PADRI KIMARO ASHINDA RUFAA YAKE



PADRI KIMARO ASHINDA RUFAA YAKE

Na Happiness Katabazi

PADRI Sixtus Kimaro (40), aliyekuwa amefungwa jela miaka 35 mwaka 2005 baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana mwenye umri wa miaka 17, ameachiwa huru jana baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, kutupilia mbali hatia zote mbili na kifungo.

Akitoa uamuzi huo jana Jaji wa Mahakama Kuu, Robert Makaramba alisema amemwachia huru Padri Kimaro kwa kuwa upande wa Mashitaka haukutoa ushahidi wa uhakika kwa mashtaka anayodaiwa kuyatenda kwa kijana aliyekamatwa akiwa naye katika eneo la Changanyikeni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pia Jaji Makaramba alifuta amri ya awali iliyotolewa ya Mahakama iliyomtaka Padri huyo alipe faini ya Sh milioni mbili.

Jaji Makaramba alitupilia mbali hatia aliyokutwa nayo ya ulawiti akisema hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba wawili hao walikuwa wakitenda jambo lililodaiwa kutendeka.

Baada ya kutolewa uamuzi huo Padri Kimaro alinyanyua mikono yake juu na macho ikiwa ni ishara ya kumshukuru mungu kwa hatua iliyofikiwa na mahakama.

Padre Kimaro alionekana kububujikwa machozi wakati Jaji akiwa amefikia katikati kusoma hukumu hali iliyomfanya atumie kitambaa kujifuta.

Awali akiwasilisha ushahidi wa mteja wake, Wakili wa Padri Kimaro alisema upande wa mashitaka ulishindwa kuwasilisha ushahidi wa kuridhisha kumuunganisha na makosa aliyodaiwa kukutwa nayo.

Padri huyo alihukumiwa kifungo hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupatikana na hatia katika mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakimkabili ya kulawiti, shambulio la aibu na kumdhalilisha mvulana huyo.

Alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela katika kosa la kwanza la kulawiti na miaka mitano katika kosa la pili la shambulio la aibu na kumtaka mshitakiwa huyo kumlipa Sh2 milioni mvulana aliyelawitiwa. Adhabu hizo zilikwenda sambamba.

CHANZO: Gazeti La Tanzania Daima.
15/3/2008

NIMEPONA TATIZO LA MACHO BILA KUVAA MIWANI

NIMEPONA TATIZO LA MACHO BILA KUVAA MIWANI

Na Happiness Katabazi

MEI 16 Mwaka 2017  saa tano asubuhi  nilikwenda Katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi ( JWTZ) Lugalo Dar es Salaam   ,kwaajili ya kuonana na Daktari wa macho ili anipatie  matibabu ya macho yangu ambayo yamenisumbua kwa Takribani Miaka  Nane  sasa maana nilishaanza kuona ukipofu unaninyemelea kabisa.

Nilipokelewa vizuri katika Hospitali hiyo na baadhi ya maofisa wa JWTZ ambao ni watumishi wa kikosi hicho cha JWTZ  ambao ni rafiki zangu kisha nikafuata taratibu zote za kumuona daktari na ilipofika saa 8:11 Alasiri  niliingia chumba cha daktari wa macho wa hospitali hiyo  ambayo mimi nilizaliwa   25/12/1979 hapo ambaye anaitwa Dk.Seth Japhet .

Dk.Seth alinipokea vizuri nanilipojitambulisha kwakwe kwa Majina yangu yote mawili ( Happiness Katabazi) alinitazama akaanza kucheka sana akaniuliza wewe ni Yule Mwandishi wa habari Happiness Katabazi usiyemuandika Katika makala Mchungaji Antony Lusekelo Kuwa ulimkuta akiwa amelewa na anafanya Fujo ?Nikavuta pumzi ,Kisha nikamjibu ndiyo Mimi.


Dk.Seth alinitaka nianze kujieleza hayo macho yangu yanatatizo gani hadi nikafika hatua ya kujileta Mwenyewe Hospitali kwaajili ya kupata matibabu.

Huku nikicheka ,nikamweleza Kuwa kwa Miaka Saba sasa Macho yangu yamekuwa yakinisumbua sana wakati ninapokuwa eneo lenye Giza na eneo ambalo halina Mwanga wa kutosha wakati wa usiku ambapo eneo Hilo Hilo lenye Giza watu wengine wanatembea na kuona vizuri ila Kwangu Mimi Inakuwa ni tatizo siyoni vizuri.

Mfano usiku unapoingia eneo ambalo lina Giza au Mwanga hafifu macho yangu hayaoni vizuri na ifikapo usiku njiani kama kuna Giza natembea kwa tabu ,Mara kwa Mara najikwaa,napiga watu vikumbo,natembea kwa kunyatanyata maana Sioni Mbali naona Giza.

Nilimweleza Dk.Seth kutokana na tatizo Hilo nilishakwenda Katika Hospitali zenye vitengo vya  macho Mara mbili   kwa Nyakati tofauti nakufanyiwa vipimo  na madaktari wote wa Wawili wa Hospitali hizo mbili tofauti ambazo (Majina yake nayaifadhi) kati ya Mwaka 2009 na 2014 waliniambia macho yangu ni mabovu sana hivyo wakanitaka ninunue miwani nivae haraka sana .

Dk.Seth akanihoji huku anacheka hiyo miwani iko wapi ?Nilimjibu miwani nilishaitupaga nalalani muda mrefu na nilimweleza kabisa  niliinunua hiyo miwani ile kwa Sh.150,000 Mwaka 2014 lakini roho yangu ilisita na kunikataza nisivae miwani.

Kweli nikaamua kabisa licha macho yalikuwa yakinitesa eneo lenye  Giza na mwanga wa hafifu nilisema kwa jina la Yesu sivai miwani na Mungu anitafutie  njia nyingine ya Kuponya hili tatizo la macho ambalo lilinifikisha Hatua ya kuonekana Mimi ni kichekesho Katika eneo la Giza hata kama ni ndani jinsi ninavyotembea kwa kunyatanyata  na kujiona siku za Kuwa kipofu zimekaribia .

Kweli Mei 16 Mwaka huu, Mungu alisikia  kilio changu na kwa uweza wake nilijikuta naenda   Hospitali ya Jeshi Lugalo na nikakutana na Dk.Seth ambaye kwanza kabisa naomba nimuombe msamaha Dk.Seth kwasababu  wakati akinipima macho alikuwa akinipima Taratibu mno na alichukua zaidi ya saa 1:30 .

Kimoyo moyo   Nikawa namlaumu Dk.Seth Kuwa mkono wake mzito, anafanya Kazi Taratibu Kwani Mimi nilikuwa nataka nikitoka hapo Hospitali niende Kazini kwangu Mikocheni Kisha jioni niende zangu GYM  nikafanye  mazoezi ya viungo kama kawaida yangu.


Baada ya kumaliza kumpatia historia ya tatizo langu la macho, alianza kunipima macho yangu Taratibu bila haraka kwakuniweka vifaa Kwenye macho huku akivibadilisha na akawa ananitaka  nisome maandishi yaliyokuwa yametundikwa mbele ukutani .Nikafanya hivyo kama alivyonielekeza.

