SAMIA SULUHU HASSAN "STYLE"











Na Happiness Katabazi

SAMIA ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushika wadhifa wa mgombea mwenza wa Chama hicho Katika mchakato wa kumpata mgombea Urais wa CCM uliomalizika Julai 12 Mwaka huu Mkoani Dodoma ,tangu  CCM ilipozaliwa rasmi Mwaka 1977.

Uteuzi huo ni sifa kubwa kwa sisi Wanawake kwasababu imethibitisha pasiposhaka Kuwa Kumbe wanawake  tunaweza na tu nauwezo.

Pili imethibisha  kile kilio cha wanawake cha muda mrefu cha kutaka wanawake nao wamepewa nafasi za juu za uongozi ndani ya vyama siasa ,serikalini na kwenye taasisi zingine kimesikika kwa kikishindo kwa chama dola CCM kumteua Mwana mama Samia ambaye ni msomi,asiyena na makuu ,mwenye Hekima,Mzalendo,Mzoefu Katika siasa za CCM na ameishapata  fursa ya kushika nafasi ya ubunge katika jimbo la Makunduchi Zanzibar,  Waziri hapa  Tanzania Bara na Zanzibar kupewa nafasi hiyo.

Uchaguzi Mkuu wa taifa letu uliopangwa kufanyika Oktoba Mwaka huu, na CCM ikifanikiwa  kupata ushindi , basi Samia atakuwa  ndiye Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wa kwanza mwanamke tangu Tanzania ipate Uhuru wake Mwaka 1961. Na hivyo ndivyo itakavyokuwa ,tuombe uzima na historia hiyo mpya ya Tanzania Kuwa na Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke itaandikwa Kwenye vitabu Vya Kumbukumbu na Kwenye vichwa Vya watu wanaofikiri Sawasawa.

Binafsi Leo natangaza wazi kupitia ukurasa wangu huu Kuwa Nitamuunga mkono Samia na Patna wake "Bwana Pombe " yaani John Pombe Magufuli ambaye ni Mgombea urais  kwa tiketi ya CCM Katika safari Yao ya " Ukweli" waliyoianza rasmi Julai 12 - Oktba 25 Mwaka huu.

Nawaamasisha  Watanzania wote wanaofikiri Sawasawa Kumuunga mkono Mwana mama Samia Mwanamke  Mtanzania  wa asili ya Zanzibar na Patna wake Bwana Pombe yaani Magufuli.

Nimefanya utafiti wangu nimebaini Samia ni mwanamke anayependa kufunika kichwa chake kwa hijabu,vilemba ikiwemo aina hiyo niliyojitanda Mimi kichwani Katika hii picha yenye sura yangu.

Hivyo kwa wale wanawake wenzangu  ambao  hawana tabia za kuchukia wanawake wenzao pindi wanapoona wanawake wenzao wamefanikiwa kupata madaraka, mali,Fedha siku Moja Moja ikiwa ni Kumuunga mkono mwanamke mwenzetu Samia Katika Safari yake ya Kweli.

Tuwe tunajitanda ushungi wa aina anayependa kujitanda Samia ikiwa ni Ishara ya Kumuunga mkono nakuonyesha Sisi wanawake wa Tanzania Bara,tupo nae sambamba kwasababu Samia ni Mzanzibar na tukifanya hivyo pia kwa njia Moja au nyingine tutakuwa tunauenzi Muungano wetu ambao kwakweli ni wa aina yake licha kuna Mahasidi wachache wanataka Muungano Uvunjike na Hilo haliwezekani.

Mungu Ibariki Tanzania

Chanzo: Blogg: www.katabazippy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
22/7/2015.

ANSBERT NGURUMO CHALI





Na Happiness Katabazi

NGURUMO ni Mwandishi wa habari Mwandamizi nchini na ni Mwandishi wa Safu maarufu ya "MASWALI MAGUMU "  Katika  Gazeti la Tanzania aliwai Kuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti  hilo na ni miongoni mwa waandishi waanzilishi wa Gazeti Hilo la Tanzania Daima.

Ngurumo alikuwa  ni mgombea Ubunge ndani ya Chadema jimbo la  Jimbo la Muleba Kaskazi Mkoani Kagera. Jimbo Hilo lilikuwa likiongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage.

Leo umefanyika uchaguzi wa kula za maoni wa Chama hicho na kwa upande wake ameshindwa kutimiza ndoto yake ya Kuwa mbunge baada ya kuangushwa  vibaya na mpinzani wake ndani ya Chama hicho aitwaye  Injinia Najim Kassange kula 247 na Ngurumo amepata kula 55. 

Kwa Matokeo hayo ni wazi zile ndoto za Ngurumo kwenda Bungeni zimeyeyuka. 

Ila Chadema na nyie hata huruma kidogo hamna kwa kaka yangu? Kuwapiganieni kote kule kupitia makala zake lakini mmempa za uso?

Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu mwishoni mwa wiki alikuwepo huko jimboni kaja kumnadi Ngurumo na akamsifia sana  ni kiongozi makini lakini mkapuuza Lissu na Leo mkambwaga vibaya hivi Ngurumo?Aisee Mnatisha sana  Chadema Muleba Kaskazini.

Pole Ngurumo hiyo ndiyo siasa na hiyo ndiyo Demokrasia, nisisikie unahama CHADEMA eti kwasababu hujapitishwa  Kuwa Mbunge, vumilia huko huko.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi.
21/7/2015

LOWASSA UMEPIGWA KWENZI NA DOLA LA CCM ,BONYEA



Na Happiness Katabazi

KWA zaidi ya wiki Moja sasa kumekuwa na taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na mhusika ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM),Edward Lowassa kuwa anakusudia kuamia  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA).

