MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO USIRUDIE TENA KUFANYA USHETANI HUU

MITHALI 20: 1 Katika Biblia inasema : " Mvinyo hudhihaki ,kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo Hana Hekima".

Nimelazimika kutumia nukuu hiyo ya Biblia Kuonyesha matendo ya kishetani yaliyotendwa Jana hadharani na Kiongozi wa Kanisa la Maombezi nchini lenye masikani yake Ubungo Kibangu Dar Es Salaam,Anthony Lusekelo yana baraka  za kitabu cha Mithali 20:1 Katika Biblia Kwani matendo Yale aliyoyatenda ambayo nimeyaamisha ndani ya makala hii yalithibitisha Hana Hekima .

Jana 23/11/2016   nikitoka nyumbani kwetu    Sinza  C nakuelekea  University of Bagamoyo eneo la Kawe Beach Dar es Salaam  Ambapo chuo hicho kimepakana na Ofisi ya Redio Times kwaajili ya kukamilisha mambo yangu ya kitaaluma.

Hatua chache kabla ya kufika chuoni hapo ni kama nyuma Tatu kurudi  nyuma kushoto kuna Ukumbi unaitwa Mtana Multipose Hall  na katikati kuna barabara ya vumbi inayotenganisha nyumba zilizopo upande wa kushoto na kulia .Ni barabara ndogo ambayo Dereva hawezi geuza Gari  hadi aende Mbele zaidi.

 Upande wa kulia wa ukumbi huo wa Mtana Multipose Hall kunanyumba ya ghorofa ambayo inalimdwa na walinzi wa makampuni ya walinzi ambayo ni Waaafrika na wanaishi pia raia wa kigeni .

Nyumba ina namba  KAW / MZN/ 1348  ambayo imebandikwa katika ukuta wa geti la nyumba hiyo na mabango ambayo yanayoonyesha nyumba hiyo nalindwa na kampuni ya ulinzi nyuma ya nyumba hiyo ni  Bahari ya Hindi .

Saa 12: 32 asubuhi nilipita Katika njia hiyo nikiwa nimepanda usafiri wa Bajaji wa kwaajili ya kwenda Chuoni kukamilisha mambo yangu ya kitaaluma  nilipofika  katika eneo la nyumba hiyo yenye namba KAW /MZN / 1348
inayotenganisha nyumba zilizojengwa  upande wa kulia na kushoto na Kabla ya kufika chuoni ambapo ni mwisho kabisa ya barabara hiyo nyembamba nilikuta Gari limesimama katikati ya barabara yenye namba za usajili  T126 DFN  huku watu kama nane  wakiwa wamesimama pembeni ya Gari Hilo huku wakimtazama mtu mmoja aliyekuwa akiongea kwa sauti ya juu karibu na nyumba hiyo.

Mimi nilipofika karibu nione kuna nini na kwanini Gari limeziba njia na nani Kaziba njia Yule anayeongea kama kuna ugomvi ninani niliposogea Karibu nikabaini aliyekuwa anafoka ni Mchungaji Anthony Lusekelo  maarufu " Mzee wa Upako.

Nilishtuka nikamtaka Dereva anishushe Mara Moja licha safari yangu ilikuwa haujafika mwisho licha ni Hatua Chache kufika chuoni Kwangu ili niwahi kwenda kumsihi Mchungaji Lusekelo aondoke eneo lile Mara Moja Kwani yeye ni kiongozi wa Kiroho na Mtumishi wa Mungu haifahai kidini, kujibizana na watu tena hadharani.

Nilimkaribia Mchungaji Lusekelo na kumshuhudia kwa macho yangu akiwa anatoa lugha za matusi na zisizofaa kwa wakazi wa nyumba Namba KAW / MZN/ 1348 huku akiwa amesimama nje ya geti la nyumba hiyo ambayo wanaishi Raia wa kigeni huku akisikika akisema wamezidi kumchokoza kwa kumuita yeye ni Mlevi.Nilihisi  kuchanganyikiwa kabisa maana sikuamini nilichokuwa nilikushuhudia.

Mzee wa Upako ni miongoni wa wasomi wa makala zangu sana na zaidi ya Mara Tatu alishanipigia simu kunipongeza kwa ujasiri wangu wa kuandika makala zenye Lengo la Kujenga nchi na Akawa anasema ananiombea kwa Mungu azidi kunilinda.

Namimi pia nimekuwa nimekuwa Nilikuatilia mahubiri yake kupitia Chanel Ten Mara kwa Mara ila sikuwahi kubahatika kuonana ana kwa ana na yeye hadi Jana saa 12 asubuhi nilipomuona akiwa Katika Hali ile ambayo siyo ya binadamu wa kawaida .

Ambapo nilimsabahi nikamwambia Mimi ni Muhumini wake na ni mwanafunzi wa Univeristy of Bagamoyo chuo ambacho kipo nyumba ya pili kutoka nyumba ya pili kutoka nyumbani kwake.

Licha  ukweli ni kwamba Mimi siyo Muhumini wa Kanisa lake .Niliamua kuficha jina langu ili asinijue kwani ningemtajia jina langu tu lazima angenifahamu kuwa mimi ni Mwandishi wa habari ambaye amekuwa akiwasiliana namimi na kunipongeza kwa makala zangu kwani angekosa amani.

Kwa mujibu wa wale watu Saba  niliyowakuta eneo la tukio saa 12 asubuhi walinieleza Mzee wa Upako asubuhi hiyo alikuwa anatoka alikokuwa atatokea ndiyo muda huo alikuwa akirudi nyumbani kwake ndipo aliposimamisha Gari lake Hilo Mbele ya geti ya nyumba Na.KAW/MZA 1348 ambapo ndani ya geti Hilo kuna walinzi alianza kujibizana na walinzi akidai wamekuwa wakimkebehi yeye hafai Kuwa Mchungaji kwasababu ni Mlevi kupita kiasi.

Nilimsii sana hadi saa Moja asubuhi ikanikuta eneo Hilo la tukio huku Mvua ikitunyeshea nikimwomba alisikiliza aache kutukana,kufoka Katika eneo la nyumba ya watu kwasababu yeye ni mtumishi wa Mungu anajidhalilisha ,a avunje Sheria za nchi Kwani kutoa lugha chafu ni kosa la jinai,na pia kuziba njia ili watu wasipite kwasababu eti anaugomvi na wale watu siyo ustaarabu na anavunja Haki za watu wengine za kwenda Kokote watakako Katika eneo hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sasa yeye Mzee wa Upako kwa kitendo Chake kile kuegesha Gari katikati ya barabara ile nyembamba ni kuvunja Haki za watu wengine wanatumia usafiri wa Magari Katika barabara ile wasiende wanakotaka kwenda kwaajili yake na kweli alifanikiwa Kuzuia Magari  yasipitr eneo Hilo kwa zaidi ya muda Kadhaa huku Mvua ikinyesha.

Baadae alinisikia huku akiwa ameloana maana Mvua ilionyeshea alikuwa akisikika akinuka kileo huku akiyumbayumba akafungua Gari lake akatoa Kikapu kilichokuwa kinachupa za Maji ya Kunywa ,kavaa viatu Vya wazi  na kashika miwani huku akiwa amekunja suruali.

Nikamsaidia Kubeba Kikapu kwenda nyumbani kwake ambapo ni jirani kabisa na eneo la tukio huku tukinyeshewa na Mvua tutafika nyumbani kwake tukufunguliwa geti na vijana wake nikamuingiza hadi ndani ya geti la nyumba yake .

Vijana wake wakatupokea Mzee wa Upako akaweka chini kile Kikapu akaanza  Kuwaeleza vijana wake Kuwa yeye hata siku Moja hataki kudharauliwa,kuonewa  na anapambana .

Akasema anaishukuru kwa kumfikisha nyumbani kwake salama ila akaniambia ananiheshimu sana Mimi ni kama binti yake .Ila anarudi Kupambana .Nikamsiii sana Aiingie ndani akalale kwanini yeye mwenyewe ndiyo ameniambia muda ule wa asubuhi ndiyo alikuwa akirudi nyumbani kwake akitokea katika matembezi yake ya jioni lakini akakakata akaanza Kuwaeleza vijana wake amefanyiwa vurugu.

Vijana wake wale walivyokosa akili na busara waka pandisha Mori wanamtaka Mzee wa Upako warudi akawaonyeshe Hilo eneo wanajibu mapigo.

Mimi ndiyo nilikuwa nimeshika ufunguo Gari la Mzee wa Upako na miwani yake .Nikawataka wale vija na wake waache upumbavu huo Mzee wa Upako ni mtu mashughuli nchini na kiongozi wa kidini wasiruhusu tena baba Yao kurudi tena eneo la tukio kwenda tena kufanya Fujo siyo vizuri Kwani mwisho wa siku Atakayedhalilika ni baba Yao.

Nikawataka wale vijana wasikilize ushauri wangu wamfungie ndani Baba yao ( Mchungaji Lusekelo ) a kalale Kwani anaonekana amechoka sana hajapumzika maana kanieleza alfajiri ile ndiyo anarudi nyumbani kwake.

Ili Mimi niwapatie ule ufunguo wa Gari la baba Yao ili wao vijana ndiyo n uongozane nao Mimi nikawaonyeshe eneo la tukio na Gari lilipoegeshwa Katikati ya barabara ,wale vijana walinijibu ' uwa hawatakagi Ujinga'.

Haraka sana wakanitaka niwape funguo nikawapa , huku Mzee wa Upako  akiiondoka hapo ndani kwake kurudi Katika eneo la tukio Kujibu mapigo huku Mzee wa Upako akiwa miguu peku ,vile viatu vyake Vya wazi ( Open Shoes ) Nikiwa nimevishika Mimi wakitembea Mwendo haraka na vijana wake ambapo njia nzima Mzee wa Upako alikuwa akifoka .

Na alipofika tena eneo la tukio la wale vijana wake huku Mimi Nikiwa nimebeba Open Shoes zake ambazo nimezipiga picha .Tayari kulikuwa kumeishapambazuka watu wamejaa anaendelea kufoka Magari hawawezi kupita kwasababu Mchungaji Lusekelo aligoma kuondoa Gari lake katikati ya barabara huku akisema siondoi Hilo Gari hadi Rais John Magufuli na RPC Simon Sirro waje ndiyo wataliondoa Hilo Gari.

Nilisikitika sana Kwani jitihada zangu za Kuzuia Mchungaji Lusekelo asidhalilike  Mbele ya umati wa watu kadri kinavyozidi kupambazuka Kwani watu walizidi kujaa na kumshuhudia Vituko alivyokuwa akivifanya ambavyo Mtumishi wa Mungu hapaswi kufinya.

Nikahamua kukaa Mbali kujifanya natuma SMS Katika simu yangu Kumbe napiga  picha vile viatu vyake alivyoniachia ,na Gari yake iliyokuwa imageshwa katikati ya barabara Mbele ya geti la nyumba Na.KAW/MZA 1348 ambapo tukio Hilo la aina yake lilitokea hadi saa mbili asubuhi Jana .

Hata Hivyo wale wale vijana wake walinishuku napiga picha tukio lile walitaka kunipiga kisa napiga picha baba Yao.

Makusudi Niliamua kukanusha Kuwa sijapiga picha na kusingizia Mimi Nina matatizo ya macho hivyo nilikuwa Nasoma SMS lazima simu niinue juu na nisiongeze karibu na macho yangu.

Mmoja wa kijana wake akanitishia kunipiga ikabidi nimbadilikie  na kumtaka kwanza anikome, cha pili jeuri ya kunipiga Hana,Tatu yeye ni shetani ndiyo maana wameshindwa kumshawishi Mzee wao aache kufanya Fujo Mbele ya umati wa watu wakati baba Yao Huyo ni kiongozi wa kiroho anajishushia heshima.Akawa mpole.

Akageuka pembeni nikawaweka mkono wangu nyuma nikairusha  simu yangu kwa nyuma Kwenye  majani na kulikuwa majani yanaunywevu wa Maji ya Mvua ili hata akitaka kunipora simu aikose.


Kijana Yule alivyoona sijamuogopa Akaamua kuondoka nilipokuwa nimesimama mimi na akasogea  eneo la tukio na kumshuhudia Mzee wao  Mchungaji Lusekelo akizidi kufoka nikageuka nyuma haraka nikaokota simu yangu nikaenda kusogea Mbali nikampa mwanamke mmoja anafanyakazi chuoni kwetu anishikie tukasogea mbali  aneo la tukio tukasoma mbele ya geti la Redio Times na kuendelea   Kutizima  Sinema yote ilivyokuwa ikiendelea..

Kumbe vile vitendo vilivyokuwa vikifanywa na Mchungaji Lusekelo Jana Mbele ya Hadhara viliwakera   wakazi wa eneo hilo na watumiaji wa eneo hilo  licha ni la makazi ya watu lina ofisini pia na chuo wakaamua kupiga simu polisi kwa siri .

Baada ya muda mfupi polisi wa Kituo cha Kawe walifika eneo la tukio na kushuhudia tukio hilo na kuondoka na Mchungaji Lusekelo na kwenda kumuifadhi ndani ya kituo hicho kwa muda .

Hata hivyo taarifa toka ndani ya Kituo hicho zilieleza Kuwa licha ya Mchungaji Lusekelo kuifadhiwa ndani ya Kituo hicho  aliendelea kutoa lugha zisizo na staha kwa baadhi ya Askari Polisi ambao walikuwa wakimshangaa Kuwa imekuwaje yeye ni mtumishi wa Mungu halafu amekunywa Pombe kiasi kile na anatoa lugha zisizo na staha .

Hata hivyo mchana wa jana kuna taarifa ambazo sikuwa nimedhinitisha Kuwa Mchungaji Lusekelo alihamishwa pale Kituo cha Polisi Kawe na kupelekwa Katika Kituo kingine.

Kwa mujibu maelezo hayo ya tukio Hilo la ' Sinema ya Bure' nililolishuhudia kwa macho yaliyokuwa yanafanywa  na Mchungaji Lusekelo huku akiwa Katika Hali isiyokawaida kwa zaidi ya saa mbili ya kufoka na kutoa lugha chafu na kuleta Usumbufu Katika eneo la nyumba ya jirani yake  limenifundisha mambo mengi ikiwemo Mimi Leo kukubaliana ule usemi usemao ' Mungu adhihakiwi' Kwani ukimdhihaki atakuumbua.

 Mchungaji Lusekelo ni muhubiri maarufu nchini na ana waumini wengi sana nchini ndani na nje ya nchi na wamekuwa wakimuamini na hata serikali ya sasa inayoongozwa na Rais John Magufuli Inamuamimi na hata Rais Magufuli Mwenyewe siyo Siri anamuamini mtumishi huyu wa Mungu Mchungaji wa Lusekelo na alishampongeza Lusekelo kwa Kazi nzuri anayoifanya ya kutoa huduma ya Kiroho kwa Watanzania ambao ni waumini wake .

Juni 5 mwaka huu, Rais Magufuli alipofanya ziara ya kushitukiza katika kanisa hilo ambapo alienda kwaajili ya kusali katika kanisa linaloongozwa na Mchungaji Lusekelo na Rais Magufuli akatumia fursa hiyo kuzungumza kanisani hapo eneo la Ubungo Kibangu na alisema

Kwa mamlaka aliyonayo ameishaagiza mamlaka zake zianze Kujenga barabara Inayopita Katika Kanisa la Mzee wa Upako ili waumini na wananchi wa eneo wasiendelee kupata tabu kwasababu barabara ile ni Mbaya sana.

Hata hivyo baadhi ya watu walipinga uamuzi huo wa Rais Magufuli na walidai uamuzi huo ni wa upendeleo waziwazi na wakukurupuka.

Licha ya Lusekelo ya Kuwa na heshima kubwa nchini hadi Rais Magufuli Akaamua kwenda kusali kanisani kwake lakini Jana alishindwa kutunza Umaarufu,heshima yake aliyokuwa Katika Jamii kama kiongozi wa Kanisa lenye waumini Wengi Akaamua kuporomosha matusi hadharani ,kuyumbayumba wakati amesimama Na kutembea Mithili ya mtu aliyelemewa na kilevi.  Uzuni.

Vituko vile alivyovifaya Jana Mchungaji Lusekelo pia vimenifundisha Mimi binafsi Kuwa kuanzia Jana niache tabia ya Kuwa mgumu kuamini baadhi ya  taarifa za mambo  machafu yanayofanywa na baadhi ya watumishi wa Mungu.

Miezi mitatu iliyopita kuna watu Wawili toka vyombo Vya Ulinzi na Usalama walinieleza Huyo Mchungaji Lusekelo ni Mlevi mzuri tu wa Pombe aina ya Konyagi na walishamnasa katika matukio mawili akiwa hoi kwa kilevi ,kwakeli nilikuwa mgumu kuwakubali maelezo hayo kwasababu kwanza sikuamini na niliwaona wale maofisa ni wazushi .

Ila Jana asubuhi nilichokiona kilichokuwa kikifanywa na Mzee wa Upako Mbele ya umati watu ,nilikubaliana na Yale waliyonieleza watu wale na nikachukua simu nikamupigia mmoja baada ya mwingine na kuwaambia kweli waliyonieleza Leo Mungu amenileta eneo la tukio nithibitishe Yale waliyonieleza.

Hata hivyo mama yangu Mzazi kwa zaidi ya Miaka minne sasa tukikaa wote sebuleni tukiwa tunaangalia Kipindi cha Mchungaji Lusekelo kinachorushwa na Channel Ten ,mama amekuwa akiniambia huyu Mzee wa Upako ana michango ana maanisha Kuwa licha ni Mchungaji ila bado anafanya mambo ya kidunia ambayo Mungu hayapendi.

Basi mama akisema hivyo namwambia aache hiyo tabia ya kumsema Mzee wa Upako kwasababu Hana ushahidi.Mama anasema haya anafunga mdomo ila ipo siku Mungu atamuanika hadharani ndipo nitakapoamini.


Kweli kupitia tukio la Jana aliyofanya Mchungaji Lusekelo ,Nimelazimika kukubaliana na maneno ya Mama yangu Mzazi kuhusu Mzee wa Upako Kuwa licha ni mtumishi wa Mungu bado anafanya matendo ambayo Mungu hawataki mfano Fujo, kutoa lugha zisizonastaa,kulipa kisasi wakati Mungu anatutaka tusamehe ,tusi lipe kisasi kwa watesi wetu lakini Mchungaji Lusekelo alishindwa kuwasamehe watesi wake na Akaamua Kupambana na maneno makali huku alipokuwa Kaipamba nao wakiwa wanamtazama hawamjibu.

Lusekelo ni binadamu kama Sisi ila tofauti yetu yeye amejipambanua kama mtumishi wa Mungu ambaye ni kiongozi wa Kiroho hivyo Hakupaswa kufanya Yale yote aliyoyatenda Jana ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu ambayo kwa kiasi Fulani yanavuruga akili na akili zangu za kawaida Jana jioni maana sikutengemea kumkuta kiongozi wa dini akiwa Katika Hali kama ile aliyokuwa nayo Mzee wa Upako na kufanya matendo Yale ambayo huwafanywa na watu wasiyo na hofu na Mungu na hawajishina neno la Mungu.

