EDSON KAMKARA AMEFARIKI DUNIA LEO

BURIANI MHARIRI WANGU WA HABARI WA ZAMANI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA, EDSON KAMKARA AMBAE AMEFARIKI  JIONI YA LEO.
MBELE WEWE NYUMBA SISI.
By Happiness Katabazi, 25/6/2015.

PAPA MSOFFE AFUTIWA KESI YA MAUAJI LEO

PAPA MSOFFE AFUTIWA KESI YA MAUAJI  LEO

Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemfutia kesi ya Mauji iliyokuwa ikimkabili mfanyabishara maarufu  
Marijani Abdubakari Msoffe baada ya kupokea  taarifa  toka kwa 
MKurugenzi  wa Mashitaka (DPP) , Biswalo Mganga Leo Kuwa Hana nia ya kuendelea kumshitaki tena.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 ,inampa mamlaka DPP kuifuata kesi ya jinai bila kuhoji wa na mtu yoyote wala mamlaka yoyote ile.

Hata hivyo dakika Chache baada ya Kufutiwa Kesi hiyo ya mauji kinyume na Kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002 ambapo kisheria Mahakama ya Kisutu ilikuwa haina mamlaka ya kuisikiliza na haina dhamana na hivyo kwa Kipindi chote hicho tangu Agosti 10 Mwaka 2012 hadi Leo alikuwa akiishi Gereza la Keko Kisha aamishiwa gereza la Ukonga .

Leo pia upande wa Jamhuri umemfungulia Kesi mmoja ya kughushi Nyaraka za Viwanja ambayo  akitiiza Masharti ya dhamana anapata dhamana na hivyo kurudi nyumbani kwake kuungana na familia yake.Kesi hiyo mpya imearishwa hadi Julai 9 Mwaka huu.

Hata hivyo hadi sasa bado hajatekeleza Masharti ya dhamana bado yupo chini ya Ulinzi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

WOSIA WANGU KWA PAPA MSOFFE

 Pole Msoffe na hongera kwakufutiwa Kesi ,hiyo  ndio Sheria lazima Sheria zifuatwe  na wale waliopewa jukumu la kusimamia na kutekeleza Sheria.

Na Imani kwa kupata tuhuma zile za Kesi za Mauaji  na kukasababisha ukaishi gerezani ni wazi utakuwa umejifunza sasa Kuwa Sheria zipo ,hazibagui masikini wa  Tajiri wala Mtu maarufu,na dola linanguvu sana kuliko mwananchi wa aina yoyote yule na linamkono mrefu .

Ushauri wangu jiepushe kukaribia au Kutenda mambo yanavunja Sheria.
Msoffe ambaye wewe ni shabiki mwenzangu wa Bendi ya FM Academia nakushauri kaa mbali na tuhuma mbaya ambazo umekuwa ukisifika nazo sina haja ya kuzitaja hapa.

Nakumbuka Uliwahi kushitakiwa kwa Kesi Moja katika Mahakama ya Kisutu ukaenda Jela kwa kukosa dhamana na Kesi ile ikaisha ila Kesi hii ya Mauaji ilisababisha licha na Umaarufu wako wote ukasota  Jela kwa Kipindi chote hicho.

Nimelazimika kuandika stori hii ya Msoffe Kufutiwa Kesi hii Kwani Mimi nilikuwa ni miongoni mwa waandishi wa Habari za mahakamani  tuliokuwa siku ya kwanza anafikishwa mahakamani hapo kuandika Habari yake mfululizo hadi baadhi ya ndugu zake wakawa wanatuzuia tusimpige picha na kututolea maneno machafu bila kujua tulikuwa tukitimiza wajibu wetu hadi nilipoachakazi ya uandishi wa habari katika gazeti la Tanzania Daima Agosti mwaka 2014 ndipo nilipoacha kuandika kesi hii.Tulishawasamehe.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
24/6/2015

Tujikumbushe habari niliyoiandika siku ya kwanza wakati Papa Msoffe alipofunguliwa Kesi hiyo ya Mauji ambayo Leo amefutiwatiwa na DPP.

10/8/2012
PAPA MSOFFE KORTINI KWA KESI YA MAUJI

Na Happiness Katabazi 

HATIMAYE mfanyabaishara maarufu jijini Dar es Salaam, mfanyabaishara maarufu jijini Marijani Abdubakari Msoffe(50) maarufu kwa jina la “Papa Msoffe chuma cha reli akishi kutu’ amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kesi ya mauji. Wakili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka alidai mbele ya Hakimu Mkazi Agnes Mchome alidai kuwa Msofe ambaye ni mkazi wa Mikocheni,anakabiliwa na kosa m

oja la mauji ambalo ni kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.

 Wakili Kweka alidai kuwa Novemba 6 mwaka 2011 huko Magomeni Mapipa Papa Msoffe anayetetewa na wakili wa kujitegemea Majura Magafu alimuua Onesphory Kitoli na kwamba upelelezi wa kesi ya hiyo bado haujakamilika. Kwa upande wake hakimu Mchome alisema kesi hiyo ambayo ipo mbele yake ni mauji na mahakama yake haina mamlaka ya kuisikiliza na kwamba mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza ni Mahakama Kuu hivyo akamtaka mshitakiwa huyo asijibu chochote. 

“Kwa sababu hiyo naiarisha kesi hii hadi Agosti 23 mwaka huu, kesi hii itakuja kwaajili ya kujatwa na kwa kuwa kesi hii haina dhamana naamuru mshitakiwa apelekwe gerezani”alisema Hakimu Mchome. Msofe ambaye alifikishwa kwenye eneo la mahakama hii jana saa 3:30 asubuhi chini askari kanzu watatu ambao mmoja alikuwa amebeba silaha na kisha kumuingiza kwenye selo ya mahabusu hiyo kwaajili ya kumuifadhi hadi ilipofika saa tano saa asubuhi mshitakiwa huyo aliingizwa kwenye chumba namba tisa cha mahakamani hapo na kuanza kusomewa maelezo yake huku ndugu na jamaa zake walikuwa wamefika mahakamani hapo kwaajili kusikiliza kesi hiyo ya ndugu yao.

 Msofe ambaye jina lake limekuwa likitajwa mara kwa mara kwenye nyimbo zinazopigwa na Bendi za Miziki ya Dansi nchini ikiwemo Bendi ya FM Academia na Acudo Impact aliletwa na askari kanzu hao akitokea kwenye sero ya jeshi la polisi ambako kwa zaidi ya wiki moja sasa alikuwa akiishi ndani sero hiyo ya polisi kwaajili mahojiano na mshitakiwa huyo na hatimaye jana akafikishwa mahakamani hapo kwa kesi ya mauji.

 Itakumbukwa hivi karibuni mjane mmoja aishie Mbezi Beach alilalamika kupitia vyombo vya habari kuwa Papa Msofe anataka kumdhuru nyumba aliyoachiwa na marehemu mumewe wake kupitia vyombo vya habari, hali iliyosababisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuingilia kati sakata hilo na hatimaye mjane huyo akarudishiwa nyumba yake aliyokuwa akidai Msofe anataka kumdhurumu. Aidha itakumbukwa kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Papa Msofe kufikishwa katika mahakama hiyo kwa makosa mbalimbali ya jinai. 

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi,Agosti 11 mwaka 2012
Juni 24 Mwaka 2015.

FM ACADEMIA "NGWASUMA" FAMILIA MOJA

Happiness Katabazi,Godluck,Royer Mziray,Josee ndani ya Meeda Club Kwenye show ya Band ya Fm Academia, Juni 20 Mwaka 2015.

