LOWASSA UNA TATIZO



Na Happiness Katabazi

LEO  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi Mkuu Katika Viwanja Vya Jangwani Dar Es Salaam. Na ukweli kampeni za UKAWA zimefana hongereni sana.

Nimefuatulia kwa makini Uzinduzi huo mwanzo hadi mwisho kupitia Kwenye Televisheni.Nimewasikia wote waliopewa nafasi ya kuzungumza a amezungumza waliyozungumza hata Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye nimemsikia yote aliyoyasema licha yote aliyoyasema Sumaye siyo mapya.

Lakini wenye akili timamu tunayapuuza yote aliyoyasema Sumaye Leo kwasababu Sumaye ambaye  amewahi kugombea urais mara mbili kupitia CCM na hakufanikiwa.

Enzi akiwa   Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu aliwahi kusema "UKITAKA BIASHARA ZAKO ZIKUNYOKEE  VIZURI UJIUNGE NA CCM". Hadi sasa Sumaye hajafuta Kauli hii ambayo ilizua mjadala Mkali nchini.

Nirudi Kwenye mada yangu ya Msingi ya Leo.Mada hiyo nitajadili uamuzi wa Mgombea Urais wa CHADEMA kwa muunganiko wa UKAWA, Edward Lowassa  Leo  saa 11 jioni alipopanda jukwaani kuanza kuhutubia  alisema ameishauriana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Kuwa asisome hotuba yake ya Uzinduzi wa kampeni hiyo kwasababu eti muda umekwenda na Polisi wa Dar Es Salaam, hawampendi kabisa kwahiyo eti wakizidisha muda Polisi hao watapata Sababu.

Kwasababu hiyo eti Mbowe na viongozi wengine wamemshauri asiisome hiyo hotuba ndefu badala yake hiyo hotuba itawekwa Kwenye Website ili wananchi waisome.

Jamani , hivi huyu Lowassa yupo Siriazi kweli ?Lowassa hayupo Siriazi kuutaka urais wa Tanzania. 

Leo Ndio ilikuwa siku rasmi ya Lowassa ambaye ni mgombea urais kuja  Uwanjani kueleza wanachi atayafanyia nini kupitia Katika kinywa Chake na kuwaomba kura wananchi .

Lakini Lowassa Hilo Leo lime mshinda kashindwa  kueleza kwa wananchi atayafanyia nini na mipango ya serikali yake akafanikiwa Kuwa rais itakuwa ni ipi kwa Sababu dhahifu kabisa.

Mgombea urais kabisa bila aibu Katika mkutano wa Uzinduzi wa kampeni yako bila aibu na woga unasema eti hutasoma hotuba yako badala yake Utaiweka Kwenye website? 

Tumuulize huyu Lowassa ambaye amekuwa akijigamba Kuwa anachukizwa na umaskini na amekuwa akiwa tembelea watu wa Haki ya chini Kwenye masoko .

Sasa Nimuulize hao masikini ambao hawana simu za Smartphone wataweza kuisoma hiyo hotuba yake kupitia website? 

Jibu ni Jepesi Watanzania Wengi hawataisoma hiyo hotuba yako kwa Sababu hata hela za kuweka Bando Kwenye simu hawana uhakika wa kuzipata.

Sasa ikitokea wasikupigie kura za Ndio kwasababu umeshindwa kusimama jukwaani kunadi sera zako utakapoingia Ikulu utawafanyia nini utakuja Kulalamika umeibiwa kura?

Maana hata unapotaka Mwanamke kimapenzi lazima usemezane naye ,umwage sera zako ili akakubali au aukataee wewe Leo Lowassa Hilo limekishinda la kututongoza wananchi wenye akili timamu ili tu kuipigie kura kwasababu dhahifu?

Kama Mbowe na viongozi wenzake walijua muda ni Mdogo, kwanini wasinge panga Ratiba ikaanza mapema ili upate muda mrefu wa kusimama jukwaani usome hotuba yako?

Lowassa unataka kutuchezea akili, yaani unataka tukupe urais wakati umeshindwa kusoma hotuba ya ufunguzi wa kampeni zako? 