Alipomaliza kunipima hiyo awamu ya kwanza ,Dk.Seth akaingia awamu ya pili ya upimaji wa macho yangu ambapo hiyo awamu ya pili alininyunyizia  dawa ya Matone ndani ya macho yangu na Alipomaliza akanitaka nikaa nje ya chumba anachopimia macho na nifumbe macho yangu nisifumbue hadi dakika 25 zipite ataniita tena Nirudi ndani ya hicho chumba aendelee kunifanyia vipimo Vya macho.Nilitii maelekezo yako.

Kweli Nilifanya hivyo huku nikiwa na baadhi ya Wanajeshi na manesi ambao ni marafiki zangu wakinicheka na kunitania Kuwa ndiyo Tayari nimeishakuwa kipofu. 

Baada ya dakika 25 kumalizika Mwanajeshi mmoja alinishika mkono huku nimefumba macho hadi ndani ya chumba cha Dk.Seth  nikaa Kwenye Kiti , Dk.Seth akanitaka nifumbue macho nikafumbua.

Tukaingia awamu ya Tatu ya matibabu  ambayo Dk.Seth alichukua tena vifaa akaziwekea Kwenye macho yangu na kunitaka nisome maandishi yaliyokuwa yamebandikwa ukutani ni kayasoma vizuri.  


Baada ya dakika 10 kupita Dk.Seth akaniondoa Katika hicho chumba akaniamishia Katika chumba kingine ambacho kilikuwa kimefungwa vifaa Vya kupima wagonjwa wa macho kilikuwa na Giza Kwani alikuwa amezima taa. 

Tukaingia  awamu ya nne ya Upimaji ndani ya chumba hicho ambacho alinivaisha  vifaa Vya kupimia macho Kwenye macho yangu na kusogeza zile mashine za kupimia macho karibu kabisa na macho yangu ambazo zilikuwa Mbele yangu.

Alivyomaliza awamu hiyo ya nne ya matibabu, aliwasha taa ndani ya chumba hicho kukawa na Mwanga akanitaka Nije Kwenye viti vilivyokuwa Kwenye meza ya kuzungumzia mgonjwa na Daktari anieleze alichokibaini Katika macho yangu baada ya kufanya vipimo vyote hivyo.

Dk.Seth ambaye siyo mzungumzaji sana kama Mimi Kwani wakati wote Mimi ndiyo nilikuwa natawala mjadala kwasababu napenda kudadisi vitu hivyo nilikuwa namchimba anieleze mambo mbalimbali yahusianoyo na macho bila kujua.

Nilienda kukaa nae meza Moja Katika hicho chumba ambapo Anaongea kwa Taratibu akasema amebaini macho yangu bado hayajafikia Hatua ya kutakiwa nivae miwani na uchunguzi wake wa kitabibu umebaini tatizo langu la kushindwa kuona vizuri Gizani ,usiku ni kwasababu ninakabiliwa na upungufu mkubwa VITAMIN A mwilini na kwamba upungufu huo ndiyo umenisababishia matatizo hayo.

" Happiness,naheshimu taaluma yangu ya udaktari wa macho na jinai tendea haki kweli kweli.....sitakuandikia uvae miwani kwasababu uchunguzi wa vipimo haujanionyesha Unatakiwa uvae miwani kwasasa  ,wewe una upungufu wa VITAMIN A mwilini hivyo  nakuandikia vidonge vyenye vitamin na Madini mbalimbali ukameze jumla ni vidonge 90 " alisema Dk.Seth.

Dk.Seth ambaye alichukua zaidi ya dakika tano kutafakari kunichagulia vidonge vitakavyonifaa ambayo siyo tu vina ' Vitamin A 'peke yake ,akafungua makabrasha yake akasema ameamua kunichagulia dawa hii ambayo siyo dawa ni virutubisho inaitwa  ONCE A DAY    ( Vitamins and Food Supplements ) akasema Kwenye Bima ya Afya pia ipo .

Katika mazungumzo yetu nilimweleza Mimi uwa Nina desturi ya kumeza ( Food Supplement) yaani virutubisho vyenye baadhi ya vitamin ila hivyo virutubisho havina Vitamin A. 

Akanipongeza Kwa Hilo akaniambia hiyo ya ONCE A DAY ambayo box moja lina jumla ya vidonge 30 aliyoniandikia ina mchanganyiko wa vitamin nyingi na Madini mbalimbali ambayo binadamu anatakiwa awe nayo mwilini na kwamba madini ,vitamini baadhi zikikosekana mwilini binadamu Huyo lazima atapatwa na tatizo la kiafya na ni wachache Wanaofahamu Hilo Kwani Wengi hawafahamu Umuhimu wa Food Supplement and Mineral .

Baada ya Kumaliza kuniandikia  hivyo vidonge ,akaniambia ile dawa ya macho aliyoniwekea Machoni iliyokuwa kwa mtindo wa kimiminika Katika awamu ya pili ya matibabu kwa siku nne kuanzia siku hiyo aliyoniwekea Machoni sitaweza kusoma maandishi madogo Kwenye simu,kompyuta,hata karatasi ila nitaweza kutembea  na kweli Hilo likatokea tangu   Jumanne jioni ya (16/5/2017) nilipomaliza kupata matibabu nikaenda Duka la madawa la Nakiete lililopo Mwenge Dar es Salaam, nakuchukua hizo ONCE A DAY boxi tatu.

Siku ya Ijumaa ya 19/5/2017  macho yangu yakaanza kuona Mbali Na uwezo wa kuona hata Kwenye Mwanga ukaongezeka kupita siku zile ambazo nilikuwa sijapewa Tiba hiyo na Dk.Seth wa Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Kwa kweli nilimshukuru Mungu kwakunikutanisha na Dk. Seth  ambaye yeye alipingana na maamuzi ya madaktari wenzake wa Hospitali zingine ambao wao walivyonipima Miaka ya nyuma kwa tatizo Hilo Hilo la Mimi kushindwa kuona Gizani ambao wao walisema tatizo langu linanitaka nivae miwani uamuzi ambao hata Mimi nilipatwa Mara mbili lakini Dk.Seth akaja na uamuzi wake ambao ulisema macho yangu hayastahili kuvaliwa miwani Kwasabababu tatizo lilokuwa likinisumbua  ni upungufu wa VITAMIN A mwili hivyo akanitaka nikale  vyakula vinaongeza  Vitamin  A kwa Wingi  mwilini ,pia nianze kumeza ONCE A DAY ili nipate Vitamin A  kwa haraka na akanitaka kwa siku Moja nimeze vidonge vitatu yaani asubuhi,mchana na jioni.

Kweli nimemeza vidonge hivyo jumla 90 na tatizo Hilo limekwisha kabisa natembea kwa miguu siku hizi usiku,tena Umbali mrefu bila kupiga watu vikumbo, kuanguka,kujikwaa au kutumbukia Kwenye mashimo maana siyo Siri miguu yangu ina harama nyingi zilizotoka na na kujikwaruza usiku kwasababu ya Macho yangu yalikuwa hayana uwezo wa kuona mbalimbali Nyakati za usiku hasa sehemu yenye Mwanga Hafifu.


