Na Happiness Katabazi
Mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Shule Kuu ya
Sheria ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, na wakili maarufu Profesa
Michael Wambari utaagwa leo Jumatatu, saa mbili asubuhi katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa heshima zote za kisomi na kisha mwili
huo kusafirishwa kupelekwa Wilayani Mpanda kwa ajili ya kuzikwa .
Marehemu alikuwa akisumbuliwa na uvimbe ambao kwa mujibu wa ripoti za madaktari walisema alipata uvimbe huo kwa njia ya hewa.
Na Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuongoza wasomi,wananchi katika
kutoa heshima za mwisho za mwili wa nguri huyo wa sheria.
Mungu ailaze roho ya marehumu mahali pema peponi.
Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com
No comments:
Post a Comment