MBOWE AJAPOTEZA SIFA YA KUGOMBEA URAIS,UBUNGE

Na Happiness Katabazi

JUNI  17 Mwaka huu, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Hai, Denis Mpelembwa alimhukumu  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  kulipa faini ya Sh milioni Moja  au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kumkuta na  hatia ya kumshambulia mwangalizi wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 na Mbowe alilipa faini hiyo.

Mbowe alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kumfanyia shambulio , mwangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu Mwaka 2010, Nassir Yamin katika kituo cha kupigia kura kilichokuwa katika Zahanati ya Lambo.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mpelembwa alisema kitendo kilichofanywa na Mbowe hakikubaliki na kinapaswa kukemewa na kupewa Adhabu.

Tangu hukumu hiyo itolewe ,kumezuka mjadala Katika Jamii na vyombo Vya Habari ambapo kundi Moja linadai hukumu hiyo imepotezea imefanya Mbowe kupoteza sifa ya kuwa nia  nafasi ya Ubunge na urais endapo Atakuwa na nia ya Kugombea nafasi hiyo na kundi jingine linadai hukumu hiyo haijamuondolea sifa ya Kugombea nafasi hizo.

Binafsi kupitia makala hii naungana na wale wote wanaodai Kuwa hukumu hiyo haijamuondolea Mbowe sifa ya Kugombea nafasi ya rais,Ubunge pindi akitaka Kugombea nafasi hizo.

Makala yangu hii kabla ya kwenda Mbali imetazama aina ya makosa aliyotiwa nayo hatiani Mbowe na Mahakama.

Pia nimefanya utafiti wangu wa kisheria kuona Je makosa hayo aliyotiwa nayo hatiani Je ni makosa yanaangukia Katika Ibara ya 39 na 67 ya Katiba ya Jamhuri Muungano ya Mwaka 1977 ? Kwani Katika Ibara hizo kuna aina ya makosa ambayo yameanishwa wazi Kuwa endapo MTu atatiwa hatiani na makosa ya aina hiyo atakuwa  amepoteza  sifa Kugombea urais  au Ubunge.

Ibara ya 39 (e) ya Katiba hiyo inasomeka hivi ; " katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi     Mkuu.  hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali;

Ibara ya 67(2) (c)  Ikiwa  mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu; au

Ibara 67(2) (d) ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma".

Kwa mujibu wa Ibara hizo  mbili ni wazi kabisa makosa aliyotiwa nayo hatiani Mbowe hayaangukii Katika Ibara hizo mbili na kwa maana hiyo Mbowe licha ametiwa hatia kwa kosa la shambulio ,sio kosa la kukwepa kulipa kori kwa serikali,kosa la kukosa uaminifu.

Hivyo Mbowe anayohaki ya Kugombea nafasi hizo pindi akitaka kwasababu Katiba haikulitaja kosa la shambulio Kuwa endapo mtu atapatikana na kosa basi hataruhusiwa Kugombea nafasi hizo.

Pia nimejiuliza Je adhabu aliyopewa Mbowe Juzi inamzuia Kugombea nafasi ya Rais au Ubunge pindi akitaka kufanya hivyo?

Baada  ya kujiuliza pia nilifanya  utafiti  wangu kisheria ambapo nimebaini Adhabu ile ya kulipa faini ya Sh.milioni Moja haimzui pia Kugombea nafasi hizo Kama anaitaji Kugombea .

Kwa Sababu Ibara ya 67 (7) ya Katiba inasomeka hivi;    Kanuni zifuatazo zitatumika kwa ajili ya ufafanuzi wa aya ya ( c), ya (d) na ya (e) za ibara ndogo ya (2) ya ibara hii, yaani-

(a) ikiwa mtu amepewa adhabu mbili au zaidi za kufungwa gerezani na imeamuliwa afungwe kwa muda wa mfululizo, basi adhabu hizo zitahesabiwa kama ni adhabu mbalimbali iwapo muda uliotajwa katika kila moja ya adhabu hizo hauzidi miezi sita; lakini iwapo muda uliotajwa katika adhabu yoyote kati ya adhabu hizo unazidi miezi sita basi adhabu hizo zote zitahesabiwa kama ni adhabu moja; zitahesabiwa kama ni adhabu moja;

(b) ikiwa mtu atapewa adhabu ya kufungwa gerezani
ikifahamika kuwa adhabu hiyo ya kifungo imetolewa badala ya adhabu ya kutozwa faini au imetolewa kwa sababu mtu huyo ameshindwa kulipa faini aliyoamriwa kulipa, basi muda wa kifungo cha namna hiyo hautahesabiwa.

Kwa Tafsiri   nyepesi Ibara ya 67(a)(b) zinazungumzia muda wa Kifungo. Na Mbowe hajatumikia Kifungo gerezani  maana alilipa faini .

Na hata Kama kosa alilotiwa nalo hatiani Mbowe la shambulio lipo Katika  Sheria  ya Maadili ya Viongozi wa Umma, bado haiwezi kumwondolea sifa  Mbowe ya Kugombea nafasi hizo Kwani Mbowe hajatumikia Adhabu ya Kifungu kwa muda usioidi  Miezi Sita Kwani Mbowe alilipa faini .

Kwa Tafsiri ya Ibara hizo hapo juu nilizozitaja hapo juu Katika makala yangu hii ,  Mbowe sio kweli Mbowe amepoteza sifa za Kugombea urais au Ubunge.

Mbowe naamini hukumu hiyo itakuwa imekupa  funzo la  kuacha kujichukilia Sheria mkononi Kwani hukumu hiyo imekutia doa Kuwa wewe ni kiongozi wa kisiasa mwenye hadhi ya Ubunge, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bunge na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema), lakini ukashindwa kutii Sheria bila shuruti ukaamu kujichukulia Sheria mkononi na kuamua kumpiga Mkurugenzi wa Uchaguzi Mwaka 2010.

Kwa Mara Kadhaa nilikuwa nikiandika makala mbalimbali za kukemea baadhi ya matendo ya Uvunjifu wa Sheria yaliyokuwa yakufanywa na baadhi ya wanachama wa Chadema yakiwemo makosa ya kuandamana bila kutoa taarifa Polisi,nanilikuwa nikikemea vitendo hivyo na Kama kawaida Yao walikuwa wakinupitukana minilikuwa madharau kwasababu niliwaona ni wajinga ambao hawafahamu Sheria za nchi zipo ,zitatumika na Hazina macho zinatakiwa kukuadhibu mtu yoyote Yule anayepatikana na hatia ya kuzivunja.

Na kweli Juni 17 Mwaka huu,sote ni mashahidi Sheria hizo hizo ambazo baadhi ya wafuasi wa Chadema wamekuwa wakidai ni Sheria Mbaya mara nzuri zilimtia adabu Mbowe kwani zilimia hatiani.

Licha Sheria hizo hizo wanazodai ni Mbaya siku Mahakama ikizitumia kutoa hukumu Katika baadhi ya Kesi zinazowakabili wanachama wa Chadema na wanachama Hao wakashinda Kesi hizo wanachama hao usema Mahakama imetenda Haki ila siku Mahakama ikitumia Sheria hizo hizo kuwaita hatiani baadhi ya wafuasi wa Chadema, wafausi hao ulalamika na Kusema Mahakama ni a CCM na wamuonewa. Ajabu..

Kama Utakumbuka makala yangu ya Mwaka Jana iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho " DOZEE DOZEE FREEMAN MBOWE ' ndani ya makala hiyo nilikuasa sana kuheshimu Sheria za nchi Kwani Sheria zinakutaka wewe na wananchi wote kuheshimu Sheria.