Baada ya kupata Tiba hiyo ya kumeza virutubisho hivyo (ONCE A DAY) ambayo imeniponya ,niliwaeleza watu wangu wa karibu Kuwa jamani Nilichojifunza kitu Kimoja Kuwa siyo kila mtu mwenye tatizo la macho anastahili kuandikiwa na Daktari avae miwani, wengine wanaupungufu wa vitamini na Madini mwilini lakini baadhi ya madaktari wasiyo na weledi au tamaa tu ya kutaka kuuza miwani wamekuwa wakiwaandikia wagonjwa wa macho wa kavae miwani wakati hawastahili kuvaa miwani wanau upungufu wa Vitamin A mwilini kama Mimi Happiness Katabazi ambaye madaktari Wawili wa Hospitali mbili tofauti walishawahi kunipima macho tena wala hawa kuchukua muda mrefu kunipima kwa umakini kama alivyonipima Dk.Seth wa Lugalo Hospital ambaye yeye alikataa kunipa miwani akasema sistahili kuvaa miwani bali anastahili kumeza vidonge Vya kuongeza Vitamin A ili viweze kujisaidia macho yangu kuona vizuri.

Mama yangu Mzazi yeye alipimwa akapewa miwani kwasababu hawezi kusoma, kuandika wala kutumia simu bila kuvaa miwani na hata akishavaa miwani ili aanze kutumia simu au kusoma magazeti,Biblia lazima hiyo Biblia ,simu ataisogeza karibu kabisa na Macho huku akiwa amekunja sura ndani ya miwani ndiyo anaweza kusoma.

Mama yangu mzazi ambaye Julai mosi mwaka huu anatimiza umri wa miaka 60 naye ametumia Box mbili za ONCE A DAY hivi sasa ameacha kabisa kuvaa miwani na Kasema havai tena Kwani lishe mbovu zina sababisha baadhi ya watu washindwe kuona halafu madaktari wanawaandikia wavae miwani na Ngozi yake imekaa vizuri tofauti na Kabla hajaanza kutumia ONCE A DAY .

Aidha kuna rafiki yangu ambaye ni Ofisa wa Polisi mstaafu naye alikuwa anavaa miwani Macho yake haya wezi  kuona Mbali licha anavaa miwani nikampa Ushuhuda wangu naye akaenda kununua ONCE A DAY  anameza na Jana usiku  nimewasiliana naye amenieleza   hivi sasa Macho yake yana anga za  sana kupita zamani  na uwezo wa kuona Mbali ,kusoma umeongezeka  ukilinganisha na siku za nyuma Kabla ya kuanza kutumia Once A  Day hadi anajishangaa.

Hadi Jana usiku niliwasiliana naye Ofisa Huyo wa Polisi mstaafu ambaye asema jana ameanza kutumia box la pili la ONCE A DAY amesema hivi sasa yupo Katika  Hatua za mwisho za kuacha kabisa kutumia miwani Kwani macho yake yanaona vizuri hivi sasa kutokana na kumeza vidonge hivyo na kwamba hivi sasa amefikia hatua ya kukaa siku hata tatu bila kuvaa miwani na anaweza kutumia simu ,kusoma maandishi ya mbali na karibu bila Shida yoyote.

Aidha kuna baadhi ya watu ambao nao wana tatizo la macho kama niliyokuwa nayo Mimi nao nimpe washauri licha wanatumia miwani wameze ONCE A DAY Kwani mama yangu Mzazi alikuwa anatumia miwani baada ya kumtaka ameze ONCE A DAY amemeza vidonge 60 ambavyo ni box mbili miwani havai tena na ngozi yake imekaa vizuri tofauti na awali.

Tujiulize ni wangapi kumbe wanatatizo la upungufu wa VItamin A mwilini ambao unasababisha macho yasione vizuri kama mimi ( Happiness) walipimwa na madaktari wakaambiwa wavae miwani wakakubali wanavaa miwani wakati ukweli ni kwamba imekuja kubainika tatizo lao la macho halikustahili kuambiwa wavae miwani?

Hivi daktari unavyompa tiba isiyo sahihi mgonjwa wako ,ufikiri kuwa unamsababishia mathara makubwa huyo mgonjwa wako Mbele ya safari?

Tujiulize mimi ( Happiness ) ningekubaliana na maagizo ya wale madaktari wawili mwaka 2009 na 2014 walionitaka nivae miwani mimi nikagoma leo macho yangu siyangekuwa yameishaaribika bure ? Siyo vizuri baadhi ya madaktari Mnachotufanyia baadhi ya wagonjwa wenu.

Wakati Leo nikitoa Ushuhuda huu kwa umma ,napenda Kusema Kuwa kwanza unapopatwa tatizo mshirikishe Mungu ili akusaidie kutatua tatizo lako kwa kutumia watu waliosahihi hapa duniani kwasababu mimi nilimshirikisha Mungu katika tatizo hilo na kweli akanitafutia mtu "Dk.Seth" akanipa matibabu sahihi ambayo yameniponya.

Aidha  nimejifunza pia ukileta ubishi katika  katika  baadhi ya mambo ,ubishi unalipa / faida  wakati mwingine kwasababu bila ya mimi kukaidi maagizo ya wale madaktari wawili waliyonipa kati ya mwaka 2009/ na 2014 walionipima na kuniambia nastahili kuvaa miwani na nikainunua lakini nikagoma kuivaa .

Je  ningekuwa nimekubalina nao ningeivaa miaka yote hiyo kumbe tatizo langu limekuja kubainika sikustahili kuvaa miwani leo hii macho yangu siyangekuwa yamearibika kabisa? Ubishi wakati mwingine unalipa .

Lakini kingine Nilichojifunza na ninachotaka Kuwaasa wagonjwa, ndugu wa wagonjwa muwapo mahospitalini   waache tabia ya kuwalazimisha madaktari wanachotoka wao na Kuwalazimisha madaktari wawatibie harakaharaka waondoke  ,hii tabia tuache Mara Moja haitasaidii zaidi ya kutuaribia Kwani Daktari naye ni binadamu anaweza akakerwa na hiyo tabia akaamua Kumpa huduma mbovu mgonjwa.

Nakemea tabia hiyo kwasababu hata Mimi siku hiyo hiyo ya 16/5/2017 nilipokuwa nikitibiwa macho hospitalini hapo, kimoyo moyo nilikuwa nakereka na Dk.Seth alivyokuwa ananipima macho Taratibu .

Bahati nzuri sikuropoka nilivumilia Kumbe ndiyo Dk.Seth alikuwa ananiponya kwa kutumia Taaluma yake. 

Hivyo Tujenge tabia ya kuwapa nafasi madaktari pindi wafanyapo Kazi zao ,tuwavumilie tusiwaingilie wala kuwaharakisha wafanyapo Kazi Yao ya kitabibu.

Kingine Nilichojifunza wakati Leo nikitoa Ushuhuda huu ni kwamba Kuwa siyo kila mtu anayesumbuliwa na ugonjwa wa macho anastahili kuandikiwa na Daktari avae miwani .Kwani Maradhi ya macho yanasababishwa na sababu mbalimbali na matibabu ya macho ni tofauti.