Taarifa hizo zimekuja ikiwa ni siku Chache tu tangu CCM imalize mchakato wake Julai 12 mwaka huu, wa kumpata  mgombea urais ambapo Lowassa wenzake kushindwa kufikia hatua ya tano bora hali iliyosababisha wafuasi wake akiwemo Mbunge wa Songea Mjini,Dk.John Nchimbi,Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kujitokeza hadharani kupinga mchakato ule na Kudai  Kanuni za CCM zilivunjwa na wengine wameamua kuamia  Chadema.

CCM waliitimisha mchakato wao kwa kumpata Mbunge wa Chato,John Pombe Magufuli Kuwa mgombea wao wa urais na mgombea mwenza  ni Samia Suluhu Hassan.

Kwanza nataka Ieleweke wazi kuwa kila Mtu ana Haki ya kujiunga na Chama chochote za siasa  na haki hiyo umewekwa Katika Ibara  ya 20 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 , inasomeka hivi; 

"Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo."

Hivyo basi Kama taarifa hizo zinaukweli basi Lowassa atakuwa anatumia haki yake hiyo ya Kikatiba ya kujiunga na Chama cha siasa anachokitaka.

Waswahili wanamsemo usemao lisemwalo lipo Kama halipo linakuja na Dalili za Mvua ni mawingu,Dalili hizo Tumeanza kuziona kwa Mbali .

Ushauri wangu kwa Mzee Lowassa Kuwa Kama kweli anawazo hilo la kuama CCM kwenda Chadema kwasababu CCM haijapitisha Jina lake Kuwa mgombea  urais ,aliache  wazo Hilo Mara Moja Kwani halitakuwa na manufaa kwake  binafsi na familia yake .

Halitakuwa na manufaa kwake  kwasababu wewe Lowassa amekaa ndani ya serikali,CCM kwa muda mrefu sana, anafahamu  jinsi hivyo vyombo viwili vinavyofanyakazi zake .

Kama utaamua kuama CCM kwenda upinzani ujiandae kukabiliana na Changamoto zifuatazo Kesi mbalimbali na karaha mbalimbali.Je upo Tayari Katika Hilo? Na Je Una ubavu wa kuvumilia vibweka hivyo?

Lowassa usisikitike sana jina Lako kutopitishwa na CCM, bali kaa chini utafakari ni kwanini Hilo lilitokea. 

Je ulikidhi  vigezo? Na Kama  Kanuni zilipindishwa ,kwanini basi  Mungu alishindwa Kuzuia uhuni huo usitendeke na Kanuni zisivunjwe?

Kwa wanasiasa ninavyowajua wanasiasa wa nchi hii walivyotawaliwa na mizengwe tena wakati wa uchaguzi hata kama mlikuwa ni marafiki uwa manageukana utafikiri hamjawahi kufahamiana na kushughulikiana Kavu Kavu.

Hivyo kwa Kuwa wewe Lowassa na genge lako la kampeni mlikuwa mkianza vitendo Vya kuvunja Kanuni wakati mwingine hali iliyosabisha Kuzua mjadala Katika Jamii,uenda basi Ndio maana viongozi wako wa CCM nao wakaamua kutumia kile kinachodaiwa na wafuasi wako 'uhuni ' kukata jina lako  maana wakati mwingine mtu mwenye mamlaka unaweza kutumia njia za kihuni kutoa maamuzi dhidi ya Mtu mhuni idi mradi tu nchi Inakuwa salama.


Mapema kabisa nilikushauri kupitia makala zangu Kadhaa zilizokuwa na kichwa Cha Habari ( LOWASSA UWEND URAIS UTAUSIKIA REDIO TBC1) na (MADA SITA CCM  HAMMO KWENYE URAIS),hukuta kunisikia hadi yaks kufika yaliyokufika ambayo yamekusababishia majeraha moyoni.


Lowassa je uoni  hayo yaliyokufika ni malipo ya Mwenyezi Mungu kwako?Maana Kama Mungu angetaka CCM ipitishe jina Lako CCM ingelipitisha.

Kwa tunaofuatilia siasa za nchi hii kwa wazi na Siri Minasema yaliyomkuta Lowassa kule CCM alistahili .

Tujikumbushe Wimbo iliotungwa na mwanamuziki wa Muziki wa Dansi nchini,Ally Choki ' Mzee wa Farasi' usemao Mtenda kanitendewa .Baadhi ya maneno yaliyomo  ndani ya wimbo huo ni ;

" Mtenda akitendewa uisi kaonewa Yale yote aliyofanya uwa yanamrudia ....mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu unauma...aliyoyatenda yeye yote kasahau...malipo ni hapa hapa Duniani Eeeh,usimzalau Mkunga na uzazi ungalipoo Aaah...."

Mzee Lowassa Maudhui ya Wimbo hayo yatafakari sana naninaomba yakurejeshe Mwaka 2005 Katika Kipindi cha mchakato wa kumsaka mgombea urais CCM, wewe Lowassa na genge la wahuni maarufu la Wanamtandao mlishiriki kikamilifu wakati mwingine kuwachezea rafu baadhi ya wagombea wa CCM akiwemo Dk.Salim Hamed Salim,Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye na Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara,John Malecela kuwachafua chafua kupitia baadhi ya waandishi wa habari mliokuwa mmewaweka mfukoni  kupitia vyombo Vya Habari .

