JENERALI MWAMUNYANGE UMEACHA ALAMA JWTZ
Na Happiness Katabazi
Uteuzi huo ni Ishara Kuwa aliyekuwa Mkuu wa JWTZ Jenerali Davis Mwamunyange ambaye aliapishwa kushika wadhifa huo Septemba 15 mwaka 2007 ,amestaafu Kazi hiyo kwa mujibu wa Sheria.
Awali ya yote napenda kumpongeza Mwamunyange kwa kustaafu Kazi ya Jeshi akiwa na wadhifa huo salama na kuliacha Jeshi likiwa bado lipo imara na mshikamano.
Pia Nampongeza Jenerali Mpya wa JWTZ ,Mabeyo na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Hilo Luteni Jenerali ,James Mwakibolwa Kwa kuteuliwa kushika nyadhifa hizo ambapo Nawaomba mkatende Haki, mzingatie Sheria Katika majukumu yenu na mazuri yaliyoachwa na Mtangulizi wenu mkayaendeleze na myaenzi ,Yale ambayo hakufanya vizuri mkayaboreshe pia nanyie mkaanzishe mambo ya maendeleo mapya ambayo mnafikiri yatasaidia kulijenga Jeshi letu.
Makala hii ambayo ni mahususi kwaajili ya Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ambao baadhi wa Wanajeshi wao upenda kumuita 'Mwamunyange ni Kipenzi cha Wanajeshi' ambaye wamestaafu kwa mujibu wa Sheria ,itaeleza mambo Mbalimbali ya kimaendeleo yaliyofanyika ndani ya JWTZ Enzi za Mwamunyange akiwa Mkuu wa Jeshi Hilo ambayo mengine hawakuwahi kufanywa chini ya Tawala za watangulizi wake.
Septemba 15, 2007 saa nne asubuhi na Rais Jakaya Kikwete ( Mstaafu), alimuapisha Mwamunyange kuwa Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini.
Sherehe za zilifanyika katika viwanja vya Ikulu na mimi nilipata fursa ya kushiriki sherehe hizo kama Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima ambapo kwasasa siyo Mwandishi tena wa gazeti hilo hivi sasa mimi ni Ofisa Habari wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo ,Mikocheni , Dar es Salaam na ni Mwanafunzi wa Shahada ya Pili ya Sheria chuoni hapo.
Na baada ya kula kiapo sisi waandishi wa Habari tulifanya mahojiano na Mwamunyange pamoja na mambo mengine alisema Katika Utawala wake atahakikisha anakomesha tabia chafu ya baadhi ya Askari wa JWTZ kutojichukulia Sheria mkononi kwa kupiga Raia kwakisingio Kuwa ni Askari na kwamba ataheshimu Utawala wa Sheria Utawale hadi ndani ya JWTZ.
Hilo ameweza kulitekeleza kwa kiasi kikubwa kama alivyoaidi kwa vitendo kwa sababu tumeshuhudia vile vitendo vya kihuni Vya kupiga Raia vilivyokuwa vinafanywa na baadhi ya Askari wa JWTZ wasiyokuwa na Maadili vimepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na Enzi za Tawala zilizomtangulia .
Licha Katika Utawala wa Jenerali Mwamunyange kuna baadhi ya Askari wa JWTZ walituhumiwa kupiga Raia walifikishwa katika mahakama mbalimbali na vituo vya polisi na wengine walishitakiwa .
Tulishuhudia chini Uongozi wa Mwamunyange , waliokuwa vigogo wa SUMA JKT ,Luteni Kanali , Felix Samilani na wenzake wakishitakiwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Enzi hizo Aloyce Katemana, wakishitakiwa kwa makosa ya matumizi Mabaya ya madaraka lakini hata hivyo vigogo hao wa SUMA JKT walishinda Kesi hiyo na Kurejea Kazini na baadhi ya hivi sasa wamestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Hii Kesi tuliyoipachika ' kesi ya Vigogo Suma JKT 'nilipata fursa ya kuiripoti mwanzo hadi mwisho enzi hizo nikiwa Mwandishi wa habari za mahakamani wa Gazeti la Tanzania Daima.
Kupitia kesi hiyo Nilijifunza jambo Moja kubwa sana Kuwa kweli JWTZ ni Jeshi lenye nidhamu na pia linaheshimu mahakama za kiraia Kwani nakumbuka siku ya kwanza maofisa Hao kufikishwa Mahakamani walikuwa wakilindwa na maofisa wengi wa JWTZ na wala hawa kufanya Fujo mahakamani hapo.
