MAHAKAMA YAKATAA KUMWONDOLEA DPP NGUVU YA KUZUIA DHAMANA KESI ZA UHUJUMU UCHUMI


Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Mahakama ya Rufani nchini imekataa kutamka Kuwa  Kifungu cha 36(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ,sura ya 200 ya Mwaka 2002  kinachompa mamlaka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuzuia dhamana kwa washitakiwa wa kesi za Uhujumu uchumi kinavunja ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 .

Kifungu hicho cha 36(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ,kinampa mamlaka Mkurugenzi wa Mashitaka ( DPP), Kuwasilisha hati ya Kuzuia dhamana kwa sababu ya maslahi ya taifa kwa mshitakiwa anayekabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi na Mahakama Inakuwa haina mamlaka ya Kuzuia hati hiyo ya DPP. Ibara ya 13(2) (a) ya Katiba ya nchi inatoa Haki ya mshitakiwa kupata dhamana.

Hukumu hiyo ya kihistoria Imetolewa Februali 21 Mwaka huu na jopo la Majaji wa tatu wa mahakama hiyo ya juu nchini, Mbarouk Mbarouk ,Mziray na Mkuye Katika rufaa ya jinai namba 252 ya Mwaka 2016  iliyokuwa imekatwa na Mwomba rufaa ,Emmanuel  Simforiani Massawe dhidi ya Jamhuri iliyokuwa ikipinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam  , wa Aprili 12 Mwaka 2016 Katika ombi dogo la kesi ya jinai Na.51 ya Mwaka 2016 .

 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitupilia  mbali ombi la Massawe lilokuwa likiomba mahakama hiyo impatie dhamana katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwasababu dhamana ni haki yake Kikatiba na kwamba anaomba mahakama hiyo itupilie mbali hati ya DPP aliyoiwasilisha chini ya kifungu cha 36(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ,ambacho DDP alikitumia kumfungia dhamana yake kwasababu makosa anayoshitakiwa nayo yana dhamana  ambapo Mahakama Kuu ilikataa kumpatia dhamana Massawe kwasababu Kifungo hicho kinampa mamlaka DPP ya Kuzuia dhamana kwa washitakiwa wa Kesi za uhujumu uchumi kwa maslahi ya taifa.

Massawe ambaye alikuwa akitetewa na wakili Dk. Lugemeleza Nshalla ,Fulgence  Massawe na Jeremiah Mtobesya ni Mwanasheria  wa Reli Asset Holding Company ambaye pia  alikuwa akishitakiwa kwa kosa la matumizi Mabaya ya madaraka kinyume Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007  na kusababisha serikali Hasara kinyume paraghrafu ya 10(1) ya Jedwari  na Kifungu Cha 57(1) na 60(2) ya  Sheria ya Uhujumu Uchumi ya Mwaka 2002.

Mawakili wa Mwomba rufaa, Dk.Nshalla na Mtobesya ,Fulgence walipinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu wakakata rufaa Mahakama ya Rufani na kutaja Sababu Sita za kupinga uamuzi ule Kuwa Mahakama Kuu ilikosea kisheria Kusema haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa mshitakiwa pindi tu DPP anapowasilisha hati ya Kuzuia dhamana ya mshitakiwa.

Sababu ya pili Wakili Dk. Nshalla na Mtobesya alidai ,jaji alikosea kisheria kusema kuwa pindi tu DPP anapokuwa amewasilisha mahakamani hati hiyo ya kuzuia dhamana ,mahakama inakuwa haina tena mamlaka ya kusikiliza maombi ya dhamana.

Tatu, Jaji alijielekeza vibaya wakati akitoa uamuzi wake aliposema Mahakama Kuu aipaswi kujua kilichopo nyuma ya pazia ya hiyo Hati ya DPP ya kufunga dhamana.

Aidha Jaji huyo wa Mahakama Kuu alijielekeza vibaya  kisheria kukataa kumpatia dhamana mteja wao (Mwomba rufaa) kwa kigezo cha kulinda usalama na maslahi ya Jamhuri ya Muungano kwasababu dhamana ni haki ya Kikatiba.

Sababu ya Sita ,Mawakili Hao walidai Jaji Huyo alikosea kisheria kwasababu alishindwa kuzingatia uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam ,Katika Kesi Madai namba 29 ya Mwaka 2015 iliyokuwa imefunguliwa na Wakili Jeremiah Mtobesya  dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo Mtobebesya aliomba Mahakama hiyo itamke kuwa Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai ,kinachompa mamlaka DPP Kumfungia mshitakiwa dhamana ni kinyume na Katiba ambapo Mahakama hiyo ilitamka Kifungu hicho kinakwenda kinyume na Ibara ya 13 (6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 .

Itakumbukwa Kuwa  Januari 31 Mwaka 2018 , Mahakama ya Rufani chini ya jopo la majaji sita  ilitupilia Mbali rufaa iliyokuwa imekatwa  na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Jeremiah Mtobesya ambapo Mahakama hiyo ya Rufaa ilisisitiza Kuwa Kifungu hicho cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinafunja Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya nchi.

Kwa mujibu wa nakala hiyo ya hukumu ambayo ninayo, upande wa Jamhuri ulikuwa ukiongozwa na Wakili Mkuu wa serikali, Tumaini Kweka aliyekuwa akisaidiwa na Beata Kitau na Faraji Nguka  walipangua hoja za Mawakili wa Mwomba rufaa kama ifuatavyo.

Wakili wa serikali Kweka alisema anaomba rufaa hiyo it upwe kwasababu hoja ya Mawakili wa Mwomba rufaa iliyotumia maamuzi ya Kesi ya Mtobesya haina mantiki yoyote Katika shauri Hilo kwasababu Kesi ya Mtobesya iliyotolewa uamuzi Mahakama Kuu ilikuwa ni Kesi ya Kikatiba na rufaa hii ya Mwomba rufaa ( Massawe) siyo Kesi ya Kikatiba na Jamii ya Kesi ya jinai  na kusisitiza Kuwa DPP anayomamlaka ya Kuzuia dhamana ya mshitakiwa kwa maslahi ya sera ya nchi.

Wakitoa hukumu ya rufaa hiyo ya jinai Jopo Hilo la Majaji watu ,Jaji Mziray alisema kwanza wanataka Ieleweke Kuwa Mahakama hiyo Katika shauri Hilo lilokuwa Mbele Yao lilikuwa siyo Kesi ya Kikatiba ..