Na hukumu hiyo naamini umeamini hata kimoyo moyo Kuwa Sheria zipo, Hazina  macho na zimekushughulikia.Pole sana ,ila nakushauri hukumu hiyo iwe ni Funzo kwako na usirudie tena Kutenda matendo hayo ya kihuni ya kumpiga mtu ambayo tunatazamia anayefanya makosa ya aina hiyo ni wahuni na siyo MTu mwenye hadhi ya Kama yako.

Mbowe Mzee wangu hivi sasa jitambue Kuwa umeishakuwa Mtu mzima ,mambo mengine Kama haya ya kihuni huni ya kujichukulia Sheria mkononi ,kutoa maagizo ya kwa wanachama wako wafanye maandamano bila kikomo tena bila kutoa taarifa Polisi achana nayo Kwani mwisho wa siku yanakushushia heshima wewe na familia yako na Chama unachokiongoza.

Ni wazi kabisa haipendezi Kuwa Mwanachama wa Chama Fulani halafu Mwenyekiti wa Chama hicho anashitakiwa na kukutwa na hatia ya Kutenda kosa Kama Hilo lako ulilotiwa nalo hatiani.

Ni aibu sana ,licha unaweza kujitutumua Mbele za watu Kuwa hujali ila ukweli ni kwamba hukumu hiyo imekutia doa.

Jirekebishe,kuna vitu vingine Kama hivi Vya kihuni huni acha usivifanye maana vinashusha heshima yako ndani na nje ya nchi na siyo sifa ya kila siku kiongozi Kama wewe,mfanyabiashara mkubwa Kutwa kushinda kwenye vyumba Vya Mahakama ukikabiliwa na Kesi za kipuuzi puuzi ambazo zilipaswa zifanywe na watu wasiyo na hadhi Kama yako Katika Jamii.

Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya nchi, inatoa haki ya kukata rufaa. Hivyo Kama ujaridhika  na hukumu ya Mahakama ya Wilaya Hai iliyokukuta na hatia , unayo hadi ya kukata rufaa ili Mahakama ione Mahakama  Kuu itamke hukumu hiyo iliyokutia hatiani ilikuwa na uhalali wa kisheria au laa. 

Mbowe amka usingizini,jitambue wewe ninani?Una madaraka gani?.Acha 'use la Mavi'.

Matendo  uyatendayo  yanayosababisha ufunguliwe Kesi zaidi ya Moja,uitwe Polisi kuhojiwa chini ya Ulinzi Mkali.

Hata  kama watu wako wa karibu yako hawakuambii ukweli,minakwambia matendo hayo yanakupunguzia heshima Mbele ya watu wastaarabu Kwani tangu Juzi ulipotiwa hatiani watu wamekuwa wakisema hivi sasa Chadema Inaongozwa na Mwenyekiti Mhalifu na wanahaki ya kukuita wewe ni mhalifu  kwasababu Mahakama imekutia na hatia ya Kutenda kosa la kumshambulia mtu.

'Mume wangu wa zamani'  ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour(TLP), Augustine Mrema , Mabere Marando, Mwenyekiti wa Chama cha Democraty  (DP) Mchungaji Christopher Mtikila, Miaka ya nyuma walifanya sana wazimu huo wa kuvunja Sheria za nchi mwisho wa siku walivyojitambua, na kufahamu madhara ya kukabiliwa na Kesi za jinai mahakamani waliamua kuachana na vitendo vile Vya kiuno Vya kuvunja Sheria za nchi.

Jifunze kutoka Kwao maana wamekutangulia kuingia Kwenye ulingoni siasa za vyama Vya upinzani nchini uaacha  'Usela Mavi' yaani Kutenda vitendo vya kihunihuni Vya kujichukulia Sheria mkononi.

Mungu ibariki Tanzania

Facebook: Happy Katabazi
Juni 19 Mwaka 2015.

NILIJIUNGA TENA NA CCM 2011: JAJI AUGUSTINO RAMADHAN

.

Na Happiness Katabazi

MGOMBEA urais wa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania , Augustino Ramadhan amesema alijiunga tena na CCM  Septemba Mwaka 2011 Katika Tawi la Chama hicho ,Oysterbay, Jijini Dar es Salaam.

Jaji Ramadhani ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la Anglikana, aliyasema hayo Leo saa Tatu asubuhi wakati akihojiwa na Mwandishi wa Habari hizi Katika mahojiano maalumu .

"Nilijiunga tena kwa Mara ya pili na CCM , Septemba Mwaka 2011 katika Tawi  langu la CCM lililopo Oysterbay ,Jijini Dar es Salaam  na Mimi naviachia vikao Vya Chama viamue Kama muda huo niliyojiunga tena na CCM Unatosha kuniruhusu  kugombea nafasi yoyote Kwenye Chama ikiwemo nafasi hiyo ya Urais au laa" alisema Jaji Ramadhan.

Jaji Ramadhaman alisema anaomba wananchi anafahamu Kuwa Mwaka 1966 akiwa ni Mwanafunzi wa kozi ya Sheria Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kulitokea mgomo wa wanafunzi ambao wanafunzi hao walikuwa wakipinga Masharti ya kujiunga na mafunzo ya National Services Hali iliyosababisha  chuo Kufungwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wote kufukuzwa chuo kwasababu ya mgomo ule licha yeye hakuwa miongoni mwa wanafunzi walioanzisha vurugu zile na hivyo kufanya Mwaka mmoja kukaa majumbani.

Alisema Julai  Mwaka 1967 ,Chuo Kikuu kilisamehe wanafunzi wote waliokuwa wamefukuzwa Chuo mwaka 1966 kutokana na vurugu zile hivyo na hivyo wakarejea chuoni hapo na kuanza upya Mwaka wa kwanza kozi ya shahada ya Sheria na walivyorejea chuoni wanafunzi Wengi Walikata Kadi na kujiunga na TANU YOUTH LEAGE.

Jaji Ramadhan  ambaye ni Jaji wa  Mahakama ya Afrika Ya Haki za Binadamu , alisema alipofika mwaka wa tatu wa kozi yake ya Sheria Mwaka 1969 ,  Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) , lilitangaza ajira  na kwamba yeye alienda kuomba kazi ya jeshi na aliitwa kwenye usahili na wakati alipokuwa akihojiwa katika usahili huo maswali  mbalimbali na akawauliza Kuwa yeye ni Mwanachama wa TANU YOUTH LEAGE  akawajibu Kuwa ni kweli ni Mwanachama .

Alisema Maofisa  wale wa JWTZ wala mwambia hiyo haitoshi wakimtaka awapatie Kadi inayoonyesha yeye ni Mwanachama wa Chama cha TANU ,kadi ambayo halikuwa Hana Hali iliyosababisha Mwaka 1969 kwenda  kwenye  Tawi la TANU  ,Temeke Dar es Salaam , kukata Kadi ya TANU na kuwapatia na hivyo hicho nacho kikawa ni Kigezo cha kupata ajira ya JWTZ hadi anastaafu Kazi ya JWTZ alistaafu akiwa na Cheo cha Brigedia Jenerali wa Jeshi Hilo.

" Nikaendelea Kuwa Mwanachama wa TANU  ambapo Mwaka 1977 I kazaliwa CCM  Nikiwa na Jaji na Ofisa wa JWTZ  hadi Ilipofika Mwaka 1992 , Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho ambapo ziliingizwa Ibara ambazo zilikuwa zinakataza Majaji na Askari Kuwa wanachama wa vyama Vya siasa  Ndipo nikipoacha kuwa  Mwanachama wa CCM "alisema Jaji Ramadhan.