Nilienda Kuwauliza marafiki zangu Polisi ambao tulikuwa tunashinda nao pale Mahakama ya Kisutu Kuwa ni kwanini siku ya Kesi ya vigogo wa Suma JKT Mbona Sioni Askari Polisi mkienda kuwalinda kama washtakiwa wengine ambao siyo Wanajeshi mnavyowalinda tena kwa virungu ?
Baadhi ya Polisi walinijibu huku wanacheka Kuwa wanajeshi wale walikuwa na wanajeshi waliokuwa wanawalinda kiaina .
Lakini hata hivyo Askari wa JWTZ wamefunzwa nidhamu ya Hali ya juu hawawezi Kukimbia na wakaniambia Kuwa wangelikuwa ndiyo Wanajeshi wa majeshi ya nchi za wenzetu ni wazi wangeanzisha machafuko hapo mahakamani .
Tulishuhudia wahitimu wa Mafunzo ya JKT Mwaka 2015 , wakitangaza kutaka kuandamana kwasababu hawajapewa ajira na JKT lakini JWTZ / JKT chini ya Mstaafu Huyo haikutumia nguvu ,vitisho kuwashughulikia,
.
Tulichokishuhudia Utawala wa Sheria uliruhusiwa utawale ambapo Polisi iliwakamata baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya JKT na Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) , Biswalo Mganga alie afungulia Kesi ya jinai katika Mahakama ya Kisutu na hadi sasa wazimu uliokuwa ukiwasumbua wahitimu wale JKT umepona .
Maana naweza kusema uweenda walikuwa wakisumbuliwa na wazimu vichwani mwao ndiyo maana Wakataka kuandamana huku wakijua wazi walikuwa hawana mkataba wowote na JKT ya Kuwa siku wakimaliza Mafunzo ya kujitolea ,JKT itakuwa na jukumu la kuwapatia ajira.
Itakumbukwa kwamba Mwaka 2015 , zilizagaa nchini taarifa Kuwa Jenerali Mwamunyange amelishwa sumu hivyo kapelekwa nje ya nchi kutibiwa na Hali yake ni Mbaya sana .
Taarifa hiyo ilizusha hofu nchini na kufanya ndugu wa Jenerali Mwamunyange waliongozwa na rafiki yangu ambaye aliwahi Kuwa Msemaji wa Jeshi la Polisi, ACP- Aden Mwamunyange kuitisha mkutano na waandishi wa Habari kukanusha taarifa hizo ambapo walisema ndugu Yao ni mzima wa Afya .
Hata hivyo upande wa Jamhuri ulimfungulia Kesi Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI) cha mkoani Arusha, Allan Mbando, ya kusambaza ujumbe huo kwenye Facebook ambao ulikuwa ukimtaka Mwamunyange apindue nchi na Mwaka Jana kijana Huyo alishinda Kesi hiyo.
Jenerali Mwamunyange kama as ingekuwa mtu mwenye hofu ya Mungu,na mwenye kufikiri sawa sawa ,Anayeheshimu utawala wa sheria angeamua kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwatumia Wanajeshi wake Waende kimya kimya wakamshughulike Allan na Hakuna mtu yoyote asingeweza kumhoji Kwani uwezo wa kufanya ushenzi huo alikuwa nao ila hakuona Haja ya kufanya hivyo.
Jenerali Mstaafu Mwamunyange akuwa limbukeni wa madaraka na wala hukuwa CDF mwenye hulka za kujitokeza hadharani na kutoa Kauli za makalipio kwa watu ambao mnadhani wanatishia Usalama wa wanchi Kwani tumeshuhudia baadhi ya Wakuu wa Majeshi ya Nchi za Jirani kama Mkuu wa Majeshi wa nchi ya Jamhuri ya Kongo na kwingine wakijitokeza hadharani na kutoa Kauli za kufoka na Kuonyesha haziheshimu Utawala wa Sheria hadhara .
Tulimshuhudia aliyekuwa Rais wa Malawi , Jocye Banda Akizusha mgogoro wa Kugombea mipaka ya Ziwa Nyasa baina ya Malawi na Tanzania .
