Muhongo ni Miongoni mwa Mawaziri wa Nishati na Madini ambao nimewashuhudia Kuwa ni mawaziri ambao wameacha alama ya kukumbukwa.

Pia tangu mwanzo nilisema wazi kupitia makala zangu mbalimbali kwa jicho la Sheria Katika zogo la Escrow Hakuna Mashitaka ya wizi Kama baadhi ya watu walivyokuwa wakiwa hukumu Moja kwa Moja watu  waliotajwa kwenye zogo la Escrow Kuwa ni wezi na kwamba Fedha za Escrow zimeibwa.

Waswahili wanasema penye ukweli, uongo ujitenga. Hivyo ipo siku ukweli wa hili zogo la Escrow utakuja kujulikana nani muhasisi wake?  Kwanini waliliasisi zogo hili?,Muhongo alishiriki kwa kiasi gani Katika jambo Hilo?Ni kweli Katika Utawala wa Muhongo Wizara ya Nishati ilipata Hasara na kwamba Hakuna jambo lolote la maendeleo alilolifanya?

Nchi hii Ilipofika hivi sasa, majungu, fitna,ushirikina, uzandiki Ndio umetawala na umeshika hatamu.Watu wasiyo na hatia na siyo kwenye Nyanja za siasa tu wanaangamia kwa ushenzi huo.

Imekuwa nchi ya watu tunaopenda Ujinga Ujinga na uzushi halafu na mbaya zaidi tabia hizo zinafaywa na wanaume amba wanawake nyumbani eti tunajiaminisha nchi hii itapata maendeleo kwa haraka.

Hivyo Muhongo muachie Mungu, yeye ndiyo muweza wa yote, endelea kulitumikia taifa Lako kwa uaminifu ila kwa taadhari pia  Kwani Tulipofika sasa watendaji waaminifu na wachapakazi nchi hii HIvi sasa nikama hawatakiwi.


Narudia tena wale wote mabingwa wa kufanya binadamu wenzao kwa Lengo tu la kupata maslahi Fulani ikiwemo biashara, vyeo Mkae mkijua ipo siku Mungu atawaadhibu.

Kumbukeni hawa mnao wafanyakazi ufedhuli nao wana Mungu na Mungu wao wala siyo kipofu wala kiwete anayetembelea Magongo.Ipo siku Mtalipwa Ubaya mnaofanyia  wenzenu.Aminini  hivyo.

Mungu akutangulie Muhongo nenda kafanyekazi na wasomi wenzio achana na hawa wanaume 'wachambue Michele'  ambao wametawaliwa na husuda na fitna na unafki na vichwa vyao wanavitumia kwaajili ya Kufugia nywele badala ya kufikiri.

Pia niliandika na makala nyingine nyingi tu za Kusema Katika Sakata la Escrow kuna uzushi mwingi tuwe makini na nilichokiambulia kutoka kwa baadhi ya watu wenye akili za kipuuzi ni matusi ,vitisho na kuambiwa Mimi ni Kimada wa Profesa Muhongo wakati Si kweli.

Mungu si Athuman wala Juma, Ripoti za Balozi Sefue kuhusu Escrow zimethibitisha pasipo shaka  kuwa watuhumiwa wale yaani Muhongo, Maswi waliokuwa wakitajwa kwenye kashfa ya Escrow hawana hatia.

Sijui wale wanasiasa waliotuaminisha uongo ambao ulipandikiza chuki za wazi na taharuki katika jamii dhidi ya wananchi na Maswi na Muhongo sijui wanajisikiaje hivi sasa maana ni kama watu waliojisaidia bila kujitawaza.

Na wanasiasa ambao wengi wanajinsia ya kiume ambao ndiyo walikuwa wazushi wakubwa na vizabinazabina ,washambenga na wazushi walikuwa  wakiongozwa na Kafulila, Zitto,Filikunjombe, Ole Sendeka na wengine.

Itakumbukwa Sakata la Escrow lilivyopamba Moto wabunge Hao na wengine walikuwa ni watu wenye Mithili waliopandwa na Pepo mchafu wa kuwazushia watu uongo.