Natoa Rai kwa umma Kuwa makala   hii isitafsiliwe Kuwa inaamasisha  wagonjwa wa macho waliopimwa wakabainika wana matatizo ya macho Na wakatakiwa wavae miwani  na wanavaa miwani hadi sasa waache kuvaa kwasababu ya makala hii imetoa Ushuhuda wa jinsi Mimi, mama yangu Mzazi tulivyopimwa Tunaambiwa tuvae miwani Mimi nikakaidi ila mama yangu Mzazi kwa zaidi ya Miaka Kumi Ana anavaa miwani ila baada ya kutumia ONCE A DAY ameamua kuachana na miwani kwasababu anaona vizuri kuliko hata akivaa hiyo miwani .


Shukurani zangu za dhati nazipeleka Kwa Uongozi wa Kikosi cha 521 Hospitali  ya Rufaa ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi ( JWTZ) kinachoongozwa na Brigedia Jenerali Dk.Paul Masawe   ambaye kitaaluma ni daktari wa magonjwa moyo ambaye ni miongoni walioniimiza sana nianze kufanya mazoezi ya kupunguza mwili Mwaka 2011 alipokuwa na Cheo Cha kwasababu aliniona na uzito mkubwa sana ,wafanyakazi wa hospitali hiyo na Dk.Seth na Mwenyezi Mungu. 

Mungu ampe Afya na Maisha Marefu Dk.Seth Japhet wa Hospital ya Rufaa ya Jeshi Lugalo na ninaamini kupitia Mimi utawaponya Wengi zaidi.

 Niitimishe kwa Kusema nilichokigundua Kuwa Kumbe siyo kila mgonjwa anayedai anasumbuliwa na matatizo ya macho basi Daktari anaona Tiba inayomfaa nikimpatia Tiba ya kuvaa miwani tu Kumbe sasa kupitia Ushuhuda wangu huu wa makala hii mtakubaliana na Mimi Kuwa siyo wote wanaovaa miwani ya macho au waliondikiwa wavae miwani ya macho kama Tiba siyo sahihi Kwani wengine hawakustahili kuandikiwa wavae miwani Kwani tatizo Lao la macho ni la kama langu mie ( Happiness) la upungufu mkubwa wa VITAMIN A mwili ambao ulisababisha macho yangu yashindwe kuona sehemu yenye Giza na yenye Mwanga hafifu  hivyo madaktari wale wawili walipaswa wanishauri nikale vyakula vyenye Vitamin A au waniandikie nikanunue vidonge vyenye madini na vitamin nimeze ili niongeze vitamini A mwili na baadhi ya madini. Ndugu zanguni Akili Kumkichwa.

Mwandishi wa Makala hii ni ;

Ofisa Habari wa University Of Bagamoyo (UoB ) na Mwanasheria.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi

21/6/2017






















TANGULIA 'KIFAA' AFANDE MWAUZI




TANGULIA  'KIFAA' AFANDE MWAUZI

Na Happiness Katabazi

JANA mchana maofisa wa tatu wa ngazi ya juu Jeshi la Polisi ambao ni marafiki zangu katika mazungumzo nao ya kawaida tu walinijulisha kuwa wamefiwa na mfanyakazi mwenzao ambaye ni Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Lutenta   Modest Mwauzi  ambaye alifariki Juni 12 Mwaka huu na akazikwa Jana Kijijini Kwao Ibwera,Bukoba Mkoani Kagera. 


Taarifa hizo zilisababisha siku nzima ya Jana nikose na nimwage Machozi kwasababu SACP- Mwauzi licha ni ' Nshomile ' mwenzangu pia aliwahi Kuwa mwalimu wangu wa kozi ya Sheria ngazi ya Cheti.

Kwa Tuliofundishwa na mwalimu wa SACP -Mwauzi ' Kifaa' enzi hizo wakifundisha pamoja na Afande Nasser Mwakambonja ambaye ni ofisi wa Juu wa Jeshi la Polisi na ni Mwanasheria Kitaaluma .

Alishawahi Kuwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria  wa Sheria Jeshi la Polisi, mratibu wa silaha ndogondogo small arms and light weapons , 

Afande Mwakambonja na Afande Nasser Mwakambonja waliopata fursa ya kufundishwa nao somo la Criminal Law na Criminal Procedure walipata fursa Adimu ya kuwafahamu Polisi wanapokuwa wakifanyakazi zao kwasababu masomo hayo mawili Tulifundishwa na maofisa Hao wa Polisi ambazo Sheria hizo ndiyo zinaongoza makosa yote ya jinai ambayo makosa yote ya jinai yanashughulikiwa na Taasisi kama Jeshi la Polisi mfano kukamata,kuhoji na kupeleleza .Kifngu cha 10 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 inatoa jukumu Hilo kwa Ofisa wa Polisi.

SACP- Mwauzi ' Kifaa' ,kifo Chako Mimi binafsi kimeniuzunisha sana tena Kwani Natambua mchango wako Katika elimu ya Sheria ya nchi hii , na mchango wako  Katika taifa hili.

Mwauzi ni Ofisa wa Polisi alikuwa siyo mtu wa kujikweza na hata ungekutana naye mitaani usingefikiri ni Polisi mwenye Cheo cha juu ndani Aidha alipenda utani sana.

Nitaendelea kukumbuka ule usemi wako wako iliyowahi kuniambia hivi ; " Ukiwa mwimbaji Kwaya lazima uje kutabasamu". Kila nikikumbukaga huo Msemo wako nacheka sana.

Nilizoea nikifika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar Es Salaam,Kwenye majukumu yangu pia nilikuwa nikipita Ofisini wake kumsalimia sasa kwakuwa umefariki Duniani ndiyo sitakuona tena.Nimeumia sana.

Aidha SACP-Lutenta Mwauzi Mbaye ni Mwanasheria Kitaaluma  Utakumbukwa sana ' wagonga fegi ' wenzio.

Pole Jeshi la Polisi ,familia, ndugu Jamaa na marafiki kwa kuondokewa na Mpendwa wetu SACP - Mwauzi.

Mungu aiweke roho ya SACP-Mwauzi Mahali panapostahili.

Mwandishi wa Makala hii ni ; 
Ofisa Habari wa University of Bagamoyo(UoB)
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
16/6/2017

MIPANGO YENU YA UDHALIMU DHIDI YANGU NIMEIBAINI



Na Happiness Katabazi

LEO Mchana Mara ya kwanza mtu mwenye namba 0624 317172  alijitambulisha kwa jina la Justine alijitambulisha yeye ni mwanakywa ya wa Kanisa la KKKT Temeke ,wanataka kurekodi video hivyo wamepewa namba yangu ili ni wasaidie kuwaandikia Makala nikamwambia nilishaachaga Kazi Katika magazeti ila msaada nitakao mpa ni kumu unganisha na waandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania ,Happy Mnale akawaandikie hiyo makala Yao.

Nikamtaka anitumie ujumbe mfupi  whatsup ili nione namba yake ili nimrushie namba ya Happy Mnale na kweli Nikafanya hivyo nitamtumia .

