Header Ads

KESI YA LWAKATARE YAIVA MAHAKAMANI







Na Happiness Katabazi

UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya tuhuma za ugaidi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph,ulieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Mbele ya Hakimu Mkazi Alocye Katemana, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Peter Mahugo  alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kutajwa na kwamba  kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na hakimu Katemana aliiarisha kesi hiyo hadi Mei 13  kwa ajili ya kutajwa na akaamuru washitakiwa warejeshwe rmumande.

Machi 20 mwaka huu, ilidaiwa mawakili wa serikali  waandamizi Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na Peter Mahugo, kuwa kosa la kwanza ambalo linawakabii washitakiwa wote kuwa ni la kula njama kutenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha 284  cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , na kwamba mnamo Desemba 28 mwaka jana, huko Kimara King’ong’o  Stopover, wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kutaka kutumia  sumu kwa lengo la kumdhuru  Denis Msaki  ambaye ni Mhariri wa habari wa Gazeti la Mwananchi ambalo ni kinyume na kifungu cha 227 cha sheria hiyo.

Wakili Rweyongeza alilitaja  kosa la pili kuwa ni la kula njama  ambalo pia ni kwaajili ya washitakiwa wote  ambalo ni kinyume na kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, ambapo washitakiwa hao walitenda kosa la ugaidi la  kutaka kumteka Msaki  kinyume na kifungu  cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

Shitaka la tatu ni la washitakiwa wote ambapo wanashitakiwa kwa kosa la  kupanga kufanya makosa ya ugaidi  kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana,walishiriki katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki  kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi.

Shitaka la nne, Rweyongeza alidai linamkabili Lwakatare peke yake  ni aliwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi , kwamba Desemba 28 mwaka jana, Lwakatale akiwa ni mmiliki nyumba hiyo ilipo Kimaraka King’ong’o  kwa makusudi  aliliruhusu  kufanyika kwa kikao hicho baina yake na Ludovick  cha kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka nyara Msaki hata hivyo walikanusha mashitaka hayo.

Chanzo: www.katabazihappy.blosgpot.com; Mei Mosi mwaka 2013.


No comments:

Powered by Blogger.