CELINA KOMBANI AMETUTOKA




WAZIRI  NCHI OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA,NA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ULANGA MASHARIKI(CCM), CELINA KOMBANI (56)AMEFARIKI DUNIA HIVI PUNDE NCHINI INDIA ALIPOKUWA AMELAZWA KWA SIKU KADHAA WAKATI AKIPATIWA MATATIBABU.
MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PANAPOSTAHILI. By Happiness Katabazi.24/9/2015


MEMBER OF PARLIAMENT CV

GENERAL
Salutation Hon. Member picture

First Name: Celina
Middle Name: Ompeshi
Last Name: Kombani
Member Type: Elected Member
Constituent: Ulanga Mashariki
Political Party: Chama Cha Mapinduzi
Office Location: P.O.Box 9050, Dar es Salaam
Office Phone: +255 787 330 211 Office Fax:
Office E-mail: ckombani@parliament.go.tz
Member Status: Active
Date of Birth 19 June 1959
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
Kwiro Primary School CPEE 1968 1975 Primary School
Kilakala Secondary School CSEE 1975 1978 Secondary School
Tabora Girls' Secondary School ACSEE 1979 1981 Secondary School
Institute of Development Management, Mzumbe B.A (Public Administration) 1982 1985 Bachelor
Mzumbe University M.A in Public Administration 1994 1995 Masters Degree
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
Prime Minister's Office (Regional Admin & Local Govt.) Minister 5/12/2008 2010
Ministry of Justice and Constitutional Affairs Minister 2010 Todate
The Parliament of Tanzania Member - Ulanga West Constituency 2010 2015
Prime Minister's Office (Regional Admin & Local Govt.) Deputy Minister 2006 5/12/2008
Sokoine University of Agriculture Principal Administration Officer 1995 2005
Morogoro Canvas Mill Manager 1994 1995
Kilosa District Council Officer 1985 1992
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi - CCM UWT Chairperson (Morogoro District) 2002 2005
Chama Cha Mapinduzi - CCM UWT Implementation Committee Member - Kilosa 1987 1992.







UKAWA SASA NI ZAMU YENU KULIA


Na Happiness Katabazi

KWA Takribani Miezi miwili sasa vyama vinavyounda UKAWA vimekuwa vikipata dhoruba Kali kutoka kwa baadhi ya waliokuwa Viongozi wa juu wa UKAWA kuamua kuachia madaraka vyama vyao Vya siasa walivyokuwa wakivitumikia sambamba na wanachama wao.

Tumewashuhudia waliokuwa Majemedali wa UKAWA  ambaye aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha  Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba kuamua  ukajiudhuru wadhifa wake huo ikiwa  ni muda mfupi tu baada ya Waziri Mkuu aliyejidhuru Edward Lowassa kujiunga na Chadema na siku tatu baadae kutangazwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na hivyo Kuwa mgombea urais kupitia UKAWA unaunganisha vyama vinne Vya siasa ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD.

Septemba Mosi Mwaka huu, aliyekuwa Jemedari wa UKAWA na Chadema, Dk.Wilbroad Slaa alijitokeza hadharani mbele ya waandishi wa Habari uliofanyika Katika Hoteli ya Serena Dar Es Salaam na kuibua tuhuma nyingi  kwa viongozi wa Chadema,UKAWA na kukanusha tamko la Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe ambalo alitamkia umma Kuwa Chama kimeamua kumpumzisha Dk.Slaa kwasababu alikuwa Haifiki Lowassa kujiunga na Chadema.

Dk.Slaa yeye alisema anakanusha taarifa Kuwa alikuwa likizo,Bali yeye aliandika barua ya kustaafu siasa Julai 27 Mwaka huu.Hivyo Si kweli Kuwa alikuwa likizo Kama ilivyokuwa ikidaiwa na baadhi ya watu na Mbowe ambaye alidai Dk.Slaa amepumzishwa na Chama.

Pia tulishuhudia aliyekuwa Mwanachama mkereketwa wa muda mrefu wa CUF, Juma Duni Haji Akiama CUF na kuamia Chadema na siku hiyo hiyo akamtangazwa Kuwa mgombea mwenza wa Chadema na mgombea urais akatangazwa Kuwa ni Edward Lowassa ambaye alijiunga na Chadema ndani ya siku Tatu na ndani ya siku hiyo akapewa Kadi ya uanachama na jina lake kupitishwa Kuwa mgombea urais. Kioja cha aina yake.

Pia tulishuhudia baadhi ya waliokuwa wabunge wa Chadema ,Said Khalif, Chiku Abwao na baadhi ya wananchi wengine wakiama Chadema kwenda ACT na Magale Shibuda ambaye alikuwa Chadema amekihama Chama hicho kwa Kusema Kuwa amechoshwa na siasa za Amira zinazoendeshwa na Chadema licha Shibuda ajasema amejiunga na Chama gani.

Na Baadhi ya walioshindwa Katika kura za maoni za Ubunge CCM wakiamia Chadema na siku Chache baadae wakaamua kuhama Chadema na kurudi CCM akiwemo Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sikonge( CCM), Said Mkumba.

Ester Bulaya ambaye alikuwa mbunge Viti Maalum CCM aliamua kuondoka  CCM kwa mbwembwe Kabla ya kura za maoni ndani ya CCM kupigwa na kuamia Chadema na hivi sasa ni mgombea Ubunge Jimbo la Bunda na wachambuzi wa mambo wanatabiri Bulaya hawezi kumshinda mgombea Ubunge wa CCM wa jimbo Hilo Steven Wassira.

Na tangu Dk.Slaa ,Septemba Mosi azungumze na waandishi wa Habari Mara mbili wiki iliyopita na kueleza mambo mambo mbalimbali yaliyosababisha afikie uamuzi wa kustaafu Siasa ndani ya Chadema tena wakati wa kipindi hiki kigumu cha kampeni za Uchaguzi Mkuu Unaotarajia kufanyika Oktoba 25 Mwaka huu.

