SERIKALI INA BEMBELEZA PENZI KWA MADEREVA?





Na Happiness Katabazi

KWA wale wote waliopo au wanataka kuingia Kwenye mahusiano ya kimapenzi basi watakubaliana mwanamke au mwanamme Katika mahusiano mmoja Kati Yao wakati mwingine at afanyiwe Vituko Vya aina gani na mwenzi wake basi uvumilivu Vituko hivyo ukiwemo Usaliti kwasababu eti anabembeleza penzi,mahaba kutoka kwa Mpenzi wake.

Nimelazimika kutumia mfano kwasababu makala yangu ya Leo nitazungumuzia uwendawazimu unaofanywa na baadhi ya madereva wa mabasi ya kawaida na yaendayo Mkoani ambao pindi wanapojisikia wanatangaza kuanzisha migomo haramu ya  kutoa huduma ya usafiri na wakitishia kidogo serikali inafyata Mkia.

Leo ni Mara ya pili madereva Hao watagoma ,mgomo wa kwanza ulikuwa ni Aprili Mwaka huu ambao ulileta Usumbufu wa Hali ya juu kwa wananchi ambao wanatumia huduma hiyo.

Katika makala hii naamanisha serikali ni Mwanaume na madereva na Wamiliki wa mabasi ni wanawake Katika mahusiano hayo ambayo nimeyapachika ni kama mahusiano ya kimapenzi.

Katika mahusiano haya ni wazi Mwanaume (serikali) anaonekana amelewa na mahaba mazito anayopewa na Mpenzi wake huyu ambaye ni Madereva na ndiyo maana mwanamke amekuwa sasa anataka kujifanya ana sauti ndani ya nyumba hii(ndani ya nchi), lolote analotaka kufanya hata Kama yanavunja Sheria za nchi anafanya kwasababu anaamini Tayari mumewe (serikali) hapindui.

Na kweli serikali ilisema madereva waende shule wa kasome ,matumizi ya vitochi (mwanamke ) yaani madereva wakaja juu na mgomo juu ,mume yaani serikali akafyata Mkia na serikali ikamtuma Waziri wa Kazi na Ajira ,Gaudencia Kabaka na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Katika Kituo cha Mabasi ya Ubungo, kwenda Kumbembeleza Mke wake yaani madereva na Waziri Kabaka akamruka futi Sita Usawa wa choo ,Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Kuwa lile agizo alilolitoa kwa madereva wakasome ni lake na Si la serikali.

Na Kamanda Kova na yeye akaagiza madereva na makonda waliokuwa wamekamatwa waachiwe Mara Moja na kweli walipachiwa na madereva Wakarudi kutoa huduma mtaani na kujiona wao ni washindi na serikali imesalimu amri Kwao na wanajitapa ukikaa nao madereva na makonda Hao.


Kwa tabia hii ya migomo nalazimika Kusema Kuwa ipo siku Ombaomba 'Matonya' wa mitaani wataamka nao watasema wanagoma kwasababu tumekataa kuwapatia Fedha wanazotuomba huko mitaani tunapokutana nako wamekaa huku wakiwa wamekaa chini na vibakuri au wanatembea na serikali Itatuma viongozi wake kwenda kuwasikiliza.

Lakini Mbona makundi mengine ya Ambayo yalikuwa yanaandamana, kuanzisha migomo likiwemo kundi la Wahitimu wa JKT ,Februali Mwaka huu walivyoonza kuleta Chokochoko ,haraka sana walishughulikiwa na sasa hawasikiki tena?

Au hawa madereva na Wamiliki wa mabasi ni watoto wa mwisho Kuzaliwa na serikali ndiyo mAana serikali inawadekeza HIvi? Maana Inasifika Kuwa mtoto wa mwisho kuzaliwa ndiyo uwa kipenzi cha wazazi na umekerwa sana.

Polisi Kazi yako kulinda Raia na mali zao na Kupambana na wahalifu sio kufanya Doria kwa waliogoma.Waliogoma Leo siyo wote ni wachache kwanini serikali isiwafutie leseni hawa watu?

Nasema HIvi sumu haionjwi,madereva hawa ni wazi wanaonja sumu.