Baada ya muda mchache mtu Huyo aliyekuwa akijifanya Mwema sana Kwangu na kunisii sana nionane naye Mimi moyo wangu ukawa inasita ,akanipigia tena simu yangu akisema Tayari wameishaonana na Happy  Mnale na amewapokea vizuri na wameishafanya mahojiano naye ya makala hivyo hiyo makala itachapishwa Katika Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili ya wiki hii na anaishukuru  Sana kwa wema wangu.

Mtu Huyo nikiwa na Askari wa JWTZ ( namuifadhi kwa jina) nikuzungumza naye alipiga tena simu nikakatisha mazungumzo na Askari Huyo wa JWTZ ambaye nilikuwa nazungumza naye nakumpa ushauri wa kitaaluma  nisimamisha mazungumzo naye nikapokea simu ya Huyo mtu aliyedai yeye ni mwimbaji wa kwaya ya KKKT akaniuliza  mchana ule nikipo wapi nikamjibu Si desturi yangu kutaja sehemu nilipo kama msaada nimeishampa.

Saa Tisa nikiwa na mazungumzo na rafiki yangu ambaye ni mtumishi wa umma Kwenye Gari lake mtu Huyo ( Justine) alipiga simu tena Kabla ya kupokea nilimweleza Huyo dada ambaye ni rafiki yangu Kuwa huyu mtu uenda ametumwa kunidhuru na kuniteka Kwanini analazimisha kuonana na Mimi harakahara kawakati Shida yake nimeishatatulia kama makala nimeishamuunganisha na Mwandishi wa Habari Happy Mnale ,Nikajikuta Nasema YESU ni saidia nikapokea simu yake akasema anaomba aonane namimi nikamsisitiza Aiwezekani.

Saa 12 jioni ya leo roho yangu ikanituma nivunje ratiba yangu ya kwenda mazoezi (GYM) nikaenda kukaa sehemu kubadilishana mawazo nawatu namba hiyo ya ( Justine) ikanitumia ujumbe mfupi ukisema NAWEZA KUKUONA? kwakuwa sikuwa nimeikariri namba yake nimamjibu wewe nani? Hakujibu hadi hivi sasa saa nne usiku.

Saa Mbili usiku Leo nikapokea simu kutoka Mama na Mdogo wangu zikinihoji niko wapi natafutwa vibaya sana nikamatwe wamepewa na watu wameambiwa Kuwa Hao watu walienda hadi Ofisi za Tanzania Daima kuniuliza.

Haraka sana akili ikanituma nimpigie simu Mwandishi wa Habari Happy Mnale kumhoji nakumwonya asijaribu kunificha chochote aseme .

Mnale akasema nikweli Yule mtu niliyemwelekeza kwake mchana ambaye alijitambulisha ni muimba kwaya anaitaji kuandikiwa makala alifika ofisini kwake na akatoa nje ya Ofisi yake akampeleka nje ya Ofisi wa kamuuliza maswali Mnale wakishinikiza Mnale a walete ofisini Kwangu Mnale ni kweli hapajui ofisini Na nikweli Mnale hapajui ofisini Kwangu na Mnale Katika mazungumzo yangu naye alinitaadharisha misiseme hayo waliolezwa na Hao watu ambao wakijitambulisha kwakwe kama ni maofisa  wa serikali na vitambulisho wakamuonyesha ila iwe Siri baina ya Mnale na Huyo mtu ambaye kwa mujibu wa Mnale anasema walikuwa ni kundi la watu zaidi ya Watano na wakiwa na mwanamke mmoja.

Mnale najua utachukia kwa kuyaandika yote uliniambia nisiyaandike kuhusu mazungumzo yako na hao watu na mazungumzo yangu mimi na wewe nimelazimika kufanya hii kwasababu ya usalama wangu.

Nimejiuliza kama hao ni maofisa wa serikali  kweli na wananitafuta mimi na simu yangu wanayo kwanini hawajanipigia simu kunitaka niende kituo chochote cha polisi kwa mahojiano na hatua zaidi za kisheria?
 
Kama kweli mtu Huyo mwenye namba hii     0624 317172 ( Justine)        aliyejitambulisha ni mwimbaji kwaya anataka kuandikiwa makala ,kama kweli alikuwa nania njema na Mimi Kwanini aendelee kunisumbua Kwenye simu na kwanini afike Ofisi za Gazeti la Tanzania Daima hayo mahojiano ya Makala ha kuyafanya  Matokeo yake wamweleze  Mnale Kuwa Lengo Lao siyo kuandikiwa makala Lengo ni kumsaka Happiness Katabazi wa mkamate na  Mnale asitoe Siri ?

Mungu yupo na naweza na atanilinda na siku zote ananilinda na ndiyo maana mmepanga mipango yenu michafu kwa siri na dhamira yangu ilikuwa ni njema na msaada mlioutaka nikawasaidia ndiyo maana mipango yenu dharimu mliyoipanga kwa siri Mungu ameianika. 

Na kwa taarifa yenu wewe Justine ambaye namba yako hivi sasa haipatikani na genge lako Nyie siyo kwanza kunipangia mipango ya kidharimu na kunijia na mbinu za kipuuzi kama hizi lakini Mungu aliniokoa.Amini Mungu yupo na at alisambaratisha mipango yenu.

Nasiwaogopi ,Jeuri yangu ni Yesu na Mkae mkijua na Mimi siyo "Mwepesi kihivyooo"  na ndiyo maana majaribo yako yote ya kunishawishi nionane nawewe yameshindikana na ni Mungu wangu aliingilia Kati akasambaratisha mipango yenu.

Nawarahisishia Kazi kama nyie ni wanausalama kweli wa serikali jitajeni Nyie ni wanausalama toka Kituo gani  cha Polisi nitakuja Mwenyewe kuliko njia za kipuuzi mnazotumia za kujifanya Kuwa ni watu wa dini kwakuwa mmesikia Mimi nasali basi mkaamua kuiniingilia Gia hiyo.Poleni sana.

Na Nina Mashaka kama Nyie kweli ni wana Usalama kweli wa serikali ila kwa Mungu hamfichi mnafki itabainika kweli Nyie ni wanausalama toka serikalini kama mlivyomweleza Happy Mnale mkataka asinieleze Kuwa Nyie siyo wanausalama ila kwakuwa Mnale ni rafiki yangu nanimepokea Kazi hawezi nificha chochote maana tunasaidiana naye Katika Shida na raha.Mungu amfichi mnafki atawasukuma Mtaje mnachonitafutia.


Mungu ibariki Tanzania 

Mwandishi wa Makala hii ni ;
Ofisa Habari wa University of Bagamoyo(UoB) na Mwanasheria
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
23/5/2016.

JENERALI MWAMUNYANGE UMEACHA ALAMA JWTZ




Na Happiness Katabazi

FEBRUALI  2 Mwaka 2017, Rais John Magufuli alimteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo Kuwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania .

 Uteuzi huo ni Ishara Kuwa aliyekuwa  Mkuu wa JWTZ   Jenerali Davis Mwamunyange ambaye aliapishwa kushika wadhifa huo Septemba 15 mwaka 2007  ,amestaafu Kazi hiyo kwa mujibu wa Sheria.

