Header Ads

BURIANI KANALI GODFREY MAKAYA


Kanali Makaya afariki dunia
Na Happiness Katabazi

ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni enzi hizo wilaya hiyo ilikuwa ikiitwa Mzizima, Kanali Mstaafu Godfrey Kajana Makaya(63) amefariki dunia.
Akizungunza ba gazeti hili nyumbani kwa marehemu Sinza Madukani Dar es Salaam, jana, mtoto wa marehemu Doreen Makaya alisema kwamba baba yake alifariki Ijumaa iliyopita saa 4:20 katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dare-es salaam. Kanali Mstaafu Godfrey Makaya alifanyiwa upasuaji mdogo wa Henia mapema Novemba 19 mwaka huu, na kuruhusiwa kutoka hospitali Novemba 25 Mwaka huu.

Hali yake ya afya ilibadilika ghafla Ijumaa, akiwa katika hospitali ya Agha Khan alipokwenda kwa ajili ya kuangaliwa maendeleo ya operesheni yake aliyokuwa amefanyiwa.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa alitakiwa arudi baadaye ili kumuona daktari majira ya saa nane mchana lakini akiwa anatembea kurudi kwenye gari, hali yake ilibadilika ghafla na kufariki muda mfupi baadaye saa nne asubuhi hospitalini hapo.

Kanali Mstaafu Makaya aliiongoza Wilaya ya Mzimzima sasa Kinondoni kwa Kipindi cha zaidi ya miaka 17 mfululizo kwa kuchaguliwa na wananchi na hadi mauti yalipomkuta alikuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni na Mjumbe wa Tawi la Sinza D.
Kanali Mstaafu Makaya alizaliwa Septemba mosi mwaka 1944. Alijiunga na jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na kustaafu kazi Desemba 9 mwaka1997 akiwa Mkuu wa Chuo cha Mgambo Mbeya.
Aidha mazishi yatafanyika kesho katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na hataazikwa kwa heshima zote za kijeshi baada ya baada ya kutolewa heshima za mwisho nyumbani kwake Sinza Madukani.Marehemu ameacha watoto kumi na sita na wajuu 29.
Mungu ametoa na bwana ametwa jina la bwana liimidiwe.

1 comment:

Anonymous said...

Unapoandika makala zako kabla ya kuziweka mtandaoni tafuta wanaojua kiswahili wakusahihishe au km una maneno unataabu ya kuyatamka usiyaandike kwa mfano:aikupambwa ni haikupambwa,waliusika ni walihusika,wameaidiwa ni wameahidiwa n.k,kazi njema.

Powered by Blogger.