Hata hivyo Fedhea iliyomkuta Jana Mchungaji Lusekelo pia naweza Kusema licha Mimi nilikuwa anajitahidi kumuokoa Lusekeo asidhidi Kuaibika Mbele ya watu Wengi Kumbe Mungu  naye aliamua kuruhusu mtumishi wake Huyo wa Mungu adhalike Mbele ya watu Wengi ili watu wa mjue Kuwa mtumishi Huyo wa Mungu ambaye Kutwa analia ubiri neno lake naye Si mtakatifu na kwamba anayefanya Mambo ambayo Mungu ameyakataza.Na kweli Mungu Jana kumdhalilisha kweupe Lusekelo. Uzuni.

Nilikuwa najiuliza hivi ndiyo mmoja wa waumini wake angepata fursa ya kushuhudia Vituko alivyokuwa akivifanya Mchungaji Lusekelo Jana au kama Alikuwepo muumini Akawa anashuhudia tukio lile ,wamejisikiaje?

Hata hivyo tukio la Jana pia limenifanya nikubaliane na Kauli ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipokuwa madarakani alisema  hivi : ' Kuna baadhi ya viongozi wa dini Si wa safi,ni wachafu na wengine wanauza dawa za kulevya'.

 Nimuulize Mchungaji Lusekelo hivi kupitia tukio hili ,atapata wapi tena ujasiri wa kusimama madhabau ni kuwataka waumini wake wasitumie vileo,wasilipize Ubaya kwa Ubaya ,wasiingie Katika vita ya maneno na watesi wao?

Sikutaka kuandika makala hii ila ni mejikuta nikijiuliza ni kwanini Mungu alipenda nikutane na Mchungaji Lusekelo kwa mara ya kwanza ana kwa ana akiwa katika hali ile na akiwa anafanya matendo yale ya kishetani?

Kwanini Mungu asingepanga nikutane na Mchungaji Lusekelo akiwa Mzima ananukia harufu  ya mafuta mazuri badala ya halufu ya kileo na akiwa anafokea na kutoa lugha chafu dhidi ya jirani yake na kuziba njia na kusababisha kuziba njia kwa muda na hali ya sintofahamu ?

Na Kwani Mungu asinge ya kuruhusu waandishi wa Habari wengine nchini asubuhi ile washuhudie tukio Lile isipokuwa Mwandishi wa Habari Mimi Happiness Katabazi?

Nikahitimisha  kwa Kusema huyu ni Mungu ndiyo ananisukuma niandike makala hii ambayo imeanika   matendo hayo ya kishetani yaliyotendwa na Mchungakondoo wake Lusekelo ili watu matendo anayoyatenda nje ya madhabau, wapi me  Je kiongozi wa kidini anafaa  kuendelea tena kulitangaza neno la Mungu na kuongoza waumini wake?

Nikajikuta nachukua Kompyuta na kuacha kwenda GYM kufanya mazoezi ya viungo  Jana jioni nikaa chini hadi usiku wa manane kuandika makala ambayo nimeimaliza kuiandika  saa Tisa usiku wa kuamkia Leo .

 Kwa  kupitia makala hii ambayo itamfedhehesha Lusekelo kwa kiasi Fulani  na Imani kwa baadhi ya watumishi wa Mungu itazidi kutiliwa Shaka lakini neno la Mungu litasimama .

 Uenda makala hii  akiisoma anaweza kuachana na matendo yasiyompendeza Mungu Kwani yeye Lusekelo ni mtumishi Mungu anapaswa asitende mat endo ya kishetani kama hayo aliyoyafanya jana badala yake abaki na kazi moja ya kumtumikia Mungu tu .Na ni aomba iwe hivyo.

Kwani hata EZEKIELI 3:19 Katika Biblia inasema , " Lakini ukimwonya mtu Mbaya ,wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake Mbaya ,atakufa Katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.

Hivyo kupitia kitabu maneno hayo yaliyopo Katika kitabu cha Ezekiel ,Mimi nimeitimiza wajibu wangu kwako wewe Mtumishi wa Mungu Lusekelo kukuonea ili uache michanganyo ya mambo ya kidunia badala yake Ubaki na jambo Moja tu la kumtumikia Mungu.

Kumbuka Biblia inasema Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu na hata michanganyo.Ukiamua kumtumaini / kumtumikia basi uyafuate na uyatii maandiko yake Kwani Mungu anauwezo wa kukuinua na kukushusha .

Lusekelo Mungu ameinua huduma yako lakini sasa umeanza kurudi nyuma ,u na michanganyo kama hiyo.Siyo vizuri .Mungu hapendi.

Nina Hakika ungekuwa mzima usingetenda matendo ya kishetani uliyoyatenda Jana asubuhi Mbele ya kadamnasi .Au ulivamiwa na mapepo ndiyo ya kwakutuma utende ushetani ule ambao ulikufedheesha ?Kwa lugha nyepesi ulikuwa umepata kileo .

Ingia ndani tubu kwa Mungu wako atakusamehe songa Mbele ila tu wale watu wote waliokushuhudia Jana ukiwa Katika Hali ile na kufanya vitendo vile Vya kishetani siyo rahisi tena kuiamini huduma ya Kimungu unayoitoa.Nisamehe sana.Licha Nitaendelea kukuheshimu na kukupenda.

Kama  kweli Mchungaji Lusekelo umeitwa na Mungu umtumikie ,sikutegemea kabisa mimi binafsi au umati ule watu huku ukiwa umelewa Pombe na huku hujavaa viatu   ukifanya ushetani ule hadharani tena asubuhi asubuhi. Inatisha.

Mchungaji Luseleko kama kweli umeweza Kutenda ushetani huo wa kuporomosha matusi hadharani ,nakuwa Katika Hali ile isiyoyakawaida ambayo unafahamu Mungu hataki matendo Yale ,Kesho wewe utashindwa kuingia tamaa ya kufanya mambo yasiyompendeza Mungu kama kwenda kufanya matendo ya kishirikina ili uwapumbaze waumini wako waendelee kuamini Kuwa ni mtumishi safi wa Mungu Kumbe unatenda matendo sirini yasiyompendeza Mungu?

Hivi Leo hii watu wakikurushia vijembe Kuwa Sadaka zinazotolewa na waumini wako pia unazitumia Katika ulevi ,Utakataa au utasema wanakuonea wivu?

Pombe inavishawishi Vingi sana na inaweza kumshawishi mtu aliyekunywa kufanya chochote anachokisia ikiwemo hata kufanya  zinaa.Hivi ule ushetani ulioutonda Jana  wewe Mzee wa Upako ,wakiibuka watu wakisema unywagi Pombe tu pia hata dhambi ya uzinzi unatenda ,utakuja kukataa useme wakuzushie?


Pole waumini wa Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Lusekelo Kwa makala hii Kwani nafahamu baadhi yenu itawakwaza ila ndiyo mvumilie ukweli ndiyo huo niliyoohushudia Mimi kwa macho yangu nanilitahidi kumsitili kiongozi wenu ili asidhalilike bila mafanikio na mwisho wa siku nilichoambulia nikutaka kupigwa na vijana wake .

Ila roho yangu nyeupe na wala makala hii haina Lengo la kuwazuia muache kumuabudu Mungu kupitia Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Lusekelo.

Namimi ni madhaifu yangu sikatai ila bado sijafikia Hatua ya kama alifikia Lusekelo ya Kuwa mtumishi wa Mungu halafu kufanya matendo hayo ambayo kila Mara amekuwa akisimama madhabauni Kukataza waumini wake wasiyafanye kwasababu Mungu ameyakataza Kumbe yeye Anayafanya .

Lengo la Makala hii ni Kuonyesha Mchungaji Lusekelo ambaye anasimamaga madhabau ni anakemea dhambi Kumbe na yeye anatenda baadhi ya dhambi.Mtaamua wenyewe.Ila nawashauri sote tumuombee maana sote sisi ni binadamu Hakuna Mkamilifu .

Ila kuna utofauti wa upokewaji wa Jamii wa baadhi ya matendo ya dhambi yanayofanywa hadharani na viongozi wa kidini na matendo hayo hayo ya dhambi yakifanywa Na mtu ambaye siyo kiongozi wa kidini.

Mtumishi wa Mungu akitenda  dhambi za aina hizo alizozitenda Mzee wa Upako Jana za kutukana ,ulevi Jamii zitaipokea kwa uzito wa aina yake na kwa Mshangao mkubwa sana.

Hakuna ubishi Mchungaji Lusekelo umefedheheka Jana tena sana Katika eneo unaloishi Kawe Beach Karibu Univeristy of Bagamoyo na Redio Times .Kaa utulie,maana Hasira ya Mungu Jana imekushukia ,tubu Mungu atakusaidia uondokane na shetani wa Kupenda Konyagi na aina nyingine za Pombe Kali.

Mchungaji Lusekelo kama utashindwa kuachana na anasa za Dunia basi achana na Kazi ya Mungu ili uwe huru kufanya mambo ya anasa kuliko Jumapili na siku za katikati ya wiki Una Simama  madhabauni unaubiri neno la Mungu Kumbe ukitoka madhabauni unaenda kufanya mambo yasiyompendeza Mungu ukiwemo Kunywa Pombe.

Mchungaji Lusekelo jana kweli ilikuwa ni mara yako ya kwanza kunywa pombe kwa kiwango kile hadi zikakutuma kufanya matendo yale hadharani ambayo Mungu hapendi?

Je Mchungaji Lusekelo jana ni mara yako ya kwanza kurudi nyumbani kwako saa moja asubuhi ? Maana miminilikufika nyumbani kwako saa moja asubuhi huku nikiwa nimekubeba baadhi ya vitu vyako kama funguo wa gari ,miwani  huku wewe ukiwa umebeba Kikabu chenye chupa za maji ya kunywa ;

 Baada  ya kufanikiwa kumuondoa Kwenye eneo la tukio la ugomvi uliotokea na Kisha baada ya kukufikisha ndani ya nyumba yako wewe na vijana wako wewe ukatoka miguu pekupeku bila kuvaa viatu maana viatu ulikataa kuvaa nimevishika mkononi mkarudi tena eneo la tukio huku ukiwa Ujavaa viatu unakanyaga matope na Mvua inatunyeshea unafoka Katika nyumba ya jirani yako kuishinikiza walinzi wakifungulie Mlango uwaonyeshe Kazi?

Nakupenda kwasababu unapenda kuzungumza ukweli na mimi naupenda ukweli .

Hivyo nakushauri jirekebishe ,tubu kwa Mungu wako, na ukipata muda omba msamaha majirani zako kwa Usumbufu uliowasababishia Jana asubuhi wakuwazibia njia wenzio wasiende makazini na Magari Yao kwasababu Lako ulilipaki katikati ya barabara kumalizima tangu saa 12 asubuhi hadi saa mbili  huku ukisikia hutaliondoa Hilo Gari Hali RPC Sirro,Rais Magufuli waje kuliondoa. Nilikushuhudia ukiyasema haya sina Sababu ya kunisingizia .

Pia Hao vijana wako unaoishi nao hapo ndani baadhi yao wana akili mbovu wote watatu waliotufungulia geti kwasababu wao waliochangia kukurudisha tena   eneo la ugomvi Matokeo yake  ukaenda kudhalilika zaidi wakati Mimi nilifanikiwa kukuondoa  mapema eneo la tukio mapema na watu walikuwa  wachache na Magari yalikuwa hawajaanza kupita Wingi Katika njia ile .

Vijana Hao kama wangekubali ana na ushauri wangu niliyotoa wakati nome kufikisha ndani kwako wa kukuingiza ndani na kukufungia na Kisha wao vijana ndiyo ni wapeleke eneo la tukio niwape ufunguo wa Gari la Baba Yao Mchungaji wa Luseko wafike eneo la tukio wachukue Gari walioleta nyumbani bila kujibizana na watu kwani lakini walinipuuza Matokeo yake ndiyo hayo umati ulifurika ukakushuhudia ukibwatuka .

Polisi wa Kituo cha Kawe Dar es Salaam wakaitwa na wasamalia wema kwa siri wa kakukuta  eneo la tukio ukibwatuka  wakakupeleka kituoni ukiwa bado pombe hazijakuisha ukaifadhiwa  Kituo hapo kwa muda  ukasababisha hata Polisi ambao walikuwa hawafahamu Kuwa unakunywa Pombe wakajua,wakakudharau maana matendo yako ya Jana yalitukanisha pia watumishi wa Mungu .


Mchungaji Lusekelo na wale vijana wako mngeuzingatia ule ushauri wangu   Kuwa uende ndani ukaoge kisha ukalale  ile saa Moja asubuhi maana ulikuwa umechoka ungefanikiwa kukwepa Kadhia na Fedhea hiyo.

Mchungaji Lusekelo wewe ni mtumishi wa Mungu ,jiheshimu ,usijaribu kumgeuza Mungu Kuwa ni Mwanasesele labda aoni mambo unayoyafanya Gizani.Mungu siyo Mwanasesele anatuona yote tunayoyafanya hadharani na Gizani Akiamua kukuumbua anakuumbua na wewe Jana ni Mungu Yule ndiyo aliyekuumbua .


Ni itimishe kwa kukubaliana  na maneno haya yaliyoandikwa Katika  MITHALI 20: 1 Katika Biblia inasema : " Mvinyo hudhihaki ,kileo huleta ugomvi; Nakosaye kwa vitu hivyo Hana Hekima".

Kwasababu maneno hayo yametimia kwa Lusekelo ambaye alikuwa amepata kileo amefanya ugomvi na alipofanya ugomvi Jana alithibitisha umati ule wa watu  Hana Hekima Kwani Angekuwa na Hekima asingekubali kufanya ushetani ule  ambao umefedheesha Vya kutosha.


Mungu Ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494.
24/11/2016.