Kama ulishauriana na viongozi wa UKAWA usisome hotuba yako ,sasa kulikuwa na maana gani ya kufanya mkutano huo Leo ?Simngeweka hiyo hotuba Kwenye Mtandao tukajua Moja.

Hilo limekushida,Je ikitokea ufanikiwe urais wa Tanzania, licha naamini huwezi kufanikiwa kupata nafasi hiyo unaweza kwenda Umoja wa Mataifa na Kusimama Mbele na kusoma hotuba au mhadhara  kwa Niaba ya Tanzania zaidi ya saa Moja?

Kwanza Ulipaswa uonyeshe kwa vielezo Kuwa ni kweli Polisi Dar Es Salaam wanakuchukia na wanakuchukia kwasababu gani? Lini walianza kukuchukia?

Polisi wakikukataza kisheria kufanya ziara zako ambazo zinahatarisha Usalama wako na kuleta Usumbufu Katika Jamii ndiyo wanakuchukia? 

Lowassa wewe ni kiongozi wa ajabu sana na unageuka kuchekesha Mbele ya watu tunaofikiri sawa sawa.

Leo umetumia dakika nane jukwaani kuzungumza mambo ambayo siyo mapya ,jipya nililoliona ni lile la kumshukuru aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani,Fredrick Sumaye  eti amefanyakazi nzuri sana ya kuwapa vidonge vyao serikali ya CCM.

Hili Mimi Ndio nimeliona jipya kutoka mdomoni mwako kwasababu umemsifia aliyekuwa hasimu wako wa kisiasa Sumaye.

Na pia nimeliona jipya pia kwa mdomo wa Sumaye kutoa maneno ya kujisafisha wewe Lowassa Kuwa ni Msafi wakati ni Sumaye huyu huyu alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanakupiga vijembe.

Sielewi kabisa ni kwanini watu wazima Mmekuwa na tabia za kinafki  mna misimamo  inayoyumbayumba na ya msimamimii maneno yenu?

Itoshe Kusema tu kwa nilichokiona Leo nimeitimisha kwa Kusema mkutano wa Leo wa UKAWA ulikuwa Una sura mbili.

Sura ya kwanza ni ya Uzinduzi wa Kampeni na sura ya pili ni Sumaye kutumika kurusha makombora Moja kwa Moja kwa Rais Jakaya Kikwete na serikali na CCM.

Na kweli Sumaye amefanyakazi hiyo kikamilifu ya kurusha vijembe Kwani watu walikuwa watu livu sana wakamsikiliza na kushangilia licha Lowassa Katika zile dakika zake wakati akizungumza watu baadhi ya wananchi walikuwa hawamsikilizi Kwani walikuwa wakiondoka uwanjani hapo.

Yaani mgombea Urais kabisa wa UKAWA, huyu Lowassa anasimama jukwaani anasema eti akiwa Rais Atalishughulikia Kesi ya Babu Seya,kuwaachiria huyu Masheikh wa UAMSHO  Sheikh Farid na wenzake ambao wapo gerezani,elimu ya Darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu Bure. Kwa hiyo hayo yapo ndani ya Ilani ya UKAWA?

Lowassa Leo Kasema anajua tu ataibiwa kura zake .Sasa Kama unajua utabiwa kura zako kwanini unaendelea kushiriki Katika uchaguzi Mkuu?Maana hadi umediriki Kusema utaibiwa kura Ina maana utashinda.Kwanza Hao watakaokuibia ni wakinanani na kwasababu gani?

Msimnajipata Kuwa UKAWA mmejipanga kisawasawa na kwa upande wa wanausalama mmpo vizuri.Sasa Kama mmejipanga vizuri na wanausalama wa UKAWA wapo imara kwanini uibiwe kura?Basi hamna wanausalama UKAWA?

Hivi Lowassa kwa usanii huu unaoufanya kabisa unaamini utakuwa rais wa Tanzania baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu Oktoba 25 Mwaka huu? Pole sana Lowassa kwasababu huwezi kushinda urais kwa Sababu haupo Siriazi na urais ,unafanya mzaa na usanii wa wazi kabisa.