Bila haya wabunge Hao vijana kiumri waliuaminisha umma Kuwa Maswi, Muhongo ni mafisadi wa Escrow huku mioyoni mwao wakijua siyo kweli ila kwasababu roho wa kishetani alikuwa amewavaa alikuwa akiwatuma kuwashuhudia wenzao uongo mzito Kama ule kwasababu wanazozijua wao.

Lakini kuna Msemo usemao Mnafki hafi hadi ameumbuka. Sasa Zitto na wajumbe wake wa Kamati ya PAC, Kafulilia na wazushi wenzao bado wapo hadi hivyo siku hadi siku wanazidi Kuumbuka kwa unafki na uzandiki wao walioufanya Katika Escrow.

Aliyekuwa wa kwanza kuwaumbua ni Rais Kikwete Katika hotuba yake kwa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, ya Disemba 23 Mwaka 2014  ambapo pamoja mambo mengine Kikwete aliwaambu wazandiki hao Kuwa Fedha za Escrow siyo mali za umma, na Fedha za Escrow hazijaibwa Kama ilivyokuwa ikidaiwa na ' mashushushu wa Kichina' yaani Kamati ya PAC iliyokuwa ikiongozwa na Zitto.

Wa pili kuwaumbua mabingwa hao wa uzushi   ni Balozi Sefue , ambaye kupitia ripoti ya Sefue aliyoitoa kwa waandishi wa Habari kuhusu uchunguzi wa Sakata la Escrow ni kwamba uchunguzi umebaini Maswi, Professa Muhongo hawana hatia ya jinai wala Maadili kinyume na ilivyodaiwa na Kamati ya Bunge ya Bunge ya PAC iliyokuwa ikiongozwa na Zitto Kuwa walihusika na wana makosa ya jinai na walinufaika na Fedha za Escrow. 

Baada ya Balozi Sefue kutoa ripoti yake ,Kafulila Jana alinukuliwa  na Gazeti la Mtanzania akisema hivi ; " Uamuzi wa Ikulu  kumsafisha Maswi na Muhongo ulitarajiwa kwa Sababu ninao ushahidi  wa barua  unaonyesha  Ikulu kuhusika  Katika Sakata  hili  na Ndio  Sababu  Rais  Kuvuta miguu".

Wakati Kafulila akitaka Kuanza kuaminisha umma Ujinga wake huo wa kupinga vitu visivyopingika anasahau Ikulu hiyo hiyo iliruhurusu Mnikulu , Shabani Gurumo , Mbunge wa Jimbo la Sengerema,William Ngeleja , Andrew Chenge, Professa Tibaijuka  kushitakiwa Katika Sekretarieti ya Maadili na mashauri Yao yanaendelea.

Kafulila tulia unyolewe nywele Kwani hivi sasa wewe na wazushi wenzake Katika Escrow ni zamu yenu kuumbuliwa na ukumbuke Kuwa bado ile Kesi ya Madai ya kashfa ya Sh.  Bilioni 310 iliyofunguliwa na Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL)  kwa kushirikiana na kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited na Mwenyekiti Mtendaji   wa kampuni hizo, Harbinder Sigh Seth imemfungilia Kafulila kesi hiyo ya madai ya kashfa.


Katika kesi hiyo, walalamikaji kwa pamoja wanaiomba mahakama imwamuru Kafulila   awalipe fidia ya Sh.Bilioni 310   kwa madai ya kutoa kashfa dhidi yao kwa kuwatuhumu kujipatia fedha kutoka katika Akaunti ya Escrow, kwa njia zisizo halali na Kesi hiyo inaendelea na ipo siku itafikia Tamati kwa kufahamu Kafulila alisema kweli au aliizushia uongo kampuni hizo Kama alivyowazushia wakina Maswi na Muhongo.Tuvute subira.