MAKONDA TULIA UNYWE DAWA

Na Happiness Katabazi WIKI Iliyopita Mkuu wa MKoa wa Dar Es Salaam ,Paul Makonda Mara Kadhaa amenukuliwa Katika vyombo Vya Habari akisema yeye amejitahidi kadri ya uwezo wake Kupambana na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo Shisha lakini Jeshi la Polisi limekuwa likisita kuwachukulia Hatua wahusika. Makonda alitoa tuhuma hizo Mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Katika Uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa upatikanaji wa Umeme Katika Mkoa wa Dar Es Salaam dhidi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda . Kuwa Mara kwa Mara amekuwa akimuuliza Sirro Kuwa Mbona wananchi wanampatia taarifa wauzaji wa Shisha bado wanatamba na Sirro Amekuwa akimjibu Kuwa Hali ni shwari . Makonda aliwashushia tuhuma Makamanda hao Wawili Wamelambishwa ile hongo aliyoikata kutoka kwa wafanyabiashara wale wa Shisha ndiyo maana wanasita kuwachukulia Hatua wauzaji wa Shisha.Shisha imepigwa marufuku kutumiwa hapa nchini. Mkuu Huyo wa Mkoa Alidai kuna wafanyabiashara 10 bila ya kuwataja majina walimfuata wakitaka Kumhonga Sh.Milioni 50 kila mwezi ,lakini alikataa. Hata hivyo Waziri Mkuu Majaliwa alimtaka Makonda aache Kulalamika badala yake akatekeleze maagizo yanayotolewa na viongozi wa juu wa serikali. Kauli hiyo Makonda dhidi ya makamanda hao wa polisi imeibua mjadala katika jamii huku wengine wakitofautiana na yeye vikali. Kwa upande wa Jeshi la polisi Makao Makuu Kamanda Robert Boaz mwishoni mwa wiki alizungumza na umma na akasema taarifa hizo za tuhuma za Rushwa dhidi ya makamanda wa jeshi Lao wamesikia na jeshi hilo limefikia uamuzi wa kuanza kufanyia uchunguzi tuhuma hizo ( Inquiry). Kwanza Napongeza Hatua hiyo ya Jeshi la Polisi kwa uamuzi huo wa uweledi wa kuchukua Hatua za kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo zilizotolewa barabarani yaani Kwenye vyombo Vya Habari na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam ,Paul Makonda. Aidha pia Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai 2002 , kinatoa mamlaka kwa Ofisa wa Polisi kuhoji mashahidi,watuhumiwa au mtu yoyote ambaye Polisi inaitaji kupata maelezo yake kutokana na tuhuma au uchunguzi wa jambo lolote . Hivyo Jeshi la Polisi wapo sahihi kufanyia uchunguzi taarifa hizo zilizotolewa na Makonda wiki iliyopita. Kifungu cha 7 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 ,kina Mtaka mtu yoyote ambaye anafahamu taarifa za kutendeka au kutaka kutendeka kwa tukio ka Uhalifu apeleke taarifa hizo Katika mamlaka husika za kiserikali ili zifanyiwe Kazi na akishindwa kufanya hivyo atashitakiwa kwa kosa lolote chini ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya Mwaka 2002. Tumuulize Makonda yeye Kabla ya ile Sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa umeme aliyotoa tuhuma hizo nzito dhidi ya Makamanda Hao wa Polisi alishazipeleke taarifa hizo za watu wale walifika ofisini kwake kutaka Kumhonga Fedha Katika mamlaka gani za kidola? Makonda ana anakofia Ya Mkuu wa Mkoa wa Dar e Salaam na kofia ya Pili ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam. Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambaye Mkuu wa Mkoa husika ndiyo Mwenyekiti , baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo ni Jeshi la Ulinzi la Wananchi ( JWTZ), Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa ( TISS) ,TAKUKURU ,Uhamiaji ,Magereza na vyombo vingine. Namuuliza Makonda alivyokuwa akiendesha vikao vya Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwa na kofia ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo alishawahi kuwasilisha taarifa zake hizo za wafanyabiashara 10 aliyodai eti walifika ofisini kwake kutaka Kumhonga Fedha kila mwezi ili aachane na mapambano ya Shisha? Makonda uliwai Kuwasilisha taarifa Katika Kamati ya Ulinzi na Usalama kuwa Kamanda Sirro anasita kuchukua Hatua dhidi ya wafanyabiashara hao na uenda ile hongo iliyokataa kutoka kwa wafanyabiashara wale wa Shisha uenda imewapitia? Makonda uliwahi kuwasilisha mezani taarifa Katika Kamati hiyo unayoiongoza Kuwa Jeshi la Polisi kupitia RPC- Sirro amekuwa akikupa taarifa za uongo kuhusu Biashara ya Shisha? Maana kupitia mahojiano yako na Redio Clouds umesikika ukisema Mara kadhaa umekuwa ukipewa taarifa na Jeshi la Polisi kupitia Kamanda Sirro Kuwa Shisha Hakuna Dar Es Salaam na kwamba Jeshi la Polisi lomefanikiwa Kudhibiti Shisha wakati wewe Makonda umekuwa ukipewa taarifa na wananchi wanaoichukia Shisha Kuwa Shisha ipo ,na ukaenda kukamata na vielelezo unavyo . Kama uliiwasilisha Taarifa hizo katika Kamati ya Ulinzi na Usalama Tueleze. Taarifa hizo zilijadiliwa ? Na wajumbe wa Kamati hiyo walijibu nini ulivyosasilisha taarifa hizo walikujibu nini ?Je wajumbe wa Kamati Walisema hawatafanyia Kazi ?Au Walisema watafanyia kazi?Walikupa tarehe ya mwisho ya kujifanyia Kazi 'deadline'? Nafahamu Hilo Swali kwa mwana Usalama aliyefundwa akafundika hawezi lijibu hadharani ila kwakuwa wewe Makonda ni Mlopokaji na hufahamu majukumu ya kofia zako zote mbili unaweza ni jibu hilo swali. Au Makonda ndiyo ameamua kuleta Habari zako za Kimbea ,majungu ,kujipendekeza Mbele Waziri Mkuu Majaliwa ?Ili uonekane wewe ni mfanyakazi bora kuliko Jeshi Polisi kupitia makamanda wao Sirro na Kanda ? Upuuzi mtupu. Je tukisema wale wahongaji hawakurudi tena kukuletea ile Rushwa ndiyo maana umeamua Kusema taarifa hizo hadharani? Mbona walivyokufuata ofisini kwako hukujitokeza hadharani kutuambia kuna wafanyabiashara 10 wa Shisha wamekufuata ofisini kutaka wakuhonge kiasi hicho cha Fedha na ukakataa? Kama uliamua kunyamaza kimya wakati walipokufuata kutaka kukuhonga Fedha kama unavyodai ,Tukuulize ni kitu sasa kimesukuma utoboe Siri hiyo hadharani hivi sasa? Hivi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hasa ya Mkoa wa Dar Es Salaam, Ina uwezekano mkubwa ikawa imefungwa CCTV kamera. Hivyo ni vyema Makonda atoe ushirikiano atakapotakiwa kufanya hivyo aseme Hao wafanyabiashara wa Shisha walikuja Lini ofisini kwake , ili watu wanaohusika na CCTV Kamera waweze kuwabaini kwa sura ikibidi na mazungumzo Yao ili ithibitike ni kweli walifika ofisini wake?walitaka Kumhonga kiasi hicho cha Fedha ?Na Hao watu 10 wasakwe wako jiwe waseme ni kweli walitaka Kumhonga Makonda kama Makonda alivyodai Mbele ya Umma? Aiingi akilini Mkuu wa Mkoa mzima anasema wafanyabiashara Hao haramu eti walifika ofisini kwake , anawafahamu kabisa ni wafanyabiashara haramu ,. Akakaa na kufanya nao mazungumzo ofisini kwake hadi wakamtajia na kiasi cha fedha watawachmpa halafu yeye Mkuu wa Mkoa ambaye lazima Atakuwa na walinzi ashindwe Kuwaeleza walinzi Hao wawakamate wafanyabiashara Hao ambao yeye amejinasibu Kuwa anawajua ni wanafanya Biashara hiyo haramu ya Shisha. Na katika mtazamo wa yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar Es Salaam, Hilo suala la yeye kutaka kuhongwa kiasi hicho cha Fedha na wafanyabiashara hao haramu 10 Narudia tena kumuuliza aliwasilisha mezani taarifa hiyo ? Inaoenekana Makonda alikuwa nania ovu ya kutaka kuzipokea maana kama alikuwa hatamani kuzipokea hizo Fedha kwanini hukuwasilisha taarifa hizo za yeye kutaka kuhongwa Kwenye Kamati ya Ulinzi Usalama ya Mkoa ambayo yeye ndiyo Mwenyekiti? Kwanini umesubiri Waziri Mkuu aje Kwenye sherehe za Uzinduzi wa Maboresho Upatikanaji wa Umeme Dar Es Salaam ,ndiyo useme Hilo? Makonda kijana mwenzangu umeacha Mashaka mengi sana Katika hili kwa sisi wananchi wako wa Mkoa wa Dar Es Salaam unaotuongoza . Umeonyesha hujui wajibu wako kwasababu wewe Ndiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na wewe ndiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo .Hufahamu sehemu ya kutoa taarifa au kushitaki ? Unasubiri shughuli za uzinduzi wa mradi maboresho ya umme ndiyo ushitaki hadharani mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa? Ni dhahiri hutufai maana tayari umeishapata doa. Nina mashaka na uwezo wake wa kiutendaji na uwezo wake wa kuchanganua mambo.Makonda umetuacha na maswali kama anajua majukumu yake ya Ya kofia ya Mkuu wa Mkoa na kofia ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa. Nashawishika kusema kuwa Makonda kama RC ,Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa ,akiwa pia ndiyo anayesimamia utendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam hafahamu majukumu yake tena hata kwa wale watendaji wake wa Moja kwa Moja yaani wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama. Na Pia Makonda kupitia matamko yake mbalimbali kuhusu sakata hilo ameonyesha hafahamu Maadili ya Kazi yake Kwani kama Angekuwa anajua Maadili ya kiongozi mwenye hadhi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa asingethubutu kupayuka Yale aliyoyatamka hadharani dhidi ya Kamanda Sirro na Kaganda pia asingethubutu kwenda Redio Clouds kwenda kuzungumzia ule upuuzi aliouongea kupitia Redio hiyo. Nasema ni upuuzi kwasababu Makonda kama Kweli an ajitambua yeye ni nani,ana madarakani siku ile ile aliposikia Waziri Mkuu Majaliwa alivyomshushua mbele za watu kwa kumtaka Makonda aache kulalamika afanyekazi na atekeleze maagizo toka viongozi wa juu, alivyosikia Kamanda Sirro alipozungumza na waandishi wa habari akisema kuwa operesheni ya kukamata waharifu wa makosa ya aina mbalimbali ikiwemo wauza dawa mbalimbali za kulevya imekuwa ikifanyika na inaendelea kufanyika na kwamba majarada ya uchunguzi wa watuhumiwa hao polisi wameyapeleka ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwaajiili ya hatua zaidi za kisheria na tayari na maana polisi hawana mamlaka ya kufungulia washitakiwa kesi za jinai mahakamani mwenye jukumu hilo ni Mkurugenzi wa Mashitaka ( DPP) . Na ni kweli kifungu cha 9 cha Sheria ya Taifa ya Huduma ya Uendeshaji wa mashauri ya Jinai Na. 27 ya Mwaka 2008 , inasema DPP ndiyo mwenye Mahakama ya Kufungua na kuendesha Kesi za jinai mahakamani kwaniaba ya serikali. Na aliposikia Jeshi la Polisi Makao Makuu Kupitia Kamanda Robert Boaz Kuwa Jeshi la Polisi limeanza kufanyia uchunguzi wa shutuma za Makonda dhidi ya Makamanda wake Sirro na Kaganda, RC -Makonda angefunga mdomo wake kwa kunyamaza kimya kimya lakini sijui ni Utoto ,ulimbukeni akaendelea kuongea tu Mara kuhojiwa Redio Clouds Mara kunukuliwa na Gazeti moja akitamba Kuwa ataendelea kuwachongea. Aibu gani hii jamani! Ni wakati mwafaka wa Makonda arudishwe darsani ili akapewe mafunzo yatakayomwezeka kufahamu majukumu yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na majukumu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Waswahili wanasema Dalili za Mvua ni Mawingu. Hivyo kama Leo hii Mwenyekiti Huyo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama RC Makonda ameshindwa kutumia majukwaa sahihi ( Proper Forum) yakupeleka malalamiko yake badala yake anatumia vyombo Vya Habari na kusubiri kudandia mkutano wa Waziri Mkuu kulalama tena mambo mengi ambayo ambayo yanapandikiza Chuki baina ya wananchi na Jeshi la Polisi Kuwa Jeshi la Polisi ndiyo linalowalea wauza Shisha kwasababu ha liwachukulii Hatua basi ipo siku Makonda Atakuja kuropoka mambo Siri ya vikao Vya Kamati ya Ulinzi Usalama kupitia Vyombo Vya Bahari kwa Lengo la kutaka kujionyesha yeye ni mchapakazi kuliko watumishi wengine wowote . Na ushahidi ni Yale mahojiano aliyoyafanya a Redio Clouds ambayo Clip yake ninayo ambayo Makonda kwa kinywa Chake anamtuhumu Sirro ambaye ni mjumbe wake wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Kuwa amekuwa alimpa taarifa za uongo kuhusu Biashara ya haramu ya Shisha. Sasa kama Mwenyekiti wa Kamati hiyo analalamikia mjumbe wake wa Kamati hiyo hadharani tena Kwa zaidi ya Mara Moja , ni wazi RC Makonda Hana Imani na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam ambalo ndilo Hilo Hilo Askari wake wanamlinda nyumbani anakoishi na ofisini. Lakini hata kama ni kweli Kamanda Sirro alikuwa akikupa taarifa za uongo kuhusu Shisha ,Sirro na wewe Makonda wote ni wateule wa Rais John Magufuli . Je Makonda ulishawahi pia kwenda kumweleza Rais Magufuli,au boss wa Sirro ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Kuwa Sirro amekuwa akikupa taarifa za uongo na auridhishwi na Utendaji wake? Makonda umedai Jeshi la Polisi limekuwa likisita kuchukulia Hatua wafanyabiashara haramu ya dawa za kulevya, hivyo Jeshi la Polisi Leo Hii likiibuka na takwimu za Kuonyesha Jeshi Hilo limekuwa likichukua Hatua Kabla hata ya wewe kufikiri wa au wewe kufikiria utakuja Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam sura yako Utaiweka wapi? Maana Mimi ni shahidi mahakamani nimekuwa nikishuhudia Mkurugenzi wa Mashitaka aliwashitaki watuhumiwa mbalimbali wa makosa ya dawa kulevya ambao Chanzo cha washitakiwa Hao kushitakiwa ni walidaiwa Kutenda makosa hayo na walikamatwa na Jeshi la Polisi. Elewa Uhalifu ulikuwepo toka enzi na Enzi na serikali ya awamu ya tano imeukuta na itauacha na haiwezi kuukomoesha maana kila kukicha wahalifu wanabuni mbinu mpya za kufanya Uhalifu. Hivyo hata wewe Makonda Biashara ya dawa kulevya umeikuta hapa Dar Es Salaam na Duniani kwa ujumla. Usijidanganye Huna Nguvu wala mamlaka ya Kupambana nayo kwasababu Huna Mafunzo ya kutambua hizi dawa za kulevya, kukamata wenye hiyo taaluma wapo ndani ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Kuthibiti Dawa za Kulevya Chenye Ofisi zake Barabara ya Kilwa Dar es Salaam. Umejitapa kupitia Redio Clouds Kuwa umekamata dawa za kulevya aina ya Shisha . Mina Kuuliza una Hakika gani hizo ni dawa za kulevya? Hivi hizo unazodai ni Shisha ulizokimata zikichukuliwa zikapelekwa kwa wataalamu wakazikagua kitaalamu Kisha wakaja kutoa ripoti Kuwa hizo siyo Dawa za kulevya utasema nini?Acha wenye taaluma za Kupambana na dawa za kulevya wafanyakazi Yao.Wewe taaluma hiyo Huna. Mkuu wa Mkoa Mzima unaacha kushughulika na mambo makubwa makubwa unaamua kujigeuza 'korokoroni 'unaenda kukamata Shisha na vifaa Vya Kuvutia Shisha wakati Polisi wenye vyeo Vya chini wa kufanyakazi ya ukamataji wapo na wala hawakueleza wameshindwa kukamata hivyo wa naomba utasaidie. Hivi Hao wahalifu wa Shisha unaowafuata hadi Kwenye vijiwe vyao Vya Kuvuta Shisha na bangi wakikumwagia Kinyesi usoni utalia na nani? Fanyakazi yako uliyotumwa na vyombo Vya Ulinzi na Usalama ambayo ndiyo wenye taaluma ya Ulinzi na Usalama wafanyakazi Yao kwa Uhuru .Heshimu wakubwa wako ,Chagua matamshi ya kuzungumza Mbele ya hadhara dhidi ya viongozi wenzako. We bado ni kijana Mdogo sana bado unaitaji kulelewa na wanasiasa wenzako,wanausalama hivyo haina maana wewe kujiingiza Katika msuguano na Jeshi la Polisi kupitia Kamanda Sirro na Kaganda. Kushangaa siku Moja kitendo hicho kikaja kukugharimu. Aidha Makonda kaa chini ujitathimini na utafakari hicho ulichokifanya ambacho kutokana na matamshi yako ambacho kimezusha mjadala na kufanya watu Tutulie Mashaka uwezo wa Utendaji wako . Kisha wewe binafsi ujiulize Je ulikuwa sahihi wakati ukifanya hayo uliyoyafanya kwa mujibu wa maadili ya kofia zako mbili za kimadaraka? Kisha ujipime wewe mwenyewe mwisho uchukue maamuzi. Nimalize makala hii kwa kukushauri Makonda Kuwa ' Usiwe na haraka kuliko Upesi'. Mji huu wa Dar Es Salaam Una Masharti hadi ufanikiwe ,sio kuvaa Masharti /Suti ukajiona wa maana . Acha tabia na kutaka kujipatia Umaarufu wa chee kwa mambo yasiyo na tija . Naomba kutoa hoja. Mungu ibariki Tanzania Chanzo: Facebook: Happy Katabazi Blogg: www.katabazihappy.com 0716 774494 21/11/2016

SERIKALI IAINISHE HAYA MISAADA YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

Na Happiness Katabazi ITAKUMBUKWA Kuwa 10/9/2016 saa 9 Alasiri maeneo ya Kanda ya Ziwa na hasa MKoa wa Kagera yalipatwa na tetemeko la Ardhi linalokadiriwa Kuwa na ukubwa wa 5.9 Katika vipimo Vya Richter. Tetemeko Hilo lilisababisha athari mbalimbali zikiwemo Vifo ,majeruhi,uharibifu wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi . Jumla ya watu 17 wa lipoteza Maisha na 560 kujeruhiwa kutokana na maafa hayo. Kwa siku Kadhaa sasa Kumekuwa na taarifa zikisambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyama Vya siasa Vya upinzani vimetoa matamko ya kupinga uamuzi wa Serikali kutumia Rasilimali zilizopatikana kwa michango ya kuwasaidia waathirika na kuendelea kuwarekebishia miundombinu muhimu kwa Maisha na manufaa ya wakazi wa Kagera. Wanaopinga uamuzi huo wa serikali wengine wamediriki Kusema " serikali ya Rais John Magufuli imetafuna Fedha za Waathirika wa Tetemeko Kagera', ' serikali ya CCM imekula hela za Ubani' ,wengine wanasema serikali ingie tafuta Fedha zake zenyewe ndiyo ijengee miundombinu na siyo Kujenga miundombinu kwa kutumia Fedha za michango waliochangiwa waathirika wa tetemeko la Kagera. Lakini Novemba 15 Mwaka huu ,serikali ilitoa tamko lake na kupinga Madai hayo na Kusema huo ni upotoshaji kuhusu Hatua zikizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa Katika kukabiliana na maafa hayo. Serikali ikasema ukweli ni kwamba serikali kwa kushirikiana na wadau Imechukua Hatua kubwa za kuwasaidia waathirika na inaendelea kufanya Hivyo . Ili kuleta uhalisia wa takwimu za Fedha ya maafa zilizotolewa kwa walengwa na wahisani mbalimbali,wananchi wangependa kupata data zifuatazo ili kuwaondoa wasiwasi ; Jumla ya Majina ya watu 17 waliopokea Maisha pamoja na kutaja familia zao. Majina ya majeruhi 569 kwa kutaja kila kaya na Hospitali zilizotoa matibabu na tarehe waliopatiwa matibabu na aina gani ya matibabu. Gharama za Mazishi kwa Kila kilichochogharamiwa kwa watu 17. Majina ya Wahanga waliyopewa Chakula kwa kutaja kiasi cha Chakula kwa kila Mhanga ,Madawa,nguo za aina gani na makazi yapi kwa kutaja kila Muhanga na kaya yake. Huduma za Tiba, Matunda aina gani na mangapi kwa kila mwathirika na vifaa gani na kwa kila shule na thamani. Vyote Hivyo viwekwe Kwenye Tovuti ya serikali ili watu waone na wale wanaosambaza kile serikali inachoita ni upotoshaji waumbuke na hiyo ndiyo sifa Moja ya wapo ya serikali yoyote Duniani inayowajibika kwa uwazi. Hata hivyo baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu niliyozungumza nao wamenitbitishia Kuwa kweli serikali ilitoa Sh.Milioni 1.8 kwa familia ya marehemu kama mkono wa pole .Ni jambo Jema. Baadhi ya wananchi wangependa kufahamu tathimini ya maafa yaliyotokea ya Yalifanywa Kwa watu gani ,majengo ya aina gani na kwa watu wa aina gani kama masikini ,wazee,matajiri,majeruhi . Kwa mujibu wa taarifa ya serikali inaonyesha jumla ya Fedha taslimu iliyopo kelewa Katika Akaunti ya Benki ya Maafa ni Sh.5,412,984,934.82 na Sh 17,579,427.00 zilipo kelewa na serikali kwa njia ya mitandao ya simu. Serikali ilisema imeishapokea misaada mingine yenye thamani ya Sh.bilioni 2.25 kama ifuatavyo : Unga Tani 58.12, Sukari Mifuko 1,150 , Mchele gani 133.96 ,Maharage Tani 19.666,mahindi Tani 70.1 na majani ya chai Tani 3. Wananchi wangependa vilevile kupata orodha ya Majina waliyopatiwa vitu hivyo toka kila Wilaya ,Mkoa na Kaya na kiasia gani kwa kila mtu na vilevile wangetaka kujua kama kulikuwa na Tatizo la Maji Katika Mkoa wa Kagera hadi ukatolewa msaada wa Maji kwa walengwa. Kuhusu miundo mbinu ya barabara Je ni barabara ngapi zimejengwa na Tenda ilifanyakazi lini gharama?gharama ya utengenezaji wa barabara ulifikiwaje na makandarasi na Wakandarasi wapi walipewa Kazi hiyo ? Mifuko ya Saruji 2,300 yenye thamani ya Sh.39,000,000 iliyotolewa na Shirika la World Vision iligawiwa kwa akina nani Katika Kaya 460 zilizotajwa na kila mfuko uligharamia kiasia gani? Wananchi wanataka kujua serikali ilivyokuwa ikiwaamasisha wachangie misaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi walioanisha Makundi ya watu Maskini ,wazee,wajane na walemavu? Au waathirika? Na tathimini ya kipato imefanyika lini? Kama ndivyo Mbona serikali inapanga Kujenga Taasisi kwa kutumia Fedha za misaada badala ya kutumia Fedha za serikali? Je serikali inawekwa katika kundi lipi Kati ya walemavu ,wajane na wazee au ni Maskini ?Kama ndivyo kwa nini msaada haukufikishwa kwa kila Muhanga? Kama watu waathirika mtaji mkubwa ni nyumba zilizoharibika na hatakuwa na taarifa za Njaa kwa Sababu zilizoharibika ni nyumba za makazi na si Mazao Kwa hayo machache baadhi ya wanachi tungependa kumjulishwa na kumfafanuliwa vizuri kuhusu jinsi gani misaada iliyotolewa ilivyogawiwa na Sababu ya kufanya msaada hiyo kugeuzwa Kujenga Taasisi za serikali wakati Taasisi hizo zinapaswa Kujengwa kwa Fedha za serikali. Ikumbukwe Fedha hizi haziitaji Uhakiki kama Fedha za mikopo ya wanafunzi wa Elimu yaVyuo Vikuu ambazo Fedha za Bodi ya Mikopo zinataja vigezo wa wanufaika wa mikopo Kigezo Kimoja wapo ni watoto wa masikini . Misaada na Fedha zilitolewa na makundi mbalimbali kwa waathirika wa Kagera zilitolewa kwa waathirika wote bila kubagua kundi lolote. Mungu ibariki Tanzania Chanzo:Facebook: Happy Katabazi Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com 0716 774494 19/11/2016.