'Kesi iliyokuwa mbele yetu ilikuwa  ni rufaa ya Kesi ya jinai ambayo Mwomba rufaa (Massawe) alikuwa akiomba Mahakama Kuu impatie dhamana ikakataa kumpatia kwasababu DPP aliwasilisha hati ya Kuzuia dhamana kwa kutumia Kifungu cha 36(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi  ndipo Mwomba rufaa Huyo akakata rufaa Mahakama ya Rufaa kuomba apatiwe dhamana ....hivyo tunasisitiza Kesi hii siyo ya Kikatiba ni rufaa ya Kesi ya jinai' alisema Jaji Mkuye.

Jaji Mziray  alisema jopo Hilo linatupilia Mbali hoja ya Mawakili wa Mwomba rufaa kuwa mwomba rufaa akupewa Haki ya kusikilizwa na Mahakama Kuu  wakati DPP alipowasilisha hati ya kumfungia dhamana na  kwa mujibu wa rekodi iliyopo   mahakamani hapo (Memorundum of Appeal ) inaonyesha  Mwomba rufaa (Rufaa)alipewa nafasi na Mahakama Kuu ya kusikilizwa na kwamba pindi DPP  anapowasilisha hati hiyo ya Kufunga dhamana ,Mahakama Inakuwa haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa mshitakiwa hivyo Mahakama Kuu ilikuwa sahihi kukataa kumpatia dhamana mshitakiwa kwasababu DPP aliwasilisha hati ya Kufunga dhamana .

Alisema Kesi ya DPP dhidi ya NURU  DIRIE imeweka msimamo wa kisheria kuhusu hati ya DPP ya Kufunga dhamana kwa kutumia Kifungu hicho cha 36(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba DPP atalazimika kuzingatia vitu hivi vitatu ambavyo ni 1. DPP lazima hiyo hati yake iwe Katika mfumo wa maandishi (2) Hati hiyo ya DPP ya Kuzuia dhamana aitoe kwaajili ya Usalama na maslahi ya Jamhuri ya Muungano .(3) Hati hiyo ya DPP ya Kuzuia dhamana itatolewa Katika Kesi za jinai ama Katika Kesi ambazo hazijamalizika au rufaa ambazo bado hazijatolewa hukumu.

 " Jopo hili linakubaliana na hoja ya Wakili kiongozi wa serikali Tumaini Kweka kesi ya Mtobesya ni kesi ya Kikatiba na kwamba rufaa ya jinai iliyopo mbele yao siyo kesi ya Kikatiba ni rufaa ya kesi ya Jinai Kuwa rufaa hii ya jinai siyo Kesi ya Kikatiba hivyo ....hivyo siyo matakwa ya Kisheria yanamtaka DPP kutoa Sababu za Kuwasilisha hati ya Kumfungia mshitakiwa yoyote dhamana Kwani DPP anachotakiwa ni kuzingatia Usalama au maslahi ya Jamhuri ya Muungano na kwamba hati hiyo ya DPP inaweza kuonekana haina Msingi pale tu itakabothibitika Kuwa aliwasilisha hati hiyo kwania ovu au matumizi Mabaya ya Mahakama kitu ambacho akijawahi kutokea na kuthibitishwa Mbele ya Mahakama na kwasababu hiyo Mahakama hii inatupilia Mbali rufaa hiyo " Alisema Jaji Mziray

Itakumbukwa Kuwa Junuari 31 Mwaka 2018 , Mahakama ya Rufani nchini chini ya jopo la Majaji Sita,  hukumu iliyokuwa imekatwa  na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Jeremiah Mtobesya ambapo Mahakama hiyo ya Rufaa ilisisitiza Kuwa Kifungu hicho cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 ambacho kinampa mamlaka (DPP ) Kufunga dhamana ,kinavunja Ibara  ya 13(6)(a) ya Katiba ya nchi ambayo inatoa Haki ya mshitakiwa kupata dhamana.

Hukumu hiyo ya Kesi ya Kikatiba maarufu kesi ya Mtobesya  ilipokelewa kwa Shangwe na wanaharakati na Wanasheria na Mawakili wa kujitegemea ambao wengine walinukuliwa wakipongeza Mahakama ya Rufani  Kuwa imetenda na kwamba DPP alikuwa na mamlaka makubwa yanayovunja Katiba ya nchi.

CHANZO: www.katabazihappy.blogspot.com
FACEBOOK: Happy Katabazi

24/2/2018.

PROFESA ABDALLAH SAFARI


Na Happiness Katabazi

PROFESA SAFFARI ni Mbobezi,Mhadhiri wa Fani ya Sheria na Mwandishi wa vitabu vingi tu.

Nakushukuru Mzee wangu Profesa Safari kwakuikubali makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho , (RAIS AANZE KUREJESHA NYUMBA YAKE  SERIKALINI) , iliyochapichwa na Gazeti la Tanzania Daima  13/3/2008.

Ambayo aliichukua na kutumia maudhui ya makala yangu hiyo katika ukurasa wa nne wa kitabu chako kiitwacho ( HAJA YA KUWA NA TUME HURU YA UCHAGUZI YA TAIFA TANZANIA).

Nimepata fursa ya kukisoma kitabu hicho chote chenye kurasa 34 ambacho alinipatia jana nilipomtembelea ofisini kwake Dar es Salaam na kubadilishana nae mawazo, nimejifunza mambo mengi.

Aidha kesho nitaanza kukisoma kitabu chake kingine kiitwacho (PROSECUTION AND DEFENCE OF CRIMINAL CASES).

Safari ambaye ni Profesa wa Sheria ni miongoni mwa wahadhiri wa chache nchini ambao wameandika na wanaendelea kuandika  vitabu vingi nchini.

Amewahi andika kitabu ambacho kimetumika kufundishia shule ya msingi na sekondari na hivi sasa anaandika kamusi ya Lugha ya kisheria kwa kutumia lugha ya kiswahili pia anaandaa kitabu cha changamoto alizokutana nazo wakati akiwa wakili amenidokezea baadhi ya mambo aliyoyasema atayaweka kwakweli yatatufundisha sisi wanasheria wachanga.

Safari pia amewahi kuwa wakili wa serikali ,wakili wa kujitegemea ambaye ameendesha kesi nyingi maarufu nchini pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Diplomasia.

Jana nilifurahi sana nilivyofika ofisini kwake na kupiga nae stori nyingi sana za kisiasa,kisheria kwani wakati nilopokuwa Mwandishi wa habari katika magazeti,Mzee Safari tulikuwa tukikutana nae mahakamani anakuja kutetea wateja wake katika kesi mbalimbali na mimi nilikuwa nikienda mahakamani kuandika habari za mahakamani.

Mungu akupe maisha marefu Mzee wangu  Profesa Abdallah Safari.

 Ms.Happiness Katabazi  ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi na Mwanasheria.

13/2/2018.