Aidha alisema Disemba 28 Mwaka 2010  alistaafu rasmi Kazi ya jaji wa Mahakama ya Rufaa akiwa na wadhifa wa Jaji  ya Jaji Mkuu wa Tanzania  na kwamba Septemba Mwaka 2011 ndipo alipojiunga tena kwa Mara ya pili  CCM.

Juni 17 Mwaka 2015 ,Jaji Ramadhan alichukua fomu ya Kugombea nafasi ya urais kupitia CCM, Hali iliyosababisha Kuibuka maswali yasiyo na majibu Kuwa ni lini alijiunga na CCM wakati yeye aliwahi Kuwa jaji.

Facebook: Happy Katabazi
Juni 18 Mwaka 2014.

MFAHAMU KWA UNDANI JAJI AUGUSTINO RAMADHAN

HONGERA JAJI AUGUSTINO   RAMADHAN

Na Happiness Katabazi

JUNI 17 Mwaka 2015 ,Jaji wa Mahakama ya Afrika Ya Haki za Binadamu ,Agustino Ramadhani alichukua fomu ya Kugombea nafasi ya rais kupitia Chama cha Mapinduzi .

SEPTEMBA 9 mwaka 2014, vyombo habari nchini vilichapisha habari kuwa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu   imemteua Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania Agustino Ramadhan kuwa rais wa mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka miwili uteuzi na kwamba  uteuzi huo unaanza  mara moja baada ya aliyekuwa rais wa mahakama hiyo Sophia Akuffo wa Ghana kumaliza muda wake.

Jaji Ramadhani Mtanzania wa kwanza kushikilia kiti hicho tangia kuanzishwa kwa mahakama hiyo baada ya kupata kura 7 kwa kura nne dhidi ya mpinzania wake katika nafasi hiyo ya rais wa mahakama hiyo huku nafasi ya makamu wake ikichukuliwa na jaji  Eisie Thompson kutoka nchi ya Nigeria.

Katika nafasi hiyo ya makamu walikuwepo majaji watatu waliokuwa wakiwania nafasi hiyo na baada ya upigaji wa kura mara ya kwanza wawili walifungana kwa kura 4 na mmoja kupata kura tatu ndipo uchaguzi ulirudiwa na jaji Thompson kuibuka mshindi kwa kupata kura 6 dhidi ya tano za mpinzani wake.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya uteuzi huo jaji Ramadhan alisema kuwa ni heshima kwa Taifa la Tanzania kwani ndio mara yake ya kwanza kupata nafasi hiyo huku akisema kuwa nafasi hiyo ni heshima kwake na kwa taifa lake.

“Kesi yeyote inayohusu nchi yangu mimi sitakuwepo kutokana na sheria zetu za mahakama hii na kuwa tayari watanzania watano wamefungua kesi kwenye mahakama hii na kesi mbili zimetolewa hukumu ya mchungaji mtikila na Zongo”alisema jaji Ramadhan

Alisema kuwa mpaka sasa ni kesi tano zimefunguliwa  katika mahakama hiyo na mbili teyari zimetolewa ikiwemo dhidi ya serekali ya Tanzania kesi iliyofunguliwa na mchungaji Christopher Mtikila iliyohusu mgombea Binafsi huku akisema kuwa kuchukuwa hatua kwa utekelezaji wa hukumu kunategemea na serekali kama imejiunga na mikataba ya kimataifa.

Jaji Agustino alisema  kutokana na sheria za mahakama hiyo wakati wa usikilizaji wa kesi zinazoihusu Tanzania   yeye hawezi kuisikiliza na kuwa atajitoa kuisikiliza kama Sheria inavyomtaka Kuwa huwezi Kuwa Jaji Katika Kesi inayokuhusu na Kusema Kuwa Mahakama hiyo  inaundwa na majaji 11 kutoka nchi tofauti za bara hili .

Aidha mahakama hiyo iliwaapisha majaji watatu wa mahakama hiyo kabla ya kuanza mchakato wa upigaji kura kumteuwa jaji wa mahakama hiyo huku ripoti ya mahakama hiyo kila mwaka ikipelekwa kwa Umoja wa Nchi za Afrika.

Uchaguzi huo huwa ni vipindi vya miaka miwili miwili na iwapo ukimaliza muhula wa kwanza kama utateuliwa tena kushika nafasi hiyo utakuwa ndio kipindi chako ya mwisho kushikilia nafasi hiyo.

Binafsi Nampongeza Mzee wangu Jaji Ramadhan kwa kushinda nafasi hiyo ambayo ushindi huo ni Tanzania pia Kwani ushindi huo umeandika historia mpya wa Tanzania Kwa Mtanzania Huyo Ramadhan kuwa Mtanzania wa kwanza kushika wadhifa huo.

Nilipokuwa Mwandishi wa Habari za mahakamani nimekuwa nikiripoti Kesi mbalimbali ikiwemo baadhi ya Kesi zilizokuwa zikisikilizwa na Jaji Ramadhan ikiwemo Kesi yakihistoria ya Rufaa iliyokuwa imekatwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mchungaji Christophe Mtikila , ambapo jopo la Majaji Saba wa Mahakama ya Rufaa iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Ramadhan  ambapo mwisho wa siku jopo Hilo lilikubaliama na hoja za Mwomba rufaa (AG) Aliyekuwa akiwasilishwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali George Masaju, Kuzuia kuwepo Kwa mgombea binafsi.

Katika Utawala wa Jaji Ramadhan wa Ujaji Mkuu  na ' mpiganaji wake' Msajili wa Mahakama ya Rufaa alikuwa ni Jaji Francis Mutungi ambaye Kwasasa ni Msajili wa Vya Vya Siasa nchini, binafsi nilikuwa nikifanya nao Kazi  Kwa karibu na alikuwa wakinipa ushirikiano wa kikazi na nasaha  mbalimbali.

Jaji Ramadhan ana vitu viwili ambavyo navipenda sana kutoka kwake .Moja ,Ramadhan ni mtu anayependa Kusema ukweli na ukweli huo upenda kuweka adharani.

Pili; Jaji Ramadhan ni miongoni mwa Majaji wakuu wachache ambao ni nimewaona ambao wanaingilika kirahisi pindi mwanahabari unapotaka kufanya mahojiano naye kuhusu mambo mbalimbali na ushahidi wa Hilo ni hizo makala zangu mbili niliyofanya nae mahojiano wakati alipoteuliwa Kuwa Jaji Mkuu na alipostaafu wadhifa huo.

Hivyo nakuombea Afya njema ,Mungu akutangulie Katika wadhifa wako huo mpya wa Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, Kwani ni Miezi michache tu ulimaliza kutumikia wadhifa wako wa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Septemba 10 Mwaka 2014

(Makala hiyo hapo chini , nilifanya mahojiano na Jaji Ramadhan muda mfupi baada ya kustaafu Utumishi wa umma kwa mujibu wa Sheria)

DISEMBA  2013

JAJI RAMADHANI AWA MCHUNGAJI  

 Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawazwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi Zanzibar.

JAJI RAMADHANI AWA MAKAMU MWENYEKITI TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

APRILI 7 Mwaka 2012, Rais Jakaya Kikwete aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo alikuwa Jaji Augustino  Ramadhani.

AUGUSTINO RAMADHAN: KESI YA MGOMBEA BINAFSI SITAISAHAU

Na Happiness Katabazi

“KESHOKUTWA,yaani Desemba 28 Mwaka 2010  nitakuwa nikikumbuka siku yangu ya kuzaliwa na nitakuwa ninatimiza umri wa miaka 65, siku hiyo pia itakuwa ya kihistoria kwangu kwani ndiyo nitakuwa nastaafu kazi ya utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria na Katiba ya Nchi.”