SPIKA SAMUEL SITTA AMEKWENDA HATORUDI

Na Happiness Katabazi KWELI udongo auvimbiwi. Utammeza pia mpendwa wetu,Wakili msomi na mwanasiasa machachari Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano WA Tanzania, Samuel Sitta ambaye amefariki Alfajiri ya Leo 7/11/2016 katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa amelazwa kwaajili ya matibabu. Mwanasiasa huyu nilimpenda licha kuna kipindi alivyokuwa spika wa bunge alikuwa Anatoka nje ya mstari na niliwahi kumuonya kupitia makala yenye kichwa cha habari kisemacho: " SPIKA SAMUEL SITTA NI FISADI PIA?". Sitta alichukuia dhuruma, ubadhilifu wa mali za Umma. Enzi akiwa spika, bunge Lake ndiyo liliunda kamati ya kuchunguza mkataba wa kampuni ya Richmond ambayo kamati ya Bunge Februali 2008 iliyokuwa inaongozwa na Mbunge Wa Kyela ambaye sasa ni Waziri, Dk.. Harrison Mwakyembe kusababisha aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo, Edward Lowassa, waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, Msabaha kujiudhuru nyadhifa zao. Nitamkumbuka Sitta kwa kauli yake hii aliyowahi kumjibu aliyewahi kuwa Mbunge Wa Mkuranga, Adam Malima ulipotokeaga mzozo bungeni Sitta akiwa Spika. Mzozo huo ulimhusu mmiliki wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi Kuwa anatumia vibaya vyombo vyake Malima akalalamika. Spika Sitta alitoa kauli hii "Malima apuuzwe'. Malima aliendelea kulalamika Sitta akajibu hivi " Akashtaki hata kwa Shetani". Kila nikikumbuka majibu hayo ya Sitta nacheka Sana. Sitta nitamkumbuka na msemo wake wa Mafisadi. Naweza kusema Sitta alikuwa mwanasiasa jasiri, mwenye historia ya kupanda na kushuka katika ulingo wa Siasa. Mara ya kwanza kukukutana na Sitta ilikuwa January 2007 ,sebuleni kwake Masaki, Dar es Salaam, nikiwa Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima., nilienda kufanya naye mahojiano kuhusu mchakato wa Kamati Richmond umefikia wapi. Tulizungumza Mambo mengi sana na akanitazama akasema Huku akinitazama usoni akasema "Amebaini mimi ni mwanamke jasiri".Na akanitaka nisibadilke. Sikumuelewa Sitta kwa kauli yake hiyo lakini kadri siku zinavyosonga mbele pia kuna watu wazima na wenye madaraka na wasiyo na madaraka kwa nyakati tofauti wamekuwa wakinitamkia hivyo Kama alivyonitamkia Mzee Sitta Kuwa Mimi Happiness Katabazi ni jasiri Sana. HISTORIA YA MAREHEMU SPIKA SAMUEL SITTA Samuel John Sitta alizaliwa Desemba 18, 1942 huko wilayani Urambo Mkoa wa Tabora. Sitta alisoma Shule ya Msingi Urambo kati ya mwaka 1950 – 1953, kisha alikwenda Wilaya ya Sikonge mwaka 1954 - 1957 na kuendelea na masomo ya “Middle School” katika shule ya “Sikonge Middle School”. Baadaye mwaka 1958 – 1963 alianza masomo ya sekondari Shule ya Wavulana Tabora yaani “Tabora Boys” kidato cha I – IV na cha V – VI. Mara tu baada ya kuhitimu masomo ya sekondari, Sitta alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusomea Shahada ya Sheria (L LB) mwaka 1964 na kuhitimu mwaka 1971. Sitta amesoma shahada yake kwa miaka 7 kwa sababu mwaka 1966, wakati yuko mwaka wa pili na akiwa kiongozi wa wanafunzi UDSM, wanafunzi waligoma na kuandamana kupinga kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kukatwa mishahara yao baada ya JKT. Hoja ya wanafunzi ilikuwa na mantiki kubwa, kwamba mbona vigogo wa serikali na wanasiasa wanalipwa mishahara minono na marupurupu makubwa? Baada ya shinikizo hilo la wanafunzi Mwalimu Julius Nyerere alikubali kupunguza mshahara wake wa Sh4,000 bila kodi akaagiza pia mishahara ya mawaziri ipunguzwe kwa asilimia mbili. Miezi miwili baadaye akatangaza Azimio la Arusha (Februari 5, 1967) kuyapa uzito malalamiko ya wanafunzi hao. Watukutu wawili – Sitta na Wilfred Mwabulambo (sasa marehemu) na wengine kadhaa – waliojitia wazimu na kutetea kile walichokiita haki zao, (haki za wakulima na wafanyakazi), walimshutumu Mwalimu Nyerere kwa maneno makali wakidai “…ni heri wakati wa ukoloni kuliko utawala wa Mwalimu”. Mwalimu Nyerere alikasirika na kuwafukuza chuo wanafunzi wote 400 kwa kile alichokiita “kwenda kufunzwa adabu majumbani mwao”. Miezi kumi baadaye, baada ya Nyerere kushawishiwa na hasira kutulia akaamua kuwarudisha chuoni wanafunzi 392. Viongozi wa mgomo; Sitta na wenzake 7 walitiliwa ngumu, hawakurejeshwa chuoni. Busara za viongozi wa chuo zilifanya Mwalimu aliliwe zaidi na kuandikiwa barua mbili maalumu na chuo zenye Kumb. Na. C3/Sa.13 ya 2/3/1967 na C3/Ss.13 ya 9/07/1967. Mwalimu alikubali kilio hicho na kuwaruhusu vijana hao wanane warudi kwa sharti kwamba wale watukutu wawili (Sitta na Mwabulambo) watandikwe viboko na “Mwalimu Nyerere” mwenyewe. Hii ndiyo ilikuwa pona ya Sitta ambaye alirejea UDSM na kuendelea na masomo kwa miaka kadhaa hadi alipohitimu mwaka 1971. Wakati Sitta anarudi chuoni tayari alikuwa mwajiriwa wa Kampuni ya Mafuta ya “CALTEX OIL” kama Meneja wa Tawi (1967 – 1969) na mwaka 1969 – 1975 aliajiriwa na Shirika la Maendeleo la Taifa kama Katibu na Mkurugenzi wa Utawala. Baadaye mwaka 1976 Sitta aliamua kujiendeleza kielimu katika masuala ya Usimamizi nchini Uswisi kwenye Chuo Kikuu cha IMEDE ambako alihitimu Stashahada ya Juu ya Usimamizi mwaka huohuo 1976. Chini ya mfumo wa chama kimoja, Sitta amekuwa kiongozi wa juu wa CCM na serikali akiwa mbunge, mkuu wa mkoa na waziri katika nyakati tofauti na ameendelea kuwa mbunge na waziri katika mfumo wa vyama vingi. Sitta amemuoa Margareth Simwanza Sitta na wana familia imara. Mbio za ubunge Enzi za chama kimoja 1975 - 1995 Sitta amekuwa mbunge wa Jimbo la Urambo (kabla halijagawanywa na kuwa Urambo Magharibi na Mashariki) na pia alifanikiwa kuwa waziri kwa nyakati tofauti. Kwa mfano wakati wa kipindi cha mwisho cha Mzee Mwinyi, Sitta alikuwa Waziri za Katiba na Sheria. Mwaka 1995 Sitta aliingia kwenye mapambano mapya ya siasa za vyama vingi na kwa bahati mbaya akawa mmoja wa vigogo walioangushwa na wabunge wa NCCR. Mshindani wake mkuu alikuwa Msina Jacob Abraham. Msina alishinda kwa kura 10,788 dhidi ya 9,497 za Sitta. Sitta alirudi tena kwenye jukwaa la siasa mwaka 2005 kwenye uchaguzi mkuu na aliwashinda wapinzani wake wakuu Lumatiliza Yotamu Lubungila wa NCCR na Wilson George Ntakamulenga wa CUF. Sitta alipata kura 28,660 (72.3%) na kurejesha heshima yake jimboni Urambo Mashariki. Kurudi kwa nguvu kulimpa nafasi ya kuwania na kuteuliwa na CCM kugombea uspika wa Bunge la Tanzania na akaliongoza Bunge la Tisa kwa mafanikio na changamoto nyingi. Mwaka 2010 Sitta alishiriki tena uchaguzi Urambo Mashariki akawashinda wapinzani wake wakuu Msafiri Abdulrahmani Mtemelwa (Chadema) na Zombwe Lotto Edward (CUF) kwa kupata kura 19,947 (70.47%). Baada ya ushindi huo, Sitta alijaribu tena kuwania uspika bila mafanikio; utendaji wake wa kuiuma serikali na wakati mwingine kuipuliza kwenye Bunge la Tisa ulimfanya achukiwe na serikali. Ilipoonekana ana nguvu akatengenezewa “chui wa karatasi” (mshindani), Andrew Chenge. Chenge naye akachukua fomu ya uspika ghafla, likatengenezwa ‘zengwe’ kuwa wagombea wote wana nguvu, hapo CCM ikapata mwanya wa kutamka kuwa haiwataki wote ili kuondoa mvutano. Sitta akapoteza ndoto za uspika na ukahamia kwa mwanamama Anne Makinda. Rais Jakaya Kikwete alipotangaza Baraza la Mawaziri mwaka 2010 alimpa Sitta Wizara ya Afrika Mashariki kama Waziri, wadhifa aliodumu nao hadi mwaka jana mwanzoni alipobadilishwa na kupelekwa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi. Mbio za urais Samuel John Sitta alianza mbio za urais “kimyakimya” tangu alipokuwa Spika wa Bunge la Tisa (2005 – 2010). Kuna nyakati alikuwa akitoa kauli zinazoashiria kuwa nchi inayumba na haina uongozi thabiti huku akionyesha kuwa nchi ina viongozi thabiti na hawajapewa uongozi mkuu wa nchi, akiwemo yeye. Hata alipoliongoza Bunge la Katiba mwaka 2014, mara nyingi Sitta alionekana kama mtu mwenye shauku kubwa na urais na alipohojiwa, mara kwa mara, juu ya urais alionyesha ana ndoto hizo. Mara kadhaa, alilalamika kuwa wala rushwa wakubwa wanampiga vita kwa sababu ni msafi. Mungu aiweke roho ya Marehemu Spika Sitta mahali panapostahili. Chanzo:Facebook.Happy Katabazi Blog. www. katabazihappy.blogspot.com 7/11/2016. 0716 774494

RAIS MAGUFULI BADILIKA



Na Happiness Katabazi

EZEKIELI 3:19 Katika Biblia inasema , " Lakini ukimwonya mtu Mbaya ,wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake Mbaya ,atakufa Katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.

Nimelazimika kutumia nukuu hiyo ya Kitabu cha Ezekieli kinachopatikana Ndani ya Biblia kwasababu Leo Rais Dk.John Magufulianatimiza Mwaka mmoja tangu alipo apishwa 5/11/2015 Kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Makala hii ambayo itajadili mazuri,  mazuri yaliyofanywa,Udhahifu iliyojitokeza na nitatoa ushauri / mapendekezo yangu ya mambo gani yarekebishwe ili taifa liweze kupiga Hatua zaidi Katika Kipindi cha Mwaka mmoja wa Utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli.


Hakuna Siri  Kuwa  Katika kampeni za uchaguzi Mkuu Mwaka 2015 ,Mimi niliutangazia umma Kuwa nitafunga mkono mgombea wa urais wa CCM ambaye alikuwa Dk.Magufuli ambaye alifanikiwa na ndiyo amekuwa rais wa Tanzania kwasasa .

Wakati nilipotangaza uamuzi huo wa Kumuunga mkono mgombea urais wa CCM ,pia nilisema licha Katika kampeni hizi Nitamuunga mkono mgombea urais wa CCM pia uchaguzi ukimalizika mgombea Huyo akafanikiwa akiwa rais wa nchini, nitaendelea Kumuunga mkono kwa Hali yoyote ile na sitamuonea haya kumkosoa kupitia kalamu yangu pindi ninapoona anatoka nje ya mstari.

Uamuzi wangu huo uliwakera wale ambao walikuwa wanaichukia CCM na walikuwa wakinitukana  matusi ya nguoni, kunitolea lugha za vitisho mkebehi na kusababisha nikabadili nyendo zangu ki aina  na wengine walidiriki kunipachika jina la Happiness Katabazi ni ' awala wa Magufuli 'ndiyo maana nampigia  debe lakini ukweli ni kwamba Magufuli hanifahamu hata kwa sura. 

Nimewasamehe bure ila walichobakiza hivi sasa wananitania jina ' Happiness Katabazi ni Mrs Magufuli ' mke wa Magufuli na Mimi nawajibu sawa Magufuli ni My Husband'.

Turejee Kwenye  mada yetu ya Msingi.Kwanza kabisa Nakupongeza Rais Magufuli Leo kuweza kutimiza Mwaka mmoja ukiwa madarakani ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kukupa Afya hadi umefikisha umri huo pia nipongeze Timu yako yaani watumishi wa ngazi zote unapofanya nao Kazi Kwani Katika Kipindi hiki cha Mwaka mmoja kuna baadhi ya mambo ya maana nimeyafanya ambayo yanastahili pongezi nanitayataja hapa chini.

Jambo la kwanza ni la chini ya serikali ya Magufuli ,Watanzania tumefundishwa uchumi/ Kubana matumizi.

Hapa namaanisha Kuwa tangu Magufuli Aingie madarakani upatikanaji wa fedha umekuwa mgumu kwa wananchi waliowengi kwasababu mbalimbali na hili kumethibitishwa na Gavana wa Benki Kuu Professa Benno Ndullu hivi karibuni.

Hali hiyo imesababisha Leo hii Watanzania tuondokane na tabia ya kutumia Fedha Katika matumizi yasiyo ya lazima, Umuhimu.

Pia Hali hiyo imetufanya tuwe na nidhamu na fedha tunazozimiliki au tunazotarajia kuzipata kwasababu Tayari tumeishaona ukizifuja  Fedha hivi sasa kuzipata tena siyo Kazi rahisi.

Tuwe wa kweli hapo awali Watanzania Wengi  tulikuwa Hatuna nidhamu ya matumizi ya Fedha, ukipata Fedha Leo wakati mwingine unaziingiza Katika matumizi yasiyo na Umuhimu kwa wakati ule kwasababu unauhakika Kesho utapata Fedha kirahisi na kweli Fedha ilikuwa nyingi mitaani na mikononi mwa watu tofauti na ilivyo hivi sasa. Hali hiyo ina faida zake na Hasara pia Hilo pia tulijue.

Pili, Utawala wa serikali ya awamu ya Tano umeondoa ile Hali ya baadhi ya genge la watu kujiona wao wapo juu ya Sheria kuliko wengine.

 Napongeza Katika Hilo Kwani hapo awali Kabla ya serikali hii kuingia madarakani kuna baadhi ya wananchi wenzetu walikuwa wakiwafanyia baadhi ya wananchi wenzao mambo yasiyofaa kwakigezo wao wapo juu ya Sheria na wanajua na viongozi.

Katika Kipindi hiki kwa uchunguzi wangu Hali hii ni kama imepungua kila mmoja anaogopa kujitapa Kuwa atakufanyia uhuni na huwezi kumfanyia chochote kwasababu anafahamia na vigogo serikalini.

Tatu, serikali ya awamu ya tano ndani ya muda mfupi imeweza kununua Ndege ili kutoa huduma na kuongeza pato la taifa.Napongeza licha siyo kipaumbele kwa Watanzania waliowengi Kwani ni Watanzania Wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za kununua Ndege.

Nne, watu wamekuwa na Mwamko mkubwa wa kulipa kodi mbalimbali kwakuogopa kushughulikiwa na serikali.Napongeza hili.Licha hata Katika Enzi za Utawala wa Serikali ya Rais Mstaafu Kikwete watu walikuwa Wakilipa kodi pia .

Tano,Bar za kuuza Pombe zenye leseni za kufanya Biashara mwisho saa Sita usiku kweli Bar nyingi nimeshuhudia ndani ya Kipindi ya serikali ya awamu ya tano kweli zinatekeleza agizo la kufayabiashara kwa mujibu wa leseni zao zinavyowataka hazikeshi kama zamani licha kuna baadhi ya bar hizo zina funga bar hizo Polisi wakipita wanaona zimefungwa ila zinawaingiza vyumba Vya ndani   wateja wake wanaendelea Kunywa Pombe kama kawaida.

Hata hivyo lile agizo la rais Magufuli alilotaka mchezo wa Pulltable usichezwe wakati wa kazi nikama halitekelezwi kwa vitendo kwani katika uchunguzi wangu baadhi ya bar ,watu wamekuwa wakicheza mchezo huo kama kawaida wakati wa kazi na kuuza Pombe muda wa kazi wakati wa hawana leseni ya kuuza pombe muda wakazi licha wafanyabiashara wengine wanauza kwa vificho.

Kwa asilimia 50 Napongeza Katika hili licha utekelezaji huu unawakera wanywaji Pombe wanaopenda Kunywa Pombe mchana hadi usiku wa manane na pia wafanyabiashara wa Bar Kwani wafanyabiashara Hao wanadai linawakoseshea wateja Wengi.

Tano,ni dhamu Katika baadhi ya Ofisi za watumishi wa umma imerejea Kwani kuna baadhi ya watumishi umma walikuwa hawana nidhamu Katika Ofisi zao na walikuwa hawatoi huduma kwa wananchi inavyotakiwa kwasababu tofauti ikiwemo Rushwa, jeuri,dharau au Ujinga wao tu.

Licha Katika hili la nidhamu ,napenda nisema Kuwa kuna baadhi ya watumishi wa umma tangu Magufuli Aingie madarakani wamekuwa wakifanyakazi kwa nidhamu ya woga wa kumuogopa Magufuli atafukuza kazi ,kuwasimamisha, au,kuwakaribia mbele za watu hivyo wamekuwa wakitenda Kazi kwa hofu badala ya taaluma zao na hili ni jambo Moja baya sana Kwani mtu anayefanya kazi kwa hofu,nidhamu ya woga mtu Huyo hawezi kufanyakazi vizuri mwisho wa siku ataaribu Kazi.

Licha Mara Kadhaa Rais Magufuli amekuwa akinukuliwa akiwata watumishi waache hofu wafanyakazi na kwamba mtu ambaye si mchafu kwanini awe na hofu?. Ukweli ni kwamba baadhi ya watumishi wa umma hivi sasa  hofu .

Katika maumbile ya ki binadamu lazima tukubaliane kwamba binadamu wote hatulingani kuna wanaojiamini ,hawana hofu na kitu chochote hata kama anatenda matendo machafu lakini kuna binadamu mwingine tena wengine ni wasomi wazuri tu lakini hawajiamini ,ni Waoga wapo tayari kuacha kufanyakazi kwa umakini lakini kwa woga walionao wanaamua kufanyakazi chini ya Kiwango kwa Lengo la kumfurahisha kiongozi .

Watu wa aina hii wapo Katika Jamii yetu. Ila Kwasisi tunaosali Biblia inasema hofu ni dhambi.

