CCM MNAIKUMBUKA FAMILIA YA MAREHEMU JOHN KOMBA?




Na Happiness Katabazi

KWA wiki Tatu sasa kuna kitu kinanisukuma niandike Kuuliza Swali hili ; " CCM inakumbuka familia ya aliyekuwa kiongozi wa bendi wa TOT,marehemu John Komba?

Kabla ya kampeni za uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 niliiandika Wimbo wa CCM Mbele Kwa Mbele Uliotungwa na Komba na nilitabiri Kuwa Wimbo huo utakuja Kuwa ni Wimbo maarufu wakati wa kampeni zikianza  na utaibeba sana CCM na ndivyo ilivyokuwa Kuwa Kwani Wimbo ulikuja Kuwa maarufu sana ndani na nje ya nchi  kutokana na Maudhui yake.

Hivyo kuisababishia CCM kuzidi kupata mashabiki Wengi na hata kuna baadhi ya watu waliokuwa wameichukia  CCM, kupitia Wimbo huo wa CCM Mbele kwa Mbele Walijikuta wakianza kuipenda CCM na kuweka Wimbo huo Kwenye miito ya simu zao za mikononi,pikipiki,Kwenye Magari,kompyuta na baadhi ya maneno yaliyomo Kwenye Wimbo huo ya natumiwa mitaani na baadhi ya watu kufikisha ujumbe Fulani.

Lakini kwa bahati Mbaya Mtunzi wa Wimbo huo Komba alifariki mapema Kabla ya Wimbo wake aujaanza kupigwa Kwenye kampeni na hivyo haukuweza Kuwa Shuhuda wa jinsi Wimbo alioutunga ulivyojizolea Umaarufu.

Komba Enzi za Uhai wake alitunga nyimbo nyingi ambazo ziliiletea sifa CCM na ushindi pia. Wimbo wa CCM Mbele kwa Mbele tulishuhudia aliyekuwa mgombea urais wa CCM ambaye kwasasa ndiye rais wa Tanzania, Dk.John Magufuli alipokuwa jukwaani akinadi sera zake alikuwa akiutumia wimbo huo kupiga push up , kucheza kwa madoido Hali iliyosababisha na yeye kujiongezea wa shabiki wake ambao walimpa kura .

Je ,Rais Magufuli na Makamu wako wa Rais, Samia Suluhu maana ndiyo mmpo madaraka kwasasa na Wimbo huo ilitumika hasa kuwanadi wewe Magufuli,Samia na wabunge hivi mlishawahi kukaa chini kila mtu kwa nafasi yake minafikiria kwenda kumjulia Hali familia ya marehemu Komba nyumbani kwake au hata basi mmuite Mkewe ofisini wake mmjulie Hali ?

Au ndiyo mtasema mpo Bize sana na kufukuza watu kazi,kuwasimamisha watu kazi,kuamrisha Polisi wakamate watu wahalifu, kuvunjia nyumba wakazi wazi wa mabondeni na kufanya ziara za kushtukiza?

Ni Mwendawazimu peke ya anayeweza Kusema wimbo wa CCM mbele kwa Mbele haukuchangia ushindi CCM. Kama CCM mna ikumbuka   familia ya Komba Mungu awabariki ,ila kama hamuikumbuki familia yake itakuwa siyo jambo Jema na mtalaaniwa.

Nimesema hayo kwasababu wanasiasa Wengi wanatabia Moja Mbaya sana wanamtaka mtu na kumthamini mtu kinafki pale wanapokuwa wanaitaji ajenda Yao ikamilike kupitia mtu Fulani,akishafanikiwa hawana wanahabari nae.

Komba mchango wako wa utunzi, uimbaji hautasaulika ,umeacha harama ya kuigwa hasa sauti yako ambayo hadi sasa bado haijapatikana mtu wakuweza kuiga sauti yako.

Mungu ibariki Tanzania

0716 774494
Chanzo:Facebook.Happy Katabazi
Blogg: katabazihappy.blogspot.com
30/12/2015

' NJAGU" VALENTINO MULOWOLA KAIMU MKURUGENZI MKUU TAKUKURU





Na Happiness Katabazi

BINAFSI simfahamu Valentino Mulowola ,ila napenda Kumpa pongezi zangu za dhati kwa kuteuliwa na Rais Dk.John Magufuli Kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ikiwa ni siku Chache tu tangu Rais Magufuli akutoe Polisi na Kukuteua Kuwa Naibu Mkurugenzi wa Takukuru na Leo ametangaza Kukuteua Kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.

Watu waliokaribu na Valentino Mulowola  na waliwahi kufanya na wewe  kazi Katika Jeshi la Polisi yaani "Manjagu wenzake ' ambao ni nawaheshimu sana wamekuwa  wakinieleza wewe ni mchapakazi na muadilifu na ni Njagu kweli kweli.

Rai yangu kwako nakuomba ukafanye kazi hiyo Katika wadhifa huo mkubwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni ili uudhiirishie umma kuwa kweli wewe ni mchapakazi na utaendana na hiyo kasi ya Rais Magufuli maana mwenzio Dk.Hosea uteuzi wake umetenguliwa kwasababu Rais Magufuli kasema Hosea hawezi kwenda na kasi yake.Yangu Macho.

Usikubali kutumiwa na wanasiasa uchwara kuumiza watu wasiyo na hatia kwa Sababu tu unataka kuwafurahisha na kujikomba kwa watawala.

Hata Dk.Hosea Kabla ya Kuteuliwa Kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru naye aliteuliwa kwanza Kuwa Naibu wa Ofisi hiyo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Marehemu Meja Jenerali Anatory Kamazima, licha Dk.Hosea alikaa kwa muda mrefu Kwenye Cheo Naibu Naibu Mkurugenzi wa Takukuru kuliko wewe ambaye umeshikilia Cheo cha Naibu Mkurugenzi kwa muda mfupi sana.

Sasa basi Waswahili wanasema hivi " Mwenzio akinyolewa na wewe Tia Maji". Dk.Hosea Leo huko aliko lazima Atakuwa anajisikia vibaya kwa uamuzi huo wa rais Magufuli dhidi yake ila wewe Leo unachekelea.

Narudia tena nenda kafanyekazi kwa Haki, Usikubali kutumiwa na wanasiasa,wala usiruhusu Wakubali vae kama Masharti Hao wanasiasa uchwara mAana hawanaga maana na wa fahamu na Mtangulizi wako Hosea anayafahamu sana maana alipambana nao kadri ya uwezo .

Usieende Kutengeneza kambi ndani ya Takukuru kwamba mfanyakazi Huyo alikuwa Kibaraka wa Hosea humtaki,usifanye hivyo.

Dk.Hosea kuna mazuri yake aliyafanya kama kiongozi Katika Taasisi hiyo na tuliyaona Kwani hivi sasa Chini ya Uongozi wa Hosea tumeshuhudia Ofisi za Takukuru zimesambaa Katika Wilaya nyingi nchini, na Mabaya yake usiyafuate na amazuri aliyoyaanza hakuyamaliza basi yaendeleze.

Nakutakia Afya njema na Mungu akupe busara na hekima yakuongoza Katika nafasi hiyo mpya watumishi wako .Taaluma na weledi ndiyo vita wale Katika kuendesha hiyo Ofisi usifanye ,usiruhusu vijana wako kuharakisha Kufungua Kesi mahakamani bila Kuwa na ushahidi wa kutosha mwisho wa siku mkaja kushindwa hizo Kesi.

Ofisi ya Takukuru chini ya Uongozi wako Ifanye kila linalowezekana kujiepusha na malalamiko Kuwa Takukuri inabambikia watu Kesi.

Mwisho sitaki kusikia na wewe unaiga hii old fasheni yakufanya ziara ya kushtukiza maana Manjagu hawana Michezo hiyo ya kitoto.

Nakutakia Sherehe njema ya Christmas na Mwaka Mpya Mulowola wewe na familia yako.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: Katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
16/12/2015

DK.EDWARD HOSEA OUT TAKUKURU








: Kweli yaliyomkuta Boko na Mamba pia yatamkuta kwasababu wote wanaishi Kwenye Maji.

Katika utawala wa Dk.Hosea aliongoza hatua za kimaendeleo za taasisi hiyo zikapatikana ikiwemo upatikanaji wa jengo la makao makuu ya Takukuru,ofisi za Taasisi hizo kujengwa kwa wingi kwenye wilaya,main USA. wengi kupelekwa vyuoni kujiendeleza kielimu na mambo mengi.
Hata hivyo chini ya utawala wake kuliibuka malalamiko ya taasisi hiyo kubambikia baadhi ya wananchi kesi,rushwa.

Ila mimi binafsi nasema licha Dk.Hosea kaondolewa kwa fedhea katika nafasi hiyo ila kuna mazuri aliyafanya yanaitaji kuenziwa na kuendelezwa na mabaya aliyozembea yakafanyika tusiyafuate .

Namtakia kila la kheria Dk.Hosea katika maisha yake mapya atakayoyaanza mazuri aliyoyafanya serikalini yaheshimie na yaendelezwe siamini kipindi chote cha miaka 10 ,akiwa na wadhifa alitenda mabaya.

By Hap



MIAKA 5 LEO BILA REMMY ONGALA








 MIAKA MITANO LEO BILA REMMY ONGALA 

Na Happiness Katabazi
LEO Disemba 13 Mwaka 2015 , aliyekuwa mwanamuziki mashughuli wa muziki wa dansi Ramadhan Mtoro Ongala 'Dk.Remmy Ongala ambaye alizaliwa Februali 10 mwaka 1947 Leo anatimiza Miaka Mitano tangu alipofariki Dunia.

Binafsi nilipata fursa ya kumuona Remmy akiwa hai kwasababu Moja tulikuwa tukiishi naye Katika Kata Moja ya Sinza  Dar Es Salaam.Pili nilipata fursa ya kumuona alipokuwa akitumbuiza Katika majukwaani .

Enzi za Utawala wa serikali ya awamu ya Tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa, Remmy alikuwa akialikwa Mara kwa Mara yeye na bendi ya Msondo kwenye kutumbuiza Katika sherehe za Kitaifa Mara nyingi Katika Uwanja wa Mnazi Mmoja na Mimi nilikuwa nikienda Katika sherehe hizo Kwa Kofia ya Kazi ya uandishi wa Habari wa Habari Miaka ya 1999 nilikuwa nikimshuhudia Remmy akitumbuiza majukwaani, ikiwemo katika hatua zake za mwisho kabla ya ajaamua kuoka alikuwa akitumbuiza kwenye bar moja iliyopo eneo la Sinza Kamanyola karibu na iliyokuwa Hoteli ya 92 Shekilango kisha baadae ikaitwa Sunciro iliyopo kando kando ya barabara ya Shekilango.