Hii ni nukuu ya maneno ya Jaji Mkuu, Augustino  Ramadhan, alipoanza kuzungumza na jahazi Jumapili kuhusu maisha yake na kazi

Anasema kuwa katika kipindi chote cha utawala wake amefanya kazi kwa ushirikino mkubwa na watendaji wa serikali pamoja na wale wa mahakama.

Anabinisha kuwa anajivunia kuwa katika uongozi wake aliheshimu sheria na Katiba na hata watendaji wenzake kwa kiasi kikubwa walijitahidi kufuata mambo hayo Yafuatayo ni mahojiano ya Jaji Ramadhani na Jahazi Jumapili.
Swali: Ulijisikiaje wakati ukiteuliwa kuwa jaji mkuu mwaka 2007 na changamoto zipi ulizozikuta?

Jibu: Nilifarijika kuteuliwa kushika wadhifa huo wa kuongoza mhimili wa mahakama kwa sababu ni nadra kupata nafasi kuu kama hii.

Changamoto kubwa niliyoikuta ni uhaba wa watendaji, ambapo majaji wa Mahakama Kuu na Rufaa kwa wakati huo walikuwa 11 na hivi sasa tuko 16.

Katika Mahakama Kuu, Rais Kikwete, aliteua majaji 30 kuanzia mwaka 2008 hadi sasa ambapo ni wastani wa majaji 10 kila mwaka.

Mahakimu wa mahakama za mwanzo wapatao 100 wameajiriwa kuongoza mahakama hizo jambo ambalo kwa kiasi fulani limeharakisha usikilizaji wa kesi.

Hivi sasa Mahakama Kuu ina Kanda 13 na kanda hizo zina majaji wawili wawili isipokuwa Kanda ya Tabora, Mwanza majaji wanne, Arusha watatu.

Changamoto nyingine ni uhaba wa vitendea kazi na teknolojia za kizamani za kurekodi mashauri lakini nashukuru Desemba 6 mwaka huu, tulizindua mfumo wa kidigitali wa kurekodia mwenendo wa kesi pamoja na tovuti ya mahakama.

Teknolojia hiyo ya kidijitali imeishafungwa inatumika kwenye Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na vitengo vyake vya Kazi, Ardhi na Biashara.
Swali: Ushirikiano wa mahakama na mhimili mingine ulikuwaje Jibu: Kimsingi wakati nikiingia mambo yalikuwa si mazuri, watendaji wa mahakama tulikuwa tukilalamikiwa na wabunge, wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa serikali.

Jibu: Tatizo hilo nililitatua kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali na Rais Jakaya Kikwete pamoja na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta kwenye shehere zetu mbalimbali.
Nami pia nilikuwa nikihudhuria sherehe za kiserikali pamoja na vikao vya Bunge hasa vile vya bajeti.

Kupitia ushirikiano huo mpya tuliweza kuhabarishana changamoto zinazotukabili na namna ya kuzitatua kulingana na uwezo tuliokuwa nao.

Swali: Kwa nini mahakama huchelewesha usikilizaji wa kesi?

Jibu: Kuna aina mbili za ucheweshwaji wa kesi, mosi mahakama pili ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), ofisi ya Mwanasheria, polisi na mawakili wa kujitegemea.
Wakati mwingine hakimu au jaji anakuwa yuko tayari kusikiliza kesi lakini upande wa mashtaka unadai haujakamilisha upelelezi au unashindwa kuleta mashahidi kwa wakati.
Sababu nyingine ni baadhi ya mawakili wa kujitegemea wanakuwa hawajajiandaa kuendesha kesi husika sasa kwa sababu hizo ndiyo maana kesi zinashindwa kumalizika mapema.
Wananchi wengi hawatambui mchakato wa uendeshaji wa kesi ndiyo maana mwisho wa siku huishia kuitupia lawama mahakama kuwa inachelewesha kesi.

Lakini pia mhimili wa mahakama umeweza kusimamia sheria na Katiba. Pia mfumo wenyewe na baadhi ya sheria kwani tumeweza kubadilisha kanuni za uendeshaji wa kesi za Mahakama ya Rufani.

Kanuni za awali zilizotungwa mwaka 1979 zikafutwa na kanuni hizo mpya zilizopitishwa mwaka 2009 zimeanza kutumika Februari mwaka huu.
Swali: Wazee wa baraza wa mahakama wamekuwa wakilalamika kutolipwa posho kwa nini hali hiyo inajitokeza?

Jibu: Ni kweli kulikuwa na malalamiko hayo na wazee wa baraza walikuwa wanapata posho ya sh 1,500. Ila kuanzia Julai mwaka huu posho yao imeongezeka wanapata posho ya sh 5,000.
Wakati mwingine wazee hao walikuwa wanakopwa na mahakama wanakwenda kusikiliza kesi, hili lilikuwa linasababishwa na ufinyu wa bajeti ya mahakama.

Swali: una maana gani unaposema uongozi wako mahakama ilizingatia sheria na Katiba?

Jibu: Aah! Namaanisha kwamba mahakama imeangalia Katiba kwa mtizamo mpya unaopaswa uwe, ibara za Katiba zinazohusu majaji na ajira zao.
Huko nyuma majaji wa mahakama kuu walikuwa wanastaafu kwa mujibu wa sheria wakiwa na umri wa miaka 60 na wale wa mahakama ya rufaa miaka 65, halafu wanapewa mafao yao na kisha wanaweza kurejeshwa kufanya kazi hiyo kwa mkataba.
Hivi sasa hivi Rais wa nchi anaweza kuongeza umri wa kustaafu wa jaji anayekaribia kustaafu, Mfano Jaji wa Mahakama Kuu ana miaka 59;
Rais anaruhusiwa kumuongezea hata miaka mitatu mbele ya utumishi kabla ya umri wa miaka 60 kustaafu na akishastaafu katika umri huo alioongezewa na rais ndiyo anatapewa mafao yake yote.

Swali: Serikali imefanya jambo gani kwa mahakama mbalo utalikumbuka?
Jibu: Kubwa zaidi ni kukubali ombi letu la kutaka tuwe na mfuko wa mahakama ambao tunaamini utatusaidia kutatua matatizo yetu yanayokwamishwa na uhaba wa fedha.
Kilio chetu kikubwa kilikuwa ni kuiomba serikali ituwekee angalau asilimia mbili ya bajeti ya seriakli katika mfuko huo, sasa hivi mahakama inapewa asilimia 0.4 ya bajeti ya serikali.
Kiwango hiki ni kidogo sana kwani hata mikoa ya Lindi na Mtwara bajeti yake ni kubwa kuliko bajeti ya mahakama ambayo ina ofisi katika kata, wilaya na mkoa.

Pia naishukuru serikali kwa kutujengea mahakama za mwanzo mbili za kisasa zilizopo Kerege na Lugoba mkoani Pwani ambazo zimezinduliwa mapema wiki hii na ujenzi wake umegharimu zaidi ya sh milioni 600.
Swali: Kipi unajivunia katika utawala wako?

Jibu: Ni kuanzisha mchakato wa mahakama kupata mfuko wake na ninaamini hadi kufikia Julai mwakani mwakani mfuko huo utapatikana.

Jibu: Ikumbukwe kwamba licha ya kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, mimi ni Jaji wa Mahakama ya Haki za Binadamu na za watu ya Afrika yenye makao makuu yake jijini Arusha.