Hali iliyosabisha Dk,Salim ,Malecela,Sumaye kunuka kwa uzushi tu ambao ulikuwa ukienezwa na genge la wahuni la wanamtandao ambao wewe Lowassa ulikuwa Mfuasi Mtiifu wa genge Hilo ambalo hivi sasa genge Hilo limesambaratika na wafuasi wa genge Hilo wamekorofishana wamekuwa ni maadui wa kuitisha na wanalaluana wao Kwao.

Dk.Salim aliizushiwa siyo Raia wa Tanzania na alikuwa Mwanachama wa Chama Kimoja kule Zanzibar ambacho kilikuwa kinapingana na serikali iliyokuwa madarakani ,wakati Sumaye aliizushiwa kajilimbikizia mashamba na amepora mashamba ya wananchi Mkoani Morogoro ,na pia ameficha Sh.Tilioi  Tatu Kwenye Akaunti yake.

Hali iliyosababisha Dk.Salim ,Sumaye Kufungua kesi Katika Mahakama Kuu Kulishitaki Gazeti la Mwananchi na Tanzania Leo kwa kuchapisha Habari hizo za uongo na viongozi Hao walishinda Kesi hizo .

Na Hakuna kitu kilichonifurahisha hapa nchini Kama genge Hilo la wahuni maarufu Kama Wanamtandao liliposambaratika na hivi sasa Ndio limekufa kabisa Kwani endapo genge hili lisingesambaratika hivi sasa Kama taifa tungekuwa  Katika Hali Mbaya Kwani liliumiza watu ambao wengine walikuwa hawana hatia kwasababu ya Sababu zao kijinga na kihunihuni tu .

Sasa kwa mazingira hayo ya Kuwa Kwenye kundi liloshiriki kuwashuhudia wenzao uzushi na uongo, kwanini Isifike mahali Mungu nae akalipa kisasi kwaniaba ya Hao walioumizwa na kundi la wanamtandao Mwaka 2005 kwako  wewe Bwana Lowassa Katika mchakato wa CCM 2015?

Minakushauri Lowassa ukae chini utulize akili zako vizuri ,ujielewe Kuwa wewe ulishawahi Kuwa Waziri Mkuu,waziri ,mbunge na Mwana CCM wa muda mrefu Na hii siyo Mara yako ya kwanza jina Lako kuenguliwa na CCM Katika mchakato wa Kugombea urais .Mara ya kwanza ilikuwa Katika uchaguzi wa CCM Mwaka 1995 jina Lako lilikatwa ulipogombea urais CCM ulitulia.

Na hadi sasa bado unapata Stahili zako toka serikalini na utambue wewe pia ni mfanyabiashara ,unamke,watoto na Una ndugu na Jamaa wanakutegemea na bado wanakuitaji ili uwa saidie  wakiwemo baadhi ya wabunge waliokuwa Kwenye kambi yako kufa na kupona ila hawafiiki kichinichini wewe kuamia Chadema wanasema Katika Hilo hawatakuwa pamoja na wewe.

Lowassa utambue Kuwa huna nguvu ya asili ya kukubarika na ndani na nje ya Chama  Kama aliyokuwaga nayo Mwenyekiti wa Chama CHA NCCR - Mageuzi enzi hizo, Augustine Mrema ambaye alikuwa akipendwa na watu Wengi tena bila kutoa Fedha wala kutoa ahadi za kuwapa watu vyeo wala kuzungukwa na watu wanaosaka madaraka na wale waganga wa serikali ya awamu ya nne Kama ulivyozungukwa wewe na watu wa aina hiyo.

Lowassa Kama kweli unataka kuamia Chadema, ukumbuke ni Katibu wa Chadema, Dk.Wilbroad Slaa Katika Viwanja Vya Mwembeyanga Temeke Dar Es Salaam, na Katika maeneo mengine amenukuliwa akikuita wewe Lowassa ni fisadi wa mali za umma.

Na siyo peke yake ,pia baadhi ya wafuasi wa Chadema nao wamekuwa wakikuita wewe ni fisadi uliopindukia, sasa eti ghafla CCM imekata jina Lako Leo hii wafuasi wa Chadema tena wengine ni viongozi wa juu wa Chama hicho n marafiki zangu wanajitapa kwakukusifu Lowassa ni mtu safi na wanamsubiri Chadema.

Minimewauliza hao baadhi ya viongozi wa Chadema wanawazimu kichwani au wanamatege ya akili?

Nimelazimika Kuwauliza maswali hayo kwasababu hadi sasa Hakuna mahala  popote panapoonyesha  Chadema imekusafisha  Lowassa Kuwa ni Mtu safi na siyo fisadi tena Kama walivyokuwa wakimuita awali.

Lowassa Kama kweli unataka kuamia Chadema, jiulize kwanini Leo Chadema wanaokuona ni Mtu safi,una sifa za kiongozi bora?

Je kwakuwa wameona una wafuasi Wengi ndani ya CCM na una wafadhili Wengi wenye Fedha wanaokufadhili Katika siasa zako Ndio maana Chadema hivi sasa Ndio wanakutaka uamie Katika Chama chao?

Tumewasikia hao Madiwani na wana CCM   waliojiunga na CHADEMA wiki iliyopita wamesema wameamua kuama CCM kwasababu eti Lowassa amekutwa jina lake.

Swali langu Je ikitokea kweli ukaamia Chadema nako huko Chadema wasipopitisha jina Lako ,wewe na hao wafausi wako Mtaama Chadema kwenda Chama gani kingine?

Minaisi hawa wanaojiita ni wafuasi wako uwenda sio wazima katika vichwa vyao.

Najiuliza hivi CCM walijiunga kwaajili tu Lowassa lazima apitishwe jina lake na lisipopitishwa Ndio wanaama Chama ?