Leo Katika makala hii Fupi namuelezea Remmy kuwa alikuwa ni mwanamuziki anayeona mbali,mkweli na muwazi .Na wakati huo baadhi ya watu walishindwa kubaini Remmy alikuwa ametunukiwa vitu hivyo.Ukituliza akili na kuisikiliza nyimbo nyingi za Remmy utakubaliana na Mimi. 

Uthibitisho wa Hilo ni ule Wimbo wake uliopigwa marufuku na serikali wa "MAMBO KWA SOKSI" isipigiwe redioni.

Wimbo huu ulikuwa umebeba Maudhui ya kuamasisha umma Utumie Kondomu wakati wakifanya tendo la kujamiana ili waweze kujikinga na Maradhi ya Ukimwi. 

Enzi hizo kondomu zilikuwa hazipatikani ovyo mitaani wala kutangazwa Kwenye vyombo Vya Habari na uamasishaji wake ulikuwa bado haujafanyika.

Lakini Remmy aliamua kujiripua na kutunga Wimbo huo wa Mambo kwa Soksi ili kuamasisha Jamii itamke usingizini, isione aibu ,ipambane na Ukimwi kwa kutumia Mpira ya Kiume Katika tendo la kujamiana na wapenzi wake waliupenda Wimbo Hao hadi Wimbo huo ukageuzwa na baadhi ya wa Kuwa salamu pindi wakuta napo na wanaposalimiana.

Ilikuwa mtu akimkuta mtu anaanza kumsalimia 'Mambo ?' Yule mwingine anajibu " 'KWASOKSI'. 

Lakini Leo hii watu wenye akili timamu Tunaona ule uamuzi waserikali wakuufungia Wimbo ule wa Remmy aukuwa sahihi Kwani baadhi ya watu uenda Walijikuta wakipata Maradhi kwasababu ya kukosa elimu ya matumizi ya Mipira ya Kiume kutoka kwa Remmy.

Tunaposema Remmy alikuwa akitazama Mbali Katika nyimbo zake ni pamoja na Wimbo huo Kwani aliamasisha mapema matumizi ya Kondomu lakini serikali ikafungia Wimbo wake lakini Leo matangazo ya kondomu yatatangazwa kila kona Duniani na serikali hiyo hiyo nayo ni Moja wapo ya kusisitiza wananchi wake watumie kondomu.

Hata hivyo baadhi ya watu walikuwa wakimchukulia Remmy kama ni mhuni,kweli watoto wa mjini kwa jicho jingine tunamuona Remmy alikuwa mtoto wa mjini kwasababu alikuwa akitumia vileo kama Pombe Kali kama Konyagi na vilevi vingine vikali na wakati mwingine alikuwa akichomeka maneno yasiyofaha majukwaani wakati akitumbuiza Katika maonyesho yake.

Ila ukweli utabaki Kuwa Remmy alifanyaka za yake nzuri ya muziki na ameacha alama ambayo haitafutika.Itakumbukwa Kabla ya kufariki Remmy alikuwa Amemrudia Mungu wake na kutubu madhambi yake na Remmy alishawahi kunukuliwa na magazeti baada ya Kuokoka Kuwa alitenda sana dhambi ya uzinzi na kwamba Katika Kumbukumbu zake a nakumbuka aliwahi kufanya ngono na wanawake zaidi ya 100.

Mbali na wimbo wa Mambo kwa Soksi, Remmy ambaye alikuwa akitamba na bendi yake ya Super Matimila na mwanamuziki mwenye vituko vingi alitamba na Wimbo wa Dodoma, Mrema, Kifo,Kilio Cha Samaki,Hamisa na nyingine nyingi.

Mungu aiweke roho ya Remmy Ongala mahali panapostahili wakati Leo tukiazimisha Miaka Mitano ya kifo Chake.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
13/12/2015


HISTORIA YA DK. REMMY ONGALA

Na: Kiyungi Moshyi

Desemba 15, 2012

DISEMBA  13, 2012 ilikuwa ni siku ya majonzi kwa wapenzi wa muziki wa dansi hapa Tanzania, Afrika ya Mashariki na ulimwenguni kwa ujumla. Siku hiyo ilikuwa ni miaka miwili kamili toka kifo cha mwanamuziki nguli Ramadhan Mtoro Ongala ‘Dk. Remmy’ aliyefariki usiku wa kuamkia Jumatatu Desemba 13, 2010 nyumbani kwake Sinza, jijini Dar es Salaam.

Alikuwa kipenzi cha watu aliyewaacha wapenzi wake na wananchi kwa ujumla katika dimbwi la majonzi yasiyosahaulika kufuatia tungo za nyimbo zake zenye maudhui maridhawa, ambazo hadi leo zinarindima katika vituo vingi vya redio hapa nchini hata nje ya mipaka yetu.