TAMBWE HIZZA 'TAJIRI WA MANENO ' UMEKWENDA


Na Happiness Katabazi

KWA wafuatiliaji wa masuala ya siasa nchini tangu Miaka 1998 ni wazi kabisa masikioni mwao jina la mwanasiasa maarufu nchini,Richard Tambwe Hizza ambaye amefariki Leo asubuhi siyo geni masikioni mwao.

Tambwe Hizza alikuwa ni miongoni mwa Chanzo changu cha Habari muda mrefu Enzi zile za mwishoni mwa Mwaka 1999 hadi 2000-2005 Enzi hizo Mimi nikiwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi na Kisha Gazeti la Mtanzania na Tanzania Daima.

Hizza ambaye Enzi hizo alikuwa akitamba Katika medani ya siasa za upinzani Kwani alikuwa ni  Katibu Mwenezi  wa Chama cha Wananchi (CUF) ,chenye ofisi zake Buguruni ,Dar es Salaamu ,enzi hizo CUF kilikuwa ni chama cha upinzani chenye nguvu,ushawishi na mara kwa mara Jeshi la Polisi lilokuwa chini ya Inspekta Jenerali (IGP) , Omar Mahita lilikuwa likieleza nguvu zake kwa wafuasi wa chama hicho hicho cha CUF ambao walikuwa wakikaidi amri za jeshi hilo ambazo zilikuwa zikipiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara iliyokuwa inapangwa kufanya na Chama hicho siku ya Ijumaa baada ya ibada ya waumini wa dini kumalizika ,Mara nyingi CUF maandamano Yale ambayo yalikuwa yamepigwa marufuku na Jeshi la Polisi yalikuwa yakianzia Buruguru kuelekea Uwanja wa Kidongo Chekundu Dar Es Salaam.

Nikiwa kama Mwandishi wa Habari wa siku nyingi ambaye nilipata fursa ya kuripoti Habari za vyama Vingi Vya siasa Katika mikutano ,maandamamo ya halali, haramu kisheria toka 1998-2014 , lazima nikiri wazi CUF ya Enzi zile ya 1999-2005  kilikuwa ni Chama Chenye wanachama ambao walikuwa na umoja na ujasiri na walikuwa na baadhi Yao walikuwa na ujasiri wa kukaidi amri za Jeshi la Polisi na kuamua kuingia barabarani kuandamana , mikutano na Matokeo yake walikuwa wakiambuliwa kupokea vipigo ,kurushiwa mabomu ya Machozi na Jeshi l Polisi na wengine kufunguliwa Kesi za jinai mahakamani.

Nadiriki Kusema hadi sasa bado akijitokea hapa nchini Chama cha upinzani Chenye wafuasi wenye misimamo usiyoyumba kama waliyokuwa nayo wafuasi wa CUF wa zama zile .

Binafsi Hizza nawe kumweleza ni mwanasiasa aliyekuwa na ushawishi wa maneno yaani kwa maana Kuwa Hizza awapo jukwaani au Mbele ya vyombo Vya Habari alikuwa ni Hodari sana wa kupangilia maneno aliyokuwa akiyaongoza ambao yanamzaa ndani yake ,misimamo na ujasiri ndani yake.

Mwanasiasa Huyo pia aliwahi kugombea ubunge Jimbo la Temeke alikuwa akipenda kutumia siasa za kurusha vijembe kwa wapinzani wake wa kisiasa hadi ikafikia Hatua akapachikwa Majina yafuatayo ( TAJIRI WA MANENO YA KISIASA ) , ( MTOTO WA TEMEKE) .

Maandamano mengi ya CUF ambayo Jeshi la Polisi ilikuwa iliyapiga marufuku kupitia aliyekuwa Msemaji wa Jeshi la Polisi Enzi za IGP -Mahita, Aden Mwamunyange na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar Es Salaam Enzi hizo , Alfred Gewe,Hizza ndiyo alikuwa akituita sisi waandishi wa Habari licha Jeshi la Polisi kuwazuia maandamano hayo ,yeye anajitokeza anasema maandamano hayo lazima yafanyike na Anawataka wafuasi wa CUF washiriki maandamano hayo bila kukosa na kweli walikuwa walishiriki kikamilifu na Kuishia kupata kipondo kutawanywa kwa mabomu ya Machozi na Jeshi la Polisi.

Kifo Tambwe Hizza Leo kimenifaya nimkumbuke Mwandishi wa masuala ya siasa marehemu Joyce Mmasi aliyefariki usiku wa kuamkia 6/12/2017 baada ya kuugua kwa muda mrefu , Kwasababu Joyce ambaye nilikuwa nafanya naye Kazi Katika Gazeti la Mwananchi ndiyo Mara kwa Mara nilikuwa naenda naye pamoja na Mpiga picha Leah Samike au Marehemu Joseph Senga kuchukua Habari za CUF na Katika maandamano Yao haramu ambayo mwisho wa siku vurugu zikianza tulikuwa tukikaa upande wa madefenda ya Polisi kwaajili ya Usalama wetu .

Kuna siku Niliwahi kumuuliza Hizza ni Kwani amekuwa Kinara wa kuhamasisha  watoto wawatu  washiriki maandamano yaliyoharamishwa na Jeshi la Polisi Enzi hizo CUF ilikuwa ikiitwa CUF NG'ANG'ARI halafu yeye hapokei Katika maandamano hayo haramu ?alinijibu kwa kifupi Kuwa bado anaitaji kuishi.

Nilimtazama Hizza baada ya kunipa Jibu Hilo na kuanza kuwasikitikia wafuasi wa vyama Vya siasa wanaondamana Katika maandamano haramu na wengine niliyokuwa karibu Yao nilikuwa naninaendelea kuwashauri wasikubali kutii amri za baadhi ya viongozi wa kisiasa zinazowataka washiriki maandamano haramu Kwani mwisho wa siku watakaoumia ni wao siyo viongozi wao wa kisiasa.

Kuelekea kampeni za Mwaka 2005 , upepo wa kisiasa Ulianza kuvuma vibaya upande wa Hizza ndani ya CUF Hali iliyosababisha kuanza kusuasua kisiasa .

Na kwakuwa sisi waandishi wa Habari ' Wachokonozi' tulikuwa tukipata taarifa hizo toka ndani ya Vyanzo vyetu CUF . Na binafsi Hizza alipoondoka CUF Nilimhoji Hizza ameondoka  CUF amatarajia kwenda kujiunga na Chama gani cha upinzani Kwani hapo awali akiwa CUF alishajiapiza Kuwa hawezi kujiunga na CCM Kwani  'YEYE KUHAMIA CCM NI SAWA NA KUZINI NA MAMA YAKE MZAZI'?