Hatukumsikia wala kumuona Jenerali Mwamunyange kupayuka kwenye vyombo vya habari kuhusu jambo hilo wala akitoa ushauri kwa aliyekuwa Rais wa wakati huo ,Kikwete Tanzania ipeleke vikosi Vya JWTZ vikapambane na taifa la Malawi na Moja la jukumu la JWTZ ni kulinda mipaka ya nchi badala yake ilitumika na inaendelea kutumika Diplomasia ya Intelijensia .
Matokeo yake Diplomasia ya Inteligensia ilitawala badala ya matumizi ya Nguvu za kijeshi ,kauli za kibabe .Likaundwa jopo la wa wasuluhishi ambalo lina jukumu la kuzisuluhisha nchi za Malawi na Tanzania katika mgogoro huo wa kugombea mpaka wa Ziwa Nyasa Kazi ambayo inaendelea. kisheria tunaita ( Conciliation) .
Tulishuhudia mabomu yaliyolipuka Katika ghala la kuifadhia silaha la JWTZ ,Gongolamboto , kitendo kilicholeta taharuki Katika nchi na kusababisha baadhi ya watu kupoteza Mali zao kuharibika huku vyombo Vya Habari vikishiniliza JWTZ itoe adharani ripoti ya uchunguzi wa Chanzo cha milipuko ile lakini JWTZ iliitisha mkutano na waandishi wa Habari Katika Makao Makuu ya Jeshi Hilo Upanga ,na kuzungumza nao na kutoa fursa kwa waandishi wa Habari waulize maswali lakini mwisho wa siku JWTZ ilisema haiwezi kuanika hadharani ripoti ile ya uchunguzi kwasababu ni ya Siri na hadi Leo waliokuwa wanataka ianikwe ripoti ile bila kufahamu Jeshi Hilo lina mamlaka ya kutangaza kwa umma baadhi ya taarifa zake na taarifa zake zingine hazipaswi kuzitangaza walishasahau .Safi sana JWTZ.
Aidha tulishuhudia vitendo Vya kuhatarisha Usalama wa viongozi wa dini, wageni kule Zanzibar ambao baadhi ya viongozi wa dini, wageni wakiwemo Raia Wawili wa kigeni wakimwagiwa Tindikali .
Pia chini ya Utawala wa Mwamunyange tuliona pia kwa baadhi ya siku za Ijumaa baadhi ya Waislamu ambao walidaiwa ni wafuasi waliokuwa Sheikh Ponda Issa Ponda wakiandamana Katikati ya Mji wa Dar Salaam ,Posta Mpya na Kariakoo Hali iliyosababisha siku za Ijumaa watu kuacha Kwenda Kariakoo kuhofia vurugu na kuna siku Moja Magari maalum ya JWTZ yaliamua kupita mitaa ya Kariakoo siku ya Ijumaa na Kuzusha taaruki.
Hata hivyo tulishuhudia Mwamunyanye kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hakujitokeza hadharani kutoa Kauli yote bali tuliona mamlaka zingine kama Polisi ,Mahakama zikiwashughulikia wahusika wote kwa mujibu wa Sheria .
Binafsi Maofisa wa JWTZ nayaifadhi Majina yao ulipoteuliwa Kuwa CDF niliwabembeleza sana wanipatie maelezo binafsi yako yaani CV ,waliniita sehemu ( CHIMBO) wakanionyesha nikaisoma yote na CV ya Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo nikabaini jambo Moja ulipata fursa ya kuhudhuria kozi nyingi za Mafunzo ya kozi Kijeshi na kozi za usalama pia na Una rekodi ya Kuwa kiongozi ndani ya JWTZ.
Hata hivyo maofisa Hao wa JWTZ ambao Wengine ni wastaafu niliyokuwa nimekaa nao sehemu waliniambia nimemaliza kusoma CV ya boss wao na hivyo nimepata fursa ya kumfahamu Mwamunyange ni mtu wa aina gani na amepitia ngazi gani hadi Amefika Hatua ya kuwa Jenerali , nisiende kuuandika hicho nilichokisoma ambacho ni maelezo binafsi ya Jenerali Mwamunyange .
Enzi hizo nilikuwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima, na kweli nilitii maagizo Yao ila nilipata fursa ya kumfahamu maelezo binafsi ya Jenerali Mwamunyange.