Ni wazi maelezo yaliyotolewa na Dk.Slaa kwa siku tatu tofauti  na Telebisheni tatu tofauti yaani mara ya kwanza Dk.Slaa alizungumza na umma Septemba Mosi, mara pili Dk.Slaa alifanya mahojiano maalum na Televisheni ya Star TV Septemba 4 na Septemba 6 katika Azam TV.

Kishindo cha Dk.Slaa tumekiona na tunazidi kukiona Kwani baada ya kutoa hotuba yake tumeshuhudia baadhi ya wanachama waliojitambulisha ni Chadema Katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Tabora,Dar Es Salaam, wakifanya maandamano ya kuunga mkono hotuba ya Dk.Slaa na wengine wakichana na kuchoma Moto Kadi na Kudai Kuwa wa akihama Chama hicho wanajiunga na CCM na ACT.

Hotuba ile ya Dk.Slaa pia umesababisha baadhi ya watu waliokuwa wakiunga mkono UKAWA na Chadema kukata tamaa ,na hata wale waliokuwa wakereketwa wa Chadema na UKAWA kwa ujumla huku mitaani wamepooza sana yale makeke na zile tambo zao na matumaini ya Lowassa na UKAWA kwenda Ikulu zimeyeyuka kabisa.

Binafsi napenda kujadili na kufuatilia mambo ya siasa sana hapa nchini na Mara nyingi napenda kuzungumza na watu wa vyama vyote na wasiyo navyama kuhusu Mitazamo Yao ya masuala ya kisiasa tena uwa napenda kukaa Katika vijiwe ,mikusanyiko ya watu na kujadiliana masuala hayo ya siasa kwa njia ya simu na mitandao ya kijamii.

Nimejiridhisha Kuwa wale Watani zangu waliokuwa wakiunga mkono UKAWA kwa Nguvu zote wamepoaaa baada ya Dk.Slaa kutoa hotuba yake.

Nimekuwa  nikiwahoji kwanini wamenyong'onyea  ghafla hivyo baada ya Dk.Slaa kurusha makombora kwa Chadema?.wanaishia Kunijibu HIvi: "Dk.Slaa amenukuliwa na CCM ili aje kutuaribia UKAWA yetu.Na kweli hotuba yake imesababisha kutuvunja moyo kabisa.

Wana UKAWA wengine Watani zangu wanasema kwanini Slaa asingesama hayo mapema ?Kwanini kayasema sasa wakati Kampeni zimeanza?ana Hasira za kukosa kupitishwa Kuwa mgombea urais.

Lakini wote hao hawataki kuzungumzia hoja zilizotolewa na Dk.Slaa ni za kweli au uongo.Wao wanaishia Kusema Slaa anatumika na CCM.Dk.Harrsion Mwakyemba alikutana naye kwa Sababu gani? Wewe CCM Ndio maana una muunga  mkono Dk.Slaa.

Na hata  Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia alidai anamjibu Slaa ameshindwa Kupangua hoja za Slaa alizozitoa Septemba Mosi Mwaka huu, na Ndio maana Septemba 4 Mwaka huu, Dk.Slaa alisisitiza Kuwa hoja zake bado hazijajibiwa na kumrushia Kijembe Mbatia Kuwa " pilipili asiyoila inamuwashia nini?. Kwasababu Dk.Slaa akumtaja Mbatia.

Itakumbukwa Kuwa kwa Miaka Kadhaa Katika Kipindi hii cha Serikali ya awamu ya nne inyoongozwa na Rais Jakaya Kikwete imekuwa ikaishambuliwa  na wapinzani, wana CCM wenyewe na wananchi wa kawaida ni serikali na Chama cha mafisadi na kweli baadhi ya viongozi wa Chadema walikuwa wakimasisha wafuasi wao wawaite na wa wazomee wafuasi wa CCM Katika mikutano Yao na misafara Yao ,mitandao ya kijamii,kwenye vyombo vya habari kwa kuwaita ni Mafisadi .

Kweli agizo la baadhi ya viongozi wa Chadema lilitekelezwa  kikamilifu na wafuasi Wengi wa Chadema na wananchi wengine kwa kuamini CCM ni Chama Cha Mafisadi  Hali iliyosababisha baadhi ya wananchi kuondoa Imani kwa CCM na CCM kuchokwa na baadhi ya watu.

Pia ndani ya CCM Kukazuka Makundi yanayohasimiana vibaya Hali ambayo ilisababisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kukemea Hali hiyo ambayo ilisababisha wana CCM wakutoaminiana hata kumwachia Mwanachama mwenzio glasi ya Maji anaogopa .

Si hayo tu wakati CCM ikiwa Katika vuguvugu la kumpata mgombea urais wao ,wabunge na udiwani mwaka huu napo kulikuwa na mtifuano miongoni mwa wana CCM.

Lakini baada CCM kupitisha Majina ya wagombea wake wa urais,ubunge,udiwani uhasama wa kisiasa ndani ya CCM baina ya wana CCM kwa wana CCM umekwisha,wamekuwa wakitu Kimoja wameamua kuwaunga wagombea wote wa lipitishwa na CCM ilikuisaidia CCM ishinde kwa kishindo Oktoba 25 Mwaka huu.

Leo hii Katika Kipindi hiki cha kampeni hatujasikia Mwana CCM yoyote akijitokeza hadharani kumrushia makombora Mwana CCM mwenzake ,tunachokiona hivi sasa wana CCM kuanzia ngazi ya Taifa wamekuwa kitu Kimoja wanashirikiana kumuangamiza adui wao wa kisiasa UKAWA majukwaani,Kwenye mitandao na vyombo Vya Habari .

Na wakati CCM Ilipitia  Kipindi hicho kigumu  vyama Vya upinzani vilikuwa vikifurahishwa na mtifuano huo uliokuwa ukiikumba  CCM ,serikali ikiwemo Chadema ,CUF vilikuwa vikishangilia sana na Kusema CCM na serikali yake hatakiwi na wanachi wanamchukia na imemeguka vipande vipande haifai kuendelea kuwepo madarakani.

Lakini mabalaa hayo yaliyokuwa yakiiandama CCM sasa hivi yameikumba Chadema,CUF.