Hizza alinijibu hivi ; " Amehama  ghorofani  ataenda kuhamia ghorofani'. Kwa maana anatoka Katika Chama kikubwa yaani CUF anaenda kujiunga na Chama kikubwa ambacho hakukotaja kwa siku hiyo.

Baada ya uchaguzi Mkuu 2005 kumalizika na Dk.Jakaya Kikwete kushinda kuapishwa Kuwa Rais wa awamu ya nne na Mwenyekiti wa CCM, Hizza na aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha TLP, Leo Lwekamwa walitangaza kujiunga na CCM .

Na muda mchache baada ya Hizza kujiunga na CCM, CCM ilimpa Cheo Mkurugenzi wa Kitengo cha Propaganda Katika Idara ya Itikadi na Uenezi Makao Makuu ya CCM nchini ya Katibu Mkuu wa CCM wa Enzi hizo, Mzee Yusuf Makamba.

Hizza aliweza kufanyakazi hiyo ndani ya CCM licha alikuwa akinieleza alikuwa akifanya Kazi Katika mazingira magumu Kwani wale CCM  kindakindaki walichukia yeye kupewa nafasi ile Kwani yeye Hizza alivyokuwa CUF alikuwa akiisumbua CCM sana .

Lakini hata hivyo Hizza akufumu ndani ya CCM aliamua kuhama Chama hicho cha CCM na kwenda kujiunga na Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA)  ambapo hadi Leo hii umauti unamkuta ghafla alikuwa akikitumikia Chama hicho kikamilifu.

Na ushahidi wa Hilo ni Katika kampeni za uchaguzi Mdogo jimbo la Kinondoni, Hizza ndiyo amekuwa akisimama Katika majukwaa kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo Hilo kwa tiketi ya Chadema, Mwanahabari  Salum Mwalimu.

Hizza tume fahamu nae Miaka mingi sasa Aliniona wakati Nina mwili mdomo na baadae uzito uliongezeka sana .Ilipofika Mwaka 2013 nilikuwa na uzito wa Kg.130 Niliamua kuanza kufanya mazoezi ya viungo kupunguza uzito ambapo hadi sasa Nina Kg.80 .

Kwa tunaomfahamu Hizza hapo zamani akuwa na uzito mkubwa kama huu aliyokuwa nao hadi Leo anafariki Duniani. Amefariki akiwa na uone Kano wa uzito mkubwa( Mnene sana) na hata Nilipokuwa nikikutana naye na kukaa naye tunajadili masuala ya siasa alikuwa akionekama akihema kwa tabu na ule uzito mkubwa unamnyima raha.

Mara Kadhaa nilikuwa kumshauri apunguze huo uzito ,uzito umemuelemea na umemualibia mwonekano wake alikuwa akiniambia amesikia ushauri wangu atakufanyia Kazi ila akawa anania kama kweli nataka nimsaidie apunguze ule uzito nikubali anioe ili GYM tuwe tunaenda nae.

Hata hivyo Mara kwa Mara amekuwa akinieleza ugonjwa wa PUMU umekuwa umkimsumbua sana na kuamini ipo siku utakuja kukatisha Maisha yake.Nilikuwa nikimpa pole Sana.

Mara ya mwisho Kuwasiliana naye ilikuwa wiki  iliyopita kupitia namba yake 0755 263798, Tulijadili Hali ya siasa zinavyokwenda na akasema anakerwa na serikali ya awamu ya nne kupiga marufuku mikutano ya vyama Vya siasa na kwamba anashangazwa na Uongozi wa Chadema sijui ni Kwani hawampi nafasi ya use maji wa Chama hicho na kwamba endapo angepewa basi kila kukicha serikali ingekuwa inamfungulia Kesi za uchochezi. Nilicheka sana.

Poleni familia, wanasiasa wenzake, Chadema ,CCM,ndugu na jamaa na marafiki kwa kuondokewa na Mpendwa wetu Hizza ambaye  alikuwa aishiwi mzaha ,,kurusha vijembe kwa mahasimu wake wa kisasa hasa CCM , na kukosoa pale anapoona mambo ayaendi  sawa.

Kila binadamu Ana madhaifu yake , na Hakuna ubishi Kuwa Hizza ameweka rekodi ya kuhama Hama vyama na kuhama vyama siyo kosa Kwani Ibara ya 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ,inatoa Haki Mtanzania yoyote kujiunga na Chama chochote akipendacho.

Pia Hizza Katika siasa hasa siasa katika vyama vya upinzani ameacha harama na kwasisi tuliopataga fursa ya kumshuhudia  akifanya siasa Enzi zile akiwa CUF,CCM na sasa CHADEMA.

Na Hizza alitumia kikamilifu Haki yake hiyo ya Kikatika alikuwa CUF akaondoka akahamia CCM akatoka akajiunga na CHADEMA hadi umauti ulivyo mkuta Leo asubuhi.

Tajiri wa Maneno ya Kisiasa Tambwe Hizza, sisi  tulikupenda ila  Mungu amekupenda zaidi.

Utakumbukwa sana na waandishi wa habari tuliokuwa karibu yako kwa miaka mingi nikiwemo mimi (Happiness Katabazi), Martin Malela ( Tanzania Daima ) ,Ezekiel Kamwaga na wengine wengi.Tutakukumbuka .
Imenichukia muda kaumini Hizza kama amefariki kwasababu hadi Jana Hizza alishiriki mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu .

Na  kila nikikumbuka vibweka vyake majukwaani Leo Nikawa naangua kicheko na Kuishia  kukubaliana na ule Msemo usemao ' HAPA DUNIANI SISI TUNAPITA' Kweli Hizza umefariki ,nitakukumbuka  Kwani nilimpenda sana aina yako ya siasa uliyokuwa ukiifanya majukwaani ya kurusha vijembe kwa maasimu wa Chama Chako cha siasa.

Mungu aiweke roho yako Mahali panapostahili.Amina.

CHANZO: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
8/2/2018

DPP ANYANG'ANYWA TENA MAMLAKA YA KUZUIA DHAMANA


Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Ya Rufani nchini imeifukuza kwa gharama   rufaa ya Kesi ya Madai iliyokuwa  imekatwa  na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya mjibu    Rufaa, Jaremia Mtobesya iliyokuwa inaiomba  Mahakama hiyo itengue uamuzi  uliotolewa  na Mahakama Kuu Kanda Dar es Salaam ambayo ulisema  Kifungu cha 148 (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 Kuwa unakwenda  kinyume na Ibara ya 13 (6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Kwa mujibu wa nakala ya hukumu hiyo inaonyesha imesainiwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani ,John Kahyoza ,Januari 31 Mwaka huu, inasema jopo la Majaji wa Tano walioketi Dar Es Salaam.