 Basi hao wafuasi wako ni madikteta ambao wanataka uamuzi wao tu na wala hawaheshimu uamuzi wa mamlaka ya Chama chao Cha CCM na Kama ni hivyo basi hawana nidhamu?

Mzee Kingunge Yule pale amepinga mchakato uliompata mgombea urais CCM lakini hatujamshuhudia akihama CCM.

Siwezi kumbeza kirahisi rahisi  Mzee Kingunge kwasababu naamini Kingunge ni mtu mzima Anaujua mazuri na Mabaya yote  yanayofanywa  na CCM wakati wa uchaguzi ,hivyo Mzee Kingunge uwenda anajua kilichofanyika Katika mchakato uliompata mgombea urais CCM Mwaka 2015 ambao Mimi na wengine hatuji Je ni kweli Kanuni zilivunjwa au laa Kwani ukweli wanaujua wao wenyewe.

Hata hivyo mapema kabisa Kabla ya CCM kupitisha jina la mgombea Kingunge ambaye yeye alitangaza na kusema anamuunga mkono Lowassa na  alitahadharisha  Kuwa kuna Dalili chafu za CCM kupitisha jina la mtu asiye kubalika na Wengi na kukata Majina ya watu wanakubalika Hali ambayo itasababisha vurugu.

Na ndivyo ilivyokuwa CCM ilitumia vigezo vyao ikampitisha Magufuli mgombea ambaye watu walikuwa hawampi uwezekano mkubwa wa kushinda Kama Lowassa,Membe na hivyo kufanya Lowassa ,Membe ambao walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushindwa na Kuwa na wafuasi Wengi kutopitishwa na CCM  .

Hali iliyosababisha watu wanaodaiwa ni wafuasi wa Lowassa kufanya fujo na Jeshi la Polisi kuweka Ulinzi mkali  katika  Mji wa Dodoma wakati vikao hivyo Vya CCM vikiendelea na Katika Kikao cha NEC baadhi ya wajumbe wakati Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete akiingia Katika mkutano ule walikuwa wakiimba   Wimbo wa ' Tunaimani na Lowassa" Hali iliyosababisha Kikwete akiri Kuwa Hali hiyo haijawahi kutokea.

Hata hivyo mchakato ulimalizika salama Magufuli amekubalika na watu Wengi kwasababu Hana rekodi chafu na anauzika kwa wananchi vizuri tu na kwakuwa Watanzania Wengi ni Kama tuna ubongo wa Ndezi tumeishasahau vibweka vilivyotokea Dodoma  Katika kumpata mgombea urais wa CCM ,tu naendelea na mambo mengine ila baadhi ya watu wacheche bado wanavinyongo.

Sasa hiyo kambi ya Lowassa iache nongwa Kama ndugu wa mume,ikubali Matokeo yaliyotokea na iache kumjaza Ujinga Mzee Lowassa wa kuama CCM kwenda Chadema.

Kwasababu ushauri wa kuama CCM ni  wa Kikatiba ila siyo mzuri kwa Lowassa Mwenyewe Kwani mwisho wa siku atakayekuja kuumia Moja kwa Moja ni Mzee Lowassa na siyo wapambe wake. 

Wapambe wake mwisho mwisho wa siku  watamkimbia Kama baadhi ya wapambe wake walivyoonza kumkimbia hivi sasa.

Aidha hakuna ubishi kuwa Lowassa alikuwa na kundi kubwa ndani ya CCM lilokuwa likimuunga mkono naliliumiza sana watu vichwa,na baadhi ya wafausi wa kundi la Lowassa ukizungumza nao mitaani wanasema kitendo cha CCM kukata jina la Mpendwa kimewavunja moyo na kimesababisha wamepoteza mahaba kwa CCM na kwamba hawataipigia kura CCM.

Kauli hizi sio njema kwa CCM,binafsi nashauri  wazee wa CCM kwa muda wao wamtafuta Mzee Lowassa wazungumze nae kiutu uzima ili amrishe wafuasi wake wa achane na kinyongo cha yeye kukutwa Kisha Lowassa awaambie wafuasi wake waiunge mkono CCM.

Halafu Nyie Kambi Lowassa kwa taarifa yenu kambi zilizopaswa Kulalamika sana ni kambi Kama za waliokuwa wagombea urais mfano kambi ya Makamu wa Rais, Dk.Mohammed Gharib Bilal,Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhan ,Profesa Sospiter Muhongo  na kambi nyingine ambazo wagombea wake walikuwa hawana rekodi chafu za tuhuma Kama alivyo Lowassa ambaye hadi CCM ili muweka kifungoni yeye ,Januari Makamba na Bernad Membe.

Lakini Dk,Bilal, Professa Muhongo,Mizengo Pinda Walikatwa Majina yao Kama wewe Katika hatua za awali kabisa hata tano bora hawajaingia licha siku tatu  kabla ya kukatwa Majina Yao Boss wako ,Rais Kikwete alikuwa akisimama Katika majukwaa mbalimbali akimsifia  Waziri Mkuu wake, Makamu wake wa Rais Kuwa ni  viongozi wazuri sana,wamemsaidia sana Kazi na wana sifa hasa za uongozi.

Lakini Kikwete huyo siku mbili baadae aliongoza 'wachinjaji wenzake' kule Dodoma katika vikao vya CCM na kuchinja majina ya wasaidizi wake hao wawili ambao alikuwa akiwasifia sana kwa kile kilichodaiwa kuwa sababu ya kuwachinja viongozi hao kuwa wana umri mkubwa.