Kwasababu baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wanahama vyama na kutoa tuhuma mbaya dhidi ya vyama walivyovihama, baadhi ya wanachama hasa waliojitambulisha Kuwa wanachama wa Chadema wiki hii Tumewashuhudia wakifanya maandamano Katika Mikoa mbalimbali wakiunga mkono hotuba ya Dk.Slaa na wanatangaza kuhama Chadema kwa kile walichokieleza Mbowe amemkaribisha mtuhumiwa wa ufisadi(Lowassa) ,hivyo anakiua Chama.

Pia tumeshuhudia baadhi ya wana UKAWA wakishindwa kukubaliana makubaliano waliyoyaingia baina ya vyama hivyo vinne ambapo Moja ya makubaliano Yao ni mgawanyo wa majimbo na kwamba mgombea wa Chama Fulani mfano wa Chadema akipitishwa Kugombea Jimbo la Ubungo ,basi mgombea wa CUF,NLD,NCCR haruhusiwi Kugombea nafasi hiyo.

Lakini tumeshuhudia huko Masasi Katika mkutano wa mgombea Mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji mkutano ulivunjika baada ya Kuzuka kwa tafrani ya wananchi wa Masasi kupinga mgombea Ubunge (NLD), Emmanuel Makaidi kunadiwa Kuwa ndiye mgombea Ubunge wa jimbo Hilo ambapo wananchi wa eneo walitaka asiendelee kuomba kura jukwaani na kwamba mgombea wanaotaka wao ni mgombea Ubunge wa CUF.

Hali hiyo pia imejitokeza Katika jimbo la Segerea ambapo UKAWA imepitisha mgombea Ubunge  ,Julias Mtatiro lakini mgombea Ubunge aliyepitishwa na Chadema naye anaendelea na harakati zake za kulitwaa jimbo Hilo Hali inayosababisha Mtatiro Kulalamika kupitia mitandao ya kijamii Kuwa mwanamama huyo wa Chadema , Ana vurugu na haheshimu makubaliano ya UKAWA.

Vivyo hivyo jimbo la Ubungo, UKAWA imepitisha mgombea Ubunge wa Chadema, Saed Kubenea lakini wiki iliyopita tulivyoamka asubuhi Kwenye Nguzo za umeme zilizokuwa zimebandikwa  picha za Kubenea ,juu yake zimeandikwa picha za mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CUF ,Mashaka Ngole Vichekesho.

Pia Inaelezwa zaidi ya majimbo 20 likiwemo jimbo la Nkenge Mkoani Kagera pia kuna mvutano kwasababu vyama vinavyounda UKAWA vimeshindwa kuheshimu makubaliano ya kuachiana majimbo.

Uongozi wa UKAWA ulipitisha Majina ya wagombea lakini baadhi ya wagombea toka vyama vingine nao ambao Majina Yao haya kupishwa na uongozi wa UKAWA wamegoma kuwaachia majimbo wagombea waliopitishwa na uongozi wa UKAWA.

Kitendo hicho ni cha kihuni na I imethibitisha ndani ya UKAWA kuna wahuni ambao hawaheshimu maagizo ya wakuu wao wa UKAWA na pia viongozi wa UKAWA nao ni wa dhahifu na hawafai kupewa nchi kuongoza kwasababu haiwezekani uongozi wa juu wa UKAWA uingie makubaliano ya kuachiana majimbo Kisha atokee mtu Kwenye hicho Chama ayakiuke na asichukuliwe hatua.

Na madhara ya kushindwa kuheshimu makubaliano hayo ya kugawana majimbo kwa UKAWA, ni UKAWA watapoteza majimbo mengi sana na hivyo kuipa CCM nafasi ya Kuwanyakua majimbo mengi kirahisi.

Lengo la UKAWA la kugawana majimbo ni kutaka Yule mgombea toka Chama Kimoja kilichomo Kwenye UKAWA jina lake likipitishwa mfano mgombea Ubunge kwa tiketi ya CUF jina lake likipitishwa na UKAWA Kugombea Ubunge basi vyama vingine Kama NCCR Mageuzi,Chadema,NLD vishirikiane naye Katika kampeni ili ashinde na akishinda UKAWA ndio Inakuwa imeshinda.

Sasa Hilo limeshindikana mapema kabisa,UKAWA hivi sasa wamekuwa Kama Mbuzi aliyekata Kamba anaenda njia anayejijua Mwenyewe,ule umoja wa kweli Katika ngazi ya Ubunge  kwa baadhi ya majimbo hakuna na wanamfuatilia siasa za nchi hii ha watabisha.

Ndio maana siku zote nasema bado sijaona Chama CHA upinzani hapa nchini ambacho kipo Siriasi kuiondoa serikali ya CCM madaraka maana vyama vyama Vya upinzani licha wakati mwingine vimekuwa vikifanyakazi nzuri ,vimekuwa vikifanya mzaa na vimejaa wahuni wengi .

Aidha lile balaa la zomeazomea lilokuwa likiwakumba vi kiongozi wa CCM sasa hivi limeamia kwa viongozi wa Chadema Kwani tumeshuhudia Mgombea Mwenza wa Chadema,Katika ziara yake ya Kampeni Katika Mikoa ya Kusini akizomewa na wananchi.

Naye mgombea Ubunge NCCR Mageuzi Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila naye mwishoni mwa wiki wakati akinadiwa na Lowassa alizomewa.

Na baadhi ya wananchi wamekuwa wakiwashambulia viongozi wa Chadema na UKAWA Kuwa UKAWA na Chadema imepoteza mwelekeo kitendo ambacho hapo nyuma kilikuwa akuna kwani baadhi ya wananchi walikuwa waliaminishwa Chadema ni Chama cha Ukombozi na kina viongozi malaika ambao ni watu safi hawana dosari wala Kutenda makosa jambo ambalo kweli.