Awali ya yote napenda kumpongeza  Mwamunyange kwa kustaafu Kazi ya Jeshi akiwa na wadhifa huo salama na kuliacha  Jeshi likiwa bado lipo imara na mshikamano.

Pia Nampongeza Jenerali Mpya wa JWTZ ,Mabeyo na Mnadhimu Mkuu  wa Jeshi Hilo Luteni Jenerali ,James  Mwakibolwa   Kwa kuteuliwa kushika nyadhifa hizo ambapo Nawaomba mkatende Haki, mzingatie Sheria Katika majukumu yenu  na mazuri yaliyoachwa na Mtangulizi wenu mkayaendeleze na myaenzi ,Yale ambayo hakufanya vizuri mkayaboreshe pia nanyie mkaanzishe mambo ya maendeleo mapya ambayo mnafikiri yatasaidia kulijenga Jeshi letu.

Makala hii ambayo ni mahususi kwaajili ya Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ambao baadhi wa Wanajeshi wao upenda kumuita 'Mwamunyange ni Kipenzi cha Wanajeshi' ambaye wamestaafu kwa mujibu wa Sheria ,itaeleza  mambo Mbalimbali ya kimaendeleo yaliyofanyika ndani ya JWTZ  Enzi za  Mwamunyange akiwa Mkuu wa Jeshi Hilo ambayo mengine hawakuwahi kufanywa chini ya Tawala za watangulizi wake.

 Septemba  15,  2007   saa nne asubuhi na Rais Jakaya Kikwete ( Mstaafu), alimuapisha  Mwamunyange kuwa Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini.

 Sherehe za zilifanyika katika viwanja vya Ikulu na mimi nilipata fursa ya kushiriki sherehe hizo kama Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima ambapo kwasasa siyo Mwandishi  tena wa gazeti hilo hivi sasa mimi ni Ofisa Habari wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo ,Mikocheni , Dar es Salaam na ni Mwanafunzi wa Shahada ya Pili ya Sheria chuoni hapo.

Na baada ya kula kiapo sisi waandishi wa Habari tulifanya mahojiano na Mwamunyange  pamoja na mambo mengine alisema  Katika Utawala wake atahakikisha  anakomesha  tabia chafu ya baadhi ya Askari wa JWTZ kutojichukulia Sheria mkononi kwa kupiga Raia kwakisingio Kuwa  ni Askari na kwamba ataheshimu   Utawala wa Sheria Utawale hadi ndani ya JWTZ. 

Hilo ameweza kulitekeleza kwa kiasi kikubwa kama alivyoaidi  kwa vitendo kwa sababu tumeshuhudia vile vitendo vya kihuni Vya kupiga Raia vilivyokuwa vinafanywa na baadhi ya Askari wa JWTZ wasiyokuwa na Maadili vimepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na Enzi za Tawala zilizomtangulia .

Licha Katika Utawala wa Jenerali Mwamunyange kuna baadhi ya Askari wa JWTZ walituhumiwa kupiga Raia walifikishwa katika mahakama mbalimbali na vituo vya polisi na wengine walishitakiwa .

Tulishuhudia chini Uongozi wa Mwamunyange , waliokuwa vigogo wa SUMA JKT ,Luteni Kanali , Felix Samilani na wenzake wakishitakiwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Enzi hizo Aloyce Katemana, wakishitakiwa kwa makosa ya matumizi Mabaya ya madaraka lakini hata hivyo vigogo hao wa SUMA JKT walishinda Kesi hiyo na Kurejea Kazini na baadhi ya  hivi sasa wamestaafu kwa mujibu wa Sheria.

Hii Kesi tuliyoipachika ' kesi ya Vigogo Suma JKT 'nilipata fursa ya kuiripoti mwanzo hadi mwisho  enzi hizo nikiwa Mwandishi wa habari za mahakamani wa Gazeti la Tanzania Daima.

Kupitia kesi hiyo Nilijifunza jambo Moja kubwa sana Kuwa kweli JWTZ ni Jeshi lenye nidhamu na pia linaheshimu mahakama za kiraia Kwani nakumbuka siku ya kwanza maofisa Hao kufikishwa Mahakamani walikuwa wakilindwa na maofisa wengi wa JWTZ  na wala hawa kufanya Fujo mahakamani hapo.

Nilienda Kuwauliza marafiki zangu Polisi ambao tulikuwa tunashinda nao pale Mahakama ya Kisutu Kuwa ni kwanini siku ya Kesi ya vigogo wa Suma JKT Mbona Sioni Askari Polisi mkienda kuwalinda kama washtakiwa wengine ambao siyo Wanajeshi mnavyowalinda tena kwa virungu ?

 Baadhi ya Polisi walinijibu   huku wanacheka Kuwa  wanajeshi wale walikuwa na wanajeshi waliokuwa wanawalinda kiaina .

 Lakini  hata hivyo Askari wa JWTZ wamefunzwa nidhamu ya Hali ya juu hawawezi Kukimbia na wakaniambia Kuwa wangelikuwa ndiyo Wanajeshi wa majeshi ya nchi za wenzetu ni wazi wangeanzisha machafuko hapo mahakamani .

Tulishuhudia wahitimu wa Mafunzo ya JKT Mwaka 2015 , wakitangaza kutaka kuandamana  kwasababu hawajapewa ajira na JKT  lakini JWTZ / JKT chini ya Mstaafu Huyo  haikutumia nguvu ,vitisho kuwashughulikia,
.

Tulichokishuhudia Utawala wa Sheria uliruhusiwa utawale  ambapo Polisi iliwakamata baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya JKT na Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) , Biswalo Mganga alie afungulia  Kesi ya jinai katika Mahakama ya Kisutu na hadi sasa wazimu uliokuwa ukiwasumbua  wahitimu wale JKT umepona .

Maana naweza kusema uweenda walikuwa wakisumbuliwa na wazimu vichwani  mwao  ndiyo maana Wakataka kuandamana huku wakijua wazi walikuwa hawana mkataba wowote na JKT ya Kuwa siku wakimaliza Mafunzo ya kujitolea ,JKT itakuwa na jukumu la kuwapatia ajira.

Itakumbukwa kwamba Mwaka 2015 , zilizagaa nchini taarifa Kuwa Jenerali Mwamunyange amelishwa sumu hivyo kapelekwa  nje ya nchi kutibiwa na Hali yake ni Mbaya sana .

Taarifa hiyo ilizusha hofu nchini na kufanya ndugu wa Jenerali Mwamunyange waliongozwa na rafiki yangu ambaye aliwahi Kuwa Msemaji wa Jeshi la Polisi, ACP- Aden Mwamunyange kuitisha mkutano na waandishi wa Habari kukanusha taarifa hizo ambapo walisema ndugu Yao ni mzima wa Afya  .

Hata hivyo upande wa Jamhuri ulimfungulia Kesi Mwanafunzi wa  mwaka wa tatu wa  Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI) cha mkoani Arusha, Allan Mbando, ya kusambaza ujumbe huo kwenye Facebook ambao ulikuwa ukimtaka Mwamunyange apindue nchi na Mwaka Jana kijana Huyo alishinda Kesi hiyo.