Lakini hatujasikia mahali popote wafuasi wa kambi hizo wakitangaza kuama CCM eti kwasababu wagombea wao Walikatwa Hatua za awali kabisa hata tano Bora Majina Yao hawajapelekwa yakapelekwa Majina matano yakiwemo majina mawili ya waliokuwa Wafungwa wa CCM ya Makamba na Membe.


Lowassa usiame CCM kwenda Chama chochote cha upinzani  kwa kigezo eti CCM haijakupitisha kuwa mgombea urais ,ukifanya hivyo utajimaliza Mwenyewe kisiasa na hao wa naokushauri Leo hii  uame CCM ndiyo watakuwa wakwanza kukucheka na kukubeza .

Lowassa nafahamu una mchango mkubwa ndani ya serikali,CCM na siwezi kukubeza Katika Hilo na ninaheshimu mchango wako licha Una madhaifu yako pia ya kiutendaji.Narudia tena Mzee Lowassa kukushauri Tulia,usiame CCM.

Usifanye maauzi mazito Kama hayo wakati bado una makandokando. Tulia hiyo Hali ya uchungu uliyonayo ya CCM kutopitisha jina lako itakwisha,utasahau na utakubaliana na Hali  halisi .

Mbona Mwaka 2008 Bunge lilikushinikiza ujiudhuru wadhifa wa Waziri Mkuu kwa kashfa ya Mkataba wa Richmond , na ulichafuka kila kona ukajiudhuru Uwaziri Mkuu ukukaa pembeni lakini baadae nyota yako ikaja kung'ara.

Ni magumu mangapi umeyapitia na Mungu akakupa moyo wa kuvumilia na ukayavumilia? Kuna watu walijiapiza hapa Kuwa hutafika ukiwa hai Katika uchaguzi wa urais CCM Mwaka 2015 lakini Mbona umefika na ukashiriki ukiwa hai na bado upo hai?

Ila Mikasa yote hiyo inayokukuta Ndio iwe Funzo kwako na kwa wana CCM wenzio kuacha tabia chafu za kuwafanyia mizengwe wenzenu ndani ya Chama serikali kwani mliowafanyia mizengwe na hira nao walilia na kumshitakia Mungu wao na Mungu alisikia kilio chao ndio anawalipia kwa mtindo huo wa kuruhusu mpate mabalaa ya kila aina  yakiwemo kukosa nafasi mnazowania, maradhi ya kila namna.

Na Kama Madai haya yanayotolewa na Mzee Kingunge, Dk.Nchimbi, Kimbisa, Dk.Mzamili Kalokola,Sophia Simba yanayodai CCM inayoongozwa na Rais Kikwete ilivunja Kanuni Katika kumsaka mgombea urais CCM Mwaka huu ni ya kweli basi minaamini malipo ni hapa hapa Duniani,Kama alivunja Kanuni kwa makusudi basi ajiandae naye kupokea malipo yake hapa hapa Duniani na Kama Madai hayo sio ya kweli basi Mungu at ambariki.

Niitimishe kwa kumwambia Lowassa umepigwa  Kwenzi na dola la ccm ,Bonyea chini,yaani utulie na utambue kila likuepukalo   Lina kheri kwake na siyo lazima  awe rais wa Tanzania.Ukizingatia ushauri wako haya usipouzingatia shauri zako.

Mungu ibariki Tanzania
Facebook: Happy Katabazi
20/7/2015.






BANZA STONE LEO KAFARIKI KWELI


Na Happiness Katabazi


MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa Dansi nchini, Ramadhani Masanja "Jenerali  Banza Stone " amefariki Dunia hivi punde nyumbani kwao Mtaa wa Sinza D,Dar Es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mrefu na hivi sasa mwili wake unapelekwa kufadhiwa Hospitali.

Sisi watoto tuliokuwa na Banza Kata ya Sinza Dar Es Salaam, tuliishi vyema na Banza Kabla ajaanza kuugua na hadi alivyoumbukwa NA Maradhi.
Binafsi siku zote uwa name heshimu kubwa Banza pamoja na mapungufu yake ya kibo adabu ambayo yalisababisha Katika Uhai wake ajiingize Kutenda baadhi ya matendo Katika Jamii ambayo hayakutupendeza sisi wana Sinza wenzake na mashabiki wake wa muziki.

Daima Nitamkumbuka Banza,kwasababu Banza ni miongoni mwa watu mahususi walioshiriki kuitaka Kata ya Sinza kupitia taaluma yake ya muziki Kwani baadhi ya Nyimbo zake alikuwa  eneo la Sinza Hali iliyosababisha eneo la Sinza Kuwa ni eneo maarufu sana.

Banza alikuwa ni rafiki mkubwa wa Kaka yangu Liston Mwesiga Katabazi.
Banza ulishindwa kwenda sambamba na Maudhuhi ya Wimbo wako wa KUMEKUCHA.Ndani ya Wimbo huo kuna maneno yake mayo ' Unapotaka kuanza Maisha Anza sasa usisubiri Kesho Kwani Utamkuta Mwana siwako Oooh,upatapo fahamu Jua Umepotea kweli Umepotea.

Wimbo huo naupenda sana kuliko Nyimbo zake zote alizowahi kuimba Banza.

Pole familia ya Banza na wapenzi wa muziki wa dansi na wakazi wenzangu wote tunaoshi Kata ya Sinza .

Mungu aiweke roho yake mahali panapostahili.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
 17/7/2015.