Itakumbukwa Kuwa ni Kafulila huyu huyu kipindi kile alipozusha Sakata la Escrow ,Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema amesikia taarifa zake hizo kuhusu Escrow na Pinda akamwagiza Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) afanye uchunguzi wake Kama Fedha za serikali Katika Sakata Hilo la Escrow ziliibwa au zilitumika vibaya au hizo Fedha zilikuwa ni za umma.

Lakini Pinda baada ya kutoa agizo hilo kwa CAG  ,Kafulila huyu huyu aliibuka na kumdhalilisha Pinda Kuwa anataka kuficha ukweli kuhusu Escrow na anataka kuwalinda mafisadi wa Escrow  Hali iliyosababisha watu wenye akili timamu nikiwemo Mimi kuandika makala ya kumshambulia Kafulila na kumuonyesha ni jinsi gani asivyoheshimu Utawala wa Sheria na Kanuni,kwani Kafulila yeye Katika Escrow alikuwa ni Mtoa taarifa tu lakini ghafla akawaka kujitwika majukumu mengine ya Ujaji,upelelezi majukumu ambayo siyo yake.

Na siku Muhongo alipojiuzulu,Maswi aliposimamishwa Kazi,Tibaijuka alipofukuzwa Kazi na rais , huyu huyu Kafulila, Zitto na wenzake waliitokeza hadharani na kujisifia Kuwa wao ni wanasiasa wanaipenda  nchi Yao Kwani wamefanikisha kuibua tuhuma za ufisadi na kushikilia Bango hadi vigogo hao wakaondoshwa madarakani na Kafulila akapewa  Tuzo na akachekelea sana.

Juzi Balozi Sefue katoa ripoti ya uchunguzi wa Sakata la Escrow dhidi ya Muhongo na Maswi na Kusema Kuwa  hawana hatia, eti Kafulila kafufuka sijui katokea makaburi gani  anasema alitarajia Ikulu ingewasafisha sasa najiuliza Ikulu sikuhizi ni Maji,sabuni au dodoki maana vifaa hivyo ndiyo vinamsafisha Mtu aendapo bafuni kuoga.

Uwenda Kafulila Ana wazimu siyo bure. Kama Kafulila alitarajia  Ikulu ingewasafisha viongozi hao ni kitu gani kilimuwasha Kipindi kile hadi akashupalia lile  Sakata la Escrow? 

Ni kitu gani kilikutuma  ukapokee ile Tuzo uliyopewa na wanaharakati wale na wakati akipokea ile Tuzo akachekelea sana na kujitapa yeye ni mwanaume wa Shoka Kwani skendo aliyoibua imeweza kuwaondoa madarakani viongozi hao wa serikali na kwamba Sakata Hilo la Escrow eti itaiangusha serikali na CCM.

Kwa ripoti ya Balozi Sefue , ni wazi kabisa Taasisi iliyompa tuzo  Kafulila nayo imeumbuka Kwani ilifanya papara Kumpa Tuzo hiyo bila kusubiri taarifa ya Matokeo ya uchunguzi wa kashfa hiyo ilitolewa.

 Hiyo Tuzo  bora ukaitupe jalalani maana haina maana tena kwasababu ripoti ya uchunguzi ambayo ilifanya uchunguzi kwa mujibu wa sheria kwani chombo kilichofanywa uchunguzi kipo kwa mujibu wa sheria, kimebaini tuhuma zilizoibuliwa na Kafulila ni uzushi na zimeshindwa kuishawishi Timu ya uchunguzi imkute na hatia Muhongo na Maswi.

Namshauri  Kafulila ,Zitto hivi sasa wafunge   Midomo Yao   na Wakubali  Kuwa sasa ni zamu yako ya kuumbuliwa kwa uzushi wao  na sisi waandishi wachokonozi na wananchi tusiyopenda  uzushi hatutakubali tena kuendelea kuwavumilia kusikiliza uzushi wenu ambao umeligharimu taifa na kuwathiri watu wasiyo na hatia tutawaanika adharani na kuwashushua.