Sita, Hali ya Usalama wa nchi ni shwari kwa kiasi kikubwa licha ya kuwepo matukio ya hapa na pale ya Uhalifu lakini vyombo Vya dola vinajitahidi kadri ya uwezo wake kukabiliana na matukio hayo na moja ya ushahidi wa Hilo tangu serikali ya awamu ya tano ingie madarakani Mara kwa Mara tumeshuhudia Makamanda wa Polisi wa Mikoa Kadhaa waliripotiwa kutoa taarifa Kuwa Askari Polisi wa Mikoa Yao wamefanikiwa kuwaua kwa risasi watu waliwashuhuku Kuwa ni majambazi Kabla ya watu Hao kutekeleza matendo ya ujambazi na baadhi ya mapolisi kujeruhiwa na Kuuwawa Katika mapambano hayo na kuwakamata na kuwafikisha mahakamani.

Saba, Katika Kipindi cha Mwaka mmoja cha Utawala wako Rais Magufuli ameonyesha nia ya  kukuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ,kwasababu mikutano yako na viongozi mbalimbali ya Kimataifa iliyofanyika Ikulu Dar Es Salaam,Rais Magufuli umekuwa ukitumia lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano.

Oktoba 24 Mwaka huu,Mfamle wa Morocco ,Mohamed VI. Julai 10 Mwaka huu Waziri Mkuu wa India ,Narendra Modi .Machi 8 Mwaka huu, Rais wa Vietenam,Trouung Tan Sang.

Oktoba 2 Mwaka huu,Makamu wa Rais wa Cuba ,Savador Antonio , Julai Mosi Mwaka huu , Rais wa Rwanda ,Paul Kagame ,Oktoba 12 Mwaka huu, Rais wa Congo ,Joseph Kabila wote waliwasili nchini kwa tarehe hizo nilizozitaja hapo juu na walifanya mazungumzo na Rais Magufuli ambapo Rais Magufuli alitumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano.

Nakupongeza Katika hili Kwani unakuza lugha ya Kiswahili kama kiongozi wa nchi inayozungumza lugha ya Kiswahili.

Nane, Mwamko wa elimu bure imeongeza usajili wa wanafunzi Kwani wanafunzi 800,000 wamedahiliwa  ndani ya Miezi miwili.Inaelezwa Kuwa Januari Mwaka huu,wanafunzi wa darasa la kwanza milioni 1.8 sawa na asilimia 84.5 walidahiliwa kujiunga Darasa la kwanza tofauti na Mwaka na Mwaka Jana ambao wanafunzi 128,000 tu ndiyo walidahiliwa. 

Wanafunzi waliojiandikisha na elimu ya kidato cha kwanza wameongezeka  kwa asilimia  26  .

Na kila mwezi serikali inatoa Sh.bilioni 18.77   kwaajili ya kwenda kutekeleza elimu bure licha inachangamoto zake.


Aidha Katika Mpango wa elimu bure pia  Julai 14 Mwaka huu, Rais Magufuli Alizindua Mpango wa ugawaji wa madawati Kwenye majimbo y uchaguzi nchini,alisema tangu atoe agizo la kila Halmashauri inapaswa kuhakikisha shule zake zina madawati ya kutosha ,wananchi ,Wadau na Mashirika mbalimbali waliitikia kwa Mwamko.


Tisa,serikali imeongeza mikopo ya elimu ya juu kutoka Sh Bilioni 340 Mwaka 2015/2016 hadi Sh .Bilioni 483 Mwaka huu wa Fedha na Tayari mikopo hiyo imeanza kutolewa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Vya vikuu licha ya kuwepo kwa dosari za hapa na pale.

Kumi,Julai 7 Mwaka huu, ilibaini Mabadiliko madogo ya sheria zilizoandikwa ( The Written Laws ( Miscellaneous Amendments ) Act 2016 Act No.3 of 2016'.

Mabadiliko hayo yalifuta  baadhi ya maneno yaliyokuwa yanasomeka Katika ki fungu cha 18  (a,b) Magistrates Court Act, ambacho kilikuwa kinatoa mamlaka kwa Mahakama za Mwanzo kusikiliza kesi zenye thamani ya Sh.Milioni tano kushuka chini  na Act  (CAP .11 ) ambapo Kifungu cha 20 kilichofanyia marekebisho ya Kifungu cha 18 ,Mahakama za mwanzo zimepewa mamlaka kusikiliza Kesi zenye thamani ya sh.milioni 30 badala ya sh.milioni tano.ni jambo la kupongeza Kwani litasaidia kuondoa mrundikano wa Kesi Katika Mahakama za Wilaya ,Mikoa na Mahakama Kuu kwasababu Kesi hizi zitakuwa zinasikilizwa Mahakama za Mwanzo na kumalizika kwa haraka.

Aidha imekuwa ikielezwa Kuwa  uchumi wa nchi yetu mwaka jana ulikuwa wa asilimia 7  ,mwaka huu tumekusudia ukue kwa asilimia 7.2.

  Mfumuko wa bei umeshuka kutoka asilimia 7 hadi asilimia 4.5. Ni Ishara nzuri sote tushirikiane tufikie Malengo tuliyojiwekea.Ni jambo Jema.

MAPUNGUFU

Pungufu la kwanza ambalo tayari limeishamtia doa na linazidi kumpaka matope   Rais wetu ni hili la wananchi Wengi wamekuwa wakituhumu serikali yake inakandamiza Demokrasia waziwazi ,rais Magufuli wakati mwingine anatoa kauli za kibabe ,serikali yake inaua upinzani ukilinganisha na serikali ya awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na Rais Kikwete ambapo watu walikuwa huru kutoa maoni Yao kwa huru.

Ibara ya 18(a) ya Katiba ya nchi, inasema ; " Kila mtu anao Uhuru wa Kuwa na maoni na kueleza fikra zake".

Hivyo Kimsingi mtakubaliana na Mimi  Kuwa haki ya watu kutoa maoni ni ya Kikatiba .

Wakosoaji wa serikali ya Magufuli na hata wale wanaoiunga mkono serikali na CCM kadri siku zinavyozidi kwenda Mbele chini kwa chini wamekuwa wakilalamika serikali ya awamu ya tano siyo rafiki kwa watu wanaotoa maoni Kwani baadhi ya watu wanaojaribu kutoa maoni Yao wamekuwa wakikamatwa  na kufikishwa mahakamani na mmoja alifungwa huko Arusha na mmoja alishinda Kesi Na wengine bado Kesi zao hazijamalizika huko mahakamani.

Siyo Siri tena siyo wasomi, watu wenye udhoefu wa mambo mbalimbali, wanasiasa ,wanaharakati na wananchi wa kawaida baadhi yao wameingiwa na woga  ya kutoa maoni Yao hadharani Kuhusu kutoa ushauri unaousu mambo mbalimbali yanayojenga nchi kwa hofu ya Kukamatwa na vyombo Vya dola na kushitakiwa.

Lakini mapema wiki hii Kikao cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma, tumeshuhudia baadhi ya wabunge wa CCM ,Hussein Bashe, Mbunge wa Solwa ,Ahmed Ally Salum ,Mbunge wa Jimbo la Mtera ,Livingstone Lusinde walipongeza jitihada za serikali lakini waliikosoa serikali kwa Nguvu zote kwa uwepo wa uhaba wa mzunguko wa Fedha na mambo mengine mengi.

Wewe Magufuli ndiyo Rais wa nchi ,mwisho wa siku sifa Mbaya  au nzuri hata kama matendo hayo yalisababisha upate sifa nzuri au Mbaya hukuyatenda wewe Moja kwa Moja yametekelezwa na wasaidizi wako basi zitaelekezwa kwako .

Hivyo minashauri kwanza wewe binafsi na vyombo vyako vya ulinzi hasa Jeshi la Polisi katika baadhi ya mambo muwe wavumilivu  na mstahimilivu pale mnapoona  baadhi ya wananchi wenu  wakitoa maoni ya kutofautiana na wewe na serikali unayoiongoza.

 Maoni Yao yapi me kama yanalengo la Kujenga yachukue yafanyiwe kazi kama ni ya kipuuzi achana nayo na siyo kila Mwananchi anayetoa maoni ambayo yanawakera ni lazima mshitaki mahakamani, wengine wapuuzeni serikali iendelee kuchapa Kazi .

Magufuli wakati mwingine Jifunze uvumilivu kutoka Kwa Mtangulizi wako Rais  Mstaafu Kikwete ambaye alibezwa,kudharauliwa na picha za uchi zenye sura uchi aliyengenezewa zinafundikwa Kwenye Mtandao maarufu wa picha chafu wa THE UTAMU ,ambayo ulifutwa na wataalamu .

Rais Kikwete alivumilia yote Akaamua kuchapa Kazi licha ya kuwepo kwa mapungufu lakini Kazi alizozifanya za kimaendeleo wakati akibezwa na kudharauliwa na Watanzania hadi msafara wake kupopolewa kwa mawe Mkoani Mbeya ndiyo Leo hii wewe Magufuli una zindua  na kuendeleza Miradi hiyo iliyoanizishwa serikali ya awamu ya nne ya Rais Kikwete ambapo wewe ulikuwa ni Waziri wa Ujenzi.

Wakati mwingine kukaa kimya ni Jibu la Mjinga.Na ukikaa kimya utayahepuka Mengi.Wale wale waliokuwa walimtukana na kumdhalilisha Kikwete alipokuwa madarakani Leo hii bila aibu wamejitokeza kwenye vyombo vya habari wanasema wa namkumbuka na wanatamani hata sasa hivi Kikwete arudi Kuwa Rais wewe utoke maana serikali yako Ina minya Demokrasia na I wanaletea umaskini.

Na wananchi wale wale Katika kampeni waliokuwa wakikushangilia wewe kadri siku zinavyozidi kwenda wameanza kukuchukia na wengine hawataki hata kukuona na nikiweka Habari zinazokuhusu wewe Kwenye ukurasa wangu wa Facebook ,blog hawataki kuziona wanasema zina wachafu a hata kulike hawataki na nikikaa Katika vijiwe ambavyo  nilikuwa nikienda kukaa Katika Kipindi cha kampeni kwaajili ya kakupigia debe tena baadhi Yao ndiyo hawataki kusikia jina Lako na matusi wana kutukana na Mimi wananitukana na wamekupachika jina unaitwa (KIVURUGE) .

KIVURUGE maana yake wewe uliopo chaguliwa Kuwa Rais ndiyo umekuja kuvuruga kila kitu ( MVURUGAJI) Maisha Yao yamekuwa magumu kwasababu yako,umewabomolea nyumba,safari umefuta ,posho za muda wa nyongeza wa kazi umezifuta .Minachekea sina mbavu naambulia  kuyakoga matusi.


Hadi uimalize Miaka Kumi panapo Uhai serikali yako ikawafungulia Kesi za uchochezi watu wangapi Mahakamani?

 Kwani wakituolea maneno ya shombo/ kukudhihaki  wanakuchubua ngozi au ndiyo wa nafanya nafasi yako ya Rais ikome? Yesu  alidhihakiwa Msalabani na hadi Leo kuna binadamu wanatenda matendo na kutoa maneno ya kumdhihaki Mungu wazi wazi lakini wala Mungu awatoi Uhai,anawavumilia na anawapasha muda wa kutubu dhambi zao mwisho wa siku wanakuja kumrudia Mungu na Hao Hao walikuwa wanamdhihaki Mungu wakageuka Kuwa mashabiki wa kubwa wa Mungu wanakuwa Askari wa Yesu Wanahubiri Injili.


Achana nao waambie Hao Askari wako washughulike na mambo makubwa makubwa licha kwa Yule anatumia lugha za matusi kukosoa achukuliwe Hatua.

Magufuli Kumbuka ni vyombo hivi hivi Vya dola vilimvimbisha kichwa aliyekuwa Rais wa Zanzibar ,Dk.Salimin naye kweli akavimba kichwa Leo hii Dk.Salim yuko peke yake Zanzibar  na Maradhi yake ya macho.Kuwa makini .

Nimefanya mahojiano yangu kwa Siri na madereva BodaBoda Kabla ya kuandika makala hii kila Nilipokuwa nikipanda pikipiki zao makusudi nilikuwa naanza mada za siasa na kuwahoji hii Hali ya kisiasa ikoje na Je Biashara Yao hivi sasa inakwenda vizuri ukilinganisha na Enzi za Kikwete .

Madereva wengine waliniambia kama niachane na hizo story hawataki kunisikia maana eti Magufuli kamwaga Mashushushu ambao madereva Hao wanawaita "Vihelehele" nao wamejigeuza abiria wanawachota akili madereva BodaBoda na wakibai ni madereva Hao wanaisema vibaya serikali wanawakama hivyo wanasema serikali ya Magufuli ya Moto" hawataki kuzungumzia Habari hizo licha Biashara Yao siyo nzuri sana ukilinganisha na Enzi za Kikwete Kwani hivi sasa abiria wao wa zamani wamekuwa hawapandi pikipiki zao kwa Wingi kama zamani wa nawaeleza Kuwa   Fedha " Magufuli kabana".


Hivyo baadhi nilizungumza hata wananchi wa kawaida wanasema wameamua kukaa kimya waone  mwisho wake utakuwa je.Na wengine wana mawazo mazuri tu ila wana hofu na serikali ya awamu ya Tano itawakamata .

Kwa mtazamo wangu Katika Kipindi hiki cha Mwaka mmoja, nimeona Rais Magufuli amekuwa akipenda kuzungumza kupita kiasi / kuwatolea lugha za ukali  Hadharani baadhi ya watendaji wake wa chini kabisa  mambo ambayo kama rais wa nchi kiuungwana na kidiplomasia hapaswi yamtoke kinywani Mwake Mbele ya hadhara .

Mifano ni mingi ila nitaiweka michache hapa, mfano Oktoba 17 mwaka huu, alipokuwa akiongoza Mamia ya wananchi kutoa heshima za mwisho wa mwili wa marehemu aliyekuwa Meya wa Jiji  la Dar Es Salaam, Dk.Didas  Massaburi, Msemaji wa familia ya marehemu Katika risala yake pamoja na mambo mengine alisema marehemu aliacha Mke mmoja .

Lakini Rais Magufuli alipopata fursa ya kuzungumza kweli alitoa maneno ya busara kwa watoto wa marehemu nay akubali lakini Rais Magufuli akatofautiana na msemaji wa familia Kuwa marehemu aliacha Mke mmoja akasema yeye anafahamu Kuwa marehemu Dk.Masaburi ameacha zaidi ya wake wanne  na watoto zaidi ya 20.

Sawa inawezekana ulipata taarifa za Siri Kuwa kuna mchezo mchafu wa baadhi ya wake ,watoto wa marehemu kutaka kudhulumiwa au kutotambuliwa lakini kweli Rais wa nchi unasimama Mbele ya umati wa watu  kuzungumzia mambo binafsi ya marehemu Dk.Masaburi? 

Kauli yako hiyo inaweza kusaidia wake na watoto marehemu Masaburi wasigombanie mgawanyo wa mali lakini pia inaweza isisaidie pia kwani Tayari hapo kuna mchanganyiko wa mama tofauti na Damu tofauti na kila mmoja Ana hira zake na roho yake hivyo anaweza Kuzuka mtoto au Mke akazusha zogo la Kugombea mgawanyo wa Mali za marehemu na Mifano Hipo mingi Kwani hata baadhi ya watoto wa marehemu Mzee Mfaume Kawawa bila haya baba Yao alipofariki walimuanzishia vurugu Mke wa marehemu Kawawa na vyombo Vya Habari tuli ripoti tukio Hilo .Sitaki Hilo litokee Kwa familia ya mtani wangu Marehemu Dk.Masaburi.

Kweli Rais mzima wa Tanzania Mbele ya umati wa watu vyombo Vya Habari Vya Kimataifa vipo Unazungumzia   mambo binafsi ya marehemu Masaburi hata kama Angekuwa ni rafiki yako vipi kiasi gani?


Siyo kwa kiasi hicho.Kama ulitaka ujumbe wako ufike ungempa basi hata Mwenyekiti wa CCM Mkoa alisemehe Hilo  basi hata Ungetuma wasaidizi wako waende kwenye familia ya marehemu wakufikishie nasahaa zako .Badilika .

Mfano mwingine hivi karibuni Rais Magufuli ulitembelea Bandari ukiwa umevalia suruali,Kofia,shati jeusi na ulipofika Katika kitengo Kimoja, ukawa unamtaka kiongozi wa kitengo kile apige picha mizigo iliyokuwa nje halafu kompyuta za kitengo kile halafu hapo hapo uzione zile picha palepale.

Yule kiongozi wa kile kitengo cha Bandari kila alivyokuwa akijitahidi kukuelekeza kwamba ile Idara yake haiwezi kupiga picha ya mizigo iliyopo nje Moja kwa Moja kwasababu Idara yake inapokea picha za aina hiyo kutoka Katika Idara nyingine inayojitegemea ambayo ina kiongozi wake ambayo imeishapiga picha za mizigo inazituma picha hizo katika Idara yake lakini bado Rais Magufuli ulionyesha mashaka waziwazi na kutoridhika na maelezo Yale kwasababu ulionekana ukisema hivi' kama kompyuta hizi ni mbovu semeni, nataka mnionyeshe picha za mizigo iliyopo pale nje Mara Moja ....' Baada ya Yule Mkuu wa kitengo Kusimamia taaluma yake wewe Rais Magufuli Ukaondoka Katika kitengo hicho kwa haraka '.

Mimi sikupenda kile kitendo ulichokifanya Kwani licha ya Yule Mkuu wa kitengo bandarini kutumia lugha ya Upole kukupa maelekezo wewe ulikuwa ukionekana kuongea kwa Ukali ,na Kuonyesha kama vile ulitilia Mashaka maelezo ya Yule Mkuu wa kitengo na ukasema hata wewe hiyo Kazi ya mizani unaifahamu fika.

Rais Magufuli Kumbuka Hao watumishi wa umma nao wanastahili utu, heshima na wenyewe pia ni wanaume na wanawake zao majumbani,watoto na wakwe wanaheshimika hivyo sivyema ukafika Katika maeneo Yao ya Kazi na kuanza kuwahoji baadhi Yao kwa kutumia lugha za Ukali ambazo zina wafanya baadhi ya watumishi ukiwa unawahoji kuingiwa na uwoga ,kudhalilika Mbele ya Jamii kupitia Televisheni .

Ibara ya 12(2) Katiba ya nchi inasema ; " Kila mtu anastahili heshima ya kutambua uwa na kuthaminiwa utu wake".

Kitendo kile uchokifanya hakioendezi kwa jamii ya waungwana Kwani pia kitasababisha watu kupunguza molari ya kufanyakazi kwasababu ya kisasi cha kutolewa maneno ya makali na Mkuu wa nchi,Kumbuka nao ni binadamu hawajataliwa nyongo.

Katika Hilo la bandarini la Huyo Mkuu wa kitengo uliyokuwa unamshinikiza akuonyeshe picha za mizigo iliyopo bandarini.Minakushauri ingekuwa busara na bado Hujachelewa unaweza kumuita Mkurugenzi wa Bandarini na wale wakuu wa vitengo vile ulivyotembelea Ikulu uwaeleze wewe unataka hivyo vitengo vifanye Kazi kwa mtindo ambao unaoutaka wewe ambao labda Mataifa mengine wanafanya hivyo Kisha wape muda waseme hadi lini watakuwa wametekeleza Kisha wakuletee ripoti ya utekelezaji.