Jaji Bernad  Luanda,Kipenka Mussa,Bethuel  Mmilla, Stellah Mugasha  na Jacob Mwambegele kwa Kauli Moja walitoa hukumu hiyo ya  ya kutupilia   rufaa hiyo Na.65/2016 iliyokuwa imekatwa mahakamani hapo na Mwomba Rufani ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mjibu Rufani ( Mtobesya ) .

Jaji Kipenka  alisema jopo Hilo baada ya kupitia Sababu nne za Mwomba rufaa kukata rufaa ambazo miongoni mwa Sababu hizo Kuwa Mahakama Kuu ilikosea Kusema Kifungu hicho kinamnyima fursa  mshitakiwa kupinga hati hiyo ya DPP ya Kuzuia dhamana na kwamba Mahakama Hiyo ilikosea kisheria kukubali kutolea uamuzi shauri ambalo Mwombaji alikosea kunukuu Ibara ya Katiba    hoja ambazo  Jaji Mussa  azina mashiko.

" Mahakama ya rufaa imetupilia  Mbali kwa gharama rufaa iliyokatwa Mbele yetu na Mwanasheria Mkuu wa serikali iliyokuwa ikiomba  Mahakama hii itengue uamuzi  ya Mahakama Kuu uliokuwa umetamka  kuwa  Kifungu 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwasababu kwasababu ni kweli Kifungo kicho kinakwenda kinyume na Ibara ya 13 (6)(a)  ya Katiba ya nchi;

"Na Mahakama hii ya Rufani nayo inakubaliana na hukumu ya Mahakama Kuu Kuwa Kifungu hicho cha 148(4) Sheria hiyo ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinafunja matakwa ya  Ibara hiyo ya Katiba hivyo uamuzi wa Mahakama Kuu ulikuwa sahihi na Mahakama hii imekataa   kutengua uamuzi ule hivyo utabaki kama ulivyo na Mwanasheria Mkuu wa serikali alipe gharama za Kesi kwa Mjibu  Rufani( Mutobesya) aliyekuwa anatetewa na Wakili wa kujitegemea ,Mpare Mpoki.

Ibara ya 13(6) (a) ya Katiba ya nchi inasomeka hivi ;   " Wakati Haki na wajibu kwa mtu yeyote inapoitajika kufanyiwa maamuzi na Mahakama au Chombo kingine chochote kinachohusika, basi mtu Huyo Atakuwa na Haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia Haki ya kukata Rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya Mahakama au Chombo hicho kingine kinachohusika" .

Disemba  22 Mwaka 2015 , Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam Katika Kesi ya Kikatiba Na 29 /2015 ,Shabani Lila ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa sasa,Kihiyo  na Ruhangisa  ambaye alistaafu Ujaji wa kwa Hiari mwaka 2017 ,ambapo jopo hilo lilikubaliana na hoja za malalamikaji Mtobesya Kuwa Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ,kina kwenda kinyume na Ibara ya hiyo ya Katiba ya nchi.

Mwaka 2016 ,Mwanasheria Mkuu wa serikali alikataka rufaa Mahakama ya Rufani nchini, kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu akiomba utenguliwe uamuzi huo kwasababu nne ambazo miongoni mwa Sababu hizo ni kwamba Mahakama ilikosea Kusema hati ya Kufunga dhamana ya mshitakiwa inayowasilishwa mahakamani na DPP inammnyima mshitakiwa Haki ya kuipinga hati hiyo ya DPP Katika Chombo kingine.

Desemba 22 Mwaka 2015 , Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam Katika Kesi ya Kikatiba Na 29 /2015 ,iliyofunguliwa na Mtobesya dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Shabani Lila ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa sasa,Kijiyo na Ruhangisa  ambaye alistaafu Ujaji wa kwa Hiari ambapo jopo lilikubaliana na hoja za malalamikaji Mtobesya Kuwa Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ,kina kwenda kinyume na Ibara ya 13 (6)(b) ya Katiba ya nchi.

Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ni Kifungu ambacho kinampa mamlaka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) , Kuwasilisha mahakamani kwa maandishi hati ya Kufunga dhamana kwa mshitakiwa yoyote wa makosa ya jinai ambayo makosa hayo kwa mujibu wa Sheria yana dhamana ila DPP Ana mamlaka ya kutumia Kifungu hicho Kufunga dhamana ya mshitakiwa kwa Sababu ya Usalama wa mshitakiwa na pindi DPP akiwasilisha hati hiyo ya Kufunga dhamana Mahakama Inakuwa haina uwezo wa kupingana na hati hiyo kama imebidhi matakwa yote ya kisheria.

Kwa Mujibu wa hati yake ya Madai ilioambatanishwa na kiapo Chake   Chake Juni 30 mwaka 2015 ,Mutobesya alidai  Kuwa Ibara 26 ( 2) ya Katiba ya nchi inasomeka kama ifuatavyo;  " Kila mtu Ana Haki , kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria , kuchukua Hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na Sheria za nchi".

Na Kuwa Kifungu cha 4 na 5 Cha Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Binadamu(BRADEA)

Hivyo alitumia  Kifungu na Ibara hizo za Katiba kwenda Kufungua Kesi Mahakama Kuu ili kuiomba Mahakama Kuu itamke Kuwa Kifungu cha 148(4) cha Sheria hiyo  kinakwenda kinyume na Ibara 13(b)(a) ya Katiba ya nchi na kwamba Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya nchi inampa Haki ya kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi  ya Katiba na sheria  za nchi.

Itakumbukwa Kuwa   Kifungu hicho cha 148(4) cha Sheria hicho ,ndicho kilichotumika  Kumfungia dhamana Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu ,Sheikh Issa Ponda aliyekuwa anatetewa na wakili wa kujitegemea na wakili Nasoro Juma wakati upande wa Jamhuri ulikuwa ukiwakilishwa na wakili mwandamizi wa serikali ,Tumaini Kweka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa ambapo DPP wa enzi hizo, Dk.Eliezer Feleshi aliwasilisha hati ya kufunga dhamana ya Sheikh Ponda ambaye yeye na wenzake 49 walikuwa wakikabiliwa na makosa ya wizi,uchochezi ,kuingia kwa jinai na  makosa aliyokuwa akishitakiwa nayo katika kesi hiyo namba 245/2012 yalikuwa na dhamana ambapo na  Sheikh Ponda alikaa gerezani tangu Oktoba 18 mwaka 2012   hadi Mei 9 mwaka 2013  mwanzo wa kesi hadi kesi ilipomalizika ambapo alipatikana na hatia ya kutenda kosa la kuingia kwa jirani akaacbiwa huru ila mahakama ikamtaka awe mtu mwenye tabia njema.