Tumechoka na vitendo Vya kizushi vinavyofanywa na wanasiasa wa aina yako ambao Inadaiwa Kabla ya Kuzusha Sakata fulani mnahongwa  kwanza Fedha na wafanyabiashara walionyimwa Tenda au Kuzuiwa mambo Yao na baadhi ya viongozi wa serikali wasiyotaka Rushwa na kuburuzwa na wafanyabiashara hao halafu nyie  baadhi ya wabunge uchwara mnamchukua ugomvi huo mnaingiza ndani ya Bunge na kuanza Kuzusha na kuchafua baadhi ya watendaji wa serikali na mawaziri na hii tabia ya kishenzi inayofanwa na wabunge washenzi washenzi imeota mizizi hapa nchini.

Na hotuba ya Rais Kikwete ya Disemba 23 Mwaka 2014, Ripoti ya uchunguzi ya Escrow iliyotolewa na Balozi Sefue hazina Ishara nzuri Katika hatima yako ya kushinda tena Kiti cha Ubunge Katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu na pia siyo Ishara nzuri Katika ile Kesi ya Madai inayokukabili pale Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Na ile Kesi ya kumtolea lugha ya matusi Mkuu wa Wilaya Kule Kigoma bado inakukabili. Tatizo Lako Kafulila hujui madhara ya kushitakiwa ndiyo mAana unaamua Kujitoa fahamu kufanya vitendo Vya kihayawani vinavyosabisha kushitakiwa .

Nakutuma nenda kwa Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustine Mrema, wakili Mabere Marando hata Tundu Lissu watakueleza madhara na Usumbufu,Kadhia waliyoipata wakati waliposhitakiwa Katika Kesi mbalimbali.

Lissu na umwamba wake aliposhinda Kesi ya kupinga Ubunge wake alilia Machozi nje ya Viwanja Vya Mahakama Kuu na kulaani waliokuwa wamemshitaki Kwani walikiwa wakimkera na kumsababishia Usumbufu.Sasa wewe bado unawashwa na ukae ukijua hizo Kesi zitakusumbua sana.

Kama ni watu wa Kupenda kujifunza basi Watanzania na wafadhili ambao ni mabingwa wa Kupenda kuhukumu watuhumiwa wa kashfa mbalimbali bila kusikiliza upande wa pili na kufanya utafiti mtakuwa mmejifunza sasa na kuacha kuamini harakahara tuhuma zinazoiburiwa na hawa wanasiasa wetu uchwara dhidi ya watendaji wa umma na wanasiasa wenzao.

Minilishajifunza  muda mrefu sana ndiyo maana hata katika  Sakata la escrow lilipoibuliwa nilitaadhalisha kwani  hawa wanasiasa Wengi wanatabia za uzushi sana na Chuki na kupitia ripoti ya Sefue, hotuba ya Kikwete ya Disemba 23 Mwaka 2014 .

Ripoti  ya uchunguzi kuhusu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo  ambaye nae alisimamishwa Kazi na Katibu Mkuu Kiongozi kufuatia azimio la Bunge lilomuusisha na Madai ya kutoa Rushwa wa Bunge ili Bajeti ya Wizara ipite lakini mwisho wa siku Katibu Mkuu Kiongozi baada ya Timu yake kufanya uchunguzi ikamuona Jairo Hana hatia.

Pia azimio la Bunge Mwaka 2008 lilivyoona eti kulikuwa na Rushwa Katika mkataba wa Richmond na hivyo kufanya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kujiuzulu na mawaziri wengine wa Nishati na Madini Nazir  Karamagi,  Msabaha kujiuzulu.

Lakini Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa inayoongozwa na Dk.Edward Hosea ilifanya uchunguzi kuhusu azimio Hilo la Bunge kuhusu mkataba wa Richmond na kubaini Hakuna Rushwa yoyote na wabunge hao akiwemo Waziri wa sasa Dk.Harrison Mwakyembe walishiriki kikamilifu kuipata matope TAKUKURU Kuwa inakumbatia mafisadi. Dhambi sana.