Katika mahakama hiyo tuko majaji 11. Ila majaji wa mahakama hiyo hatufanyi kazi muda wote, tunakutana mara nne kwa mwaka na kwa siku 10.
Kwa hiyo nafasi hiyo ya ujaji wa mahakama hiyo ya Afrika nayo itaniwezesha kuniingizia kipato. Pia nitakuwa nikilipwa pesheni za kustaafu na serikali yetu.
Nakusudia kuwa mhadhiri wa sheria (Visiting Lecturer), katika baadhi ya vyuo vikuu na ninakusudia kuandika vitabu.

Swali: Ni kesi gani ulishiriki kuisikiliza na kuitolea maamuzi ambayo hutoisahau?
Jibu: Ni kesi ya Kikatiba ambayo mwanasheria mkuu wa serikali alikata rufaa katika Mahakama ya Rufaa, dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila, kwamba mahakama inaweza kutamka kwamba ibara ya Katiba inaweza kuvunja ibara nyingine ya Katiba?

Nitaikumbuka kesi hiyo kwa sababu ni mara ya kwanza kwa mahakama ya rufani nchini kuketi majaji saba kusikiliza rufaa moja , pia ni mara ya kwanza kwa mahakama ya rufaa kuwaita marafiki wa mahakama-Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Paramaganda Kabudi.

Alikuwapo pia aliyekuwa mhadhiri mwandamizi wa sheria wa UDSM, marehemu Profesa Jwani Mwaikusa na Mkurugenzi wa Mashtaka wa Zanzibar (DPP), Masoud Othman Masoud.
Sababu hasa inayonifanya niikumbuke kesi hiyo ambayo mimi nilikuwa kiongozi wa jopo hilo la majaji ni muda niliotumia kufanya utafiti na hatimaye tukafikia uamuzi wa kutoa hukumu; kesi ile ambayo wananchi wengi hupenda kuita kesi ya mgombea binafsi.
Ila mimi siiti kesi ya mgombea binafsi bali naiita kesi ya Kikatiba.

Swali: Wosia gani unautoa kwa majaji na mahakimu?

Jibu: Ninawaasa waendelee kuzingatia sheria na Katiba ya nchi katika utendaji wao wa kila siku kwani wakumbuke wao ndiyo kimbilio la wananchi wenye kudhulumiwa au kuminywa haki zao.
Ni vema wakaendelea kuilinda heshima ya mahakama kwa kutoa haki bila upendeleo wowote.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Desemba 26 mwaka 2010

(Makala hii hapa chini ,nilifanya mahojiano na Jaji Ramadhani ikiwa ni siku Chache tu tangu ateuliwe na Rais Kikwete kushika wadhifa wa Jaji Mkuu )

HUYU NDIYE AGUSTINO RAMADHAN: JAJI MKUU MTEULE TANZANIA

Na Happiness Katabazi
Mapema wiki hii Rais Jakaya Kikwete, alimteua aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Augustino Ramadhani (62) kuwa Jaji Mkuu mpya, Mwandishi Wetu Happiness Katabazi, alifanya mahojiano maalumu na Jaji Mkuu huyo mteule na katika makala hii amezungumzia historia ya maisha yake kwa mapana na masuala mengine mbalimbali yanayohusu Mahakama ambayo ni mhimili mahususi.

Swali: Umepokeaje uteuzi wa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania?

Jibu: Nimepokea uteuzi huu kwa furaha. Na nimechukulia kwamba Rais Kikwete ana imani nami na pia ameridhishwa na utendaji kazi wangu na kabla ameamini kuwa mimi nitaendeleza yaliyofanywa na watangulizi wangu yaani Jaji Augustino Saidi, Jaji Francis Nyalali na Jaji Barnabas Samatta.
Sikutazamia, uteuzi umenijia ghafla. Hivyo nataka nipate muda wa kujipanga ili siku za usoni aliyeniteua asione alichagua mtu asiyestahili kushika wadhifa huu.

Swali: Watanzania wangependa kusikia kauli yako kwamba ni mambo yapi umejipanga kuyafanya katika uongozi wako?

Jibu: Ni mapema mno kusema nimejipanga kuanza kukabiliana na jambo gani maana nafasi hii ni ya kuteuliwa, labda kama nafasi hii ingekuwa ya kisiasa ningeweza kutamka mapema namna hii kwamba nimejipanga kufanya nini.
Sipendi kuwadanganya Watanzania kwamba ooh, nitafanya ili na lile, kwakuwa mimi ni mwanasheria mwandamizi, hivyo leo hii nikurupuke na kusema kitu ambacho sijakifanyia utafiti, nitakuwa nadhalilisha taaluma ya sheria na Mahakama kwa ujumla.

Nitakapoingia ofisi mpya nakuona ofisi hiyo mambo yanaendeshwaje, kuna ‘miba gani’, na kushirikisha wenzangu hapo ninaweza kutoa kauli ya nini tumejipanga kukifanya.
Ila ninachoweza kuwahakikishia wananchi ni kwamba, nimelenga kusimamia mambo matatu. Moja nitahakikisha haki inapatikana haraka iwezekanavyo, maana imekuwa ni tatizo linalolalamikiwa na watu wengi wanapotafuta haki katika vyombo vya sheria.
Nitahakikisha pia haki inapatikana bila rushwa na kwamba nitajipanga na watendaji wenzangu kuona ni jinsi gani tutakabiliana na tatizo hilo.

Pia nitahakikisha haki inapatikana kwa gharama nafuu, maana haki imekuwa ikipatikana kwa gharama kubwa hasa inapokuja gharama za kuwalipa mawakili, lakini nitaweka mipango na wenzangu na kuandaa mazingira ya kupatikana haki kwa gharama nafuu.

Swali: Kuna malalamiko mengi ya ucheleweshwaji wa usikilizaji wa kesi hasa za mauaji, hili umelipangia mkakati gani?

Jibu: Maoni yangu. Si ucheleweshwaji wa kesi za mauaji tu, bali kesi zote zinacheleweshwa. Kwa upande wa kesi za jinai, kuna sababu tatu ninaweza kuzitaja kuwa zinachangia ucheleweshwaji wa kusikiliza, upande wa kwanza ni serikali ambao waendesha mashitaka huwa wanasema upelelezi kwa kesi fulani bado haujakamilika.
Na sisi kama Mahakama ni vigumu kujua ni matatizo gani yanawakabili katika upelelezi, kwa kweli hili ni tatizo kubwa na kila kukicha limekuwa likipigiwa kelele.

Upande wa pili ni mshitakiwa mwenyewe, wakati mwingine unachelewesha kuleta mashahidi mahakamani ila hali hiyo katika upende huu wa mshitakiwa hutokea mara chache mno.
Upande wa tatu ni Mahakama yenyewe, sasa kwenye Mahakama yenyewe kuna mambo ambayo yanasababisha kesi kuchelewa kusikilizwa. Uchache wa vyumba vya kuendeshea kesi na mfano halisi pale Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ina vyumba vinne tu vya kuendeshea kesi, hapa Mahakama ya Rufani ina vyumba viwili vya kuendeshea kesi. Sasa majaji ina wabidi wasubiriane kuendesha kesi na kesi nyingine zinachukua muda mrefu wakati zikiendeshwa.

Jingine linalochangia ucheleweshwaji wa kusikiliza kesi ni uhaba wa majaji na mahakimu, hili ni tatizo na hata kama unao mahakimu na majaji wengi, lakini vyumba vya kuendeshea kesi ni vichache kama ilivyo sasa hapa nchini, bado tatizo kesi kuchelewa kusikilizwa litakuwa pale pale.
Tatizo jingine la ucheleweshwaji ni uhaba wa nyenzo, leo hii hapa majaji na mahakimu kurekodi mienendo ya kesi kwa mkono badala ya kutumia teknolojia ya kisasa ya kurekodi sauti kama ilivyo kwa mahakama za nje. Kwa hiyo muda mwingi sisi majaji na mahakimu kuandika. Mfano Mahakama ya Afrika Mashariki, majaji wake wanatumia teknolojia ya kisasa ya kurekodi sauti.