Kifungu hicho pia kulitumika Kumfungia dhamana kwa Mara ya pili Katika kesi ya kutoa maneno ya uchochezi Na.128/2013  iliyokuwa imefunguliwa na Jamhuri dhidi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro mwaka 2013  ambapo Hakimu Mkazi Mary Moyo alimwachiria huru Sheikh Ponda .

Katika kesi hii Ponda muda wote alikuwa amekaa gerezani kwasababu DPP alitumia kifungu hiyo kumfunga dhamana.

Hata hivyo Sheikh Ponda kupitia wakili wake Juma Nassor alikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,kupinga hukumu ya mahakama ya Kisutu ilimfunga kifungo cha mwaka mmoja na alishinda rufaa yake .

Na upande wa Jamhuri akurudhishwa na hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro iliyomwachiria huru Sheikh Ponda ambapo Jaji Edson Mkasimongwa  alisema hakuna mahali popote  ambapo imethibitishwa kuwa mtu fulani alichochewa kufanya mkusanyiko usio halali wala mtu aliyeumizwa imani yake.
Pia Kifungu hicho ambacho Tayari Mahakama Kuu ,Mahakama ya Rufani nchini imeisha kitangaza Kifungu hicho kinakwenda kinyume  na Katiba ,Ndio kimetumika na DPP Kuzuia  dhamana Mbunge wa Mbeya Mjini , Joseph Mbilinyi ( SUGU)  ambaye anasota gerezani wakati kosa a alishitakiwa nalo
Lina dhamana .

CHANZO: www.katabazihappy.blogspot.com
5/2/2018.

WAZIRI KIGWANGALA HIVI UNA AKILI TIMAMAMU?


Na Happiness Katabazi

JANUARI 25 mwaka huu, Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kuwakamata wahusika wakuu wa Mtandao wa Ujangili wa nyara za serikali na kupanga Mauaji ya aliyekuwa Mkurugenzi wa kampuni Palms Foundation na Mtetezi wa wanyama pori, Wayne Lotter ,Augosti  Mwaka 2017.

Waziri Dk. Kigwangala alisema  hayo mjini Dodoma alipokuwa Akizungumza na waandishi wa Habari na kulitaka Jeshi la Polisi kutekeleza agizo la kuwakamata majangili Hao ndani ya siku Saba ili Hatua nyingine zichukuliwe na Jeshi Hilo likishindwa kufanya hivyo ataenda kuwashitaki kwa  Rais John Magufuli.

Baada ya kusikia agizo Hilo lilotolewa na Waziri Kigwangwala nimeishia kujiuliza hivi huyu Waziri Kigwangwala Ana akili timamu?

Na Je Mbona mwanaume mzima anaonyesha anatabia za umbea umbea za Kupenda kuchongeachongea wenzake kwa Rais wa nchi?

Nimefikia uamuzi wa kujiuliza hivyo kwasababu ukilitafakari agizo Hilo Katika jicho la Sheria ni wazi Waziri Huyo Hana mamlaka ya kisheria ya kulipa Jeshi la Polisi lililioanzishwa kwa The Police Force And Auxiliary Service Act  Cap 322 ,  aimpi Waziri Huyo mamlaka ya kutoa amri kwa Jeshi Hilo.

Nakuuliza wewe Waziri Kigwangala hayo mamlaka ya kulipa Jeshi la Polisi siku Saba Umeyapata kwa mujibu wa Sheria hipi?

Maana Tanzania ni dola linaloongozwa kwa mujibu wa Sheria na siyo hizo porojo zako ambazo mtu mweye hadhi ya Waziri awezi kuziongea Mbele ya umma kupitia vyombo Vya Habari.

Umesema eti unayo Majina ya Hao waliopanga Njama na kumuua Huyo mwanaharakati Wayne Lotter na ushahidi unaona.

Yaani we Waziri Kigwangala Umepewa taarifa za Mauaji ya Wayne na ma Infoma wako tena ukute wamekulisha TANGOPORI yaani taarifa za uongo basi na wewe unaenda katika vyombo ya habari kana kwamba wewe ulikuwepo katika mauaji hayo wakati ukuwepo .

Mimi kama Mwanasheria wewe kupitia hayo maelezo yako wewe ushahidi  wako ni ushahidi wa kusikia ambao autapokelewa  mahakamani.

Kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(CPA) ,kinatoa madaraka kwa Polisi kufanyia uchunguzi taarifa za Uhalifu.

Kwa vifungu hivyo kisheria mtakubaliana na mamimi Kuwa Polisi ndiyo wenye mamlaka ya kuchunguza ,kukamata na pindi wakijiridhisha wana vielelezo Vya kuweza kumfungulia Kesi mtu wanayemtuhumu Kutenda kosa Fulani basi Polisi wakapeleka vielelezo hivyo Katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ( DPP).

Kwa mujibu wa Ibara ya  59 B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 .

Na Kifungu  cha 9 cha National Prosecution Service Act ,2008 , Mkurugenzi wa Mashitaka ( DPP) ,ndiyo mwenye mamlaka ya Kufungua Kesi za jinai mahakamani Kwaniaba ya Serikali .

Kifungu cha 5   The Police Force Force And Auxiliary Service Act , kimeanisha wazi  majukumu ya Jeshi la Polisi ambapo Moja majukumu yake kulinda Amani ,Sheria ,Kuzuia Uhalifu usitendeke,kulinda Raia na Mali zao

Ndiyo maana namuuliza huyu waziri hayo  mamlaka ya kutoa amri ya kushinikiza Polisi wachukue Hatua ndani ya siku Saba ameyapata wapi?

Nani kakupa hayo mamlaka ?Atueleze ili Tujue maana Tanzania ni dola lililoanzishwa na kinaongozwa kwa mujibu wa Sheria na wewe Kigwangala Uliapa kulinda Sheria za nchi?

Jeshi la Polisi limeanzishwa kwa mujibu wa The Police Force and Auxiliary Services Act Cap 322 .

Na ni chombo kinachotakiwa kifanyekazi kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu au wanasiasa.

Sasa kwanini wewe unatoa amri hizo za ovyo ambazo kwanza Huna mamlaka ya kutoa amri kwa Jeshi la Polisi kukamata watu Hao ambao wewe kupitia matamshi yako umeonyesha umeishawahukumu watu Hao Kuwa ni wauaji wakati Chombo Chenye mamlaka ya mwisho yautoaji Haki ni Mahakama kwa mujibu wa Ibara ya 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Kwani Mahakama ndiyo Chombo Chenye mamlaka ya Kumtia hatiani mshitakiwa Fulani kwa makosa aliyokuwa Akishitakiwa nayo.