Dk. Remmy alikuwa wa kwanza kupata ujasiri wa kukemea ngono zembe, akatunga wimbo ‘Mambo kwa soksi’ Lakini jamii ikambeza kwamba wimbo huo haukuwa na maadili mema. Baadaye  viongozi wa serikali,vyama na dini na wengine kwa ujumla walielewa nini alichokuwa akisema Dk. Remmy, wakaanza kuhubiri majukwaani  tahadhari hiyo.

Alizaliwa akiwa na meno mawili ya mbele kinywani mwake  na akaonekana kana kwamba ni  mtoto wa ajabu. Aidha hakuwahi kunyolewa nywele zake kwa miaka yote hadi alipokuja kuokoka akiwa hapa nchini Tanzania.

Dk. Remmy alijipatia umaarufu katika jiji la Dar es Salaam hususan maeneo ya Sinza. Alikuwa na gari yake ndogo ‘soloon’ lililokuwa la aina yake popote lipitapo watu walilishangaa. Lilikiwa na maandishi nyuma ya gari hilo yakisema ‘ Baba yako analo’?

Historia ya maisha ya Dk.Remmy Ongala yaelezwa kwamba mara Dk. Remmy Ongala alipozaliwa, wazazi  wake walimuita Ramadhani Mtoro Ongala. Alizaliwa mwaka 1947 katika mkoa wa Kivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Familia yake iliishi katika eneo lililoitwa Kindu eneo ambalo halikuwa mbali sana kutoka mpakani na Tanzania.
Baba yake alikuwa ni mwanamuziki mashuhuri pia alikuwa mpiga ngoma kwa kutumia mkono na pia mbira. Baada ya kuzaliwa kwake haikuchukua muda mrefu familia yake ilihamia katika mji wa Kisangani huko DRC.

Ipo habari kwamba kabla ya kuzaliwa kwake, mama yake alipata ujauzito mara mbili lakini kwa bahati mbaya kila alipojifungua, mtoto alifariki. Alipopata ujauzito mara ya tatu alienda kwa mganga wa kienyeji kumuomba ushauri afanye nini ili mtoto atakayezaliwa asiiage dunia pia.

Bila kusita mganga wa kienyeji akampa ushauri wake. Akamwambia kwanza safari hii asiende kujifungulia hospitali bali akajifungulie maporini. Pia alipewa ushauri kwamba mtoto akishazaliwa asije akamkata nywele zake. Yote hayo yalitendeka na ndio kisa cha Dk. Remmy Ongala kutokata nywele hadi alipozidiwa na maradhi yaliyompelekea kuokoka ndipo aliponyoa nywele zake akiwa hapa nchini Tanzania.

Mwenyewe aliwahi kusema kwamba mwanzoni alikuwa anajisikia aibu sana kwa kuwa na nywele ndefu namna ile. Lakini baadaye jina na taswira ya mfalme wa reggae ulimwenguni, hayati Bob Marley ilipopata umaarufu nchini Congo, ndipo alipoipenda staili ile ya nywele kwani hata watu wengine pia walianza kuikubali na kuionea ufahari.

Pia inasemekana Remmy alizaliwa akiwa tayari na meno mawili ya mbele kitu ambacho kilichukuliwa kama ishara ya baadaye kuja kuwa mganga wa kienyeji. Ingawa utabiri huo haukutimia, inasemekana huo ndio mwanzo wa yeye kujulikana hapo baadaye kama Doctor Remmy Ongalla.

Baba yake ndiye aliyeanza kumfunza mambo ya muziki tangia akiwa mdogo kabisa. Jambo lililomfanya aamini kabisa kwamba kama jinsi ambavyo watu wengine wamezaliwa kuwa madaktari, wanasheria, waalimu, wakulima nk, yeye alizaliwa ili awe mwanamuziki.

Kwa bahati mbaya baba yake huyo mwaka 1953 alifariki dunia na kumuacha Remmy akiwa na miaka sita, akiwa tayari ameshaanza shule. Lakini kutokana na ukosefu wa fedha na kwa sababu mama yake hakuweza kuendelea kumlipia karo za shule, Remmy ilibidi aache shule.

Ilipofika miaka ya 1960, Remmy tayari alikuwa ameshajifunza mwenyewe kupiga gitaa.
Mwaka mmoja baada ya kifo cha Baba yake mzazi, mwaka uliofuatia wa 1964 ulikuwa si mzuri kwa Remmy kwani mama yake mzazi naye alifariki dunia jambo ambalo lilimuacha Remmy na mzigo wa kuwalea wadogo zake kwani yeye sasa ndio alikuwa mkuu wa familia licha ya umri wake mdogo.

Bila elimu na ujuzi mwingine wowote, alilazimika kuanza rasmi kujitafutia riziki kupitia muziki. Ujuzi wake wa kupiga gitaa uliongezeka kwa kasi ya ajabu kitu ambacho kilimuwezesha kutumbuiza kwa kupiga ngoma na gitaa katika hoteli nyingi na  sehemu mbalimbali nchini ya Congo akiwa na bendi yake iliyokuwa imesheheni vijana wenzake iliyoitwa ‘Bantu Success’.