Hivi karibuni tumeshuhudia Katika mitandao ya kijamii idadi ya wakosoaji wa Chadema na UKAWA ikiongezeka ukilinganisha na Kipindi cha nyuma kwani watu waliokuwa wakuonyesha ni wafuasi wa Chadema Kutwa nzima walikuwa wameiteka mitandao hiyo na shughuli Yao kubwa kuipaka matope CCM,serikali  na viongozi wake na walifanikiwa kwa kiasi Fulani ila kwasababu kasi ya wafuasi hao wa Chadema Mtandao ambao baadhi Yao walikuwa wakitumia hata lugha za matusi dhidi ya wale waliokuwa wakosoaji wa Chadema umepungua sana sana.

Maana wale nao waliochoshwa na uzushi huo wafuasi Hao wa Chadema nao wameamua kutumia mitandao hiyo hiyo Kujibu mapigo kwa lugha za kistaarabu.

Yale yaliyokuwa yakipingwa na Chadema Kuwa CCM Imechoka ,imelegea na watu hawataki ndiyo maana itumia wasanii wengi ,inatumia mabasi na maroli Kubeba watu kuwaletea uwanjani , nao mchezo huo hivi sasa Chadema unaoufanya vizuri sana nayo inaleta wananchi Kwenye mikutano yake kwa maroli na inaleta wasanii pia Katika mikutano Yao ya kampeni. 

Unafki wa aina hiyo nayo ni Sababu pia ya watu wanaofikiri sawa kuiona Chadema nao sio watu wanaoamika na ni wanafki maana CCM ikifanya hayo Chadema inakosoa ila Chadema Mbona inafanya hayo hayo?

Kwa mabalaa hayo yanayoikumbuka Chadema na vyama vinavyounda UKAWA ni sawa na Kusema hivi ; Mwiba uliokuchoma unaweza kuung'oa ukautupa kisha ukaenda kumchoma mtu mwingine.

Lowassa alipokuwa Mwana CCM alikuwa ni Kama Mwiba unaoichoma CCM kwasababu alikuwa akiandamwa mno na tuhuma za ufisadi CCM ikashindwa 'kukimbia' ikawa Ina Chechemea ,wakaamua kuing'oa Mwiba huo  yaani kwa CCM kukataa kupitisha jina Lowassa Kuwa mgombea urais Julai Mwaka huu ,wa kaugua Mwiba ule.

Chadema wakaukanyaga Mwiba ule uliong'olewa Katika mguu wa CCM na kuutupa.Yaani kwa maana Chadema wamemchukua Lowassa hivyo Mwiba huo umewachoma hivi sasa Chadema nayo niachechemea ,haiwezi kufika safari ya Riadha wanayoikimbia kwenda Ikulu.

CCM itakapofika  mwisho wa safari yake Oktoba 25 Mwaka huu na kufanikiwa kukamata dola ,Chadema waiombe CCM iwaondolee Mwiba huo ili wakapumzike salama.

Chadema ya Miaka ya nyuma na uchaguzi Mkuu wa 2010 sio Chama ya sasa ambayo ni wazi imenyesha kudhoofu Kwani zile Shangwe na vibweka vilivyokuwa vinafanywa na baadhi ya makada wake Kama aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, Dk.Slaa,John Nyika na Timu Yao hatuvioni kabisa Katika kampeni za Mwaka huu.

Na kuhusu CUF Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu, aitambi tena Kama Miaka ya nyumba ipo kimya CUF hapa Tanzania Bara.Hali inayosababisha kupoteza mvuto kwa vyama hivyo ambavyo ninawafuasi wengi.

Pia Chadema imeanza kupoteza mfuko kwasababu mgombea urais waliomsimamisha Lowass anaandamwa na tuhuma za ufisadi hivyo Chadema imekuwa kukichukua muda Mwingi  Kujibu wala wanaomuita mgombea urais wao Lowassa ni fisadi badala ya kunadi sera ili wananchi wawasikilize.

Itakumbukwa Chadema Ndio ilikuwa mstari wa Mbele kumuita Lowassa ni fisadi wakati Lowassa akiwa CCM .Lakini ajabu ni kwamba Chadema hii iliyokuwa iki rushiwa mawe Lowassa Ndio Mbowe na genge lake wamekamribisha Lowassa Chadema licha sio kosa .Wanasiasa jamani Mungu a wasamehe bure.

Aidha jambo jingine linaloendelea mvuto mgombea urais wa UKAWA, ni Mwenendo  wa mgombea urais Lowassa kuchukua si chini ya dakika Kumi kuwahutubia wananchi ukilinganisha na wagombea wenzake  wa urais Kama John Magufuli ambaye anasimama muda mrefu jukwaani na kueleza mipango yake  atakapofanikiwa Kuwa rais wa Tanzania.

Katika mikutano ya kampeni za Lowassa,tumeshuhudia Lowassa Anachukua muda kidogo kuhutubia utafikiri anaenda kuweka Kibwagizo lakini watangulizi wake Ndio wanachukua muda mrefu Kabla ya yeye Kupanda jukwaani kuzungumza kwa kutumia muda mrefu. 

Baadhi ya watu huko mitaani ninaozungumza nao wanasema wanakerwa na hiyo Hali Kwani inafanya washindwe kufahamu mengine yaliyofangwa kutekeleza na Lowassa akiwa Rais.

Niitimishe kwa Kusema Kuwa Chadema na UKAWA yenu  sasa ni zamu yenu kulia,CCM sasa inacheka.Na ule Mwiba uliokuwa umeichoma CCM ikawa Ina Chechemea kwa zaidi ya Miaka Saba waliung'oa wakautupa sasa umeichoma Chadema na Ukawa hivyo sasa Chadema na Ukawa mnachechemea.

Kwa sababu waswahili wanamsemo wao usemao yaliyomkuta Mamba na Boko pia yatamkuta kwasababu wote wanaishi kwenye maji .UKAWA sasa ni zamu yenu kulia.

Mungu ibariki Tanzania 

Chanzo: Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook.Happy Katabazi
0716 774494
7/9/2015.







GWAJIMA 'MSHENGA' NI MTUMISHI WA MUNGU KWELI?