WABUNGE UKAWA WALIOADHIBIWA NI WAHUNI TU



Na Happiness Katabazi

NENO Mhuni Utumiwa kupachikwa Mtu yoyote anayefanya matendo ambayo Si ya kistaarabu na kuungwana Mbele ya Jamii iliyostaarabika ,heshimika na inayojari Utawala wa sheria na Kanuni na asiye heshimu mamlaka wala kiongozi anayemuongoza mahali pake pa Kazi.

Nimelazimika kutumia neno la Mhuni kwasababu makala yangu ya Leo Inajadili uamuzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa Adhabu ya kuwasimamisha idadi hiyo ya wabunge kutoudhuria Katika vikao Vya Bunge vilivyosalia kabla ya Julai 9 Mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge Hilo baada ya wabunge Hao Kukiri Kutenda vitendo Vya kihuni (utovu wa nidhamu ) ndani ya Bunge.

Baada ya kuwakuta na hatia kushindwa kuheshimu Kiti cha Spika na kupiga makelele ovyo Mithili ya watu waliopandisha Mapepo au wagonjwa wa Maradhi ya akili.

Spika Makinda alisema ametumia Kifungu cha 74(1) cha Kanuni za Bunge kuwadhibu wabunge hao.

Bila kumung'unya maneno Mimi binafsi nawaita wabunge hao WAUKAWA  ni wahuni kwasababu  mhuni siku zote ni mtu asiyetaka kuheshimu Sheria na Kanuni na kufanya vitendo vya kihayawani ambavyo  vinamshushushia heshima hata yeye binafsi Mbele ya watu waliostaarabika.

Hivyo wabunge hao wahuni ,uhuni ule walioufanya ndani ya Bunge wakuoiga makelele utafikiri wamekumbwa na Mapepo wachafu 'Mashetani" siyo tu umelipaka matope Bunge letu Kuwa Kumbe ndani ya Bunge letu tuna wabunge (watunga Sheria/Kanuni) ni wahuni,na uwenda wana Kichaa cha muda ' Temporaly Insanity' ambao hawajui Sheria na Kanuni wanazozitunga na hawaziheshimu na ni vinara wakazivunja na Spika Makinda amekiri Hilo Kuwa Bunge hilo la 10   Lina malizika lakini wabunge Wengi hawajui Kanuni. Nimechoka kabisa.

Maana Mtu mwenye akili timamu kichwani hawezi kufanya ushenzi uliofanywa na wabunge Hao wa UKAWA ndani ya Bunge. Ni ayawani na MTu mwenye wazimu kichwani ndiyo anaweza kufanya uhuni ule wa kupiga makelele ndani ya Bunge na kudharau mamlaka ya Spika wa Bunge kwa Kiwango kile kilichofanywa na wabunge hao wahuni toka UKAWA wiki iliyopita ambao Kutwa wamekuwa walijinasibu Kuwa wanaweza kuongoza Tanzania.Ajabu.


Zaidi ya  Wabunge  40 wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni (Ukawa), wamepewa adhabu ya kutoingia vikao vyote vya bunge hadi litakapovunjwa na Rais, Julai 9, kulipwa nusu mishahara na posho.

Jumla ya wabunge wa upinzani  90, waliotolewa siku ya kwanza (Julai 3) ni 11, na Julai 4 ni 35 hivyo kufanya idadi ya waliofukuzwa kuwa 46, huku 43 ambao hawakuwepo ndani ya Bunge kutoguswa na adhabu hiyo. 


Hatua hiyo imefikiwa baada ya wabunge hao kuwa kwenye harakati za kupinga miswada mitatu ya mafuta na gesi, kuingizwa bungeni kwa hati ya dharura na kujadiliwa kwa pamoja. 

Julai 3 Mwaka huu. wabunge 11 walitajwa kwa utovu wa nidhamu Bungeni, na kati yao, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini na Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa, wamepewa onyo baada ya kujutia makosa yao.

Waliotimuliwa Ijumaa iliyopita  ni John Mnyika (Ubungo), Tundu Lissu (Singida Mashariki) na Pauline Gekulu ( Viti Maalum) wote wa Chadema.
Wengine ni Filex Mkosamali (Muhambwe) na  Moses Machali (Kasulu Mjini) wa NCCR-Mageuzi.Wabunge  wawili wakipewa adhabu ya kutohudhuria vikao viwili.

Miswada iliyozua mtafaruku ni ule wa Sheria ya Petroli wa mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa mwaka 2015 na Muswada wa Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji wa mwaka 2015.

Spika Anne Makinda akifafanua hoja hiyo, alisema wabunge hao hawajui kanuni, "nilitamani mjue kusoma kanuni, nilifikiri mnajua kumbe tunamaliza kipindi wala hamjui, mngekuwa mnajua utaratibu wa kupinga kikanuni upo, tumefanya miswada mingi sana inasomwa kwa wakati mmoja...nipeni muda niwaletee orodha ya miswada hiyo."

Alisema kanuni zinaruhusu kwa kuwa maudhui ya miswada ni mmoja, hivyo hakuna kanuni iliyovunjwa.

Spika Makinda alisema kuwa ametumia kanuni ya 74(i) kuwatimua wabunge hao kwa kushindwa kuheshimu kiti kwa kupiga kelele.

Kwa siku tatu mfululizo, Spika Anne Makinda amekuwa akipata shida kuendesha chombo hicho cha kutunga sheria kutokana na mbinu waliyogundua wapinzani ya kupiga kelele kukwamisha shughuli za Bunge.

Ijumaa iliyopita Spika Makinda,  aliamua kuwapeleka wabunge 11 mbele ya Kamati ya Maadili kwa makosa ya kudharau kiti chake na chombo hicho kikaibuka na adhabu ya kuwafungia wabunge wanne kutohudhuria vikao vyote vilivyosalia, wengine wawili kufungiwa vikao viwili.