Kwa miongo kadhaa iliyofuatia Dk. Remmy Ongala alizunguka katika sehemu mbalimbali za Congo akiambatana na bendi kadhaa maarufu za wakati huo nchini Congo zikiwemo Success Muachana na ile ya Grand Mickey Jazz nchini Uganda.

Japokuwa kwa ujumla Dk. Remmy alijifunza mwenyewe kupiga gitaa, lakini aliwahi kukiri kwamba muziki wa kutoka nchini Cuba ambao wakati huo ulikuwa unaanza kujipatia umaarufu barani Afrika, ulimsaidia katika kupata staili ya pekee katika upigaji gitaa.

Kwa upande wa uimbaji anasema uimbaji wa Joseph Kabasele ‘Grand Kale’ na ule  wa Franco Lwambo Makiadi ulimsaidia kupata staili yake ya uimbaji kama tulivyoizoea kusikia enzi za uhai wake.

Mwaka 1978 Remmy aliingia jijini Dar es Salaam baada ya kuitwa na mjomba wake mzee Kitenzogu Makassy  ili aje ajiunge na bendi maarufu ya wakati huo ya Orchestra Makassy, iliyokuwa chini ya uongozi wa mjomba wake huyo.

Huo ukawa ndiyo mwanzo wa maisha ya Dk. Remmy nchini Tanzania. Akiwa na bendi ya Orchestra Makassy, alitunga wimbo wake wa kwanza uliojulikana kama ‘Siku ya Kufa’, wimbo ambao aliuandika kumkumbuka rafiki yake aliyefariki. Wimbo huo ulianza kumpatia umaarufu mkubwa na kujulikana kwa haraka hapa nchini.

Mzee Makassy  aliamua kuihamishia bendi yake keipeleka nchini Kenya, kitendo hicho cha mjomba wake kilichomfanya Dk. Remmy  kujiunga na bendi ya  Matimila baada ya kudumu kwa katika bendi ya Orchestra Makassy kwa takriban miaka mitatu hivi.

Jina la bendi hiyo ya  Matimila lilitokana na jina la kijiji kimoja kilichoko kusini mwa Tanzania. Kujiunga kwa  Remmy katika  bendi ya Matimila, alijiongezea umaarufu katika anga za muziki nchini Tanzania wakati huo. Chini ya uongozi wake Dk. Remmy aliisuka upya bendi hiyo na kuibadilisha  jina ikaitwa Orchestra  Super Matimila.

Miaka iliyofuatia Watanzania tulishuhudia umaarufu wa Remmy ukiongezeka hususan kutokana na mashairi ya nyimbo zake ambayo yaliegemea katika kuzungumzia mambo halisi ya kijamii kama vile umasikini, afya, siasa , majanga ya Ukimwi nk.

Mafanikio ya Remmy na kundi lake zima la Orchestra Super Matimila hayakuishia nchini Tanzania kwani katika miaka ya mwishoni ya 1980 walianza kujipatia umaarufu nje ya mipaka ya Tanzania na Afrika.

Dk.Remmy Ongala aliwahi kusema kwamba kupata mialiko ya nje lilikuja kama mchezo tu. Kasseti yenye nyimbo zao rafiki yake mmoja mzungu aliyekuwa akiondoka nchini Tanzania kurejea kwao Uingereza.

Rafiki yake huyo alipofika huko aliwapatia jamaa wa WOMAD (World of Music, Arts and Dance) shirika linalopandisha chati wanamuziki na wasanii mbalimbali kutoka katika nchi za dunia ya tatu. WOMAD  walivutiwa na nyimbo zao, hivyo kuwapa mwaliko kushiriki katika maonyesho yao barani Ulaya ya mwaka 1988.

Baada ya kurudi kutoka Ulaya bendi ya Super Matimila ilitoa album yenye jina la ‘Nalilia Mwana’ ikiwa na  mkusanyiko wa nyimbo zao zilikuwemo nyimbo zilizopendwa sana kama vile ‘Ndumila Kuwili’ na ‘Mnyonge Hana Haki’

Mwaka 1989 Remmy na Matimila walirudi tena Ulaya kufuatia mwaliko mwingine wa WOMAD. Ni wakati huo huo ambapo walipata nafasi ya kurekodi kwenye studio ya kisasa zaidi ya Stud Real World Studios,
ambayo ilikuwa inamilikiwa na mwanamuziki maarufu aitwaye Peter Gabriel.

Dk. Remmy aliwahi kufafanua kuwa wimbo maarufu ya ‘Kipenda roho’ aliuimba mahsusi kwa ajili ya mkewe ambaye ni ‘mzungu’ muingereza ambaye wakati huo tayari walikuwa wameshazaa naye watoto watatu.

Mwaka 1990, Remmy na bendi yake ya Super Matimila walirejea tena katika studio za Real World ambako walirekodi album nyingine yenye nembo ya ‘Mambo’  ambayo ilikuwa na nyimbo kama hiyo ya ‘Mambo’ ambayo aliimba kwa lugha ya kiingereza na kuweza kukidhi kiu ya wapenzi wake wasiojua Kiswahili. Zingine ni pamoja na ‘No money, no life’ na ‘One World’.