Tumeshuhudia Ujenzi wa nyumba nyingi za makazi wa Askari wa JWTZ Katika maeneo mbalimbali yanayomilikiwa na JWTZ ukiendelea na maeneo mengine umekamilika kwa nyumba mpya za askari ,Askari wakiishi na familia zao.
Licha baadhi ya Askari wa jeshi hilo wamekuwa Wakizilalamikia nyumba mpya ambazo ni maghorofa Kuwa zina nafasi finyu mno na kwamba nyumba hizo Hazina uwezo wa Kubeba familia kubwa na vifaa Vingi Vya ndani hata hivyo wanasema wa nashukuru wa Kujengewa nyumba hizo Kwani zimewasaidia kuishi karibu na Ofisi wanaofanyia Kazi.
Aidha tumeona baadhi ya Hospitali za JWTZ zilitanuliwa na Raia wamekuwa na mwamko wa kwenda kutibiwa Katika Hospitali za JWTZ .
Mfano mmoja wapo ni Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Brigedia Jenerali Dk.Josiah Makele ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria mapema wiki hii na ameagwa jana na wafanyakazi wa Kikosi cha 521 ambapo kwa sasa Kanali Masawe ndiye anakaimu nafasi hiyo ya Mkuu wa Kikosi cha 521 Lugalo Hospitali ,ambayo imepanuliwa na kuboreshwa licha ya bado inakabiliwa na Changamoto ikiwemo baadhi ya vipimo kama Kipimo cha kubaini Alegi.
Aidha hivi sasa Ujenzi wa jengo Maalum kwaajili ya kutibia wagonjwa wanasumbuliwa na Maradhi ya Figo ikiwemo usafi shwaji wa Figo unaendelea ndani ya Hospitali Lugalo ambayo hivi sasa ina hadhi ya Hospitali Rufaa ambayo ilipata hadhi hiyo muda mchache baada ya kutokea mgomo wa madaktari nchini ambapo Kinara wa mgomo alikuwa ni Dk.Steven Ulimboka pia hadhi ukipatikana wakati Mwamunyange akiwa Mkuu wa JWTZ.
Chini ya Utawala wa Mstaafu Huyo tumeshuhudia Jeshi likianzisha Hospitali ya Watoto JWTZ iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Ambapo Hospitali hiyo ya Watoto ya JWTZ ina laza watoto wanaostahili kulazwa,ina mahabara ,chumba cha upasuaji na Duka la kununulia Madawa limefunguliwa hapo huku wa nawake wajawazito wakiendelea kupata matibabu hapo .
Na taarifa za uhakika toka ndani ya JWTZ nilizonazo ,wodi ya kuzalishia wajawazito iliyokuwa ndani ya Hospitali ya Lugalo itahamishiwa yalipo majengo ya Hospitali ya Watoto JWTZ ,Mwenge.
Mbali na Jenerali Huyo Mstaafu kuheshimu Utawala wa Sheria Utawale kikwelikweli ndani ya Jeshi alilokuwa akiliongoza bila kuwakingia Kifua baadhi ya Wanajeshi wake waliokuwa wakituhumiwa na tuhuma mbalimbali huku uraiani ;
Pia alijitahidi kuliendesha Jeshi Hilo kisasa ,kisomi ,uwazi na kuakikisha anatengeneza mazingira Wanajeshi wanakuwa rafiki wa Raia Kwani Raia JWTZ ni Jeshi Lao.
Tumeshuhudia chini ya utawala wa Mwamunyange iliyokuwa Shule ya Tiba ya Kijeshi ( SKT)ambayo ilikuwa ipo chini ya kikosi 521 Lugalo Hospitali , Ikipanuliwa kwa Kujengwa majengo mapya mengi ambapo Ujenzi wa upanuzi huo Ulianza Mwaka 2013 chini ya ufadhili wa Wajerumani .
Kisha shule hiyo ikapandishwa hadhi na kuanza kutambulika Kuwa ni ,Chuo cha Tiba cha JWTZ , kinachoongozwa na Brigedia Jenerali Dk. Robison Mwanjela kimefunguliwa rasmi 2016 na kinatoa elimu ya Tiba ngazi ya Diploma na kwa mujibu wa taarifa nilizonazo ni kwamba jitihada za makusudi za kufanya chuo hicho siku za usoni kianze kutoa elimu ya Tiba ya Sayansi kwa ngazi ya Shahada zinaendelea .