Hivi unasema unayo Majina ya watu waliomuua Huyo mtu. Nakuuliza hayo Majina uliyapata lini? Na kutoka Katika mamlaka zipi?

We Waziri Kigwangala hivi ulikuwepo wakati hao watu wanne ambao majina yao umasema unayo wakimuua Huyo Raia wa kigeni?

Au ulivyoona Kamera zinakumuulika basi ukaamua kujiongelea mambo ambayo mwisho wa siku umechekesha walionuna?

Dk.Kigwangala hivi Jeshi la Polisi likija Kuibuka na Kusema hayo  Majina uliyonayo hayafanani na waliyonayo  utasema nini?

Au Jeshi la Polisi likisema waliomuua Huyo Raia wa kigeni ,Jeshi la polisi lilivyokwenda  kuwakamata washitakiwa wale walipambana  na Polisi na polisi likaamua kutumia silaha likawaua   utasema nini?

Maana kama walikufa katika majibishano na polisi , polisi wataendaje kwa DPP kutaka marehemu washitakiwe? Chunga mdomo wako nakushauri.

Uoni hilo agizo lako la siku saba kwa polisi ulilolitoa kwa umma linaweza kusaidia baadhi walioshiriki kutenda mauaji hayo kukimbia,kuvuruga ushahidi na hivyo kulipa wakati mgumu Jeshi la polisi kuendelea kufanya upelelezi wake katika tukio hilo la mauaji ya huyo Mwanaharakati ?

Kwanza  minakushangaa sana sijui wewe ni Waziri wa aina gani .Basi tufanye nikweli hayo Majina unayo kweli na Hao watu wamelimua kweli Huyo Rai wa kigeni hivi nafasi yako ya Uwaziri ulishindwa nini kwenda kimya kimya kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na kueleza hayo ili yeye awasiliane na Mapolisi ?

Lengo Lako hasa lilikuwa ni Kujenga au Kubomoa?

Minaona Lengo Lako hapa ni Kubomoa kwasababu kupitia Hilo agizo Lako ni wazi umelipaka matope Jeshi letu la Polisi na Taifa kwa ujumla Kuwa Raia wakigeni aliyeuawa hapa kwetu  Tanzania ,Jeshi letu la Polisi linafumbia macho wauaji.

Hivi kupitia agizo Lako ambalo halina  hadhi ya kisheria umepeleka ujumbe gani kwa serikali ya Huyo Raia aliyeuwawa kikatiri hapa nchini?

Kigwangala hivi unajielewa kweli wewe ni nani na una wadhifa upi na matamshi yako Katika Jamii ya achukuliwa kwa uzito gani na Jamii na hiyo serikali ya kigeni aliyotokea Huyo Raia aliyeuwawa? Una matatizo sana .

Halafu Kumbe mwenzetu unajitapa utaarifa za uhakika za Mauaji ya mwanaharakati Huyo sasa kwanini usiende Polisi kuwapatia taarifa na ushahidi wa Mauaji hayo?

Maana Kifungu  cha 7 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai, kinamtaka Mtu yoyote mwenye taarifa za kutendeka au kutaka Kutenda kwa Uhalifu ikiwemo Mauaji akatoe taarifa Katika mamlaka husika ikiwemo Jeshi la Polisi na akishindwa kufanya hivyo atashitakiwa .

Sasa na usomi wako na uwaziri wako ni kwanini umeshindwa kutimiza matakwa ya Kifungu hicho cha Sheria kwenda kutoa taarifa Katika Jeshi la Polisi unakimbilia Katika vyombo Vya Habari ?

Vyombo Vya Habari sikuhizi ndiyo vimekuwa Jeshi la Polisi la kupelekea taarifa za kihalifu?

Hivi ukienda kushitaki kwa Rais Magufuli ndiyo Magufuli yeye atakusaidia kuandaa Jalada la Kesi kufunguliwa mahakamani hata kama vielelezo bado haijapatikana Vya kutosha Vya kuwafungulia Kesi washitakiwa au ndiyo unaenda kuwashitaki awafute Kazi?

Maana sikuelewi kabisa ,maana hata ukienda kuwashitaki polisi kwa Rais mwisho wa siku Huyo Rais Hana mamlaka ya kuchunguza Kesi wala Kufungua Kesi mahakamani .

Naninalishangaa sana Jeshi la Polisi hadi sasa alijatoa amri ya kumuita na kumhoji Waziri huyu ili awapatie hizo taarifa na Majina ya Hao washukiwa?

Ni Jeshi hili hili uwa linafanya  haraka sana kuwakamata viongozi wa upinzani pindi wanapotoa matamshi mbalimbali na Kudai zinawahoji kwa kutoa Kauli za uchochezi?

Ajabu ni kwamba hadi Leo hii huyu Waziri ,Jeshi alijamuita kumhoji na awapatie ushahidi hayo maelezo aliyoyatoa  maana inaonenaka anajua mengi kuhusu Mauaji hayo.

Hivi Kigwangwala Mbona unapenda sana kuingilia Uhuru wa kufanyakazi wa taasisi zingine kama Polisi wewe nani kukuingilia Katika Wizara nayoiongoza?

Nani anakutuma kuingilia Uhuru wa Utendaji Kazi wa Jeshi la Polisi?

Kesi za jinai hazina  ukomo wa muda ( Limitation of Time) ya Kufungua Kesi mahakamani hata kama mtu  katuhumiwa kufanya kosa leo  anaweza kuja kushitakiwa hata miaka 40 ijayo tofauti na Kesi za  Madai  ( Civil Case) ambapo zinaukomo wa muda wa kuzifungua mahakamani.

Sasa  kwanini wewe Waziri Dk.Kingwangala unashinikiza Polisi ambao ndiyo wenye taaluma ya upelelezi wa Kesi za jinai wafanyekazi  kwa mashinikizo yako wewe badala ya taaluma? Una maslahi gani na hayo Mauaji ya Huyo Raia wa kigeni ?

Kuna watu wangapi hapa wanauwawa Katika mazingira yanayoaacha maswali, maiti zinaokotwa Kwenye fukwe za Bahari ya Hindi atujakusikia ukitoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kukamilisha uchunguzi?

Nakuasa   Dk.Kigwangala punguza sana kutumia vyombo Vya Habari Katika Utendaji wako wa Kazi Kwani siku zote Kizuri kinajiuza Kibaya  kinajitembeza.

Ndiyo wewe maana kupitia hivyo vyombo Vya Habari unavyovitumia tena wakati mwingine siyo  unatumia kutaja majina ya watu  Katika tuhuma ambazo tukikusikiliza mwisho wa siku tunaona unaweza kuja Kumpa Kazi bure DPP  mahakamani .