Lowassa jiulize kwanini Hilo limetokea uliopoanza kuongea wananchi walianza kuondoka Hawakutaka kuusikiliza .Jibu ni Jepesi walilokuwa wanalitajarajia  kutoka kwako hawajalipata  maana umewaambia wakasome Kwenye Mtandao.

Kumekuwa na Madai Kuwa Afya ya Lowassa sio nzuri ,licha yeye Mara kwa Mara amekuwa akikanusha taarifa hizo. Sasa kwa kitendo hicho cha Leo cha kushindwa kusoma hotuba kwa kisingizio cha muda kumalizika.

Je hatuoni hii ni mbinu iliyotumiwa na viongozi wa UKAWA ya kumuepusha Lowassa asisome hotuba hiyo kwasababu hawezi kusimama jukwaani muda mrefu ? Lowassa unatatizo.

Mungu ibariki Tanzania

0716 774494
Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
29/8/2015













LAWRENCE MASHA KORTINI KWA LUGHA CHAFU



LAWRENCE MASHA KORTI KWA LUGHA CHAFU

Na Happiness Katabazi

ALIYEKUWA  Waziri wa Mambo ya Ndani na sasa ni Kada Mpya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wakili Lawrence Masha amefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Leo akikabiliwa na kosa Moja tu la kutoa chafu maofisa wa Jeshi la Polisi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, Wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi alidai Kuwa Kesi hiyo ya jinai Na.190 ya Mwaka huu, mshitakiwa ametenda kosa Hilo la kutoa lugha chafu kinyume cha Kifungu cha 89(1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.

Wakili Kishenyi alidai Kuwa Agosti 24 Mwaka huu, ndani ya Kituo Cha Polisi Oysterbay  Jijini Dar Es Salaam, Masha ambaye ni Wakili kitaaluma alitumia lugha chafu dhidi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Juma Mashaka na maofisa wenzake wa Polisi kwa Kuonyesha Kuwa Juma na maofisa wenzake wa Polisi Kuwa ni ' washenzi na waonevu hawana shukrani,huruma wala dini maneno ambayo yalikuwa yanataka kuatarisha Amani. 

Hata hivyo Masha alikanusha kosa Hilo na Hakimu Lema alisema ili mshitakiwa Huyo apate dhamana ni lazima awe na wadhamini Wawili watakao saini bondi ya sh.milioni Moja.

Baada ya Hakimu Huyo kutoa Masharti hayo upande wa jamhuri uliomba muda utahaki barua za wadhamini na muda ulikuwa umeishakwenda hivyo Hakimu Lema akaairisha Kesi hiyo hadi Septemba 8 Mwaka huu,kwaajili ya kutajwa na akaamuru mshitakiwa apelekwe gerezani kwasababu Masharti ya dhamana bado hayajatimizwa.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg:www.katabazihappy.blogspot.com

071











ABBAS MAZIKU BUNDALA



Maziku na Mohammed Dewji

 
MTANZANIA WA KWANA KUFANYA BIASHARA YA KUPELEKA KOROSHO NCHINI VIETNAM  
 
 NA EDNA BONDO
 
BIASHARA ya kusafirisha mazao ina ushindani mkubwa kutokana na kutawaliwa na matajiri wenye asili ya Kiasia.
Sababu hiyo imewafanya Waafrika wengi kutokuwa na uthubutu katika biashara hiyo kwa kuhofia kutofanikiwa na kujitanua kibiashara.
Mbali na ugumu huo lakini pia wengi hasa Watanzania wamejikuta wakiishia kuwa wafanyabiashara wa kawaida na kupoteza fursa za kimataifa.
Kupoteza fursa muhimu za kimataifa kumefanya wakose nafasi ambazo zingeweza kuwafanya kufikiri nje ya boksi.
Makala hii inamwangazia mfanyabiashara wa kwanza wa Kitanzania kufanya biashara ya kusafirisha korosho kwenda nchini Vietnam , Abbas Maziku Bundala .
 
Alipoanzia
 
Maziku anasema alianza biashara ya kusafirisha mazao mnamo mwaka 2013 baada ya kuvutiwa na mjomba yake ambaye alikuwa na mashamba yaliyokuwa na mazao mbalimbali.
 