Na Happiness Katabazi

SEPTEMBA mosi mwaka huu ,aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ,  Dk.Wilbroad Slaa alimrushia tuhuma chafu kiongozi wa Kanisa la  ufufuo na uzima Askofu Josephat Gwajima.

Dk.Slaa aliyasema hayo Jana mchana Katika mkutano wake na waandishi wa Habari uliofanyika Katika Hoteli ya Serena Dar Es Salaam.

Mkutano ule wa Dk.Slaa ni wakwanza kufanya tangu alipostaafu rasmi siasa  Julai 27 Mwaka huu, baada ya kushindwa kuvumilia na siasa zinazoondelea ndani ya Chadema ambayo alishiriki kukijenga cha hicho kwa muda mrefu .

Nilimfuatilia Dk.Slaa kupitia Televisheni Jana mchana na Jana saa nne usiku hadi saa Saba usiku.Dk.Slaa amezungumza mambo mengi mazito yanayohusu Chadema ilivyokuwa awali na Chadema ya sasa ambayo ameiita imepoteza mwelekeo kwasababu imeamua kufanya machafu yanayofanywa na Chadema ambayo Chadema hiyo hiyo walikuwa wakiyakemea sasa Chadema wameamua kuyafanya wazi wazi.

Tuachane na watu wengine waliotuhumiwa na Dk.Slaa Jana, mada yangu ya Leo itamjadili mtu mmoja tu aliyetuhumiwa pia na Dk.Slaa .Mtu huyo Si mwingine ni  Askofu Gwajima ambaye Jana Dk.Slaa amempachika jina la Mshenga.Jina Hilo la Mshenga limenichekesha sana.

Tuhuma hizo za Dk.Slaa dhidi ya Askofu Gwajima minaziita hivi. ( Dk.Slaa kampiga ngumi za mbavu Askofu Gwajima.)

Kweli nimeamini kuwa sio wote waitao bwanabwana watauona ufalme mbinguni.

Ebu Mtumishi wa Mungu Josephat Gwajima ,kama kawaida yako jitokeze Jumapili hii ujibu tuhuma hizi maana madai aliyoyatoa Dk.Slaa jana dhidi yako ni kama ya yameishakuzika ukiwa hai. 

Umechafuka sana na sio siri taratibu waumini wako wanaweza kuamua kuacha  kukuamini tena na wakalihama Kanisa Lako  na usije kumtafuta mchawi maana mchawi ni wewe unaeleta michanganyo  katika hekalu  la Bwana.

Na ushahidi wa moja kwa moja "Direct evidence" na ushahidi wa mazingira "Circumstantial evidence" unaonyesha unafanya michanganyo ya mambo ya kidunia na Mungu.

Na Mungu hapendi michanganyo na watu wanaofanya matendo yasiyompendeza kwa kutumia mwamvuli wa jina lake lazima atakuumbua tu.

Lakini ni kwanini Askofu Gwajima mtumishi wa Mungu umeshindwa kusimama na kofia moja ya utumishi wa Mungu ukaamua  kujiingiza kwa siri katika siasa za makundi ya kumpigani Edward Lowassa alipokuwa CCM na kwenye mkutano wa Lowassa kutangaza nia ha kugombea urais ndani ya CCM ulikwenda kushiriki katika mkutano ule mkoani Arusha kwa kigezo wewe ni mtumishi wa Mungu unaongoza misa ya mkutano ule na kweli uliongoza sala na kuishia kurusha vijembe kwa wasiomtaka Lowassa kwamba wakalambe malimao.

Wakati ukimuunga mkono Lowassa alipokuwa bado CCM pia ulikuwa ukimuunga mkono Chadema na UKAWA kwa ujumla wake  huo ukawa unaiunga mkono Chadema na Mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za UKAWA katika viwanja vya Jangwani Agosti 29 mwaka huu,kupitia sala zako ukaonyesha wazi wewe upo upande Lowassa,Chadema na UKAWA kwa ujumla .

Sio kosa kisheria lakini turudi kwenye maadili ya viongozi wa kidini mnaongoza makanisa mnaruhusiwa kweli kuonyesha mnamuunga mkono mgombe yupi NA wachama gani tena hadharani?

Kiongozi wangu wa kanisa la Elshadai la Boko Basiaya Dar es Salaam,Kanali Mstaafu wa JWTZ, Bruno Kinunda anakata viongozi wa makanisa kujionyesha wanaunga mkono mgombea wa chama gani .

Kwani kiongozi wa kidini akifanya hivyo lazima atakuwa anawagawa waumini wake kwani sio waumini wote wanaofika makanisani wanayoyaongoza watakuwa wakimuunga mkono mgombea wa chama anayeungwa mkono na kiongozi  wa kanisa aliyeamua kufanya kitendo hicho kisichompendeza Mungu .
Gwajima uliyataka mwenyewe yakufanya michanganyo ya siasa na dini.

Ukawekwa kwapani na wanasiasa akiwemo huyo Dk.Slaa ambae nae alipokuwa Katibu Mkuu Chadema wakashiriki kukutumia na kukugeuza Vuvuzela lao ,wanakufahamu vizuri sana na sasa hivi Slaa ambae alikuja kukutazama hospital ulipolazwa hospitali ya TMJ  ametofautiani na wanasiasa wenzake jana kaamua kumwaga yote uliyoshiriki kufanya kwa siri na mwisho wa  siku anayeathirika ni Gwajima kwa  tuhuma hizi na  zile za  awali maana usipokaa mbali na wanasiasa waumini wasiopenda kusikia kila siku tuhuma zikielekezwa kwako watalihama kanisa  lako.

Gwajima jitokeze utoe ufafanuzi wa tuhuma zilizotolewa na Dk.Slaa jana dhidi yako kuwa wewe ni mshenga wa Lowassa na ulishiriki katika  michezo michafu isiyompendeza Mungu ya kupokea fedha wewe na  maaskofu wengine.

Ni hatari sana taifa kuwa na viongozi wa dini aina ya Gwajima ambao kila  kukicha wanazongwa na tuhuma mbalimbali.