Hakuna ubushi Kuwa Bunge hili lililoongozwa na Spika Makinda tulishuhudia mazuri na vitendo Vya utovu wa nidhamu Mara kwa Mara vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya wabunge ambao hawa jiheshimu kwahiyoa lugha zisizofahaa na kubishana na Spika wakati mwingine bila kuwepo na Sababu za Msingi za kufanya hivyo.

Tulimshuhudia Spika Makinda na hiyo Kamati yake wakiwachekea sana na kulea vitendo vile Vya kihuni vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya wabunge ikiwemo Kuzusha vurugu ndani ya Bunge na kusababisha vikao Vya Bunge kuahirishwa   kwasababu ya  vurugu, matumizi ya lugha chafu hali iliyosababisha heshima ya Bunge letu kuporomoka na Makinda kushindwa kuwachukulia Hatua na Kuishia Kulalamika tu utafikiri kulikuwa Hakuna Kanuni za kuwashughulikia wabunge wahuni wanaovunja Kanuni.

Hali iliyosababisha baadhi ya watu kuanza kumhisi vibaya Spika Makinda Kuwa enda Ananufaika na vitendo hivyo Vya kihuni na utovu wa nidhamu uliokuwa ulifanywa na baadhi ya wabunge Ndio maana Bunge lake lilikuwa linashindwa kutumia Kanuni kuwashikisha adabu.

Na baadhi ya wasomi Washeria chinichini walifika hatua ya Kusema kuna haja ya kufanyika Mabadiliko ya Kikatiba ili Nafasi ya Spika ishikiliwe na Spika ambaye amesomea fani ya Sheria kwasababu wanaamini endapo Spika mwenye taaluma ya Sheria Kamwe hawezi kulea uhuni huo ,atasimamia Sheria na Kanuni na atatumia Kanuni na Sheria kuwadhibu wabunge wasiyotaka kuheshimu Kanuni na Sheria na mfano mzuri Enzi za Msomi wa Sheria Samuel Sitta alipokuwa Spika wa Bunge,hakulea wabunge wahuni waliokuwa wajivunja Sheria na Kanuni akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini(Chadema), Zitto Kabwe alimtimua Bungeni kwa kuvunja Kanuni.

Lakini mwishoni mwa wiki Spika Makinda kupitia Kamati ya Bunge aliizinduka usingizini na kuwadhibu wabunge Hao wahuni ambao walifanya vitendo Vya utovu wa nidhamu.

Napongeza uamuzi huo wa Makinda wa kuamuru Kamati ya Bunge iwashughulikie wabunge hao licha uamuzi huo umekuja ukiwa umechelewa sana Kwani zimebaki siku Chache Bunge kuvunjwa na wabunge baadhi ambao walishabobea Katika Nyanja ya kufanya vurugu bungeni walishafanya sana uhuni ndani ya Bunge na kufanikiwa kulipaka matope Bunge letu KWA Kipindi chote cha Uhai wake .

Baba wa Taifa Marehemu Julias Nyerere aliwahi Kusema hivi ; " Uhuru bila mipaka ni sawa na wendawazimu".

Na nikweli kabisa, Uhuru wa kujieleza ndani ya Bunge letu linaloongozwa na Makinda tumeshuhudia kuna wakati ulivuka mipaka na limegeuka kuwa kama lina baadhi ya wabunge ni wendawazimu maana wanafanya vitendo vya kiuwendawazimu licha Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatoa Uhuru kwa wabunge kujadili Kwa Uhuru ndani ya Bunge.

Ibara ya 100 ya Katiba hiyo inasomeka hivi : " 100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri  Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo".

Lakini Tulishuhudia baadhi ya wabunge waliokuwa na Chuki zao kijinga  ,kutumiwa na wafanyabiashara kutumia Uhuru huo kuwatuhumu watu ambao sio wabunge ndani ya Bunge Hilo, kujadili hoja za kizushi na kupaka matope wabunge wenzao na baadhi ya mawaziri ,wakuu wa Wilaya na wafanyabiashara wakati wakijua wazi unapomjadili Mtu ndani ya Bunge wakati mtu Huyo siyo mbunge wala waziri ambaye anaweza.

Na Katika Sakata la Escrow ,Spika Makinda alitamka ndani ya Bunge Kuwa wabunge waache tabia ya kutumiwa vibaya na wafanyabiashara Kuja kuamishia magomvi ya wafanyabaisha na watu wengine ndani ya bunge.

Niitimishe kwa Kusema Kuwa nimefurahishwa sana na uamuzi wa Kamati hiyo ya Bunge ya kuwatia adabu wabunge Hao wahuni wasiyojiheshimu kwanza wao binafsi ,Kanuni na kuto heshimu Kiti cha Spika.

Maana wahuni hawa walikosa adabu Katika baadhi ya vikao Vya Bunge walivyokuwa wasishiriki na kwakuwa walikuwa Hawachukulii hatua walikuwa Tayari wameishaota mapembe ambayo Ijumaa yamekatwa na Bunge na Kuonyeshwa Kuwa hawako juu ya Kanuni za Bunge.

Na Wengi wenu Nyie wabunge wahuni mliotimuliwa mnahali Mbaya Katika Majimbo yenu kwakuwa baadhi ya Wapiga kula wenu wanasema hamjawaletea maendeleo yoyote badala yake mlitumia  muda mwingi kubwatuka ovyo bungeni na Kwenye vyombo Vya Habari  na sasa ndiyo Mmeishafungiwa kuudhulia vikao Vya Bunge ambalo Bunge Hilo Uhai wake unakoma Julai 9 Mwaka huu, kwa maana hiyo nyie mmejiondosha mapema kwasababu ya vitendo vyenu Vya utovu wa nidhamu.