Miongoni mwa mazao  ambayo Maziku alianza nayo na anaendelea nayo ni korosho, ufuta, mbaazi, choroko, mtama, alizeti, mashudu ya pamba  na pilipili Manga.
Anasema mazao hayo huyakusanya kutoka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, wakulima pamoja na kwenye minada  inayofanywa na vyama vya ushirika katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma , Singida, Shinyanga na Tanga. 
 
Anayasafirisha kwa njia gani?
 
Akizungumzia jinsi anavyosafirisha mazao hayo, Maziku anasema hutumia gari kuyatoa mikoani hadi kuyafikisha maghalani na kuyahifadhi kabla ya kufungasha.
“Wakati wa kuyafungasha unapofika huwa nayafungasha  kwa kutumia vibarua na katika vifungashio vyangu huwa na nembo  inayoonyesha jina la kampuni yangu  na baada ya hapo sampuli hupelekwa katika maabara za kupima ubora wa mazao kimataifa iitwayo SGS  na ndipo hufuatiwa na hatua ya mwisho ya usafirishaji  ambayo huwa natumia meli za mashirika mbalimbali ikiwamo IPTL, MAERSK  na nyinginezo kwa ajili ya kwenda nchini Vietnam,” anasema  Maziku.
Anabainisha baada ya hatua zote hizo hufuata taratibu zinazotakiwa ikiwemo kulipia ushuru kwa Mamlaka ya mapato nchini, (TRA), wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo na ufugaji, wanasheria pamoja na maofisa wa Usalama wa Taifa ambao huhakikisha hatua zote halali zimefuatwa.
 
 Maziku anasema kwamba kwa biashara za kimataifa Shirika la Viwango (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)  hawahusiki bali wahusika wakuu ni SGS.
  
Anajiendeshaje kibiashara?
 
Maziku anajinasibu kwamba biashara ya kuuza mazao nje ya nchi ina ushindani mkubwa.
Anasema anakumbuka alianza na mtaji wa sh. 2,000,000 na sasa anazungumzia mtaji wa sh. milioni 200.
 “Si rahisi kufika nilipofikia  kwasababu biashara hii ina  ushindani mkubwa, ninashindani na matajiri wakubwa wenye uwezo wa kujipangia bei za mazao hivyo ingawa nimepiga hatua lakini bado ninahitaji kupanua biashara yangu zaidi na zaidi”anasisitiza .
Anaeleza kwamba mwaka 2013 alipata hasara ya baada ya ubora wa mazao aliyopeleka kupimwa na kuonekana upo kwenye kiwango cha 48 badala ya 51 inayotakiwa hivyo ilimpa wakati mgumu na kuyumba  kibiashara na  mtaji wake kukata ndipo alipolazimika kukopa fedha benki ambapo hadi sasa  bado analipa deni hilo .
“Nilipata hasara kubwa sana ambayo hadi leo hii bado ninalipa hilo deni nililokopa benki  ingawa pia fedha kutoka kwenye vyanzo  mbalimbali vya mapato ya biashara zingine ninazozifanya zinaendelea kuifanya bishahara ya mazao kwenda nje ya nchi iendelee kuwepo,” anasema.
 
Vikwazo vya kibiashara
 
Maziku anakwenda mbali na kueleza katika jambo lolote lenye mafanikio vikwazo huwa havikosekani lakini kubwa katika ni mtaji.
 
Pia analia na ukiritimba unaofanywa na benki mbalimbali ambao hutaka dhamana kubwa kuliko uwezo wa mfanyabiashara.
Ukiachilia mbali suala la benki, Maziku anasema kikwazo kingine ni ukiritimba kwenye vyama vya ushirika  katika suala zima la upangaji wa bei ambazo hukinzana na bei ya katika soko la dunia hivyo inakuwa ngumu kwa wafanyabiasahara kufikia malengo kutokana na kuepuka kupata hasara.
Aidha, anataja vikwazo vingine ni wizi wa fedha unaofanywa na baadhi ya watu anaowaamini kumnunulia mazao ambao  hutoroka na fedha hivyo kufanya suala la uaminifu kuwa mdogo na vikwazo vya ubora wa mazao.
 