Na ninajiuliza ni kwanini ni askofu Gwajima kila siku na sio watumishi wengine wa Mungu watuhumiwe kila siku tuhuma chafu chafu na za ovyo ovyo Kama hizi?

Mke wa mfalme aitaji kutuhumiwa.Mtumishi wa Mungu hapendezi kila kukicha kuandamwa na tuhuma za ovyo ovyo kama unazoandamwa nazo wewe mara Umepora Mke wa mtu,unatukana watu,umeacha kumtumikia Mungu umejiingiza Kwenye siasa ,unaweza kufufua wafu wakati si kweli na tuhuma nyingine mbalimbali ?

 Askofu Gwajima nakushauri sema na Mungu wako .Kaa chini  ufunge na kusali ili  Mungu akuonyeshe umemkosea wapi ndio maana kila kicha unapata mapigo ya kuelekezewa uchafu kibao,kufunguliwa kesi na tayari baadhi ya  watu wameanza kuwa na mashaka  nawewe na tunajiuliza Gwajima kweli anamtimikia Mungu?

Na ni nataka ujue wazi kuwa wanasiasa wao wakirushiwa tuhuma hata za uzushi wala hawaathiriki sana Kama utakavyoathirika wewe kiongozi wa dini .Hakuna kitu Kibaya Kama kiongozi wa kidini usiaminiwe na kutiliwa Mashaka na waumini wako au watu wasiyo Sali Katika Kanisa Lako.

Jiadhari na wanasiasa hasa wa nchi hii ,Wengi ni washenzi sana na minafikiri ukubwa fahamu awali ndiyo maana ukaamua kuingia kichwa kichwa na Kujenga mahusiano nayo na wakawa wanakutumia kwa Siri kukamilisha mambo Yao sasa walioshiriki kuutumia akiwemo huyo Dk.Slaa kupitia Chadema amekuvua nguo na bado watakuanika ndiyo utapata akili.

Tunaowafahamu wanasiasa wa nchi hii tunakwenda nao kwa akili sana hatukubaki kuingia 'kwa miguu yote miwili' katika mission zao.Unaingia na mguu lakini wewe Gwajima uliingia mzima mzima tena kwa miguu yote miwili.

Mwisho tunaomba uongozi wa makanisa ambao Dk.Slaa ambaye awali alikuwa ni Padri wa Kanisa Katoriki wamtafute Dk.Slaa awapatie Majina ya hao maaskofu na mapridi walioshiriki kufanya ushetani huo uliolezwa NA Dk,Laa mtoe tamko Kwani tamko la Dk.Slaa Jana limeibua hisia tofauti baadhi ya watu wasiyopenda kwenda makanisani kumuomba Mungu wamesema ndiyo maana hawapendi makanisani kwasababu viongozi wa dini baadhi Yao ni wachafu na pia ni hatari Kuwa na viongozi wa kidini wanaojiusisha na tuhuma za Rushwa .

Na hapa ndipo ninapokubalina na Rais Jakaya Kikwete ambaye aliwai Kusema Kuwa kuna baadhi ya viongozi wa dini wanajihusisha na Biashara ya dawa kulevya.

Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
2/9/2015.

TLS KWA NINI LAWRENCE MASHA PEKE YAKE?


                                                             
Na Happiness Katabazi

AGOSTI 27 Mwaka huu,Chama Cha Wanasheria nchini (TLS), kilitoa taarifa yake kwa vyombo Vya Habari kuhusu Kukamatwa na kuwekwa Katika Gereza la Segerea kwa Mwanasheria Mwenzao Lawrence Masha ambaye ni Mwanachama mpya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anayekabiliwa na Kesi  ya kutoa lugha chafu Na.130/2015  kwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Juma Mashaka na wenzake.

Agosti 25 mwaka huu, Mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, Wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi alidai Kuwa Kesi hiyo mshitakiwa ametenda kosa Hilo la kutoa lugha chafu kinyume cha Kifungu cha 89(1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.

Wakili Kishenyi alidai Kuwa Agosti 24 Mwaka huu, ndani ya Kituo Cha Polisi Oysterbay  Jijini Dar Es Salaam, Masha  alitumia lugha chafu dhidi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Juma Mashaka na maofisa wenzake wa Polisi kwa Kuonyesha Kuwa Juma na maofisa wenzake wa Polisi Kuwa ni ' washenzi na waonevu hawana shukrani,huruma wala dini maneno ambayo yalikuwa yanataka kuatarisha Amani na kwamba upelelezi wa shauri bado haujakamilika.

Hata hivyo Masha alikanusha kosa hilo na Hakimu Lema alisema ili mshitakiwa Huyo apate dhamana ni lazima awe na wadhamini Wawili watakao saini bondi ya sh.milioni Moja na barua za utambulisho.

Baada ya Hakimu Huyo kutoa Masharti hayo upande wa jamhuri uliomba muda ukafanye Uhakiki wa  barua za wadhamini na muda mahakama wa kufanyakazi saa 9.30 alasiri ulikuwa umemalizika  hivyo Hakimu Lema akaairisha Kesi hiyo hadi Septemba 8 Mwaka huu,kwaajili ya kutajwa na akaamuru mshitakiwa apelekwe gerezani kwasababu Masharti ya dhamana bado hayajatimizwa.

Kwanza ieleweke wazi Kuwa dhamana ni mkataba baina ya Mahakama na mshitakiwa.

Mshitakiwa anapotimiza Masharti ya dhamana aliyopewa na Mahakama ndiyo Mahakama umpatia dhamana na mshitakiwa Huyo akishindwa kutimiza Masharti hayo ya dhamana Mahakama haitampatia dhamana.

Barua za wadhamini  hizo ufanyiwa uhakiki na Jeshi la Polisi na kisha polisi wanarejesha taarifa za matokeo ya uhakiki huo kwa waendesha mashitaka (Upande wa Jamhuri) .

Na hili zoezi la Uhakiki lilianza kutiliwa Mkazo muda mfupi tu tangu aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashitaka Dk.Eliezer Feleshi  alipoteuliwa Kuwa DPP Miaka sana iliyopita.