Na kwa baadhi yenu mmeishasoma alama za Nyakati Kuwa mna nafasi finyu sana ya kutetea nafasi Zenu za Ubunge, mkaamua muanzishe vurugu Hilo la kupinga miswaada hiyo kwa njia ya kihuni ili mliotimuliwa Ndio mpate Sababu ya kwenda Kuwaahada wananchi wenu Kuwa mmetimuliwa na Bunge wakati bado mlikuwa mkitakeleza majukumu yenu ya kuwapiga nia wapira wenu. Mmechemsha ,hadanganyiki Mtu.

Ukweli ni kwamba mmefurushwa bungeni kwasababu Nyie mmefanya vitendo Vya kihuni yaani utovu wa nidhamu ambavyo havipaswi kufanywa na wabunge . 

Ni Wasela Mavi peke yake ndiyo wanapaswa Kutenda uhuni ule mliojifanya wakuligeuza Bunge Kama Soko au klabu ya Pombe chafu ambayo kila Mtu anazungumza bila kufuata mpangilo.

Waswahili siku zote wanasema Muungwana Asifiwi ushenzi,sasa Nyie baadhi ya wabunge wa UKAWA,mnasifiwa kwa ushenzi.

Acheni hiyo tabia ,siyo sifa nzuri hata kidogo,mmejidhalilisha na rekodi imebaki Kuwa Nyie ni wabunge ambao ni wabovu wa nidhamu .Hivi hata watoto wenu, wake Zenu na wakwe Zenu na watu wanaowaheshimu mnafikiri watawaheshimu   tena Kama dhamana?

Ninavyofahamu Mimi Demokrasia ya vyama Vingi,haikuqnzishwa  kwa kuwapatia ruhusa wapinzani wakiwemo wabunge wao kupinga mambo yanayofanywa na Chama kinachounda  serikali iliyopo madaraka CCM kwa njia za kihuni kama hizo za wabunge wa upinzani kuamua kupinga miswaada bila kufuata Na kuheshimu Kanuni.

Jifunzeni kupinga mambo kwa kutumia lugha zenye staha,ustaarabu na siyo uzushi, makelele na Zogo mwisho wa siku hata kama mlichokuwa mkikipinga mlikuwa sahihi,mnaonekana ni wahuni kwasababu ya kushindwa kutumia njia za kistaarabu ,nidhamu na Kanuni kupinga mambo.

Haya Kama siyo mnawazimu ni kitu gani?mmetumia njia za kihuni kupinga miswaada ile isisomwe na imesomwa?Hivi mweu hapa ni nani Kama siyo Nyie wabunge wa UKAWA mlioadhibiwa ambao wengine baada ya Kuitwa Kwenye Kamati ya Bunge mmekiri Kutenda kosa? Watu wazima ovyoooooo.


Julai 5 Mwaka huu, Bunge  waliokuwa Ndani ya Bunge  walipitisha Muswada wa Sheria ya Petroli wa Mwaka 2015, ambao ni miongoni mwa miswaada ya sekta ya mafuta na gesi iliyokuwa ikipigiwa kelele na wabunge wa upinzani.

Nyie ni watu wazima,maji heshimu na mjitambue ,huo usela Mavi mnaoufanya huku mkiwa mnahadhi ya Ubunge unawashushia heshima kwanza Nyie Binfasi,familia zenu na Taifa letu.Mmelidhalilisha sana vazi la Suti Kwani mtu unapovaa suti Unatakiwa uwe na staa kwasababu vazi la suti linaheshima yake lakini nyie kwakuwa ni wahuni licha mlivaa suti ham kujificha mkaendelea kufanya uhuni wenu wa kupiga makelele huku mkiwa nimevalia suti.

Wabunge Nyie wahuni mliotimuliwa ,rudi mkamueleze Yule 'Bwana yenu' anayewatuma kupinga miswaada hiyo kwasababu tu amenyimwa vitalu Vya gesi kwasababu Hana sifa za kupewa na hata Kwenye Sakata la Esrow aliwatumia sana kwasababu alikuwa na Chuki Binfasi dhidi ya Aliyekuwa waziri mmoja lakini mwisho wasiku aliumbuka tena mkamwambie Huyo bwana wenu Kuwa hivi sasa ananguvu Kama zamani maana serikali,na Jamii imeisha baina tabia yake chafu ya uzushi,Chuki pindi anapokosa Ulaji Katika eneo Fulani.

Niitimishe kwa Kusema Kuwa nimefurahishwa sana na uamuzi wa Kamati hiyo ya Bunge ya kuwatia adabu wabunge Hao wahuni wasiyojiheshimu kwanza wao binafsi ,Kanuni na kuto heshimu Kiti cha Spika.

Kwani Ibara  ya 13  (1) ya Katiba ya nchi inasema hivi ; "  Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria".

Hivyo wabunge  hawapo juu ya Sheria , wanapovunja  Sheria,Kanuni ni lazima wachukuliwe hatua na Bunge lilipo wakuta na hatia ya kuvunja Sheria wabunge hao wa UKAWA limewachukulia hatua za kisheria kwa mujibu Kanuni za Bunge na huo ndiyo Utawala wa Sheria.Sheria ni Msumeno na msumeno huo umewakata wabunge hao wa UKAWA  na Sheria hainaga macho.Kanuni hizo za Bunge Nyie wabunge mlishiriki kuzitunga na Kanuni hizo hizo zimewameza.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
6/7/2014