Mafanikio
 
Akizungumzia mafanikio Maziku anabainisha, tangu alipoanza biashara ameweza kuwa na kampuni mbili zijulikazo kama Agromart Company Limited (GEFU) na Lyone Investment Company Limited  ambazo kwa pamoja ameajiri wafanyakazi watano akiwemo Ofisa Rasilimali Watu, Mhasibu, katibu Muhtasi, Mwanasheria na Meneja Mwendeshaji wa shughuli za kampuni.
Anaeleza kwa biashara anayoifanya ameweza kujenga nyumba yake mwenyewe, kumiliki usafiri na kupata fursa za kusafiri nchi mbalimbali kuhudhuria makongamano na maonyesho ya biashara ya mazao jambo ambalo limemkutanisha na watu na kupanua wigo wa biashara yake kimataifa.
Maziku anasema anatarajia kufungua kampuni ya ujenzi ili mtaji wake uzunguke pamoja na kutoa ajira kwa vijana mbalimbali wa Kitanzania.
 
Matarajio mengine ni kuanzisha  kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa  ndogo ndogo za majumbani kama vile juisi, mafuta ya alizeti, mifuko ya plasitik pamoja na maji ya kunywa kwa ushirikiano na wawekezaji kutoka nje kwa lengo moja tu la kukuza uchumi wa Tanzania.
Aida anasema anajihusisha kikamilifu na masuala ya kijamii hasa kusaidia wasiojiweza ikiwemo yatima lakini mambo hayo huyafanya nyuma ya pazia pasipo kujitangaza.
“Kidogo nilicho nacho huwa nakitoa kwa wenye mahitaji maalum lakini huwa sijitangazi” anasema.  
Maziku ni kijana wa Kitanzania aliyezaliwa mwaka 1990, kitaaluma yeye ni mtaalamu wa masuala ya benki na fedha  fani ambayo alisoma katika chuo kikuu cha Zanzibar .
 Pia aliwahi kufanya kazi Benki ya Exim kama ofisa wa kawaida wa benki ambayo alidumu nayo kabla ya kugeukia katika biashara ya mazao.
Maziku ni mtoto wa mwisho kwenye familia yao yenye watoto watatu, ndoto yake ni kuwa mfanyabiashara mdogo mwenye mafanikio makubwa kama alivyo Mohammed Dewji(Mo).
Aidha Maziku anawashauri vijana wenzake wawe na uthubutu kama aliokuwa nao yeye, aliiona fursa kaichangamkia.
“Vijana tusibweteke,vikwazo ni vingi,hatupaswi kukata tamaa, hata waliofanikiwa kama  akina Mo hawakuanzia juu, walipambana  na uzuri ni kwamba Mo si mchoyo, ni mtu anayejitoa, mwenye msaada katika mambo mbalimbali ya ushauri wa kibiashara jambo ambalo linanifanya nimuheshimu na amechangia  katika mafanikio yangu ya kibiashara hivyo sitaacha kumshukuru,” anasema.
 
MWISHO
 
 
 
 Caps 
 
 
 01.
 
 
Mfanyabiashara wa kimataifa  anayejihusisha na biashara ya mazao, Abbas Maziku Bundala  akifafanua  jambo katika mahojiano na Tanzania Daima kuielezea shauku yake ya kutaka kuwa mfanyabiashara mkubwa kama Mohammed Dewji(Mo).
 
02.
 
 Abbas Maziku akiwa katika moja ya shughuli zake za kusafirisha mazao kuelekea mataifa mbalimbali katika Bandari ya Mtwara  kama makontena yaliyohifadhiwa  mazao hayo yanavyoonekana  nyuma yake.
 
 
 03.Mfanyabiashara wa kimataifa, Abbas Maziku Bundala akiwa ofisini kwake  maeneo ya Posta Mpya jijini Dar es Salaam.
 
 
 04.Mfanyabiashara wa kimataifa,  Abbas Maziku Bundala  akiwa na  mfanyabiashara tajiri na mwenye umri mdogo anayemiliki Kampuni ya Mohammed Interprises(Metl)Mo Dewji.
 