Mstaafu Huyo aliruhusu uwazi kwa kiaisi fulani kwasababu tumeshuhudia kikosi cha Makomandoo kwa zaidi ya Mara nne kikishiriki sherehe mbalimbali za Kitaifa Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam na Zanzibar na wakaonyesha baadhi ya mbinu wanazozitumia kukabiliana na adui kitendo ambacho kimendika historia mpya Katika Utawala wake kwasababu Katika Tawala zilizokuwa zikiongozwa na watangulizi wake hazikuwahi kuruhusu Makomandoo Kuonyesha maonyesho Yao hadharani na Televisheni zikawa zinawarekodi.
Binafsi nakiri Kuwa ni Mpenzi sana wa 'show 'ya Makomandoo . Hakuna ubishi ' Show' ya Makomandoo ilisababisha wale ambao Hawajawahi kuwaona Makomandoo wawaone ,Kupamba sherehe hizo za Kitaifa na kufanya wananchi Wazidi kulipenda Jeshi Lao na Kuwa na Imani nalo.
Uhusiano wa JWTZ na majeshi mengine ulizidi kuimarika Kwani tulishuhudia Wanajeshi wetu wakienda Katika majeshi mengine kwaajili ya kubadilishana uzoefu Katika kushiriki Mafunzo mbali Mbali, na Wanajeshi wa majeshi ya kigeni wakija Tanzania kutoa huduma za kujitolea na kujifunza mambo mbalimbali.
Itakumbukwa hapo zamani mafunzo ya awali ya JKT yaliyokuwa ni ya lazima lakini serikali ikaja kuyafuta lakini hivi karibu serikali wakati Mwamunyange akiwa Mkuu wa JWTZ ,ili rudisha Mafunzo hayo ya JKT kwa wahitimu wa Kidato cha Sita Ambayo hadi Sasa yanaendelea kutolewa.
Pia Mwamunyange anaelezewa Kuwa alitetea maslahi ya Wanajeshi wake na ya kuboreshwa , Jeshi lake lilishiriki Katika Michezo mbalimbali kama ilivyo Ada ya Jeshi Hilo.
Wosia wangu kwako Jenerali Mwamunyange,chondechonde nakuomba usije ukadanganyika ukaamua kujitia wazimu ukajiingiza Kwenye tamaa ya kupata madaraka ya Siasa kama eti Kugombea Ubunge,vyeo katika vyama vya siasa .Sitaki kusikia hizi Habari hapo Mbele ya safari.
Umestaafu kwa heshima zote ,tunza hiyo heshima yakokakaa nyumbani Katulie fanya mambo yako.Ukiingia Kwenye siasa ukae ukijua heshima yako yote uliyojijengea w itafutika, na sikufichi mimi ndiyo nitakuwa mtu wa kwanza kukushughulikia kwa kalamu licha nafahamu fika Ibara 21 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ina kupa haki ya kuchagua, kuchaguliwa na kuteuliwa .
Nimelazimika kukupata taadhali hiyo kwasababu aliyewahi Kuwa Mkuu JWTZ, Jenerali Mstaafu Robert Mboma alivyostaafu Akaamua kwenda Kugombea Ubunge Jimbo la Mbeya Vijijini ( CCM) kitendo kilichosababisha watu nikiwemo mimi kumshambulia vikali kwa makala ,akachafuka na kuonekana ana tamaa ya madaraka na watu wakahoji ni lini alijiunga na CCM na misho wa siku katika mchakato wa kumpata mgombea mmoja wa ubunge wa kupeperusha bendera ya CCM,jina la Jenerali Mstaafu Mboma lilikatwa na vikao Vya CCM likapitishwa jina la Kada mwingine wa CCM.
Karibu uraiani Jenereli Mstaafu Mwamunyange Kwani hivi sasa wewe ni Mwanajeshi Mstaafu. Mazuri uliyoyafanya ndani ya JWTZ yataenziwa na kuendelezwa .
Nakutakia Afya njema na Maisha Marefu Katika Maisha haya mapya ulivyoanza kuyaishi kama Mwanajeshi Mstaafu .Hakika Jenerali Davis Mwamunyange' Kipenzi cha Wanajeshi' umeacha alama ya kukumbukwa ndani na nje ya JWTZ kutokana .
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg:www.katabazihappy.blogspot.com
No comments:
Post a Comment