Ulipotembelea bandarini ulisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea Bandarini hapo akaamuru baadhi ya mashine zinunuli we lakini hadi wewe umeenda bandarini bado hazijanunuliwa na ukasema Fedha zipo.

Labda nikuulize Rais Magufuli hivi unafahamu kuwa Sheria ya Manununuzi ya Umma ipo na inafanyakazi na usipoifuata unashitakiwa na ukipatikana na hatia unafungwa? 


 Mali za serikali lazima zinunuliwe kwa kufuata tarabu za Sheria ya Manunuzi ya Umma, Leo hii Mkurugenzi wa Bandari hawezi kukurupuka kununua hivyo vifaa walivyotakiwa wanunue na Waziri Mkuu, wewe Rais Magufuli bila kufuata Taratibu za Sheria ya Manunuzi ya Umma. 

Akikiuka Taratibu za Manunuzi ya Mali ya umma kwa Kigezo eti Waziri Mkuu,Rais Magufuli alisema hadharani basi  ajiandae kufikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ama Mahakama zingine kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kusababishia serikali Hasara kwasababu Mlikiuka matakwa ya Sheria ya Manunuzi na Jela mtakwenda peke yenu Hao wanasiasa waliyokuwa wakiwapa maelekezo hamtokuwa nao watakuwa majumbani mwao wamelala na wake zao,nawafahamu vizuri sana wanasiasa akili zao.

Akili kumkichwa nunue Mali za serikali kwa kufuata Taratibu za kisheria Puuzeni mashinikizo ya ununuzi kutoka kwa mabosi wenu ambayo hayapo Katika mfumo wa maandishi.

Na Mifano ipo Si ya Kutafuta waliokuwa vigogo wa SUMA JKT ,aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ndege David Mattaka, Aliyekuwa Mkurugenzi wa TBS , Charles Ekelege ambaye huyu hata gerezani alifungwa na Kesi zao nimeziripoti vizuri sana  pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam.

Mfano Mwingine Rais Magufuli hivi karibuni ulipoenda  kutembelea Shirika la Ndege ATCL na ukawahutubia pamoja na mambo mengi ulivyozungumza nayo ambayo ya aonyesha umedhamiria kuliongezea Nguvu Shirika Hilo uliongea maneno ambayo kama Rais hakupaswa kuyasema .

Rais Magufuli ulisema kuna wake wa mawaziri bila kuwataja majina yao wanafanyakazi hapa ATCL na ATCL inafanya vibaya wao bado wanang'ang'ania tu.  

Mimi sikufurahishwa na Kauli hii Kwani Kauli hiyo inaweza kutafsiri wa Kuwa wake Hao mawaziri ndiyo wa nasababisha ATCL isifanye vizuri .

Lakini baada ya muda Kauli hiyo ili zusha mijadala Katika Jamii na baadhi ya vyombo Vya Habari vikaamua kwenda kufanya uchunguzi ndani ya ATCL kubaini Hao wake wa mawaziri ni nani lakini walibaini Mke wa waziri ni mmoja tu ambaye ni Mke wa Waziri wa Ardhi ,William Lukuvi ambaye ni  Germina  Lukuvi ambaye aliajiwa hapo Mwaka 1987 Kabla hajaona   na Lukuvi.

Mama Lukuvi alihojiwa na baadhi ya vyombo Vya Habari akaeleza jinsi alivyojiunga na ATCL hadi hivi sasa alipo. Lakini siku Chache baadaye Mama Huyo aliamua kuandika barua ya kuacha Kazi kwa Hiari yake.

Simfahamu huyu mama ila nafikaga katika Moja ya Duka linaloelezwa Kuwa ni lakwake katika Jengo la Benjamin Mkapa kununua vipodozi Vyangu .

Kwanza Nampongeza sana kwa uamuzi wake wa kuachakazi hiyo namedhihirisha ni mwanamke makini sana, anajua kusoma alama za Nyakati na anaamini Kuwa anaweza  vile vile kupata riziki na kuendesha Maisha hata kama Hana  ajira ya serikali.

Hivi Katika akili ya kawaida Rais wa nchi alienda  ATCL kazungumza maneno kama hayo licha anakutaja jina ,hivi mamlaka nyingine za juu zinaongoza ATCL zingekuwa zinamchukuliaje huyu Mke wa waziri Angeendelea kufanyakazi Katika Shirika Hilo?

Maana watu wengine ni kama machizi hapa nchini Rais akiongea jambo hawana muda wa kulitafari ndiyo wanalichukulia ni Sheria, Kigezo cha kusurubu wengine Kumbe wakati mwingine Rais anaweza kukosea maana na yeye ni binadamu.

Kwahiyo hapo Tunajifunza pia Rais anaweza akapewa taarifa za uongo ambazo bila kujua akazitumia kutolea maamuzi ambayo yataumiza baadhi ya watu na baadaye Rais anakuja  kubaini taarifa zile alizopewa awali  akazitumia kutolea maamuzi Fulani zilikuwa za uongo na wakati huo uamuzi wa Rais uliotokana na taarifa za uongo umeishaaribia watu Maisha Yao na Kuwaumiza na kuwachafua Katika Jamii.

Masononeko ya Mama Lukuvi Mbele za Mungu hay atakwenda bure ipo siku Mungu atamlipia.

Mfano mwingine wa Rais Magufuli Kuonyesha Anaongea sana na kuamini sana baadhi ya taarifa za kupelekewa Vyanzo vyake kana kwamba hizo taarifa alizichunguza alizutafuta yeye binafsi  wakati akitakiwa Kumbe taarifa hizo anapewa na vyombo vyake ni  siku ile Magufuli alipitembelea  Benki Kuu ,pamoja na mambo mengine alisema ndani ya BOT kuna wafanyakazi hewa Kauli iliyoshtua Wengi na baadhi ya watu kuanza kuitazama  tofauti BOT.

Lakini siku Chache baadaye Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alihojiwa na Gazeti la Mtanzania ,Kuwa ni je ni kweli BOT kuna wafanyakazi hewa .

Gavana Ndulu ambaye ni Mchumi   mbobezi alimtaka Huyo Mwandishi aliyemuuliza Swali Hilo kwanza   aende akamhoji Huyo aliyemweleza Kuwa ndani ya  BOT kuna wafanyakazi hewa. 

Na taarifa toka ndani ya BOT zinaeleza ndani ya BOT Hakunaga wafanyakazi hewa ndiyo maana hadi Leo hatujasikia Zoezi la kusaka Wafanyakazi hewa limebaini ndani ya BOT kuna wafanyakazi hewa.

Mfano mwingine wa Rais Magufuli Anaongea sana ni hivi karibuni alivyofaya  ziara yake Zanzibar na kuwahutubia  wananchi wa Zanzibar .  mambo mengi ya kujenga na kusisitiza upendo ,mshikamano Umoja  lakini Rais alishindwa kujizuia hisia zake na kujidhiirisha yeye ni mtu wa kulipa  kisasi jambo ambalo Mungu halipendi Kwani jukumu la kulipa kisasi ni la   Mungu.

Rais Magufuli alisema hivi atoe mkono wake halafu mtu aukatae Kisha mtu Huyo aliyoikataa kuupokea mkono wake aje kutaka mkono wake umsainie Nyaraka zake  yeye hatoweza kusaini Nyaraka za mtu Huyo kwasababu eti alikataa kupokea mkono wake wakati alipo msalimia.

Itakumbukwa Kuwa Katika msiba wa marehemu Aboud Jumbe Mwaka huu huko Zanzibar ,Rais wa Zanzibar Dr.Ally Mohammed Shein walikutana ana kwa ana mpinzani wake Maalim Seif Sharif Hamad na Dk.Shein alikuwa akimsalimu Seif kwa njia ya kumshika mkono lakini inaelezwa Kuwa Seif alikataa kupokea mkono wa Dk.Shein kwasababu anazozijua yeye.

Vyovyote Iwavyo, mtu yoyote aliyeshiba Mafundisho ya dini, muungwana na Rais wa nchi hakupaswa kutoa Kauli kama hiyo hadharani ambayo ni wazi inaonyesha ni mtu asiye na desturi ya kusamehe,uvumilivu na mtu mwenye kinyongo kwa mtu anayefikiri amekosea wakati Mungu Mwenyewe ni mvumilivu,anasamehe na Mungu anatukaza kulipa visasi kwanini jukumu la kulipa visasi kwa watesi wetu ni lake.

Ni hatari Kuwa na Rais wa nchi anayetoa Kauli kama hii hadharani zinazoonyesha ni mtu mwenye kinyongo na mlipa visasi   kwa mtu atakayebaini atakwenda kinyume na matakwa yake.  

Maalim Seif ni Makamu wa Pili  Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ana Stahili zake anatakiwa kuzipata kwa mujibu wa Sheria sasa mtu anayefikiri Sawasawa hawezi Kutamka hadharani Kuwa kwakuwa amekataa kupokea mkono wake basi siku Seif akitaka kutibiwa nje ya nchi hatoidhinisha Maombi yake .

Kukataa Kupokea salamu ya mtu siyo kosa kisheria linaloweze sababisha mtu ashitakiwe au Rais amnyime mtu Stahili zake anazostahili kwa mujibu wa Sheria kisa amekataa kupokea mkono wake.

Rais Magufuli alipokuwa akihutubia wananchi wa Kaliua Katika mikutano yake  ya kampeni za urais CCM Mwaka 2015  alinukuliwa akifanikiwa akisema akifanikiwa Kuwa  Rais wa Tanzania ataakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanapata mikopo kwa wakati na kwamba hatokubali kuona wanafunzi wamefika tayari vyuoni na bado hawajapatiwa mikopo ,waliowacheleweshea wanafunzi hao mikopo atawashughulikia.

Lakini tumeshuhudia Katikati ya Oktoba Mwaka huu, kulizuka mvutano wa ,Wanafunzi  wa baadhi wa Vyuo Vikuu  wakilalamikia utaratibu mbovu wa mikopo kwa Mwaka huu Tayari walikua wameishafika vyuoni .

Haki iliyosababisha Rais Magufuli wakati akiweka jiwe la Msingi Katika Ujenzi wa Mradi wa mabweni wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam,    Oktoba   Mwaka huu, alikiri  kutokea kwa dosari za kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo na kuitaka Bodi ya Mikopo kajipange sawa sawa iondoe hizo dosari  na hadi sasa hajamchukulia Hatua mtu yoyote aliyesababisha dosari hizo.

Lakini ushahidi wa Video unaonyesha ni Magufuli huyu huyu Kwenye kampeni zake za CCM Mwaka 2015 alisema akiwa Rais ole wake anatakaye mcheleweshea mwanafunzi wa Chuo Kikuu mikopo atamshughulikia na video ipo inayomuonyesha akisema hayo wakati wa kampeni za kusaka urais.

Ila kwakuwa amekiri dosari ni vyema, ila hii inatufundisha binadamu hasa wanasiasa tuwe na tabia ya kuweka Akiba ya maneno.

Tusipende kuzungumzia mambo ambayo hatutayafikia kuyapata au kuyatenda  Kuwa nikipata kitu Fulani nitafanya hivi Mara vile tena Mbele za watu mwisho wa siku ukipata hayo madaraka unashindwa kutekeleza kwa vitendo Yale uliyoyasema Kabla hujapata madaraka hayo.Ni Mbaya sana Kwani wakati mwingine ni Kigezo Kimoja wapo kinachokuondolea sifa ya kuaminiwa Taratibu.


Mapema kabisa wakati umeshika madaraka ya urais ulitamka hadharani Kuwa  utahakikisha unawabana wale waliokuwa wanaishi Maisha kama wapo pepo ili waanze kuishi kama mashetani.

Hii Kauli ni Mbaya sana  Kwani  Mungu Mwenyewe anasamehe Saba Mara sabini na hat hivyo   Mtoa riziki ni Mungu .Vidole vyenyewe Vya mikono havilingani kuna virefu na vifupi hivyo kuna matajiri na masikini.

Hivyo mtu Kuwa Tajiri siyo dhambi na Kuwa masikini siyo dhambi yote ni mipango ya Mungu. Unaweza usiwe Tajiri lakini ukawa Kinara wa Kutenda dhambi na kuvunja Sheria.

Hadi  sasa Hakuna Mahakama yoyote nchini hadi sasa haijamkuta  na hatia mshitakiwa  yoyote  wa Kesi za wizi,uhujumu uchumi au matumizi Mabaya ya madaraka walioshitakiwa katika utawala wako Kwani kwa mujibu wa Ibara ya 107A ( 1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 , inasema ; " Mamlaka yenye Kauli ya mwisho ya Utoaji Haki Katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama'.  

Na Mungu hapendi watu wake aliyowaumba waishi kama mashetani sasa wewe  Rais wetu huu uhalali wakutaka watu walioumbwa na Mungu waishi kama mashetani umepata wapi?Ni Mungu gani huyo Kakupa madaraka hayo ya kuwafanya watu aliyowaumba waishi kama mashetani?

Hagai 1:7-8 Katika Biblia Mungu anasema  ; " Nami nitatikisa Mataifa yote ,na vitu vinavyotamaniwa na Mataifa yote vitakuja ,nami nitaijaza nyumba hii utukufu ,asema Bwana wa Majeshi . Fedha ni Mali yangu na dhahabu na dhahabu ni Mali yangu ,asema Bwana wa Majeshi".

Hivyo kwa mujibu wa nukuu hiyo ya Kitabu cha Hagai 1:7-8  ,Mungu anatumbia Kuwa Fedha Mali na dhahabu ni Mali yake siyo Mali ya binadamu. Ndiyo maana kuna Msemo maarufu usema binadamu Hana mamlaka ya Kuzuia riziki za watu ila anachelewesha tu.

Licha hii aimaanishi watu wanahusika na vitendo Vya kuhujumu uchumi wa nchi wakichukuliwe Hatua ,Nasema wachukuliwe Hatua kwa Taratibu za Sheria za nchi.

Jambo jingine ni ule uamuzi wako wa Kuzuia wakuu wa Mikoa, Wilaya wasiende kushiriki sherehe za kilele za Kuzima Mwenge Mkoani Simiwi dakika za mwisho wakati taasisi ulifahamu kuwepo kwa sherehe hizo 
Posho Simiwi , kuwafanyia viongozi wako  wameadhirika,waathirika kisaikolojia .na Hao


MAPENDEKEZO

Ili Rais wetu Magufuli ondokana  na tabia ya kuongea mambo ambayo hayafai  kutamkwa kwa umma na mtu mwenye hadhi ya Rais wa nchi. 

Ni vyema sasa Wasaidizi wa Rais wajenge utaratibu wa kumbana Rais awapo Kwenye baadhi ya shughuli mbalimbali za kiserikali awe anazungumza kupitia hotuba zilizoandaliwa na wasaidizi wake Kwani kama Hilo halitofanyika ipo siku tusije kushangaa Rais akatoa maneno ambao yataleta Shida. 

Maana Kauli za Rais ni nzito jamani na wakati mwingine zinaweza kutumika kuanzisha mchako wa kutunga Sheria mbalimbali .

Pendekezo la pili, Nashauri kama Rais Magufuli kama alishawahi kuhudhuria kozi ya Diplomasia ,sawa na kama hadi sasa bado haja pelekwa kuudhurulia kozi ya Diplomasia basi hajachelewa .

Uandaliwe  utaratibu wa kumtafutia walimu wa Mafunzo hayo   ili wamfundishe zaidi mambo ya kidiplomasia ambayo pia yatamsaidia Kuwa na subira ,uvumilivu Katika Utendaji Kazi wake ikiwemo wakati akitoa matamshi yake Mbele ya umma na jinsi ya Kutenda Kazi za watumishi wake wa umma bila kutolea watu Kauli za Ukali ambazo baadhi ya watu wanasema Kauli za aina hiyo zinatolewa na ' WAKUDA' ,hazipaswi kutolewa na mtu mwenye hadhi ya Rais wa nchi.

Katika Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Mwaka huu Dodoma, muda mchache baada ya kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa CCM na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu ,Rais Mstaafu Dk.Jakaya Kikwete  Katika hotuba yako uliongea mambo mengi na mipango mingi unayopanga kuifanya ndani ya CCM na Moja ya Kauli yako ulisema unawaomba wananchi wakuombee uwe na moyo wa uvumilivu kwasababu moyo wa uvumilivu kama aliyokuwa nayo Rais Kikwete wa kuvumilia watu unaona wanakwenda nje ya mstari kama wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mwaka Jana Katika mkutano wa kumchagua mgombea mmoja wa CCM ili awe mgombea urais wa CCM .

Ambapo  baadhi ya wajumbe Katika mkutano ule wakati Mwenyekiti wa CCM Enzi hizo Rais Kikwete alipokuwa akiingia ukumbini baada ya Jina la aliyekuwa Kuwa Kada wa CCM ambaye alikuwa na wafuasi waliokuwa wakimuunga mkono kukatwa jina lake waliamua kuimba ' Tunaimani na Lowassa oya oya oya...badala ya kuimba Tunaimani na Kikwete ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa mkutano' .

Magufuli alitamka wazi wazi Kuwa yeye ndiyo angelikuwa ni Mwenyekiti wa CCM halafu wajumbe wa mkutano wanamfanyia vile as ingeweza kuwavumilia angewashughulikia kikamilifu. Kwa Kauli hiyo ni uthibitisho Kuwa Rais Magufuli Hana moyo wa uvumilivu kwa wale wanaotenda mambo ambayo hayapendi.

Hata hivyo ni hatari pia kwa Rais wa nchi kutamka hadharani Kuwa Huna moyo wa kuvumilia watu unaowaona wanakwenda kinyume na wewe au Sheria za nchi Kwani Kumbuka Shetani naye yupo Kazini hajalala ,unapoanika Udhahifu wako huo kwa umma na wewe ni kiongozi wa nchi tambua Kuwa kuna watu ambao wanauwezo wa kukufikia wewe na unawaamini sana Kumbe wengine wana roho za kishetani,wachonganishi,watu wanaotaka kulipiza visasi dhidi ya watu ambao hawawezi kukufikia wewe wakaja kwako wakakujaza maneno ya umbea ,fitna dhidi ya ha watu na kwakuwa wewe Tayari umeishaanika Udhahifu wako hadharani Kuwa Huna roho ya uvumilivu utawaamini unakurupuka utaamuru washughulikiwe au wewe wewe Mwenyewe utoe uamuzi wa Kuwafukuza Kazi au utengue Teuzi zao. 

Na hili linawezekana sana maana hii nchi kuna watu shetani amewabariki Kauli ,kila wanapokwenda kupeleka uzushi,uzandiki dhidi ya wenzao wanasikilizwa na kuaminiwa sana baadaye na baadhi ya watu wale Wahanga wa uzushi wameishaumia na kuharibiwa Maisha Yao ndiyo ukweli unakuja kujulikana Kuwa walisingiziwa .

Wewe Magufuli ni shahidi Katika hili ,na Mimi pia ni shahidi Katika hili na mfano  mzuri ni wa jinsi Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Ricky Mahalu ,mashetani wachache ndani ya serikali ya awamu ya nne walivyomharibia Maisha yake na kumfanya Aisha Maisha mateso ,Fedhea kwa uzushi tu na Kesi ya uhujumu uchumi wakambakia pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  siku chache tatu tangu Rais Kikwete alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza.