Waandishi wa Habari wenzangu wote wale waliokuwa wakitumiwa au kutumika vibaya kuchafua watu Katika Sakata la Escrow Ndio ripoti ya Balozi Sefue, hotuba ya Kikwete iwafunze na muache kutumiwa kuchafua watu wasiyonahatia maana hakuna ubishi kuwa baadhi ya vyombo vya habari vilitumika kikamilifu kuchafua Muhongo,Maswi katika sakata la Escrow na kulikuza jambo hilo.

Wosia wangu wa Zitto,Kafulila na wabunge wengine acheni tabia ya kujifanya Nyie ndiyo wabunge vijana mnaopenda kujitanguliza mstari wa Mbele Kudai mnakashfa dhidi ya wanasiasa wenzenu halafu mna wachafua wee na kuwaletea madhara hadi wanaamua kujiuzulu nyadhifa zao na wengine kusimamishwa Kazi na wengine kusababisha kupotea Katika ulingo wa siasa uzushi wenu.

Siwakatazi msiibue machafu ila Kabla ya kuyaibua akikisheni mnafanya hivyo mkiwa na nia safi  siyo nia ovu. Katika Sakata hili la Escrow tangu mwanzo ushahidi wa mazingira na mlituhumiwa wazi wazi Kuwa mlikuwa mkitumika vibaya Kuwaumiza kwa Niaba Mbaya Muhongo, Maswi kwasababu eti Maswi na Muhongo waliwataka kuendeshwa na mfanyabiashara mmoja  ambaye mfanyabiashara Huyo alikuwa akiwatuma ila baadhi ya wabunge,wanasiasa wengine na vyombo Vya Habari kuwapaka matope Muhongo,Maswi na serikali kwa ujumla Kuwa serikali ni ya kifisadi na haijali wafanyabiashara wazawa. 

Na Spika Anne Makinda baada ya Kamati ya PAC siku ile kumaliza kusoma mapendekezo yake ,mama huyo alisema hivi ' Nyie baadhi ya wabunge acheni kuwazushia wenzenu uongo na kwamba siku mtakapokamatwa na kuweka Rumande sitamsaidia Mtu maana kuna wengine mnatumiwa na wafanyabiashara huko nje magomvi yao mnayaamishia ndani ya bunge'. 

Taifa linalokuwa na aina ya wabunge wa aina hii ambao ni wazushi, Wapika majungu dhidi ya mawaziri wetu na watendaji wa serikali ni hatari sana.

Ndiyo maana siku zote Nawapongeza wale wote walitangulia Mbele za Haki ambao walioanzisha kitu SHERIA na UCHUNGUZI.

Hakuna ubishi Katika Sakata la Escrow Kama Wanasheria na wachunguzi ambao ni wanataaluma ya Sheria na wachunguzi wasinge shirikishwa kufanyakazi zao za kitaaluma Katika Sakata hili ni wazi Muhongo na Maswi Wangezidi kuzikwa wakiwa hai na wanasiasa hawa wenye hulka za mapakashume ambao haya taaluma ya uchunguzi na Sheria hawana  kwa uzushi na Chuki tu ambazo Hazina tija kwa taifa letu.

Mbunge mzima tena mwanaume yaani Zitto, Kafulila Mishipa ya fahamu ilikuwa ikiwasimama kuwazushia uongo Muhongo na Maswi huku wakijua ni uongo, ni hatari ya Mungu na ndiyo maana wanasiasa wamekuwa anaaminiki kwa Yale wanayoyasema kutokana na baadhi ya wanasiasa wenzao Kama hawa ambao wanazushia wenzao uongo na kuwaletea madhara makubwa kisaikolojia,kuwashushia heshima Katika Jamii na sehemu wanaofanya kazi .


Hivi mlifikiri ukweli hautokuja kujulikana? Na kwa Kuwa Zitto na Kafulila hamnaga aibu sidhani hata kama mmeshtushwa na ripoti hiyo ya Balozi Sefue ya kuwaona hawana hatia Maswi na Muhongo.

Na bado Mungu ataendelea kutumia watu wake hapa hapa Duniani kuwadhibu hasa wewe Zitto maana Tayari Mungu alilitumia  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kukuadhibu Kuitupilia Mbali Kesi yako dhidi ya Chadema ambayo ulikuwa umeomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia vikao Vya Chadema visikujadili.