Kwani Dk.Feleshi ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu natimu yake wakitilia Mkazo jambo hili la kutaka kila barua za wadhamini zifanyiwe Uhakiki ili wajiridhishe hizo barua ni halisi au  feki maana Mimi Binfasi nimekuwa Mwandishi wa Habari za Mahakamani kwa Miaka 16 nimekuwa nikishuhudia baadhi ya wadhamini feki wakiteta mahakamani baa feki ili kuwadhamini washitakiwa na Matokeo yake washitakiwa walipokuwa wakifahaminiwa NA barua hizo feki walikuwa wakikoroka .

Na wakati polisi wanaenda  kufanya uhakiki wa barua za wadhamini wa Mshitakiwa Lawrence Masha  muda wa Mahakama kufanyakazi ulikuwa umeishamalizika  hivyo Hakimu Lema akahairisha  Kesi hiyo hadi Septemba 8 Mwaka huu,kwaajili ya kutajwa na akaamuru mshitakiwa apelekwe gerezani kwasababu Masharti ya dhamana bado hayajatimizwa. 

Agosti 26 Mwaka huu, Masha  alitolewa gerezani na kuletwa Katika Mahakama ya Kisutu    kwaajili ya kutimiza mashartia ya dhamana .Kweli alitimiza   masharti ya dhamana na Mahakama ikamuachia kwa dhamana.

Itakumbukwa Kuwa Masha aliwahi Kuwa mbunge wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na akateuliwa kushika nafasi ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini na kisha kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani lakini hata hivyo Rais Jakaya Kikwete alipofanya Mabadiliko ya Baraza lake la mawaziri alimtupa nje ya Baraza lake la Mawaziri.

Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka  2010 ,Masha akigombea Ubunge wa Jimbo la Nyamagana lakini alishindwa na  alishindwa .

 Agosti Mwaka huu, CCM iliendesha  Mchakato wa kura za maoni ndani ya chama kwa ngazi ya Ubunge na udiwani na Masha alikwenda Kugombea Ubunge Katika jimbo la Sengerema akashindwa vibaya na hatimaye William Ngeleja (CCM) aliibuka mshindi na siku Chache baada ya kushindwa Ubunge Jimbo la Sengerema ,Masha alitangaza rasmi kuiama CCM na kujiunga na Chadema. 

Turejee Kwenye mada yangu ya Msingi ya Leo ambayo itazungumzia tamko Hilo la TLS Katika aya yake ya  mwisho  ya tamko lake ambayo inasomeka hivi;

(What TLS disapproves and will challenge is the lawfulness and prudence of the court abdicating its role and allowing the prosecution to deny Mr. Masha the right to enjoy his right to bail).

TLS wanasema Kuwa wamekerwa na kitendo cha Mahakama kuruhusu upande wa Waendesha Mashitaka kuvunja haki ya Mshitakiwa Masha kupata dhamana.

Haki ya Mtu Kuwa huru Imetolewa katia Ibara ya 15 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977,

Lakini   Ibara ya   15(2) ya Katiba ya nchi inasema hivi ;

 " (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu-

(a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, au
(b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au na mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai".

Kila Kesi Ina mazingira yake na kwa mujibu wa mazingira ya Kesi ya dhamana ya Kesi ya Masha siku ile ya kwanza alipofikishwa mahakamani, Upande wa Jamhuri haukupinga dhamana ,upande wa jamhuri Mbele ya Hakimu Lema uliomba upewe muda wa kwenda kuhakiki barua za wadhamini wa Masha .

Na Hakimu Lema alikubaliana na ombi hilo la upande wa Jamhuri la kwenda kuhakiki barua hizo za wadhamini (verification) ili wajiridhishe Kama hizo barua ni sahihi au laa.

Na muda wa Mahakama ulikuwa umeishamalizika hivyo upande wa jamhuri ulioshindwa kuhakiki muda huo Kabla ya muda wa Mahakama kumalizika na hivyo kusababisha Mahakama kuamuru Masha aende gerezani hadi siku upande wa jamhuri utakapokuwa umekamilisha zoezi kuhakiki barua hizo na Kesho yake Masha aliyetaja Mahakamani hapo akapewa dhamana kwasababu tayari  upande wa Mashitaka ulikuwa umekamilisha zoezi la kuhakiki barua za wadhamini wa Mshitakiwa Masha.

Kwa Sababu hiyo napinga hoja ya Chama Cha Wanasheria nchini, inayosema eti Mahakama il iwaruhusu upande wa jamhuri kuvunja Haki ya Masha ya kupata dhamana kwasababu Ibara ya 15(2) ya Katiba  ya nchi Inajieleza wazi kabisa Kuwa;

 " (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu-

(a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, au
(b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au na mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai".

Sasa Mahakama iliamuru Masha apelekwe gerezani siku hiyo kwa mujibu wa Ibara hiyo  ya 15(2)(a) ya Kataba ya Nchi .

Na Ieleweke kwamba Katika rekodi ya Mahakama kwa mujibu wa Kesi hiyo Na.130/2015 Jamhuri dhidi ya Lawrence Masha, akuna  rekodi inayoonyesha Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), amewasilisha hati ya Kumfungia dhamana Masha .

DPP ,Biswalo Mganga anayo mamlaka hayo ya Kufunga dhamana kwa mshitakiwa yoyote Yule anayekabiliwa na Kesi ambayo ambayo inadhamana  kwa mujibu wa Kifungu cha 148(4 ) ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002.

Lakini  DPP ,Mganga ajazuia dhamana ya Masha na angependa kufanya hivyo angefanya.

Mhimili wa Mahakama  umeanzishwa    kwa mujibu wa Ibara ya 107A  ya Katiba ya nchi na ndiyo utakuwa na jukumu la kutoa haki. Lakini ibara 107B ya Katiba hiyo  Unaizungumzia Uhuru wa Mahakama na inasomeka hivi; 

"  Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya Katiba na yale ya sheria za nchi.