Umaarufu wake ulizidi kung’ara mwaka 1990 alipotoa wimbo wa ‘Mambo kwa soksi’ ingawa baadhi ya watu waliupinga kwa kusema kwamba haukuwa na maadili mema kwa jamii, ingawa kimsingi alikuwa anawaasa watu hususani vijana kutumia kondomu ili kuepukana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

Akiwa Super Matimila Dk. Remmy alitoka na nyimbo ningi zikiwemo za ‘Bibi wa mwenziyo’, ‘Kipenda roho’, ‘Asili ya muziki’ na ‘Ngalula’. Zingine  ni pamoja na ‘Mwanza’, ‘Mama nalia’, ‘Harusi’, ‘Hamisa’, ‘Mnyonge hana haki’, ‘Ndumila kuwili’ na ‘Mataka yote’ ambazo  zilimuongezea sifa kubwa Dk. Remmy kufuatia maudhui yaliyokuwa yakikidhi jamii.

Baadaye Dk. Remmy Ongala akaanza kusumbuliwa na maradhi ya kisukari iliyompelekea kuamua kuachana na muziki wa dansi kwa madai ya kwamba umejaa mambo mengi ya kishetani.
Remmy akaokoka, akatubudu dhambi zake na akaanza kupiga muziki akimuimbia bwana.
Kabla ya kifo chake Dk. Remmy alitoa albamu yake ya Injili aliyooiita ‘Kwa Yesu kuna furaha’. Remmy alikuwa katika hatua  za mwisho za kukamilisha albamu yake ya pili, lakini mungu akampenda sana usiku wa kuamkia Jumatatu ya Desemba 13, 2010 nyumbani kwake Sinza. Eneo hilo alilokuwa akiishi lilipewa jina la ‘Sinza kwa Remmy’ kufuatia umaarufu wake alipokuwa hai.

Mungu aiweke roho yake pahala pema peponi, Amina.

Desemba 15, 2012

NYIMBO ZA DANSI,BAIKOKO

Watch "Mbilia Bel - La beauté d'une femme" on YouTube - Mbilia Bel - La beauté d'une femme: http://youtu.be/pFQuqrsb8oI

PROFESA MUHONGO UZI NI ULE ULE





Na Happiness Katabazi
ASANTE SANA RAIS JOHN MAGUFULI "NGOSHA" , kwa Kumteua msomi Professa Sospeter Mwijarubi Muhongo Kuwa Waziri wa Nishati na Madini Leo  wakati Ulipokuwa ukitangaza Baraza Lako la mawaziri.Ngosha Una akili sana.

Itakumbukwa Kuwa Profesa Muhongo alijihudhuru nafasi ya waziri wa Nishati na Madini Katika serikali ya awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na rais Mstaafu Jakaya Kikwete. 

Kwa lugha nyepesi Profesa Muhongo alikuwa ni muathirika wa siasa za Chuki, uzushi zilizokuwa zimetamalaki Katika Utawala wa serikali  iliopita lakini Ikulu kupitia vyombo vyake ilifanya uchunguzi wake kuhusu Muhongo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliachim Maswi ambaye kwasasa ni Katibu Tawala Mkoa wa Manyara kama walikuwa wamehusika Katika skendo ya Escrow na uchunguzi ulionyesha walikuwa hawajahusika licha baadhi ya wanasiasa uchwara ,wafanyabiashara na wananchi walimshikia Bango Kuwa ni fisadi kuusikia.

Siri Siri Muhongo licha ya kupakwa matopwe sana lakini kuna baadhi ya watu ambao hatuna ukaribu naye na wala hatujawahi kuonana naye tulisimama kidete hadharani kumtetea Kuwa anasingiziwa na tulitishiwa lakini mwisho wa siku ripoti ya Ikulu ilikuja kumsafisha na hivyo kumuweka Kwenye rekodi safi na ikawashushua wazushi.

Wito wangu wa Muhongo, kwanza wasamehe watesi wako wote waliokuzulia Janga la Escrow Kwani uteuzi huu ni Ishara kwamba ni bakora ya Mungu dhidi ya watesi wako. 

Nenda wizarani kafanye kazi uliyotumwa na rais wako na siyo vinginevyo.

Katumie taaluma ,maarifa yako ,busara na Hekima kuiongoza Wizara hiyo.

Naamini jungu lile la ESCROW ulilopigwa licha lilikuumiza pia limekupa  Mafunzo Fulani.Hao ndiyo Binadamu uwaelewe na uwavumilie ila Ishi nao kwa makini.

Sasa wale wachawi "wazushi" mlimzushia Muhongo kuhusu Escrow hadi aka chafuka na akajiudhuru kama mnaubavu wa kufanya uzushi wenu katika Utawala huu wa NGOSHA  zusheni tena tuwaone .

Na kitendo hiki cha Magufuli   kumteua Muhongo kushika tena nafasi hiyo ya Waziri wa Nishati na Madini  kimetoa funzo .

Funzo la kwanza watesi wa Muhongo watambue wao sio Mungu wa kuweza kuzuia mipango la Mungu kwa mtu wake .Watambue Wao binadamu wanapanga yao na Mungu anapanga yake.Jiepusheni na uzushi maana mwisho wa ubaya ni aibu na leo kwa Magufuli kumteua Muhongo kushika tena wizara ya Nishati na Madini ni aibu kwenu.