Llakini kwakuwa Balozi Mahalu ana rekodi ya uadilifu ndani na nje ya serikali na ni shabiki namba Moja wa Mungu tatizo Hilo akimkabidhi Mungu na ndani ya serikali ile ile ya Kikwete kwa Siri kuna maofisa wa serikali walijitokeza kumpiga nia kwa Nguvu zote hadi akashinda Kesi hiyo ambayo iliandika historia hapa nchi ambapo mmoja wa shahidi wa Mahalu alikuwa ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye alifika mahakamani kutoa ushahidi wa kumtetea Mahalu na alishinda serikali ikaumbuka .

Binafsi Nilipokuwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania nilipata fursa ya kuripoti Kesi hii mwanzo hadi mwisho Katika ngazi ya Mahakama Kuu pia hata DPP alipokata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam pia niliiripoti Kesi hadi siku DPP wa enzi hizo alikuwa Dk.Eliezer Feleshi ambaye kwasasa ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alipoamua kuifuta rufaa hiyo kwasababu alikuwa Hana Haja ya kuendelea kumpatia rufaa Balozi Mahalu na Grace Martin.

Hivyo nakushauri sana kila siku omba Mungu akupe moyo wa subira, uvumilivu ,Hekima kikweli kweli Mungu atakupatia kwani ukisoma Kitabu cha 1 Wafalme  3 :5-14 katika Biblia ,utaona Mfalme Selemani aliomba Mungu ampe hekima na alimpa.Binafsi ,Kiongozi wa Kanisa ninalosali la Elshadai Temple lililopo Boko Basiaya Dar Es Salaam, linaloongozwa na Nabii ,Kanali Mstaafu, Bruno Kinunda na waumini wote Kabla ya kuanza ibada ya Jumapili tu nakuombea Ulinzi,Hekima ,busara na uvumilivu Katika kuongoza taifa hili na Mimi ndiyo niliyoenda Kwa Siri kumweleza Nabii Kinunda aongezee maneno ya Busara,Hekima na uvumilivu wakati tukikuombea Kwani hapo awali alikuwa akituongoza kukuombea kwa kukuomba Mungu akupe Ulinzi ,Afya njema .

Hekima ,uvumilivu ,busara  vitakusaidia sana kuondokana na Hali kuongea sana hadharani mambo ambayo kama Rais Hupaswi kuyatoa kinywani mwako.

Wapuuzi wachache wanaweza Kusema makala hii ina Lengo la kukudhihaki, Si kweli Kwani hata Mimi kwa asilimia Fulani nilikuwa na tabia kama yako ya kutaka jambo Fulani lifanyike kwa wakati huo huo haraka tena nilikuwa Mkali sana na watu waliniogopa sana na hiyo Hali ilisababisha nikose vitu vingi Vya maana .

Kwa Kuwa nia yangu ilikuwa ni njema ya kutaka wahujumu wa nchi hii na wavunja Sheria wachukuliwe Hatua kupitia makala mbalimbali nilizokuwa  naziandika, Na wakati huo nilikuwa sijitambui Kuwa hiyo Hali niliyonayo ya Pupa,jazba ya kutaka vitu vifanyike haraka bila kuvuta subira nilikuwa nakosea sana na kugeuka Kituko Mbele ya wasomi wa Sheria .

Ndipo mtu mmoja ambaye alikuwa Ni Mkurugenzi wa Mashitaka ( DPP), Dk.Eliezer Feleshi ambaye alipokuwa DPP nilifanya kazi sana na Ofisi yake kwa kuripoti Kesi zao bila kuchoka, ndiyo alikuwa mtu wa kwanza kulibaini Hilo tatizo langu la Kuwa na pupa ,kutokuwa na uvumilivu pindi ninapokuwa nimekerwa na wavunja Sheria ,ha kujificha alinieleza Hilo tatizo langu na akaniambia kama nipo Tayari kuondokana nalo kwanza nikiri Mimi binafsi kwa Mungu silitaki tatizo Hilo liendelee kuwepo Ndani ya mwili wangu na akaniambia nijiendeleze kielimu na ya kuchoka Mara kwa Mara kunifundisha mbinu ya kuondokana na tatizo Hilo kwa zaidi ya Miaka Saba yote a lilipokuwa DPP .

Haikuwa Kazi rahisi kwakwe kunio ndoa Katika hicho kilema cha kukosa uvumilivu,Kuwa na Pupa lakini alifanikiwa kwa asilimia 90  na asilimia 10 zilizobakia zilikwenda kuondolewa na Mzee wangu ambaye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo( UB) ambaye ni Boss wangu ,Profesa Costa Ricky Mahalu Kwanini Mimi ni Ofisa  Habari wa Chuo hicho,ambaye muda wote Mahalu amekuwa akiniambia Mimi na wasomi wenzake Happiness Katabazi ana akili sana ila hakuwa amepata mwongozo wa kupata elimu tangu alipokuwa Mdogo na kwamba ataakikisha ananisaidia ananisaidia nijiendeleze kielimu na niachane na tabia ya pupa Katika kuchukua maamuzi,niwe mfumo livu,subira na kumtegemea Mungu kwasababu siyo Siri sisi waandishi wa Habari Wengi ni wachangamfu kupita kiasi na ni waongeaji kupita kiasi na bila Kuwa na tabia hizo huwezi Kujenga marafiki/ Vyanzo Vingi Vya Habari na hutopata taarifa nyingi .

Balozi Mahalu ni Mwanasheria ambaye amebobea Katika Sheria za Kimataifa na ni Mwanadiplomasia vile vile , University of Bagamoyo walitaka niache Kazi Gazeti la Tanzania Daima ili niende University of Bagamoyo kama Ofisa Habari wa Kwanza wa hicho hadi sasa ni Ofisa Habari wa hicho chuo ,Balozi Mahalu siyo mwongeaji sana Kumbe alinibaini ni tatizo la kukosa uvumilivu,kushindwa kuvumilia ninapokasirishwa na sijui mambo ya Diplomasia hata chembe.

Nakumbuka Boss wangu Mahalu alimuita Naibu Makamu Mkuu wa chuo anayeshughulikia Taaluma, Dk.William Kudoja na Aliyekuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Fedha na Utawala, Dk.Elifuraha Mtaro akawaambia Happiness ni binti mwenye akili na uwelewa mpana wa mambo hivyo hili mwisho wa siku asije kukitia aibu chuo kwa kukukosa uvumilivu kuropoka inabidi atafutwe mwalimu anayefundisha kozi ya Protocol and Etiquette amfunishe kozi hiyo peke yake hapa chuoni ili aondokane na tabia za ajabu ajabu.

Kweli alitafutwa Mwanadiploma Mkongwe Mstaafu ambaye aliwahi kufayakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na ambaye amewahi kuwa Mhadhiri wa kozi ya Diplomasia Katika Chuo cha Diplomasia ,Mr.Edward Kadiri aliletwa chuoni hapo na kunifundisha kozi hiyo ya muda mfupi Mimi peke yangu Katika maeneo yafuatayo ;

1. Diplomatic and Consular Relations and Practices,
2.Diplomatic ,Official and Social Protocol.
3.Diplomatic,Official and Social Etiquette


Kadri  siku alivyokuwa alinifundisha mhadhiri huyo Mr.Edward Kadiri nilifikiri a zile tabia za kishenzi kishenzi za kuropoka,kukosa uvumilivu ninapokerwa nilizokuwa nikizifanya  Kabla Jaji Feleshi  kunikosoa , Mr.Kadiri ajaanza kunifunda  na nikajiona nilikuwa ni mpumbavu  wa Hali ya juu na nikakubali kuzidi kujishusha kwako pindi wanaponirekebisha pindi ni endapo ofisini kwako,kwa njia ya simu  na kubadilika na nilipomaliza kozi hiyo nilienda kuwashukuru  kwa maboss wangu Kuwa kozi ile imenisaidia sana kuniondolea kilema cha kukosa uvumilivu ,kuropokaropoka walicheke sana na wa kafurahi lakini Leo maboss wangu wanajivunia Kuwa Fedha waliyonilipia ya kujisomesha kozi hiyo Fupi ya Diplomasia imesaidia kumjengea uwezo Ofisa Habari wao ambaye ni Mimi na wamekiri imenibadilisha tabia yangu.

Aidha Jaji Dk.Feleshi ambaye ni miongoni wa wanasheria wachache wabobezi katika Sheria ya Sayansi ya Jinai na,Balozi Mahalu ambao ni Wanasheria kitaaluma  waliniakikishia wataendelea kunishape niondokane na ule ulemavu wa kupayuka payuka,kukosa uvumilivu na Kuwa na papara wa kaniambia kwakuwa nilikuwa Mwanafunzi wa Shahada ya Sheria ninakutana na Alternative Dispute Resolution (ADR ) na kwamba somo Hilo pia litachangia kuniondolea hicho kilema cha kuropoka,kukosa uvumilivu na kukataa kusikiliza wenzangu wanasema nini pindi ninapopandwa na jazba.

Hakika Nilipokuwa mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu 2016 , Somo la ADR Nilifundishwa na Mwanasheria Aghatha Lend .

Ndani ya kozi  Hiyo kuna Topiki Moja ya kutatua Migogoro nje ya Mahakama na Hatua zake .

Kwakweli nililifuatulia kwa makini kozi  hiyo na nikajifunza Kuwa msuluhisi/Mtoa Haki yoyote Yule   anatakiwa kwanza asiwe na upande,awe anajua kutunza Siri,awe mvumilivu,afuate Taratibu Katika kuendesha mambo ya kisuluhishi kwakweli hapa napo palinisaidia sana kunitibu tatizo langu.


Lakini  wakati nikipitia Hatua zote hizo la kutibu tatizo langu Hilo Kila ninapoenda  Kanisani kusali na n ikamkabidhi Nabii jina langu nanikaorodhesha Shida zangu kwa maandishi Kuwa anapokuwa anaomba kwa muda wake namimi ninapokuwa naomba nyumbani na kanisani naomba Mungu aniondolee tatizo la kuropoka,anipe uvumilivu,subira na kweli namshukuru Mungu hivi sasa nimebadilika hata mtu akinitukana Leo hii naweza kuvumilia nisimjibu au naweza Kumjibu sentensi Fupi ambayo itafamnya ajione yeye ni shetani  Hana akili na mwishowe atataka kuanzisha vurugu na Mimi nitamkwepa.

Nimelazimika kuanika Hatua hizo nilizo pita kumaliza tatizo langu Hilo la kukosa uvumilivu kwa watu wanaokukosoa au wanaovunja Sheria ,papara,kuropoka ili liwe Funzo kwako Rais Magufuli ambaye Mara Kadhaa kwa kinywa Chako umesema Huna moyo wa uvumilivu kwa wanaokosea,na pia wengine wasiyokuwa na moyo wa uvumilivu,Hekima ambao wanataka wabadilike wajifunze kupitia Mimi maana tatizo Hilo lilinisababishia ni kukosa mambo mengi mazuri nanilikuwa sitambui kama nakosea nilikuwa najiona Mimi ndiyo Mwamba napatia Kumbe nakosea Kwani unaweza kumrekebisha mtu unayefikiri anakosea kwa sauti ya Upole tu na akalelewe vizuri kuliko kumkaripia na kumuonyesha ubabe.


Hata hivyo dada yangu wa Hiari ambaye ni mkwe wa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini India, Warda Divaz pia nimiongoni mwa watu ambao waame saidia sana kuniondolea tatizo la kuropoka na pupa ,Nawashukuru sana sina chakuwalipa ila Mungu ndiyo anatawalipa


Tatu, Rais Magufuli ameishagundulika Kuwa nia yake ni njema ya kutaka kuiletea  taifa hili maendeleo na Mimi binafsi sitaacha Kumuunga mkono kwa harakaharaka .

Ila  Nashauri Rais kuanzia hivi sasa apunguze au aache kutoa Kauli mara kwa mara hadharani za Kulalamika Kuwa nchi unayoiongoza  ndiyo imekithiri kwa ufisadi na kwamba kila eneo linanuka ufisadi.

Hakuna ubishi kuna baadhi ya Sekta zilikuwa zikiandamwa na tuhuma chafu licha siyo zote na siyo wafanyakazi wote wa umma ni wachafu ,wapo wasafi na waadilifu kwa Taifa Lao na ndiyo maana muda wote wamefanya kazi serikali kupitia taaluma zao na uadilifu wao hadi wewe ukawa Rais wa nchi na Leo unatimiza Mwaka mmoja.

Siyo sifa kwa kiongozi wa nchi kusimama majukwaani iwe Kwenye shughuli za Kitaifa,nyuma za ibada  Kulalamika Kuwa nchi hii imekithiti kwa ufisadi.Kwani wewe ndiyo baba mwenye nyumba unavyosimama nje ya nyumba Yako/ majukwaani unalalama Kuwa watoto wangu ni Malaya sana ,unategemea hata kama kuna mwanaume jirani alikuwa anataka kuwachumbia Hao watoto wako Atakuja kweli kuchumbia watoto wako?

Kwanini hao watoto wako usiwaite ndani ukawakanya kama mzazi kwa lugha za stahaa watakuelewa.

Hawezi kwasababu Tayari baba mwenye nyumba umeishatamka mtaani Kuwa watoto wako ni Malaya sana.

Hivyo basi hata kwa wewe Rais ambaye Leo unatimiza Mwaka mmoja tangu uwe Rais ,achana na Kasumba ya kurudiarudia tena Hilo neno la kwamba Tanzania ufisadi ulikithiri,Mara Watanzania ni Wapiga Dili Kwani ukumbuke Mataifa mengine yapo macho yanafuatilia kila unachokozungumza wanakipa na kukiranyiakazi na mwisho wa siku Watanzania Mbele ya sura ya Dunia tutakuwa hatuaminiki tena kwasababu ya Kauli zako unazozitoa Mara kwa Mara wakati wanaotenda mambo hayo machafu ni wachache siyo Wengi .

Usije ukashangaa hata baadhi ya wawekezaji wengine wanaogopa Kuja kuwekeza hapa nchini kwasababu ya Kauli zako za kila Mara Kuwa kila sehemu Katika nchi kuna Wapiga Dili.Na Wapiga Dili kila nchi wapo umewakuta utawaacha .


Sasa hivi hao ' wazee wa mishemishe 'nikama wanausoma mchezo unaocheza ,wa nakuvutia kasi tu na hivi bado una safari ndefu Katika Kipindi Chako cha urais lazima  ' watakufurahisha' .

Kuna watu hapa duniani wao Maisha Yao yote ni kupiga Dili tangu vijana, wa nazeeka ndiyo shughuli zao hizo utawawezea wapi?Utawabana wachache kwa muda Fulani wengine hutafanikiwa kuwabadili tabia Kwani hizo tabia za kufanya Mishemishe,kupiga Dili zipo Kwenye Damu Yao.

Nne, Acha kuzungumza hadharani Kuwa wanaolalamika  Maisha magumu hivi sasa walikuwa ni 'Wapiga Dili' Utawala uliopita. Siyo kweli Kuwa wote wanaolalamika Maisha ni magumu Katika Utawala wako eti wote ni Wapiga Dili siyo kweli ni uongo wa wazi Kwani siyo Siri tena kila pembe hivi sasa watu wanalalamika Maisha yamekuwa magumu Kwani upatikanaji wa Fedha mitaani umekuwa ni mgumu kwasababu mbalimbali .

Kweli miongoni mwa Wanaolalamika walikuwa ni 'Wapiga Dili',lakini kuna hata wafanyabiashara halali tunawajua, wafanyakazi wa Sekta za umma na binafsi wanapata kipato halali na uadilifu wao hautiliwi shaka wanalalamika pia na huo ndiyo ukweli Kuwa upatikanaji wa Fedha umekuwa mgumu hivi sasa kwasababu wewe Rais Magufuli ulitangaza serikali yako imeanza kwa kubana matumizi kwakufuata posho, safari.

Watumishi wa umma pamoja na kulipwa mishahara pia posho za vikao, safari ndiyo zilikuwa zina wasaidia kuwapunguzia makali ya Maisha ambayo wanayaona hivi sasa.

Hivyo Huyo aliyekwambia utamke siku ya sherehe za kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kuwa wanaolalamika Mara kwa Mara  ugumu wa upatikanaji wa Fedha ni wachache ndiyo hao wachache walizoea vya dezo.

Ukweli ni kwamba kadri siku zinavyozidi kusonga Mbele wanaolalamika wanazidi kuongezeka hivyo siyo wachache na kwamba ni Wapiga Dili peke yake ,hivyo waliyokupa taarifa Kuwa wanaolalamika ni wachache amekudanganya sana.


Serikali ndiyo yenye hela Ikiziminya Fedha zake na isipofanya manunuzi kwa wingi,ikafuta safari,posho kwa watumishi wake  ni wazi watu wanaotegemea kufanyabiashara na serikali watateteleka na wengine wanasema wameishateteleka  kiuchumi na huo ndiyo ukweli Leo hii baadhi ya mahoteli yanakosa wateja Wengi kama zamani,zinashindwa kujiendesha kwasababu serikali haipeleki tena mikutano yake Katika baadhi ya Hoteli za watu binafsi kama zamani.

Kuna hata watumishi wa umma wengine ni wateule wako,viongozi wa dini ,watu wazima na heshima zao ambao uadilifu wao hautiliwi Mashaka nao pia wanalalamika Kuwa mzunguko wa Fedha tangu Rais Magufuli ulipoingia madarakani hadi sasa umekuwa mgumu mno na Mimi binafsi naungana nao Kuwa ni kweli Hali ya upatikanaji wa Fedha umekuwa mgumu sana kwasababu wewe Mwenyewe Rais Magufuli umenukuliwa serikali yako inabana matumizi na umesema utaendelea kubana matumizi .

Na kama Mnasema ni Wapiga Dili/ mafisadi ndiyo wanalalamika Hali ya Maisha na upatikanaji wa Fedha umekuwa mgumu Mbona hivyo vyombo vyako Vya Ulinzi Usalama haviwakamati basi Hao Wapiga Dili/ wahalifu?

 Tano, Katika fikra zako kuanzia sasa acha kutoa Kauli zinaonyesha wazi Kuwa upo kwaajili ya kuwasaidia na kuwatetea sana watu masikini .Hii Kauli umekuwa ikiirudia Mara kwa Mara .

Nakukumbusha wewe ni Rais wa Watanzania wote Maskini,matajiri na watu wenye kipato cha Kati.Hata matajiri pamoja na utajiri wao nao wanashida zao tena ukute Shida zao ni kubwa kuliko masikini.

Ibara 13(4) ya Katiba ya nchi inasema ; " Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya Sheria yoyote au Katika utekelezaji wa Kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi".


Napendekeza kaa na vyombo vyako mtijitafakari kwanza ni kwanini hivi sasa baadhi ya wananchi wamekuwa na woga wa kujitokeza adharani kutoa maoni Yao kuhusu serikali yako kwa Madai Kuwa serikali hii haitaki  kukosolewa na ukiikosoa unashitakiwa?

Mkishabaini fanyeni mbinu ya kuondoa hiyo Hali kwa wananchi wenu maana hivi sasa hata wasomi pia wanafahamu mambo mengi mazuri ambayo wakiyatoa adharani yataisidia kuleta maendeleo Katika taifa letu Lakini wanaogopa kuyatoa adharani kwa Kigezo cha kuanza kufatiliwa na serikali ya Magufuli.