Kwani madereva wanagoma kutoa huduma mwaka huu tena Katika Kipindi hiki cha uzandikishaji wa Daktari la kupiga kula ,Fukuto la kuelekea uchaguzi uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka huu kinafukuta Kwani limekaribia?


Kwani madereva Hao hawakugoma Mwaka Juzi ,Mwaka Jana au tufanye Januari Mwaka huu?Hivi Mwaka Jana suala la wao kutakiwa kwenda chuoni kusoma na kupata mikataba hali kuwepo?

Isiwe hawa madereva wanatumiwa na wanasiasa wanaotoka ndani ya CCM na vyama vingine kufanya huu uwendawazimu Wanaojifanya Ambao unasababisha wananchi wanaotumia huduma ya usafiri huo wa sipende kufanya shughuli za kuzalisha uchumi wa nchi na mwisho wa siku uchumi wa nchi utetelekea ili mambo ya hapa nchini Kwenye Ramani ya Kimataifa yaonekane ni ovyo ovyo hasa tunapoelekea Katika Uchaguzi Mkuu Oktoba.

Tusipowadhibiti sasa HIvi hawa wahuni wasiotaka kujiendeleza kielimu kwa visingizio Vya kijinga ambavyo vimesababisha Leo wanafunzi wa sipende mashuleni wafanyakazi wengine washindwe kwenda makazi ni na watu wengine washindwe kwenda kulitumikia taifa Lao kwasababu ya kukosa huduma ya usafiri.

Ikitokea siku ya Uchaguzi Mkuu wakagoma ,Wapiga kura watafikaje Katika Vituo Vya kupiga kura ili wapige kura?Tujifunze Kwenye migomo iliyopita kwanini hatutaki kujifunza?

Suala la Usafirishaji ni nyeti mabasi yanabeba wafanyakazi wa kila Sekta  na watendaji wa serikali .

Hivyo kitendo cha kuendesha mgomo wa mabasi  kufanya watendaji wa serikali wa kila Idara kutufanyakazi  kwa maana hiyo  serikali siku hiyo ya mgomo inakuwa na baadhi ya watendaji wake ambao hawajafika ofisini kwasababu ya kukosa huduma ya usafiri kwasababu eti madereva wamegoma.

Nyie madereva uchwara wateja wenu ni sisi abiria siyo serikali, sasa Kama ni abiria na wao wanagombana na serikali  kwanini madereva wanatuadhibu sisi abiria kwa kutunyima Kwa makusudi huduma ya usafiri?

Mnachotufanyia ni sawa na Mchunga Ng'ombe ambaye siku zote anakuwa anatembea nyuma ya Ng'ombe anaowaswaga   Kuwapeleka Kwenye Josho  sasa yule Ng'ombe aliyetangulia Mbele agome kuingia kutumbukia ndani ya Josho na kugoma kwake kutasababisha wale Ng'ombe waliokuwa nyuma yake kushindwa kusonga Mbele.

Maana yake ukitaka Mchunga Ng'ombe akitaka kumchapa bakora yule ng'ombe wa kwanza aliyegoma , ni wazi mchungaji hatoweza kumfikia haraka yule ng'ombe aliyegoma na matokeo yake mchungaji ataanza kuwachapa  Ng'ombe waliokuwa Mbele yake ili aweze kumfikia Yule Ng'ombe wa Mbele aliyegoma kuingia Kwenye Josho.

Kwa Tafsiri nyepesi hapa kosa aliyofanya Ng'ombe wa Mbele anaadhibiwa Ng'ombe wa nyuma ambaye Hana hatia.

Hivyo Kama madereva wana ugomvi na serikali (Ng'ombe wa Mbele) kwanini  madereva wanakuja kutoadhibu abiria ambao ni Ng'ombe wa nyuma ?

Hii dhana  ya Ng'ombe wa Mbele Kutenda kosa halafu Ng'ombe wa nyuma ndiye adhibiwe ni dhana ya kipuuzi sana na haikubaliki kwa watu wenye akili timamu na ambao hawana utapiamlo wa akili.

Madereva wa usafiri wa umma wakumbuke wanaogoma kutoa usafiri wa umma wakae wakijua wanadhibu pia hata ndugu na Jamaa zao maana nao ni abiria na hasa pale wanapousisha  Makundi ya wahuni kuwafanya vitendo Vya kihuni 
 madereva ambao hawataki kushiriki mgomo huo.