Halafu pia katika hili la nyenzo, kutokuwepo kwa mfumo wa kompyuta ‘computerization’, unakuta jaji anaandika hukumu kwa mkono kisha hukumu hiyo inapelekwa kuchapwa kwa mchapaji sasa unakuta hukumu moja inaandikwa mara mbili. 
Kwa hiyo hayo matatizo niliyoyataja hapo juu yanachukua muda mwingi na si siri yanachangia ucheleweshwaji wa usikilizaji wa kesi kwa wakati.

Swali: Mahakama yako ina majaji, mahakimu na wataalamu wa kutosha kuweza kukabiliana na changamoto zinazoikabili sasa?

Jibu: Majaji, mahakimu na watalaamu katika mhimili wa Mahakama hawatoshi na kuna haja waongezwe kwa kuwa uchache wao nao ni sababu moja wapo inayopelekea ucheleweshwaji wa kesi.

Swali: Unazungumziaje madai kwamba kuna mahakimu hawana ujuzi wa kutosha na kwamba mishahara midogo wanayopata inawafanya baadhi yao wajihusishe na vitendo vya rushwa?

Jibu: Wakisema mahakimu hawana uzoefu wa kutosha nitawaelewa, siyo hawana uzoefu, hili nakataa kwakuwa mahakimu wote wamehudhuria kozi katika vyuo husika na kozi zao zinatofautiana kwa muda, kwani mahakimu wa mahakama za mwanzo na wilaya kozi zao huwa ni za muda mfupi tofauti na mahakimu wa Mahakama za Hakimu Mkazi, kwakuwa hao ni wanasheria kamili, ila nasema hivi kinachotakiwa hapa ni kwa mahakimu hao kupenda kujifunza zaidi kila mara bila kuchoka kwa kuwa elimu haina mwisho na mtu au kiongozi yeyote anayependa kujifunza mara kwa mara anapata fursa ya kujua vitu vingi na uzoefu wake unaongezeka na ninatoa changamoto kwa watendaji wote wa mahakama kupenda kujisomea na kuifunza.

Kweli mishahara ni midogo kama ilivyo sekta nyingi nyingine, lakini mishahara kuwa midogo siyo sababu ya mfanyakazi wa Mahakama kuchukua rushwa kwa sababu kuna wanaopata mishahara minono na kila kukicha wanapokea na kudai rushwa. Binafsi yangu nasema hivi rushwa ni urafi wa mtu binafsi.

Swali: Unaridhika na mfumo wa Mahakama ya Tanzania?

Jibu: Hadi sasa mfumo wa Mahakama hapa nchini unaridhisha ila nitahakikisha ninakaa na wenzangu kuona ni jinsi gani tunaweza kuuboresha zaidi.

Swali: Ni tukio gani unalikumbuka, liwe zuri ama baya katika maisha yako?

Jibu: Tukio ambalo sitalisahau lilikuwa ni kule kufiwa na baba yangu mzazi, Mathew Douglas Ramadhani, Machi mosi mwaka 1962, nilikuwa na umri wa mika 15, tukio hili lilinishtua sana na siwezi kulisahau kwa sababu nilikuwa bado mtoto mdogo, nilikuwa nikiwaza nani angenisomeshwa.
Tukio lililonifurahisha ni siku nilipomuoa mke wangu kipenzi Luteni Kanali Saada Mbarouk, ambaye anafanya kazi Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Nilifunga naye ndoa Novemba mosi mwaka 1975.

Swali: Ni kitu gani kilikutuma kujiunga na fani ya sheria?

Jibu: Nilipenda kusoma sheria kwanza pale Tabora Sekondari (Tabora School) nilipokuwa nasoma kuliwa na mwalimu akiitwa Butterworth, alikuwa akitufundisha somo la historia tangu kidato cha kwanza hadi cha sita, yeye alikuwa mwanasheria, sasa huyu vile alivyokuwa anazungumza ni tofauti na walimu wengine kwa namna alivyokuwa anabishana na kuchukulia mambo tofauti na walimu wengine.

Basi tangu hapo alinivutia na zaidi ya hapo marehemu baba yangu alisomea somo la sheria, alichukua shahada ya BA na moja ya masomo ya hiyo digrii ilikuwa ni sheria na nyumbani kulikuwa na vitabu vya sheria na katika maktaba ya nyumbani.
Lakini si hivyo tu baba yangu mzaa mama, Masoud Than, alikuwa mkalimani wa mahakama na babu alimlea mama Justine Dodo naye alikuwa mkalimani wa jaji enzi za ukoloni na kutembea naye miji mingi hapa Tanganyika. Sasa haya yote nalazimika kusema yalifanya nipende sheria na hadi nikaenda kuisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Swali: Unafikiri idadi ya wanawake waliobahatika kuchaguliwa kuwa mahakimu na kuteuliwa kuwa majaji wanatosha na kama hawatoshi nini kifanyike?

Jibu: Majaji na mahakimu wanawake hawatoshi na chakufanya Mahakama iwezeshe wanawake ili waweze kufikia vigezo vinavyotakiwa ili siku moja wateuliwe kuwa majaji au wachaguliwe kuwa mahakimu. 

Nasema kuwa idadi ya majaji wanawake ni ndogo, kwa mifano hai, mfano mmoja wapo unapatikana hapa Mahakama ya Rufani, mahakama hii ina jumla ya majaji 13 na watatu kati yao ni wanawake waliosalia ni majaji wanaume. Sasa hii ni tofauti kubwa sana.

Hapo awali Mahakama ya Rufaa ilikuwa na jaji mwanamke mmoja tu ambaye pia ni mwanamke wa kwanza kuwa hakimu hapa nchini anaitwa Eusebio Mnuo, na Rais Jakaya Kikwete alivyoingia madarakani akateua majaji wawili katika mahakama hii nao ni Jaji Natalia Kimaro na Engela Kileo.

Swali: Ni changamoto zipi zinaikabili Mahakama ya Tanzania?

Jibu: Changamoto ni nyingi, moja ya changamoto kubwa inayotukabili ni kutoa haki zote katika mashauri ya jinai na madai haraka, kupiga vita rushwa na suala la rushwa nalitazama katika sehemu mbili ya kwanza ni rushwa ya kweli na ya pili rushwa ya kudhaniwa.

Hivyo watendaji wa Mahakama wanatakiwa waweke juhudi kwamba kusiwepo na mazingira ya rushwa ya kweli na ya kudhaniwa. Na changamoto ya tatu inayoikabili mhimili mahususi wa Mahakama ni kuhakikisha haki inapatikana kwa watu wengi kwakuwa haki ina gharimu hasa inapokuja suala la mawakili, sasa tuhakikishe haki inapatikana kwa wote wenye madai yao mahakamani.

Swali: Hivi sasa kuna mchakato wa waumini na taasisi ya dini ya Kiislamu wanataka irejeshwe Mahakama ya Kadhi, nini msimamo wako na kama ikija itakaaje katika mtiririko wa mahakama?

Jibu: Kwa kweli kuhusu hili la Mahakama ya Kadhi siwezi kulizungumzia kwakuwa ninavyofahamu mimi suala hili lipo kwenye mchakato katika ngazi husika hata hivyo sina taarifa rasmi kama utekelezaji wa suala hilo umefikia wapi, hivyo binafsi siwezi kuzungumzia jambo kama sina taarifa za uhakika.