Pia Mungu akatumia watu wake hapa hapa Duniani yaani Mwanasheria wa Chadema,Tindu Lissu na uongozi wa Chadema, kukutimua uanachama na ulivyotimuliwa uanachama ukajiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa PAC na ukajiuzulu nafasi ya Ubunge.

Ukaenda kuanzisha Chama cha ACT  ,kitendo ambacho sio Moja ya vipaumbele Vya Watanzania na ukajinasibu eti ipo siku utashika nafasi ya juu ya uongozi Katika taifa hili.

Watanzania tumeishakubaini tabia yako hivyo hatuitaji Kuwa na kiongozi mwenye tabia za kizushi kushika madaraka ya juu ya taifa hili maana atakitumbukiza taifa mtoni.

Yote hayo yanayokukuta ni malipo ya Mungu maana Mabaya uliyowatendea wenzako Hao ,wenzako walilia na Mungu wao na Mungu ndiyo anawalipia kwa kasi  na Ikulu ndiyo imeisha msafisha Maswi, Muhongo Kuwa hawana hatia lakini wewe hadi Leo Hakuna aliyetengua uamuzi wa kufukuzwa Kwao na Chadema unahesabika Kuwa ni Mwanachama aliyefukuzwa na Chadema kwa tabia chafu na kuvunja Katiba ya Chadema na tuhuma Usaliti.

Lakini wale wakina Muhongo, Maswi na wengine wao hawajafukuzwa vyama vyao, na wameonekana hawana hatia hivyo Zitto umeumbuka Kwani ulilolikusudia kwa watu hawa halijakuwa na bado utazidi Kuumbuka na kuchapwa bakora ya Mungu hadi utakapoungama dhambi hiyo maana watu Wengi sana walilia na kusikitika nakumshitakia Mungu ,Kwa uzushi mlimzushia Profesa Muhongo na Maswi ambao walikuwa wakichapakazi vizuri Katika Wizara ya Nishati na Madini.

Kilichokuwa kikiniuma Katika Sakata la Escrow Kuwa kuna watu Kama Maswi, Muhongo wanaangamizwa bila hatia kwasababu nilikuwa nafahamu fika kuna mchezo mchafu ndani ya Sakata Hilo na Mlengwa mkubwa alikuwa ni Muhongo na Maswi ambao wakikataa kuburuzwa na 'Bwana'  wa wanasiasa ambao machakubimbi .

Ni huyu huyu Zitto ,Kafulila na wanasiasa uchwara wenzao Mara kwa Mara wamekuwa wakilalama majukwaani na Kwenye vyombo Vya Habari Kuwa serikali inatumia Fedha za umma  vibaya   Kumbe wakati mwingine uzushi 
Wanaouzushaga Ndiyo  unasababisha serikali itumie Fedha kuunda Timu za uchunguzi kuchunguza ukweli    wa tuhuma za uzushi unaoanzishwagwa  na wanasiasa hao uchwara mahiri wa Kuzusha uongo Katika baadhi ya mambo wanayoyazusha Kwenye Escrow.

Hivi Zitto,Kafulila na wenzako uwa mtapataga  raha gani tena  mnavyo shiriki  kuangamiza wenzenu kwa kuwashuhudia uongo ili wafukuzwe kazi na kufikishwa Mahakamani ,kitendo ambacho ni wazi Zitto,Kafulila hamumuogopi  Mungu kabisa maana moja ya amri ya Mungu inakataza binadamu usimshuhudie mwenzio uongo.

Na pia Mungu alituagiza binadamu wote tu pendane.Lakini Kwa kitendo hiki cha uzushi  wewe Zitto ,Kafulila na wazushi wenzako katika  Escrow ambapo mlimzushia  uongo Muhongo na Maswi ni wazi mmepuuza   agizo la Mungu lilotutaka  kila mmoja ampende jirani yake Kama a navyopenda nafsi yake . 