Jenerali Mwamunyange kama as ingekuwa mtu mwenye hofu ya Mungu,na mwenye kufikiri sawa sawa ,Anayeheshimu utawala wa sheria angeamua kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwatumia Wanajeshi wake   Waende kimya kimya wakamshughulike Allan na Hakuna mtu yoyote asingeweza kumhoji Kwani uwezo wa kufanya ushenzi huo alikuwa nao ila hakuona Haja ya kufanya hivyo.

 Jenerali Mstaafu Mwamunyange akuwa  limbukeni wa madaraka na wala hukuwa CDF mwenye hulka za kujitokeza hadharani na kutoa Kauli za makalipio kwa watu ambao mnadhani wanatishia Usalama wa wanchi Kwani tumeshuhudia baadhi ya Wakuu wa Majeshi ya Nchi za Jirani kama Mkuu wa Majeshi wa nchi ya Jamhuri ya  Kongo na kwingine wakijitokeza hadharani na kutoa Kauli za kufoka na Kuonyesha haziheshimu Utawala wa Sheria hadhara .

Tulimshuhudia aliyekuwa Rais wa Malawi , Jocye Banda Akizusha mgogoro wa Kugombea mipaka ya Ziwa Nyasa baina ya Malawi na Tanzania .

Hatukumsikia wala kumuona Jenerali Mwamunyange kupayuka kwenye vyombo vya habari kuhusu jambo hilo wala akitoa ushauri kwa aliyekuwa Rais wa wakati huo ,Kikwete Tanzania ipeleke  vikosi Vya JWTZ vikapambane na taifa la Malawi  na Moja la jukumu la JWTZ ni kulinda mipaka ya nchi badala yake ilitumika na inaendelea kutumika Diplomasia ya Intelijensia .

Matokeo yake Diplomasia ya Inteligensia ilitawala badala ya matumizi ya Nguvu za kijeshi  ,kauli za kibabe .Likaundwa  jopo la wa wasuluhishi ambalo lina jukumu  la kuzisuluhisha nchi za  Malawi na Tanzania  katika mgogoro huo wa kugombea mpaka wa Ziwa Nyasa Kazi ambayo inaendelea. kisheria tunaita ( Conciliation) .

Tulishuhudia mabomu yaliyolipuka Katika ghala la kuifadhia silaha la JWTZ ,Gongolamboto , kitendo kilicholeta taharuki Katika nchi na kusababisha baadhi ya watu kupoteza Mali zao kuharibika huku vyombo Vya Habari vikishiniliza JWTZ itoe adharani ripoti ya uchunguzi wa Chanzo cha milipuko ile lakini JWTZ iliitisha mkutano na waandishi wa Habari Katika Makao Makuu ya Jeshi Hilo Upanga ,na kuzungumza nao na kutoa fursa kwa waandishi wa Habari waulize maswali lakini mwisho wa siku JWTZ ilisema haiwezi kuanika hadharani ripoti ile ya uchunguzi kwasababu ni ya Siri na hadi Leo waliokuwa wanataka ianikwe ripoti ile bila kufahamu Jeshi Hilo lina mamlaka ya kutangaza kwa umma baadhi ya taarifa zake na taarifa zake zingine hazipaswi kuzitangaza walishasahau .Safi sana JWTZ.

Aidha tulishuhudia vitendo Vya kuhatarisha Usalama wa viongozi wa dini, wageni kule Zanzibar ambao baadhi ya viongozi wa dini, wageni wakiwemo Raia Wawili wa kigeni wakimwagiwa Tindikali .

Pia chini ya Utawala wa Mwamunyange tuliona pia kwa baadhi ya siku za Ijumaa baadhi ya Waislamu ambao walidaiwa ni wafuasi waliokuwa Sheikh Ponda Issa Ponda wakiandamana Katikati ya Mji wa Dar Salaam ,Posta Mpya na Kariakoo Hali iliyosababisha siku za Ijumaa watu kuacha Kwenda Kariakoo kuhofia vurugu  na kuna siku Moja Magari maalum ya JWTZ yaliamua kupita mitaa ya Kariakoo siku ya Ijumaa na Kuzusha taaruki.

Hata hivyo tulishuhudia Mwamunyanye kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hakujitokeza hadharani kutoa Kauli yote bali tuliona mamlaka zingine kama Polisi ,Mahakama zikiwashughulikia wahusika wote kwa mujibu wa Sheria .

Binafsi Maofisa wa JWTZ nayaifadhi Majina yao ulipoteuliwa Kuwa CDF niliwabembeleza sana wanipatie maelezo binafsi  yako yaani CV ,waliniita sehemu ( CHIMBO)   wakanionyesha nikaisoma yote  na CV ya Luteni Jenerali Mstaafu  Shimbo nikabaini jambo Moja ulipata fursa ya kuhudhuria kozi nyingi za Mafunzo ya kozi Kijeshi na kozi za usalama pia na Una rekodi ya Kuwa kiongozi ndani ya JWTZ.

Hata hivyo maofisa Hao wa JWTZ ambao Wengine ni wastaafu niliyokuwa nimekaa nao sehemu waliniambia nimemaliza kusoma CV ya boss wao na hivyo nimepata fursa ya kumfahamu Mwamunyange ni mtu wa aina gani na amepitia ngazi gani hadi Amefika Hatua ya kuwa Jenerali  , nisiende kuuandika hicho nilichokisoma ambacho ni maelezo binafsi ya Jenerali Mwamunyange .

Enzi hizo nilikuwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima, na kweli nilitii maagizo Yao ila nilipata fursa ya kumfahamu maelezo binafsi ya Jenerali Mwamunyange.

Tumeshuhudia Ujenzi wa nyumba nyingi za makazi wa Askari wa JWTZ Katika maeneo  mbalimbali yanayomilikiwa na JWTZ ukiendelea na maeneo mengine umekamilika kwa nyumba mpya za askari ,Askari wakiishi na familia zao.

Licha baadhi ya Askari wa jeshi hilo wamekuwa Wakizilalamikia nyumba mpya ambazo ni maghorofa Kuwa zina nafasi finyu mno na kwamba nyumba hizo Hazina uwezo wa Kubeba familia kubwa na vifaa Vingi Vya ndani hata hivyo wanasema wa nashukuru wa Kujengewa nyumba hizo Kwani zimewasaidia kuishi karibu na Ofisi wanaofanyia Kazi.

Aidha tumeona baadhi ya Hospitali za JWTZ zilitanuliwa na Raia wamekuwa na mwamko wa kwenda kutibiwa Katika Hospitali za JWTZ .

Mfano mmoja wapo ni Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Brigedia Jenerali Dk.Josiah Makele ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria mapema wiki hii na ameagwa jana na wafanyakazi wa Kikosi cha 521 ambapo kwa sasa Kanali Masawe ndiye anakaimu nafasi hiyo ya Mkuu wa Kikosi cha 521 Lugalo Hospitali ,ambayo imepanuliwa na kuboreshwa licha ya bado inakabiliwa na Changamoto  ikiwemo baadhi ya vipimo  kama Kipimo cha kubaini Alegi.

