Header Ads

UPELELEZI KESI YA MADABIDA WAKAMILIKA



Na Happiness Katabazi 

UPANDE wa jamhuri Katika Kesi ya kusambaza dawa za kupunguza MAKALI ya ugonjwa wa ARVs inayomkabili  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam Kuwa upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika.


Wakili wa serikali Jacline Nyantori adai Mbele yaHakimu Mkazi  Nyigulila Mwaseba, 
Kuwa upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika na wa naomba wapangiwe tarehe ya kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa.

Hakimu Nyigulila aliarisha kesi hiyo hadi Aprili 23 Mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya upande wa jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa.

Mbali na Madabida washitakiwa wengine  ni Seif Salum Shamte ,Simon Msoffe, Fatma Shango ,Sadiki Materu na Evance Mwemezi na kwamba hati ya mashitaka ina jumla ya mashitaka matano.

Februali 10 Mwaka huu, washitakiwa Hao walifikishwa wa Mara ya kwanza Mahakamani hapo wakikabiliwa makosa matano yakiwemo makosa ya    la kusambaza dawa za ARVs zilizokwisha muda wa matumizi kinyume na kifungu cha 76(1) cha Sheria ya Taifa ya Vyakula, Madawa na Vipodozi ya mwaka 2003 na kuisababishia Bohari yaMadawa Hasara  ya sh 148,350,156.48

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 19  Mwaka 2014.


No comments:

Powered by Blogger.