 
05.Magunia ya korosho  yakisubiri kupakiwa kwenye makontena tayari kwa kusafirishwa kwenda  nchini Vietnam ambapo mfanyabiashara, Abbas Maziku Bundala hufanya nao biashara kwa mkataba maalumu.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

35c795ee-8f0f-bbb1-3369-00c12713fc5f@yahoo.come3ea28a2-0050-0d8e-a71a-ece6dccce8d4@yahoo.come580aca4-459b-7a19-5fe4-ad8fc7d3be69@yahoo.com4fe2515d-79f0-1b82-7f68-364138fb2cc7@yahoo.com245d3391-d84f-9a21-7bb0-70072f09cab0@yahoo.com




Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima, Agosti 25 Mwaka 2015.

0658 266406

KAMATI YA KAMPENI YA CCM HII HAPA



1. Ndugu Abdulrahman Kinana  - Mwenyekiti
2. Ndugu Rajab Luhwavi   - Makamu Mwenyekiti - Bara
3. Ndugu Vuai Ali Vuai    -  Makamu Mwenyekiti - Z'bar
4. Ndugu Sofia Simba
5. Ndugu Mohamed Seif Khatib
6. Ndugu Asha-Rose Migiro
7. Ndugu Samwel Sitta
8. Ndugu Nape Nnauye
9. Ndugu Mwigulu Nchemba
10. Ndugu Harrison Mwakyembe
11. Ndugu January Makamba
12. Ndugu Amina Makillagi
13. Ndugu Christopher Ole Sendeka
14. Ndugu Stephen Wasira
15. Ndugu Abdallah Bulembo
16. Ndugu Hadija Aboud
17. Ndugu Mohamed Aboud
18. Ndugu Lazaro Nyalandu
19. Ndugu Issa Haji Ussi
20. Ndugu Waride Bakari Jabu
21. Ndugu Mahmoud Thabit Kombo
22. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
23. Ndugu Maua Daftari
24. Ndugu Stephen Masele
25. Ndugu Pindi Chana
26. Ndugu Shaka Shaka
27. Ndugu Makongoro Nyerere
28. Ndugu Bernard Membe
29. Ndugu Sadifa Juma Khamis
30. Ndugu Antony Diallo
31. Ndugu Livingston Lusinde
32 . Ndugu Ummy Mwalimu

Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,  

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI

18/08/2015

HAPPY KATABAZI: FM ACADEMIA 'NGWASUMA'FAMILIA 'MOYA'

Happiness Katabazi


HAPPINESS Katabazi na Lemutuz Malecela

Happiness Katabazi na 33 mwanamuziki wa FM Academia.
KATABAZI na Mulemule,Alan Mulumba Kashama ,Balateli
HAPPY Katabazi na Balateli mwanamuziki wa Fm Academia

Happiness Katabazi na Wema Sepetu


Happiness Katabazi na Wema Sepetu,Balateli,Mulemule,Alan Mulumbakashama,Adelta Paul,Bahati,Lemutuz Malecela ndani ya ukumbi wa Mzalendo ,Agosti 15 mwaka 2015 kuangalia show ya  Bendi ya Fm Academia.





KUZIKWA NA WATU WENGI SIO KWENDA MBINGUNI




UMATI uliomzika aliyekuwa Msanii maarufu wa filamu nchini,marehemu Steven Kanumba  unatofauti gani na umati uliomshindikiza jana mgombea urais wa Chadema,Edward Lowassa?

Na ule umati wa uliojitokeza kwenye msiba,mazishi ya  Kanumba unamsaada gani na familia ya Kanumba kipindi hiki?

Huo huo umati uliojitokeza kumsindikiza Lowassa kuchukua fomu ya urais jana katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hautakua na msaada wowote pindi Lowasa atakaposhindwa urais Oktoba 25 mwaka huu.Na hivyo ndivyo itakavyokuwa.

Hivyo wingi wa watu katika maandamano na mikutano ya hadhara  si hoja ya ushindi.

By Happiness Katabazi.
0716 774494
11/8/2015.