Binafsi naona  kuna Chanzo kikichosababisha baadhi ya wananchi Hao kukutwa na Hali hiyo na Kuishia kunung'unika chinichini, kwa kuandika maoni Yao kwa njia ya mafumbo,wengine kukaa na madukuduku Yao kifuani  wa kuogopa kutoa madukuduku /maoni Yao hadharani kwa Sababu eti watakamatwa na wengine wa nadiriki Kuita ni ya kidikteta.

Kwani Rais Magufuli utambue jambo Moja binadamu yoyote huwezi kumzuia asifanye jambo analolitaka kujifanya ana uwezo wa kutumia njia yoyote ile kufikisha ujumbe kama ni wabunge wa CCM, watumishi wa umma ambao wanaogopa hawaridhiki na mambo yanavyoendeshwa na serikali wanaweza kuwapatia taarifa viongozi wa vyama Vya upinzani au watu wenye sauti Katika Jamii wa siyoogopa wakapaza sauti kwaniaba Yao bila wewe Kufahamu na ujumbe ukafika kwa Jamii vizuri tu na Dalili hizo nimeanza kuziona .

Pendekezo jingine, naomba serikali ya awamu ya tano uwezekano wa kuibadilisha hii sera ya Utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwasababu hayo Masharti yaliyomo Katika hiyo sera ni ya Kibaguzi na yenye Lengo la kutaka kundi Fulani la vijana wa nchi hii wasipate elimu ya juu kwa Kigezo eti walivyokuwa wakisoma shule za Sekondari rekodi zao zinaonyesha walikuwa wakisoma Sekondari za kulipigia kwa gharama kubwa hivyo wazazi wao wanauwezo wa kifedha wa kuwalipia elimu ya Chuo Kikuu na hivyo hawastahili kupewa mkopo.Huu ni ushenzi wa Hali ya juu na au vumiliki.

Kwasababu mambo uenda ya kubadilika Leo Mzazi /Miezi/mfadhili wa mtoto anaweza Kuwa na kipato cha uhakika kama mshahara ,Biashara ,au Mali zisiozamishika ambazo ndiyo zikawa ni Chanzo Chake cha kipato kwa wakati huo kilichomuwezesha kwa wakati huo kumsomesha mtoto shule za Msingi, Sekondari za kulipia .

Lakini Ilipofika wakati mtoto Huyo amefanikiwa kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu hivyo Vyanzo Vya Mapato Vya Huyo Mzazi,Mlezi, mfadhili vimekufa kwasababu mbalimbali ikiwemo kufilisiwa, nyumba kubomolewa na serikali ,kufukuzwa Kazi au kustaafu hivyo anajikuta anashindwa kumlipia Ada ya Chuo Kikuu mtoto Huyo wakati huo sera ya Bodi ya Mikopo nayo inasema haiwezi kumpatia mkopo kwasababu rekodi zinaonyesha eti wazazi wake ni vigogo wanauwezo wa kumlipia Ada na sababu nyingine kuwa hawasomi kozi zenye kipaumbele chakupewa mkopo.Hatari sana.

Hivi mtu anataka mkopo akope kwanini serikali inashindwa kuweka utaratibu wa kuwawekea dhamana wanafunzi Katika mabenki ili mabenki Iweze kuwapa mikopo wanafunzi Hao waweze kusoma Kisha wakarejesha mikopo hiyo?

Tunajitapa kila kukicha Tunataka taifa hili liwe la wasomi wakati sera ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ni ya Kibaguzi? 

Kwa hiyo mtoto akose Haki yake ya Kikatiba ya kunufaika na Rasilimali za taifa hili kwa Kigezo eti Mzazi wake anauwezo wa kumsomesha mara eti kozi aliyoichagua siyo miongoni mwa kozi zenye vipaumbele .  Wazimu wa aina yake ndiyo huu.

Enzi taifa hili halina Fedha wala Miradi mingi ya maendeleo ,serikali ilikuwa ikiwa peleka wanafunzi kusoma vyuo vikuu Leo hii taifa hili limepiga Hatua za kimaendeleo Tunaambiwa makusanyo ya kodi yameongezeka yanaibuka Masharti kibao Kandamizi ya kunyima wanafunzi mikopo .


Pendekezo jingine ,naomba utambue kwamba kila jambo /uamuzi unaofanya kwa maslahi ya taifa hili kama unavyoeleza fahamu fika lina faida na Hasara zake. Uamuzi wa Kufuta safari za nje ,posho za vikao na posho muda wa ziada wakazi una faida na Hasara pia Hilo ulijue.

Katika mazungumzo yangu ya baadhi ya watumishi wa umma Wengi tu toka Ofisa mbalimbali wanasema uamuzi wako wa Kufuta posho ya muda wa ziada wa Kazi umewaondolea molari ya kufanya Kazi kabisa na tangu ulipotangaza Kufuta hizo posho za Muda wa ziada wa Kazi ,Wawapo Kazini akili zao na Nguvu nyingi wanazielekeza Katika shughuli zao Binafasi za kuwaingizia kipato kwasababu kwanza mshahara wa watumishi wa umma ni Mdogo na tangu uwe Rais wa nchini, hujawaongezea mshahara unategemea wao wanaishi vipi ?

Nani kweli nimekuwa nikifika Katika Ofisi za umma mbalimbali hivi sasa ikifika saa 9:30 Alasiri kila mfanyakazi anafunga virago vyake anaondoka hata kama Kazi alipopewa na boss wake Hajazimaliza ,wanaziacha kiporo na wengine wa nadiriki Kusema kwa Kauli hizi za vitisho zinazotolewa na baadhi ya watawala Kuwa asiyetaka Kazi na aache pia zimewafanya baadhi ya watumishi Kuwa na hofu ya kufukuzwa Kazi jambo ambalo siyoni kama lina Tina kwa taifa kwasababu Kimsingi tukubaliane Utendaji wa Kazi n wa kushirikiana .


Ni kweli una nia ya kutaka kuleta maendeleo Katika taifa hili ni vizuri ila naona kama speed yako ni Kali sana hivyo nilikuwa nakushauri ukumbuke ule Msemo usemao 'kawia ufike' , nenda Taratibu na Timu yako Katika baadhi ya maamuzi  Utendaji tutafika salama Kwani harakahara haina baraka.Tanzania haiwezi Kuwa kama Japan Leo hii.

Kwani ukumbuke hata Rais Kikwete alikiri hadharani Kuwa amestaafu urais ameweza Kutenda mambo ya kimaendeleo kwa kadri ya uwezo yake na yale ambayo alishindwa kutekeleza anatuachia mrithi wake ayatekeleze

Pendekezo jingine nakushauri Tazama upya uamuzi wako wa kuondoa Fedha Katika mabenki ya Kibiashara na Kisha Fedha hizo ukaamuru ziamishiwe Benki Kuu .

Misiyo mchumi ila nimeshuhudia baadhi ya watu wakikosoa uamuzi wako huo kwa Madai Kuwa unaathiri uchumi kwasababu Benki Kuu haifanyi Biashara.

Lazima ulipata  ushauri huo na wachumi lakini wachumi nao ni binadamu wanaweza kukosea hivyo Huna budi tena kukaa na wachumi wengine  idi mradi ujiridhishe wachumi Hao ni wazalendo kweli ,pia kaa na wakuu wa mabenki ambayo yalikuwa yakikaa na hizo Fedha ukaziamishia Benki Kuu wakupe maoni Yao kwamba Je tangu hilo agizo Lako litekelezwe Benki hizo na wananchi wamenufaika vipi na wameadhirika kwa kiasi gani?Je ushauri wao ni upi kwako Je agizo Lako Hilo liendelee Kubaki  kama lilivyo au ul itengue?

Na kama fikra zako zilikutuma Kuwa kuamisha Fedha toka Kwenye mabenki ya kawaida ukaziamishia Fedha hizo Benki Kuu  kwa Kigezo Kuwa Fedha za umma zikikaa Benki Kuu zitakuwa salama zaidi, kwa asilimia Fulani  utakuwa unakosea sana kwasababu hata Fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA)  zilikuwa zikitunzwa kwa muda mrefu Katika Benki ya Taifa ya Baishara ( NBC) lakini baadaye serikali ya Rais Benjamin Mkapa iliamuru Akaunti hiyo uamishiwe Benki Kuu na Fedha hizo zitunzwe ili mwisho wa siku wanaodai Fedha hizo wakija kuzidai serikali iwalipe.

Mwisho wa siku watu wenye akili zao ' wasiyotaka  Ujinga', waliingia ndani ya Benki Kuu wanashirikiana na Baadhi ya maofisa wa Benki Kuu wakazichota kwa nafasi mabilioni ya shillingi ya Fedha za EPA tena wengine walitumia Nyaraka Fedha na walinufaika nazo vizuri sana mwisho wa siku baadhi Yao walishitakiwa Katika Mahakama ya Kisutu akiwemo Kada wa CCM, Rajabu Maranda ambaye alishitakiwa kwa jumla ya kesi tano za wizi wa fedha za EPA alifungwa Katika baadhi ya Kesi Akakaa gerezani kwa muda mfupi ,Rais Kikwete alimpatia msamaha  Katika baadhi ya Kesi hivi ,Kesi nyingine alishinda hivi sasa yupo uraiani anaendelea na Maisha .

Sasa kama Kigezo Chako cha kuamisha Fedha Katika mabenki yetu ukaziamishia Benki Kuu kwaajili ya eti Benki Kuu kuna Ulinzi zaidi nau kukwepa liba kubwa katika hayo mabeni ya kati kwa asilimia Kadhaa unajipotosha Kwani nchi hii kuna watu washenzi sana na hawawezekani na hutakaa uwaweze maana walishashindikanaga muda mrefu kwa wazazi wao ,Jela hawaliogopi,Polisi ndiyo nyumbani Kwao na wala hawana hofu na Mungu. 


Aidha nakushauri Kuwa makini sana na baadhi ya watu wanaokusifu hadharani kwa kila jambo unalotenda baadhi Yao ni wanafki tena wazandiki wakubwa maana baadhi Yao wana kusifia hadharani wakikaa na sisi pembeni wanakukandia hatari.

Nakushauri usiwachukie wala kuwawekea visasi wale wote wanaokosoa baadhi ya matamshi na matendo yako kwa nia ya Kujenga .Tazama vigezo walivyotumia kukukosoa ,mapendekezo Yao kama yanalengo ya Kujenga yachukue yafanyie Kazi Kwani tukubaliane Kimsingi wewe ni Rais wa nchi ni binadamu kama sisi ,kuna wakati unakosea ,unafanya vizuri lazima wananchi wako tukueleze na uwe Tayari kujifunza,kubadilika.

Kuanzia sasa nakushauri uache kuendelea kutamka hadharani Kuwa 'utaunda Mahakama ya Mafisadi' licha nafahamu Mahakama hiyo ambayo wewe ndiyo umepachika  jina Hilo kwasababu kitendo cha Kuita majukwaani  Mahakama hiyo ya  mafisadi ni Tayari kwamba wale washitakiwa wote watakao Kuwa wanaoshitakiwa Katika Mahakama hiyo Tayari watakuwa wameishahukumiwa Katika macho ya Jamii Kuwa ni Mafisadi Kabla ya Mahakama hiyo haijatoa hukumu yake  .

Ikumbukwe kuwa  Ibara ya 107A (I) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, inasema hivi " Mamlaka yenye Kauli ya mwisho ya Utoaji Haki Katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama'.

Leo hii kupitia Kauli zako mbalimbali Katika kampeni za kuomba uchaguzi we Kuwa Rais ,na ulivyokuwa Rais umetaka Mahakama hiyo ianzishwe na kweli imeanzishwa  mwisho Mahakama hiyo sasa watu tunaofikiri Sawa sawa tunajiuliza Rais wa nchi Magufuli na baadhi ya watu Mahakama hiyo wamejipachika  jina Hilo huku mitaani,majukwaani Kuwa Mahakama hiyo ni Mahakama ya mafisadi lakini Je ikija kutokea washitakiwa Hao mliokwisha hukumu Kuwa ni mafisadi wakija kushinda Kesi zao Katika Mahakama hizo Je sura Zenu mtaziweka wapi? 

Maana Sheria ni kitu kingine kabisa na porojo za wanasiasa ni  Kitu kingine .S iyo  mwisho wa siku upande wa Jamhuri ushindwe  kupeleka ushahidi thabiti mahakamani kuhusu Kesi hizo zitakazofunguliwa Katika Mahakama hiyo mnayoiita huku mitaani 'Mahakama ya Mafisadi ',washitakiwa wakishinda  hizo Kesi Nyie wanasiasa msije kuanza kupaka matope Mahakama hiyo Kuwa Imepokea Rushwa na inahujumu serikali ya awamu ya tano maana hiyo tabia mnayo sana  wanasiasa wapenda sifa za kijinga.

Pendekezo jingine naomba Timu yako msikilize nakuofanyia Kazi haya Madai ya baadhi ya wananchi ,wabunge na wafanyabiashara kwamba zile kodi za ushuru wa mizigo ni nyingi za viwango vyake ni Vya juu ukilinganisha na viwango Vya kodi Vya Mataifa mengine Hali inayosababisha baadhi ya wafanyabiashara wa Mataifa mengine wasipitishe mizigo Yao Katika Bandari yetu.

Binafsi siyo mtaalamu Katika eneo hili ila napenda kufanya majadiliano na watu wa Kada mbalimbali na kufuatilia mijadala mbalimbali kadri siku zinavyozidi kwenda watu wamekuwa walilalamikia na Kamati Moja ya Bunge ilishatoa mapendekezo yake ziondolewe zitaletea Shida taifa,hivyo Nashauri wataalamu wa eneo hili wafanye utafiti wa kubaini Madai hayo ya wanaolalamika kodi hizo yangu kweli wowote au laa.

Kumekuwa na malalamiko ya mzunguko hafifi wa Fedha ,Nashauri serikali iongeze juhudi za kulipa  Madeni ya ndani ili hela iingie Kwenye mzunguko .

Minakwambia usipo badilika na kuanza Kuwa na moyo wa uvumilivu wa kuvumilia kuona au kusikia yale usiyoyataka kusikia siku ukistaafu akiingia madarakani Rais mwingine na Rais Huyo Akaamua Kuja na Taratibu zake mpya na kuanza Kubomoa Misingi uliyoyaacha unaweza kujikuta unazirai kitandani kwasababu ni lazima utakasirika kupita kiasi Kwani ukitumia Nguvu nyingi kuirekebisha nchi na Utaiweka Kwenye mstari huku ukiamini mrithi wako atakayekuja atayaendelea uliyoyaacha halafu asiyaendeleze . 

Omba Mungu akupe uvumilivu na kunyamaza na ndiyo maana tunaambiwa Mwanaume ameumbewa na Koromeo hili awe kuhifadhi baadhi ya mambo maana nchi hii ni kubwa unaongoza watu wa kila aina wengine ni machizi huwezi kufanikiwa wote waende au waishi unavyotamani wewe waishi .Mimi nakuombea Hilo.

Ukae ukijua huku mitaani pia umepachikwa jina la ' Rais Mlopokaji au Rais Lopolopo' . Yaani manaake hata sisi mashabiki wako hiyo tabia yako ya kuropoka mambo ambayo kistaarabu hayapaswi Kusemwa na mtu kama wewe mwenye hadhi ya urais wa nchi, na inatutukanisha sana,tu najikaza kwamba eti tulimpigia debe Rais ' Mlopokaji' ,Saa Mbovu yaani Kichaa.


Ni Mungu peke yake asiyebadilika  ila binadamu tunajadilika.Rais Magufuli badilika  la Katika baadhi ya madhaifu niliyoyainisha hapo juu yanayokuhusu wewe binafsi  utafanikiwa zaidi na sitaacha kuinga mkono serikali unayoiongoza inanitokana na CCM  .

Ila sikufichi tabia yako ya kutamka  baadhi ya maneno yasiyopaswa  kuyatamka na mtu  kama wewe mwenye hadhi ya Rais kwa Kigezo Chako kile unachokitumiaga use macho ' eti huo ndiyo ukweli,tuwe wa kweli' siipendi tena siipendi kabisa.

Rais wa nchi ana hadhi yake tena kubwa tu na lazima ajitofautishe na watendaji wake wa chini  na wananchi wengine wakawaida kabisa.

Rais Magufuli Hupaswi kuzungumzia masuala ya vitafunwa Katika sherehe zinazofanyika  Ikulu  kwa Kigezo eti unabana matumizi,watu wale Korosho warudi makwao.Hiyo Idara ya vitafunwa,vinywaji siyo yako inawenyewe wache wenye Idara hiyo waizungumzie.

Leo unatimiza Mwaka mmoja tangu    ulipoapishwa 5/11/2015 Kuwa Rais wa awamu ya tano.

Ninaamini haya madhaifu niliyowataja na mengine ambayo sijayataja Katika makala hii ondokana nayo Kwani Tunaweza Kusema labda ulionyesha Udhahifu huo kwasababu ulikuwa ni mgeni na Ikulu na mgeni wa Cheo cha Urais.Badilika utakuwa bora zaidi Kwani nitafurahi zaidi kama utaandokana hiyo tabia ya kuongea maneno ambayo wewe kama Rais Hupaswi kuyatamka hadharani .

Kwani utambue nchi hii unaongoza watu wasomi wa taaluma tofauti,wenye uzoefu na wajuzi wa mambo mbalimbali kuliko wewe kila unachokifanya au kukiongea hadharani wanakipima na kunijadili Katika maeneo Yao na wengine wamekuwa wakiku sanifu sana wewe hujui .Badilika.

Kuanzia Leo tuna hesabu ule ushamba ,ugeni wa urais, Ikulu umekutoka hivyo umekua sasa hivyo basi baadhi ya mambo achana nayo na ukubali kujishusha ili watu 'wakushape 'uwe Rais bora zaidi Kwani pia huku mtaani jina jingine umepachikwa unaitwa ' ONE MEN SHOW' .

Yaani eti wewe Rais Magufuli ' ONE MEN SHOW ' unajifanya unajua kila kitu  wakati Hakuna binadamu anayefahamu kila kitu.

Misina Hakika na Hilo Kuwa wewe ni ONE MEN SHOW  kwasababu sipo karibu na wewe ila jichunguze kama ni kweli acha hiyo tabia Kwani itakukosesha mengi kutoka kwa watu ambao wanafahamu baadhi ya mambo wanataka wakueleze au kukufundisha ili uwe kuyatumia Katika Utawala wako ufike Mbali  hawataki. Kumbuka bado una safari ndefu .

Mwisho wa siku Ibara ya 37.-(1) ya Katiba ya nchi  inasema hivi ; " Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote".

Hivyo hulazimishwi na Sheria yoyote kufuata ushauri wangu niliyotoa Katika makala hii ila nimeitimiza wajibu wangu kama mwanachi wa nchi wa kutoa maoni yangu kwa mujibu wa Ibara ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977  na pia nimeitimiza wajibu wangu kama Mkristo kama tulivyotakiwa na Mungu Katika  Kitabu cha 
EZEKIELI 3:19 Katika Biblia inasema , " Lakini ukimwonya mtu Mbaya ,wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake Mbaya ,atakufa Katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.

Mungu ibariki Tanzania 

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi

5/11/2016.