Rais Magufuli aogopi maneno ya watu na amesikiliza kilio cha baadhi ya watu ambao walikuwa wanapenda sana Muhongo arudishwe katika wizara ile ya Nishati na Madini na mimi nikiwa ni mmoja wao kwasababu Muhongo ni miongoni mwanasiasa wachache sana ambao ni wakweli,wawazi ,wenye misimamo isiyoyumba na ni wazalendo.

Kila la kheri  Profesa Muhongo Mungu akutangulie.


Chanzo: Facebook.Happy Katabazi
Blogg:www.katabazihappy.blogspot.com
10/12/2015.






MAGUFULI TUOKEE SINZA VUMBI LINATUTESA


Na Happiness Katabazi

AWALI ya yote napenda kutangaza maslahi yangu Katika makala hii kuwa Mimi ni miongoni mwa wakazi wa Mtaa wa Sinza C ,Kata ya Sinza Dar Es Salaam, ambapo Nyumba zetu zimetazamana uso kwa uso na Kituo kipya cha Daladala  Simu 2000 na ni muathirika mkubwa wa vumbi.

Kituo hicho cha mabasi ambacho pia kumepakana na Shule ya Sheria nchini, ni kipya na kimejengwa hapo baada ya kilichokuwa Kituo cha mabasi Ubungo kuondolewa ndiyo kikaamishiwa hapo.

Kilipoanza Kazi rasmi Kituo hicho cha mabasi simu 2000 ,Makala yangu ya Oktoba 28 Mwaka 2014 iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho ; ( MANISPAA YA KINONDONI MTATUUA KWA TB).

Makala hiyo na ile Habari ya kupongeza serikali kuamishia Kituo hicho hapo zote niliziifadhi Katika ukurasa wangu wa Facebook book .

Na ndani ya makala hiyo niliomba serikali ijenge barabara hiyo kwa Kiwango cha lami kipande cha barabara kutoka Kituo cha Basi Mawasiliano kilichopo katika  Barabara  ya Samnujoma karibu na Kituo cha watoto yatima (SOS VILLAGE ) hadi Barabara ya Shekilango Katika Kituo cha basi Shule ya Mugabe Kwani kipande hicho cha barabara ndicho kinachotumiwa na madaladala kuingia na kutoka Katika Kituo hicho cha mabasi cha Simu 2000.

Nirejee Katika mada yangu ya Msingi. .5/12/2015   alfajiri Gari kubwa lilopita Katika kipande hicho cha barabara kama kawaida yake na kuchonga hiyo barabara ambayo ni ya vumbi na Kisha kuondoka bila hata kumwagia Maji.

Na hiyo siyo Mara ya kwanza ni zaidi ya Mara Sita sasa tangu Kituo hicho Kujengwa hapo, Gari kubwa linakuja kufanya danganya toto kinachoangaliwa barabara likishamaliza Kuchonga hiyo Barabara wakazi wa eneo tunaanza kuteseka kwa vumbi nje na ndani ya nyumba hata udeki Mara nne kwa siku ni Kazi bure.

Wananchi wa eneo hili Tumeishalalamika weee bila mafanikio ,hatusikilizwi tunazidi kuteseka na vumbi ambalo hadi hivi sasa makabati ya nguo ,makapeti, nguo ukifua ukianika nje ni Kazi bure vumbi la hatari watu wanaugua mafua, vikoozi,Hakuna Amani na Furaha tena kukaa eneo hili kwaajili ya vumbi hilo ambayo yanahatarisha   Afya za wakazi wa eneo Hilo.

Wananchi tunajiuliza hivi hawa viongozi wa Manispaa ya Kinondoni wanaakili timamu au ni wendawazimu? 

Hivi ni kwanini hata kwa wiki Mara mbili wasitoe Fedha wakaja Maji Kwenye Gari    likaja kumwagia Maji hiyo barabara hili vumbi litulie  wakati wakisubiri kama ni Fedha za Bajeti za Kuja Kujenga hiyo barabara ?

Ni mikusanyiko mangapi ya kodi Manispaa inakusanya  kila siku hadi washindwe kuleta Gari la Maji Lije limwagie Maji hiyo barabara vumbi litulie?

Mbona Fedha za kuweka mafuta Magari ya Kuja Kuzuia mama tilie wasipike Chakula wanazo?

Disemba 7 mwaka huu,  Askari polisi wa Kinondoni na watu wa Afya walifika eneo Hilo  lilopakana na Kituo hicho cha mabasi huku wakiwa na Mabunduki wakiwa wamebeba chupa zinazozaniwa zilikuwa na mafuta ya taa na kuanza kupita Kwenye vyakula vyote vilivyokuwa vimepikwa na Mama Ntilie Katika Migahawa hiyo na makarai yaliyokuwa yamefadhi mafuta ya kupitia Chips na chips zenyewe na kuanza kumiminia humo Kwenye vyakula vimiminika hivyo kwa Madai Kuwa walishawapa mapema taarifa mama Ntilie wasipike kuna kipindupindu lakini wakakaidi.

Hata hivyo dakika Chache baada ya askari Polisi kumaliza kuwatia Hasara mama Ntilie Hao ambao waliingia Hasara kweli na wa kamwaga Chakula na kuanza kupika tena .