Swali: Huoni wakati umefika wa shughuli za Mahakama ya Tanzania kuendeshwa kwa Kiswahili ili wananchi waridhike na maamuzi yanayotolewa, kwakuwa hivi sasa mahakama zinaendeshwa kwa lugha ya Kiingereza na wananchi wengi wanaona hawatendewi haki na hasa unapofikwa wakati wa mawakili wa pande mbili wanapobishana kisheria wawapo mahakamani? 

Jibu: Nakubali kwamba ipo haja ya kuendesha shughuli za mahakama kwa lugha ya Kiswahili. Na kwakweli tayari limefanyika hilo la kuendesha mahakama kwa kutumia lugha ya taifa, sasa hivi mahakama za mwanzo zinaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili na sehemu kubwa ya Mahakama za Wilaya.

Lakini hata Mahakama ya Rufani tunaendesha Kiswahili inapobidi kuwa kanuni za Mahakama ya Rufani zinaruhusu kuendesha mashauri kwa Kiswahili au Kiingereza ila kumbukumbu lazima ziandikwe kwa lugha ya Kiingereza.
Na ninaamini ikitumika lugha ya Kiswahili mahakamani itaondoa manung’uniko ya wananchi na itasaidia watu waone haki inavyotendeka.

Swali: Huoni wakati umefika sheria zote za nchi ziandikwe kwa lugha ya Kiswahili kama ilivyo Katiba ya Tanzania ambayo ndiyo pekee imeandikwa kwa lugha ya taifa?

Jibu: Katika hili siwezi kusema wakati umefika kwa sababu hadi sasa hakuna maneno ya Kiswahili yaliyowekwa katika lugha ya kitaaluma ya sheria (many legal technical terms yet produced) yakipatikana hapo tunaweza kusema wakati umefika sheria za nchi ziandikwe katika lugha ya Kiswahili.

Swali: Wadhifa huu mpya wa ujaji mkuu, huoni kwamba unaweza kukuzuia usiendelee kupiga kinanda kanisani?

Jibu: Kwanza kabisa kupiga kinanda nachukulia kama ibada, yaani kama vile ninavyokuwa na uhuru wa kwenda kusali hivyo ninao uhuru wa kuingia kanisani na kupiga kinanda. 
Kwahiyo ieleweke uteuzi huu hautanizuia kupiga kinanda kwani hata nilivyokuwa Jaji Mkuu Zanzibar nilikuwa nahudhuria ibada na kupiga kinanda hata Jumapili ijayo (leo) nitakwenda kanisani St. Albano kusali na kisha nitapiga kinanda kama kawaida.

Enzi nasoma Tabora School ndipo nilipojifunza kupiga kinanda na mwanangu aitwaye Francis ndiye anayeonyesha kufuata nyayo zangu katika upigaji kinanda.
Licha ya kupendelea kupiga kinanda pia napenda kucheza mpira wa kikapu, na nimeanza kucheza mchezo huu tangu nasoma hadi nilivyokuwa ndani ya JWTZ niliupenda sana mchezo huu hadi nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tanzania Basketball Association (TABA, sasa BFT baada ya kuwa shirikisho) na mimi na wanamichezo wengine akiwemo Ofisa Habari na ofisa Utamaduni Manispaa ya Kinondoni Iddi Chaulembo, mwaka 1972 tulifufua chama hicho mkoani Iringa kitaifa.

Swali: Tueleze historia ya maisha yako kwa mapana?

Jibu: Nimezaliwa Desemba 28, mwaka 1945 Zanzibar mjini nikiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto wanane, wa kike wanne na wanaume wanne. Ni Mkristo wa dhehebu la Anglikana.

Nimesoma shule mbalimbali za msingi Mpwapwa mkoani Dodoma 1952 -1953 nikaenda Town School-Tabora nikasoma darasa la tatu hadi la nne mwaka 1954-1956 na darasa la sita na saba nilisoma Kazel Hill sasa inatwa Shule ya Msingi Itetemia mwaka 1957-1958. Na darasa la nane tu mwaka 1959 nikarudi kusoma Mpwawa.
Mwaka 1960-1965 nilijiunga na Tabora School kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza hadi cha sita. Kwakuwa nilifaulu nilichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1966, na nilisoma shahada yangu ya Sheria na ilipofika Machi 1970 nilihitimu masomo.

Na mwishoni mwa Machi mwaka huo huo wa 1970 nikajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), niliingia jeshini kama mwanasheria raia mpaka kipindi cha mafunzo ya kijeshi nikaenda kwenye mafunzo na kisha nikarudi kuitumikia JWTZ.
Ilipofika mwaka 1971 nikapewa kamisheni kambi ya Mgulani nikawa Luteni (nyota mbili). Nikaendelea na jeshi hadi mwaka 1977, nikahamishiwa Brigedi ya Faru-Tabora nikiwa na cheo cha Meja.

Sasa mwaka 1978, wewe mwandishi ulikuwa hujazaliwa, ndiyo mzee Aboud Jumbe Mwinyi, wakati huo akiwa ni rais akaniita Zanzibar na kuniteua kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar na kipindi hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Damian Lubuva.

Aidha Oktoba 1978 niliteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar. Na ilipofika Machi 1979 nilirudishwa JWTZ na baada ya muda mfupi nikapelekwa kwenye vita ya Uganda , nikiwa na cheo cha Luteni Kanali na kwenye vita hiyo nilikuwa naendesha mahakama za kijeshi.
Vita ilipokwisha nikarudi Zanzibar. Januari 8 mwaka 1980 nikaapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar, wakati huo nikiwa na cheo cha Luteni Kanali. Nikaendelea na Ujaji Mkuu Zanzibar hadi Septemba 1989 alipoapishwa Jaji Mkuu Zanzibar Hamid Mahamod Hamid.

Hata hivyo Juni 23 mwaka 1989 niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania hadi mapema wiki hii nilivyoteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Nilipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani hapa Bara ndiyo sababu ya kuacha ujaji Mkuu Zanzibar.

Januari 1993 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na niliendelea na nafasi hiyo hadi Januari 2003 na Oktoba 2002 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambapo kipindi changu cha miaka mitano katika tume ZEC kinamalizika Oktoba mwaka huu.

Mwaka 1997 nilistaafu JWTZ nikiwa na cheo cha Brigedia, na niliagwa kwa heshima zote za kijeshi licha sikupewa mafao yangu kwakuwa mafao hayo yameunganishwa kwenye kazi yangu ya ujaji hivyo mafao yangu yote nitalipwa wakati nikistaafu kazi hii ya Ujaji Mkuu, kama mungu atanipa uzima.

Novemba 2001, niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki nafasi ambayo natakiwa nimalize kipindi changu cha miaka sita Novemba mwaka huu.
Nina mke mmoja ambaye Mungu ametujalia tumebahatika kupata watoto wanne, wawili ni wasichana na wawili ni wavulana. 
Mtoto wangu wa kwanza anaitwa Francis (30) huyu ni mwanasheria na anafanyakazi ya uwakili Manchester, Uingereza, Brigeth, huyu ana shahada ya Uandishi wa Habari na anafanyakazi ICAP hapa nchini, Marina ni mfamasia, yuko Liverpool, Uingereza na Mathew naye ni mfamasia, anafanya kazi Liverpool.”

Blog: www.katabazihappy.blogspot.com

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Julai 22,2007.

Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Juni 18 Mwaka 2015.

MFAHAMU KWA UNDANI  JAJI AUGUSTINO  RAMADHANI 

Juni 1Mwaka 2015.