Heshimu mgawanyo wa madaraka , fanyakazi na Taasisi zingine za serikali kwa ushirikiano wa kweli siyo kwa kuwavizia kama hivi unavyolivizia Jeshi la Polisi ambayo Kimsingi wao ndiyo wapelelezi ,wakamataji.

Waziri Kigwangala  siku zote unapoamua kudili na Wapelelezi  ' Makachero' nakushauri  udili nao kwa akili sana siyo njia hii ya kitoto unayotumia kudili nao , ukijifanya  Mjuaji dhidi yao watoto wa mjini tunasema  Wapelelezi  'WATAKUFURAHISHA  ' na UTAFURAHII  .Yaani watakushangaza .

Mtangulizi wako Katika Wizara hiyo ya Maliasili , Balozi Sued Kagasheki naye alijaribu kufanya kama hili ulilofanya ambalo aliituhumu ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoani Arusha Mwaka 2014   Kwamba aipelelezi ipasavyo Kesi za Ujangili lakini mwisho wa wasiku Jeshi Hilo lilifanya uchunguzi wa Madai ya Kagasheki nakubaini alikuwa akisema uongo dhidi ya Ofisi ya RCO - Arusha .

Mwandishi wa Makala ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini na Mwanasheria.

Mungu ibariki Tanzania

CHANZO: www.blogger.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
27/1/2018

AGNES YAMO ,MDOGO WANGU SISI TULIKUPENDA ILA MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI



Na Happiness Katabazi

JANA  saa sita mchana mimi na mama yangu tulikupokea pale Hospitali ya Jeshi Lugalo,ukiwa huna fahamu na madaktari na manesi wa Lugalo walijitahidi kadri ya uwezo wao...

kuokoa maisha yako bila mafanikio.Jana saa 12 jioni manesi wa hospitali hiyo walitupatia vipimo walivyomchukua Agnes wakitaka twende Hospitali ya Mhimbili tukavipime na kisha tuwaletee majibu na kweli mimi na kaka wa Agnes, Injinia wa JWTZ, Samwel Yamo, tuliamua kwenda maduka ya madawa Kawe na kununua dawa moja na kisha kwenda kwenye Mahabara ya Hospitali ya Mhimbili kwaajili ya kupima vile vipimo zaidi ya vitano na pale tulikaa pale Mhimbili na kupatia majibu yetu na ilipofika saa mbili usiku tukaanza safari ya kurudi Lugalo,na tulipofika Lugalo saa tatu suki mimi na Samwel tulikabidhi majibu ya vipimo hivyo kwa manesi na kidogo tulimkuta Agnes akianza kupata nafuu kwa mbali huku akiwa ametundikiwa Drip la Damu.Kumbe jana saa nne usiku mimi, mama yangu na ndugu zao pamoja na kaka yako Sam tulipokuwa tunazungumza na wewe wodini ukiwa umeanza kupata fahamu kwa mbali na ukaanza kuongea na Ishara,huku ukiwa unamngang'ania mama yangu Oliva asiondoke kwenda nyumbani alale na wewe kumbe ndiyo ulikuwa unatuaga kwa mara ya mwisho.Sisi tuliondoka usiku huu tukiwa na matumaini makubwa kuwa angalau umeanza kupata nafuu ukilinganisha na jana mchana wakati unaletwa hospitalini hapo kumbe ndiyo ulikuwa unatuaga.Na leo asubuhi ndio mama yangu ananipigia kumuuliza hali yako mama ananificha ananitaka mimi na bossi wetu Absalom Kibanda twende kwanza Lugalo hadi pale nilipoaza kuzungumza na mama kwa ukali anieleze unaendeleaje ndipo mama akaanieleza ukweli kuwa umefariki na Kibanda naye ambaye alifika asubuhi ya leo Hospitalini hapo naye akanipigia simu kunithibitishia kuwa umefariki.Nilisikitika sana na kuanza kulia mwenyewe.Agnes alikuwa ni mdogo wangu ni kitaaluma kwani nilimpokea alipoanza kazi pale Habari Corporation mwaka 2004,nilimfundisha jinsi ya kusaka habari na kumuunganisha na vyanzo kadhaa vya habari, lakini mwanzoni mwaka mwaka 2005 Agnes alipunguzwa kazi hapo na alikuwa katika kipindi kigumu kwani bado alikuwa ni mchanga kwenye taaluma,nilimfariji na kumwambia asikate tamaa na nikammwambia msaada nitakaompa ni wakumtafutia chombo kingine cha habari ambapo nilimtaka aende kwenye Gazeti la Tanzania Daima,aonane na mhariri wa Michezo wa gazeti hilo enzi hizo alikuwa Erick Antony na kabla hajakwenda kumuona mimi nilimpigia simu kaka Erick Antony na kumwomba amsaidie mdogo wangu huyo apate nafasi hapo ya kuandika na Erick alikubali na kuniambia nimruhusu Agnes aje ofisini kwakwe kumuona nikamjulisha Agnes aende kumuona Erick ambaye kwasasa ni Mhariri wa gazeti la Serikali la Habari Leo, alipokwenda kumuona alimkubalia aanze kazi na Agnes alikuja kunishukuru kwa msaaada huo niliyompatia,na kweli akiwa Tanzania Daima ,Agnes ndipo alipoanza kuchomoza kwenye fani ya Uandishi wa habari hapa nchini.Lakini kumbe wakati nampatia msaada huo Agnes naminilikuwa najiandalia mtu wa kuja kunipokea kikazi.Ilipfika mwaka 2006 nilipunguzwa kazi pale gazeti la Tanzania Daima, na niliamua kumpigia simu aliyekuwa Mhariri mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Deodatus Balile kumuomba aniruhusu nije kufanyakazi katika gazeti analoliongoza, Balile alinikubalia na ilipofika mwaka 2007 ,chini ya uongozi wa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima,Absalom KIndanda nilipata ajira hadi sasa, ila Agnes alionekana kukata tamaa baadaye akaamua kuacha kazi ya uandishi na kuamua kufanyakazi ya kutafuta matangazo katika gazeti hili,kazi ambayo alikuwa akiifanya hadi anafikwa na mauti.Agnes ,kaka yako Samwel anakulilia,mimi na wafanyakazi wenzako pamoja na ndugu zako tunakulilia na kipenzi chako Kibanda ambaye katika kipindi chote cha kuugua kwako hukupenda kuwasiliana na sisi wote isipokuwa Kibanda na Betty Kangonga wanakulilia.

Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.Hakika Nitakukumbuka mdogo wangu Agnes,nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuakikisha wamadaktari wanaokoa maisha yako lakini kume mungu alikuwa na mipango yake ya kukuchukua.Nakulilia Agnes Yamo.

CHANZO.www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
25/9/2012