Mama Ntilie hao Walisema wataendelea na Biashara hiyo kama kawaida Kwani ni Rais John Magufuli Katika kampeni zake alisema akiwa rais ataakikisha mamtilie hawatabughudhiwa  sasa wa nashangaa Polisi wanawabughudhi.

Na Mamantilie Hao ambao nilipata fursa ya kuwahoji Walisema wa nashangazwa na Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kuwazuia wasipike kwakisingizio eti cha ugonjwa wa Kipindupindu wakati wao wanafanya shughuli ya Mama Ntilie Katika mazingira safi kwa kiasi Fulani  isipokuwa tu ni vumbi linalotokana na hiyo barabara ya vumbi ambayo inatumiwa na Magari mengi muda mwingi hivyo linatibuka.

Hivi Manispaa ya Kinondoni Kipindupindu ndiyo mnajifanya mnakiogopa sana kuliko Maradhi kama vifua vikuu, vikoozi na uhalibifu wa Mali za watu kutoka na vumbi ambalo Nyie Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kama mnawatumishi wanaofikiri sawa sawa vichwani mnawaweza kulidhibiti vumbi Hilo lisiendelee kuwanatesa wananchi wenu wa eneo Hilo?

Sisi tunaitaji lami hatuitaji danganya toto ya kutuletea Hilo Ligali Lenu Lije alfajiri kama Wachawi litifue barabara na Kisha kutuachia vumbi Hilo ambalo linasababisha watu Kuishi kwa mateso na bila raha ndani nje ya maeneo hayo ya nyumba zao.

Mbona mmiliki wa Hoteli ya City Style,Picknick Villa wameweza Kuwa Kila asubuhi kumwagilia Maji eneo Lao linalopakana na Hoteli zao tu ili kudhibiti vumbi na wamefanikiwa kwa kiasi Fulani.

Nyie serikali ambao Kutwa mnakusanya kodi kitu gani linawashinda kutumia akili na sehemu ya kodi kujaza Maji Katika Gari na Kuja kumwagia kipande kile  cha barabara hili Nasisi tu nisikie kweli serikali inatujali?

Hivi kwanini mlikuwa na kihelehele cha Kujenga hicho Kituo cha mabasi wakati mkijua mlikuwa hamna Fedha za Kutengeneza hii barabara inayotumiwa na madaladala Kuwa Kiwango cha lami?

Mnatutesa na mmetutesa Vya kutosha.Wananchi wanalalamika watu tunakula na kuvuta na kugusa vumbi .Watu wanaugua  mafua, vikoozi Kutwa tunashindia na kulalia maziwa kwaajili ya kuhofia kupata TB kwasababu tunavuta sana vumbi.

Na kama Mimi ni muongo wa haya ninayoyasema kwamba wananchi wa eneo hili kwanza wamechoshwa na hiyo tabia ya kuona Hilo Gari linakuja kuchimba barabara kwa Madai eti kinachonga barabara ambapo hata hivyo likishachonga baada ya wiki Chache barabara Inaaribika tena .

Rais Magufuli tuma watu wako kimya kimya wafike eneo lote Hilo nililolitaja hadi Katika nyumba zilizopo kama na Mto Ng'ombe ,mjionee vumbi linanavyowatesa wananchi na wananchi wanalalamika sana ila malalamiko yako ni kama kilio cha Samaki Machozi yanaishia Baharini.

Na Mimi ni Mkazi wa muda mrefu wa maeneo hayo,eneo hili wakazi wake hawana historia ya uchafu wa kutililisha Maji machafu au kutupa taka ovyo ovyo au mama Ntilie kupika Katika mazingira machafu na hatuna rekodi ya watu kufariki kwa ugonjwa wa Kipindupindu.

Uchafu mkubwa unaowakabili wakazi wa eneo hili ni Hilo vumbi utafikiri kiwanda cha kuzalisha ciment ambalo vumbi  Hilo limeshika kasi baada ya Kituo hicho cha mabasi kufunguliwa, barabara hiyo ambayo siyo ya lami ilipoanza kutumiwa na Magari mengi na vumbi ndiyo likaanza kuongezeka na vumbi Hilo linaongezeka Mara Dufu na kutishia Usalama wa Afya zetu pindi Gari linalokaa Kuchonga barabara a.

 Rais Magufuli, sitanii ,Nasema ukweli, tunaomba utuukoee tunaangamia wenzio na Hali hii Leo hii watoto hawawezi kukaa hata barazani wanakaa ndani napo hata wakikaa ndani mambo ni Yale Yale vumbi kama tupo nje au ndani ya kiwanda cha kuzalisha cimenti.

Naandika makala hii kwa masikitiko makubwa, kweli tunaangamia wenzenu Tuokoeni.Naimani ombi langu Rais Magufuli na Timu yako mtalo fanyia Kazi maana Manispaa ya Kinondoni siyo kama anawachongea kwako ni wazi Hilo tatizo hawalii maanani wangekuwa wanalitia maanani basi wangejitutumua kwa kufanya kama wanavyofanya Wamiliki wa Hoteli ya City Style au Picknick Villa ambazo hoteli hizo zipo kando kando ya barabara hiyo ya vumbi kumwagia Maji hiyo barabara.

Nawatakia Watanzania wote sikukuu njema ya sherehe ya Uhuru wa Tanzania ninayofanyika Leo.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Facebook: Happiness Katabazi
9/12/2015.