Aidha hivi sasa Ujenzi wa jengo Maalum kwaajili ya kutibia wagonjwa wanasumbuliwa na Maradhi ya Figo ikiwemo usafi shwaji wa Figo unaendelea ndani ya Hospitali Lugalo  ambayo hivi sasa ina hadhi ya Hospitali Rufaa ambayo ilipata hadhi hiyo  muda mchache baada ya kutokea mgomo wa madaktari nchini ambapo Kinara wa mgomo alikuwa ni Dk.Steven  Ulimboka pia hadhi ukipatikana wakati Mwamunyange akiwa Mkuu wa JWTZ.

Chini ya Utawala wa Mstaafu Huyo  tumeshuhudia Jeshi likianzisha Hospitali ya Watoto JWTZ iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Ambapo Hospitali hiyo ya Watoto ya JWTZ ina laza watoto wanaostahili  kulazwa,ina mahabara ,chumba cha upasuaji na Duka la kununulia Madawa limefunguliwa hapo huku wa nawake wajawazito wakiendelea kupata matibabu hapo .

Na taarifa za uhakika toka ndani ya JWTZ nilizonazo ,wodi ya kuzalishia wajawazito iliyokuwa ndani ya Hospitali ya Lugalo itahamishiwa  yalipo majengo ya Hospitali ya Watoto   JWTZ ,Mwenge.


Mbali na Jenerali Huyo Mstaafu  kuheshimu  Utawala wa Sheria Utawale kikwelikweli ndani ya Jeshi alilokuwa akiliongoza  bila kuwakingia Kifua baadhi ya Wanajeshi wake waliokuwa wakituhumiwa na tuhuma mbalimbali huku uraiani ; 

Pia alijitahidi   kuliendesha Jeshi Hilo kisasa ,kisomi ,uwazi na kuakikisha anatengeneza mazingira  Wanajeshi wanakuwa rafiki wa Raia Kwani Raia JWTZ ni Jeshi Lao.

Tumeshuhudia chini ya utawala wa Mwamunyange iliyokuwa Shule ya Tiba ya Kijeshi ( SKT)ambayo ilikuwa ipo chini ya kikosi 521 Lugalo Hospitali  , Ikipanuliwa kwa Kujengwa majengo mapya mengi ambapo Ujenzi wa upanuzi huo Ulianza Mwaka 2013 chini ya ufadhili wa Wajerumani .

Kisha shule hiyo ikapandishwa hadhi na kuanza kutambulika Kuwa ni ,Chuo cha Tiba cha JWTZ ,    kinachoongozwa na Brigedia Jenerali Dk. Robison Mwanjela     kimefunguliwa rasmi 2016 na kinatoa elimu ya Tiba ngazi ya Diploma na kwa mujibu wa taarifa nilizonazo ni kwamba jitihada za makusudi za kufanya chuo hicho siku za usoni kianze kutoa elimu ya Tiba ya Sayansi kwa ngazi ya Shahada zinaendelea .


Mstaafu Huyo  aliruhusu  uwazi kwa kiaisi fulani kwasababu tumeshuhudia kikosi cha Makomandoo kwa  zaidi ya Mara nne kikishiriki  sherehe mbalimbali za Kitaifa Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam na Zanzibar na wakaonyesha baadhi ya mbinu wanazozitumia kukabiliana na adui kitendo ambacho kimendika historia mpya Katika Utawala wake kwasababu  Katika Tawala zilizokuwa zikiongozwa na watangulizi wake hazikuwahi kuruhusu Makomandoo Kuonyesha maonyesho Yao hadharani na Televisheni zikawa zinawarekodi.
Binafsi nakiri Kuwa ni Mpenzi sana wa 'show  'ya Makomandoo . Hakuna ubishi ' Show' ya Makomandoo ilisababisha wale ambao Hawajawahi kuwaona Makomandoo wawaone ,Kupamba sherehe hizo za Kitaifa na kufanya wananchi Wazidi kulipenda Jeshi Lao na Kuwa na Imani nalo.

Uhusiano wa JWTZ na majeshi mengine ulizidi  kuimarika Kwani tulishuhudia Wanajeshi wetu wakienda Katika majeshi mengine kwaajili ya kubadilishana uzoefu Katika kushiriki Mafunzo mbali Mbali, na Wanajeshi wa majeshi ya kigeni  wakija Tanzania kutoa huduma za kujitolea na kujifunza mambo mbalimbali.

Itakumbukwa  hapo zamani mafunzo ya awali ya JKT yaliyokuwa ni ya lazima lakini serikali ikaja kuyafuta  lakini hivi karibu serikali wakati Mwamunyange akiwa Mkuu wa JWTZ ,ili rudisha Mafunzo hayo ya JKT kwa wahitimu wa Kidato cha Sita Ambayo hadi Sasa yanaendelea kutolewa.

Pia Mwamunyange anaelezewa Kuwa alitetea maslahi ya Wanajeshi wake na ya kuboreshwa , Jeshi lake lilishiriki Katika Michezo mbalimbali kama ilivyo Ada ya Jeshi Hilo.

Wosia wangu kwako Jenerali Mwamunyange,chondechonde nakuomba  usije ukadanganyika ukaamua kujitia wazimu ukajiingiza   Kwenye tamaa ya kupata madaraka ya Siasa kama eti Kugombea Ubunge,vyeo katika vyama vya siasa .Sitaki kusikia hizi Habari hapo Mbele ya safari. 

Umestaafu kwa heshima zote ,tunza hiyo heshima yakokakaa nyumbani Katulie fanya mambo yako.Ukiingia Kwenye siasa ukae ukijua heshima yako yote uliyojijengea w itafutika, na sikufichi mimi ndiyo nitakuwa mtu wa kwanza kukushughulikia kwa kalamu  licha nafahamu fika Ibara 21 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ina kupa haki ya kuchagua, kuchaguliwa na kuteuliwa .

Nimelazimika kukupata taadhali hiyo  kwasababu aliyewahi Kuwa Mkuu JWTZ, Jenerali Mstaafu Robert Mboma alivyostaafu Akaamua kwenda Kugombea Ubunge Jimbo la  Mbeya Vijijini ( CCM) kitendo kilichosababisha watu nikiwemo mimi kumshambulia vikali kwa makala ,akachafuka na kuonekana ana tamaa ya madaraka na watu wakahoji ni lini alijiunga na CCM na misho wa siku katika mchakato wa kumpata mgombea mmoja wa ubunge wa kupeperusha bendera ya CCM,jina la Jenerali Mstaafu Mboma lilikatwa na vikao Vya CCM likapitishwa jina la Kada mwingine wa CCM.

Karibu uraiani Jenereli Mstaafu Mwamunyange Kwani hivi sasa wewe ni Mwanajeshi Mstaafu. Mazuri uliyoyafanya ndani ya JWTZ yataenziwa na kuendelezwa .

Nakutakia Afya njema na Maisha Marefu Katika Maisha haya mapya ulivyoanza kuyaishi kama Mwanajeshi Mstaafu .Hakika Jenerali Davis Mwamunyange' Kipenzi cha Wanajeshi'  umeacha alama ya kukumbukwa ndani na nje ya JWTZ kutokana .

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg:www.katabazihappy.blogspot.com