Header Ads

KORTI KUU ,KUMSIKILIZA SHEIKH PONDA NOVEMBA 18







Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Novemba 18 mwaka huu, itasikiliza ombi la Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda linayoiomba mahakama hiyo ipitie uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro uliokataa kumfutia kosa la kwanza
Kwa mujibu wa wakili wa Ponda, Juma Nassor alilithibitishia gazeti hili kuwa ni kweli tayari mahakama imeishawapangia tayari hiyo ya kuja kusikiliza ombi hilo na tayari Jaji Rose Temba ndiye amepangwa kusikiliza ombi hilo la kufanyia mapitio.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro hivi karibuni alikataa kumfutia kosa la kwanza ambalo anatuhumiwa kutenda kosa la uchochezi wakati akiwa ndani ya adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja Hali iliyosababisha Ponda kupatia Wakili wake kuwasilisa Mahakama Kuu ombi la kufanyiwa mapitio kwa uamuzi huo Kwani wanaaminj Hakimu alikosea kisheria kupatia kumfutia Ponda kosa Hilo.

Agosti 27 mwaka huu, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongola mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Richard Kabate alidai  kuwa Sheikh Ponda alitenda makosa ya uchochezi Agosti 10, mwaka huu saa 11.45 jioni kwenye maeneo ya Kiwanja cha Ndege, Morogoro.

Wakili Kongola alidai  siku hiyo, Ponda alialikwa akihutubia kwenye  Kongamano la siku ya  Eid lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri Mkoa wa Morogoro (Uwamo) na kwamba akiwa hapo alitamka maneno : “Ndugu Waislamu, msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), ambao ni vibaraka wa CCM na Serikali na kama watajitokeza kwenu watu hao na kujitambulisha kwamba wao ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, fungeni milango na madirisha ya misikiti yenu na muwapige sana,” huku akijua kutoa maneno hayo ni kosa kisheria.

Alidai  kwa kufanya hivyo, Sheikh Ponda ambaye anatetewa na wakili Juma Nassoro, alivunja masharti ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, ambayo Mei 9 mwaka huu, ilimtia hatiani kwa kosa moja la kuingia kwa jinai katika kiwanja cha Chang’ombe Markas, na mahakama ikamfunga kifungo cha nje kwa masharti ya kumtaka Ponda awe mtu mwema na asijihusishe na vitendo vya uvunjifu wa sheria.
 
Katika shtaka la pili, Sheikh Ponda anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kutenda kosa la jinai kwa kuwaambia: Serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Waislamu, lakini haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo waliokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Wakristo.” Shtaka la tatu ni kudaiwa kutamka maneno yaliyoumiza imani ya watu wengine kama yalivyo katika shtaka la pili.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Novemba 14 Mwaka 2013.
 

No comments:

Powered by Blogger.