Kama kweli mnatekeleza agizo Hilo la Mungu la Mpende jirani yako Kama unavyoipenda nafsi yako ,Zitto na PAC na wazushi wengine msingediriki kushupaza shingo kuwashuhudia uongo wakina Muhongo na Maswi Kama mlivyo wafanyia unyama ule.

Sasa hata Kama maagizo hayo ya Mungu na amri yake hiyo ya usimshuhudie mwenzio   uongo lakini mkapuuza amri hiyo ya Mungu  ,ni wazi Nyie ni watu anakuogopwa sana na sisi watu wa Mungu maana Kama mmediriki kupuuza maagizo ya Mungu aliyewaamba ndiyo mtaacha kupuuza maagizo yanayotolewa na binadamu wenzenu ?

Mngekuwa na upendo wa kweli kwa Muhongo,Maswi msingediriki kuwatendea ule unyama na ukatiri mliowatendea wa kuwazushia uongo mtakatifu Kama ule uliosababisha Muhongo, Maswi kuchukiwa na umma na kunuka bila hatia na kuachia nyadhifa zao.

Mara kwa mara kupitia mitandao ya kijamii nimekuwa nikisema dhambi aliyotendewa Muhongo,Maswi Katika Escrow itamtafuna Zitto na genge lake liloungana kutunga uzushi ule ambao uliwaletea madhara makubwa Maswi na Muhongo lakini kwakuwa ni majasiri na walikikabidhi jambo hili kwa Mungu na walijua hawana kosa walilotenda walikaa kimya na kuacha vyombo husika vifanye kazi yake na mwisho wa siku ukweli utabainika na kweli ukweli imebainika Kuwa Zitto na wazushi wenzake wakiwashushia uongozi kwa Sababu wanazozijua.Mtakuja kulaaniwa.

Sisi watu wa Kabila la Wanyambo toka Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera tuna msemo unasema   hivi;    "Kabambone, " ahemuka omu mbaga. 

Kwa tafsiri ya lugha ya Kiswahili manayake  ni ; ' Atakaye kutamba hadharani ,aibu zake huanikwa juani.'

Sasa Msemo huu unatufandisha  kwamba Zitto na wazandiki wenzake waliozusha Sakata la Escrow dhidi ya Profesa Muhongo na Maswi  awali wakati wakizusha Sakata Hilo walitamba sana hadharani lakini sasa aibu zao zimeanikwa juani na ripoti ya uchunguzi wa Balozi Sefue imeachwa uchi mchana kweupe Kamati ya PAC iliyokuwa ikiongozwa na Zitto, Filikunjombe  na muhasisi wa uzushi wa Escrow Kafulila na wazandiki wengine. 

Uwa najiuliza hivi Zitto,Kafulila na wazushi wenzake walinyonya kweli maziwa ya mama zao Miezi Tisa?Au walinyweshwa uji wa Muhogo badala ya kunyonya maziwa ya  Mama zao  ndio maana  wanatabia hizi  za uzushi uzushi?

Wakati mwingine uwa najiuliza ya wanaume hawa wazushi sijui wa naishije na wake zao majumbani?

Aipendezi kabisa mwanaume tena Ana ndevu anavaa suruali na Kufunga Mkanda kiunoni kusifika kuwa na tabia za kizandiki kama hizi za kizushi na kuwashuhudia binadamu  wenzenu uongo na  mzushi kwa maslahi yenu binafsi.

Nasielewi  hawa wanasiasa wazushi wa Escrow wanaishi vipi na wake zao majumbani  Maana mwanaume kuwa  na tabia chafu Kama hii ya uzushi tena kuzushia uongo watu waliowazidi  umri Kama Professa Muhongo,Maswi ni wazi hawa wanasiasa vijana wana matatizo   makubwa na wasiyo acha hiyo tabia ya uzushi watalaaniwa.