Sasa Leo hii TLS inapoibuka na Kudai Kuwa Mahakama imeshindwa kutumia mamlaka yake kuwazuia  waendesha Mashtika kuvunja Haki ya Masha ya Kuwa huru ,nashindwa kabisa kuielewa TLS Ina ajenda gani na Mshitakiwa Masha hadi kufikia kutoa tamko la aina hiyo ambalo kwakweli halina mantiki yoyote ,na lime acha maswali yasiyokuwa na majibu kwa baadhi ya Wanasheria wenzao,wapenda Haki na Usawa wa Sheria na kuipaka matope Mhimili wa Mahakama na Ofisi ya DPP Kuwa imepindisha Sheria na kupora Haki ya Masha ya Kuwa huru.

Tuiulize TLS kwahiyo TLS Ilitaka Mahakama itoe dhamana kwa mshitakiwa Masha bila Masha kutimiza masharti ya dhamana yaliyotolewa na mahakama?

TLS kwanini mnaishambulia Mahakama na upande wa Mashitaka Katika Kesi hii Moja tu ya Masha?

Mbona huruma hii ambayo mmeionyesha kwa Masha kwa kutaka Sheria ipindishwe ili Masha apewe dhamana Mbona TLS huruma hii ya Uvunjifu wa Sheria hamuionyeshi kwa washitakiwa wengine?

 TLS  onyesheni  ushahidi unaonyesha Waendesha Mashitaka walivunja   Haki ya Masha ya Kuwa huru na Mahakama ilishindwa Kuzuia Haki ya Masha ivunjwe na waendesha Mashitaka?


 TLS  lakini kwa nini iwe kwa Masha  tu?  Je  ni kwa sababu Masha ni Wakili Mwandamizi  ?TLS tuelezeni mna maslahi gani na Masha?  Mbona wapo  wapo Watanzania   wengi wanateseka kwa masharti au technicalities za namna hiyo kila siku mahakamani na hamuwwatetei?

Mbona nyie TLS hatujawahi kuwasikia mkiibuka kwenye vyombo vya habari na kutoa tamko la kushutumu Mahakama na ofisi ya DPP kwa kuvunja haki ya kuwa huru za Watanzania hao Kama mlivyojitosa kumtetea Masha wiki iliyopita tena kwa hoja za uongo.

Mbona wakili wa kujitegemea Ademba Agomba, Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Wanawake Taifa (CHADEMA), ambao wanakesi hapo hapo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na walikosa dhamana kwa mazingira kama hayo hayo yaliyotokea kwa Masha, mbona TLS atukuwaona wala kuwasikia kutoa tamko?Maana na hao ni wanasheria wenzenu.

Mbona aliyekuwa waziri wa Fedha,Basil Mramba ,Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona nao walipelekwa gerezani kwa Sababu Kama hiyo ya waendesha Mashitaka katika Kesi ya Masha,Mbona hatukuwasikia TLS mkitoa tamko ?

TLS mnanini na Masha? Kwanini  hayo malalamiko yenu hamkuyapeleka rasmi kwa Jaji Mkuu Othaman Chande au Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga  ili way afanyiziwe  Kazi na kuona kuna hira kweli zilifanywa na watendaji wao wa chini ya Hakimu Lema na waendesha Mashitaka wa Kesi hiyo ?

Hamuoni uamuzi wenu wa kupeleka lalamiko Lenu hiyo ambalo binafsi nasema halina kichwa wa miguu linaweza kuamsha hisia Mbaya baina ya TLS na mahakama na Ofisi ya DPP na washitakiwa wengine Mbali na Masha?


TLS mlichofanya ni 'double standard' , hasa kipindi hiki cha Nchi ipo kwenye kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu.

Umma unaweza kuwaona kuwa mna hisa na mtu fulani kwakuwa labda yuko upinzani au vyovyote vile. Kwa nini wajibu wenu huu Msiufanye siku nyingi na kwa wengine? 

Labda  sasa kama mnataka kutuambia kuwa ndio mmeanza, lakini kwa sisi wengine hii tunaiona ni nguvu ya soda tu au kuna sababu.


TLS  kwa mujibu wa tamko Lenu hiyo mmetuhumu Mahakama wazi wazi Kuwa imeruhusu upande wa Mashitaka Katika Kesi hiyo ya Masha kuvunja Haki ya Uhuru ya Masha.

Sasa Kama mmesema  hivyo basi ni wazi Kuwa Mahakama haipo huru kufanyakazi zake na kwamba upande wa Mashitaka ndiyo wenye Nguvu kupita Mhimili wa Mahakama Katika Kesi hiyo ya Masha, maana ni Nyie wenyewe mmesema Mahakama imewaruhusu upande wa jamhuri kuvunja Haki hiyo ya Masha.

Basi pia Mahakama nayo ilivunja mihiko na Katiba ambayo inaitaka Mahakama itoe Haki bila upendeleo wa aina yoyote lakini Mahakama ya Kisutu ikaamua kupora  Haki ya Masha ya Kuwa huru .

Sasa Kama ni hivyo mnavyodai,mnafikiri  Mahakama ya Kisutu itaweza Kutendea haki Mshitakiwa Masha Katika Kesi hiyo ambayo itakuja kutajwa tena mahakamani hapo Septemba 8 Mwaka huu?

TLS  kwa tamko Lenu ambalo Kabla ya kulitoa hamkulifanyia utafiti wa kina na kubaini ukweli ni upi   nawashauri aliyeandaa,kuruhusu tamko hili litoke arudi Katika darasa la Sheria akasome .

Maana somo la Legal Reseach ambalo ufundishwa vyuoni kwa wanafunzi wa kozi ya Sheria umtaka Mwanafunzi au msomi wa Sheria asizungumze jambo Kabla hajalifanyia utafiti sasa TLS Katika suala la dhamana ya Mahakama mmekutupuruka ,hamkufanya utafiti Matokeo yake mkatoa tamko la Kusema Haki ya Uhuru wa Masha ilipovunjwa kinyume na Sheria wakati Si kweli.

Chanzo: Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook. Happy Katabazi
0716 774494
1/9/2015.