Ni wendawazimu tu wanaweza kuendesha mgomo wa mabasi kwa mtindo huo mnaoutumia. Maana Leo Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekubali Leo mchana kukutana Na Nyie mzungumze lakini Nyie Tayari mmeishagoma na mmeleta madhara Kwa abiria ,watu tumeshindwa kwenda Kanizini,madarasani na shughuli nyingine mbalimbali kwasababu ya kukosa usafiri.

Kwani mngetuma wa wakiishi wenu Katika mkutano huo wa Pinda halafu Nyie mngeendelea kutoa huduma ya usafiri Kama kawaida huku mkisubiri Yale makubaliano yatakayokuwa yamefikiwa Katika Kikao chenu na Pinda ,mngechubuka Ngozi?

Hilo ni sawa na mshitakiwa aliyetenda kosa la kuua kwa kukusudia halafu mwisho wa siku anakiri kosa Hilo.Hata akikiri kosa haisaidii chochote Kwani Kukiri kwake Hakuwezi kurudisha Uhai wa marehemu.

Ni serikali gani inao uwezo wa kuwafungia baadhi ya madereva wanaosababisha ajari kizembe lakini serikali hiyo hiyo inashindwa kuwabana madereva kwenda kusoma vyuoni?

Lakini nimejiuliza sana kuhusu Kauli ya Waziri Kabaka aliyoitoa Mbele ya madereva siku walipogoma Katika mgomo kwamba lile agizo la madereva kutakiwa kwenda chuoni kusoma zaidi siyo agizo la serikali ni agizo la Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji, hivi chuo cha Usafirishaji Si ni mali ya serikali?

Binafsi namuunga mkono Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji wa Taifa, kwa agizo lake la kuwataka madereva warudi vyuoni wakasome zaidi mAana Hakuna ubishi baadhi ya matendo yanayofanywa na baadhi ya madereva Kama kujihusisha na ulevi wa Pombe, mirungi wakati wa Kazi ni wazi Kabisa Kama madereva hawa watarudishwa vyuoni wakapewe elimu ya kisasa ni wazi wengine wakaachana na matendo hayo ya ulevi ambayo yanashusha heshima ya Kazi Yao.

Kwani madereva Hao hawakugoma Mwaka Juzi ,Mwaka Jana au tufanye Januari Mwaka huu?Hivi Mwaka Jana suala la wao kutakiwa kwenda chuoni kusoma na kupata mikataba hali kuwepo?

Hivi serikali hii haina Mbadala wa kupata mabasi ya usafiri ili yatumike kutoa huduma kwa wananchi wake hadi wananchi wake wanateseka kwa kukosa huduma hiyo kutoka hawa madereva ambao kwanza mgomo wao haupo halali kisheria na bado serikali inaendelea kucheka nao?

Na ninachokiona hapa tangu mgomo wa kwanza ni serikali inachokiangalia ni Kutafuta utatuzi wa mgomo kwa Kipindi kifupi tu siyo utatuzi wa muda mrefu.

Nasema hivyo kwasababu haiingii akili ni Aprili tu ,mgomo wa kwanza uliotikisa nchi umetokea serikali ikajitokeza kuzungumza nao lakini Leo tena wamegoma tena?

Na Mbaya zaidi hawa Wamiliki wa vyombo Vya usafiri ni Kama sasa wao ndiyo wapo juu ya Sheria na wao ndiyo kila kitu wakiamua kugoma bila kufuata Taratibu wanagoma Hakuna wa kuwachukulia Hatua. Uhuni huu hadi lini?

Ifike mahali sasa serikali itafute njia nyingine ya kuweza kumiliki mabasi yake yenyewe ili kuondokana utegemezi wa huduma ya usafiri itolewe na watu binafsi.

Madereva wako Wengi tu mitaani hawana ajira tena wasome Katika vyuo Vya VETA,kwanini serikali inawabembeleza madereva wanaotesa wananchi wake?

Kisheria Tunaambiwa pande mbili zinazolumbana zinapoamua kwenda Kwenye meza ya Usuluhishi basi kila upande Unatakiwa Kwenda Katika meza hiyo ikiwa na nia safi ya kutoka ufumbuzi wa tatizo.

Sasa Leo Pinda tumeambiwa anaenda kuzungumza na hao wenye mabasi ,lakini sote ni mashuhuda upande wa watoa huduma ya usafiri wanaingia Kwenye kikao hicho  wakiwa hawana nia safi Kwani Tayari tangu asubuhi wamezuia vyombo vyao Vya usafiri visitoe huduma na siyo Siri Mimi ni miongoni mwa waathirika wa mgomo huu.

Niitimishe kwa Kusema hivi, sisi Kama wananchi Tumechoshwa na hii tabia ya migomo hasa mgomo huu wa madereva ,umetuchosha kabisa na hatuoni serikali ikionyesha Ukali kwa kuwachukulia Hatua Kali hawa madereva Kama serikali ulivyokuwa Kali KWA kuwachukulia Hatua wanafunzi wa vyuo vikuu, wahitimu wa JKT na migomo ya madaktari.Tumechoshwa na uhuni huu.

Na hawa madereva wanaendelea kutufanyia uhuni huu sisi abiria tusiyo na hatia kwasababu Tayari wameishabaini wakitikisa serikali ,serikali na Jamii inatikisika ndiyo maana wanaendelea na siku zote (Ukicheza na Nyani utavuna Mabua), sasa Leo tuna vuna Mabula kweli kwasababu serikali imewachekea sana hawa madereva Kwani ilikuwa na uwezo wa kisheri  wa kuwachukulia hatua Kali ikiwa ni pamoja na kuwafutia leseni.

Naishauri serikali isibembeleze penzi la aina hii yaani huduma ya usafiri kutoka kwa mwanamke huu wa aina hii ambaye ni madereva kwani ni wazi hapo hakuna mahaba tena ya dhati zaidi ya mwenzi mmoja kujifanya yeye ndio yeye na anamdharau mume wake serikali na watoto wa serikali ambao ni abiria ambao wananyima huduma ya usafiri na mwanamke huyo ambaye ni madereva.

Mapenzi gani hayo kila kukicha mmoja anajifanya yupo juu ya mwenzio na anajichukulia maamuzi anayoyataka yeye ambayo yanaumiza watoto?

Umefika wakati sasa wa Mwanaume yaani serikali kusimama Kama mwanaume na kutoa maamuzi ambayo yatofautisha nani ni mwanaume na ni nani ni mwanaume.

Kwa mtazamo wangu mimi namshauri Mwanaume(serikali) , itoke kwenye ulevi wa kulishwa Dawa za kupumbaza wanaume katika mapenzi ambazo wenyeji wa Mkoa wa Kagera wanaita ( Shuntama) na Wenyeji wa Mkoa wa Iringa wanaita Limbwata. 

 Huyo mwanamke aliye naye sasa yaani madereva wa usafiri wa umma siyo mwanamke wa kuendelea Kuishi naye ndani ya nyumba Kwani kupitia matendo yake hayo ya kuvunja Sheria za nchi ya kuamua kugoma kutoa huduma ya usafiri  ni wazi ameishalichoka penzi Lako sasa wakati umefika wakumpa talaka aende kuolewa na Hao mabwana wapya aliyoyapata ambao wanamtia wazimu wa kuanzisha migomo haramu kila kukicha ambayo inatesa wananchi wao.

Na serikali itakuwa ni Baba wa ajabu sana kuendelea kukumbatia Mke wa aina hii yaani hawa wa Madereva hawafahi kabisa kuendelea Mke wa serikali. Serikali ikachumbie mwanamke mwingine mwenye elimu,adabu,mzalendo kwa taifa hili asiye kubali kuingiza siasa uchwara Katika Biashara yake imuone atupatie huduma ya usafiri ya uhakika yaani wabia wengine tena wenye Fedha zao waruhusiwe Kuleta mabasi watoe huduma.

Ni taifa la ajabu sana hili eti tuna madereva ambao hawataki kwenda vyuoni kujiendeleza.Mungu atusaidie sana. 

Mungu Ibariki Tanzania

Chanzo: Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Mei 4 Mwaka 2015



No comments:

Post a Comment