Biblia inatuambia Kuwa Shetani ni Baba wa uongo, hivyo wale wote walimzushia uongo Profesa Muhongo, Maswi  kuwa walipata mgao wa fedha za Escrow wakati ni uongo baba Yao ni shetani na wao ni mashetani maana Mtoto wa Mungu azungumzi wala kumshuhudia jirani yake uongo lakini Ituo,Kafulila na wazandiki wenzao waliwashuhudia majirani zao yaani (Maswi,Muhongo uongo) .

 Naviomba  vyombo ya dola vimsake Kafulila awapatie huo ushahidi wa hiyo Nyaraka anayodai ni ya Ikulu  inayoonyesha Ikulu  ilikuwa imepanga kuwasafisha Muhongo na Maswi ili Ikulu ione hiyo barua kweli ni ya Ikulu?Ilitoka Ikulu kwenda kwa Kafulila kwa kufuata utaratibu?

Na Kama hiyo barua anayodai ni ya Ikulu na ikaja kubainika siyo ya Ikulu haraka sana Huyo afikishwe mahakamani kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa umma maana serikali ikiendelea kumlea Mzushi huyu ataendelea na tabia yake chafu ya kulala na kuamka na Kuzusha mambo mazito ambayo yanaligharimu Maisha watu ikiwa ni kuaribia Maisha,hadhi zao, kuliingiza taifa Katika matatizo makubwa ikiwemo  kunyimwa misaada na wafadhili .


Professa Muhongo,Maswi kwakuwa Nyie ni wa kristo ,ni watu wazima na mnaakili timamu mlitangulia kuliona jua najua mliumizwa  sana na uzushi wa Zitto na wazandiki wenzake nawashauri wasameheni kabisa,msilipe kisasi Kwani jukumu la kulipa kisasi ni la Mungu na  ZABURI ya 35 katika Biblia inasema wazi jukumu la kulipa kisasi ni la Mungu Mwenyewe siyo binadamu na ripoti ya Balozi Sefue, Hotuba ya Kikwete ya Disemba 23 Mwaka Jana, niwazi Mungu ameishatumia ZABURI ya 35 kupigana nao wote waliokuwa wakipingana nanyi.

Niitimishe Kwa kunukuu nukuu ya Koffi Olomide " Uongo Una panda lifti ,ukweli Una panda ngazi'. 

Na ni kweli ,ukweli  katika Sakata la Escrow ulipoanda ngazi ukachelewa kufika ,wasiyo na hatia wakasurubiwa kwa uzushi lakini hatimaye Juzi ukweli ule wa escrow uliokuwa unakuja taratibu kwa kupanda   ngazi ulifika ulikokuwa unakwenda na hatimaye Balozi Sefue akasema Timu yake ya uchunguzi imebaini Muhongo,Maswi hawana hatia Katika Escrow.

Zitto,Kafulila na wazushi wenzenu mmeumbuka, nendeni mkajipange upya ili mje na jungu jingine tena Kama mnafikiri mnaweza kuaminiwa tena Kuzusha majungu maana  mmeishajulikana Kuwa Nyie ni wataalamu wa kuwazusha baadhi ya mambo ambayo yanaleta taharuki Katika taifa na mwisho wa siku vyombo Vya upelelezi vikifanya uchunguzi tuhuma hizo inabainika ni uongo.

Na mfano  mzuri kipindi kile  Zitto alipozusha Kuwa anayoorodha ya Majina ya vigogo walioficha mabilioni nchini Uswiss   lakini Zitto alipotakiwa   na aliyekuwa  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema ambaye akilazimika kujiuzulu wadhifa wake kwa uzushi wenu  wa Escrow ulishindwa kutoa ushahidi huo wa majina hayo.

Zitto na Kafulila ,Filikunjombe katika ulingo wa siasa na hasa katika sakata la Escrow .  Mlikikuja na Spidi  ya moshi wa treni sasa    zimekwisha    zimebaki Kama vile  moshi wa sigala (fegi).Mtasubiri.

Hivi sasa mmekuwa  kama Midori. Mbele hamchezi ,nyuma hamtikisiki. Aibu yenu.

Mungu Ibariki Tanzania.

Facebook: Happy Katabazi
Mei 10 Mwaka 2015.