Header Ads

TUME YA MAADILI NI KICHAKA CHA UFISADI

Na Happiness Katabazi

IJUMAA iliyopita, asasi tano zisizokuwa za kiserikali zilifungua kesi ya kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kupinga kanuni ya 6(1) na 2 na 7(2)(c) ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kanuni ya 6(1) na (2) inakataza vipengele ambavyo vinaweka pingamizi visivyo vya lazima, vya kumzuia mwananchi kuwa na haki ya kupata taarifa zinazotolewa na viongozi wa umma kuhusu rasilimali, mapato au madeni yao.

Asasi zilizofungua kesi hiyo ni Mtandao wa Asasi zilizo Kusini mwa Afrika zinazojishughulisha na Masuala ya Haki za Binadamu (SAHRINGON), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISATAN), Asasi inayojishughulisha na Haki za Wanawake (KIVULINI) na Shirika la Kitaifa la Msaada wa Sheria (nola) na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA).

Hati ya madai ya asasi hizo, inadai kwamba kifungu cha 7(2) (c) kinachozuia mtu aliyepata fursa ya kuona mali za kiongozi wa umma kuzitangaza hadharani, kinapingana kabisa na Ibara ya 18 ya katiba ya nchi yenye vipengele (a), (b), (c) na (d) ambavyo vinampa raia wa Tanzania haki ya kupata habari.

“Vifungu hivyo vinavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 132 kifungu kidogo cha 4 na cha 5(b), na pia kwenye sheria hiyo ya maadili kanuni ya 9, kifungu kidogo cha (1) na kanuni ya 14, ambavyo vinatoa mwanya wa kufunguliwa kesi ya jinai kwa mtu au chombo chochote kitakachotoa taarifa kuhusu mapato, rasilimali na madeni ya viongozi wa umma,” ilisema sehemu ya hati hiyo ya madai.

Kutokana na hali hiyo, asasi hizo zimefungua kesi hiyo kuomba tafsiri ya mahakama na pia kuitaka mahakama itamke kuwa kanuni hizo za Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 ni batili kwa kuwa inapingana na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo ndiyo sheria mama ya nchi yetu.

Hii ina maana kwamba yeyote anayetaka kujua ni lazima aende mwenyewe kwa Kamishna wa Tume ya Maadili alipe ada ya sh 1,000 na akishapata habari hizo arejee nyumbani akalale usingizi. Kwa kifupi vipengele hivyo vinatumika kama kichaka cha kuficha ufisadi.

Sisi Watanzania tuna wajibu wa kutumia kila njia kujenga miundombinu ya kiutawala na kisheria itakayoweza kuzuia ufisadi.

Moja ya miundombinu ya kisheria ni Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, lakini sheria hiyo kwa kuweka vipengele hivyo ni kukumbatia ufisadi kwa maana ingekuwa mali za viongozi zinawekwa hadharani, leo hii tungejua wazi Andrew Chenge ana vijisenti kwenye akaunti yake huko Kisiwa cha New Jersey au bingo aliyopata.

Kutoturuhusu tujue hilo, ni kutunyima fursa ya kumpima huyu kiongozi kama ni mkweli au mlaghai.

Na hii ina maana kwamba Chenge hajataja akaunti yake hiyo kama sehemu ya akaunti zake. Ameidanganya tume na anastahili kufunguliwa mashtaka.

Vivyo hivyo sheria hii imetunyima fursa ya kujua kwamba Rais mstaafu Benjamín Mkapa ‘Bwana Msafi’ na washirika wake, walitangaza mali zao na kuwa wanamiliki Kampuni ya Tanpower.
Ukweli ni kwamba lipo kosa la jinai kama viongozi hawa hawakuandikisha mali zao hizo kwa Kamishna wa Tume hiyo na wanastahili kushtakiwa haraka iwezekanavyo.

Hii ni sehemu tu ya mashtaka ambayo yanaweza kuwakabili waheshimiwa hawa kama Rais Jakaya Kikwete ataacha tabia yake ya kuwakumbatia mafisadi na badala yake kusimamia sheria na katiba kama alivyoahidi kwenye kiapo chake pale Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Desemba 21 mwaka 2005.

Vipengele viwili tunavyovijadili vya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ni vichache tu kati ya sheria nyingi mbovu zinazowaletea wananchi wasiwasi na mkanganyiko wanapojadili uvunjwaji wa katiba na ufisadi.

Mfano, tunajua kwamba katiba inamlinda rais aliye madarakani na mstaafu na kuwawekea kinga wasishtakiwe kwa makosa yatokanayo na utekelezaji wa madaraka yao ya urais.

Swali ni je, pale rais aliyepo madarakani au mstaafu wanapogundulika kwamba wametumia madaraka kujinufaisha binafsi, kinga hiyo bado itasimama?

Kwa fikra zangu, naona kinga hiyo haiwezi kuwalinda viongozi wanaotumia nafasi zao za uongozi kwa maslahi yao binafsi.

Hivyo sitaki kusikia ile hoja ya Rais Kikwete aliyoitoa mwaka jana, kwamba ‘hatafuatilia tuhuma za ufisadi au uvunjwaji wa sheria na katiba zinazomkabili mtangulizi wake Mkapa.’

Naamini kwamba hoja hiyo ya rais si sahihi kwa kuwa tumeanza kugundua kwamba, Rais mstaafu Mkapa, hakuwa mwadilifu kwa taifa letu.

Itatusaidia sana kupambana na ufisadi kama uchunguzi huru ungefanyika kuthibitisha kama kweli Mkapa alitumia muda wake wa urais kujilimbikizia mali, yeye na familia yake.

Kwa vyovyote vile, hilo lisipoeleweka, vita dhidi ya ufisadi itakuwa imetushinda. Lakini vile vile tujadili hoja ya mwenendo wa hivi sasa wa viongozi waliotuhumiwa kuhusika na ufisadi, kung’ang’ania madaraka mpaka walazimishwe kujiuzulu.

Kweli hiyo inathibitisha kwamba utamaduni wa uwajibikaji unaozingatia usafi usiotiliwa shaka wa viongozi wa umma, haujajengeka bado hapa Tanzania.
Kwa hiyo, kiongozi anapotuhumiwa anawajibu kwa kiburi, dharau, kejeli wale wanaomtuhumu kana kwamba wamemzulia kashfa zisizo na msingi.

Hii ni tamaa na ulafi wa madaraka, na ni ushahidi tosha kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa kulea viongozi waadilifu na wenye kuheshimu wananchi.

Kero hii inaenda sambamba na kero ya Rais Kikwete kushindwa kufanya maamuzi na kuchukua hatua kali na kuwawajibisha viongozi wa aina hii.

Rais Kikwete amekuwa mtumwa wa tume za uchunguzi, kana kwamba hana vyombo vya dola vya kumshauri. Pia kwa tabia hii ya kuwaruhusu mafisadi wajiuzulu, inathibitisha kwamba rais anawakumbatia, na kwamba hayuko tayari kuwawajibisha.

Lakini athari za hili ni kwamba, viongozi wanaondoka na marupurupu yao na haki zingine ambazo wangenyimwa kama wangefukuzwa kazi.

Pia inaonekana kana kwamba kwa kujiuzulu, viongozi hawa wamekwepa msumeno wa sheria ambao ni kufunguliwa mashtaka mahakamani na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Kwa mantiki hiyo, mawaziri wanapojiuzulu kwa kashfa za ufisadi, wamekuwa na tabia ya kutojiuzulu ubunge kana kwamba ni jambo la heri kuwa na wabunge mafisadi.

Sifa za uongozi na maadili ya uongozi yanayowabana mawaziri, ni sawa na yale yanayowabana wabunge. Kwa hiyo, haitoshi kujiuzulu uwaziri ukabaki kuwa mbunge.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

0755 312859
katabazihappy@yahoo.com

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, April 30, 2008

2 comments:

Anonymous said...

Happiness: Kwanza nikupongeze kwa mchakoto wko wa maswala ya nchi yetu kwa ujumla na hasa inapokuja upande wa sheria na maslahi ya sisi walala hoi ambao ndio wengi hapa nchi. Mimi nimekuwa nikifuatilia sana hoja zako. Nina omba unisaidi maswali haya machache: Je mtanzania wa kawaida kama mimi nitawezaje kutumia sehemu yangu kama raia wa tanzania kuhakisha kuwa hoja zako hizi hazipotei bure na zina zaa matunda? Je kama serikali haiwezi kumshitaki mtu kama mkapa na mafisadi wengine mimi kama mtanzania ninaweza kumshktaki kwa manufaa ya taifa? Kama ninao ushahidi? Je kama serikali kweli haitaki kumshitaki unafikiri mtu binafsi kama mimi ninaweza kushinda kesi hio? Kwasababu wajaji wote wa mahakama kuu akiwepo jaji mkuu ndio wanateuliwa na Rais unafikiri kweli hapo kunautendaji wa haki? Je kwanini hawa majaji wakuu wanateuliwa kila mara anapoingia raisi mpya? Huoni kwamba wanakuwa wanafungamana na raisi aliekuwa madarakani na kufuata maamuzi ya raisi? Kwa nini nafasi ja jaji mkuu isiwe nafasi ya utumishi kwa kipindi chote cha maisha ya jaji mkuu mapaka anapopoteza uhai wake au kushindwa kufanya kazi kutokana na afya yake? Ilikuepuka kila raisi kuja kuchagua mtu wake atakaye mlinda? Kuna maamuzi mengi sana yanatolewa na serikali kinyume cha katiba na sijui kwanini hatuoni waandishi wengi wa habari wakishilia bango mambo haya badala ya kukaa kusifia ujinga unafanywa na serikali? Swali la mwisho.Je hizi maada zako unazichapisha kwenye magazeti? Na ni gazeti gani?Unatusaidia sana kutuelimisha sisi watanzania lakini nafiri unahitaji mshikamano wa watu ili nguvu zako zisipotee bure sasa sijui unaushauri gani ilituweze kufanya hii harambee yakuwashirikisha wananchi walio wengi waweze kusimama na kupigania haki zao za msingi kabisa. Kweli inakuwaje fisadi anajiuzulu uwaziri lakini hajiuzulu ubunge? Je ubunge ni cheo cha mafisadi? Rais anatamko gani juu la hili swala? Najua ukiuliza atasema anasubiri sheria ifuate mkondo wake kwa madai nchii hii inaongozwa na mfumo wa sheria a yeye sio hakimu.Nimesema hivyo kwasababu nimeshawahi kumsikia akiota majibu hayo na waandishi wanarithika na jibu hilo.Lakini ukiangalia ukweli nchi yetu inaendeshwa kwa matakwa binafsi ya kundi fulani.Kila mtu anajiamulia mambo yake kulingana na maslahi yake hakuna utawala wa sheria hata chembe.Sheria anayoizumngumzia JK ni sheria ya mwizi wa ng'ombe lakini sio sheria ya wao waliokuwa serikalini.Kama nchi ingekuwa inaendeshwa kwa utawala wa sheria mbona zaidi ya nusu ya serikali yake wangekuwa wako jela?Je ni kwa nini kashfa kubwa kama hizi raisi anachukua muda mrefu sana kutoa msimamo wake kama raisi? Na wakati mwingine anakuwa hata hazungumzii kabisa kashfa hizi kana kwamba hazipo? Hii inatujengea picha gani? Je anajali kweli matatizo haya yanayoifilisi nchi? Lini raisi huyu ataacha kuwakingia kifua mafisadi? Je kwa nini huwa kashafa hizi zinachukua muda mrefu sana kama vile ni kesi za mauaji? Inakuwaje mpaka leo hii report ya Mwakyembe bado serikali haijatoa tamko lake? Au ndio imefikia mwisho? Inavyooneka awamu hii ya kwanza itakwisha bado tunazungumzia EPA,BOT, Richmond,(Lowassa, Karamagi) Mkapa, Yona, Chenge na wengineo.Ombi lingine je unaweza kutuwekea hotuba za JK za mwisho wa mwezi kwenye website yako tukawa tunasikiliza au hata kama ikishindikana kusikiliza basi hata kusoma. Najua ilitakiwa kila mwandishi wa habari aweamesha pata kopi ya hotuba hio walau mud mfupi tu baada kabla ya mwenyewe raisi kuitangaza ili waandishi wa habari wawe wanapata muda wakipitia na kuuliza maswali lakini ninashaka kama huwa hilo linatokea. Kwasababu hata kwenye maktaba ya raisi ilokuwa kwenye mtandao hotuba zake za mwisho wa mwezi hazipo na badala yake zimejaa bajeti za tangu mwaka 2005 na hotuba za waziri wa fedha.Naomba utusaidie kwa hilo. Pia jaribuni kumshauri JK ajijengee utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari mara kwa mara na kupokea maswali ambayo hayajaandaliwa.Yaani maswali ya papo kwa papo.Ambayo yanagusa maisha ya kila mtanzania. Waende waandishi kama wewe ambao wanaweza wakauliza maswali kama haya unayotuandikia sio waandishi wa IPP. asante sasna kwa kutuelimisha. Mtanzania mwenye uchungu na nchi yake.

Anonymous said...

JE HUKUMU HII YA HAKI KWETU?
Sisi Viongozi (Rais, Makamu Rais, Mawaziri na Wawakilishi wa Madarasa) wa serikali ya wanafunzi ya chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine,tunapenda kufikisha kwako kilio chetu tukiomba utusaidie kwani tumefukuzwa chuo bila kupewa sababu hasa zilizotufanya tufukuzwe.
Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 14/11/2008 wanafunzi wote wa vyuo saba vya umma tulifukuzwa kwa muda usiojulikana.Baadaye tulipotakiwa kujaza fomu na kukubaliana na masharti yote kama yalivyoamuliwa na chuo ili tudahiliwe upya chuoni.Nasi kama wanafunzi wengine tulijaza fomu hizo kukubaliana na masharti hayo.

Hapo baadae mnamo tarehe 14 Decemba, 2008,Uongozi wa chuo kikuu Sokoine ulitoa majina 32 ya wanafunzi ukidai tulihusika kuanzisha na kuongoza mgomo ikiwamo kufanya vikao visivyo halali,kuwalazimisha wanafunzi wenzetu kuandamana,kuharibu mali za wanafunzi wenzetu na za chuo.Hivyo tulitakiwa kujibu tuhuma hizo kwa barua za maelezo ndani siku nane (8) tu ,kweli tulijibu barua hizo kama ilivyotakiwa.

Baada ya kufungua chuo mnamo tahere 8, tuliitwa kuhojiwa na tume ya uchunguzi iliyokuwa imeandaliwa na tume ya nidhamu.Baada ya kuhojiwa tuliruhusiwa kudahiliwa na kuendelea na masomo kama wanafunzi halali.

Mnamo tarehe 9/2/2009 majira ya saa nne tulipewa barua zikituhitaji kumwona kiongozi wa wanafunzi, tulipokwenda kumwona kiongozi wa wanafunzi tulilazimishwa kuweka saini pasipo kujua kusudio la barua tulizopewa, kwani kusudio la barua liilikuwa ni kutufukuza chuoni. Chuo kiuu cha Sokioine kimediliki kutusajili kuendelea na masomo tena kwa muda wa mwezi mmoja tukiwa tumelipa ada ya mwaka mzima hata mhula wa masomo ambao hatujasoma na kuamua kuchukua fedha tulizopewa na wazazi waliolala njaa kwa siku kadaaa ama kuuza baadhi ya vitu,mifugo na hata mashamba ili tu tupate hizo fedha za kulipa tuendelee na masomo,wengine tukiwa tumekubali kwa dhati kukatwa kiasi cha fedha toka fedha za mkopo toka bodi ya mikopo ilimradai kutimiza masharti ili tuendelee na masomo lakini tarehe 9 februari kwa mabavu,bila sababu za msingi za kufukuzwa,tulilazimishwa kuweka saini na kupewa barua za kufukuzwa chuo tena tukilindwa na kundi la maaskari zaidi ya 5 kana kwamba tu maahabusu walio na kesi ya kuua au ya uahini.Je huu si wizi wa waziwazi na uonevu tena wa kibabe kuchukua fedha yetu ya ada ya mwaka mzima pasipo kusoma?.

Sisi binafsi hatukulidhishwa na maamuzi ya kamati ya nidhamu kutokana na sababu zifuatazo,

1. Kipengele cha (vii) katika fomu ya masharti tulizojaza ilitudahiliwe upya chuoni, kilieleza kuwa kwa mwanafunzi yoyote atakaye bainika kuchochea mgomo ama kuvunja sheria hatadahiliwa.Sisi tulidahiliwa tena tukitakiwa kulipa ada ya mwaka mzima wa masomo,hata muhula ambao hatujasoma,tulifanya hivyo,tukadahiliwa na kusoma kwa takribani mwezi mmoja hadi mnamo tarehe 9/2/2009 tulipopatiwa barua tena tukilazimishwa kutia saini kukubaliana na barua hizo pasipo maelezo ya kina.
Kama tulionekana kuwa chanzo cha mgomo kwanini tuliruhusiwa kudahiliwa,tukalipa ada ya mwaka mzima,kwa kuwasumbua wazazi n hata tena kukubali kukatwa katika fedha za mkopo,Je huo si uonevu?,Kama ulisitahiri hukumu hii basi tungeachiwa kiasi chetu hiki kidogo cha fedha kitusaidie sisi binafsi au hata kukirudisha kwa familia zetu zilizojipigapiga na kukopa huku na kule.

2. Hakuna Ripoti yoyote tuliyopatiwa wala kuoneshwa kutoka tume ya uchunguzi wala kamti ya Nidhamu ikionyesha ushahidi kuwa sisi tumepatikana na makosa waliyotutaka kuyajibu kutokana na Mgomo uliopelekea wanafunzi wote wa kampasi ya mazimbu kufukuzwa kwa muda usiojulikana.

3.Tulipoitwa kuhojiwa na tume ya uchunguzi,tulijieleza kulingana na shutuma dhidi yetu,Hakukuwa na kithibitisho tuliochoonyeshwa kuthibitisha kweli tulihudhuria vikao visivyo kuwa halali kama wanavyodai,hatukuonyeshwa mali za wanafunzi wala za chuo tulizoshutumiwa huharibu, hakukuwa na mashahidi waliothibitisha makosa yetu,Je kamati ya Nidhamu imepata wapi uthibitisho kuwa tulihusika na makosa tuliyoshutumiwa?.

4.Matokeo ya mahojiano kati yetu na kamati ya uchunguzi yalikuwa siri kwao kwani hakuna ripoti tulizopewa wala kuonyeshwa ili kujua matokeo ya mahojiano yetu na kamati iliyotuhoji.

5.Utetezi wetu haukusikilizwa kabla ya kufukuzwa kwetu na wala hatukupewa sababu halisi ama ripoti iliyoonyesha makosa halisi tuliyopatikana na hatia,Je walijuaje na wakati hakuna mashaidi wala vithibitisho vilivyothibitisha kuwa tulipatikana na hatia.

6.Barua ya kutufukuzwa haikuonyesha makosa halisi tuliyopatikana na hatia isipokuwa walitaja vipengele vya ujumla kutoka sheria na kanuni za chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine kuonyesha kuwa tulipatikana na hatia na kusitahili kufukuzwa chuo.

7.Tume ya nidhamu haikutenda haki kwani imetufukuza baadhi ya viongozi na kuwaacha viongozi wengine ambao tulituhumiwa kuwa na hatia sawa na kutoa utetezi sawa,Je ni uthibitisho upi tume ilitumia kuonyesha kuwa hawakuwa na hatia na kutufanya sisi tupatikane na hatia na hatimaye kufukuzwa chuo?.

8.Ukisoma sheria na kanuni za chuo PART IV namba 11 inasema twanukuu” In the exercise of his statutory theRregistrar as Disciplinary Authority shall normally be assisted by an Advisory Disciplinary Panel consisting of:
1. A senior academic member of staff who shall serve as chairperson
2. the dean of students university Legal officer (secretary)
3. Two students appointed by the students organization
4. The Dean or his/her associate of the Faculty of which the charged student belongs
5. One person appointed by the academic Staff Assembly (SUASA) from amongst members
Nadiliki kusema kuwa Registrar as Disciplinary Authority katoa maamuzi yake pekee ama kuwashirikisha watu walio na mlengo kama wake ili kutimiza adhima ya kutufukuza pasipo kuwashirikisha watu waliotajwa hapo juu,kwani hakuna wanafunzi,Dean from faculties waliohudhuria kiao hicho,taarifa wamesikia tukiwa tumefukuzwa tayari.

Tukinuukuu toka SUA CHARTER,first schedule under rule 52 kinasema,

52.-(1) No formal proceedings for a disciplinary offence shall be instituted against a student unless he is previously served with a copy of the charge setting out the nature of the offence which he is alleged to have committed, and the charge shall be prepared by the disciplinary authority after carrying out such preliminary investigations as he may consider necessary.
(2) The charge shall state briefly the nature of the offence which the accused is alleged to have committed, and shall set out in concise form the allegations made against the accused student.
(3) The charge under sub-rule (1), drawn up shall then be served upon the accused student, together with a notice addressed to him, inviting him to state in writing, within twenty one days, the ground upon which he relies to exculpate himself.
(4) The disciplinary authority shall within thirty days from the day on which the charges were served to the accused student appoint an inquiry officer or officers, to hold an inquiry into the charge together with an accused student’s defence if any.
(5) The Inquiry Officer shall notify the accused student of the day, date, time and place and at which the inquiry shall be held. The inquiry shall not be open to the public.
(6) The accused student shall have a right to appear before the Inquiry Officer, examine witnesses and be heard in his own defence, save that failure by the accused student to appear at the inquiry shall not vitiate the proceedings.
(7) The accused student shall have a right-
(a) to cross-examine any witness examined by the inquiry officer or by the disciplinary authority or his representative;
(b) to examine and make copies of any document
produced as evidence against him; and
(c) to call witnesses on his own behalf and produce any document relevant to the inquiry.
(8) The Inquiry Officer may take into consideration any evidence which he considers relevant to the subject of the inquiry before him, notwithstanding that such evidence would not be admissible under the law relating to evidence, and shall record the gist of the evidence adduced before him.
(9) Upon the conclusion of the inquiry, the inquiry officer shall forward the record of proceedings before him, together with his report on the proceedings to the disciplinary authority.
(10) A report under sub-rule (8) shall-
(a) state whether in the opinion of the Inquiry Officer the charges against the accused student have been proved;
(b) state the reason or reasons for holding that opinion;
(c) state any fact which, in the opinion of the Inquiry Officer, aggravates or mitigates the gravity of the act or omission which was the subject matter of the charge;
(d) state any other fact which in the opinion of the Inquiry Officer is relevant but shall not contain any punishment to be awarded;
(11) Upon receipt of the record of proceedings and the report, the disciplinary authority shall, after considering the evidence and the report of the inquiry officer within thirty days after receiving report, make and record a finding whether or not, in his opinion, the accused student is guilty of the disciplinary offence with which he was charged.
(12) Where the disciplinary authority's finding as to the guilt or innocence of the accused is contrary to the opinion of the inquiry officer as expressed in his report, the disciplinary authority shall record his reasons for the finding.
(13) Where the disciplinary authority finds the accused student guilty, he shall proceed to award the punishment prescribed by the regulations in respect of the disciplinary offence or such lesser punishment as he deems appropriate.
Hivyo ukisoma na kama tulitakiwakujibu barua ya maelezo ndani ya siku 8 kuanzia tarehe 14/12/2008 mpaka tarehe 22/12/2008 ambazo ni siku nane(8) na si ndani ya siku 21 hawaoni wametunyima haki yetu ya kupitia na kujibu kwa makini shutuma zao kwa kuvunja kipengele 3 under rule 52?

Pia kwa kutotuonyesha mashaidi,document zao zinazotuonyesha tunahatia wanekiuka sheria katika kipengele 7(a,b and c) under rule 52.

Hivyo kutokana na kipengele 9 under rule 52 of first scheduleof SUA CHARTER tunaona Mwanasheria wa chuo katoa hukumu kulingana na maamuzi na anavyojisikia yeye(Aidha kutokana na kukwaruzana ama kujibizana kwa jaziba ziku ya mahojiano)ndiyo maana hata hakuweza kutoa uthibitisho kwa kila kosa katika barua waliyotufukuza na hivyo kutupatia shutuma zilizo too general ili mradi tu tuonekane na hatia.

Tumepatiwa mwezi mmoja wa kukata rufaa kama hatukulidhika na maamuzi ya kamati ya nidhamu,

(a) wasiwasi wetu ni kuwa je rufaa yetu itasikilizwa mapema na kutufanya kurudi chuoni mapema wakati wenzetu wanaendelea na masomo na mitihani kama kawaida.
(b) Je tume iliyotusikiliza wakati uliopita na kutoa maamuzi haya(Ya kufukuzwa chuo) tena bila,kuleta mashaidi kuthibitisha makosa yetu,kutojali ushahidi wetu wala kutuonyesha matokeo ya mahojiano yetu na wao,Je ikisikiliza tena rufaa zetu itatoa hukumu sahihi tena kulingana na haki na hatimaye kutufanya turudi chuoni?.

MUNGU TUBARIKI SISI VIONGOZI WOTE WA CHUO KIKUU SOKOINE TULIOFUKUZWA TUTOKANA NA MGOMO WA WANAFUNZI WOTE ULIOFANYIKA NOVEMBA, 2008.

Powered by Blogger.