MAUJI,MAUAJI JAMANI
Watanzania
huyu ni binadamu mwenzetu ambaye leo alfajiri ya kuamkia leo Aprili 20
amekutwa na mauti.Sisi wakazi wa Mtaa wa Sinza 'C' eneo la Ukuta wa
Posta maarufu kama ukuta wa Kesi ya Abdallah Zombe, leo saa 11 alfajiri
tulijikuta tukiamkia kuona mwili wa marehemu huyo ukivuja damu katikati
ya barabara na ukiwa umelazwa chini baada ya kuua na watu
wasiyojulikana.Nikiwa kama raia mwema na Mwandishi wa habari baada
yakufika eneo hilo la tukio nilichofanya nikumpigia Simu mkuu wa
Upelelezi wa Mkoa wa Ilala,ACP-Duwani Nyanda na Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kinondoni, ACP- Charles Kenyela kuwapa taarifa na kweli baada ya
muda mchache waliwaagiza askari wao wakafika eneo la tukio na kuuchukua
mwili huo ambao ulikuwa unavuja damu.Inasikitisha sana, na inaendelea
kudhiirisha kuwa baadhi ya watanzania hivi sasa wamezidi kuwa na roho
katili na hawana hofu ya mungu.(Picha na Happiness Katabazi)
Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook:happy katabazi
Aprili 20 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment