Header Ads

SERIKALI ISIKUMBATIE WAWEKEZAJI WABABAISHAJI

Na Happiness Katabazi

SERIKALI imeamua kuikopesha kampuni ya (TRL) Sh.bilioni 3.6 kwa miezi mitano sawa na Sh milioni 700 kila mwezi ili iweze kuwalipa wafanyakazi wake.

, baada ya kudai kuwa haina uwezo wa kuwalipa kima cha chini Sh.160,000 hali iliyosababisha wafanyakazi kugoma.

Imefikia hatua hiyo ,baada ya kampuni hiyo kudai kuwa haina uwezo kuwalipa wafanyakazi wake kima chini sh 160,000.Hali iliyosababisha wagome kufanya kazi.

Aliyetangaza kuikopesha TRL ni Waziri MKuu, Mizengo Pinda , wakati akijaribu kumaliza mgogoro wa mgomo wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo.Hapa nadhani Pinda alilazimika kukubali serikali kubeba mzigo huo ili kuwalainisha wafanyakazi warejee kazini.

Pinda alilazimika kuingilia mgogoro wa wafanyakazi na menejimenti ya TRL baada ya wafanyakazi hao kugoma mwanzoni mwa mwezi huu wakidai makato ya mshahara wao.

Menejimenti ya TRL ilishwa kuwalipa kima cha chini cha Sh 160,000 kama ilivyokuwa imeahidi Machi mwaka huu.

Katika mkataba uliofikiwa baina ya wafanyakazi na menejimenti ya TRL, mshahara mpya ungeanza kutolewa Machi mwaka huu.Mshahara huo ulikuwa ukipanda kutoka sh 87,000 hadi sh 160,000.

Inawezekana Watanzania tumeungalia mgomo ule kama ni wawafanyakazi kudai maslahi yao tu, tukaacha hoja kubwa kuhusu mwenendo wa ubinafsishaji wa mashirika ya Umma .Shirika la reli likiwa ni moja wapo.

Tayari tulishaandika kueleza kwamba sera ya ubinafsishaji wa mali za umma ni mbovu .Ubovu wa sera ile upo, umejikita kwenye msingi wa kuabudi na kutukuza wawekezaji toka nje badala ya kutegemea kwanza nguvu za wananchi.

Nakuona jinsi nguvu hizo zikiwekwa pamoja zinaweza kuzaa mtaji mkubwa kuliko mitaji wanayoweza kuleta mwekezaji yeyote.

Hivyo basi tulikosea tulipo binafsisha mali zetu kwa wageni bila kuangalia kwanza uwezekano wa sisi wenyewe kujibinafsishia sekta hizo.

Somo kuu ni Benki ya Taifa ya Biashara(NBC),TTCL na mashirika mengine ambayo tuliwapa wawekezaji kwa bei ya kutupa mithili ya bei ya nazi sokoni wakati mtaji wa kuyaendesha tunayo.

Shirika la Reli limebinafsishwa kwa kampuni ya TRL kampuni ambayo haina sifa katika Sayansi ya Teknolojia ya reli na uendeshaji wake duniani.

Tunajua kwamba nchi zinazoongoza katika Teknolojia hiyo ni Ujerumani,Japan,China na Ufaransa.Inashangaza kwamba Watanzania tumejifunga kwa wawekezaji njaa wa Kihindi kwa miaka 25 ijayo. Wawekezaji ambao hata fedha ya kuwalipa wafanyakazi kwa wakati hawana.

Sasa wawekezaji kama hawa tunatizamia vipi walete vichwa vipya ,injini mpya na mabehewa mapya ya treni?

Aiyumkini hawa watapaka rangi mabehewa yaliyopo na kukarabati vichwa vya treni vilivyopo na labda kama wataagiza,wataagiza vichwa vilivyochoka kufanya kazi huko India.

Hivi Watanzania tumekosa nini hadi tunajidharirisha kiasi hicho?

Lakini hoja nyingine kubwa kuhusu ufumbuzi mwingine uliofanywa na Waziri Mkuu Pinda, walipa kodi watamlipia mwekezaji mishahara ya wafanyakazi kwa miezi mitano .

Je huo ndiyo wajibu wetu katika mkataba wa mwekezaji huyu wa Kihindi?Kama sivyo, si anayeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa, si anafutiwa mkataba?

Ikiwa kwamba kila mwekezaji atashindwa kutekeleza wajibu wake, kisha serikali itambebea mzigo wake, kuna sababu gani ya kuwaita wawekezaji wa aina hii kuja kuwekeza hapa nchini kwetu?

Kwa lugha nyepesi, sisi walipa kodi hatukufurahishwa na hatua iliyochukuliwa na serikali ya kuwalipa mishahara wafanyakazi wa reli, kwasababu hatua hiyo ni sawa na serikali inamfunga nepi mwekezaji.

Nianavyo mimi, alichotakiwa kufanya Pinda katika mgogoro huo ni kumwamuru mwekezaji kufungasha vilivyo vyake na kuondoka kwa sababu haiingi akilini kwa mtu tulimpa kutuendesha mradi wetu wa mabilioni kushindwa kulipa mshahara wa wafanyakazi wake.

Pinda asidhani kwamba kwa kufanikiwa kumaliza mgogoro huo kwa njia ya kuchukua fedha zetu na kumpa mwekezaji kutainusuru serikali na maswali kutoka kwa hawa wanaochukuliwa fedha na kupewa mgeni ambaye anachuma faida kubwa kutoka kwenye mradi tuliompa.

Namshauri, athubutu kuchukua hatua ngumu katika mambo magumu kama haya, kwa sababu Watanzania hawataki kuiona serikali ikikumbatia wawekezaji uchwara na wababaishaji.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika

0755 312859

Chanzo:Gazeti la Tanzania Jumapili la April 27,2008

2 comments:

Innocent Kasyate said...

Hongera bibie kwa mtizamo yakinifu. Mimi nadhani hawa viongozi wetu wavivu kufikiri wao maslahi binafsi mbele.Ya nchi hawayajui, ni tatizo la kizazi cha wazazi wetu, nakwambia kama si kusubiri kustaafu ama kufa, nchi hii haitabadilika.
Lakini pia, nakosa jibu kuwa hivi ni vipi tumeshindwa kuendesha shirika hili wenyewe, tumeliua, tukaiba kila kitu alafu sasa tumeleta muwek#ezaji feki, nae hawezi; je tumelaaniwa? Kwanini hatuwezi simamia mashirika haya?
Tukubali, sisi watz, wengi wetu ni wezi sana, tunalalamika tu lakini hata hao wafanyakazi wentgi wa TRL wemechangia sana kwa shirika kufika hapa lilipo leo.
Tumekwisha.

Anonymous said...

Asante sana Happiness kwa hoja yako nakubaiana na wewe 100%.Mimi mwenyewe nilishangaa jinsi walivyotatua hilo tatizo.Hiyo inaamanisa kuwa kama serikali iliweza kuwakopesha hao wawekezaji ili kuwalipa wafanyakazi huo mkataba ulitakiwa usiwepo kwani hiyo niishara kuwa hiyo kampuni ya india haina uwezo.Mimi nashangaa zaidi Viongozi wetu huwa wanafikiria nini kwani mambo mengine yanonekana wazi kuwa ni utapeli,sasa sijui ni mambo ya 10% wanazopewa au la.Napia ningeomba wabunge waangalie huo mkataba kwani unamashaka makubwa.

Powered by Blogger.